Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1207 | 1208 | (Page 1209) | 1210 | 1211 | .... | 1896 | newer

  0 0

  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha pamoja na Wananchi wa Kata ya Madibira wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
  Sehemu ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.

  ………………….

  Halimashauri ya Wilaya ya Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng’ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa chapa ili kurahisisha kuweza kujua ng’ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia kila mfugaji awe na ng’ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia uharibifu wa mazingira uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi. Katika maagizo hayo pia Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa kushirikiana na Wananchi wake kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira unaosababishwa na kuingizwa kwa mifugo katika mto Ndembela kwa ajili ya kunywa maji.

  Maagizo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard Muyungi alipokua akiongea na Wananchi wa kata ya Madibira wakati wa mkutano na Wananchi juu ya kujua na kufahamu changamoto mbalimbali zinazosababaisha uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito inayozunguka Mto wa Ruaha Mkuu ukiwemo mto Ndembela.

  Akiongea katika Mkutano huo Bwana Muyungi pia ameahaidi kushughulikia Wawekezaji ambao siyo waaminifu wanaotumia maji bila kibali cha Serikali au wale ambao wanazidisha kiwango cha uchukuaji maji tofauti na kile kilichoanishwa katika kibali . Alisema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inaratibu na kuhakikisha rasilimali zote zilizopo Nchini zinatumika kwa usahihi .

  Akijibu hoja hizo Mhe. Diwani wa Kata ya Madibira kwa niaba ya Mkurugenzi aliahidi Halimashauri hiyo kuyafanyia kazi mambo yote waliyoagizwa kuyafanya. Aliongeza kuwa atasimamia yote na pia atashirikiana na Wananchi wa Madibira kuhakikisha maagizo yote yanapatiwa ufumbuzi.

  Baada ya Mkutano huo pia Wajumbe wa Kikosi kazi hiko walipata fursa ya kutembelea shamba la mpunga la chama cha Wanaushirika Madibira (MAMCOS) kwenda kujionea shughuli mbalimbali za utunzaji wa maji kwa ajili ya kilimo zinavyofanyika. Akiongea baada ya kutembelea shamba hilo la hekta 3000, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja aliwapa agizo la kuweka geji itakayodhibiti kiasi cha maji yanayotoka shambani baada ya matumizi ya umwagiliaji kufanyika. 
   
  Pia wametakiwa kutengeneza miundo mbinu shambani ili kuwezesha barabara ya shambani hapo kupitika kwa urahisi na maji kutomwagika hovyo. Pia kusafisha shamba lao mara moja kuondoa nyasi na magugu yalioota kwenye mifereji ya kupitishia maji shambani hapo.

  Kikosi hiko cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kiliundwa na Makamu wa Rais wa Tanzania kikijumuisha Wajumbe kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kikosi kazi hiko kimegawanyika katika makundi matatu (Iringa, Mbeya na Njombe.

  0 0

  Mkurugenzi wa kituo cha mazoezi ya Bodyline Health &Fitness, Abbas Jaffer Ali  (katikati) akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza tamasha la michezo linalotarajiwa kufanyika Aprili 22, 2017 Mayfair jijini Dar es Salaam. Pembeni ni Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (kulia) na mwalimu wa mazoezi.
  Kituo cha mazoezi cha Bodyline Health& Fitness kimeandaa tamasha la mazoezi litakalofanyika kesho jumamosi Mayfair Msasani jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza mkurugenzi wa Bodyline Health& Fitness, Abbas Jaffer Ali alisema kuwa lengo la tamasha hilo ni kuwajenga watanzania wapende kufanya mazoezi ili kuimalisha afya zao.
  Aliongeza kuwa katika tamasha hilo kutakuwa na michezo mbali mbali ikiwemo shindano la kutunisha mishuli, kuogelea na viungo vya mwili.
   Waandishi wa habari wakifuatilia mkutano.
  Katibu Mkuu - Shirikisho la Watunisha Misuli Tanzania, Francis Mapugilo (katikati) akisisitiza watzania kujitokeza kwa wingi kushiriki mazoezi.
   Baadhi ya washiriki wa mchezo wa kutunisha misuli wakionyesha umahili wao.

  0 0

   Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye amekuwa akifanya vyema ndani na nje ya nchi (anga za Kimataifa),Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU,mapema leo jijini Dar.
  Wakati wa uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza manukato 'pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la Taifa kwa kulipa Kodi.

  Amesema kuwa kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.

  Katika mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
  Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi chupa ya Pafyum,mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Aisha Azori,wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia anafanya vyema katika kazi zake za Muziki,kushototo ni Mmoja wa mameneja wa Diamond Plutnamz almaarufu kwa jina la Babu Tale. 
   Msanii Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
   Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika jijini Dar Es Salaam mapema leo.
  Baadhi ya Wanahabari wakimsikiliza Diamond alipokuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa Pafyum hiyo ambayo tayari imekwisha sambaza kwenye maduka mengi jijini Dar.
   Mmoja wa Meneja wa Diamond Platnumz almaarufu kwa jina la Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana kwa jina la CHIBU
   Diamond Platumz akiendelea kuzungumza na Wanahabari pamoja na Wadau wake waliofika kulishuhudia tukio la uzinduzi huo


  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameungana na wabunge katika kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Dkt. Elly Macha aliyefariki Machi, 31, 2017 katika hospitali ya New Cross Wolverhampton nchini Uingereza.

  Akizungumza katika tukio hilo Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia marehemu pamoja na wabunge wote. Amesema enzi ya uhai wake marehemu Dkt. Elly alitoa mchango mkubwa na ushauri mzuri katika masuala ya elimu na uboreshaji wa maeneo ya watu wenye ulemavu.

  Awali akisoma wasifu wa marehemu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mheshimiwa Mchungaji Peter Msigwa alisema Dkt. Elly alipata ulemavu wa macho akiwa na umri wa miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa surua.

  Mchungaji Msigwa alisema pamoja na kuwa na ulemavu huo wa macho lakini haukuwahi kuwa kikwazo kwake kwani aliweza kufanya jambo lolote lililokuwa ndani ya uwezo wake.

  Mwili wa marehemu Dkt. Elly umesafirishwa leo kwenda nyumbani kwake Usa River mkoani Arusha na anatarajiwa kuzikwa kesho nyumbani kwa wazazi wake katika kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro.

  Dkt. Elly alizaliwa Juni 18, 1962 kwenye kijiji cha Kirua Vunjo mkoani Kilimanjaro, ambapo mbali na wadhifa wa ubunge pia  aliwahi kuwa Mshauri Mwelekezi wa Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu vya Afrika Mashariki.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (Kulia), Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) wakishuhudia mwili wa Marehemu Mhe. Elly Macha ukiwasili, Marehemu aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza  baada ya mwili kuwasili  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza  wakati wakati wa kuagwa kwa mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza  wakati wa kuagwa kwa  mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton, nchini Uingereza na mwili umeagwa  leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
  Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson akiaga mwili wa marehemu Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross,Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
   Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akisalimiana na Waziri Mkuu Mhe, Kassim Majaliwa wakati wa kuagwa kwa mwili wa Mhe. Elly Macha aliefariki Mwezi uliopita katika Hospitali ya New Cross, Wolverhampton nchini Uingereza na mwili wake umeagwa leo katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.

  0 0  0 0

  Mchezo wa Robo Fainali ya Nne ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na Tanzania Prisons FC utafanyika kesho Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

  Mchezo huo utatoa mshindi ambaye ataungana na timu nyingine tatu ambazo tayari zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali. Timu zilizotangulia Nusu Fainali ya ASFC ni za Mbao FC, Simba SC na Azam FC.

  Jumapili Aprili 23, mwaka huu kutakuwa na droo ya wazi kwa timu nne zitakazokuwa zimefuzu kwa hatua ya Nusu Fainali ya ASFC, itakayofanyika Kituo cha Televisheni cha Azam ambao ni wadhamini wakuu wa jina la michuano na haki ya kuonesha mubashara michuano hii ambayo inafanyika kwa msimu wa pili mfululizo.

  Azam FC ilikata tiketi ya kucheza Nusu Fainali ya ASFC baada ya kuifunga Ndanda FC mabao 3-1, kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam Aprili 5, 2017 ikitanguliwa na Mbao iliyoishinda Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo ulifanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, 2017 ilihali Machi 19, mwaka huu Simba iliwatoa Madini ya Arusha kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

  Nusu Fainali inatarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu, kabla ya fainali ambako Bingwa wa michuano hii ambayo msimu huu ilishirikisha timu 86 ikiwa ni pamoja na za Ligi Kuu ya Vodacom (timu 16); Ligi Daraja la Kwanza (timu 24); Ligi Daraja la Pili (timu 24) na mabingwa wa mikoa timu 22, atazawadiwa Sh. 50 milioni na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho - CAF.

  0 0

  Bw. Justine Ngaile Mkurugenzi wa Kinga na Mionzi kutoka Tume ya Atomiki akiwasilisha mada kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Luhaga Mpina. Waziri Mpini alikutana na Taasisi zinazohusika na usimamizi wa kemikali kujadilili mkakati wa pamoja wa kusimamia kemikali nchini.
  Baadhi ya wataalamu kutoka Taasisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Tume ya Nguvu za Atomiki wakifuatilia majadiliano na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina (hayupo pichani), kikao kazi hicho kimefanyika katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dodoma.

  ……………..

  Na Lulu Mussa,Dodoma

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, hii leo amekutana na taasisi zizohusika na uratibu na usimamizi wa kemikali hapa nchini.

  Akiongea na Taasisi hizo, Waziri Mpina amewaagiza watendaji hao kudhibiti na kusimamia kemikali hatarishi nchini ikiwa ni pamoja na kuratibu usafirishaji, usambazaji na matumizi ya kemikali hizo hapa nchini kwa namna bora zaidi.

  Waziri Mpina amezitaka taasisi hizo kutoa taarifa za utendaji wa kazi kila robo ya mwaka kwa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimizi wa Mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira kifungu namba 170. “Nawaagiza kuwasilisha takwimu za kemikali zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa au kusafirishwa nje ya nchi, pamoja na kuainisha viwanda vinavyozalisha kemikali vilivyosajiliwa na maghala yaliyosajiliwa kuhifadhi kemikali hizo” alisisitiza Mpina.

  Katika kikao hicho Waziri Mpina pia ameliagiza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini ndani ya miezi miwili kuandaa muongozo na kuupitisha katika hatua zote wa namna bora ya kuteketeza taka hatarishi bila kuathiri mazingira.

  Aidha Waziri Mpina ameagiza kuandaliwa kwa andiko litakalobainisha umuhimu wa kuteketeza taka hatarishi. “Kama taifa ni lazima tuwe na “dedicated Incinerator” kubwa kutekeza taka hizo hatarishi kwa kuzingatia taka zinazozalishwa hapa nchini” Mpina alisisitiza.

  Katika hatua nyingine, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini, Wakala wa Maabara ya Veterinari Tanzania, Tume ya Nguvu za Atomiki, Taasisi ya Utafiti ya Viuatilifu katika Kanda za Kitropiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa, OSHA na Mkemia Mkuu wa Serikali kwa pamoja wametakiwa kuanda Hati ya Makubaliano ya kuratibu utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhuisha Sheria zao na kuleta mapendekezo Serikali ya vifungu vya kufanyiwa marekebisho.

  Taasisi alizokutana nazo ni pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), Taasisi ya Nguvu za Atomiki, Mamlaka ya Chakula na Dawa na Mkemia Mkuu wa Serikali.

  0 0

  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng. Joseph Nyamhanga (Wa pili kulia), akizungumza na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi zilizo chini ya Wizara katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
  Mmoja wa wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Bw. Shukuru Sikunjema, akitoa maoni yake kwa Mwenyekiti Wa Baraza la Wafanyakazi Eng. Joseph Nyamhanga katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) wakifuatilia maelekezo ya Baraza la Wafanyakazi wakati wa kikao hicho kilichofanyika Mkoani Morogoro.
  Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Wakiimba nyimbo ya ‘Solidarity forever’ kuonyesha mshikamano katika utendaji kazi wakati wa Kikao cha Baraza la Wafanyakazi, Mkoani Morogoro.

  Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika Mkoani Morogoro.

  Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  …………..

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Eng.Joseph Nyamhanga, amewataka watumishi wa Wizara hiyo kutekeleza majukumu yao kwa weledi na uadilifu ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano.

  Akisoma hotuba ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Profesa Makame Mbarawa, katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi leo, mkoani Morogoro, Eng. Nyamhanga, ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yao ili kuleta tija kwa Serikali na Taifa kwa ujumla.

  “Naliomba baraza hili la wafanyakazi kuhakikisha linahamasisha watumishi wote wa Wizara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili, weledi na ushirikiano ili kuleta ufanisi”, amesema Eng.Nyamhanga.

  Aidha, Eng. Nyamhanga amelisisitiza Baraza hilo kuandaa mkataba wa kupima utendaji kazi wa watumishi katika majukumu yao ya kila siku ili kupima ufanisi wa watumishi hao kuanzia ngazi ya juu hadi ya chini.

  Katibu Mkuu Nyamhanga , amelitaka Baraza hilo kuweka mazingira maalum kwa watumishi ikiwemo kuandaa mpango wa mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuongeza ujuzi kwa watumishi wa Wizara hiyo.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi Tawi la Ujenzi Bw. Samuel Mticco, amemhakikishia Katibu Mkuu huyo kutekeleza maagizo yote yaliyosemwa katika Baraza hilo ikiwemo la uandaaji wa mkataba wa utendaji kazi kwa watumishi.

  Kikao hicho cha siku moja cha Baraza la wafanyakazi la Sekta ya Ujenzi pamoja na mambo mengine kimekubaliana kupunguza matumizi ya fedha za Serikali yasiyo ya lazima pamoja na kupambana na vitendo vya ufisadi na rushwa.

  Imetolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

  0 0  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na uongozi wa Chama cha Ngoma na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) wakati alipokutana nao Ofisini kwake Mjini Dodoma kujadili masuala mbalimbali ya Sanaa za Ngoma na Muziki Asili Tanzania Leo April 21, 2017.
  Mwenyekiti wa Chama cha Ngomana Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Wanne Salim Kutoka Kikundi cha Wanne Star akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili wasanii wa Ngoma na Muziki Asili kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017.

  Katibu wa Chama cha Ngoma na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Richard Muro akifafanua jambo kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21,2017.
  Mmoja wa wasanii kutoka Chama cha Ngoma na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Zuhura Khatib akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017.
  Mmoja wa wasanii kutoka Chama cha Ngoma na Muziki wa Asili Tanzania (CHANGAMATA) Zuhura Khatib akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe wakati walipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma Leo April 21, 2017.

  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.

  0 0

  Meneja Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini, uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanza.
  #BMGHabari
  Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
  Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
  Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro (mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo kitaifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
  George Binagi-GB Pazzo
  Wakazi wa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu inayosambazwa na kampuni ya Sun King.

  Meneja Masoko wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo Jijini Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.

  “Kila Kijiji nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.

  Mkuu wa Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.

  Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa Tawala wilayani Nyamagana, amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia itazalisha ajira zaidi kwa vijana. Tazama hapa uzinduzi zaidi

  0 0  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea jambo wakati alipotembelea Viwanja vya Jamhuri Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Maadhimisho Bi.Flora Mazeleng’we alipotembelea uwanja wa Jamhuri Dodoma ili kuangalia maandalizi ya maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano. Aprili 21, 2017.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano katika viwanja vya Jamhuri Dodoma Aprili 21, 2017.

  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Muungano wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya sherehe hizo Aprili 21, 2017 Dodoma.
  Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Muungano Bw.Yusto Chuma akionesha michoro ya muonekano wa uwanja wa Jamhuri kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe.Jenista Mhagama wakati wa maandalizi ya Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano yanayoendelea Dodoma Katikati ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza jambo wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya sherehe za Muungano katika viwanja vya Jamhuri Dodoma wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.January Makamba na kulia Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maelekezo ya kuboresha maeneo kadhaa katika Uwanja wa Jamhuri wakati wa maandalizi ya Shereha za Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano Dodoma.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akiongea jambo wakati alipotembelea Viwanja vya Jamhuri Dodoma ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.
  (PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

  0 0

  Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya TBL Afrika Mashariki, Thomas Kamphuis akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya bia ya Castle Lite 'Castle Lite Unlocks' jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


  TAARIFA KWA UMMA
  KUONGEZA MUDA WA KUBADILISHA CHETI CHA CHANJO YA HOMA YA MANJANO

  Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo  watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale  wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya.

  Wizara inapenda kutoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kama ifuatavyo. Kabla ya kuanza matumizi ya vyeti vipya, wastani wa wasafiri 800 walikuwa wanapatiwa chanjo kwa mwezi kupitia vituo vilivyoruhusiwa na Wizara. Baada ya kuzindua vyeti vipya na kuongeza udhibiti wa vyeti feki idadi ya wanaopata chanjo imeongeza kutoka 800 hadi 2,445 kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la mara 3 ya waliokuwa wanachanja hapo awali. Ongezeko hili limesababishwa na wasafiri zaidi ya 1,644 kusalimisha vyeti feki kwa mwezi na kuchanjwa na kupewa vyeti halali. 

  Kwa ujumla tangu matumizi ya vyeti vipya vianze mwezi wa Agosti mwaka 2016 mpaka mwezi Machi 2017, jumla ya wasafiri 19,557 wamepatiwa chanjo ambapo kati yao 13,157 wamesalimisha vyeti feki na kupatiwa chanjo, hii ni sawa na asilimia 67.2. Halikadhalika, watu 11,644 wamebadilisha vyeti vyao halali vya zamani. 

  Kupata cheti bila kupata chanjo ni kosa na kunahatarisha afya yako na Afya ya Jamii, kwani ukienda katika nchi zenye hatari ya ugonjwa wa homa ya manjano, unaweza kuambukizwa kwasababu huna kinga na hatimaye kuleta ugonjwa huo nchini. Vile vile zoezi hili limebaini uwepo wa vituo vinavyotoa chanjo hii bila kuwa na kibali cha Wizara, hili ni kosa na hivyo ni marafuku kituo chochote kutoa chanjo hiyo hadi hapo vituo hivyo vitakapopata kibali. Aidha, kwa wale ambao wananunua au kutoa vyeti bila kupata chanjo nao wanatenda kosa hivyo, waache mara moja kwani mkono wa sheria utachukua mkondo wake.

  Tarehe 16 Februari 2017 Wizara ilikumbusha kubadili vyeti vya zamani katika muda uliopangwa yaani Januari 1 hadi Machi 31, 2017. Kutokana na tathmini tuliyoifanya imeonekana kuwa watu wengi bado hawajabadili vyeti vya zamani na kutokana na umuhimu wa zoezi hilo kwa afya ya jamii, tumeamua kuongeza muda wa mwezi mmoja ili watu wapate nafasi ya kubadili vyeti vyao, hivyo zoezi hili litaendelea na litaitimishwa tarehe 30.04.2017. Wizara inatoa wito kwa watu ambao bado wana vyeti vya zamani kufika katika vituo vya kutolea huduma na kuvibadilisha. Baada ya muda huo kupita hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza.

  Wizara inawakumbusha tena kuwa ugonjwa wa homa ya manjano haupo nchini ila kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, Tanzania ipo katika ukanda wa nchi zenye kiwango kidogo cha maambukizi ya ugonjwa huo (low risk country). Hata hivyo, tupo katika hatari ya kuupata ugonjwa huo kutokana na kuzungukwa na nchi zilizopo kwenye ukanda wa kiwango cha juu cha hatari ya ugonjwa huo (High risk countries). Hivyo ni jukumu la kila mtu kuhakikisha tunajilinda dhidi ya ugonjwa huo kuingia nchini.

  Ugonjwa huu husambazwa na mbu jike aina ya Aedes aliye na virusi vya ugonjwa huo. Mpaka sasa duniani hakuna dawa ya kutibu ugonjwa huo na mgonjwa hupatiwa matibabu ya kupunguza maumivu au kutibu dalili zinazojitokeza. Njia pekee ya kujikinga na ugonjwa huu ni kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huo. Chanjo hiyo huanza kufanya kazi kiufasaha siku kumi baada ya mtu kupata chanjo hiyo. Hivyo, nawasihi wanaosafiri kupata chanjo hiyo angalau siku kumi au zaidi kabla ya kusafiri kwenda kwenye nchi zenye maambukizi.  Aidha, kwa watu wasio na safari hawahitajiki kupata chanjo hiyo.

  Vile vile, kwa wale ambao hawastahili kupata chanjo kwa sababu za umri (miaka 60 na kuendelea), wajawazito na watu wenye sababu za kiafya zilizothibitishwa na Daktari, watapatiwa cheti maalaumu kijulikanacho kama“International Vaccination Exemption certificate” pamoja na kupewa ushauri wa hatua za kiafya za kuchukua dhidi ya kujikinga na ugonjwa huo.

  Mwisho, Wizara inapenda kuwashukuru wale wote walioitikia wito wa zoezi hili la kubadili vyeti kwani wamefanya hivyo kwa manufaa yao na ya Taifa. Halikadhalika, wale ambao hawajabadili vyeti vyao watumie muda huu wa nyongeza kufanya hivyo.

  Imetolewa na;
  Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya
  21-04-2017.

   

  0 0  NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt, Juliana Palangyo, (pichani anayezungumza), ametembelea miradi ya kuzalisha umeme wa Gesi Asilia ya upanuzi wa Kinyerezi I pamoja na ule wa Kinyerezi II.

  Akizungumza katika ziara yake ya kukagua miradi hiyo, Dkt Pallangyo ameridhishwa sana na jitihada zinazofanywa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati, ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi wa kinyerezi II umefikia asilimia 53%.

  “Niwapongeze sana TANESCO kwa jitihada kubwa mnazozifanya katika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati, ambapo mmewezesha Majenereta 8 yenye jumla ya Megawati (MW) 240 mpaka sasa yameshafika, hii ni hatua nyingine kubwa sana ,hivyo kupitia Mradi huu wa kinyerezi nina amini Tanzania ya Viwanda inawezekana”.

  Akielezea maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Kinyerezi II, Meneja wa Kituo hicho Mhandisi Steven Manda alisema kuwa kituo hicho kinaendelea vizuri na ujenzi katika kuhakikisha kinakamilika Desemba 2018, ambapo mpaka sasa ukamilifui wa Mradi huo unategemea Kinyerezi I kutokana na Baadhi ya mitambo kuingiliana hasa mitambo ya mfumo wa upozaji maji ambao utaunganishwa na mtambo wa Kinyerezi I.

  Naye Kaimu meneja wa Kituo cha Kinyerezi I Mhandisi Lucas Busunge amesema kuwa Mradi huo wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 150, Umeongezewa uwezo wa kuzalisha Megawati zingine 185 ikiwa ni Awamu ya pili ya upanuzi wa Mradi huo.

  Kwa ujumla miradi yote miwili itakapokamilika, jumla ya Megawati 575MW za umeme utokanao na Gesi Asilia, zitazalishwa na kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa na hivyo zitasaidia kuongeza upatikanaji wa Umeme wa Uhakika na kuwezesha wananchi wengi kupata huduma ya umeme na kufikia malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuhakikisha Umeme unatumika kama njia moja wapo ya kuleta maendeleo ya wananchi na kuinua vipato vyao binafsi na Taifa kwa ujumla. Naibu waziri Pallangyo alifanya ziara hiyo Aprili 20, 2017.
  Mafundi wakiendelea na kazi katika moja ya jengo lilopo katika mradi wa kufua umeme wa gesi asili megawati 240 wa Kinyerezi I ambapo unafanyiwa upanuzi.
  Naibu katibu Mkuu wa wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Pallangyo (wa pili kutoka kushoto) akiambatana na viongozi wa TANESCO alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Miradi ya Umeme Kinyerezi I&II. Kulia kwake ni kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Bi.Joyce Ngahyoma akifuatiwa na Kaimu Meneja Uhusiano Bw. Yasini Didas Slayo Kulia pamoja na Meneja Mradi wa Kinyerezi II, Mhandisi Stephen Manda, (Kushoto)

  0 0

  Na Alex Mapunda, Ruvuma 
  KATIBU wa timu ya Daraja la Pili, The Mighty Elephant Fc toka Songea Rajabu Dau, amesikitishwa na viongozi wa Shirikisho la soka hapa nchini TFF kwa kushindwa kupokea simu yake zaidi ya mara nne pindi anapowapigia ili kuulizia kuhusu Rufaa yao kuhusu upangwaji wa Matokeo kati ya Timu ya Mawenzi dhidi ya Saba Saba zote za Morogoro. Dau amesema kila akiwapigia simu TFF simu zao zinaita bila Majibu, suala ambalo linaleta mashaka kwa kuwa rufaa yao toka walipopeleka ina takribani miezi Miwili na TFF wako kimya hadi leo wakati wao walifuata Taratibu zote za kukata rufaa zilizowekwa na TFF.  
  “TFF wanatukosea, napiga simu ya Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa hapokei, Eliud Mvela naye hapokei simu. Kwanini wanakaa Kimya wakati Rufaa walishapokea na uthibitisho walishanipa? Mbona rufaa za timu kubwa wanazifanyia maamuzi mapema? Au sisi kwa kuwa tupo ligi daraja la pili hatuna haki?, TFF naomba watume majibu ya rufaa yetu, kabla hatujafanya maamuzi magumu. ” “Sisi tulikata rufaa kuhusu kupinga matokeo ya Sabasaba na Mawenzi, matokeo ambayo yalipangwa na chama cha soka mkoa wa Morogoro ili kuipandisha timu moja kwa nguvu. 

  Tuna sauti ya dakika 23 ya kikao cha siri ambacho kiliwakutanisha viongozi wa soka Morogoro, viongozi wa SabaSaba pamoja na Mawezi ambapo wote walikubaliana Sabasaba acheze chini ya kiwango ili Mawenzi apate pointi tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria na taratibu za mpira wa miguu” “ Lakini baada ya Mawenzi kupata pointi Tatu toka kwa Sabasaba, kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Soka Morogoro aliahidi kuisaidia Saba Saba isishuke daraja kwa kutumia fedha. Katika kikao hicho walikuwepo hadi viongozi wa Serikali na sauti zao zimesikika” alisisitiza Dau. 

  Lakini taarifa toka kijiweni kwa wadau wa soka wao wanasema TFF wanashindwa kutolea uamuzi kuhusu suala la The Mighty Elephnt Fc kwa kuwa Uchaguzi umekaribia na Chama cha Soka cha Morogoro ni moja ya Kambi muhimu upande wa Malinzi. Timu ya Mawenzi, Sabasaba na The Mighty Elephant wote walikuwa kundi moja katika ligi daraja la pili ambayo imemalizika hivi karibuni.

  0 0
 • 04/22/17--00:17: Article 8

 • 0 0

   Kaimu Kamishna wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Wilson Ruge akizungumza na Waandishi wa Habari wakati ufunguzi wa mafunzo wa Waandishi wa habari wa Masuala ya ardhi nchini juu ya kutambua umuhimu wa Kulipa Kodi ya Ardhi kwa Wizara ya Ardhi na Kodi ya Majengo kwa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)
   Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mboza Lwandiko akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara
   Afisa Msaidizi wa huduma kwa mlipa kodi Maya Magimba akitoa somo kwa Waandishi wa Habari juu ya umuhimu wa kulipa kodi ya majengo na kutofautisha kodi hiyo na kodi ya Ardhi maya ambaye aliwataka waandishi wa habari kutumia mafunzo hayo kwa ajili ya kuwa elimisha Watanzania hili waweze kulipa kodi za ardhi kama inavyohitajika kwa mujibu wa sheria
   Afisa Ardhi kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Denis Masami akifafanua masuala muhimu ya Ardhi kwa Waandishi wa Habari
  Mmoja ya Waandishi wa Habari akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusu ulipaji wa kodi

  0 0

  Na Mohammed Hammie Rajab

  "Hujambo msikilizaji wa Pangani Fm na karibu katika kipindi cha Sauti Ya Mwanamke, kipindi hiki ni mahsusi kwa ajili ya kujadili changamoto mbali mbali anazokabiliana nazo mwanamke...." Ni sauti yake Maajabu Ally Madiwa anapokuwa redioni akitangaza kipindi.
   
  Sauti yake iliyojaa bashasha ya kumfanya kila msikilazaji wa redio Pangani Fm iliyopo wilayani Pangani mkoani tanga atake kuisikia awapo redioni ndiyo iliyomfanya mpaka sasa awe miongoni mwa waandishi wa habari wadogo Tanzania wenye vipaji vya hali ya juu.
   
  Uwezo wake wake kutangaza na kutambua aina gani ya habari inapaswa kutolewa kwa jamii anayoifanyia kazi uligunduliwa na shirika la Uzikwasa lenye kufanyanshughuli zake wilayani Pangani, ambalo linaelimisha jamii kwa kutimia sanaa.
   
  Shirika hili limekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha jamii ya Pangani kuachana na tabia hatarishi, kupinga ukatili dhidi ya watoto, wasichana na wanawake, na kuhakikisha viongozi
  wanatekeleza majukumu yao kwa mguso.
  Huko ndipo ambapo Maajabu Ally Madiwa aliponogesha uwezo wake  mpaka kuwa miongoni mwa wateule 66 wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2016 kati ya washindani 810.
   
  Maajabu Ally anakuwa mwandishi wa habari pekee kwa tuzo za Ejat za mwaka 2016 kutokea mkoani Tanga, kati ya waandishi 31 kutokea mkuo huo ambao waliwasilisha kazi zao kupitia tuzo hizo zenye heshima ya hali ya juu kwa sasa nchini Tanzania.
   
  Endapo mwandishi huyu chipukizi kutokea mkoani Tanga atafanikiwa kutunukiwa tuzo na zawadi kwenye sherehe za kilele mnamno April 29 2017 basi atakuwa anachukua tuzo yake ya pili na itakuwa faraja si tu kwa Pangani Fm na Uzikwasa pekee bali kwa waandishi wa Tanga nzima.

  Ikumbukwe mnamo mwaka 2015 Pangani Fm ilifanikiwa kutoa waandishi wawili kwenye tuzo za Ejat, Pili Mlindwa ambaye kwa sasa yupo Azam Media pamoja na Maajabu Ally Madiwa ambaye bado mpaka sasa anafanya kazi na Uzikwasa/Pangani Fm.
   
  Maajabu Ally kuwa miongoni mwa wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mkoa wa Tanga wote, ni kielelezo cha ubora wa kazi nzuri na usimamizi uliotukuka kupitia shirika la Uzikwasa/Pangani Fm.
   
  Kila la kheri Maajabu Ally Madiwa, nyota ya uwandishi wa habari inayong'aa kwa kasi nchini Tanzania kwa sasa, Pangani inakutegema, Tanga inakutegemea, leta tuzo nyumbani.

    Maajabu Ally Madiwa akiwa na Mhe January Makamba na mwandishi wa makala haya
  Maajabu Ally Madiwa akiwa studio akitangaza kipindi.

older | 1 | .... | 1207 | 1208 | (Page 1209) | 1210 | 1211 | .... | 1896 | newer