Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

KAIMU JAJI MKUU WA TANZANIA AKAMILISHA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA KWA KUONGEA NA WATUMISHI WA MAHAKAMA WA KANDA HIYO

$
0
0


 A 4
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, akiongea na Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama (hawapo pichani), katika maongezi yake na Watumishi hao Mhe. Jaji Prof. Juma amewataka na kuwasisitiza Watumishi hao kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili ikiwa ni pamoja na kuwa na lugha nzuri kwa Wateja/Wananchi wanaowahudumia. kulia ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha na kushoto ni Mhe. Rumisha, Naibu Msajili-Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha.
 A 5
 Mahakimu na Watumishi wengine wa Mahakama wakimsikiliza Mhe. Kaimu Jaji Mkuu alipokuwa akizungumza nao.
 A 7
Mtendaji, Mahakama Kuu-Arusha, Bw. Edward Mbara akiwasilisha taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo mbele Mhe. Kaimu Jaji Mkuu na Watumishi wa Mahakama, katika taarifa yake Bw. Mbara alikiri kuwa Kanda ya Arusha inakabiliwa na changamoto kubwa ya miundombinu chakavu ya majengo ya Mahakama n.k (picha na Mary Gwera,Arusha)A
Kaimu Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Mhe. Kamugisha akimsomea taarifa ya hali ya utendaji kazi wa Mahakama katika mkoa huo. Lengo la ziara ya Mhe. Kaimu Jaji Mkuu katika Kanda hiyo ni kujifunza na kuona hali halisi ya mazingira ya kazi na utekelezaji wa majukumu.
 A 1
Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Rumisha (wa kwanza kulia) akimuonesha Mhe. Kaimu Jaji Mkuu, moja ya kumbi za Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha pindi alipokuwa akikagua ofisi mbalimbali za Mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu katika Kanda hiyo.
 A 2
Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Juma akiwa katika Kompyuta Mpakato akikagua Mfumo wa Kuratibu takwimu za Mashauri kwa njia ya Kielektroniki (JSDS) kuhakikisha kama inafanya kazi ipasavyo, pembeni ni Afisa TEHAMA, Mahakama Kuu-Kanda ya Arusha, Bw. Athuman 
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisamiliana na Watumishi wa Mahakama, Kanda ya Arusha alipowasili katika viwanja vya Mahakama Kuu-Arusha kukamilisha ziara yake ya siku mbili mkoani humo.



CCM Z’BAR YAWAFARIJI WALIOATHIRIWA NA MAFURIKO.

$
0
0

Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma akipokea maelezo kutoka kwa viongozi wa mtaa akiwemo sheha wa shehia ya Tomondo, Mohamed Omar katika eneo la Ziwa maboga ambapo zaidi ya nyumba 200 zimeathiriwa na mvua za masika zinazoendelea kunyesha.
Nyumba mbali mbali zilizoathiriwa na maji ya mvua katika eneo la Tomondo Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Nyumba zilizovamiwa na maji katika eneo la Meli nne Makaburini Unguja.
Katibu wa Tawi la CCM Tomondo, Hassan Kipanga Abdalla akimweleza Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar hali ya waakazi wa shehia hiyo kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Saadala akiwafariji wananchi wa eneo la Mwanakwerekwe Meli nne, waliopata maafa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa.
Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala akimfariji mmoja wa wananchi ambaye nyumba yake imeporomoka kutokana na mvua za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa nchini, uko Fuoni Migombani Zanzibar.

……………………………………..

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

ZAIDI ya Nyumba 300 katika maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi zimeathiriwa na Mvua za masika zinazoendelea kunyesha hivi sasa.

Akizungumza katika mtaa wa ziwa maboga sheha wa shehia ya Tomondo, Bw. Mohamed Omar Said alisema zaidi ya nyumba 200 katika eneo hilo zimeathiriwa na mvua kwa kujaa maji na zingine kuporomoka.

Bw. Said alifafanua kwamba baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamehama katika makaazi yao na kuomba hifadhi katika maeneo mengine yaliyokuwa salama, huku idadi ya nyumba zinazoathiriwa na mvua hizo zikiendelea kuongezeka kadri mvua zinavyioendelea kunyenyesha.

Mbali na maeneo hayo pia katika mitaa ya Meli nne, Fuoni janga mizini na Fuoni Migombani kuna nyumba zaidi ya 100 zimeathiriwa na mvua hizo.

Akizungumza juu ya athari hizo, Mjumbe wa sheha wa shehia ya kibondeni, Bi. Zuhura Ame alisema hali za baadhi ya wananchi waliopata maafa hayo sio nzuri hivyo wanahitaji msaada wa dharura.

Alisema kwamba licha ya viongozi wa majimbo hasa Wabunge, wawakilishi na madini baadhi yao tayari wameanza kutoa msaada na wengine ndio wanajipanga kufika kwa ajiri ya kuwafariji wananchi lakini bado panahitajika nguvu za pamoja baina ya wananchi, vyama vya kisiasa na serikali ili kuinusuru nchi kuingia katika maafa makubwa.

Naye Mkaanzi wa Mwanakwerekwe, Mwajuma Salum aliomba serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara inayohusika na masuala ya Miundombinu kutoa kipaumbele cha kujenga madaraja makubwa na yenye viwango katika maeneo mbali mbali nchini ili kuepusha hasara inayotokana na mvua hizo kila mwaka.

“ Tumesikia juzi tu serikali yetu imetangaza bajeti ya mwaka inayofikia Trioni moja, hivyo tunaomba kama inawezekana baadhi ya fedha zitumike katika uimarishaji wa miundombinu yetu kwani wengi tunateseka kwa sasa, mfano pale Mwanakwerekwe Gari za Shamba kuja mjini ni tabu kwani pale katika Bwawa la maji hakupitiki.”, alisema Mwajuma.

Alisema licha ya serikali kufanya ziara katika maeneo hayo bado baadhi ya wananchi hawana makaazi ya kuishi hivyo wanaiomba serikali iwapatie misaada ya dharura ili nao wapate huduma muhimu kwa kipindi hichi kigumu.

Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” aliwaagiza viongozi wa Serikali za Mitaa Zanzibar kuacha tabia ya kuruhusu uuzaji wa viwanja na ujenzi katika maeneo hatarishi hasa mabondeni na sehemu zinazotwaama maji ili kuepuka athari za mafuriko zinazoweza kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Maelekezo hayo aliyatoa katika Mtaa wa Tomondo Ziwa maboga na maeneo mengine wakati katika ziara yake ya kuwafariji wananchi waliopata athari za mafuriko katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Alisema wananchi wanatakiwa kujenga utamaduni wa kujilinda dhidi ya maisha yao kwa kuchukua tahadhari ya kutoishi katika maeneo wanayojua kuwa ni hatari juu ya afya na maisha yao.

Aliahidi kwamba CCM kwa kushirikiana na serikali inaendelea kutafuta ufumbuzi wa kuwasaidia wananchi waliopata athari hizo kwa Unguja na Pemba.

“ Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi natoa pole sana kwa wananchi wetu wa Zanzibar kwa Unguja na Pemba walioathiriwa na mvua hizi zinazoendelea kunyesha hivi sasa, kwa upande wa CCM tutaendelea kuwa nanyi kwa kutoa msaada wa Ari na Mali ili kuhakikisha mnarudi katika hali yenu ya kawaida.

Pia nakuombeni wananchi ifikie wakati na sisi tuisaidie serikali yetu kwa kuepuka kuishi ama kununua sehemu ambazo tunajua kwamba hazifai kuishi binadamu wakati mvua zinapoanza kunyesha.”, alisema Dkt. Mabodi na kuongeza kwamba CCM itaendelea kuwa karibu zaidi na wananchi kwa lengo la kuwapunguzia changamoto hizo.

Dkt. Mabodi aliishauri serikali kuchukua hatua za haraka za kurekebisha miundo mbinu ya barabara, maji na umeme kwa baadhi ya maeneo yaliyokubwa na mafuriko hayo ili wananchi waendelee kupata huduma muhimu za kijamii.

Aidha alitoa wito kwa wananchi ambao kwa sasa makaazi yao bado yapo salama kujitolea kwa kuwasaidia wenzao waliopata maafa huku Chama kwa kushirikiana na serikali wakitafuta njia mbadala za kusaidia katika maeneo hayo.

Sambamba na hayo aliitaka Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kutembelea katika maeneo yaliyopata athari hizo kwa kugawa dawa za kutibu maji ya kunywa sambamba na kutibu visima ambavyo maji yake hayo salama kwa lengo la kuwanuru wananchi wasipate maradhi ya miripuka kwa kipindi hichi cha kuelekea katika Mwezi wa Ramadhani.

Alisema sululisho la kumaliza tatizo la maafa hayo yanayotokea kila mwaka ni lazima wananchi waache kujenga katika mitaro ya kusafirisha maji, hali inayosababisha maji hayo kukosa njia za kupita na kuwaathiri wananchi wengine wasiokuwa na hatia.

Naibu Katibu Mkuu huyo, Dkt. Mabodi katika ziara hiyo amefuatana na uongozi wa Mkoa wa Magharibi na Wilaya ya Dimani akiongozwa na Mwenyeji wake Mwenyekiti wa Mkoa huo , Yussuf Mohamed Yussuf na alitembelea maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi mengi yakiwa katika Wilaya ya Maghatibi ‘’B” ambayo ni Tomondo, Mwanakwerekwe Sokoni, Mwanakwerekwe Meli nne, Fuoni Migombani na Fuoni Chunga.

Mbunge Prof Maji Marefu ashiriki kuokoa wananchi wake huko Korogwe kufuatia mvua kubwa kunyesha

$
0
0
  Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani maarufu kama Prof Maji Marefu akitoa msaada wa kuwaokoa wananchi wa Jimbo lake kwenye mafuriko yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mengi ya Mji wa Korogwe na maeneo mengine mengi ya nchi.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani akijadiliana jambo na baadhi ya wananchi wake.






JPM AWAHAKIKISHIA MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI WAFANYABIASHARA WA AFRIKA KUSINI.

$
0
0
  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

RAIS Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wafanyabiashara na wawekezaji wa Afrika Kusini kujitokeza na kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ina mazingira yaliyo salama, bora na fursa wezeshi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wafanyabiashara wa Tanzania na Afrika Kusini mkutano wa wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliojadili fursa na vivutio vya uwekezaji katika mataifa hayo.

Rais Magufuli amesema Tanzania ina vivutio mbalimbali vya uwekezaji vyenye kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Afrika Kusini kuwekeza katika sekta yoyote nchini kwani uwekezaji huo una uhakika wa kuzaa matunda mazuri.

 “Napenda kuwahakikishia wafanyabiashara wanaotaka kuwekeza Tanzania kuwa nchi hii ina amani tangu tupate uhuru mnamo mwaka 1961,ina mazingira mazuri ya kibiashara,utulivu wa kiasiasa pamoja na uchumi unaotabirika hivyo nawasihi wafanyabiashara wa Afrika Kusini kuwekeza nchini kwetu,”alisema Dkt. Magufuli.

 Ameongeza kuwa Tanzania ina soko kubwa la kuuzia bidhaa na kutoa huduma mbalimbali kwani tumezungukwa na nchi nane ikiwemo ya Burundi, Congo, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia kwa kiasi kikubwa zinashirikiana na Tanzania katika kufanya biashara za kimataifa hivyo wakiwekeza Tanzania watapata soko la nchi nyingi.

Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusini. Jacob Zuma amesema kuwa wamekubaliana na Rais Magufuli kukuza ushirikiano hasa wa kiuchumi wa nchi zote mbili ikiwa ni moja ya kichocheo kitakachosaidia kuleta faida na kutunza ushirikiano wa kihistoria uliopo baina ya nchi hizo mbili.

“Hadi sasa kuna zaidi ya Makampuni 200,000 kutoka Afrika Kusini ambayo yamewekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali zikiwemo za kilimo, mawasiliano, sekta za fedha, ujenzi, madini na utalii lakini kwa kuwa Tanzania ina mazingira mazuri ya kuwezesha ukuaji wa uchumi tunaamini kampuni hizo zitaongezeka,”alisema Rais Zuma.

Ametoa rai kwa nchi hizo mbili kuacha kujikita katika bidhaa pekee kwani sio endelevu na haitengenezi ajira za uhakika na badala yake kuwekeza nguvu katika uzalishaji. 
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wafanyabiashara wa nchi za Afrika Kusini na Tanzania uliofanyika leo Alhamisi Mei 11, 2017 Jijini Dar es Salaam, ambao ulijadili fursa mbalimbali za uwekezaji na biashara zilizopo baina ya Mataifa hayo.

HIVI NDIVYO VIGEZO VINAVYOTUMIKA KATIKA KUZIPA HADHI HOTELI

$
0
0
Na Jumia Travel Tanzania

Hivi ushawahi kujiuliza ni kwanini hoteli fulani inatajwa kuwa ni ya nyota tatu, nne au tano? Najua itakuwa ni vigumu kuelewa kama haupo katika tasnia ya masuala ya hoteli au utalii mpaka upatiwe ufafanuzi wa kutosha.
Hivi karibuni Serena Hotel ya jijini Dar es Salaam ilifanikiwa kupewa hadhi ya kuwa hoteli ya nyota tano katika hafla ambayo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe. 

Umuhimu wa kuzipatia hadhi hoteli husaidia sana kuchochea ushindani katika biashara hasa kwa upande wa uboreshaji wa huduma.   

Kupitia makala haya Jumia Travel imekukusanyia vigezo ambavyo mara nyingi huzingatiwa mpaka hoteli kupewa hadhi fulani.  

Nyota moja. Mara nyingi hoteli hizi humilikiwa na watu binafsi katika utoaji wa huduma za malazi kwa wateja. Huwa ni ndogo na za ukubwa wa saizi ya kati zikipatikana katika maeneo ambayo gharama za maisha ni ya kawaida kabisa. 

Kikubwa kinachozingatiwa ni kuweza kukidhi mahitaji ya msingi kwa gharama nafuu. Baadhi ya huduma zinazopatikana ni pamoja na mapokezi, kiti, meza, simu, luninga vyumbani, bafu na usafi wa kila siku. Ni chache zenye migahawa kwa ajili ya  chakula, mbali na hapo huduma na mhudumu kwa vyumbani huwa hakuna. 

Kwa hapa nchini Tanzania nyingi huwa ni nyumba za kulala wageni. Mfano wa hoteli  hizi ni kama vile Perfect Hotel na Sharon House Hotel.   

Nyota mbili. Hoteli za namna hii hazina tofauti sana za nyota moja kwani nazo zinapatikana kwenye maeneo ambayo gharama za maisha ni za kawaida pia. 

Mazingira na vitu vyake kama vile samani ni vya kawaida lakini vikiwa katika hali nzuri na safi. Asilimia kubwa huwa na huduma ya kifungua kinywa lakini si mgahawa. Pia zipo karibu na maeneo ambayo mteja anaweza kupata chakula kwa gharama nafuu. Wateja wanaweza kwenda muda wowote ingawa kuna ukomo ikifika muda fulani kama vile labda kuanzia saa tano usiku. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Golden Coins Hotel  na Four Points Hotel.  

Nyota tatu. Kwa kawaida hoteli za aina hii hutoa huduma ya vyumba vizuri, vikubwa vikiwa na mapambo ya kuvutia. 

Hupatikana katika maeneo makuu ya kibiashara na ya kisasa pamoja na maduka kwa ajili ya mununuzi. Huwa na mgahawa unaotoa huduma ya chakula kuanzia asubuhi mpaka usiku na dawati la mapokezi huwa wazi kwa takribani masaa 14. Mbali na hayo, mteja hufikishiwa huduma mpaka chumbani, maegesho ya magari, huduma ya kubebewa mizigo inapohitajika, sehemu ya kufanyia mazoezi na bwawa la kuogelea pia huwa vinapatikana. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Keys Hotel Moshi na Kilimanjaro Wonders Hotel.     
Nyota nne. Mara nyingi hoteli zenye hadhi hii huwa kubwa. Zina mandhari nzuri kuwavutia wageni, huduma ya mapokezi ambapo lugha zaidi ya moja inazungumzwa na wabeba mizigo kwa ajili ya wateja pia wapo. Hupatikana kwenye maeneo yaliyo karibu na hoteli zenye hadhi sawa na zao vilevile karibu na maduka makubwa ya manunuzi, sehemu za chakula na mandhari yenye vivutio vya hali ya juu. 

Huduma ni zenye ubora mkubwa, vyumba vya kisasa na samani za kupendeza. Huwa na mgahawa wenye vyakula zaidi ya aina moja kwa  machaguo ya wateja wa aina tofauti na pia huduma ya mteja kuhudumiwa hata akiwa chumbani kwake hupatikana. 

Hoteli zingine hutoa huduma ya kuwaegeshea magari au matengezo wateja wa pamoja na kuwasaidia na usafiri wa ndani ya eneo alilofikia. Kwa kuongezea, sehemu ya kufanyia mazoezi, bwawa moja la kuogelea au zaidi pia kawaida kupatikana kwenye hoteli za namna hii. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Gold Crest Hotel na Ramada Resort Dar es  
Salaam.     

Nyota tano. Hizi ni hoteli ambazo hutoa huduma za malazi na nyinginezo katika kiwango cha hali ya juu kabisa. Huwa na huduma kwa wateja binafsi zenye ubora wa 
kipekee. 

Ingawa mara nyingi hoteli za namna hii huwa ni ushirikiano wa makampuni makubwa lakini pia baadhi ya watu wachache huweza kutoa huduma sawa au kuzidi ushirika au makampuni 
makubwa. Maeneo zilizopo hutofautiana kutoka maeneo maalum au kuwa katikati au kitovu cha jiji kwenye shughuli nyingi za kibiashara. 

Unaweza kukuta hoteli ina migahawa mpaka mitatu na yote ikiwa na vyakula vya aina tofauti. Huduma mpaka vyumbani ni masaa 24 kwa kawaida pamoja na nyinginezo lukuki ambazo mteja 
atazihitaji. Mfano wa hoteli hizi ni kama vile Singita Sasakwa Lodge na Essque Zalu Zanzibar.

Kwa ujumla vipo vigezo vingi tu ukiachana na hivyo vichache viliyotajwa hapo juu.Mitandao na mashirika kutokea nchi mbalimbali imejaribu kufafanua na kuorodhesha kwa mujibu wa mahali walipo. 
Hivyo basi vigezo ambavyo vinatumika hapa Tanzania vinaweza visitumike au vikawa tofauti na kwingineko.

TADB, TAHA WAPANGA KUSAIDIA SEKTA YA MALI MBICHI NA MATUNDA (HORTICULTURE)

$
0
0
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) akimkaribisha Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) wakati wawili hao walipokutana kujadiliana juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano.
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kushoto) akihimiza jambo juu ya umuhimu wa sekta ya malimbichi na matunda katika uchumi wa Tanzania kwa Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (hayupo pichani) wakati wawili hao walipokutana kujadiliana juu ya kushirikiana katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha. Kulia ni Meneja Mkuu wa Maendeleo wa TAHA, Anthony Chamanga.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kulia) akimuelezea Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (hayupo pichani) nafasi ya TADB katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara, Augustino Chacha.
Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi akieleza utayari wa TAHA wa kushirikiana na TADB katika kukwamua changamoto zinazoikabili sekta ya malimbichi na matunda nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) nafasi ya TADB katika kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Timu ya Maandalizi ya Makubaliano ya ushirikiano kati ya TADB na TAHA katika kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini wakiwa katika majadiliano wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wao. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arusha.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Francis Assenga (kushoto) akizungumza na Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi (kulia) mara baada ya mkutano wao unaolenga kuisaidia sekta ya malimbichi na matunda nchini. Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya TAHA, Jijini Arush


Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (TADB) na Asasi Kilele ya wakulima wa Malimbichi na Matunda Tanzania (TAHA) zinajipanga kusaidia sekta Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuongeza tija kwa kilimo hicho.

Watendaji wakuu wa taasisi hizo wamesema kuwa kuna haja ya makusudi ya uwekezaji mkubwa katika sekta ya Malimbichi na Matunda (horticulture) ili kuchagiza na kusaidia mapinduzi katika sekta hiyo na kilimo kwa ujumla nchini.

“Tunajipanga kuchochea ukuaji wa sekta hii ili kuwakwamua wakulima wa malimbichi kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini,” anasema Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA, Jacqueline Mkindi amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa ushirikiano kati ya TADB na TAHA kwa kuwa taasisi zote ni za Kilele (apex institutions) zenye kulenga katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Waziri Mkuu Majaliwa kuongoza mkutano wa Tasnia ya Korosho

$
0
0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utakaofanyika kwa siku mbili kuanzia Jumamosi, Mei 13, 2007, mjini Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho (CBT) Hassan Jarufu, amesema ya kuwa Mkutano huo Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho utawajumuisha washiriki wapatao 600 na utafanyika kwenye Ukumbi wa Chuo cha Mipango, Dodoma.

“Kama tulivyokwishakueleza, Mkutano huu Mkuu utafunguliwa na Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa na watakuwapo pia Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dk. Charles Tizeba, Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa inayolima Korosho ya Lindi, Pwani, Tanga, Mtwara na Ruvuma.

“Tumealika pia waheshimiwa Wabunge wanaotoka katika Mikoa hiyo, wakulima wa Korosho na watendaji wa Vyama vya Ushirika vya zao la Korosho. Mkutano huu utajadili kwa kina changamoto zinazoikabili Tasnia ya Korosho nchini,” alisema Jarufu.

Mkutano huu Mkuu wa Wadau wa Tasniaya Korosho unakuja katika wakati ambao Tasnia ya Korosho imepata mafanikio muhimu katika msimu uliopita ambayo ni pamoja na kuweka udhibiti uliosababisha Korosho nyingi kuuzwa kwa kutumia mfumo wa Stakabadhi Ghalani na hivyo kupunguza matumizi ya Kangomba, kipimo ambacho kwa muda mrefu kimekuwa kikimnyonya mkulima.

Udhibiti huo ulisababisha makusanyo ya Korosho kuongezeka kutoka tani 155, 244.645 msimu wa 2015/2016 hadi tani 264, 887. 527 katika msimu wa 2016/2017.

Kadhalika, Mkutano huu Mkuu wa Wadau wa Tasnia ya Korosho unafanyika katika wakati ambao bei ya Korosho imepanda kutoka 2,800/= kwa kilo ya Korosho ghafi daraja la kwanza msimu wa 2015/2016 hadi 4,000/= kwa kilo katika msimu wa 2016/2017.

Aidha, katika hatua inayolenga kupanua kilimo cha Korosho nchini, CBT imekuwa, kuanzia Februari mwaka huu, ikigawa bure miche ya mikorosho kwa wakulima ili waongeze uzalishaji wa zao hilo.

Kwa mujibu wa Jarufu, kwa kuanzia, jumla ya miche milioni 10 itagawiwa kwa wakulima wa Mikoa ya Lindi, Pwani, Tanga, Mtwara na Ruvuma mwaka huu.

 Tumeanza kugawa bure kwa wakulima miche ya mikorosho. Tutafanya hivyo kwa miaka mitatu mfululizo kwa kila mwaka miche milioni 10. Sisi tumeigharimia lakini wao tunawapa bure. Tunataka waitunze mpaka ikue ili hatimaye tuongeze kwa kiasi kikubwa uzalishaji,” anasema Jarufu.

CHAMA CHA CCM CHATOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KUFUATIA KIFO CHA MZEE PAUL SOZIGWA


DKT SALIM: “VIJANA TAMBUENI MCHANGO WA VIONGOZI NA MISINGI YA TAIFA LENU”

$
0
0
Utambuzi wa historia ya nchi una mchango mkubwa kwa vijana kuweza kufahamu madhila yaliyotokea na jinsi viongozi walivyopigana katika kuleta uhuru na maendeleo ya Taifa. Katika makala haya Judith Mhina wa Idara ya Habari MAELEZO anaelezea.

Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Kwanza na Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Dkt Salim Ahmed Salim amesema kuwa vijana barani Afrika wana wajibu wa kujua historia ya nchi na viongozi waliojitolea kuleta uhuru, umoja, amani na maendeleo ya watu.

Amesema, athari za vijana kutojua historia ya nchi na viongozi waliopigania uhuru ni pamoja na kukosa uzalendo na uwajibikaji katika kutekeleza malengo ya Serikali katika kuleta mapinduzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Ameeleza kuwa, nafasi waliyonayo kama vijana ni kujifunza jinsi viongozi wetu walivyoweza kuweka misingi ya umoja, amani, mshikamano na changamoto zilizowakabili na jinsi walivyoweza kuzitafutia ufumbuzi badala ya kukata tamaa na kuilaumu Serikali kuwa haiwasaidii.

Dkt Salim amefafanua kuwa nchi yetu imeonyesha muelekeo mzuri katika kulikomboa kundi kubwa la vijana kuelekea kwenye uchumi wa viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. “Mimi binafsi naipongeza Serikali yetu kwa kuonesha nia njema ya kupunguza au kuondoa changamoto, zinazowakumba vijana wetu. Vijana ni wengi kuliko kundi lolote nchini na hawana uhakika wa maisha yao ya kila siku hivyo wanahitaji kubadilika.”

Mwana-diplomasia huyo mkongwe nchini ameendelea kusema kwamba maamuzi ya Serikali ya Tanzania kuelekea kuwa Taifa la viwanda yatahamasisha vijana kupenda kujishughulisha na kazi mbalimbali za uzalishaji kama vile kilimo nk.

“Jambo la msingi kwa Serikali ni kuhakikisha kwamba inaweka mazingira mazuri na rafiki kwa vijana kuvutiwa katika sekta mbalimbali kwani nchi yetu inayo ardhi ya kutosha tofauti na nchi nyingine barani Afrika. Lakini pia napenda kuchuku fursa hii kuwaasa vijana kuchangamkia fursa hiyo kwani ni mtaji mkubwa kwao katika kujiletea maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.”

“Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba malighafi zote zinapata masoko katika viwanda, miundombinu ya uhakika. Aidha, hii itachochea uzalishaji na ajira kuongezeka maana bidhaa zote zitaongezwa dhamani hapa nchini badala ya kuagiza nje bidhaa zilizoongezwa thamani na kudidimiza uchumi wa nchi yetu.” Amesisistiza Dkt Salim.

Akitoa Mfano wa athari za vijana kutojua historia yao Dkt Salim amesema Afrika ya Kusini ni moja kati ya nchi za Afrika amabazo vijana wake wamekata tamaa na kutowathamini Wazee walioshiriki katika harakati za kuleta ukombozi. Amesema, kitendo hiki cha kuwadharau wazee kimepelekea mfarakano kati ya makundi haya mawili ambayo yanawajibu mkubwa wa kushirikiana na kuijenga Afrika ya Kusini yenye neema kwa wananchi wake wote bila kubagua.

Ameeleza kwamba vijana hao wamejenga chuki na kuwachukia vijana wenzao waliotoka katika nchi nyingine za Afrika na kuwaona maadui kwa kwenda nchini mwao na kufanya kazi ambazo wao wanadhani ni za kwao. Athari hii inajitokeza kwa kuwa hawajui historia ya nchi yao na nini viongozi wao walipigania katika kuweka misingi ya umoja, amani na mshikamano Barani Afrika.

Hata hivyo siwalaumu vijana hata kidogo kwa hakika vijana wana hali ngumu ya maisha kweli kweli, wanahangaika kutafuta riziki, bila mafanikio. Ni vema kukaa nao na kuongea kuhusu hali zao za maisha na changamoto zinazowakabili kwa pamoja kutafuta ufumbuzi wa changamoto husika.

Bara la Afrika lina changamoto nyingi, kama za uongozi, vita vya madaraka, makundi yanayohamisiana, vita vya wenyewe kwa wenyewe , ukabila na mengineyo ambayo hayaleti picha nzuri kwa Afrika na yanadhoofisha ustawi wa Bara letu na vijana kukata tamaa.

Taasisi ya Mwalimu Nyerere ina jukumu la kutoa elimu kwa vijana wote Barani Afrika juu ya mustakabali wao na kuweka misingi imara ya umoja, amani, mshikamano na Maendeleo kwa watu wote katika nchi zao bila kubaguana.

Tunaendesha makongamano, midahalo na semina katika majukwaa mbalimbali ili kuwaelimisha vijana kuhusu historia za nchi zao , viongozi wao na misingi waliyoiweka na umuhimu wa kutanzua kwa pamoja changamoto zilizopo na kuongea yale yote ambayo wanadhani hayaendi vizuri.

Dkt. Salim amewomba vijana kuzingatia elimu wanayopewa maana Taasisi ya Mwalimu Nyerere inahitaji kupata viongozi miongoni mwa vijana wa Tanzania. Ni vema kujua changamoto zilizopo ili vijana hao watakaochukua uongozi kuendelea kuelezea, kufundisha, kuuisha katika misingi ya umoja, amani, mshikamano na maendeleo kwa watu wote na pia ustawi wa Mataifa yote ya Afrika.

Akizungumzia suala la uongozi na ushiriki wa vijana katika kujenga Taifa, Dkt Salim amesema ni vema vijana kushirikishwa katika uongozi kwa kuwa bado wana nguvu ya kuleta maendeleo katika nchi zao. Hata hivyo alitoa tahadhari na kusema “Kijana sio kigezo cha uongozi hata kidogo”,

Akitoa mfano Dkt Salim amesema, “Mimi niliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri nikiwa na miaka 22, nadhani ni umri mdogo kuliko vijana wa sasa wanaoteuliwa, lakini niliaminiwa na kutimiza wajibu wangu kwa nchi na viongozi wangu walioniteua, kwa kuwa nilijua tulikotoka, tulipo na tunakotaka kuelekea. Hayo nilijifunza kutoka kwa viongozi wangu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.”

Dkt Salim muda wote wa uongozi kama Balozi na mwakilishi wa nchi kimataifa alielezea msimamo, matakwa na mapendekezo tunayokubaliana nayo kimataifa. Aidha, alisisitiza suala la umoja, amani, mshikamano na jinsi ya kuleta maendeleo katika nchi zote za Afrika kwa kuwa nchi yetu inaona bila umoja hakuna suluhisho la amani katika nchi zetu na alifanya hayo kwa kuwa nilijua historia ya nchi yangu.

“Wito wangu kwa vijana ambao watakuja kuiongoza Taasisi ya Mwalimu Nyererer ni vema wakajipanga kwa kuwa kazi iliyopo mbele yao ni kuwaelimisha vijana wenzao ili kuthamini na kuuisha umoja, amani na kuleta maendeleo kwa watu wote iwe ni sehemu ya maisha yao.”

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume ni mfano wa kuigwa katika kudumisha umoja, amani na mshikamano katika Bara la Afrika. Umoja wao ulizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Dkt. Salim alimalizia kwa kusema Mwalimu Nyerere siku zote za maisha yake, alikuwa akitembea na kuwaasa Watanzania juu ya umoja, aman, mshikamano na Maendeleo kwa watu wote bila ubaguzi. Mwalimu alitambua wajibu wake.

Akitoa hitimisho Dkt Salim amesema: “Hapa Tanzania asilimia 60 ya idadi ya watu milioni 50 ni vijana, hawa wasipoelewa na kuuisha misingi ya Taifa lao yaani umoja, amani, mshikamano na Maendeleo kwa watu wote bila ubaguzi tutakuwa tumefanya kosa kubwa sana na dunia itatulaumu kwa hilo, kwa sababu Tanzania ndio mfano wa kuigwa.”

RAIS WA AFRIKA KUSINI JACOB ZUMA ALIVYOSHIRIKI KATIKA DHIFA YA KITAIFA ALIYOANDALIWA JANA USIKU NA MWENYEJI WAKE RAIS DKT. MAGUFULI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni mbalimbali (hawaonekani pichani) waliohudhuria katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, Mama Janeth Magufuli (Mke wa Rais), Mama Sizakele Zuma wakwanza kulia (Mke wa Rais wa Afrika Kusini) wakati nyimbo ya Taifa ikipigwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyomwandalia Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akizungumza katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. 
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiwa amemshika mkono Waziri Mkuu Mstaafu Salim Ahmed Salim wakati akizungumza jambo na Rais Msaafu wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa mara baada ya kumalizika kwa Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na mgeni wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma wakati Bendi ya Kilimanjaro “Wana njenje” ilipokuwa ikitumbuiza katika Ukumbi wa Ikulu katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais Zuma.
 Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo Anna Mghwira mara baada ya Dhifa ya Kitaifa Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni ni Rais Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais huyo wa Afrika Kusini Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi mbalimbali wa Kisiasa na Serikali wakiwa katika Dhifa ya Kitaifa aliyoandaliwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma Ikulu jijini Dar es Salaam. 

PICHA NA IKULU

BENKI KUU YA TANZANIA YAFUTA LESENI YA MBINGA COMMUNITY BANK PLC

$
0
0
Benki Kuu ya Tanzania imeamua kuifunga Mbinga Community Bank Plc, kusitisha shughuli zake zote za kibenki na kufuta leseni yake ya biashara ya kibenki kuanzia tarehe 12 Mei, 2016.

Aidha Benki Kuu ya Tanzania imeiweka Mbinga Community Bank Plc chini ya ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia tarehe 12 Mei, 2017, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Benki Kuu leo asubuhi imeeleza.

Uamuzi huu umechukuliwa baada ya Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na matakwa ya Sheria ya Mabenki an Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.

“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza.

Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”

Benki Kuu ya Tanzania imechukua uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2) (a), (b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.

FILBERT BAYI AFUNGA KOZI YA MAFUNZO YA UTAWALA BORA KWA WADAU WA MPIRA WA MIGUU

$
0
0

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 

KATIBU mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi amefunga kozi ya utawala bora iliyoendeshwa na mkufunzi wa FIFA Henry Tandau iliyokuw ainafanyika katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam 

Kozi hiyo inayosimamiwa na Kamati ya Olimpiki ilianza Mei 08 na kufungwa Mei 12 huku kukiwa na washiriki 15 kutoka klabu mbali mbali za ligi kuu na taasisi za michezo. 

Akizungumza wakati wa kufunga kozi hiyo Bayi amesema kuwa hii ni kwa mara ya kwanza kwa wawakilishi kutoka klabu mbalimbali za Ligi Kuu kushiriki katika mafunzo haya ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo ya michezo nchini. 

Amesema kuwa, ana imani kubwa sana kuwa elimu hii waliyoipata wataenda kuitumia vizuri katika kuziendesha klabu zao na kuzieletea maendeleo kwani msingi mkubwa wa maendeleo ya soka ni kuwa na utawala bora. 

"Elimu hii mliyoipata leo nina imani kubwa sana mtaitumia vizuri kwani wengi wenu mnatoka katika klabu za Simba, Yanga na Azam na maendeleo ya mpira wa miguu yanaletwa na utawala bora na wasiende kuweka vyeti ndani bali wanatakiwa kuvitumia kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo,"amesema Bayi. 

Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau amemshukuru Bayi kwa kuweza kukubali kuwa mgeni rasmi kaika mafunzo hayo na kumuahidi kuwa elimu hii waliyoipata wanaimani kuwa washiriki wote wataenda kuelimisha na wengine na kuleta utawala bora kwenye klabu zao. 

Mafunzo hayo ya siku 5 yameratibiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza tofauti na miaka mingine kufanyika mikoani pia yameweza kuleta tija kwa washiriki kufahamu mambo mbalimbali yanayohusu michezo ikiwemo riadha. 
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam.
Mkufunzi wa FIFA Henry Tandau akizungumza wakati wa kufunga kozi wa mafunzo ya utawala bora iliyoendesha na Shirikisho la Mpia wa Miguu (FIFA) kupitia kamati ya Olimpiki iliyoanza Mei 08 mpaka Mei 12 Jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Kituo cha JKM Park Kassim Liogope mafunzo yaliyomaliza leo Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka klabu ya Yangaa ambaye ni afisa masoko na mratibu wa matawi Omari Kaya mafunzo yaliyomalizaleo Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Azam Saad Kawemba ambaye ni Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini Wilfred Kidau katika mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
\
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka Klabu ya Simba Said Tuli ambaye ni mjumbe wa kamati ya utendaji wa Simba mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akitoa cheti cha mafunzo ya utawala bora kwa Mshiriki kutoka bodi ya ligi Fatma Abdala mafunzo yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa Kamati ya Olimpiki Nchini (TOC) Filbert Bayi akiw akatika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya utawala bora yaliyomalizika leo Jijini Dar es salaam.Picha na Zainab Nyamka.

WADAU WAOMBWA KUICHANGIA TIMU YA KIKAPU YA VIJANA U-16 INAYOJIANDAA KUSHIRIKI MICHUANO YA 2016 ZONE 5 MOMBASA KENYA

$
0
0
 Kaimu Katibu Mkuu Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) Michael Mwita akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu kuwaomba wadau kuichangia shilingi milioni 30 kwa timu ya Vijana U-16 wa mchezo ikiwa ni ghalama ya kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Mchezo wa kikapu chini ya umri wa miaka 16, Bahati Mgunda akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akielezea programu nzima ya maandalizi ya hiyo inayojiandaa kwenda kushiriki mashindano ya 2016 Zone 5 Mombasa Kenya. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

MBUNGE AZZA ATEMBELEA ZAHANATI YA SOLWA,AKABIDHI VITANDA VYA KISASA KUNUSURU VIFO VYA MAMA NA MTOTO

$
0
0

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,Mheshimia Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ametembelea Zahanati ya Solwa iliyopo katika kijiji cha Solwa,kata ya Solwa,jimbo la Solwa mkoa wa Shinyanga kisha kutoa msaada wa viti vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia na viti vya wagonjwa (wheel chairs) vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne.

Vifaa hivyo ni miongoni mwa vifaa tiba alivyovipata kutoka Ubalozi wa China nchini Tanzania kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto katika zahanati,vituo vya afya na hospitali mkoani Shinyanga.

Akitoa msaada huo jana Alhamis May 11,2017 Mheshimiwa Azza Hilal Hamad alisema msaada huo utasaidia katika kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa kuwarahishia akina mama kupata huduma karibu badala ya kutembea umbali kufuata huduma za afya.

“Mimi ni mama nazifahamu changamoto wanazokabiliana nazo akina mama,nilitafakari na kuangalia nani wa kuweza kutusaidia,nikaenda ubalozi wa China nchini kuomba wasaidie akina mama wa Shinyanga,walikubali na leo nimeleta vitanda vya kisasa kwa ajili ya akina mama,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia”,alieleza Hamad.

Katika hatua nyingine mbunge huyo aliwapongeza wananchi wa Solwa kwa kujitolea na kuanza ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo ameahidi kuwapatia mabati 20 kwa ajili ya paa la jengo hilo.

Aidha aliwataka wananchi kuachana na tabia ya kuwaozesha watoto wa kike na badala yake wawatafutie shughuli zingine za kufanya wanapofeli mtihani wa darasa la saba kwani wakiolewa wangali wadogo husababisha wapoteze maisha wakati wa kujifungua hivyo kuchangia ongezeko la vifo vya mama na mtoto katika jamii.

Mheshimiwa Hamad pia aliahidi kutafuta namna ya kumsaidia mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa na kupatiwa huduma za kiafya katika zahanati hiyo baada ya mzazi wake Grace Richard kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo katika zahanati ya Solwa,ametuletea picha 25 za matukio yaliyojiri,Tazama hapa chini

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad, (CCM) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Solwa kata ya Solwa jimbo la Solwa mkoani Shinyanga alipotembelea zahanati ya Solwa kisha kukabidhi msaada wa viti viwili vya kisasa vya kujifungulia kwa akina mama,viti viwili kwa ajili ya wagonjwa na vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia kwa akina mama

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nne katika zahanati ya Solwa

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati wa kumkabidhi Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim (kulia) vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia akina mama (alivyoshikilia Dkt. Ibrahim )

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akishikana mkono na mwenyekiti wa kijiji cha Solwa Emmanuel Ngamba wakati akikabidhivitanda vya kujifungulia,viti vya wagonjwa na vifaa vinavyotumika kwenye chumba cha kujifungulia akina mama

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad (CCM) akionesha baadhi ya vifaa vinavyotumika katika chumba cha kujifungulia

Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Hellena Daudi akiwa na baadhi ya madiwani wa CCM wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba katika zahanati ya Solwa

Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa tiba katika zahanati ya Solwa

Diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh akielezea matatizo yanayokabili wananchi wa kata hiyo
Wazee wa kata ya Solwa wakikabidhi zawadi ya mbuzi kwa mbunge Azza Hilal Hamad Msanii wa nyimbo za asili Rasi Nyanda Kagwata kutoka Solwa akitoa burudani wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa tiba
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifurahia jambo na wananchi wa kata ya Solwa baada ya kumaliza zoezi la kukabidhi vifaa tiba kwa ajili ya zahanati ya Solwa
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiteta jambo na mmoja wa wazee wanaoishi katika kata ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amebeba mtoto katika chumba kinachotumika kama wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa ambapo aliahidi kutoa mabati 20 kusaidia ujenzi huo ambao umetokana na nguvu za wananchi walioamua kuchangishana pesa na kuanza kujenga ili kukabiliana na changamoto ya vifo vya akina mama na watoto
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama katika zahanati ya Solwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiweka tofali wakati akishiriki ujenzi wa jengo la wodi ya akina mama zahanati ya Solwa
Wa pili kutoka kushoto ni mganga mfawidhi katika zahanati ya Solwa, Dkt. Edwin Ibrahim akielezea kuhusu mradi wa Lishe wanaoutoa katika zahanati hiyo kukabiliana na tatizo la utapiamlo kwa watoto lililokithiri katika jimbo la Solwa. Dkt. Ibrahim alimweleza mbunge Azza Hilal Hamad kuwa zahanati hiyo imekuwa ikitoa elimu ya lishe kwa akina mama na kutoa chakula dawa kwa ajili ya watoto ambao hali zao kiafya siyo nzuri (wenye utapiamlo)
Ndani ya chumba cha lishe-Mheshimiwa Azza Hilal Hamad na diwani wa kata ya Solwa Shadrack Awadh wakiangalia chakula dawa ( unga maalum wenye lishe) 'Multiple Micronutrient powder) kinachotolewa kwa watoto wenye utapiamlo wanaofika katika zahanati ya Solwa

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwa amembeba mtoto Salawa Mihangwa (03) ambaye ana tatizo la ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati ya Solwa baada ya mzazi wake Grace Richard (kushoto) kukosa shilingi milioni 2.6 kwa ajili ya mtoto huyo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga,mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akimweleza mama wa mtoto huyo kuwa ameguswa na hali ya mtoto huyo ambaye afya yake siyo nzuri hivyo kuahidi kutumia mbinu mbalimbali ili mtoto aweze kufanyiwa huduma ya upasuaji

Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha mheshimiwa Azza Hilal Hamad vyeti vya mtoto Salawa Mihangwa anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo na amekuwa akilelewa katika zahanati ya Solwa ambayo sasa inalea watoto 95 wenye tatizo la utapiamlo huku mtoto anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo akiwa mtoto wa kwanza kulelewa katika zahanati hiyo Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na akina mama wenye watoto wanaolelewa katika zahanati ya Solwa kutokana na watoto kukabiliwa na utapiamlo ambapo aliwasisitiza kuwapatia watoto mlo kamili na kuzingatia ushauri wanaopewa na wataalam wa masuala ya afya

Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akigawa matunda kwa watoto wanaopata huduma ya lishe katika zahanati ya Solwa
Mganga Mfawidhi wa zahanati ya Solwa Dkt. Edwin Ibrahim akimwonesha mheshimiwa Azza Hilal Hamad shamba la viazi lishe vilivyolimwa katika zahanati ya Solwa kwa ajili ya watoto wanaohudumiwa katika zahanati hiyo kukabiliana na tatizo la utapiamlo

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiondoka katika zahanati ya Solwa baada ya kukabidhi vifaa tiba vitakavyosaidia kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BALOZI DK.MAHIGA AKABIDHIWA MAGARI NA SERIKALI YA KUWAIT

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa  Balozi Dk. Augustine Mahiga amepewa msaada wa magari kutoka serikali ya Kuwait ilikuweza kusaidia katika shughuli mbalimbali za kiutendaji.

Balozi Mahiga amesema hayo wakati akipokea msaada wa magari kwa ajili ya wizara yake amesema wizara yake sio yenye tatizo ya usafiri bali ni suala wizara mbalimbali na taasisi zingine za serikali .

Amesema serikali ya Kuwait inatoa msaada katika serikali ya Tanzania zaidi ya dola za kimarekani milioni 200 kwa kila mwaka.Balozi Mahiga amesema ubalozi wa Kuwait nchini amekubali kusaidia magari kwa sekta zingeni kwa kutaka kuorodhesha mahitaji ya usafiri ili kuweza kusaidia serikali ya Tanzania Kiutendaji.
 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukabidhiwa magari kutoka ubalozi wa Kuwait nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhii magari yenye thamani ya dola za Kimarekani 100,000 leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmauel Massaka,Glob ya Jamii.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi funguo za Magari kwa Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akiteta jambo na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem
 Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa wizara hiyo.

KINONDONI YAJIPANGA KATIKA UBORESHAJI WA ELIMU-MANYAMA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama amesema kuwa manispaa imejipanga katika katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

Manyama ameyasema hayo katika kilele cha wiki ya elimu kwa Manispaa ya Kinondoni iliyofanyika leo katika shule ya Sekondari ya Mbezi Beach jijini Dar es Salaam amesema watakuwa bega kwa bega na shule zilizo katika manispaa hiyo katika kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

Amesema kuwa katika awamu wa tano wamejipanga katika kutatua changamoto ambazo zinakabili manispaa hiyo ikiwa ni vyumba vya madarasa baada kwa kuisha kwa changamoto ya madawati.

Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri amesema kuwa alijituma na kuweza kupata ufaulu huo.

Taus amesema kuwa wanafunzi wenzake wajitume waweze kuwa na ufaulu utaofanya wawe na malengo ya kuendelea kufanya vizuri,Mwalimu Mkuu Msaidizi Mikocheni Islamic, Maulid Omari amesema kuwa shule yao ilikuwa ya pili katika manispaa ya kinondoni kwa kubebwa na Taus kwa kupata alama kubwa katika masomo yote .

Mama wa Taus , Hiba Msasi amesema mwanae amekuwa na bidii katika masomo ndio maana ilimuwezesha kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni , George Manyama akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha maadhimisho ya elimu yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwanafunzi aliyefanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana kwa kupata ufaulu wa juu katika shule ya Msingi Mikocheni Islamic , Taus Amiri akizungumza na waandishi habari juu ya ufaulu wake katika matokeo ya darasa la saba mwaka jana.
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, George Manyama akitembelea maonesho ya shule katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya elimu .
Wanafunzi wakifanya maonesho ya kilele cha wiki ya elimu leo jijini Dar es Salaam.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 23, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 12, 2017

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Andrew Chenge akiongoza kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiongea jambo na Mbunge wa Rombo(CHADEMA) Mhe.Joseph Selasini katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Mbunge wa Viti Maalum(CCM) Mhe.Neema Mgaya akiuliza swali katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Mbunge wa Kibamba(CHADEMA)Mhe.John Mnyika akiuliza swali katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Angelina Mabula akijibu hoja Mbalimbali za Wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki katika kikao cha Ishirini na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akizungumza jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama katika kikao cha Ishirini na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri wa Maji Mhe.Eng Gerson Lwenge akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mhe.William Ole Nasha akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Mhe.Hussein Bashe akizungumza na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Dk.Ashatu Kijaji akizungumza jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani katika kikao cha Ishirini na moja cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Washiriki wa Shindano la Miss Udom wakiwa Bungeni Kujifunza shughuli mbalimbali zinazoendelea katika kikao cha Ishirini na tatu cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 12, 2017.


Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

SERIKALI YA INDIA KUTOKA DOLA MILIONI MILIONI 500 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI NCHINI.

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India imeahidi kutoa dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji katika miji 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar katika awamu ya tatu katika mwaka wa fedha 2017/18.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe akijibu Swali la Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni Mjini Dodoma.

“Katika bajeti ya mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa inaoupata kutoka Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali hiyoa”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe.

Aidha katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya manunuzi ya Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa miradi na uandaaji wa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya ujenzi zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.

Amesema kuwa katika awamu ya kwanza Serikali ilipata dola za kimarekani Milioni 178.125 ambapo kazi zilizotekelezwa katika awamu hiyo ni upanuzi wa mradi mkubwa wa Ruvu Juu,Ujenzi wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi Kimara,Pia Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Dar es Salaam pamoja na ujenzi wa mradi Chalinze.

Katika awamu ya Pili Serikali ya India itatoa dola milioni 268.35 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kutoa maji katika mradi wa KASHWASA kutoka kijiji cha Solwa kwenda katika miji ya Tabora,Igunga,Nzega,Tinde na Uyui pamoja na Vijiji 89 vinavyopitiwa na bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande uku wakandarasi wa kutekeleza mradi huo wamepatikana na wapo katika hatua za utekelezaji.

Karata 15 - The new Chart show in town

$
0
0
Katika kukuongezea burudani wewe msikilizaji wa 93.7fm Dar es salaam, Pwani na 91.3fm Mwanza, kituo cha E- fm redio kinakuletea kipindi kipya cha The chart show kitakacho husisha ngoma kali zinazoshikilia chart na stori kemkem za wanamuziki kutoka ndani na nje ya nchi kiitwacho KARATA 15 kaa tayari kukutana na watangazaji wako Jabir Salehe“KUVICHAKA- Bonge Tozz” na Allen Mushi “BIG ALLEN” kila Jumamosi kuanzia tarehe 13/05/2017, saa 6:00 – 8:00 Mchana.

“E-FM NI KWIKWI”

MKUU WA WILAYA AONGOZA KILELE CHA SIKU YA WAUGUZI KISHAPU

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiwa amembeba mtoto aliyezaliwa katika Hopsitali ya Wilaya (Dk. Jakaya Kikwete) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani kiwilaya.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba akimpa msaada mmoja wa mama anayeuguza mtoto katika hopsitali ya wilaya.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza na wauguzi (hawapo pichani) katika sikukuu ya Wauguzi Duniani viwanja vya hospitali ya wilaya.
 Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kangese akitoa neno kumkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya
 Wauguzi wakila kiapo cha utii wakati wa sikukuu hiyo.

Wauguzi wilayani Kishapu wamepongezwa kwa kazi nzuri na kutakiwa kuendelea kuipenda kazi yao kuchapa kazi katika mazingira yoyote waliopo kwani wao ni chachu ya afya katika jamii.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba wakati kwenye kilele cha Siku ya Wauguzi Duniani iliyofanyika katika viwanja vya Hospitali ya Wilaya ya DK. Jakaya Kikwete.  
Talaba ambaye aliwaongoza wauguzi hao na watumishi wa halmashauri kutoa misaada na kufariji wagonjwa hospitalini hapo aliwapongeza kwa huduma nzuri kwa wagonjwa.

Alisema kuwa bila ya wauguzi afya haijakamilika na kuwa uuguzi ni zaidi ya wito na ni huduma inayohitaji upendo na huruma kwa wale unaowahudumia.

“Kama huna upendo na ukarimu basi wewe siyo muuguzi na ukionesha ukarimu na upendo ndiyo mwanzo wa kupona kwa mgonjwa ukifika tu pale mgonjwa anapona hata kabla hujampa dawa,” alisisitiza.
Aidha, aliwataka wauguzi waendelee kuwa na ushirikiano baina yao huku akiwapongeza kwa mafanikio katika sekta ya afya pamoja na kuwa wana changamoto ya mazingira ya kazi.

Mkuu huyo wa wilaya aliwaomba kuendelea kutimiza wajibu na kuzingatia viapo vyao vya uuguzi na kanuni za utumishi huku akionya kushindwa kufanya hivyo ni kukiuka taratibu za kazi na hivyo kutengeneza migogoro isiyo ya lazima.

Kwa upande wake, Kaimu Muuguzi Mkuu Hospitali ya wilaya hiyo ya Dk. Jakaya Kikwete, Rehema Jumanne akisoma risala alitaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni mafunzo kazini.Alisema mafunzo hayo yamesaidia wauguzi kuboresha huduma za jamii zikiwemo uzazi wa mpango, huduma za dharura kwa wajawazito na kusaidia wachanga kupumua.

Pia alitaja mafanikio mengine ni kuendeleza wauguzi katika ngazi za juu za elimu na hivyo kutoa huduma kwa kiwango cha juu pamoja na kutoa huduma bora tofauti na mazingira yao.

Hata hivyo alisema kuna changamoto ya uhaba wa watumishi hiyo husababisha kutokuwepo kwa uwiano sawia wa watumishi katika kutoa huduma katika vituo vya afya na zahanati mbalimbali katika wilaya hiyo.
Siku ya Wauguzi Duniani huadhimisha kila Mei 12 ikiwa ni kumuenzi  muuguzi mwanzilishi Florance Nightingale aliyoanzisha mwaka 1844 ambapo kaulimbiu ni Wauguzi, mbiu ya kuyafikia malengo endelevu ya millennia.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images