Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1243 | 1244 | (Page 1245) | 1246 | 1247 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akiwaonesha shamba la mfano la mahindi ambalo lipo nje ya ofisi yake wataalamu hao wa kilimo pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
  Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akionesha shamba la mfano la alizeti ambalo lipo nje ya ofisi yake. Kushoto ni Mratibu wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
  Zao la alizeti likioneshwa.
  Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF, Suleiman Okoth (wa nne kutoka kulia), akiwa na wataalamu hao wakilimo wakati wakiangalia bwawa la samaki la mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.
  Ofisa Uvuvi wa Mkoa wa Geita, Tito Mlelwa akiwa mbele ya bwala la samaki la mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa huo huo wakati akizungumza na wanahabari.
  Jengo la Ofisi la Halmshauri ya Wilaya ya Chato linavyoonekana.
  Maofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato wakiwa kwenye mafunzo ya kilimo chenye tija.
  Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila (kulia) akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
  Maofisa Ugani wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
  Maofisa Ugani wakiandika wakati wa mafunzo hayo.
  Mafunzo yakiendelea.
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Martin Ndilanha (kulia), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
  Mafunzo yakiendelea. Kutoka kulia ni Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF, Suleiman Okoth, Ofisa Ugani wa Wilaya ya Chato, Charles Ntaki na Mratibu wa OFAB Tanzania, Philbert Nyinondi.
  Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Elias Makory akifungua mafunzo hayo.
  Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo. 
  Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa mada katika mafunzo hayo.

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.
  Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba kabla ya kuanza ziara ya mafunzo hayo.

  Na Dotto Mwaibale, Chato

  MAOFISA Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wameombwa kuwa weredi zaidi katika masuala ya kilimo ili elimu waliyonayo waweze kuitoa kwa wakulima ili nao waweze kulima kilimo chenye tija cha zao la mihogo ili zao hilo liweze kukubalika katika soko la kimataifa.

  Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon wakati akitoa mafunzo kwa maofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi ya Teknolojia (Costech) kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

  Alisema hivi sasa nchi ya China na Tanzania zimesaini mkataba wa ununuzi wa zao la muhogo jambo ambalo ni fursa kwa wakulima wetu wa hapa nchini wakiwemo wa kutoka wilaya ya Chato.

  "Hii ni fursa kubwa kiuchumi lakini ni vema sasa tukaingia katika kilimo chenye tija ili mihogo yetu iweze kuingia katika soko la kimataifa badala ya kuendelea na kilimo kisicho na tija" alisema Simon.

  Katika kuonyesha kuwa swala la kilimo na shuguli za ugani ni muhimu katika kusaidia kuboresha kilimo na kuongeza tija kwa wakulima katibu tawala wa mkoa wa Geita, Selestine Gesimba ameanzisha mashamba darasa ya mfano ya mazao mbalimbali nje ya ofisi yake.

  Amesema lengo la kufanya hivyo nje ya ofisi yake ni kuonyesha kwa vitendo dhana nzima ya ugani kwani anaamini mkulima anaamini akiona kwa macho yake kuliko kusikia.

  Hata hivyo amesema kila halmashauri itatakiwa kuwa na mashamba madogo ya mfano kwenye ofisi zao kuonyesha kilimo bora cha mazao muhimu kwenye wilaya pamoja na ufugaji bora wa mifugo na samaki.

  Katibu tawala huyo wa mkoa wa Geita amesema kwa kufanya hivyo kuanzia mkoani wilayani na kwenye kata na vijiji kwa kusimamiwa na wataalamu wa mazao na mifugo wakulima watajifunza na tija itaonekana.

  Nje ya ofisi hiyo ya katibu tawala wa mkoa na mkuu wa mkoa wa Geita wameweka vishamba vidogo vya mahindi, Alizeti, Maharage pamoja na bwawa la kufugia samaki ambalo wananchi watakwenda kujifunza lakini wanajiandaa kuweka na mifugo mingine kama ng'ombe,kuku na mifugo mingine.

  Akiwasilisha mada yake juu ya kilimo bora cha zao la pamba mtafiti na mtaalamu wa magonjwa ya mazao kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Ukiliguru Stellah Chirimi amewataka maafisa Ugani hao kushauri wakulima kila mtu kuwa na ekari moja ya Pamba iliyolimwa na kuhudumiwa kisasa ili kupata tija.

  Amesema wakulima wengi hawazingatii kilimo bora cha kupanda kwa mstari ili kuwa na idadi inayotakiwa ya miche kwenye shamba na kujikuta wanalima ekari nyingi ambazo hazina matunzo kabisa hali ambayo inawapekea kupata mavuno yasiyo na tija.

  Amesisitiza umuhimu wa kila Ofisa Ugani kuwa na mashamba madogo ya mfano kwenye kata zao ambayo wakulima watakwenda kuona na kujifuza kuliko kutumia mashamba ya wakulima pekee.

  0 0

  Serikali imeitaka Bodi ya Chuo Cha Bahari Dar es Salaam (DMI), kuhakikisha inaboresha miundombinu ya chuo na kuzingatia miiko na kanuni za ufundishaji ili wanafunzi wanaohitimu chuoni hapo waweze kukidhi mahitaji ya soko.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akizindua bodi hiyo na kusisitiza kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha majengo kwa kutangaza zabuni kwa uwazi ili kuepuka mianya ya rushwa.

  “Hakikisheni mnakuwa na mpango madubuti wa kuboresha majengo ya chuo ili chuo kibaki na hadhi yake, lakini pia hakikisheni mntoa elimu bora kwa wanafunzi wanaokuja kusoma hapa ili waweze kupata misingi imara itakayowawezesha kuajiriwa ndani na nje ya nchi mara baada ya kuhitimu masomo yao”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.

  Ameongeza kuwa Serikali ina uhitaji wa wataalam wengi kwenye masuala ya bahari hivyo ni wajibu wa bodi kusimamia chuo na kuhakikisha wataalam hao wanazalishwa kwa wingi chuoni hapo ili kukidhi mahitaji ya soko kitaifa na kimataifa.

  Amewataka wakufunzi wa chuo hicho kuhakikisha wanatumia lugha nzuri kwenye ufundishaji ili kuwaweka wanafunzi karibu na kuhakikisha wanapata taaluma inayotakiwa kwani kuwepo kwa waalimu hao kunategemea kuwepo kwa wanafunzi.

  “Ni lazima tufungue milango kwa wanafunzi sababu wapo wanaoelewa haraka na wanaoelewa taratibu, hivyo tukae nao muda mrefu ili kubaini changamoto zao lakini pia tuwe waangalifu juu ya matumizi ya lugha tunazotumia kwa wanafunzi wakati tunapofundisha”, amefafanua Prof. Mbarawa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya DMI, Kapteni Ernest Bupamba, amemuahidi Waziri huyo kuwa watafanya kazi ya kusimamia chuo hicho kwa juhudi zote na kwa maarifa yote ili chuo kizalishe wataalam wenye sifa kwenye sekta ya uchukuzi,

  “Naahidi kushirikiana vyema na Wajumbe wezangu wa bodi, Menejimenti ya Chuo na watumishi katika utekelezaji wa majukumu ili kuleta tija’ amesisitiza Kapteni Bupamba.

  Aidha, Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Erick Massami amemuomba Waziri Mbarawa kukisaidia chuo hicho kuanza kutumia fedha za mfuko wa Usafirishaji ambazo zimekusanywa tangu mwaka 2013 bila kutumika ili fedha hizo zitumike kuzalisha wataalam wengi katika sekta ya usafiri wa majini.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amezindua bodi ya chuo ambayo iko chini ya uenyekiti wa Kapteni Ernest Bupamba na wajumbe wanne ambao ni Kapteni Andrew Matilya, Dkt. Mwamini Tulli, Bi Tumaini Silaa na Eng. Alfred Waryana.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

  0 0


  BancABC has been announced as the Best Emerging Bank in Tanzania for the year 2017. The bank won the award during The Banker Africa – East Africa Awards 2017 which were held in Nairobi last week.

  Speaking during the event which was held at Kenya’s capital crown plaza, Robin Amlot who is the CEO of CPI Financial, the organizers of the Awards, said that the annual Banker Africa Awards are continent – wide programmes open to all banks and financial institutions in Africa. ‘The aim of this award is to recognize outstanding performance and excellence in the financial services industry’, said Amlot.

  To his part, BancABC Managing Director Dana Botha said that winning the award has proven the bank’s commitment which is fully aligned to our vision to be the premier financial service institution in sub – Saharan Africa and to obtain top 5 market position in countries of operation.
  ‘We have always been working hard to achieve better results and would like to thank our customers who voted for us. BancABC which is part of Atlas Mara has been named in the 2017 Banker Africa, East Africa Awards as the Best Emerging Bank in Tanzania. The results are based on nominations and votes from the Bankers’ subscribers. It has been our objective for the bank to have awards whilst we fix our value propositions for excellence’, said Botha.
  BancABC wins Best Emerging Bank in Tanzania Award during The Banker Africa – East Africa Awards 2017 at the ceremony held last week in Nairobi at the crown plaza. From left to right: Mr. Robin Amlot CEO of CPI Financial, Ms Upendo Nkini , Head of Marketing - BancABC, Ms Joyce, Malai Head of Retail & Business Banking, Mr. Dana Botha Managing Director, Mr. Imani John – Head of Finance and Mr. Matthew Amlot Editor of Banker Africa.

  0 0  Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar yazinduliwa rasmi.

  Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar zilizinduliwa rams tarehe 19 Mei 2017. Shughuli za ufunguzi ziliongozwa na Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Qatar ambaye alisaini kitabu cha wageni kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Ubalozi.


  Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya Watanzaia wanaoishi nchi Qatar walishiriki katika hafla hiyo.

  Mhe. Balozi alitumia fursa hiyo kuzungumza machache na Watanzania walioshiriki. Aliwaeleza kwamba kufunguliwa kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar ni sehemu ya kutekeleza malengo ya Serikali ya Tanzania ya kusogeza huduma zake kwenda kuwekeza Tanzania hususan katika sekta ya viwanda. Aliwahakikishia kwamba Ubalozi utawapatia ushirikiano watakaouhitaji katika kufanikisha azma hiyo.

  Balozi aliwapongeza Watanzania hao kwa kuendelea kuwa na sifa nzuri nchini Qatar na kudumisha mshikamano miongoni mwao. Aliwahimiza waendelee kuwa raia wema na kulinda haiba na jina la Tanzania kwa kufuata sheria za nchi wanapoishi. Alisema milango ya Ubalozi itakuwa wazi kupokea ushauri wao katika mambo ambayo yatalenga kuleta tija na mafanikio kwa taifa. 

  Naye Bw. Said Ahmed, Mwenyekiti wa Watanzania wanaoishi Qatar aliishukuru Serikali kwa kusikia kilio chao na hatimaye kufungua Ubalozi na kuwa na Balozi Mkazi nchini Qatar. Alimueleza Balozi kwamba jamii ya Watanzania wanaoishi Qatar itashirikiana na Ofisi za Ubalozi na kufanya kazi bega kwa bega katika kuitafutia maslahi Tanzania. Wawakilishi hao waliomba Ubalozi uandae mkutano mkubwa utakaowawezesha Watanzania wengi zaidi kushiriki ili kusikia maoni yao na changamoto zinazowakabili. Balozi aliahidi kufanya mkutano huo mapema iwezekanavyo. 

  Imetolewa na:

  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Doha, Qatar 24 Mei, 2017 .
  Mhe. Fatma Mohammed Rajab, Balozi wa Tanzania nchini Qatar akiongea na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar 
  Mhe. Balozi Fatma Mohammed Rajab akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar

  0 0

  Dr. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrioka Mashariki na Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa SADC akizungumza na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho, Mhe. Jaji Mstaafu Lesao Lehohla (wa pili kutoka kulia) alipotembelea tume hiyo mjini Maseru Lesotho kabla ya kuzindua rasmi Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC. 
  Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Mkuu wa Umoja wa Makanisa wa Lesotho Archbishopp Gerald Tlali Lerotholi na ujumbe wake alipotembelea ujumbe huo kusikiliza maoni yao kuhusu uchaguzi mkuu nchini humo unaotarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017. 
  Dkt. Mahiga na ujumbe wake wakikamilisha majumuisho ya mikutano mbalimbali waliyoifanyana na wadau . 
   Dkt Mahiga akiagana na wenyeji wake nje ya Tume Huru ya Uchaguzi.   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, amezihimiza taasisi za Serikali na za dini nchini Lesotho kudumisha amani na usalama kwenye kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi mkuu nchini hapa ili kuwezesha Serikali itakayoingia madarakani kufanya kazi kwa ufanisi zaidi kwa ajili ya wananchi wa Lesotho. 

  Uchaguzi huo mkuu wa wabunge ambao ni wa tatu kufanyika ndani ya kipindi cha miaka mitano, unatarajiwa kufanyika tarehe 3 Juni 2017 ambapo vyama 26 kati ya 30 vilivyojiandikisha, vitashiriki kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuchagua wawakilishi Bungeni. 

  Kwa mujibu wa Katiba ya Falme ya Lesotho, kiongozi wa chama kitakachoshinda viti vingi zaidi vya ubunge kwenye uchaguzi huo ndiye atakayeapishwa kuwa Waziri Mkuu na Kiongozi wa Serikali, ambapo mkuu wa nchi na mtawala mkuu anaendelea kuwa Mfalme Letsie III. 

  “Wakati umefika sasa kwa Jumuiya yetu ya SADC kushiriki kwenye uangalizi wa uchaguzi huu tukiwa na habari njema ya kurejesha matumaini kwa wananchi kuhusu mustakabali wa uongozi. Lakini pia tuwe na ujumbe mzito kwa Serikali ijayo ili iweze kufanya mageuzi ya kweli kwenye nyanja mbalimbali kwa manufaa ya wananchi” Mhe. Mahiga amehimiza kwa wajumbe wa timu ya waangalizi wa uchaguzi.

  Tangu alipowasili nchini hapa tarehe 22 Mei 2017, Dkt. Mahiga na ujumbe wake wamekutana na wadau mbalimbali wakiwemo Tume Huru ya Uchaguzi ya Lesotho na Umoja ya Makanisa wa Lesotho kwa lengo la kupata maoni ya kina kabla ya kuzindua Timu ya Uangalizi ya SADC (SADC Elections Observersion Mission - SEOM) tarehe 25 Mei 2017. 

  Mhe. Dkt. Mahiga anaongoza timu hii ya waangalizi wa uchaguzi ya SADC kwasababu kwa sasa Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye Mwenyekiti wa Asasi ya Ushirikiano ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Organ).

  Akiongoza mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Lesotho Mhe. Mampono Khaketla, Mhe. Mahiga alipongeza jitihada za Serikali kuhakikisha kuwa usalama wa raia na amani vinatawala nchini humo wakati wa uchaguzi. Hata hivyo aliongeza kuwa yeye na ujumbe mzima wa asasi hiyo muhimu ya maamuzi ya SADC ipo Lesotho kwa mara ya tatu, kama waangalizi wa uchaguzi ambapo mara ya kwanza na ya pili ilikuwa uchaguzi wa mwaka 2012 na 2015. 

  Alisema ni matarajio yake na ujumbe mzima kuwa uchaguzi wa mwaka huu utazaa matunda yatakayoleta matumaini kwa wananchi ya kuwa na Serikali imara itakoyoongoza na kusimamia mageuzi ya kweli. “Haya ni matumaini ya wananchi wa nchi hii, na mimi kama kiongozi wa SEOM nimekuja kuwahakikishia ndugu zangu, tutasimama pamoja nanyi, tutawasindikiza kwenye uchaguzi huu, kama misingi ya Jumuiya yetu inavyoelekeza lakini pia wananchi wanatarajia hayo”

  Timu ya Waangalizi wa Uchaguzi ya SADC imewasili nchini Lesotho tarehe 18 Mei, 2017 na inaundwa na nchi tisa ambazo ni wananchama wa Jumuiya hiyo. Wajumbe wapatao 41 watasambaa kwenye majimbo yote ya uchaguzi kama waangalizi na kutoa taarifa ya kina siku chache baada ya uchaguzi huo, kuhusu mwelekeo na mwenendo wa uchaguzi huo.


  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 

  Maseru, Lesotho 23 Mei, 2017

  0 0

  DROO ya nane iliyochezeshwa leo jijini Dar es Salaam na waendeshaji wa Bahati Nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ imefanyika huku mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko akifanikiwa kuibuka na mkwanja wa Sh Milioni 10. 

  Hiyo ni siku chache baada ya wakazi wa Ubungo, Sospeter Muchunguzi na Stanley Kapondo, mfanyakazi wa TANESCO nao kuibuka na mamilioni ya Biko kwa siku tofauti ndani ya wiki moja.

  Akizungumza katika droo hiyo, Balozi wa Biko, Kajala Masanja alisema kwamba siri kubwa ya ushindi ni kucheza Biko mara nyingi zaidi, akiamini kuwa kila anayecheza ana nafasi kubwa ya kuibuka kidedea na ushindi huo.
  Picha tofauti tofauti Balozi wa Biko Kajala Masanja akimkaribisha mgeni wake mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe katika droo ya nane ya Sh Milioni inayoondeshwa na Biko Tanzania ambapo mkazi wa Tabata, jijini Dar es Salaam, Daniel Dancan Mwakaboko alifanikiwa kutangazwa mshindi katika droo iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam. Picha na Mpigapicha wetu. 
  Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Chiku Salehe kushoto akiwa na Balozi wa Biko, Kajala Masanja wakati wanamtafuta mshindi wa droo ya nane wa Biko ambaye mkazi wa Tabata, Daniel Mwakaboko alitangazwa mshindi na kuzoa jumla ya Sh Milioni 10 atakazokabidhiwa jijini Dar es Salaam.

  Alisema mchezo wa Biko ni mzuri na rahisi kucheza kwake, hivyo ni jukumu la kila Mtanzania kutumia nafasi yake vizuri kwa kucheza bahati nasibu hiyo iliyojizolea umaarufu katika kipindi kifupi baada ya kuanzishwa kwake.

  “Hakuna njia ya mkato ya kuweza kushinda donge nono la Biko badala yake dawa ni kucheza kwa wingi kwa kufanya miamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456,” Alisema Kajala.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven, aliwataka Watanzania kuingia kwa wingi katika mchezo wa Biko hususan wakazi wa mikoa mbalimbali ya Tanzania nao wakiwa kwenye nafasi kubwa ya ushindi.

  “Tumetoa zawadi kwa washindi zaidi ya 30,000 nchi nzima kwa zawadi kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja nchini kote, hivyo tunawaomba watu wa mikoani nao kuongeza mwendo kuwania mamilioni ya Biko yanatotoka kila siku, huku droo kubwa ya Sh Milioni 10 ikifanyika siku mbili kwa wiki, yani Jumatano na Jumapili,” Alisema Heaven. 

  Naye Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Chiku Salehe, alisema anajisikia faraja kuwa mwangalizi katika droo iliyompa ushindi mkazi wa Tabata, Mwakaboko, akiamini kuwa kila Mtanzania anaweza kuzoa mamilioni ya Biko.

  “Mchezo wa Biko ni rahisi kucheza, ni salama na tunaangalia kwa kina ili kila Mtanzania aweze kushinda kihalali na kuongeza kipato chake kama walivyokusudia, ukizingatia kuwa endapo mtu anaibuka na mamilioni ya Biko anaweza kufika mbali kiuchumi,” Alisema Chiku. 

  Mshindi wa droo hiyo, Mwakaboko hakusita kuonyesha furaha yake kwa kutangazwa mshindi, huku akisema licha ya kuchelewa kushinda, lakini hakuvunjika moyo akiamini kuwa siku moja bahati inaweza kuwa yake.

  “Nashukuru sana kwa kutangazwa mshindi wa Biko wa Sh Milioni 10, sasa nitaipata lini,” Alihoji Mwakaboko kwa kupitia simu wakati anahojiana na balozi wa Biko, Kajala.

  Kwa ushindi huo, Mwakaboko anatarajiwa kukabidhiwa fedha zake mapema ili aweze kuziingiza katika matumizi yake ya kimaisha hususan ya kumkwamua kiuchumi kwa kupitia mchezo wa Biko uliojizolea umaarufu mkubwa ukitambulika kama nguvu ya Buku.

  0 0

   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job akipokea zawadi kutoka Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi.
   Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai  (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kuhusu Bunge la Kenya linavyofanya kazi kutoka kwa Spika wa Bunge hilo Mhe Justin Muturi.Mhe Ndugai yuko katika ziara ya kibunge nchini Kenya kwa mwaliko Bunge la Kenya ambapo amembatana na wajumbe wa Tume ya Utumishi ya Bunge, Mhe Mary Chatanda, Mhe Salim Turky na Mhe Mch.Peter Msigwa.

  (Picha na Ofisi ya Bunge)

  0 0

   Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka (wa pili kutoka kulia), akijibu maswali mbalimbali kutoka kwa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la Mererani, wakati wa mafunzo maalum kuhusu usalama migodini yaliyofanyika hivi karibuni. Wengine pichani (kutoka kulia) ni Mkaguzi Mkuu wa Migodi Tanzania, Mhandisi Ally Samaje, Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Juma na Fundi Sanifu Migodi kutoka Ofisi ya Madini Dar es Salaam, Stanslaus Basheka.
   Mkaguzi Mkuu wa Migodi Tanzania, Mhandisi Ally Samaje, akiwasilisha mada kuhusu Usalama, Afya na Utunzaji wa Mazingira katika Migodi ya Wachimbaji Wadogo wa Madini, wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa eneo la Mererani yaliyozinduliwa rasmi hivi karibuni.
   Fundi Sanifu Migodi kutoka Ofisi ya Madini Dar es Salaam, Stanslaus Basheka, akiwasilisha mada kuhusu Matumizi salama na utunzaji wa baruti migodini, wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la Mererani hivi karibuni.
   Ofisa wa Sheria kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Hadija Ramadhan, akiwasilisha mada kuhusu Ufafanuzi wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009, Ufafanuzi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2010, wakati wa mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la Mererani hivi karibuni.
   Sehemu ya umati wa wachimbaji wadogo wa madini wa eneo la Mererani, wilayani Simanjiro, wakifuatilia mafunzo maalum kuhusu usalama migodini yaliyotolewa hivi karibuni wilayani humo.
   Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini, eneo la Mererani, wilayani Manyara, wakiuliza maswali kwa watoa mada (hawapo pichani), wakati wa mafunzo maalum kuhusu usalama migodini, yaliyozinduliwa rasmi kitaifa wilayani humo hivi karibuni.

  Na Veronica Simba
  Serikali imesema itaifungia migodi yote ya madini ambayo itapata ajali kutokana na uzembe na haitafunguliwa hadi hapo Mkaguzi Mkuu wa Migodi atakapojiridhisha kuwa hali ya usalama imeboreshwa na hatua stahiki za kisheria zimechukuliwa kwa Meneja wa Mgodi au Msimamizi aliyehusika na uzembe huo.

  Hayo yalisemwa hivi karibuni na Kamishna wa Madini Tanzania, Mhandisi Benjamin Mchwampaka wakati akifungua mafunzo maalum kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini, kwa lengo la kuwakumbusha kuzingatia kanuni zote za usalama mahali pa kazi ili kuepusha ajali za mara kwa mara zinazotokea na kusababisha vifo.

  Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini, kupitia Idara yake ya Madini, yalifunguliwa rasmi Mererani, wilayani Simanjiro, Mkoa wa Manyara, ambapo Kamishna Mchwampaka aliwaambia wachimbaji wadogo wa madini wa eneo hilo kuwa, kwa sasa uchimbaji mdogo wa madini nchini umegubikwa na ajali nyingi ambazo zinaweza kuepukika endapo tahadhari za kiusalama zitachukuliwa.

  “Ajali zinazotokea katika Migodi mingi ya wachimbaji wadogo hapa nchini, zimesababisha vifo, vilema vya maisha na pia gharama kubwa wakati wa shughuli za uokoaji.”

  Kamishna Mchwampaka alisema kuwa, Serikali imelazimika kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha kuwa uchimbaji madini nchini, unafanyika kwa mujibu wa Sheria ya Madini kwa kuzingatia usalama na pia utunzaji wa mazingira.

  Akizungumzia kuhusu takwimu za ajali migodini, Mhandisi Mchwampaka alifafanua kuwa, taarifa zinaonesha kwamba kuanzia mwaka 2008 hadi mwezi Mei mwaka 2017, ajali zilizotokea katika Migodi yenye leseni ya wachimbaji wadogo wa madini, nchini ni 125 na wachimbaji waliopoteza maisha kutokana na ajali hizo ni 213.

  Aidha, aliongeza kuwa, ajali zilizotokea katika maeneo ya wachimbaji wadogo wasiokuwa na leseni hususan maeneo ya mifumuko ya uchimbaji madini, katika kipindi hicho, ni 56 na kusababisha vifo vya wachimbaji 140.
  “Kwa mwaka huu pekee, hadi kufikia tarehe 19 Mei, jumla ya ajali zilizotokea ni 11 na jumla ya wachimbaji waliofariki ni 26.”

  Kamishna Mchwampaka alisema kuwa, kutokana na takwimu hizo za ajali na vifo, Serikali imeazimia kuhakikisha hali hiyo inadhibitiwa na usalama unaimarishwa katika migodi yote ya wachimbaji wadogo nchini. Alifafanua kuwa, Wizara imepanga kutoa mafunzo husika nchi nzima kupitia Kanda zote 10 za Madini na kwamba mafunzo hayo yatasimamiwa na Maafisa Madini wa Kanda husika.

  Akielezea zaidi kuhusu mazingira ya ajali zinazotokea, alisema kuwa uchambuzi wa takwimu unaonesha kuwa vyanzo vikubwa vya ajali hizo ni kuangukiwa na vifusi kutokana na kukatika kwa ngema, kulipukiwa na baruti, kukosa hewa na kuteleza na kuangukia mashimoni. “Hivyo, ni dhahiri kuwa ajali nyingi zingeweza kuepukika kama tahadhari za kiusalama zingechukuliwa.”

  Kamishna Mchwampaka alitumia fursa hiyo kutoa maagizo kwa wamiliki wote wa migodi nchini, kuhakikisha wanateua mameneja wa migodi kama Sheria ya Madini ya mwaka 2010 inavyoelekeza ambao alieleza kuwa mojawapo ya majukumu yao ya msingi ni kusimamia usalama, afya za wachimbaji na uhifadhi wa mazingira migodini.

  Alielekeza kuwa, Meneja anapokuwa hayupo, lazima kuwe na msimamizi atakayewajibika na kusimamia masuala husika na kwamba, ajali itakapotokea, Meneja au Msimamizi atakuwa wa kwanza kuwajibika.
  Aliwataka Maafisa Madini wa Kanda nchi nzima, kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo ambapo Msimamizi Mkuu wa suala hilo ni Mkaguzi Mkuu wa Migodi Tanzania.

  Aidha, Kamishna Mchwampaka alieleza kuwa, tayari amemwelekeza Mkaguzi Mkuu wa Migodi, Mhandisi Ally Samaje, ambaye kwa upande wake ametoa maelekezo maalum kwa wakaguzi wote wa Migodi nchini, kuhakikisha kuwa Migodi yote nchini inakaguliwa ipasavyo na ile itakayobainika kuwa haina usalama, itafungwa mara moja hadi pale marekebisho stahiki yatakapofanyika.

  Kwa upande wake, Mhandisi Samaje, akitoa mada inayohusu usalama migodini kwa wachimbaji hao wa Mererani, alibainisha kuwa, inawezekana kuweka Migodi salama iwapo kila mmoja kwenye Mgodi, kuanzia Meneja hadi mfanyakazi wa chini, atajenga utamaduni wa kuheshimu sheria, kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa.

  Mada nyingine zilizotolewa katika mafunzo hayo ni pamoja na Ufafanuzi wa Sera ya Madini ya Mwaka 2009, Ufafanuzi wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za Mwaka 2010, Kanuni za Afya na Usalama Migodini, Matumizi salama na utunzaji wa baruti pamoja na utunzaji wa mazingira kwa wachimbaji wadogo na wa kati.


  0 0


  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Linaweza kuwa si jambo la kushangaza kuwaona watu wakisafiri kwenye usafiri wao binafsi kuelekea mikoa mbalimbali nchini Tanzania. Na hii ni kutokana na maendeleo na mabadiliko ya kiuchumi miongoni mwa watanzania wengi ambapo hapo awali walikuwa wanategemea usafiri wa umma.

  Sababu za kusafiri zinaweza kuwa nyingi kama vile kifamilia, kutembelea ndugu na jamaa au vivutio mbalimbali vya kitalii. Lakini je ni wangapi wanayafahamu mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kuingia barabarani na usafiri binafsi kwenda umbali mrefu? Jumia Travel imekukusanyia masuala muhimu ambayo usipokuwa makini kuyafuata basi safari yako itakuwa ni shubiri badala ya asali huko njiani.

  Jipange kwa safari nzima. Sidhani kama kuna jambo ambalo unaweza kufanikiwa bila ya kujipanga. Vivyo hivyo unapotaka kusafiri ni lazima uweke mipango madhubuti tangu mwanzo mpaka mwisho wa safari yako. Kwa mfano, safari itachukua muda gani, hoteli gani mtafikia, gari utakalolitumia litawatosha watu wangapi, gari litahitaji mafuta kiasi gani mpaka kumaliza safari, nini cha kufanya inapotokea dharura na kadhalika.   

  Chunguza usafiri wako. Barabarani kuna mengi yanatokea ingawa kuna mengi unaweza kuyadhibiti endapo utachukua tahadhari kabla. Kwa mfano suala la gari kuharibika njiani linaweza kuepukika endapo utachukua muda wako kulipeleka kwa fundi kufanyiwa uchunguzi na matengezo pale yatakapohitajika. Huwezi jua inawezekana injini isingeweza kukupeleka hata nusu ya safari yako au jaribu kuvuta picha gari linapokuharibikia katikati ya msitu wenye wanyama wakali bila ya msaada.

  Hakikisha usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwa barabarani. Kusafiri umbali mrefu hususani kutoka katikati ya jiji haimaanishi kwamba huko barabarani sheria hazifuatwi. Kwa hiyo hakikisha kuwa usafiri wako umekidhi vigezo vyote vya kuwepo barabarani kama vile leseni ya udereva, bima ya gari, leseni ya barabarani na sheria nyinginezo. Usipofanya hivi unaweza kujikuta unalipishwa faini, kukamatwa na hivyo kupotezewa muda ambao ilibidi uutumie kukufikisha huko uendako. Kwa mfano sio umefika Bagamoyo tu askari wa barabarani wanakukamata na kukuambia vibali vya gari lako kuwa barabarani vimekwisha muda wake.

  Tarajia changamoto mbalimbali barabarani. Ni mara chache kusafiri barabarani bila ya kukutana na changamoto zozote kama vile foleni, njia kuwa mbovu, ukaguzi wa mara kwa mara, ajali na kadhalika. Hivyo lazima ujiandae kiakili wewe kama dereva pamoja na watu unaosafiri nao.

  Usibebe mizigo mingi sana. Sawa mizigo ni muhimu kwa kuwa unasafiri umbali mrefu lakini kwa kufanya hivyo unaweza kujinyima fursa ya kubeba vitu vingine utakavyovutiwa navyo njiani. Hivyo basi hakikisha unabeba mizigo ambayo ni muhimu kwako kwani unaweza kupita sehemu na ukakuta vitu vya gharama nafuu ambavyo unaweza kununua.

  Beba ramani ya kukusaidia huko uendako. Wengi wetu huwa tunapenda kwenda sehemu ambazo tunazifahamu hivyo inakuwa sio lazima sana kuwa na ramani ya kukupa mwongozo. Lakini siku hizi maendeleo ya teknolojia yamekuwa ni makubwa kwani sehemu nyingi zimewekwa kwenye ramani kupitia vifaa mbalimbali kama vile kompyuta, tabiti na simu. Mbali na teknolojia kurahisisha hilo lakini unashauriwa kubeba ramani ya karatasi, kwa mfano kama unanda Zanzibar unaweza kuwa na ramani inayokuonyesha sehemu zote za kule.

  Kuwa na nyimbo au vitu vya kukuburudisha njiani. Kazi na dawa huwa wanasema Waswahili. Haimaanishi kwa sababu unasafiri umbali mrefu basi ndiyo uwe makini na usukani pasipo kujiburudisha. Beba vitu kama vile CD za muziki zenye nyimbo uzipendazo pamoja na michezo mbalimbali kwa ajili ya watoto wako kama unasafiri nao. Lakini pia hata vinywaji na vitafunwa vinaweza kuifanya safari iwe ni fupi na ya kuifurahia.

  Beba pesa ya akiba. Unaposafiri njiani unaweza kukutana na changamoto ambazo zitahitaji pesa ya papo kwa papo ili kuweza kuzitatua. Hivyo hakikisha unakuwa na kiasi cha pesa taslimu kwani mara nyingi sehemu za kuzipata huwa ni nadra. Pia itakusaidia hata kununua vitu vya njiani, kwa mfano Morogoro kuna bidhaa nyingi sana kutoka kwa wakulima.  

  Jaribu kuipumzisha simu yako kwa muda. Itakuwa haileti maana kuwa upo kwenye usafiri pamoja na wenzako au familia yako lakini unawasiliana na watu uliowaacha ulipotoka. Lengo la safari za namna hii mara nyingi ni kujaribu kubadili na kufurahia mazingira mapya. Basi jaribu kuendana na mazingira hayo kwa kuzungumza na wenzako ndani ya gari ninaamini kutaifanya safari kuwa ni ya kusisimua zaidi.  
  Piga picha kwa ajili ya kumbukumbu. Ni muhimu kuwa na kumbukumbu ya baadhi ya matukio unayoyaona. Siku hizi kamera inapatikana kwenye simu za mkononi hivyo kurahisisha kuhifadhi kumbukumbu ya matukio mbalimbali. Basi hakikisha unapiga picha za sehemu na matukio utakayovutiwa nayo au hata wewe mwenyewe ukiwemo ili iwe kama ni ukumbusho kwako. Kwa mfano haiwezekani ukapita mbuga yaMikumi bila ya kupiga picha ya Tembo au pundamilia wanaokatiza barabarani.

  Kusafiri kwa kutumia gari binafsi hususani umbali mrefu ni starehe kubwa ambayo wengi bado hawajaigundua. Wapo wengine wanapanda ndege ili kuwahi kufanya vitu vingi huko waendapo pamoja na kuepuka uchovu. Lakini Jumia Travel inasisitiza kwamba kusafiri kwa njia ya barabara kunakupa fursa kubwa ya kujionea ni jinsi gani nchi yako imebarikiwa na fursa ya kujifunza mengi zaidi. 

  0 0

   By Jumia Travel Tanzania

  Nowadays, it's not a strange thing to find people on a road trip in Tanzania. Things are different now compared to some few years back when most Tanzanians depended on commuter buses or trains.  

  An initiative to decide to take a road trip could be for family tour, visiting other siblings or leisure. But we must ask ourselves how many do know and consider tips to be on a road trip? Below are the things which Jumia Travel suggests if you think about would serve a big time ahead.
  Plan your trip. I don’t think you can succeed in anything without prior planning. That applies the same when you want to travel, make sure you have a proper plan from the starting to the ending point. For instance, you should be aware for how long your trip will take, ahotel you will stay in, how many people will fit in a vehicle, fuels the vehicle will need, what do when you have a flat tire and so forth.  

  Check your vehicle. Lots of things happen on road but some of them could be avoided if precautions are taken in advance. For example, to experience a car-breakdown while on road can be prevented by having a mechanic do a thorough check-up on it. You never if your car’s engine couldn’t manage to take you a half of your trip or break down in the middle of nowhere.

  Make sure your vehicle has all the documents. To travel out of the city does not mean that rules and regulations do not apply out there. So for your own safety make sure you vehicle has all the necessary documents such as driving license, road licence, insurance and all the requirements according to national laws and regulations. Failing to do that may result to your vehicle to be seized, impounded or being fined. Hence wasting much of time and money while you could you use it to driving. For example, how does it feel to be impounded by traffic police in Bagamoyo just a few kilometers away from Dar es Salaam for your car having expired road licence?  

  Expect challenges on road. It is very rare to travel on road without experiencing traffic jams, car breakdowns, accidents or regular traffic inspections. Therefore, it would be useful to prepare yourself and your colleagues for such incidents.

  Don’t pack too much. Travelling for a long distance does not mean you should carry a bunch of stuffs. By doing so you will be denying yourself opportunities to pack some interesting and cheap stuffs while on road.  

  Carry a map with you. Most of people like to go to place which they’re familiar with. Therefore, there would no need most of the time to carry a map. To some extent the technological advancement has facilitated easy access of maps through devices such as computers, tablets and smartphones. Apart from that, it is suggested to carry a paper map which you could use in any conditions. For example, there are paper maps which shows and guides you to every corner of Zanzibar when you visit.     

  Don’t forget some entertainment. Make sure you bring some entertainments with you on a road trip such as a CD with the best songs that you love, games as well as bites and drinks.

  Carry some cash. While on a road trip you might face some challenges which will need instant cash money in order to be solvent on the spot. Hence, make sure you have some cash in your pocket because some areas have no points for such services. Also that will help you to buy stuffs on road, for example,Morogoro regions has got lots of fresh farm products which most people stop and buy.  

  Keep your phone away. It will not make sense to be on a trip with either your family or friends and still be glued with your phone speaking or chat to friends back at home. Most of the times, purposes for road trips is to disconnect to the world and experience new surroundings. Therefore, make sure you interact and make new friends in a car, you never know how interesting it will be.

  Take photos. I don’t know how you are going to convince your colleagues that you’re on a road trip without showing them photos! Things have been easy nowadays, camera are just on your smartphone unlike some few years back. If that is the case, then make sure you take all the photos of the things and places and you in them while on a road trip. It will be unforgivable to pass through Mikumi National Park without taking photos of elephants and zebras passing across the road.

  People have not yet discovered how wonderful it would be to be on a road trip. Some people prefer to take flights so as to arrive early and do many things where they are heading or escape fatigue. But still Jumia Travel suggests to you that a road trip is the only way which could make you to discover and learn a lot of things about your country.  

  0 0

  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akiwasili chuo cha cha Bahari Dar es Salaam(DMI) kuzindua bodi ya Ushauri ya Chuo hicho kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Dk. Erick Massami na kulia ni Mwenyekiti wa wa Bodi hiyo Nahodha Ernest Mihayo Bupamba Uzinduzi huo ulifanyika jana Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam 
  Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa akizungumza wakati akizindua bodi ya Ushauri ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) kushoto Mwenyekiti wa wa Bodi hiyo Nahodha Ernest Mihayo Bupamba na kulia ni Mkuu wa Chuo hicho Dk. Erick Massami.Uzinduzi huo ulifanyika jana Chuoni hapo Jijini Dar es Salaam.
  Dk. Tumaini Gurumo, Naibu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Mipango, Fedha na Utawala akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa (kushoto) jana wakati Waziri huyo akizindua bodi ya Ushauri ya Chuo hicho wa pili kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Dk. Erick Massami na wa tatu kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma,Utafiti na Ushauri.
  Mhasibu Mkuu wa Chuo Cha Bahari Dar es Salaam(DMI) Haika Kessy akijitambulisha kwa Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa wakati Waziri huyo kuzindua bodi ya Ushauri ya Chuo hicho wengine pichani Maofisa wa Chuo hicho.

  0 0

   Mwenyekiti   wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Azzan Zungu akiongoza kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.Selemani Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
    Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akizungumza jambo  na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  katika kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM) Mhe.Ally Keissy akiuliza swali katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mhe.Kiteto Koshuma akiuliza swali katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt,Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mhe.Amina Mollel  akiuliza swali katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Waziri wa Sera,Bunge, Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akijibu hoja mbalimbali  katika kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.

   Wabunge wa CHADEMA,Mhe.John Mnyika(Kibamba) na Mbunge wa Bunda Mhe.Esther Bulaya wakifuatilia hoja mbalimbali  katika kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Mbunge wa Monduli (CHADEMA) Mhe.Julius Laizer akiuliza swali katika kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
  Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akimskiliza Mbunge wa kaliua(CUF) Mhe.Magdalena Sakaya   katika kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
   Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng Stella Manyanya akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 24, 2017.

  Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

  0 0

  Mmoja wa wasimamizi wa Mdahalo huo, Dorothy Kipeja akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari Zanaki na Msimbazi katika Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.  
  Afisa Mipango wa Taasisi ya Friedrich Naumann, Veni Swai akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari Zanaki na Msimbazi katika Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Mkuu wa Kitengo cha Elimu wa Taasisi ya Doris Mollel, Erick Kajahurwa akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule za Sekondari Zanaki na Msimbazi katika Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya Wasimamizi wa Mdahalo huo wakifatilia.
  Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Zanaki, akizungumza wakati akichangia mada katika Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Afisa Mipango wa Taasisi ya Friedrich Naumann, Vena Swai akikabidhi zawadi ya mpira kwa Mwanafunzi Mwanahamisi Ally wa Shule ya Sekondari ya Zanaki, baada ya kuwa mmoja wa washindi katika Mdahalo uliozikutanisha shule mbili za Zanaki na Msimbazi, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zanaki wakiwa katika Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili za Zanaki na Msimbazi, ulioambatana na uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Picha ya pamoja ya Wasimamizi wa Mdahalo uliozikutanisha shule mbili za Sekondari za Zanaki na Msimbazi pamoja na Walimu wao baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Katika Mdahalo huo, Shule ya Sekondari ya Zanaki ndiyo iliibuka na ushindi.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Shule za Sekondari za Zanaki na Msimbazi, wakiwa katika picha ya pamoja na Wasimamizi wa Mdahalo uliozikutanisha shule hizo mbili pamoja na Walimu wao baada ya uzinduzi rasmi wa Mradi wa Kuwa Mfano, ulioratibiwa na Taasisi ya Doris Mollel kwa kushirikiana na Taasisi ya Friedrich Naumann, uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Zanaki, Jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki. Katika Mdahalo huo, Shule ya Sekondari ya Zanaki ndiyo iliibuka na ushindi.  

  0 0


  0 0

  Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

  Katika kuendana na kasi ya Rais John Pombe Magufuli benki ya biashara ya TIB imeanzisha huduma za kibenki kwa masaa 24 katika tawi dogo la benki hiyo lililopo katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege amesema huduma hiyo inawawezesha wananchi wote kulipia kodi za aina mbali mbali pamoja na tozo zote za bandari.

  Amesema hivi karibuni TIB benki na TRA ziliingia mkataba kwa kuunganisha mfumo wa malipo ya kodi ambapo mtu akilipa kodi kupitia mfumo huo katika tawi lolote la benki hiyo, taarifa zake zitaonekana moja kwa moja kwenye mtandao wa TRA.

  Amesema kuwa, benki hiyo ya biashara (TIB), ndiyo benki pekee yenye dhamana ya kusimamia sehemu kubwa ya akaunti za TPA hivyo mwananchi atakapolipia tozo yoyote bandarini taarifa zake huonekana mara moja katika mtandao wake hivyo kurahisisha na kuwezesha kuendelea na taratibu zingine za utoaji mizigo kwa haraka zaidi.

  “TIB bank inatoa huduma mbali mbali kutokana na mahitaji ya mteja, zikiwemo za akaunti za aina mbalimbali kwa makampuni na watu binafsi, mikopo ya muda mfupi na muda wa kati dhamana za kibenki uuzaji na ununuaji wa fedha za kigeni na shughuli zote za kibenki”, amesema Nyabundege.

  Aidha amesema, benki hiyo ya kibiashara yenye matawi 6 nchini, Dar esSalaam matatu, Mwanza, Arusha na Mbeya inamilikiwa na serikali kwa asilimia 100 na pia inatoa huduma kwa watu binafsi taasisi binafsi na serikali.


  Mkurugenzi wa Benki ya Biashara ya TIB Frank Nyabundege, akizungumza na Waandishi wa habari juu ya benki hiyo kufanya kazi saa 24 Bandari ya Dar es Salaam
  Mkurugenzi mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya TIB  Theresia Soka akizungumzia ubora wa huduma hizo.
  Watendaji wa Benki ya Biashara ya TIB
  Sehemu ya Waandishi wa Habari walifika katika mkutano huo

  0 0

  Babalozi kutoka nchi mbali mbali wakiwasha mishumaa wakiongozwa na Balozi wa Rwanda nchini Tanzania Mhe. Eugene Kayihura kwenye maaadhimisho ya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari dhidi ya Watusi iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Saalam.
   Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akiongozana na Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakati wakiwasili kwenye Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam, kulikofanyika Maadhimisho ya  Kumbukumbu ya Mauaji wa Kimbari dhidi ya Watusi yaliyotokea miaka 23 iliyopita huko nchini Rwanda.
  Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe Edzai Chimonyo akizungumza kwenye maadhimisho ya Mauaji ya Kimbari yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Rwanda nchini Tanzania, Eugene Kayihura akizungumza kuhusu mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda wakati wa maadhimisho ya miaka 23 yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim  akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 13 ya mauaji ya kimbari ya nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Nyimbo za mataifa mawili Tanzania na Rwanda zikiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbali nchini Rwanda yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
  Sheikh Hamis Mtonga akiomba dua wakati wa kuanza maadhimisho ya miaka 23 ya Kimbari ya nchini Rwanda leo.


  0 0


  Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo (wa kwanza kushoto) akimkabidhi nyaraka za gari aina ya Heicher lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka huu wa fedha 2017.wanaoshuhudia katikati ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,na Baraka Kilimba Meneja Mauzo Baraka Kilimba na mwishoni ni Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha .
  Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo Akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu zawadi ya msambazaji bora ambapo MM Group kutoka Mpanda aliibuka mshindi ,kulia kwake ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy na kushoto kwake ni Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

  Waandishi wa habari wakichukua matukio katika mkutano huo wa kutangaza mshindi mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
  Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa kutangaza mshindi wa shindano la msambazaji bora ambapo MM Group toka Mpanda aliibuka mshindi ,anayefuatia katikati ni Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo na mwishoni kulia ni ni Meneja Usambazaji wa SBL Malalia Mmasy ,mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.
  Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akijaribu gari lake mara baada ya kukabidhiwa baada ya kuibuka kama msambazaji bora ,Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

  Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya Heicher lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 mapema leo katika ofisi za SBL Temeke Jijini Dar es salaam.

  Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetoa zawadi ya gari aina ya Heicher lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 50 kwa MM Group, ambaye ni msambazaji wa kanda aliyeibuka msambazaji anayeongoza katika kipindi cha kwanza cha nusu mwaka huu wa fedha 2017.

  Kampuni ya MM Group ambayo ina makao yake wilayani Mpanda Mkoa wa Katavi iliwashinda wasambazaji wengine 85 walioshiriki kwa ajili ya kupata zawadi hiyo ya kipekee.

  Akiendesha hafla hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya SBL Temeke, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mauzo wa SBL, Alain Tayo alimpongeza mshindi huku akithibitisha kujikita kwa kampuni hiyo ya bia katika kutambua juhudi zinazofanywa na wateja wake katika kuunga mkono ukuaji kwa kampuni.

  “Wakati tunapongeza mchango wa MM Group kwa kuongoza na kushika nafasi ya juu katika kipengele chake kulikomwezesha kupata zawadi hii, tunatambua pia kazi nzuri inayofanywa na wasambazaji wengine, wateja na hali kadhalika wadau wetu. Kupitia uungwaji mkono huu wa dhati, SBL imekua katika uzalishaji na kufikia kiwango cha juu katika sekta ya uzalishaji bia ndani ya nchi na hata katika ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Tayo.

  Akitoa wito kwa wasambazaji wengine wa SBL kuiga mfano wa MM Group, Tayo aliwahahakishia washirika wa SBL kibiashara wakiwamo wasambazaji na wateja kwamba SBL itaendelea kuwaenzi na kusikiliza mahitaji yao.

  “Tunawashukuru wadau wetu wote kwa kuzingatia kwamba wamekuwa pamoja nasi katika katika safari yetu ndefu na ya mafanikio kibiashara”, alibainisha Tayo.

  Kwa upande wake, Mwakilishi wa MM Group Joseph Chanika, wakati akiishukuru SBL kwa zawadi hiyo, aliwapa changamoto wasambazaji wengine kuendesha na kuenenda na ukaribu wa SBL kwa kufanya kazi kwa bidiii ili kufuzu kwa ajili ya tuzo kama hiyo.

  “Naishukuru sana SBL kwa kuheshimu ahadi yake na kunituza gari hili Heicher. Hili gari ni zana muhimu katika biashara yangu ambayo itaniwezesha kukuza shughuli zangu za usambazaji wa bidhaa za SBL,” alisema Bw Joseph Chanika kwa bashasha.

  0 0


  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Taarifa ya uchunguzi wa mchanga wa madini mbalimbali uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiingalia Taarifa hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini mara baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine pichani ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakwanza kulia wakishuhudia tukio hilo.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigusia baadhi ya mambo yaliyomo kwenye Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
   Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Abdulkarim Hamis Mruma akisoma dondoo za Ripoti aliyoikabidhi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakisikiliza wakati mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Uchunguzi wa Mchanga wa Madini   Profesa Abdulkarim Hamis Mruma alipokuwa akiiwasilisha.
   Baadhi ya Mawaziri  pamoja na Wabunge wakifatilia kwa makini uwasilishwaji wa Ripoti hiyo ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Ripoti hiyo ya Kamati.
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya kupokea Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
   Wasanii mbalimbali wa Nyimbo za Bongo Flavour na Dansi wakiimba wimbo wa Amani Tanzania kabla ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi wakati Wasanii mbalimbali wa Nyimbo za Bongo Flavour na Dansi walipokuwa wakiimba wimbo wa Amani Tanzania kabla ya kuwasilishwa kwa Ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliotakiwa kusafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo mbalimbali  ya madini nchini.
   Viongozi mbalimbali wa Dini na Siasa nao wakifatilia Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kupokea Taarifa ya Kamati Maalum ya uchunguzi wa Mchanga wenye madini Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa , Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi wa mchanga wenye Madini Profesa Abdulkarim Hamis Mruma pamoja na Wajumbe wa Kamati Hiyo mara baadaya kupokea Taarifa ya Uchunguzi huo Ikulu jijini Dar es Salaam. 

  PICHA NA IKULU

older | 1 | .... | 1243 | 1244 | (Page 1245) | 1246 | 1247 | .... | 1897 | newer