Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

AHADI ZA SERIKALI YA MKOA WA DAR ES SALAAM ZAZIDI KUKAMILIKA..

$
0
0
Katika kutimizwa kile kinachoitwa Deni la serikali ya Mkoa kwa wakazi wake wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Mh Paul Makonda leo hii ametembelea ujenzi wa Hospitali ya Kinamama ya Chanika unaofadhiliwa na ubalozi wa Korea Kusini na kugharimu zaidi ya Tshs. 8.8 Bilioni za kitanzania uliokamilika  kwa 90% hadi hivi sasa.

Ujenzi huo ambao ulizinduliwa kwa kuwekewa jiwe la msingi  na Mh Paul Makonda mwishoni mwa mwaka jana baada ya ombi la ujenzi wa Hospitali ya kisasa kwa wamama wakazi wa Dar es salaam kupokelewa na kukubaliwa na ubalozi wa Korea kusini hapa nchini.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu unasindikizwa pia na ujenzi wa nyumba 28 za makazi kwa ajili ya wauguzi na madaktari watakaohudumu hospitali hiyo masaa 24.

Ukamilishwaji wa ujenzi huu ambao hadi sasa umebakiza hatua ya mwisho ya ufungaji wa vitanda 160 vya wagonjwa na 10 vya kujifungulia wakina mama wajawazito  (ambayo ni 10% ya mradi wote), ni uthibitisho tosha wa kuonesha nia ya dhati ya Serikali ya Dr John Pombe Magufuli ya kuhakikisha huduma bora za kiafya zinawafikia wananchi wote wa Tanzania kwa wakati.

Hospitali hii ya kihistoria na aina yake itakuwa ni mahusisi kwa wakina mama wa Mkoa wa Dar es salaam na wamama wote wa maeneo jirani na inatarajiwa kufunguliwa mwezi Juni mwaka huu (2017) na Mh rais wa JMT Dkt John Pombe Magufuli.

Pongezi nyingi zimfikie Mh Paul Makonda kwa jitihada za kutatua changamoto mbalimbali za wananchi wa Dar es salaam kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo hapa nchini.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala,Mh Sophia Mjema.
Majengo ya hospitali hiyo kama yaonekanavyo pichani, iliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea Kusini,ampapo inatarajiwa kuzinduliwa Juni 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipata maelekezo ya vifaa kutoka kwa Daktari wa Manispaa ya Ilala, Willy Sangu leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akitazama baadhi ya vifaa vya kisasa vilivyofungwa katika hospitali hiyo,alipotembelea mapema leo kuangalia vifaa mbalimbali katika Hospitali ya Koica Chanika, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Vifaa vya kisasa ambavyo tayari vimeishafungwa katika hospitali hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimsikiliza Mganga wa Manispaa ya Ilala,Willy Sangu (hayupo pichani) alipokuwa akitoa maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyofungwa katika hospitali hiyo mapema leo jijini Dar.

BODI YA ZABUNI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YAIPA WIKI TANO KAMPUNI YA UJENZI YA KOBERG KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAMISHNA WA UHAMIAJI, JIJINI D’SALAAM

$
0
0
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (watatu kushoto), Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani (kushoto), wakati wajumbe wa Bodi hiyo walipotembelea nyumba za makazi za Makamishna wa Uhamiaji, Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Bodi hiyo ilitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo.
Katibu wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo, wakati wajumbe hao walipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi ya makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (kushoto) akiangalia kabati la nguo katika moja ya chumba cha nyumba za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wajumbe wa Bodi hiyo walizikagua nyumba hizo na kutoa wiki tano kwa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg kukamilisha ujenzi.
Mkuu wa Kitengo cha Majengo wa Idara ya Uhamiaji, Hamza Shabani akiwaonyesha Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, nyumba za makazi za makamishna wa Uhamiaji zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga. Wapili kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi, watatu kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Uhamiaji, Peter Chogero, na kulia ni Mhasibu Mkuu wa Wizara hiyo, Edwin Makene.
Mhandisi wa Kampuni ya Ujenzi ya Koberg ambayo inajenga nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, Leonard Leonidace, akiwafafanulia jambo Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, walipozitembelea nyumba hizo wakikagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo, hata hivyo Wajumbe wa Bodi walitoa wiki kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara hiyo ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga, na wanne kulia ni Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Zabuni, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Kamishna wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga (Katikati) na Katibu wa Bodi hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manunuzi wa Wizara hiyo, David Mwangosi (wanne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi hiyo, mara baada ya wajumbe hao kumaliza ziara yao ya kukagua ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji, zilizopo Mtoni Kijichi, jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Wajumbe wa Bodi hiyo walitoa wiki tano kwa Kampuni hiyo kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imeipa muda wa wiki tano Kampuni ya Ujenzi ya Koberg Construction Co.Ltd kukamilisha ujenzi wa nyumba za makazi za Makamishna wa Idara ya Uhamiaji hapa nchini zilizoko katika eneo la Mtoni Kijichi jijini Dar es Salaam ambazo zitatumiwa na Makamishna hao.

Uamuzi wa Bodi hiyo umekuja baada ya Kampuni ya Koberg Construction ya nchini hapa kuonyesha kusuasua na kushindwa kukamilisha ujenzi wa nyumba hizo kwa wakati.

Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga na Katibu wake Bw. David Mwangosi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imefanya maamuzi hayo baada ya kufanya ukaguzi na kujionea hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa nyumba hizo.

Kwa upande wake Katibu wa Bodi hiyo amesema kitendo cha Mkandarasi huyo kusuasua kukamilisha kwa wakati kazi ya ujenzi wa nyumba hizo ulioanza tangu mwaka wa Fedha wa 2014/2015 ndicho kilichoifanya Bodi ya Zabuni ya Wizara hiyo kuamua kutembelea eneo ambalo kazi ya ujenzi wa nyumba hizo unaendelea na kumpatia wiki tano tu kuhakikisha anakamilisha kazi hiyo.

Makao Makuu ofisi ya Taifa ya Takwimu kukamilika baada ya miezi kumi

$
0
0
Benjamin Sawe-Maelezo,Dodoma.

MKURUGENZI Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dk. Albina Chuwa ametaka ujenzi wa makao makuu ya ofisi hiyo unaoendelea mjini Dodom ukamilishwe kwa wakati.

Akizungumza mjini hapa jana baada ya kukagua ujenzi wa ofisi hiyo, Dk. Chuwa alisema ni wakati sasa kwa NBS kuwa na ofisi yenye hadhi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha shughuli za takwimu nchini.Dk. Chuwa alisema NBS ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini na ambayo imekuwa ikibadilika na kwenda na wakati hivyo kupatikana kwa jengo hilo ni jambo linalopaswa kutimia haraka.

“Jengo letu ni la ghorofa tano tu, kwa kuwa mkandarasi umepewa muda wa miezi 10 sioni sababu ya kuchelewa kukamilishwa.“Hivi karibuni nilizungumza na wenzetu wa Uganda wao walijenga jengo lao la ghorofa 12 kwa mwaka mmoja tu sasa sioni sababu kwa nini letu lisikamilike kwa wakati,”alisema.

Kwa mujibu wa Dk. Chuwa jengo hilo litakuwa ni la ghorofa tano na kwamba kwa kuwa wanazo ofisi katika kila mkoa nchini, makao makuu hayo yatatumika kuratibu uendeshaji wa shughuli za takwimu na mambo mengine ya maendeleo yanayohusiana na NBS.

Dk. Chuwa alisema jengo hilo litagharimu sh. Bilioni 11.6 hadi kukamilika kwake fedha ambazo zinatokana na mkopo kutoka Benki ya Dunia.

Kwa upande wake, Msimamizi Mkuu wa ujenzi huo, Mtumwa Shomvi kutoka kampuni ya Y&P Achtects Limited, alisema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kuusimamia mradi huo.Shomvi  alisema jukumu kubwa wanalolisimamia ni kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati, gharama na ubora uliokubaliwa.

Aidha, Msimamizi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya Hainani International Limited ya China, Lan Shuiqing alisema kazi ya ujenzi inaendelea vyema na kwamba anaamini kila kitu kitakamilika kwa wakati.

Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa akitoa maelekezo wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo jipya la Makao Makuu ya Ofisi hiyo unaondelea Mkoani Dodoma leo (jana), wa kwanza kulia ni Injinia Lan Shuiqing kutoka Kampuni ya Hainan Internationa.
Msimamizi Mkuu kutoka Kampuni ya Y and P Bw. Mtumwa Somvi wa kwanza kulia akitoa maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Albina Chuwa wakati menejimenti ya Taasisi hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi mkoani Dodoma leo (jana).
Baadhi ya mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu lenye urefu wa ghorofa tano linaloendelea kujengwa Mkoani Dodoma.
Muonekano wa ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu unavyoendelea mkoani Dodoma.(Picha na Benjamin Sawe -Maelezo) .
 

MATUKIO YA AJALI BARABARANI NA KAMERA YA GLOBU YA JAMII

$
0
0
Ajali mbalimbali zilizonaswa na kamera ya Globu ya jamii katika barabara ya Iringa.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA SABA CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA LEO APRIL 13, 2017.

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiwasili katika ukumbi wa Bunge kuongoza kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akiongoza kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
AA
 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Philip Mpango akiwasilisha Ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu Taarifa za Fedha za Serikali kuu , Fedha za Miradi ya  Maendeleo, Fedha za Mashirika ya Umma na majibu ya hoja na mpango wa  kutekeleza mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa Fedha 2015/2016.
A 1
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Suleimani Jafo akiwasilisha Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI,UTUMISHI NA UTAWALA BORA) kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 2
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 3
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Usimamizi wa Mikataba iliyoingiwa kati ya Serikali na Hospitali za Binafsi Nchini katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 4
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Isack Kamwelwe akiwasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Ufanisi katika Usimamizi wa uchukuaji wa Maji kutoka Vyanzo vya Maji katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 5
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Ufundi Mhe. Stella Manyanya akiwasilisha Ripoti  ya Ukaguzi wa Ufanisi juu ya Uzalishaji wa Wahitimu katika Sekta ya Mafuta na Gesi Asilia katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 6
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 7
 Naibu Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Edwin Ngonyani akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 8
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medrid Kalemani  akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
A 9
 Mbunge wa Bunda Mjini (CHADEMA) Ester Bulaya akiuliza swali  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z
 Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo  akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 1
 Mbunge wa Mafia (CCM) Mhe. Mbaraka Kitwana Dau akiuliza swali  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 2
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angelah Kairuki  katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 3
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhe. Isack Kamwelwe akijadiliana jambo na Mbunge wa Mtama Mhe. Nape Moses Nnauye katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 4
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Jenista Mhagama akijadiliana jambo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
Z 5
Ujumbe kutoka Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakiongozwa na Mkaguzi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof Mussa Assad wakifuatilia kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017.
S
Wabunge wakifuatilia hoja mbalimbali katika kikao cha saba cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017. 
S 1
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai akitoka  katika ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairisha  Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017 kwa mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.
S 2
 Baadhi ya wabunge wakitoka katika Ukumbi wa Bunge mara baada ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuhairisha  Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Aprili 13, 2017 kwa mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.
Picha Zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

Taifa Moja kunogesha Pasaka kwa matamasha

$
0
0
Kampeini ya Taifa Moja inatarajiwa kuendelea mwishoni mwa wiki hii kwa matamasha ambayo yatafanyika kwenye mikoa mitano hapa nchini ikiwa na lengo ya kuendelea kutoa burundani pamoja elimu kwa Watanzania juu ya kutuma na kupokea fedha kutoka kwenye mtandao wowote kwa gharama ile ile.

Taifa Moja ni kampeini ambayo imedhaminiwa na taasisi za Financial Sector Deepening Trust of Tanzania (FSDT) pamoja na Bill & Melinda Gates Foundation huku ikiratibiwa na International Finance Corporation (IFC) chini ya muungano ya makampuni matatu ya simu za mkononi za Airtel Tanzania, Tigo Tanzania na Zantel kupitia huduma zao za Airtel Money, Tigo Pesa na Ezy Pesa.

Akizungumza jijini leo Jijini Dar es Salaam, Liginiku Milinga ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Fern Tanzania ambao ndio waratibu na waandaaji wa matamasha hayo alisema maandalizi yote yamekamilika na kuwaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi kupata burundani toka kwa wasanii wakali hapa nchini na pia kupata elimu juu ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote hapa Tanzania kwa gharama ile ile.

Milinga alitajwa mikoa ambayo matamasha hayo yatafanyika ni pamoja na Mbeya (Mwenge Primary School), Dar es Salaam (Zakhiem Grounds), Arusha (Kilombero Grounds), Mwanza (Furahisha Grounds na Tabora (Uyui Grounds) huku msanii Chege akitumbuiza Mwanza, Stamina na Jambo Squad wakitumbuiza Arusha, Belle 9 Mbeya, Cassim Mganga Tabora huku Mkubwa na wanae wakifanya yao Jijini Dar es Salaam. Matamasha hayo yatafanyika Jumapili ya tarehe 16 April mwaka huu.

Kuhusu kutoa elimu kwa wananchi juu ya huduma ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao kwa gharama ile ile Meneja Chapa kutoka kampuni ya Tigo Tanzania William Mpinga, Moses Alphonce ambaye ni Meneja wa Airtel Money, Patric Dumulinyi ambaye ni Mobile Money Manager walitoa wito kwa wananchi kwenye mikoa hiyo kujitokeza kwa wingi kwani matamasha haya ni ya wazi na hakuna kiingilio.

‘Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza na kupata elimu ya kutosha ya jinsi ya kutuma na kupokea pesa kwenda mtandao wowote kwa gharama ile ile, alisema,’ alisema Mpinga.

Mpinga alisema huduma hiyo itawanufaisha wananchi kupunguza gharama za kutuma fedha kwenda mitandao mingine na upotevu wa fedha uliokuwa ukijitokeza hapo awali.

Alisema kampeni ya Taifa Moja itaongeza uelewa wa watumiaji wa simu za mikononi nchini juu ya namna ya kutuma na kupokea pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwa gharama ile ile.

“Watumiaji wa huduma za simu-pesa watatumiana pesa kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine na kuingia moja kwa moja kwenye akaunti za simu –pesa ya mteja aliyetumiwa, hakutakuwa na sababu ya kuhofia pesa hiyo uliyotumiwa kwenda kuitoa haraka ukihofia kumrudia aliyekutumia kama ilivyokuwa hapo awali," aliongeza Moses Alphonce kutoka Airtel Money.

Kwa upande wake, Rukia Mtingwa ambaye ni Meneja Chapa na Mawasiliano alisema njia hii ya sasa ni tofauti na utaratibu wa zamani ambao mteja akimtumia mwenzake ambaye yupo mtandao mwingine hutumiwa ujumbe wa meneno (sms) kwa aliyetumiwa kwenda kuchukua pesa hiyo kwa wakala.

“Kuanzia sasa tutaendelea kutoa elimu kwa watumiaji wa mitandao yetu juu ya utumaji pesa kutoka kwenye mtandao mmoja kwenda mwingine anavyoweza kukatwa kiasi cha fedha kile kile kama ambacho angelikatwa kutoka mtandao kama wake.”Aliongeza Mtingwa.

WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA UNUNUZI HISA ZA AWALI ZA VODACOM

$
0
0

Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma

Serikali imewataka watanzania kuchangamkia fursa ya ununuzi wa asilimia 25 ya hisa za awali za kampuni ya simu za mikononi ya Vodacom zinazouzwa kwa watanzania pekee ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya fedha ya mwaka 2016 kwa lengo la kuwawezesha watanzania kuwa wamiliki makampuni ya simu za mikononi hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bi Beng’i Issa amesema hi ni fursa kubwa na muhimu kwa watanzania kuwa sehemu ya wamiliki wa makampuni ya simu za mikononi kupitia ununuzi wa hisa hizi za awali.

‘’Ni uwekezaji ambao ni salama sana na hauna hasara, kwa kuwa ukiwa hutaki kuendelea kuwa mwanahisa unauza hisa zako na kurudisha pesa zako na unaweza kupata faida’’.

Ununuzi wa hisa hizi utawawezesha Watanzania kuwa wamiliki wa kampuni, watapata gawio la faida, wanaweza kutumia hisa kama dhamana za mikopo benki na wanaweza kuziuza hisa wanapokuwa na shida ya fedha.

Hisa hizi zinauzwa kwa mtanzania mmoja mmoja, watumishi walioajiriwa, wastaafu, makampuni yanayomilikiwa na watanzania, mashirika ya kitanzania, VICOBA, SACCOS, vikundi vya kijamii, wanawake na vijana. Aidha hisa moja inauzwa kwa shilling 850 na kiwango cha chini cha ununuzi ni hisa 100 na hakuna kikomo cha juu cha ununuzi wa hisa.

Baraza linatoa rai kwa Mashirika ya Hifadhi ya Jamii Nchini, Taasisi za fedha, Vikundi vya fedha vya kijamii kuwezesha wanachama na wateja wao kununua hisa hizi za awali.

Ununuzi wa Hisa hizi unapatikana kupitia matawi ya benki ya NBC, NMB, CRDB nchi nzima, mawakala wa soko la Hisa la Dar es Salaam, M-PESA na matawi mbali mbali ya benki za biashara nchini.

Baraza linawahamasisha watanzania wote kuchangamkia fursa hii muhimu ili kushiriki kikamilifu katika kumiliki uchumi wao na kufikia ndoto ya kuwa Taifa la uchumi wa kati kama ilivyoainishwa katika Dira ya Taifa ya Mwaka 2025.

Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi linashirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari kama radio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii kuhamasisha watanzania kunua hisa hizi za awali.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’i Issa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Bw. Edward Kessy, akitoa ufafanuzi wa namna ya kununua hisa hizo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifatilia kwa makini maelezo ya Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Bi. Beng’I Issa (hayupo pichani) alipokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu umuhimu wa kununua hisa kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mkoani Dodoma.(Piha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango).

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRILI 14, 2017


Balozi Masilingi awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Mexico

$
0
0
Mheshimiwa Balozi Wilson Mutagaywa Kajumula Masilingi, akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mheshimiwa Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico.

Tarehe 11 Aprili, 2017, Mhe. Balozi Wilson Mutaganywa Kajumula Masilingi aliwasilisha hati za utambulisho kwa Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico, Ikulu Katika Jiji la Mexico. 
 
Hafla hiyo ilishuhudiwa na Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Mexico na mke wa Mhe. Balozi, Marystella Masilingi. Wakati wa kuwasilisha hati hizo, Mhe. Balozi alipata fursa ya kuongea na Mhe. Rais wa Mexico na kumpa salam kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico akimpokea Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Mexico. Katikati akitizama ni Mhe. Luis Videgaray Caso, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico. 
Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico na Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi, Balozi mpya wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, nchini Mexico.
Kutoka kushoto, Mhe. Balozi Wilson M. Masilingi na Mhe. Enrique Peña Nieto, Rais wa Mexico; Mke wa Balozi Bi. Marystella E. Masilingi na Mhe. Luis Videgaray, Waziri wa Mambo ya Nje wa Mexico.
Mhe. Balozi Wilson M. K. Masilingi na Mke wake Bi. Marystella Masilingi (kulia) na Bi. Swahiba Mndeme, Mkuu wa Utawala wa Ubalozi (kushoto).

Maandalizi ya Dasani Marathon 2017 yakamilika

$
0
0
                          Dar Running Club ikishirikiana na Kampuni ya maji ya kunywa Dasani, leo imeanza kufanya usajili kwa washiriki  wa mbio za km 10 na 21km zijulikanazo kama Dasani Marathoni zitakazofanyika Jumapili  ya Mei 14, 2017 jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya tatu sasa kwa Dar Running Club kuendelea kuihamasisha jamii kufanya mazoezi kwa kuandaa mashindano haya, ambayo yatafanyika tarehe  Jumapili  ya Aprili  2017. Awali mashindano haya yalikuwa yakijulikana kama May Day Marathon lakini kutokana na kushirikiana na kampuni ya maji ya Dasani kuyaandaa mwaka huu yatajulikana kama Dasani Marathon 2017.
Akizungumzia mashindano haya, Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Coca-Cola Kwanza LTD, kampuni ya inayotengeneza maji ya Dasani, Nalaka Hettiarachchi amesema kuwa maji ya kunywa ya Dasani ni murua na yenye kuondoa kiu, hususani wakati wa kufanya mazoezi au unapojisikia kuburudika na ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki kwa wingi ili kujenga afya zao kwa mazoezi. 
 Pia akiamini kuwa tunaweza kuleta uzoefu mkubwa kwa wahsiriki na kulifanya kuwa tamasha la kukumbukwa. Pia tutalifanya tukio hili kuwa maarufu zaidi na lakusisimua kwa miaka ijayo likiwa na vivutio vingi kwa washiriki kutoka katika matembezi mbali mbali”. Lengo letu kubwa ni kusaidia vijana na kuhamasisha Watanzania wenye vipaji kufikia viwango vya Kimataifa and kuleta heshima kwa nchi yako… aliongeza Nalaka
Kwa upande wake, rais  wa Dar Running Club,  Goodluck Elvis, alisema kauli mbiu ya klabu yao ni "Active. Wherever. Whenever" na  imefarijika kuungana na Dasani katika kuandaa mashindano haya Dasani Marathon 2017 ambayo umaarufu wake umekuwa ukiongezeka kwa kasi mwaka hadi mwaka.
Kama ilivyokuwa kwenye mashindano ya miaka miwili iliyopita, mbio hizo zitaanzia na kumalizikia  Police Officers Mess Oysterbay. Mbio za 21km zitaanza saa kumi na mbili kamili alfajiri, zikifuatiwa na zile za 10km ambazo zitaanza saa kumi na mbili na nusu asubuhi. Washindi watano wa mbio za 21km na washindi watatu wa mbio za 10km watazawadiwa zawadi nono ikiwemo fedha taslimu.
Kiwango cha kusajili ni TZS 30,000/= kwa mbio zote na mwisho wa usajili ni tarehe 13 Mei, 2017.
Vituo vya awali vya usajili vitakuwa  Colosseum Gym - Masaki, Shoppers plaza – Mikocheni, China Plaza: Ghorofa ya 11 mtaa wa Uhuru na Mheza Kariakoo na Mlimani City Mall. Washiriki wote watafanikiwa kupata fulana zenye kiwango cha juu na vilevile watazawadiwa medali pindi watakapokamilisha mbio hizo kwa wakimbiaji elfu moja wa kwanza.

Kwa Taarifa Zaidi wasiliana na:
Goodluck Elvis, Dar Running Club President, 0715 302 336
Erick Kahwa, Dar Running Club Secretary, 0784024422
Dorothy Kipeja, Dasani Marathon Marketing Manager 0754 291 291

TAARIFA KWA UMMA

Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya askari 8 waliouawa Kibiti Pwani

CHUO CHA SHENYANG CHA CHINA CHATOA UFADHILI KWA AIR TANZANIA NA NIT

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Chuo kikuu cha shenyang kutoka nchini China kimeahidi kutoa ushirikiano na Shirika la ndege la Air  Tanzania kwa kutoa msaada wa kuwasomesha wafanyakazi wa kampuni hiyo,ili waweze kumudu ushindani wa soko la kimataifa.

Hayo yamesemwa na mwalimu wa malezi wa chuo cha Shenyang, Shi Guangda katika mkutano ulioandaliwa na Taasisi ya Global Education Link kwa wazazi ambao watoto wao wanasoma urubani na Masuala ya anga katika chuo hicho.

“Tangu Rais wetu wa China alipofika hapa tumekuwa na mahusiano makubwa na nchi hizi mbili, hivyo kwa kuanza kama chuo chetu tutatoa ufadhili kwa wafanyakazi wa shirika la ndege la Air Tanzania na kubadilishana mafunzo katika chuo cha usafirishaji cha NIT na Shenyang” Amesema Guangda .

Kwa upande wa Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Air Tanzania,Ladislaus Matindi ameishukuru tasisi ya Global Education Link kwa  kuwaunganisha na chuo hicho ambacho kwa sasa kimekuwa msaada mkubwa kwa kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa shirika hilo.

Matindi ametaja kuwa upatikanaji wa nafasi hiyo itasaidia kutoa motisha kwa vijana wetu ambao wanafanya kazi katika shirika hilo na wengine ambao wako nje kuwa na hamu ya kusoma masuala ya usafirishaji .

Kwa upande wake mkurugenzi wa Global Education link , AbduMalik Molell alitumia fursa hiyo kuzungumza na wazazi hao juu ya swala la bima ya wanafunzi amabo wanasoma chuo hicho katika swala zima la matibabu na majanga mengine ambayo yatawakuta wanafunzi.


Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akimkabidhi hati ya ufadhili wa masomo Mkurugenzi wa shirika la ndege nchini Air Tanzania,Ladislaus Matindi kwa ajili ya wafanyakazi wa shirika hilo watakotakiwa kwenda kusoma China
Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la Air Tanzania Ladislaus Matindi akizungumza na wazazi ambao watoto wao wanasoma masuala ya Anga nchini China
Mkurugenzi wa Global Education Link, AbdulMalik Mollel akifafanua jambo kuhusu masuala ya bima ya matibabu kwa wazazi ambao wamefika katika mkutano huo
Mlezi wa wanafunzi kutoka chuo Shenyang, akizungumza juu ya mazingira na ufadhili walio utoa nchini kwa shirika la ndege
Afisa Biashara mkuu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara upande wa Tantrade, Stephene Kobelo akizungumza na wazazi juu ya namna watoto wanavyotakiwa kuitangaza nchi 
Baadhi ya Wazazi ambao wamefika katika mkutano huo wakisikiliza kwa makini juu ya swala zima la bima ya matibabu kwa wanafunzi
Baadhi ya wakurugenzi  wenza wa Tasisi ya Global Education Link wakisikiliza 
Mmoja wa wazazi akichangia jambo juu ya kuboresha bima ya wanafunzi wanaosoma China
Wazazi na baadhi ya ndugu ambao watoto wao wanasoma nchini China wakifatilia mkutano.

HAKUNA VIKWAZO TENA TAMASHA LA "NYANZA FESTIVAL" JIJINI MWANZA.

$
0
0
Baadhi ya wadau wanaosaidia kufanikiwa kwa Tamasha la Nyanza Festival 2017 ni SBL-Pepsi, Delta Media Studios, Kali Boy Music, Lake Fm, Passion Fm, Metro Fm, City F, Barmedas Tv, Binagi Blog-BMG, Tanzania Bloggers Network-TBN na Tamara Entertainment.

BMGHabari
Hatimaye uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, umethibitisha kwamba tamasha la burudani la Nyanza Festival 2017 litafanyika katika uwanja huo kama ilivyokusudiwa.

Meneja wa uwanja huo, Steven Shija, ameyathibitisha hayo baada ya kutokea figisu figisu kwamba siku ya tamasha hilo kutakuwa na mchezo wa soka wa Ligi Kuu nchini na hivyo kusababisha tamasha hilo kutofanyika.

"Ndugu Wasanii na Waandaaji wa Nyanza Festival napenda kuwajulisha kuwa ratiba ya Tamasha ipo pale pale hakuna kitakachoiathiri, tunasimamia utaratibu na misingi ya haki kwa tunaowahudumia. Nawatakia maandalizi mema ya Tamasha lenu". Amebainisha Shija.

Tamasha la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Jijini Mwanza la Nyanza Festival 2017, litafanyika wikendi hii April 15 na 16 kwa kiingilio cha 5,000 tu ambapo wasanii zaidi ya 30 watapanda jukwaani.

Kumbuka Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.

WANAFUNZI WA DARASA LA TATU WA SHULE YA MSINGI YA AGA KHAN WATEMBELEA AIRTEL

$
0
0
 Mkurugenzi wa Raslimali Watu wa Airtel Tanzania, Patrick Foya akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan, waliofanya ziaraMya mafunzo katika makao makuu  ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar
es Salaam.

 Afisa Huduma kwa Wateja wa Airtel Tanzania, Stephen Makongoro akifafanua jambo Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini
Dar es Salaam.
  Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari wa Airtel Tanzania, Franky Filman akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam.

 Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan  wakiangalia bidhaa mbalimbali katika duka la kisasa la Airtel lilipo makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam
Maafisa wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Aga Khan waliofanya ziara ya mafunzo katika makao makuu ya Airtel eneo la Morocco, jijini Dar es Salaam


MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WA CCM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Ndugu Amina Makillagi (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole baada ya kukutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Aprili 14, 2017. PICHA NA IKULU 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole akiongea leo

THBUB yalaani mauaji ya Askari Polisi 8 Mkoani Pwani

$
0
0
Bahame Tom Nyanduga -

Mwenyekiti
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuwawa kwa askari wanane (8) wa Jeshi la Polisi, katika tukio lililotekelezwa na watu wasiofahamika jioni ya Aprili 13, 2017 katika kijiji cha Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani. 

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya ya kikatili ya askari polisi waliokuwa kazini na wasiokuwa na hatia. Aidha, tunaungana na Watanzania wengine kuwapa pole familia za wafiwa na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji ya askari polisi na wananchi wengine maeneo tofauti Mkoani Pwani tangu mwaka 2015 yamekuwa yakiongezeka na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu, hususan haki ya uhai inayolindwa na Katiba ya nchi, na madhara mengine kwa familia za wahanga, kwa jamii na taifa kwa ujumla. 

Haki ya kuishi kama zilivyo haki nyingine, inalindwa kisheria, na pia inalindwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia. Hakuna mtu anayepaswa kuporwa haki hii ya msingi kiholela. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 14, kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Ikumbukwe kwamba askari polisi wanapokuwa kazini wanatekeleza majukumu muhimu ya kulinda raia na mali zao, kwa hiyo usalama wao unategemewa na Watanzania wote. Yeyote yule anayewaua askari polisi siyo tu anataka kuwachonganisha askari polisi na raia, bali pia anawaweka raia hao katika hofu kubwa ya usalama wao na mali zao.

Hivyo basi, kwa mara nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inashauri kwamba:

1. Katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi ya askari polisi na wananchi wote inalindwa, Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za mauaji haya kutokea kwa kujirudia Mkoani Pwani, na kuhakikisha wahusika wote wanapatikana na wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili sheria ichukue mkondo wake.

2. Tume inawakumbusha wananchi kuwa vitendo vya ukatili, mauaji, na matendo yote yanayokiuka Sheria yanayofanywa na raia wasio wema ni ukiukwaji wa Sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala wa sheira; Hivyo Tume inakemea matendo haya na kutaka yapigwe vita.

3. Aidha, inawataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha upelelezi wa matukio hayo unakamilika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika na matukio haya.


Imetolewa na:

Bahame Tom Nyanduga

Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Aprili 14, 2017

EXIM BANK ENHANCES EFFICIENCY ITS CONTACT CENTRE

$
0
0
 Chief Financial Officer of Exim Bank Tanzania, Mr. Selemani Ponda cuts ribbon to officiate the launch of the banks new Contact Centre located at NIC Building in Posta, Dar es Salaam. Standing beside him is Exim Bank Senior Manager Customer Service, Mr. Frank Matoro [R] and Exim Bank Officer, Miss Martha Mpalale [L]
 To enhance its customer service experience, Exim Bank Tanzania has strengthened the efficiency of its Contact Centre by introducing new services and increasing its working hours.

Speaking at the official opening of the new Contact Centre located at NIC Building in Dar es Salaam, Exim Bank Chief Financial Officer Mr. Selemani Ponda said “We are pleased to inform our customers and the general public that our Contact Centre is now stronger and more efficient and it boasts a complete selection of both inbound and outbound services”.
 The Contact Centre hours are now from 7:00 am to 8:00 pm on weekdays and 9:00 am to 4:00 pm on weekends. This is a significant extension from the former hours of 8:00am to 6:00 pm on weekdays. This means that Exim Bank current and potential customers can reach out to the Bank even after office hours and be sure to have access to an Exim representative.

The Contact Centre, which can receive calls in both English and Swahili, will also have some of the harder-to-find features like warm-calling services with robust Self-Help Interactive Voice Respond   supporting TANAPA. This means any TANAPA Card holder can now use the self-service IVR to know their card balance. This removes the need for a TANAPA Card holder to visit any branch or ATM for information on their account balance.

“It is very important for our business that clients are able to conveniently access the information they need. We have dedicated and well trained agents with personalized service focused solely on our business, which means by simply calling our help line 0784107600 you can get any information on Exim products and services”, said Frank Matoro, Exim Bank Customer Service, Senior Manager.

In the near future Exim Bank plans to extend its Contact Centre work hours to a full service 24/7 call centre. In the meantime the Exim Bank customers and the general public can access the Contact Centre from 7:00 am to 8:00 pm on weekdays and 9:00 am to 4:00 pm on weekends through 0784107600.

WAIMBAJI WA TAMASHA LA PASAKA WAANZA KUWASILI LEO,SOLLY MAHLANGU KUWASILI KESHO JIJINI DAR

$
0
0
Pichani kulia ni Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akiimba moja ya wimbo wake ulioitwa Mkono wa Bwana, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani),leo mchana,jijini Dar,Mercy tayari amekwisha wasili jijini Dar tayari kutumbuiza katika tamasha la pasaka litakalofanyika April 16,2017 ndani ya Uwanja wa uhuru,ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa mambo ya Ndani Mh.Mwigulu Nchemba.Pichani shoto ni Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions,Alex Msama,ambayo ndio waandaaji wa tamasha hilo.
 Mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika akielezea namna alivyojiandaa kuwakonga mashabiki wake mbalimbali watakaofika katika tamasha la Pasaka hapo Jumapili ndani ya uwanja wa Uhuru,Mercy amesema amejiandaa vyema na amewaomba wapenzi wa Injili wakiwa na familia zao kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo adhimu ikiwemo kumtukuza na Kumuabudu Mungu kwa njia ya Uimbaji.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama akizungumza na Waandishi wa habari mapema leo mchana kuelekea kwenye kilele cha tamasha la Pasaka,linalotarajiwa kufanyika jumapili hii April 16,2017,katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar.Msama amesema kuwa kila kitu kimekamilika na Waimbaji watakaotumbuiza katika tamasha hilo wanaendelea kujiandaa vilivyo,na walioko nje ya nchi tayari wameanza kuwasili akiwemo Muimbaji Mercy Masika kutoka nchini Kenya,na kesho wanawasili waimbaji wengine akiwemo muimbaji nyota kutoka Afrika Kusini Solly Mahlangu na skwadi lake.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions ,Alex Msama,Muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya,Mercy Masika na Mdau wa nyimbo za injili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na wana habari,mapema leo mchana jijini Dar.

ASKOFU DK.ALEX MALASUSA AONGOZA IBADA YA IJUMAA KUU KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA AZANIA FRONT JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Muumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Azania Front, Moses Kombe (katikati) na wenzake wakiigiza igizo la kumbukumbu ya kuambwa msalabani kwa Yesu Kristo miaka 2000 iliyopita katika ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika katika kanisa hilo jijini Dar es Salaam leo jioni.
 Igizo likiendelea.
 Askofu mstaafu Dk. Alex Malasusa akisalimiana na waumini wa kanisa hilo baada ya ibada ya Ijumaa Kuu.
 Muonekano wa waumini wakati wa ibada hiyo.
 Kwaya Kuu ya Ushairika huo ikitoa burudani ya nyimbo za kifo chake Yesu Kristo wakati wa kuhitimisha ibada hiyo.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa nje kwa kuhitimisha ibada hiyo.
Waumini wakitakiana kheri ya Ijumaa Kuu baada ya ibada hiyo.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>