Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1206 | 1207 | (Page 1208) | 1209 | 1210 | .... | 1898 | newer

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Trade Union Congress of Tanzania -TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Trade Union Congress of Tanzania -TUCTA) mara baada ya kikao kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya mara baada ya kumaliza kikao  na kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi wa TUCTA mara baada ya Kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0


  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

  WANANCHI wanaoishi vjijini hawana elimu ya uraia ya kuweza kujadili masuala mbalimbali yanayozunguka pamoja,namna ya kufatatilia taarifa zao kwa watoa huduma wa serikali.

  Wakizungumza katika mkutano wa utoaji ripoti ya Mradi wa Elimu ya Uraia kwa Ujumbe wa Simu za Mikononi, wamesema kuwa mradi huo umesaidia wananchi kutatua changamoto zao kupitia kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu.

  Akizungumza katika mkutano wa utoaji ripoti hiyo Mkurugenzi wa C-SEMA,Joel Kiiya amesema maeneo yaliyokuwa na changamoto kwa wananchi ni migogoro ya ardhi, Ndoa za Utotoni , Mimba za Utotoni , Miradhi pamoja na juu ya upatikanaji wa yeti vya kuzaliwa.Amesema mradi huo katika wilaya saba uliokuwa ukitekelezwa wananchi wamekuwa na elimu juu ya kupata huduma katika halmashauri .

  Mrardi huo umetekezwa katika Wilaya za Karagwe, Chalinze, Bagamoyo , Shinyanga, Kyera, Kahama pamoja na Maswa.Mwakilishi wa Ofisi ya Rais , Katiba na Utawala Bora , Omary Hamis Juma , amesema kuwa Zanzibar walipokuwa wanatengeneza sera ya mtoto wamechukua sehemu ya C-SEMA kutokana vitu hivyo vitajenga katika sera hiyo.


  Mkurugenzi wa C-SEMA, Joel Kiiya akizungumza katika Mkutano wa utoaji ripoti ya Mradi wa Elimu ya Uraia kwa Ujumbe wa Simu za Mikononi uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Mwakilishi wa Ofisi ya Rais , Katiba na Utawala Bora , Omary Hamis Juma akizungumza juu ya mradi ulivyoleta matokeo masula mbalimbali yanahusu jamii uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Mwakili Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jaffari Malema akizungumza juu mradi katika matokeo watu kusajili vyeti vya kuzaliwa uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mawasiliano wa C-SEMA, Itanisia Mbise akizungumza juu ya ukusanyaji wa ujumbe uliokuwa unatumwa katika maeneo ya mradi uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.
  Picha ya pamoja washiriki wa mradi pamoja na maafisa wa serikali walioshiriki katika mradi huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa County Yard Hoteli jijini Dar es Salaam.

  0 0


  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


  IKIWA katika hali ya kuyumba kiuchumi na kushindwa kuwalipa wachezaji wao mishahara kwa wakati, neema imeanza kuwaangukia baada ya kampuni ya SportsPesa ya Kenya kutaka kuwamwagia fedha iwapo mkataba wao utafanikiwa.


  Yanga itakuwa ni ya tatu kwa timu za Afrika Mashariki kuingia mkataba wa fedha nyingi iwapo watakapofanikiwa kumalizana kumalizana na Kampuni ya SportsPesa ya Kenya.

  Iwapo mkataba huo utafanikiwa, Yanga na kampuni hiyo ya SportsPesa watasaini mkataba wenye thamani ya bilion 4.5 ambapo utakuwa ni wa miaka mitano ambapo kwa mwaka utakuwa na thamani ya Sh milioni 900.

  Uongozi wa Yanga leo unatarajiwa kutakutana na wawakilishi wa kampuni hiyo, ambapo wakikubaliana wataingia mkataba huo wa miaka mitano ambao kila mwaka utakuwa na nyongeza ya asilimia sita ya fedha.

  Awali, SportsPesa walileta mapendekezo katika klabu ya Yanga kuhusiana na mkataba huo lakini ulikatiliwa kutokana na mkataba huo kutokukidhi vigezo nan kuwa na maslahi na wakawapelekea mapendekezo yao na namna gani wanataka mkataba huo uweje.

  "\Leo wawakilishi wa SportPesa watakutana na uongozi wa Yanga ili kumalizana nao juu ya mkataba wanaotaka kuingia na hiyo ni kutokana na kufika makubaliano ya kimkataba," kiisema chanzo kutoka kamati ya utendaji ndani ya klabu hiyo.

  Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa, ambaye alisema wapo kwenye hatua za mwisho za kuingia mkataba na SportsPesa.

  "Napenda nizungumze kitu kilichokua tayari au kimekamilika hatua ya kuingia mkataba na SportsPesa bado, ila tutakutana nao kwa mazungumzo ya mwisho ambayo yatatoa jibu kama watatudhamini au la.

  "Tunazungumza na SportsPesa kwa kuwa hawa wamekuja moja kwa moja kwetu tofauti na kampuni nyingine ambazo zinataka kutudhamini, lakini ipo kampuni tuliyoipa jukumu la kufanya mazungumzo nao nasi kutuletea taarifa ya kila kinachoendelea." alisema Mkwasa.

  0 0

  Picha mbalimbali zikionesha matukio wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Victoria Foundation uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Geita ulioenda sabambamba na utoaji vyeti kwa washiriki wa mafunzo ya ujasiriamali.
  MAFUNZO ya ujasiriamali yametolewa kwa wanawake wajane na wasiojiweza wa mkoa wa Geita kupitia mfuko wa Victoria Foundation unaomilikiwa na mbunge wa viti maalum CCM, Vicky Kamata.

  Mafunzo hayo yalitolewa kwa lengo la kupunguza pengo la elimu ya masuala ya fedha kwa wanawake hao kwa kuwafundisha mbinu mbali mbali za biashara, namna ya kuweka akiba na kulipa mikipo.

  Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga alimpongeza Kamata kwa jitihada zake kwa kuinua wanawake hususani wajane na wasiojiweza kiuchumi na kuwataka wanawake kujenga utamaduni wa kufuatilia taarifa mbali mbali kuhusiana na masuala ya fursa za kibiashara ili kuzitumia katika kupanua wigo wa shughuli zao.

  Alisema wanawake wengi nchini wanashindwa kusonga mbele kibiashara kwa kuwa wanakosa taarifa ambazo zingetumiwa kuwawezesha kusonga mbele na kujikwamua kiuchumi.

  "Ni wakati sasa kwa wanawake nchini kutafuta taarifa zitakazoinua biashara, mafunzo kama haya mmeyapata bure myatumie vema kuhakikisha mnatimiza malengo yenu.”alisema.

  Kwa upande wa muandaaji wa mafunzo hayo, Vicky Kamata alisema mfuko wake mbali na kutoa misaada mbali mbali kwa walemavu, ni wakati sasa wa kusaidia elimu kwa wanawake na kuwawezesha mitaji ili waweze kufikia lengo.

  “Naamini mwanamke ni jeshi kubwa, ukimuwezesha mwanamke mmoja umewezesha jeshi kubwa lililopo nyuma yake hata watoto watasoma vizuri.”alisema Kamata

  Awali  kupitia mfuko huo wa Victoria Foundation, awamu wa kwanza ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wakazi wa Geita waliomsaidia kuchaguliwa kwake kuwa mbunge kupitia CCM , Kamata alitoa misaada ya  vyakula, mavazi, magodoro na viti vya walemavu (Wheel Chair) 30 kwa wakazi wa tarafa ya Bugando.

  Alisema kupitia mfuko wa Victoria Foundation  wakazi wa Geita watanufaika kwa misaada mbali mbali itakayowawezesha watu hususani wanawake wajane na yatima na wale wasiojiweza kuondokana na adha walizonazo na kufurahia maisha kama watu wengine.
  Source:DailyNews-Habarileo Blog

  0 0

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini - REA (hawapo pichani), wakati alipokuwa akiizindua rasmi Bodi hiyo Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Aprili 19, 2017.

  Na Veronica Simba – Dodoma
  Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, amezindua Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuiagiza kufanya kazi kwa kutanguliza maslahi ya Taifa na Watanzania kwa ujumla.
  Profesa Muhongo alizindua Bodi hiyo jana, Aprili 19, 2017 Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

  Akizungumza na Wakurugenzi wa Bodi hiyo mpya, wakati wa hafla ya uzinduzi, Profesa Muhongo aliwaagiza kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi waliochaguliwa kutekeleza miradi ya umeme vijijini ili wanunue vitendea kazi ikiwemo nguzo, transfoma na nyaya za umeme kutoka kwa wazalishaji wa ndani ya nchi.

  “Wakandarasi ni lazima wanunue vifaa hivyo ndani ya nchi. Vikiisha hapa nchini, ndiyo waagize nje. Hatutavumilia kuona mkandarasi ananunua vitendea kazi nje ya nchi wakati hapa nchini vipo tele.”

  Hata hivyo, Profesa Muhongo alisisitiza suala la ubora ambapo alifafanua kuwa, ni lazima vitendea kazi vinavyonunuliwa viwe katika ubora unaostahili. “Japokuwa tunataka vitu kutoka ndani ya nchi lakini ni lazima tuzingatie suala la ubora wake.”

  Akiendelea kutoa maagizo kwa Bodi hiyo, Waziri Muhongo pia alielekeza kwamba, Kampuni zote za kigeni ambazo zimeshinda Tenda ya kutekeleza miradi ya umeme vijijini awamu ya Tatu (REA III), ni lazima zifanye kazi na wakandarasi wadogo (sub-contractors) wa kitanzania.
  “Ni lazima wakandarasi wadogo wote watoke Kampuni za Kitanzania. Inaweza kuwa Kampuni iko hapa nchini lakini siyo ya watanzania; hiyo hatuitaki. Mradi huu unalenga kuwawezesha watanzania hivyo ni lazima wapate fursa,” alisisitiza Waziri.

  Profesa Muhongo alitumia fursa hiyo kuhamasisha watanzania wenye sifa kujitokeza kwa wingi ili wafanye kazi na kampuni kubwa za wakandarasi kutoka nje, na baadaye waweze kujitegemea na kujenga uwezo wa kufanya kazi hizo wao wenyewe.

  Aliiagiza Bodi hiyo kuhakikisha wanatatua changamoto ya baadhi ya vibarua kutokulipwa malipo yao baada ya kufanya kazi. Aliwataka kuweka usimamizi utakaowezesha kila mmoja kulipwa stahili zake kulingana na kazi aliyofanya.

  Vilevile, Profesa Muhongo aliitaka Bodi kusimamia ubora wa kazi inayofanywa na wakandarasi husika kwani kutokana na uzoefu inaonesha kwamba, baadhi yao, kazi zao hazina ubora unaoridhisha.

  Alisema, Bodi inawajibika kumfuatilia kila Mkandarasi kujiridhisha kuhusu uwezo wake, hata kama ameshapitishwa na taratibu za manunuzi. Alisema, endapo Bodi itakuwa na wasiwasi na uwezo wa Mkandarasi, ni lazima iweke hilo wazi kwani kazi isipofanyika ipasavyo, hawatakwepa lawama.

  “Iteni kampuni moja baada ya nyingine mjiridhishe na utendaji wao. Muone eneo alilopewa, ukubwa wa eneo hilo na bajeti aliyopewa. Pia mumuulize kuhusu vitendea kazi alivyonavyo pamoja na wataalam alionao,” alisisitiza.

  Aidha, Profesa Muhongo aliwataka wakurugenzi wa Bodi hiyo kujenga utaratibu wa kutembelea maeneo inakotekelezwa miradi mbalimbali ya umeme vijijini ili kujionea kwa macho maendeleo ya kazi inayofanyika.

  Suala jingine muhimu ambalo Waziri aliwaelekeza wakurugenzi wa Bodi kulifanyia kazi, ni kupitia taarifa ya utekelezaji wa REA II ili pamoja na mambo mengine, waweze kujiridhisha na majina ya wakandarasi waliopitishwa kutekeleza REA III. Aliwataka kumkataa Mkandarasi ambaye watabaini amepewa Tenda kutekeleza REA III wakati alishindwa kazi REA II.

  Pia, Waziri Muhongo aliitaka Bodi kuwafuatilia wakandarasi husika ili kuhakikisha wakati wanasambaza umeme vijijini katika awamu hii ya Tatu, wanatoa kipaumbele kwa maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na Taasisi za jamii kama vile shule, ofisi mbalimbali za uongozi, nyumba za kuabudu, sehemu za biashara na uzalishaji. “Watu wa mashambani wasiwe wanakuja wizarani kuomba umeme. Umeme upelekwe kwenye mashamba na hata kwenye Ranchi mbalimbali. Hatutaki kusikia mtu anarukwa,” alisisitiza.

  Sambamba na maelekezo hayo yote, Profesa Muhongo pia aliitaka Bodi husika, katika kikao chake cha kwanza, ijadili na kupendekeza namna ya kuongeza asilimia ya watanzania wenye fursa ya kupata umeme, kutoka ile iliyopo sasa ambayo ni asilimia 49.5.

  “Mje na mapendekezo mnataka tufike asilimia ngapi na kwa kutumia mbinu zipi.”

  Awali, akizungumza na wakurugenzi wa Bodi mpya iliyoteuliwa, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe, aliwataka kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuleta tija kwa Taifa.

  Profesa Mdoe aliwataja wakurugenzi wa Bodi mpya ya REA walioteuliwa kuwa ni Dkt. Gideon Kaunda ambaye ni Mwenyekiti pamoja na wajumbe Mhandisi Innocent Luoga, Happiness Mhina, Stella Mandago, Scholastica Jullu, Amina Chinja, Theobald Sabi na Michael Nyagoga.

  Alisema kuwa, Waziri Muhongo, amefanya uteuzi huo kutokana na Mamlaka aliyonayo, chini ya Kifungu Namba 5(1) (b) na Namba 8(3) cha Sheria ya Nishati Vijijini ya mwaka 2005, akiwa ndiye Waziri mwenye dhamana.

  Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, kwa niaba ya Wakala huo, aliahidi kutoa ushirikiano stahiki kwa Bodi iliyoteuliwa ili kwa pamoja waweze kuleta matokeo chanya katika kuwapatia umeme wananchi walioko vijijini.

  Uteuzi wa Bodi mpya ya REA ni wa miaka mitatu na umeanzia tarehe 1 Aprili, 2017.
  Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa James Mdoe (kulia), akiwasomea majukumu yao ya kazi, Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo, uliofanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Aprili 19, 2017.
  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Bodi mpya ya REA, uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
  Baadhi ya Wakurugenzi/Wajumbe wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakizungumza mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), mara baada ya kuizindua rasmi hivi karibuni mjini Dodoma. Kulia kwa Waziri ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara, Profesa James Mdoe na kushoto kwa Waziri ni Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Gideon Kaunda. Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akiwakabidhi vitendea kazi, baadhi ya wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA), wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika mjini Dodoma hivi karibuni.


  Baadhi ya Wakurugenzi wa Bodi mpya ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na maofisa mbalimbali kutoka wizarani na REA, wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo Taarifa ya Kamati Shirikishi (Teule) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kuhusu ramani ya pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumishi ya ardhi kwenye pori hilo. Taarifa hiyo ilikabidhiwa kwa Waziri Mkuu kwenye ukumbi wa Spika mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Arusha, mrisho Gambo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupoke taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Shirikishi (TEULE) ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha ya kushughulikia mgogoro wa matumizi ya ardhi kwenye pori tengefu la Loliondo kabla ya kupokea taarifa ya kamati hiyo kwenye ukumbi wa Spika, bungeni mjini Dodoma Aprili 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0


  Mtoto Arkam Salim Mbarouk (anayeonekana kwenye picha) mwenye umri wa miaka 12 amepotea tokea tarehe 19 April, 2017 mida ya jioni (alasiri) wakati anakwenda madrasa (maeneo ya Makongo Juu) na hajaonekana mpaka sasa.

   Mara ya mwisho alivaa kanzu ya msikitini rangi ya kijivu na pensi nyekundu. Tafadhali tunaomba utakapomuona popote au kupata taarifa zake uwasiliane nasi kwa namba hizi zifuatazo

   0782412840 AU 0659296329 AU 0713251344,

  0718237250 AU 0713484838 AU 0655188918 AU 0658023243 AU 0713483436 AU 0784675774.

   TAFADHALI TUNAOMBA SAMBAZA UJUMBE HUU KWENYE MAGROUP MENGINE KADRI IWEZEKANAVYO.

  0 0

    Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga (Wa pili Kulia) akipokea Tisheti kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Zurich Group, Sudi Simba, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bima mpya ya Afya, inayojulikana kwa jina la Afya Wote, iliyo chini ya Jubilee Insurance, Zurich Group waanzilishi wa Afya Wote Medical Insurance Scheme, iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe yanga Manispaa ya Temeke jijini Dar esSalaam, leo. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Uendeshaji wa Jubilee Insurance, Rogation Selengia (kushoto) ni Mkuu wa Idara ya Afya Jubilee Insurance, Kenneth Agunda. Picha zote na Muhidin Sufiani (MAFOTO)
   Wakionyesha Vipeperushi na fomu zinazoelezea huduma za Bima hiyo, baada ya uzinduzi huo.

   Na Ripota wa mafoto Blog, Dar
  WITO umetolewa kwa  wananchi wa kipato cha chini na kati kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya mpya unaojulikana ‘Afya Wote’, uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Sera na Mipango Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wzee na Watoto, Edward Mbanga, alisema kuwa uzinduzi wa mfuko huo wenye gharama nafuu ni  kimbilio la wanyonge kutokana na kuwajali wananchi wa aina zote.


  Aidha alisema kuwa wananchi wataona umuhimu wa mfuko huo pindi wanapopatwa na tatizo la ugonjwa na kwa wakati huo wakawa hawana pesa za kukidhi matibabu.


  Bima hiyo imelenga zaidi kuwafikia wananchi wote haswa wale waso na kipato kikubwa na wa kipato cha kati ili wote wanufaike na huduma za afya.

  Mbanga alitoa wito kwa wananchi wengi kutumia fursa hiyo ili kuweza kuwekeza fedha ambazo wanazitumia kwa matibabu kwaajili ya mahitaji mengine ya kiuchumi.


  “Pamoja na kwamba kuna sera mbalimbali za afya zinazozungumza juu ya upatikanaji wa huduma za afya kwa njia rahisi, lakini bado bila bima ya afya wagonjwa wengi watapoteza  maisha kwa sababu kuna watanzania  wengi ambao hali za kipato chao sio nzuri.


  Ni vyema wananchi wengi wakajiunga na mfuko huu wa bei nafuu ili kile kiasi kilichokuwa kikitumika kufanya matibabu wakiwekeze kwenye shughuli nyingine za uchumi,”alisema.


  Aidha alisema asilimia 27 tu, ndio wamejiunga na mfuko hivyo kuna wananchi wengi ambao hawajajiunga na mfuko huo.


  Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Zurich Group na Zurich Insurance Brokers (EA) Sudi Simba alisema, huduma hiyo ilianzishwa mwezi Aprili mwaka jana, lengo likiwa ni kuwasaidia watu wenye kipato cha chini na kati, ambapo kwa kila familia ya watu wanne wataweza kukatiwa bima kwa sh.174,000 tu.

  “Watu hawa ni baba, mama na wategemezi wao ambao ni watoto chini ya miaka 18 .

  Bima hii kama kuna uhitaji wa kuongeza wengine unapaswa kulipia sh. 100,000 kwa mwaka kwa kila atakaeongezeka,”alisema.  
   Khadija Kopa na kundi zima la bendi ya TOT wakitoa burudani na kuimba wimbo maalum uliotungwa nao kuhusu Bima hiyo mpya. 
  Mgeni rasmi akihojiwa na waandishi baada ya uzinduzi huo.

  0 0


  0 0


  Mch.Dr.Jerry Williamson kutoka nchi Marekani akiomba katika ibada ya katika kongamano kanisa la Zion lililopo njiro jijini Arusha ambapo kanisa hilo limeendaa semina na kongamano kwa wachungaji pamoja na washirika wengine,kulia kwake ni Ben Mangeni ambaye ni mkalimani wake

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo akiongea na waandishi wa habari , alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki kongamano hilo wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine


  Mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

  kushoto ni Mtume trice Shumbusho akiwa na mkalimani wake akihubiri katika kongamano hilo.
  Waumini wakiwa katika maombi
  Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
  Baadhi ya wageni wakiwa katika kanisa la Zion kwaajili ya kongamano
  Picha ikionyesha madhabahuni
  Picha ikionyesha jengo la kanisa


  Na Pamela Mollel,Arusha

  Wachungaji zaidi ya 300 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini bila kujali madhehebu yao wako katika semina maalumu ya neno la Mungu yenye lengo la kusaidia kupeleka ujumbe wa madhihilisho ya nguvu ya kristo katika maeneo mbalimbali ya nchi ili watu waweze kubadilika na kumjua Mungu

  Semina hiyo ya siku nane iliyoandaliwa na kanisa la Zion City Church Arusha litafanyika kanisani hapo ikiambatana na Kongamano ambalo limeandaliwa kwa ajili ya wachungaji na watu mbalimbali likiwa na lengo la kuwajengea uwezo wa kupeleka injili kwa watu wa mataifa.

  Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kongamano hilo Mch.George Mngodo alisema kuwa watu ambao wataweza kushiriki wataweza kujifunza mambo ambayo awali hawakuweza kuyafahamu ambayo yatawawezesha kuvuka kutoka hatua moja kwenda nyingine.

  Mngodo aliongeza kuwa huduma zitakazo tolewa katika katika kongamano hilo hazitawakugusa kiroho tu bali hata kwenye maisha yao ya kawaida wataweza kubadilika

  “Tunaamini kongamnao hili litagusa wachungaji hawa na jamii wanayoihudumia kimwili na kiroho”alisema Mngodo

  Kwa upande wake mmoja wa wachungaji wa kanisa hilo Paul Sulley alisema kuwa matarajio yao ni kuona kila mtumishi anayehudhuria anavuviwa upya ili aweze kumtumikia Mungu kwa bidii.

  Mch.Sule alisema kuwa ulimwengu wa sasa umeharibika hivyo unahitaji watumishi waliokutana na Mungu na si wanaomjua Mungu pekee ili waweze kuwatumikia watu.

  Miongoni mwa watumishi wa Mungu wa kimataifa watakao kuwa wasemaji wakuu katika kongamano hilo ni Askofu mkuu wa kanisa la Zion City Church Arusha John Shumbusho pamoja na mkewe Trice Shumbusho

  Wachungaji wengine ni kutoka nje ya nchi Mch.Dr.Jerry Williamson, Mch.Dr Jim Oxendine kutoka Marekani,Mch.Yoshua Masasu kutoka Rwanda,Mch.Aloysius Kiiza kutoka Uganda,Pamoja na Mch.George Mkandawire kutoka Afrika Kusini .

  0 0

  Maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam ili kuwapatia maharusi uwanja wa kuchagua mahitaji yao yote kwa ukamilifu siku ya harusi yao.

  Akizungumza na Waandishi wa habari, Meneja Biashara Hamis Omary amesema maonesho hayo ni ya kipekee kwa Afrika mashariki na hufanyika mara moja kwa kila mwaka.

  "Tunawatangazia jamii kwa ujumla watarajie maonesho yakuvutia kuburudisha pamoja na nyakati rahisi kwa bwana Harusi na bibi harusi kuandaa vitu vyao vya harusi, vilevile kutakuwa na mitindo mipya mingi kutoka kwa wauzaji bora katika sekta ya harusi kila maonesho yanavyoendelea kukua kutoka hatua moja na kwenda hatua nyingine ndivyo ubora unavyoendelea kuongezeka" amesema
  Meneja Masoko wa Kampuni ya 361 Degrees, Hamis Omar(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari akizungumza kuhusu maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanatarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13 mwaka huu kwenye hoteli ya Golden Tulip Oyststerbay Jiji Dar es salaam.
  Kaimu Meneja wa Hoteli ya Golden Tulip, Adele Johnson(kushoto)  akizungumzia na waandishi wa habari leo kuhusu jinsi walivyodhamini maonesho ya tisa ya Harusi Trade Fair yanayotarajiwa kufanyika Mei 12 hadi 13.
  Mratibu wa matukio wa Kampuni ya 361 Degrees, Naomi Godwin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio waliyoyapata kwenye maonesho yaliyopita.
  Mmoja wa waandishi wa habari akiuliza swali kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Maelezo jijini Dar leo.

  0 0

  Na Daudi Manongi-MAELEZO.

  Serikali kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imelipa madeni ya fedha za likizo kwa walimu 86,234 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016 na 2016/17.

  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

  “Serikali inaendelea kulipa madeni mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha za likizo kwa walimu/Watumishi katika sekta ya Elimu”,Aliongeza Mhe.Manyanya.

  Amesema kuwa katika kipidi cha mwaka wa fedha 2015/16 hadi mwezi Juni, 2016 jumla ya shilingi bilioni 22,629,352,309 zililipwa kwa walimu 63814, na pia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17 hadi kufikia mwezi Machi, 2017 jumla ya shilingi bilioni 10,505,160,275 zimelipwa kwa walimu 22420.

  Aidha katika malipo haya jumla ya shilingi 13,415,410 zimelipwa kwa ajili ya madeni ya fedha za likizo kwa watumishi wa chuo cha ualimu Korogwe.Akizungumzia upande wa upandishaji madaraja Mhe.Manyanya amesema kuwakwa sasa uhakiki wa watumishi unaendela na ukikamilika watapandisha madaraja kama inavyotakiwa.

  Aidha amesisitiza kuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imekuwa ikiwapandisha vyeo watumishi wake wenye sifa kila mwaka ambapo katika mwaka 2015/16 Wizara iliwapandisha vyeo watumishi 2272 kati yao watumishi 71 ni wa chuo cha ualimu korogwe.

  Uhakiki wa madeni ya miaka ya nyuma unaendelea kuratibiwa na mamlaka husika na taratibu za malipo zitakamilishwa kwa wale wanaostahili.
  Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Stella Manyanya

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mahojiano maalumu  na Mkurugenzi  Idara ya Habari (MAELEZO)  Dkt. Hassan Abbasi  kuhusu  masuala ya Muungano kwa ujumla kuelekea maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano.
  has2
  Mkurugenzi  Idara ya Habari (MAELEZO)  Dkt. Hassan Abbasi  akimkabidhi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  Jarida la Nchi yetu linalotolewa na Idara ya Habari ( MAELEZO). Jarida hilo liliandaliwa kwa ajili ya maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika.
  has3
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) katika picha ya pamoja na watumishi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya mahojiano maalumu kuelekea Maadhimisho ya Miaka 53 ya Muungano( kutoka kushoto ni Beatrice Lyimo, Dkt. Hassan Abbasi, Jonas Kamaleki na Hassan Silayo.

  0 0

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mhandisi Kapuulya Musomba akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uunganishwaji na usambazaji wa gesi asilia leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mkurugenzi wa Uhusinano na Mipango wa TPDC, Nathan Mnyawami.
  Baadhi ya waaandishi wa habari wakifuatilia mkutano baina yao na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba (hayupo pichani) uliofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.  Na: Frank Shija – MAELEZO.

  TPDC kwa kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.

  Hayo yamebainishwa na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.

  Mhandisi Musomba amesema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa ajili ya kazi hiyo.

  “Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema Mhandisi Muyomba.

  Aliongeza kuwa lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha, mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda za usambazaji.

  Aidha alisema kuwa ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu utakapomalizika.

  Mtandao huo unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na vituo vya kujazia gesi hiyo.

  Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo amesema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza Vigae cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na majadiliano na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na mtandao huo.

  Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni.

  0 0


  Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu.
  Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.
  Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.

  ……………..

  Na Nuru Juma-Maelezo

  Taasisi ya Tanzania Health Summit yaandaa mbio za nusu Marathon na Upimaji wa afya kwa lengo la kusaidia juhudi za serikali katika kupunguza magonjwa yasioambukiza, mbio hizo zinazotarajia kufanyika Aprili 26 katika barabara ya Kaole iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

  Hayo yamesemwa leo na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rebecca John wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki.

  “Kamati ya maandalizi ya ya mbio za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa sekta ya afya hapa nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji wa afya ili kuungana na serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa yasiyoambukiza” alisema Rebecca.

  Aliongeza kuwa kwa mwaka huu mbio hizi zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka rika mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye ulemavu na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza.

  Pia washiriki watapata nafasi ya kupima afya magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu ,wingi wa sukari katika damu, kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe katika matiti na kupata ushauri wa wataalam kuhusiana na vyakula bora, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

  Aidha Bi. Rebecca aliongeza kuwa washiriki watakimbia umbali tofauti, kwani kuna mbio ndefu za kilometa 21.1 kwa ajili ya wakimbiaji wazoefu, kilometa 10 kwa wakimbiaji wa kati, kilometa 5 kwa wakimbiaji wa kawaida, kifamilia na kampuni na mbio za watoto chini ya miaka 12 ni meta 700 na zawadi itatolewa kwa mshindi wa kilometa 21.1 pekee kwa kiasi cha shilingi laki tano.

  Kwa upande wake Rais wa Tanzania Health Summit Dr.Omary Chillo alisema kuwa washiriki watatakiwa kutoa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kununua flana pamoja na kifaaa maalum cha kuhesabia muda wakati wa kukimbia ila maji ya kutosha yatatolewa bure kwa ajili ya wakimbiaji.

  Aliongeza kuwa wameimarisha ulinzi kwa kushirikiana na jeshi la polisi na ili kulinda usalama kwa washiriki na wananchi watakaokuwepo katika mashindano hayo.

  “wananchi wasiwe na wasiwasi wa usalama kwani tutashirikiana na jeshi la polisi ili kuimarisha usalama na tumeweza kupata baraka nyingi kutoka kwao kwa kuweza kushirikiana nao” aliongeza Chillo.

  Pia Katibu msaidizi wa Chama cha Riadha nchini Bi Ombeni Zavala alisema anashukuru wananchi wanavyoweza kujitokeza katika mashindano hayo na pia anawaomba wananchi hasa vijana waendelee kujitokeza kwa wingi kwani wanaweza kupata nafasi ya kuunda timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17.

  Naye Sajenti Isaya Mlokozi kutoka kanda ya usalama barabarani alisema jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani litahusika vizuri katika sehem inayowahusu kuhakikisha watu wanafanya zoezi hilo kwa hali ya usalama na litajumuika na wananchi popote pale watakapokuwa wanakwenda.

  Mashindano haya mwaka jana yalifanyika katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam lakini kutokana na kuongezeka kwa watu mwaka huu yatafanyikia barabara ya kaole yenye kauli mbiu ‘piga hatua moja mbele ya magonjwa sugu’

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Dkt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda na Mjumbe maalumu wa Rais Paul Kagame alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017. Wengine ni Balozi wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura na Afisa Mwandamizi wa Ubalozi Bw. Issa Mugabutsinze.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu kutoka kwa Rais Paul Kagame wa Rwanda uliowasilishwa kwake na kt. Musafiri Papias, Waziri wa Elimu wa Rwanda  alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 20, 2017

  PICHA NA IKULU  0 0

  Shirika la Anga la Etihad (EAG) limeandaa kozi maalumu kwa wahandishi na warubani inayofahamika kama ‘Think SciencE 2017’ ili kuhamasisha taaluma ya anga ikiwa ni sehemu ya juhudi za taifa la Abu Dhab kuwahamasisha vijana kwenye masomo ya sayansi na teknolojia.

  Tukio la uzinduzi lilifanyika katika ukumbi wa Dubai World Trade Centre na limeandaliwa na Taasisi ya Emirates Foundation ikiwa ni miongoni mwa maonyesho makubwa katika ukanda huo.

  Mgeni rasmi katika maonyesho hayo, ambaye piani Mkurugenzi mtendaji wa Emirates Foundation, alizundua maonyesho hayo kisha kutembelea ofisi za Shirika la Anga la Etihad.

  Wageni watakaotembelea ofisi za shirika hilo watafahamu mambo mbalimbali ya uendeshaji yanavyofanyika na watajifunza jisni ya ndege zinavyorushwa. Marubani na watumishi wa ndege watajibu maswali mbalimbali kutoka kwa watu wanaopenda kufahamu kuhusu masuala ya anga.

  Wawakilishi wa Kitengo cha Etihad Airways Engineering watakuwepo, wataonyesha injini ya kisasa ya ndege ya jet, vilevile watatoa ufafanuzi masuala yanayohusiana na ndege ya 120-plus.

  Pia, kutakuwa na picha za video zinazoonyesha shughuli mbalimbali za Shirika la Anga la Etihad jinsi linavyojihusisha na maendeleo katika ugunduzi wa mafuta ya ya ndege ambayo ndiyo wa kwanza katika kuyatumia kupitia mradi wake wa Sustainable Bioenergy Reseach Consortium.

  Kapteni Salah Al Frajalla wa Shirika la Ndege la Etihad, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Masuala ya Usalama na Shirika la Taifa la Kuendeleza Marubani alisema, “Hii ni chachu ya maendeleo kwa Nchi ya Falme za Kiarbu kutokana na kuwahamasisha vijana kujiingiza kwenye taaluma ya urubani ambapo watakuwa na ujuzi huu.

   Tunatumaini kwamba kuwanzishwa Think Science 2017 itawavutia na kuwatia moyo vijana wengi kuanza kujadili masuala yanayohusiana na sayansi na teknolojia. Pia kuhimiza vijana wengine wa Nchi za Falme za Kiarabu kupenda taaluma hii hata kutamani kujiunga na Shirika la Anga la Etihad.

  Pia, katika kuwafanya wageni wavutiwe na kuelewa zaidi kuhusu masuala mbalimbali ya Shirika la Anga la Etihad, wageni watapata fursa ya kushindana ili kujishindia safari moja maalumu ambapo wataweza kutembelea na kufahamu shughuli za Shirika la Anga la Etihad linaloongoza kwenye sekta ya anga nchini Abu Dhab.

  Zawadi zitatolewa kwa kwa vijana watakaooonyesha ubunifu kwenye masula ya uhandishi wakati wa mashindano hayo.

  Maonyesho ya Think Science yalizinduliwa mwaka 2012 yakiwalenga kundi la miaka 15-35 na kuwapeleka maelfu ya wageni kila mwaka . Lengo la serikali ni kuhamasisha ushirikianao baina ya wanasayansi na wadau wa sekta ya saynsi na teknolojia.

  0 0

  Na Jimmy Mengele - Dodoma. 

   Mfuko wa Pensheni wa PPF unaendelea kuwakumbusha wananchi kujiunga na PPF ili kuweza kufaidika na fursa mbalimbali kama vile mikopo ya maendeleo, elimu, huduma ya afya, mafao ya uzeeni na mafao ya uzazi.

   Akiongea katika Maonesho ya uwezeshaji wananchi kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa, mkoani Dodoma, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel alisema hii ni fursa pekee kwa waajiriwa wapya wakiwemo walimu, madaktari na kada zingine kuchagua Mfuko wa Pesheni wa PPF ili kuweza kukidhi mahitaji yao ya kimaendeleo. 

   Afisa huyo alisema waajiriwa hao wapya wakijiunga na PPF watafaidika na mikopo katika maeneo yao ya kazi, mafao ya uzazi, mafao elimu, mafao ya ugonjwa, mafao ya kifo, wategemezi, kiinua mgongo na mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wakati kwa kutumia kikotoo kilichoboreshwa.
  Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Anthony Peter Mavunde akisaini kitabu cha wageni katika banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi baada ya kupata maelezo ya mpango wa ‘ Wote scheme’ ambao umekua msaada katika kuwaongezea mitaji vijana kutokana na mikopo ya mpango huo, waliosimama Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
  Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga wakitoa maelezo juu ya huduma za PPF kwa Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage wakati alipotembelea Maonesho ya Mifuko ya uwekezaji kiuchumi katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
  Afisa Mwendeshaji wa PPF, Kanda ya Mashariki na Kati Joyce Rwechungura akitoa maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na PPF kwa waliotembelea banda la PPF katika Maonesho ya Mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi inayoendelea katika viwanja vya Mashujaa mkoni Dodoma.
  Mbunge wa jimbo la Kishetu Mhe. Elias Kwandikwa akiuliza swali juu mpango wa ‘Wote scheme’ ulivyofanikiwa kwa watu wote ikiwemo walio kwenye Sekta isiyo rasmi nao kupata nafasi ya kupata mafao mbalimbali. Wanaomfuatilia kwa makini ni Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel na Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga.
  Katibu wa Chama cha Wafugaji Tanzania Magembe Makoye akimsikiliza kwa makini Afisa Mfawidhi wa PPF Astro Liganga kuhusu Mfumo wa ‘Wote scheme’ ambao kima cha chini cha kuchangia ni shilingi elfu ishirini na ndani yake kuna fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.
  Michael Silasi (mwenye miwani ) na Said Ally (aliyevaa kofia ) wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PPF Janet Ezekiel kuhusu kazi za PPF na mafao yanayotolewa na Mfuko huo ikiwemo mfumo wa 'Wote scheme' ambao  utoa fursa za mikopo ya maendeleo, mikopo ya elimu, huduma za afya na mafao ya uzeeni. Mfumo huu unawawezesha wote walio katika sekta isiyo rasmi kujiwekea akiba.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Soko la Buguruni,Furahisha Kambi akizungumza na Globu ya jamii kuhusu kuanza kwa ukarabati wa miudombinu ya soko hilo la Buguruni na kuipongeza  Manispaa ya Ilala,kwa kuchukua hatua hiyo kwa ajili ya kuwajali wafanyabishara wake ambao pia ni sehemu ya walipa kodi wakubwa katika wilaya hiyo
   Katibu Mkuu wa Soko la Buguruni,Furahisha Kambi akionesha baadhi ya nguzo zilizo wekwa kwa ajili ya ukarabati wa soko hilo,jana jijini Dar es Saalaam.
   Mafundi wakiendelea nakazi katika soko la Buguruni jijini Dar es Saalaam.
  Muonekano wa soko jinsi litakavyo kuwa badaa ya ukarabati huo.picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii

  0 0


older | 1 | .... | 1206 | 1207 | (Page 1208) | 1209 | 1210 | .... | 1898 | newer