Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

BALOZI SEIF AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA MCT

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) uliofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kubadilishana nao mawazo. Kulia ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Kushoto ya Balozi ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan .
Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan akifafanua jambo mbele ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif walipokutana nae kwa mazungumzo.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga Kulia ya Balozi Seif akielezea mikakati ya Baraza la Habari Tanzania inavyofanya kazi Zanzibar katika kuhakikisha Maadili ya Habari yanazingatiwa na Wana Habari wote Nchini.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga akimkabidhi Balozi Seif Vitabu mbali mbali vilivyochapishwa na Baraza hilo kuhusu Tasnia ya Habari Tanzania.

Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa juu wa Baraza la Habari Tanzania mara baada ya kubadilishana mawazo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Bwana Kajubi Mukajanga na Muandishi wa Makala wa MCT Yussuf Mpinga.

Kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan, Muhariri wa Machapisho wa MCT Khamis Mzee na Mkuu wa Kitengo cha Rasilmali Watu cha MCT Bivi Ziada Kilobo. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasubiri kuyapokea kwa ajili ya kuyafanyia kazi mapendekezo yatakayowasilishwa ya Rasimu ya Sera ya Habari Zanzibar katika kuona Sekta ya Habari Nchini inakuwa imara.

Alisema Taasisi zinazohusika na jukumu la kusimamia masuala hayo ni vyema zikahakikisha kwamba zinaharakisha mapendekezo hayo ili ile dhana ya Uhuru wa kupata Habari bila ya kuogopa inapatikana.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo yake na Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } ulioongozwa na Katibu Mtendaji wake Bwana Kajubi Mukajanga aliokutana nao hapo Afisini kwake Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa kila aina ya msaada katika kuona Sekta hiyo muhimu kwa jamii inawajibika ipasavyo katika kuwapasha Habari Wananchi.

“ Habari ni Sekta muhimu inayotoa Taarifa na Elimu na kuwahusisha moja kwa moja Wananchi wa kawaida wakiwemo wakulima Vijijini ”. Alisema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar.

Balozi Seif kupitia Uongozi wa Baraza hilo la Habari Tanzania aliwakumbusha Wana Habari kuzingatia sheria na Maadili yao ya kazi katika kuandika Habari wanazozifanyia Utafiti wa kina ili zisaidie Wananchi kupata Habari za ukweli.

Akizungumzia changamoto ya Vitambulisho vya Kazi inayowakumba Wana Habari wanaotokea Tanzania Bara na kupangiwa kufanya kazi Zanzibar Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliahidi kulifuatilia kwa kina suala hilo ambalo bado halijawa kero kama yalivyo masuala mengine katika utendaji.

Alisema Waandishi wa Habari wanaotokea Tanzania Bara wanapaswa kuandaliwa utaratibu maalum wa kupata vibali vya kazi kwa vile wao hawahusiani na kuwa na Vitambulisho vya Mzanzibari Mkaazi katika kuomba kibali cha kufanya Kazi Zanzibar.

Balozi Seif alieleza kwamba mfumo unaotumika katika kuwapasha Habari Wananchi wa pande zote za Muungano hauna mipaka licha ya kwamba Sekta ya Habari sio Taasisi iliyomo ndani ya masuala ya Muungano.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi wa Baraza la Habari Tanzania { MCT } kwa umakini wake wa kusimamia Sekta ya Habari Nchini Tanzania.

Mapema Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Bwana Kajubi Kukajanga alisema Kamati ya Maadili ya Bahara la Habari Tanzania imekuwa na utaratibu wa kufanya ziara za kusikiliza malalamiko yanayotolewa na Wananchi wanaoandikwa visivyostahiki katika Vyombo mbali mbali vya Habari.

Bwana Kajubi alisema Wajumbe wa Kamati hiyo kupitia ziara hizo hupata fursa za kushauri, kuelekeza pamoja na kuwaonya na wengine kuwachukuliwa hatua za kisheria Wana Habari wanaofanya makosa katika kuandika Habari chafu dhidi ya wananchi mbali mbali.

Alisema Viongozi hao pia wanajaribu kusaidia Wana Habari wanaotoka Tanzania Bara kuondokana na ukakasi wa kupata Vitambulisho vitakavyowapa fursa ya kufanyakazi kwa upana zaidi bila ya vikwazo.

Naye Mkuu wa Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania (MCT) upande wa Zanzibar Bibi Shifaa Hassan alisema Mchakato wa Sera ya Habari Zanzibar umeanza tokea mwaka 2010 kwa mashirikiano baina ya Idara ya Habari Maelezo, Tume ya Utangazaji Zanzibar pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi za Serikali.

Bibi Shifaa alisema Zanzibar imekuwa tajiri katika masuala ya Historia ya Habari kutokana na kuanza mapema kwa Sekta hiyo ndani ya Ukanda mzima wa Afrika ya Mashariki.

Alisema Ofisi ya Baraza la Habari Tanzania upande wa Zanzibar ilianzishwa mwaka 2003 na kuanza na Mpango Maalum wa harakati za kutoa mafunzo kwa Wana Habari wachanga wa vyombo mbali mbali vya Habari wakiwemo pia wale waliomaliza masomo yao ya sekondari walioamua kujiunga na Tasnia hiyo.

Bibi Shifaa alieleza kwamba mpango huo ulikwenda sambamba na kutoa machapisho ya vitabu mbali mbali, kufanya utafiti kuhusu shirika la Habari Zanzibar mambo yaliyoibua kupatikana kwa Kitabu cha Historia ya masuala ya Habari Zanzibar kilichozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mwaka ulipita.

Viongozi wa Baraza la Habari Tanzania tayari wapo Visiwani Zanzibar kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani inayofikia kilele chake ifikapo Tarehe 3 Mei ya kila mwaka ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
2/5/2017.

WAKULIMA WA KIJIJI CHA IPILIMA WILAYANI MUFINDI WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SHAMBA DARASA KUTOKA YARA TANZANIA

$
0
0
Aidan Timos (pichani kulia) ni mkulima wa mahindi na nyanya kutoka kijiji cha Ipilimo, wilayani Mufindi mkoani Iringa. Aidan amekuwa mkulima mashururi aliefanikiwa kubadili kilimo chake cha mazoea na kwenda kwenye kilimo cha biashara baada ya kupata elimu ya lishe linganifu ya mimea kutoka Yara Tanzania Ltd miaka miwili iliyopita. 

Kutokana na jitihada zake kwenye kilimo, wanakijiji walimteua kuwa Mwenyekiti wa kijiji hicho. Mwanzoni mwa msimu huu wa mahindi, Timos aliwakaribisha Yara Tanzania Ltd kijijini kwao kwa ajili ya kutengeneza shamba darasa ambalo wakulima katika kijiji hicho waliweza kujifunza kwa vitendo. "Kupitia mimi wakulima wengi wamenufaika na pia nawashukuru Yara kutuwekea mashamba darasa kwenye kijiji chetu ili wale ambao bado hawajapata elimu ya mbolea basi wajifunze kwa vitendo".Pichani kushoto ni Afisa Ugani wa Yara Tanzania Wilayani Mufindi, Andrew Mwangomile.
Afisa Ugani wa Yara Tanzania Wilayani Mufindi, Andrew Mwangomile akitoa mafunzo ya shamba darasa kwa Wakulima wananchi wa kijiji cha Ipilimo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Wakulima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mafunzo ya utumiaji bora ya mbolea kwa vitendo.

“HALI YA DAWA NCHINI IMEIMARIKA”-MHE.KIGWANGALLA

$
0
0

Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.

Serikali kupitia Wizara ya Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa hali ya upatikanaji wa Dawa nchini imeimarika na kufikia asilimia 83.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe.Khamis Kigwagalla alipokuwa akijibu Hoja mbalimbali za Wabunge leo Mjini Dodoma.

“Moja ya vipaumbele vya Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Magufuli ni kuboresha upatikanaji wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma nchini”Alisema Mhe.Kigwangalla.

Amesema kuwa katika kutekeleza azma hii Serikali ilichukua juhudi za makusudi kwa kuongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 31 katika mwaka wa fedha 2015/16 hadi kufikia bilioni 251,500,000,000 katika mwaka wa fedha 2016/17.

Aidha hadi kufikia Mwezi April 2017 Jumla ya Bilioni 112 zilikwisha kutolewa na kupelekwa Bohari ya Dawa ili kuviwezesha vituo vya kutolewa huduma za Afya vya Umma kupata mahitaji yake ya Dawa,Vifaa,Vifaa tiba na Vitendanishi.

Kufuatia Ongezeko ilo la fedha kumbukumbu zinaonyesha kuwa hali ya upatikanaji wa dawa nchini imeimarika sana.

“Hadi kufikia tarehe 15 Januari 2017,Mkoa wa Kagera pekee umepokea kiasi cha bilioni 4,150,767,216 kupitia fungu 52 kwa ajili ya kununulia dawa,vifaa,vifaa tiba na vitendanishi.”Aliongeza Mhe.Kingwangalla.

BALOZI SEIF ALI IDDI AONGOZA WADAU HABARI KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI ZANZIBAR

$
0
0
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wadau wa Habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani hapo katika Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi.
 Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar Omar akitoa ufafanuzi juu ya Umuhimu wa Wanahabri kuzingatia suala la Amani katika uandishi wao wa kila siku.
 Viongozi wa Meza Kuu kutoka kulia Katibu Mtendaji wa MCT Bw. Kajubi Mukajanga, Mkuu wa Mkoa Mjini Maghribi Mh. Ayoub, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif, Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari Nd. Hassan Mitawi wakifuatilia hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo Kilimani.
 Kikundi cha Utamaduni cha Mkoa Mjini Magharibi kilitoa Burdani katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari hapo katika Ukumbi wa Chuo cha Habari Kilimani Mjini Zanzibar.
 Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga akitoa salamu kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani Mjini Zanzibar.
 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Abdulla Hassan Mitawi akifafanua jambo kwenye maadhmisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Dunani.
 Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mheshimiwa Ayoub Mohamed Mahmoud  akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari yaliyofanyika katika Viunga vya Chuo cha Habari Zanzibar kiliopo Kilimani Mjini Zanzibar.
 Washiriki mbali mbali waliohudhuria  Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani yaliyofanyika katika chuo cha Habari Zanzibar  kilipo Mtaa wa Kilimani.
Balozi Seif Ali Iddi kati kati waliokaa vitini akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Taasisi mbali mbali za Habari Nchini mara baada ya kufungua mdahalo wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kushoto ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mahmoud, Katibu Mtendaji Baraza la Habari Tanzania Bw. Kajubi Mukajanga, kulia ya Balozi Seif ni Mkuu wa Chuo cha Habari Zanzibar Nd. Chande Omar na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo anayesimamia Habari Nd. Hassan Mitawi. Picha na – OMPR – ZNZ.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA KUMI NA SITA MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MEI 3, 2017

$
0
0
 Mwenyekiti  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Andrew Chenge akiongoza kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
 Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
  Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Isack Kamwelwe  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
  Naibu Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii ,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
 Mbunge wa Karagwe (CCM) Mhe.Innocent Bashungwa akiuliza swali  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Oliver Semuguruka  akiuliza swali  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Eng.Ramo Makani  akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama,Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Hussein Mwinyi na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira  wakifurahia jambo katika  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017. 
 Mbunge wa Bagamoyo(CCM)  Mhe.Shukuru Kawambwa akiuliza swali  kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
Wabunge wa Chama cha Demokarasia na Maendeleo(CHADEMA) Wakijadili jambo wakati wa kikao cha kumi na sita cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 3, 2017.
Picha Zote na Daudi Manongi- Dodoma MAELEZO,DODOMA



PIKIPIKI 46 NA BAISKELI 30 ZAKAMATWA KWA MAZAO YA MISITU

$
0
0

TFS, Dar es Salaam.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani pamoja na Mamlaka ya Usafirishaji nchi kavu na Majini (SUMATRA) unazishikilia pikipiki 46 na baiskeli 30 kwa kosa la kusafirisha mazao ya misitu kinyume cha sheria ya misitu na kuwa na mazao hayo yaliyopatikana kinyume cha sheria.

Pikipiki na baiskeli hizo zilikamatwa kwa nyakati tofauti katika barabara kuu zinazoingia jijini Dar es Salaam kupitia Barabara ya Bagamoyo, Kilwa, Kisarawe na Morogoro.

Pikipiki na baiskeli hizo zilizokamatwa zitatozwa faini, pikipiki moja itatozwa faini ya kuanzia sh. 500,000/= huku baiskeli zikitozwa faini isiyopungua sh.50,000/= nakuendelea.

Faini hizi ni kwa mujibu wa Sheria ya Misitu inayoeleza wazi kuwa mtu yeyote aliyetenda kosa la kusafirisha mazao ya misitu yaliyopatikana kinyume cha sheria na kupatikana na hatia atatakiwa kulipa faini isiyozidi shilingi milioni moja au mara tatu ya thamani ya mazao ya misitu yaliyokamatwa au kifungo kisichozidi miaka saba au adhabu zote kwa pamoja.

Katika muda wa wiki mbili wa zoezi hilo jijini Dar es Dar es Salaam jumla ya sh. 11,167,600/= ilitozwa kama gharama za ufifilishaji (compounding fees) kwa magari yaliyokutwa na mazao ya misitu kinyume na sheria ya misitu na kanuni zake. Aidha gari moja lipo ofisi ya meneja wilaya ya bagamoyo kwa hatua Zaidi.

Pikipiki na baiskeli zilizokamatwa zimehifadhiwa katika ofisi ya Meneja Misitu Wilaya ya Temeke, Bagamoyo na Kibaha huku magunia 451 ya mkaa ambayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya takribani sh milioni 10 yakishushwa kutoka katika pikipiki hizo na magari yaliyokaguliwa.

Mkaa uliokamatwa umehifadhiwa katika ofisi ya Meneja Misitu wa Wilaya ya Mkurunga kituo cha ukaguzi cha Vikindu na ofisi ya Meneja Misitu wa Wilaya ya Ilala.

Ukaguzi wa kudhibiti vyombo vinavyosafirsha mazao ya msitu kinyume na sheria hususani baiskeli na pikipiki nchini ulianza Aprili 14 na zoezi hilo linalofanyika usiku na mchana ni endelevu hivyo wasafirishaji wa Mazao ya Misitu wanashauriwa kufuata taratibu na sheria za Usafirishaji wa mazao ya Misitu kwani kinyume na hapo adhabu husika itatolewa.


Tulizo kilaga

Afisa Habari na Mawasiliano
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) 03 Mei 2017.

UFAFANUZI KUHUSU UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI TANZANIA WA MWAKA 2016/17

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AWAPA MAKAVU WANAOBEZA MAENDELEO YANAYOLETWA NA SERIKALI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma dkt bilinithi mahenge ashangazwa na baadhi ya watu wachache ambao wanatabia ya kubeza maendeleo yanayofanywa na serikali kana kwamba kama hayana umuhimu katika jamii,kauli hii ameitoa mara baada ya uzinduzi wandege mkoa Ruvuma ambapo shirika la ndege Tanzania ATCL limeanza kutoa huduma zake toka SONGEA HADI DAR ES SALAAM

Ufinyu wa bajeti ni kikwazo kwa huduma za Uzazi wa Mpango

$
0
0
 Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya huduma za uzazi wa mpango imekuwa ndicho kikwazo kikuu katika kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi hapa nchini ambapo katika miaka sita iliyopita kiwango cha juu sana kilichotengwa na kutolewa kwa mwaka ni shilingi bilioni tano tu.

Hayo yameelezwa na Dkt. Faustine Ndugulile, ambaye ni Mjumbe wa Chama cha Wabunge kuhusu Idadi ya Watu na Maendeleo mwishoni mwa wiki wakati akiongea jijini Dar es Salaam kuhusu changamoto cha uzazi wa mpango hapa nchini Tanzania.

Dkt Ndugulile alisema kuwa huduma za uzazi wa mpango zinahitaji shilingi bilioni 20 kila mwaka lakini kati ya mwaka 2010/11 na 2015/16 ni bilioni 5 tu zilizotengwa na kutolewa kila mwaka zilikuwa pungufu sana ukilinganisha na mahitaji halisi. Kiwango cha juu kwa mwaka kilikuwa ni kiasi cha shilingi bilioni tano tu ambazo zilitengwa na kutolewa, sawa na asilimia 25 tu ya mahitaji yote kwa mwaka husika.

‘Tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania ni moja kati nchi zenye vifo vingi vitokanao na uzazi duniani, ambapo vifo 556 hutokea kwa kila vizazi hai 100,000; ikimaanisha kuwa zaidi ya akinamama 50 hufariki kila siku kutokana na matatizo ya uzazi’, alisema Ndungulile.

Dkt Ndugulile aliongeza kuwa zaidi ya watoto 100,000 hufariki kabla ya kutimiza miaka mitano, kati ya hao zaidi ya 50,000 hufariki kabla ya kuzaliwa na nusu yao wakati wa kuzaliwa, huku wenzao wapatao 40,000 wakifariki dunia kwenye siku 28 za mwanzo baada ya kuzaliwa. Licha ya ufinyu wa bajeti, Vifo vingi vya uzazi hutokea kwa sababu wanawake wanakosa kufikia huduma ambazo wanazihitaji ikiwemo uzazi wa mpango.

Sababu zingine ni kubeba mimba wakati wa umri mdogo, kutoa mimba kwa njia zisizo salama, kuendelea kubeba mimba wakiwa na umri mkubwa ambao ni zaidi ya miaka 35, na kukosa ufahamu wa jinsi ya kutoa nafasi baada ya kujingua ili kubeba mimba inayofuata.

Mpango wa Taifa Uliokasimiwa wa Uzazi wa Mpango (NFPCIP) uliweka lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kupitia kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango hadi kufikia asilimia 60 ya wanawake walio katika umri wa uzazi ilipofika mwaka 2015. Ni asilimia 32 tu ya wanawake walifikiwa. Lengo hilo limehishwa kwa ajili ya kufikiwa mwaka 2020.

Akisisitiza kuhusu umuhimu wa za uzazi hapa nchini, Dr. Faustine Ndungulile alisema kuwa “ufinyu wa bajeti umekuwa ikiwanyima wanawake wenye umri mdogo huduma za uzazi wa mpango ambazo ni muhimu kwa afya zao, watoto wao, na maendeleo yao na taifa. Wanawake wanaoanza uzazi katika umri mdogo na kuzaa kwa mfululizo wanakosa fursa za kujiendeleza kielimu, kiuchumi, na kijamii; na kuwafanya wasiweze kufikia upeo wa ndoto zao za kimaendeleo, hali ambayo pia huwapata watoto wao.”

KONGAMANO KUBWA LA AFYA KWA WOTE KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
WADAU wa sekta ya afya, watafiti, wanazuoni na wataalamu wa masuala ya bima, wanakutana jijini Dar es salaam kesho tarehe 4 Mei, 2017 kujadili suala la Afya bora kwa wote katika kongamano litakalofanyika katika hoteli ya bahari beach jijini dar es salaam.

Kongamano hilo kubwa kufanyika nchini linafanyika chini ya mwavuli wa ushirikiano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (Public Private Partnership) linafanyika katika kipindi ambacho taifa linajiandaa kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na uhakika wa kupata huduma za matibabu kupitia bima ya afya.

Mmoja wa waandaji wa kongamano hilo Dk. Heri Marwa kutoka Shirika la PharmAcess amesema kuwa jumla ya washiriki 250 kutoka makundi mbalimbali ya kijamii, utendaji na usimamizi na wawakilishi kutoka Serikalini wanatazamiwa kushiriki. Kongamano hilo limeandaliwa kwa pamoja kati ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini (TIRA) na Shirika la PharmAccess linalosimamia huduma ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa katika mikoa ya Kilimanjaro na Manyara kazi ambayo PharmAcess wanafanya kwa kushirikiana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika mikoa hiyo.

Kwa mujibu wa Dk. Heri lengo la kongamano hilo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali kuelekea afya bora kwa wote na umuhimu wa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada hizo. Amesema pia washiriki watapata fursa kubadilisha uzoefu katika maeneo muhimu ambayo ndio dira kuu ya kuelekea afya bora kwa wote yanayohusu; kuongeza uwigo kwa makundi mbalimbali hasa sekta isiyo rasmi, umuhimu wa huduma bora na masuala ya TEHAMA pamoja umuhimu wa masuala ya utafiti.

Nchi mbalimbali hasa barani Afrika zimekuwa zikikwama kutekeleza azma hii kutokana na kukosekana kwa utashi wa kisiasa. Bahati njema hapa nchini suala hili lina utashi mkubwa wa kisiasa. Kazi kubwa katika kongamano hili itakuwa ni kubaini matarajio na changamoto na kueneza mifano bora (best practises) inayotekelezeka wakati tukielekea kutekeleza azma hiyo ya afya kwa wote alimalizia Dk Heri na kuwakumbusha washiriki wote waliothibitisha kushiriki kuwahi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA , ATEMBELEA KIWANDA CHA SUKARI (TPC)

$
0
0
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo Kutoka  kwa,  Afisa Utawala wa TPC aliyeshika kofia  Bwana Jafari Ally  kuhusiana  na Shughuli zinazo endelea katika kiwanda cha Kutengeneza  Sukari  cha TPC  , Kushoto kwa Waziri Mkuu  aliyevaa shasti jeupe ni Meneja wa kiwanda  Bwana  Pascal Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni.
 Waziri Mkuu  Kassim  Majaliwa, akipata maelezo  Kutuko  kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Sukari cha (TPC) Bwana Robert  Baissac,  kuhusu mbegu za kisasa za Miwa zinazozalishwa  kitika  Shamba Darasa  la Kiwanda cha Sukari cha TPC Kilichopo  Mkoani Kilimanjaro Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akipata maelezo  kutoka kwa  Meneja wa Kiwanda cha Sukari (TPC) Bwana  Pascal Petiot  kuhusiana na Mitambo Mipya ya Kompyuta ambazo zimefungwa  ili kuongeza Ufanisi Katika Kiwanda  cha TPC Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
 Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa,  akiangalia Mitambo  mipya   inayofungwa  katika Kiwanda cha   kutengeneza  Sukari  cha  TPC, Kilichopo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  akisalimiana na kiongozi wa Chama  cha Wafanyakzi  wa kiwanda cha Sukari  TPC (TASIWU)  Bwana Bilali Omari, waliopo katikati aliyeva  Tisheti ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPC  Bwana  Robert  Baissac na Meneja wa Kiwanda hicho Bwana  Pascal  Petiot, Waziri Mkuu alitembelea Kiwanda  hicho hivi karibuni. PICHA NA PMO

Raia wa Kenya na Tanzania kizimbani kwa kusafirisha binadamu.

$
0
0
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.

Raia wa Kenya, Samson Mbaria Pirias maarufu kama Babaa, 38, na raia wa Tanzania, Lohelo Boniphace Mwabulanga anayejulikana zaidi kama Diblo, 43, wamepandishwa  kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha binadamu kutoka nchini Kenya kwenda Afrika Kusini kuwafanyisha kazi kwa lazima.

Mwendesha Mashtaka Wakili wa Serikali, Elia Athanas amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 4(1) (a) na (1) (2) (c) na 4 cha sheria ya kusafisha binadamu sura ya sita ya mwaka 2008.

Wakili Athanas amedai kuwa, Februari 28,mwaka huu, huko Chanika wilaya ya Ilala washtakiwa hao walikutwa wakiwasafirisha watu 11 kutoka Kenya kwenda Afrika Kusini kwa lengo la kuwafanyisha kazi kinguvu.

Aliwataja watu hao kuwa ni Dhaha Maliya All, Hassen Gales Omar, Ahmed Lobiso Abdi,Dhawil Ayantu Duri, Omar Yahye Mohammed, Hikma Ibrahim Omar, Istahil Ali Shukri, Rashid Omar Yusuf,Abdul Khalid Asiis, Abbdulah Sartu na Hassen Guled Omar.

Hata hivyo, washtakiwa hao wote wawili wamekana tuhuma hizo na wamerudishwa rumande kwa sababu shtaka linalowakabili la kusafirisha binadamu ni moja kati ya mashtaka yasiyo na dhamana.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi wa shauri hilo bado haujamalika. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 17,mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa tena.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AHITIMISHA MAADHIMISHO SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI DUNIANI, KITAIFA JIJINI MWANZA.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amehitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, yaliyofanyika kitaifa Jijini Mwanza.

Mongella amewasisitizia wanahabari kujikita zaidi katika weledi kwenye utendaji wao wa kazi ili kuondokana na migogoro inayoweza kujitokeza wakati wakitimiza majukumu yao.

Amewahimiza zaidi waandishi wa habari kujikita kwenye habari za uchunguzi na utafiti wa kina katika habazi zao huku akihimiza zaidi ushirikiano.
#BMGHabari
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) akifuatilia maadhimisho hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania, Salome Kitomari.
Rais wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Deogratius Sonkolo (kulia) na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri nchini TEF, Theophil Makunga (kushoto), wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkurugenzi wa Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini UTPC, Abubakar Karsan, akichangia mada kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kitaifa Jijini Mwanza.

WAANDISHI WATAKIWA KUTUMIA KALAMU ZAO VIZURI.

$
0
0
Na Nuru Juma & Husna Saidi- MAELEZO

Waandishi wa Habari nchini wametakiwa kuzingatia kanuni,sheria na taratibu za uandishi katika kuandika habari zitakazoleta umoja,mshikamano na maendeleo na siyo uchochezi ili kujenga jamii bora.

Hayo yamesemwa leo Jijini Mwanza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison George Mwakyembe kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Dkt. Mwakyembe aliongeza kwa kusema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa siku ya uhuru wa vyombo vya habari ambapo siku hiyo huwa maalum kwa wadau wa tasnia hiyo kukutana na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwa ni njia ya kujenga jukwaa la ushirikiano.

“Uhuru wa habari una ukomo wake hivyo ni muhimu kwa vyombo vya habari hapa nchini kuajiri watu wenye taaluma hiyo kwa kuachana na makanjanja ili viheshimike kwa kutoa taarifa zenye kuzingatia maadili ya uandishi”, alisema Dkt. Mwakyembe.

Alizidi kufafanua kuwa katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, kalamu ya mwandishi wa habari itetee ukweli na si mambo ya haramu kwa sababu ya siasa au rushwa ambayo huwa kichocheo cha uvunjifu wa amani.

Aidha aliitaka Idara ya Habari (MAELEZO) kuwa na utaratibu wa kukutana na wahariri kila mwezi ili kuweza kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili tasnia nzima ya habari nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Dkt. Hassan Abbasi alisema uandishi wa habari si biashara ya kawaida bali ni kazi yenye kuhitaji uweledi mkubwa hivyo waandishi wanatakiwa kufuata taratibu na sheria za uandishi.

TAASISI YA KILIMANJARO DIALOGUE YATAKA WANAHABARI KUTUMIA KALAMU ZAO KUDUMISHA AMANI NCHINI

$
0
0
 Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. 9PICHA NA RICHARD MWAIKENDA)
  Mdhamini wa Taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Habib Miradji (katikati) akiongoza mjadala jijini Dar es Salaam leo, kuhusu umuhimu wa wanahabari kuandika habari za kudumisha amani nchini ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Mjadala huo uliandaliwa na taasisi hiyo. Kutoka kulia ni Rais wa taasisi hiyo, Ali Akkiz na Mshauri wa masuala ya Habari, Felix Kaiza.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mshauri wa Masula ya Habari, Felix Kaiza akielezea umuhimu wa wamiliki wa vyombo vya habari kuweka utaratibu wa mafunzo ya ndani (In House Training) kwa waandishi wa habari ili kuinua weledi pia alishauri kuwepo na Exchange Program kati ya vyombo vya habari nchini na nje ya nchini jambo ambalo huwaongezea uwezo wanahabari.
 Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, Esther Zaramula akielezea kwenye mjadala huo jinsi alivyonufaika na mpango wa kubadilishana uzoefu
 Habib Miradji akisisitiza jambo wakati wa mjadala huo ambapo alifafanua zaidi umuhimu wa wanahabari kuandika habari kwa kufuata maadili na kusimamia kwenye ukweli.

Pia katika kongamano hilo waliwaasa wanahabari kutojiingiza katika mkumbo wa kuingizwa mifukoni mwa wanasiasa na matajiri kwa kuandika habari za kuwasifia wao badala ya maslahi ya wananchi.
 Mwandishi wa habari, Ezekiel Kamwaga  akielezea umuhimu wa wanahabari kujiendeleza kielimu pamoja na vyombo vya habari kubadilika kwa kwendana na kasi ya mabadiliko ya kizazi hiki cha maendeleo ya teknolojia ya habari.
Rais wa taasisi ya Kilimanjaro Dialogue, Ali Akkiz aktoa shukrani kwa wanahabari walioshiriki kwenye mjadala huo uliofanikiwa.

SERIKALI YATOLEA UFAFANUZI SUALA LA VYETI FEKI

NAIBU SPIKA WA BUNGE AKUTANA NA UGENI KUTOKA JHPIEGO

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg. Jeremie Zoungana, aliyekuja kuzungumza nae na kubadilishana uzoefu wa kazi, kabla ya kuanza kikao kilichofanyika leo Ofisini kwake Mjini Dodoma
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akizungumza na ugeni uliomtembelea leo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ukiongozwa na Mkurugenzi Mkazi wa JHPIEGO nchini Tanzania Ndg. Jeremie Zoungana (wa pili kulia).
Naibu Spika wa Bunge, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi wa Mradi wa USAID wa Boresha Afya, Ndg. Dustan Bishanga (wa pili kushoto) akizungumza leo katika kikao kilichofanyika Ofisini kwake Mjini Dodoma. (PICHA NA OFISI YA BUNGE).

MSONDO VS SIKINDE KUWASHA MOTO MEI 20, TRAVENTINE JIJINI DA

$
0
0
Mratibu Abdulfareed Hussein akiwa katika picha ya pamoja na waimbaji wa bendi za  DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" wakijiandaa na mpambano wa kumsaka Mkali nani Mei 20 mwaka huu.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

HISTORIA inaendelea tena kuandikwa baada ya bendi kongwe mbili za muziki wa Dansi nchini DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" zitakutanishwa tena katika jukwaa moja kumtafuta nani mkali wa kulisakata rumba Mei 20 mwaka huu.

Bendi hizo kongwe zitakutana tena katika jukwaa  moja  na kumtafuta nani mkali huku kila upande ukitamba kumgaragaza mwenzake na kuibuka kidedea katika mpambano huo.

Pambano hilo linatarajiwa  kufanyika Mei 20 Mwaka huu katika ukumbi wa Traventine Magomeni huku mashabiki wa kila upande wakiombwa kuja kuhudhuria kwa wingi kuwaona wakali hao huku burudani za  nyimbo za zamani zikiratajiwa kutawala kwenye usiku huo.

Akizungumza kuelekea pambano hilo, mratibu Abdulfareed Hussein alisema mpambano huo wa nani zaidi utamuliwa na mashabiki wa dansi watakaojitokeza siku hiyo na zaidi kutakuw ana zawadi ambayo ni siri itakayotolewa siku hiyo.

Alisema kiingilio cha pambano hilo kitakuwa ni Sh. 10,000 ili kuwapa nafasi wadau wa dansi kushuhudia na kutoa maamuzi ya nani zaidi kati ya bendi hizo mbili.

"Hili pambano ndio litakata mzizi wa fitna, ambapo mashabiki ndio wataamua nani zaidi kati ya Msondo au Sikinde kwani ni muda mrefu sana hawajakutana jukwaa moja " alisema.

Wakati huo huo Mmoja wakilishi wa Sikinde, Abdallah Hemba alisema wamejiandaa vizuri kutoa burudani na kuhakikisha kwamba wako vizuri kuliko Msondo.

" Hawa jamaa wametukimbia sana, hivyo kila tunapotaka kukutana nao wanakuwa na safari naona Mei 20 ndio mwisho wao," alisema.

Nao Meneja wa Msondo, Said Kibiriti alisema wamejiandaa vyema hivyo katika pambano hilo wataimba nyimbo mchanganyiko na zaidi kambi hyao itakuwa Pemba na wanawaahidi mashabiki wa bendi yao kuja kwa wingi.

" Tutaimba nyimbo mchanganyiko, pia tutaimba nyimbo zetu mpya, tunaamini mpambano huo ndio utaweza kuamua nani kati yao ni zaidi," alisema Kibiriti.
 Mratibu Abdulfareed Hussein akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mpambano wa kumsaka mkali wa muziki wa dansi baina ya  DDC Mlimani Park "Sikinde Ngoma Ukae" na OTTU Jazz "Msondo Ngoma" utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Pembeni ni viongozi na waimbaji wa bendi hizo kulia ni Abdallah Hemba  kutoka Sikinde na kulia ni Meneja wa Bendi ya Msondo Said Kibiriti. 
 Muimbaji wa bendi ya Sikinde Abdallah Hemba akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu. Kushoto ni  Mratibu Abdulfareed Hussein.
  Meneja wa Bendi ya Msondo Said Kibiriti akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mpambano huo baina yao na Msondo utakaofanyika Mei 20 mwaka huu akiwa sambamba na waimbaji wa timu hiyo Romario na Juma Katundu.

Mnufaika wa Airtel Fursa baada ya kupigwa tafu na Airtel Fursa

$
0
0

· Mnufaika wa Airtel FURSA bidhaa zake ziko sokoni mikoa zaidi ya mitano

Mradi wa Airtel Fursa umeendelea kufanikiwa kwa kuendelea kuwezesha vijana nchini ambapo mmoja kati ya waliowezeshwa mwaka jana Bi Threria Maliatabu mkazi wa Mbagala jijini Dar es Saalam ameelezea jinsi mradi huo ulivyomuwezesha kukuza kipato na kupata mafanikio ya kuanza kujenga nyumba yake binafsi, kujinunulia shamba la eka 2 huku akiwaasa vijana wenzake nchni na wale wote waliowezeshwa na Airtel FURSA kuchangamkia fursa hizi pindi zinapotokea.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es saalam , Bi Maliatabu ambaye anajishughulisha na biashara ya uchoraji wa picha za sanaa alisema “ najivunia sana kuwa mmoja kati ya vijana walioshikwa mkono na Airtel Fursa kwa sababu program hii imeweza kunitoa kutoka niliopokuwa hadi kufika kwenye haya mafanikio niliyo nayo leo. 

 Kwakweli nimekuwa na mafanikio makubwa sana ikiwemo kuboresha kiwango cha bidhaa zangu , nimefanikiwa kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya vyumba vinne na pia nimeweza kukunua shamba la eka 2 Mkuranga mkoa wa pwani. lengo langu ni kuanzisha shughuli za kilimo ili kutanua wigo wa biashara yangu lakini pia kuendelea na shughuli yangu ya uchoraji nayoifanya kwa sasa”

Aidha Maliatabu alifafanua kuhusu changamoto mbalimbali katika biashara ikiwemo masoko ya nje , usafiri wa kusambaza bidhaa zake huku akieleza kuwa baadhi ya changamoto hizi ameshaanza kuzishughulikia na kuomba wadau mbalimbali kuweza kumsaidia.

“Nimeweza kuongeza masoko yangu na kufikia masoko ya Zanzibar, Moshi , Arusha na Dar, na kwa sasa niko katika mchakato wa kupeleka bidhaa zangu nchini Sweeden na Italy. Mipango hii ikikamilika kwakweli nitakuwa nimefurahi kufikia malengo yangu na naamini nitafanya vizuri zaidi na kukuza kipato changu zaidi. Natoa wito kwa vijana wenzangu kujituma na kufanya kazi kwa bidiii na kutafuta fursa mbalimbali na kujikita kwenye ujasiriamali badala ya kusubiri ajira ambazo zimekuwa ni changamoto”.

Akiongea kuhusu mafanikio haya, Meneja Huduma kwa Jamii, Bi Hawa Bayumi alisema , tunafarijika na kujisikia fahari kuona jinsi gani program hii imeweza kuwainua vijana hawa wajasiriamali wenye nia ya kukuza kipato na kufikia malengo yao. Theresia Maliatabu ni mfano wa kuigwa, alipowezeshwa alijiongeza na kufanya kazi kwa juhudi kubwa na maarifa. Nawaasa vijana wajitume na kuchangamkia fursa kama hizi zinapojitokeza wazitumie vizuri ili kuleta tija kwenye maisha yao, familia zao na taifa kwa ujumla.”

Theresia Maliatabu ni moja kati ya vijana waliochagulia kuwa kati ya wafanyabiashara wadogo wadogo watakaonufaika na mpango wa Airtel FURSA na kupatiwa vitendea kazi zikiwemo , ubao wa kuchorea, vifaa vya kuchorea na computer, mafunzo ya ujasiriamali na kutengenezewa kipindi maalumu cha Television kilichoonyesha safari yake katika biashara ambavyo vimemsaidia kukuza biashara yake. Airtel kupitia mpango wake wa Airtel fursa imewezesha vijana takibribani 5000 kwa kuwapatia mafunzo ya ujasirimali na baadhi yao kupata vitendea kazi ili kuboresha biashara zao.
Theresia Maliatabu, mnufaika wa mradi wa Airtel Fursa akimsikiliza mteja wakati alipohudhuria maonyesho ya bidhaa na kuonyesha kazi ya uchoraji wa picha za Sanaa anazozifanya hivi karibuni.

BAADHI YA WAKAZI WA KINONDONI WALALAMA NYUMBA ZAO KUZINGIRWA NA MAJI KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA.

$
0
0
Wakazi wa Kinondoni  Mahakamani wamelalakia maji yaliyozingira nyumba zao kutokana na baadhi ya wakazi hao kujenga katika mkondo wa maji.

Akizungumza leo mkazi wa eneo hilo Bi. Khadija Hamis amesema kutokana na mvua za  masika zinazoendelea kunyesha wanapata adha kubwa ya maji hayo yanayotuama kwenye eneo hilo.

Amesema kuwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamezingirwa na maji kwa wiki mbili sasa na hakuna chochote kinachofanyika.

Aidha amesema kutokana na hali hii kuendelea ,wanaiomba serikali kutatua tatizo hili mara baada ya kuisha masika.
 Mvua zinazoendelea  kunyesha  maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es Salaam iliyoanza kunyesha wiki iliyopita, zimesababisha maafa, uharibifu wa miundombinu ya baarabara pamoja na baadhi nyumba katika eneo la Kinondoni Mahakamani kuzungukwa na maji ya mvua  jijini Dar es Salaam.
 Mwanafunzi akikwepa   dimbwi la maji machafu ya mvua kama yanavyoonekana pichani leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmauel Massaka,Globu ya jamii.

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images