Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1208 | 1209 | (Page 1210) | 1211 | 1212 | .... | 1898 | newer

  0 0


  0 0

  Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha kilichoko mkoani Mbeya kimeingia siku ya tatu kwa kutembelea sehemu mbalimbali na kufanya mahojiano na Wananchi na pia kutembelea maeneo ambayo ni chanzo cha uharibifu wa maji ya mto Ruaha mkuu pamoja na mazingira. 

  Katika siku ya tatu kikosi kazi kimekutana na changamoto mbalimbali ikiwemo Wananchi kutokua na elimu ya matumizi ya maji ya mito ambapo wengi wao hutumia pampu kutoa maji kwenye mito ili kupeleka maji kwenye mashamba yao pasipo wao kujua kuwa ni kosa. 
   
  Mashamba mengi wilayani Mbalari yanatumia kilimo cha pampu kwa kuvuta maji toka kwenye mikondo ya mto Ruaha Mkuu na kupeleka mashambani. Wakulima wa vitunguu, mahindi, mpunga, nyanya, mbogamboga na matunda. 

  Hutumia umwagiliaji wa aina hiyo. Pia hufanya ufyatuzi wa matofali kwa kutumia maji yaliyoko mtoni kwa kuyavuta kwa kutumia pampu. Wakiongea Wananchi wengi wamesema kuwa walikua hawajui kama.kufanya hivyo ni kosa kwa sababu hawana elimu ya kutosha katika hilo. 

  Wengi wanalima pembezoni mwa mito bila kuzingatia sheria ya mazingira isemayo Mkulima anatakiwa alime nje ya mita sitini kutoka mtoni. Kikosi kazi bado kipo katika ziara yake Mkoani mbeya katika wilaya ya Mbalari. Kikosi kazi hiki kiliundwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania.   0 0

  ILE droo ndogo ya tatu ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili, iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu, sasa itafanyika katika Viwanja vya Bakhresa, vilivyopo Manzese jijini Dar es Salaam, Aprili 26, mwaka huu. Afisa Masoko wa Global Publishers, ambayo ndiyo waendeshaji wa bahati nasibu hiyo, Yohana Mkanda alisema jijini jana kuwa, droo hiyo itachezeshwa katika viwanja hivyo kuanzia saa nane mchana hadi 12 jioni.
  Wasomaji wa Magazeti ya Global Publishers, wakichangamkia Gazeti la Ijumaa na Championi kabla ya Droo ya Pili ya Shinda Nyumba kuanza.
  “Mipango yote kwa ajili ya shughuli hiyo imekamilika, tunawaomba wasomaji wetu kuendelea kuhifadhi kuponi zao na kujitokeza kwa wingi siku hiyo, kwani kama tulivyoahidi, zawadi kibao zitatolewa na washindi watatangazwa mubashara,” alisema Mkanda. Zawadi zitakazotolewa katika droo hiyo ya tatu ni pamoja na pikipiki, seti ya televisheni flat screen, simu ya kisasa za mkononi pamoja na dinner set ambapo washindi watapatikana hapohapo Manzese kwa Bakhresa. Droo hiyo ndogo ya tatu itafanyika baada ya mbili za awali, ambazo washindi walipata zawadi kama hizo kufanyika katika maeneo ya Mbagala ndani ya Ukumbi wa Dar Live na Mwananyamala katika Viwanja vya CCM Mwinjuma. Global Publishers, wachapishaji wa magazeti ya Ijumaa, Uwazi, Risasi, Championi, Amani na Ijumaa Wikienda ni kampuni pekee ya uchapaji magazeti kuwahi kutoa zawadi kubwa ya nyumba nchini katika bahati nasibu. Ili kupata kuponi hizo, msomaji anatakiwa kununua mojawapo ya magazeti ya kampuni hiyo na kujaza kuponi zilizopo ukurasa wa pili wa magazeti hayo na kuzipeleka kwa mawakala waliopo nchi nzima na kwa wale wa Dar, wanaweza kupeleka ofisi za Global zilizopo Bamaga, Mwenge.
  Kuponi zikichanganywa.
  Bahati nasibu hiyo ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na British School waliopo karibu na Kituo cha Daladala cha ITV na Kanisa la Lutheran Mwenge na Kilimanjaro Institute of Technology waliopo Mwenge kwa MamaNgoma na Sinza Mori.

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki akizindua Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu na kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki (katikati), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu wakionyesha Vitabu vyenye Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland mjini Dodoma leo.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi.
   Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Programu ya Mafunzo ya Uongozi kwa Maofisa wa Jeshi la Polisi Mjini Dodoma.Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Prof. Joseph Semboja.
   Baadhi ya Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala bora Mhe.Angelah Kairuki, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na  Maofisa wa Jeshi la Polisi waliopo katika Mafunzo ya Uongozi yanayoendeshwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Chuo cha Aalto cha nchini Finland.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Maofisa wa Polisi katika Uongozi ambapo baada ya kuhitimu watatunukiwa “Post-Graduate Diploma in Leadership”. Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

  0 0

  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni imezindua jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi kwa wanawake wa Wilaya ya Handeni  kwenye ukumbi wa maount Ilulu uliopo Kabuku mjini lenye ujumbe wa “Wezesha wanawake kiuchumi ili kujenga uchumi wa kati na Tanzania ya Viwanda”.

  Jukwaa hili linalengo la kuwakutanisha wanawake pamoja na kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki kikamilifu katika biashara na shughuli nyingine za kiuchumi katika Wilaya ya Handeni.

   Akizungumza kwenye uzinduzi wa Jukwaa hilo Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni  Bw. John Mahali aliyekuwa mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe alisema kuwa jukwaa la wanawake hilo  litasaidia  kuongeza uelewa kwa wanawake katika upatikanaji  wa mitaji , sheria za nchi katika masuala ya kiuchumi na jinsi ya kujitegemea.

  Aliongeza kuwa wanawake wamekuwa hawapati fursa za kutosha za kiuchumi hapa Nchini hata na duniani kote kutokana na kutokuwa na usawa katika fursa , uwezo wa kupata mitaji.

  “jukwaaa litasaidia kuondoa matabaka na sheri ambazo zitasaidia kupunguza ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake, ambalo ni jambo la muhimu sana katika kuleta maendeleo ya usawa katika pato la Taifa, jamii na familia” alisema Bw. John.

  Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe alisema kuwa  jukwaa hili litafanya kazi ya kutambua shughuli za kijasiliamari katika kutoa elimu kuhusu upatikanaji wa mitaji, kusajili biashara, kuwezesha kiuchumi na kutafuta masoko.

  Aidha, alisema katika suala la utoaji mikopo vikundi vitakavyopewa kipaumbele ni vile viliyojidhatiti kwa kusajiliwa, vyenye utawala unaoeleweka, miradi inayoonekana na zenye hesabu za kifedha zinazoweza kukaguliwa na kukosolewa inapobidi.

  Uzinduzi huo ulipambwa na maonesho ya bidhaa za kijasiliamari ya vikundi mbalimbali kutoka kata mbalimbali. Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga itaratibu shughuli zote za uchumi kwenye Wilaya zote ndani ya Mkoa na kuhakikisha kunakuwa na majukwaa ya Wilaya/Halmashauri zote ambayo yatafanya  vikao vyake kila baada ya miezi sita (6).
    
  Alda Sadango
  Afisa Habari
  Halmashauri ya Wilaya ya Handeni
   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw William Makufwe wakwanza kulia akifuatiwa na Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali wakitazama Moja ya bidhaa ya vikapu vinavyotengenezwa na kikundi cha wanawake tupendane cha segera
   Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali akizungumza na wanawake waiojitokeza kwenye Uzinduzi wa jukwaa Hilo.
   Mkurugenzi Mtendaji Bw William Makufwe akionesha katiba waliyopewa viongozi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya itakayowasaidia Katika Uongozi wao
   Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akipokea katiba kutoka Kwa mgeni rasmi Katibu tawala Wilaya Bw John Mahali.
   Mwenyekiti wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya Bi Fatuma Zuberi akishukuru wanawake waliompa dhamana ya kuwaongoza.
   Baadhi ya vikundi vya wanawake waliojitokeza kuonesha bidhaa zao wakati wa Uzinduzi.
   Baadhi ya wanawake wakishiriki wa Uzinduzi wa jukwaa la kuwezesha wanawake kiuchumi Wilaya  ya Handeni
  Viongozi wakipata maelezo kutoka vikundi vya kinamama.

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela (katikati), Balozi wa Norway wa kwanza kulia, Hanne-Marie Karstand na Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita (kushoto) wakifungua jengo la Afya ya Akili hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na kituo cha Tanga International Comperence Centre Tanga.


   MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martin Shighela, amesema vita ya madawaya kulevya inaendelea hivyo kuviagiza vikosi vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata vinara wa wasafirishaji na wauzaji.

  Akizungumza katika hafla ya fupi ya makabidhiano ya jengo la Afya ya Akili Hospitali ya Rufaa ya Bombo lililokarabatiwa na Kituo cha Tanga International Comperence Centre (TICC), Shighela alisema vita ya madawa itakuwa endelevu.

  Alisema vijana wengi wamekuwa wakiathirika na matumizi ya madawa ya kulevya na Taifa kukosa nguvu kazi ya kuleta maendeleo na kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha Tanga hakuna njia ya upitishaji.

  “Kuna wagonjwa wa akili kutokana na maumbile yao lakini kuna wagonjwa wengine wa akili wa kujitakia ambao sababu zake ni matumizi ya madawa ya kulevya” alisema Shighela na kuongeza

  “Ili kuwaokoa vijana wetu na kupunguza nguvu kazi naviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu ya mapambano ya madawa ya kulevya” alisema

  Kwa upande wake Balozi wa Norway hapa nchini, Hanne-Marie Karstand, amewataka watumishi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hilo kama ilivyo matumizi yake.

  Alisema Serikali ya Norway itaisaidia Tanzania katika Nyanja mbalimbali za kijamii ikiwemo Afya, elimu, Mazingira pamoja na wagonjwa wa Afya ya Akili.

  “Niuombe uongozi wa hospitali ya Bombo kulitunza jengo hili kwa kutumika matumizi yake kama ilivyokusudiwa, Norway itaisaidia Tanzania kila ambapo kunahitajika msaada” alisema

  Nae Mganga Mkuu wa Mkoa, Asha Mahita, alisema awali wamekuwa wakikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo kukosa uwezo wa kuwasafirisha wagonjwa kwenda vituo vinavyotoa huduma za Afya ya akili.


  Aliwataka wafadhili wengine kuiga mfano wa Norway kuisadia hospitali hiyo kutokana na changamoto ambazo imekuwa ikabiliana nazo.

  Habari kwa hisani ya blog ya kijamii ya tangakumekucha 0655 902929

  0 0

   Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiruka juu sambamba na kipa wa Tanzania Prisons, Andrew Ntala katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. Yanga imeshinda 3-0.
  Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la kwanza la timu hiyo lililofungwa na Amis Tambwe.
   Wachezaji wa Tanzania Prisons wakiomba dua kabla ya mchezo.
   Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Yanga na Prisons.
  Godfrey Taita akichuana na mchezaji wa Yanga.
  Kipa wa Tanzania Prisons, Andrew Ntala, akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
  Hekaheka katika lango la Prisons.
  Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa, akimtoka kipa wa Tanzania Prisons, Aron Kalambo, katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-0. (Picha na Francis Dande).

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wengine wakiangalia kwa vitendo majaribio ya kiyasansi kutoka kwa wanafunzi wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA kwenye sherehe za mahafali yao ambapo wanafunzi 45 wamehitimu. 

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewahimiza wanafunzi kote nchini kupenda kusoma masomo ya Sayansi hasa watoto wa kike ili Taifa liweze kujitosheleza kwa wataalamu wa fani mbalimbali nchini hasa wakati huu ambao Taifa linaelekea kwenye uchumi wa Viwanda.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwenye mahafali ya Pili ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya sekondari ya WAMA- NAKANYAMA Jijini Dar es Salaam, mahafali ambayo imehudhuriwa na wake wa Marais Wastaafu.

  Makamu wa Rais amesema haitapendeza hata kidogo ajira nyingi nchini kuchukuliwa na wataalamu mbalimbali mataifa ya nje hasa kipindi hiki wakati Serikali inahimiza ujenzi wa viwanda hivyo amesisitiza wanafunzi wajikite kwenye kusoma masomo ya sayansi ili taifa liweze kujitosheleza kwa ajili ya manufaa ya maendeleo ya taifa. Amesema katika kuhakikisha taifa lipata wanasayansi wengi, Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa maabara na kununua vifaa vya maabara ili kuhamasisha wanafunzi wengi zaidi kupenda kusoma masomo ya sayansi kote nchini.

  Makamu wa Rais pia amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya Tano inakusudia kuimarisha ufundishaji wa masomo ya Teknolojia ya habari na Mawasiliano –TEHAMA- katika shule za Sekondari na kujenga maabara za kompyuta nia ikiwa ni kuongeza wataalamu wa fani hiyo nchini. Kuhusu mila na desturi kandamizi kwa wanawake na wasichana zilizopo kwenye baadhi ya jamii nchini, Makamu wa Rais ameitaka jamii kukomesha mila hizo na iwashirikishe wanawake katika mipango na mikakati ya maendeleo ya nchi kwani watakuwa ni chachu ya maendeleo katika jamii husika.

  “Wote tunajua wanawake ni chachu na kiungo muhimu katika maendeleo ya jamii, Taifa na Dunia kwa ujumla hivyo ni wajibu wa jamii kushirikisha wanawake katika kupanga na kutekeleza shughuli za maendeleo kote nchini” amesisitiza Makamu wa Rais.

  Makamu wa Rais pia ameipongeza Taasisi ya Wanawake na Maendeleo – WAMA- kwa kujenga shule Mbili za Sekondari na kusomesha watoto wanaotoka kwenye familia maskini na yatima na kusema huo ni mfano wa kuingwa na wadau wengine wa maendeleo katika kusaidia kundi hilo ili watoto wanaotoka kwenye familia maskini nao waweze kuapata elimu itakayowasaidia katika maisha yao ya baadae. Kuhusu changamoto zinazoikabili shule ya WAMA – NAKAYAMA, Makamu wa Rais ameahidi kushughulikia changamoto hizo ikiwemo uhaba wa maji, ubovu wa barabara kuelekea kwenye shule hiyo na tatizo la uhaba wa mabweni 

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mama SALMA KIKWETE amesema aliamua kuanzisha taasisi hiyo ambayo inamiliki shule Mbili mpaka sasa ili kusaidia watoto wa maskini na yatima kupata elimu bure ambapo mpaka sasa kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaliohitimu katika shule hizo ambao wamejiunga na masomo ya elimu ya juu. Mama Salma Kikwete ameshukuru ushirikiano mkubwa anaopata kutoka Serikalini unaolenga kuhakikisha shule zinazoendeshwa na taaisisi hiyo ikiwemo ya Wama – Nakayama zinafanya vizuri.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete(kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa WAMA Bi.Zakhia Meghji wakiimba wimbo maalumu wa shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ambapo wanafunzi 45 wamehitimu. 
  Baadhi ya Wanafunzi waliohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari WAMA NAKAYAMA.

  Theresia Sanu (kulia)akisoma hotuba ya wahitimu kwa Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mahafali ya pili ya kidato cha sita ya shule ya sekondari ya WAMA NAKAYAMA.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mahafali ya pili ya kidato cha sita ya shule ya Sekondari ya WAMA NAKAYAMA ,ambapo aliwaasa wanafunzi hao 45 kusoma zaidi ili waje kulisaidia Taifa lao.
  Mwenyekiti wa WAMA Mama Salama Kikwete akihutubia katika mahafali ya kidato cha sita ya shule ya WAMA NAKAYAMA ambapo aliwataka wanafunzi hao kusoma na kufika juu zaidi.

  0 0

  Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Mazoezi, Daina Matemu, akimuongoza kuelekea kwenye ukumbi wa mahafali, mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya shule hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (kushoto), wakati wa mahafali hayo, yaliofanyika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), jijini leo. Nyuma kulia ni Mwenyekiti Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)  
  Kijana wa Skauti kutoka shule hiyo, akimvisha skafu Mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa mahafali hayo. Anayeangalia ni Mkuu wa shule hiyo, Daina Matemu. 
  Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (wa pili kulia), akiwa na wageni mbalimbali kwenye meza kuu wakipiga makofi mara baada ya kuasili ukumbini.
  Wahitimu wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Mazoezi, wakiimba wimbo wa shule hiyo, mbele ya mgeni rasmi Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, wakati wa mahafali yao leo jijini Dar es Salaam. 
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Mazoezi, Daina Matemu, akizungumza wakati akitambulisha wageni mbalimbali kwenye meza kuu katika mahafali hayo.
  Mgeni rasmi akiwa na wageni mbalimbali kwenye meza kuu wakimwombea mmoja wa wanafunzi aliyefariki wakati wakiwa kidato cha tano, wahitimu hayo. 
  Wahitimu wa kidato cha sita wakimwombea mwenzao aliyefariki wakiwa kidato cha tano.
  Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Mazoezi, Hussein Chiumbi, akisoma taarifa ya shule hiyo katika mahafali hayo. 
  Baadhi ya wahitimu wakicheza ngoma za Bongo Fleva, wakati walipokuwa wakionesha vipaji vyao.  
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma, Elly Mdundo, akitoa taarifa ya maendeleo ya taaluma kwa mgeni rasmi. 
  Baadhi ya walimu wa shule hiyo, wakiwa katika mahafali hayo. 
  Mhitimu wa kidato cha sita, Mansoor Mohamed akisoma risala ya wahitimu. Anayemsaidia ni mhitimu mwenzake, Hefsiba Nyangi.
  Wahitimu wa kidato cha sita, Mansoor Mohamed na Hefsiba Nyangi wakimkabidhi risala ya wahitimu mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha.
  Baadhi ya wazazi, ndugu na jamaa za wahitimu wa kidato cha sita, wakiwa katika mahafali hayo. 
  Baadhi ya wahitimu wakionesha mitindo ya mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 
  Baadhi ya wahitimu wakipita na mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 
  Baadhi ya wahitimu wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha na mavazi yaliyobuniwa na shule hiyo. 
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Chang'ombe Mazoezi, Daina Matemu, akizungumza wakati akimkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta (kushoto), ili amkaribishe mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), azungumze na wahitimu hao.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta, akizungumza katika mahafali hayo, wakati akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha (katikati), azungumze na wahitimu hao. 
  Mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Chang'mbe Mazoezi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Universities Abroad Link, Tony Kabetha, akizungumza na wahitimu wakati wa mahafali hayo, yaliofanyika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), jijini leo. Kushoto ni Mwenyekiti Kamati ya Taaluma (PTA), Ibrahim Samatta na kulia ni Mkuu wa shule hiyo, Daina Matemu.

  0 0  0 0  0 0  0 0


  Na Jumia Travel Tanzania

  Inaonekana mwaka 2017 umeanza vizuri katika sekta ya utalii nchini Tanzania kutokana na watu kadhaa mashuhuri kuzuru vivutio vyake. Sehemu ambazo zimeonekana kuwavutia watu wengi zaidi ni hifadhi ya mbuga ya Serengeti na bonde la Ngorongoro.

  Alianza mwigizaji maarufu wa filamu kutokea Hollywood nchini Marekani, Will Smith na mkewe Jada Pinkett-Smith. Mwanzoni mwa mwezi Machi walitua nchini kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kujivinjari katika mbuga ya Serengeti. Wakiwa huko familia ya Smith walikutana na msanii mwingine kutokea huko huko Marekani, lakini huyu yeye ni mwanamitindo na mrembo, Chanel Iman.

  Haikupita muda mrefu sana tangu watu hao mashuhuri kuwepo nchini, kwani siku chache zilizopita aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Taifa la Israel, Bw. Ehud Barak naye alitembelea mbuga ya Serengeti pamoja na Ngorongoro.

  Hii ni ishara nzuri kwa sekta ya utalii nchini ambapo kupitia watu hawa maarufu wengine nao wanapata taarifa na kuhamasika kutembelea pia.

  Lakini lazima tujiulize ni kwa nini Ngorongoro huwavutia watu zaidi na kuwafanya kufunga safari kuja Tanzania na sio sehemu zingine? Jumia Travel imekukusanyia vitu ambavyo vinapatikana katika eneo hilo la urithi wa dunia ambalo hakuna mtu atakayesimuliwa na kutotaka kulitembelea:

  Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro. Kama ulikuwa haufahamu bonde la Ngorongoro ni shimo kubwa lililotokana na mlipuko wa volkeno ambalo halijai maji wala kubomoka duniani. Eneo hili ambalo limetangazwa kuwa ni urithi wa dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO); lina urefu wa kilometa 20, kina cha mita 600 na ukubwa wa kilometa za mraba 300.

  Vifuatavyo ni vivutio vinavyopatikana katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro:

  Binadamu na Wanyama kuishi pamoja. Kwa zaidi ya miaka 200 iliyopita watu wa kabila la Wamasai walifika eneo hili na kuishi hapo. Maisha yao ya jadi yamewafanya waweze kuishi pamoja na mifugo yao kwa amani na utulivu kabisa bila ya kuwabugudhi wanyamapori. Mpaka hivi sasa kuna wafugaji wa Kimasai takribani 42,000 wakiishi katika hifadhi pamoja na mifugo yao kama vile ng’ombe, punda, mbuzi na kondoo. Kipindi cha mvua hutoka eneo hili na kuelekea maeneo ya tambarare ambapo kiangazi kikifika hujisogeza maeneo ya karibu ya mlima na misitu iliyopo. Wamasai huruhusiwa kuingiza mifugo yao kwa ajili ya kuilisha na kuinywesha lakini si kufanya shughuli za kilimo; lakini maeneo mengine ya hifadhi wanaruhusiwa kurandaranda.


  Bonde la Volkeno na Wanyamapori. Bonde la Ngorongoro lilitokana na mlipuko wa volkeno takribani miaka milioni 3 iliyopita ambapo ni kubwa, lisilobomoka wala kutojaa maji. Lilitangazwa na UNESCO kuwa ni urithi wa dunia mwaka 1979 na ni eneo pekee ambalo binadamu, mifugo na wanyama wanaishi kwa pamoja kwa amani na utulivu kabisa. Unaweza kukuta kuna wakati ng’ombe wa Wamasai wanachunga pamoja na pundamilia katika mbuga za Ngorongoro.      
  Masalia ya Kale ya Binadamu wa Mwanzo. Ngorongoro ndimo linapopatikana bonde la Olduvai ambalo kwa mujibu wa wanahistoria yanapatikana masalia ya binadamu wa mwanzo kuishi duniani. Hapa ndipo wanaikolojia maarufu Dkt. Louis na mkewe Mary Leakey walipata masalia ya kale likiwemo fuvu la mtu wa kale zaidi, Zinjanthropus, ambaye alipata kuishi miaka milioni 1.75 iliyopita. Utafiti wao uliweza kuvumbua mabadiliko ya taratibu ya ukubwa wa ubongo na zana zao za mawe walizokuwa wanazitumia.
  Vivutio vingine. Mbali na vivutio vilivotajwa hapo juu pia kuna vitu vingine chungu nzima vya kuvutia watu wanavyoweza kuvifurahia kuviona.

  Ziwa Ndutu na Masek; maziwahaya hujaa kutokana na maji yanayotiririka kutokea milimani, na maji yake hayafai kwa matumizi ya binadamu kutokana na chumvi nyingi iliyonayo.

  Oldonyo Lengai; hili ni jina la lugha ya Kimasai likiwa na maana ya ‘Mlima wa Mungu,’ unapatikana nje kidogo ya hifadhi ya Ngorongoro. Ni mlima pekee wenye volkeno hai ambapo ilishawahi kulipuka mwaka 2006 na siku za hivi karibuni mwezi Julai mwaka 2007.

  Mchanga Unaohama; safu ya mchanga mweusi umetakana na majivu ya mlima wa volkeno wa Oldonyo Lengai, umekuwa ukisukumwa taratibu kuelekea upande wa Magharibi wa hifadhi kwa kiwango cha mita 17 kwa mwaka. Una kimo cha mita 9 na mzingo wenye urefu wa mita 100, unapatikana Kaskazini mwa bonde la Olduvai.   

  Bonde la Olkarien; eneo hili nalo ni muhimu katika hifadhi kwani hutoa hifadhi kwa ndege tai aina ya Ruppell Griffon. Msimu mzuri wa kutembelea eneo hili ni miezi ya Machi mpaka Aprili ambapo tai huzaliana. Wanyama huja eneo hili pale panapokuwa na malisho ya kutosha.

  Kutazama ndege aina ya Flamingo na wengineo wa kila aina. Ndege aina ya Flamingo wanaonekana sana katika maziwa yanayopatikana ndani ya hifadhi. Mbali na ndege hao pia kuna aina mbalimbali za ndege ambao wanaweza kuonekana katika misimu tofauti ya majira ya mwaka hususani miezi ya mvua.

  Safari ya Kuizunguka Hifadhi. Utakuwa hujaifaidi Ngorongoro kama haujavizungukia vivutio mbalimbali vinavyopatikana ndani yake. Kwa kuwatumia waongozaji wa mbuga, hakikisha kwamba unatembelea sehemu kama vile bonde la Olmoti kuelekea nyanda za Embakai, shuka chini kuelekea Bonde la Ufa, pandisha Kaskazini kwenye nyanda za hifadhi ya misitu na kisha eneo la tambarare la Mashariki kuzunga miamba ya Nassera, milima ya Goli na bonde la Olkarien.   

  Kwa hakika hii ni Edeni ya sasa kama watu wengi wanavyopenda kuiita kutokana na maajabu iliyonayo pamoja na historia ya binadamu wa mwanzo kuishi mule. Sasa kama watu wanasafiri kutoka kila pembe ya dunia kuja kulitembelea eneo hili kwa nini na wewe mtanzania usitenge muda na kupanga kufanya hivyo? Haihitaji kuwa milionea kutembelea eneo hili, kunafikika kwa urahisi na hata malazi ni nafuu pia kwani Jumia Travel wamekurahisishia hilo.

  0 0  0 0

  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Jenista Mhagama ameeleza kukamilika kwa maandalizi ya kuadhimisha sherehe za miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zitakazofanyika Viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma, siku ya jumatano Aprili 26, 2017.

  Ameyasema hayo leo wakati akizungumza waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika Aprili 22, 2017 katika Ofisi yake Dodoma.

  “Nipende kuwaeleza Watanzania wote kuwa hadi sasa maandalizi ya kuifikia siku ya Maadhimisho ya Sherehe za Muungano tayari yamekamilika kwa kuangalia mambo yote yaliyopangwa katika ratiba ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Magufuli.”Alisema Waziri Mhagama.

  Amesema sherehe hizo zitakuwa na  upekee wa aina yake ukizingatia kuwa  ni mara ya kwanza tangu Serikali ilipotimiza adhma yake ya kuhamia Dodoma.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kuhusu Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kulia kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba na kushoto  ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba akizungumza na waandishi wa habari leo Mjini Dodoma kuhusu matukio mbalimbali yatakayokuwepo katika Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017.Kushoto kwake ni  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na mwishoni ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bw.Jordan Rugimbana.
  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Jordan Rugimbana akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Mkoani Dodoma 26 Aprili 2017 na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe,Jenista Mhagama na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Januari Makamba.


  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba amekutana na kufanya mazunguzo na Mabalozi Wateule wanaoenda kuiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani.Mazungumzo hayo yaliyofanyika ofisini kwake Makao Makuu ya Nchi mjini Dodoma, yalijikita katika kujadili namna bora ya kuiwakilisha Tanzania ughaibuni kwa kuzingatia sera ya nchi ya mambo ya nje, kwa lengo la kuboresha mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Tanzania na nchi hizo, na kwa kuzingatia maslahi mapana ya kiuchumi ya nchi yetu ikiwemo kutangaza shughuli za utalii zinazopatikana nchini. 
  Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisisitiza jambo 

  Balozi Mteule Baraka H. Luvanda akichangia jambo wakati wa mazungumzo. Punde baada ya mazungumzo na Mhe. Naibu Waziri, Mabalozi walikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 
  Katibu Mkuu Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt.Aziz P Mlima akiongea na Mabalozi ofisini kwake mjini Dodoma 
  Mazunguzo yakiendelea

  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amekutana na Mabalozi Wanane waTanzania Walioteuliwa hivi karibuni, Ambao Walifika Ofisini kwake Mjini Dodoma 21/April/2017 kumuaga kwa ajili ya kwenda Kuanza Kazi ya kuiwakilisha Tanzania katika nchi walizo pangiwa

  0 0


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi za Kitanzania Millioni Arobaini na Mbili kutoka kwa Kanishna wa ZRB Amour Hamil Bakari (katikati) wakati wa Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za Serikali, katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi-Zanzibar Mnazi mmoja Mjini Unguja,(kulia) Mwenyekiti wa Kamati ya Uchangiaji Madawati na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais,Sheria,Katiba,Utumishi wa Umma na Utawala Boro Mhe.Haroun Ali Suleiman,(kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali pia naibu Mwenyekiti wa kamati Mhe,Riziki Pembe Juma akifuatiwa na Naibu Kamishna wa ZRB Hadija Shamte,[Picha na Ikulu.] 22/04/2017

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa Uchangiaji wa Madawati kwa ajili ya Skuli za Msingi na Sekondari za Zanzibar kwa Viongozi mbali mbali katika ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mnazi mmoja Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 22/04/2017.

  0 0

  Na: Athumani Shariff

  Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesaini kandarasi zenye thamani ya dola za Marekani Milioni 268.35 ambazo ni zaidi ya Shilingi bilioni 600 za Tanzania mjini Tabora kwa mkopo wa benki ya Exim ya nchini India kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzani kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kutoa Ziwa Victoria na kupeleka katika Manispaa ya Tabora na Halmashauri za Igunga, Uyui, Shinyanga Vijijini na Nzega. 

  Utekelezaji wa mradi ni wa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza ya Mradi ilikuwa kufanya usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi, kazi ambayo ilifanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India na ilikamilika mwezi Desemba 2015. 

  Awamu ya pili ni ujenzi wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu ya kwanza itaanzia Kijiji cha Solwa (kilichopo Wilaya ya Shinyanga Vijijini) hadi Mji wa Nzega, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd ya India. Sehemu ya Pili inaanzia Mjini Nzega mjini hadi Manispaa ya Tabora kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, ujenzi utafanywa na Kampuni ya L&T ikishirikiana na kampuni ya Shriram zote kutoka India. 

  Sehemu ya tatu inaanzia Nzega mjini hadi Igunga mjini, ujenzi utafanywa na Kampuni ya Afcons ikishirikiana na kampuni ya SMC zote kutoka India. Usimamizi wa mradi unafanywa na Kampuni ya WAPCOS Ltd ya India. 

  Katika hotuba yake Profesa Mkumbo alisema wakandarsi hao wameanza kazi leo mara baada ya kusaini mikataba. “Wakandarasi wanaanza maandalizi yao leo na kazi za ujenzi zitaanza mwezi Mei 2017 na muda wa kukamilisha mradi utakuwa baada ya miezi 30”. Alisema Prof. Mkumbo.

  Kwa upande mwengine Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge, alisema uchumi wa Viwanda hauwezekani bila uhakika wa maji, hivyo Wizara yake itasimamia kwa kina juu ya uharaka wa mradi huo ili kuhakikisha sera na dira ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda inafanikiwa.

  “Nitahakikisha Wakandarsi hawa wanamaliza kazi kwa ubora na haraka kabla ya muda ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais katika azma yake ya Tanzania ya viwanda, kwasababu hakuna viwanda bila maji ya uhakika”, alisema Waziri Lwenge. 

  Na serikali ya awmu ya tano ni serikali ya uwazi ndiyo maana nimeagiza zoezi la kusaidi ujenzi wa miradi hii ifanyike hadharani ili ninyi wananchi wenye miradi yenu muone, sasa mushirikiane na wakandari hao na muwe walinzi wa vifaa ili kazi waifanye kwa haraka. Isitokee baadhi ya wananchi wasio waaminifu kuhujumu vifaa vya ujenzi mambo ambayo yatachelewesha mradi.” Alisisitiza Waziri Lwenge.

  Pia Lwenge aliwataka wakazi wa Tabora na maeneo mengine nchini watunze vyanzo vya maji ili miradi hii ya maji iwe endelevu. Alisisitiza kuwa sheria inakataza shughuli zote za kibinadamu kufanywa ndani ya mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji.

  “Tujiepushe kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita 60, ili tuwe na uhakika wa maji, tupande miti na kutunza mazingira yetu” alisema mhandisi Lwenge.

  Kwa upande wao wabunge wa Tabora ambao mradi utapita katika maeneo ya majimbo yao wameishukuru serikali kwa kutimiza ahadi yao ya muda mrefu ya kuwaondolea kero ya uhaba wa maji katika maeneo yao.

  Akieleza umuhimu wa mradi huo, Mbunge wa Sikonge Joseph Kakunda alisema mradi huu ni muhimu na mkombozi kwakuwa hamna vyanzo vya maji vya uhakika katika maeneo mengi ya Mkoa wa Tabora.

  Mbunge Hussein Bashe aliomba wakandarasi wa ndani nao wafikiriwe ili waweze kupata baadhi ya kazi ndogondogo (sub-contracts) ambazo zitasaidia kukuza uchumi wa ndani na kuwajengea uwezo wakandarasi wetu nchini.

  Akieleza mafanikio ya mradi Profesa Mkumbo alisema kuwa, mradi ukikamilika upatikanaji wa maji katika miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Uyui pamoja na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini, unatarajiwa kuongezeka kufikia asilimia 100 na wakazi zaidi ya milioni 1.1 watapata huduma ya maji safi na salama. 

  Pia alisema huduma bora ya maji itakayopatikana itachangia katika kuinua uchumi kupitia maendeleo ya sekta nyingine zinazotegemea maji kama Viwanda,Elimu, Utalii pamoja na kuimarisha huduma za afya wa wakazi wa maeneo hayo.


  Katibu Mkuu Wizara ya maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo na Visay Uplenchwar wa Kampuni ya Megha Engineering Infrastructures Ltd akisaini Mikataba ya ujenzi wa mradi wa maji kutoka kijiji cha Solwa Shinyanga na kupeleka maji Nzega.
   Picha ya pamoja Meza kuu pamoja na baadhi ya Wabunge wa Tabora. 
   Mbunge wa Nzega Hussein Bashe akimsalimia waziri wa Maji na Umwagiliaji Eng. Lwenge
   Waziri wa maji na Umwagiliaji Eng. Gerson Lwenge akipokewa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora wakati alipowasiri katika viwanja vya Furahisha Tabora. 
   Mbunge wa Sikonge Joseph Kakunda akimpa mkono Mkuu wa Mkoa wa Tabora

older | 1 | .... | 1208 | 1209 | (Page 1210) | 1211 | 1212 | .... | 1898 | newer