Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live

RAIS WA ZANZIBAR AREJEA NCHINI AKITOKEA DJIBOUTI.

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Moahammed Mahmoud mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Wakuu wa Vikosi vya SMZ mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein katikati akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein wa kwanza kulia akizungumza na Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kuwasili Zanzibar akitokea Djibouti kwa Ziara ya Siku Tatu.

PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

MATUKIO MBALIMBALI YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA LEO BUNGENI MJINI DODOMA

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na wabunge Mussa Ntimizi wa Igalula na Felista Bura wa Viti Maalum, bugeni mjini Dodoma Mei 10, 2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijadili jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, George Simbachawene kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma, Mei 10, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wabunge, Kange Lugora wa Mwibara (kushoto)  na Katani Ahmed Katani wa Tandahimba (katikati) kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10,2017.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA (Zanzibar) Salum Mwalimu kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma (katikati) na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Mwanne Mchemba (kushoto) na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Mtwara Vijijini Hawa Ghasia kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma Mei 10, 2017. 

MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR, BALOZI SEIF AWASILISHA HOTUBA YA MAKADIRIO NA MATUMIZI YA OFISI YAKE KATIKA KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kilichoanza leo katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Baadhi ya Manaibu Mawaziri wa SMZ na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Timu ya Uongozi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ukiongozwa na Katibu Mkuu wake Nd. Joseph Abdulla Meza wa Nne kutoka kulia wakiandika dondoo wakati wa Hotuba ya Ofisi yao ikiwasilishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Mh. Simai Mohamed Said wa kwanza kutoka Kulia na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Mheshimiwa Suleiman Sarahan Said wakiwa makini kufuatilia Hotuba ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyowasilishwa Barazani. 
Picha na – OMPR – ZNZ.



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejipanga kuimarisha zaidi huduma za Kijamii zikiwemo Elimu, Afya, Makaazi na upatikanaji wa Maji safi na salama katika azma yake ya kutoa kipaumbele kwenye mpango wake wa maendeleo katika kipindi cha mwaka 2017/2018.


Mpango huo utakwenda sambamba na uimarishaji wa Miundombinu ya uingiaji Nchini inayojumuisha Bandari, Viwanja vya Ndege , bara bara za ndani , Nishati pamoja na Tafiti zitakazosaidia kutoa maamuzi katika mipango hiyo ya Maendeleo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alieleza hayo wakati akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar katika Kikao cha Bajeti cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kilichoanza leo katika Majengo ya Baraza hilo yaliopo Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Balozi Seif alisema Serikali itaendelea kuweka mkazo katika kugharamia uendeshaji wake na kutoa huduma bora kwa Wananchi kwa kutumia rasilmali zilizopo kwa umakini mkubwa na kuhakikisha matumizi yote yanaleta tija kwa Umma.

Alisema utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya 2020 ikiwa katika kipindi cha mwisho cha miaka mitano unaenda sambamba na uidhinishwaji wa awamu ya Tatu ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini { MKUZA 111}.




Balozi Seif alieleza kwamba hiyo inamaanisha wazi kwamba Malengo ya Taifa bado yanadhamiria utekelezaji wa Mipango hiyo Mikuu ambayo imekusudia kukuza Uchumi, kuimarisha huduma za Jamii pamoja na kuimarisha Demokrasia na Utawala Bora.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema kwamba hali ya ukuaji wa uchumi wa Nchi imepelekea kuongezeka kwa Pato la Taifa kwa mwaka 2016 ambalo limeongezeka na kufikia thamani ya Shilingi 2,309.5 Bilioni ikilinganishwa na thamani ya shilingi 1,633.0 Bilioni Mwaka 2015.

Alisema uchumi wa Zanzibar umeimarika kwa asilimia 6.8 mwaka 2016 kutoka asilimia 6.5 mwaka 2015 hali iliyo tofauti na taswira inayojionyesha kwa mwenendo wa ukuaji wa Uchumi kwa Nchi za Kusini mwa Jangwa na Sahara ambapo kasi ya ukuaji wa uchumi imeshuka na kufikia wastani wa asilimia 1.6 mwaka 2016 kutoka wastani wa asilimia 3.4 mwaka 2015.

Akigusia mvua za masika zinazoendelea kunyesha hapa Nchini na kuleta athari kubwa kwa Wananchi walio wengi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwatahadharisha Wananchi kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo miripuko ya maradhi yanayosababishwa na uchafuzi wa maji.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar bado inawasisitiza Wananchi kuepuka kujenga katika maeneo hatarishi ambayo mazingira yake yanaweza kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa hasa wakati wa mvua kubwa zinazonyesha kama mabondeni, kwenye njia za asili za maji na pembezoni mwa milima hasa Kisiwani Pemba.

Balozi Seif alitoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya juu ya usafi wa mazingira ikiwemo kunawa mikono mara watokapo kujisaidia na kabla ya kula.

Kwa upande wa wafanyabiashara Balozi Seif aliwakumbusha kuendelea kufuata masharti yaliyowekwa juu ya biashara zao kwa kuzingatia suala la usafi na ulinzi wa afya za Wananchi ili kujikinga na maradhi ya mripuko.

Akigusia janga a dawa za kulevya linaloendelea kuiathiri jamii Nchini Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali yaMapinduzi ya Zanzibar kupitia Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Udhibiti wa Dawa za Kulevya imetoa mafunzo kwa wadau katika shehia zenye Banadari Rasmi na zisizo Rasmi.

Alisema hatua hiyo ililenga kuweka wazi mbinu mbali mbali zinazotumiwa na wahalifu katika kupitishia dawa za kulevya ambapo washiriki wa mafunzo hayo wapatao 186 walitoa kwenye Shehia zipatazo 94 zenye Bandari hizo.

Balozi Seif alisema Kamati ya Kitaalamu ya Tume hiyo iliweza kupanga mikakati ya udhibiti wa dawa za kulevya, uimarishaji wa kinga dhidi ya matumizi ya dawa hizo pamoja na kuzisaidia Nyumba za upataji nafuu kwa vijana walioathirika na dawa za kulevya.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alizipongeza Nchi Rafiki, Taasisi, Makampuni na washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi waliojitolea kuunga mkono harakati za Maendeleo ya Wananchi wa Zanzibar na kupiga hatua kubwa Kiuchumi na ustawi wa Jamii.

Balozi Seif alisema michango ya washirika na Mataifa hayo marafiki imewezesha kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoa huduma bora za Kijamii na kuleta maendeleo katika Taifa zima.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliliomba Baraza la Wawakilishi liidhinishe jumla ya shilingi Bilioni 44,837,577,000/- kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na Taasisi zake kwa ajili ya kutekeleza Programu zake kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

10/5/2017.

WAZIRI PROFESA MBARAWA KUMWAKILISHA RAIS DKT. MAGUFULI KIGALI, RWANDA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameondoka nchini leo kwenda Kigali Rwanda, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye mkutano wa siku mbili wa “Transform Africa Summit 2017”.

Mkutano huo utawakutanisha viongozi na wataalam mbalimbali Barani Afrika kwa lengo la kujadili masuala kadhaa ikiwemo maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT), hususan katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Katika mkutano huo, Profesa Mbarawa ataeleza kwa kina changamoto na mafanikio yaliyofikiwa na Tanzania katika uwekezaji wa Miundombinu ya Habari na Mawasiliano, Maendeleo ya Sera na Miongozo inayotumika hapa nchini katika kusimamia sekta hiyo kwa lengo la kukuza uchumi wa nchi na kuiunganisha Tanzania na Mataifa mengine.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

10 Mei, 2017

VIJUSO MAGAZETI YA LEO ALHAMIS MAY 11,2017

UMOJA WA WATANZANIA SWEDEN (TANRIKS) WATOA SALAM ZA RAMBIRAMBI

$
0
0


Sisi watanzania tunaoishi Sweden kwa majonzi na masikitiko makubwa tunatoa pole zetu kuwafikia familia zilizoguswa na msiba, shule ya Lucky Vicent Arusha na Taifa kwa ujumla kwa kupoteza watoto, dereva, na waalimu.  

Habari hizi zimetugusa sana na kuleta simanzi na masikitiko makubwa katika jamii ya Watanzania hapa Sweden. Tunapendelea pia kuipongeza serikali yetu kwa jitihada zake za kukabiliana na janga hilo bila kupoteza wakati na pia kuwafariji wafiwa katika wakati huu mgumu. 
TUNATANGULIZA UPENDO NA MSHIKAMANO KWA TAIFA LETU

KWA NIABA YA WATANZANIA SWEDEN
MWENYEKITI
NORMAN JASSON

Tanzania na Afrika kusini kuongeza maeneo ya ushirikiano ili kunyanyua uchumi

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akitoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Kamisheni ya Pamoja ya Kitaifa kati ya Tanzania na Afrika Kusini, uliofanyika mapema leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake Mhe. Mahiga alieleza mkakati wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini katika kuongeza maeneo ya ushirikiano hususan katika biashara na uwekezaji. 
Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Mhe. Maite Nkoana - Mashabane akihutubia katika mkutano huo ambao ulitanguliwa na mkutano wa siku mbili wa Makatibu wakuu. Pamoja na Mambo mengine, Mhe. Mashabane alieleza umuhimu wa kukuza uhusiano wa kihistoria uliopo baina ya mataifa hayo mawili ili kuwaletea maendeleo wananchi wa mataifa yote. Pia alitumia fursa hiyo kutoa salamu za rambirambi kwa taifa la Tanzania kwa kupatwa na msiba ambao umepunguza nguvu kazi na wataalamu wa kizazi kijacho. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akitoa utangulizi pamoja na kuratibu ratiba ya ufunguzi wa mkutano. 
Sehemu ya Mawaziri wa Tanzania na viongozi waandamizi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini wakifuatilia Mkutano. 
Sehemu nyingine ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika kusini wakifuatilia Mkutano. 
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania na Afrika Kusini ambao pia walikua wenyeviti wa mkutano huo wakitoa ufafanuzi wa ratiba kwa Bi. Mindi wakati wa mkutano huo wa ngazi ya Mawaziri. 
Picha ya Pamoja ya Mawaziri na Viongozi wa Serikali ya Tanzania na Afrika Kusini.

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHATIMIZA MIAKA 27 KATIKA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA NCHINI

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akikata keki pamoja na baadhi ya wanachama wa chama hicho katika hafla fupi ya chama hicho kutimiza miaka 27 tamgu kilipoanzanishwa baada ya kusajiliwa rasmi mwaka 1990 na kuanza kazi zake rasmi hapa nchini. 

Chama hicho kimefanikiwa kuanzisha matawi yake katika mikoa ya Tanga, Dodoma, Arusha, Mwanza pamoja na Dar es salaam na chama hicho kimeweza kusaidia mamilioni ya watanzania hasa wanawake katika masuala ya msaada wa kisheria katika unyanyasaji wa kijinsia na migogoro ya kifamili hasa ndoa na masuala mengine, hafla hiyo iliyofanyika ofisi za taasisi hiyo Ilala Bungoni
2
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akimlisha keki Mwanachama wa chama hicho Bi Mariam Mvano wakati wa hafla hiyo.
3
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akilishwa keki na Mwanachama wa TAWLA Mariam Mvano wakati wa hafla hiyo.
4
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akimlisha keki mwanachama wa TAWLA Judith Kadege.
5
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akilisha keki mwanachama wa chama hicho Chaya Mlaki wakati wa hafla hiyo iliyofanyika ofisi za taasisi hiyo Ilala Bungoni
67
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Wanasheria wanawake TAWLA wakiwa katika hafla hiyo.
8
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akizungumza na wanachama hao.
910
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Bi. Judith Kadege akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofifi za taasisi hiyo Ilala Bungoni.
11
Baadhi ya wanachama wakimsikiliza Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka wakati alipokuwa akizungumza nao katika hafla hiyo.
12
Mmoja wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Bi. Judith Kadege akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofifi za taasisi hiyo Ilala Bungoni.
13
Baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiwa katika hafla hiyo.
14
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
1516
Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini Tanzania TAWLA Bi. Athanasia Soka akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AWATAKA WATANZANIA KUNUNUA BIDHAA ZA NYUMBANI

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Biashara Wilaya alilozindua rasmi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse).

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.



Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba akiangalia bidhaa za vigae zilizotengezwa kwa kutumia majani ya mkonge wakati wa maonesho ya wajasiliamali kabla ya uzinduzi wa Baraza la Biashara Kishapu.



Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akizungumza katika ufunguzi wa Baraza la Biashara.



Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba pochi iliyotengezwa kwa mkonge na kikundi cha wanawake wajasiliamali wilayani humo.



Wajumbe wa Baraza la Biashara Wilaya ya Kishapu wakifuatilia kikao hicho.


Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Shinyanga, Dk. Meshack Kulwa akizungumza katika kikao hicho.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba (kushoto) akiangalia ngozi ghafi alipotembelea banda la kikundi cha wajasiliamali wa kutengeneza viatu cha Badimi.



Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga wakiangalia viatu vilivyozalishwa na kikundi cha wajasiliamali Cha Badimi kilichopo wilayani humo.



Ofisa Biashara Wilaya ya Kishapu, Konisaga Mwafongo akichangia mada katika kikao hicho.



Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga (SHIREMA), Gregory Kibuse akizungumza wakati wa kikao.



Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga, Jumbe Samson akifafanua jambo wakati wa kikao.



Mashine ya kupura nafaka zikiwemo mtama iliyobuniwa na mwananchi wa Kishapu, Daudi Nkende ikiwa katika viwanja vya halmashauri kwa ajili ya maonesho ya wajasiliamali.

………………………………………………………………………..

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Talaba amewataka Watanzania kupenda kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kwenda sambamba na sera ya Tanzania yenye viwanda pamoja na kuimarisha uchumi wetu.

Amesema hayo wakati akizindua Baraza la Biashara Wilaya ambapo alishangazwa na baadhi ya kuamini kuwa bidhaa zinazozalishwa nchini hazina ubora na hivyo kukimbilia za nje.

Talaba ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Biashara Wilaya alisema bidhaa zetu zina ubora kutokana na kutumia malighafi halisi akitolea mfano viatu vinavyozalishwa na Watanzania ukilinganisha na vinavyotoka nje ya nchi ambavyo vingi havidumu.

”Tufike mahali sasa tununue bidhaa zetu ili fedha izunguke kwani tutaimarisha uchumi na kama tunavyofahamu lengo la Rais katika sera ya nchi ya viwanda anataka tununue bidhaa zetu.

Mkuu huyo wa wilaya alilitaka baraza liwe chachu ya kusukuma sera ya nchi ya viwanda na kuibua fursa ambazo wananchi waananchi wanaweza kuzitumia na kuanzisha biashara.

Alilitaka baraza kuja na wazo mbadala la kibishara na kiviwanda ili wananchi waweze wawaunga mkono wajasirimali wadogo wanaojishughulisha na uzalishaji wa bidhaa wapate masoko.

Akifungua kikao cha kwanza cha baraza hilo, Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Barazaa la Biashara Wilaya, Stephen Magoiga aliwataka wananchi kutumia vizuri fursa zilizopo wilayani humo.

Magoiga ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu alisema tukitumia vizuri rasilimali zilizopo wilayani humo tutapiga hatua na kujenga historia.

”Tunapozungumzia viwanda siyo lazima viwe vikubwa hata vidogo vidogo mfano tunaweza kutumia kilimo kuibadilisha kabisa Kishapu na kuwa wilaya ya kwanza katika uchumi,” alisema.

Alitaja rasilimali kama madini na fursa za kilimo zilizopo wilayani humo kuwa kama zikitumika ipasavyo maisha ya wananchi yataboreka zaidi na uchumi kwa ujumla kuimarika.

Baraza hilo la biashara Wilaya ya Kishapu linaundwa na wajumbe 40 wakiwemo wawakilishi kutoka sekta ya umma na binafsi na litadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

SHIRIKA LA WOTESAWA LAZIDI KUSAMBAZA ELIMU YA KUTETEA HAKI ZA WATOTO WAFANYAKAZI WA NYUMBANI.

$
0
0

Mwanasheria na Msimamizi wa Mradi wa Uwezeshaji Shirikishi kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani nchini Tanzania, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina kwa Viongozi wa serikali za mitaa kutoka wilaya za Nyamagana na Ilemela mkoani Mwanza.

Semina hiyo ya siku tatu, kuanzia jana Mei 09 imewashirikisha Madiwani, Watendaji wa Kata, Maafisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii, Wenyeviti wa Mitaa na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi imelenga kuwajengea uwezo viongozi hao ili kusaidia kutetea na kulinda maslahi ya mtoto mfanyakazi wa nyumbani na kumuepusha na utumikishwaji wa kazi ngumu na maslahi duni.

Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akiwasilisha mada kwenye semina hiyo ambapo pia ameelezea juu ya umuhimu wa viongozi hao kuitambua Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 ambayo inakataza mtoto chini ya umri wa miaka 14 kuajiriwa huku wale walio juu ya umri huo wakipaswa kuajiriwa kufanya kazi zisizo hatarishi.

Aidha amekumbusha juu ya kuutambua Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 ambao unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni rai wakigeni.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akichangia mada
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwasilisha maoni yao baada ya majadiliano katika makundi
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo
Semina hiyo ilianza jana Mei 09,2017 na inatamatika kesho Mei 11,2017 Jijini Mwanza

Waraka wa Mishahara wa mwaka 2013 kwa wafanyakazi wa nyumbani



Afisa kutoka shirika la WOTESAWA akiwa kwenye semina hiyo



Diwani wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, John Kabadi, amesema semina hiyo itwasaidia katika kutetea maslahi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwaepusha na utumikishwaji pamoja na ujira duni.



Gloria Shindika kutoka dawati la jinsia, kituo cha polisi Igogo Jijini Mwanza, amesema semina imewaongezea mbinu zaidi za namna ya kuwasaidia watoto wafanyakazi wa nyumbani watakaokuwa wakikumbwa na aina yoyote ya utumikishwaji.



Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamanoro Kaskazini, Kata ya Ibungilo Manispaa ya Ilemela, ameeleza kutumia elimu aliyoipata kwenye semina hiyo katika kuwaelimisha wananchi wa mtaa wake katika kuhakikisha maslahi na haki za mtoto yanalindwa



Mwanasheria wa Shirika la WOTESAWA, Jackline Ngallo, akizungumza na Lake Fm Mwanza



Shirika la WOTESAWA linawahimiza wanajamii kwamba bado watoto wafanyakazi wa nyumbani wanayo haki ya kupata elimu hivyo ni vyema haki hiyo ikazingatiwa.

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Afanya Ziara Tripoli, Libya

$
0
0
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa AU katika Usuluhishi wa Mgogoro wa Libya jana tarehe 10 Mei amefanya ziara jijini Tripoli, Libya kuzungumza na wadau muhimu wa siasa wa Libya. Safari hiyo ni ya kwanza kuifanya nchini Libya tokea kuteuliwa kwake kuwa Msuluhishi wa mgogoro huo.

Akiwa jijini Tripoli, Rais Mstaafu na ujumbe wake kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika amekutana na Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Libya Mhe. Fayez Serraj na Rais wa Baraza Kuu la Libya (High State Council) Mhe Abdulrahman Asswehly.

Katika mazungumzo yake na viongozi hao, Rais Mstaafu amewapongeza kwa hatua madhubuti walizochukua katika kuimarisha hali ya usalama jijini Tripoli ambapo theluthi moja ya wakazi wa Libya huishi humo. Amejionea na kufurahishwa kwa kurejea na hali ya usalama na shughuli za kijamii na kiuchumi. 

Ameelezea dhamira ya Umoja wa Afrika kuendelea kusaidia pande zinazotofautiana ndani ya Libya kufikia makubaliano. Amesisitiza kuwa suluhisho la mgogoro wa Libya liko mikononi mwa wananchi wa Libya wenyewe. Ameunga mkono dhamira njema ya pande zinazotofautiana kupitia upya baadhi ya vipengele vya Mkataba wa Makubaliano wa Siasa (Libya Political Agreement) kwa lengo la kuuimarisha. 

Kwa upande wao, viongozi hao kwa nyakati tofauti wamemshukuru Rais Mstaafu kwa kufanya ziara Libya na wamepongeza kwa uamuzi wake huo. Wameichukulia ziara hiyo kuwa ni imani kubwa juu ya kuimarika kwa hali ya usalama nchini mwao. Wameelezea dhamira yao ya kuendeleza Mkataba wa Makubaliano uliopo na kutumia njia ya mazungumzo kumaliza tofauti zilizopo. Wameomba Umoja wa Afrika kuendelea kusaidia jitihada za amani na kuchangia uzoefu katika kusuluhisha mgogoro wao. 

Rais Mstaafu anaendelea na ziara yake nchini Libya kwa kukutana na viongozi wa upande wa Mashariki mwa Libya.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Baraza la Taifa (High State Council) wa Libya Mhe. Abdulrahman Asswehly jijini Tripoli, Libya
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Libya Mhe. Fayaz Serraj jijini Tripoli, Libya

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS WA AFRIKA KUSINI,JACOB ZUMA LEO JIJINI DAR

$
0
0
 
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma pamoja na mwenyeji wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya wafanyakazi wa Ikulu na wananchi waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017
 Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa sambamba na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma mapema leomara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es salaam mei 11,2017.
 Rais Dkt Magufuli akimsikiliza Makamua wa Rais,Samia Suluhu Hassan wakati wa mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini,Jacob Zuma mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar
 Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini,Jacob Zuma akisalimiana na Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassani mapema leo kwenye viwanja vya Ikulu,jijini Dar,kushoto ni Rais Dkt John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo mara baada ya kumpokea mgeni wake
 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpigia makofi mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mhe. Jacob Zuma alipokuwa akipiga ngoma,mara baada ya kuwasili na kupokelewa mapema leo katika viwanja vya Ikulu,jijini Dar Es Salaam .
  Muonekano wa njia ya kuingilia Ikulu leo tayari kwa mapokezi ya Rais wa Afrika Kusini,Mhe.Jacob Zuma
 Moja ya kikundi cha ngoma za asili kilichoshiriki kusherehesha mapokezi wa Rais wa Afrika Kusini,Mhe.Jacob Zuma katika viwanja vya Ikulu mapema leo jijini Dar.Picha kwa hisani ya Ofisi ya Makamu wa Rais.

MASAUNI AFUNGUA GEREZA LA WANAWAKE MPWAPWA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akishirikiana na Viongozi wengine kufungua Gereza  la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa  kushirikiana na wafungwa.Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa, mkoani Dodoma.
 Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, Mheshimiwa George Lubeleje , akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya Mpwapwa,mkoani Dodoma.
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa,  akizungumza wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa  lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,Mkoani Dodoma.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kulia), akiongozana na Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa (kulia) kuelekea katika eneo lilipo  Gereza la Wanawake Mpwapwa, lililojengwa na wataalamu ambao ni askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.
Wananchi wa Mpwapwa wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa lililojengwa na wataalamu ambao ni  askari magereza kwa kushirikiana  na wafungwa.Gereza hilo limegharimu jumla ya shilingi milioni 65 .Ufunguzi huo umefanyika wilaya ya  Mpwapwa,mkoani Dodoma.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Na Mwandishi Wetu, MOHA.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kushirikiana na Benki ya Exim inatarajia kujenga nyumba 9500 za askari magereza ili kukabiliana na changamoto za makazi ya askari  wa jeshi hilo hapanchini.

Akizungumzia changamoto za Makazi ya askari wa Jeshi la  Magereza Nchini, wakati wa uzinduzi wa Gereza la Wanawake wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, alisema Serikali inatambua changamoto za makazi kwa askari magereza na tayari iko katika mazungumzo na benki ya Exim ili iweze kujenga nyumba hizo.

“Nawaomba  askari wetu nchi nzima  wawe na subira  Serikali inatambua na  inashughulikia changamoto ya makazi ya  askari na tayari tuko katika mazungumzo na wadau ikiwemo benki ya Exim kuanza mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 9500, lengo ni kukidhi kiu ya makazi ya askari na familia zao,” alisema Masauni.

Awali akitoa maelezo ya ujenzi wa Gereza hilo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, Dk. Juma Malewa alisema ujenzi wa Gereza hilo umefanywa na wataalamu ambao ni askari Magereza kwa  kushirikiana na wafungwa kama sehemu ya utekelezaji wa  amri ya Mh. Rais Dk. John Magufuli ya kutaka wafungwa watumike katika kazi za uzalishaji ikiwemo kilimo,ujenzi na ufundi mbalimbali.

Ujenzi wa Gereza hilo umegharimu jumla ya shilingi milioni 65 na litasaidia pia  kuhifadhi wafungwa 148 na hivyo kupunguza msongamano wa wafungwa katika Gereza la Kongwa mkoani Dodoma pamoja na kuepuka usumbufu wa  ndugu wa wafungwa kusafiri mpaka wilayani Kongwa kwenda kuwaona ndugu zao.

KAIMU JAJI MKUU AMALIZA ZIARA YAKE, MANYARA AKUTANA NA MKUU WA MKOA WA MANYARA

$
0
0
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma, akisalimiana na baadhi ya Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Hanang/Katesh pindi alipowasili katika Mahakama hiyo kwa lengo la kujionea hali ya utoaji haki nchini.
 Kaimu, Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akiongea na Watumishi wa Mahakama ya Wilaya Hanang, kushoto ni Kaimu Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha, Mhe. Sekela Moshi.
 Watumishi wa Mahakama ya Wilaya ya Hanang wakimsikiliza Kaimu Jaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma alipokuwa akizungumza nao alipofika Mahakamani hapo kwa lengo la kujionea hali ya utendaji kazi wa Mahakama hiyo.
 Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera pindi alipomtembelea ofisini kwake mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Joel Bendera (kushoto) akimueleza jambo Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania pindi alipomtembelea ofisini kwake mkoani Manyara, katika maongezi yake Mkuu wa Mkoa huo, ameisifu Mahakama mkoani humo kwa kusaidia kupunguza mgogoro kati ya Wakulima na Wafugaji Wilayani Kiteto mkoani humo kufuatia maamuzi yaliyotolewa na Mahakama kuhusiana na mgogoro huo.

Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Mkoa na Mahakama na kusisitiza muendelezo wa ushirikiano huo kwa manufaa ya wananchi. (Picha na Mary Gwera)

MKE ANARUHUSIWA KUKOPA KWA JINA LA MME WAKE BILA RIDHAA YA MME.

$
0
0
Na  Bashir  Yakub.

Ndio  ni  kweli  mwanamke  aliyeolewa  anaweza  kukopa  hela  kwa  jina  la  mme  wake.  Tena  kukopa  kwenyewe   si  lazima  awe  amepata  ridhaa  au  ruhusa   kutoka  kwa  mme  wake.   

Pia  si ruhusa  tu  bali  si  lazima   amtaarifu  mme  huyo. Sheria  ya  ndoa  , sura  ya 20 iliyofanyiwa  marekebisho  mwaka  2010  ndiyo iliyoeleza  jambo  hili . Lipo kifungu  cha  64  cha  sheria  hiyo.

Kwa  ujumla  makala   haya  yatatizama  jambo  hili  likoje,  linahusisha nini  na  nini, vigezo   na  sifa  za  kufanya  hivyo na  mambo  mengine  ambayo  yanalizunguka  jambo  hili  lakini  kwa  ufupi.

1.MWANAMKE  GANI  ANAWEZA  KUKOPA.

Kifungu  hicho  kimesema mwanamke  anayeweza  kukopa  ni  yule   aliye  kwenye  ndoa  inayotambulika  kisheria.  Ikiwa  mwanamke  hayupo katika  ndoa  ambayo  sheria inaitambua  basi  haki  hii  ya  kukopa  kwa  jina  la  mme  wake  anaikosa. 

Ikiwa  mmetengana  lakini  ndoa  haijavunjika  kisheria  basi  haki  hii inaendelea  kubaki.  Isipokuwa  tu  itaondoka  ikiwa  mmetengana  kwa  makubaliano  maalum  ambapo  matunzo  na  matumizi  yote  mwanamke  anapata  bila  wasiwasi.

Pia  ikiwa  kuna  talaka  basi  mwanamke  hawezi  kukopa  kwa  jina  la  mme  wake  kwa  kuwa  talaka  kisheria   inavunja  ndoa  na  hivyo  tafsiri yake  ni  kuwa  hakuna  ndoa.  Lakini  kukiwa  na  shauri  la  talaka  mahakamani  na  ndoa  haijavunjwa  rasmi  na  mahakama  basi  haki  hii  inaendelea  kubaki  kwa  mwanamke  huyo.

2. KWANINI  SHERIA  IMEMRUHUSU  MWANAMKE  KUKOPA  KWA  JINA  LA  MME  .

Sheria  imemruhusu  mwanamke  kukopa  kwa  jina  la mme  wake  tena  bila  hata  ridhaa  ya  mme  wake  kwakuwa   imempa  wajibu  mume  kumtunza  mke  wake  na  mtoto/watoto  kama  yupo.  Kwa  mujibu  wa  sheria  ya  ndoa  ni  lazima  mume  kumtunza  mke  wake  pamoja  na watoto  kama  wapo. 

Kwa  upande  mwingine  mwanamke  naye  anaruhusiwa  kumtunza  mme  wake  lakini  kwake  sio  lazima.  Sheria  haijampa  ulazima  mwanamke  bali  mwanaume .  Kwahiyo  ni  katika  mazingira  haya  ambapo   suala la  mke  kukopa    bila  ridhaa  ya  mme  wake   tena  kwa   jina  la  mme  huyo  linapokuja. 

Hata  hivyo  sio  wakati  wote  mwanamke  anaruhusiwa  kukopa  kwa  njia  hiyo  bali  ni pale  tu  mume  wake  anapokaidi  wajibu  wake  wa  lazima  wa  kumpa  matunzo/matumizi.  Hapa  ndipo  mwanamke  anaweza  kukopa    kwa  jina  la  mme  wake  tena bila  hata ridhaa  ya  mme  huyo.

 Mke  hataruhusiwa  tu   kufanya  hivyo  kwa  kutopewa  mahitaji  yake  pekee  bali pia  hata  kama  ana watoto/mtoto   nao  hawajapewa  mahitaji  basi  hata  hapo  anaruhusiwa  kukopa. 

                      KUSOMA  ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUCHIMBA MABWAWA YA MAJI ILI KUPUNGUZA UHABA WA MAJI NCHINI.

$
0
0
Na Husna Saidi.

SERIKALI imesema imeandaa mpango kabambe wa uchimbaji wa mabwawa ya kutiririsha maji ya mvua katika baadhi ya maeneo nchini ili kupunguza hadha ya ukosefu wa maji kwa wananchi.

Hayo yamebainishwa leo Bungeni Mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo na Wazirti katika kikao cha Bunge la bajeti linaloendelea Mjini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema katika kutekekeleza mpango wa Serikali kumtua “Mama ndoo kichwani” Serikali imedhamiria kupunguza umbali mrefu wanaotumia wananchi kutafuta maji, ambapo imepanga kuchimba mabwawa makubwa ya maji katika  maeneo ambayo yana mtiririko wa maji.

“Tutaendelea kutoa maelekezo kwa Watendaji wetu kuhamasisha wananchi kutumia fursa ya misimu wa mvua ili kujiwekea akiba ya maji ambayo yatawasaidia wakati wa kipindi cha kiangazi hususani katika maeneo ambayo yana uhaba wa maji”.

Kwa mujibu wa Majaliwa alisema katika Bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Serikali imeandaa mpango maalum wa uchimbaji wa mabwawa ya maji sambamba na kufanya ukarabati wa mabwawa ambayo yameharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alizitaka Halamashauri zote nchini kuhakikisha zinatumika vyema mabwawa na mifereji iliyokuwa katika maeneo ili kuweza kuvuna maji ya mvua na kuyahifadhi kwa msimu huu wa mvua na ujao.

Majaliwa aliongeza kuwa Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya kukarabati miundombinu ya mabwawa yote nchini ili kuhakikisha halmashauri zote nchini zinakuwa na utoshelevu wa huduma ya maji kwa wananchi wake.
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali Mbalimbali ya Wabunge katika kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.

MATUKIO KATIKA PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA ISHIRINI NA MBILI MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 11, 2017.

$
0
0
 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dk. Tulia Ackson akiongoza  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akijibu maswali Mbalimbali ya Wabunge  katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dk.Medard Kalemani wakifuatilia hoja mbalimbali Bungeni katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
  Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Amina Mollel(CCM) akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Prof,Palamagamba Kabudi  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe.George Simbachawene akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe,Ummy Mwalimu  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais(TAMISEMI) Mhe.Suleiman Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge   katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Kiongozi Mkuu wa Kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Mhe.Freeman Mbowe akimuuliza swali Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijadili jambo na wabunge mbalimbali kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.

 Mbunge wa Same Magharibi(CCM) Mhe David Mathayo David akiuliza swali katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.
Wabunge wakijadili jambo katika kipindi cha maswali na majibu katika  kikao cha Ishirini na mbili cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 11, 2017.


Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

LAPF YADHIHIRISHA KUWA CHAGUO BORA KWA WAAJIRIWA WAPYA

$
0
0
Mfuko wa Pensheni wa LAPF umekuwa ni chaguo la wanachama hasa waajiriwa wapya kutokana na ubora wa huduma zinazotolewa pamoja na kutekeleza ahadi zake kwa wanachama. 

Hivi karibuni Serikali ilitoa ajira za walimu wa sayansi 3,084. Katika walimu hao walioripoti katika vituo vyao vya kazi walikuwa walimu 2,792 na katika hao walioripoti LAPF iliibuka kidedea baada ya walimu 1,888 kuchagua kujiunga na LAPF sawa na asilimia 68 ya walimu wote walioripoti.

Hii inadhihirisha wazi kuwa Mfuko wa LAPF ndio Mfuko bora wa Pensheni hapa Tanzania. LAPF imekuwa na ongezeko kubwa sana la wanachama kutoka sekta binafsi na serikalini kutokana na huduma zinazotolewa ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama wake na haswa waajiriwa wapya. 

Hadi kufikia mwezi Aprili 2017, Mfuko wa LAPF una wanachama zaidi ya 172,000 ambapo ndani ya mwaka wa fedha 2016/2017 pekee LAPF imeandikisha wanachama wa kisheria 16,839 na wa Hiari kupitia LAPF Jiongeze Scheme 645. 

Baadhi ya huduma zinazotolewa na Mfuko wa Pensheni wa LAPF ni pamoja na Mikopo ya kujikimu kwa waajiriwa wapya ili waweze kujikimu na mahitaji muhimu mara wanapoanza ajira ambapo hadi sasa wanachama 518 wamenufaika na mkopo huu maarufu kama Maisha Popote na LAPF. 

Kadhalika pia LAPF inatoa mikopo ya elimu kwa wanachama wake kwa ajili ya kujiendeleza kielimu. Hadi sasa LAPF imeweza kutoa mikopo hii kwa wanachama 1438 yenye thamani ya shilingi 2.4 bilioni. 

LAPF pia inatoa mafao ya uzazi kwa wanachama wake ambapo wanachama wanawake wanapojifungua hulipwa asilimia 129.3% ya mshahara wao kama mafao ya uzazi. Hadi sasa tangu kuanzishwa kwa fao hili wanachama 11,744 wamelipwa mafao uzazi yenye thamani ya shilingi bilioni 9.54. 

LAPF ndio Mfuko pekee hapa nchini ambao unaowalipa wanachama wake mapema na hata siku chache kabla ya kustaafu. Tangu kuanza kwa utaratibu huu wanachama 1691 wamelipwa mapema kabla ya tarehe ya kustaafu. 

Takwimu hizi zinadhihirisha wazi utekelezaji wa ahadi kwa wanachama wa LAPF. ISHI NA KUSTAAFU KWA UFAHARI NA LAPF.
Meneja Masoko na Mawasiliano Mfuko wa Pensheni wa LAPF James Mlowe akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Makao makuu ya Mfuko huo mjini dodoma leo. Kushoto ni meneja Matekelezo wa LAPF Victor Kikoti.
Meneja Matekelezo wa LAPF Victor Kikoti akifafanua jambo mbele ya wanahabari mapema leo mjini Dodoma,
Baadhi ya Waandishi wa Habari Mjini Dodoma walioshiriki katika mkutano wa LAPF Dodoma Leo. LAPF imedhihirisha kuwa Chaguo Bora kwa Waajiriwa wapya.

TAARIFA KWA UMMA

MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA SIMU ZA MIKONONI YA VIATTEL TANZANIA APANDISHWA KISUTU KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI

$
0
0

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Viattel Tanzania (Halotel) Do Manh Hong, kampuni amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka saba likiwemo la uhujumu uchumi.

Mshtakiwa Do Manh Hong amefikishwa mahakamani hapo na kuunganishwa na washtakiwa wengine saba waliofikishwa mahakamani hapo mapema Mwaka huu.

Wote kwa pamoja wanakabiliwa ma mashtaka kumi, kula njama. Kisimika mitambo ya mawasiliano bila kibali cha TCRA, kutoa nyaraka za uongo, kusababisha hasara kwa serikali ya Tanzania,  ya milioni 459, kutumia mitambo ya mawasilino ambayo haijathibitishwa na namba za simu.

Mbali na Hong, washtakiwa wengine ni Dilshad Ahmed (36), Rohail Yaqoob(47), Khalid Mahmood (59), Ashfaq Ahmad (38), Muhamad Aneess(48), Imtiaz Ammar (33) wote raia wa Pakistan na Ramesh Kandasamy (36) raia wa Sri-Lanka.

Kabla ya kusoma kwa mashtaka, wakili wa Serikali, Jehovanea Zacharias aliiomba mahakama kumuunganisha mshtakiwa Hong na kuwasomea washtakiwa wote makosa yao.

Imedaiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kuwa mshtakiwa Ahmed, Yaqoob,  Mahamood, Ahmad, Anees, Kandasamy na Qammar Novemba 2016 Dar es Salaam walikula njama ya kutumia vifaa vya mtandao.

Imedaiwa kuwa, watuhumiwa walitengeneza mfumo wa kutumia huduma za mtandao kwa lengo la kukwepa kodi ya  kupokea na kusambaza simu za kimataifa bila kibali cha TCRA.

Aidha imedaiwa kuwa Novemba 20, 2016 waliingiza vifaa vya kielektroniki  bila ya kuwa na leseni na kuvisimika  bila ya kuwa na kibali cha  TCRA.

Imedaiwa, washtakiwa waliunganisha  vifaa hivyo na huduma za mitandao kwa lengo la kupokea na kusambaza mawasiliano bila ya kuthibitishwa na TCRA.

Kwa upande wa Kampuni ya Viettel Tanzania Limited na Do Hong wanadaiwa kati ya Novemba 2016 na Februari 2017 maeneo ya ofisi za Halotel Victoria Kinondoni walishindwa kuthibitisha taarifa iliyotolewa na Unex Company Ltd kwa lengo la kusajili lakini za simu 1000.

Kwa upande wa washtakiwa Ahmed na wenzake sita wanadaiwa kuwa Januari 5 ,2016 walitoa Cheti chakughushi cha usajili wa kodi chenye namba 100-864-210 kuonyesha imetolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania wakati si kweli.

Mbali na mashtala hayo, watuhumiw wote kwa pamoja wanadaiwa kuisababisha hasara TCRA na serikali ya Tanzania kiasi cha milioni 459.

Hata hivyo, washtakiwa wote hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mshtaka yanayowakabili yako nchini ya sheria ya uhujumu uchumi.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29,2017.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Viattel Tanzania ijulikanayo kama Halotel,Do Many Hong,  akitoka Katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kesi yake ya uhujumu uchumi kuahirishwa.  Hong pomoja na mwenzake nane wanakabiliwa na mashtaka kumi likiwemo la kuisababishia serikali hasara ya milioni 459
Viewing all 46373 articles
Browse latest View live




Latest Images