Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 118 | 119 | (Page 120) | 121 | 122 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Na  Khadija khamis –Maelezo Zanzibar 12/7/2013a

  NAIBU wazri wa kilimo na mali ya asili  Mtumwa Kheri Mbarouk amewataka wakulima wa mboga mboga na matunda kuitumia fursa wanayoipata kupitia taasisi ya kusaidia wakulima wa mboga mboga na matunda Tanzania (TAHA) katika kukiimarisha kilimo hicho.
  Aliyaeleza hayo jana waziri huyo katika uzinduzi wa ofisi na miradi ya TAHA Zanzibar iliyofanyika katika ofisi ya mfuko wa barabara Kikwajuni mjini Zanzibar.

  Alisema ipo haja kwa wakulima hao kuimarisha kilimo hicho, kukitunza  na kuithamini ili iwe mkombozi katika kuleta mapinduzi ya kilimo. “Mafanikio tuliyoyapata yameleta tija na bado tunahitaji kilimo bora na chenye manufaa katika kukuza sekta ya kilimo katika nchi yetu .” Alisema Naibu waziri Mtumwa

  Aidha alisema changamoto iliyopo hivi sasa ni ukosefu mkubwa wa soko,  hivyo serikali iko mbioni kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo.
  Alisema, iwapo kilimo hicho kitaimarika na kuweza kumnufaisha mtumiaji na mlaji na kutaweza kupatikana matumaini makubwa kwa kupata kuzalishwa kwa mbegu ziliobora kwa wakulima waliowengi.

  Pia aliwataka wakulima hao wasivunjike  moyo wala wasiwe na wasiwasi na badala yake wakaze mkanda  nayo serikali na taasisi hiyo ya TAHA itajitahidi kuwatafutia ufumbuzi wa soko la ndani na lanje ili kuweza kuimarisha zaidi kilimo cha kisasa.

  Nae Mkurugenzi wa TAHA Jaclin Nkinda wakati akitoa nasaha kwa wakulima alisema kilimo bila ya wanawake haiwezekani kwani wanawake ni wakulima wakubwa katika kilomo cha mboga mboga na matunda hapa kwetu Zanzibar.

   Jaclin alisema Taasisis ya TAHA ina lengo la kuwasaidia wakulima wa mboga mboga na matunda kwa nia ya uzalishaji wa mbegu Tanzania bara ili kuleta na kuendeleza kilimo hicho hapo baadae.

  Sambamba na wafadhili,Mfadhili kutoka Finland Tina Huvis alisema .Zanzibar inazalisha mboga mboga nyingi ambayo ina lengo la kuisaidi serikali na wakulima wa Unguja ili kufanikisha kilimo cha mboga mboga.

  Alisema wafadhili hao wataendeleza mashirikiano yao ili kuleta maendeleo ya kilimo hicho.  Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2004 yenye lengo la kuimarisha kilimo hapa nchini ikiwa na wadgamini wawili kutoka Filand na USAID.

    IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na Naibu Waziri Mkuu wa Kuwait na Waziri wa mambo ya Nje wa Kuwait Mhe Sabah Khalifa na ujumbe wake aliyemtembelea leo Ikulu Dar es salaam.Picha na IKULU.

  0 0

   Meneja wa Ecobank Tawi la Kariakoo, Japhet Fungo (kulia) akiongea na waandishi wa habari wakati wa kongamano la wafanyabiashara na uongozi wa benki hiyo ulifanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam Julai 11 2013. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Enoch Osei-Safo na Mkuu wa sekta Umma wa Benki hiyo, Ndabu Swere.
    Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania Enoch Osei-Safo akiongea na waandishi wa habari wakati wa kongamano la wafanyabiashara na uongozi wa benki hiyo ulifanyika Kariakoo jijini Dar es Salaam Julai 11 2013. Kulia ni Meneja wa Ecobank Tawi la Kariakoo, Japhet Fungo.
      Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mada katika kongamano hilo.
    Mkuu wa Sekta ya Umma wa benki hiyo, Ndabu Swere(katikati) akisikiliza maongezi kati ya Bw. Kapya (kushoto) na mmoja wateja wao katika hafla hiyo.
    Meneja wa Ecobank Tawi la Kariakoo Japhet Fungo (kushoto) akigonganisha glass na wafanyakazi pamoja na wateja wa Ecobank.
   Meneja wa Ecobank Tawi la Kariakoo Japhet Fungo (kushoto) akigonganisha glass na wafanyakazi pamoja na wateja wa Ecobank.
      Meneja wa Ecobank Tawi la Kariakoo Japhet Fungo akichukua maoni ya wateja na kujibu baadhi ya maswali yaliyowasilishwa.
       Baadhi ya washiriki wakiuliza maswali. 
   Baadhi ya wafanyabiashara Kariakoo walioshiriki kwenyehafla hio ya jioni
    Baadhi ya wakuu wa vitengo Ecobank Tanzania

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho kikwete akimkaribisha na waziri wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe Mark Simmonds Ikulu jijini Dar es salaam july 12, 2013.
   Rais Jakaya Mrisho kikwete akiongea na waziri wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe Mark Simmonds Ikulu jijini Dar es salaam July 12, 2013.
  Rais Jakaya Mrisho kikwete akimsindikiza waziri wa uingereza anayeshughulikia maswala ya Afrika Mhe Mark Simmonds Ikulu jijini Dar es salaam July 12, 2013.PICHA NA IKULU.

  0 0

    Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali.
   Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya bilauli toka kwa  Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala wakati washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam  July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali.
   Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi ya nembo toka kwa  Mkuu wa Chuo cha UIinzi (National Defence College) Meja Jenerali Charles Makalala wakati washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali
  Amiri Jeshi Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na washiriki wa kwanza 20 na wakufunzi wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa (National Defence College walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam July 12, 2013, ikiwa ni wiki moja tu kabla ya kuhitimu mafunzo yao hayo ya mwaka mmoja. Rais Kikwete aliwapongeza washiriki hao pamoja na wakufunzi wao kwa mafanikio mazuri ya chuo hicho cha kipekee kinachojumuisha washiriki kutoka vikosi vya ulinzi na usalami pamoja na taasisi za serikali.PICHA NA IKULU

  0 0

  Mchezaji wa timu ya Texas pool klab ya Mkoa wa Tabora Salum Kazuga akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klab yao iliyofanyika mkoani hapo jana.

  Mchezaji wa timu ya Texas pool klab ya Mkoa wa Tabora Shabani Ramadhani akijitayarisha kupiga mpira wakati wa mazoezi ya klab yao iliyofanyika mkoani hapo jana picha na SUPER D

  0 0

  Taasisi  ya  RafikiElimu  Foundation  inatangaza    nafasi  za  mafunzo  ya UALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwa  waombaji  wenye  sifa  zifuatazo ;

  1.    Mtanzania    mwenye  umri  wa  kuanzia  miaka  18  hadi  45.
  2.Awe   na  elimu  ya  kuanzia  kidato  cha   nne,  sita  na  kuendelea. 
  3. Aliye   na   utashi  na malengo  ya  kufanya kazi    kama  MWALIMU  WA  UJASIRIAMALI  kwenye  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini.
  4.  Anayeweza   kuwasiliana  kwa   ufasaha  kwa  lugha  za  Kiswahili  na kiingereza.
  5.  Awe  anaishi    katika   wilaya  ya  Ilala, Kinondoni  au  Temeke.

  DHUMUNI   LA    MAFUNZO  HAYA
   Dhumuni  kuu  la  mafunzo  haya  ni  kuwaandaa  wahitimu  kufanya  kazi  kama  WAALIMU  WA  UJASIRIAMALI  katika  Mradi  Wa  Elimu  Ya  Ujasiriamali  Mijini  &  Vijijini  unaoratibiwa  na  Taasisi.  
   
  MUDA  WA  MAFUNZO  Mafunzo  haya  yatafanyika  kwa  muda  wa mwezi  mmoja  kuanzia  tarehe  01 AGOSTU  2013..

  BAADA  YA  KUHITIMU : Wahitimu  wa  mafunzo  haya, watapata  nafasi  ya   kufundisha  somo  la  Ujasiriamali    katika  vituo  vya  mafunzo  ya ujasiriamali  katika  wilaya  mbalimbali  za  Tanzania  bara.

   ADA  YA  MAFUNZOAda  ya  mafunzo   haya ni  SHILINGI ELFU  SITINI  NA  TANO  TU ( Tshs.65,000/=)
  FOMU  ZA  MAFUNZO : Fomu  za  mafunzo  haya  zinapatikana   kwa SHILINGI  ELFU  KUMI  NA  MBILI ( Tshs. 12, 000/=)  tu  katika  ofisi  zetu zilizopo  katika  eneo  la  CHANGANYIKENI  karibu  na  CHUO  CHA TAKWIMU. 
  Mwisho  wa  kuchukua  fomu   za  kujiunga  na  mafunzo  haya  ni  tarehe  25 JULAI  2013.
  Kwa  maelezo  zaidi  wasiliana  nasi 
   kwa  simu 0756606085 au 0782405936.

  0 0

   Mshambuliaji wa timu ya Taifa (Taifa Stars),John Boko (14) akiwa na mpira mbele ya Beki wa timu ya Uganda ( The Cranes) katika mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.
   John Boko akiondoka na mpira kuelekea langoni mwa timu ya Uganda.
   hapa hapiti mtu .....
   Mrisho Ngassa akitaka kuwatoka Mabeki wa Uganda wakati wa mchezo wa kuwania tiketi ya kucheza Kombe la mashindano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN),uliomalizika hivi punde kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Taifa Stars imekubali kipigo cha Bao 1-0 kutoka kwa Uganda.

  PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.

  0 0
 • 07/13/13--09:56: BWM FOR SALE


 • 0 0

  Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Lilian Vincent (leo) jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
  Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin (kulia) akisaidiana na Mkewe Tani Austin(kushoto) kumuvalisha kifaa cha kumwezesha kusikia mtoto Malechela Juma (katikati) leo jijini Dar es salaam wakati Mfuko huo ulipoendesha huduma ya kutoa vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
  Mwanzilishi wa Mfuko wa Starkey Hearing William Austin akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam juu ya huduma ya vifaa vya kusaidia kusikia kwa watu wenye matatizo ya kusikia ambayo wanatarajia kuitoa kwa wakazi wa Dar es salaam zaidi 2000 kwa muda wa siku nne katika Hoteli ya Serena.
  Baadhi ya wakazi na watoto kutoka sehemu mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa katika foleni ya kupatiwa matibabu ya huduma ya vifaa vya kuwasaidia kusikia kutoka Mfuko wa Starkey Hearing leo jijini Dar es salaam. Mfuko huo umeweka kambi katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo wanatarajia kutoa huduma hiyo bure kwa watu zaidi ya 2000 kwa kipindi cha nne.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

   Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng (mwenye fulana nyekudu) kushoto ya Sheng ni Balozi mdogo wa China Madam Chen huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar.
  Picha no.2 Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng baada ya mazungumzo yao huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

   =========  ========  ===========
  Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  .

  Kuokosekana kwa Matangazo ya Vivutio vya Zanzibar nchini China kumetajwa kuwa sababu inayopelekea Watalii wanaotoka nchini huko kushindwa kuja Zanzibar kufanya shughuli za Utalii.


  Mkurugenzi wa Kampuni ya Kimataifa ya huduma za usafiri ya China (CITS) Zou Wang Sheng ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar.


  Sheng amesema China ni miongoni mwa nchi zinazotoa Wataii wengi kutembelea nchi tofauti duniani lakini Wachina walio wengi hushindwa kuja Zanzibar kutokana na kukosa taarifa zinazohusu vivutio hivyo.


  Amedai kuwa hata katika Balozi ya Tanzania nchini China hakuna Matangazo yanayohusu vivutio vya Zanzibar badala yake kunapatikana Matangazo ya Mbuga za Serengeti na Manyara ambazo zote ziko Tanzania Bara.


  Sheng ambaye ni mara yake ya kwanza kuja Zanzibar ameongeza kuwa  kutokana na mazigira mazuri yakitalii  yaliyopo Zanzibar anaamini kama kutafanywa mkakati thabiti wa kuvitangaza Vivutio vya Zanzibar hapana shaka zaidi ya Watalii 200,000 wanaweza kuitembelea Zanzibar kwa mwaka.


  Ameelezea kuvutiwa kwao na Fukwe, hali ya hewa na mazingira ya Zanzibar kwa ujumla wake na kuahidi atakaporudi atafanya kazi ya kushawishi makundi ya Wageni kuja kujionea vivutio hivyo. “Tumetembea nchi nyingi dunia kufanya ziara za kitalii lakini ukweli nikwamba ni nchi chache sana za visiwa duniani zenye vivutio vizuri kama Zanzibar ” Alisema Sheng


  Awali Waziri wa habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Zanzibar na China zimekuwa na mashirikiano makubwa kwa muda mrefu hasa katika sekta za elimu, Afya na teknolojia na kwamba kwa sasa Sekta ya Utalii inapaswa kupewa mkazo wa pekee.


  Ameongeza kuwa Zanzibar imekuwa ikipokea Watalii kutoka nchi nyingi za Ulaya na hasa Wataliano na kwamba umefika muda sasa walau Theluthi ya Watalii kutoka China kuja kutembelea Zanzibar.


  “Taarifa zinaonesha China inatoa Watalii zaidi ya Milioni moja kwenda kutembelea nchi tofauti duniani sasa tunataka walau watalii laki tatu watembelee Zanzibar kwa mwaka ” Ameongeza Waziri  Mbarouk. Ameongeza kuwa mazingira ya Zanzibar ni mazuri kwa vivutio vingi vya utalii na hali ya kisiasa ilivyotengamaa na kulitaka Shirika hilo kufanya jitihada zake ili kuwepo kwa Safari za ndege zinazotoka China na kuja Zanzibar.

  Waziri Mbarouk amewahakikishia Wawekezaji hao kila aina ya ushirikiano ili kuona Sekta ya Utalii nchini inasonga mbele kupitia Watalii wa kichina. Kwa upande wake Balozi mdogo wa China nchini Madam Chen Queman amesema kuwa walipokea ushauri kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Menyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kusaidia kuitangaza Zanzibar ambapo ujio wa kampuni hiyo ni utekelezaji wa shauri hilo.

  Ameongeza kuwa njia pekee ya kufikia malengo yaliyokusudiwa ni kuhakikisha kunakuwepo mawasiliano na mashirikiano ya moja kwa moja kati ya Kampuni hiyo na Mamlaka ya Ukuzaji Vitegauchumi Zanzibar ZIPA.


  Madam Chen amesema ZIPA ndio watakao kuwa Wenyeji wa Kampuni hiyo ili kujua nini kifanyike katika hatua za mwanzo kuhakikisha Zanzibar inafaidika na Watalii kutoka nchi ya China. 


  0 0

   Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpa zawadi  Ofisa Kadet  Ngodoke kwa kuibuka mwanafunzi bora wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
   Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akimpa zawadi Ofisa Kadet  D.G.L. Wong- Pool toka Visiwa vya Ushelisheli kwa kuibuka mwanafunzi bora wa kigeni wa jumla mwaka huu katika Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli. 
   Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akitunuku kamisheni kwa maafisa katika Chuo cha  Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.  
   Meza kuu wakati wa sherehe za  kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na  Visiwa vya Shelisheli.
  Meza kuu wakati wa sherehe za  kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli.
    Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiingia katika uwanja wa gwaride wa Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, tayari kwa kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ leo Julai 13. Pamoja naye ni Mkuu wa Chuo hicho Meja Jenerali V.K. Mritaba. Jumla ya wahitimu 205, wakiwemo wanawake 25, wametunukiwa kamisheni na kuwa Luteni Usu, ambapo wahitimu wawili ni wa kutoka Uganda na Visiwa vya Shelisheli. 
   Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua  gwaride katika  Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli, Arusha, kabla ya kutunuku kamisheni kwa Maafisa wa JWTZ  leo Julai 13.PICHA NA IKULU.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Christine Ishengoma,leo ametoa taarifa ya mkoa juu ya mafanikio ya utekelezaji wa irani ya CCM, ya uchaguzi kuanzia januari hadi juni 2013.

   Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema  leo Ishengoma, amesema kuwa shughuli  kuu ya kukuza uchumi katika mkoa wa Iringa ni kilimo, upasuaji mbao ,uvuvi, biashara na ajira maofisini na viwandani.

  Amesema asilimia 85 ya wafanyakazi wa mkoa wa Iringa hujishugulisha na kilimo na ufugaji na katika shughuli hizo mkoa umepata mafanikio makubwa kupitia shughuli hizo.


   Amesema kuwa mafanikio yote hayo yametokana na mchango wa wadau mbalimbali wakiwemo serikali kuu,serikali za mitaa,wananchi wenyewe pamoja na washiriki wa maendeleo,

  hata hivyo amezitaja sekta hizo ambazo zinagusa maendeleo ya wananchi kuwa ni sekta ya uzalishaji mali,uvuvi,uhifadhi wa wanyama pori,misitu,miundo mbinu uwezeshaji wa wananchi kiuchumi pamoja na afya.


  Aidha amewataka wananchi kufanya kazi kwa juhudi na ushirikiano ili kuweza kusonga mbele.
  0 0

  Wananchi wa mkoa wa Iringa wametakiwa kudumisha amani na  kusitisha maandamano  yasiyo ya lazima  na kutii sheria  bila shuruti.

  Hayo yamesemwa na  DCP MICHAEL KAMUHANDA wakati wa sherehe ya kumuaga kamanda huyo na kumkaribisha kamanda mpya  wa mkoa wa Iringa RAMADHANI MUNGI  iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha Ruaha University College RUCO.


  KAMUHANDA amesema kuwa  katika harakati za uchaguzi  mkuu 2014 wanatakiwa kuwe na hali ya usalama na utulivu wakati wa hatari  na kusisitiza kuwa endapo wananchi watashindwa kuwa watulivu jeshi la polisi litaingilia kati.


  Kwa upande wake kamanda aliyekuwa anakaribishwa,RAMADHANI MUNGI amesema kuwa atahakikisha anatekeleza  na kuendeleza yale ambayoKAMUHANDA ameyaanzisha kwa kushirikiana na maaskari wote kwa kuzingatia wimbo wa maadili wa jeshi la polisi.


  MUNGI  ameongeza kuwa atatokomeza  uhalifu katika mkoa wa iringa na kulinda wananchi na mali zao.Nae mkuu wa mkoa wa iringa CHRISTINE ISHENGOMAambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo aliwaomba askari polisi  kufanya kazi kwa bidii na kwa kujituma na kuepuka na rushwa huku akiwaasa kujilinda na gonjwa hatari la ukimwi.


  WAKATI HUO HUO....

  Mkazi wa mwangata “A” WILLIAM UPETE anashikiriwa na polisi kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake CRISPINI UPETE {13} na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.


  Akizungumza na Mshika kalamu wa logu hii, CRISPINI UPETE amesema alitumwa na baba yake WILLIAM UPETE kwenda kuuza viatu aina ya YEBOYEBO na baada ya hapo hakurudi na hela ndipo baba yake akaanza kumpiga.


   Hata hivyo baba mzazi wa mtoto huyo amekiri kufanya tukio hilo, na kusema kuwa aliamua kumpiga kutokana na kuwa mtoto huyo alirudi akiwa na vitu vya thamani ambavyo alikuwa amevinunua.


   Mmwenyekiti wa mtaa wa mwangata A   bw. JULIUS LWIMBO amethibitisha kutokea kwa kwa tukio hilo na kusema kuwa alipata taarifa toka kwa wapangaji na kufika eneo hilo mapema asubuhi nakuanza kufanya taratibu za kiserikali.  0 0
 • 07/13/13--23:19: UZINDUZI WA JARIDA LA ONSPOT
 •  Mh. Dr. Faustine Ndugulile akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani),wakati wa hafla ya uzinduzi wa  jarida  hilo la la Onspot ambalo zamani ilijulikana kama Teenspot.
   Mkurugenzi wa Onspot Magazine Nd. Amin Swai akiongea na waandishi.
  Sehemu ya Wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo .

  0 0

   Mtu mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja akiwa amekamatwa na mmoja wa Polisi waliokuwa nje ya uwanja wa Taifa wakiangalia usalama,kwa kudaiwa kuuza tiketi feki za mechi ya jana iliyozikutanisha timu ya Taifa Stars dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda The Crane's,kwenye mchezo wao wa kuwania kufuzu michuano ya Afrika ya wachezaji wa ndani (CHAN).
   Baadhi ya wateja walionunua tiketi hizo zilizodaiwa kuwa ni feki wakizirejesha na kutaka fedha zao zirudishwe kwa mtuhumiwa huyo aliyewekwa chini ya Ulinzi .Aidha hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vilieleza kuwa Askari Polisi ndio wanaohujumu mapato ya Uwanja wa Taifa.

  0 0

  Aliyekuwa mgombea UWT Taifa, Maryrose Magige akionyesha kadi ya Chadema aliyokabidhiwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Wilbrod Slaa wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika Viwanja vya Shule ya Msingi Ukombozi Manzese Dar es Salaam jana. Picha kwa hisani ya Salim Shao .

  0 0

  Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akikabidhi Mbuzi kwa mmoja wa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
  Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akikabidhi sabuni na vitabu kwa mmoja wa watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,wakati wa futari ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,walioambatana na Mwenyekiti wa bodi ya Vodacom Foundation Hassan Saleh(kulia)kupitia kampeni ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
  Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi,akimsikiliza Mwenyekiti wa bodi wa Vodacom Foundation Hassana Saleh,akimfafanulia jambo wakati wa futari na baadhi ya watoto yatima kati ya 700 wa madrasa kisarawe,iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom ambayo imetenga kiasi cha shilingi Milion 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha Ramadhan.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania wakiwapa vyakula baadhi ya watoto wa madrasa wanaoishi katika mazingira magumu kisarawe Pwani wakati wa futari iliyaoandaliwa na Vodacom Foundation kupitia kampeni yake ya Pamoja na Vodacom iliyotenga kiasi cha shilingi Milioni 50 kwa ajili ya kipindi hichi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuudhuriwa na Mgeni rasmi Rais Mstaafu Mh.Ali Hassan Mwinyi hayupo pichani.

  0 0
 • 07/14/13--01:28: ok.! biashara matangazo.!


 • 0 0
older | 1 | .... | 118 | 119 | (Page 120) | 121 | 122 | .... | 1903 | newer