Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1242 | 1243 | (Page 1244) | 1245 | 1246 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mke wa Mbunge wa Mkuranga Bi Mariam Abdallah Kwa niaba ya mume wake Ndugu Abdallah Ulega akikabidhi vifaa vya ofisi,'Photocopy machine' na 'Rim papers' Kwa ajili ya matumizi ya ofisi ya CCM Mkuranga vyenye thamani ya milioni tatu na laki tano, kwa Naibu Katibu Kuu wa CCM,Ndg Rodrick Mpogolo katika ziara yake leo mkoani Pwani.
  Naibu Katibu Kuu wa (CCM),Ndg Rodrick Mpogolo akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa katika ziara yake hapo jana mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Firbato Sanga akizungumza na wajumbe wa kamati ya siasa katika ziara ya Naibu Katibu Kuu wa CCM,Ndg Rodrick Mpogolo mkoani Pwani.
  Muonekano wa Photocopy machine.

  0 0


  Kikosi cha kwaya ya Usharika wa Mabibo (waliovaa jezi za Dark Blue) na kwaya ya Usharika wa Kinondoni (waliovaa jezi nyekundu) wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi kuanza
  Mpira ukiwa unaendelea ambapo kwaya ya Kinondoni waliibuka kuwa washindi
  Baadhi ya wanakwaya pamoja na watumishi wa Sharika mbalimbali za Moravian jijini Dar wakiwa wanatazama Mpira
  Mchezo wa Netball ukiendelea ambapo walikuwa wanacheza kwaya ya Usharika wa Mabibo na Uhuru ambapo kwaya ya Mabibo waliibuka washindi.
  Kwaya ya Amani kutoka Usharika wa Mabibo wakifurahia ushindi baada ya kuibuka Videdea kwenye mchezo wa netball 
  Mpambano mwengine uliokuwa wakukata na shoka kati ya Kwaya ya Usharika wa Uhuru na Mabibo ambapo Mabibo waliibuka washindi
  Hapa ni mashindano ya kukimbia kwa wanawake
  Mashindano ya kukimbia kwa wanaume hapa watu walichomoka balaa
  Hapa ilikuwa ni mashindano ya kukimbia na majunia ambapo ngoma ilikuwa nzito kweli lakini walioweza waliibuka kidedea
  Hapa ilikuwa sasa kufukuza kuku ambapo baada ya purukushani akapatikana mshindi ambaye ndiye anaonekana hapo akifurahi.
  Mshindi wa Kukimbiza Kuku Bw. Lewis kutoka Usharika wa Kinondoni akiwa amekabidhiwa zawadi yake ya Kuku.
  Mshindi wa kukimbia na Majunia Bi. Emmy kutoka Usharika wa Uhuru akikabidhiwa nishani yake na katibu wa kwaya ya vijana kutoka usharika wa Mabibo.
  Huyu dogo anaitwa Afsa ndiye aliibuka mshindi wa riadha kwa upande wa wanawake 
  Mshindi kwa kukimbiza upepo kwa upande wa wanaume Adam ajichukua zawadi yake
  Washindi wa Mpira wa Miguu kutoka Usharika wa Kinondoni wakikabidhiwa kombe lao
  Kwaya ya vijana kutoka Usharika wa Mabibo wakikabidhiwa kombe lao baada ya kuibuka washindi katika mchezo wa Netball


  Picha zote na Fredy Njeje 

  0 0

  Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Sophia Mjema amewaomba wananchi hasa wa wilaya ya Ilala kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 29 mwezi huu katika kuukaribisha na kupokea Mwenge wa uhuru unaotaraji kukesha eneo la Kariakoo .

  Mjema ameyasema hayo leo wakati akitembelea miradi mbali mbali inayoendelea na ujenzi katika manispaa ya Ilala kwa kuanzia eneo la Kivukoni ambapo mwenge utupokelewa na kuelekea sanamu ya askari uliopo katikati ya jiji, bustani ya Kaburi moja, na miradi mingineyo.

  Amesema mwenge huo mwaka huu una kauli mbiu isemayo,’ mwenge ni kushiriki katika uchumi wa Viwanda’ na mwenge huu utakuwa unaongelea viwanda zaidi katika ukuzaji wa viwanda na ili kufanikisha hilo tutaenda maeneo ya gerezani ambapo kuna viwanda vidogo vidogo ambavyo tutavisaidia kukuza uchumi.

  “Tunaomba wananchi washiriki zaidi katika kuukaribisha mwenge na katika mkesha ambao utakuwa pale kariakoo, tunapeleka mkesha kariakoo kwa sababu pale tunajaribu na tunataka kuwatambua wamachinga rasmi, tunataka kuwafugulia ofisi yao rasmi ili wawe wanatambulika na serikali”.

  Ameongeza kuwa ili kukuza uchumi wa viwanda serikali itamsaidia kila mwananchi mwenye kiwanda kidogo katika kukuza uchumi wake ili baadae nao waweze kuja kuwa wajasiliamali wakubwa na hata kumaliza kabisa biashara ya wamachinga kama siyo kupunguza,.

  Aidha amesema Wilaya ya Ilala itatenga mitaa kama vile, Kongo, Mchikichi, Sikukuu na Nyamwezi kutumika zaidi kwa shughuli za umachinga na mingine itakuwa kwa ajiri ya maegesho ya magari ya mizigo, Tax na huduma zingine kama hizo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya mapokezi ya Mwenge wa uhuru wakati wa kukagua miradi itakayozinduliwa na mwenge huo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akijadili jambo na Katibu tawala wa Wilaya hiyo Edward Mpogolo .
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na afisa Mazingira wa Ilala , Abdon Mapunda juu ya umuhimu bustani hiyo.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akikagua bustani iliyopo nje kidogo  ya bustani
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akipata Maelekezo ya bustani ya Kaburi moja kutoka kwa Mhandisi Faizer Mbange.
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema , akikagua sehemu ya bustani ya kaburi moja
  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema, akikagu sehemu itakayopandwa miti na majani kwa ajili ya watu kupumzika

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akizungumza na wajumbe wa kamati ya kupokea mwenge wa Uhuru


  Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Sophia Mjema akionyesha bango linamuonyesha makandarasi waliotengeneza bustani hiyo
  Mazingira wa Ilala , Abdon Mapunda akitoa maelezo kwa wajumbe wa mbio za mwenge

  --

  0 0


  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege Bagamoyo Mei 23, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka baada ya kutembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrual Estate lililopo Kerege, Bagamoyo Mei 23, 2017
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mstahiki meya wa Jiji la Dar es salaam Mheshimiwa Isaya Mwita Charles leo amekabidhi rasmi magari mawili aina ya Suzuki Carry maarufu kama (Kirikuu) kwa washindi wa shindano la shika ndinga linaloandaliwa na kuendeshwa na kituo cha utangazaji cha EFM redio, washindi waliopatikana katika fainali iliyofanyika tarehe sita mwezi wa tano mwaka huu katika viwanja vya Tanganyika Packers Kawe Jijini Dar es Salaam.

  Mstahiki Meya Mheshimiwa. Isaya Mwita akijiandaa kukabidhi magari hayo.

  Mstahiki Meya akitoa pongezi zake kwa washindi Kutoka Kulia ni Meneja mkuu Dennis Busulwa, Mshindi (Michael Peter), akifuatiwa na Mshindi Joyce Daniel pamoja na Rukia Mtingwa Meneja masoko Zantel
  Washindi wa shindano hilo wakiwa wameshikilia kadi za gari Kutoka kulia ni Michael Peter na Joyce Daniel
  Shamla Shamla zikiendelea
  Wasindikizaji wa mshindi Michael Peter kutoka Salasala

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National.
  Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa tayari kumsindikiza na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja  na  Bw. Zhang Xin, Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya China National Machinery Industry Federation (CBMIF) na mjumbe wa National Congress ya China Bw. Zhang Xin na ujumbe wake na maafisa wa serikali aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkaribisha Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza Kaimu Balozi wa Korea Kusini nchini Mhe. Songwon Shin aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimlaki Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. Malika Berak aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimsindikiza baada ya mazungumzo  Balozi wa Ufaransa nchini Mhe. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Kaimu Balozi wa Uturuki nchini Mhe. Yunus Belei aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 23, 2017
  PICHA NA IKULU  0 0

  Na Tiganya Vincent-RS-Tabora

  Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Dkt. Thea Ntara ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora kuhakikisha wanakarabati upya Jengo la utoaji wa huduma ya Upasuaji katika Zahanati ya Ilolanguru lilojengwa chini ya kiwango na Mradi wa Mbola Melenia.Hatua hiyo inalenga kuzuia madhara yanayoweza kujitokeza kwa mgongwa wakati anapata huduma ya upasuaji kutoka madaktari.

  Dkt. Ntara ametoa agizo hilo jana Wilayani Uyui wakati alipokwenda kukagua vifaa vya kisasa vya upasuaji ambavyo vipo katika Zahanati hiyo toka mwaka 2013 lakini havijaanza kutumika kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubovu wa jengo lililojengwa na Mradi wa Mbola na ambalo halina ubora kwa mujibu wa Madaktari.

  Alisema kuwa wajenzi wa jengo hilo waliamua kujenga hata bila kuwashirikisha Wataalamu wa Afya na Wahandisi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wala Mkurugenzi wa Wilaya ya Tabora na hivyo majengo yao mengi kuwa mabovu na ambayo yana nyufa kabla hayajaanza kutumika.

  Dkt. Ntara aliongeza kuwa haiwezekani kwa muda mfupi baada ya kujengwa jengo liwe limeshapasuka na madirisha kuruhusu vumbi kuingia katika Chumba cha upasuaji , jambo ambalo ni hatari kwa mgongwa kupata maambukizi mengine.

  Kufuatia udhaifu wa jengo hilo Katibu Tawala huyo wa Mkoa amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kulifanyia maboresho na ukarabati katika sehemu zenye mapungufu ili lianze kutumika wakati taratibu nyingine za kisheria dhidi ya mjezni zikiendelea kufuatiliwa.

  “Siwezi kukabali kuwa ujenzi wa jengo hilo umegharimu milioni 90 ,wakati lina mapungufu mengi.… hakuna maru maru wala madirisha ya aluminia, sakafu imeshaanza kupasuka wakati jengo halijaanza kutumia ni vema kitu kinachojengwa kikalingana thamani ya fedha halisi” alisema Katibu Tawala Mkoa.

  Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tabora Hadija Makuwani alitoa ufafanuzi kwa Katibu Tawala Mkoa alisema kuwa alishindwa kulipokea jengo hilo baada ya kugundua kuwa limejengwa chini ya kiwango na wakati wa ujenzi ukiendelea hakuna mtaalamu wake hata mmoja alishirikishwa ili kuhakikisha linakuwa imara na bora kwa matumizi ya Zahanati hiyo.

  Alisema kuwa alipokuwa akimwita Meneja Mradi huo wa Mbola Melenia Dkt. Greyson Nyadzi kuja mara nyingi amekuwa akipiga chenga na kumtuma mwakilishi,jambo linaloonyesha kuwa hata yeye anatambua kuwa mradi huo uko chini kiwango.

  Mkurugenzi huyo Mtendaji aliongeza kuwa viongozi wa mradi huo wameshindwa hata kukabidhi vyombo vya usafiri kama vile pikipiki 25, magari madogo na gari kubwa la kubebea mchanga na kuvitumia kwa matumizi binafsi bali ya kuvitoa ili visaidie watendaji wa Halmashauri yake kutoa huduma kwa wananchi.

  Akijibu hoja hiyo Katibu Tawala huyo Mkoa amemwagiza Mkurugenzi Mtandaji wa Wilaya ya Tabora kuwaambia viongozi wa Mbola kurejesha mara moja vyombo vyote vya usafiri ili kuwasaidia Watendaji wa Halmashauri kuwahudumia wananchi.“Haiwezekani watu wachache wang’ang’anie magari ya umma wakati nyie hamna magari ya kutosha …nakuagiza DED mwambie huyo Meneja wa Mbola arudishe magari yote na pikipiki”alisisitiza Dkt. Ntara.

  Aidha ,Katibu Tawala Mkoa wa Tabora ameunda timu ya Wataalam kutoka Mkoani na Katika Halmashauri ya Wilaya ya Tabora kwa ajili kukagua ubora wa majengo yote , vifaa vya upasuaji alivyoweka katika jingo la upasuaji ili kuandaa taarifa kwa ajili ya kupeleka mbele kwa hatua zaidi.

  Alisema kuwa hadi kufikia Ijumaa ya wiki hii taarifa iwe tayari kwa kuwa wananchi wanahitaji sana huduma ya upasuaji kwa karibu kuliko hivi sasa wanapata tatizo na ukimbili katika Hospitali ya Rufaa Kitete.

  Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunini Kamba alisema kuwa jengo linabidi baadhi ya sehemu zivunje ili kupanua mlango wa kuingizia na kumtoa mgonjwa katika chumba cha upasuaji kuliko ilivyo sasa ambao mlango uliojengwa ni mdogo sana haurusu Kitanda cha mgonjwa kupita.

  Aliongeza kuwa ni vema dirisha yakawekwa vizuri na yawe ya aluminia na sio yaliopo sasa ambayo yanaruhusu vumbi kuingia katika chumba cha upasuaji na hivyo kuweza kumsababishia maambukizi mapya mgonjwa wakati madakitari wakiendelea na zoezi la upasuaji.

  Dkt. Kamba aliueleza Uongozi wa Halmashauri hiyo kufanyia maboresho ya mapungufu hayo ili kiweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo.

  0 0

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akiwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya fedha ya Wizara hiyo kwa mwaka 2017/2018 leo  mjini Dodoma. UNAWEZA KUSOMA HOTUBA ALIYOIWASILISHA HAPO CHINI.


  0 0

  Nenda Yusuf,Imetosha na ahsante sana,najua ni maamuzi magumu lakini naamini sasa ni wakati wa akili kubwa kufanya kazi kwa bidii na nina wakati wa kumrudisha kundini Dr Jonas Tiboroha na kuja kuongeza nguvu na Katibu mKuu Mkwassa na hakika tutasogea mbele zaidi
   
  Mengi yemeongewa na kusemwa na naamimi mengine ni ukweli mtupu na mengine ni porojo ila naamini kuna mapungufu makubwa katika uongozi wako uliopita na kubwa zaidi ya yote ni kamati ya utendaji kukosa meno ya nguvu ya kuhoji mambo kadha wa kadha juu ya matumizi na udhamini,mara kadhaa wale waliokuwa wanahoji tumeona wakifanyiwa fitina na kutolewa nje,wapo wakina Aaron Nyanda,Bin Kleb,Seif Magari,Salum Mkemi nk hapo haikuwa sawa,lazima ifike pahali tukubali kutofautiana mawazo ili tuweze kupiga hatua.
   
  Kamati ya utendaji isiyoweza kumuhoji Mwenyekiti na maamuzi binafsi ya kukataa wadhamini na kujipa udhamini mkuu kwa bei aliyopanga yeye haikuwa sahihi.

  Yanga Sc hii ya Sportpesa inamuhitaji @drjonastiboroha na kamati ya utendaji makini ipige hatua na kuachana na kuomba omba as a super brand it will attracts sponsors all over the places,its all about having the right people.

  Yanga needs to be restructured ili kuweza kwenda sawa na speed ya masoko,inahitaji the right person kwa nafasi ya Mkuu wa masoko anayeweza kuja na challenges na kuleta mawazo mapya na ku adopt marketing skills ambazo wenzetu majirani wanafanya mfano Zesco au Sofapaka.
   
  Yanga ina watu wanaoitwa wakuu wa idara za magazetini ambazo hazina tija katika day to day operations na hawa add value kwenye maendeleo ya Yanga.Hii ni timu kubwa sio ya kuomba udhamini,hii ni klabu yenye miaka 82 lets have new ways na kutumia weledi katika uendeshaji.Yanga inahitaji msemaji na kurugenzi ya mawasiliano makini inayoweza kusimamia social media links na kuweza kufanya kazi bega kwa bega na kurugenzi ya masoko kuuza bidhaa za yanga online pia.

  Its time tuwape proffessionals wafanye kazi na kuleta ufanisi...tuache blah blah bana Manji kapita kama walivyopita wakina Gulamali,Verani.

  By Mac Temba - Fan wa Yanga Sc

  0 0


  Na Dotto Mwaibale

  MAOFISA Ugani wametakiwa kuwa na mashamba ya mfano ili kutoa fursa kwa wakulima kujifunza masuala ya kilimo kutoka kwao.

  Mwito huo umetolewa na Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru, Stellah Chirimi wakati akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB). 

  "Ni vema kila ofisa ugani akawa na shamba la mfano ambalo litasaidia wakulima kwenda kwao kujifunza kilimo bora badala ya kuwaacha bila ya kuwasaidia kupitia mashamba hayo ya mfano.

  Katika hatua nyingine Chirimi alisema uzalishaji wa zao la pamba umeshuka kutokana na maofisa kilimo kushindwa kuwafikia wakulima kwa ajili ya kuwapa elimu ya kilimo bora na cha kisasa.

  Alisema kuna kila sababu ya kutolewa elimu kwa wakulima kuhusu mbegu bora ya pamba ambayo ikitumika itaongeza tija katika uzalishaji hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchumi wa viwanda hapa nchini.
   Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus (kulia), akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bushosa, Sengerema mkoani Mwanza leo hii ambayo yameratibiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.
   Mtaalamu wa magonjwa ya pamba kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Stella Chirimi akitoa mada katika mafunzo hayo.
   Ofisa Ushauri wa Kilimo wa Wilaya ya Buchosa, Sospeter Obwago (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Kaimu Ofisa Kilimo wa Wilaya hiyo, Paul Misana. Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon na Mshauri wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus.

  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezitaka benki mbalimbali nchini ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Kilimo kutoa mikopo kwa vikundi vya kilimo ili viweze kupata fedha za kununulia matrekta.

  Amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Sekta ya kilimo ili kwenda sambamba na adhma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.

  Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Mei 23, 2017) wakati alipotembelea kiwanda cha kuunganisha Matrekta URSUS-TAMCO, Kibaha mkoani Pwani.

  Amesema kiwanda hicho kinalenga kuboresha sekta ya kilimo nchini na kuongeza uzalishaji wa malighafi za viwandani kwa kuwa wakulima watakuwa na zana za kisasa.

  Aidha, amevitaka vyuo vya kilimo nchini kununua matrekta hayo kwa lengo la kufundishia wanafunzi wake ili wanapohotimu wawe na uwezo wa kutumia zana hizo vizuri na kwenda kuwasaidia wakulima katika maeneo yao.

  Pia Waziri Mkuu ametoa wito kwa Halmashauri nchini kuendelea kupanga matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo ya kilimo, uwekezaji, makazi, biashara na huduma za jamii, hivyo kuepuka migogoro ya ardhi kwa siku zijazo.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema wataunganisha matrekta 2,400,  harrow 2,400 na majembe 2,400 katika mradi huo wa kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO ikiwa ni mkataba wa awali.

  Amesema kiwanda hicho kina wafanyakazi 27 kwa hatua za mwanzo. Aidha, idadi hiyo itaongezeka kutokana na mahitaji ambapo baadhi ya wafanyakazi watapewa mafunzo nchini Poland na watakaporudi watakuwa wakufunzi wa watakaoajiriwa.

  Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kiwanda hicho kimeazima wafanyakazi wengine wakiwemo watano kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, 10 kutoka vyuo mbalimbali vya ufundi nchini, wawili kutoka CAMARTEC ambao wanashirikiana na wataalamu 10 kutoka URSUS kuunganisha matrekta.

  Bw. Mkucha amesema wafanyakazi 10 kutoka Tanzania wanatarajiwa kwenda nchini Poland kufanya mafunzo mahsusi na watakaporejea watakuwa wakufunzi kwa watumishi wengine watakaoajiriwa katika kiwanda hicho.

  Amesema mbali na ujenzi wa kiwanda hicho cha kuunganishia matrekta ya URSUS, mradi unahusisha uanzishwaji wa vituo vinane kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja na kuuzia matrekta, zana na vifaa vingine.

  Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Everest Ndikilo amesema miongoni mwa changamoto zinazoikabili sekta ya viwanda mkoani humo ni pamoja na kukatika kwa umeme, hivyo ameliomba Shirika la Umeme Tanzania (TANECO) kuongeza vituo vya kupozea umeme.

  Awali Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mheshimiwa Charles Mwijage amesema kwa sasa nchini kuna viwanda vikubwa 393 kati yake 84 viko mkoani Pwani, ambapo amewaomba viongozi wa mkoa huo kutenga maeneo kwa ajili ya wanawake na vijana kuanzisha viwanda vidogo.

  Mara baada ya kutembea kiwanda cha kuunganisha matrekta URSUS-TAMCO Waziri Mkuu alitembelea eneo la uwekezaji la Kamal (Kamal Indusrial Estate) lililoko katika Kata ya Kerege wilayani Bagamoyo.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMANNE, MEI 23,2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017.Kulia kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akikagua matrekta aina ya URSUS yanayounganishwa katika karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Wengine pichani kutoka kulia kutoka kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NDC Mlingi Elisha Mkucha, Waziri wa Viwanda, Biahara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evaresti, Ndikilo na kulia kwake ni Mbunge wa Kibaha mjini Silvestry Koka.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama moja kati ya mtrekta aina URSUS yanayounganishwa kwenye karakana ya TAMCO mjini Kibaha Mei 23, 2017. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarest Ndikilo akizungumza wakati Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerege Bagamoyo Mei 23, 2017.

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka baada ya kutembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrual Estate lililopo Kerege, Bagamoyo Mei 23, 2017
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya viongozi, wabunge na wananchi waliohudhuria wakati alipotembelea eneo la uwekezaji la Kamal Industrial Estate lililopo Kerenge, Bagamoyo Mei 23, 2017. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).

  0 0

  Darasa lililokabidhiwa na Uongozi wa kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Usharika wa Ubungo kwa Uongozi wa Manispaa ya ubungo mbele ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg john Lipesi Kayombo
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisalimiana na Mchungaji kiongozi wa kanisa La Kiinjili la Kilutheli Tanzania Mchungaji Goodlisten Nkya alipozuru katika ofisi za kanisa hilo kwa ajili ya kikao na Uongozi wa (KKKT) Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Muonekano wa Majengo ya Shule ya Msingi Ubungo Plaza yatakayofanyiwa marekebisho mara baada ya ujenzi wa Madarasa nane kukamilika
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza akizungumza na Afisa Mtendaji wa Kata ya Ubungo,Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa National Housing, Waalimu wa Shule ya msingi ubungo Plaza sambamba na viongozi wengine mara baada ya kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzuru kwa katika ofisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo leo tarehe 23, Mei 2017 
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akikagua majengo ambayo yamejengwa na kanisa la KKKT yakiwa yameingia katika eneo la shule ya Msingi Ubungo Plaza sambamba na viongozi wa kanisa hilo baada ya kikao cha pamoja na Uongozi wa Kanisa hilo Usharika wa Ubungo. Leo tarehe 23, Mei 2017.

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akizungumza wakati wa kikao na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa. Leo tarehe 23, Mei 2017 
  Muonekano wa ukuta wa kanisa la KKKT Usharika wa Ubungolinalotakiwa kuvunjwa
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya viongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo wakati wa kikao cha pamoja cha maridhiano ya utatuzi wa mgogoro wa Eneo la ardhi. Leo tarehe 23, Mei 2017


  Na Mathias Canal, Dar essalaam

  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Leo tarehe 23, Mei 2017 amefanya mazungumzo na Uongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo ulioongozwa na Mchungaji kiongozi wa usharika huo, Katibu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki ya Pwani, Kiongozi wa Kamati ya Ujenzi wa kanisa hilo na baadhi ya wazee wa kanisa.

  Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za usharika wa KKKT Ubungo kilikuwa na Agenda ya kujadili nanma bora ya uvunjaji wa Ukuta wa eneo la kanisa hilo ambao umeingia katika eneo la Shule ya Msingi Ubungo Plaza Jambo linalopelekea Kushindwa kuanza ujenzi wa madarasa nane mapya kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo ambao kwa sasa wanasoma katika madarasa ambayo majengo yake si rafiki kwa ajili ya usomaji.

  Alisisitiza kuwa ujenzi huo utakuwa maalumu kwa ajili ya kutekeleza agizo la Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Kisare Makori alilolitoa Mei 19, 2017 wakati wa mkutano wake na walimu wa shule hiyo sambamba na wananchi wa Mtaa huo ukiwajumuisha Afisa mtendaji wa Kata na wajumbe wa mitaa.

  MD Kayombo alisema kuwa baadhi ya shule katika Manispaa ya Ubungo hazifanyi vizuri katika matokeo ya mitihani ya taifa kutokana na uduni wa miundombinu ikiwemo madarasa Jambo ambalo pia limepelekea Manispaa ya Ubungo kuona umuhimu wa kuboresha miundombinu ili kuwa rafiki kwa wanafunzi kujifunzia. 

  Alisema kuwa jukumu la viongozi wanaomuwakilisha Rais Magufuli katika ngazi za Mitaa, Kata, Tarafa, Wilaya, Mikoa na Taifa ni kusimamia na kutekeleza matakwa ya jamii kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi bila kumuonea mtu yeyote. 

  Aidha ameupongeza uongozi wa kanisa hilo kwa ushirikiano waliouonyesha na kukubali kuwa na maridhiano ya pamoja kuhusiana na namna bora ya kutatua mgogoro huo ambapo pia amewaupongeza Uongozi wa KKKT Usharika wa Mabibo kwa kuamua kutoa moja ya jengo lao kwa ajili ya shule hiyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha miundombinu ya shule ili kukuza ufanisi wa elimu nchini. 

  Kwa upande wake mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Ubungo Mch Goodlisten Nkya amesifu uongozi wa Mkurugenzi Kayombo kwa kukubali kufanya maridhiano sambamba na kukubali kupokea jengo mojawapo la kanisa hilo walilotoa sadaka ambalo litatumiwa na shule ya Msingi Ubungo Plaza kama ofisi ya walimu ama darasa kwa kadri itakavyoamuliwa na uongozi wa shule. 

  Alisema kuwa adhma ya kanisa hilo ni kuona maendeleo endelevu ya elimu nchini Tanzania kwa manufaa ya watanzania wote sambamba na kupongeza ushirikiano wanaoupata kutoka serikalini na katika Uongozi wa Shule hiyo.

  0 0

  Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kuepuka ajali zisizo za
  lazima kwani tangu mwaka 2008 hadi Mei 2017 zimetokea ajali 125 kwenye
  migodi yenye leseni na vifo ni 213.

  Ajali zilizotokea kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo wasio na leseni
  nchini (maeneo ya mifumuko ya uchimbaji madini) katika kipindi hicho
  ni 56 na kusababisha vifo vya wachimbaji 140.

  Kamishna wa madini nchini, mhandisi Benjamin Mchwampaka aliyasema hayo wakati akizungumza na mameneja na wamiliki wa migodi mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

  Mhandisi Mchwampaka alisema ajali nyingi kwenye migodi ya wachimbaji
  wadogo zinasababishwa na uzembe, kwani kwa mwaka huu pekee hadi Mei 15 ajali zilizotokea ni 11 na kusababisha vifo 26.

  Alisema kwenye machimbo ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani,
  ajali zilizotokea kwa wachimbaji wadogo kwa kipindi cha 2008/2017 ni
  31 na wachimbaji wadogo waliopoteza maisha ni 40.

  Alisema uchambuzi wa takwimu za ajali hizo unaonyesha kuwa vyanzo
  vikubwa ni kuangukiwa na vifusi kwa kukatika kwa ngema, kulipukiwa na
  baruti, kukosa hewa, kuteleza na kuangukia mgodini.

  Alisema hawatafumbia macho ajali za uzembe kwenye migodi na
  wataifungia mara moja na kumchukulia hatua meneja na mmiliki,
  haitafunguliwa hadi mkaguzi mkuu wa migodi atakapojiridhisha.

  “Tunapaswa kuhakikisha uchimbaji unafanyika kwa usalama na kauli mbiu
  ya wachimbaji wadogo nchini iwe usalama kwanza, familia zetu
  zinatuhitaji na Taifa linatuhitaji,” alisema mhandisi Mchwampaka.

  Mkaguzi mkuu wa migodi nchini, mhandisi Ally Samaje alisema lengo la
  mafunzo hayo ni kupunguza matukio ya ajali zinazoweza kuepukwa na
  wachimbaji wadogo hivyo mafunzo hayo yatawajengea uwezo.

  Mhandisi Samaje alisema kila mmiliki wa leseni ya madini anazingatia
  maelekezo yote waliyoyatoa kwa kufanya kazi zao kwa usalama, kwani
  ajali hizo zimesababisha vifo na vilema vya maisha.

  “Kamishna wa madini ameshatoa maelekezo ya kuimarisha masuala ya
  usalama, afya na utunzaji mazingira hivyo wamiliki wa migodi wawape
  majukumu mameneja wayasimamie hayo,” alisema Samaje.

  Mmoja kati ya wamiliki wa migodi Hamis Juma aliishukuru wizara ya
  Nishati na Madini kwa kuendesha mafunzo hayo kwa mameneja na wamiki wa migodi kwani elimu hiyo itasaidia kupunguza ajali mgodini.

  “Kupitia elimu hii tumekumbushwa wajibu wetu na pia mameneja na
  tunatarajia watatekeleza hayo kwa faida ya wachimbaji wenyewe na jamii
  inayoishi maeneo yanayozunguka migodi yetu,” alisema Juma.
  Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenyemafunzo ya usalama migodini.
  Kamishna wa madini Tanzania, mhandisi Benjamin Mchwampaka akizungumza na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, kuhusiana na usalama kwenye migodi yao.
  Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Chama cha wachimbaji wadogo wa Madini Mkoani Manyara, (Marema) na wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, wakiwa kwenye
  mafunzo ya usalama migodini.

  0 0


  Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serilkali nchini CAG ameitunuku hati safi ya hesabu na matumizi sahihi ya Fedha za Umma Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi na kujiridhisha na matumizi yaliyozingatia taratibu, Sheria na kanuni za fedha za Umma kwa mwaka wa Fedha wa 2015 – 2016.

  Taarifa ya Afisa habari na Mawasiliano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwa vyombo vya habari Bw. Ndimmyake Mwakapiso, imefafanua kuwa CAG ametunuku hati hiyo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, baada ya kufanya ukaguzi wa kawaida wa kila mwaka kwa mujibu wa sheria za fedha zinazompa mamlaka ya kukagua hesabu za mamlaka za serikali za Mitaa.

  Mwakapiso, ametanabaisha baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa kwenye ukaguzi huo, kuwa ni pamoja na ujenzi wa miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotumika, uzingatiaji wa sharia na taratibu za Manunuzi ya tenda, matumizi mazuri ya fedha za miradi ya maendeleo na zile za zatumizi ya kawaida sanjari na uandaaji wa taarifa za fedha unaozingatia viwango vya kimataifa( IPSAS)

  "Huu ni mwaka wa 05 mfululizo Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi inapata hati safi ya CAG. Aidha kwa mujibu wa kanuni za ukaguzi, Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali mara baada ya kukamilisha ukaguzi wake kwa mwaka wa fedha husika, anaweza kutoa moja kati ya hati zifuatazo Hati safi, Hati yenye mashaka au Hati chafu",alisema .
  Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe kutoka makitaba ya Kitengo cha habari.

  0 0

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimkaribisha mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar  na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akizungumza na mgeni wake Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. Sarah Cooke,alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar

  Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi. SARAH COOKE, amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe PAUL MAKONDA na kufanya nae mazungumzo yenye lengo la kuongeza na kuimarisha Ushirikiano uliopo baina ya jiji la Dar es salaam na London, nchini Uingereza.

  Katika mazungumzo yao, Mhe MAKONDA na Bi. COOKE wamekubaliana kuongeza kasi ya Ushirikiano baina ya majiji makubwa mawili Dar es salaam Tanzania na London nchini Uingereza, makubaliano ambayo yatasaidia kupatikana kwa vifaa vya kisasa vya kuzuia na kupambana na majanga kama vile moto na mafuriko, ambapo Mhe MAKONDA ameomba kupatiwa magari ya kisasa ya shughuli za kuzima moto na uokoaji.

  Mhe MAKONDA pia ameomba kusaidiwa vifaa maalum vya UTAMBUZ*I wa mifumo ya teknolojia ya kamera za kisasa zitakazofungwa *barabarani kwa ajili ya kusaidia USALAMA wa magari, raia na mali zao mifumo ambayo inafanya kazi katika jiji la London nchini Uingereza, hatua itakayokwenda sambamba na ujengewaji UWEZO kwa maofisa wa polisi wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya mifumo hii.

  Katika kukabiliana na changamoto ya MIGOGORO ya ARDHI mkoani Dar es salaam, Mhe MAKONDA ameomba kusaidiwa kuwajengea uwezo maafisa ARDHI na Mipango miji wa Mkoa wa Dar es salaam katika matumizi ya kisasa ya upimaji na upangaji ardhi, mafunzo ambayo yatakwenda sambamba na upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya kupima ardhi, jambo litakalosaidia kuondoa KERO ya upatikanaji wa HATI pamoja na vibali vya UJENZI Mkoa wa Dar es salaam.

  Katika mazungumzo hayo, Mhe MAKONDA na Bi. COOKE wamejadili suala la uanzishwaji wa JIJI la FIKRA (brain storming center ) kwa ajili ya kuwakutanisha vijana wabunifu kama ilivyo kwa Tech City Uingereza.

  Katika kuhitimisha mazungumzo yao, Mhe MAKONDA na Bi. COOKE kwa pamoja wamekubaliana kuzikutanisha timu za wataalamu kutoka London na Dar es salaam za kukabiliana na Majanga haraka iwezekanovyo.

  Bi. COOKE, kwa upande  wake amefurahishwa na jinsi Mkuu wa Mkoa anavyopambana na vita ya dawa za kulevya ambayo imeathiri nguvu kazi kubwa sana katika jiji la Dar es salaam na kumuhakikishia kuwa Serikali ya Uingereza inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.

  Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
  23/05/2017.

  0 0


  Mkurugenzi mkuu wa mfuko Gepf , Daudi Msangi akizungumza leo na vyombo mbalimbali kuhusu, mkutano wa wadau wa mfuko huo ambao  utashirikisha wadau zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini,,mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa  Naibu waziri wa fedha na mipango  Ashatu kijaja  kufungua mkutano  huo wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (Gepf) utakaofanyika may 25 jijini Arusha.
   Mwenyekiti wa bodi Ya wadhamini, Joyce shaidi akiongea na vyombo vya habari ambapo amesema kuwa, mfuko huo unatarajia kuwekeza kiasi cha kiasi cha shs bilioni moja na milioni mia sita katika kiwanda cha kutengeneza mashine cha Kilimanjaro machine tools kilichopo Mkoani kilimanjaro Kwa ajili ya kujenga kinu kidogo cha kufua vyuma.
  Meneja masoko, Edgar shumbusho amesema kuwa, mfuko huo unalenga zaidi kutumia radio za jamii katika kuwafikishia wananchi wa vijijini elimu ambapo wamepata mafanikio makubwa Sana kupitia mfumo huo. 
   Kushoto ni Meneja wa mfuko huo Mkoa wa Arusha,Clement Saning'o akifatia kwa ukaribu mkutano na waandishi wa habari 
   Meneja wa mfuko huo Magraret Mrina wa wilaya ya Ilala akijitambulisha kwa waandishi wa habari
   Kulia ni Afisa masoko wa mfuko huo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Saalam akiteta jambo na Adam Hamza afisa masoko
  Kushoto ni meneja kutoka mfuko huo Ramadhani Sossora kutoka Mbeya akifurahia jambo na mkurugenzi wa Key Media Arusha Sarah Keiya mara baada ya kumaliza mkutano na waandishi wa habari
   Meneja wa mfuko huo kutoka Mtwara Deogratias Kakoko akijitambulisha kwa waandishi wa habari
  Naibu waziri wa fedha na mipango  Ashatu kijaja anatarajiwa kufungua mkutano wa nane wa wadau wa mfuko wa mafao ya mstaafu (Gepf) utakaofanyika may 25 jijini Arusha. 

  Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo, Daudi Msangi amesema kuwa, mkutano huo utashirikisha wadau zaidi ya mia tatu kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini. 

  Amesema kuwa,katika mkutano huo wanatarajia kujadili Mada mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa wanachama pamoja na kuwasilisha taarifa za utendaji Kwa mwaka 2015/2016.

  Msangi ameongeza kuwa, ndani Ya siku hizo mbili za mkutano mbali na kujadili taarifa za wanachama wanatarajia kutoa misaada wa mashuka Kwa watoto na wanawake wajawazito katika hospital ya dareda iliyopo wilayani babati Mkoani Manyara. 

  Hata hivyo ameongeza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa misaada Kwa kuangalia mahitaji ya jamii popote nchini na kuweza kusaidia kulingana na mahitaji hayo. 

  Mwenyekiti wa bodi Ya wadhamini, Joyce shaidi amesema kuwa, mfuko huo unatarajia kuwekeza kiasi cha kiasi cha shs bilioni moja na milioni mia sita katika kiwanda cha kutengeneza mashine cha Kilimanjaro machine tools kilichopo Mkoani kilimanjaro Kwa ajili ya kujenga kinu kidogo cha kufua vyuma. 

  Amesema kuwa,uwepo wa kinu hicho utasaidia kuinua uzalishaji wa kiwanda hicho, huku kwa sasa watawekeza kinu kidogo ambapo kwa baadaye wataendelea na kuwekeza kinu kikubwa. 

  Kwa upande wa meneja masoko, Edgar shumbusho amesema kuwa, mfuko huo unalenga zaidi kutumia radio za jamii katika kuwafikishia wananchi wa vijijini elimu ambapo wamepata mafanikio makubwa Sana kupitia mfumo huo. 

  Ameongeza kuwa, mfuko huo umekuwa ukitoa mafao mbalimbali ikiwemo fao la msaada wa mazishi Kwa wanachama wake, na sambamba na kutoa elimu kwa watoto wa wanachama. 

  Aidha kauli mbiu Ya mkutano huo ni hifadhi ya jamii kwa wote inawezekana katika uchumi wa viwanda.

  0 0


  0 0


  0 0  0 0

  Mashindano ya kombe la Standard Chartered yaliyokuwa yanafanyika nchini Uingereza yamemalizika na kombe hilo kutwaliwa na timu ya nchini Singapore. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kuwasili timu ya Azania iliyowakilsiha nchi za Afrika ya Mashariki, Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga amesema timu ya Azania ilikwenda Uingereza kushindana kwenye mashindano ya “Standard Chartered-Road to Anfield” iliyokuwa inahusisha wateja wa benki hiyo. Timu zilizoshiriki kwenye mashindano hayo zilikuwa ni timu nane kutoka Singapore, Uingereza, India, Nigeria, Botswana, Honk Kong, Korea na Tanzania.
  Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (nguo nyeusi) akiwasili na Wachezaji wa Timu ya Azania katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.

  Katika michuano hiyo timu ya Azania iliweza kutinga nusu fainali ambapo ilicheza na Uingereza na kutolewa kwa mikwaju ya penati. Timu ya Singapore iliibuka mabingwa wa kombe Standard Chartered –Road to Anfield kwa mwaka 2017. Mariam alisema timu hiyo imefanya vizuri kwenye mashindano hayo japo hawakufanikiwa kutwaa kombe hilo mara baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo. Alisisitiza wao kama Benki ya Standard Chartered Tanzania hawajakata tamaa na hii ilikuwa ni fursa nzuri kwa vijana kuonesha vipaji vyao ili kufikia malengo waliyojiwekea. 
   Na pia ameipongeza timu ya Azania kuiwakilisha vyema Tanzania kwa kuwa ni mara ya kwanza kuingia kwenye mashindano hayo na pia wamejitahidi kupigana mpaka kufikia kuingia nusu fainali ya mashindano hayo. Nahodha wa timu ya Azania, Khalid Sultan Said ameishukuru benki ya Standard Chartered Tanzania kwa kuona umuhimu wa michezo hapa nchini na wameweza kujifunza mengi kwenye michuano hiyo iliyokuwa ikiendeshwa nchini Uingereza ambapo timu yao ilitolewa kwenye nusu fainali. Lakini wao wanaamini hapa ni mwanzo na watapigana mpaka siku kombe liweze kutua hapa nchini. 
   Wachezaji wa timu ya Azania wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza. 
   Meneja Uhusiano wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Mariam Sezinga (wa tatu kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wachezaji wa Timu ya Azania mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam wakitokea nchini Uingereza kwenye mashindano ya kombe la Standard Chartered-Road to Anfield 2017.
   Wachezaji wa Timu ya Azania wakiwasiliana na ndugu jamaa na marafiki mara baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakitokea nchini Uingereza.

older | 1 | .... | 1242 | 1243 | (Page 1244) | 1245 | 1246 | .... | 1898 | newer