Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1245 | 1246 | (Page 1247) | 1248 | 1249 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0

  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella alipowasili kwenye hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na wadhamni hao na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe akimsikiliza jambo kwa makini Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(katikati) wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana, kulia ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella.
  Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi,akiongea wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo za washindi mbalimbali wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na kampuni hiyo ikiwa ndiyo wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam jana.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe, akiongea na wadau mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe,akipewa hongera na Mkurugenzi wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi baada ya kuongea na wadau walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo mbalimbali za washindi wa Ligi kuu bara, iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi Vodacom Tanzania na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC, Nandi Mwiyombella.
  Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania PLC,Nandi Mwiyombella, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 84/- Katibu mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa baada ya timu yao kuibika mabingwa wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali jana katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa masoko wa Vodacom Tanzania, Ashutosh Tiwary (kushoto) akimkabidhi tuzo ya heshima, Kitwana Manara wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi(kushoto) wakimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuchukua tuzo hiyo hapo jana wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Michezo Utamaduni na sanaa Dkt, Harrison Mwakyembe(katikati) akimshuhudia Mkurugenzi mkuu wa biashara wa Vodacom Tanzania,Hisham Hendi(kushoto)akimpongeza baba mzazi wa mchezaji wa simba, Mohamed Hussein ”Tshabalala” baada ya mtoto wake kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara 2016/2017 wakati wa halfa ya utoaji tuzo mbalimbali za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyoandaliwa na wadhamini wakuu wa ligi na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city jijini Dar es Salaam.

  Wadhamini wakuu wa Ligi ya Mpira wa miguu Tanzania Bara kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, jana ilitoa zawadi zenye thamani ya shilingi 232,974,660 kwa washindi mbali mbali wa ligi.

  Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji zawadi iliyofanyika jijini Dar es Salaama jana, Mkurugenzi Mkuu wa biashara na Masoko wa kampuni hiyo,Hisham Hendi alisema Vodacom imeongeza kiasi cha fedha zaidi mwaka huu.

  Mwaka jana tulitoa shilingi 219,502,500. Kwa ajili ya zawadi lakini mwaka huu fedha hizi zimeongezeka na kufikia shilingi 232,974,660,” alisema

  Hendi alisema, Vodacom Tanzania inavutiwa na jinsi ambavyo umaarufu wa ligi unavyokuwa ukiongezeka siku hadi siku huku ukiwavutia na kuwaburudisha Watanzania walio wengi wanaoishi mijini na vijijini bila kujali kama timu za maeneo wanayoishi zinashiriki ligi hii.

  “Pamoja na umaarufu wa ligi hii kuongezeka na mafanikio yanayozidi kupatikana, sisi kama wadhamini tunajua kuwa bado kuna changamoto mbalimbali za kuboresha ligi yetu iwe na viwango vya hali ya juu na ili kuondokana na changamoto hizi unahitajika ushirikiano mkubwa baina ya wadau wote wa mchezo wa soka nchini japo mabadiliko hayawezi kuja kwa siku moja,” alieleza.

  Mkurugenzi huyo alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kubuni mikakati ya kuboresha ligi hii na ikiwezekana wajitokeze wafadhili wengine zaidi ili wachezaji wazidi kunufaika.

  “Kama sote tunavyoelewa hivi sasa michezo sio burudani tu kama ilivyokuwa miaka ya zamani bali inasaidia kupunguza tatizo la ajira na kuinua uchumi wa nchi kwani wanamichezo wakiwezeshwa wanaweza kupitia mapato yao kuboresha pato la taifa kama tunavyosikia katika nchi za wenzetu ambako wachezaji na wasanii ni kundi la mamilionea wanaotambulika na hapa tukiamua yote haya yanawezekana na dalili zimeanza kuonekana.

  Alisema Vodacom itaendelea kuunga mkono na kufadhili mchezo wa soka na michezo mingine kwa kuwa inaamini wanamichezo ni mabalozi wazuri katika kutangaza Taifa na pia michezo huchangia kuibua na kukuza vipaji vya wanamichezo.

  “Kwa niaba ya Vodacom Tanzania naipongeza timu bingwa ya ligi ya Soka ya Vodacom msimu uliomalizika Yanga African bila kusahau timu zote zilizofanya vizuri na wote waliokabidhiwa zawadi zao leo.

  Ni matumaini yetu maandalizi ya msimu ujao wa ligi yamekwishaanza kuandaliwa vizuri na wadau wote tutashirikiana tena kuhakikisha ubora wa ligi unazidi kuwa bora zaidi,” alisema Hisham.

  0 0

  Mchoraji Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu akiwa katika Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi wa afya yake. Mzee Kanyasu amefikishwa leo MNH akitokea Hospitali ya Amana.
  Daktari Bingwa wa magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni Mkuu wa Idara hiyo Juma Mfinanga akimuhudumia Mzee Kanyasu mara baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.  Hospitali ya Taifa Muhimbili-MNH- imeanza kumfanyia uchunguzi mchoraji wa Nembo ya Taifa , Mzee Francis Maige Kanyasu .

  Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Dk. Juma Mfinanga amesema Mzee Kanyasu amechukuliwa leo asubuhi kutoka Hospitali ya Amana ambako alipelekwa jana na majirani zake na kupatiwa matibabu ya awali.

  ‘’ Tumemchukua kutoka Hospitali ya Amana baada ya kupata habari zake kwenye vyombo vya habari kuwa hali yake kiafya sio nzuri hivyo Mkurugenzi Mtendaji wa MNH , Profesa Lawrence Museru akatuagiza tumfuate ili apatiwe matibabu hapa Muhimbili ‘’ Amesema Dk. Juma.

  ‘’ Wenzetu wa Hospitali ya Amana wamemfanyia uchunguzi wa awali na wakatueleza shida yake kubwa ni kukosa nguvu na kushindwa kutembea hivyo tumemleta hapa Idara ya magonjwa ya Dharura na Ajali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Baada ya uchunguzi tutamuanzishia tiba haraka kwa kushirikiana na Idara zingine hapahapa MNH.’’ Amesema Dk. Juma.

  Kwa mujibu wa Dk. Juma kukosa lishe , mazingira magumu pamoja na umri kunasababisha mtu kupata magonjwa mbalimbali.

  0 0

  Na Daudi Manongi, MAELEZO DODOMA

  Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC) lililopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu imewataka wananchi kuitumia vyema mifuko 19 ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ili kujipatia mitaji yenye riba nafuu.

  Hayo yamesemwa leo Bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na Vijana Mhe.Anthony Mavunde wakati akijibu maswali mbalimbali ya wabunge leo Mjini Dodoma.

  “Serikali inawawezesha wananchi ili waweze kukopesheka kupitia Sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004 na Sheria ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi Na.6 ya mwaka 2004, Alisema Mhe.Mavunde.

  Amesema Sera hii imeainisha nia ya Serikali ya kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitaji kwa kuboresha vyanzo vya akiba na kuchukuwa hatua za kuondoa vikwazo mbalimbali ili kuwezesha mabenki kukopesha kikamilifu amana zilizopo kwa gharama nafuu,kupitia vikundi vidogo,SACCOS na Vicoba.

  Aidha kutokana na Sera hii Mipango, Miradi na Mifuko kadhaa imeanzishwa na Serikali ili kuwezesha wananchi kukopa kwa urahisi ambapo katika mifuko hiyo 19 baadhi yake ni pamoja na Mfuko wa kuendeleza wajasirimali wananchi,mfuko wa uwezeshaji wa mwananchi,mfuko wa pembejeo za kilimo,mfuko wa maendeleo ya vijana, mfuko wa dhamana za mikopo kwa wajasiriamali wadogo na wa kati,mfuko wa dhamana za mikopo kwa mauzo ya nje ya nchi ambapo hadi kufikia mwaka 2016 mifuko hii ilikuwa imetoa mikopo ya trilioni 1.7 kwa wajasiriamali 400,000.

  Pamoja na hayo Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa vyombo hivyo kuweza kutoa huduma kwa wananchi.

  “Serikali kupitia Benki kuu ya Tanzania kulingana na mazingira inaendelea kuangalia viwango vya riba kwa mabenki na Taasisi za fedha ili zimudu kupata fedha zaidi kwa ajili ya kukopesha wajasiriamali kwa riba ndogo,ambapo pia imechukua hatua ya kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo yake kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12 ”,Alisisitiza Mavunde.

  0 0

  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Umoja wa  Vijana wa Chama  Cha Mapinduzi (UVCMM), umenpongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk .John Pombe Magufuli kwa kuonesha Uzalendo mkubwa alionao kwa nchi yake,baada ya kuchukua maamuzi yenye maslahi ya nchi  katika sakata la zima la Makinikia.

  Hayo yamesemwa leo na Kaimu Katibu mkuu wa  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)  alipokuwa akitoa salamu za pongezi za Vijana wote katika  ukumbi wa CCM vIJANA kinondoni .

  Shaka amesema Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi unampongeza Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa  na uzalendo wa hali ya juu alionao kwa Taifa mara baada ya kuchukua maamuzi yenye masalhi ya nchi katika swala zima la Makinikia.

  Amesema Umoja wa Vijana wa CCM unaunga mkono maamuzi yote yaliyopitishwa au kutolewa na Rais Dk John Magufuli mara baada ya kupokea ripoti ya Tume ya Uchunguzi 

  “Umoja wa Vijana wa CCM hatuko tayari na hatutakubali kushuhudia tena Tanzania  ikirejea katika zama ya kiza kinene cha ukwapuaji mali,  ulaji, kufilisi mashirika ya umma au wizi wa mali za umma.tunaishauri serikali yetu iendelee na mikakati yake ya kuhakikisha ukwapuaji, ubabaishaji, wizi na ufisadi wa mali za serikali vinavikomeshwa mara moja 

        Amesema kuwa Umoja wa Vijana wa CCM unaiomba kwa dhati Serikali yetu ianze kuipitia upya mikataba yote ya madini ili kubaini kama ni yenye manufaa na maslahi mapana  kwa umma na kumuomba Rais Dk John Magufuli kuwaweka pembeni wasaidizi wake wote ambao bado wanaonekana kuwa na kigugumizi katika kuwatumikia wananchi huku baadhi yao wakiona muhali kupambana na ufisadi. 

         Ameweka wazi kuwa UVCCM Inasisitiza kuwa Watendaji wote waliokuwa na dhamana na ambao wamehusika kwa namna moja au nyingine kupoteza mapato na kulitia hasara Taifa, hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao haraka . 

  Amesema wao wanaishauri Serikali kuendelea kuwabaini na kuwachukulia hatua Viongozi na watendaji wa serikali ambao watabainika kumiliki mali, utajiri na vitega uchumi ambavyo havitokani na mapato yasiolingana na vipato vyao wataifishwe kama ilivyofanyika mwaka 1967 baada ya kutangazwa Azimio la Arusha .

  “Vijana wote tunaishauri serikali yetu isikubali na isiafiki  mali za umma zitumike kwa maslahi binafsi badala yake kila miliki ya serikali na mali ya umma ifahamike  kuwa kila mwananchi ana haki kufaidika nayo ambayo ni sehemu ya matunda ya Uhuru na Mapinduzi matukufu ya Zanzibar”.

  Alimaliza kwa kusema kuwa  Umoja wa Vijana wa CCM unawataka wana CCM na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais na Serikali yake katika mapambano dhidi ya vikundi vya rushwa, ufisadi na uzembe kwa baadhi ya watendaji  ili kuleta maendeleo endelevu katika taifa letu.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akizungumza na Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kumpongeza Rais John Pombe Magufuli kwa maamuzi aliyochukua.
   Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwa na Viongozi wa ngazi za juu wa umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM)
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akicheza muziki na baadhi ya wanachama wa UVCCM
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) Akiwa amebebwa juu  na Vijana wa CCM
  Sehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili  katika ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
   Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Shaka Hamdu Shaka (MNEC) akiwasili katika Ukumbi wa Umoja wa Vijana Kinondoni
   smsehemu ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)  wakiwa na furaha kubwa sana
   ehemu ya Vijana wa Hamasa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi  wakifurahi juu ya mamuzi yaliyochukuliwa na Rais John Pombe Mgufuli
   Mabango ya kumpongeza Rais Magufuli


  0 0

  Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2016/17 Yanga wametembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania  Mkoani Dodoma ikiwa ni katika ziara yao ya kuelekea Mkoani Arusha kwa ajili ya kulitembeza kombe.

  Yanga waliofanikiwa kulichukua kombe hilo kwa mara ya tatu mfululizo ikiwa ni mara ya 27 toka kuanz akwa Ligi Kuu Nchini, mabinhwa hao waliambatana namsafara wa viongozi ukiongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Mkemi pampja na benchi la Ufundi.
   Baadhi ya wabunge wakiwa wamelibeba kombe wakionekana kufurahi leo Mkoani  Dodoma.
  Baadhi ya wabunge, wachezaji na viongozi wa Yanga wakiwa katika picha ya pamoja leo Mkoani  Dodoma.

  0 0

   Mwenyekiti wa Bunge Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akiomba Bunge kutengua Kanuni zake na kuruhusu Bunge kuhairisha shughuli zake saa kumi na mbili jioni ili kuruhusu wabunge ambao ni waumini wa dini ya Kiislaamu kutimiza matakwa ya mfungo mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza Jumamosi.
    Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira na Kazi Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mhe. William Ole Nasha Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Prof Makame Mbarawa na Naibu wake Mhe.Edwin Ngonyani wakijadiliana jambo katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiwasilisha  Makadirio ya Maapto na Matumizi ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Mhe. Dkt Hussein Mwinyi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mbeya  Mhe. Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Rwekiza akiuliza swali katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge wa kuteuliwa Mhe. Abdallah Bulembo akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Arusha Mjini  Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
    Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medard Kalemani katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge wa Hanang Dkt Mary Nagu akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Mbunge wa Ileje Mhe.Janeth Zebedayo Mbene akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
   Timu ya Mpira ya Mbao FC kutoka Mwanza wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni, Mbao Fc wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa fainali za FA kati yao na Simba Fc zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi ya May 27, 2017.
   Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma.
   Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifurahia na mawaziri na wabunge mara baada ya kulileta kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bungeni Mjini Dodoma.
   Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.
  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.  

  Picha Zote na Raymomnd Mushumbusi Dodoma MAELEZO, DODOMA

  0 0


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

  Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako amewataka wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao kujiendeleza zaidi ili kuweza kutimiza ndoto zao pamoja na kuwapongeza Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa juhudi kubwa wanazozifanya.

  Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) yaliweza kuhitimishwa leo kwa wahitimu 33 kutunukiwa vyeti na Waziri Prof Ndalichako.

  Akizungumza kabla ya utoaji wa vyeti kwa wahitimu Prof Ndalichako alisema kuwa ana imani kubwa kuwa mafunzo waliyoyapata kutoka kwa wakufunzi wao watayatumia vizuri zaidi ni kutaka kuwaona wakiwa wamefika mbali zaidi.

  "Programu hii kwangu ni fursa kwenu na mafunzo haya mkiyatumia vizuri yatawasaidia kuendesha maisha katika nyanja mbalimbali kazini, nyumbani, kwenye jamii na kwa kizazi chetu Kijacho," amesema Prof Ndalichako.

  Kwa upande wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mkurugenzi Dkt Aggrey Mlimuka alisema kuwa ATE kupitia mpango huo wameweza kutoa mafunzi kwa wafanyakazi wa kike 33 kutoka makampuni 17 nchini.

  "Tumetoa elimu hii tukishirikiana na chuo cha Mafunzo ya Uongozi Afrika Mashariki na Kusini (ESAMI) kwa wafanyakazi wa kike 33 kutika makampuni 17 ambayi yamefadhili mafunzo haya,"amesema Mlimuka.

  Amesema na mchanganyiko huu wa wakufunzi umechochea mazingira bora ya kujifunza na kuendeleza viongozi kwa maendeleo ya makampuni na mafunzo hayo hutoa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mahali pa kazina katika maisha yao kwa kushirikiana na ESAMI.
  Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa kutoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO) na kuwapongeza kwa juhudi kubwa wanazozitumia katika kuwainua wanawake kimaendeleo.
    Mkurugenzi wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dkt Aggrey Mlimuka akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali ya mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).
   
   Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar akizungumza na wahitimu kabla ya kupatiwa vyeti hivyo kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO).
   Wakurugnezi kutoka mashirika na kampuni mbalimbali wakitoa ushuhuda wa  namna walivyoanza mpaka walipo sasa, anayezungumza wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Benki ya Barclays Abdi Mohamed.
  Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako akiwa anatoa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao ulioratibiwa na chama hicho pamoja na Shirikisho la Vyama vya waajiri Nchini Norway (NHO), kushoto Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Waajiri (ATE) Almas Maige,  Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani kwa Nchi za Afrika Mashariki Mary Kawar.

  Wahitimu wa  mafunzo ya programu ya mwanamke wa wakati ujao wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi Stadi Prof Joyce Ndalichako.

  0 0


  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Kesi dhidi ya mfanyabiashara, Ndama Shabani Hussein maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto ya Ng'ombe imeamliwa kuendelea kusikilizwa baada ya mshtakiwa huyo kukana baadhi ya maelezo ya awali (PH), licha ya mwanzoni mwa wiki hii kukubali shtaka la utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 540,000.

  Mapema wiki hii, Ndama alikiri kutenda kosa hilo ambalo ni kosa la sita kati ya anayoshtakiwa nayo, na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikapanga leo iwe siku ya kusomewa maelezo ya awali (PH), kabla ya kumsomea hukumu yake.

  Hata hivyo, wakati akisomwa Maelezo hayo na wakili wa serikali Christopher Msigwa Ndama alikana baadhi ya tuhuma na kukiri chache kitendo kilichofanya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Victoria Nongwa kuamuru kesi hiyo iendelee kama kawaida kwani tuhuma alizokataa mshtakiwa ndizo zinajenga msingi wa kesi.

  Ndama anayetetewa na Wakili Jeremiah Mtobesya alikiri baadhi ya maelezo ya awali aliyosomewa na wakili wa Serikali Msigwa ikiwamo nyaraka zilizotumika kufungua akaunti iliyotumika kuingizwa hizo fedha, hundi zilizotumika kutolea hizo fedha, maelezo ya benki ‘bank statement’ na Swift massage.

  Hata hivyo alikana baadhi ya maelezo ambayo ni sehemu ya kuunda shtaka hilo, na kusema kuwa hawajui wakurugenzi wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited wanaotambulika Brela, Bushoboka Mutamura na Mujibu Hamis Taratibu.

  Aidha alikanusha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited haikuwahi kuingia mkataba na Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited  na kwamba hakuwahi kuwagaia wabia wenzake fedha hizo taslimu kwa lengo la kuficha chanzo chake.

  Baada ya mshtakiwa kukana baadhi ya PH Msigwa alidai mahakamani hapo kuwa kwa kuwa mshtakiwa alikuwa amekiri kosa ni rahisi kuthibitisha yaliyofanyika na kwamba kwa kadiri maelezo ya awali yalivyosomwa na majibu ya mshtakiwa basi ni jukumu la mahakama kuangalia kama maelezo aliyokubali yanakidhi kumtia hatiani ama kesi ianze kusikilizwa.

  “Ili haki ionekane imetendeka na kwa vile mshtakiwa anakubali baadhi ya maelezo na mengine ameyakataa mahakama inaona ni vema kesi ianze kusikilizwa ili kila upande upate haki yake kwani mshtakiwa alitakiwa akubali shtaka hili bila ya kupinga lakini kwa kuwa amekana baadhi ya tuhuma ni wazi kuwa amekana shtaka”, amesema Hakimu Nongwa.

  Baada ya kutolewa kwa amri hiyo, Msigwa ameiambia mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi itatajwa tena Juni 6, mwaka huu.

  Mei 16, 2017, Ndama alikubali shtaka la sita la kutakatisha fedha ambapo anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 2014, Dar es Salaam, akiwa mwenyekiti na mtia saini pekee wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko kwenye  benki ya Stanbic alijihusisha moja kwa moja kwenye uhamishaji wa dola za Marekani 540,000 na kuzitoa huku akijua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kujiapatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  Mashtaka mengine anayokabiliwa nayo ni kughushi na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akipiga ngoma kuashiria uzinduzi rasmi wa Tigo 4G LTE mkoani Singida anayefuatia kulia kwake ni kamanda wa polisi mkoa wa Singida na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata na mwishoni ni Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Mjini Singinda Mapema jana.


  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akihutubia wageni waalikwa kwenye uzinduzi wa Tigo 4g LTE zilizofanyika jana mkoani singida ambapo sasa 4G LTE imeweza kufika mikoa 23
  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akimkabidhi zawadi ya simu Mama Bora mkazi wa Singida mjini.mara baada ya kujishindia zawadi katika hafla ya uzinduzi wa Tigo 4G LTE katika mkoa wa Singida iliyofanyika hapo jana
  Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo (anayefuatia kushoto kwake) na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugatana mwisho ni kamanda wa polisi wa mkoa wa Singida kulia kwake ni wateja waliojishindia zawadi kutoka tigo na mwishoni ni mtalam wa mitandao ya kijamii kutoka Tigo Samira Baamar katika hafla ya uzinduzi wa Tigo 4G LTE mapema jana mkoani Singida.
  Wafanyakazi wa Tigo wakiwa tayari kuhudumia wateja wa Mkoa wa Singida mara baada ya uzinduzi wa Tigo 4G LTE
  Mteja akiangalia simu zenye uwezo wa 4G LTE


  Singida, Mei 22, 2017-Wateja wa Tigo mkoani Singida hivi sasa wanaweza kufurahia kuunganishwa na huduma ya intaneti ya kasi kufuatia kampuni hiyo kupanua huduma yake ya 4G LTE katika mji huo uliopo katikati ya Tanzania. Teknolojia ya 4G ina takribani kasi ya mara tano zaidi ya teknolojia ya 3G ambayo inapatikana hivi sasa katika soko.

  Kwa mujibu wa Meneja wa Tigo Kanda ya Kaskazini Aidan Komba ni kwamba upanuzi wa huduma hiyo unafuatia mafanikio yaliyopatikana baada ya kuizindua katika mji mingine mikubwa nchini.

  Komba alisema kwa kuifanya huduma ya 4G kupatikana Singida, “Tigo kwa mara nyingine tena imeonesha kujikita kwake katika kuboresha mabadiliko katika mtindo wa maisha ya kidijitali na inavyoongoza katika kutoa teknolojia ya kisasa na ubunifu katika soko hili.”

  Alitangaza kuanza kwa enzi mpya za kidijitali katika historia ya mawasiliano ndani ya Singida akibainisha kwamba Tigo 4G LTE itahakikisha kunakuwepo uwezo mkubwa na muhimu katika kuwaunganisha wateja ndani ya mkoa huo.

  “Singida ni kituo muhimu kibiashara kwa mikoa ya kati na kaskazini mwa Tanzania. Tunaamini kwamba wakazi wa Singida, jumuiya ya kibiashara na wadau wataufurahia huduma Tigo 4G LTE na hivyo kuzifanya shughuli zao kwa njia ya mtandao kuwa rahisi zaidi.”

  “Mawasiliano ya simu ni nguzo muhimu kwa jamii iliyoendelea. Kwa hiyo mtandao wa 4G utachangia katika maendeleo ya sekta mbalimbali zikiwemo elimu, fedha na huduma za afya na hali kadhalika kukuza uchumi na biashara”, alisema Komba.

  “Kama mnavyojua, Tigo imekuwa mstari wa mbele katika kuzisaidia jamii zinazotuzunguka, na mfano mzuri ukiwa ni uchimbaji wa visima 12 ambavyo tulivitoa kama msaada kwa vijiji vya Singida mwaka jana,” Komba alibainisha.

  Aliongeza kwamba gharama ya vifurushi vya 4G LTE ni sawa na ile ya vifurushi vya 3G na kufafanua kuwa wateja wanachotakiwa ni kuwa na kifaa kinachowezesha 4G LTE ama simu ya kisasa (Smartphone) au modemu ikiwa na kadi ya simu ya 4G LTE ili kuwawezesha kupata muunganisho na 4G LTE. Alieleza kuwa wateja wanaweza kubadilisha au kununua kadi ya simu ya 4G LTE kutoka katika duka la Tigo la huduma kwa wateja lililopo Singida Mjini.

  Akizungumzia uwekezaji katika mtandao, Komba alisema kwamba Tigo imewekeza kwa kiwango kikubwa katika miundombinu ya kisasa, ikilenga kusaidia katika maendeleo endelevu ndani ya mkoa.

  Alihitimisha kwa kusema, “Mipango imo njiani katika kupanua huduma kwa ajili ya mikoa iliyobakia ili hatimaye kuisambaza nchi nzima.”
  Kwa upande wake, Meneja wa mkoa wa Singida wa kampuni ya Tigo, Raymond Royer alibainisha umuhimu wa huduma ya 4G na mchango wake katika kuboresha huduma za uwanda mpana wa simu za mkononi.

  Royer alisema, “Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo ongezeko kubwa la idadi ya wateja pamoja na matumizi ya data; simu za kisasa idadi yake imeongezeka kwa asilimia 90 na hivyo kubadilisha namna tunavyowasiliana.”

  Aliongeza, “Kwa hiyo teknolojia ya Tigo 4G LTE inampatia mteja faida mbili za data zilizo na kasi kubwa na kupunguza ucheleweshaji. Ni nguvu ya mabadiliko ambayo itaboresha mtindo wa maisha ya kidijitali kwa wateja wetu.”

  Mtandao wa 4G LTE unamaanisha kasi kubwa katika kurambaza (Surf) na kupakua mada kutoka katika intaneti na kupiga miito ya mawasiliano ya kuonana (Skype). Kwa kiwango kikubwa inaboresha uzoefu wa wateja katika kutiririsha video au kufanya mikutano. Hali kadhalika inaweza kuhifadhi zana nyingi kama vile mkutano wa video, muonekanao wa hali ya juu, blogu za video, michezo na kutiririsha video kutoka katika mitandao ya kijamii.

  0 0

  Baadhi ya Ndugu Jamaa na Marafiki wakiwa wamebeba Jeneza lenye mwili wa aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kigamboni na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Mzee Kitwana Kondo wakielekea kwenye maziko,leo Alhamisi baada ya swala alasiri katika makaburi ya Tambaza jijini Dar es Salaam.
  Mazishi ya aliyekuwa Meya wa Dar es salaam Mzee Kitwana Kondo jioni hii makaburi ya Tambaza jijini Dar.
  Mwili wa Marehemu Mzee Kitwana Kondo ukiingizwa msikitini kwa ajili ya kuswaliwa tayari kwa mazishi jioni ya leo ,katika Makaburi ya tambaza,jijini Dar.
  Ndugu jamaa na marafiki wakiwa Makaburi wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu kwa ajili ya Maziko katika Makaburi ya Tambaza,jijini Dar 


  0 0

  Mei 25 kila mwaka Mataifa mbalimbali Barani Afrika huadhimisha Siku ya Afrika kama sehemu ya mataifa hayo kukumbuka ukombozi wake barani Afrika.

  Jijini Mwanza, watengenezaji na wauzaji wa vitu vya kitamaduni wamewataka watanzania kuongeza kasi ya matumizi ya vitu hivyo badala ya kutegemea vitu kutoka mataifa ya Maghabiri.
  #BMGHabari
  Kulia ni Mzee Francis Gabriel pamoja na Bi.Salome Babae ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa za asili wakiwa kwenye eneo lao la biashara. Wanapatikana eneo la darajani Jijini Mwanza. Mawasiliano yao ni 0783 83 83 73
  George Binagi-GB Pazzo.

  Watanzania wameshauriwa kupenda kutumia bidhaa za asili ikiwemo mavazi na urembo ili kuondoakana na utumwa wa kutovipa thamani vitu hivyo.

  Wauzaji wa vitu vya asili katika eneo la darajani jijini mwanza, wayasema hayo wakati wakizungumza na lake fm kuhusiana na maadhimisho ya siku ya afrika hii leo.

  Maadhimisho ya siku ya afrika yalianza kuadhimishwa tangu mei 25 mwaka 1963 yakilenga kuyahamasisha mataifa ya bara la afrika kujikomboa kutoka utumwani hususani kiakiri na kifira ili kuthamini zaidi tamaduni za kiafrika.

  0 0

  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakiwa kwenye Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
  Waheshimiwa Madiwani wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo (Kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo (Kulia) wakisoma muongozo wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam

  Viongozi wa Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo wakiwasili katika Ukumbi wa Mikutano uliopo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kikao cha Baraza la Madiwan Jumatano Mei 24, 2017
  Waheshimiwa Madiwani wakijadili jambo wakati wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
  Afisa Utumishi Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Ndg Ally Juma Ally akifatilia kwa makini kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 kwenye ukumbi wa mikutano leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja kwenye ukumbi wa mkutano wa Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akipitia muongozo wa Kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Tatu Mwaka 2016/2017 leo Jumatano Mei 24, 2017 katika ukumbi wa Mikutano uliopo Makao makuu ya Manispaa ya Ubungo Mtaa wa Kibamba Chama Jijini Dar es salaam

  Na Mathias Canal, Dar es salaam
  Baraza la Madiwani Manispaa ya Ubungo kwa kauli moja limeridhia na kuagiza Idara ya Mipangomiji na Mazingira kufuatilia na kutwaa maeneo kwa ajili ya matumizi ya Umma hususani maeneo ya Shule.

  Aidha Baraza la madiwani limeagiza Idara hiyo ya Mipango Miji kutembelea na kupima eneo la shule ya Sekondari Matosa iliyopo Kata ya Goba ambalo eneo lake limesalia ekari 31 kati ya 22 huku eneo jingine likitumiwa na wananchi kinyume na utaratibu.

  Pia imebainika kuwa hali ya ukusanyaji mapato inaendelea kukua kutokana na juhudi na utekelezaji wa mikakati mbalimbali ya kuongeza mapato tangu kuanza kwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo baada ya mgawanyo wa Halmashauri hiyo kutoka Manispaa Mama ya kinondoni.

  Akijibu swali lililoulizwa kuhusu ubovu wa mashine za kukusanyia mapato POS Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alisema kuwa hajawahi kupokea malalamiko juu ya mashine hizo na kubainisha kuwa Manispaa imepata mtaalamu anayeshughulikia mashine hizo ambapo atatoa taarifa juu ya kiasi kilichokusanywa tangu kuanza kutumika kwa mashine hizo za POS.

  Akiongelea kuhusu semina kwa madiwani MD Kayombo alikiri kuwa kuna umuhimu wa madiwani kupata semina hususani kwenye eneo la kanuni na sheria mbalimbali na pia katika sheria za manunuzi hivyo ameahidi kuandaa semina hiyo ili waweze kuelimika zaidi.

  MD Kayombo akizungumzia suala la maendeleo ya jumla katika kuboresha miundo mbinu katika shule za Manispaa ya Ubungo alisema kuwa zitakuwa zikifanyika hatua kwa hatua katika kuhakikisha miundo mbinu inaboreshwa huku akibainisha kuwa katika kuinua elimu katika Shule za Manispaa ya Ubungo ujenzi wa Madarasa, Vyoo sambamba na Ukuta vitaanza kujengwa hivi karibuni katika shule ya Msingi Ubungo Plaza.

  Kuhusu hoja ya malalamiko ya kodi ya Service Levy ambayo Manispaa ya Ubungo  imekuwa ikifuatilia wafanyabiashara walipo kuhakikisha wanalipa kodi aliwataka madiwani kutambua kwamba hakuna mfanyabiashara anayependa kuona analipa kodi hivyo sio rahisi kutokuwa na malalamiko pale wanapolazimishwa kulipa kodi.

  Alisema kuwa Manispaa imefanya juhudi kubwa kuwaelimisha juu ya kodi hiyo huku akiahidi kuendelea kuwaelimisha kutokana na wao kutoielewa vizuri kodi hiyo.

  Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jackobo alisisitiza umuhimu wa semina kwa madiwani huku akitilia mkazo ulipaji wa kodi.

  Alisema Ubungo ina idadi kubwa ya watu hivyo inapelekea kuwepo kwa idadi kubwa pia ya wafanya biashara hivyo kwa asilimia kubwa pato la Manispaa linatoka kwa wafanyabishara zaidi.

  Akizungumzia mchakato mmojawapo katika kuongeza mapato alisema tayari mkurugenzi ameeleza kuandaa sheria ndogo ndogo za Manispaa zitakazosaidia katika ukusanyaji wa mapata na kuongeza pato la Manispaa hivyo aliwataka waheshimiwa madiwani kuunga mkono juhudi hizo za ukusanyaji kodi ili kuleta maendeleo.

  Baraza hili la madiwani la Robo ya tatu lilikuwa na agenda takribani nane ambapo ikiwemo kuthibitisha taarifa za utekelezaji wa kazi za kamati za kudumu za Halmashauri.

  Pamoja na hayo baraza lilikuwa na agenda ya kupokea taarifa kama vile taarifa ya wenye vyeti feki kwa manispaa ya Ubungo, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo robo ya tatu kipindi cha Januari hadi Machi 2017 na taarifa ya utendaji kazi na uwajibikaji wa Halmashauri.

  0 0

  Na. Eliphace Marwa - Maelezo.

  RAIS Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ameongoza mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika maziko ya mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Kitwana Kondo.

  Mbali na Mwinyi wengine waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Tambaza ni Makamu wa Rais Mstaafu, Mohammed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu Wastaafu, Salim Ahmed Salim na Edward Lowassa, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na wengine.

  Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Mzee Mwinyi alisema, marehemu Kondo alikuwa  ni mtu ambaye alijitoa katika kulitumikia taifa kwa moyo wake, hivyo mchango wake ni mkubwa katika kulitumikia taifa na hasa wakazi wa jiji la Dar Es Salaam.

  "Alikuwa ni rafiki yangu ambaye tumefahamiana kwa muda mrefu sana, tumepoteza mtu muhimu sana, lakini kazi ya Mungu haina makosa, tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi," alisema Mzee Mwinyi

  Kwa upande wake, Kinana alisema, taifa na hasa wakazi wa Dar es Salaan wamepata pigo kubwa kwa kumpoteza mzee huyo ambaye bado busara zake zilikuwa zikihitajika.

  "Alikuwa ni kiongozi wa jamii,alikuwa ni mwalimu wa watu wengi katika manbi mbalimbali, ni msiba mkubwa lakini nj kazi ya Mungu, tuendelee kumuombea apumzike kwa amani," alisema Kinana.

  Naye, Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa alisema, kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mzee Kondo ni vema uongoziu wa jiji kuangalia namna ambavyo barabara moja ya jiji hilo likapewa jina la KK ikiwa ni kuheshimu na kutambua mchango wake.

  "Namuomba Mstahiki Meya, barabara moja uiite KK, itakuwa ni heshima kumuenzi Mzee Kitwana Kondo kwa kazi kubwa aliyofanya wakati wa uhai wake," alisema Lowassa.

  Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) , Profesa Ibrahim Lipumba alisema, mchango wa Mzee katika taifa ni mkubwa lakini kwa bahati mbaya ni kama jmeshindwa kutambuliwa.

  "Ni mtu ambaye bahati mbaya sana historia ya nchi yetu haitambui mchango wake katika kuleta uhuru wa nchii na kudumisha uhuru wa nchii," alisema Profesa Lipumba.

  Akieleza chanzo cha kifo cha baba yake, mtoto wa kwanza wa marehemu Mzee Kondo, Stara Kondo alisema, Baba yake alilazwa katika hospitali ya Hindu Mandal Mei 18 kutokana na kuugua muda mrefu lakini alifariki juzi.

  “Alikuwa anaumwa muda mrefu lakini hadi anafariki madaktari walisema alipata stroke (Kiharusi) na shinikizo la damu, tutamkumbuka kwa mambo mengi kwa sababu ni baba lakini alikuwa ni kichwa cha familia,” alisema Stara 
   Jeneza lilobeba mwili wa Marehemu Kitwana Kondo likiwa limebebwa kuelekea katika msikiti wa Tambaza uliopo upanga jjini Dar es Salaam tayari kwa kufanyiwa ibada.Picha Emmauel Massaka,Globu ya jamii 
   Mwili wa aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo ukiwa ukiwa umeingizwa kwenye kaburi tayari kwa ajili ya maziko katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
   Rais Mstaafu wa awamu ya pili Dkt. Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
   Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
   Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombare Mwilu akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.
  Jaji Mstaafu Mark Bomani akiweka udongo katika kaburi la aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Kitwana Kondo katika makaburi ya Tambaza yaliyopo Upanga jijini Dar es Salaam.

  Baadhi ya wananchi walioshiriki mazishi ya aliyekuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam na Mbunge wa Kigamboni Mzee Kitwana Kondo wakiweka udongo wakati wa mazishi mapema leo jioni jijini Dar es Salaam.

  Picha Emmauel Massaka,Globu ya jamii

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
  Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisalimiana na Ally Khamisi Mvugalo mara baada ya kuwasili katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam kwa ziara ya kikazi. Leo Mei 25, 2017
  Moja ya Majengo yaliyochakaa Shule ya Msingi Kawawa Iliyopo katika Kata ya Mabibo Manispaa ya Ubungo
  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017
  Wazazi na Walimu wa Shule ya Msingi Kawawa wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori

  Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema akizungumza kabla ya kumkaribisha MKuu wa Wilaya Mhe Kisare Makori kuzungumza na wazazi na walimu wa Shule ya Msingi Kawawa.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Ndg Badi Ahmed Darusi akisoma Taarifa ya shule ya Msingi Kawawa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori akisisitiza jambo wakati akizungumza na walimu pamoja na wazazi katika Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam. Leo Mei 25, 2017

  Na Mathias Canal, Dar es salaam

  Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Matiku Makori Leo Mei 25, 2017 amefanya ziara ya kutembelea Shule ya Msingi Kawawa iliyopo Katika Kata ya Mabibo Jijini Dar es salaam.

  Ziara hiyo ilikuwa na dhamira ya kubaini na kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo hususani changamoto ya Upungufu wa Madarasa na Vyoo kwa ajili ya Walimu na Wanafunzi wa shule hiyo.

  Katika ziara hiyo ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo imehudhuriwa pia na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo, Afisa Tarafa ya Kibamba, Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Ubungo, Diwani wa Kata ya Mabibo, Mtendaji Kata ya Mabibo, Wenyeviti na Watendaji wa Mitaa, Uongozi wa vyama vya siasa, Kamati ya Shule, Walimu sambamba na Wazazi.

  Katika ziara hiyo Mhe Makori amefikia uamuzi wa kuchangia Shilingi Milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyoo vya shule kutokana na ubovu wa vyoo vilivyopo huku akiwasihi wananchi kwa ujumla kujitokeza kuchangia ujenzi wa vyoo hivyo.

  Aidha ameahidi kuanzisha Harambee mahususi kwa ajili ya kuchangia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa kwani yaliyopo ni Madarasa 22 Kati ya Madarasa 68 hivyo kuna upungufu wa madarasa 46.

  Kwa upande wa Matundu ya vyoo alisema kuwa upungufu ni mkubwa kwani yanahitajika matundu 136 na matundu ya vyoo yaliyopo ni 26 pekee hivyo kuna upungufu wa matundu 110.

  Mhe Makori amewasihi wazazi kushirikiana na walimu kufuatilia taarifa za wanafunzi kwani kufanya hivyo kutaongeza ufanisi wa wanafunzi hivyo kuifanya shule hiyo kuwa na ufaulu wa kiwango kikubwa.

  Katika ziara hiyo Mara baada ya Mkuu wa Wilaya kuchangia Shilingi Milioni moja pia Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema alichangia mifuko nane ya Saruji, Kamati ya Shule Mifuko 10 ya saruji huku Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kata ya Mabibo ukichangia jumla ya shilingi 200,000.

  Mhe Makori alisema kuwa katika kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wanaojiandikisha kujiunga na darasa la kwanza kutokana na serikali kuwapunguzia wazazi jukumu la kulipa ada.

  Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mabibo Mhe Kassim Lema amempongeza Mkuu wa Wilaya kwa kufanya ziara katika shule hiyo Jambo ambalo limeibua hisia za mwanzo wa ujenzi wa madarasa sambamba na ujenzi wa vyoo vya kisasa.

  Sawia na hilo pia amempongeza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo kwa kutekeleza maagizo yanayotolewa na Mkuu wa Wilaya jambo ambalo anasema kuwa litapelekea kuwa na Maendeleo katika Wilaya ya Ubungo.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Ndg Badi Ahmed Darusi akisoma Taarifa ya shule alizitaja changamoto mbalimbali zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na Uhaba wa Samani, Upungufu wa walimu sawia na ukosefu wa fedha kwa ajili ya malipo ya Mlinzi.

  Shule ya Msingi Kawawa ambayo zamani ilikuwa ikiitwa Uwanjani ilianzishwa rasmi Januari 7, 1978 ambapo ilianza na madarasa mawili na ilijengwa kwa miti ikiwa na wanafunzi 60.

  Shule hiyo inafanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba kwani kwa Takwimu za tangu mwaka 2012 Hadi 2016 haijawahi kushuka katika ufaulu chini ya asilimia 73.

  Imetolewa Na;
  Ofisi ya Mkuu wa Wilaya

  0 0


  0 0


  0 0

   Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akizindua mpango wa gharama nafuu utakao wahudumia watu wote waliojiunga na mfuko huo
  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akifungua mkutano mkuu wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF uliofanyika leo jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau wa mfuko(Picha na Pamela Mollel).
   Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Richard Kwitega akiongea katika mkutano huo akimuakilisha mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,katika risala yake alisema kuwa anaipongeza mfuko huo kwa makubaliano waliofikia na UTT-MFI wa kutoa mikopo nafuu kwa wanachama wake wajasiriamali
   Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Daud Msangi akizungumza katika mkutano huo wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya kustaafu wa GEPF
   Mwenyekiti wa bodi ya GEPF Joyce Shaidi akizungumza katika mkutano huo ambapo amesema kuwa kauli mbiu ya mkutano huo ni "Hifadhi ya jamii kwa wote inawezekana katika uchumi wa viwanda"kauli mbiu hii imewekwa maksudi na kumuunga mkono Rais katika kujenga uchumi wa viwanda

  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Daud Msangi katika mkutano huo
  Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Dr.Ashatu Kijaji akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa mfuko huo wa GEPF jijini Arusha
  Kulia ni mtendaji mkuu wa UTT James WAshima akizungumza katika mkutano huo pembeni ni Mkurugenzi mkuu wa GEPF Daud Msangi
  Wadau katika mkutano wakifatilia mada mbalimbali
  Mnufaika wa fao la elimu Joseph Mwashimaha akizungumza namna alivyonufaika na mfuko huo wa GEPF
  Mtendaji mkuu Benki ya Posta Sabasaba Moshingi akitoa neno la shukrani katika mkutano huo

older | 1 | .... | 1245 | 1246 | (Page 1247) | 1248 | 1249 | .... | 1898 | newer