Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live

NEC yaanza kutekeleza mpango wa Elimu ya Mpiga Kura kupitia Redio

0
0
Hussein Makame, NEC 

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wananchi walioko kwenye halmashauri mbalimbali nchini, kuitumia vyema fursa ya utoaji wa elimu ya mpiga kura kupitia redio za kijamii kwenye halmashauri zao ili kuondoa manung’uniko kwenye chaguzi.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo Bw. Kailima Ramadhani wakati akizungumzia mpango wa kutoa elimu ya mpiga kura nchi nzima ulioanza kutekelezwa Mei 8 mwaka huu hii katika mikoa kumi nchini.
Alisema kupitia mpango huo wananchi wanaosikiliza redio za kijamii kwenye halmashauri nchini, watapata fursa ya kujifunza elimu ya mpiga kura na kuelewa masuala yote muhimu yanayohusu mfumo mzima wa kupiga kura. 

“Tumepanga mpango, Tume itasambaa nchi nzima kuzungumzia elimu ya mpiga kura kwenye redio za kijamii zilizoko kwenye halmashauri zote za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.” alisema Bw. Kailima.

Alisisitiza kwa kutoa wito kwa wananchi walioko maeneo ambayo Tume itakwenda kutoa elimu ya mpiga kura, wasikilize na kuuliza maswali ili waweze kuelewa.

“Hii ni fursa kwa wananchi ambayo muda mrefu hawajawahi kuipata, hivyo nawaomba wafuatilie ili waweze kuelimika zaidi ili yale manung’uniko ya kura yatakuwa yamekwisha na tutakuwa na uchaguzi mzuri zaidi ya ile ambayo tumeifanya.” Alifafanua Bw. Kailima.

Utekelezaji wa mpango huo umegawanyika katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza limeanza kutoa elimu hiyo elimu hiyo kwenye mikoa ya Kagera,Mwanza, Kilimanjaro, Morogoro, Mbeya na Dodoma.

Mikoa mingine itakayojumuishwa kwenye kundi hilo ni Ruvuma, Mara, Pwani na Mtwara ambapo elimu hiyo itatolewa kuanzia tarehe 8 Mei hadi tarehe 20 Mei mwaka 2017.

Kundi la pili linatarajiwa kutoa elimu hiyo kuanzia tarehe 24 Mei hadi tarehe 7 Juni mwaka huu katika mikoa ya Geita, Tanga, Singida, Shinyanga, Lindi, Arusha, Tabora, Kigoma, Iringa, Manyara, Rukwa, Katavi, Songwe, Njombe na Simiyu.

Bw. Kailima alisema kuwa utoaji wa elimu hiyo utajikita kwenye mada kuu ya Elimu ya Mpiga Kura iliyogawanywa kwenye vipindi vitano, itakaytoolewa kwenye redio hizo kulingana mada husika na wananchi kuuliza maswali na kujibiwa na wawasilishaji wa mada hizo kutoka Tume.

“Ni mada ambayo imejumuisha masuala yote muhumu yatakayofanya mpiga kura yeyote au mdau yeyote wa uchaguzi kuisoma au kuisikiliza na akaelewa mfumo mzima wa masuala ya kupiga kura” alisema.

Mbali na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio za kijamii katika halmashauri nchi nzima, Tume pia inatoa elimu hiyo kwa njia ya magazeti na vyombo vingine vya habari na mitandao ya kijamii, kushiriki kwenye mikutano na maonesho mbalimbali nchini.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhani akitoa elimu ya mpiga kura kupitia redio A FM ya mkoani Dodoma leo Mei 9 mwaka huu huku akifuatiliwa kwa makini na watangazaji wa redio hiyo.

TAARIFA KUHUSU UTEUZI WA WAGOMBEA WA EALA-NAFASI 2 ZA CHADEMA

0
0

“SERIKALI YATENGA BILIONI 30 KAMA FIDIA KWA WAKAZI WA KIPUNGUNI”-MHE.NGONYANI

0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano imetenga Shilingi bilioni thelathini(30) katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kukamilisha malipo ya fidia kwa wananchi wa Kipunguni wanaopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege.
 
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Edwin Ngonyani Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Segerea Mhe.Bonnah Kaluwa.

“Ni kweli Serikali ilifanya uthamini wa mali za wananchi ili kupisha upanuzi wa kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Dar es Salaam mwishoni wa miaka ya 90 ambapo maeneo yaliyoainishwa kwa ajili ya upanuzi huo ni Kipawa,Kigilagila na Kipunguni”,Alisema Mhe.Ngonyani

Ameongeza kuwa kutokana na gharama za fidia na uhaba wa fedha,Serikali imekuwa ikilipa fidia kwa wakazi hao kwa awamu.Ambapo Mwaka 2009/10 wakazi wapatao 1500 wa eneo la Kipawa walilipwa fidia zinazofikia shilingi bilioni 18 ambapo zoezi hilo lilikamilika Januari 2010.

Katika mwaka wa Fedha 2010/2011 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 12 za fidia kwa wakazi 864 wa Kigilagila na Malipo yalikamilika Januari 2011.Katika mwaka 2013/14 Serikali ililipa Shilingi Bilioni 1.2 ikiwa ni fidia kwa wakazi 59 kati ya wakazi 801 kwa eneo la Kipunguni.

Aidha katika malipo hayo ni wakazi 742 wa Kipunguni ndio ambao hawajalipwa fidia zao zenye thamani ya takribani 19.“Mwaka wa Fedha 2016/17 Serikali imetenga Shilingi Bilioni tano kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi hao wa Kipunguni”Alisisitiza Mhe.Ngonyani.

Upelelezi kesi ya Masogange wakamilika.

0
0
Na Karama Kenyunko,blogu ya jamii.

Baada ya mahakama kutoa hati ya kukamatwa Video Queen Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) kwa kushindwa kutoka mahakamani mara kadhaa, hatimae leo amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Mapema mwezi uliopita, mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa amri ya kukamatwq kwa mshtakiwa Masogange kwa kushindwa kuhudhuria mahakamani mara mbili katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili.

Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange ilikuja baada ya upande wa mashitaka katika shauri lililopita, kuomba mahakama hiyo kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshitakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata mshtakiwa ambaye ni Masogange.

Hata hivyo, Masogange amefika mahakamani hapo leo mapema na alipoulizwa na Hakimu Mashauri sababu za kumfanya yeye kutofika mahakamani, amedai kuwa alifika lakini alichelewa.

Wakilli wa serikali Shadrack Kimaro, ameieleza mahakama kuwa upelelezi katika kesi hiyo umekamilika na ameiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kumsomea mshitakiwa maelezo ya awali(PH).

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu kwa ajili ya PH.
Awali ilidaiwa kuwa,Masogange anakabiliwa na tuhuma za kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Awali ilidaiwa kuwa, kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu, maeneo yasiyofahamika jijini Dar es Salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya heroin (diacety/morpline) kinyume na sheria.
Aidha anadaiwa, kutumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam

WAKAZI WA MKOA WA KAGERA WAJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA AFYA ZAO BURE

0
0


Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Muleba akipima afya katika uzinduzi wa zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza linaloratibuwa na mfuko wa bima ya afya NHIF Kagera.
Mgeni rasmi katika uzinduzi wa zoezi la upimaji afya bure wa magonjwa yasiyoambukiza Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyango akiongea na wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo(hawapo pichani).
Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiongea jambo wakati wa zoezi la ufunguzi wa upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukiza kwa wakazi wa manispaa ya bukoba.



Baadhi ya wakazi wa manispaa ya bukoba waliojitokeza kupima afya zao wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani)katika uzinduzi wa zoezi hilo
Meneja wa bima ya afya wa Mkoa wa Kagera akiwa sambamba na mgeni rasmi wakicheza ngoma ya asili ya kihaya pamoja na kikundi cha upendo katika uzinduzi wa upimaji afya bure kwa magonjwa yasiyoambukuza
Wananchi wa Manispaa ya bukoba wakiende kupima afya zao katika viwanja vya soko kuu la Bukoba



Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera.

WAKAZI wa Mkoa wa Kagera wamejitokeza kwa wingi katika viwanja vya soko kuu la Manispaa ya Bukoba kwenye zoezi la upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza bure.

Zoezi hilo linakoratibiwa na ofisi za mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na ofisi za makao makuu ya mfuko huo linatafanyika kwa muda wa wiki nzima.

Meneja wa mfuko wa Bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo la upimaji afya litahusisha magonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu(BP),Sukari,macho,uzito na urefu pia watakaokutwa na matatizo watapewa ushauri wa kitaalam.

Odhiambo alisema kuwa zoezi hilo ni sehemu ya majukumu ya mfuko wa NHIF ya kuhudumia wananchi lakini wanaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo wa matibabu ili wawe na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

Alisema lengo lao ni kuwafikia wananchi zaidi ya elf moja katika maeneo ya Manispaa ya bukoba hivyo aliwataka wananchi wa Bukoba kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la kupima afya zao.

Mgeni rasmi katika ufunguzi wa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya ya Muleba Injinia Richard Ruyangu aliwataka wananchi wote kujiunga na mfuko wa bima ya afya ili kuwa na uhakika wa matibabu pale wanapougua wao na familia zao.

"Kama mnavyojua ugonjwa huwa unakuja bila ya taarifa'nina waomba wananchi tujiunge na mfuko huu pale tutakapougua tutakuwa na uhakika wa matibabu hata kama hatuna pesa mfukoni"alisema Mkuu wa Wilaya

Alisema mpango huu wa matibabu kwa kutumia bima ya afya ni mkombozi kwa jamii zote kwani gharama zake ni nafuu na nirahisi kupatikana

Pia aliwataka wananchi wajenge tabia ya kufanya mazoezi mbalimbali ya viungo kwasababu magonjwa mengi yasiyoambukiza yanatokana na kutokufanya mazoezi pia wazingatie ulaji wa vyakula vya lishe ili kuepuka maradhi yasiyo ambukiza

TAARIFA YA TAHADHARI YA MVUA KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

0
0

WANAWAKE WA MSIKITI WA KHOJA SHIA ITHNA ASHERI WATOA MISAADA HOSPITALI YA BUTIMBA

0
0

NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

WANAWAKE wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri jijini Mwanza wametoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 2 kwa Hospitali ya Butimba ya Wilaya ya Nyamagana ili kusaidia kupunguza changamoto zinazoikabili.

Mwenyekiti wa kina mama hao Radhida Ahmed akimkabidhi msaada huo Kaimu Mganga Mkuu wa Jiji la Mwanza, Dk. Kajiru Mhando alisema utasaidia kupunguza kero kwa wagonjwa na kuzitaka taasisi zingine zijitokeze kutatua changamoto za hospitali hiyo hasa ujenzi wa wodi ya wazazi.

Alisema msaada huo umelenga kuonyesha mshikamano wao kwenye jamii katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa mjukuu wa Mtume, Imam Mahdi (A.T.F.S) ambayo hudhimishwa Mei 7, kila mwaka.

“ Tuliguswa na changamoto zinazoikabili hospitali yetu hii ya wilaya lakini pia kuonyesha mshikamano wetu na jamii tukaona tuje kutoa msaada huu kwa ajili ya kuwapunguzia wagonjwa kero na changamoto,Wapo wenye utajiri waone na kuguswa na matatizo ya wenzao na kuwasaidia hasa wagonjwa” alisema Rashida.

Aliutaja msaada huo walioukabidhi kuwa ni magodoro 10, mashuka pea 25 na foronya zake, mablanketi 50 na vyandarua 50, vifaa vya usafi (mifagio 10, brashi 10 na Squizers 10) pamoja na sabuni ya maji (Detol) lita 10 na ya unga kg 15.

Vingine ni vifaa tiba ambavyo ni mashine mbili za kupima mapigo ya moyo,Stethescope mbili na, Heavy duty Gloves(pea 5),Sterile Gloves (boksi 4) makasha ya kuhifadhia uchafu makubwa na madogo (12) na zawadi kwa watoto.

Awali Mwenyekiti mstaafu wa Msikiti huo Alhaji Sibtain Meghjee alisema jamii ya Waasia na Waislamu shughuli wanazozifanya kwenye jamii hazipewi fursa ya kutangazwa kwenye vyombo vya habari.

“Kwetu sisi Waislamu, hasa Asian Community ( jamii ya Waasia) shughuli nyingi za kijamii tunazofanya hazipewi nafasi kwenye vyombo vingi vya habari.Vyombo vingi viko mstari wa mbele kutangaza zaidi migogoro kuliko misaada inayolenga kusaidia jamii, kujenga umoja na mshikamano kwenye jamii,” alisema Meghjee.

Akipokea msaada huo Dk. Mhando aliwapongeza akina mama hao kwa moyo wao wa huruma na kujitoa kuisaidia hospitali hiyo na kwamba utawasaidia kupunguza changamoto lukuki zilizopo .“Ingawa bado tuna changamoto ya ukosefu wa wodi ya wanaume lakini vifaa hivi vimetusaidia sana na vitaanza kutumika leo hii hasa katika wodi ya wazazi ya akina mama wanaojifungua ambao wengi ndio waathirika,”alisema.

Dk. Mhando alieleza kuwa hospitali hiyo inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa madawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na miundombinu ya majengo pia haina kitanda cha kutolea damu, mashine ya kupima mapigo ya moyo ya mtoto akiwa tumboni ili kutambua kama yu hai ama la.

“Wodi zilizopo kwenye hospitali yetu ya wilaya hazitoshi na hatuna wodi ya wanaume na wanaokuja kutibiwa hapa na kutakiwa kulazwa, tunalazimika kuwapa rufaa ya kwenda Hospotali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure,”alisema Dk. Mhando.
Msaada iliyotolewa katika hospiali ya Butimba jijini Mwanza kutoka kwa wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza.
Wanawake wa Dini ya Kiislamu wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza wakabidhi Blanketi
Dk Kajiru akipokea moja ya godoro kati ya 10 yalitolewa msaada wa akinamama wa Msikiti wa Khoja Shia Ithna Asheri Mwanza
Mwenyekiti wa Wanawake wa msikiti wa Khoja Shia Ithan Ashaeri Rashida Ahmed pamoja na Mrs karimu wakimfurahia mtoto Hajida walipotelea wodi ya wazazi kwenye hospitali ya Butimba.

Dk.Shein atembelea Kampuni ya Simu ya Telecom nchini Djbouti

0
0








Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiuliza suala wakati alipotembelea kampuni ya Simu ya Telecom Nchini Djibouti akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.]
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Mawasiliano na huduma za Mitandao Bw.Abdi Youssoef wakati alipotembelea katika Ofisi ya kampuni Telecom Nchini Djibouti akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.]
Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa ofisa wa kampuni ya Simu ya Telecom Nchini Djibouti wakati alipotembelea katika Ofisi ya kampuni hiyo akiwa katika ziara ya kiserikali kwa mualiko wa Rais wa nchi hiyo Mhe,Ismail Omar Guelleh[Picha na Ikulu.]

NHIF WAISHAURI SERIKALI BIMA YA AFYA KUWA LAZIMA

0
0


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeishauri Serikali kuifanya bima ya afya iwe lazima kwa kila mwananchi na sio hiari kama ilivyo sasa.

Ushauri huo umetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Benard Konga alipokuwa akizungumza katika kipindi cha TUNATEKELEZA kinachorushwa hewani na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

“Ifike wakati suala la bima liwe ni lazima sio hiari na kwamba lengo sio kukusanya fedha nyingi bali kumpunguzia mwananchi gharama za matibabu na kuhakikisha mwananchi huyo anapata huduma bora za afya kwa wakati wote anapohitaji matibabu”alisema Konga.

Konga alieleza kuwa mpango wa baadae wa Mfuko huo ni kuongeza hamasa itakayopelekea wananchi wengi zaidi kujiunga na bima za afya ili kutimiza lengo la kufikia asilimia 75 ya wananchi wote kuwa na bima ya afya ifikapo mwaka 2020 kutoka asilimia 29 iliyopo hivi sasa.

Kaimu Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa mfuko huo hivi sasa unahudumia zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanaoishi vijijini. Kwa upande wa utoaji huduma, Konga alieleza kuwa Mfuko huo umesajili jumla ya vituo 6600 vinavyotoa huduma kwa bima ya afya pamoja na maduka ya madawa 200 yanayotoa dawa kwa kutumia bima ya Mfuko huo.

Hata hivyo, alitoa rai kwa hospitali mbalimbali nchini kuzingatia masharti na vigezo vilivyowekwa katika utoaji wa huduma za bima na kuepuka tabia ya kunyanyasa wanachama wa Mfuko huo.

Aidha, amewataka waajiri kuiga mfano wa Serikali katika suala zima la kupeleka kwa wakati michango ya wanachama.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeanzishwa mnamo mwaka 1999 baada ya Serikali kupitisha Sheria ya kuruhusu Mfuko huo ambapo mwaka 2001 ulianza rasmi kutoa huduma kwa watumishi wa umma. Mwaka huo huo,marekebisho ya sheria yalifanyika kuruhusu Mfuko huo kutoa huduma kwa wananchi walio katika sekta zisizo rasmi.

WATU WATANO WA FAMILIA MOJA WAFARIKI KWA NYUMBA YAO KUANGUKIWA NA MTI

0
0

Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo
 
Na,Vero Ignatus,Arusha

Kutokana na mvua inayonyesha mfululizo Mkoani Arusha imeleta maafa makubwa katika familia ya mzee Jonathani Kalambiya{55} mkazi wa sokoni II katika kijiji cha kinyeresi wilayani Arumeru Mkoani Arusha baada ya mti mkubwa uliong’olewa na maji kuangukia nyumba yake na kuua watoto wake wote watano.

Mkasa huo wa kusikitisha ulitokea jana majira ya saa 7 usiku baada ya mti huo kung’olewa na maji uliangukia nyumba hiyo iliyokuwa jira na mti huo.Kamanda wa polisi Mkoani Arusha,Charles Mkumbo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja watoto waliokufa katika tukio hilo ni pamoja na watoto wawili wanafunzi wa mzee huyo ambaye ni mlinzi wa hospital ya ya Dr Mohamed ya Jijini Arusha.

Mkumbo aliwataka wanafunzi ambao ni watoto wa mzee Kalambwia ambaye siku ya tukio alikuwa kazini ni pamoja na Miliamu Jonathani(16) mwanafunzi wa kidatu cha pili wa shule ya sekondari ya Inaboishu.

Kamanda alimtaja mwanafunzi mwingine ni ambaye ni mtoto wa mzee huyo ni Grolia Jonathani(11) mwanafunzi wa shule ya msingi Kinyeresi iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.Amesema watoto wengine wa mzee huyo ni pamoja na mtoto wa kwanza wa mzee huyo aliyetambuliwa kwa jina la Giliad Jonathani(31),Lazaro Lomnyaki (26) na Best Jonathani(20).

Kamanda Mkumbo alisema kuwa mti huo uliokuwa katika mlima wa Lake mana uliangukia nyumba hiyo baada ya kung’olewa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika Jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla.Alisema na kuitakia pole sana familia yam zee huyo kwani tukio hilo ni majonzi makubwa sana kwake kwani familia nzima imeondoka na kumtaka kuwa na uvumilivu katika wakati huu mgumu kwake.

Kamanda Mkumbo ametoa wito na ushauri kwa wakazi wa Arusha kuchukuwa tahadhari katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa kukarabati nyumba zao na kuacha kujenga chini ya mti ama kwenye vyanzo vya maji.

Amesema kujenga katika vyanzo vya maji ama chini ya mti ni kujitafutia majanga mengine hivyo ni vema kila mkazi wa Mkoa wa Arusha kuchukuwa tahadhali hiyo.Aidha kamanda ametoa tahadhari kutokana na habari za uzushizinazoendele kuwa jana kwenye kuaga miili ya wanafunzi kuna mtu alidondoka juu ya mti na kufariki pamoja na mama mmoja mtoto wake mdogo alifariki,amesema habari hizo siyo za kweli wananchi wazipuuze kabisa
nyumba ikiwa imeangukiwa na mti kama inavyoonekana katika picha
Mti ulioanguka ukang'ookana shina lake na kuangukia nyumba na kusababisha maafa hayo ya watu watano wa familia moja.


Jitihada za uokozi zikiendelea .
Miili ikiwa imeshapakiwa ndani ya gari la polisi

















MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASIMU MAJALIWA BUNGENI DODOMA LEO

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa zamani, Lawrence Masha kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Kiembesamaki, Ibrahim Raza kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Songea Mjini, Leonidas Gama kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017. Katikati ni Mbunge wa zamani, Hezekia Wenje. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika wa Bunge, Job Ndugai kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 9, 2017.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Sengerema, William Ngereja kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 9, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Mhe. Anne Makinda, leo.

JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUENDELEZA MICHEZO NCHINI

0
0

SERIKALI IMETENGA SHILINGI BILIONI 30 KUKAMILISHA MALIPO YA FIDIA KWA WAKAZI WA KIPUNGUNI

0
0

Mshindi wa Milioni 10 atangaza kuuaga umasikini

0
0
Meneja Masoko wa BIko Goodhope Heaven mwenye fulana ya njano akionyesha nyaraka zilizowekwa kiasi cha Sh Milioni 10 kwa ajili ya mshindi wao wa wiki, Emmanuel Philipo aliyeibuka na ushindi wa mamilioni hayo kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Kushoto kwa Heaven ni Philipo akifuatiwa na Afisa wa NMB na kulia ni Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage.

Mshindi wa MIlioni 10 Biko aahidi kuuaga umasikini

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MSHINDI wa Sh Milioni 10 wa droo ya nne ya mchezo wa kubahatisha wa BIko
IJue Nguvu ya BUku, Emmanuel Philipo, ametangaza rasmi nia yake ya kuuaga umsikini baada ya kukabidhiwa fedha zake jumla ya Sh Milioni 10.

Makabidhiano hayo yalifanyika jana jijini Dar es Salaam kwa kuhudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumuelimisha mashindi huyo wa bahati nasibu ya Biko ili azitumie vizuri fedha zake.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Philipo alisema kwamba ni wakatiwake
wa kuuaga umasikini kwa sababu amepata nafasi ya kutimiza ndoto zake kiuchumi kwa kuhakikisha kwamba anakamilisha mradi wake wa garage ya kutengenezea magari katika viunga vya jiji la Dar es Salaam.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage akionyesha namba za kucheza bahati nasibu yao inayofanikisha ushindi wa mamilioni kutoka kwa Watanzania, ambapo droo iliyopita alitangazwa Emmanuel Philipo ambaye jana alipewa kiasi cha Sh Milioni 10.
Mazungumzo yakiendelea baada ya makabidhiano hayo.
Afisa wa NMB akizungumza jambo na mshindi wa Sh Milioni wa Biko, Emmanuel Philipo baada ya kukabidhiwa Sh Milioni 10 zake kutoka Biko.
Afisa wa NMB akimkabidhi nyaraka mshindi wa Sh Milioni 10, Emmanuel Philipo katikati akishuhudiwa na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven.
Alisema fedha alizopata jumla ya Sh Milioni 10 ni nyingi, huku akizipata kwa sababu ya kushiriki bahati nasibu ya Biko, akiamini kuwa ni mpango wa Mungu kumpatia fedha hizo ukizingatia kuwa ni wengi wanaocheza bahati nasibu.

"Namshukuru Mungu kwa kuniletea zawadi hii kwa kuwatumia wachezeshaji wa biko, hivyo ni wakati wangu wa kufanikiwa kimaisha kwa sababu ndio dhamira yangu kuu kupiga hatua kubwa kimaendeleo kwa kuamua kucheza bahati nasibu hii kwa njia yaujumbe wa maandishi kwa kufanya muamala kwenye simu za Tigo, Vodacom na Airtel ambapo namba ya kampuni niliweka 505050 na ile ya kumbukumbu niliingiza 2456 na kutangazwa mshindi mwishoni mwa wiki.

"Nawaomba Watanzania wenzangu tuendelee kuthubutu katika fursa mbalimbali
ikiwamo ya kucheza mchezo wa Biko kwa sababu sio tu zawadi zao mbalimbali
kama vile Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000 na Sh MIlioni Moja za papo
kwa hapo zinaeleweka, bali pia hata unapotangazwa mshindi wa Sh Milioni 10,
huwa wanakabidhi haraka kwa mshindi wao," Alisema.

Naye Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven alimpongeza Philipo kwa
ushindi huo na kumtaka awe balozi mzuri kwa Watanzania wote kwa ajili
ya kuwapa elimu ya kuhakikisha kuwa wanacheza Biko ili nao waibuke na
mamilioni ya Biko.

Naye Meneja wa Huduma kwa Wateja wa Biko, Grace Kaijage, alisema
ushindi kwenye bahati nasibu yao ni mwepesi na kila mchezaji anaweza
kuibuka na fedha kutoka kwenye bahati nasibu yao ya Biko.

"Huu ni muda wa kulala masikini na kumka tajiri, hivyo njia ya ushindi ni
kucheza mara nyingi zaidi ambapo kila tiketi moja inayopatikana kwa sh
1000 inatoa nafasi mbili za ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia
kwenye droo kubwa ya wiki ya kushinda Sh Milioni 10," Alisema.

Philipo ni mshindi wa nne wa Sh Milioni 10 ambapo jana alikabidhiwa fedha
zake kwa ajili ya kuanza matumizi kama walivyokabidhiwa wenzake kutoka
jijini Dar es Salaam na Mwanza.

MAJALIWA AFUNGUA MAFUNZO KWA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA SERIKALI ZA MITAA

0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma leo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa  Mafunzo ya Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa baada ya kufungua mafunzo hayo katika  ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya  Rais, Selemani Jafo na kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. Aliyekaa kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiagana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja baada ya kufungua Mafunzo kwa Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Serikali za Mitaa  katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana  na  Mkuu wa Wilaya  ya  Dodoma Mjini, Christina Mndeme baada ya kufungua Mafunzo ya  Wakuu wa Wilaya  na Wakurugenzi wa Halmashauri za Seriklali za Mitaa katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma Mei 9, 2017. Wapili kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Selemani Jafo na kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


SHINYANGA APONGEZA WANANCHI KUJENGA KITUO CHA POLISI ISELAMAGAZI

0
0
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (pichani) amepongeza wananchi wa tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga kwa kujenga kituo cha Polisi kata ya Iselamagazi ili kukabiliana na uharifu ambao umekithiri eneo hilo ukiwamo wa kuvamia watumishi wa serikali hasa walimu kisha kuwapora mali na kuwajeruhi kuwa katakata mapanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akikagua jengo la kituo cha Polisi kata ya Iselamagazi ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na mbunge wao wa Solwa Ahmed Salimu

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro  akitoa maelekezo kwa  watendaji wa kata,vijiji,vitongoji,viongozi wa Sungusungu na Madiwani wa halmashauri hiyo ya wilaya ya Shinyanga juu ya kutumia jengo hilo kikamilifu kutoa taarifa ya waharifu na kuchukuliwa hatua kali za kisheria
Ukaguzi wa jengo ukiendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishukuru wananchi kuhusu  ujenzi wa jengo hilo ambalo limejengwa kwa haraka ambapo ujenzi ulianza  Januari 12,2017 na limegharimu shilingi milioni 13.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro baada ya kumaliza kukagua jengo hilo la kituo cha polisi. Matiro aliwaahidi kuwaezekea paa ili lianze kufanya kazi haraka na kumaliza matukio ya uharifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo na kudumisha amani kwa wananchi wote wakiwemo watumishi wa serikali.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akiteta jambo na viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya madiwani wa halmashauri kabla ya kuingia kwenye mkutano wa viongozi wa Sungusungu na watendaji wa vijiji,kata na vitongoji kujadili ajenda mbili za ulinzi na usalama pamoja na kuunda ushirika wa vyama vya kuuza mazao ili kuinua wakulima kiuchumi sambamba na kuhifadhi chakula cha akiba ili kukabiliana na janga la njaa hapo baadae.
Mkuu wa wilaya Josephine Matiro akizungumza na viongozi wa Sungusungu,baadhi ya watendaji wa kata ,vijiji,vitongoji na Madiwani wa halmashauri hiyo juu ya kudhibiti uhalifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo pamoja na kuwafichua wahalifu ambao huhatarisha hali ya amani. 
Wajumbe wakisikiliza maagizo ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuhusu namna ya kudumisha amani na kutunza chakula cha akiba na kutokubali kulanguliwa mazao yao mashambani na wafanyabiashara na kuwafanya kuendelea kuwa maskini. 
Ofisa Tarafa ya Nindo Budugu Kasuka akitoa taarifa ya masikitiko kwa mkuu wa wilaya juu ya baadhi ya wananchi ambapo wamekuwa wakivamia watumishi wa serikali hasa walimu kwa kupora mali zao na kisha kuwa kata kata mapanga hali ambayo iliyowagusa wananchi wengi na kuamua kuchangisha pesa ili kujenga kituo cha polisi ambacho kitasaidia kudhibiti waharifu kwenye tarafa hiyo na kubainisha kuwa kituo hicho kitakuwa kimekamilika mwezi Juni 30 mwaka huu. 
Kikao kikiendelea huku wajumbe hao wakilitupia lawana jeshi la polisi kuwa pale wanapopelekewa waharifu hususani wale wanaotuhumiwa kukata mapanga walimu ambapo wao wamekuwa wakiwapatia dhamana na kisha kurudi mitaani kuanza kuwatambia na pia kuendeleza uharifu kama kawaida na hivyo kukata tamaa na kuogopa kutoa tena taarifa polisi licha ya kuwajua watu wote wanaofanya vitendo hivyo. 
Hapa wajumbe wakisikiliza majibu kutoka kwa kaimu kamanda wa jeshi la polisi wilaya Shadrack Zambi ambaye hayupo pichani kwa kufafaunua kuwa kila mtu ana haki ya kupewa dhamana, huku akibainisha watuhumiwa wote waliowakamata na kuwapeleka kwao kesi zao zinaendelea kusikilizwa mahakamani na endapo wakibainika kukutwa na makosa hayo watachukuliwa hatua za kisheria na pia kuwasisitiza wasichoke kutoa taarifa za waharifu ,huku akiwapongeza kwa ujenzi wa kituo hicho cha polisi ambacho kitasaidia kuongeza idadi ya askari wengi na hatimaye kufanikiwa kukomesha uharifu kwenye tarafa hiyo ya Nindo
Picha zote na Marco Maduhu Malunde1 blog

TEMBO WANNE WAONEKANA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) LEO, ASKARI WA WANYAMAPORI WAANZA KAZI KUWARUDISHA HIFADHINI

0
0
Tembo wakiwa wamejificha kwenye vichaka ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) leo. Kwa mujibu wa taarifa za Wahifadhi wa Wanyamapori inaelezwa kuwa sehemu ya eneo hilo litakuwa ni njia ya tembo (maeneo ya mapito ya wanyamapori) ambayo ilipitika kwa miaka mingi iliyopita na kwamba tembo wana kumbukumbu hata kama walipita njia hiyo kwa zaidi ya miaka 50 iliyopita. Imeelezwa kuwa njia hiyo ya mapito ya wanyamapori itakua ilitumiwa na wanyamapori kuhama eneo moja hadi jengine ikiwemo maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Mikumi, Ruaha, Serengeti, Pori Tengefu la Rugwa na maeneo mengine ya hifadhi na kwamba maeneo hayo mengi kwa miaka ya hivi karibuni yameshaingiliwa na shughuli za kibinadamu ambazo hazisababishi tembo hao kusahau njia hizo au kutokuzitumia tena.
Tembo hao wakiwa ndani ya eneo chuo kikuu hicho cha Dodoma leo. Hakuna madhara yeyote yaliyoripotiwa kusababishwa na tembo hao na taratibu za kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi zimeshaanza kuchukuliwa na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo Askari wa Wanyamapori wameanza zoezi la kuwafukuza kuwarudisha kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma akitoa somo kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma namna ya kuchukua tahadhari juu ya ugeni wa tembo hao chuoni hapo. Aliwaeleza wanafunzi hao kuwa mazingira ya chuoni hapo yataendelea kuwa salama kwakuwa tembo hao wapo katika njia yao ya mapito na pengine kumewahi kukucha kabla ya wao kufika mwisho wa safari yao, hivyo kwa msaada wa askari wa wanyamapori ambao wamewasili chuoni hapo itasaidia  kuwaondoa tembo hao waweze kuendelea na safari yao hadi kwenye maeneo ya hifadhi.
Wanafunzi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dodoma walikusanyika wakiwa na shauku ya kuwaona tembo hao.
Msafara wa viongozi mbali mbali wa Serikali ukiambatana na Askari Polisi na Askari wa Wanyamapori ukisogelea eneo walilokuwepo tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza kutoka katika maeneo hayo ya chuo kwenda kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Prof. Julius Nyahongo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (wa pili kulia), Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, Paschal Shelutete (wa tatu kulia) na maafisa wengine wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wakiangalia eneo walilokuwa wamejificha tembo hao chuoni hapo.
Askari wa wanyamapori wakiingia ndani ya eneo walilokuwa wamejificha tembo hao kwa ajili ya kuanza kuwafukuza eneo hilo kuelekea kwenye maeneo yao ya hifadhi. Imeelezwa kuwa pindi tembo hao watakapofukuzwa kwa milio maalum ya risasi hutafuta njia wanazozijua wenyewe za kurudi kwenye maeneo yao ya hifadhi.
Tembo hao wakianza kuondoka katika eneo hilo baada ya askari wa wanyamapori kuanza kuwaondoa eneo hilo kwa kutumia milio maalum ya risasi. (PICHA NA HAMZA TEMBA-WIZARA YA MALIASILI NA UTALII)

Eckobank Tanzania leo yawahakikishia wateja wake kuendelea na shughuli zake nchini Tanzania

0
0

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict amefanya mkutano na waandishi wa habari leo katika ofisi za makao makuu ya benki hiyo, na kueleza kwamba hawana dhamira ya kusitisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo makubwa waliyojiwekea ya kuleta maendeleo ya kiuchumi Tanzania.

“Hii ilikuwa ni ahadi yetu tangu tulipoanza kufanya shughuli zetu hapa nchini miaka saba iliyopita na itaendelea kuwa ahadi yetu mpaka hivi sasa,” alisema Benedict.

Licha ya kukiri kwamba kumekuwapo na ongezeko la wateja kushindwa kurejesha mikopo yao mwaka jana, alisema benki hiyo imejiwekea utaratibu mzuri na hatua sahihi za jinsi ya kukabiliana na hali hiyo.

Alisema, “Tumechukua hatua muhimu ili kuwezesha urejeshaji wa mikopo mbalimbali ndani ya miezi mitatu iliyopita na tunaamini kwamba mfumo tuliouanzisha utatuletea mafanikio makubwa ndani ya miezi michache ijayo.”

Aliongeza kuwa, nguvu ya msingi ya benki hiyo ina ungwa mkono na wanahisa wakubwa ambao wanaifanya benki kuwa imara, madhubiti na kuaminika na hivyo kuwa moja ya chombo cha fedha kinachoweza kuendana na hali yoyote ya dhoruba.

Washirika wakubwa wa Ecobank ni pamoja na Nedbank ya Afrika Kusini( asilimia 21), Qatar Nation Bank (asilimia 20), Public Investiment Corporation ya Afrika Kusini ( asilimia 14) na International Finance Corporation iliyopo chini ya Benki ya Dunia (asilimia 14).

Benedict aliongeza kwamba Ecobank ina shauku kubwa ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania na kuendeleza uchumi kupitia huduma zake. Hata hivyo, mwaka 2016 ilishuhudia ongezeko la kutokulipwa kwa mikopo, jambo ambalo liliisukuma benki hiyo kubadilisha mbinu na kuja na mikakati mipya ya kukabiliana na hali hiyo.

Alielezea kwamba Ecobank Tanzania haina lengo la kufunga huduma zake na badala yake imeanza kufanya mabadiliko katika shughuli zake ili kuweza kukabiliana na hali ya sasa.

Pia aliongeza kwamba ili kuendelea kuwahudumia wateja wake kwa ufanisi zaidi, benki hiyo imewekeza zaidi kwenye huduma zake za kimtandao na malipo ili kuweza kuwahudumia wateja wake kwa urahisi zaidi na taifa kwa ujumla.

“Hivi karibuni tulizindua app ya Ecobank Mobile Banking ambapo wateja watapata huduma ya Xpress Akaunti.

Huduma ya Xpress Akaunti inawawezesha wateja kufungua na kutumia akaunti zao bila ya kufika kwenye matawi yetu, huku wakiokoa muda, pesa na kuongeza ufanisi na usalama, hii yote ikiwa ni mikakati ya Ecobank kwa Afrika.

Malengo mazuri ya Ecobank ya baadaye ni kuwa taasisi imara iliyojikita kwenye msingi mzuri.

Kwa mara nyingine ninapenda kuwahakikishia tena wateja wetu na wadau kwamba tutaendelea kuwepo hapa.
 


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuwahakikishia wateja wa benki hiyo na umma wa ujumla kuhusu dhamira ya benki hiyo ya kuendelea kutoa huduma zake hapa nchini. Kushoto Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja wa benki hiyo, Ndabu Lilian Swere.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zao nchini kutokana na ahadi na malengo yao. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati.
Mkuu wa kitengo cha wateja wakubwa wa EcoBank Tanzania Raphael Onyango akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake hapa nchini kutokana na ahadi na mikakati madhubuti waliyojiwekea. Wa pili kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha Wateja wa rejareja, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati (kulia).
Mkuu wa kitengo cha biashara wa Ecobank Tanzania, Respige Kimati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na malengo yake. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzani Raphael Benedict na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za biashara za ndani Ndabu Lilian Swere.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa EcoBank Tanzania, Raphael Benedict, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya dhamira ya benki hiyo ya kutositisha shughuli zake nchini kutokana na ahadi na mikakati waliyojiwekea. Kulia ni Mkuu wa kitengo cha biashara wa benki hiyo Respige Kimati na kushoto ni Ndabu Lilian Swere, Mkuu wa kitengo cha wateja wa rejareja.

MAWAZIRI BAINA YA TANZANIA ZANZIBAR NA DJIBOUTI WAKUTANA KWA MAZUNGUMZO

0
0



Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Djibouti (hawapo pichani) walipokutana katika kujadili mambo mbali mbali  masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baina pande mbili hizo ikiwemo Tanzaniz na Djbouti katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) [Picha na Ikulu.]
MKAS2
Waziri wa Ujenzi,Usafirishaji na Mawasiliano mhe,Balozi Ali Abeid Karume (kushoto) na Waziri wa Afya mhe mahmoud Thabit Kombo walipokuwakatika kikao cha pamoja na Mawaziri wa Serikali ya Djiboutiambapo walizungumzia zaidi ushirikiano katika nyanja za kiuchumi walipokuwa katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani)[Picha na Ikulu.]
MKAS3
Mawaziri wa Serikali ya Djibouti wakizungumza na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  (hawapo pichani) walipokutana katika kujadili mambo mbali mbali  masuala ya ushirikiano wa kiuchumi baina pande mbili hizo ikiwemo Tanzaniz na Djbouti katika ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani)[Picha na Ikulu.]

SERIKALI KUBORESHA KIWANGO CHA VYOO BORA KUFIKIA 2025.

0
0

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa kwanza kulia akifungua pazia kuashiria uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”uliofanyika mjini leo mjini Dodoma.


Waziri wa Afya, maendeleo yaJamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati akiwa amebeba nembo inayoashiria uzinduzi wa kampeni ya kutunza mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini Dodoma , wengine ni wadau mbalimbali wa mazingira pamoja na baadhi ya wabunge. 
Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza mbele ya wabunge na wadau mbalimbali wa afya na mazingira hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI”iliyofanyika leo mjini Dodoma. 

Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akiteta jambo na Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya yautunzajiwa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” uliofanyika mjini leo mjini Dodoma. Pichana Ally Daud-WAMJW DODOMA.
 

Na Ally Daud-WAMJW DODOMA

SERIKALIi imedhamiria kuboresha kiwango cha vyoo bora mjini na vijijini kutoka asilimia 35 hadi asilimia 55 kufikia mwaka 2025 ili kujenga taifa lenye afya bora na lisilo na maambukizi ya magonjwa yatokanayo na uchafu wa vyoo.

Akizungumza hayo kwenye uzinduzi wa kampeni ya utunzaji wa mazingira ijulikanayo kama “NIPO TAYARI” Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali imepania kufikisha asilimia ya ubora wa vyoo mpaka kufikia 2030.

“Hatua hii itafikiwa endapo kwa pamoja tutasukuma mbele ajenda ya usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hasa katika ujenzi wa vyoo bora,utupaji salama wa taka ngumu,upatikanaji wa maji salama kwa mikono miwili” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa yapo mafanikio yaliyofikiwa katika kupunguza kasi ya watu kujisaidia ovyo tabia ambayo ni kisababishi cha maambukizi ya magonjwa mengi katika jamii.

Mbali na hayo Waziri Ummy alitoa rai kwa wanasiasa wenginekushirikiana na wananchi katika majimbo yao ilikusukuma kwa vitendo ajenda ya Usafi wa Mazingira nchini .

Kwa upande wake Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bw. Suleiman Jaffo amesema kuwa watanzania wa wa mijini na vijijini wawe mstari wa mbele katika kuhakikisha wanatumia vyoo bora kila kaya ili kuepuka magonjwa ya kuambukiza.

Naye Naibu Waziri wa maji na umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa ili kuendana na kasi hiyo wamejipanga kuhakikisha shule zote za msingi na sekondari nchini zinapata maji safi na salama kwa wakati sahihi.
 
Viewing all 46205 articles
Browse latest View live




Latest Images