Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 120 | 121 | (Page 122) | 123 | 124 | .... | 1903 | newer

  0 0

  Na Miza Othman - Maelezo Zanzibar  16/7 2013

  Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema kwamba  Jumla ya wanafunzi 161 wamelipiwa ada ya Masomo na Posho mbali mbali kwa wale wanaoendelea na Masomo katika vyuo mbalimbali vya Nje kutokana na usumbufu wanaoupata chuoni.

  Hayo yamesemwa leo huko Baraza la wakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Aamali Ali Juma Shamuhuna wakati alipokuwa akiwasilisha Bajeti ya Wizara yake Barazani hapo kuhusu makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa mwaka 2013/2014 mwaka ujao.  

  Amesema wanafunzi hao wamelipiwa fedha hizo ikiwa ni sehemu ya serikali kuwapatia msaada huo ili waweze kujisomea vizuri.

  Amesema ni vyema kwa wanafunzi wanaofaulu kiwango cha juu kuwapatiya Mikopo hiyo ya elimu ya juu  kutokana na  chombo hicho kupewa  jukumu la dhamana la kuwapatia mikopo ya gharama za elimu kwa wanafunzi na wafanya kazi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini ilikupata wataalamu baadae.

  “Bodi ya mikopo ya Elimu ya juu imeendelea  kutowa Mikopo pamoja na kukusanya Marejesho kutoka kwa Wahitimu wa taasisi za elimu ya juu waliopatiwa mikopo hiyo”, alisema Shamuhuna.

  Aidha ameeleza kuwa mafanikio yaliopatikana katika mwaka 2012/2013 kutokana na kupatiwa mikopo ya Elimu ya juu ni misada kutoka  Falme ya Oman ambayo aliitoa kuwasaida wanafunzi hao ambayo ikiwa ni sehemu ya ushirikiano na undugu walio nao mmdamrefu.

  Amesema idadi ya wanafunzi waliogharamiwa masomo kupitia Bodi ya mikopo hiyo iliongezeka kutoka wanafunzi  1,086 mwaka 2011/2012 hadi wanafunzi 1,897 mwaka 2012/2013.

  0 0

   

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
   
  KUAMINI ni tendo la hiyari. Ila ni wazi kuwa mwendo huu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), juu ya siasa za Tanzania inajiweka kubaya.Hili ukilisema wapo watakaobisha. Watavaa vibwaya kuporomosha matusi kadri ya uwezo wao. Hao ni wale wasiopenda kuambiwa ukweli. Wakiambiwa wanachukia.
   
  Hata hivyo, ukweli siku zite unauma lakini unasaidia kumuweka mtu huru na lazima tujuwe kuwa kuamini ni tendo la hiyari. Leo hii ambapo baadhi yao wanaamini Chadema ndio kila kitu, ukiwaambia juu ya njia mbaya wanayopita ni ngumu kukuelewa.Ni wazi Chadema kwa sasa ndio Chama Cha upinzani katika siasa za Tanzania Bara. Nasema Tanzania Bara kwakuwa chama hicho kinachoongozwa na mwenyekiti wake Freeman Mbowe, upande wa pili wa Muungano, yani Zanzibar hawana chao.
   
  Kule hakuna anayeiamini Chadema. Ingawa Wazanzibar wengi hawaiamini Chadema kwa sababu za kidini, ila hata mwenendo wao wenyewe, kuangalia sana Kanda ya Kaskazini kunasababisha kuibua maswali kama wengine wanawajitaji.
   
  Katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chambani, uliofanyika mjini Zanzibar ambapo Chama Cha Wananchi CUF kiliibuka mshindi kwa mgombea wao kinyang’anyiro hicho cha Ubunge, Chadema waliambulia kura 11 tu.
  Katika hali ya kushangaza zaidi, chama kipya ambacho hakina hata mwaka mmoja, yani ADC, chenyewe kilipata kura 112, ikiwa ni ishara kuwa katika visiwa hivyo Chadema hawana chao. Katika mchanganuo wa kura hizo katika jimbo la Chambani, Chama Cha Mapinduzi CCM wenyewe walipata kura 202, wakati CUF wao 2708 na kunyakua jimbo hilo.
   
  Sio Zanzibar tu, ila katika sehemu nyingi za Tanzania Bara, pia Chadema haijulikani na haina heshima. Hii ni kwasababu sera na mpangilio wao haueleweki. Wanachoweza wao ni kubuni matamko yasiyokuwa na mashiko kwa Watanzania wote, ukiacha wale waliokuwa katika Mkoa wa Kilimanjaro, Arusha, Mbeya Mjini na baadhi ya maeneo wanapokubalika.
   
  Wajuzi wa mambo ya siasa wanajua kuwa ili chama kifanikiwe kushika dola, walau kinastahili kuungwa mkono na watu wengi. Chama kinachojulikana Tanga tu na kuheshimiwa, kamwe haiwezi kuwa njia ya kuwapatia Dola.
  Wakati haya yanaendelea kutokea, Chadema wanajikuta wakiubua maswali yasiyokuwa na majibu. Viongozi wao wa chama na serikali mtazamo wao unasua utata.
   
  Kwa mfano, mara baada ya kutokea mlipuko wa bomu uliosababisha vifo vya watu watatu katika Mkutano wa Kampeni za udiwani uliofanyika jijini Arusha, Mbowe kama Mwenyekiti alitangaza kuwazuia wabunge wake kuingia bungeni. Lengo la Mbowe lilikuwa ni kuwataka wabunge hao washiriki mazishi ya wafuasi wao waliokufa kwa mlipuko wa bomu. Mazishi ambayo Chadema walijua kuwa walitakiwa wasiandamane au kuaga kwa makundi kwa sababu za kiusalama.
   
  Kwakuwa wanajua mtaji wao ni propaganda chafu dhidi ya wananchi na serikali yao iliyopo madarakani, Chadema waligoma. Wakaamua kufanya wanavyotaka wao. Hii ilisababisha kuzua mgogoro baina yao ni Jeshi la Polisi. Jeshi ambalo kila siku ya Mungu Chadema wamekuwa wakitoa lawama, wakiwadhihaki na kuwatusi pia.
   
  Mara kadhaa tunasikia Jeshi la Polisi likitwa PoliCCM. Maneno mengi dhidi ya walinzi hawa wa raia na mali zao yanatoka katika vinywa vya watu wanaojipambanua kuwa wanahitaji kuwaongoza Watanzania.
  Huu sio mpango mzuri. Ili Watanzania waendelee kuwa na heshima na vyama vya siasa, ni wazi Chadema kama Chama Kikuu cha upinzani Tanzania Bara, lazima kijisahihishe.
   
  Kabla ya kuzungumza jambo, lazima wakae na kufanyika tathimini. Huu ndio ukweli wa mambo. Kinyume cha hapo Chadema wataendelea kuwagawa wananchi, huku wale wanaowaunga mkono pia wakitafakari uwapo wao. Kwa mfano, Chadema kwa kupitia kikao cha Kamati Kuu kimetangaza kuwafundisha vijana wao namna ya kujilinda.
   
  Hii ndio kusema kuwa Chadema wameona jeshi halali la Tanzania limeshindwa kuwalinda. Ingawa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekataza vikundi vya namna hiyo, kikiwamo hiki cha Red Brigade kilichotangazwa na Chadema.Wataalamu wa mambo wanahisi kuunda vikundi vya aina hii ni kuzalisha chuki na machafuko. Kwa Chadema ambao wamekuwa wakilalamikia jeshi la Polisi kesho vijana wao hawatafanya fujo?
   
  Leo hii wakiwa wakomavu na mafunzo hayo hawatawarushia mabomu askari wetu? Haya ni maswali yanayotakiwa yajibiwe na kila Mtanzania juu ya siasa za Tanzania, hususan Chadema. Chama ambacho dhamira yao inaweza kuyeyuka kama watashindwa kujiweka sawa. Mwendo wao si mzuri. Kauli zao nyingi inaonyesha inatoka bila kufanyiwa uchunguzi.
   
  Kwa mfano, Chadema wao waliweza kususia vikao halali vya Bunge kwa kisingizio cha mazishi ya wafuasi wao. Mbaya zaidi, waligomea katika Bunge la Bajeti.Bunge ambalo tangu lilipomalizika, tayari kumekuwa na matokeo magumu ya kupandishwa kwa kodi katika baadhi ya huduma, zikiwapo za simu za mikononi.
   
  Leo hii Mtanzania ambaye hata kula yake haijulikani, bado atapaswa kulipia kiasi cha Shilingi 1,000 kwa namba yake (simcard). Hii ni kodi tofauti na gharama nyingine za muda wa maongezi ambazo zimepanda mara dufu.
  Ingawa wabunge wa CCM wapo wengi bungeni, wakifikia 245 tofauti na wale wa upinzani hususan Chadema, ila kuwapo kwao kungesaidia kuibua hoja katika mrejesho wa hutuba ya Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa na wataalamu wake.
   
  Kitendo cha uwapo wao, huenda kingezindua zile hoja zenye mashiko na Watanzania wote. Lakini waligoma kuingia kwasababu ya Arusha, wabunge wao wote wakiwapo huko, bila kujua kuwa Tanzania ina mikoa mingine inayohitaji uwapo wa wapinzani.
  Bado kuna mikoa kama vile Mwanza, Geita, Morogoro, Tanga, Ruvuma, Pwani na mingineyo, hivyo si vizuri pia kwa chama hiki kuangalia zaidi Kanda ya Kaskazini.
   
  Aidha tunahitaji hoja zaidi badala ya kupayuka maana huko kunaoanyesha mapungufu ya hadharani kabisa. Kwa mfano, katika makala yangu ya Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya Chadema, Joseph Mbilinyi Sugu, nilipinga kumuita Mpumbavu Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Wapo waliokosoa na waliosifia pia. Katika makala ile, nilijaribu kusisitiza wanasiasa wetu, viongozi wetu kupenda kuweka hoja badala ya mihemko isiyokuwa na tija. Huu ndio ukweli. Hivyo hata hili suala la Red Brigade la Chadema linaweza kuwa baya zaidi kama litatumiwa tofauti. Chadema lazima wajuwe wana kila sababu ya kuilinda amani ya nchi yetu.
   
  Sioo Chadema tu, ila vyama vyote vya siasa vinastahili kupigania amani maana ndio msingi wa maendeleo. Leo hii kama kila mtu ataweza kuunda vikosi anavyojua mwenyewe tutasababisha mwingiliano na machafuko yasiyokuwa na mpango. Shughuli za ulinzi wa Taifa letu tushiriki kwa pamoja, ila zaidi jeshi la Polisi lina imudu zaidi kazi hiyo. Muhimu ni kuwapa moyo na kuwapa ushirikiano pia.
   
  Hakuna haja ya mwanasiasa kutoa maneno ya kejeli kwasababu Dola ipo chini ya CCM. Tusipokuwa makini na kufanya siasa za kuvumiliana, hata kesho Chadema wakiingia Ikulu au ama CUF basi machafuko, lawama za mtindo huo zitashika kasi.
   
  Angalia nchini Misri. Mwaka jana wananchi waliweza kuandamana kushinikiza rais wao Hosni Mubarak ajiuzulu. Walifanikiwa. Mubarak alitoka na uchaguzi huru wa kwanza kufanyika.
   
  Lakini wakati watu wakiwa hawajui kinachotokea, wananchi hao hao tena wanaingia barabarani kumtaka rais wao Mohamed Morsi ang’oke kwa madai kuwa ameshindwa kuliongoza Taifa hilo.Pia wakafanikiwa, hasa baada ya jeshi kumsaliti na kumuengua. Hii ni ishara kuwa hata Tanzania hayo yanaweza kutokea. Kama wananchi watafundishwa kufanya vurugu, maandamano, matusi na kejeli dhidi ya serikali au jeshi, basi hata kama Chadema wakiingia Ikulu, mtindo huo utaendelea kushika kasi.
   
  Ni vyema tukajifunza katika hili. Tanzania tunakabiriwa na changamoto nyingi has azan ugumu wa maisha. Ni vyema basi tukatumia muda mwingi kuwaza namna ya kujiletea maendeleo na sio kupanga namna ya kulisumbua Taifa kwa namna yoyote ile.
   
  Ni wakati wa wanasiasa wetu kutumia busara na siasa za uvumilivu ili iwe nafasi ya kujiletea maendeleo. Vyama vya upinzani kama kweli vinahitaji kuwakomboa Watanzania kama wenyewe wanavyosema, wasimamie kwanza katika suala zima la amani yetu inayoelekea ukingoni, ukizingatia kuwa kaatika siku za hivi karibuni, kumekuwa kukitokea matukio ya kuogofya, hasa ya utekwaji na uteswaji.
  Mwisho

  0 0

   Baadhi ya watoto  yatima wakipakuliwa futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu jioni
  Wtoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam 
  Watoto  yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam 
   Yatima wakipata futari Ikulu
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimbeba mmoja ya watoto  yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watot yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo. Picha na Freddy Maro

  0 0

  dealmoja_logogg
  Fursa ingine kwa watu wote WANUNUZI NA WAUZAJI DUNIANI
  Ni website ya kisasa yenye sifa za kimataifa www.dealmoja.com Yaap ni DEAL MOJA katika wavuti hii kuna mengi waeza fanya bila GHARAMA YOYOTE.

  · TANGAZA BIASHARA YAKO KATIKA Category ya Business directory
  · UZA AU NUNUA bidhaa kupitia wavuti hii.

  · KWA WALE WENYE BIASHARA AU HUDUMA ZA KUPANGISHA au KUUZA – Unaweza Tangaza kupitia wavuti hii BUREEEEEEE.

  Waweza jiuliza kwanini tunatumia lugha ya KIINGEREZA katika wavuti hii…. Sababu kubwa ni kuwa tunataka kwenda mbali … na hii itasaidia watanzania kufanya biashara na watu wote DUNIANI lugha kuu ikiwa ni KIINGEREZA.

  Ni rahisi sana unajisajili kisha unaanza kurusha bidhaa zako katika website hii ya kisasa naya uhakika kabisa.
  WAWEZA POST BIDHAA/HUDUMA
  KUPITIA SIMU YAKO.

  0 0

  Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akionyesha waandishi wa Habari (hawapo pichani) jinsi droo ya Airtel Yatosha inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.
  Meneja Uhusiano wa Airtel  Bw, Jackson Mmbando akiongea na moja ya washindi wa promosheni ya Airtel yatosha mara baada ya kuibuka mshindi katika droo ya wiki ya kwanza inavyochagua mshindi wa kila siku wakati wa droo ya kwanza ya   promosheni hiyo ya Yatosha iliyotoa jumla ya washindi 7 toka mikoa mbalimbali, katikati anaefuatilia droo hiyo ni  Msimamzi wa  bodi ya michezo ya Kubahatisha Tanzania Bw, Mrisho Milao na Meneja Masoko wa Airtel Bi Aneth Muga wakwanza kulia. Droo ya Airtel Yatosha imetoa jumla ya ashindi 7 ambapo kila mmoja amejishindia shilingi milioni moja.

  0 0

   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (wa tatu kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mikopo, Andrew Lyimo, Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale na Kaimu Mkuu wa Hazina, Ivan Tarimo.   
   Mkuu wa Mikopo wa Benki ya NBC Tanzania, Andrew Lyimo (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa  jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkuu wa Huduma za Rejareja, Raymond Mutagahywa, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Bi. Mizinga Melu na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale. 
   Mkuu wa Huduma za Rejareja wa Benki ya NBC Tanzania, Raymond Mutagahywa (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo ya Wafanyakazi Waajiriwa jijini Dar es Salaam leo. Wengine kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Bi. Mizinga Melu,  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Bi. Mwinda Kiula Mfugale na  Kaimu Mkuu wa Hazina wa NBC, Ivan Tarimo. 
  Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC, Bi. Mwinda Kiula Mfugale (wa pili kulia) akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Kampeni ya Mikopo kwa Wafanyakazi Waajiriwa ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei akipimwa afya yake.
   Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Dk. Akwilina Kayumba akimpima afya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam leeo.  Zoezi la upimaji afya likiendelea.
  Baadhi ya Madkatari wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), wakiwa katika ofisi za benki ya CRDB tayari kwa kuanza zoezi la upimaji afya za wafanyakazi wa benki hiyo.
  Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDBEsther Kitoka akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei  akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Benki ya CRDBEsther Kitoka. 
  Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya mahali pa kazi (OSHA), kutoka Wizara ya Kazi na Ajira Dk. Akwilina Kayumba akizungumza wakati wa uzinduzi wa upimaji afya kwa wafanyakazi wa benki ya CRDB. 

  0 0

  IMG_0073

  Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira alipomtembelea ofisini kwake mjini Kayanga mkoani Kagera kutambulisha mradi wa Amani na Demokrasia wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania. Mradi huo utakuwa unaratibiwa na UNESCO kwa kushirikiana na UNDP.
  IMG_0085
  Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akifafanua jambo kuhusiana na mradi wa Amani kwa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Dary Lwegasira (wa tatu kulia) namna utakavyoendeshwa kwa wakazi wa Wilaya yake. Kushoto ni Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku na wa pili kulia ni Mshauri wa Radio Jamii kutoka UNESCO Rose Haji Mwalimu.
  IMG_0221
  Picha juu na chini ni Bw. Omary Hassan akikusanya maoni ya vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (KDVTC) kilichopo kitongoji cha Kayanza wilayani Karagwe mkoa wa Kagera.
  IMG_0182IMG_0208
  Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan na Mkurugenzi wa Radio jamii FADECO ya Wilaya ya Karagwe Joseph Sekiku (fulana ya Blue) kwenye picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wa Chuo cha ufundi stadi (KDVTC) mara baada ya kumaliza zoezi la ukusanyaji maoni kwa wananchi wa Karagwe.


  IMG_0254
  Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Omary Hassan akizungumza na uongozi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na ukusanyaji maoni ya Utekelezaji wa Mradi wa Amani na Demokrasia Wilayani Karagwe. Kushoto ni Mkuu wa taasisi ya PETI Devotha Brassio na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo Fravian Gedion.
  IMG_0271
  Bw. Omary Hassan akizungumza na wanafunzi wa Perfect Education of Tourism and Institutions (PETI) kuhusiana na utekelezaji wa mradi wa Amani ambapo vijana nao wanahusika katika kujenga Amani ya nchi kwa sababu wao ndio taifa la leo.
  IMG_0295
  Bw. Omary Hassan katika picha ya pamoja na uongozi wa taasisi ya PETI na baadhi ya wanafunzi wa taasisi hiyo.
  IMG_0324
  Mweka hazina wa Shirikisho la Vijana la Umoja wa Mataifa (YUNA) Tanzania Bara na Visiwani Bw. Omary Hassan akikusanya maoni kwa wananchi wa wilaya ya Karagwe kufanya tathmini ya utekelezaji wa mradi wa Amani na Demokrasia.
  IMG_0378
  Kina mama nao walihusika katika kuchangia maoni ambapo wengi wao wameomba mradi huo utakapoanza kuwepo na kipindi maalum katika radio jamii ya wilaya ya Karagwe cha kuwaelimisha waume zao kuhusu swala la unywaji Pombe kupita kiasi ambao unapelekea uvunjifu wa amani katika nyumba zao.

  Mashirika ya UNDP na UNESCO yameanzisha mradi wa pamoja wenye lengo la kuhamasisha ushiriki wa jamii miongoni mwa vijana, wanawake na walemavu katika maendeleo na kudumisha amani nchini Tanzania.
  Kama inavyojulikana haiwezekani kuwa na maendeleo bila kuwa na amani, na haiwezekani kuwa na amani bila kuwa na maendeleo.
  Kwa sababu hiyo Jumuiya ya Kimataifa inatambua kuwa moja ya mikakati msingi ya kujenga amani ni kuwa na msingi thabiti wa uchumi jamii.

  Pia kuwezesha raia wote kuhusisha katika kutoa maamuzi ni kuweka msimamo katika maendeleo endelevu.

  0 0

   MAREHEMU JAJI (MSTAAFU) BUXTON DAVID CHIPETA.

  Kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa SUMATRA anasikitika kuufahamisha umma kuwa aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa SUMATRA Jaji (Mstaafu) Buxton David Chipeta amefariki dunia tarehe 16 Julai, 2013 katika Hospitali ya Hindu Mandal, Dar es Salaam.

  Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa Marehemu, Oysterbay Mtaa wa Chole/Lincon, Plot No. 580.

  Tunaomba tuungane na Familia ya Marehemu Jaji (Mstaafu) Chipeta katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo ya msiba huu mkubwa.

  Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!


  Kaimu Mkurugenzi Mkuu
  SUMATRA
  17 Julai, 2013.

  0 0

  Na Khadija Khamis Maelezo Zanzibar  17/07/2013 .

  Imeelezwa kuwa iko haja ya Serikali kuandaa mitaala ya pamoja katika Skuli za maandalizi ili kuepuka kutofautiana kiuwezo wa elimu  kwa wanafunzi wa Skuli za Serikali na Skuli za Kibinafsi.

  Wamesema elimu ya maandalizi ni msingi wa kumuezesha mtoto kujiandaa ili akianza elimu ya msingi  aweze kuwa na ufahamu mzuri .

  Wajumbe wa baraza la wawakilishi wameeleza hayo wakati wakichangia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni  nje kidogo na mji wa Zanzibar .

  Aidha wawakilishi  hao walisema pamoja na mitaala ya masomo pia wameishauri Wizara ya elimu kuandaa mitaala ya  michezo  ili kuweza kukuza kiwango cha michezo nchini.   

  Wakizungumzia suala la hatimiliki,  wachangiaji hao walisema kuna skuli nyingi za Unguja na Pemba hazina hatimiliki  licha ya kwamba baadhi ya skuli hizo zina umri  wa miaka mingi .

  Aidha walisema kuwa iko haja ya kuandaliwa vifaa kwa ajili ya elimu mjumuisho na walimu wanaosomesha masomo hayo waangaliwe kwa maslahi kwani wanakabiliana na kazi ya ziada katika kufundisha wanafunzi hao . 

  Aidha walisema Wizara ya Elimu imeajiri walimu 578 katika kipindi cha mwaka huu  lakini hadi sasa walimu waliomaliza mwaka  2008  hawajapata ajira .
    
  Wakieleza changamoto zilizojitokeza ni ukosefu wa walimu  katika wilaya za Pemba. Wete.Chakechake na mkoani . Wakifahamisha kwamba walimu wanaopata ajira wazingatiwe na wilaya zao wanazoishi  kwa kurahisishiwa masafa. 

  Aidha walieleza kuwa walimu hawafanani na chochote hivyo wanahitaji kuenziwa kutunzwa na kuthaminiwa.


  0 0

  MANYARA 2 PICS 252Kushoto Mkurugenzi wa Event Planners na muandaaji wa shindano la Modo wa Utalii Graysson Kijo a.k.a Chinaa akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa shindano hilo Bi.Buya Ernest(19) wa pili ni Simon na Jairos kutoka kampuni ya Megatrade Investment, wadhamini wakuu wa shindano hilo kupitia kinywaji chake cha K-vant gin lililofanyika mjini Babati
  MANYARA 2 PICS 255Mkurugenzi Graysson Kijo akiwa na mshindi wa shindano hilo Buya Ernest mara baada ya kutangazwa mshindi wa modo wa utalii ambaye atawakilisha Mkoa wa Manyara
  MANYARA 2 PICS 256Kulia ni mshindi wa pili katika shindano hilo Veronica Christopher(20),Mkurugenzi wa Event Planners Graysson Kijo pamoja na Buya Ernest(19)mshindi wa shindano hilo.
  MANYARA 2 PICS 283Wafanyakazi wa Events Planner wakiwa katika pozi na mshindi Buya Ernest atakaye wakilisha Mkoa wa Manyara.

  0 0

  MWILI  wa mwandishi mkongwe  David Michael Majebelle.  aliyefariki alfajiri ya Jumapili iliyopita unatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam Julai 18

  Kwa  mujibu wa taarifa rasmi ya familia iliyotolewa leo, mwili huo utaletwa  kutoka katika hospilai ya Mwananyamala  ulikohifadhiwa kisha kupelekwa nyumbani kwake eneo la Sinza  jirani na Lion Hotel   ambapo heshima za mwisho zitatolewa majira ya saa sita mchana kisha  kulepekekwa katika kanisa katoliki la Maria Mama wa Mwokozi  lililopo Sinza na baadaye saa tisa kupumzishwa katika makaburi ya Kinondoni.

  Marehemu Majebele alizaliwa tarehe 03/05/1941 katika kijiji cha Ibiri, Wilaya ya Tabora Vijijini, Mkoa wa Tabora, akiwa mtoto wa tatu (3) wa familia ya watoto 10 wa Mzee Michael Kanyata Majebelle na Mama Theresia Malwa Majebelle ambao wote kwa sasa ni marehemu.

  SHULE

  Alisoma shule ya Msingi ya Bukene (1950) Puge, Wilaya ya Nzega, Mkoa wa Tabora tangu mwaka 1951, Baadaye katika Shule ya Kati (Middle School) ya Sikonge, Wilaya ya Sikonge, Mkoa wa Tabora, mwaka 1954 mpaka 1957.
  Alijiunga na Tabora Boys School kwa masomo ya sekondari mwaka 1958 mpaka mwaka wa 1961.

  Marehemu alikuwa mpenzi wa mpira wa miguu na aliwahi kushiriki kwenye mashindano ya SUNLIGHT CUP enzi zake.

  KAZI
  David aliajiriwa na kampuni ya Almasi ya Williamson Diamonds Ltd ya Mwadui, Shinyanga mwaka 1962 kama Public Relations Trainee. Mwaka 1963 alipelekwa Uingereza kusomea Stashahada ya Uandishi wa Habari/Upigaji Picha za Uandishi. 

  Baada ya kuhitimu alibaki nchini humo kwenye Kampuni ya The Anglo American Corporation kupata uzoefu kable ya kurejea Mwadui kuendelea na kazi ya Afisa Uhusiano wa kampuni ya Williamson Diamonds Ltd hadi Septemba 1967 alipojiuzulu na kuajiriwa na Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways) na kituo chake cha kwanza kikiwa ni Uwanja wa Kimataifa wa Embakasi – Nairobi. Oktoba 1971 alipewa uhamisho na kupelekwa London Uingereza kuwa mwakilishi wa Shirika hilo kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa HEATHROW – London.

  Julai 1974 alihamishwa kutoka Uingereza na kuletwa Tanzania kuwa Meneja Mauzo wa Kampuni Tanzu ya Shirika lililojulikana kwa jina la SIMBA AIR. Lilipovunjika Shirika la Ndege la Africa Mashariki (East African Airways)’

  David Majebelle alijiunga na Shirika jipya la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) kama Meneja Mauzo. Mwaka 1978 aliacha kazi katika Shirika hilo na kujiunga na wamiliki wa magazeti ya AFRICA NEWS na baadaye NEW AFRICA mpaka mwaka wa 1990 kituo chake kikiwa Uingereza. Baada ya pale alianzisha Kampuni yake binafsi kwa jina la MEDIA ADVERTISING CO.Ltd iliyojihusisha na Uhusiano, Matangazo, Upigaji Picha ikiwemo za magazeti mbalimbali kama;

  The Financial Times of London, New Africa African Business, Profit Magazine ,The African Review  na magazeti ya hapa nyumbani
  Kadri umri wake ulivyokwenda aliandamwa na magonjwa ya kisukari na shinikizo la damu. Ilibidi apunguze kasi ya kushughulikia Kampuni hiyo mpaka alipoifunga.

  FAMILIA

  David Michael Majebelle alifunga ndoa mwaka 1975. ameacha mke na watoto wane (4), wa kiume mmoja na wa kike watatu.

  UMAUTI

  Katika miaka miwili ya mwisho wa maisha yake, marehemu amekuwa akisumbuliwa na kisukari na shinikizo la damu. Jumatano iliyopita alifanyiwa vipimo huko hospitali ya Agha Khan ambako aligundulika kuwa amepata “multiple mild strokes”. Jumamosi kuamkia Jumapili iliyopita alifariki dunia.

  Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.

  Raha ya milele umpe ee Bwana; na mwanga wa milele umuangazie, apumzike kwa amani, Amina.

  0 0

   Waziri Mkuu Mizengo kayanza Pinda akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hospital ya Wilaya ya Namtumbo
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa machinjio ya kisasa katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma
   Baadhi ya Viongozi wakishangilia baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kukata utepe
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizundua  mitambo ya kuzalisha umeme katika mji mdogo wa Namtumbo akiwa katika ziara ya mkoa wa Ruvuma.
  -------------------------------------------------
  WAZIRI Mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda ameweka jiwe la msingi na kuzindua miradi miwili ya maendeleo wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma  yote ikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.6.

   Miradi hiyo iliyotembelewa kuwekwa jiwe la msingi  na kuzinduliwa katika siku ya tatu ya ziara ya Waziri mkuu  mkoani Ruvuma ni pamoja na hospitali ya wilaya ya Namtumbo iliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ujenzi  uliofikiwa na itakapokamilika itagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.4 huku akizindua mradi wa machinjio ya kisasa ya mji wa Namtumbo ambayo yamegharimu kiasi cha shilingili milioni 148.

  Katika hatua nyingine Waziri mkuu amewasha rasmi umeme wa jenereta katika mji huo wa Namtumbo ambao ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi milioni 800  na kuwata wananchi wilayani humo kuitumia miradi hiyo yote kujiletea maendeleo ambayo yanapaswa kuibuliwa na wao wenyewe na serikali itatoa ushirikiano mkubwa katika kuifanya wilaya ya Nmtumbo kuwa ya kisasa zaidi.

  Amesema kuwa kuwepo kwa umeme,hospitali na huduma nyingine za muhimu katika maendeleo kutawezekana kwa wananchi wenyewe kujituma katika kufanya kazi zaidi na hsa katika kilimo cha mazao mbali mbali kwa sababu ardhi ya wilaya ya Namtumbo inaruhusu kilimo cha mazao ya chakula na biashara.

  Amesema kuwa maendeleo  yoyote duniani huletwa na wananchi kwa kutumia ipasavyo fursa zilizopo katika maeneo yanayowazunguka hivyo amewataka wananchi wilayani Namtumbo na mkoani Ruvuma kwa ujumla kuzitumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo na serikli itaunga mkono kwa dhati jitihada zozote za wananchi katika suala zima la kujiletea maendeleo.
  Aidha amesema kuwa dhamira ya maendeleo huanza kwa mwananchi mmoja mmoja kwa kukubali kutumia fursa mbali mbali zilizopo katika eneo husika na siyo kwa kukaa na kulalamikia serikali kwa kuitaka iwaletee maendeleo bila wao kujishughulisha katika kuyatafuta maendeleo na amewataka wananchi kuitunza miradi yote ya maendeleo iliyopo kwa ajili ya manufaa yao na kizazi kijacho.

  Waziri mkuu amewataka kutambua kuwa miradi hiyo yote imetumia gharama kubwa ambazozimetokana na kodi zao pamoja na wafadhili ambao nao wanatoa kama msaada kutoka kwenye kodi za wananchi wao hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuithamini miradi hiyo kwa ajili ya maendeleo yao.

  Picha na habari kwa hisani ya demashonews.blogspot.com

  0 0


  0 0

  Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akionyesha moja ya mambo muhimu na yanayotakiwa kuzingatiwa kwa mtu yeyote awapo Mgodini.
  Meneja Mkuu wa Maswala ya Usalama, Afya, Mazingira na Ubora wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Cornelis Van Den Berg akifafanua jambo kuhusu mradi huo wa Madini ya aina ya Uranium wakati wa semina fupi na baadhi ya Wanahabari walioweza kutembelea Mgodi huo leo,na kuweza kujionea na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Mgodi huo.
   Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania inayoshughulika na Mradi wa Uchimbaji Madini aina ya Uranium,uliopo kwenye Kijiji Mkuju,Wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma,Fredrick Kriel akitoa mada ya maswala ya Usalama Mgodini wakati wa Semina fupi kwa Baadhi ya Wanahabari waliofanikiwa kutembelea Mradi huo uliopo pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seluu na kufahamu mambo mbali mbali juu ya Madini hayo ya Uraniuam.
  Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo akielezea namna Kampuni yake inavyoweza kutoa kipaumbele katika kusaidia jamii inayouzunguka mradi huko.
  Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na wahusika wa Mradi huo.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda ambaye ameambatana na wanahabari hao,na wa pili kulia ni Mkuu wa Kitengo ya Mahusiano wa Kampuni ya Mantra Tanzani,Khadija Palangyo.
  Sehemu ya Mandhali ya Mahema ya maofisi ya Kampuni hiyo wakati huu wa Utafiti wa Madini ya aina ya Uranium.
  Wanahabari hao wakiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya viongozi wasimamizi wa Mradi huo.
  Afisa wa Kitengo cha Usalama wa Kampuni ya Mantra Tanzania,Fredrick Kriel akitoa maelezo ya namna mambo yanavyokuwa pindi wawapo kazini.Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage,Teddy Mapunda na kushoto ni Mwanalibeneke Othman Michuzi wakisikiliza kwa umakini.

  0 0

  Mshindi wa Taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2013, Hadija Saidi ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro 2012/13, sambamba na washindi wa Taifa na Dunia wa Miss Utalii Tanzania, wataongoza warembo na washindi wa mashindano yote ya urembo nchini na nchi jirani, katika mbio za nyika za kimataifa za Ant Poaching International Marathon, National Parks International Marathon na Wildlife International Marathon 2013, zitakazo fanyika wakati wa Tamasha la kimataifa la Safari Kuu ya Utalii Tanzania la "Tanzania Great Safari Tour ' 2013, litakalo fanyika kuanzia mwezi Agosti hadi Septemba mwaka huu , katika Ukanda wa Kaskazini, Kusini,Mashariki na Magharibi wa Utalii.

  Mbio hizo za kimataifa za Nyika za ANT POACHING MARATHON 2013, NATIONAL PARK MARATHON 2013 na WILDLIFE MARATHON 2013 ni sehemu ya Tamasha la kimataifa la SAFARI KUU YA KITALII TANZANIA 2013 yaani "TANZANIA GREAT SAFARI TOUR 2013" ambalo pamoja na malengo mengine linalenga katika kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili ikiwemo Uwindaji Haramu, Uvunaji Haramu wa maliasili za Misitu na Baharini ikiwa ni pamoja na Uvuvi haramu na Uharibifu wa Mazingira. Ujangili limekuwa ni janga la kitaifa na tishio kubwa la Ustawi na ukuaji wa Utalii nchini na Duniani, ambapo hatua na juhudi za pamoja zisipochukuliwa sasa basi wanyama waliopo katika hifadhi za Taifa na Mapori ya akiba watatoweka na kuziacha hifadhi hizo zikiwa hazina wanyama tena hasa Tembo,Vifaru,Twiga na jamii nyingi za wanya ambazo hutumika kama kitoweo kwa binadamu.

  Upo ujangili wa uvunaji na usafirishaji haramu wa Misitu ambayo hutoa  magogo na mbao, na kuliacha Taifa likipoteza mapato ,huku uvunaji huo haramu ukitishia maeneo ya misitu hiyo kuwa jangwa. Ujangili ukiachiwa utakosesha watoto wetu na vizazi vijavyo Urithi wa Taifa, lakini pia Taifa litapoteza Mapato yatokanayo na Utalii na Uvunaji mwingine wa Maliasili za nchi. Ujangili ni uhujumu uchumi, kwani sekta ya Utalii inachangia zaidi ya 17% ya Pato la Taifa kila mwaka, zaidi ya 25% ya pato la fedha za kigeni la Taifa na zaidi ya 12% ya ajira zote nchini na Duniani.

  Tamasha la "Tanzania Great Safari Tour 2013, nisafari kuu ya kitalii, ambayo itawajumuisha na kuwaweka pamoja Waandishi wa Habari, Vyombo Vya Habari vya TV,Redio,Magazeti, Majarida, Mitandao ya Internet, Mitandao ya Kijamii na Tovuti. Warembo,Wanamitindo,Wanamichezo, Wana Muziki na Wasanii wa Ngoma za Asili na Filamu, wakitembelea Hifadhi za Taifa ,Ngorongoro Crater, Mapori ya Akiba, Hifadhi za Bahari, Maeneo ya Kitamaduni na Kihistoria huku wakipiga picha za vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa vya Televisheni, Filamu,Video ,Minato, Matangazo ,Makala, Promo DVD'S ,Vipindi vya Televisheni na Majarida huku wakihamasisha Utalii wa Ndani, Vita Dhidi ya Uwindaji Haramu, Uvuvi Haramu, Ujangili na Uharibifu wa Mazingira, huku pia wakitangaza Vivutio vya Utalii Vya Tanzania kitaifa na kimataifa.

  Mbali ya washiriki wa kitaifa , pia kutakuwa na washiriki wa kimataifa, wanadiplomasia, Viongozi wa Serikali, Mashirika ya Kimataifa, Umma, Binafsi na Washiriki binafsi ambao wataandikishwa au watakao hamasika kushiriki. Tamasha la "Tanzania Great Safari Tour 2013 ni Tafsiri vitendo ya Sera ya Taifa ya Utalii, Wanyama Pori, Misitu, Utamaduni ,Uvuvi na Mazingira. Hii itakuwa ni fulsa nyingine kwa Tanzania na mamlaka zake za Utalii sio kutangaza Vivutio vya Utalii Tuu bali kupiga vita Ujangili hususani uwindaji haramu kitaifa na kimataifa. Aidha hii itakuwa ni fulsa kwa Makampuni, Mashirika, Asasi za Umma na binafsi kujitangaza kupitia Tamasha hili kwani litarushwa moja kwa moja (LIVE) katika Televisheni na Internet , na kuangaliwa na zaidi ya watazamaji 680 Milioni Duniani kote. Tamasha hili linaandaliwa na Africa Tourism Promoshen Centre kwa kushirikiana na Miss Tourism Tanzania Organisation.
  Asante,
  Erasto Chipungahelo
  Mwenyekiti Mtendaji – AfricaTourism Promotion Centre / Miss Tourism Tanzania Orgaisatio

  0 0


  0 0
 • 07/17/13--13:30: T.F.T.C Talent Show 2013.
 • Tanzania  Film Training  Center – TFTC ni kituo kwa ajili ya mafunzo
   yanayohusu shughuli za  sanaa  hasa kwa tasnia ya filamu Tanzania,

   TFTC imeanzishwa ikiwa na lengo la kuondoa tatizo la elimu miongoni

   mwa wasanii wa Filamu  waigizaji, Waongozaji, Waandishi wa

  miswaada ya filamu na tamthilia na Wahariri wa filamu na kuongeza

   ajira kwa vijana mbalimbali hapa Tanzania .


  Ndugu Waandishi, mpaka kufikia mwezii Juni  2013 tayari  TFTC

   imeshapokea wanafunzi zaidi ya mia moja (100) katika mihula 

  sita tofauti tangu kilipoanzishwa 2011 na tarehe  25 Julai 2013 TFTC inaaza kuingiza wanafunzi kwa ajili ya Muhula wa Saba. Wanafunzi hao walisajiliwa katika kozi  tofauti za uigizaji, uongozaji, uandishi wa miswaada, uhariri pamoja  na upigaji wa picha za miondoko (picha jongefu) n.k.


  TFTC  Talent  Show 2013.

  TFTC  Talent show ni mpango wa makusudi wa kuibua na kuendeleza vipaji  vingine vya  wanafunzi  walioko  ndani ya TFTC. Ni program inayokusudia kuonesha vipaji kadhaa walivyo navyo wanafunzi ukiondoa vipaji vya uigizaji viliyowaleta hapa TFTC pamoja na kuonesha baadhi ya mambo waliyojifunza wakiwa hapa TFTC kwa  kipindi cha miezi kadhaa  waliyojifunza.


   Malengo ya TFTC Talent Show.

  Malengo mahsusi ya TFTC talenti show  ni kuhamasisha, kuendeleza na kulinda  vipaji vya wanafunzi  ili vipawa hivyo viwe ni sehemu ya nyenzo muhimu ya kuwa  ajira za uhakika  katika Nyanja ya sanaa katika mawanda mapana zaidi lakini pia kuanzisha mahusiano ya kisera, kimkakati na kusaidiana kati ya TFTC na taasisi au Kampuni nyingine .

  TFTC Talent show itafanyika kwa Wanafunzi kuonesha uwezo wao katika fani zifuatazo;

  1.       Maigizo ya Jukwaani

  2.       Vichekesho

  3.       Muziki Bongofleva (R & B, Hiphop n.k)

  4.       Kupiga na kucheza Ngoma za Asili

  5.       Muziki wa Taarabu na dansi

  6.       Kick Boxing

  7.       Kucheza show za nyimbo mbalimbali za ndani na nje

  8.       Sarakasi

  9.       Kuigiza Sauti za watu mbalimbali walio maarufu wa hapa Tanzania.

  10.   Kuigiza kazi za Watangazaji maarufu wa vipindi vya Radio na Televisheni vya Tanzania.

  11.   Burudani Maalumu kutoka  kwa Pastor Myamba (Mkurugenzi wa TFTC ) na Ndugu Wilson Makubi  (Afisa Uhusiano TFTC)


  Ndugu Waandishi shughuli zote zitazofanywa siku hiyo zitafanywa na Wanafunzi wenyewe kuanzia Mc’s, Ma  DJ’s, Wapambaji na watoa burudani.TFTC Talent  Show 2013 inatafanyika 17.8.2013 katika ukumbi wa Ubungo Plazza.


  Aidha tarehe 31.7.2013 katika ukumbi wa TFTC kuanzia saa 5 asubuhi kutakuwa na onesho maalumu kwa Waandishi wa habari  TFTC Mini  Media Talent Show  ukiwa ni sehemu ya maandalizi  tunakualika. 


  Nawakaribisha TFTC


  WILSON  MAKUBI

  AFISA  HABARI  NA  MAHUSIANO.
  0 0
 • 07/17/13--23:13: Edward Lowassa alonga na VOA
 • SONY DSC
  Katika Mahojiano yetu na waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Edward Lowassa pamoja na mambo mengine amebainisha msimamo wake katika mabadiliko ya katiba kuhusu mfumo wa serikali(mbili au tatu), nini dawa ya rushwa na ufisadi nchini Tanzania,hali ya afya yake,kuhusu mabomu ya Arusha na Je atawania urais 2015?Karibu ujiunge nasi kaa standby kuweza kusikiliza mahojiano hayo na Edward Lowassa yatakujia hivi karibuni. SONY DSC
  Mazungumzo kabla ya interview na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa akiperuz kwenye ipad yake. SONY DSCTukiwa na katibu wa Lowassa Bw.Tendewa. SONY DSCNikiwa na Mama Regina Lowassa. SONY DSCNikiwa na Raymond Maro. www.sundayshomari.com

  0 0

   
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili kulia), Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, Hawa Ghasia (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Philippe Dongier (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Uendelezaji wa Miji (OWM-TAMISEMI), Anna Mtani (kushoto) katika tukio la Uzinduzi wa mradi wa kuboresha Miji wa ULGSP, mradi uliozaliwa na mradi Mkakati wa Undelezaji Miji (TSCP) chini ya OWM-TAMISEMI kwa mkopo wa Banki ya Dunia. 
   Wawakilishi wa Benki ya Dunia na Timu ya Mradi wa Kuendeleza Miji Tanzania (TSCP) ulio chini ya OWM-TAMISEMI, wakikagua ujenzi wa Mifereji jijini Mwanza wakati walipokuwa na ziara ya kutembelea miradi hio na kuona maendeleo yake.

    Standi mpya ya Mabasi ya Dala dala iliyopo katikati ya mji wa Kigoma, Ni moja kati ya matunda ya Mradi wa Kuendeleza Miji hapa nchini  (TSCP) chini ya OWM-TAMISEMI.  

  Ujenzi wa Dampo Jijini Arusha, wa TSCP, mradi chini ya OWM-TAMISEMI, ukikaguliwa na wawakilishi wa Banki ya Dunia na timu ya TSCP.


  =======  =======   ==========
  MRADI WA UENDELEZAJI MIJI TANZANIA (TSCP) WAZAA MATUNDA KWA MIJI 18 NCHINI

  Takwimu zinaonyesha mabadiliko ya idadi ya wakazi vijijini kwenda mijini ni kubwa. Katika nchi ya Tanzania idadi ya watu waishio mjini wataipiku idadi ya watu waishio vijijini ifikapo mwaka 2030. Tanzania pia upatikanaji wa miundombinu ni hafifu kwa sekta zote, na hivyo ni vigumu kwenda sambamba na ongezeko la idadi ya watu.


  Tanzania kama zilivyo nchi nyingi zinazoendelea, imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali za maendeleo ya miji zikiwemo; ongezeko la watu kwa kasi mijini; miundombinu isiyokidhi mahitaji ya uendeshaji wa miji; uwezo mdogo wa rasilimali kwa ajili ya kutoa huduma toshelevu za jamii na kupanuka kwa kasi kwa maeneo ya miji bila kuzingatia taratibu za Mipango miji na Usimamizi usiokidhi kasi ya maendeleo ya miji katika Halmashauri zetu


  Hata hivyo jitihada zinazoendelea kufanyika nchini Tanzania katika miradi mbalimbali zitaleta ahueni ya tatizo linalofikiriwa kutokea, ikiwa ni pamoja na miradi ya TSCP, Mpango wa Kuimarisha Serikali za Mitaa Mijini (ULGSP) na hata mradi unaofanana na TSCP na ULGSP, mahususi kwa Jiji la Dar es Salaam, (Dar es Salaam Metropolitan Development Project - DMDP), ulio katika mchakato wa kujiandaa  kwa utekelezaji wake.


  Mradi wa uendelezaji Miji (TSCP) unaoendelea kutekelezwa katika Miji 7 nchini (Arusha, Dodoma,Tanga, Mbeya, Mwanza, Mtwara na Kigoma), umezaa matunda kwa mradi mwingine wa ULGSP. Hali hii ilielezwa rasmi na Waziri Mkuu, Mizengo K. Pinda (Mb.) wakati akizindua mradi huo wa ULGSP – 18 juni, Kuringe Hall – Moshi. 


  Akitoa pongezi zake kwa timu ya TSCP, alisema kuwa mafanikio yaliyoonekana katika mradi wa TSCP yamerahisisha kupatikana kwa mkopo mwingine kutoka Banki ya Dunia kwa ajili ya kuendeleza azma hiyo hiyo, mradi huo umejikita katika kuimarisha Halmashauri za Miji 18, ambazo ni Miji yote iliyobaki ya Tanzania Bara, na mradi utagharimu kiasi cha Dola milioni 255 kwa kipindi cha miaka mitano.


  Aidha Mhe. Pinda alieleza kuwa jambo muhimu sana la kuzingatiwa na kuhakikisha kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kiasi cha watu kujidhihirishia wenyewe kwa kuona kwa vitendo mafanikio, alieleza kuwa Serikali haitafumbia macho uzembe au ubadhirifu wa fedha au vifaa utakaosababisha kazi hii kukwama au kutekelezwa chini ya kiwango.


  Pia Mhe.Pinda alisisitizia Wananchi kushirikishwa kikamilifu, alisema; “Nasisitiza wadau wote washirikishwe katika ngazi zote na taarifa za utekelezaji wa mradi ziwekwe wazi ili wadau wote wajue, watoe maon ya kukosoa au kuboresha”. Aliendelea kusema; “Kwa wale wanasiasa wenzangu, ni fursa ya kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha mradi unafanikiwa kama tunavyotarajia”.


  Aidha Mkurugenzi wa Benki ya Dunia – Tanzania, Bw. Philippe Dongier alieleza furaha yake ya kuona maendeleo mazuri ya utekelezaji wa TSCP, na kueleza kuwa ana matarajio makubwa zaidi na ULGSP. Alisema; “Lengo kuu la Mpango ni kujenga na kuimarisha uwezo wa Halmashauri kutoa huduma na usimamizi wa Miji.  Kupitia mpango huu, mabadiliko ya ufanisi ya muda mrefu yanatarajiwa katika maeneo ya Mipango Miji, mfumo wa kudhibiti fedha, uwajibikaji, uendeshaji na matengenezo na ukusanyaji wa mapato”.


  Miji husika (18), imeshaandaa Mipango Mikakati tayari kwa kuanza utekelezaji ifikapo mwezi Julai 2013.Mradi umelenga kuendelea kuziimarisha Halmashauri za Miji katika maeneo makuu matano ili ziweze kutoa huduma bora zaidi kwa kuzingatia sera ya Ugatuaji Madaraka (D by D). Maeneo yaliyolengwa ni pamoja na; Uboreshaji wa mfumo wa Mipango miji, ukusanyaji wa mapato ya ndani hususan mapato yatokanayo na kodi ya majengo, uboreshaji wa mifumo ya udhibiti wa fedha, manunuzi na masuala ya mazingira na kijamii, uboreshaji wa mifumo ya utekelezaji, uendeshaji na utunzaji wa miundombinu kwa ajili ya huduma za jamii, na kuboresha uwajibikaji na uwazi. Na baadhi ya shughuli husika zitahusisha; ujenzi wa barabara, masoko, maeneo ya kupumzika na kudhibiti taka ngumu.


  ULGSP ni mradi wa kwanza katika Bara la Afrika chini ya “Mpango kwa Matokeo” (Program for Results – P for R). “Mpango kwa Matokeo” ni mbinu ya utoaji fedha kulingana na matokeo ya utekelezaji malengo mliyojipangia.  Chini ya Mpango huu, Halmashauri husika zitafanyiwa tathmini ya utekelezaji wa vigezo vilivyopangwa kila mwaka na fedha zitatolewa baada ya matokeo kuhakikiwa.

  Mbali na mradi wa TSCP na ULGSP,  Serikali  ya Tanzania ikishirikiana na Benki ya Dunia na Wadau wengine kuanzia miaka ya 1990 imetekeleza Miradi ya Ukarabati wa Miundombinu Mijini [Urban Sector Rehabilitation Project (USRP)]kuanzia 1997 hadi 2004 kwa gharama ya dola za Kimarekani million 104.9. Mradi huu ulitekelezwa katika miji 9 ya Tanga, Moshi, Arusha, Mwanza, Tabora, Morogoro, Mbeya, Iringa na Dar es Salaam na Mradi wa kuzisaidia Serikali za Mitaa zote (Local Government Support  Project - LGSP) kuanzia 2004 hadi 2012 nao ulikuwa ni mkopo wa Benki ya Dunia kwa gharama ya dola za Kimarekani million 52.


older | 1 | .... | 120 | 121 | (Page 122) | 123 | 124 | .... | 1903 | newer