Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1244 | 1245 | (Page 1246) | 1247 | 1248 | .... | 1896 | newer

  0 0

   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe. Hamad Masauni akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati anawasili katika ukumbi wa mikutano wa AICC kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO). Kulia ni Mkuu wa INTERPOL kanda ya Kusini Mubita Nawa.
   Katibu Mtendaji wa SADC, Dk. Stegnomena Tax akizungumza na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu kabla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) unaofanyika mkoani Arusha. IGP Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki.
   Baadhi ya Wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika SADC wakitoa heshima wakati wimbo wa taifa unapigwa wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania, Ernest Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki. 
   Katibu Mtendaji wa SADC, Dk.Stegnomena Taxi, akitoa hotuba wakati wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) Mkutano huo ulifunguliwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni Mkoani Arusha. IGP wa Tanzania Mangu ndiye Mwenyekiti wa shirikisho hilo kwa kipindi hiki.
   Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi, Mhe.Hamad Masauni akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa afrika (SARPCCO) baada ya ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika unaofanyika Mkoani Arusha.
  Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,  IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akiwa ameambatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi la Angola, Paulo de Almeida (kushoto) na Mkuu wa jeshi la Polisi la Msumbiji, Paulo Chachine (kulia) wakati wa Mkutano mkuu wa mwaka wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi kutoka nchi za kusini mwa Afrika (SARPCCO) uliofanyika Mkoani Arusha.(Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.

  0 0


  Dar es Salaam, Tanzania – Jumatano, tarehe 24 Mei, 2017….Uber leo watawakirimu abiria wake jijini Dar es Salaam kwa ‘pizza’ ya bure kama chakula cha mchana, hii ikiwa sehemu moja ya kampeni yetu ya kuongeza kuhitajiwa kwa kuwafurahisha wasafiri wanaoabiri Uber. Toleo hili maalum litakuwepo kwa muda wa saa 3 pekee (Saa 12:pm-3:pm) na litaweza kufikiwa na abiria wa Uber

  katika maeneo ya kati ndani ya jiji.

  Akizungumzia kuhusu shughuli hii, Meneja Mkuu wa Uber nchini Tanzania, Alfred Msemo alisema, “Sisi katika Uber, siku zote huwa tunatafuta njia bunifu, za kuhusisha na za usanifu zakuwachangamsha abiria pamoja na dereva-washirika wetu – bila shaka, wao ndio sababu ya yote tunayoyatekeleza. Kwa kugusa ya kitufe tu ifikapo muda wa chakula cha mchana hivi leo, abiria wa Uber watapokea kasha la pizza yenye ladha tamu, bila ya wao kuhitajika kuondoka ofisini mwao au makazi yao.”

  Ili kupokea pizza ya bila malipo, wasafiri wa Dar es Salaam sharti wawe katika maeneo ya kati ndani ya jiji la Dar es Salaam. Ofa hii, itadumu kwa muda wa kati ya saa 12pm (saa sita mchana) hadi 03pm (saa tisa mchana) siku ya Jumatano, tarehe 24 Mei pekee, ni rahisi msafiri wa Uber anahitaji tukufungua programu ya Uber wakati huo wa kufunguliwa toleo, bonyeza bango la UberPIZZA chini ya skrini yako na kuomba UberPIZZA moja. Kama ombi limefanikiwa, dereva wa Uber atawasili mahali ulipo akiwa na UberPIZZA yako ya bure.

  “Huku tukiwa tunapenda wengi wa abiria wetu iwezekanavyo wafaidike kutokana na kampeni hii, pizza za bure zitatolewa kwa misingi ya wanaokuja mwanzo- watawahi mwanzo. Ni wasafiri waliyo ndani ya eneo lililotajwa pekee watakaoweza kuona bango la UberPIZZA kwenye vifaa vyao;aliongeza Bw. Msemo

  Kabla ya kampeni hii ya UberPIZZA, Uber walifanya kampeni ya kuzidisha mahitaji sawa na hii iliyopewa jina UberCHOMA ambapo wasafiri mjini Nairobi, Mombasa na Kampala walipokea nyama choma; ya bure kwa kubonyeza bango la UberCHOMA katika nyakati maalum. Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado, alisema, “Tunajua kwamba moja ya mambo ambayo yanatufafanua sisi zaidi, hata katika miji mikuu, ni utamaduni wetu. Kampeni hii ya UberPIZZA jijini Dar es Salaam na ile ya awali ya UberCHOMA tuliyotekeleza katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kampala ni moja tu ya njia ya kuadhimisha umaahiri wa utamaduni wa wana Afrika Mashariki na inatuunganisha na abiria wateja wetu na dereva-washirika wetu - kwa njia ambayo ni ya kukumbukwa.”

  0 0


  0 0


  0 0

   Mjumbe wa Bodi wa  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael akifungua Semina ya uelimishaji kwa Waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro leo (jana), kulia ni Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine Mungu.
   Mwanasheria Mwandamizi Bi. Irine Mungu kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi jijini Morogoro leo.
   Afisa Uhusuano Mwandamizi kutoka Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) akitoa mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi mkoani morogoro leo.
   Bw. Fabian Felician akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliofanika mkoani Morogoro leo.
   Afisa Kazi Mfawidhi mkoa wa Morogoro Bw. Simbo Swai akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanyika mkoani Morogoro leo.
   Bi. Hilda Msemo kutoka Mzinga Corporation akichangia mada katika semina ya uelimishaji kwa waajiri kuhusu haki na wajibu wa mwajiri na mfanyakazi iliyofanika mkoani Morogoro leo.
  Baadhi ya washiriki wa semina ya uelimishaji kwa waajiri wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye ni Mjumbe wa Bodi wa  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Francis Michael mkoani Morogoro leo.

  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeendesha semina ya siku moja kwa waajiri nchini katika mikoa minne, ili kutoa elimu juu ya shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika kujisajili na kuwalipa michango kwa niaba ya waajiriwa wao.

  Akizungumza katika semina hiyo mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko Dkt. Francis Michael .
  Amesema kuanzishwa kwa mfuko huo kumekuja wakati muafaka ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa viwanda hivyo kupelekea ongezeko la wafanyakazi ambapo chombo hicho ndio mkombozi wa majanga yatokanayo na kazi.                

  “Ni muda muafaka kwa waajiri kutambua wajibu wenu katika Mfuko huu na pia kutambua madhara ya kutotekeleza wajibu wenu” Alisema Dkt. Michael.

  Katika hotuba yake, Dkt. Michael alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatapo na majanga wakiwa kazini.

  Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi ni Taasisi ya Serikali chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.

  Dkt. Michael amesema, Mfuko umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa waajiri  kwa kutambua kuwa waajiri ndio wadau wakuu wa Mfuko huo na semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.

  Akitoa mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi.

  Naye Mwanasheria Mwandamizi wa Mfuko huo Bi.Irene Mungure amesema, ni muda mwafaka kwa waajiri kutambua wajibu wao katika mfuko ikiwa ni pamoja na kutambua madhara ya kutokutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria.

   Katika uzinduzi wa semina hizo jana Makao Makuu ya Nchi Dodoma, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Bw. Emmanuel Humba, alifafanua zaidi juu ya haja ya waajiri kuufahamu vizuri Mfuko namna unavyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kulipa fidia kwa wafanyakazi watakaoumia, kuugua ama kufariki. Aidha, alisema kuwa waajiri ni wadau wakuu wa uendelezaji Mfuko.

  Bw. Humba aliwaasa waajiri kutokufanya udanganyifu  na ubadhilifu hasa katika uwasilishwaji wa michango kwani itakuwa ni kuudidimiza Mfuko na ni kosa kisheria na waajiri watakaojihusisha watachukuliwa hatua za kisheria kwa mujibu wa Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi Sura ya 263 iliyorejewa Desemba, Mwaka 2015.

  Semina hiyo imefanyika katika mikoa ya Dodoma,Kilimanjaro, Morogoro na Arusha.

  0 0

   Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia) katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini Geoffrey Mwambe akiwashukuru viongozi wa Mkoa wa Singida kwa ushirikiano katika kikao kifupi cha kumuaga.
   Mkurugenzi wa TIC Geoffrey Mwambe (wa kwanza kushoto) akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi (wa kwanza Kulia) katika kikao cha kumuaga, Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo na Mkuu wa Wilaya Mkalama JacksoN Masaka.
    Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi na Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo wakifungua zawadi ya saa ambayo ina picha ya mazao ya alizeti na vitunguu ambavyo huzalishwa kwa wingi na ubora Mkoani Singida.
  Mkuu wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo akimpongeza Mkurugenzi Mpya wa TIC kwa uteuzi bw. Geoffrey Mwambe ambaye alikua Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, kulia kwake ni mkurugenzi Mwambe na kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Injinia Jackson Masaka.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) Geoffrey Idelphonce Mwambe ametoa tahadhari kwa wawekezaji wote wa nje na ndani ambao hawana nia njema na maendeleo ya taifa kuwa hawana nafasi nchini na kwamba hawatapata fursa yoyote Tanzania.

  Mwambe ametoa tahadhari hiyo jana jioni katika kikao kifupi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi kwa ajili ya kumuaga rasmi Mkurugenzi huyo mara baada ya uteuzi wake ambapo hapo awali alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

  Amesema kituo cha uwekezaji kitashirikiana na wawekezaji wenye nia njema tu ila wale ambao wanataka kujinuafiasha wao na kuliacha taifa bila faida yoyote hawatapewa fursa yoyote ya kuwekeza nchini.

  Mwambe ameongeza kuwa atahakikisha kuwa wawekezaji wenye ubora na ambao uwekezaji wao unamgusa mtanzania moja kwa moja wanapatikana hasa wale ambao watasaidia kutoa ajira kwa wananchi na kukuza uchumi.

  “Nina imani na wawekezaji wadogo ambao nitajitahidi kuwaunganisha na wawekezaji wakubwa ili wakue na wajenge uchumi wa taifa itawasaidia pia hao wawekezaji wadogo watapata uzoefu na hivyo kuwa wawekezaji wakubwa”, amesema.

  Mwambe ameongeza kuwa hatausahau Mkoa wa Singida kwenye fursa za uwekezaji na kuongeza kuwa mkoa wa Singida una fursa nyingi hasa vitunguu ambavyo vimekuwa vikisafirisha nje ya nchi na kufungashwa kwa jina la nchi hiyo ya jirani.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi amempongeza Mkurugenzi Mwambe kwa kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Raisi kutokana na uchapakazi na uadilifu wake.

  Dokta Nchimbi amesema Mkoa wa Singida umekuwa ukizalisha bidhaa nzuri na zenye ubora pamoja na kuzalisha watendaji waadilifu na wachapakazi na hivyo uteuzi wake utaendelea kuwapa hamasa vijana na watumsihi wengine waendelee kuwa waadilifu.

  Ameongeza kwa Singida ina fursa za kutosha kuleta maendeleo ya Mkoa huu pamoja na taifa kwa ujumla pia unajivunia fursa hizo ambazo baadhi yake ni kilimo cha alizeti, vitunguu na asali bora.

  Dokta Nchimbi amemuasa Mkurugenzi Mwambe kuiwakilisha Singida katika majukumu yake na pia kutumia uchapakazi wake katika kuboresha mazingira ya uwekezaji ili yawavutie wawekezaji wa nje na ndani ili kufikia lengo la tanzania ya Viwanda.

  Aidha amemkaribisha tena Singida na kumuahidi kuwa Mkoa uko tayari kwa ajili ya uwekezaji wowote wenye tija kwa wananchi na pia Singida iwe sehemu ya viwanda na kuipa nafasi Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.

  0 0


  0 0

  Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akizungumza na Viongozi wa Vyama vya Siasa na watendaji wao wakati wa mkutano wa siku moja uliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kujadili na kuweka mikakati ya kuondoa mapungufu yanayojitokeza katika kutekeleza Sheria na Kanuni za usajili wa vyama vya Siasa hapa nchini. Kushoto ni Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza na kulia ni Msajili Msaidizi Bi. Piencia Kiure.

  Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akisisitiza jambo kwa viongozi wa vyama vya Siasa (hawapo pichani),wakati wa mkutano wa siku moja na viongozi hao leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza.
  Msajili Msaidizi Bw. Sisty Nyahoza akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali yanayovihusu vyama vya siasa ikiwemo utekelzaji wa Sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992.
  Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Chama cha CCK Bw. Renatus Muhabi mara baada ya kumaliza mkutano wa siku moja uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa na Msajili wa vyama vya siasa kukutana na viongozi wa vyama hivyo na watendaji wao.
  Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Goodluck Ole Medeye akipongeza utaratibu wa Msajili wa Vyama vya Siasa kusimamia sheria na kanuni zinazosimamia vyama vya siasa ikiwemo kufanyika kwa ukaguzi wa mahesabu katika vyama vyao.

  (Picha na Frank Mvungi-Maelezo)

  ……………………..

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imepongezwa kwa kusimamia vyema Sheria na Kanuni zinazoongoza vyama vya Siasa hapa nchini hali inayochochea kukua kwa demokrasia.

  Akizungumza katika mkutano wa kawaida wa siku moja iliyoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa, Katibu Mkuu wa Chama cha UDP Dkt. Goodluck Ole Medeye amesema utaratibu wa kuvisimamia vyama na kuvikagua ili kuhakikisha kuwa vinazingatia Sheria na Kanuni ni mzuri na ni wa kupongezwa.

  “Napongeza kwa kazi nzuri ya kukagua hesabu za vyama inayofanywa na mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa vyama vinavyopata ruzuku na visivyopata ruzuku hali ambayo inachochea uwajibikaji katika vyama ” alisisitiza Ole Medeye.

  Akifafanua Ole Medeye amesema kuwa Serikali kupitia Msajili wa vyama vya Siasa anafanya kazi nzuri ya kuhakikisha kuwa kila chama kinafuata taratibu na kuomba ofisi hiyo kuendeleza utaratibu wa kukutana na viongozi wa vyama na wale wanaosimamia rasilimali za vyama kwa lengola kuhakikisha kila kimoja kinatimiza na kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.

  Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa chama cha ADA – TADEA, Bibi Ziada Athumani amesema ukaguzi unaofanywa na CAG katika vyama umekuwa sehemu ya elimu kwa watunza hazina na vyama hivyo na hivyo anapongeza utaratibu huo na kuomba ushirikiano zaidi kutoka Ofisi ya Msajili, vyama vya siasa na CAG ili kusaidia kazi ya ukaguzi.

  “Msajili wa Vyama vya Siasa ni mlezi na msimamizi wa vyama vya Siasa hapa nchini hivyo tunayo kila sababu ya kumpongeza kwa kuwa anasimamia sheria vizuri , hivyo tumuunge mkono kwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni zilizopo,”alisisitiza Bi Ziada.

  Kwa upande wake Msajili wa Vyama vya Siasa Mhe. Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Ofisi yake itaendeleza utaratibu wa kukutana na viongozi wa vyama vya Siasa ili kujadiliana na kukumbushana sheria na taratibu zinazosimamia vyama hivyo.

  Aliongeza kuwa utaratibu huo unaimarisha uhusiano na vyama hivyo na pia Ofisi yake inapata fursa ya kubaini changamoto zinazojitokeza wakati wa ukaguzi wa hesabu za vyama hivyo hali inayosaidia kuweka mikakati ya pamoja katika kuzitatua kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali.

  Pia Jaji Mutungi aliviasa vyama vya siasa kuendelea kuzingatia taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa sheria ya vyama vya Siasa.

  Kwa upande wake Msaidizi wa Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali Bw. Majura Blugule amesema Ofisi hiyo itaendelea kushirikiana na vyama pamoja na ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa ili kuhakikisha kuwa hesabu za vyama hivyo zinakaguliwa kwa kuzingatia sheria na kanuni.

  Utaratibu wa Msajili wa vyama vya Siasa kukutana na vyama hivyo umeanzishwa hivi karibuni kwa nia ya kuangalia changamoto zinazojitokeza kati ya pande hizo mbili na jinsi ya kuzitatua. Takribani vyama 17 vilishiriki katika warsha.

  0 0

  Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha akielezea juu ya uhusiano wa ukusanyaji kodi na maendeleo katika sekta ya elimu kwenye mafunzo ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini mkutano huu umewakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida.
  Mkufunzi wa Mafunzo, Wakili Dominic Nduguru akitoa mada ya uhusiano wa Makusanyo ya Kodi Na Maendeleo ya Sekta ya Elimu kwa baadhi ya wadau na mbalimbali wa elimu mkoani Singida leo kwenye mkutano ulioandaliwa na TENMET wakishirikiana na ActionAid Tanzania.
  Meneja Mradi Wa Elimu ActionAid Tanzania, Karoli Kadeghe akichangia mada wakati wa Mafunzo ya wanachama na viongozi wa Chama cha Walimu na Asasi za Kiraia waliokutana mkoani Singida leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe akielezea hali ya elimu mkoani Singida na namna ambavyo uwekezaji wa Elimu ni muhimu kuinua Sekta ya Elimu hapa nchini Tanzania.
  Baadhi ya wadau mbalimbali wa elimu mkoani Singida wakifuatilia mafunzo 
  Washiriki wakijadili juu ya upotevu wa kodi nchini kwenye mafunzo yaliyowakutanisha wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam.
  Picha ya Pamoja

  Katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto za utoaji wa elimu bora hapa nchini leo Mtandao wa Elimu Tanzania (TENMET) wakishirikiana na ActionAid Tanzania wameandaa mkutano uliowakutanisha wanachama wa chama cha walimu Tanzania (CWT/TTU) na wadau wa elimu katika mkoa wa Singida kwa siku tatu ili kupanga mpango kazi wa utetezi na ushawishi wa masuala ya elimu yatakayoleta matokeo chanya kwenye masuala ya elimu hapa nchini.

  Mkutano huu  ulikuwa ulingazia changamoto zinazoikabili elimu ya msingi hapa nchini ikiwemo upungufu wa vyumba vya madarasa, upungufu wa ofisi za walimu, upungufu wa vyoo vya wanafunzi, uwiano usiokubalika kitaratibu wa mwalimu na wanafunzi, shule nyingine kukosa kabisa mwalimu wa kike, upungufu wa nyumba za walimu, kutokutosha kwa fedha za ruzuku, utegemezi wa bajeti ya nchi unaoathiri pia bajeti ya elimu na kusababisha Serikali kushindwa kugharimia kiufanisi utoaji wa elimu.

  Mgawanyo wa ruzuku usiozingatia mahitaji ya wenye uhitaji maalumu, jinsia na mahitaji ya kijiografia na pia shule changa na zile ambazo ni kongwe. Kuwa na mipango ya kibaguzi kwa shule inayofanya vizuri ndiyo inapewa fedha (payment for results- P4R) kutoka mpango wa BRN bila kujali mizania ya usawa wa mazingira kati ya shule na shule. Kukosekana kwa mafunzo kazini kwa walimu, kutopandishwa madaraja walimu na utolipwa kwa wakati stahiki za walimu wanaohamishwa/kustaafu mfano pesa ya usafiri.

  Katika majadiliano washiriki walichangia juu Upotevu wa kodi nchini hususani katika sekta ya madini na viwanda ndio chanzo cha kukosa fedha za kutosha kugharimia sekta ya elimu nchini. 

  Akizungumza leo Afisa Mradi wa Elimu kutoka TENMET, Bi. Alistidia Kamugisha aliwasisitiza serikali kuimarisha vyanzo vya mapato yetu kama nchi hasa kwa kukusanya kodi stahiki kwa kila mtu anayepaswa kulipa kodi. Ili tuondokane na utegemezi toka kwa wahisani. Kwa bajeti ya elimu 2016/17 takribani bilioni 277 sawa na asilimia 31% ilitarajiwa kukusanywa kutoka kwa wahisani na washirika wa maendeleo. Hata hivyo hadi kufikia mwezi Machi 2017 wahisani walikuwa wametoa kiasi cha shilingi bilioni 132 tu, sawa na asilimia 47.6%. 

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida, Bw. Aran Jumbe  alisema ni vyema serikali iimarishe  vyanzo vyake vya mapato vya ndani, ili kuepuka aibu hii, na pia walisisitizwa wadau wa elimu wanalo jukumu la kuisimamia serikali katika kutimiza wajibu wake. Kila mtu akilipa kodi stahiki kadri ya kile anachozalisha na pia serikali ikidhibiti mianya ya upotevu wa kodi, hata kodi ya PAYE itapungua na kumpa mwalimu ahueni katika makato hayo.

  0 0

  Kituo cha utangazaji cha EFM redio kimecheza mechi ya kirafiki baina yao na madereva daladala siku ya leo ya tarehe 24/05/2017 katika Kiwanja cha Tanganyika Packers kuanzia saa kumi Jioni, ambapo watangazaji  wa Redio hiyo wamechuana vilivyo na wadau wao wakubwa.

  Redio hii ya vijana na jamii kwa ujumla imezidi kutoa kipaumbele kwenye michezo hususani mpira wa miguu kwani imekua ikicheza mechi nyingi za kirafiki kila inapobidi ili kuhakikisha inajenga mahusiano mazuri na jamii inayoizunguka kama wadau wa taasisi mbalimbali ili kukuza vipaji vyao.

  Mechi hizi za kirafiki ni kati ya michezo ambayo husaidia jamii kukutana kwa pamoja na kujenga mahusiano mazuri na vile vile husaidia kuhamasisha vijana kufanya mazoezi katika kuunga mkono kampeni ya serikali ya kufanya mazoezi  katika jamii ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.  0 0

  Rais mahmuud Abbas  na mwenzake Donald Trump,wakiwa katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mjini Beit Lehem

  Rais Mahmuud Abbas wa Palestina amesema kwamba,Matakwa ya wafungwa wa kipalestina walio katika jela za Israeli ni ya haki na ni wajibu wa Israli kuyatekeleza, vilevile kupatikana kwa uhuru wa taifa lake ndio ufunguo wa amani na utulivu katika ukanda huo wa Mashariki ya Kati na Dunia nzima kwa ujumla.

  Rais Abbas ameyasema hayo jana Jumanne Ikulu mjini Beit Lehem, alipokuwa na mkutano wa pamoja na mgeni wake Rais Donald Trump wa Marekani, huku akitilia mkazo dhamira yake ya kushirikiana nae katika kufanikisha mpango wa amani wa kihistoria na Waisraeli,pia kushirikiana nae Rais Trump kama washirika katika suala zima la kupiga vita Ugaidi duniani.

  Mheshimiwa Rais Mahmuud Abbas pia ametilia mkazo msimamo wa Palestina unaotegemea utatuzi wa uwepo wa dola mbili chini ya mipaka ya mwaka 1967, ambazo ni dola ya Palestina ikiwa na mji mkuu wake Jerusalemu ya Mashariki na dola ya pili ni Israeli,huku ukipatikana utatuzi wa mwisho kabisa wa masuala yote husika, kwa misingi ya maazimio ya kisheria za kimataifa na makubaliano ya pande mbili za Palestina na Israeli.

  Aidha Rais Abbas ametilia mkazo pia kwamba mzozo uliopo sio wa kidini,kwani kuheshimu dini zote na mitume yake ni sehemu ya imani ya taifa la Palestina, bali tatizo lililopo ni uvamizi, ujenzi wa makazi ya walowezi na kutokubali Israeli uwepo wa dola ya Palestina.

  Rais Abbas pia amezungumzia usumbufu wanaoupata wafungwa wa kipalestina wanaoendelea na mgomo wa kula uliofikisha siku 37 mfululizo katika jela za Israeli,huku akitilia mkazo ya kwamba madai yao  ni ya kibinaadamu na ya haki,ni wajibu wa Israeli kuyatekeleza.
  Kwa upande mwingine,Rais Abbas amelaani vikali shambulio baya  la kigaidi, lililotokea hivi karibuni mjini Manchester Uingereza lililopelekea vifo kadhaa na majeruhi,huku akitoa rambirambi zake za dhati kabisa kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo na familia za wahanga hao.

  Rais Abbas pia amemsifu Rais Trump kwa mapokezi mazuri ya hivi karibuni katika Ikulu ya Marekani na yaliyojiri katika mazungumzo yao, kwani yamewapa Wapalestina matarajio mapya ya kufikia ndoto yao ya muda mrefu,nayo ni kufikia  katika amani ya kudumu iliyo katika misingi ya haki na usawa. Pia amesifu umuhimu wa kufanyika mkutano wa pamoja wa wakuu wa kiarabu,kiislamu na kimarekani,kilichofikia maazimio kadhaa hivi karibuni.

  Mwishowe Rais Abbas amemkaribisha tena Rais Trump wa Marekani na ujumbe wake kuitembelea Palestina,huku akiwaombea ufanisi katika ziara yao itakayowafikisha kuonana na Papa Francis,ambae tunathamini sana mchango wake wa kuleta amani.Rais amemalizia kwa kutamani historia imuandike Rais Donald Trump kuwa ndiye Rais wa Marekani aliyeweza kuleta amani na utulivu kati ya Palestina na Israeli.

  Nae Rais Trump kwa upande wake, amesema anatarajia kufanya kazi kikamilifu na Rais Abbas  ili kuleta amani na utulivu Mashariki ya Kati,kuinua uchumi wa Palestina na kupiga vita ugaidi. Ameongeza kuwa,mchakato wa kuleta amani ni lazima ufanyike katika mazingira yasiyo na vurugu,huku nchi yake itasaidia pande mbili hizo ili kufikia ufumbuzi wa kudumu.

  Amesisitiza kuwa wamekuja mjini “Beit Lehem” ambao ni mji wa amani ili kushirikiana katika kuleta dunia iliyo na amani, wanaamini kuwa Palestina  na Israeli zinaweza kufanya hivyo,huku akimpongeza Rais Abbas kwa kuhudhuria Mkutano wa mjini Riyadh Saudi Arabia, ulioshirikisha viongozi wa kiarabu,kiislamu na Marekani kwa lengo la kupiga vita Ugaidi na misimamo mikali ya kiitikadi.


  0 0


  ESTOM SANGA-TASAF

  Wadau wa maendeleo wanaochangia fedha za utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotekelezwa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF nchini wameonyesha kuridhishwa na kasi ya kupambana na umaskini kupitia mpango huo ulioanza kutekelezwa takribani miaka minne iliyopita.

  Wadau hao wa maendeleo kutoka nchi na mashirika kadhaa ya misaada ya kimataifa wameonyesha kuridhishwa na namna walengwa wa Mpango huo wa kunusuru kaya maskini wanavyotumia fedha za ruzuku katika kuanzisha miradi midogo midogo ya kiuchumi inayowaongezea kipato na kuwawezesha kuboresha maisha hususani katika sekta za elimu,afya na kuboresha makazi yao kwa kujenga nyumba za kudumu.

  Wadau hao wa maendeleo ambao wako kisiwani Zanzibar kuona namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya maskini wanavyonufaika na shughuli za Mpango huo,wametembelea shahia ya Potoa kaskazini Unguja ambako wamekutana na walengwa wa Mpango huo na kujionea shughuli walizozianzisha kwa kutumia fedha ya ruzuku inayotolewa na serikali kupitia TASAF ikiwemo uundaji wa vikundi vya ususi wa vikapu,mikeka na mapambo mbalimbali ya nyumbani .

  Aidha wadau hao wa maendeleo wameshuhudia namna walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika shehia ya Potoa walivyoanzisha kitalu cha miche ya matunda na miti chenye jumla ya miche 40,000 chini ya utaratibu wa TASAF wa kuwapa fursa walengwa wake kuibua miradi na kuitekeleza wakati wa kipindi cha hari na kisha kuwalipa ujira ili kuwaongezea kipato.

  Walengwa hao wamewaeleza wadau hao wa maendeleo kuwa licha ya kuiuza miche hiyo ,lakini pia huipanda kwenye maeneo yao kama njia mojawapo ya kutunza mazingira na kujiongezea kipato na pia kuongeza ujuzi wa namna ya kuotesha miche na kuitunza kitaalam kinyume na hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kwa Mpango huo katika shehia yao.

  Mwakilishi wa Shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia, Bwana Muderis Mohamed amesema kasi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini nchini Tanzania ni ya kuvutia na kutia matumaini makubwa ya kupunguza umaskini miongoni mwa walengwa kutokana na mwitiko mzuri wanaouonyesha katika matumizi ya fedha na uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kiuchumi kama ufugaji wa bata, kuku na hata mbuzi kwa kutumia fedha za ruzuku zinazotolewa na serikali kupitia TASAF.

  Picha ya kwanza nay a pili chini wadau wa maendeleo wakiangalia baadhi ya vifaa vilivyotengenezwa na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wa eneo la Potoa kisiwani Zanzibar.

  Mmoja wa wadau wa maendeleo hakusita kununua kikapo kutoka kwa walengwa wa Mpango wa Kunusuru kaya maskini baada ya kuvutia na kazi hiyo ya mikono. Kikapo kimoja huuzwa kwa takribani shilingi 15,000 hadi 20,000.
   Mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Potoa  kisiwani Zanzibar bi. Munono Mohamed (wa pii kushoto) akizungumza na baadhi ya wadau wa maendeleo juu ya hatua yake ya kujenga nyumba kwa kutumia ruzuku ya fedha kutoka TASAF. Picha ya chini ni nyumba anayoendelea kuijenga Bi. Munono mama wa watoto  SABA.Aliyeshika daftari ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Bwana Ladislaus Mwamanga.

   Wadau wa Maendeleo wa TASAF, wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika eneo la Potoa  Bi. Panga Makame juu ya mradi wa kufuga bata aliouanzisha baada ya kupata ya kupata ruzuku. Bata mmoja huuzwa kwa takribani shilingi elfu 30.
   Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini katika shehia ya Potoa wameanzisha kitalu cha miche ya matunda na miti kupitia utaratibu wa ajira ya muda ambao ni sehemu ya Mpango huo wenye lengo la kuongezea kipato hususani wakati wa kipindi cha hari.


   Wadau wa Maendeleo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya maskini katika shehia ya Potoa kisiwani Zanzibar.


  0 0


  0 0

  Tiba hii inaitwa JIKO. Kila mwanaume anae itumia, INAMPONYESHA KABISA tatizo la UKOSEFU na UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Imethibitishwa na MKEMIA MKUU WA SERIKALI YA TANZANIA

  Kufahamu jinsi tiba hii inavyo fanya kazi, bofya link hii hapa chini :


  Kwa mahitaji yako ya tiba hii, wasiliana na duka la NEEMA HERBALIST & NUTRITIONAL FOODS CLINIC kwa simu namba 0766 53 83 84.

  Tunapatikana UBUNGO jijini DAR ES SALAAM, jirani na SHULE YA MSINGI UBUNGO NATIONAL HOUSING nyuma ya jengo la UBUNGO PLAZA. · Kwa wateja waliopo DAR ES SALAAM, wasio na nafasi ya kufika ofisini kwetu, watapelekewa dawa mahali walipo ( HOME & OFFICE DELIVERY ).

  · Kwa wateja waliopo mikoani, watatumiwa dawa kwa njia ya mabasi mbalimbali.

  · Kwa wateja waliopo Zanzibar, watatumiwa dawa kwa njia ya usafiri wa boti.

  · Kwa wateja wa Mombasa, watatumiwa dawa kwa basi la TAHMEED COACH.

  · Kwa wateja wa NAIROBI watatumiwa dawa kwa basi la DAR EXPRESS.

  · Na kwa wateja wa UGHAIBUNI ( DIASPORA), watatumiwa dawa kwa njia ya POSTA au DHL.

  · Kwa taarifa zaidi kuhusu huduma zetu, tembelea kila siku website yetu www.neemaherbalist.com


  0 0

   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) akiwakaribisha maafisa kutoka Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu. Katikati ni Kaimu Msajili wa Bodi, Dkt. Mayasa Simba na Afisa Habari na Mawasiliano wa TDB, Queenter Mawinda (kulia).
  Menejimenti ya TADB ikifuatilia majadiliano hayo.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Mayasa Simba (kulia) kuhusu nafasi ya wadau katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.
  Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Mayasa Simba (katikati) akizungumza kuhusu Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu. Wengine pichani ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (kushoto) na Afisa Habari na Mawasiliano wa TDB, Queenter Mawinda (kulia).
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga akihimiza umuhimu wa wadau kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu ili kutambua umuhimu wa kuchagiza unywaji wa maziwa nchini kama inavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani.
  Pichani ni makabidhiano ya baadhi ya vifaa vitakavyotumika wakati wa Kampeni hiyo. Wanaonesha ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) na Kaimu Msajili wa Bodi ya Maziwa, Dkt. Mayasa Simba (wapili kushoto). Wengine ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (kushoto) na Afisa Habari na Mawasiliano wa TDB, Queenter Mawinda (kulia).

  …………………………..

  Na Mwandishi wetu,

  Katika kuhamasisha Watanzania wengi wanaongeza hamasa ya unywaji maziwa, Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeunga mkono juhudi za Serikali na Bodi ya Maziwa (TDB) nchini kwa kutoa vifaa vitakavyotumika katika Kampeni ya Kitaifa ya Unywaji Maziwa inayotarajia kufanyika Kitaifa mkoani Kagera kuanzia Mei 28 – Juni 1 mwaka huu.

  Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ofisi za TADB jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Kampeni hiyo kwa kutambua umuhimu wa kuchagiza unywaji wa maziwa nchini kama inavyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani.

  “Kwa kutambua umuhimu wa Kampeni hii, TADB kwa kushirikiana na TDB na wadau wengi tumeazimia kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kufikia viwango vya kimataifa ya unywaji wa maziwa ambao unakadiriwa kufikia walau lita 200 kwa mwaka kutoka 47 za sasa,” alisema.

  Aliongeza kwa kutambua umuhimu wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa TADB ilijumuisha mnyororo wa thamani wa Ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa kuwa ni miongoni mwa minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo kwa ajili ya uongezaji wa thamani wa mifugo nchini.

  Akasisitiza kuwa Benki yake imejipanga kuendeleza uongezaji wa thamani wa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa ili kuchagiza juhudi mbalimbali za Serikali katika ustawi wa tasnia ya maziwa nchini.

  “Benki inatoa mikopo na kusaidia uwekezaji kwa ajili ya ujenzi, ununuzi wa mitambo na ufungaji wa mitambo ya kuhudumia ng’ombe ikiwemo majosho na mabwawa ya kunyweshea na pamoja na usindikaji wa maziwa kwa ajili ya kuongeza thamani maziwa,” alisema Bw. Assenga.

  Kwa upande wake Kaimu Msajili wa TDB, Dkt. Mayasa Simba amesema kuwa Kampeni hiyo ya kitaifa yenye kaulimbiu ya ‘Okoa Jahazi, Jenga Afya, Jenga Uchumi kupitia Maziwa’ imelenga kuchagiza dhamira ya Bodi ya Maziwa katika kusimamia, kuratibu na kutoa huduma bora ya ushauri kwa wadau ili kukuza na kuendeleza tasnia ya maziwa iliyo endelevu na yenye ushindani nchini.

  “Lengo la Kampeni hii ni kuhamasisha unywaji wa maziwa ili kuhakikisha Watanzania wengi wanafikia viwango vya kimataifa na pia ili kutimiza lengo la Bodi katika kuhakikisha kuwa tasnia ya maziwa inayosimamiwa na kuratibiwa vizuri, yenye ushindani kwa lengo la kuboresha maisha ya watanzania na kuongeza mchango wa tasnia ya maziwa katika uchumi wa Taifa,” alisema.

  Bodi ya Maziwa imeundwa kwa Sheria ya Tasnia ya Maziwa Sura (262) ambayo iko chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yenye jukumu la kusimamia, kuratibu na kuendeleza tasnia ya maziwa. Bodi ina jukumu la kuhamasisha na kuwawezesha wadau katika shughuli za uzalishaji, ukusanyaji maziwa, usindikaji, kuboresha masoko na unywaji wa maziwa na bidhaa zake.

  0 0  Napenda kuungana na mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Joseph Magufuli kwa uzalendo na mapenzi ya dhati anayoonyesha kivitendo kwa Wananchi na Taifa kwa ujumla kwa kuhakikisha analinda rasilimali, Mali, haki na maslahi.

  Hivi karibuni Rais Magufuli alizuia makontena 277 yenye mchanga wa madini kusafirishwa kwenda nje ya nchi na kuunda kamati kuchunguza hasara au faida tuliyokuwa tukiipata Watanzania kutokana na kusafirisha mchanga huo ambapo kamati imewasilisha taarifa ya awali imeonyesha thamani ya makontena hayo 277 ni Tsh. Bilioni 112.1 kumbe thamani halisi ni Tsh. Trilioni 1.44. Taarifa hiyo imeonyesha hayo makontena tu tulikuwa tumepoteza zaidi ya Tsh. Bilioni 829.4 ambapo kwa mwaka mmoja tu tulikuwa tukipoteza Trilioni 25 ambayo Serikali ilikuwa haipati hata senti moja.  

  Kupitia mchanga huo tu tulikuwa tukiibiwa hivyo kwa takribani miaka 18 huku tukipoteza Tsh. Trilioni 829.4 sawa na bajeti ya miaka 26 ya Tsh  Trilioni 32 kwa kila mwaka.

  Tunapoteza pesa hizo huku tukiangalia mahospitali hayana madawa, miundombinu mibovu, mishahara haikidhi, tunakopa kukamilisha bajeti ya nchi maumivu ambayo hatukustahili kabisa kuyapata sisi Watanzania.

  Ahsante sana Rais Magufuli kwa kuonyesha uzalendo wa kuzuia unyonyaji na uhujumu uchumi huu wa kikatili uliokuwa ukiendelea nchini. Ni viongozi wachache sana Afrika waliosalia wenye kariba ya uzalendo kama alionao Rais Magufuli.

  Huu ni mwendelezo wa uzalendo wa kivitendo unaoonyesha na Rais Magufuli. Tukumbuke ni Rais Magufuli huyu huyu anasimamia vyema upotevu wa mapato bandarini, kuzuia matumizi ya ovyo Serikalini ya kodi za Wananchi kwa kufuta safari za nje, kulipana posho zisizo na tija na kupunguza matumizi ya kawaida kwa kuongeza fedha zaidi kwenye matumizi ya kimaendeleo.

  Kiukweli ninaiona Tanzania mpya ikijengwa na uzalendo alionao Rais Magufuli kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla. Watendaji, viongozi na Wananchi yatupasa tuige Uzalendo wa Rais wetu mpendwa Dk. John Pombe Magufuli kwa kuungana nae kupambana na wahujumu uchumi wa nchi yetu.

  Rais Magufuli fanya uliyotumwa na wanyonge usiogope wanaojiita wachambuzi ambao kila kitu hukuchambua kinyume, hao ni changamoto ya wewe kusonga mbele!

  Tunakuombea Rais Magufuli ulinzi, Baraka, hekima na busara zaidi toka kwa Mwenyezi Mungu.

  Mungu Ibariki Tanzania
  Mungu mbariki Rais wetu Dk. Magufuli.

  Na Emmanuel J. Shilatu
  25/05/2017
  0767488622

  0 0

  Vyombo vya habari nchini hususani redio za kijamii zimetakiwa kuandika habari ambazo zinaelezea changamoto ambazo zinawakabili wananchi katika maisha yao ya kila siku na jinsi ambavyo wanaweza kuzitatua.

  Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  Alisema wanahabari na vyombo vya habari ni muhimu nchini kwa maendeleo ya Taifa lakini kama wasipokuwa makini katika utendaji wao wa kazi kunaweza kuwa na madhara makubwa hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia maadili ya uandishi wa habari.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (wa kwanza kulia) akizungumza na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura (wa pili kulia) kabla ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  Alisema sehemu kubwa ya wananchi ambao wanaishi vijijini hawapati taarifa muhimu zinazohusu maendeleo yao zikiwepo taarifa za kilimo, afya, mazingira na haki za kibadamu hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanaandika habari ambazo wananchi wamekuwa hawazipati kwa muda mrefu.

  “Ni jukumu lenu sasa kuhakikisha redio hizo zinatimiza malengo yake hususani katika kumuelimisha wanajamii, kuwajengea uwezo wa kutambua na kupambana na mazingira ili kuinua hali zao za kimaisha,” Mhe. alisema Wambura.

  Alisema mafunzo hiyo ni muhimu kwao kama wawakilishi wa redio za kijamii sababu itawapa mbinu ambazo wanaweza kuzitumia ili waweze kujisimamia wao wenyewe bila kuwa tegemezi kwa kuomba fedha kutoka sehemu zingine.
  Picha juu na chini ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Anastazia Wambura akisoma hotuba ya kufungua mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  “Natambua changamoto zilizopo katika uendeshaji wa redio za kijamii ambazo ni kama upatikanji wa habari endelevu na zinazolingana na mahitaji ya jamii husika, uhaba wa rasilimali fedha za kuendeshea redio husika, na udhaifu katika usimamizi stahiki wa taasisi hizo lakini kwa hakika mafunzo haya ni muhimu kwa vile yanalenga kutatua changamoto hizo,” alisema Wambura.

  Aidha Naibu Waziri Wambura amewashukuru Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kutoa mafunzo hayo ambayo yatasaidia kujenga Taifa lenye waandishi na wasimamizi wa habari wenye weledi na kazi zao pia mafunzo hayo yanakwenda sambamba na dira ya wizara ya kuwa na Taifa lililohabarishwa vizuri ifikapo 2025.
  Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida amesema mafunzo hayo yamekuja baada ya kufanyika utafiti mwaka 2014 kwa ufadhili wa UNDP, utafiti ambao ulifanyika kwenye wilaya tano nchini na kugundua kuwa njia bora ya upashaji habari katika maeneo hayo ni kwa kutumia redio.

  Amesema baada ya matokeo hayo ya utafiti walipendekeza kuanzishwa kwa redio jamii katika maeneo ambayo utafiti ulifanyika ili kurahisisha taarifa mbalimbali za kuelimisha wananchi ambazo zitakuwa chachu kubwa ya maendeleo kuwafikia wananchi kwa urahisi.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho katika mafunzo ya siku mbili kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini ambayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii na wawakilishi wa Halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.

  “ESRF kwa ufadhili wa UNDP ilisimamia uanzishwaji wa redio jamii nne ambazo ni Redio Unyanja (Nyasa), Redio Bunda (Bunda), Redio Kagera (Bukoba Vijijini) na Redio Ileje (Ileje) na redio zingine mbili Redio Sengerema (Sengerema) na Redio Mazingira (Bunda) zilipata misaada mbalimbali kwa ajili ya kujiendesha,” alisema Dk. Kida.

  Mafunzo hayo yamehusisha wasimamizi wa redio za kijamii kutoka wilaya tano nchini ambazo ni Ileje, Bukoba Vijijini, Bunda, Nyasa na Sengerema pamoja na wawakilishi wa halmashauri wa wilaya hizo ambao wanawakilisha halmashauri zao katika shughuli za uendeshaji wa redio hizo za jamii.Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki akitoa taarifa kwa washiriki wa mafunzo kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC), Dotto Kuhenga akitoa mafunzo kwa washiriki kuhusu redio jamii na jinsi zinavyotakiwa kufanya kazi.
  Picha juu na chini ni Mtaalamu wamasuala ya Tehama kutoka ESRF, Joseph Ngonyani akitoa mafunzo kwa washiriki jinsi wanavyoweza kutumia mitandao kuapata taarifa ambazo wanaweza kuzitumia kwenye redio zao.
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo kuhusu wajibu wa redio za kijamii kwa maendeleo vijinini.

  Washiriki wa mafunzo ya siku mbili

  0 0  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron (wa pili kulia) wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT leo jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akishuhudia. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (katikati) akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi wa NMB FANIKIWA ACCOUNT uliofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron kushoto ni Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard akiwa katika mkutano huo. Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya NMB, James Meitaron akifafanua jambo katika uzinduzi wa 'NMB FANIKIWA ACCOUNT'. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Biashara, Donatus Richard (kushoto)

   BENKI ya NMB imezindua akaunti mpya kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ijulikanayo kama 'NMB FANIKIWA ACCOUNT' ili waweze kukua kibiashara pamoja na kupata maendeleo ya biashara wanazozifanya. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa akaunti hiyo ya wafanyabiashara wadogo na wakati, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker, alisema kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu wakati wa kuifungua pamoja na uendeshaji wake hivyo kuwataka wafanyabiashara wote kuitumia. 

  Alisema kuwa NMB imebuni akaunti hiyo kutokana na kuwepo kwa changamoto ya wafanyabiashara wadogo kukosa mikopo na kukabiliwa na riba kubwa kwenye mikopo. Akifafanua zaidi juu ya bidhaa hiyo, Mkuu wa Idara ya Biashara, James Meitaron alisema Benki ya NMB imeweza kufikia kila kundi katika kuwanufaisha wafanyabiashara wadogo hasa kimikopo ambapo imewanufaisha katika kuendeleza biashara zao.
   Alisema Benki ya NMB imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na serikali pamoja na taasisi zake, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha inawakuza wafanyabiashara wadogo na wakati wakiwemo 'mama lishe'. Mkutano huo ukiendelea Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker (kulia) akizungumza na mmoja wa wateja wa Benki ya NMB kushoto.

  0 0

  Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi amewataka wananchi wa Mbogwe watoe ushirikiano wa kutosha kwa Mradi Pendekezwa wa ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi (EACOP) linalotarajiwa kujengwa kutoka Ziwa Albert kupitia Kabaale (Uganda) hadi Rasi ya Chongoleani iliyo karibu na Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

  Mkuu wa wilaya ameyasema hayo alipofungua kikao cha maoni ya wadau (scoping) kwa Wakuu wa Idara na watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe kuhusu Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Jamii (TAM) ya mradi wa EACOP. Akiongea wakati wa ufunguzi bi Martha amesema mradi huo utaleta maendeleo kwa wanambogwe wote hivyo ni jukumu lao kuulinda .

  Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirishia Mafuta Ghafi kutoka Uganda (Ziwa Albert) hadi Tanzania (Tanga) lenye urefu wa kilometa 1445 linatarajiwa kupita katika wilaya ya Mbogwe. Akiongea wakati wa kikao hicho ,mwezeshaji kutoka kampuni ya JSB Envi-Dev Ltd Dr. Godfrey Kamukara ameelezea faida zitakazopatikana kutokana na mradi huo zikiwemo upatikanaji wa ajira kwa wakazi wa Mbogwe .

  Hata hivyo alitahadharisha kuwa mradi huo unatarajiwa kusababisha mwingiliano wa makabila mbali mbali hivyo kuwataka watendaji hao wawaelimishe wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo ugonjwa wa ukimwi.

  Dr.Kamukara amewataka watendaji kuwaelimisha wananchi kuhusu mafuta ghafi ili wananchi wasitoboe bomba wakidhani ni mafuta yanayofaa kwa matumizi . Alieleza kuwa mafuta ghafi ni mafuta ambayo bado hayajasafishwa kwa matumizi ya kawaida.

  Kampuni ya RSK ya Uingereza na washirika wake kutoka Uganda ( ECO partners ) na Tanzania ( JSB Envi-Dev Ltd) wameanza kazi ya Tathimini ya Athari kwa Mazingira na Jamii kwa kushirikisha jamii yote inayopitiwa na mradi kwa kutoa maoni ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo. 
  Mkuu wa wilaya ya Mbogwe bi Martha Mkupasi

  0 0

    Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akisalimiana na Rais wa Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa la Kenya iliyoandaliwa na Bunge la nchi hiyo. Wengine katika  pichani kutoka kushoto ni Spika wa Bunge la Kenya  Justin Muturi, Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe  Ekwee Ethuro na Jaji Mkuu wa Kenya Jaji David Maraga. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai (katikati ya waliokaa kulia) akizungumza na Rais wa Kenya Mhe Uhuru Kenyatta na Makamu wake Mhe William Rutto walipokutana wakati wa ibada Maalum ya kuliombea Taifa hilo. Wengine katika picha ni Spika wa Bunge la Kenya  Mhe Justin Muturi (kulia kwa Mhe Ndugai),Spika wa Bunge la Seneti la Kenya   Mhe. Ekwee Ethuro  (wa kwanza kulia),Mke wa Rais wa Kenya Margaret Kenyatta na Mke wa Makamu wa Rais wa Kenya Rachel Chebet.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (wa pili kulia) Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  (wa pili kushoto). Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.
  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai akizungumza na Spika wa Bunge la Seneti la Kenya Mhe Ekwee Ethuro  alipomtembelea Ofisini kwake Jijini Nairobi, Kenya. Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la nchi hiyo.

  (Picha na Ofisi ya Bunge)

older | 1 | .... | 1244 | 1245 | (Page 1246) | 1247 | 1248 | .... | 1896 | newer