Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1187 | 1188 | (Page 1189) | 1190 | 1191 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ziara ya siku mbili ya kitaifa ya Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Dessalegn nchini. Waziri Mkuu huyo atawasili nchini tarehe kesho 31 Machi, 2017 asubuhi na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Akiwa nchini atakutana kwa mazungumzo na Mhe. Rais Magufuli pamoja na kutembelea Bandarini. Wengine katika picha ni Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Balozi Naimi Aziz (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Innocent Shiyo (kulia). 
  Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Aziz naye akielezea jambo wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari 
  Waziri Mkuu wa Shirikisho la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia, Mheshimiwa Hailemariam Dessalegn anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini tarehe 31 Machi hadi tarehe 1 Aprili 2017 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. 

  Ziara ya Mhe. Dessalegn inakuja kufuatia mkutano kati yake na Mhe. Dkt. Magufuli uliofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Kawaida wa 28 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia mapema mwaka huu.

  Mhe. Dessalegn anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 31 Machi, 2017 asubuhi na atapokelewa na Mhe. Rais Magufuli. 

  Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

  Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo ya faragha yatakayofuatiwa na mazungumzo rasmi yatakayowahusisha wajumbe wa pande mbili. Aidha, Viongozi hao watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari.

  Jioni ya siku hiyo, Mhe. Dessalegn na ujumbe wake watashiriki Dhifa ya Kitaifa ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima yake na Mhe. Rais Magufuli.

  Tarehe 01 Aprili, 2017 Mhe. Dessalegn ataendelea na ziara yake kwa kutembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kujionea shughuli mbalimbali Bandarini hapo. Mhe. Dessalegn na ujumbe wake wataondoka siku hiyohiyo kurejea Ethiopia.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
  30 Machi, 2017

  0 0

  Picha ya pamoja ya mawaziri wa jumuiya ya umoja wa Afrika Mashariki Mara baada ya ufunguzi wa Kongamano LA kupanga jinsi ya kukabiliana na majanga.Kongamano hilo lilizinduliwa na Rais Pierre Nkurunzinza Mganga Mkuu wa Serikali toka Tanzania (wa kwanza kushoto) Prof.Bakari Kambi akichangia mada katika mkutano huo uliokutanisha wadau wa afya kutoka Afrika mashariki. Baadhi ya wajumbe toka Kenya wakifuatilia mada zilizowasilisha kwenye mkutano huo.

  …………….

  Bujumbura,Burundi

  Nchi wanachama wa Umoja wa Afika mashariki pamoja na sektarieti ya umoja huo(EAC) wamehimizwa kuharakisha mchakato wa kuhakikisha kada zingine za afya ikiwemo ya uuguzi na kada nyingine zenye sifa na viwango vinavyofanana na madaktari kuajiriwa kwenye nchi yeyote ya Afrika Mashariki

  Hayo yamesemwa jana na Waziri WA Afya,Maedeleo ya Jamiii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kisekta la mawaziri wa Afya wa Afrika mashariki kwenye kikao cha 14 nchini hapa

  Waziri ummy alisema amefurahishwa sana na hatua iliyofikiwa na nchi wanachama wa Jumuiaya hiyo ambapo hivi sasas madaktari wanaotoka katika jumuiya hiyo kuajiriwa

  Katika hatua nyingine kikao hivho kimejadili kuhusu kuimarishwa kwa mafunzo na usimamizi wa pamoja wa waraalam wa afya,udhibiti wa magonjwa ya milipuko pamoja na magonjwa ya kuambukiza kama vile Ebola,Mafua makali ya ndege kifua kikuu(TB) na UKIMWI

  Kuhusu kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ,mawaziri wamekubaliana hao wamekubaliana kuongeza juhudi Zaidi ili kupunguza vifo vya wanawake wajawazito na watoto ndani ya Afrika Mashariki

  “Bado Afrika Mashariki hatufanyi vizuri katika afya ya uzazi na mtoto na hivyo kusababisha kutofikia malengo ya kidunia ya Millenia yaliyowekwa,hivyo tuongeze jitihada katika hili”,alisema Waziri Ummy.

  Aidha, Waziri Ummy ameelekeza Tume ya Utafiti wa masuala ya Afya ya EAC ihamie mapema makao makuu yake mjini hapa kama ilivyokubaliwa kwenye vikao vya baraza la mawaziri vilivyotangulia

  Wakati huo huo Waziri Ummy akiwa nchini humo ameshiriki uzinduzi wa kongamano la Kimataifa la afya ya Sayansi lililofunguliwa na Rais wa Burundi Mhe.Piere Nkurunzinza ambalo limeandaliwa na Kamisheni ya Utafiti wa Masuala ya Afya ya Jumuiya ya Afrika Mashariki

  Kongamano hilo la siku tatu lina lengo la kujadili na kujipanga katika kukabiliana na majanga ikiwemo ya magonjwa mapya yanayojitokeza(Emerging Diseases) na yale yanayojirudia (Re-emerging Diseases) na linawawashirikisha wataalam wa afya na watafiti kutoka nchi mbalimbali.

  0 0

  Pamoja na jitihada zinazofanyika kuhakikisha kuwa na vyumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri wanapokuwa katika hedhi lakini bado changamoto kubwa ni upatikanaji wa vitambaa wakati wa hedhi "pedi"kwa watoto wa kike hasa kwa watoto wasio na uwezo.

  Hayo yamebainika wakati wa ziara ya waandishi wilayani Kishapu walipotembelea shule mbalimbali kuangalia hali ya upatikanaji wa vyumba kwa ajili ya kujisitiri watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi na upatikanaji wa vitambaa ‘pad’ ili kuimarisha usafi wa mtoto wa kike anapokuwa shuleni.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti walimu wa wakuu wa shule za msingi na walimu walezi wa wanafunzi wa kike wilayani Kishapu walisema wamejitahidi kuwa na vyumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kujistiri wanapokuwa kwenye hedhi lakini changamoto ni upatikanaji wa pad kwani watoto wengi hawana uwezo wa kununua pedi.

  Walisema shule nyingi hazina uwezo wa kifedha kuweza kununua pedi na kuzigawa bure kwa wanafunzi hivyo kuwaomba wadau mbalimbali wa watoto kujitokeza kusaidia watoto wa kike kwani wazazi wengi wamekuwa wakidai hawana uwezo wa kununua vitambaa hivyo.

  Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyenze iliyopo katika kata ya Mwadui Lohumbo,Yohana Saraton alisema changamoto waliyonayo sasa ni upatikanaji wa vitambaa ‘pad’ kwa ajili ya watoto wakiwa katika hedhi.

  “Sisi tuna chumba maalum kwa ajili ya watoto wa kike kujisitiri lakini pad hazipo tunaomba mashirika na wadau mbalimbali wajitokeze kufadhili ugawaji wa pad katika shule hiyo”,alisema Saraton.

  Naye Mwalimu Mlezi wa wanafunzi wa kike katika shule hiyo Leanita Kalinjuna alisema ukosefu wa pad unawafanya baadhi ya wanafunzi wa kike kutohudhuria masomo wanapokuwa katika siku zao ‘hedhi’.

  “Kutokana na kukosekana kwa vitambaa hivyo wanafunzi huwa wanatoa taarifa kama wapo hedhi na huwa tunawapa ruhusa,tunaomba kupatiwa vifaa hivyo maana sisi tuna chumba maalum na tuna vifaa vya kuhifadhia pad zilizotumika”,aliongeza mwalimu Kalinjuna.

  Kwa upande wake Ofisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi alisema ni kweli kuna tatizo la upatikanaji wa vitambaa hivyo kwani bajeti inayotolewa na serikali haijitoshelezi kuhudumia wanafunzi wote wa kike katika shule kwa kuwanunulia pedi.

  “Asilimia 10 ya fedha za huduma ya kwanza katika shule haitoshi kuhudumia wanafunzi wote kwani shule zetu zina wanafunzi wengi lakini tunaendelea kuangalia namna ya watoto hawa ili waweze kuhudhuria masomo yao ikiwemo kuwahamasisha walimu walezi wa wanafunzi hao kuwa karibu na watoto wa kike”,aliongeza Kahundi.

  “Kuweka chumba maalum katika shule ni sera mpya tuliyoianzisha kupitia mradi wa “School Wash” ambao unatekelezwa kila halmashauri ya wilaya zote japokuwa siyo katika shule zote,pale tunajenga vyoo vipya tumeamua tuwe tunatenga chumba kwa ajili ya watoto wa kike ili kupunguza utoto shuleni”,alieleza Kahundi.

  Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba alishauri vifaa kwa ajili ya watoto wa kike visamehewe kodi vinapoingizwa nchini kwa sababu vina gharama kubwa ukilinganisha kuwa watoto hao hawana ajira.

  “Ukisema kwamba shule zitumie pesa za vifaa zinunue haviwezi,kila mtu aangalie kuwa ni jukumu lake kuwahudumia watoto wa kike ,jamii kama jamii ituone sisi wanawake kuwa tuna mahitaji mengine ambayo yanahitaji yaonwe kwa jicho la ziada”,aliongeza Talaba.
  Vyoo vya wanafunzi (kushoto) na cha walimu (kulia) katika shule ya msingi Nyenze iliyopo katika kata ya Mwadui Lohumbo wilayani Kishapu
  Choo cha wanafunzi katika shule ya msingi Nyenze ambacho kina chumba kimoja maalum kwa ajili ya wanafunzi wa kike kinachotumiwa na wanafunzi hao wanapokuwa katika hedhi
  Chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike/wanafunzi wa kike wanaosoma katika shule ya msingi Nyenze.Pamoja na kuwepo kwa chumba hicho lakini hakuna kifaa chochote kwa ajili ya watoto wa kike wanapokuwa katika hedhi

  Chumba maalumu kwa ajili ya wanafunzi wa kike kikiwa hakina pedi yoyote.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0


  Mwili wa Marehemu utawasili nchini kutokea Leeds, Uingereza siku ya Ijumaa tarehe 31/03/2017 majira ya saa nne usiku.

  Taratibu zote za mazishi zitafanyika tarehe 01/04/2017 Mbezi Beach, Tangi bovu jijini Dar es salaam mtaa wa Almasi nyumba namba 7, Kuanzia saa tatu asubuhi.


  Ibada ya kuaga mwili wa marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Gasper, Mbezi Beach, Tangi bovu jijini Dar es salaam.


  Mazishi yamepangwa kufanyika Jumamosi 01/04/2017 katika Makaburi ya Kondo, Bahari Beach jijini Dar es salaam. 

  0 0  Finance and Planning Minister Dr Philip Mpango (right) chats with the BancABC Board Chairman Dr Jonas Kipokola (centre), the banks Managing Director Dana Botha (left) and the banks Head of Retail Banking Joyce Malai after launching of the BancABC Tegeta branch in Dar es Salaam on Wednesday.
  Finance and Planning Minister Dr Philip Mpango chats with BancABC staff after launching of the banks Tegeta branch in Dar es Salaam on Wednesday.


  BancABC has opened up a new branch in Tegeta, Dar es Salaam in order to cater for the growing customers demand for financial and banking services necessary in speeding up the economy. Tegeta branch is the fifth branch of BancABC in the country.

  Speaking during the official inauguration of the branch, the Minister of Finance and Planning Dr Philip Mpango said it was a good move for the bank to extend its services near the customers in the outskirts of Dar – es- salaam instead of concentrating in the city centre where all banks have branches.
   ‘I take this opportunity to congratulate the management of the bank for coming up with this good idea of opening a branch in Tegeta. It is good to note that areas like these is where you find a large number of Tanzanians who don’t use financial services like banks and therefore this branch will help penetrated into the unbanked population in this area’.

  Commenting on the services offered by the bank, Dr Mpango expressed his satisfaction that the bank services over 60,000 government employees by offering loans and investing opportunities. ‘The way that you have been serving government employees, do the same to the private sector, let them have a trust in your services and they will be good customers.’ Said Mpango.

  Dr Mpango called Tanzanians to develop a culture of savings as it’s by saving that one can reach their goals. Savings has a lot of advantages not only achieving your goals but also a bank can have trust, when it comes to offering loans, said the Minister. Dr Mpango also urged BancABC and other banks in the country to consider reducing lending rates among their customers as they are many Tanzanians who are willingly to borrow but higher rates discourage them from doing so. Mpango further insisted that is good for Tanzanians to develop a trust of paying their debts each time they borrow’.

  Speaking at the same occasion, BancABC Tanzania Managing Director Dana Botha said that launching of branch is a key milestone in bringing closer the banks products and services to the people of Tegeta. ‘This is a key milestone to BancABC as we align our vision to the premier financial service institution in Sub- Saharan Africa and obtain top five market position in countries we operate, said Botha.

  The Managing Director urged Tegeta residents to come up and make use of the services offered by the bank. ‘We have always been working hard to achieve better results. BancABC which is part of Atlas Mara has been named in the 2017 Banker Africa, Southern Africa Awards as the Best Emerging Bank – Southern Africa. The results are based on nominations and votes from the Bankers’ subscribers. It has been our objective for the bank to have brag awards whilst we fix our value propositions for excellence, said Botha.

  The Managing Director said that BankABC is planning to open other two branches in Dodoma and Mwanza before the end of this year.

  0 0

   Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akimpa pole   Mama janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya  Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. 
  C 1
  Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akishiriki katika sala na Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George  Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ na ndugu, marafiki na jamaa wa familia ya marehemu aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
  C 2
   Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiweka saini kitabu cha maombolezo baada ya kumfariji  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe na Waziri wa Kwanza wa  Ushirika na Masoko katika Baraza la Mawaziri chini ya Serikali ya  Madaraka na baadaye Waziri wa Kwanza wa Mambo ya Ndani baada ya Uhuru, Marehemu Clement George Kahama maarufu kama  `Sir George Kahama’  aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam. Wengine katika picha kutoka kulia ni Mama Janeth Kahama, Mama Evelyn Warioba, Anna Kahama-Rupia, Mama Rahma Bomani,Mama Getrude Luangisa, Mama Ishengoma, Mama Feruzi na Mama Tunu Mwapachu.
  C 3
  Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli akiagana baada ya kumpa pole  Mama Janeth Kahama, Mjane wa mwanasiasa  mkongwe Marehemu Clement George Kahama maarufu kama `Sir George Kahama’ aliyefariki dunia hivi karibuni jijini Dar es salaam.
   
  PICHA NA IKULU

  0 0

  Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki  Benki Kuu ya Tanzania
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  IDADI ndogo ya Watanzania wanaotumia huduma za kibenki kunachangia pakubwa kuchakaa haraka kwa fedha.

  Hayo yamesemwa na Meneja Msaidizi wa Benki Kuu, (BoT) , kutoka Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Bw.Abdul M.Dollah, wakati akijibu maswali ya Washiriki wa Warsha ya Waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, inayoendelea kwenye ukumbi wa BoT tawi la Zanzibar, leo Machi 30, 2017 waliotaka kujua ni kwa nini fedha za noi zinachakaa haraka hususan shilingi 500 na shilingi 1,000/_

  “Ubora wa karatasi zinazotumika kutengenezea noti zetu unalingana, lakini matumizi makubwa ya noti hizo zilizotajwa, zinapita kwenye mikono ya idadi kubwa ya watu na hivyo kupelekea kuchoka haraka.” Alifafanua
  Akifafanua zaidi alisema, Idadi ya Watanzania kwa sense iliyofanyika mwaka 2012 ni Milioni 48, lakini kati ya hao ni Watanzania Milioni 4 tu ndio wanatumia huduma za kibenki, (kuwa na akaunti benki), na idadi ya waliosalia, hutunza wenyewe fedha hizo.

  Utunzaji mbaya wa fedha na hali ya hewa ya baadhi ya maeneo nchini, huchangia kuchakaa haraka kwa fedha “ Kwa mfano, kule Tanga maeneo ya Lushoto na Kibondo mkoani Kigoma, kutokana na rangi ya udongo wa sehemu hizo, utakuta fedha inachakaa haraka sana, alisema Bw.Dollah.
  Akielezea majukumu ya Kurugenzi ya Huduma za Kibenki ya Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bw. Dollah alisema, Sheria namba Nne (4) ya BoT, imeipa kurugenzi hii jukumu la kusanifu, kutoa, kusambaza na kuharibu fedha,(noti na sarafu), zilizochakaa.

  Pia Kurugenzi hii ina jukumu la kutoa huduma za kibenki kwa serikali zote mbili, (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi Zanzibar).
  Alisema jukumu lingine kubwa la Kurugenzi hiyo ni kuhakikisha uwepo wa noti na sarafu kwa uwiano wa kutosha kwenye uchumi, “hatuwezi kuingiza fedha nyingi kwenye uchumi bila ya kuangalia uwiano wa uzalishaji na kiwango cha fedha”.aliongeza.

  Akizungumzia kushuka na kupanda kwa thamani ya fedha ya Tanzania, (TZS), Mchumi Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, alisema, miongoni mwa sababu zinazopelekea hali hiyo ni uhitaji wa fedha yetu, (TZS), katika soko(mzunguko).

  “Ili fedha yetu (TZS), iwe na thamani lazima uhitaji wake uwe mkubwa katika soko, na ikitokea kwamba fedha yetu inahitajika kwa wingi basi fedha yetu itapanda thamani na hii itatokana na kuongeza uzalishaji na kuuza bidhaa zetu nje, lakini endapo uzalishaji utapungua, na Nchi ikaingiza kwa wingi bidhaa kutoka nje, itapelekea uhitaji wa Shilingi kupungua na hivyo thamani yake pia itapungua.” Alisema Lusajo. Na kushauri taifa kama taifa liongeze thamani ya bidhaa ili ziweze kuuzwa nje na hivyo kuongeza uhitaji wa fedha yetu.

  Aidha, BoT, imesema, utafiti mdogo iliyofanya umeonyesha kuwa wateja wengi katika benki za biashara, wanapokwenda kuchukua fedha, hupokea fedha (noti), za thamani ya juu yaani 10,000, na 5,000 licha ya kuwa wengine wangependa kupewa fedha ndogo ndogo kwa ajili ya urahisi wa kupata chenji.

   “Ni haki ya mteja wa benki za biashara anapokwenda kuchukua fedha benki, kudai apewe fedha za chenji (fedha ndogo ndogo, yaani 500/- 1,000,000/ na 2,000/=, ili kumrahisishia anapokwenda kufanya manunuzi asipate shida ya chenji.” Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, Bi Vicky Msina alibainisha.
  Washiriki wa semina, wakiangalia noti ya Sh. 10,000, ili kutambua kama ni halali au so halali.
  Maafisa wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, (kulia), na Bw. Mohammed na Mohammed Kailwa, wakijadiliana jambo kwenye komppyuta
  Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi.Vicky Msina, (kulia), akizungumzia kuhusu haki ya mteja wa benki ya biashara kupewa Fedha ndogondogo kama atahitaji. Kushoto ni Bw. Abdul M. Dollah. 
  Bw. Abdul M. Dollah, akitoa mada juu ya Huduma za Kibenki
  Bi. Flora Nkondola kutoka EFM, akitazama uhalali wa noti ya Shilingi elfu 10,000/=

  Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada iliyokuwa ikitolewa
  Baadhi ya maafisa kutoka BoT
  Mtangazaji wa Channel Ten, Bi. Dorcas R. Mtenga, akizungumza

  Bw. Dollah akitoa mada

  Mchumi Mwandamizi wa BoT, kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, wa BoT, Bw. Lusajo Mwankemwa, akitoa ufafanuazi kuhusu kwa nini thamani ya shilingi ya Tanzania inapanda na kushuka
  Bw. Dollah(kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano Mkuu, Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki, BoT, Bw. Lwaga Mwambande
  Maafisa wa BoT

  0 0

  Mratibu wa Mafunzo kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Bi. Eliet Magogo akiwasilisha mada katika warsha ya kuhamasisha raia kujiunga katika jeshi la ulinzi wa amani la jumuiya hiyo iliyofanyika leo katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Watumishi kutoka katika Wizara, Idara na Taasisi za Serikali. Katikati ni Mkuu wa Kitengo kinachoshughulikia raia katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, Bw. Ernest Kantchentche na kushoto ni Bi. Caroline Chipeta, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

  Sehemu ya Maafisa waliohudhuria warsha hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kutoka kulia ni Bi. Felista Rugambwa, Bw. Deogratius Dotto na Bw. Abdallah Mrisho.

  Sehemu nyingine ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.

  Warsha ikiendelea
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Na Mathias Canal, Dodoma

  Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe Hailemariam Desalegn anataraji kuwasili nchini kesho Machi 31, 2017 katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa ziara ya Siku tatu kwa kuitikia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye ndiye atakuwa mwenyeji wake.

  Taarifa ya ujio wa waziri Huyo Mkuu wa Ethiopia imetolewa hii Leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio huo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.

  Rc Makonda ameeleza kuwa Mhe Desalegn anataraji kuwasili nchini saa tatu kamili asubuhi Machi 31, 2017 hadi April 1, 2017 ambapo atakuwa nchini kwa shughuli mbalimbali za kidiplomasia zinazogusa nyanja muhimu za kiuchumi, Biashara, na Ushirikiano baina ya Nchi ya Ethiopia na Tanzania.

  Mhe Makonda alisema kuwa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia pamoja na shughuli hizo za kidiplomasia pia atasaini mikataba mitatu, Kutembelea bandari na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli.

  Makonda alisema kuwa Tanzania itapata fursa ya kujifunza mambo mengi kupitia kwa ugeni huo juu ya kukabili changamoto mbalimbali zinazolikabili bara la Afrika katika masuala ya kilimo cha kisasa katika maeneo yenye uoto wa asili wenye changamoto kama milima hapa nchini Tanzania.

  "Tutajifunza mengi sana kama ilivyo kwa Ethiopia ambao mbali ya kukabiliwa na uoto usio rafiki wa milima na miinuko mikali kwa asilimia kubwa bado wameweza kutumia vyema maeneo machache ya tambarare na Kuwekeza kufanya kilimo cha kisasa na kuzalisha chakula kwa wingi, hivyo tutapata ufahamu pia katika mambo haya muhimu" Alisema Mhe Makonda

  Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda amesema kuwa uongozi wa Mkoa wake unamkaribisha nchini Tanzania kwani ujio wake utaibua zaidi fursa za kukuza uchumi na Maendeleo.

  Hata hivyo amesema kuwa Ethiopia imepiga hatua kubwa kwenye usafiri wa Anga Duniani hivyo kupitia rekodi hiyo nzuri Tanzania pia itapata wasaa wakujifunza mambo mengi katika sekta hiyo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.(Picha Zote Na Mathias Canal)
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akisikiliza na kujibu maswali ya waandishi wa habari mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
  Baadhi ya Wakurugenzi wa Manispaa za Jiji La Dar es salaam wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na Waandishi wa habari
  Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akielezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia
  Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul C. Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuelezea dhamira ya ujio wa Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini Tanzania mapema leo katika Ukumbi wa Benjamin Mkapa Mjini Dodoma.

  0 0

  Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii pamoja na Waziri, Naibu Waziri na watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi zilizo chini yaWizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakijadili Bajeti ya Wizara hiyo Mjini Dodoma.
  Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Mussa Azzan Zungu akizungumza katika kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
    
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akieleza juu ya mikakati ya Wizara katika kushirikisha Sekta binafsi katika kuleta maendeleo katika Sekta za Wizara wakati wa kikao cha kuijadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.
   
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii wakifuatilia hoja mbalimbali wakati wa kikao cha kujadili Bajeti ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mjini Dodoma.


  Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  0 0

  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Kim Doanh. Tukio hilo limefanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017

  Dkt. Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Vietnam, Mhe. Nguyen Kim Doanh mara baada ya kupokea nakala zake za hati za utambulisho

  Balozi Mteule Mhe. Nguyen Kim Doanh naye akizungumza.

  Dkt. Kolimba na Balozi Mteule Mhe. Nguyen Kim Doanh wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Magabilo Murobi na Afisa kutoka Ubalozi wa Vietnam nchini
  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini, Mhe. Dina Mufti Sid.Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 30 Machi, 2017.

  Dkt. Kolimba akizungumza na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini, Mhe. Dina Mufti Sid.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa(kulia).
  Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Peter Kisenge akifafanua jambombele ya waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 Machi katika Taasisi hiyo ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Katikati ni Mwakilishi Mkazi wa Madhebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upandikizaji wa Mishipa kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai, India Dkt. Yunus Loya.
  Daktari Bingwa wa kupandikiza mishipa ya damu kwenye moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Yunus Loya akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kutoka kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini, Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa (kulia).
  Daktari wa anayeshughulikia maumivu na usingisi wakati wa upasuaji kutoka India Dkt. Shilpa Bhojraj akielezea jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Dkt. Bashir Nyangasa.
  Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa moyo kuzibua njia mbili, Athumani Waziri akielezea namna alivyofarijika baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktari hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu aina ya upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba ( CABG-Coronary Artery Bypass Graft) aliyofanyiwa mgonjwa Vinod Bhaggan (katikati) wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016. Kushoto ni Mwakilishi Sheikh Tayabali Hamzabhai na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala.
  Mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kuipandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) Vinod Bhaggan akielezea namna alivyofarijika baada ya kupata matibabu hayo wakati wa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo iliyofanyika kuanzia tarehe 26 hadi 29 mezi Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Sheikh Tayabali Hamzabhai.
  Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo wa JKCI Dkt. Bashir Nyangasa na Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI Dkt. Peter Kisenge (katikati) mara baada ya kumaliza kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari wa JKCI walishirikiana na Madaktari 6 kutoka nchini India. Madaktaria hao wamekuja nchini kufuatia ahadi ya Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Mabohora Duniani Mtakatifu Syedana Muffadal Saifuddin Saheb kwa Rais Dkt. Magufuli alipomtembelea Ikulu Jijini Dar es Salaam mapema tarehe 13, Oktoba 2016.
  Afisa Uhusiano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Anna Nkinda akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Madhehebu ya Mabohora nchini Tanzania Sheikh Tayabali Hamzabhai (wapili kushoto) mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa kambi ya siku tatu ya upasuaji wa Moyo katika Taasisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kutoka Hospitali ya Saifee, ya Mumbai nchini India Dkt. Aliasgar Behranwala(kulia) na Dkt. Hussein Hassanali wa JKCI.

  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  ……………………………………………………………..

  Frank Mvungi-Maelezo

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amepongezwa kwa kuiwezeshaTaasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kufanya upasuaji wa kihistoria tangu kuanzishwa kwake.

  Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangassa wakati wa hafla fupi ya kuwaaga madaktari bingwa wa moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya Mumbai nchini India waliosaidia kufanikisha upasuaji huo wa kuvuna mishipa ya damu mguuni na kupandikiza katika mishipa ya moyo iliyoziba (CABG-Coronary Artery Bypass Graft) kwenye moyo .

  Upasuaji huu uliwahusisha madaktari 6 toka Hospitali ya Saifee umesaidia kuwaongezea ujuzi wataalamu wa Taasisi hiyo na kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kuwasafirisha nje wagonjwa ili waweze kupata matibabu.

  “Kama wagonjwa hawa wangeenda kutibiwa nchini India Serikali ingelipia zaidi ya shilingi bilioni 2.1 kama gharama za matibabu” Alisisitiza Dkt. Nyangassa. “

  Akizungumzia upasuaji mwingine uliofanyika kwa wagonjwa 8 Dkt. Nyangassa amesema kuwa ni upasuaji wa milango miwili hadi mitatu ya moyo ambayo ilikuwa na matatizo kwa kuibadilisha.

  Kwa upande wa upasuaji wa bila kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa Cath Lab tumetoa huduma mbalimbali za matibabu ya moyo bila kufungua kifua (catheterization) kwa wagonjwa 12 ambao tumezibua mishipa ya damu ambapo mgonjwa mmoja mshipa wake ulikuwa umeziba kwa asilimia 100” Aliongeza Dkt. Nyangasa.

  Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kutoka Hospitali ya Saifee ya nchini India Dkt. Yunus Loya amesema kuwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete umeonyesha mafanikio makubwa na utakuwa wa kudumu.

  Aliongeza kuwa Taasisi ya Moyo ya Kikwete ina wataalamu wazuri na siku za usoni watakaobobea zaidi na hivyo Tanzania itanufaika sana na uwepo wa Taasisi hiyo.

  Tangu kuanza kwa mwaka huu Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wake wa nje ya nchi imefanya upasuaji bila kufungua na kufungua kifua kwa wagonjwa 79.

  Mwaka 2016 Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohara Duniani Mtakatifu Dkt. Syedna Aliqadr Mufaddal Saifuddin alifanya ziara yake hapa nchini na katika ziara hiyo kiongozi huyo alikutana na kufanya mazungumzo na Rais Dkt. John Magufuli na kumuahidi kuleta madaktari wa moyo. nchini watakaoshirikiana na Madaktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete na kufanya matibabu kwa wagonjwa.

  0 0

  SERIKALI imepanga kuondoka katika uchumi wa chini na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025 ambapo katika kufikia azma hiyo imeweka juhudi kwenye uanzishwaji wa viwanda mbalimbali kuanzia vidogo hadi vikubwa.

  Mpango wa kufikia uchumi wa kati unalenga kuiwezesha serikali kujitegemea na tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa ili kuweza kufikia azma hiyo.

  Dira ya Taifa ya Maendeleo, imeainisha malengo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujenge uchumi imara wenye uwezo wa kukabiliana na ushindani.

  Katika kuhakikisha mkakati huo unafanikiwa Serikali imeweka sera na mazingira mazuri kwa ajili ya kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuwekeza kwenye viwanda.

  Hivi karibuni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikwenda nchini Mauritius kumwakilisha Rais Dk. John Magufuli kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Uchumi Barani Afrika (AEP).

  Baada ya kumaliza uzinduzi huo Waziri Mkuu alipata fursa ya kutembelea viwanda mbalimbali nchini Mauritius na kuhamasisha wawekezaji waje nchini ili kuongeza uzalishaji utakaokuza uchumi na kuongeza pato la taifa.  KIWANDA CHA SUKARI CHA ALTEO


  Akiwa kiwandani hapo Waziri Mkuu alipata maelezo ya uendeshaji wake kuanzia hatua ya utayarishaji wa mashamba ya miwa hadi uzalishaji wa sukari.

  Waziri Mkuu alifurahishwa na teknolojia ya kisasa inayotumika kiwandani hapo hali iliyomfanya ashawishike kuwashawishi wawekezaji hao kuja nchini kupanua uwekezaji kwa kuongeza mashamba ya miwa na uzalishaji wa sukari.

  Kiwanda cha sukari kinachomilikiwa na kampuni ya Alteo kina uwezo wa kukamua tani 400 za miwa kwa saa na kuzalisha tani 170,000 za sukari kwa mwaka.

  Kampuni ya Alteo inamiliki kiwanda cha sukari cha TPC mkoani Kilimanjaro kwa ubia na Serikali ya Tanzania na kinazalisha tani 110,000 kwa mwaka.

  Aidha, Waziri Mkuu amefanya mazungumzo na uongozi wa kiwanda hicho na kuwashawishi waongeze maeneo ya uwekezaji nchini.

  “Tekonolojia wanayoitumia katika uendeshaji wa kiwanda chao ni nzuri hivyo tumewashawishi waje kuongeza maeneo ya uzalishaji wa sukari nchini ili tuweze kukidhi mahitaji,” amesema.

  Waziri Mkuu amesema Tanzania kuna viwanda vitano vya sukari ambavyo ni Mtibwa, Mahonda (Zanzibar), TPC, Kilombero na Kagera ambavyo uzalisha tani 320,000 kwa mwaka wakati mahitaji ya ndani ya nchi kwa mwaka ni tani 420,000.

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohammed amesema Zanzibar kuna kiwanda kimoja cha sukari ambacho uzalishaji wake haukidhi mahitaji kutokana na uhaba wa malighafi.

  Dk. Khalid amewakaribisha kampuni ya Alteo kwenda Zanzibar kushirikiana na Serikali katika uwekezaji hususani kwenye viwanda vya sukari.

  Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Patrick de Labauve amesema wamekubali kuongeza maeneo ya uwekezaji wa mashamba ya miwa nchini.

  Pia ameomba Serikali iwapatie fursa ya uwekezaji katika sekta ya utalii mkoani Kilimanjaro kwani kuna vivutio vingi vya utalii ukiwemo mlima Kilimanjaro.

  Akizungumzia kuhusu ajira amesema kiwanda cha TPC kimeajiri wafanyakazi 3,000 wakiwemo 1,900 wa kudumu wa ndani utakaotosheleza mahitaji na kupata ziada.

  Kusimamia mfumo mzima wa usambazaji wa sukari nchini ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wafanyabishara wenye tabia ya kuhodhi soko la sukari kwa lengo la kusababisha upungufu usio halisi wa sukari (artificial shortage).

  Kuendelea kuhamasisha na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wazalishaji wa sukari wa ndani ya nchi.  KIWANDA CHA SAMAKI

  Waziri Mkuu pia alitembelea kiwanda cha kusindika samaki aina ya jodari na kuwakaribisha viongozi wa kiwanda hicho kuja nchini kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya samaki.

  Amesema Serikali imeweka sera nzuri za uwekezaji na pia ina maeneo mengi na mazuri kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda vya samaki, ambayo ni bahari, mito na maziwa ambayo aina mbalimbali za samaki.

  Waziri Mkuu amesema hayo wakati alipotembelea kiwanda cha samaki cha Mer des Mascareignes kilichoko jijini Port Louis nchini Mauritius.

  “Tanzania kuna fursa nyingi za uwekezaji hasa kutokana na mazingira yake. Mnaweza kuja kuwekeza kwenye viwanda vya usindikaji wa samaki tuna bahari, mito na maziwa yenye samaki wa aina mbalimbali,” alisema.

  Majaliwa alisema Serikali imedhamiria kuimarisha uchumi wake kupitia sekta ya viwanda ili kuongeza tija kwa Taifa na kwa wananchi kiujumla hivyo wanahitaji wawekezaji waliotayari kuja kuwekeza nchini.

  Kwa upande wake Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohammed alisema Tanzania inahitaji wawekezaji watakaowekeza kwenye uvuvi wa kina kirefu na ujenzi wa viwanda vya samaki.

  Dk. Khalid alisema lengo la uwekezaji huo ni kukuza uchumi wa Taifa pamoja kupanua soko la ajira na kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi wake.

  Naye Meneja Mkuu wa kiwanda hicho, Bw. Patrick Hill alisema wamefurahia mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia fursa na uwekezaji na kwamba wako tayari kushirikiana na Serikali.

  Alisema kampuni yao inajishughulisha na usindikaji wa samaki aina moja tu ya jodari na wananunua kutoka kwa makampuni makubwa ya uvuvi huku wateja wao wakubwa wakiwa ni bara la Ulaya.  KIWANDA CHA NGUO

  Akiwa kwenye kiwanda cha nguo cha Compagnie Mauricienne De Textile Ltee kinachotengeneza nguo kwa kutumia teknolojia ya kisasa nchini Mauritius chenye uwezo wa kutengeneza tani milioni 40 hadi 50 kwa mwaka.

  Waziri Mkuu aliwakaribisha wawekezaji hao kuja nchini kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi na nguo kwa kuwa kuna malighafi za kutosha kwa ajili ya uzalishaji huo.

  “Tumefarijika na uwekezaji wenu na tumejionea namna ambavyo mnavyoendesha kiwanda chenu kuanzia utengenezaji wa nyuzi hadi nguo, hivyo tunahitaji viwanda kama hivi nchini Tanzania kwa sababu sisi tunazalisha pamba nyingi na yenye ubora unaokubalika kimataifa,” alisema.

  Waziri Mkuu alisema madhumuni ya kuwakaribisha wawekezaji hao kuja Tanzania na kuwekeza katika viwanda vya kutengeneza nyuzi yanalenga kuboresha kilimo cha pamba na kuwawezesha wakulima kupata tija.

  “Tunalima pamba nzuri na hawa hawalimi wananunua kutoka nje ya nchi yao, hivyo wakija kuwekeza Tanzania itawarahisishia kupata malighafi ya uhakika na kwa urahisi ” alisema.

  Alisema viwanda hivyo vitasaidia maendeleo ya kilimo cha pamba kwa sababu vitatoa ajira kwa wananchi wengi hivyo kuwawezesha kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umasikini wa kipato.

  Mbali na kuwakaribisha wawekezaji hao, Waziri Mkuu alitoa wito kwa wananchi wenye uwezo kuhakikisha wanajenga viwanda vya nyuzi kwenye mikoa yote inayozalisha pamba ili waweze kuiongezea thamani kabla ya kuiuza.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha wa kiwanda hicho David Too Sai Voon alisema wamefurahishwa na mualiko wa kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia maeneo ya uwekezaji wa viwanda vya nyuzi na nguo.

  David alisema kiwanda chao kilianzishwa mwaka 1986 na kwa sasa kimeajiri wafanyakazi 18,000 ambapo mauzo yao kwa ni dola milioni 200. “Nguo tunazotengeza ni za kiwango cha kimataifa na tunauza katika maduka makubwa barani Ulaya,”


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  SLP 980, DODOMA
  ALHAMISI, MACHI 31, 2017.

  0 0

   Jumapili March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapera.

  Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.
  Tazama video hii chini.

  0 0

  Frank Mvungi-Maelezo

  Watanzania wametakiwa kujitolea kuchangaia Damu ili kuwasaidia wagonjwa wanaofanyiwa upasuaji wa moyo wanaohitaji kuongezewa damu wakati wa kupatiwa mat

  ibabu.

  Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Upasuaji wa Moyo na Daktari Bingwa wa Moyo Dkt. Bashir Nyangasa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

  “Tunatarajia kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa watoto itakayoanza tarehe 3/4/2017 hadi tarehe 7/4/2017 ambapo Taasisi yetu itashirikiana na Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Healinga Little ya London Uingereza.”Alisisitiza Dkt. Nyangasa

  Akifafanua Nyangasa amesema kuwa wagonjwa 12 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji katika kipindi hicho kwa ushirikiano na Madaktari hao kutoka Taasisi ya Healing Little ya London Uingereza.

  Kufuatia upasuaji huo Dkt. Nyangasa amewaomba wananchi kuendelea kuchangia damu ili kusaidia kuokoa maisha ya wale wanaohitaji kuongezewa damu.

  Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete imekuwa Moja ya Taasisi Bora katika ukanda wa Afrika mashariki na Kati katika kutoa matibabu moyo kwa wagonjwa kutoka hapa nchini na katika mataifa mbalimbali yanayoizunguka Tanzania.

  Upatikanaji wa damu yakutosha imekuwa moja ya changamoto zinazoikabili Sekta ya afya kutokana na mwitikio mdogo wa wananchi kujitolea damu ili kusaidia wale wenye uhitaji hivyo ni wajibu wa kila mtanzania kuunga mkono juhudi za Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete katika kuhamasisha wananchi kujitolea kuchangia damu.

  0 0

  *Amtaka Waziri wa Maji avunje mkataba ifikapo Mei 31
  *Ni mkandarasi aliyenyang’anywa pasipoti na Rais Magufuli

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haitavumilia wakandarasi wasio na uwezo na ambao wanapewa kazi lakini wanashindwa kuzimaliza katika muda uliopangwa.

  Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo, leo (Alhamisi, Machi 30, 2017) wakati akizungumza na watumishi wa Halmamshauri ya Chalinze na wale wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (CHALIWASA) katika ofisi zao, karibu na daraja la mto Wami, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani.

  Alikuwa ameenda kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo wa maji Chalinze na ujenzi wa mfumo wa kusafirisha na kusambaza majisafi pamoja na matenki ya kuhifadhia maji ambao umechukua muda mrefu lakini haujakamilika. Awamu ya kwanza ilianza mwaka Septemba mosi 2001 na kukamilika Desemba mosi 2003.

  Amemuagiza Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ahakikishe kuwa kazi ya ujenzi wa mradi huo inaimarika na kufikia asilimia 80 la sivyo, wakamilishe taratibu za kukatisha mkataba na kutafuta mkandarasi mwingine.

  Agizo la Waziri Mkuu linafuatia taarifa aliyopewa kwamba mkandarasi wa mradi huo, Overseas Infrastructure Alliance (OIA) Pvt Ltd ya India alipaswa kumaliza kazi hiyo Februari 22, mwaka huu lakini hadi sasa mradi huo umekamilika kwa asilimia 23 tu.

  “Nimeelezwa kwamba mmempatia nyongeza ya siku 100 ambayo inaisha tarehe 31 Mei 2017, kama kazi yake haitakuwa ya kuridhisha na kufikia walau asilimia 80, itabidi Mheshimiwa Waziri uendelee na taratibu zako za kukatisha mkataba, tuanze kutafuta mkandarasi mwingine,” amesema.

  “Hii kampuni niliikuta Lindi kwenye mradi mwingine wa maji kama huu. Nilitoa maagizo ya kuharakisha ujenzi ukamilike lakini hawakufanya hivyo hadi Mheshimiwa Rais alipoenda na kuagiza mkandarasi anyang’anywe pasi yake ya kusafiria mpaka atakapomalizia kazi.”

  “Kwa kifupi ni kwamba hii kampuni haina uwezo wa kufanya hizi kazi, na ndiyo maana hadi sasa wamekamilisha asilimia 23 tu ya mradi wakati walipaswa kuwa wamemaliza hivi sasa,” amesema Waziri Mkuu na kuongeza: “Mheshimiwa Waziri endelea na utaratibu wa kuwaondoa kisheria sababu hata tukiwaongezea muda bado hawatakamilisha kazi.”

  “Nimesikitika sana kukuta mkandarasi hajafikia malengo. Mtu akipewa kazi anapaswa awe na uwezo wa kifedha wa kuifanya ile kazi ili hata Serikali ikichelewesha malipo yake, yeye aendelee na kazi,” ameongeza Waziri Mkuu.

  Akizungumzia kuhusu ufanisi wa mradi huo, Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa CHALIWASA, Eng. Christer Mchomba, ahakikishe kuwa wanapeleka maji hadi majumbani mwa wateja na kuweka mita ili wananchi waweze kulipa bili zao badala kuishia kutoa huduma hiyo kwenye vioski (viula).

  “Kazi ya kupeleka maji majumbani ni yenu CHALIWASA na siyo ya Wizara. Pelekeni maji na mfunge mita ili watumiaji waweze kulipa bili zao. Pia toeni elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya hadhara, waelezeni mipango yenu na wapi mlipofikia. Kazi yenu siyo kutandika mabomba tu, bali kutekeleza majukumu mliyopewa kwa niaba ya Serikali,” amesema.

  Kuhusu mitambo inayotumika, Waziri Mkuu amesema mashine zilizopo ni za siku nyingi tangu 2003; hivyo amemuagiza Waziri Lwenge afuatilie upatikanaji wa mashine za kisasa kwani hilo suala ni kubwa na haliwezi kubebwa na CHALIWASA. “Bora mngeanza kuagiza mashine mpya hivi sasa, badala ya kusubiri zichakae kabisa, ndipo muanze kufikiria kuagiza.”

  Mapema, akitoa taarifa ya mradi huo, Eng. Mchomba alisema awamu ya tatu ya ujenzi wa mradi huo ilisainiwa Mei 18, 2015 kati ya DAWASA na OIA yenye ubia na kampuni ya Pratibha Industries kutoka India kwa gharama ya dola za Marekani milioni 41.36 ambazo zilikuwa ni fedha za mkopo nafuu kutoka benki ya Exim ya India.

  “Kazi zilizopangwa kufanyika ni upanuzi wa mtambo wa maji ili kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 500 hadi 900 kwa siku; ujenzi wa mfumo wa mabomba ya kusambaza maji wenye kilometa 1,022; ujenzi wa matenki makubwa 19 ya kuhifadhia maji; vituo tisa (9) vya kusukumia maji (booster stations) na vioski (viula) vya kuchotea maji 351.”

  Alisema hadi sasa mkandarasi huyo amekwishalipwa dola za Marekani milioni 15.81 sawa na asilimia 38 na anaendelea na ulazaji mabomba ambapo hadi sasa amekwishalaza mabomba yenye urefu wa km.141 sawa na asilimia 12.4.

  Alisema mradi huo umelenga kuvinufaisha vijiji 68 ambavyo 19 kati ya hivyo viko Kaskazini mwa mto Wami na 49 viko Kusini mwa mto huo.

  Akizungumzia utendaji kazi wa mkandarasi huyo, Eng. Mchomba alisema Serikali imechukua hatua za kimkataba dhidi yake kwa kumtoza gharama ya kuchelewa kumaliza mradi (liquidated damages) kuanzia Februari 23, 2017.

  “Pia mkandarasi amepewa notisi ya siku 100 ya kumtaka aongeze kasi ya kazi, vinginevyo tutasitisha mkataba ifikapo terehe 31 Mei, 2017 kulingana na kipengele namba 8.7 cha mkataba,” alisema.  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  ALHAMISI, MACHI 30, 2017.

  0 0


  Mkurugenzi wa Kiwanda cha zinga Dkt.Mary Mayige akiwaeleza wageni mipangilio ya Zinga Pharmaceuticals watakavyotumia utaalam wao kuzalisha dawa nyingi za binadamu zenye viwango vya kimataifa hapa nchini.

  Mwakilishi wa Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto,Siana Mapunjo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.
  Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mhe. Happyness William Seneda akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani
  Mbunge wa jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga leo mkoani Pwani.

  Mshauli Mkuu wa kiwanda cha dawa za binadamu Zinga kutoka Ujerumani Mhandisi Bernt Kleinmann akifafanua jambo.
  Wadau wa mradi katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi wa ujenzi wa kiwanda cha dawa ya binadamu cha Zinga Pharmaceuticals mkoani Pwani.Habari na picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
   
  SERIKALI imesema ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Zinga Pharmaceuticals katika kitongoji cha Zinga mkoa wa Pwani utasaidia sana katima kupunguza gharama za ununuaji wa dawa kutoka nje ya nchi.

  Pia imesema gharama ambazo hutumia kwa mwaka kwa ajili ya ununuaji wa dawa kwa mwaka ni dola za kimarekani milioni 100.

  Taarifa hiyo imetolewa na Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Siana Mapunjo kwa niaba ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa kiwanda cha dawa cha Zinga, uliofanyika Bagamoyo mkoani, Pwani leo.

  Mapunjo amesema kutokana na gharama ambayo serikali hutumia kunulia dawa kwa mwaka inakadiriwa kuwa hadi ifikapo mwaka 2021 kiasi cha dola za Kimarekani 350 zitatumika kwa ajili ya ununuzi huo.

  “ Hadi sasa nchini tuna viwanda vya dawa za binadamu 13 ambavyo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 na kuisababishia serikali kupoteza sh. milioni 100 kwa ajili ya ununuzi wa dawa,” alisema.

  Amesema kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals kitasaidia kupata dawa muhimu kwa wakati na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.

  Mkurugenzi wa Kiwanda hicho, Dkt. Mary Mayige alisema kiwanda hicho kitagharimu kiasi cha sh.bilioni 70 za Kitanzania na kutarajiwa kukamilika baada ya mwaka mmoja na nusu.

  “Uzalishaji wa dawa za binadamu nchini bado ni upatikanaji wake kwa hospitali binafsi na serikali umeshuka kwa kiwango mkubwa ukilinganisha na miaka iliyopita kwa hiyo kupitia kiwanda hiki tutafikia malengo,” amesema.

  Dk. Mayige alizitaja dawa zitakazotengenezwa kuwa ni dawa wa kufubaza makali ya virusi vya ukimwi, antibiotiki, dawa za maumivu, malaria, magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza, shinikizo la damu na kisukari.

  Naye Mwakilishi tokaWizara ya Viwanda na Uwekezaji, Elly Pallangyo, amesema uwekezaji huo umejizatiti kuweka mazingira mazuri kwa kutafsiri Tanzania ya viwanda kwa vitendo. “ Hatutaweza kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda kama watu wake hawatakuwa na afya nzuri,” alisema.

  Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, Dk. Shukuru Kawambwa alisema atahakikisha anashirikiana na wawekezaji hao ili serikali iweze kutekeleza mradi huo kwa wakati.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mhe. Happyness Seneda alisema mkoa wa Pwani una jumla ya Viwanda vikubwa na vidogo 264 kati ya hivyo 88 ni vikubwa na kati, na ameahidi kwamba mkoa wa Pwani utatoa ushirikiano utakaotakiwa ili kufanikisha mradi huo ni mingine yote.

  0 0  Na Bakari Madjeshi,Globu ya Jamii

  Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) imekutana na wadau wake kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (Common Market Protocol 2010)  tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.

  Wanachama wa Jumuiya hiyo walingia makubaliano ya pamoja ili kuongeza utengamano ambao ulilenga zaidi kuongeza uhuru wa watu kupita nchi za Afrika Mashariki, Kuongeza uhuru wa kusafirisha Mizigo na Biashara pamoja Uhuru wa Mitaji (Free Movement of Capital).

  Akizungumza na Waandishi wa Habari katika majadiliano hayo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri amesema kuwa wamekutana kufanya tathmini kujua changamoto pamoja na uboreshaji katika soko hilo.

  Amesema wamekutana kujadili  ili baadae kutoa maoni kwa Serikali pamoja na viongozi wa Jumuiya hiyo, pia ni jinsi gani Tanzania inaweza kunufaika zaidi na soko la pamoja.

  Katika soko hilo Tanzania inanufaika zaidi kupata Kodi,Wananchi kupata ajira kutokana na soko kubwa, familia kupata kipato pamoja na kukua kwa Teknolojia ya uzalishaji.
   
   Sehemu ya Wadau wa Taasisi ya Sekta Binafsi wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Sera wa TPSF, Gilead Teri.
   Mkurugenzi wa Sera – Taasisi ya Sekta Binafsi, Gilead Teri akizungumza na baadhi ya wadau wa Taasisi hiyo juu ya kujadili utekelezaji wa Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika  Mashariki (Common Market Protocol 2010)  tangu ilipoanzishwa upya mwaka 2010.

  0 0


  Na Faustine Ruta, Bukoba

  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo kwenye uwanja wa Kaitaba imeanza mchezo wake wa kwanza wa kirafiki kwa kichapo cha bao 3-0 na Timu ya Vijana
  maarufu kwa jina la Serengeti Boys. 


  Bao la kwanza lilifungwa dakika ya 20 na Muhsin Malima Makame bao la pili lilifungwa dakika ya 38 na Nickson Clement Kibabage huku bao la tatu likifungwa kwa mkwaju wa penati na kepteni  Kevin Nashon Naftal dakika ya 72 baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.
  Mchezo wa marudiano wa timu hizi utachezwa Jumamosi hapa hapa kwenye uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Jijini Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
  Kikosi cha Burundi chini ya Miaka 17 kilichoanza dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania. Picha  na habari/ Faustine Ruta.

  Kikosi cha Serengeti Boys kilichoanza leo kwenye mchezo wa kirafiki kwenye Uwanja wa Kaitaba
  Viongozi mbalimbali walikuwepo


  Mgeni rasmi akisalimiana na Wachezaji wa Serengeti Boys

  Mgeni Rasmi na viongozi wengine wakisalimiana na Viongozi na wachezaji wa akiba wa Burundi

  Nyimbo za mataifa yote mawili ziliimbwa kabla ya mechi kuanza

  Taswira kabla ya mtanange

  Viongozi wa Timu ya Serengeti Boys

  Serengeti Boys wakipasha kabla ya Mtanange

  Picha ya pamoja  Kipindi cha pili kilimalizika Serengeti Boys wakiwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Timu ya Burundi.
  Picha  na habari/ Faustine Ruta.Wanaangalia Mubashara  bila Kiingilio!!!

  Mchezaji wa Serengeti Boys Yohana Oscar Mkomola wa Serengeti akiendesha mpira kipindi cha pili
  Oscar Mkomola(katikati) wa Timu ya Serengeti akiwekwa kati
  Kim na Bakary Shime wakiteta huku mtanange ukionekana kuwa mtelezo kwao kipindi cha pili katika mchezo wa karafiki leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba. Kocha Bakar Shime ataiongoza tena Serengeti Boys siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa pili.


  Kipa hakuona kitu!

  Nahodha wa Serengeti Boys  Kevin Nashon Naftali dakika ya 72 ndiye aliyewafungia bao hilo baada ya beki wa Burundi kujichanganya kwa kuunawa mpira ndani ya boksi.

  Mchezaji wa Serengeti Boys (kushoto) akipeta kwa bao lao la tatu

  Bao tatu 3-0

  Serengeti wakifurahia moja ya bao la mkwaju wa penati


  Shangwe! 3-0

  Chupuchupu afunge bao lingine!

  Assad Ally Juma wa Serengeti Boys(kushoto) akiufukuzia mpira

  Clement Kibabane akimiliki mpira kipindi cha pili mwishoni

  Kibabane tena na mpira

  Mchezaji wa Serengeti Boys (kulia) Ibrahim Abdallah Ally akimnyatia mchezaji wa Burundi

  Burundi wakiwa hoi baada ya kuzidiwa ujanja

  Dakika 90 zilikamilika

  0 0older | 1 | .... | 1187 | 1188 | (Page 1189) | 1190 | 1191 | .... | 1904 | newer