Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

SERENGETI YAREJESHA UDHAMINI TAIFA STARS, YAIMWAGIA BILIONI 2.1

$
0
0

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) akipeana mkono na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kushoto) mara baada ya kukabidhiana
mfano wa hundi ya Sh. Bilioni 2.1,Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.


Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kushoto) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) kwa pamoja wakionesha mikataba waliotiliana leo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye hafla fupi iliofanyika jioni ya leo jijini Dar.Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Mkurugenzi Mkuu wa SBL, Helene Weesie (kulia ) na Rais wa TFF, Jamal Malinzi (kulia) kwa pamoja wakionesha mikataba waliotiliana leo mbele ya Waandishi wa habari,kwenye hafla fupi iliofanyika jioni ya leo jijini Dar.Pichani kati anaeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe.

Baadhi ya Waandishi wa Habari na baadhi ya wafanyakazi wa TFF na Wizara wakishuhudi tukio la utiliaji saini mkataba wa udhamini kwa timu ya Taifa Stars wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 uliotolewa na kampuni ya SBL na hatimaye kuifanya kampuni hiyo kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars,hafla hiyo imefanyika jioni ya ya leo jijini.

Pichani kati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jioni,kwenye hafla fupi ya utiliaji saini kati ya kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wenye thamani ya sh.bilioni 2.1 .
Wakitiliana saini mikataba hiyo.
 =======  ========  ======== =========
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa timu ya Taifa Stars itafanya vizuri katika mashindano mbalimbali itakayoyakabili  hapo baadae,kutokana na wadau wanavyojitokeza kuiunga mkono.

Mwakyembe ameyasema hayo wakati kishuhudia utiaji saini mkataba kati kampuni ya ya Bia ya Serengeti (SBL) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) wenye thamani ya sh.bilioni 2.1,utakaodumu kwa miaka mitatu na  kuifanya SBL kuwa mdhamini mkuu wa timu ya Taifa Stars.

“Kwa niaba ya serikali,tunaishukuru sana kampuni ya SBL kwa kurejea tna kuwa mdhamini mkuu wa Taifa Stars,lakini pia tunatoa wito kwa kampuni zingine na watu binafsi wenye mapenzi na michezo kujitokeza na kutoa michango ya hali na mali ili kuendeleza sekta hiyo hapa nchini”,aliesema Waziri Mwakyembe.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa SBL ,Helene Weesie amesema kuwa SBL imekuwa mdhamini kwa kipindi cha pili baada ya kampuni hiyo kufanya udhamini wa timu ya taifa stars mwaka 2007 hadi 2011.

Amesema timu ya Taifa Stars itakuwa inapokea sh.milioni 700 kila mwaka ambapo itakuwa ni pamoja na kutangaza chapa ya SBL wakati wa mechi za ndani na ugenini zitakazochezwa na timu hiyo.

Kwa upande wa Rais wa TFF, Jamal Malinzi ameishukuru SBL kwa kuunga mkono katika kusaidia maandalizi ya timu ya taifa Stars,akaongeza kusema kuwa udhamini huo utasaidia katika kufanikisha maandalizi mazuri na ushiriki kikamilifu wa timu hiyo katika mashindano mbalimbali, ndani na nje ya nchi.

“Udhamini wa SBL umekuja kwa wakati mwafaka, wakati ambapo timu yetu ya taifa ipo katika hatua za maandalizi kwa mashindano ya kikanda na kimataifa,” alisema Malinzi.

MUHIMBILI KUANZA UPANDIKIZAJI WA VIFAA VYA USIKIVU JUNI, MWAKA HUU

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imesema kwamba huduma ya kupandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio na watu wengine itaanza kutolewa Juni, mwaka huu.Huduma ya upandikizaji huo utaipunguzia serikali gharama za kuwapeleka wagonjwa wenye matatizo hayo nchini India.

Kauli hiyo imetolewa leo na Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo katika Hospitali ya Muhimbili, Edwan Liyombo wakati wa kutoa elimu kwa wazazi wa watoto wenye matatizo ya masikio jinsi ya kutunza vifaa vya usikivu kwa watoto waliopatiwa huduma hiyo.

Dk Liyombo amesema kwamba huduma itaanza kutolewa nwezi Juni, mwaka huu na kwamba Hospitali ya Muhimbili imeboresha miundombinu na tayari imenunua vifaa kwa ajili ya kuanza kwa huduma hiyo.

Kuhusu gharama za mtoto mmoja kuwekewa kifaa cha usikivu amesema ni ndogo kuliko akiachwa bila kupatiwa huduma hiyo kwani maisha yake yote atakuwa hasikii wala hataweza kupata uelewa wa masomo shuleni.

“Sisi tunaona hakuna gharama ya mtoto kuwekewa kifaa cha usikivu kwa sababu huduma hii ataitumia katika maisha yake yote na akipelekwa shule atakuwa na uwezo wa kusikia na kuzungumza, kwa kifupi atakuwa sawa kama watoto wengine ambao hawana matatizo ya kusikia,” amesema Dk Liyombo.

Akizungumzia lengo la kuwaita wazazi wa watoto wenye matatizo ya kutokusikia, Dk Liyombo amesema ni kuwaelekeza jinsi ya kutunza vifaa hivyo na endapo vina matatizo wanapaswa kutoa taarifa ili virekebishwe.
Amewataka wazazi wenye watoto wenye matatizo ya kusikia kuwapeleka katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa huduma na pia amewataka kinamama wajawazito kuudhuria kliniki ili kuchunguzwa afya zao pamoja na mtoto kwa lengo la kuzuia mtoto kuzaliwa na tatizo la usikivu.

 Daktari Bingwa wa Masikio, Pua na Koo, wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu huduma ya upandikizaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto wenye matatizo ya masikio. Kutoka kushoto ni Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Nitesh Patel.
 Baadhi ya wazazi wenye watoto ambao wana matatizo ya usikivu wakimsikiliza Dk. Liyombo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Maneja wa Bidhaa, Shalini Srivatsan wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu namna wanavyosaidia jamii
 Watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa kwenye mkutano huo leo.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Hospitali ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha (kulia), Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanguard (T) Limited, Nitesh Patel na Maneja wa Bidhaa wa kampuni hiyo, Shalini Srivatsan (kushoto) wakimsikiliza Dk Liyombo wa Muhimbili kabla ya kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari wakiwamo wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu. Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

KAMPUNI YA SPORTPESA YAINGIA MKATABA WA MIAKA MITANO WA KUIDHAMINI KLABU YA SIMBA

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .

Kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu nchini Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya uwekezaji kwa klabu mbalimbali za mpira wa miguu.

Utiaji saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa mpira nchini.

Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza kuwasaidia katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri zaidi.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema kuwa wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao utakuwa katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.

Amesema kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba watapata milioni 880 na katika miaka mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6  huku mwaka wa mwisho wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni 1.08.

Mbali na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba itafaidika kwa kupata fedha mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa kupewa bonus ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.

Kabla ya utiaji saini wa mkataba huo Simba iliweza kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya stand United magoli yakifungwa na Laudit Mavugo na Juma Luizio huku la Stand likifungwa na Kasim Selembe.

TAARIFA KUTOKA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

SI KWELI KWAMBA TUMEMKADIRIA SHILINGI MILIONI 400 MSANII DIAMMOND-KAYOMBO

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said .

MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya,Nassib Abdul ( Diamond Platnamuz) kulipa kodi ya shilingi Milioni 400. 

Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam. 

“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza .

“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo. 

“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo. Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi. 

“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo. 

Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chombo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma. 

“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania, (TRA), Bw. Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.Mwangosi 
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi .
Mkutano huo ukiendelea
Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi .

HOSPITALI YA MKURANGA YAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA WODI YA WAZAZI KUTOKA TAASISI YA DHI-NUREYN

$
0
0


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii .

HOSPITALI ya Wilaya ya Mkuranga imepata msaada wa wodi ya wazazi vyenye thamani ya sh. Milioni 65 kutoka kwaTaasisi ya Dhi Nureyn .

Akizungumza baada ya makabidhiano ya vifaa wodi ya wazazi , Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega amesema kuwa wodi ya wazazi katika hospitali hiyo ilikuwa na hali mbaya kwa kukosa vitu muhimu ambavyo vinasababisha kupoteza maisha kwa mama au mtoto .

Amesema kuwa kutokana na wanawake wa Wilaya walikuwa hawana uhakika katika masuala ya uzazi lakini sasa suluhisho limepatikana kwa taasisi hiyo kutoa vitu hivyo katika kuokoa maisha ya mama na mtoto katika hospitali hiyo .

Ulega amesema kuwa kutokana tatizo hilo aliamua kwenda kuomba katika taasisi ya Dhi-Nureyn ambao waliangalia mahitaji katika wodi ya wazazi na kuamua kutoa msaada huo licha kuwa na changamoto zingine katika hospitali ya Mkuranga .

Nae Mwenyekiti wa taasisi ya Dhi-Nureyn , Sheikh Said Abri amesema kuwa baada ya kupata maombi kutoka kwa Mbunge wa Mkuranga ,Abdallah Ulega juu ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga hasa katika kuokoa maisha mama na mtoto tuliona jambo la msingi kutekeleza.

Amesema kuwa wataendelea kuwa kusaidia kadri ya uwezo unapopatikana ili hospitali hiyo kuendelea kutoa huduma bora kwa kuwa na vifaa vinavyostahili katika kuhudumia wananchi.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkuranga, Steven Mwandambo amesema kuwa msaada huo umekuja kwa wakati mwafaka kutokana na vifaa hivyo kukosekana kwa muda mrefu huku mipango ilikuwa ikifanyika.
 Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhibiano ya vifaa katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Mkuranga leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Msaidizi wa Taasisi ya Dhi-Nureyn Mkoa wa Dar es Salaam, Mukhtari Iddi akisoma lisala juu ya juhudi zilizofanywa katika upatikanaji vifaa hiyo kutoka mfadhili wa Saudia Arabia, Salehe Al-Sheikh leo Mkuranga.
 Mwenyekiti wa Taasisi ya Dhi-Nureyn,Shekh Said Abri akizungumza juu msaada huo waliotoa katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
 Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga wakikabidhiwa vifaa vya Wodi ya wazazi kutoka kwa watendaji wa Taasisi ya Dhi-Nureyn katika Hafla ilyofanyika Mkuranga.
 Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Steven Mwandambo akitoa shukurani kwa kupata msaada huo katika kuokoa maisha ya mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.
Mshauri wa masuala ya Afya wa Taasisi ya Dhi-Nureyn, Dk Saleh Juma akitoa maelekezo jinsi vifaa walivyotoa vinavyofanya kazi yake katika kutoa huduma katika wodi ya wazazi .

RC TABORA AONGOZA WAFANYAKAZI WA NBC KUPANDA BARABARA YA URAMBO

$
0
0
Na Tiganya Vincent-Tabora

Uongozi wa Mkoa wa Tabora umeamua kuendesha zoezi la kudumu la kuhamasisha jamii kuanzia ngazi za wanafunzi hadi jamii nzima juu ya zoezi upandaji miti ili kukabiliana na uharibifu mkubwa wa mazingira ulisababishwa na shughuli mbalimbali za kibinadamu mkoani humo.

Hatua hiyo inalenga kuijengea jamii na wanafunzi katika shule na vyuo tabia ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti kwa ajili ya faida yao na kizazi kijacho.

Kauli hiyo imetolewa jana mjini Tabora na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri wakati akiongoza zoezi la upandaji wa miti zaidi ya 150 katika eneo la Malolo barabara ya zamani ya kutoka Tabora mjini kuelekea Urambo.

Alisema kuwa zoezi hili ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais ambapo kwa kuanzia amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zaote kuhakikisha kila Wilaya inatekeleza agizo hilo kwa miti isiyopungua milioni moja na laki tano kila mwaka.

Mkuu huyo wa Mkoa aliongeza kuwa miti waliyopanda watakikisha inahimili wakati wa kiangazi kwa kuimwagilia kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya umwagiaji kwa matone ya chupa.

Alizitaja baadhi ya sababu zilizosababisha kuwepo ya uharibifu huo mkubwa ni pamoja kilimo cha tumbaku, ulimaji katika vyanzo vya maji na ufugaji usio rafiki wa mazingirana.

Bw. Mwanri aliongeza kuwa hatua nyingine ambazo zimeanza kuchukuliwa katika kudhibiti uharibifu wa mazingira hasa maeneo ya mijini ni pamoja na kukamata mifugo yote inayozurura.

Aidha , aliwashukuru wanyakazi wa NBC tawi la Tabora kupanda miti hiyo na kuahidi kuitunza ili ije iwe ukumbusoa wao wa kufanyakazi katika Mkoa huo.

Bw. Mwanri alisema kuwa kitendo chao cha upandaji wa miti katika Mkoa huo sio tu kwamba watakuwa wanahifadhi mazingira bali watabakiza alama ambayo itakuwa ukumbusho kwao na kwa kizazi chao.

Kwa upande wa Meneja wa NBC wa Kanda (Tabora, Shinyanga, Kigoma na Mara) Daudi Edgar Mfalla alisema kuwa Benki hiyo imefurahishwa na juhudi za Uongozi wa Mkoa huo na kuamua kuunga mkono zoezi linaloendelea kwa sababu ya kutambua bila mazingira mazuri hakuna uhai.

Alisema kuwa upandaji wa miti hiyo ni sehemu ya utaratibu wa Benki hiyo wa kurudisha inachokipata katika jamii. Bw.Mfalla alisema kuwa zoezi linaloendwa na uongozi wa Mkoa wa Tabora ni zuri na litasaidia kuijenga jamii hasa kuanzia watoto hadi wazee kuwa na mazoea ya upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa ya faida yao , jamii, Taifa na dunia kwa ujumla.

Mmoja wa wafanyakazi wa Benki hiyo mkoani Tabora Bibi Grace Mwanri alitoa wito wa kujenga tabia ya kupanda miti na kuitunza kwani inahusika sana na uhai na maisha ya kila ya mwanadamu.

Alisema kuwa jamii kama itakata miti ovyo bila kupanda mingine kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vyanzo itasababisha ukame na hivyo hakutakuwepo na maji na uhai utakuwa shakani.

Bibi Mwanri alisema kuwa wao kama wafanyakazi na wakazi wa Tabora wanalitambu hilo na ndio maana wameungana na viongozi na wadau wote ambao wamekwishapanda miti kushiriki zoezi hilo. Mkoa wa Tabora kabla ya uharibifu wa mazingira ulikuwa ukipata mvua za wastani wa milimita 1800 lakini kutokana na uharibifu huo hivi unapata wastani wa milimita 650.

MAKUSANYO YA KODI YA PANGO LA ARDHI YAONGEZEKA MARADUFU.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na watumishi wa wizara hiyo katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na kuwataka waongeze jitihada za makusanyo ya kodi ya pango la ardhi.

Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.


Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.


Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila katikati, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiruka kushoto na Mjumbe Baraza kuu la Wafanyakazi Serikalini (TUGHE) kulia, wakiimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi.


Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila katikati, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Dkt. Moses Kusiruka kushoto na Mjumbe Baraza kuu la Wafanyakazi Serikalini (TUGHE) kulia, wakiimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi.


Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.


Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi wakiimba wimbo wa mshikamano kwa wafanyakazi wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.

………………………………………………………

Na. Hassan Mabuye, Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi.

Serikali imefanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi hadi kufikia tarehe 13 Mei 2017 kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa.

Akiongea katika mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Yamungu Kayandabila amesema kiwango cha makusanyo ya kodi ya ardhi hakijawahi kufukiwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Wizara ya Ardhi imeisha kusanya kiasi cha shilingi bilioni 76 cha kodi ya pango la ardhi.

Juhudi za kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa viwanja vilivyopimwa zinaendelea vizuri licha ya changamoto iliyopo hususan muamko wa wananchi katika kulipa kodi, amesema Dkt. Kayandabila.

“Ni matumaini yangu kuwa katika kipindi kilichobaki Wizara itafikia lengo la kukusanya kiasi cha makusanyo ya kodi ya pango la ardhi kilichowekwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ambacho ni kiasi cha shilingi bilioni 111.7”. Amesema Dkt. Kayandabila.

Amesema, Serikali kuanzia mwezi julai, 2017 kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itaanza kukusanya kodi ya pango la ardhi kwenye viwanja na mashamba yasiyopimwa. Lengo la utaratibu huu ni kuongeza wigo wa mapato yatokanayo na kodi ya pango la ardhi.

Utaratibu huu utawafanya wananchi wote wanaomiliki ardhi waweze kulipa kodi. Hata hivyo, ni vema ieleweke kuwa uamuzi huu hauna lengo ya kupunguza juhudi za Wizara katika kupanga, kupima na kumilikisha ardhi kwa wananchi, isipokuwa utaratibu huu unajenga dhana ya uwajibikaji kwa wananchi wote katika kulipa pango la ardhi kwenye maeneo yao.

Aidha, serikali imeanza Ujenzi wa mfumo wa kielektronic wa kumbukumbu za Ardhi (Integrated Land Management System) ambao umeanza kutekelezwa. Mfumo huo ukikamilika utasaidia sana kuwa na kumbukumbu sahihi za wamiliki wa ardhi na hivyo kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Ardhi.

WMA REKEBISHENI MIZANI KWENYE MAGHALA YA KOROSHO-MAJALIWA

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma .(PICHA NA OWM)
Wadau wa Tasnia ya Korosho wakimsikilza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini ambao umefunguliwa na Waziri Mkuu May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho , Mama Anna Abdala baada ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wawa Dau wa Tansnia ya Korosho Nchini katikati ni Waziri wa Kilimo ,Mifugo na Uvuvi Dr Chales Chizeba , Waziri Kuu amefungua Mkutano huo May 13, 2017 katika Ukumbi wa Chuo cha Mipango Mkoani Dododma.
(PICHA NA OWM)



*Serikali kugawa salpha bure kwa wakulima wa korosho

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya mizani katika maghala ya kuhifadhia korosho ili kuepuka changamoto ya kutofautiana kwa uzito wa bidhaa hiyo kila inapofikishwa kutoka katika vyama vya msingi.

Amesema kitendo cha mizani za kwenye maghala hayo kupunguza uzito wa korosho zinazopelekwa kutoka kwenye Chama cha Ushirika cha Msingi (AMCOS) hakivumiliki, hivyo Wakala wa Vipimo ipendekeze aina ya mizani zitakazotumika katika upimaji wa korosho.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Mei 13, 2017) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Wadau wa Tasnia ya Korosho uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma.

“Kuna jambo baya sana linaendelea kila korosho inayofikishwa katika ghala kuu lazima kilo ziwe zimepungua kwa zaidi ya kilo mia moja mpaka elfu, kwa nini korosho tani kumi zikiletwa kwenye mizani yenu zinasoma tani nane kwa nini?

“Na huwa haitokei ikasoma tani kumi na mbili, wakati wote huwa inasoma chini tu, watu wa WMA mpo fanyesni marekebisho, haiwezekani tukavumilia wizi huu. Huna mkorosho hata mmoja lakini mwaka huu utasikia umeuza tani zaidi ya elfu tano.Jambo hili lisijitokeze tena,” amesisitiza.

Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali imeendelea kuimarisha na kuboresha utaratibu wa stakabadhi ghalani na kupambana na biashara ya kangomba, hivyo viongozi wa Mikoa inayolima korosho wahakikishe wanawashughulikia watu wote watakaobainika kushiriki kwenye biashara hiyo bila ya kujali wadhifa wao.

Amesema mwelekeo wa Serikali kwenye sekta ya kilimo ni kuhakikisha kuwa kilimo kinakuwa sehemu muhimu ya kuimarisha uchumi, kuongeza kipato cha mkulima na kuchochea ukuaji wa viwanda ili kuongeza ajira.

Kwa upande wake, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba amesema takwimu zilizotolewa na Benku Kuu ya Tanzania (BoT) mwezi Februari mwaka huu, zinaonyesha zao la korosho linaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni. Zao la korosho limeliingizia Taifa Dola milioni 346.6, likifuatiwa na zao la tumbaku dola 276 na kahawa dola 152.9.

“Zao la korosho linakuwa zao kuu la biashara nchini na tayari mikoa ya Dodoma, Morogoro, Iringa, Njombe na Mbeya imeanza kulima, hivyo kuongeza idadi ya mikoa inayolima zao hilo nchini na kufikia 11 na wilaya 40,” amesema.

Aidha, Dkt. Tizeba ameitaka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) kuhakikisha inakuwa makini na viuatilifu vinavyoingizwa nchini kwa kuvipima kwa kutumia wataalamu wa Serikali ili kujiridhisha ubora wake kabla ya kuwafikishia wakulima.

Pia Dkt. Tizeba amesema katika msimu wa mwaka huu Serikali itagawa salpha bure kwa wakulima wa zao la korosho kwa ajili ya kupuliza kwenye mikorosho yao ili isishambuliwe na wadudu.

BENKI YA NBC YAIKABIDHI SERIKALI GAWIWO LA SHILINGI BILIONI 1.7

$
0
0


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania Bw. Edward Marks, akizungumza jambo wakati wa maadhimisho ya Benki yake kutimiza miaka 50, tukio lililofanyika Mjini Dodoma Jana usiku.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya NBC, Bw. Nehemiah Mchechu, akitaja mafanikio makubwa yaliyofikiwa na Benki hiyo, wakati wa uzinduzi rasmi wa maadhimisho ya Benki hiyo kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena, Mjini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Josephat Kandege, akipokea tuzo kwaniaba ya wabunge, tuzo iliyotolewa na NBC kutambua mchango wa Bunge katika kuanzishwa kwa Benki hiyo miaka 50 iliyopita.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akionyesha alama ya dole! akifurahia gawiwo la shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki asilimia 30 za hisa katika Benki hiyo
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), akishukuru baada ya kupokea gawiwo la shilingi bilioni 1.7 zilizotolewa na NBC kwa Serikali, ambayo inamiliki asilimia 30 za hisa katika Benki hiyo

Waziri Mkuu Mstaafu, Mzee Samwel Malecela, akitoa neon la shukurani kwenye hafla ya Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kutimiza miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, sherehe zilizofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Morena mjini Dodoma.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango)


Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa mara ya kwanza imetoa gawiwo la shilingi bilioni 1.7 kwa Serikali ambayo inamiliki asilimia 30 ya hisa za Benki hiyo.

Hundi kifani ya kiasi hicho cha fedha alikabidhiwa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), kwaniaba ya Waziri Mkuu, katika tukio la Benki hiyo kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwake, tukio lililofanyika katika Hoteli ya Morena Mjini Dodoma.

Hii ni Mara ya kwanza kwa Benki hiyo kutoa gawiwo kwa wanahisa wake katika kipindi cha miaka 9 baada ya kuanza kupata faida ya uwekezaji wake hapa nchini.

Dkt. Mpango aliishukuru Benki hiyo kwa kuanza kutoa gawiwo kwa wanahisa wake baada ya ukame wa muda mrefu na kuelezea matumaini yake kwamba kiasi cha gawiwo kitaongezeka zaidi miaka ijayo.

Hata hivyo alizitaka Benki zote hapa nchini kupunguza riba za mikopo inazotoza kwa wateja wao hasa baada ya Benki Kuu ya Tanzania-BOT kupunguza riba za mikopo kwa mabenki kutoka asilimia 16 hadi asilimia 12.

Alizitaka pia taasisi za fedha nchini, kuwekeza fedha katika kutekeleza Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo kwa njia ya mikopo kwa wateja wao kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vitakavyosisimua uchumi na kukuza ajira nchini.

Alipongeza pia juhudi zilizofanywa na Benki hiyo kufanya uwekezaji mkubwa kwenye mtandao wa malipo ya kielektroniki ikiwa ni maagizo ya Serikali kwamba malipo yote ya Serikaloi yafanyike benki au kupitia miamala ya kielektroniki

“Nimefurahi kuthibitishiwa kwamba, kutoka tarehe 1 Julai 2016 hadi kufikia tarehe 30 Aprili 2017, NBC imekusanya fedha za Serikali na kuzituma kielektroniki katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) jumla ya Shillingi Billioni 991” aliongeza Dkt. Mpango.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Nehemiah Mchechu, alieleza Mkakati wa Benki hiyo ya tatu kwa ukubwa hapa nchini ikitanguliwa na Benki za NMB na CRDB, huku ikiwa imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi trilioni 1, kwamba imejipanga kusogeza huduma zake kwa wananchi na wafanyabiashara wa kati na wa chini kabisa.

“Mwaka jana Benki yetu imepata faida ya zaidi ya shilingi bilioni 13 na katika mkutano Mkuu wa wanahisa tuemekubaliana kutoa gawiwo kwa wawekezaji” aliongeza Bw. Mchechu.

NBC inamilikiwa na wabia watatu, wakiwemo kundi la Mabenki ya Barclays (ABSA Group ltd) ya Afrika Kusini, inayomiliki hisa nyingi zaidi, Serikali ya Tanzania yenye hisa asilimia 30 huku Benki ya Dunia kupitia Taasisi yake ya Fedha ijulikanayo kama The International Finance Corporation (IFC), ikiwa na hisa asilimia 15.

CCM Z’BAR YAAHIDI KUISHAURI SMZ IHARAKISHE MISAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO

$
0
0
Ni msafara wa ziara ya Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” kulia mtu wa nne aliyafaa sare za CCM fulana na kofia za kijani huko shehia ya Koani Wilaya ya Kati Unguja.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akizungumza na mmoja kati ya wananchi waliopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha, Bw. Kassim Vuai huko Shehia ya Kizimbani Wilaya ya Magharib “ A” Unguja.
Mwananchi wa shehia ya Miwani iliyopata athari ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara Bw. Mohamed Sheweji Mohamed ambaye pia ni miongoni mwa waasisi wa ASP akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” katika ziara hiyo ya kuwafariji wananchi.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar , akiingia ndani ya nyumba ya mkaazi wa shehia ya miwani Bi. Christina John kumfariji juu ya maafa hayo.
Bw. Edward Maziku mmoja kati ya wananchi waliopata maafa hayo ambaye nyumba yake imepotomoka kutokana na mvua hizo kama inavyoonekana pichani na Dr. Mabodi alimpa msaada wa sh.200,000 ili aweze kujikimu huku CCM na SMZ zikitafuta wa changamoto hizo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdalla Juma Saadala “ Mabodi” akiangalia ukuta uliobomoka kwa mvua wa vyoo vya Skuli ya msingi na sekondari Bwejuu na kuchangia sh.200,000 na gari moja la mawe ili ukuta huo ujengwe haraka ili shule ikifunguliwa wanafunzi wapate huduma ya vyoo.
Baadhi ya nyumba za shehia ya Chwaka zilizojaa maji kutokana na mvua hizo. PICHA NA AFISI KUU CCM ZANZIBAR.

………………………………………………………………………

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimesema kinaendekea na juhudi za kuishauri serikali iharakishe utaratibu wa kutoa misaada kwa wananchi walioathiriwa na maafa ya mvua ili waweze kupata huduma za msingi kama walivyo wananchi wengine waliosalimika na tatizo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar, Dkt.Abdalla Juma Saadala ” Mabodi” katika mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maeneo mbali mbali nchini yaliyopata maafa ya mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Dkt.Mabodi aliwambia wananchi hao kwamba serikali ya Mapinduzi ya zanzibar inayotokana na chama hicho ni sikivu na inathamini maisha na utu wa wananchi wote bila ya kujali itikadi za kisiasa, hivyo itaendelea kutoa mapendekezo kwa Idara ya Maafa nchini ifike kila pembe ya visiwa vya zanzibar kuhakikisha wananchi wote waliopata maafa wanaratibiwa na kupatiwa misaada.

Alieleza kwamba pamoja na taasisi hiyo kufanya kazi za kisiasa bado ina jukumu la kuwalinda na kuwasaidia wananchi wakati panapotokea majanga mbali mbali ya kitaifa ili waweze kubaki salama na kuendelea na shughuli za kimaendeo.

” Wananchi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atuvushe salama katika hii neema ya mvua iliyochanganyika na mitihani, ili turudi katika maisha ya kawaida na kuondokana na hofu.

Jukumu letu kama chama cha kisiasa wakati wa maafa ni kuhakikisha kila mwananchi ana kuwa salama na kupata huduma za msingi sambamba na kuwafariji huku serikali ikiendelea kukamilisha taratibu za kutafuta ufumbuzi wa kumaliza changamoto zinazotokana na maafa hayo.” alieleza Dkt. Mabodi wakati akitoa msaada wa fedha sh.200,000 kwa mwananchi wa Shehia ya Miwani Unguja, Bw.Endward Maziku ambaye nyumba yake imebomoa na kukosa makaazi ya kuishi.

Akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa maeneo ya shehia ya Miwani kuwa changamoto ya miundo mbinu ya barabara inayowakabili , alisema SMZ ina mpango wa kuanza ujenzi wa barabara hiyo kwa awamu pamoja na Vijiji vya Koani, Jendele, Unguja Ukuu na Jumbi.

Alifafanua kuwa baadhi ya barabara hizo tayari zilikuwa zimeanza kutengenezwa lakini baadae serikali ikabaini kuwa Mkandarasi aliyepewa tenda hiyo hana sifa na ikaamua kumfuta.

Sambamba na hayo Naibu Katibu Mkuu huyo, aliendelea kuwasisitiza waakazi wa maeneo mbali mbali kutibu maji kabla ya kuyatumia pamoja na kuwa karibu na watoto wadogo wasicheze karibu na mabwawa ya maji ya mvua kwa lengo la kuepuka athari za maafa.

” Nakiri kwamba mvua hizi ni kubwa sana hazijawahi kutokea kwa miaka ya hivi karibu, kwani mvua kama hizi nakumbuka zilitokea miaka ya 1972-1973 na kuacha maafa makubwa.

Pia nawaomba wanasiasa nchini tusitumie maafa haya kama ajenda ya kisiasa bali tuwafariji na kutoa nasaha za kuwashauri mambo mema na kuwaeleza hali halisi kwani SMZ na CCM hazipendi wananchi wapate majanga na migogoro, hivyo mitihani hiyo ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu”.alifafanua Naibu Katibu Mkuu huyo.

Mapema wananchi hao kwa nyakati tofauti walisifu kasi ya usimamizi wa Ilani ya CCM inayotekelezwa na Serikali kwa kuimarisha huduma za msingi katika sekta mbali mbali za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza Mkaazi wa Chwaka Wilaya ya Kati alisema licha ya kuwepo kwa changamoto za maafa zilizoharibu miundombinu ya maji, barabara na umeme lakini bado wana matumaini kwa serikali itafanya marekebisho ya haraka kwa baadhi ya huduma ili zilidi katika hali ya kawaida.

Naye Mkaazi wa Jambiani Kikadini, Ramadhan Kassim, aliwaomba wananchi wa maeneo mbali mbali nchini kuwa na utamaduni wa kuwa na tahadhari ya kujipanga mapema kwa kufuata ujenzi unaozingatia ushauri wa kitaalamu ili kuepuka maafa wakati wa mvua zijazo.

MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM AFUNGUA UZINDUZI WA MCHEZO WA DRAFTI KATIKA VIWANJA VYA MWEMBEYANGA

$
0
0

NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amewaomba wadau wamichezo nchini kujitokeza kudhamini mashindano hayo kwakuwa ni michezo kama ilivyo michezo mingine.

Meya Mwita aliyasema hayo jiji hapa leo katika uzindua wa mashindano ya mchezo wa Drafti yaliyofanyika katika viwanja vya mwembe yanga, halmashauri ya Temeke.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Meya wa jiji Mwita , yalihudhuriwa pia na Mbunge wa jimbo la Temeke Abdala Mtolea , Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa Drafti ambapo jumla ya washiriki 64 walishiriki.

Meya Mwita alisema kuwa mchezo huo ni mzuri lakini umekuwa ukizaraulika na kuonekana kwamba wanaoshiriki mchezo huo niwatu ambao hawana kazi za kufanya.

Alisema wapo wadau wengi ambao wanatoa vipaumbele kwenye michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete na michezo mingine huku wakiusahau mchezo huo , jambo ambalo linaonyesha kuwatenga makundi ambayo wamejikita kwenye mchezo huo.

Alisema “ Niwaeleze tu kwamba, huu mchezo ni mchezo mzuri kama ilivyo michezo mingine, leo hii wanaocheza mchezo huu wanazaraulika na kuonekana kwamba niwatu ambao hawana kazi, wasiojua kujishugulisha, jambo ambalo sio kweli natamani mchezo huu ufahamika kama michezo mingine.

“ Kama kweli tukiunga mkono mchezo huu, ipo siku tutajenga majina yetu kupitia mchezo huu kama ilivyokuwa kwenye mpira wa miguu, mpira wa pete, na hata mataifa ya nje yakatuunga mkono kupitia huu mchezo” aliongeza.

Aidha Meya Mwita katika hatua nyingine alisema kwamba ataunga mkono chama cha mchezo huo ili waweze kukisajili na kutambulika rasmi.

Aliongeza kuwa katika mashindano mengine , baada ya kusajiliwa kwa chama hicho, yatakutanisha kila halmashauri iliyopo jijini hapa na hivyo kupata mshindi kutoka kwenye halmshauri husika.

“ Jiji lina halmashauri tano, nataka kwenye mashindano mengine ambayo tayari chama hiki kitakuwa kimesajiliwa , kila halmashauri itashiriki, na mshindi atapatikana kutoka kwenye halmashauri nasio mmoja mmoja kama ambavyo tumefanya leo, ila huu ni mwanzo.

Hata hivyo Meya Mwita ameahidi katika mashindano yajayo kugharimia nauri na chakula kwa wachezaji watakao shiriki mashindano hayo na kuwa himzi wachezaji hao kuuthamini mchezo huo.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Meya wa jiji , Mwenyeiti wa Chama cha mchezo wa huo mkoa wa Dar es salaam , Kiraba Ngibombi amesema chama kinakabiliwa na changamo nyingi ikiwemo ukosefu wa ofisi na fedha za kuhudumia na kufanya usajili wa chama hicho.

Mwenyekiti huyo amemuomba Mstahiki Meya katika mashindano yajayo kuwagharimia wachezaji chakula na pamoja na nauri kwa ajili ya wachezaji hao.

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abdala Mtolea akicheza mchezo wa Drafti na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita

Mrema: Serikali ya JPM Itafanikiwa Vita Dhidi ya Dawa za Kulevya

$
0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR). Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Emmi Ally Ghahae na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Uzinduzi huo ulienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Agustine Lyatonga Mrema( kulia) aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wenzake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii akiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale na Mrema aliyepokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.Tuzo hizo zimetolewa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema na Mrakibu wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Scholastica Luhamba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mama’s and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Bi. Emmi Ally Ghahae akionyesha tuzo maalum kwa kutambua mchango wa Mhe. Agustine Lyatonga Mrema (mwenye kofia) katika kuthamini jamii wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam. Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale ambapo Mrema alipokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akipokea risala kutoka kwa mmoja wa wanufaika wa Taasis ya Mama’ and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Sempeho Samweli Mtangi wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Bi. Emmi Ally Ghahae. Hafla hiyo ilienda sambamba na utoaji wa tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wa masuala ya kijamii wakiwemo Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi, Mohamed Dewji, Mustafa Sabodo, Mchungaji Dkt. Getrude Rwakatale ambapo Mrema alipokea tuzo zote kwa niaba ya wengine.
Mwakilishi wa kundi la wasanii Bi. Rahmaty Shariffu (Najma) akitoa nasaha kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni iliyoko Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.Program hiyo inaratibiwa na Taasis ya Mama’ and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR).
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni iliyopo Wilayani Kigamboni Jijini Dar es Salaam Kheri Rajab akitoa neno la shukrani kwa Taasis ya Mama’ and Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.
Paschal Gideon Mtenzi akitoa ushuhuda na nasihi kwa wanafunzi walioshiriki hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana iliyofanyika katika Shule ya Msingi Maweni iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam jana.Kushoto ni Ally Baadeni Farahan, ambao wote kwa pamoja walikuwa waathirika wa dawa za kulevya lakini kwa sasa wamejinasua kwa kupata huduma ya matibabu.


Kikundi cha sanaaa kutoka ofisi ya Kata ya Mji Mwema, Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakitumbuiza wakati wa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana Jijini Dar es Salam.


Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Maweni na wakazi wa Kigamboni Jijini Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni iliyofanyika katika Shule ya Maweni jana.
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole nchini Tanzania Agustine Lyatonga Mrema akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Maweni iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa program ya uanzishaji wa Klabu za Kupambana na dawa za Kulevya mashuleni jana.


Picha na: Frank Shija – MAELEZO

WANACHAMA WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA TIBA ASILI TANZANIA (SHIVYATIATA) ILALA WAKUTANA KUJADILI MASUALA MBALIMBALI YA VYAMA VYAO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (Shivyatiata), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Luwongo (katikati), akizungumza na wajumbe wa mkutano wa shirikisho hilo wilayani Ilala, wakati wa mkutano wao wa kujadili masuala mbambali yahusuyo vyama vyao pamoja na shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Katibu wa Shivyatiata, Wilaya ya Ilala, Johanes Chamushala na kushoto ni Katibu Mwenezi wa Shivyatiata, Ilala, Venance Mwamunyange. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wilayani Ilala wakimsikiliza Mwenyekiti wa Shivyatiata, Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Luwongo wakati akizungumza nao kwenye mkuano huo, wa kujadili masuala mbambali yahusuyo vyama vyao pamoja na shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Katibu wa Shivyatiata, Wilaya ya Ilala, Johanes Chamushala. 
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo, wilayani Ilala wakisikiliza hoja na michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na baadhi wa wajumbe wenzao kwenye mkuano huo, wa kujadili masuala mbambali yahusuyo vyama vyao pamoja na shirikisho hilo, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, wilayani Ilala, akitoa mchango wake katika mkutano huo.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, wa Shivyatiata wilayani Ilala, akitoa mchango wake katika mkutano huo. 
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo, wilayani Ilala, akitoa mchango wake katika mkutano huo. 
Wajumbe wakisikiliza michango na hoja mbalimbali zilizokuwa zikiolewa katika mkutano huo, wa Shivyatiata wilayani Ilala.  
Katibu wa Shivyatiata, Wilaya ya Ilala, Johanes Chamushala, akifafanua jambo kwa wajumbe wa mkutano huo. 
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Wilaya ya Ilala, Sophia Ntomola, akizungumza wakati akiwasilisha moja ya mada katika mkutano huo. 
Wajumbe wakimsikiliza Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Wilaya ya Ilala, Sophia Ntomola, wakati akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wajumbe wa mkutano huo. 
Mratibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Wilaya ya Ilala, Sophia Ntomola, akijibu hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wajumbe kwenye mkutano huo. 
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Tiba Asili Tanzania (Shivyatiata), Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Luwongo (wa tatu kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa mkutano huo, wilayani Ilala, mara baada ya kumalizika kwa mkuano huo.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MAY 14,2017


MBUNGE WA CCM AMWAGA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH. MILIONI 33 VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI SHINYANGA

$
0
0


 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ametoa msaada wa vifaa tiba ikiwemo vitanda vya kisasa vya kujifungulia,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa katika vituo vya afya na zahanati katika halmashauri ya Shinyanga vijijini na Kishapu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 33.



Mbunge huyo amekabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha afya Tinde,zahanati ya Solwa,zahanati ya Nyashimbi,kituo cha afya Samuye katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga vijijini na kwa upande wa Kishapu ni Kituo cha afya Nhobola,Mwang’haranga,Dulusi na Songwa.
 
Vifaa hivyo vinatokana na jitihada zilizofanywa na mbunge huyo Azza Hilal Hamad kufika katika ubalozi wa China nchini Tanzania kuomba asaidiwe vifaa tiba hivyo ili kukabiliana na vifo vya mama na mtoto mkoani Shinyanga.

Akizungumza leo Jumamosi May 13,2017 wakati wa kukabidhi vitanda vitatu vya kisasa vya kujifungulia,vitanda 9 vya wagonjwa na viti vitatu (wheel chairs) vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7 katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini,mheshimiwa Hamad alisema vitasaidia kupunguza adha ya upungufu wa vitanda katika kituo hicho kilichojengwa mwaka 1920.

“Kituo cha afya Tinde kinahudumia tarafa yote ya Itwangi na kata za jirani,kilikuwa na upungufu wa vitanda 28,leo nimeleta vitanda hivi kusaidia wananchi wapate huduma bora,naomba wananchi muwe mstari wa mbele kuunga mkono shughuli za maendeleo,ni aibu kuona kituo hiki kilichojengwa kabla ya uhuru kikiwa hakina majengo ya kutosha ikiwemo nyumba za watumishi na wodi kwa ajili ya wagonjwa”,alieleza Hamad.

Mwandishi wetu,Kadama Malunde alikuwepo wakati mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba katika kituo cha afya Tinde,ametusogezea picha za matukio yaliyojiri…Tazama hapa chini
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akipokelewa kwa shangwe katika kituo cha afya Tinde kilichopo Shinyanga vijijini alipofika kukabidhi vitanda vya kisasa na viti vya wagonjwa vyenye thamani ya shilingi milioni 9.7
Wacheza ngoma ya Kiswezi “Waswezi” wakimpokea mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwahutubia wakazi wa kata ya Tinde wakati akikabidhi vifaa tiba hivyo 


Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad  (CCM) akizungumza katika kituo cha afya Tinde


Wananchi wakimsikiliza mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akiwasisitiza wananchi kuchangia shughuli za maendeleo ikiwemo kujitokeza kuchangia ujenzi wa majengo katika kituo cha afya Tinde ambacho kilijengwa mwaka 1920 lakini mpaka sasa hakina majengo ya kutosha
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliwataka watoa huduma katika kituo cha afya Tinde na wananchi kutunza vifaa tiba alivyokabidhi katika kituo hicho
Viti vya wagonjwa,vitanda vya kujifungulia kwa akina mama na vitanda vya kulalia wagonjwa vilivyotolewa na mbunge Azza Hilal kwa ufadhili wa ubalozi wa China nchini Tanzania
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akizungumza na wananchi wa Tinde
Vitanda vikiwa eneo la tukio
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  akimkabidhi Mganga Mkuu wa kituo cha afya Tinde,Dkt. Dama s Mnyaga Nyansira,shuka kwa ajili ya vitanda vya kulalia wagonjwa
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akikabidhi vitanda vya kujifungulia akina mama,vitanda vya wagonjwa na viti vya wagonjwa
Mtoto akiwa amekaa katika kiti cha wagonjwa wakati mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal Hamad kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akikabidhi vifaa tiba katika kituo cha Tinde
Wananchi wa Tinde wakimpa zawadi ya Kondoo,mbunge Azza Hilal Hamad baada ya kufurahishwa na zawadi ya vitanda na viti vya wagonjwa katika kituo cha afya Tinde
Furaha ikaendelea kuonekana-Mkazi wa Tinde akiwa amembeba mheshimiwa Azza Hilal Hamad
Wakazi wa Tinde wakifurahia na mbunge wao 


Diwani wa kata ya Tinde Japhary Kanolo akizungumza katika kituo cha fya Tinde


Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea

Katibu wa Wazazi CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Abdallah Kirobi akimshukuru mheshimiwa Mbunge Azza Hilal Hamad kuwakumbuka akina mama kwa kuwaletea vitanda vya kisasa vya kujifungulia
Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga vijijini Secilia Ismail akizungumza katika kituo cha afya Tinde ambapo alisema Mbunge Azza Hilal Hamad ni mbunge anayetakiwa kuigwa katika jamii kwani anajua thamani ya maendeleo na anajali wananchi 
Watoa huduma katika kituo cha afya Tinde na wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Katibu wa Jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Shinyanga Masanja Salum akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Angel Robert akizungumza katika kituo cha afya Tinde
Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga vijijini Dkt. Amos Mwenda akimshukuru mbunge Azza Hilal Hamad kwa kuwakumbuka akina mama wa wilaya ya Shinyanga kwa kuwaletea msaada wa vifaa tiba kwani zahanati na vituo vya afya vinakabiliwa na changamoto nyingi hivyo msaada huo utasaidia kupunguza adha wanazopata wa akina mama na wagonjwa
Wakazi wa Tinde wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Watumishi katika kituo cha afya Tinde wakisoma taarifa ya kituo hicho,Kulia ni Peter Zabron,mwingine ni Mary JosephBurudani ikaendelea- Waswezi wakiimba na kuchezaMtaalam wa Mashairi Anthony Meja akisoma shairi kwa ajili ya Mheshimiwa Azza Hilal
Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri akiimba wimbo wa kumpongeza mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa kutoa msaada wa vitanda kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati mkoa wa Shinyanga
Mbunge Azza Hilal Hamad akicheza na Mama Ushauri
Burudani inaendelea
Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikumbatiana na Msanii Mama Ushauri
Wanenguaji wa msanii Mam Ushauri wakicheza kwa madoido
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakionesha mbwembwe zao wakati wakitoa elimu ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa njia ya vituko
Vijana wa msanii Mama Ushauri wakiendelea kuonesha mbwembwe zao.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

KMTC YAJIPANGA KUJENGA JIKO LA KUYEYUSHIA CHUMA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), Mhandisi Adriano Nyaluke akiwaonyesha Waandishi wa habari (hawapo pichani) baadhi ya mitambo itumikayo kutengeneza vipuri mbalimbali vya mashine 13 Mei, 2017 Moshi, Kilimanjaro.
Meneja Mkuu wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), Mhandisi Adriano Nyaluke (kushoto) akiwaonyesha Waandishi wa habari mashine ya kutengeneza randa zitumikazo katika kazi za useremala, 13 Mei, 2017 Moshi, Kilimanjaro.
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), wakiwa kazini Moshi, Kilimanjaro 13 Mei, 2017.
Afisa Mawasiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Bw. Abel Ngapemba akiangalia moja ya mashine itumikayo kuchonga chuma wakati alipotembelea katika Kiwanda cha Uzalishaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC), kilichopo Moshi, Kilimanjaro 13 Mei, 2017.

………………………………………………………………….

Na. Benedict Liwenga-WHUSM, Moshi.

Kiwanda cha Utengenezaji Vipuri vya Mashine Kilimanjaro (KMTC) iko mbioni kujenga mtambo utakaotumika katika kuyeyusha chuma kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake za utenegenezaji wa dhana mbalimbali za mashine ikiwemo kukarabati mifumo ya umeme ya kiwanda hicho ambaye ilikua haijatumika kwa muda mrefu,

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja Mkuu wa Kiwanda hicho, Mhandisi Adriano Nyaluke wakati alipokutanana Waandishi wa habari na kueleza mikakati ya kukiendeleza kiwanda hicho ikiwemo shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo ili baadaye kiweze kutoa ajira rasmi kwa Watanzania.

MhandIsi Nyaluke amesema kwamba, kwa sasa katika amamu ya kwanza wana mahitaji ambayo yanahitajika kukamilika ikiwemo mpango wa kutafuta fedha toka katika Mifuko ya Jamii ili kuweza kujenga mtambo huo pamoja na fedha za mtaji wa kutengeneza zana mbalimbali kiwandani hapo.

“Mpaka sasa tuna bajeti ya shilingi bilioni 1.6 na tuna mpango wa kuendelea kutafuta fedha zaidi toka katika Mifuko ya Kijamii na tunaamini fedha hizo tutazipata ili tuweze kuendelea na mpango wa kujenga mtambo huo pamoja na utengenezaji wa zana za kiwanda”, alisema Nyaluke.

Ameongeza kuwa, hapo awali kiwanda kilijipanga kuwa na sehemu kuu mbili ikiwemo sehemu ya kuyeyusha chuma na nyingine ni sehemu ya kuchongea vipuri mbalimbali vya mashine (Mashusho) lakini mpaka 1984 sehemu iliyokuwa imejengwa ni ya kuchongea vipuri tu, hivyo mtambo wa kuyeyusha chuma ulikuwa bado haujakamilika ndiyo maana kwa sasa lengo kubwa ni kufanya maandalizi ya kuujenga mtambo huo.

“Kwakuwa mtambo wa kuyeyusha chuma ulikuwa bado haujajengwa mpaka 1984, ilibidi baadhi ya malighafi za chuma zitoke nchini Bulgaria hivyo hapa tulikuwa tunazifanyia uunganishaji na umaliziaji yaani uchongaji na upakaji rangi (Finishing and assembling) kuanzia 1984 hadi 1992”, aliongeza Nyaluke.

Aidha, amefafanua kuwa, sababu kubwa iliyokifanya kiwanda hicho kufungwa Desemba 1998 kulitokana na uhaba wa malighafi kwa ajili ya kiwanda, lakini baadaye Serikali ikatafuta Mwekezaji ambaye angeweza kukiendeleza kiwanda hicho lakini mpaka 2006 hakupatikana ndipo ikaamua kukifufua upya ili kiendelee na uzalishaji na mwaka 2008 kikakabidhiwa kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Mhandisi Nyaluke ameeleza pia, katika kukifufua kiwanda hicho, iliwekwa mipango ya kiwanda kuweza kutengeneza vifaa ambavyo hapo awali vilikua vinaagizwa toka Bulgaria na ndiyo maana mpango wa kujenga mtambo wa kuyeyushia chuma ulipangwa, mpango mwingine ni utafutaji wa soko la vifaa vinavyohitajika nchini.

Amebainisha shughuli mbalimbali wazifanyazo kiwandani hapo ikiwemo mashine za kuchonga vyuma, mashine za kuchonga maumbo mbalimbali ya vyuma, mashine za kukata vyuma, mashine za kutoboa, mashine za uselemala kama vile randa, mashine za kukata mbao pamoja mashine za kukereza na kuchonga mbao.

“Eneo kubwa tuliloona linahitaji mashine zaidi nchini ni eneo la kusindika mazao mbalibali kama vile mashine za kusaga mazao, mashine za kukamua mafuta, za kusindika matunda na mpango wa mwanzo tuliona kwa miaka mitano ya kwanza tunaweza kutengeneza mashine mbalimbali zipatazo 700 ambazo zitauzwa hapa nchini na nyingi ni za kusindika mazao, ujenzi na mashine za uchimbaji madini migodini”, aliongeza Mhandisi Nyaluke.

Kuhusu suala la ajira kiwandani hapo, amefafanua kuwa, ajira watatoa ingawa sio kwa kiasi kikubwa kwasababu bado uzalishaji sio mkubwa lakini ajira kubwa ni zile zitokanazo na mashine zinazotengenezwa kiwandani hapo.

Ameeleza kuwa, kwa sasa wamepanga awamu mbalimbali za kukifufua kiwanda hicho ikiwemo ya kwanza itayochukua miaka miwili ya kutafuta fedha za kuunda mtambo wa kuyeyusha chuma, ya pili ni ya kuendelea kutengeneza vipuri vya mashine kiwandani hapo ili kuongeza bidhaa zaidi na ya tatu ni ndiyo ya ujenzi wa mtambo huo mkubwa wa kuyeyushia chuma.

Kiwanda cha KMTC kilianzishwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Bulgaria mnamo mwaka 1980 hadi 1983 na kilianza kufanya kazi 1984 ambapo dhumuni la kuanzishwa lilikuwa ni kutengeneza mashine zitakazotumika kutengeneza mashine za uzalishaji mbalimbali ikiwemo zana za kilimo, samani na dhana nyingine muhimu kama vile vipuri vya uzalishaji viwandani ambapo kwa sasa kampuni hiyo iko chini ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

WAZAZI WATAKIWA KUWAEPUSHA WATOTO NA MIMBA NA NDOA ZA UTOTONI.

$
0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akikata utepe kuashiria kuanza kwa mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
MN6
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Deodatha Makani akiongea jambo na Mkurugenzi wa Ubora na Maendeleo  wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
MN7
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake.
MN1
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akivishwa skafu na mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule hiyo.
MN2
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
MN3
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akioneshwa baadhi ya jumbe zilizopo katika mabango zilizoandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
MN4
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongozwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwendakulima Bi.Neema Daniel iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama kupanda mti wa kumbukumbu, alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.

MN8
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiongea na wanafunzi na wazazi waliohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita katika shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama ambapo aliwataka wazazi kuwalinda watoto na ndoa za utotoni pamoja na kuwasisitiza kuendeleza vipaji vyao.
MN9
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akitoa vyeti pamoja na zawadi kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama alipohudhuria mahafali ya 5 ya kidato cha sita ya shule hiyo.
MN10
MN11
MN12
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama pamoja na walimu wao.
MN13
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya Sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama wakifuatilia mahafali.
……………………………………………………………………
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Wazazi nchini wametakiwa kutekeleza wajibu wao kwa watoto kwa kuhakikisha wanawaendeleza na kuwawezesha wafanikishe ndoto zao kwa kuwaepusha na ndoa pamoja na mimba za utotoni.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto (Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii) Bi.Sihaba Nkinga katika Mahafali ya 5 ya kidato cha sita ya shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama.
Bi.Sihaba amesema kuwa wazazi wanajukumu la kuhakikisha wanawalea na kuwalinda kwani wazazi wanahaki ya kisheria ya kuwalinda watoto dhidi ya viashiria vyote vinavyoweza kuwaweka katika mazingira hatarishi.
Bi.Sihaba aliongeza kuwa wazazi na walezi wana haja ya kushirkiana na serikali katika kuwalinda watoto wakike kwani watoto wa kike ni nyenzo muhimu hasa kwenye mpango wa serikali katika kuelekea uchumi wa kati kupitia viwanda.
Aidha,Bi.Sihaba kuwa Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya Elimu sura namba 33 inayotoa katazo kumpa ujauzito motto wa shule chini ya miaka 18 hivyo wazazi wahakikishe wanalisimamia kwa pamoja ili kuweza kufanikisha sheria.
Naye Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Bw.Timothy Ndaya alieleza dhamira ya ofisi yake kuendelea kusimamia ubora wa shule hiyo pamoja na kushughulikia changamoto zake ili kuendana na mipango ya serikali ya awamu ya tano katika kuipa kipaumbele sekta ya elimu.
Mkurugenzi wa Ubora na Maendeleo  wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Save the Children Amy Schmiot amesema kuwa mahafali hayo ni ishara ya ushirikiano mzuri wa wazazi,walezi pamoja na uongozi wa shule utakaowezesha watoto hao kuvuna kile walichokipanda kwenye miaka 6 ya masomo yao.
Mkuu wa shule hiyo Bi.Neema Daniel alimuahidi Bi.Sihaba kuendelea kufanya vizuri katika mitihani ya kitaifa pamoja na kuiomba serikali kuwashika mkono hasa katika kurekebisha miundombinu ya shule hiyo ikiwamo mabweni na uzio wa shule.
Naye Mhitimu katika mahafali hayo Rose Bryton amewataka wazazi na walezi kutekeleza maagizo ya serikali ya kuwalinda watoto ili kuwawezesha kutimiza ndoto na matarajio yao kielimu.
Akitoa ushauri kwa wazazi wenzake Bi Rebecca Peter amewataka wazazi kuachana na mila zilizopitwa na wakati za kuwaozesha watoto wa kike katika umri usiotakiwa kisheria bali kuwaendeleza kufikia ndoto zao.
Jumla ya wanafunzi 143 wamehitimu masomo ya kidato cha sita katika shule ya sekondari Mwendakulima iliyopo Halmashauri ya Mji wa Kahama

MABALOZI WA VIJANA WA EAC WATOA SOMO KWA WANAFUNZI WA CHUO CHA STELLA MARIS, MTWARA

$
0
0
Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel wamekutana na Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, kwa lengo la kutoa mafunzo na kuwahamasisha Wanafunzi wa vyuo vikuu (Vijana) nchini kote, kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha katika Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, katika Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017. Jumla ya Wanafunzi 230 walihudhulia Warsha hiyo.
Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga akikabidhi Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara akikabidhi Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho.
Mabalozi wa vijana wanaoiwakilisha Tanzania katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga pamoja na Suzane William Mollel (wa tatu na nne kushoto) wakiwa wameshika Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na baadhi ya Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, wakati wa Warsha ya siku moja iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017.
Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (aliyesimama) akiwasilisha mada katika Warsha ya siku moja kwa Wafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, juu ya umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuuimarisha Mchakato wa Jumuiya hiyo Kikanda, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo, Mei 12, 2017. 
 Wanafunzi wa Chuo cha Stella Maris kilichopo Mkoani Mtwara, wakimsikiliza kwa makini Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Yohana Lambo Mayenga.
Sehemu ya wanafunzi hao wakiwa kwenye Warsha hiyo.

SHINDANO LA MISS USTAWI KUFANYIKA MEI 19 UKUMBI WA KING SOLOMON JIJINI DAR ES SALAAM.

$
0
0
Mashindano ya Miss Ustawi wa Jamii 2017 yanatarajia kufanyika siku ya ijumaa, Mei 19 katika Ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa Warembo hao, Clara Nyaki amesema maandalizi yafanyika kwa ustadi kutokana jinsi walivyowachuja. Amesema kuwa mshindi atakayepatikana atakuwa ameonyesha uwezo wake binafsi ikilinganishwa wengine wataofuata.

Clara amesema siku hiyo itakuwa ya kipekee kutokana na maandalizi watapopata mshindi wa kuwakilisha warembo wenzake. Pia, Clara amewakaribisha Watanzania wote kwa ujumla kuja kushuduhia tukio hilo.
Kwa upande wao hao Walimbwende hao wamesema wamejinada kila mmoja kuondoka na ushindi kulingana na maandalizi waliyoyafanya katika kipindi chote walichokuwa na mwalimu wao. Warembo watakaojimwaga siku hiyo ni Ruth Deouratius ,Melody Thomas, Elizabeth Julius, Careen Kileo, Loyce Jeck ,Diana Wambura , Angela Milanzi pamoja na Elice Mwakajila .
 Warembo wakiwa katika picha ya pamoja kwa pozi mbalimbali watavyokwenda katika kinyanganyilo hicho kitachofanyika Mei 19 katika ukumbi wa King Solomon jijini Dar es Salaam. 
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images