Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live

TV 1 YAJITOSA KUTAFUTA FEDHA ZA MASHINDANO UA TENIS YATAYOFANYIKA MEI NCHINI ITALY

$
0
0
 Katibu mkuu wa Chama cha Tennisi nchini , Irene Jackson Mwasanga  akizungumza na waandsihi wa habari juu ya mpango wa kuiwezesha timu ya mchezo wa Tennisi kwa walemavu
 Meneja Masoko wa TV 1 Tanzania , Gllian Rugumamu akizungumza na waandishi wa habari juu ya mpango wa T V 1 Kusaidia timu hiyo hili iweze kusafiri kwenda Italy kushiriki mashindano ya Dunia.
 Promotion Meneja wa kituo cha radio cha Times Fm, Namiundu Ngutupari  akizungumza juu ya kituo hicho kujiingiza katika kusaidia kupatikana kwa fedha za wachezaji hao kuwawezesha kufika nchini Italy katika mashindano ya Dunia
 Meneja Masoko wa kampuni ya bima ya Tanzania Management Insuarance ,Johnson  Wariko akizungumzia jinsi kampuni yake ilivyojipanaga kuwawekea bima wachezaji hao ambao watasafiri kwenda nchini Italay



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Timu ya Magongo ya Tennis inahitaji milioni 120 ili kuweza kushiriki mashindano ya kimataifa yanayotarajia kutimua vumbi Mei 1 hadi Mei 6 nchini Italy.
Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam, Rais wa timu hiyo,  Denis Makoi amesema kuwa hadi sasa wamepata dola 3500 ambazo dola 3000  zimetolewa na  Kampuni ya TPS  na dola 1500 zimetolewa na shirikisho la Tenis la Kimataifa.
Amesema mashindano  hayo ni mhimu kwa timu hiyo kwani wao ndio mabingwa wa Afrika hivyo kushiriki kwao kutaongeza kuwa na uwezo na kuiletea Taifa heshima ya mchezo huo.
Makoi amesema kuwa TV One wamejitoa kuungana na katika kutafuta fedha hizo ili timu hiyo iweze kushiriki mashindano hayo yatayoifanya Tanzania kuingia katika ramani mchezo wa Tenis.
Meneja wa Masoko wa TV 1, Gillian Rugumamu amesema wamejitoa katika kuhamasisha watanzania kuchangia timu hiyo ili iweze kushiriki mashindano hayo.
Gillian amesema kama chombo cha habari wanawajibu wa kuhamasisha mchezo wa tenis kutokana na vjana kuwa na uwezo wa mchezo huo.
Amewaomba watanzania kuchangia kwa njia mbalimbali ikiwemo kwa M-Pesa kwa kuingiza namba 5590901 kwa Benki ya NIC kwa fedha ya Kitanzania  A/C No.2000021086  na dola za Kimarekani kwa akaunti  A/C NO. 2000021094.

 Mcheza Tenisi Vosta Piter akijaribu kurudisha mpira uliopigwa na mwenzie katika mazoezi ya mchezo huo katika Viwanja vya Gymkhana  Dar es Salaam
mcheza Tennisi akiwa katika mazoezi ya kawaida katika uwanja wa Gymkhana jijini Dar es Salaam leo

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA ZIARA FUPI HIFADHI YA TAIFA RUAHA NA KUJIONEA UTIRIRISHAJI HAFIFU WA MAJI KATIKA MTO RUAHA.

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na wa Mkoa wa Iringa kuwa Serikali italifanyia kazi tatizo la ubovu wa barabara kutoka Iringa mjini Hadi katika hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na Viongozi wa Hifadhi hiyo na wa mkoa wa Iringa baada ya kufanya ziara fupi katika hifadhi hiyo pamoja na kujionea utiririshaji hafifu wa maji katika Mto Ruaha uliosababishwa na shughuli za kibinadamu hasa kilimo.

Makamu wa Rais amesema serikali itahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami kama hatua ya kuongeza maradufu idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo kutokana na ubovu wa barabara kuelekea hifadhi hapo idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo imeendelea kupungua kila uchao.

Kuhusu vitendo vya ujangili hifadhi hapo, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa hifadhi hiyo kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ili kuwabaini majangili na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Amesema idadi kubwa ya majangili wanatoka miongoni mwa jamii zinazozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha hivyo wananchi wakishirikishwa kikamilifu katika kutoka taarifa za siri majangili wengi watakamatwa na kuwajibishwa.

Awali akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais, Kuhusu utendaji kazi wa Hifadhi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ALLAN KIJAZI aliiomba serikali isaidie kulinusuru bonde la Usangu ili liweze kurejesha mtitiriko wa maji kwa ajili ya matumizi ya hifadhi hiyo na kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi na wananchi ambao umedumu kwa muda mrefu bila suluhu kupatikana.

Amesema mapaka sasa TANAPA imeshatumia zaidi ya shilingi bilioni SABA kwa ajili ya kulipa fidia wananchi na gharama nyingine ili kunusuru bonde hilo lakini bado kuna changamoto ambazo zinaathiri usimamizi wa eneo hilo na zinahitaji maamuzi ya serikali.

Mkurugenzi huyo Mkuu wa TANAPA pia amepongeza msukumo wa dhati wa serikali ya awamu ya Tano katika kusimamia hifadhi ya mazingira na maliasili kwani jitihada hizo zitasaidia kuboresha mazingira na viumbe hai kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais

Iringa 12-April-2017.





 

WABUNGE WAIPITISHA BAJETI YA OFISI YA WAZIRI MKUU LEO APRILI 12, 2017 MJINI DODOMA.

$
0
0
 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai akiongoza Kikao cha sita cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 kipindi cha jioni Leo Aprili 12, 2017 Mjini DODoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka Fedha 2017/2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka Fedha 2017/2018.
Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde  akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka Fedha 2017/2018.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Naibu Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu  Kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakifuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018.
Wabunge na Mawaziri wakifuatilia Hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa  akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliochangia katika Hotuba yake ya Bajeti leo Mjini Dodoma na baadae wabunge hao kuipitisha kwa pamoja Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.

WAZIRI MKUU: TOENI TAARIFA ZA AJIRA KILA ROBO MWAKA

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka ya serikali za mitaa, wizara na taasisi zote zitoe taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kila robo mwaka.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Aprili 6, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akitoa maelezo ya kuhitimisha majadiliano ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe ambaye aliitaka Serikali itoe maagizo kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kutengeneza ajira angalau 20,000 kila mwaka katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri zao, na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo iwe inatolewa kila mwaka kwenye Bunge la Bajeti.

“Napenda, kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015, Ibara ya 59 inazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kuzingatia viashiria vya ukuzaji ajira katika mipango ya maendeleo ya ngazi husika pamoja na kutoa taarifa za mwenendo wa ajira kila robo mwaka,” amesema.

Waziri Mkuu amesema maelekezo hayo, yanazingatiwa katika Mwongozo wa kuandaa Bajeti ya Serikali unaotolewa na HAZINA kila mwaka ambao unazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote zibainishe fursa za ajira zinazotarajiwa kupatikana kila mwaka kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Vilevile mwongozo huo unazitaka taasisi hizo kutoa taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo kila robo mwaka. Ninatoa agizo, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote ziendelee kuzingatia maelekezo haya,” amesema.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema ndani ya mwaka mmoja, jumla ya viwanda 2,169 vimesajiliwa vikiwemo viwanda vya mbolea, saruji, chuma na vya usindikaji wa mazao.

“Serikali pia inaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuvutia uwekezaji nchini. Uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda nchini ni dhahiri na tayari tumeanza kuona matokeo. Kwa mfano, mkoa wa Pwani peke yake una viwanda vikubwa 83 na vingine vidogo vidogo zaidi ya 200. Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alisema Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Fedha Vijijini (MIVARF) ilipanga kukarabati barabara zenye jumla ya kilomita 148.5, kujenga masoko manne na kukarabati kituo kimoja cha mafunzo ya utunzaji mazao baada ya kuvuna.

Akijibu hoja za utekelezaji wa programu hiyo kwa upande wa Pemba na Unguja, Waziri Mhagama alisema miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara ilianza Agosti na Novemba 2014 na kazi hiyo kwa Pemba ilikamilika Desemba  2015 wakati kwa upande wa Unguja ilikamilika Januari  2016.

“Kazi  za ujenzi  wa  masoko  ya  Kinyasini  na Mombasa  (Unguja)  pamoja  na Konde na Tibirinzi  (Pemba) zilianza Desemba  2016 na zinatarajiwa kukamilika Julai 2017. Wakandarasi wamehimizwa kuhakikisha wanakamilisha kazi hizo katika muda uliopangwa ili kuendana na ratiba iliyopangwa,” alisema.

Akijibu hoja kuhusu uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma, Waziri Mhagama alisema uamuzi wa kuhamia Dodoma na kuifanya Makao Makuu ya Serikali ilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alitaka kuona Dodoma ikistawi na Serikali kuweza kuhamia huko ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya Mji Mkuu.

Alisema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma siyo suala la kisiasa kama baadhi ya watu wanavyodai bali ni utekelezaji wa maamuzi kamili kama yalivyoelekezwa kwenye Ibara ya 151 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kama ilivyotamkwa kwenye GN namba 273 ambayo ni tamko la Serikali na sheria halali.

Naye Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Anthony Mavunde alisema kila mwaka vijana kati ya 800,000 hadi milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira wakati soko la ajira ni dogo.

Hata hivyo, Naibu Waziri Mavunde alisema Serikali imeanza kubadilisha mtazamo wa vijana kuhusu ajira kwani wengi wao hudhani kwamba kuwa na ajira ni lazima mtu avae tai, awe na ofisi yenye meza na kiti kinachozunguka.

(mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA,
JUMATANO, APRILI 12, 2017.

PICHA ZA MATUKIO KUMBUKUMBU YA HAYATI SOKOINE,LEO WILAYANI MONDULI

$
0
0
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Marehemu Edward Moringe Sokoine
 Wajane wa Marehemu Sokoine Mama Napono Katrika (kati) Mama Nekiteto (kulia), wakiwa na waziri wa maliasili na utalii Profesa Jumanne Maghembe nyumbani kwao Wilayani Monduli
 Msaidizi wa Askofu, Prosper Lyimo akihubiri wakati wa ibada ya kuadhimisha miaka 33 ya kifo cha Waziri Mkuu wa Zamani, Marehemu Edward Moringe Sokoine
 Binti wa Sokoine Namelok na Kaka yake, Balozi Joseph Sokoine wakiwa na wageni wengine walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya baba yao wilayani Monduli.
 Wajane wa marehemu Sokoine wakiweka shada la maua katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe akiweka shada la maua katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli wakati wa kumbukizi ya kifo cha kiongozi huyo kilichiotokea miaka 33 iliyopita  nyumbani kwa Sokoine
 Mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigedia Jenerali Anderson Ghulila akiweka shada la maua katika kaburi la Hayati Edward Sokoine, wilayani Monduli katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo kilichotokea miaka 33 iliyopita 
 Wajukuu wa Hayati Edward Sokoine wakiwa katika ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine 
 Mtoto wa Hayati Sokoine, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na wageni waalikwa katika misa maalum ya kumuenzi baba yake.
 Baadhi ya wageni kutoka sehemu mbalimbali waliohudhuria misa ya kumbukumbuku ya Sokoine.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka akibadilishana mawazo na mwakilishi wa mkuu wa Majeshi Tanzania, Brigedia Jenerali, Anderson Ghulila pamoja aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, Balozi Daniel Ole Njoolay
 Baadhi ya viongozi walioshiriki ibada ya kumbukumbu ya miaka 33 ya Sokoine, kutoka kushoto ni Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Mkoani Arusha, Solomon Masagwa, Mwakilishi wa Shehe Mkuu, Rajab Kiungiza, Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka na Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe
 Wanakwaya wakiandamana kuelekea eneo la ibada tayari kwa Misa Maalum
Msaidizi wa Askofu, jimbo kuu Katoliki Arusha, Prosper Lyimo akiweka shada la maua kwenye kaburi la Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Moringe Sokoine wakati wa ibada ya kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo miaka 33 iliyopita, iliyofanyika nyumbani kwa Sokoine wilayani Monduli. Picha zaote na Pam Mollel wa Globu ya Jamii, Monduli

UJUMBE WA MASHIRIKA YA UMOJA WA MATAIFA (UN) TANZANIA WATEMBELEA HOSPITALI KUU YA MNAZIMMOJA

$
0
0




Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Dkt. Naufal Kassim Mohd akitoa maendeleo na changamoto za Hospitali ya Mnazimmoja wakati Ujumbe wa Mashirika ya UN ulipotembelea Hospitali hiyo.
 A 1
 Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodriguez akiuliza swali kwa uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja alipotembelea Hospitali hiyo kujuwa maendeleo yake.
 A 2
Mhandisi Mkuu wa Hospitali ya Mnazimmoja Mathna Kassim Marine akitoa maelezo kwa Mratibu wa Mashirika ya UN alipotembelea sehemu ya kuzalisha gesi ya Oxygen inayotumika katika Hospitali hiyo.
 A 3
Ujumbe wa Mashirika ya UN Tanzania ukiongozwa na Alvaro Rodriguez wa kwanza (kushoto) ukitembelea Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
 A 4
 Wajumbe wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania wakitembelea wodi mpya ya wazazi ya Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA STANDARD GAUGE KUTOKA DAR HADI MOROGORO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiweka jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia majina ya baadhi ya wataalamu mbalimbali waliohusika katika mchakato wa Ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza. Wakwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akiwa ameshika majina hayo.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akichota mchanga na kuweka kama ishara ya kushiriki katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia kibao cha jiwe la msingi cha Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Mama Janeth Magufuli wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielezea kuhusu ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amechuchumaa kwenye mfano wa Reli ya Kisasa (SGR) na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Masanja Kadogosa, Mwenyekiti wa Kamati  ya Kudumu ya Miundombinu Profesa Norman Sigala mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli hiyo, wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli pamoja na Hawa Ghasia (Mb).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mabarawa wakati akipita katika katika ya mfano wa Reli hiyo itakayojengwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi Ujenzi wa Reli ya Kisasa Standard Gauge itakayoanzia jijini Dar es Salaam hadi mkoani Morogoro na baadaye kuendelea hadi Kigoma na Mwanza.
Mfano wa Reli hiyo ya Kisasa ya Standard Gauge SGR itakayojengwa kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro na baadae kuendelea hadi mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Mtendaji Mkuu wa RAHCO Masanja Kadogosa wakati akielekea kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia kabla ya kuweka jiwe la Msingi ujenzi wa Reli hiyo ya Kisasa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Shekhe Abubakary Zubeiry mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza msanii Mrisho Mpoto mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika ujenzi huo wa Reli ya Kisasa Pugu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.


VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 13, 2017


PROFESA MUHONGO AKUTANA NA WENYE NIA KUWEKEZA SEKTA YA NISHATI NCHINI

$
0
0

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akimsikiliza mwekezaji kutoka Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta (kulia). Katikati ni Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary.
 Kutoka kulia ni Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya umma katika Benki ya Stanbic, Noella Kimaro, Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo, Thomas Buonga na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary, wakimsikiliza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), walipomtembelea ofisini kwake Dodoma hivi karibuni na kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiagana na Ujumbe kutoka Benki ya Stanbic, waliofika ofisini kwake mjini Dodoma, kueleza nia yao ya kuwekeza katika sekta ya nishati nchini. Kushoto kwa Waziri ni Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hillary.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisisitiza jambo wakati wa kikao baina yake na mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer (katikati), aliyemtembelea ofisini kwake Dodoma hivi karibuni na kueleza nia ya kuwekeza kwenye sekta ya nishati nchini. Kulia ni Ofisa kutoka Ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer (kushoto) na Ofisa kutoka Ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi (kulia).


Na Veronica Simba - Dodoma

Wawekezaji mbalimbali wamemtembelea Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ofisini kwake mjini Dodoma na kumweleza nia yao ya kuwekeza kwenye miradi mbalimbali katika sekta ya nishati nchini.

Akizungumza na Waziri Muhongo, mwakilishi wa Kampuni ya L&T ya India, Sanjay Gupta aliwasilisha nia ya Kampuni hiyo ya kujenga njia ya kusafirisha umeme kutoka Chalinze hadi Dodoma.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Stanbic, Thomas Buonga akiwa ameambatana na Mkuu wa Sekta inayoshughulikia masuala ya Umma wa Benki hiyo, Noella Kimaro, walimweleza Waziri kuwa wanaangalia fursa ya kuwekeza katika miradi ya sekta ya nishati.

Naye, mwekezaji kutoka Denmark, Malte Meyer, akiwa amefuatana na Ofisa kutoka ubalozi wa nchi hiyo, Derrick Katunzi, alisema nia ya kampuni yake ni kuwekeza katika sekta ya nishati hususan uzalishaji wa umeme kwa kutumia upepo.

Waziri Muhongo aliwakaribisha wawekezaji hao na kuwahakikishia kupata ushirikiano kutoka serikalini endapo watakidhi vigezo stahiki vya uwekezaji vilivyowekwa.

TUKITAKA NCHI YA VIWANDA TUPIGE VITA DAWA ZA KULEVYA-ASKOFU BANZI.

$
0
0

ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi akizungumza na wanafunzi kutoka shule mbalimbali Jijini Tanga wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu wilaya ya Tanga ambapo kiwilaya lilifanyika kwenye shule ya Sekondari Tanga Don Bosco iliyopo eneo la Maweni jijini Tanga inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga.
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi wa pili kulia akimkiliza mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo wakati alipokuwa akifafanua jambo
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi katikati akionyesha jambo na Sista ambaye anafanya kazi kwenye shule hiyo
ASKOFU wa Jimbo Katoliki la Tanga, Mhashamu Anthony Banzi amesema iwapo Serikali inataka nchi ya viwanda hawana budi kuweka msukumo mkubwa kwenye kupiga vita dawa za kulevya vitendo ambazo zimechangia kwa asilimia kuwaharibu vijana wengi hapa nchini. 

Banzi aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu wilaya ya Tanga ambapo kiwilaya lilifanyika kwenye shule ya Sekondari Tanga Don Bosco iliyopo eneo la Maweni jijini Tanga inayomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Tanga. 

Alisema ili kutimiza azma hiyo ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi lazima kuwepo na juhudi kubwa za kuuteketeza mtandao wa dawa za kulevya hapa nchini uliyoharibu vijana wengi ambao wangekuwa nguvu kazi kubwa ya Taifa la kesho. 

“Kama tunataka kuifanya nchi kuwa ya viwanda maana yake kila mmoja apate elimu ya madhara ya dawa za kulevya lengo kubwa likiwa kuliondoa tatizo hilo kwa vijana ambalo limekuwa likipoteza nguvu kazi ambayo ingeweza kutumika katika shughuli mbalimbali lakini pia kuwepo kwa mapambano ya kupiga vita hali hiyo “Alisema. 

“Lazima kuwepo kwa dhamira ya dhati na mipango ambayo itawezesha kuutokomeza mtandao wa dawa za kulevya unaoangamiza vijana wengi ambao wangewezesha kufanya shughuli za uzalishaji mali na kujiingizia kipato halali na kuendesha maisha yao bila kuwa tegemezi “Alisema Askofu Banzi. 

“Vijana tuachane na matumizi ya dawa za kulevya ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha kuharibu vijana ili kuendana na sera ya maendeleo ya viwanda kwa kuyapiga vita”Alisema. 

Akizungumzia suala la utunzaji wa mazingira,Askofu Banzi aliitaka
jamii kuacha kukata miti ovyo,kuchimba mahandaki ambayo kwa asilimia kubwa yamekuwa yakichangia uharibifu wa mazingira. “Kwani suala la ukataji miti ovyo limekuwa tishio kubwa hapa nchini na kuifanya kugeuka jangwa kitendo ambacho kimeweza kuchangia uharibifu mkubwa wa mazingira kwa jamii hivyo lazima tuachana na jambo hilo“Alisema. 

Awali akizungumza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Don Bosco Gregory Mhuza alisema waliamua kupanda miti ili kuhakikisha wanatunza mazingira ambayo ni muhimu kwa jamii. 

“Sisi kama shule leo hii tumepanda miti lakini tutahakikisha
tunaitunza na kuilinda kwa vizazi vya sasa na vijazo ili kuiepusha
nchi yetu kukumbwa na janga “Alisema. 

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi Maweni,Wales Janga alisema uzinduzi wa Juma la Elimu kwa kupanda miti katika shule hiyo ni ishara ya kuthamini uwepo wa mazingira kutokana na usemi usemao tunza mazingira yakutunze hivyo jamii haina budi kufanya hivyo ili kuendena na suala hilo.

“Pamoja na kupanda miti pia tutatembelea maabara ya ufundi kwani shule hii ni shule ya Ufundi ili tuweze kuona namna vijana wetu wanajifunza katika masomo yao ya ufundi kuelekea Tanzania ya Viwanda ya Mwaka 2025 “Alisema. 

Alisema kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii majukumu yake katika suala zima la elimu duni kwani baadhi yao wamelipokea suala la elimu bila malipo tofauti na kujisahau kuwa wao ni mdau namba“Alisema.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii Tanga Raha.

MFUMO WA STAKABADHI GHALANI MKOMBOZI KWA WAKULIMA.

$
0
0
Jovina Bujulu- MAELEZO

Kuwepo na mfumo wa stakabadhi ghalani kumekuwa ni mkombozi pekee kwa wakulima wadogo na wa kati kwa kuwawezesha kupata bei nzuri ya mazao yao, ukilinganisha na bei zilizokuwa zinatolewa na wafanyabiashara wanaponunua mazao yakiwa shambani kwa kutumia vipimo ambavyo sio sahihi.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya usimamizi wa Stakabadhi za Ghala imesema kuwa kabla ya mfumo huo kuanza wakulima walikuwa wakipunjwa bei ya mazao na wafanyabiashara na kutolea mfano zao la korosho ambapo katika msimu wa 2015/2016, kilo moja ya korosho ilinunuliwa kwa shilingi 2900 na msimu wa 2016/2017 bei ilipanda na kufikia shilingi 4,000 kwa kilo ambazo ni sawa na ongezeko la asilimia 15.9

Mfumo huo umewanufaisha wakulima kwa kutumia ghala ambazo ziliachwa kwa muda mrefu bila matumizi ambazo zimekuwa na tija kwa wakulima.

Kupitia ghala hizo zenye ujazo wa kuanzia tani 200 hadi 5000 na kuendelea wameweza kuhifadhi mazao yao vizuri na kwa ubora unaotakiwa kwa matumizi ya sasa nay a baadaye.

Aidha, mfumo huo umeongeza ajira kwa wakina mama na vijana hasa katika maeneo ya kuchambua, kupokea na kupanga mazao ghalani. Vijana wengi wameajiriwa kwa kazi ya kushusha, kupanga na kupakia mazao na wameweza kujiajiri katika kilimo baada ya kuona mfumo huo unavyofanya kazi vizuri na kuwa na uhakika wa soko la mazao yao.

Wakulima pia wamepata mafanikio kwa kuwa na uhakika wa vipimo vya mazao yao yanayohifadhiwa ghalani kupimwa kwa kilogramu na si vinginevyo ambapo kabla ya mfumo huo wakulima walikuwa wakiibiwa mazao yao kutokana na matumizi ya vipimo ambavyo si sahihi.

Kwa kuhifadhi mazao yao katika ghala zenye leseni, wakulima wamekuwa wanatumia mazao hayo kama dhamana ya kupata mikopo kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha. Hii imewezekana kutokana na wakulima hao kujiunga katika umoja kupitia vikundi au vyama vya ushirika .

Wafanyabiashara pia wameneemeka na mfumo huu, ambapo kwa sasa wameweza kupunguza gharama za kufuata mazao maeneo mbalimbali mazao yanapatikana kwa wingi badala yake mazao hayo wanayapata katika eneo moja kkwenye ghala zilizosajiliwa na hivyo kuondoa hatari ya kuibiwa pesa zao na madalali wasio waaminifu.

Mfumo huo pia umekuwa na faida kwa bodi za mazao katika kuandaa bajeti za mahitaji ya pembejeo na kuongeza ili kuboresha na kuongeza uzalishaji.

Aidha, mfumo huo umechochea na kuharakisha uanzishwaji wa soko la bidhaa nchini, kutokana na kuwepo kwa bidhaa zenye ubora na zinazopatikana kwa wakati. Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala, inatoa wito kwa wakulima kuunga mkono uhamasishaji wa matumizi ya soko hilo ili kuongeza tija na kasi ya kukuza biashara ya mazao ya kilimo hapa nchini.

Mfuko wa Stakabadhi Ghalani ulianza mwaka 2000 ukifadhiliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Bidhaa. Lengo la mfuko huo ni kuwezesha wakulima kufaidika na ongezeko la bei katika msimu wa mazao, kuongeza mapato ya wakulima na kuboresha kipato chao ikiwa ni pamoja na kuwapa wakulima nguvu ya soko kwa kuhamasisha utumiaji wa vikundi vya wakulima na ushirika.

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA TBA

$
0
0
                JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
      WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO





Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo. 

Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-

1.    Eng. John Bura – Mkandarasi  kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
2.    Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
3.    Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
4.    Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
5.    Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)

12.04.2017

MAKALA YA KUMBUKIZI LA KUZALIWA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Na Judith Mhina-MAELEZO

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ulikuja hapa duniani Aprili 13, 1922 kupitia kwa Mpendwa Marehemu Bibi Mgaya wa Buritho kama zawadi kwa nchi ya Tanzania.

Mwalimu tunamshukuru Mungu kwa kutupa wewe ambaye umeitendea mambo makubwa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.

Mwalimu wakati nakumbuka kuzaliwa kwako nimepata fursa ya kuangalia kazi ulizozifanya mara baada ya kuacha madaraka ya Urais na kujikita katika kazi kuu tano; Mosi pamoja na kubaki na kofia moja ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ya kuimarisha Chama na alianza maandalizi ya kukabidhi Uenyekiti huo kwa Rais aliyepokea madaraka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye alikuwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Pili, mwaka 1986 baadhi ya Viongozi wa nchi za Kusini mwa Dunia, walikuomba kuanzisha Tume ya Uchambuzi wa maendeleo ya nchi za Kusini tangu miaka 30 iliyopita na kuweza kuona hatua za maendeleo na changamoto zilizopo katika mataifa hayo na mapendekezo ya nini kifanyike ili kuboresha ustawi wa wananchi.

Mwalimu Nyerere alikubali jukumu hilo, ndipo alianza kutembelea nchi 19 katika Bara la Asia na Marekani ya Kusini kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa majukumu hayo mapya. Safari ya kutafuta maoni hayo ilikuwa ni pamoja na kupata uthibitisho wa kuwaelewesha wananchi na nchi hizo kuhusu majukumu ya Tume na aina ya maoni yanayokusanywa.

Kazi hiyo aliifanya kwa miaka mitatu na kutoa ripoti kuwa nchi za Kusini zifanye maendeleo yao yenyewe yalenge maslahi ya wananchi walio wengi kwa kielelezo kuwa ili nchi za Afrika ziweze kupiga hatua za maendeleo ni vyema ziwe na mshikamano kama zinahitaji kushindana na nchi za Kaskazini.

“Nchi za Kusini zishirikiane kibiashara, kwa kuwa nchi za Kusini zina mazoea ya kufanya biashara na nchi za Kaskazini lakini hakuna utaratibu mzuri wa nchi za Kusini kufanya biashara wenyewe kwa wenyewe, au hata katika uwekezaji rasilimali” alisema Mwalimu Nyerere.

Aidha, Mwalimu Nyerere alisema Wataalam wengi wako Kusini lakini nchi za Kusini zinatafuta wataalam kutoka Kaskazini, hivyo ni wajibu wa nchi za Kusini kujenga na kuimarisha ushirikiano wa pamoja baina yao.

Tatu, Mwalimu alianzisha kituo cha muda cha Nchi za Kusini pale Geneva ambapo Mwalimu na Viongozi wengine walifanya kazi kwa muda wa miaka miwili, jukumu lao likawa kuelezea shughuli za maamuzi na mapendekezo ya Tume.

Nne, kuanzisha Ofisi ya kudumu ya Nchi za Kusini pale Geneva kwa ajili ya Mataifa hayo kutoa hoja kupitia vuguvugu la nchi za kundi la 77 ambazo hazikuwa na chombo cha kuwasaidia kupaza sauti zao.

Mwalimu akapokea jukumu hilo na kuanzisha Ofisi ya kudumu ambayo ilikuwa chombo cha Serikali badala ya chombo cha kiraia na kuhusisha nchi 49 ambazo ziliweka sahihi, pamoja na nchi kubwa ulimwenguni ikiwemo India, Brazil na Afrika ya kusini.

Tano, alikuja na wazo la kuanzisha Taasisi ya Mwalimu Nyerere, hatua iliyotokana na harakati za kazi yake ya kuunganisha nchi za kusini, ambapo alitaka taasisi hiyo kufanya kazi zake katika ukanda wote wa nchi za Bara la Afrika.

Miongoni mwa kazi hizo ni pamoja na kuangalia maendeleo ya watu, kupitia dhana ya umoja na ushirikiano miongoni mwao.

Nakumbuka hotuba ya Mwalimu Nyerere aliitoa mwezi Februari mwaka 1960, akiwa Rais wa chama cha Tanganyika African National Union (TANU) , alikaribishwa nchini Marekani katika Kongamano la Afrika katika Chuo cha Wellesley Massachusetts kuongelea kuhusu “Nafasi ya Afrika Duniani” .

Katika hotuba hiyo, Mwalimu alizungumzia hatua mbalimbali za ukombozi wa Bara la Afrika, mchango wa Waafrika katika Mataifa ya Ulaya na Marekani. Mwalimu alilisemea Bara la Afrika Kama Bara la matumaini kwa ubaguzi wa rangi.

Mwalimu alisisistiza kwa kusema “Muda utafika ambapo Marekani na Ulaya Magharibi watajisikia vibaya jinsi walivyoitumia Afrika” huku akitolea mifano ya mateso na manyanyaso waliyoyapata Waafrika ikiwemo vita vya Mau Mau nchini Kenya, vifo vya watu wa kabila la Waherero nchini Namibia, vita vya Majimaji nchini Tanzania.

Hotuba hiyo ilikuwa ya kwanza kwa Mwalimu Nyerere kuchapishwa kimataifa, hakika imeonyesha kwa dhati, Mwalimu hata kabla ya Uhuru alitambua nafasi ya umoja katika kupigania uhuru wa Bara la Afrika.

Aidha, ndoto hii ya umoja alisafiri nayo katika kujenga Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Nafasi ya Uenyekiti Jumuiya wa Nchi zilizo mstari wa mbele katika Ukombozi Kusini mwa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na nyingine nyingi.

Taasisi ya Mwalimu Nyerere dhumuni lake kuu ni kuendeleza Amani, Umoja na Utulivu wa Maendeleo ya pamoja Barani Afrika. Mwalimu alikuwa muanzilishi na Mweneyekiti wa kwanza wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere.

Septemba 14, 1996 alikaribishwa Kilimanjaro hoteli kuhutubia na kuzindua Taasisi ya Mwalimu Nyerere. Umuhimu wa Umoja, umuhimu wa ukubwa wa soko, Amani baina ya nchi ndani na nje ya nchi na Maendeleo katika Afrika.

Alipata fursa ya kukutana na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwaeleza juu ya Taasisi hiyo na madhumuni yake. Katika kipindi hiki Mwalimu alikuwa msuluhishi wa mgogora wa Burundi.

Mwalimu leo ungetimiza miaka 95 tangu kuzaliwa, kimwili hatupo pamoja nawe, lakini fikra zako, mitazamo yako, utendaji wako bado ni dira na muelekeo wa Taifa letu Daima tutazifuata. Hakika siku ya leo ni siku muhimu sana kwa nchi yetu. Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA MTERA

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amesimama kwenye kituo cha Kufua Umeme cha Mtera akiwa njiani kuelekea Dodoma ambapo Meneja wa Kituo hicho Mhandisi John Sikauki alimpa taarifa ya kituo ambapo alimueleza kuwa kina cha maji kipo chini sana na wanapokea maji kutoka Mto Ruaha Mdogo na Kisigo (hasa wakati wa mvua)na kwa sasa hawapati maji kabisa kutoka Mto Ruaha Mkuu.

Makamu wa Rais alisikitishwa na taarifa hii na aliahidi kuwa Kikosi Kazi cha Kitaifa alichozindua cha kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu kitatoa majawabu ya tatizo hili na aliomba Tanesco kutoa ushirikiano kwa kikosi kazi hiki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akipokea taarifa ya kina cha maji katika kituo cha kufua umeme cha Mtera kutoka kwa Meneja wa Kituo hicho Mhandisi John Sikauki wakati akiwa njiani kuelekea Dodoma baada ya kumaliza shughuli za kuzindua Kikosi Kazi cha Taifa cha kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu mjini Iringa. (PichA na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wafanyakazi wa kituo cha kufua umeme cha Mtera akiwa njiani kuelekea Dodoma baada ya kumaliza shughuli za kuzindua Kikosi Kazi cha Taifa cha kunusuru ikolojia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu mjini Iringa.


 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza Viongozi wa mikoa wa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya kukabiliana na tatizo la kilimo karibu na mito ambacho kimechangia kupungua kwa maji kwenye bwawa la Kufua Umeme la Mtera.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo baada ya kufanya ziara fupi katika bwawa la Kuzalisha umeme la Mtera wakati akielekea Dar es Salaam ili kujionea utendaji kazi wa Bwawa hilo baada ya kumaliza ziara ya kikazi ya Siku Tatu mkoani Iringa.

Makamu wa Rais amesema uharibifu mkubwa unaondelea kwenye mito inayotiririsha maji kuelekea Bwawa la Mtera ndio chanzo cha maji kuendelea kupungua mwaka hadi mwaka hivyo hatua za kukabiliana na hali hiyo ni lazima zikuchuliwe ili kukokoa bwawa hilo kukauka.

Amesema bwawa la kufua umeme la Mtera ni muhimu kutokana na uzalishaji wake wa umeme ambao unatumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi hivyo Serikali haitakubali hata kidogo bwawa lisitishe kuzalisha umeme kutokana na uharibifu huo wa mazingira.

Makamu wa Rais amewahimiza wafanyakazi wa kituo hicho kufanya kazi kwa uzalendo ili kuhakikisha kituo hicho kinaendelea kufanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa pamoja na changamoto zinazojitokeza.

Akitoa Taarifa ya Hali ya Uzalishaji Umeme kwenye kituo hicho kwa Makamu wa Rais, Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera Mhandisi John Sikauki amemueleza Makamu wa Rais kuwa hali ya mitambo ni nzuri ambapo mpango wa matengenezo kwa kuzingatia umri wa mitambo wa miaka 28 umekwiza anza.

Amesema matengenezo makubwa katika kituo hicho yamefanyika ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Jenereta Mbili.

Mhandisi Sikauki ameeleza kuwa kina cha maji kwa sasa katika bwawa hilo hadi kufikia Aprili mwaka 2017 ni mita 693.76 juu ya usawa wa bahari na kina hicho cha maji kina uwezo wa kuzalisha umeme hadi mwisho mwa Octoba mwaka huu.

Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme cha Mtera amesema jitihada za sasa zinazofanywa na Serikali za kunusuru Hifadhi ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu maana ndio chanzo cha kuaminika cha kufanya Bwawa la Mtera kuwa na maji ya uhakika na hivyo kutaleta ufanisi katika ufuaji wa umeme katika kituo hicho na cha Kidatu kwa mwaka mzima.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Iringa 13-April-2017.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZAIARA KATA YA MASANGA NA KUZUNGUMZA NA WANANCHI, APIGA MARUFUKU UUZAJI WA CHAKULA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba amepiga marufuku wananchi kuuza mazao ya chakula wanayovuna hususan mtama na badala yake waweke akiba. 

Taraba alipiga marufuku hiyo jana wakati akifanya ziara katika kata za Lagana, Mwamashele, Mwakipoya na Masanga baada ya kubaini kuwepo kwa baadhi ya wananchi kufanya biashara hiyo. 

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika kata ya Masanga alisema kuna baadhi ya watu huwahadaa na kununua mtama kwa bei ya juu hali inayowafanya wananchi wabaki bila chakula. 

“Nasikia hapa kuna baadhi watu wanapita kwenu wananchi na kununua debe moja la mtama kwa shilingi elfu ishirini na tano msidanganyie na kuuza wewkeni akiba,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya. 

Aidha alionya tabia ya baadhi ya watu kuuza mazao yakiwa shambani baada ya kukadiriwa kiasi cha mazao yao kabla ya kuyavuna aliwataka wananchi wakatae kufanya hivyo. 

Kwa upande mwingine aliwataka kuandaa mashamba yao mapema na kupanda mazao yanayohimili ukame yakiwemo mtama ili yaweze kustawi na kuwapa chakula. 

Taraba aliwataka wananchi hao kuwatumia wataalamu wa kilimo kwenye kata zao ili kupata ushauri wa kutumia mbegu zilizo bora ambazo zinaweza kuota na kukua kwa haraka.
 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba (katikati) akizungumza na wananchi (hawapo pichani) katika mkutano wa hadhara kata ya Masanga. Wengine pichani kulia ni Afisa Kilimo (Ubora wa mbegu), Maduhu Masunga na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wajumbe aliowakuta wakifanya kikao cha kujadili maendeleo ya kata, Mwamashele alipokuwa katika ziara ya kutembelea kata tatu. 
Mwananchi wa kata ya Masanga akitoa kero yake kwa Mkuu wa Wilaya, Nyabaganga Taraba wakati wa mkutano wa hadhara. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza na wananchi wa kata ya Masanga katika mkutano wa hadhara. Wengine pichani ni kuanzia kushoto ni Afisa Tawala wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Juvenalis Beyakwasho, Mtendaji Kata wa Masanga, John Zablon, na Mwenyekiti wa kijiji cha Masanga, Gambishi Malele. 

OFISI YA MDHIBITI NA MKAGUZI WA MAHESABU YA SERIKALI YAWASILISHA RIPOTI YAKE KWA MWAKA WA FEDHA UNAOISHIA 2015/2016.

$
0
0
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad na Mwenyeketi Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe.Naghenjwa Kaboyoka  wakiangalia moja ya kitabu cha Ripoti kutoka Ofisi yake wakati alipokutana na  na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi MAELEZO Dodoma.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Prof Musa Assad akizungumza na waandishi wa Habari(hawapo Pichani) kuhusu Ripoti ya Ofisi yake kwa mwaka wa Fedha unaoisha 2015/2016 Leo Aprili 13,2017 Mjini Dodoma.

TTB YAWAPELEKA NGONGORO WASHINDI WA KUTUMA PICHA KATIKA KUTEMBELEA UTALII WA NDANI

$
0
0
 Washindi wa shindano la kupiga picha wakiwa mbugani kutangaza utalii wa ndani wakiwa wameongoza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya utalii Tanzania(TTB) ,Devotha Mdachi (katikati) wakiwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNA Dar es Salaam kwa ajili ya Safari ya kuelekea Ngorongoro  na Serengeti kujionea vivutio zaidi ili kuweza kuwavutia watanzania wengine kutembelea vivutio hivyo.
 Washindi wa shindano hilo wakiwa na wenza wao wakijadili jambo kabla ya kuondoka na ndege ya shirika la ndege nchini Air Tanzania kuelekea katika mbuga za wanyama za Ngorongoro na Serengeti,ikiwa ni moja ya sehemu ya Safari zilizoratibiwa na bodi ya utalii nchini (TTB) kwa ajli ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa Watanzania
Afisa uhusiano wa Bodi ya utalii Tanzania  akizungumza jambo na washindi wa shindano la kutuma picha kwa wapenzi ambao walishawahi kutembelea mbuga za wanyama ambao walipata kushinda tena fursa ya kutemmbelea Mbuga ya Ngorongoro na Serengeti.

SALAMU ZA PASAKA KUTOKA KWA MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA DAR ES SALAAM KWA WAKAZI WA MKOA WA DAR ES SALAAM

$
0
0
 
Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Napenda kutumia nafasi hii kwanza kabisa kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuniwezesha kuwa mzima hadi siku hii ya leo. Ni dhahiri kwamba mmekuwa pamoja tangu nilipochaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam. 

akini pia mmekuwa bega kwa bega na mimi Meya wenu wa Jiji, katika juhudi kubwa za kulifanya jiji letu kuwa la kuvutia. Hivyo nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwapongeza sana.

Ushirikiano ambao mnaunyesha na kuendelea kuuonyesha unanipa matumani makubwa kwamba tuko pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaleta mabadiliko makubwa katika jiji letu na hivyo kuondokana na changamoto mbalimbali zinazo likabili jiji letu. hivyo naomba tuendelee kushirikiana na kuzidi kuniombea Meya wenu niweze kufanya kazi ambazo mmenituma katika jiji letu la Dar es Salaam.

Ni wazi mnafahamu kwamba, maendeleo ya jiji letu hajawezi kuletwa bila ya nyinyi wannachi kuonyesha ushirikiano kwa viongozi wenu ambao mmetuchagua kuanzia ngazi za Mitaa, Kata, Halmashauri pamoja na jiji.


Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imekuwa na mipango mingi mizuri ambayo imelenga kuboresha maendeleo ya wananchi wake. Miongoni mwa mambo ambayo niweka na kuendelea kusimamia ili kuhakikisha kwamba wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanapata huduma mbalimbali za kijamii kwa uhakika.


Ndugu wananch wa Jiji la Dar es Salaam.

Hivi sasa tunaingia kwenye kipindi cha sikuu ya pasaka. Tunapoungana na wenzetu Wakristo katika kusherehekea Sikukuu ya Pasaka, niwaombe wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendeleza kushirikiana na vyombo vyetu vya usalama katika suala zima la uimarisha wa usalama wenu.

Vyombo vya usalama vimekuwa rafiki kwa kipindi chote jambo ambalo limefanya kupungua kwa matukio ya kiuhalifu ndani ya jiji letu.

Hivyo basi nitoe rai kwa wakazi wote wa jiji la Dar es Salaam, kusherehekea siku kuu hii kwa Amani na utulivu bila kuwepo kwa vurugu zozote. Salamu zangu za upendo katika sikukuu hii ya Pasaka ziwe chachu ya kuendelea kutunza amani katika jiji letu, huku mki hakikisha kwamba kila eneo ambalo watoto wenu watashiriki kwa namna moja ama nyingine kuwe na usalama wa uhakika. Tusijenge utamaduni wakukubali matukio ya kuvunja amani kwenye siku kuu maana hizi ni sherehe sio vita.


Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam,

Mtakubaliana name kwamba, Siku kuu hii imekuja na neema ya mvua, ukizingatia ni jambo ambalo tulikuwa tukililia kwa muda mrefu sana ili kuondokana na hali ya ukame. Napenda kutumia fursa hii kuwataka wale wote ambao wapo maeneo ya hatarishi (mabondeni), kuanza kuchukua tahadhari mapema kabla ya kukumbwa na adha ya mafuriko.

Sote ni mashahidi kwamba, wakati wa mvua kama hizi kumekuwa na madhara makubwa ambayo hujitokeza kwa wale ambao huishi mabondeni. Hivyo kama jiji linampango mkakati wa kuboresha miundombinu ya maji ili kuepukana na adha hii ya mafuriko. lakini basi wakati jiji likiwa kwenye mkakati huo, tuchukue tahadhari mapema kabla ya kuleta maafa.


Ndugu wananchi wa jiji la Dar es Salaa.

Nimekuwa katika majukumu mbalimbali ya kitaifa kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wetu. Nitoe rai kwa wananchi kushirikiana na viongozi mliowachagua ili kuweza kuwasilisha kero zenu sehemu husika ili mamlaka ziweze kushughulikia kero hizo mapema.

Aidha Ofisi ya Meya wa jiji imekuwa rafiki kwa wananchi wote katika kuhakikisha kwamba tunakuwa na Jiji ambalo linajali mahitaji mbalimbali ya wananchi wake hususani wafanyabiashara wadogowadogo, Bodaboda, Mama lishe, na makundi mengine mbalimbali.


Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Halikadhalika pia, napenda kuvipongeza vyombo vyote vya habari kwa mchango mkubwa ambao mnaonyesha wa kuhabarisha Umma wa wa Tanzania mambo mbalimbali yanayofanywa na jiji. na kwamba mmekuwa ni chachu kubwa ya kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na jiji. Niseme tu kwamba jiji la Dar es Salaam, linatambua mchango wenu mkubwa na kuwaomba muendelee kufanya kazi zenu kwa weledi mzuri na kwamba tuko pamoja na nyie.

Ndugu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam.

Mwisho kabisa niwatakie maandalizi mema ya sikukuu ya Pasaka ,iwe na heri na fanaka kwa watu wote, na kwamba mapumziko haya ya siku tatu, muyatumie kwa kulijenga jiji lenu badala ya kulibomoa.



Mwisho kabisa napenda kuwatakia sikukuu njema

Mungu ibariki Tanzania , mungu libariki jiji la Dar es Salaam.

Imetolewa na Mstahiki Meya wa jiji

…………………….

Isaya Mwita Charles.

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KULIPOKEA TAMASHA LA "NYANZA FESTIVAL" KWA KISHINDO

$
0
0



Judith Ferdinand, BMGHabari


Wakazi wa Jiji la Mwanza na viunga vyake, wanatarajia kupata burudani ya kukata na mundu kutoka kwa wasanii mbalimbali Kanda ya Ziwa katika tamasha la burudani "Nyanza Festival 2017".

Burudani hiyo ambayo itakua ya aina yake kwa kuwakutanisha wasanii kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, itafanyika Siku Kuu ya Pasaka kuanzia saa nne asubuhi mpaka majogoo kwa kiingilio cha shilingi 5,000 tu katika Uwanja wa CCM Kirumba.

Mratibu wa tamasha hilo, Fabian Fanuel, amesema mbali na burudani ya mziki pia kutakua na mchezo wa mpira wa miguu kati ya Waandish wa habari za michezo Kanda ya Ziwa LASPOJA Fc na Bongo Movie, na Madjs na Watangazaji wa vipindi vya burudani watacheza na wafanyakazi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Naye Afisa Habari wa tamasha hilo, George Binagi, amebainisha kwamba wanatasnia wa burudani hususani wanamuziki mastaa na chipukizi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, wameahidi kudondosha burudani kali siku hiyo.

"Zaidi ya wasanii 30 kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa tayari wamethibitisha kupanda jukwaa la Nyanza Festival 2017 hivyo niwasihi wapenzi wa burudani wakae tayari kwa burudani hiyo ambapo kiingilio itakuwa elfu tano tu". Amesema Binagi.

Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.

BALOZI WA KUWAIT AZINDUA KISIMA CHA 27 KATIKA SHULE YA MSINGI MAJANI YA CHAI JIJINI DAR

$
0
0

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem amezindua kisima cha 27 katika shule ya msingi Majani ya Chai iliyopo Vingunguti ikiwa ni ka

Katika tamati ya awamu ya kwanza ya mpango wa Ubalozi wa Kuwait wa kuchimba Kisima kwa kila shule mpaka sasa kumezinduliwa visima vya maji 27 katika shule 27 mbalimbali katika kipindi cha miezi mitatu tu jijini Dar es salam.

Mpango huo wa Ubalozi wa Kuwait umeweza kufanikiwa ambapo visima 16 kati ya hivyo vilichimbwa na Jumuiya ya mwezi mwandamo ya Kuwait (Kuwait Red Crescent Society ).

Visima vingine vilichimbwa na wasamaria wema wa Kuwait kwa kushirikiana na asasi nyingine za nchin Tanzania na Kuwait.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Jasem Al-Najem akizindua kisima katika Shule ya Msingi Majani ya Chai iliyopo ya Vingunguti akiwa pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo na walimu ikiwa ni mpango wa kwanza wa ubalozi wa nchi hiyo kuchimba kisima katika Shule za Msingi Jijini Dar es salaam
Viewing all 46371 articles
Browse latest View live




Latest Images