Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1226 | 1227 | (Page 1228) | 1229 | 1230 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza nas Wananchi wa Shehia tatu za Bungi, Ubago na Tunguu wakati wa kukabidhi vifaa kwa ajili ya shehia hizo tatu kwa matumizi ya Kijamii wakati wa shida na raha, Vifaa walivyokabidi majiko ya gesi 3, sinia 800  mitungi ya gesi 6 na mabusati. kwa ajili ya matumizi yao katika shughuli za kijamii, hafla hiyo ya makabidhiani imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Wilaya ya Kati Unguja. Na kuhudhuriwa na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja. 
  Mbunge wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe. Khalifa Salim Suleiman akizungumza na wananchi wa jimbo lake wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao ikiwa ni kutimiza ahadi kwa wananchi wa jimbo lao walioitowa wakati wa kampeni ya uchaguzi.hafla hiyo imefanyika katika tawi la CCMTunguu Wilaya ya Kati Unguja.
  Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi vifaa mbalimbali waliohidi kwa wananchi wa jimbo lao wakikabidhi vifaa hivyo kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja Ndg Ramadhan Abdallah na Uongozi wa jimbo hilo, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Tawi la CCM Tunguu Unguja. wakikabidhi mabusati na sinia.
  Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar wakikabidhi majiko ya gesi kwa ajili ya shia tatu kila shehia imepata jiko moja na mitungi ya gesi miwili. na sinia 200, kwa ajili ya matumizi ya kijamii katika shehia zao.Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika Tawi la CCM Tunguu Unguja. 
  Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi sufuria kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata sufuria mbili kubwa.
  Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu wakikabidhi mitungi ya gesi kwa Uongozi wa Jimbo kwa ajili ya matumizi ya Shehia za Jimbo hilo tatu kila shehia imepata mitungi miwili ya gesi mikubwa kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii katika jimbo lao zilizotolewa na viongozi hao..
  Mwenyekiti wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mzee Khatib Ramadhani akitowa shukrani kwa Mwakilishi na Mbunge kwa msaada wao huo kwa ajili ya kuwajali wananchi wa jimbo lao kwa msaada huo na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliokusudiwa katika shughuli za kijamii katika shehia husika za jimbo hilo. 
  Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali dhamira wa msaada huo kwa wananchi wa jimbo lao kuweza kuwasaidia katika matumizi yao ya shughuli za kijamii zinazotokea kwa wananchi hao ili kuweza kuvitumia kupunguza gharama za kukodi vifaa hivyo.

  Imetayarishwa na OthmanMapara,zanzinews.com.
  email. othmanmaulid@gmail.com.


  0 0


  0 0


  0 0  0 0

   Mratibu  wa Masuala ya Usalama wa Afya, Mazingira na  Udhibiti wa Ubora kutoka Kampuni ya Puma Energy, Rehema Madoffe akimvisha Abubakar Selemani mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Ungindoni iliyopo Kigamboni Dar es Salaam moja ya fulana inayoakisi mwanga ikiwa ni sehemu ya shehena iliyotolewa kwa shule hiyo kwa  ushirikiano na Taasisi ya Amend Tanzania kusaidia kampeni ya kupunguza ajali za barabarani hususani kutetea maisha ya watoto wa shule jana  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)
   Ofisa Mipango wa Taaasi ya Amend Tanzania, Neema Swai akigawia fulana maalum zinazoakisi mwanga kwa waendesha bodaboda wa Manispaa ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam, jana, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Usalama barabarani ya Umoja wa Mataifa(UN-Global Road Safety Week)


  0 0

  Mhe. Sylvester Mabumba Balaozi wa Tanzania ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Visiwa vya Komoro jana tarehe 09 Mei aliwasilisha nakala za hati zake za uwakilishi kwa Mhe. Mohambed Baccar Dossar, Waziri wa Mambo ya Nje wa Komoro. Hafla hiyo ilifanyika siku hiyo hiyo ambayo Mhe. Balozi aliwasili Visiwani Komoro jambo ambalo linaonesha jinsi gani nchi hizi mbili zimedhamiria katika kuboresha na kukuza mahusiano yaliopo baina yao.

  Katika hafla hiyo Mhe. Dossar alichukua fursa hiyo kumkaribisha Mhe. Balozi Mabumba Visiwani Komoro na kumtakia kila la kheri katika kipindi chake ambacho atakuwa Balozi Visiwani hapa. Aidha Mhe. Waziri alimuahidi Mhe. Balozi Mabumba kuwa nchi yake itampatia ushirikiano maradufu na kwamba milango yake ipo wazi muda wowote ambapo Mhe. Balozi atakuwa na shida ya kuonana nae na kufanya mazungumzo.
   
  Kwa upande wake Mhe. Balozi Mabumba alionyesha furaha yake kwa kumuelezea Mhe. Waziri kuwa amejiskia faraja sana kwa kuchaguliwa kuwa Balozi wa Pili kuiwakilisha Tanzania Visiwani Komoro na kwamba anaimani kuwa Serikali ya Komoro itampatia ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake. 
   
  Aidha Mhe. Balozi Mabumba alieleza kuwa uhusiano uliopo baina ya Tanzania na Komoro ni wa Kihistoria na unapaswa kudumishwa. Mhe Balozi alimueleza Mhe. Waziri kuwa moja ya agenda zake za mwanzo ambazo anataka kutekeleza ni ile ya utiaji saini wa Mkataba wa Kudumu wa Ushirikiano baina ya Tanzania na Comoro (Joint Permanent Commission).

  0 0

  Waziri wa Mambo ya NdaniyaNchi, Mwigulu Nchemba akiwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapo aliliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjini Dodoma. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa na Wabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kulia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo,Mhandisi Hamad Masauni.

  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akijibu maswali yaliyoelekezwa kwa wizara yake wakati wa kipindi cha maswali yaliyoulizwa naWabunge wakati wa Bunge la Bajeti mjini Dodoma.Kushoto ni Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba. 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na makamanda wa Jeshi la Polisi muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Bunge la Bajeti ambapo wizara yake iliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akifurahia abaadhi ya wabunge mara baada ya kumaliza kuwasilisha makadirio ya Bajeti yake kwa mwaka 2017/2018 ambapoa liliomba Bunge liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 930,396,817,000 wakati wa kikao cha Bunge la Bajeti,mjiniDodoma.PichanaWizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 


  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0

  Wakazi wa Mikocheni B wanaounda Chama cha FRIENDS OF OCEANS wakisafisha fukwe ya Escape One katika uzinduzi wa kampeni ya OKOA BAHARI ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT ,na usafi huo ulifanyika mapema mwisho wa wiki iliyopita. 
  Friends of oceans wakiendelea na usafi wa fukwe ya Escape one ikiwa kama uzinduzi wa kuanza usafi huo kwa kila mwezi na pia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na rasilimali za bahari 
  Usafi ukiendelea katika fukwe ya Escape One ambapo kulikutwa chupa za bia,makopo ya maji, sindano na vingi ambavyo ni hatari kwa afya ya watumiaji wa fukwe hiyo mapema mwishoni wa wiki iliyopita . 
  Friends of Ocean wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza usafi katika fukwe ya Escape One Mikocheni B kama uzinduzi wa kampeni ya OKOA BAHARI yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT 

  Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye tisheti nyekundu) ambao ni waratibu wa kampeni hii ya OKOA BAHARI akiwa na wadau wa Friends of Ocean wakati wa usafi uliofanyika katika fukwe ya Escape One 
  Muasisi na Kiongozi wa Friends Ocean Boss Brown (mwenye tisheti ya kijani) akifafanua jambo mara baada ya kumaliza usafi katika fukwe ya Escape One ikiwa ni uzinduzi wa kampeni ya Okoa Bahari ambayo katika uzinduzi wa kampeni ya OKOA BAHARI yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa .Kampeni hiyo inaratabiwa na kampuni ya KONCEPT 
  Mkurungezi Mtendaji wa Koncept Krantz Mwantepele (mwenye tisheti nyekundu) ambao ni waratibu wa kampeni hii ya OKOA BAHARI akifafanua jambo kwa wadau wa Friends of ocean mara baada ya kumaliza usafi katika Fukwe za Escape One . OKOA BAHARI yenye lengo ikiwa ni moja ya juhudi za kuweka mazingira safi ya bahari ikiambatana na kuunga kampeni ya kimataifa ya kutunza fukwe na mazingira ya bahari kuelekea kutimiza Agenda ya mwaka 2030 ya mpango wa maendeleo ya Umoja wa mataifa 
  Fukwe ya Escape One mara baada ya kusafishwa na wadau wa Friends Of Ocean mwishoni wa wiki iliyopita

  0 0


  Rais Mstaaafu Dkt Jakaya Kikwete akifuatilia Mkutano wa Nchi Majirani wa Libya
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Mgogoro wa Libya Balozi Martin Kobler jijini Algiers
  Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akitoa msimamo wa Umoja wa Afrika kuhusu Mgogoro wa Libya .

  Rais Mstaafu katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo na Mwenyekiti wa AU Mhe. Jean-Claude Gakosso. Kushoto ni Mkuu wa Ofisi ya Uwakilishi wa AU kwa Libya Bi. Wahida Ayari .


  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika katika Mgogoro wa Libya ameendelea na juhudi zake za usuluhishi wa mgogoro wa Libya kwa kushiriki katika Kikao cha 11 cha Mawaziri wa Nchi Jirani na Libya kilichofanyika jijini Algiers, Algeria tarehe 8 Mei, 2017.

  Katika Kikao hicho, Rais Mstaafu amepongeza juhudi zinazoendelea za kupatanisha pande zinazogombana nchini Libya na mafanikio yanayopatikana ikiwemo kuimarika kwa hali ya usalama, kudhibitiwa kwa vitendo vya kigaidi, kuongezeka kwa shughuli za uzalishaji wa mafuta na kufufuliwa kwa mawasiliano kati ya pande zinazohasimiana.
   
   Ameunga mkono jitihada zinazochukuliwa na nchi za Algeria, Misri, Tunisia na UAE katika kuhimiza mazungumzo ya Amani. Amesisitiza umuhimu wa pande mbili za mgogoro kuheshimu Makubaliano ya Amani ya Libya (Libya Political Agreement) na kutekeleza vipengele vyake bila ajizi.

  Akiwa jijini Algiers, Rais Mstaafu amefanya pia mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo anayemuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati wa Wakuu wa Nchi za Umoja wa Afrika kuhusu Libya Mhe Jean-Claude Gakosso na Balozi Martin Kobler, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Mgogoro wa Libya (UNSMIL).

  Rais Mstaafu anatarajiwa kumalizia ziara yake nchini Libya kukutana na viongozi wakuu wa pande zinazotofautiana nchini humo.

  0 0


  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwahakikishia wateja wa benki hiyo na umma wa ujumla kuhusu dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa huduma zake hapa nchini. Kushoto Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja wa benki hiyo, Ndabu Lilian Swere.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo yao. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati.
  Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa EcoBank Tanzania Raphael Onyango akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake hapa nchini kutokana na ahadi na mikakati madhubuti waliyojiwekea. Wa pili kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati (kulia).
  Mkuu wa kitengo cha biashara wa Ecobank Tanzania, Respige Kimati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na malengo yake. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za biashara za ndani Ndabu Lilian Swere.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na mikakati waliyojiwekea. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati na kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja.   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict amefanya mkutano na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, na kueleza kwamba hawana dhamira ya kusitisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo makubwa waliyojiwekea ya kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

  “Hii ilikuwa ni ahadi yetu tangu tulipoanza kufanya shughuli zetu hapa nchini miaka saba iliyopita na itaendelea kuwa ahadi yetu mpaka hivi sasa,” alisema Benedict.

  Licha ya kukiri kwamba kumekuwapo na ongezeko la wateja kushindwa kurejesha mikopo yao mwaka jana, alisema benki hiyo imejiwekea utaratibu mzuri na hatua sahihi za jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

  Alisema, “Tumechukua hatua muhimu ili kuwezesha urejeshaji wa mikopo mbalimbali ndani ya miezi mitatu iliyopita na tunaamini kwamba mfumo tuliouanzisha utatuletea mafanikio makubwa ndani ya miezi michache ijayo.”

  Aliongeza kuwa, nguvu ya msingi ya benki hiyo ina ungwa mkono na wanahisa wakubwa ambao wanaifanya benki kuwa imara, madhubiti na kuaminika na hivyo kuwa moja ya chombo cha fedha kinachoweza kuendana na hali yoyote ya dhoruba.

  Washirika wakubwa wa Ecobank ni pamoja na Nedbank ya Afrika Kusini( asilimia 21), Qatar Nation Bank (asilimia 20), Public Investiment Corporation ya Afrika Kusini ( asilimia 14) na International Finance Corporation iliyopo chini ya Benki ya Dunia (asilimia 14).

  Benedict aliongeza kwamba Ecobank ina shauku kubwa ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendeleza uchumi kupitia huduma zake. Hata hivyo, mwaka 2016 ilishuhudia ongezeko la kutokulipwa kwa mikopo, jambo ambalo liliisukuma benki hiyo kubadilisha mbinu na kuja na mikakati mipya ya kukabiliana na hali hiyo.

  Alielezea kwamba Ecobank Tanzania haina lengo la kufunga huduma zake na badala yake imeanza kufanya mabadiliko katika shughuli zake ili kuweza kukabiliana na hali ya sasa.

  Pia aliongeza kwamba ili kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa ufanisi zaidi, benki hiyo imewekeza zaidi kwenye huduma zake za kimtandao na malipo ili kuweza kuwahudumia wateja wake kwa urahisi zaidi na taifa kwa ujumla.

  “Hivi karibuni tulizindua app ya Ecobank Mobile Banking ambapo wateja watapata huduma ya Xpress Akaunti.

  Huduma ya Xpress Akaunti inawawezesha wateja kufungua na kutumia akaunti zao bila ya kufika kwenye matawi yetu, huku wakiokoa muda, pesa na kuongeza ufanisi na usalama, hii yote ikiwa ni mikakati ya Ecobank kwa Afrika.

  Malengo mazuri ya Ecobank ya baadaye ni kuwa taasisi imara iliyojikita kwenye msingi mzuri.

  Kwa mara nyingine ninapenda kuwahakikishia tena wateja wetu na wadau kwamba tutaendelea kuwepo hapa.
   


  0 0

  Meneja Masoko wa BIko Goodhope Heaven mwenye fulana ya njano akionyesha nyaraka zilizowekwa kiasi cha Sh Milioni 10 kwa ajili ya mshindi wao wa wiki, Emmanuel Philipo aliyeibuka na ushindi wa mamilioni hayo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwa Heaven ni Philipo akifuatiwa na Afisa wa NMB na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

  Mshindi wa MIlioni 10 Biko aahidi kuuaga umasikini

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa BIkoIJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.

  Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.

  Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwakewa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
  Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10.
  Mazungumzo yakiendelea baada ya makabidhiano hayo.
  Afisa wa NMB akizungumza jambo na mshindi wa Sh Milioni wa Biko, Emmanuel Philipo baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 10 zake kutoka Biko.
  Afisa wa NMB akimkabidhi nyaraka mshindi wa Sh Milioni 10, Emmanuel Philipo katikati akishuhudiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
  Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi, huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi wanaocheza bahati nasibu.

  "Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko, hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050 na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa wiki.

  "Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuthubutu katika fursa mbalimbaliikiwamo ya kucheza mchezo wa Biko kwa sababu sio tu zawadi zao mbalimbalikama vile Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 na Sh MIlioni Moja za papokwa hapo zinaeleweka, bali pia hata unapotangazwa mshindi wa Sh Milioni 10,huwa wanakabidhi haraka kwa mshindi wao," Alisema.

  Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alimpongeza Philipo kwa
  ushindi huo na kumtaka awe balozi mzuri kwa Watanzania wote kwa ajili
  ya kuwapa elimu ya kuhakikisha kuwa wanacheza Biko ili nao waibuke na
  mamilioni ya Biko.

  Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema
  ushindi kwenye bahati nasibu yao ni mwepesi na kila mchezaji anaweza
  kuibuka na fedha kutoka kwenye bahati nasibu yao ya Biko.

  "Huu ni muda wa kulala masikini na kumka tajiri, hivyo njia ya ushindi ni
  kucheza mara nyingi zaidi ambapo kila tiketi moja inayopatikana kwa sh
  1000 inatoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia
  kwenye droo kubwa ya wiki ya kushinda Sh Milioni 10," Alisema.

  Philipo ni mshindi wa nne wa Sh Milioni 10 ambapo jana alikabidhiwa fedha
  zake kwa ajili ya kuanza matumizi kama walivyokabidhiwa wenzake kutoka
  jijini Dar es Salaam na Mwanza.

  0 0

  Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Biashara litakalofanyika kesho May 11 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

  Katika Kongamano hilo, Mhe. Zuma ataongozana na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, pamoja na Wafanyabiashara wakubwa kutoka nchi hizo.

  Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari amesema kuwa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia kituo hicho wameandaa Kongamano hilo, na kutoa wito kwa Wafanyabiashara wa Tanzania kujitokeza kwa wingi kukutana na Wafanyabiashara wenzao wa nchi hiyo ya Afrika Kusini.

  Tandari amesema kuwa Sekta kubwa zitakazojadiliwa katika Kongamano hilo ni Sekta ya Nishati, Viwanda, Miundombinu, Uchukuzi, Usafirishaji, Huduma ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA), Maji na Madini.

  Pia amesema Afrika Kusini ni Taifa ambalo lipo katika nchi kumi bora zilizowekeza kwa wingi hapa nchini, hivyo ni fursa kuchamshana kiuchumi, pia wameandikisha miradi 63 ambayo imeajiri vijana wengi.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Clifford Tandari akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam kuhusu Kongamano la Biashara litakalofanyika May 11 mwaka huu jijini Dar na kuhudhuriwa na Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Magufuli. 

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhandisi Evarist Ndikilo, akiwa ametembelea shamba la mfano la zao la biashara la korosho lililopo Ruvu JKT, wilayani Kibaha. (picha na Mwamvua Mwinyi) . …………………………………………………………………..

  Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

  MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo,amemaliza ziara yake ya kutembelea wilaya sita kimkoa,ambapo amehimiza mambo makuu manne ikiwemo ulinzi na usalama,uwekezaji,kilimo cha matunda na korosho.

  Aidha amekemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu na wengine kujeruhiwa pasipo sababu za msingi.

  Akimaliza ziara yake wilayani Kibaha,mhandisi Ndikilo,alieleza mkoa wa Pwani una viwanda vitatu vikubwa vya kusindika matunda kwa sasa ambavyo endapo wakulima watavitumia watanufaika kwa kiasi kikubwa.

  Alisema,kiwanda cha Bakhresa ambacho kipo Mwandege -Mkuranga kimeshaanza kazi na kile cha Elven Agri co.ltd kilichopo kata ya Mapinga -Bagamoyo huku cha Sayona kinachojengwa kata ya Mboga kikiwa kwenye hatua za mwisho za ujenzi.

  Mkuu huyo wa mkoa alisema kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhresa kina uwezo wa kusindika tani 350 za matunda kwa siku na uwekezaji wake umegharimu sh.bil.261.

  Mhandisi Ndikilo alisema uwekezaji wa viwanda hivyo ni mkubwa na utawatengenezea kipato na soko wakulima wa matunda .

  “Niwasihi wakulima wa mkoa wa Pwani na mikoa mingine kulima kwa bidii maembe,nyanya,mananasi,mapeasi,pilipili “

  “Sio tu mlime kwa kilimo chetu tulichokizoea ,hapana kwasasa inabidi twende na mabadiliko ya teknolojia ya kisasa kwa kutumia mbegu,pembejeo bora na mpalilie na kutumia madawa ili kupata matunda yatakayouzika”alifafanua.

  Hata hivyo mhandisi Ndikilo aliwaomba wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kukimbilia kuwekeza mkoani Pwani kwani unaelekea kuwa ukanda wa viwanda na uwekezaji.

  Alisema kwasasa viwanda vilivyopo ni 200 ambavyo vipo vikubwa,vidogo na vya kati na mabavyo vimeanza kazi,vinavyoendelea na mchakato na vingine hatua za mwisho za ujenzi .

  Akizungumzia masuala ya ulinzi na usalama ,aliwataka wananchi kila mmoja kuwa mlinzi wa mwenzake na kuacha kuamini wageni wanaoingia katika maeneo yao.

  “Ukiona kuna mtu yupo kijijini ama kwenye mtaa wako humjui na unamtilia shaka basi toeni taarifa kwenye vyombo vya dola ili viweze kumfuatilia”

  Hakusita kukemea migogoro ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa ikigharimu maisha ya watu kwa kujeruhiwa ma kupoteza maisha.

  Kwa mujibu wa mhandisi Ndikilo,migogoro hiyo haina tija miongoni mwao na kusisitiza umoja,upendo na amani katika pande hizo mbili .

  Alisema wamejipanga kuongea na mhimili husika ili kuuomba kumaliza migogoro ya wakulima na wafugaji kwa kutoa hukumu badala ya kupiga faini.

  Mhandisi Ndikilo alisema wafugaji wakitozwa faini wamekuwa na kiburi na dharau kutokana na kuwa na uwezo wa kulipa hivyo kuanzia sasa wapigwe kifungo ili kukomesha jeuri yao.

  Katika hatua nyingine amewataka wazazi na walezi kusomesha watoto wao wa kike na wakiume pasipo kuwabagua kwani elimu ni ufunguo wa maendeleo ya maisha yao ya baadae.

  Nae katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji mkoani Pwani,Shangwe Twamala alisema ziara hiyo ililenga kutembelea maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya kilimo cha biashara kama kwenye maghala ya korosho na viwanda vya matunda.

  Pia kutembelea mashamba ya wakulima wa mihogo na kuhimiza kilimo kinachostahimili ukame ikiwa ni pamoja na mhogo,mtama,mikunde na viazi vitamu.

  Twamala alisema wananchi wanapaswa kujiwekea utaratibu wa kucheza na misimu ya mvua kwa kulima mazao yanayotakiwa ili kukabiliana na uhaba wa njaa.

  Katika ziara hiyo mkuu wa mkoa wa Pwani,mhandisi Ndikilo alitembelea maeneo ya Mji wa Rufiji,Mkuranga,Kibiti,Bagamoyo,Chalinze,Kisarawe na Kibaha.

  0 0

  Katika kufanikisha azma ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti, kampuni ya mawasiliano ya Halotel imeendelea kuunganisha huduma yake ya Halopesa na huduma nyingine zaidi ili kuendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa Watanzania .

  Katika kulifanikisha hilo Halotel imeingia makubaliano ya mkataba wa utoaji wa huduma na kampuni ya Selcom, ushirikiano utakaowawezesha mamilioni ya wateja wa mtandao huo kutoa na kutuma pesa, kununua vocha za muda wa maongezi na kufanya manunuzi mbalimbali.

  Hatua hii itawawezesha watanzania wengi zaidi kufikiwa na huduma za kifedha kwa njia ya mtandao ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya serikali ambayo inazitaka taasisi mbalimbali za kifedha kuwafikia wananchi na huduma zao hasa kwa maeneo ya vijijini.

  Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel, Bw. Le Van Dai amesema kuwa ni hatua nyingine kubwa katika utoaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi nchini Tanzania. Sasa kupitia huduma ya Halopesa itakuwa imewezesha kupanua wigo kwa wateja wa mtandao huo kuweza, kutoa na kuweka fedha, pamoja na kufanya malipo mbalimbali kwa urahisi zaidi.

  “Ushirikiano huu ni wa kipekee katika kurahisisha maisha ya watanzania ambao wamekuwa wakipata tabu kupata huduma za kifedha kutokana na maeneo wanayoishi. Sisi kama Halotel hadi sasa tumewafikia watanzania kwa zaidi ya asilimia 95. Hivyo ni dhahiri kwamba wateja watakaojiunga nasi wataweza kutoa au kuweka fedha huko huko waliko kupitia kwa mawakala wetu ambao wameenea nchi nzima,” alisema Dai.

  “Tunatambua changamoto ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwasibu Watanzania hasa wa kipato cha chini. Kwani wengi wao walikuwa wanakwama kuweza kupata huduma za kifedha kutokana na miundombinu kutowafikia. Mpaka hivi sasa Halotel ina mawakala zaidi ya 30,000 walioenea nchi nzima.
   
   Hii itawawezesha wakazi wa maeneo ambayo hayakuwahi kuwa na mawasiliano kabisa au huduma za kibenki sasa kuweza kupata huduma za kifedha kupitia simu zao za mkononi huko huko walipo,” alihitimisha Mkurugenzi huyo.

  Vilevile wateja wa Halopesa wataweza kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti zao za Halopesa kupitia mawakala wa Selcom zaidi ya 17,000 wanaopatikana nchi nzima. 
    Afisa Uhusiano wa Selcom Sabrina Muniru akimuelekeza namna ya kufanya miamala kupitia mashine ya Selcom, kampuni hizo zimeingia makubaliano yatakayo wawezesha wateja wa Halopesa kufanya miamala ya kifedha kupitia mawakala wa selcom nchi nzima.
   Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo kwa pamoja wakionesha mkataba wa makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima.
    Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima.
    Mkuu wa Halotel, Le Van Dai (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mipango wa Selcom, Benjamin Mpamo wakitia saini mikataba ya makubaliano ya kibiashara baina ya kampuni hizi yatakayo wawezesha wateja wa  Halopesa kutoa na kuweka pesa, pamoja na kununua muda wa maongezi kupitia mawakala wa Selcom nchi nzima, Wanaoshuhudia ni wafanyakazi wa kampuni hizo.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA. 

  Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano imesema itajenga daraja la juu kwa ajili ya kivuko cha waenda kwa miguu(Over head Pedestrian Bridge) eneo la Kawe Bondeni. 

  Hayo yamesemwa Bungeni leo na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe aliyekuwa akijibu swali la Mbunge wa Kawe Mhe.Halima Mdee kwa Niaba ya Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano. 

  “Tatizo la kivuko cha waenda kwa miguu eneo la Kawe Bondeni hadi Jeshini Kata ya Mbezi Juu na Kawe Tayari limeshapatiwa ufumbuzi”,Aliongeza Mhe.Kamwelwe. 

  Amesema kwa sasa Mkandarasi wa kujenga daraja hilo yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi katika eneo hilo muhimu. 

  Aidha Serikali ina mpango wa kuweka taa za kuongozea magari katika Barabara ya Mwenge-Tegeta ambapo Mkandarasi ameshapatikana wa kuweka taa hizo katika makutano ya Afrikana na anatarajia kuanza kazi wakati wowote. 

  Mbali na Hayo tatizo la Udogo wa mapokeo na matoleo ya maji ya mvua yanayosababisha kero katika eneo la Makonde hadi Mbuyuni,Serikali inakamilisha taratibu za kusaini mkataba wa ujenzi wa mtaro mkubwa eneo la Mbezi Samaki ambao utatatua kero ya barabara kujaa maji nyakati za mvua. 

  “Serikali ya Awamu ya Tano ni makini sana na itahakikisha changamoto hizi inazifanyia kazi ili wananchi waweze kutumia barabara zetu vyema”Aliongeza Mhe.Kamwelwe.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe

  0 0
 • 05/10/17--07:04: TANGAZO LA TTCL


 • 0 0

  KIKOSI Mbeya City Fc , leo kimeanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Yanga uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii. 

  Afisa habari wa kikosi hicho Dismas Ten amesema kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi. 

  Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu na matarajio yao ni kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi, kwani wanafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo haliwapi hofu kwa sababu wana kikosi kizuri. 


  Ten amesema katika duru ya kwanza waliweza kupata matokeo mazuri na sasa wanakwenda Jijini Dar kuhitimisha dhamira yao ya kupata pointi sita msimu huu kutoka kwao

  Akiendelea zaidi Ten alisema City imekuwa na wiki nne za kujindaa vizuri ili kuikubali Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru. 

  "Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye uwanja wa Sokoine April 13,hivyo nguvu zetu zote tunaziweka siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,".amesema Ten. 

  Miongoni mwa nyota waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Mrisho Ngassa,Hassan Mwasapile,Tumba Lui na Zahoro Pazzi 

  Kwa upande wake kocha mkuu Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Yanga hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi. 

  "Sina wasiwasi,wakati huu ambao sikuwa na mchezo wa ligi nilikuwa nawafuatilia, najua mbinu zao na nimewandaa vijana wangu vizuri ni wazi tutashinda tena dhidi yao kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa duru ya kwanza".

  0 0  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (kushoto) akisalimiana na Mbunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya Mhe. Alojz Peterle (kulia) pale ugeni wa Wabunge kutoka Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  A
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza jambo pale ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya ulipomtembelea leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  A 1
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akizungumza  jambo pale alipopata ugeni wa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya, katika Kikao kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  A 4
  Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wanne kulia) akipiga picha ya pamoja na Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakiongozwa na Mhe. David Martin (wanne kushoto) baada ya kumalizika kikao kilichofanyika  leo katika Ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.
  A 3
  Wageni wa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai ambao ni Wabunge wa Bunge la Umoja wa Ulaya wakifwatilia Vikao vya Bunge vinavyoendelea leo Mjini Dodoma.
  (PICHA NA OFISI YA BUNGE)

  0 0

  Rais wa Heshima wa shirikisho hilo, Leodegar Chilla Tenga
   
  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limempongeza Rais wa Heshima wa shirikisho hilo, Leodegar Chilla Tenga kwa kuteuliwa kuwa Rais wa Kamati ya Usimamizi wa Leseni za Klabu katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).

  Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Afisa Habari wa TFF ,Alfredy Lucas amesema kuwa kwa mujibu wa taarifa ya CAF, Tenga atasaidiwa Dany Jordaan wa Afrika Kusini katika kusimamia mpango huo muhimu kwa maendeleo ya mpira wa miguu barani Afrika.

  “Uteuzi wake ulitangazwa na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad Jumatatu Mei 8, 2017 mara baada ya Kikao cha Kamati ya Utendaji CAF, chini uongozi mpya kilichofanyika katika Hoteli ya Sheraton, Manama, Bahrain.Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji, Rais wa TFF Jamal Malinzi alimpongeza Tenga akisema: “Hii ni fursa nzuri inayojenga taswira ya thamani na uwezo viongozi wetu wa mpira wa miguu nchini na kutambulika nje ya nchi katika taasisi za kimataifa kama CAF.

  “Kwa niaba ya Kamati ya Wanafamilia wote wa mpira wa miguu, Wajumbe wa Kamati Utendaji, nachukua nafasi hii kumpongeza sana sana Rais wa Heshima wa TFF, Mzee wetu, Ndugu Leodegar Tenga kwa nafasi nyeti ya kusimamia Kamati ya Leseni za Klabu. Tunamtakia kila la kheri tukiamini nafasi hiyo ana uwezo nayo na bila shaka Mwenyezi Mungu, atakuwa pamoja na Tenga,” amesema Tenga.

  Katika katika mkutano wa Bahrain, Rais wa CAF alipendekeza majina ya viongozi wawili kuwa Makamu wa rais, wa kwanza ni Kwesi Nyantakyi kutoka Ghana na wa pili ni Omari Selemani kutoka DR Congo na pendekezo hili lilipitishwa na kamati.

  Uteuzi wa wajumbe wawili wa ushirikiano wa Kamati ya Utendaji. Kwa mujibu wa masharti ya sheria, Rais wa CAF alifanya mapendekezo ya wanachama mawili wa ushirikiano kwenye kamati ya utendaji ya CAF ambako wanachama waliopitishwa ni Moses Magogo (Rais wa shirikisho la mpira wa miguu Uganda na Ahmed Yahya – Rais wa Shirikisho la Mpira wa Maurtania.

  Muundo wa Kamati ya dharura, Mwenyekiti ni Rais wa CAF, Ahmad Ahmad na wajumbe wake ni Kwesi Nyantakyi (Ghana), Omari Seleman (DR Congo), Fouzi Lekjaa (Morocco), Souleiman Waberi (Djibouti) na Musa Bility (Liberia).

  Awali, Rais wa CAF alitoa mapendekezo ya uanzishwaji wa kamati mbili za dharula, kamati hizi zitajumuisha hasa marais wa mashirika wanachama. Moja itakuwa katika malipo ya marekebisho ya katiba na nyingine katika malipo ya fidia, semina zitaandaliwa kwa marais wa mashirika wanachama ili kuwasilisha kazi ya kamati ya marekebisho ya katiba na mchango wao kabla ya kukamilisha rasimu ya kuwasilishwa kwa Kamati ya utendaji na baraza kuu, muundo wa kamati ya dharura ni kama ifuatavyo.

  Kamati ya Marekebisho ya Katiba Rais wake ni Kwesi Nyantakyi (Ghana) huku wanachama ni Lamine Kaba Badjo (Gambia), Sita Sangare (Burkina Faso), Moses Magogo (Uganda), Mclean Letshwiti (Botswana), Edouard Ngaissona (Jamhuri ya Afrika ya Kati), Elvis Chetty (Shelisheli) na Ahmed (Misri)


  Rasilimali Watu: Ludovic Lomotsy (Mshauri wa Rais CAF).

  Kamati ya fidia, Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) huku wanachama wake ni Monteiro Domingos Fernandes (Sao Tome), Ahmed Yahya (Mauritania), Hani Abo Rida (Misri)

  Rasilimali Watu: Essam Ahmed (CAF Kaimu Katibu Mkuu), Mohamed El Sherei (CAF Mkurugenzi Fedha)

  Kongamano la mashindano ya CAF. Kamati hii inatarajiwa kupangwa nchini Morocco Julai 15-16, 2017. Shirikisho la soka nchini humo lina mpango wa kubeba gharama kuhusiana na kongamano hili, ambapo litaleta wadau pamoja mbalimbali ya mpira wa miguu Afrika (Wachezaji, Waamuzi, makocha, vyombo vya habari.

  Kongamano hilo litajadili masuala yote kuhusiana na mashindano ya CAF ikiwa ni pamoja na shirika, muundo na ratiba na kufuatiwa na mkutano wa Kamati ya Utendaji ya CAF wa Julai 17, 2017 ambako utajadili pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa maazimio makuu ya kongamano.

  Uteuzi ya marais na makamu wa rais wa Kamati za Kudumu. Kamati ya Fedha, Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) huku Makamu wa Rais ni Monteiro Domingos Fernandes (Sao Tome). Kamati nyingine ni ya maandalizi kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambapo Rais ni Amaju Pinnick (Nigeria) na Makamu wa Rais ni Philip Chiyangwa (Zimbabwe)

  Kamati ya maandalizi kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika Rais ni Musa Bility (Liberia) huku makamu akiwa ni Wadie Jari (Tunisia). Kamati ya maandalizi kwa ajili ya Interclub Mashindano Rais ni Fouzi Lekjaa (Morocco) na Makamu ni Mutassim Jaafar (Sudan).

  Kamati ya maandalizi kwa ajili ya U-20 Kombe la Mataifa Rais ni Tarek Bouchamaoui (Tunisia) na makamu ni Rui Da Costa (Angola). Kamati ya maandalizi kwa ajili ya mpira wa miguu wanawake Rais ni Isha Johansen (Sierra Leone) na makamu ni Moses Magogo (Uganda).

  Kamati ya Maandalizi kwa ajili ya Mpira wa Ufukweni Rais ni Moses Magogo (Uganda) na Makamu Rais ni Kalusha Bwalya. Kamati ya waamuzi Rais ni Soleimani Waberi (Djibouti) na Makamu Rais ni Lim Kee Chong (Mauritius).

  Kamati ya ufundi na maendeleo ya mpira wa miguu Rais ni Kalusha Bwalya (Zambia), makamu ni Souleiman Waberi (Djibouti) wakati Kamati ya Mambo ya Sheria, Rais ni Ahmed Yahya (Mauritania) na Makamu Rais ni Augustin Senghor (Senegal). Kamati ya mchezo wa uungwana (fair play), Rais ni Almamy Kabele Camara (Guinea) na Makamu Raisi ni Isha Johansen (Sierra Leone)

  Kamati ya Habari Rais ni Amaju Pinnick (Nigeria) na Makamu Rais ni Hedi Hamel (Algeria). Kamati ya matibabu, Rais ni Adoum Djibrine (Chad) na Makamu Rais ni Yacine Zerguini (Algeria) na Kamati ya Masoko na TV Rais ni Danny Jordaan (Afrika Kusini) huku Makamu Rais ni Rui Da Costa (Angola).

  0 0

    Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho, Dkt.Chuwa amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuboresha zaidi upatikanaji wa takwimu rasmi nchini. (Picha na Veronica Kazimoto)
    Kaimu Mkurugenzi wa Utawala, Fedha na Masoko Bi. Lilian Karumuna wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. 
   Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania tawi la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (TUGHE) Bi. Raya Mikidadi akifafanua jambo wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu Dkt. Albina Chuwa (hayupo pichani) wakati wa kikao cha wafanyakazi wa ofisi hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam. (Picha na Veronica Kazimoto)

older | 1 | .... | 1226 | 1227 | (Page 1228) | 1229 | 1230 | .... | 1897 | newer