Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1220 | 1221 | (Page 1222) | 1223 | 1224 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Brass band ya Chipikizi ikiongoza maandamano ya wakunga na wauguzi kupita mbele ya mgeni rasmi Waziri Afya Mhmoud Thabit Kombo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar. 
    Mama Mariyam Othmani Mihale akiongoza wakunga na wauguzi katika wimbo maalum wa maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani katika ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
   Mwenyekiti wa Baraza la Wuguzi na Wakunga Zanzibar Amina Abdulkadir Ali akitoa maelezo juu ya siku ya Wuguzi duniani katika maadhimisho yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo.
   Mwakilishi wa Shirika linaloshughulikia  Idadi ya watu duniani (UNFPA) Zanzibar  Sabina Luoga akizungumza na washiriki wa maadhimisho hayo katika Ukumbi wa wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar.
   Waziri wa Afya Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na wakunga na wauguzi walioshiriki maadhimisho ya siku ya wakunga duniani yaliyofanyika ukumbi wa wasanii Rahaleo Mjini Zanzibar.
  Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi Waziri wa Afya Zanzibar na viongozi wa Baraza la Wauguzi na Wakunga na Jumuiya ya Wauguzi Zanzibar katika maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani yaliyofanyika Rahaleo Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar
  Hospitali na Vituo vya Afya vya Wilaya vinaweza kupunguza idadi ya akinamama kujifungulia Hospitali kuu ya Mnazimmoja iwapo juhudi za kuandaa mazingira mazuri zitachukuliwa na wakunga na wauguzi  wa vituo hivyo.

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo ameeleza hayo katika maadhimisho ya siku ya wakunga Duniani yaliyofanyika Ukumbi wa Wasanii Rahaleo.
  Amesema akinamama  wengi wamejenga imani ya kujifungua  Hospitali kuu ya Mnazimmoja na kupelekea upungufu wa nafasi katika Hospitali hiyo huku vituo vya Afya vijijini vikiwa na akina mama  wacheche wanaokwenda kwa huduma ya kuzaa.

  Ameongeza kuwa Hospitali ya Mnazimmoja inazalisha zaidi ya akinamama 50 kwa siku na Mwembeladu wanawake 30 wengi wao kutoka vijijini wakati vituo vya afya vya huko vinazallisha wanawake wawili hadi watano kwa siku.
  Waziri Mahmoud amewataka wakunga na wauguzi wa vituo vya afya vya Wilaya vinavyotoa huduma ya kuzalisha  kuandaa mazingira yatakayowavutia wanawake kujifungua katika vituo vyao.

  Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea na mkakati wa kuandaa mazingira mazuri na kuweka miundo mbinu bora  ikiwemo vifaa vya kisasa hivyo amewataka wafanyakazi nao kubadilika na kuwapa faraja wagonjwa ili wajenge imani kwao.

  Amesema Serikali imetoa kibali cha kuajiri wafanyakazi wa sekta ya afya 201 kuanzia fani ya ukunga mpaka madaktari bingwa ili kuondosha upungufu wa wafanyakazi wa kada hizo katika Hospitali na vituo vya afya.
  Amewataka wakunga na wauguzi kujenga moyo wa upendo, huruma na kuweka mbele maadili ya kazi na kuwahudumia wagonjwa bila ya kuwabagua kwa rangi, kabila ama nyadhifa zao na kutumia lugha nzuri.

  Aidha amewashauri kutumia fursa walizonazo  kujiendeleza kitaaluma kwa vile nafasi zipo katika vyuo vya ndani na nje ya nchi na Wizara iko tayari kuwasaidia.

  Mwenyekiti wa Baraza la Wakunga na Wauguzi Zanzibar (ZNMC)  Amina Abdulkadir Ali amesema lengo kubwa la siku ya wauguzi Duniani ni kutoa mwamko kwa wananchi juu ya mchango wa wakunga katika jamii na kuwa pamoja nao.

  Katika risala iliyosomwa na Mwenyekiti wa Jumuia  ya Wakunga Zanzibar (ZANA) Valeria Rashid Haroub wameeleza changamoto zinazowakabili ikiwemo uhaba wa vitendea kazi wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua na uhaba wa madaktari bingwa katika kiliniki hizo.

  Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ‘Wakunga, Akinama na Familia ni washirika wa kudumu’. Ukiwa na maana ya kufanyakazi kwa karibu na familia, sio mama peke yake katika kutunza familia pamoja na kuwalinda watoto katika afya bora na kuwaepusha katika vitendo vya ukatili.                                                                       

  0 0

   Mwenyekiti wa  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge  akiongoza kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Naibu Waziri  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  akiwasilisha randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI Mhe.Selemani  Jafo akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Naibu Waziri  Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura  na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia wakifatilia hoja mbalimbali  katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
    Wabunge wa CCM wakijadili  jambo katika  kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Waziri wa Sera,Bunge,Kazi ,Vijana ,Ajira na wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama wakizungumza jambo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe.Peter Msigwa  katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.
   Mbunge wa Konde,Khatib Said Haji(CUF) akiuliza swali katika kikao cha kumi na Saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 4, 2017.

  Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO, DODOMA

  0 0

  Wanafunzi wa Shule wa Sekondari ya Arusha wakimsikiliza Mkufunzi kutoka  Taasisi ya  Gemological Insitute of America (GIA) , Elizabeth  Bokaba (hayupo pichani). Wanafunzi hao wamepata mafunzo kuhusu mafunzo ya Jimolojia.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakifuatilia mafunzo kwa vitendo kuhusu elimu ya madini ya vito yanayopatikana chini, wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.
  Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC), Eric Mpesa akiwaeleza jambo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakati wa mafunzo ya Jemolojia yaliyotolewa na Taasisi ya GIA wakati wa Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito Arusha yanayoendelea jijini Arusha.
  Mkufunzi kutoka Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA), Elizabeth  Bokaba, akiwafundisha elimu ya Jemolojia wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Arusha wakiangalia madini ya Tanzanite katika Banda la Kampuni Gliters Gems Limited  wakati walipotembelea mabanda ya maonesho baada ya kupata mafunzo ya Jemolojia.
  Mfanyabiashara wa Madini wa Kampuni ya Abdulhakim Mulla akiwaonesha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Madini ya Tanzanite. Mulla alitumia nafasi hiyo kuwafundisha tofauti ya madini yaliyonakishiwa na ambayo bado hayajakatwa.

  Na Asteria Muhozya, Arusha.

   Jumla ya Wanafunzi 55 kutoka  Shule za Sekondari za Arusha Day, Arusha Sekondari na Wining Sprit wenye  umri kati ya miaka 12- 15 wamepatiwa mafunzo ya Jemolojia katika Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Madini ya Vito yanayoendelea jijini Arusha.

  Mafunzo hayo yanayojulikana kama GemKids yametolewa na  Wakufunzi kutoka  Taasisi ya Gemological Institute of America (GIA) na kuratibiwa na Kituo cha Jimolojia  Tanzania  Cha Arusha, (TGC).

  Akizungumzia umuhimu wa mafunzo hayo, Mratibu wa TGC,  Erick Mpesa amesema kuwa, mafunzo hayo  ya Jemolojia, yanalenga kuwapa ufahamu wanafunzi ili kuwa na uelewa wa madini ya vito, kujua matumizi yake, kuyatumia na baadaye kuwawezesha  kuingia katika biashara ya madini huku wakiwa na uelewa mzuri na rasilimali hizo ambazo zinapatikana katika maeneo mbalimbali nchini.

  Akizungumzia mahusiano ya TGC na Taasisi ya GIA, Mpesa amesema kuwa, TGC imelenga kuendeleza ushirikiano na Taasisi hiyo kwa siku za baadaye hususani katika masuala ya utafiti na mafunzo na kuongeza kuwa, uhusiano uliopo baina ya taasisi hizo, umewezesha baadhi ya watumishi wa kituo hicho kupata mafunzo katika taasisi hiyo.

  Kuhusu mpango wa TGC kutoa mafunzo  kwa Watanzania, alisema kuwa, tayari kupitia Maonesho ya Vito ya Arusha, kituo hicho kuanzia mwaka 2014 kimetoa mafunzo ya ukataji na unga'rishaji wa madini ya vito kwa  jumla wanawake 47 na kueleza kuwa,  hivi sasa jumla ya wanawake 18 wanaendelea na mafunzo hayo na wanatarajiwa kuhitimu ifikapo tarehe 19 ya mwezi huu.

  "Kutokana na changamoto ya ajira wahitimu wetu tunawashauri kujiunga katika vikundi ili kuwawezesha kupata ruzuku pale zinapotolewa na Serikali. Hii inawezesha rasilimali inayotumika kuwafundisha kuwawezesha vijana hawa isipotee bure. Lengo letu ni kuwawezesha waweze kujiajiri na kuajiriwa," alisisitiza Mpesa.

  Maonesho ya 6 ya Kimataifa ya Vito ya Arusha yalianza  rasmi tarehe 3 Mei na yanataajiwa kufungwa tarehe 5 Mei,2017.

  0 0

  Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi ametembelea Ubalozi wa Tanzania Nairobi Kenya na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania Nchini Kenya Mheshimiwa Balozi Mteule Dkt. Pindi Hazara Chana.

  Prof. Kabudi alifanya ziara hiyo tarehe 4/5/2017 wakati akihudhuria Mkutano wa 56 wa Mwaka wa Jumuiya ya Mashauriano ya Masuala ya Kisheria ya Nchi za Asia na Afrika (Asian-African Legal Consultative Organisation –AALCO) unaofanyika mjini Nairobi.

  Katika ziara hiyo Prof. Kabudi aliongozana na Mheshimiwa Balozi Baraka Luvanda Balozi Mteule wa Tanzania Nchini India yalipo makao makuu ya Jumuiya hiyo na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje.

  Prof. Kabudi alimpongeza Balozi Pindi Chana kwa uteuzi na alishukuru kwa maandalizi waliyoyafanya kuhakikisha ujumbe wa Tanzania unashiriki ipasavyo mkutano huo. Vile vile alimuhakikishia kuwa Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na taasisi zake zitampa ushirikiano stahiki katika utekelezaji wa majukumu yake, na kwamba Ubalozi uwe tayari kwa kufuata taratibu zilizopo kiserikali kuwasiliana na Wizara pindi yanapoibuka masuala yanayohitaji ushiriki wa Wizara.

  Kwa upande wake Balozi Dkt. Pindi Chana alimshukuru Prof. Kabudi kwa kutenga muda kuja kuutembelea Ubalozi na kumpongeza kwa uteuzi alioupata. Balozi Chana alimuahidi Prof. Kabudi kuwa Ubalozi utaendelea kushirikiana ipasavyo na Wizara kwa kutumia taratibu zilizopo utahakikisha kuwa masuala ya Wizara yanaifikia Wizara kwa wakati. 
  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, kushoto akifurahia jambo katika Sikukuu ya Muungano wa Tanzania iliyoadhimishwa nchini humo kwa kukutanisha Watanzania wanaoishi Saudi Arabia, wazawa na viongozi mbalimbali kama sehemu ya kuitangaza vyema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.

  Na Mwandishi Maalum, Riyadh Saud Arabia

  SHEREHE za Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, zimetumika kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania katika tukio maalum lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wan chi hiyo.

  Akizungumza hivi karibuni katika sherehe hizo za Sikukuu ya Muungano wa Tanzania, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza, alisema kwamba Tanzania ni eneo zuri la uwekezaji kutokana na sera zake nzuri pamoja na dhamira njema za viongozi chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli kwa Tanzania Bara pamoja na Dr Ali Mohamed Shein kwa upande wa Visiwani Zanzibar.
  Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, H.E Hemed Mgaza wa nane kutoka kushoto mstari wa mbele akiwa na wageni mbalimbali katika maadhimisho ya Sikukuu ya Muungano nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kusherehekea pamoja katika siku hiyo muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Picha kwa Hisani ya Ubalozi wa Tanzania Saudi Arabia.
  Balozi Mgaza akiwa na mgeni rasmi Prince Muhammad bin abdullahman wakikata keki ya sherehe.
  Balozi Mgaza kushoto akikata keki
  Balozi Mgaza akihutubia katika hafla hiyo

  Alisema kutokana na sera hizo pamoja na kusimamia vyema rasilimali za utalii kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga mbalimbali za wanyama ni sehemu thabiti ya utalii kwa wageni, wakiwamo wananchi wa Saudi Arabia.

  “Nchi yetu ina mbuga za wanyama 16 ambazo zimekuwa zikitunzwa na kuhifadhiwa vema kama sehemu ya kuhakikisha kwamba rasimali hiyo inakuza uchumi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  “Nchi yetu ina wakaribisha wote kutembelea kujionea mambo mbalimbali yanayovutia katika utalii pamoja na kuwekeza katika sekta muhimu zikiwamo za viwanda ambazo ndio agenda kuu kwa sasa nchini mwetu,” Alisema Balozi Mgaza.

  Sikukuu ya Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeadhimishwa wiki iliyopita Aprili 26 ambayo hutumiwa kama kioo cha kuangalia matunda yanayojitokeza kutokana na Muungano huo kati ya Tanzania Bara na Visiwani.

  0 0


  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Joelson Mpina anakumbuka siku yake ya kuzaliwa Leo.Mungu akupe  azidi kuku Afya njema na Maisha Marefu.

  0 0

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa maelekezo kwa Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), wakati alipokagua mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na kulia ni Meneja wa Uwanja huo Julius Mlungwana.
  Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), akionesha Taa za Kisasa za Umeme Jua (hazipo pichani), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), zilizofungwa kwa ajili ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akionesha kifaa (Remote Controller) cha kuwashia Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa waandishi wa habari, wakati akikagua Taa hizo uwanjani hapo.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (katikati), na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Leonard Chimagu (kushoto), wakati alipokagua mfumo wa kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
  Muonekano wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Taa hizo zitatumika kuongozea ndege nyakati za Usiku na zina uwezo wa kuwaka masaa laki moja.

  Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi wa kufunga Taa za kuongozea ndege ili kuruhusu Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuweza kutumika masaa 24. Akizungumza hayo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa uboreshaji wa uwanja huo katika kuruhusu ndege za aina zote kutua masaa 24 kwa wiki.

  “Hii ni hatua ya pili ya uboreshaji wa uwanja huu ambapo hatua ya kwanza tumeimaliza ya upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege (runway) hadi kufikia KM 2.5”, amesema Waziri Profesa Mbarawa. Aidha, ameongeza kuwa ufungaji wa taa hizo umegawanywa kwa hatua tatu ambapo awamu ya kwanza imekamilika kwa kujumuisha ufungaji wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), katika barabara za kuruka na kutua ndege na maeneo ya maegesho, hatua ya pili ni kufunga taa za kumsaidia Rubani kuweza kuona uwanja wote na hatua ya mwisho ni taa zitakazofungwa mita 400 kila upande uwanjani hapo.

  Amefafanua kuwa Taa hizo za kisasa (Aviation Solar Powered Light) zitapunguza gharama za uendeshaji uwanjani hapo ikiwemo matengenezo yake kwani zinadumu muda mrefu. Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho, amesema kuwa nia ya Serikali ni kuendelea kurefusha uwanja huo ambapo italipa fidia kwa nyumba zilizopo pembeni ya uwanja huo ili kuongeza usalama wa uwanja na ndege kwa ujumla.

  “Tutaweka uzio katika uwanja huu kulingana na matakwa ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na pia kupitia uzio huu taa zitakuwa salama”, amesisitiza Dkt. Chamuriho. Naye, Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), amesema mfumo wa taa hizo za kisasa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light), zimefungwa kwa siku 14 na zina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 12 na kuwaka kwa masaa laki moja ukilinganisha na nyingine ambazo zinawaka kwa masaa elfu kumi.

  Mfumo wa uwekaji Taa za Kisasa ni mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inaendelea kuboresha viwanja vyake vya ndege ili kukidhi viwango vianavyostahili katika usafiri wa anga.


  0 0


  Katika azma yake ya  kuhakikisha Watanzania wengi wanapata matangazo yake, Kituo cha Utangazaji cha EFM  kimetanua matangazo yake kwa kuongeza masafa ya 91.3 fm Mkoani Mwanza huku Uongozi ukibainisha kuwa matarajio ni kuhakikisha Matangazo hayo yanafika katika mikoa mingine kumi, ikifuatiwa na Mkoa wa Mbeya, Singida, Kilimanjaro, Manyara, Mtwara, Tanga , Kigoma na  Dodoma.

  Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa EFM Radio Bwana Denis Ssebo, amesema lengo la kuanza na Mkoa wa Mwanza ni baada ya kuangalia idadi ya watu ambao wanapatikana kupitia Kanda ya Ziwa Victoria lakini pia ukubwa wa jiji hilo baada ya jiji la Dar es salaam.

  "Lengo la Efm Radio ni kuhakikisha inahabarisha, inaburudisha, kuwezesha pamoja na kuwapa elimu wasikilizaji wake wote katika kila mkoa itakaposikika.  Hivyo mikoa mingine ikae mkao wa kula - tutawafuata mlipo…" amesema Denis Ssebo”, akimalizia na EFM NI KWIKWI!

  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.
  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akivishwa beji ya uanachama wa Rotary Club na Dk. Manoj Desai kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017.
  aziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Rotary Club kwenye mkutano wa 92 wa mwaka unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha Mei 4, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameutaka uongozi wa Klabu ya Rotary nchini uangalie uwezekano wa kuisaidia Serikali kupambana na ugonjwa wa Malaria.

  Waziri Mkuu Majaliwa ambaye leo hii (Alhamisi, Mei 4, 2017) amekuwa mwanachana wa 651 kujiunga na klabu hiyo,  ametoa wito huo wakati akifungua mkutano wa 92 wa mwaka wa Rotary unaojumuisha nchi za Uganda na Tanzania (District 9211) katika ukumbi wa AICC jijini Arusha.

  "Ninatambua kazi nzuri inayofanywa na Rotary Club katika kuisaidia jamii kwa vile na mimi mwenyewe nimekuwa nikisaidia jamii. Kwa hiyo mimi na mke wangu Mary Majaliwa tunajiunga tukiwa ni wanachama wa 651 na 652 ili kuongeza nguvu ya Rotary kusaidia jamii," alisema huku akishangiliwa na washiriki zaidi ya 1,000 waliohudhuria mkutano huo kutoka Uganda, Tanzania, India, New Zealand na Australia.

  Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa klabu hiyo uongeze mikakati ya kutangaza kazi wanazozifanya ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa watu wengi kwamba wanaojiunga na klabu hiyo ni watu matajiri na watu maarufu.

  "Kazi mnazozifanya ni kubwa na nzuri mno kwa jamii. Lakini itabidi mjitangaze zaidi ili watu wengi zaidi watambue kazi zenu na waweze kuwaunga mkono," alisema.

  Waziri Mkuu aliahidi kuwashawishi viongozi wengine wa Serikali, taasisi za umma pamoja na Wabunge wajiunge kwa wingi na klabu hiyo. Tanzania ina klabu za Rotary 36 zenye wanachama 650 wakati Uganda ina klabu za Rotary 93 zenye wanachama 2,700. Tanzania na Uganda zinaunda District 9211 katika mfumo wa kimataifa wa rotary.

  Waziri Mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza wana-Rotary kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kusaidia jamii hasa kwenye sekta za maji, elimu, na afya.

  Alisema Rotary inatambulika duniani kwa kampeni yake ya kutokomeza ugonjwa wa polio; na kupitia michango ya wana-Rotary, Tanzania hivi sasa haina mgonjwa yeyote wa polio.

  "Licha ya uchache wenu, natambua mchango mkubwa unaotolewa na Rotary Club hapa nchini. Hivi karibuni, Rotary Club saba ziliungana na Benki M na kujenga hospitali kubwa ya watoto pale Muhimbili (MNH) na Kituo cha Ujasiriamali kwa Vijana pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)," alisema.

  "Miradi mingine inayofadhiliwa na Rotary Club ni ujenzi wa hospitali ya akinamama wajawazito mkoani Dodoma, utoaji wa vitabu vya ziada 20,000 kwenye shule za sekondari zaidi ya 40 mkoani Tanga pamoja na miradi ya maji safi kwenye  wilaya za Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro.

  Kwa upande wake, District Gavana wa Rotary 9211 ambaye anamaliza muda wake, Bw, Jayesh Asher wana-Rotary duniani wanaamini kwamba Serikali za nchi mbalimbali haziwezi kutekeleza majukumu yote kwa wananchi wake kwa hiyo wanajiunga na kutoa rasilmali zao ili kusaidia jamii zenye uhitaji.

  Akizungumzia kuhusu uchahe wa wanachama hapa nchini, Bw. Asher alisema Rotary Club ya Uganda imepata umaarufu kwa sababu viongozi wengi wamejiunga na klabu hiyo wakiwemo Mawaziri, Spika wa Bunge la Uganda, wabunge na mabalozi.

  “Hapa Tanzania itabidi tutangaze zaidi kazi zetu ili tuweze kuwavuta viongozi wa kisiasa na wa umma na pia kuongeza wanachama zaidi,” alisema.

  Mkutano huo wa siku tatu, utamalizika Juni 6, mwaka huu.


  0 0

   Ujenzi wa madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda 
   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiwa katika  ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda
   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akitoammaagizo wakati wa ziara yake ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda

   Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea  kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda.

  Mkuu wa wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela leo amefanya ziara ya kukagua madarasa na mabweni katika shule ya sekondari Tagamenda ikiwa ni maandalizi ya kupokea kidato cha 5 mwezi wa 7. Katika ziara yake aliyo ambatana na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa Bwana Omar Mkangaa, Mhe Kasesela aliagiza kasi ya ujenzi wa madarasa hayo na mabweni iongezeke ikiwezekana wajenge hata usiku ili tuweze kupokea wanafunzi wa kidato cha 5, huku akisisitiza kwamba mpaka sasa fedha za ujenzi zimeishapatikana kinachotakiwa ni kasi ya ujenzi. 

  Kwa sasa shule ya sekondari ya Tagamenda ina wanafunzi 882 wakiwemo wasichana 503 na wavulana 379. Inatarajia kupokea wasischana 120 kidato cha tano. Ujenzi wa madarasa 4 kwa thamani ya shilingi milioni 80, mpaka sasa kiwanja kimoja kipo katika hatua ya kupaka rangi na vyumba 3 na ofisi ya mwalimu vipo katika hatua ya kupiga kenchi. Akitoa taarifa fundi mjenzi Bwana Emmanuel Mhelamvi alisema mpaka sasa kiasi cha shilingi 56,447,102.40 zimekwisha tumika bado shilingi 23,552, 897.60 .  Pia Mabweni 2 ambayo yako katika hatua za kenchi yatagharimu kisi cha shilingi 150,000,000. 

  Changamoto kubwa ni gharama ya vifaa bei zake kubadilika mara kwa mara, pia gharama za ujenzi zimeonekana kuwa juu kutokana na eneo lenyewe kuwa mlimani . Mkuu wa wilaya aliaomba wadau na wananchi wajitokeze kusaidia ujenzi na vifaa vya shule hiyo. “nia yetu ni kuifanya shule ya mfano ili iweze kushindana na shule kama Feza na St Francis na zinginezo zinazo fanya vizuri, la msingi ni kuboresha miundo mbinu” 
  Mhe Kasesela pia alimshukuru sana Bwana Tibba Guyayi kutoka Dar Es salaam ambaye ameahidi kutoa kompyuta 2 kwa ajili ya shule na kuwaomba wengine waige mfano wa bwana Guyayi.


  0 0


  0 0

   Mhandisi wa kudhibiti mapato TANESCO mkoa wa Ilala, Daniel Kimaro, akizungumza na waandishi baada ya kusitisha huduma ya umeme kwenye kampuni ya Iprint.
   Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, wakiwa na kifaa cha kukatia umeem, tayari kwa kazi kwenye transfoma ya kupeleka umeme kwenye eneo la kiwanda eneo la Vingunguti    Mfanyakazi wa TANESCO kivaa gloves tayari kukata umeme
   Meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam, MhandisiAthanasius Nangali, (kulia), akiwa na Afisa kutoka idara ya fedha TANESCO makao makuu, akizungumza na waandishi wa habari


  0 0

  Aliyekuwa Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta  ambaye anajiandaa kustaafu, Bw. Fortunatus Kapinga akizungumza wakati wa kuwatuza wafanyakazi hodari wa shirika. Kushoto ni Kaimu Postamasta Mkuu mpya, Deo Kwiyukwa na kulia ni Meneja wa Fedha, Cyprian Mugemuzi.
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Bw. Deo Kwiyukwa akiwa na baadhi ya watendaji washirika hilo, wakiimba wimbo wa wafanyakazi wa mshikamano.  
  Mmoja wa wafanyakazi wa shirika la Posta, Zainabu Ukwaju akigogesha glasi na Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa.
  Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la Posta wakiwa katika hafla ya kuwatunuku wafanyakazi hodari.  
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa akizungumza wakati wa hafla hiyo. 
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi hodari wa shirika, Arubee Ngaruka  wakati wa hafla hiyo.
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Bw. Deo Kwiyukwa akimkabidhi cheti mmoja wa wafanyakazi hodari wa shirika, Christina Chale, wakati wa hafla hiyo. 
  Wafanyakazi hodari wa shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa shirika wakati wa hafla hiyo. 
  Wafanyakazi hodari wa shirika la Posta wakiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Deo Kwiyukwa wakati wa hafla hiyo. 
  Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakipita mbele ya mgeni rasmi, Rais mstaafu wa Chama cha Walimu (CWT), Magreth Sitta na mabango wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Uwanja wa Uhuru. 
  Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakipita mbele ya mgeni rasmi na miavuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Uwanja wa Uhuru. 
  Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakipita mbele ya mgeni rasmi na miavuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Uwanja wa Uhuru. 
  Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakipita mbele ya mgeni rasmi na miavuli wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Uwanja wa Uhuru. 
  Wafanyakazi wa usafirishaji vifurushi na barua wakipita na pikipiki, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi duniani (Mei Dei), Uwanja wa Uhuru.
  Magari ya kusafirishia vifurushi pamoja na mizigo mingine kwenda kwa wateja wa shirika yakipita mbele ya mgeni rasmi. 
  Magari ya kusafirishia vifurushi pamoja na mizigo mingine kwenda kwa wateja wa shirika yakipita mbele ya mgeni rasmi. 
  Magari ya kusafirishia vifurushi pamoja na mizigo mingine kwenda kwa wateja wa shirika yakipita mbele ya mgeni rasmi. 
  Kaimu Postamasta Mkuu mpya wa Shirika la Posta, Bw. Deo Kwiyukwa akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuwatunuku wafanyakazi hodari wa shirika.

  0 0

  Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmoud Thabit Kombo akipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.

  Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Viongozi wa Wizara ya Afya na Jumiya ya Wakunga, Wauguzi na Wadau wa Afya Tanzania wakati wakipokea maandamano ya Wakunga na Wauguzi katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo Zanzibar.  
  Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
  Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao

  Wauguzi na Wakunga wakipita mbeli ya mgeni rasmin Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombe katika viwanja vya ZBC Redio rahaleo wakati wa maadhimishi ya siku hiyo maalum kwao
  MC wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Zanzibar akisoma utaratibu wa hafla hiyo iliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar 


  Kaimu Msaidizi wa Mrajisi wa Wauguzi na Wakunga Zanzibar Ndg. Rajab Mussa akisoma kiapo cha wauguzi na wakunga wakati wa hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar yalioaza kwa maandamano ya Wakunga na Wauguzi Zanzibar.  
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakunga Zanzibar Bi Amina Abdulkadir Rajab akizungumza wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimishwa katika ukumbi wa Sanaa rahaleo kwa maandamano yaliopokelewa na Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo
  Mwakilishi wa Jumuiya ya Tanzania Midwives Assossiotion Bi Priscilah Godwin akitowa salamu za TAMA wakati wa hafla hiyo ya Maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wauguzi Zanzibar Bi Valeria Rashid akitowa salamu za jumuiya yao wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yalioadhimisha Zanzibar katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. 
  Rais wa Jumuiya ya CHORA (Construction Health and Relief Acts) Bi Carol Mcdonald akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani yaliofanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar
  Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNFPA Bi Sabina Luoga akitowa salamu za Shirika lake wakati wa maadhimishi ya Siku ya Wakunga Duniani katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar katika hafla hiyo.
  Waziri wa Afya Zanzibar akiwahutubia Wauguzi na Wakunga wakati wa hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani, na kutowa nasaha zake kwa Wauguzi na Wakunga katika utowaji wao wa huduma kwa Mama na watoto, wakati wa kutowa huduza zao katika jamii.   

  Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa sekta ya Afya Zanzibar wakifuatilia hafla hiyo ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani.
  Washiriki wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Wakunga Duniani wakimsikiliza Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Mohmuod Thabit Kombe akiwahutubia na kutowa nasaha zake kwa waugunzi na wakunga katika kutowa huduma kwa wananchi wakiwa katika ukumbi wa sanaa rahaleo
  Viongozi wa Wakunga na Wauguzi wakifuatilia hutuba ya Waziri wa Afya Zanzibar Mhe Mahmoud Thabit Kombo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani huadhimishwa kila mwezi wa Mei 5, Duniani kote, hafla hiyo ya maadhimisho hayo yamefanyika katika ukumbi wa sanaa rahaleo Zanzibar.
  Imeandaliwa na Othmanmapara.Blog.com
  Zanzinews.com
  Email othmanmaulid@gmail.com

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi (katikati) akisikiliza kwa maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta, wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa Dkt Angelina Lutambi na kushoto ni Mtathmini wa mazingira Bi Saada Juma kutoka kampuni ya JSB.
  Ramani inayoonyesha maeneo ya wilaya tatuza Mkoa wa Singida ambapo tathmini ya athari za mazingira na kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
  Wadau wa sekta mbalimbali zinazohusika na mazingira kutoka mkoa wa Singida wakifuatilia kwa umakini maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na jamii kwa ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akisikiliza kwa maelezo ya tathmini ya athari za mazingira na kijamii kwa mradi wa bomba la mafuta, wa kwanza kulia kwake ni Katibu Tawala Mkoa Dkt Angelina Lutambi.

  Mtaalamu Bw. Lalit Kumar kutoka kampuni ya RSK itakayohusika na ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita kutoka Uganda hadi Tanga.

  …………………………………………………………………………….

  Wananchi wa Wilaya tatu za Makalama, Iramba na Singida Mkoani Singida ambazo bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga linapita wanapaswa kutoka ushirikiano wa kutosha katika hatua zote za ujenzi wa bomba hilo ili wanufaike na fursa zitakazopatikana kwa uwepo wa mradi huo.

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi ametoa rai hiyo katika kikao cha tathmini ya athari za mazingira na za kijamii katika mradi wa bomba la mafuta ambapo watathmini watapita maeneo yote ambapo bomba hilo litapita ili kupata maoni yao ili yaweze kuzingatiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

  Dkt. Nchimbi amesema wananchi wanapaswa kuwajulisha watathmini hao kila kitu kuhusu hali ya mazingira na kijamii ili mradi huo usiharibu mazingira au upunguze baadhi ya athari wakati wakujenga bomba hilo.

  Ameongeza kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusu fidia kwa maeneo ambapo bomba litapita kwakuwa watalipwa vizuri fidia zao na hivyo wanapaswa kuruhusu mradi huo upite katika maeneo yao bila wasiwasi na pia wasianze kuendeleza maeneo ambayo wamesikia mradi utapita kwa kigezo tu cha kupata fidia kubwa.

  Kwa upande wake Mtathmini wa Mazingira Saada Juma kutoka kampuni ya JSB ambayo inafanya tahmini hiyo amesema wanatekeleza matakwa ya kisheria katika kufanya tahmini hiyo na wataifanya kwa kasi kubwa ili ujenzi rasmi wa mradi uwahi kufanyika.

  Saada amesema mradi huo utakua kambi mbalimbali na kwa mkoa wa Singida kambi itakuwa katika kata ya Msisi ambapo uwepo wa kambi hiyo utaongeza uchumi wa kata na wilaya hiyo.

  Amesema vijana wa Singida wajiandae kwa ajili ya kupata ajira mbalimali katika mradi huo, baadhi ya miundombinu itaboreshwa pamoja na uchumi kukukua kwa kuuza bidhaa na kutoa huduma kwa watakaokuwa wakiishi katika kambi hiyo.

  Tathmini ya athari za mazingira na za kijamii kwa wilaya za Singida, Mkalama na Iramba ambapo mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda mpaka Tanga itaana mapema wiki ijayo.

  0 0


  Waziri wa Viwanda,Biashara naUwekezaji Mhe. Charles Mwijage kulia akipokea cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Afisa Afya Bw. Fadhili Kilamile mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
  Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Zungu wa kwanza kulia akisubiria kupewa cheti cha chanjo cha kimataifa kijulikanacho kama cheti cha homa ya manjano kutoka kwa Kaimu Mkuu wa Kitengocha Afya Mipakani Bw. Remidius Kakulu kushoto mara baada ya kupata chanjo hiyo leo kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
  MbungewaVitiMaalumjimbo la SingidaMhe. Martha Mlatawa kwanza kuliaakiandikiwacheti cha chanjo cha kimataifakijulikanachokamacheti cha homayamanjanokutokakwa Afisa Afya Agnes Shirima katikatimarabaadayakupatachanjohiyoleokwenyeviwanjavyabungemjini Dodoma aliyesimamani Afisa Habari wa WizarayaAfya Bi. Catherine Sungura.

  …………………………

  Na.Catherine Sungura, WAMJW

  Dodoma


  Watanzania hususan wale wanaosafiri nje ya nchi zile zenye ugonjwa wa homa ya manjano wanatakiwa kujitokeza kwenye vituo vilivyoainishwa na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa ajili ya kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha vyeti vipya.

  Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati alipofika kupata huduma ya chanjo ya homa ya manjano ambayo inatolewa bungeni hapa

  Waziri Mwijage amesema duniani ugonjwa huu upo na zipo nchi nyingi ambazo zimepoteza wananchi wake kwa kuugua ugonjwa huo“Suala hili ni muhimu sana kwa afya zetu,pamoja na kwamba nchi yetu haina mgonjwa wa homa ya manjano

  Aidha amesema maambukizi ya ugonjwa huu endapo mtu ataupata gharama za matibabu yake ni ghali sana na inaweza kupelekea kupoteza maisha,hivyo ni vyema kujitokeza kwa wingi kupata chanjo hiyo pamoja na kubadilisha kadi zao kwani usiweke reheni maisha yako

  Hata hivyo aliwatahadharisha wafanyabiashara,wanafunzi wale wanaosafiri au kusoma nje ya nchi ni vyema wahakikishe wanapata chanjo hiyo kuliko kupewa kadi kwa njia nyingine kwani kadi hizi zimeboreshwa na zina alama za siri ambazo nchi za kimataifa zina uwezo wa kusoma alama zetu.

  Naye Mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe.Mussa Zungu ameipongeza Wizara ya Afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto kwa kubadilisha kadi hizi mpya kwa kuepukana na vyeti vingi ambavyo vilikua vinanunuliwa mtaani bila kupata huduma za kupata chanjo,hivyo ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanapata chanjo hizo kwani ilikua ni hatari sana hususan nchi zile zenye milipuko wa homa za manjano na hivyo kupata vyeti ambavyo ni halali

  Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto limeongeza muda wa kubadilisha vyeti vya zamani hadi mwisho wa mwezi huu na baada ya hapo vyeti vya zamani havitatambulika tena.

  0 0

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akielekezwa jinsi ya kujaza fomu  za kununua hisa  za Vodacom Tanzania PLC na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities,Gerase Kamugisha  (kushoto) wakati alipokuwa akinunua hisa zake na mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani)zenye thamani ya shilingi milioni 20 katika hafla fupi  iliyofanyika ofisini kwake  jijini Dar es Salaam leo.Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji, Bi.Beng’i Issa  na Mkurugenzi  mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao.

   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikabidhiwa fomu ya kununua hisa za Vodacom Tanzania PLC   na Mkurugenzi wa wakala wa hisa wa Orbit Securities ,Gerase Kamugisha   wakati wa hafla fupi ya kununua hisa zake na mke wake,Mary Majaliwa(hayupo pichani) zenye thamani ya shilingi Milioni 20.Hafla hiyo ilifanyika  ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo,Anaeshuhudia kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Vodacom Tanzania PLC,Ian Ferrao.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akipongezwa na Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Ian Ferrao  baada ya kununua hisa zake na za mke wake Mary Majaliwa(hayupo pichani) kutoka Vodacom Tanzania PLC kampni hiyo zenye thamani ya Shilingi Milioni 20.
   Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiongea wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa za Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zake pamoja na mke wake Mary Majaliwa zenye thamani ya shilingi Milioni 20, wapili kutoka kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwekezaji Bi.Beng’i Issa , Mkurugenzi  Mtendaji  wa Vodacom Tanzania  PLC,Ian Ferrao na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo,Rosalynn Mworia.

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa  akiwa katika picha ya pamoja na wadau wakati wa hafla ya ununuzi wa hisa Vodacom Tanzania PLC iliyofanyika ofisini kwake jijini Dar es Salaam, ambapo alinunua hisa  zenye thamani ya shilingi Milioni 20 pamoja na mke wake Mary Majaliwa.

  0 0  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye kilele cha siku ya Wakunga Duniani ambapo Kitaifa imefanyika mjini Dodoma.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Samia akihutubia Wakunga kwenye kilele cha Sherehe za Siku ya Wakunga Duniani iliyofanyika Kitaifa mkoani Dodoma kwenye ukumbi wa Julius K. Nyerere Chuo cha Mipango.
  Wakunga wakirekodi hotuba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za Siku ya Wakunga Duniani ambapo kitaifa zimefanyika mjini Dodoma.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia Wakunga waliojitokeza kwa wingi kwenye kilele cha Siku ya Wakunga Duniani ambayo Kitaifa imefanyika mkoani Dodoma na mgeni rasmi ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

  .............................................................

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameziagiza Halmashauri zote nchini zihakikishe zinajenga nyumba kwa ajili ya watumishi wa afya hasa maeneo ya vijijini na kipaumbele kitolewe kwa wakunga ambao mara nyingi ndio wanatoa huduma za dharura kwa wanawake wajawazito na watoto.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa agizo hilo mjini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wakunga Duniani sherehe ambazo zimehudhuriwa na Mamia ya wakunga kutoka mikoa mbalimbali nchini.

  Makamu wa Rais amesema kuwa halmashauri zikijenga nyumba karibu na vituo vya kutolewa huduma za afya zitasaidia kupunguza matatizo ya mama na watoto wanaotaka kupata huduma za dharura ikilinganishwa na hali ilivyo sasa ambapo baadhi ya watumishi wa afya hasa wakunga wanakaa mbali na maeneo yao ya kazi hivyo utoaji wa huduma za dharura kuwa duni.

  Makamu wa Rais amewahimiza Wakuu wa mikoa na wilaya kusimamia ujenzi huo kikamilifu kama walivyoshughulikia matatizo ya madawati katika maeneo yao ili kuhakikisha Taifa linafikia malengo yake ya kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi nchini.

  Kuhusu changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini, Makamu wa Rais amewahakikishia wakunga na watumishi wengine wa sekta ya afya nchini kuwa Serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto hizo ikiwemo uboreshaji wa maslahi kwa watumishi wa kada hiyo pamoja na kuongeza maradufu vifaa tiba,dawa na vitendanishi ili kuhakikisha wananchi kote nchini wanapata huduma bora za afya.

  Amesema mpaka sasa upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya afya nchini ni imefikia asilimia 83 hadi kufikia mwishoni mwa Marchi 2017.

  Makamu wa Rais pia amewahimiza wakunga kufanya kazi kwa bidii na kwa kuzingatia maadili na waache tabia ya kutoa lugha mbaya kwa wanawake wajawazito na wakunga watakaobainika kufanya vitendo hivyo wachukuliwe hatua kali ili kukomesha tabia hiyo.

  Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Wizara yake itaendelea kusimamia ipasavyo utoaji bora za afya kwa wananchi pamoja na kusimamia maadili kwa watumishi wa sekta ya afya kote nchini.

  Amesema anaimani kubwa kuwa baada ya Serikali kuiongezea Wizara ya Afya bajeti kutoka bilioni zaidi ya 700 katika mwaka wa fedha za 2016/2017 hadi Trilioni Moja kwa mwaka wa fedha 2017/2018 inaonyesha wazi dhamira ya dhati ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za afya kwa kiwango hali ya juu nchini ikilinganishwa na miaka iliyopita.

  Kauli mbinu ya maadhimisho ya Siku ya Wakunga mwaka huu ni Wakunga,Akina mama na Familia ni washirika wa Kudumu.(Midwives,Women and Families Partners)

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0


  0 0

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo muhimu unaokutanisha wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi wa kiserikali unalengo la kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo barani Africa kukutana na kujadili mustakhabali wa maendeleo na uwekezaji barani Afrika.

  Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu aliwakilisha Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu (The Education Commission) ambapo alikutana na wadau wa elimu na vyombo vya habari kuelezea Mpango wa Kizazi cha Elimu barani Afrika.

  Rais Mstaafu pia alipewa heshima ya kuhutubia hafla ya chakula cha jioni kutathmini mafanikio ya mpango wa Kilimo wa Grow Africa ambao chimbuko lake ni Mkutano wa WEF Africa uliofanyika Tanzania Mei, 2010 na Mpango wa Uwekezaji wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT). 

  Katika hotuba yake, Rais Mstaafu alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuchochea ushiriki wa Sekta Binafsi na uwekezaji katika Kilimo barani Afrika. Alitoa angalizo kuwa mafanikio ya mapinduzi ya kilimo hayawezi kufanikiwa kwa kuondoa wakulima wadogo bali kuwaongezea tija. Alitoa rai kwa viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa kilimo cha Wakulima wakubwa kinashamirisha na kustawisha kilimo cha wakulima wadogo na kuwa ni vitu vinavyoweza kwenda pamoja.

  Akiwa Durban, Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum. 
   Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akishiriki katika mdahalo wakati wa Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. 
    Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini pembezoni mwa mkutano huo mjini Durban.
    Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum.  
  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho akiwa na Mkurugenzi wa World Economic Forum kanda ya Afrika kwenye mkutano huo  unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Kabla ya hapo Bi kanza alikuwa mshauri wa Uchumi wa Rais Mstaafu Kikwete wakati wa uongozi wa awamu ya nne.

  Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshiriki Mkutano wa World Economic Forum for Africa unaofanyika Durban, Afrika Kusini. Mkutano huo muhimu unaokutanisha wafanyabiashara, wanasiasa na viongozi wa kiserikali unalengo la kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo barani Africa kukutana na kujadili mustakhabali wa maendeleo na uwekezaji barani Afrika.

  Katika Mkutano huo, Mheshimiwa Rais Mstaafu aliwakilisha Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu (The Education Commission) ambapo alikutana na wadau wa elimu na vyombo vya habari kuelezea Mpango wa Kizazi cha Elimu barani Afrika.

  Rais Mstaafu pia alipewa heshima ya kuhutubia hafla ya chakula cha jioni kutathmini mafanikio ya mpango wa Kilimo wa Grow Africa ambao chimbuko lake ni Mkutano wa WEF Africa uliofanyika Tanzania Mei, 2010 na Mpango wa Uwekezaji wa Kilimo wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT). 

  Katika hotuba yake, Rais Mstaafu alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuchochea ushiriki wa Sekta Binafsi na uwekezaji katika Kilimo barani Afrika. Alitoa angalizo kuwa mafanikio ya mapinduzi ya kilimo hayawezi kufanikiwa kwa kuondoa wakulima wadogo bali kuwaongezea tija. Alitoa rai kwa viongozi wa Afrika kuhakikisha kuwa kilimo cha Wakulima wakubwa kinashamirisha na kustawisha kilimo cha wakulima wadogo na kuwa ni vitu vinavyoweza kwenda pamoja.

  Akiwa Durban, Rais Mstafu amehudhuria pia amefanya mazungumzo na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini na Profesa Klaus Shwab ambaye ni Mtendaji Mkuu wa World Economic Forum.


older | 1 | .... | 1220 | 1221 | (Page 1222) | 1223 | 1224 | .... | 1897 | newer