Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1219 | 1220 | (Page 1221) | 1222 | 1223 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini wakati wa hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam hao iliyofanyika Ofisi ya Rais-Utumishi leo.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akiwa katika picha ya pamoja na Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini.
  Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bi. Susan Mlawi akizungumza na Mwakilishi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo Japani (JICA) nchini, Bw. Toshio Nagase mara baada ya hafla fupi ya kuwakaribisha Wataalam wa kujitolea kutoka Japani waliokuja kutoa huduma nchini.

  0 0

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo amesema tatizo la kuharibika kwa mashine ya kusagia taka katika Hospitali Kuu ya Mnazimmoja siku za karibuni kulipelekea kurundikana kwa taka na kusababisha usumbufu kwa wananchi.

  Amesema baadhi ya wafanyakazi wakorofi wa Hospitali hiyo walitumia kasoro hiyo kuzitupa taka kwenye ufukwe wa bahari, nyuma ya Hospitali, ambapo ni kosa kwa mujibu wa sheria na kanuni za afya na uhifadhi wa mazingira.

  Waziri Mahmoud ametoa kauli hiyo alipofanya ziara ya kutembelea mashine ya kusagia taka zinazozalishwa katika Hospitali hiyo ambayo hivi sasa imefanyiwa matengenezo na ipo tayari kufanyakazi na kuondosha kero hilo.

  Amesema wafanyakazi saba waliobainika kufanya kosa la kutupa taka sehemu ya ufukwe wamechukuliwa hatua za nidhamu na kuuagiza uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kutomvumilia mfanyakazi atakaekiuka kanuni za afya.

  Hata hivyo Waziri wa Afya amekiri kuwa uzalishaji wa taka katika Hospitali ya Mnazimmoja umekuwa mkubwa kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa baada ya kutanuliwa na kufikia daraja la kuwa Hospitali ya rufaa.

  Ameyashauri Makampuni yanayohitaji taka kwa ajili ya kuzisarifu na kuzigeuza kwa ajili ya matumizi mengine waonane na uongozi wa Hospitali kwani sehemu kubwa ya taka hizo zinaweza kutumika kwa shughuli nyengine.

  Amesema hivi sasa uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja umeandaa utaratibu mzuri wa kukusanya taka ambapo za aina moja zinatiwa katika pipa moja na mapipa hayo yamewekwa katika wodi ili kuondosha usumbufu kwa wafanyakazi, wagonjwa na watu wanaofika kwa shughuli mbali mbali.

  “Nataka wananchi wawe waangalifu wakati wa kuhifadhi taka kwani kila pipa linatiwa taka maalumu na hakuna kuchanganya taka zote katika pipa moja,” alisisitiza Waziri Mahmoud. 

  Amewataka wafanyakazi wa Hospitali kusimamia na kuwaelimisha wananchi matumizi ya mapipa hayo ili kila pipa liingizwe taka zinazostahiki ili kuondosha usumbufu wakati wa zoezi la kuzisaga.

  Mtaalamu wa mashine ya kusagia taka kutoka Kenya Benard Abere amemueleza Waziri wa Afya kwamba kazi ya kuifanyia matengenezo mashine hiyo imekamilika na katika kipindi cha wiki moja mkusanyiko wa taka utaondoka.
  Waziri wa Afya Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akipata maelezo ya mashine mpya ya kusagia taka za hospitali kwa Mtaalamu wa mashine hizo kutoka Kenya Benard Abere. Picha na Makame Mshenga. 

  0 0

  Na. Hassan Mabuye & Muhammad Salim.

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi ameamuru kusimamishwa kazi Afisa Mipango Miji wa Lindi Ndugu Castory Manase Nkuli baada ya kunyang`anya ardhi ya vijiji vya Ruvu na Mchinga hekari 4000 na kumilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate kinyume cha sheria ya Ardhi.

  Mhe. Lukuvi aligundua hayo baada ya kuona utaratibu wa umilikishaji wa ardhi haukufuatwa  na badala yake kuonekana kuwa na mianya ya rushwa kwa kuwa ardhi hiyo imehamishwa kutoka ardhi ya kijiji hadi kumilikishwa kwa kampuni ya Azimio ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais.

  Aidha, Afisa Mipango Miji huyo aligundulika kuwa na kosa la kughushi kwa kujifanya ni Afisa ardhi baada ya kuandika barua na kuisaini kwa niaba ya Afisa ardhi wakati yeye ni Afisa Mipango Miji ili kuimilikisha kampuni ya Azimio Housing Estate ambalo pia ni kosa kisheria.

  Akithibitisha makosa hayo Kaimu Mkurugenzi Mipango Miji na Vijiji kutoka Wizara ya Ardhi Bi Immaculate Senje amesema kwamba utaratibu wa umilikishaji wa ardhi hiyo haukufuatwa ambapo kisheria ilitakiwa hati ya eneo hilo itoke kwa idhini ya Rais na baada ya Tangazo la Serikali na kuridhiwa na wana kijiji. 

   “Kama nyie hamna uwezo wa kumfukuza kazi basi mie namsimamisha kazi kuanzia leo hafai kuwa mtumishi wa serkali” alisema Mhe. Lukuvi na kuagiza eneo hilo lirudi na kuwa mali ya serikali “ Sasa hiyo ardhi lazima irudi itakua mali ya serikali kuanzia leo” .

  katika ziara hiyo, Mhe. Lukuvi ametembelea ofisi za ardhi Lindi na kufanya ukaguzi katika Masijala za ardhi na kuangalia mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi, kisha kuwaagiza watendaji wa ardhi mkoani hapo kuhakikisha wanatoa hati kwa wakati na kukusanya kodi ya pango la ardhi kwa kila mmiliki wa ardhi ili kuongeza pato la serikali.

  Pia alitembelea ofisi za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani hapo na kupokea taarifa kutoka kwa Meneja wa shirika hilo mkoani Lindi Ndugu Gibson Mwaigomole. Katika taarifa hiyo Mhe. Lukuvi amelishauri Shirika la Nyumba la Taifa kufanya uwekezaji mkoani Lindi kwa kujenga ofisi za kisasa pamoja na Nyumba zenye gharama nafuu.

  Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi akiwa pamoja na waziri Lukuvi na watendaji wa mkoa ameeleza kuwa sekta ya ardhi mkoani hapo inachangamoto nyingi lakini ofisi yake inaendelea kufanya jitihada za makusudi kuhakikisha changamoto hizo zinapungua au kuzimaliza kabisa kwa maslahi ya watu wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. 
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimsimamisha kazi Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi kuhusu tuhuma za kumilikisha ardhi kinyume cha sheria.
    Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (kushoto) wakihakiki nyaraka na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi (kulia) katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi, watendaji na viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiwa katika mkutano wakati wa ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
      Kaimu Mkurugenzi wa Mipango Miji na Vijiji Bi. Imaculate Senje akizungumza kuhusu utaratibu za upangaji miji  na umilikishaji ardhi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
   Ndugu Castory Manase Nkuli Afisa Mipango Miji wa Lindi akijieleza kuhusu tuhuma zinazomkabili mbele ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi katika ziara ya Mhe. Lukuvi mkoani Lindi.
   Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akikagua mafaili katika masijala ya ardhi mkoani Lindi ambapo alibaini mapungufu ya kutokuwa na usahihi wa uwekaji kumbukumbu za ardhi.
     Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakikagua mfumo wa ukusanyaji kodi ya pango la ardhi mkoani Lindi
   Ndugu Gibson Mwaigomole Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Lindi.

  0 0


   Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam jana.
   Mdau  Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
   Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
   Sadick Juma mkazi wa Mbezi Beach, akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
   Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
   Moses Benard akizungumzia wajawazito kujinunulia vifaa vya kujifungulia na suala la dawati la ukatili wa kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
   Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
   Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
   Semina ikiendelea.
   wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
  Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.

  Na Dotto Mwaibale

  WANANCHI wameiptia bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili kuona vipau mbele vyake waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na ukubwa wake.

  Kwa mwaka wa fedha wa 2016/ 2017 wizara hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni 845 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambayo tofauti yake sio kubwa.

  Akizungumza katika semina hiyo, Neofita Kunambi alisema katika wizara hiyo kunachangamoto kubwa bila ya kuongezewa fedha katika bajeti yake hazitaweza kuisha.

  "Bila ya kuongeza bajeti katika wizara hii wajawazito wataendelea kujinunulia vifaa vya kujifungulia tunaomba jambo liangaliwe kwa karibu" alisema Kunambi.

  Anna Sangai alisema huduma za afya zinapaswa kuboreshwa kuanzia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na bila kuongezwa kwa bajeti katika wizara hiyo itakuwa ni ndoto.

  Mkazi wa Mbezi Beach, Sadick Juma alisema upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, miundombinu na ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa katika wizara hiyo.

  Alisema licha ya kuwepo duka la Bohari ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili (MNH), upatikanaji wa dawa umekuwa mgumu hivyo kuifanya Muhimbili kuwa na majengo mazuri bila ya kuwa na dawa.

  "Ukitaka kuona changamoto hata ukiwa ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ugua au uwe na mgonjwa ambaye ni mwanachama uende katika hospitali hiyo kwanza kupokelewa tu pale mapokezi ni balaa na ukifika muda wa kutakiwa kupata dawa utaambulia panado na kuambiwa dawa hazipo" alisema Juma.

  Juma aliongeza kuwa huduma ya bure kwa watu wenye msamaha hiyo ni ndoto kwani wagonjwa hao hawasikilizwi kabisa jambo ambalo ni hatari.

  Alisema serikali imekuwa ikijipodoa kuwa inaboresha huduma za afya lakini hali halisi haipo hivyo akitolea mfano kwa nchi nzima maduka ya dawa ya MSD yapo nane tu je upatikanaji wa dawa na vifaa tiba utafikia katika kiwango cha kukidhi mahitaji alihoji Juma.

  Janeth Mawinza alisema bajeti hiyo iangalie zaidi jinsi ya kutibu magonjwa kama ya homa ya ini ambayo matibabu yake kwa hapa nchini hayapatikani mpaka dawa itoke nchini India.

  Moses Benard alisema ikiwa mjamzito aliopo mjini anatakiwa kujinunulia vifaa vya kujifungulia hali ikoje kwa yule ambaye yupo kijijjini ambaye anachangamoto ya kutokuwa na fedha na kukimbiwa na mwenza wake hivyo akaomba Waziri wa wizara hiyo kutoa tamko rasmi la kuwataka wajawazito kutonunua vifaa hivyo wanapokwenda hospitali kujifungua.

  Wadau wengine waliongelea jijini Dar es Salaam maeneo mengine kama Kipunguni wilayani Ilala kukosa kuwa na zahanati au hospitali hivyo kulazimika kwenda wilaya ya Kisarawe kupata matibabu jambo ambali linashangaza hivyo wakaomba bajeti ya wizara hiyo iongezwe ili kufanikisha upatikanaji wa zahanati au hospitali katika maeneo yao.


  0 0  0 0

  Katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani,Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC),leo Mei 3,2017 imefanya mkutano na wadau wa habari mkoani Shinyanga kujadili namna klabu hiyo ilivyo na wajibu wa kuendeleza amani katika jamii.
  Mgeni rasmi katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Liga Hotel mjini Shinyanga alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga.
  Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari huadhimishwa duniani kote kila ifikapo tarehe 3 mwezi Mei ya kila mwaka ambapo pamoja na maadhimisho ya kitaifa kufanyika kitaifa jijini Mwanza,lakini yamefanyika pia katika kila mkoa nchini yakiwa na kauli mbiu inayosemayo “Klabu za Waandishi wa Habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii”.
  Awali akitoa hotuba yake,Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde alisema Klabu za waandishi wa habari zina wajibu wa kuendeleza amani katika jamii hivyo kuwataka waandishi wa habari kutumia kalamu zao vizuri kuandika habari zinazojenga utaifa na kuleta mshikamano katika jamii.
  Malunde alisema Klabu za waandishi zinawaweka pamoja waandishi wa habari hivyo kupitia umoja huo zinawabijika kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza amani katika jamii kwani pasipo na amani hakuna maendeleo.
  Aliongeza kuwa kutokana na nguvu ya vyombo vya habari,amani katika jamii itaendelea kuwepo endapo tu waandishi wa habari watazingatia maadili ya kazi yao na kuepuka kushabikia mambo yasiyo na maana.
  Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack aliwataka waandishi wa habari kutanguliza utanzania na uzalendo katika habari wanazoandika.
  “Ndugu zangu waandishi wa habari mnajukumu kubwa la kulinda amani ya nchi hii,tumieni kalamu zenu vizuri,epukeni kuandika habari za kujenga hofu na mnapoandika basi msiegemee upande mmoja,sikilizeni hata upande wa pili ili kutenda haki”,alieleza mkuu wa mkoa.
  Katika hatua nyingine Telack aliwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano walionao na kujiendeleza kielimu huku akiwashauri kuanzisha miradi itayowakomboa kiuchumi kwani fursa mbalimbali za kiuchumi zipo mkoani humo.
  “Nitoe wito kwa waandishi wa habari kuunga mkono sera ya uchumi wa viwanda,andikeni habari kuhusu viwanda na kilimo na kupitia umoja wenu anzisheni mashamba ya pamba na alizeti na mnao uwezo wa kuanzisha viwanda vidogo ili kuinua uchumi wenu,andikeni proposal mnaweza kuanzisha hata kiwanda cha maziwa”,aliongeza Telack.
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack akifungua mkutano wa wadau wa habari wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani ngazi ya mkoa wa Shinyanga
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack. Kushoto ni Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.Kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde
  Katikati ni Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Zainab Telack
  Wa kwanza kulia ni  Afisa Uhamiaji Mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akifuatiwa na Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga
  Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa habari mkoa wa Shinyanga kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani Mei 3,2017
  Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa hotuba ukumbini
  Wadau wa habari wakiwa ukumbini
  Katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi akisisitiza jambo ukumbini
  Wadau wakiwa ukumbini
  Mwandishi wa habari Suleiman Shagata akichangia hoja ukumbini
  Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde(kushoto) na katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi wakiwa ukumbini
  Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiongoza majadiliano ukumbini
  Kaimu Mwenyeti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Shaaban Alley akizungumza ukumbini
  Mratibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Nunu Abdul akiandika dondoo muhimu
  Wadau wakiwa ukumbini
  Mkutano unaendelea
  Mkutano unaendelea
  Wadau wakiwa ukumbini
  Mkutano unaendelea
  Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akizungumza ukumbini
  Msaidizi wa Askofu Kanisa kuu la KKKT Shinyanga Usharika wa Ebenezer Trafaina  Assery Nkya akizungumza ukumbini
  Sheikh wa wilaya ya Shinyanga Soud Kategire akizungumza ukumbini
  Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani akizungumza ukumbini
  Kanali Mussa Kingai ambaye ni mwakilishi wa vikosi JWTZ Shinyanga kwenye kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga akichangia hoja ukumbini
  Mdau Gelard Ng'ong'a kutoka shirika la Rafiki SDO
  Afisa habari kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mji wa Kahama (KUWASA) bwana Mkama akichangia hoja
  Mdau wa habari bwana Chief Abdallah Sube akichangia hoja
  Bwana John Myola kutoka Shirika la AGAPE Shinyanga akizungumza ukumbini
  Mkurugenzi Msaidizi Radio Faraja,bwana Anikazi Kumbemba akizungumza ukumbini
  Mwakilishi wa Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga,Bi Alice Mazoko akichangia hoja 
  Mwandishi wa habari Patrick Mabula akifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
  Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack akizungumza ukumbini
  Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wadau wa habari na waandishi wa habari
  Picha ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Zainab Telack,wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Shinyanga na waandishi wa habari.Picha zote kwa hisani ya Shinyanga Press Club

  0 0


  Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi akifungua maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani kimkoa yaliyofanyika kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga (Tanga Press Club) leo kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George

  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim akizungumza katika maadhimisho hayo leo
  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George akizungumza katika maadhimisho hayo kushoto ni Katibu Msaidizi Alex Abraham

  Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim kushoto akifurahia jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi mara baada ya kupokea cheti cha kuripoti habari za majanga na hali hatarishi jana mafunzo waliyoyapata mkoani Morogoro hivi karibuni katika halfa iliyofanyika

  Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Lulu George naye akipokea cheti hicho kushoto ni Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba kulia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Hassan Hashim

  Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga,Amina Omari naye akipokea cheti hicho

  Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na Mwandishi wa Clous TV Mkoani Tanga Zawadi Kika naye akipokea cheti
  Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa Habari na mwandishi wa gazeti la Citizen Paskal Mbunga naye akipokea cheti .

  Mmiliki wa Blog ya Tanga Kumekucha na Mwanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani Tanga,Salum Mohamed naye akipokea cheti hicho

  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Dorah Killo akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo
  Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Benedict Wakulyamba akizungumza jambo kwenye maadhimisho hayo

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza umuhimu wa kujiunga na mfuko huo ili kuweza kunufaika na fursa zinazopatikana kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tanga Press Klabu,Lulu George

  Afisa Uchunguzi kutoka Takukuru Mkoani Tanga,Frank Mapunda akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo leo
  Afisa kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Sophia akisisitiza jambo kwenye maadhimisho hayo kulia ni Meneja wa Mfuko huo Mkoani Tanga,Ally Mwakababu anayefuatia ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Club) Lulu George

  Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo
  Sehemu ya waandishi wa habari mkoani Tanga wakiwemo wadau wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa ziki wakilishwa kwenye maadhimisho hayo leo


  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF),Ally Mwakababu kulia akiteta jambo na Mwandishi wa gazeti la Mtanzania katikati Amina Omari kushoto ni Ofisa wa Mfuko huo mkoani Tanga Sophia
  Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga (Tanga Press Klabu)Neema Omary kulia na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu hiyo,Amina Omari wakifuatilia matukio mbalimbai

  KATIBU Tawala Mkoa Tanga Mhandisi Zena Said ameziagiza taasisi za Serikali na mashirika ya umma kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye taasisi hizo kwa ajili ya kuhabarisha umma.

  Ameyazungumza hayo leo wakati wa kuadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari Duniani ambapo Mkoa Tanga maazimisho hayo yalifanyika katika ukumbi wa klabu ya waandishi wa habari na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka taasisi za serikali na zisizo za kiserikali.

  Hatua hiyo imekuja mara baada ya waandishi wa habari kutoa malalamiko yao mbele ya Katibu Tawala huyo wa Mkoa ambae alikua mgeni rasmi katika maazimisho hayo ya kuwa zipo baadhi ya taasisi za Serikali kushindwa kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari pindi wanapohitaji kutekeleza majuku yao ya kazi.

  Burhan Yakubu ambae ni mjumbe na mwaandishi wa habari alisema kumekuwepo na utaratibu usioendana na maadili ya kiuwandishi katika Hospitali kuu ya Rufaa ya Bombo kwa kutengeneza urasimu wa kupatikana kibali kutoka kwa katibu tawala Mkoa wakati mwandishi anapohitaji kupatiwa tariifa zozote kutoka katika Hospitali hiyo

  “Tumekuwa tukikwama kutekeleza wajibu wetu hasa tunapohitaji kupata taarifa katika Kuu ya Rufaa ya Bombo na kulazimishwa mpaka tupate kibali kutoka kwa katibu Tawala jambo ambalo limekuwa liktkwamisha katika shughuli zetu”Alisema Yakubu.

  Akitolea ufafanuzi malalamiko hayo Mhandisi Zena alisema taasisi zote zinapaswa kutambua kuwa wanahabari wanahaki ya kupatiwa taarifa sahihi kwa lengo la kuihabarisha jamii na hakuna sababu za kuweka vikwazo kwao kwa lengo la kuwakwamisha kutimiza majukumu yao.

  Mhandisi Zena alisema zimekuwepo taarifa za malalamiko kwa waandishi kuwa zipo baadhi ya tasisi kama Hospitali ya Rufaa ya Bombo kutokutoa ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari pindi wanapotaka kutekeleza wajibu wao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

  “Tusiwawekee mipaka waandishi wakati wanapotaka kutekeleza majuku yao na tayari nimekwisha toa agizo sio Hospitali ya Bombo tu hili ni kwa taasisi zote,hakuna jambo linaloweza kufanyika na mwananchi akaweza kulipata kwa wakati ikiwa hakuna waandishi,tunatambua umuhimu wenu na thamani yenu ni kubwa kwa Taifa Hili.”Alisema

  Hata hivyo alitumia fursa hiyo kuwaomba waandishi wa habari kutumia kalamu zao vema na kuwepo na maadili yatakayokuwa na maslahi mapana kwa ajili ya amani ya nchi na kujiepusha na taarifa zitakazoweza kuliingiza Taifa kwenye machafuko.

  Katika hatua nyingine Mwandishi wa Tanzania Daima Mkoani Tanga Mbaruku Yusuph alitaka kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa Tanga,Kamishna Msaidiz,Mwandamizi wa Polisi Benedict Wakulyamba,juu ya usalama wa waandishi wa habari wanapotekeleza wajibu wao hasa katika mikutano ya kisiasa.

  Mbaruku alisema hivi karibuni kumeripotiwa kutokea matukio kwa baadhi ya waandishi wa habari maeneo mbalimbali hapa nchini kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kushindwa kuwajibika katika harakati zao za kupata habari kwa lengo la kuhabarisha umma na kujenga hofu kubwa kwa baadhi yao juu ya usala wa maisha yao.

  Kamanda wakulya alisema jukumu la usalama lipo mikononi mwa jeshi hilo na wajibu wa polisi kutambua uwepo wa waandishi na umuhimu wao katika kila tukio ambapo alitoa rai kwa waandishi hao kuziona dalili za uvunjifu wa amani na kuanza kujiepusha mapema kabla ya madhara makubwa hayaja tokea.


  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Wageni wa meza kuu wakifurahia jambo wakati wa kuanza kwa fainali ya mashindano ya Habibu cup katika uwanja wa Cleopa Msuya wilayani Mwanga.
  Kikosi cha timu ya Kifaru kikipasha misuli joto.
  Kikosi cha timu ya Nyerere kikipasha misuli joto.
  Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Mashindano ya Habibu Cup ,Thabit Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Nyerere.
  Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali za Mashindano ya Habibu Cup ,Thabit Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Kifaru.
  Mgeni rasmi katika mchezo wa fainali kati ya timu za sekondari za Nyerere na sekondari ya Kifaru,Thabit Mndeme akizungumza kabla ya kuanza kwa mchezo wa fainali baina ya timu hizo mbili.
  Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Nyerere .
  Kikundi cha ushangiliaji cha timu ya Kifaru.
  Sehemu ya hekaheka katika mchezo huo wa fainali.
  Mchezaji wa timu ya Sekondari ya Kifaru akipiga penati iliyopelekea ushindi wa jumla ya bao 5 kwa 3 kwa timu ya Kifaru katika mchezoo wa fainali dhidi ya timu ya sekondari ya Nyerere .
  Baadhi ya mashabiki walijitokeza kushuhudia michezo ya fainali katika mashindano hayo.
  Mgeni rasmi Zuhura Mndeme akielekea katika uwanja wa mchezo wa Netiboli kwa ajili ya ufunguzi ya kuanzisha fainali ya mchezo huo kati ya timu ya Green Bird Collage na Sekondari ya Usangi Girls Day.
  Timu ya Netiboli ya Shule ya sekondari ya Usangi Girls Day
  Timu ya Green Bird Collage.
  Mgeni rasmi kwa upande wa mchezo wa Netiboli ,Zuhura Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Green Bird Collage.
  Mgeni rasmi kwa upande wa Netiboli,Zuhura Mndeme akisalimiana na wachezaji wa timu ya Sekondari ya Usangi Girls Day.
  Mwamuzi wa mchezo huo wa fainali akimkaribisha mgeni rasmi Zuhura Mndeme kufungua rasmi mchezo huo wa fainali.
  Mgeni Rasmi Zuhura Mndeme akirusha mpira kwenye mlingoti wa goli wakati wa ufunguzi rasmi wa mchezo wa faiali ya Netiboli.
  Mchezo wa fainali ukiendelea baina ya timu ya Green Bird Collage na Sekondari ya Usangi Girls Day mchezo uliomalizika kwa timu ya Green Bird kutangazwa malkia mpya wa mchezo huo baada ya kushinda kwa point 17 kwa 15 za Usangi Girls.
  Mshindi wa kwanza katika mbio za Habibu Marathon Km 21 Musa Hassan akipokelewa baada ya kuhitimisha mbio katika uwanja wa Cleopa Msuya wilayani Mwanga.
  Mshindi wa Pili katika Mbio za Habibu Marathon Peter Michael akihitimisha mbio hizo katika uwanja wa Cleopa Msuya.
  Washindi Sita bora katika mbio za Habibu Marathon 2017 wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mbio hizo.
  Mgeni rasmi katika mashindano ya Habibu Cup ,Thabit Mndeme akikabidhi kombe la ubingwa wa mashindano hayo kwa Nahodha wa timu ya soka ya Kifaru ,Zuber Zuber mara bada ya timu hiyo kujinyakulia ubingwa wa mashidano hayo kwa mara ya pili mfululizo.
  Wachezaji wa timu ya soka ya Kifaru wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la ubingwa.
  Mgeni rasmi katika mashindano ya kumbukumbu ya Habibu Mndeme ,Thabiti Mndeme akimkabidhi kikombe cha umalkia wa mchezo wa netiboli wa timu ya Green Bird Collage .
  Mgeni rasmi katika mashindano ya kumbukumbu ya Habibu Mndeme ,Thabiti Mndeme akimvisha medali mshindi wa kwanza wa mbio za Habibu Marathon Km 21 ,Musa Hassan.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

  0 0


   Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe  akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari mapema jana jijini Dar kuhusiana na zawadi mbalimbali zitakazotolewa katika Mashindano hayo,na pia vigezo vitakavyotumika katika ushiriki wake.
   Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. (kulia),ambao ndio wadhamini wa Mashindano hayo,akizungumza mbele ya Waandishi wa habari,mapema jana jijini Dar,naona ya kuyaboresha mashindano hayo ambayo yamekuwa yakiwavutia mashabiki wengi wa mchezo huo
  Pichani kushoto ni Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda akitoa ufafanuzi kuhusiana na mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.,mbele ya Waandishi wa habari mapema jana,ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kurindima ndani ya mwezi huu wa Mei na kufikia tamati mwezi Julai,mwaka huu.Pichani kati ni Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe na kulia ni Afisa Masoko wa Sprite-Tanzania,Pamela Lugenge. 

  ==== ==== ==== ========
  Kituo cha East Africa Television (EATV) na East Africa Radio kwa udhamini wa Kinywaji cha Sprite, kiimeandaa mashindano ya mpira wa kikapu yanayojulikana kama ‘Bball Kings’.

  Akizungumza na Waandishi wa habari mapema jana jijini Dar,Mwakilishi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),  Mwenze Kabinda alisema kuwa 
  yanatarajia kufanyika katika viwanja tofauti ndani ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia mwezi huu wa Mei na kufikia tamati mwezi Julai mwaka huu.

  Kabinda alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali za mpira wa kikapu kutoka pande mbalimbali za Tanzania.

  " Dhumuni kuu la mashindano haya ni kuutangaza na kuibua vipaji vipya katika mchezo wa kikapu hapa nchini.Mashindano haya yamepatiwa kibali kuendeshwa hapa nchini kwa kuzingatia sheria za Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania - Tanzania Basketball Federation (TBF),na kwamba mashindano haya yatakuwa na hatua kuu saba",alisema Mwenze Kabinda.

  Kabinda alizitaja hatua hizo saba kuwa ni :-1. Usahili,2. Warsha 3. Kufuzu,4. Kumi na sita bora,5. Robo fainali,6. Nusu fainali 7. Fainali

  Nae Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe alizitaja zawadi za mashindano hayo kuwa Mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia zawadi ya kitita cha shilingi milioni kumi (10 Milioni) pamoja na kombe la ubingwa wa Bball Kings kwa mwaka 2017. Mshindi wa pili atapata shilingi milioni tatu (3 Milioni). Mchezaji bora wa mashindano atapata shilingi milioni mbili (2 Milioni).

  Mbowe alivitaja vigezo vya kushiriki mashindano hayo kuwa ni;  Kwa mwaka huu wa mwanzo, mashindano haya yatajumuisha vijana wa kiume pekee,Watu wataruhusiwa kuunda timu zao za mtaani, kila kikosi kitaruhusiwa kuwa na wachezaji wasiozidi wa 3 kutoka timu za daraja la kwanza,Kwa timu shiriki isipungue wachezaji 10,Timu itaruhusiwa kuwa na -Mshiriki awe na umri usiopungua miaka 16,Mshiriki awe ni raia wa Tanzania.

  Katika hatua nyingine Meneja Mauzo na Masoko (EATV),Ronald Mbowe amewashukuru kwa dhati wadhamini wao Sprite kwa kuwaunga mkono mkono na kuonesha imani yao kwa kituo hicho cha EATV, pia kwa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kutoa kibali cha kuendesha mashindano hayo.

  0 0

  Mshindi wa Sh Milioni 10 wa Biko Tanzania kutoka jijini Mwanza Pildas Emmanuel kushoto akipeana mikono ya shukrani na Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven baada ya kumkabidhi fedha zake jijini Dar es Salaam kama sehemu ya ushindi wa Bahati Nasibu ya Biko inayoendelea nchini Tanzania na kugawa mamilioni kwa washindi wake.

  Mshindi wa Mwanza atua Dar kubeba mamilioni yake

  Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
  SHINDANO la mchezo bahati na nasibu la Biko Ijue Nguvu ya Buku, limemkabidhi mshindi wake wa wiki ya tatu ya Sh Milioni 10, ambaye ni Pildas Emmanuel, anayeishi jijini Mwanza baada ya kutangazwa mshindi wa wiki katika droo iliyochezeshwa Jumapili iliyopita.

  Makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika jijini Dar es Salaam sambamba na kumfungulia akaunti ya benki ya NMB kwa ajili ya kuingiza fedha hizo kwa mshindi huyo aliyejitambulisha kama mjasiriamali wa vileo jijini Mwanza Tanzania.

  Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyohudhuriwa na baadhi ya wataalam wa benki ya NMB kwa ajili ya kumpa elimu ya kifedha mshindi huyo, Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven, alisema sasa Biko limekolea na wameendelea kumwaga fedha kwa kila mshindi wao, akiwamo Emmanuel aliyeletwa kwa Ndege kwa ajili ya kumkabidhi fedha zake.
  Meneja Masoko wa Biko Tanzania, Goodhope Heaven kulia, akishuhudia jinsi mshindi wao wa Sh Milioni wa bahati nasibu ya Biko, Pildas Emmanuel anavyofurahia baada ya kumkabidhi fedha zake mapema wiki hii jijini Dar es Salaam. Na Mpiga Picha wetu.

  Alisema kila siku wamekuwa wakilipa zawadi za papo kwa papo kuanzia Sh 5000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh 1,000,000, pamoja na zawadi kubwa ya wiki ya Sh Milioni 10 kwa kila mshindi wao, huku wakiwa wameshalipa kiasi hicho kwa washindi wawili ambao ni Christopher Mgaya, Nicholaus Mlasu ambao wote wameshapokea fedha zao.

  “Biko limekolea na linaendelea kuwapatia utajiri wananchi wa Watanzania wanaothubutu kucheza Biko kwa kufanya miamala kwenye simu zao za Tigo, Vodacom na Airtel, ambao ni mchezo wa ujumbe mfupi wa maandishi kwa kuingiza namba ya kampuni ambayo ni 505050 na kumalizia namba ya kumbukumbu ambayo ni 2456, huku tiketi moja ikipatikana kwa sh 1000.
  “Na kila Sh 1000 itakayolipwa itakuwa na nafasi mbili ya ushindi wa papo kwa hapo pamoja na kuingia kwenye droo kubwa ya wiki ya kuwania Sh Milioni 10, huku mshiriki akiruhusiwa kucheza kuanzia Sh 1000 au zaidi ambapo kucheza mara nyingi zaidi ndio kujiweka katika nafasi nzuri ya ushindi,” Alisema Heaven na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko ili wavune mamilioni ya Biko.

  Naye Emmanuel alisema kwamba amefurahishwa na huduma zote alizopewa na Biko ikiwamo ya kumpa fedha zake katika benki ya NMB pamoja na kumleta jijini Dar es Salaam kwa ndege kutoka Mwanza jambo ambalo halijawahi kumtokea katika maisha yake.

  “Ingawa nimepata fedha nyingi ambazo sijawahi kuzishika tangu nizaliwe, pia nimeingia kwenye historia kwa sababu na mimi nimepanda ndege kwa mara kwanza huku fedha zote zikilipwa na Biko, hivyo ni kampuni nzuri na mchezo wao ni mzuri kutokana na malipo ya ushindi kulipwa haraka,” Alisema Emmanuel na kuwataka Watanzania waendelee kucheza Biko.

  Emmanuel aliwasili jijini Dar es Salaam Jumatatu akitokea jijini Mwanza ikiwa ni siku moja baada ya kutangazwa mshindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja katika droo iliyoshuhudiwa pia na Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Abdallah Hemed.

  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Kama biashara zingine, kuna msimu pia wateja hukauka mahotelini na wanakuwa ni wa kuhesabika tu. Kwa kawaida biashara ya hoteli huwa ni ya msimu yaani kipindi ambacho kunakuwa na sikukuu au mapumziko ndicho watu hufurika. Na hii ni kwa sababu kwamba wasafiri wengi huwa ni watalii ukilinganisha na wafanyabiashara.

  Kipindi hiki ndicho wamiliki/mameneja wa hoteli hutakiwa kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kuwa wanawavutia wateja. Zipo mbinu kadhaa ambazo Jumia Travel ingependa kukushirikisha hizi chache ili kukabiliana na kipindi hiko kikifika ukiwa umejiandaa:     

  Zitambue tabia za wateja wako. Kitu cha kwanza kabisa kukizingatia ni kujua tabia za wateja wanaopenda kutembelea hotelini kwako. Tumia taarifa ulizonazo kwenye kumbukumbu yako kuangalia wengi ni wa aina gani, vipindi wapendeleavyo kutembelea na huvutiwa na huduma zipi zaidi. Kwa mfano, meneja wa hoteli ya Kendwa Rocks anaweza kulitumia tukio la ‘Full Moon Party’ kujifunza hadhira inayofika pale na namna ya kuwavutia tena endapo tukio hilo halitokuwepo.      

  Buni na toa ofa maalum za kuvutia. Baada ya kutambua ni wateja wa aina gani hupenda kutembelea zaidi hoteli yako, unaweza kubuni ofa maalum kuwalenga wao. Kwa kawaida kuna watu wanapenda kwenda kupumzika hotelini kipindi wateja wanakuwa sio wengi sana kwa sababu ya utulivu na gharama kushuka. Kama meneja wa hoteli unaweza kuitumia fursa hii kubuni ofa zitakazowavutia wateja wa aina hii. Itumie orodha ya wateja ambao wanaipendelea hoteli yako mara kwa mara kuwajulisha juu ya ofa hizo. Kwa sababu huwezi kujua kama wasipokuja wao wanaweza kuzipendekeza kwa marafiki, ndugu na jamaa zao.

  Chunguza matukio yanayotarajia kutukia eneo ulilopo. Kipindi cha msimu ambao wateja sio wengi ni vema kutafiti shughuli ambazo zitawavutia watu kutembelea hotelini kwako. Unaweza kujua matukio yanayoendelea eneo ulilopo kupitia njia mbalimbali kama vile tovuti zinazoweka mtangazo nakadhalika. Ukishafahamu hayo jaribu kuwasiliana na waandaji ili ujue unaweza kushiriki kwa namna gani. Unaweza kushiriki kama washiriki wengine ili kuitangaza hoteli yako au kama mdhamini pengine hata kwa kutoa fursa kwa tukio hilo kufanyika hotelini kwako. Unaweza kuona kama ni gharama kufanya hivi lakini kuna faida nyingi kwani hoteli itajulikana kupitia matangazo, wahudhuriaji na pia huduma zako kutumika wakati wa tukio.
  Boresha mwonekano na taarifa kwenye tovuti ya hoteli. Lakini pia kipindi ambacho pilikapilika za wateja zinakuwa sio nyingi sana hotelini, unaweza kukitumia kwa kuboresha mwonekano na taarifa mbalimbali kwenye tovuti. Kwa mfano, huduma, picha, matukio na habari unazoona zinafaa kwa wateja wako kuzifahamu.

  Tumia fursa ya wateja wanaoependa kutembelea hotelini kwako. Kama ulikuwa haufahamu wateja wanaweza kutumika kama njia mojawapo ya kujitangaza na kuvutia wengine wapya. Mara nyingi watu huamini na kushawishika kiurahisi kutokana na maneno wanayoambiwa na watu wao wa karibu. Kwa kutumia orodha uliyonayo unaweza kuwaomba kuwataarifu wenzao na kisha kuwapatia ofa hotelini kwako kama chachu.

  Tumia barua pepe kuwafikia wateja wako. Makampuni mbalimbali hutumia mbinu hii pia ambapo huwa na kumbukumbu ya anuani za wateja wao. Nadhani hata wewe utakuwa ushawahi kupokea jumbe za namna hiyo zikikutaka kutumia huduma fulani. Kwa hiyo baada ya kuandaa ofa zako kadhaa unaweza kuzituma kwa wale wateja ambao unajua huwa wanakuja hotelini kwako mara kwa mara.

  Tumia mitandao ya kijamii kuongeza hamasa ya ofa na kampeni zako. Kwa sasa, hakuna njia rahisi na ya haraka zaidi inayowafikia na kuwaunganisha wateja wengi na makampuni kama mitandao ya kijamii. Hakikisha unaitumia vema mitandao hiyo kujenga na kueneza hamasa kwa kile unachotaka kukifanikisha. Watu wengi siku hizi wanatumia zaidi mitandao hiyo kwa kuwasiliana pamoja na kupata taarifa mbalimbali.

  Zipo njia tofauti ambazo mahoteli huzitumia katika kukabiliana na kipindi hiki ikiwemo kukitumia kufanya maboresho. Kikubwa ni kutokukubalina na hali ya kwamba msimu huu huwa hakuna wateja au kushusha gharama ili kuwavutia wengi zaidi. Mbinu hizo hapo juu zilizoorodheshwa na Jumia Travel endapo zikizitumika ipasavyo basi hutoona tofauti ya misimu ya wateja kufurika hotelini kwako.

  0 0  0 0

  TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (second left) exchanges partnership agreement with SUA’s Principal of College of Agriculture, Prof. Susan Nchimbi-Msolla. Witnessing are TADB’s Head of Legal Services, Neema-Christina John (Left) and SUA’s Deputy Principal of College of Agriculture, Prof. Benard Chove (right). The eve took place at TADB’s premises in Dar es Salaam.
  TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (second left) and SUA’s Principal of College of Agriculture, Prof. Susan Nchimbi-Msolla display their exchanges partnership agreement. The agreement that aims at facilitating collaboration in the development and implementation of capacity building programs for smallholder farmers, medium and large scale farmers and agro-processors in Tanzania and SUA Graduates for practical training and employment at TADB and its partner institutions.Witnessing are TADB’s Head of Legal Services, Neema-Christina John (Left) and SUA’s Deputy Principal of College of Agriculture, Prof. Benard Chove. The eve took place at TADB’s premises in Dar es Salaam.
  TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (second left) and SUA’s Principal of College of Agriculture, Prof. Susan Nchimbi-Msolla display their exchanges partnership agreement. The agreement that aims at facilitating collaboration in the development and implementation of capacity building programs for smallholder farmers, medium and large scale farmers and agro-processors in Tanzania and SUA Graduates for practical training and employment at TADB and its partner institutions. Others in the photo are management members of TADB and SUA’s Deputy Principal of College of Agriculture, Prof. Benard Chove (right). The eve took place at TADB’s premises in Dar es Salaam.
  TADB’s Acting Managing Director, Mr. Francis Assenga (centre) chairs an agreement meeting on research and development cooperation when SUA’s Principal of College of Agriculture, Prof. Susan Nchimbi-Msolla (second right) and her assistant Prof. Benard Chove (right) paid a visit at TADB premises. Looking on are some of TADB’s management members.


  0 0


   
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
   Wajumbe  wa Mkutano wakimsikiliza kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Makandarasi Mhandisi Consolata Ngimbwa akihutubia wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,Viongozi wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi  na Wajumbe waliohudhuria mkutano wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 nje ya  ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Wakandarasi Wanawake mara baada ya kufungua Mkutano wa siku mbili wa Mashauriano Wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi kwa Mwaka 2017 kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kikwete mkoani Dodoma.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameagiza kuwa miradi yote yenye thamani isiyozidi bilioni 10 wapewe Wakandarasi wa ndani hasa kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za ndani kwani wakandarasi hao watasaidia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania na kuongeza uwekezaji ndani ya nchi.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini DODOMA wakati anafungua mkutano wa siku Mbili wa mashauriano wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi mwa mwaka 2017.

  Makamu wa Rais amesisitiza wakandarasi hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili na sheria pamoja na kumaliza kazi wanazopewa ndani ya muda uliopangwa kwa kuzingatia ubora wa kazi na gharama zilizokubalika kwenye mikataba na sio vinginenevyo.

  Makamu wa Rais amewataka wakandarasi kote nchini kuacha mara moja tabia ya kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wanayopewa.

  Amesema kuwa Serikali itaendelea kuwapa kipaumbele wakandarasi wazawa ili wathubuti kujitosa na kumudu zabuni za ujenzi kwani kwa kufanya hivyo kutaleta faida mbalimbali ikiwemo fedha watakazopata watawekeza ndani ya nchi na kutoa ajira za kutosha kwa vijana wa Kitanzania.

  “Hatuwezi kuwa na Tanzania ya Viwanda huku tukiwanufaisha Makandarasi wa nje pekee ni lazima Makandarasi wa ndani wanufaike pia.”

  Kuhusu madeni ya wakandarasi, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakandarasi kuwa Serikali haijawasahau na bajeti ya Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano ambayo imepitishwa na bunge imezingatia kilio hicho cha wakandarasi.

  Ameahidi kuwa Serikali itaendelea kulipa madeni inayodaiwa na wakandarasi ili kujenga mahusiano mazuri ya wakandarasi hao.

  Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesisitiza kuwa Wizara hiyo inaendelea kusimamia sheria na maadili kwa wakandarasi ili kuhakikisha miradi ya ujenzi inayotekelezwa kote inakuwa na ubora unaotakiwa.

  Waziri Profesa Mbarawa amekiri kuwa kuna baadhi ya wakandasiri ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo hivyo kujenga miradi jinsi ya kiwango hivyo ni muhimu kwa wakandarasi hao kufanya kazi kwa ubora ili waweze kuaminiwa na Serikali na kupewa kazi.

  Amesema kuwa Wizara yake itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwajengea uwezo wakandarasi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa viwango vinavyotakiwa.

  Naye, Msajili wa Bodi ya Wakandarasi Nchini Rhoben Nkori amesema bodi hiyo imefuta usajili wa wakandarasi 3,000 kwa kushindwa kutimiza matakwa ya Usajili wa Wakandarasi ya mwaka 1997 na kwa sasa bodi hiyo inawakandarasi 9,000 kote nchini.

  Msajili huyo pia amesema kuwa katika kuratibu mwenendo wa kazi za makandarasi bodi hiyo ilikagua miradi 3,813 ambapo kati ya miradi hiyo miradi 2714 sawa na asilimia 71.2 haikuwa na kasoro na miradi mingine ilikuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo miradi hiyo kutofanywa na wakandarasi waliosajiliwa na kutozingatia usalama wa wafanyakazi.

  Kasoro nyingine ni wakandarasi kufanya kazi zaidi ya viwango vya madaraja yao,miradi kutosajiliwa na miradi kutokuwa na bango.

  Imetolewa na

  Ofisi ya Makamu wa Rais

  IKULU- DODOMA. 4-May-2017.

  0 0

   
  Kampuni ya Coco- Cola Kwanza kupitia Maji ya Dasani imedhamini mashindano ya riadha marathon ‘Dasani Marathon’ itakayofanyika Mei 14 jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca –Cola Kwanza , Nalaka Hattiachchi , amesema kampuni imedhamini mbio hizo ili kuweza kuchochea riadhaa nchini.

  Amesema kuwa wanariadhaa wanaotakiwa kushiriki mbio za Kilomita 10 na 21 na tayari usajili umeanza kufanyika kwa kuwa washiriki 1000.
  Rais wa Dar Running Club, Goodluck Elvis amesema mbio hizo zilianza miaka mitatu iliyopita na zimeendelea kwa kuibua wanariadha wengi ambao baadaye wanaweza kuleta historia ya nchi kama ilivyokuwa.

  Mshindi wa Dasani Maradho wa kwanza atapata sh. Milioni mbili na wa pili atapata sh.700000 na zawadi mbalimbali zitatolewa na washiriki wanatakiwa kujisajili kwa sh.30000 kulipa kwa M-pesa 243388.
  Vituo vya kujiandikisha Colosseum Gym, Masaki,Shoppers Supermarket , Mikocheni na Mlimani City.

  Mwanariadha Mkongwe Juma Ikangaa amesema kuwa watu wakiwa tayari kwa kujitoa katika kushiriki riadhaa wanaweza kuwa na rekodi katika dunia.Amesema kinachotakiwa katika ushiriki ni kujiandaa na kuwa na tamaa ya kupata ushindi bila kufanya hivyo riadha itakuwa jina kwa Tanzania.
  Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Coca Cola Kwanza , Nalaka Hattiachchi akizungumza na waandishi habari juu ya udhamini kampuni hiyo katika Dasani maradhoni, kushoto ni Rais Dar Running Club , Goodluck Elvis Kulia Mwanariadha Mkongwe , Jumaa Ikangaa.
   
   

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akizungumza katika uzinduzi wa mpango wa mafunzo kwa vitendo kutoka Kwa Chama Cha Waajiri nchini ATE kwa kushulikiana na Shirika la Kazi Duniani ILO leojijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akionyesha Vitabu vya programu vya mafunzo kwa vitendo mara baada ya kuzindua programu hiyo katika ukumbi wa Hyatt Kempiski leo Jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akikata utepe kuashiria uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa vitendo kutoka kwa Chama cha Waajiri nchini ATE, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa ATE nchini , Almas Maige(MB) akishuhudia uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Shirika la kazi Duniani (ILO) ukanda wa Afrika Mashariki ,Dk Mary Kawar akizungumza wakati wa ufunguzi proamu hiyo
  Katibu Mtendaji wa ATE ,DK.Aggrey Mlimuka akizungumza katika mkutano wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Chama Cha Waajiri nchini (ATE), Almas Maige(MB) akichangia jambo katika mkutano huo uliowashirikisha wadau mbalimbali iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mstaafu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),Mhandisi Zebadiah Moshi akichangia jambo katika mkutano huo uzinduzi wa program ya vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Bridge for Change, Ocheck Msuva akichangia maada katika uzinduzi ya programu ya mafunzo kwa vitendo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
  Kiongozi wa Asasi ya kuhamasishaVijana ya Tanzania Zalendo ,Victoria Mwanziva akichangia jambo juu ya umuhimu wa vijana kujifunza kwa vitendo pindi wanapokuwa mashuleni

  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Anthony Mavunde akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa uzinduzi wa programu ya mafunzo kwa Vitendo kwa Vijana
  Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii


  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema Vijana zaidi ya Milioni Nne nchini watafikiwa na programu ya mafunzo kwa Vitendo ili waweze kuhimili ushindani pindi wanapohitimu vyuo.

  Mavunde amesema hayo leo alipokuwa akizindua programu ya mafunzo kwa vitendo iliyoandaliwa na Chama cha Waajiri nchini (ATE) kwa kushirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO) Kanda ya Afrika Mashariki.

  “Kwenye program hii ya miaka mitano tunakwenda kuwafikia vijana Milioni Nne nchini ambapo katika mwaka huu wa fedha 2017/2018 vijana 27,000 watapewa mafunzo kwa vitendo” amesema Mavunde.

  Waziri Mavunde amewashukuru ATE kwa kuungana na serikali katika kusaidia vijana wa kitanzania kuingia katika mpango huo ambao unaondoa pingamizi la kuwataka vijana kuwa na uzoefu hili waajiriwe katika taasisi mbalimbali.

  Kwa Upande wake Mwenyekiti wa ATE , Almas Maige amesema mpango huo utawasaidia waajiri kupata wafanyakazi ambao wataweza kuwasaidia kwa uzalishaji bila ya kuchukua muda mrefu kujifunza.

  0 0


    Ndugu Catherine Nyakao Ruge 


  KUHUSU UTEUZI WA CATHERINE NYAKAO RUGE KUWA MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA
  CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO

  Kwa mujibu wa Ibara ya 78(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika kikao chake cha tarehe 04 Mei, 2017 imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalum katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Dkt. Elly Marco Macha. 

  Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemteua Ndugu Catherine Nyakao Ruge baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa mujibu wa Kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343, alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwepo nafasi wazi ya Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Dkt. Elly Marko Macha kufariki dunia na hivyo kuwepo nafasi wazi. 

  Imetolewa leo tarehe 04 Mei, 2017 na:- 

  Kailima, R.K 

  MKURUGENZI WA UCHAGUZI

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

  Serikali imesema kuwa haina mpango wowote wa kusitisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kusisitiza kuwa dhana hii ni endelevu na itaendelea kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa kusisitiza misingi hii bila kuchoka.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi , Vijana , Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakati akijibu hoja mbalimbali  Mjini Dodoma.

  “Kutokana na faida na Mafanikio makubwa yanayopatikana kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru Serikali inaamini kuwa zipo faida nyingi ndani yake na mwenge huu utaendelea kudumu”,Alisisitiza Mhe.Muhagama.

  Amesema kuwa Kimataifa Mwenge wa Uhuru umeendelea kusimamia dhana na maudhui yake ya kumulika hata nje ya mipaka yetu kwa kuwa msuluhishi wa Amani Afrika na mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kote.

  Aidha amesisitiza kuwa Umoja ,Mshikamano ,Upendo na Ukarimu wa Watanzania  ni matunda ya Mwenge wa Uhuru.

  Mhe.Muhagama ametoa takwimu ambazo zinaonyesha kuwa Miradi ya Maendeleo iliyozinduliwa pamoja na kuwekewa mawe ya msingi kupitia Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2015 ni miradi 1342 yenye thamani ya bilioni 463,519,966,467.

  Pamoja na hayo amezitaja faida za Mwenge wa Uhuru kuwa ni kuendelea kuamasisha ari ya wananchi kujitegemea na kuwekeza katika maeneo mbalimbali katika Taifa letu,pia kimekuwa ni chombo pekee cha kujenga umoja na mshikamano na kudumisha amani pale unapopita bila kujihusisha na itikadi za kisiasa.

  Aidha Mwenge wa Uhuru umeendelea kuhamasisha na kuimarisha umuhimu wa Muungano kwa Watanzania wa pande mbili za nchi yetu na kila mwaka huweka mawe ya msingi kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi na kuhamasisha uzalendo wa kuendelea kujitolea.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ina mkakati wa kufanya yote nchini yawe na barabara za viwango vya kimataifa na zinazopitika kwa urahisi.

  “Tumeanza kujenga barabara za kisasa katika jiji la Arusha ambalo ni jiji la utalii, tutakwenda Mwanza na Dar es Salaam kwa kujenga barabara zenue njia za juu (flyovers) zikiwemo za magari na za waenda kwa miguu,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Alhamisi, Mei 4, 2017) wakati akizumngumza na wananchi wa Tengeru, wilayani Arumeru, mkoani Arusha mara baada ya kukagua barabara ya Sakina-Tengeru yenye urefu wa km. 14.1 ambayo itakuwa na njia nne za magari.

  “Nimekuja kukagua ujenzi wa barabara hii ya Sakina hadi Tengeru lakini mkandarasi akimaliza anajenga barabara nyingine ya kilometa 42.1 na hivyo hapa Arusha tutakuwa na kilometa 56.5 za awamu ya kwanza,” alisema.

  Alisema maboresho ya barabara za Jiji la Arusha yanafanyika ili kuwezesha wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao kwa urahisi na viwanda vitakapoanza kujengwa, itakuwa hawana shida ya mawasiliano.

  Akizungumzia tatizo la uhaba wa ardhi aambalo lililibuliwa na mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw, Mrisho Gambo aendelee na zoezi la kuuzungukia mkoa wake ili kubaini maeneo yenye matatizo sugu.

  Mapema, akitoa taarifa ya ujenzi wa barabara hiyo kwa Waziri Mkuu, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Arusha, Eng. Mgeni Mwanga alisema ujenzi wa barabara hiyo ambao ulianza Juni 2015, unatarajia kukamilika Juni 2018.

  “Ujenzi wa barara ya Sakina –Tengeru ni wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa km. 230 ya kutoka Arusha –Holili- Taveta –Voi ambayo ujenzi wake unatarajiwa kugharimu sh. bilioni 139.34. Ujenzi huo unagharimiwa na Serikali ya Tanzania pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

  Sambamba na barabara hiyo, Eng. Mwanga alisema mkandarasi wa barabara hiyo ataanza kujenga barabara nyingine ya km. 42.1 inayoanzaia Usa River hadi Kisongo kwa kiwango cha lami ambayo itakuwa na madaraja saba wakati ile ya Sakina hadi Tengeru ina madaraja makubwa mawili.

  Naye mbunge wa Arumeru Mashariki, Bw. Joshua Nassari alisems uhaba wa ardhi bado ni tatizo kubwa kwenye wilaya hiyo kiasi kwamba hawana hata eneo la kujenga shule au zahanati.

  “Maeneo yote yameuzwa na wenyeviti wa vijiji na madiwani, hivi sasa ukitaka kujenga shule au zahanati hakuna eneo hata moja. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utusaidie kufuatilia suala hilo licha ya kuwa Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi alishakuja na kuelezwa hali halisi ilivyo,” alisema.

  0 0

   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akiwasili katika ukumbi wa Ledger Hotel Jijini Dar es Salaam kufungua Kongamano la Kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii .
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akizungumza wakati wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii  lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Pharm Access Dkt. Heri Marwa akizungumzia uhuhimu wa Sekta binafsi kushirikiana na Serikali katika kuboresha huduma za Afya hasa kwa wananchi wasio na uwezo.
   Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware akizungumza wakati wa kongamano hilo kuhusu umuhimu wa kuwa na Sera ya Bima hapa nchini ili kuwalinda wananchi .
   Mkurugenzi wa  kuendeleza miradi, Pharm  Access, Ewout  Irrgng akizungumza wakati wa akizungumza wakati wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii  lililofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
   Spika Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF)Mhe.  Anna Makinda akifurahia jambo na Mkurugenzi msaidizi anayeshughulikia Afya toka Ofisi ya Rais-TAMISEMI Dkt. Anna Nswilla kabla ya ufunguzi wa kongamano la  kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii
   Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Afya ya Jamii Slvery Mgonza akiwasilisha mada katika kongamano la kwanza la Bima ya Afya na Kinga ya Jamii, lililofanyika Kunduchi katika hoteli ya Ledger plaza Bahari Beach leo jijini Dar es Salaam.​​​​ 
  Frank Mvungi-Maelezo
  Serikali  ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa kuimarisha na kuendeleza miundo mbinu ya Afya,uboreshaji huduma kupitia teknolojia  na Usambazaji wa madawa  hadi kwenye vituo vya kutolea huduma.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar  es Salaam na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Bi Anna Makinda wakati akifungua Kongomano  la kwanza la bima ya afya na kinga ya jamii .

  “’Lazima tuangalie na kuwatambua wale ambao hawawezi kulipia huduma za afya na tuangalie namna gani tutahakikisha wanapata huduma na isitokee wakati wowote wengine wakpoteza maisha kwa kukosa fedha za kujiunga na Bima ya Afya.’’ Alisisitiza Makinda.

  Akifafanua Makinda amesema kuwa kuna umuhimu wa kuangalia namna huduma zinavyotolewa katika vituo vya kutolea huduma,upataikanaji wa vifaa tiba na dawa,hali inayochochea upatikanaji wa huduma bora kwakuwa ndiyo dhamira ya Serikali kupitia mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.

  Kuhusu Afya bora kwa wote Makinda alibainisha kuwa azma hiyo itafikiwa kupitia utaratibu wa Bima ya Afya na na mpango wa CHF iliyoboreshwa katika Halmashauri 50 hapa nchini.

  Akizungumzia mkakati wa kutoa huduma bora Makinda amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umejipanga kuhakikisha kuwa huduma zinazotolewa na watoa huduma zinaendana na dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma bora za afya .

  Aliongeza kuwa watoa huduma watakao toa lugha zisizofaa kwa wagonjwa,kuwanyanyapaa, kuonyesha tabia ya ukatili watafungiwa kutoa huduma kama kituo hicho kimesajiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  Kwa Upande wake Kamishna wa Mamlaka ya Udhibiti wa Bima nchini Dkt.Baghayo Saqware  amesema kuwa kuna umuhimu wa kuwa na Sera ya Taifa ya Bima itakayowezesha wananchi huduma bora za Afya.

  “Sera ya Taifa ya Bima tasaidiakuondoa tatizo la watoa huduma za Bima wasio waaminifu “ alisisitiza Dkt.Saqware.Tanzania kama nchi imekuwa na historia ndefu ya kutoa huduma bora za matibabu kupitia bima ya Afya, Kuanzishwa kwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF)Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na Bima Binafsi zikiwa ni juhudi za kuboresha huduma hizo hapa nchini.

  Kongamano la Bima ya Afya na Kinga limeandaliwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Bima Nchini (TIRA) na shirika la Pharm Access International.

older | 1 | .... | 1219 | 1220 | (Page 1221) | 1222 | 1223 | .... | 1897 | newer