Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 119 | 120 | (Page 121) | 122 | 123 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Na Father Kidevu Blog.

  MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.

  Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.

  Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.

  Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.

  "Marehemu Wende, anataraji kuzikwa Makaburi ya Kinondoni kesho  lakini kabla ya mazishi kutakuwa na ibada itakayofanyika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kinondoni, "alisema Lwendo.

  Lwendo amesema ibada hiyo itaanza majira ya saa 8:00 mchana ambapo pia ndugu jamaa na marafiki watapata wasaa wa kutoa heshima za mwisho kwa marehemu Wende.

  Mmmoja wa wanafunzi wa IFM, Ester Boswell, ambaye walikuwa wakishi chumba kimoja na marehremu huko Kigamboni ameelezea msiba huo kuwa ni pigo chuoni kwao na kwake kwani Marehemu alikuwa ni rafiki yake mkubwa si chuoni lakini hata kabla hawaja jiunga na chuo hicho.

  Boswell amesema kuwa Marehemu alikuwa ni Rais wa taaasisi ya Wanafunzi wa IFM ijulikanayo kama AIESEC na alikuwa mhim,ili mkubwa wa taasisi hiyo.

  Aidha amesema kuwa hadi sasa binafsi haamini kifo cha Wendi, huku akielezea kuwa Marehemu alikuwa ni mtu mcheshi na kuogelea ilikuwa ni moja ya vitu vikubwa anavyo vipenda.

  "Marehemu alikuwa mpenzi kumbwa sana wa kuogelea na siku zote alikuwa anapenda kwqenda kuogelea na hata anapokuwa mpweke hosteli huamua kwenda Beach kuogelea na siku ya tukio aliniaga kuwa anaenda kuogelea na wanafunzi wengine wakiwapo wazungu ambao wapo katika kubadilishana uzoefu wa kimasomo," alisema Boswell.

  Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam ukisubiri maziko.

  0 0

  Nyumba ipo MBEZI GOIG, mita chache kutoka Barabara Kuu (Bagamoyo Road), upande wa kushoto kama unatokea Mbezi Tangi Bovu. Ina vyumba 3 vikubwa vinavyojitosheleza (3 Master Bedrooms), Two kitchens, Two Sitting Rooms, Garage ya kuweka magari na Fencing.

  HAKUNA DALALI. KUJUA BEI NA MALEZO MENGINE, TAFADHALI PIGA SIMU NAMBA:
  +255 0657 803 139

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais wa Nigeria, Isaiah Balat, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikwe, jiji Abuja leo Julai 14, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa 12 wa Afrika unaojadili Magonjwa ya Ukimwi, Malaria, Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ambukizi, unaotarajia kuanza kesho Julai 15 na kumalizika Julai 16. Kushoto ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal. 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mshauri Mkuu wa Makamu wa Rais wa Nigeria, Isaiah Balat, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nnamdi Azikwe, jiji Abuja leo Julai 14, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria mkutano Mkuu wa 12 wa Afrika unaojadili Magonjwa ya Ukimwi, Malaria, Kifua Kikuu na Magonjwa mengine ambukizi, unaotarajia kuanza kesho Julai 15 na kumalizika Julai 16. Nyuma yao ni Mke wa Makamu, Mama Asha Bilal. Picha na OMR

  0 0

   The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (centre) cuts a ribbon to launch the Eximite Magazine, a quarterly in-house publication produced by the bank during an event held in Dar es Salaam at the weekend.Looking on at the left is the bank’s Chief Executive Officer Dinesh Arora and the bank’s Managing Director Anthony Grant (right). 
   The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (centre) displays a dummy magazine for the Eximite Magazine, a quarterly in-house publication produced by the bank during an event held in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the left is the bank’s Chief Executive Officer Dinesh Arora and the bank’s Managing Director Anthony Grant (right). 
   The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (right)  stresses a point to the bank’s staff and media during an event held in Dar es Salaam at the weekend to unveil the Eximite Magazine, a quarterly in-house publication produced by the bank. Looking on at the left is the bank’s Managing Director Anthony Grant . 
  The Exim Bank Board Chairman Yogesh Manek (centre) stresses a point bank’s staff and media during an event held in Dar es Salaam at the weekend  to unveil the Eximite Magazine, a quarterly in-house publication produced by the bank. Looking on at the left is the bank’s Chief Executive Officer Dinesh Arora and the bank’s Managing Director Anthony Grant (right). 
  =======   =======  ========
  Exim Bank re-affirms commitment to support Tanzania’s economic development

  By Staff Reporter

  EXIM Bank Tanzania has re-affirmed its commitment to support economic development in Tanzania as the country braces for more investment opportunities.  Speaking during the launch of the first issue of the Eximite Magazine, a quarterly publication by the bank, the Exim Bank Tanzania 

  Board Chairman Yogesh Manek noted the increased FDI inflows in Tanzania and the East African region will create more opportunities for the banking sector adding that his bank will continue playing a pivotal role in supporting various investment initiatives across the country. “Reports have shown that EAC economies including Tanzania brace for more Foreign Direct Investment (FDI) inflows. Banks have a major role to play as financial intermediaries.

  “Exim Bank will play an important role in supporting various investment activities as they unfold. Our focus is now to ensure that our bank offers unmatched banking services that will help us to embrace more investment opportunities within the years to come,” Manek said.

  The Exim Bank Managing Director Anthony Grant during the event said the bank is set to continue on a confident programme of deliberate expansion and is preparing to open additional branches across the country.

  “We are set to within weeks to open a new state-of-the art corporate branch in Arusha and another branch in Tabora at the end of the year or very early next year as part of our expansion strategy. The strategy wills geographic reach for our services as we also deepen our delivery channels with agency banking, mobile banking and internet banking options,” Grant said.

  The Exim Bank Senior Manager - Training & Development Priti Punatar during the event said the magazine will create for staff another platform to share and celebrate professional and personal achievements.     Punatar said her bank is committed to reinforcing effective communication within the bank and recognizes the importance of keeping staff and stakeholders up to date on current events in the organization.

  “The ‘EXIMITE’ Magazine, loaded with wonderful photos, will be released quarterly and all staff will engage in conceptualization and development of each issue in house, giving the magazine a fresh and unique look in every quarter.  “We believe ‘EXIMITE’ magazine will be an efficient communication tool that will accomplish many goals that include educating, informing, as well as entertaining,” she said.

  She added that EXIMITE magazine aims to unify the Bank’s family members who are challenged by Exim Bank’s geographical spread across Tanzania and in two other countries, and will build relationships with our customers.

  0 0

   Kutoka kushoto ni : Eng. Christopher Sayi  ( Katibu mkuu Wizara ya Maji ), Godfrey Matola, Mh. Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa Maji ) , Reinhard Paulsen , Ully Mbuluko, Moses Haule, Eng. Christian Gunner ( Kutoka Hamburg Wasser ) , Mh. Christopher Mvula ( Kaimu Balozi wa Tanzania Ujerumani ) na Godwin Msigwa .  Wakipiga picha ya pamoja baada ya Hotuba kutolewa na Waziri wa maji Tanzania na pia kutoka upande wa wenyeji Hamburg Wasser.  ( Picha : Hamburg, Ujerumani )
  Prof. Jumanne Maghembe ( Waziri wa maji ) akisisitiza jambo kwa Petra Hammelman  ( Balozi wa Heshima wa Jamhuri ya Tanzania – Hamburg ) baada ya kutoa Hotuba ndani ya jengo la Seneti Hamburg . ( Picha : Hamburg, Ujerumani ).Dar es Salaam ni moja ya majiji ambayo yanakua kwa kasi kiuchumi. Hii ni kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, uwekezaji, Viwanda nk. Haya yote yamekuwa yanachangia kwa sehemu kubwa ongezeko la uhitaji wa maji na inakadiriwa kuwa kwa miaka 15 ijayo uhitaji utaongezeka mara mbili zaidi.

  Inakadiriwa kuwa zadi ya asilimia  50 ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam hawajafikiwa na huduma ya maji ya bomba. Matumizi ya maji ya kisima kwa jijini Dar es Salaam ni tatizo kutokana na uchafuzi wa mazingira utokanao na Viwanda, maji taka na taka za wakazi wa jiji hilo.

  Hii sasa yawezekana ikawa neema kwa wakazi wa jiji hilo kwa ushirikiano huu uliongiwa baina ya Wizara ya Maji na Idara ya Maji ya hapa Hamburg, Ujerumani  iitwayo Hamburg Wasser  .  Ushirikiano huu utalenga kusaidia tatizo la maji katika jiji hili la Dar es Salaam.

  0 0

   Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akizungumza katika majumuisho ya ziara yake  ziara ya mkoa wa Njombe, Julai  14, 2013.  Kulia  ni  Mkuu wa mkoa wa Njombe, Kapteni Msangi. Na wa wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo, Deo sanga.
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alipopokea taarifa ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye Ikulu Ndogo ya Songea kwa ziara ya siku nane mkoani humoJulai 14,2013.Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Thabit Mwambungu. 
   Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akizungumza wakati Waziri Mkuu, Mizengo  Pinda alipopokea taarifa ya mkoa wa Ruvuma baada ya kuwasili kwenye Ikulu Ndogo ya Songea kwa ziara ya siku nane mkoani humoJulai 14,2013.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mkuu wa wilaya ya Njombe, Sarah Dumba baada ya kumaliza ziara ya kikazi mkoani Njombe Julai 14, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ametembelea kambi ya kusaidia watu wenye ulemavu wa kusikia katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam asubuhi hii.  Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa hiyo Taasisi  hiyo ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.

  Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation Bwana Bill Austin  Starkey amesema tayari huduma hiyo imeshatolewa katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro.

  “Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika juhudi zetu.

  Madaktari wa kitanzania walioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.


  0 0

  Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar .
  Naibu waziri wa kilimo na maliasili Zanzibar Mtumwa Kheir Mbarak  amesema wakulima wa Muyuni wamepata athari kubwa katika mabonde yao ya mpunga, jambo ambalo limepelekea athari kubwa na kukatisha tamaa kupata mavuno mazuri mwaka huu.
  Amesema jambo hilo lilisababishwa na wakulima kulimiwa mapema na kupanda mapema ili kuwahi msimu huku jua kali likiwa limetawala baada ya mvua za mwanzo za kupandia kunyesha.
   Hayo ameyasema leo huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar,wakati akijibu suala la Mwakilishi wa jimbo la Muyuni Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua serikali inampango gani wa kuwasaidia wakulima wa muyuni walioharibikiwa na kilimo hicho msimu huu.
  Aliseam ni kweli ilitokea kwa wakulima hao lakini alisema  kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar badala  ya kuona sehemu kubwa ya mpunga katika bonde hilo umeathirika kwa jua kali kilichofanyika ni kuwapa mbegu fupi fupi ili kuwahi msimu huo.
  “Walipewa mbegu fupifupi ilikuwasaidia kuwahi msimu huu usijemalizika”.alisema Mtumwa Kheir .
  Aidha alifahamisha kuwa pamoja na msaada wa mmbegu  mpunga huo ulio kufa, baadhi ya mashamba yalionekana kupata uhai na kuleta matumaini  ya kupatikana mavuno japo sio makubwa badala ya kuja mvua za mwanzo wa masika zilipoanza kunyesha hapo mwanzoni  mwa mwaka huu.
   Alisema halihiyo iliwapa moya wakulima kwavile badhi ya mashamba yalionekana kupona.
  Aidha alisema kwa yale mashamba yalio kufa kabisa hayakuwezekana kuburuga tena  kutokana na mvua zilikuwa tayari zinanyesha kwakasi. wizara ya kilimo iko tayari kuwapatia mbegu za makongo wakulima hao waliokua  tayari kulima mpunga huo wa kupandikiza.
   Hata hivyo wizara ya kilimo na maliasili imetayarisha mpango mkuu wa kitaifa wa umwagiliaji kwa mabonde yote yenye ukubwa wa hekta 8521 katika mpango huu bonde la Muyuni limo na tayari limeshafanyiwa michoro na kuekewa mipaka, mpango huu unatarajiwa kuanza mwaka huu kwa kupitia mkopo kutoka EXIM BANK ya Korea na msaada wa USAID na KOICA.
  Pia amesema serikali ya Vietnam ambayo inatarajia kusaidia utaalamu wa kilimo pamoja na fedha kwa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ili kuweza kuboresha kilimo.
  Naibu huyo  aliwaomba wakulima kuwa wastahamilivu hadi mpango huo wa umwagiliaji maji utakapokamilika.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na mmoja wa wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni akiwa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapongeza wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni baada ya kupatiwa vifaa na  mwanzilishi na mkuu wa Taasisi ya Starkey Hearing Foundation Bw. Bill Austin alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
    Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanafunzi wa shule ya walemavu wa kusikia ya  Buguruni  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013. 
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Bw. Sholloh Challi, katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa mstaafu,  alipohudhuria shughuli ya utoaji wa vifaa vya kuongeza usikivu kwa walemavu wa kusikia katika viwanja vya hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo Julai 15, 2013.PICHA NA IKULU. 

  0 0

  KWA SABABU:- Sisi wananchi hatujashirikishwa kupitia mjadala wa Bunge kuhusu kodi hii kwani Waziri wa fedha hakusoma hiki kipengele wakati wa hotuba yake na tulikosa taarifa mpaka baada ya kupitishwa kwa sheria ya kodi hii.


  KWA SABABU:- Kodi hii inamkandamiza mtanzania wa hali ya kawaida na wa hali ya chini ambao ni 67% ya wananchi wanaoishi chini ya kipato cha dola 1.25 (shs 2,000) kwa siku. Takwimu zinaonyesha kuwa kati wa wamiliki wa laini za simu milioni 22, milioni 8 wanatumia chini ya shilingi 1,000 kwa mwezi. Kuwaongezea mzigo wananchi hawa kwa kiwango ambacho tayari wanashindwa kumudu ni kuwanyima kabisa fursa ya kutumia huduma hii muhimu.

  KWA SABABU:- Kodi hii haifuati misingi ya kulipa kwa kadri ya matumizi na ni kodi kandamizi inayowatoza wamiliki wa laini ya simu wote kiasi kimoja bila kuzingatia kiwango cha matumizi. Hii inamkandamiza mwananchi wa hali ya chini kwa kumlazimisha kulipa kiwango kikubwa cha kodi kulingana na mapato yake. Tukichukulia mfano wa mtu anayetumia shilingi laki tano kwa mwezi kama muda wa maongezi na yule anayetumia shilingi elfu tano - na tukilinganisha uwiano wa malipo haya na matumizi yao – basi yule anayetumia shilingi laki tano analipa 0.2% ya matumizi yake, ila yule anayetumia shilingi elfu tano anatozwa 20% ya matumizi yake.

  KUTOKA KWA MDAU BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA ZAIDI.

  Kaka tafadhali ninaomba utuwekee patition hii kwenye blog yako ili watanzania washiriki katika kuweka sahihi katika kupinga zuio la ongezeko la kodi katika line za simu. Asante

  0 0

  Kutoka Kulia niMwenyekiti wa TEHAMA Class na Msanii wa Kizazi
  Kipya Bongo Flave, Inspector Haorun aka Babu akiwa na watalaamu wa
  TEHAMA(ICT) wapili ni Diana Mtambalike ambaye ni Katibu wa kampuni
  hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Fahamu Campany ambao ndio waandaji na
  watoaji wa elimu ya TEHAMA kwa shule za msingi Bw, Mstafa Rubunda
  ,Mtalamu wa maswala ya TEHAMA, na Meneja wa Ufundi wa Fahamu Campany.Yusuph Kannokole wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizaka semina ya Viongozi  ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya semina ya wasanii zaidi ya 100.
  =========   =======  =======
  Kampuni ya Fahamu inayojihusisha na utoaji wa elimu Tehama( ICT) kwa
  shule za msingi jijini Dar es Salaam, imeamua kuingia ndani zaidi
  katika kutoa elimu kwa shule za msingi kwa kushirikiana na wasanii wa
  muziki wa kizazi kipya bongo freva na wasanii wa filam nchini
  .

  Akizungumzia umuhimu wa utoaji wa elimu hiyo ya TEHAMA kwa shule za
  msingi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Bwana Mustafa Rubunda alise ameona kuna umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa watoto wa shule za msingi kuanzia darasa la pili hadi la saba hii ni kutokana na
  changamoto ya mabadiliko ya kisayansi na teknolojia amba vijana hao
  watakuwa na uwezo wa kiubunifu pamoja na kibiashara.


  Pia alisema mafunzo hayo yatawafanya wanafunzi kujua teknolojia
  nini,umuhimu wa habari,matumizi ya mawasiliano,huwa wepesii wa kuelewa na kuwa wabunifu hii itawafanya wanafunzi kuendana na mfumo wa Sayansi na Teknolojia itakayowawezesha  kuingia katika ushindani zaidi na wanafunzi wenzao wa Afrika mashariki,na Duniani kwa ujumla

    Mstafa alisema kuwa ili kuhakikisha lengo linakamiliaka Kampuni yake
  ya Fahamu imeamua kuandaa semina kwa wasanii mbalimbali zaidi ya 100, ambao wataongozwa na Msanii mkongwe Inspector Haorun aka babu,ambaye ndiye Mwenyekiti wa TEHAMA CLASS,na mwakilishi wa wasanii.


  Semina hiyo inategemea kufanyika Mwezi huu jijini Dar es Salaam,
  ambapo itawajumuisha wasanii ,wanafunzi wa sekondari, pamoja na wa
  Vyuo Vikuu  lengo la kuwa jumuisha katika semina ni kuona umuhimu wa
  kuweza kuwasaidia wadogo zao katika kuhakikisha wanakuwa watumiaji wa TEHAMA ambayo sasa ndiyo iliyobeba Teknolojia ya Habari na
  Mawasiliano.

   
  Kulingana na uzoefu ambao tayari Fahamu Company  kutokana na kutoa
  mafunzo kama hayo kwa shule za msingi za Mapinduzi na Rutihinda
  zilizopo Kigogo katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam,
  alisema kuwa watoto watapata fursa ya kusoma kwa bidii kwani hata
  wenzao wamekuwa na morali mkubwa wa kujifunza masomo hayo.

  Kwa upande wa serikali kupitia TAMISEMI, wamekuwa bega kwa bega kwa kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Fahamu Campany kwa ajili ya kutoa elimu hiyo kwa watoto wa shule za msigi nchini.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na uongozi wa Benki ya Maendeleo ya TIB uliofika
  Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na vitega uchumi. miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya Maendeleo ya TIB, Bw Peter Noni, Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 13, 2013. Bw. Noni na ujumbe wake walifika Ikulu kumwelezea Rais Kikwete mipango na mikakati kabambe ya kuijenga upya benki hiyo iliyokuwa ikijulikana kama Tanzania Investment Bank (Benki ya Rasilimali Tanzania) ikiwa ni pamoja na miundo mbinu na upanuzi wa wigo wa biashara.

  0 0

    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mfalme Mswati wa Swazland (ii) wakati walipokutana kwenye Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Katikati yao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Mahadhi (kulia) ni Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Seif Rashid. 
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa na baadhi ya Viongozi wenzake wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Gudluck Jonathan, ulioanza leo Julai 15, 2013 mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika. Picha na OMR 


  0 0

  Proxy War au Proxy Warfare ni vita inayopiganwa kwa kupitia sehemu nyingine. Katika vita 'ya kawaida' mapigano huwa kati ya nchi na nchi.Kwa mfano, Vita ya Kagera ilkuwa kati ya Tanzania na Uganda, na mapambano yalitokea katika nch zote mbili.

  Katika proxy war hali ni tofauti. Nchi A inaweza kupigana vita na nchi B katika nchi C.Yaani kwa ufasaha zaidi, kwa mfano, kuna mapambano katika nchi C kati ya jeshi la nchi hiyo na waasi, kisha nchi A inapeleka askari wake kuilisaidia jeshi la serikali la nchi C, na nchi B inapeleka askari wake (au inasaidia kwa siri) kusaidia waasi wanaopigana na serikali ya nchi C.

  Naomba ieleweke kuwa mie sio nabii wa waangamizi, kwa kimombo 'prophet of doom.' Ninachoongelea hapa kinatokana tu na hali halisi ilivyo kwenye mapigano yanayoendelea nchi DRC kati ya jeshi la Serikali ya nchi hiyo na kikundi cha waasi cha M23.

  Nchi yetu imetoa wanajeshi kadhaa kushirikiana na Malawi na Afrika Kusini kuunda kikosi cha kulinda amani nchini DRC. Lakini kuna taarifa kuwa waasi wa M23 wanapewa sapoti na Rwanda (kama ni kweli au la,mie sina hakika...lakini lisemwalo lipo...kwanini Rwanda ituhumiwe na si Kenya au Msumbiji?)

  Sasa tukiangalia hali ya uhusinao kati ya Tanzania na Rwanda katika siku za hivi karibuni, na tukijikumbusha kauli ya Rais Paul Kagame kuwa "atamsbiri (Rais Jakaya) Kikwete mahala mwafaka kisha mtandike" kuna uwezekano "mahala hapo mwafaka" kuwa ni DRC. 

  Kwanini ninasema hivyo? Uwezekano wa Rwanda kuivamia Tanzania au Tanzania kuivamia Rwanda ni mdogo sana,kutokana na sababu mbalimbali. Lakini nchi hizo mbili zinaweza 'kupigana vita kirahisi' kupitia mapigano yanayoendelea kati ya Jeshi la DRC linalosaidiwa na 'Kikosi cha Kimataifa' (kinachojumuisha Jeshi la Tanzania) na waasi wa M23 (wanaodaiwa kusaidiwa na Rwanda.)

  Vyovyote itakavyokuwa, vita ni kitu kibaya, natunapaswa kuombea kistokee kwa gharama yoyote ile.Mwanafalsafa mahiri wa 'Sanaa ya Vita' (Art of War), Mchina SUN TZU anatahadharisha kuwa "vita ni suala la uhai na kifo, barabara inayoelekea kwenye usalama au maangamizi..."

  Kuna wanaojidanganya kuwa Rwanda "ni kijinchi kidogo kisicho na uwezo wa kupambana na Tanzania." I wish wangekuwa sahihi.Kwa mujibu wa SUN TZU, ushindi katika vita yoyote ile unategemea sana matumizi ya mashushushu (wapelelezi) wa ndani na wa nje.Hivi tunafahamu kuwa tuna Wanyarwanda wangapi Tanzania ambao wapo mahsusi katika kufanikisha azma yoyote ile ya nchi yao?Kwa maafisa wetu uhamiaji ambao bia mbili tatu tu wapo tayari kumpa mtu passport ya Kitanzania, tuna maadui wangapi wanaotengeneza idadi yetu kukaribia milioni 50? 

  Soma hapa http://suntzusaid.com/book/13 kufahamu zaidi kuhusu matumizi ya mashushushu katika vita, kwa mujibu wa SUN TZU.(na jaribu kupigia mstari uhusiano wetu wa Malawi na uwezekano wao kuwa mojawapo ya aina hizo za mashushushu)

  Anyway, kama nilivyobainisha hapo awali, mie sio nabii wa majanga.Ningependa sana askari wetu waliokwenda huko DRC watimize jukumu lao haraka na kurejea nyumbani wakiwa salama WOTE. Nilichoeleza kuhusu PROXY WAR ni uchambuzi tu unaozingatia hali halisi.

  0 0

   Mgeni rasmi, Rais Jakaya Kikwete akizindua huduma mpya ya Benki ya Posta iitwayo TPB POPOTE mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Kushoto ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kulia kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.
  Rais Jakaya Kikwete akijaza fomu yake ya huduma hiyo mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha Dkt.William Mgimwa, Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya na kushto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo Bw.Moshingi wakishuhudia tukio hilo adhimu kabisa.

   Rais Kikwete akipewa maelezo mafupi namna ya kuitumia huduma hiyo ya TPB POPOTE kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Benki ya Posta.
    Rais Jakaya Kikwete akikabidhiwa kadi yake mpya ya huduma mpya TPB POPOTE  na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki  ya Posta Bw.Moshingi ,mara baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema leo .
    Mgeni rasmi,Rais Kikwete akikabidhiwa zawadi kut0ka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Posta,Profesa Lettice Rutashobya 

  Picha pamoja.
  Rais Jakaya Kikwete akiondoka mara baada ya kuzindua huduma mpya ya TPB POPOTE iliyozinduliwa na Benki ya Posta mapema leo mchana kwenye hotel ya Serena jijini Dar ,hafla hiyo imewakutanisha wadau mbalimbali wa mambo ya kibenki na wengineo, lengo kuu ya uzinduzi wa huduma hiyo ikiwa ni kuweka na kutoa  fedha kupitia Mawakala wa Benki ya Posta nchini Tanzania.

  0 0

   Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akikabidhiwa mfano wa hundi na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire, kushoto kwake ni mama mdogo wa Blanca, Mwalimu Theresia Masashua kutoka Turiani, Bianca ni mshindi wa tatu kujishindia shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
  Mshindi wa shilingi milioni moja wa shindani la Winda na Ushinde Bi. Blanca Maliti (katikati) mkazi wa mjini Morogoro akifurahia mfano wa hundi pamoja na familia yake baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Mauzo wa Serengeti Breweries kanda ya kati Octavian Migire, kushoto kwake ni mama mdogo wa Blanca, Mwalimu Theresia Masashua kutoka Turiani, na Dada yake. Bianca ni mshindi wa tatu kujishindia shilingi milioni moja katika promosheni hiyo ya Winda na Ushinde inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

  0 0

   Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohammed Bahari(katikati) akizungumza na vyombo vya habari juu ya Juhudi za Serikali katika kuchangia Maendeleo katika ya Sekta ya Mifugo na Uvuvi kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana, kushoto ni Mkuu wa Idara ya Uzalishaji na Masoko Bi. Anunciata Njombe kutoka Wizara hiyo na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
   Baadhi ya waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya  habari nchini wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini dar es salaam jana.
  PICHA ZOTE NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

   Msemaji wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Mohammed Bahari akiwaeleza waandishi wa habari namna bora ya utunzaji wa ngozi na madhara ya upigaji mihuri ya moto katika ngozi kama alama kwa wafugaji kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana.
   Mkuu wa Idara ya Uzalishaji na Masoko Bi. Anunciata Njombe wa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuchangia Maendeleo ya sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana, kulia ni Msemaji wa Wizara hiyo Dkt. Mohammed Bahari.
  Mkurugenzi wa Idara ya Huduma Mifugo kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dkt. Gopray Nsengwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuchangia Maendeleo ya sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari jijini Dar es salaam jana.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, baada ya mazungumzo yao walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi, UNAIDS, Michel Sidibe, wakati walipokutana katika Mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan na baadhi ya Marais wengine baada ya kufunguliwa mkutano wa 12 wa Afrika unaojadili magonjwa ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Abuja +12) uliofanyika jana Julai 15, 2013 na kufunguliwa na Rais wa Nigeria Dkt. Goodluck Jonathan, mjini Abuja Nigeria na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika.Picha na OMR .

  0 0  Airtel na UNESCO kuzindua radio jamii  Karagwe Bukoba

  ·         Mawasiliano ya radio yaboreshwa kufikia vijiji vingi zaida kulinganishwa na awali
  ·         Zaidi ya radio 8 kuzindua chini ya mradi huu

  Jumanne 16 Julai 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki hii

  Uzinduzi huo unafatia ushirikiano kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio

  Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema  “ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.

  Tumejipanga kufanya uzinduzi wa ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya Ijumaa tarehe 19 julai 2013

  Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa wa Bukoba LutenFabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo

  TunaamiNi kwa kupitia radio hizi jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.

  Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu na mengine mengi.  kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.

  Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.

  nawashukuru sana Airtel na UNESCO kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007  na kuanza  kurusha matangazo yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni. Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari, 

  “Tunagemea kuzindua rasmi ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya” aliongeza Sekiku

  Mradi wa radio jamii umeanzishwa mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe Bukoba

  0 0

   Mwakilishi wa Shirika la UNICEF nchini Tanzania Dk.Juma Gulaid,(katikati) alipokuwa akimtambulisha Mama Francesca Moranditi,(kushoto) kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(kulia) walipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo mchana.
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Dk.Juma Gulaid,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kumtambulisha Mkuu mpya wa Shirika hilo Mama Francesca Moranditi,(hayupo pichani).[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwakilishi wa UNICEF Ofisi ya Zanzibar Mama Francesca Moranditi,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar,kujitambulisha kwa Rais,     [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]


older | 1 | .... | 119 | 120 | (Page 121) | 122 | 123 | .... | 1903 | newer