Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1186 | 1187 | (Page 1188) | 1189 | 1190 | .... | 1897 | newer

  0 0

            Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
  Wanawake na vijana wanaopewa mikopo na Serikali kupitia Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro wamekumbushwa kupeleka marejesho kwa wakati ili kuwapa fursa na wananchi wengine kupata mikopo hiyo.

  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Christopher Msimbe ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu nafasi ya vijana walemavu waliomaliza mafunzo kupitia Mradi wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi (YEE) unaoratibiwa na Shirika la Plan International.

  Msimbe amesema pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali, Halmashauri inatambua nafasi ya vijana katika jamii hasa vijana wenye ulemavu na ndio sababu wanawakumbuka katika fursa nyingi zinazokuja katika Halmashauri hiyo kutoka kwa wadau  mbalimbali.

  “Katika Halmashauri yetu tumebahatika kupata mradi wa YEE unaowashirikisha hata vijana wenye ulemavu, mradi huo unalenga kuwapatia mafunzo ya ufundi vijana ili waweze kujitegemea hivyo sisi kama Serikali tumetoa jumla ya shilingi 4,000,000 kwa vikundi viwili vya vijana wenye ulemavu ili waweze kuinua shughuli zao,”alisema Msimbe.

  Amefafanua kuwa Halmashauri zote nchini zinatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwapatia mikopo vijana na wanawake ili kuwasaidia kujikwamua kimaisha kwa kuendelezea biashara zao lakini asilimia kubwa wamekuwa hawapeleki marejesho kwa wakati na kusababisha Halmashauri kushindwa kutoa mikopo kwa watu wengine.

  Nae, Mwenyekiti wa Mtaa wa Kiungwile “A” iliyopo wilayani Kilombero Mkoa wa Morogoro, Emmanuel Sama amesema mradi huo umewasaidia vijana wengi kwa sababu kabla ya mradi huo vijana walikuwa wakizurura mitaani bila kazi yoyote pia vijana walemavu walikuwa wakikaa ndani bila kujua hatima yao.

  “Mtaani kwangu nina vijana watano waliopewa mafunzo na shirika hili ambao wamefanikiwa kuunda kikundi chao kijulikanacho kama ‘Baraka Farmers Group’ ambacho kinatumia elimu waliyoipata pamoja na mkopo wa shilingi 1,500,000 kutoka katika Halmashauri yetu kujiendeleza kiuchumi, nawashkuru vijana hawa kwani wanatumia vizuri fursa waliyopewa na kurejesha fedha walizokopeshwa kwa wakati,”alisema Sama.

  Sama ametoa rai kwa wananchi wanaopewa mikopo na Serikali hasa wananchi wasio na ulemavu ambao wanaweza kufanya kazi kwa uhakika kurejesha fedha za mikopo kwa wakati ili Halmashauri iweze kuendelea kuwasaidia wananchi wengine na watakaokaidi watachukuliwa hatua stahiki ili warudishe fedha hizo.
  Mradi huo wa miaka mitatu umeanza mwaka 2015 hadi 2018 unatekelezwa kwa ushirikiano wa mashirika ya VSO, CCBRT, VETA, UHIKI, CODERT pamoja na Serikali ya Tanzania huku ukiratibiwa na Shirika la Plan International chini ya ufadhili wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU).

  0 0

   Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akizungumza wakati wa uzinduzi wa Warsha ya umuhimu wa taasisi katika Maendeeo ya Viwanda nchini kwa watafiti iliyoandaliwa na taasisi ya REPOA
   Mkurugenzi mkuu wa REPOA Tanzania, Dr Donald Mmari akizungumza juu ya taasisi hiyo na mudhui ya mkutano kwa watafiti
   Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakifuatilia kwa makini
   Baadhi ya wabunge wa Bunge la jamhuri ya Muungano Tanzania wakiwa katika mkutano huo
   Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo
   Kiongozi wa umoja wa Ulaya  Roeland Van De Geer akizungumza wakati wa mkutano huo
   Profesa Lant Pritchett  kutoka chuo kikuu cha Havard Marekani akizungumza mara baada ya ufunguzi wa Warsha hiyo Prof Lant ni mmoja wa watoa mada wakuu waliofika katika mkutano huo
   Baadhi ya Washiriki wakiwa katika mkutano huo wakisikiliza mada kutoka kwa Prof Lant
  Waziri wa Fedha na Mipango , Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki

  0 0


  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

  Watanzania wenye vipaji wametakiwa kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza na wamewataka wajitokeze kwa wingi katika mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa na Mtanzania Emanuel Houston anayeishi Nchini Ujerumani.

  Emanuel ameambatana na baba yake Luis Houston ambao wote wanaishi nchini Ujeruami na wataendesha mafunzo hayo kupitia taasisi ya Unleashead Academy iliyo chini ya Halila Mbowe.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Emanuel amesema kuwa anafurahi kuja kuwafundisha vijana wa kitanzania namna ya kucheza na watapata fursa ya kumuuliza kitu chochote.

  Emanuel amesema kuwa, kuja kwake nchini Tanzania anategemea kuona vijana wengi kuja kujifunza kwani katika nchi za Ulaya watu wanaanza kujifunza mapema zaidi wakiwa na umri mdogo ndiyo maana wanaweza kufika mbali katika sekta mbalimbali.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe amesema wanafuraha sana kuweza kuwakaribisha vijana katika kituo chao na pia kushirikiana na Emanuel Houston pamoja na Ben Pol kuja kuandaa mafunzo hayo kwa vijana.

  Halila amesema kuwa kituo chake kinajihusisha na masuala ya kuinua vipaji katika kucheza mziki na kuandika mashairi na wameweza kupata vijana wengi na na takribani 25 tayari wameshaingia katika mashindano makubwa.

  Baba yake na Emanuel, Luis Houston amesema kuwa alianza kukijua kipaji cha mwanae toka alivyokuwa mdogo na akamwambia kuwa utakuja kuwa mcheza mziki (dancer) na kweli mpaka sasa ameweza kuendesha maisha yake kupitia kucheza na ameshafungua kituo cha mafunzo nchini Ujerumani na ana wanafunzi takribani 15000.

  Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwa kesho katika studio za Unleashead zilizopo Mikocheni B na itaanza saa 9-11 alasiri na hakutakuwa na kiingilio chochote.
  Mtanzania Emanuel Houston akizungumza na waandushi wa habari kuhusiana na mafunzo ya kucheza yatakayoendeshwa nae hapo kesho chini ya Unleashed Academy, kushoto ni msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed 
  Academy Halila Mbowe.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Unleashed Academy Halila Mbowe akizungumzia jinis kituo chake kinavyofanya kazi katika kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania katika kucheza na kutunga mashairi, Kulia ni Luis Houston ambaye ni baba yake na Emanuel Houston (wa pili kushoto) na 
   msanii na mratibu wa mafunzo hayo Bernad Paul 'Ben Pol' 

  0 0  Ø Waahidi kuendelea kusaidia sekta ya nishati nchini

  Na Veronica Simba – Singida

  Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hamme-Hanie Kaarstad na Balozi Katarina Rangnitly anayewakilisha Sweden hapa nchini, wameipongeza Serikali kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi ya umeme vijijini, hivyo wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano hususan katika sekta ya nishati.

  Wakizungumza hivi karibuni, kwa nyakati tofauti, katika uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji wa Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida, Mabalozi hao walisema Serikali za nchi zao zinafurahi kuona jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wananchi, hususan wa vijijini wanapata umeme wa uhakika na wa bei nafuu.

  Akizungumzia kuhusu Mradi wa REA III mkoani Singida, Balozi Kaarstad, mbali na kumshukuru Rais John Pombe Magufuli, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na watendaji wengine wa Wizara kwa kuwezesha kutekelezwa kwa miradi husika ya umeme vijijini, alisema kuwa ni matarajio yake kwamba Mradi utawezesha maisha ya wananchi wa Singida kuwa mazuri zaidi.

  Aidha, alisema kuwa anaamini Mradi huo utaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya wanawake wa Mkoa huo.

  “Mradi huu utaleta mabadiliko kimaisha kwa watu wote lakini zaidi kwa maisha ya wanawake.”

  Akifafanua zaidi, Balozi Kaarstad alisema kuwa, matumizi ya umeme katika kuwezesha miradi ya maji, yatawasaidia wanawake kupata muda wa kutekeleza majukumu mengine ya kiuchumi.

  Alisema, kwa muda ambao utaokolewa kwa wanawake kuacha kwenda kutafuta maji mbali, utasaidia wasichana kupata muda wa kujisomea nyumbani baada ya muda wa masomo, hivyo kufanya vizuri katika masomo yao.

  Aliongeza kuwa, matumizi ya taa za mitaani, ambazo zitatoa mwanga, zitawezesha wanawake kutembea bila hofu hata nyakati za usiku.

  Vilevile, alisema kuwa, kupatikana kwa umeme kutawezesha siyo wanawake tu bali jamii nzima kupata mafanikio katika maisha yao.

  Halkadhalika, Balozi Kaarstad alieleza kuwa, matumizi ya umeme katika viwanda vidogo vidogo, yataongeza thamani ya mazao pamoja na kuzalisha kazi mbalimbali kwa wananchi hivyo kuwezesha nchi kukua kiuchumi.

  “Katika nchi yangu ya Norway, uzalishaji wa nishati kutokana na maporomoko ya maji ulikuwa ni msingi mkubwa wa kupatikana kwa maendeleo. Tumeshuhudia maendeleo makubwa yanayobadilisha maisha ya watu kutokana na umeme. Ndiyo maana ninafurahi kushuhudia uzinduzi wa mradi huu wa umeme kwani najua hata hapa Singida, tunaweza kutumia nishati kupata maendeleo hayo.”

  Alisema kuwa, Norway iko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika jitihada za kuiwezesha itoke katika kundi la nchi za Ulimwengu wa Tatu kwenda kundi la nchi za Ulimwengu wa Pili.

  Balozi huyo wa Norway aliwashauri wananchi kuwa umeme watakaounganishiwa utumike katika kuendeleza jamii zao na kwamba anatarajia akirudi tena Singida atakuta maendeleo na mabadiliko makubwa kiuchumi.

  Kwa upande wake, Balozi Rangnitly alisema kuwa, Sweden imekuwa mshirika wa Tanzania kuanzia miaka ya 1960 na kwamba kwa muda wote huo nchi yake imekuwa ikiunga mkono sekta ya nishati.

  “Hii inajumuisha hatua mbalimbali, kuanzia kwenye uzalishaji wa umeme mathalani Mtambo wa kuzalisha umeme wa Hale pamoja na usafirishaji na usambazaji wa umeme,” alifafanua.

  Alisema kuwa, upatikanaji wa umeme wa uhakika, utabadili maisha ya wananchi na kwamba utawezesha wanafunzi kufanya kazi zao za shuleni wakati wa usiku. 

  Balozi Rangnitly alitolea mfano wa maendeleo ambayo nchi yake ilipata baada ya kuunganishwa na nchi nyingine za jirani ikiwemo Ujerumani kwa kuuziana umeme kati ya nchi na nchi.

  “Kwa kawaida bei za umeme hushuka na pia kunakuwa na umeme wa uhakika. Itakuwa hivyo hata hapa Tanzania, kupitia Mradi wa Umeme wa Backbone.”

  Aidha, Balozi huyo wa Sweden alitilia mkazo umuhimu wa matumizi ya nishati jadidifu ambapo alisema uwepo wa jua la kutosha Tanzania, unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuzalisha umeme wa jua.

  Hata hivyo alitanabaisha kuwa, upatikanaji wa umeme pekee hautoshi katika kuleta maendeleo isipokuwa, umeme ukipatikana kunatakiwa kuwepo na mazingira mazuri na wezeshi ya kibiashara pamoja na upatikanaji wa mitaji.

  “Sweden itashirikiana na Tanzania katika Nyanja hizo pia. Hata hivyo, umeme ni msingi wa mambo hayo yote,” alisema.

  Kwa upande wake, Waziri Muhongo, ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo, aliwashukuru wafadhili wote wanaochangia katika miradi ya umeme nchini, hususan Mabalozi hao wawili waliohudhuria hafla ya uzinduzi.

  Waziri Muhongo alisema kuwa, wafadhili hao wameshawishika kuendelea kufadhili miradi ya umeme nchini kutokana na Tanzania kuwa nchi inayoheshimika kimataifa, yenye uongozi safi, rasilimali za kutosha na yenye wananchi wanaojituma.

  Awali, akitoa maelezo ya utangulizi katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alisema kuwa wafadhili mbalimbali wamekuwa wakichangia fedha katika miradi ya umeme vijijini na kwamba jumla ya fedha zilizotolewa na wafadhili katika Mradi wa Umeme wa Backbone kwa ajili ya kuunganishia umeme vijiji vilivyopitiwa na Mradi huo ni Euro milioni 28 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 60.

  Alisema kuwa, fedha hizo ni kwa ajili ya kugharamia usambazaji wa umeme katika vijiji 121 katika Mikoa mitano (5) ambayo imepitiwa na Mradi wa Usafirishaji wa Umeme mkubwa wa kilovolti 400. Mikoa hiyo ni Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga.
   Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akiwatambulisha Balozi wa Norway nchini Tanzania, Hamme-Hanie Kaarstad (katukati) na Balozi wa Sweden nchini, Katarina Rangnitly (kulia); kwa wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.
   Kamishna wa Nishati na Masuala ya Mafuta, Mhandisi Innocent Luoga (mwenye suti nyeusi) na Afisa kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) (wa pili kutoka kushoto), wakiwatafsiria kwa lugha ya kiingereza wageni walioambatana na Mabalozi wa Sweden na Norway katika hafla ya uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.
  Sehemu ya umati wa wananchi waliohudhuria katika hafla ya  uzinduzi wa Mradi Kabambe wa Usambazaji Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (REA III) kwa Mkoa wa Singida.


  0 0


  0 0
 • 03/29/17--12:38: Wakazi - Tanganyika #Video

 • 0 0

  Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Longido ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Godfrey Daniel Chongolo, imeendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.

  Sehemu ya Bhangi ikichomwa moto,kuhakikisha haitumiki tena kwa matumizi mengine ya ulevi.

  Mkuu wa wilaya ya Longido,Godfrey Daniel Chongolo akijiandaa kuanza kuongoza oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya Bhangi akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo. Jumla ya mashamba yenye ukubwa wa ekari 5 yaliyokuwa yamelimwa bangi yameteketezwa.
  Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya pamoja na DC wa wilaya ya Longido,Mh Daniel Chongol ( pichani kulia) wakiendelea na oparesheni ya kuteketeza dawa za kulevya aina ya bhangi katika kata ya Lang'atadabash wilayani humo mkoani Arusha

  0 0

  Ally Songoro Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma Bodi ya Ununuzi na Ugavi(PSPTB) akitoa mada kwa wanafunzi wa Ununuzi na Ugavi katika Chuo cha (IPS) kilichopo Chanika jijini Dar es salaam. wakati wataalamu wa bodi hiyo walipotoa mafunzo ya taaluma hiyo katika chuo hicho, Bw. Ally Songoro amehimiza kufuatwa kwa maadili wakati wa kutekeleza majukumu yao ambapo unatakiwa umakini mkubwa huku wakifuata maadili, Kanuni na taratibu za ununuzi na ugavi wakati watakapokuwa katika ajira zao kwenye taasisi mbalimbali hapa nchini na kwingineko.
  Baadhi ya wanafunzi hao wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wataalamu kutoka Bodi ya ununuzi na ugavi (PSPTB) kwenye chuo hicho.
  Mmoja wa wakufunzi wa chuo hicho akiwaeleza jambo wanafunzi hao wakati alipokuwa akiwakaribisha wataalamu kutoka Bodi ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB) ili kutoa mafunzo kwa wanafunzi hao.
  Shamim Mdee Afisa Mwandamizi wa Masoko na Mahusiano ya Umma(PSPTB) akizungumza jambo na wanafunzi wa taaluma ya Ununuzi na Ugavi katika chuo cha (IPS) Chanika jijini Dar es salaam.

  0 0  0 0


  0 0


  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizungumza na watumishi,watoto yatima katika Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini katika ziara ya kutembelea miradi mbalimbali jijini Dar es Salaaam.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa kwenye viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akipanda mti katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi bengu za mbogamboga, Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia) leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii,Siman Panga
  Kamishina Msaidizi wa Ustawi-wa Jamii, Simon Panga akizungumza katika hafla ya kutembelea miradi mbalimbali katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaaam.

  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akiwakatika picha ya pamoja katika Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akitembezwa viunga vya Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam.
  Afisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini,Beatrice Lawrance(kulia)akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.ambapo alishukuru Ubalozi wa Kuwait nchini kwa msaada wa miradi mbalimbali na kuomba taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga taifa bora
  Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikagua mradi wa maji Makao ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

  0 0


  Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren akikabidhi vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 kwa Mkurugenzi wa chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid ukiwa ni msaada kwa chuo hicho kutoka Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin.


  Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid (kushoto) akifurahia msaada wa vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 vilivyotolewa na Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel kwa shule yake jana kisiwani Unguja, Zanzibar. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin na kulia ni Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa.


  Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren akikabidhi msaada wa vitabu vyenye thamani ya Tsh. milioni 10 kwa Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na ufundi Haji Abdulhamid katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika juzi Unguja-Zanzibar. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin.
  Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto) akikabidhi vitabu kwa Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi, Haji Abdulhamid. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour na kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania, Benoit Janin wakishuhudia.
  Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na ufundi Haji Abdulhamid (katikati) akitoa shukrani mara baada ya kupokea msaada wa vitabu 152 vyenye thamani ya Tsh 10 milioni kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour, Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kulia) na Mkuu wa Zantel Zanzibar, Mohamed Mussa.
  Mkuu wa Chuo cha Karume cha Sayansi na ufundi Haji Abdulhamid akitoa shukrani baada ya kupokea msaada wa vitabu 152 vyenye thamani ya Tsh 10 milioni kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Kushoto ni Mkurugenzi wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour, Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Tanzania Benoit Janin.

  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour (kushoto) na Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren wakifuatilia historia ya Chuo cha sayansi na ufundi cha Karume walipofika chuoni hapo kutoa msaada wa vitabu zaidi ya 152 vilivyogharimu Tsh milioni 10. Kulia ni Mkuu wa chuo hicho, Haji Abdulhamid. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Afrika, Mohamed Ali Dabbour (kushoto) akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi katika hafla ya kukabidhi vitabu 152 vilivyotolewa na Zantel kwa Chuo hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa Zantel, Rachel Samren. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi wakishuhudia hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitabu zaidi ya 152 kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja.
  Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Karume cha Sayansi na Ufundi wakishuhudia hafla ya kukabidhiwa msaada wa vitabu zaidi ya 152 kutoka kwa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel. Hafla hiyo ilifanyika juzi kisiwani Unguja. 

  0 0
 • 03/30/17--00:11: tangazo


 • 0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel, Isaack Nchunda (kulia), akitoa elimu kuhusu ofa mpya ya Hatupimi Bando kwa wafanyabiashara katika Soko la Tandale, wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam jana, kuitambulisha  huduma hiyo. 
   Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano Mallya akitoa elimu kuhusu ofa mpya ya Hatupimi Bando kwa Mfanyabiashara katika Soko la Shekilango Ubungo, Godwin Rwekubya, wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam jana, kuitambulisha  huduma hiyo. 
   Meneja Mauzo wa Airtel Kanda ya Dar es Salaam, Robert Sanyagi (kushoto),  akitoa elimu kuhusu ofa mpya ya Hatupimi Bando kwa wafanyabiashara katika Soko la Tandale, wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam jana, kuitambulisha  huduma hiyo.

   Mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa ndani, Nestory Malewo (kushoto)  pamoja na Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde pamoja na kwa pamoja wakitoa elimu kuhusu ofa mpya ya Hatupimi Bando kwa wafanyabiashara katika Soko la Tandale, wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam jana, kuitambulisha  huduma hiyo.
   Baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakitembea kwa pamoja kuipeleka ofa ya Hatupimi Bando kwa wateja sokoni
   Meneja Mauzo wa Airtel , Frederick Mwakitwange akitoa maelezo kwa  wafanyakazi wa Airtel kkabla ya kuingia sokoni kwenda kutembelea wateja sokoni
   wafanyakazi wa Airtel katika picha ya pamoja 
   baadhi ya wafanyakazi wa Airtel wakiongea na wateja wao katika maeneo ya Tiptop mapema leo wakati walipotembelea wateja na kutoa elimu juu ya ofa mpya ya Hatupimi Bando 
  Meneja Kitengo cha Network, Charles Matinga akitoa elimu juu ya ofa mpya ya Hatupimi Bando kwa mfanyabiashara wa soko la Tandale leo wakati wafanyakazi wa Airtel walipotembelea wateja wake Sokoni

  0 0

  Waandish wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya Habari wakisubiri kuanza kwa Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mjini Dodoma hivi sasa.

  0 0

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 kwa ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM). Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma akimsikiliza kwa makini.
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. George M. Lubeleje (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Ahmed Juma Ngwali (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Margaret S. Sitta (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Saada Mkuya (Mb) akichangia hoja mara baada ya Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakimsikiliza Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Mwanne I. Mchemba (Mb) (hayupo pichani) wakati akiongoza kikao cha kamati hiyo na Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora cha kupokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa mara baada ya kuwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
  Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakipitia kwa makini taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/17 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha wa 2017/18 ya Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora iliyowasilishwa na Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa Utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

  0 0

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akitoa Maelekezo kwa Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwa pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, wa kwanza kulia ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamadi Massauni na wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Hassan Simba Yahaya, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
  Baadhi ya Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakipitia bajeti za taasisi zao, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa [NIDA] Massawe, akifuatiwa na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala, watatu kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye na wanne ni Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Dr. Juma Malewa. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba akiwa pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara yake wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
  Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakipitia bajeti zao, wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
  Baadhi ya Makamishna wa Uhamiaji, Magereza, na Zimamoto na Uokoaji pichani, wakipitia bajeti zao, wakati wa Kikao cha Mapitio ya Bajeti ya Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi muhimu kabla ya kuanza kwa Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu. Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. [PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI]  IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0


  - Aandaa kongamano la Elimu Mkoa wa Mbeya
  - Ni mjadala wa wazi na wadau wa Elimu Kujadili changamoto za Elimu na mikakati ya kukabiliana nazo
  - Lengo ni kuongeza Ufaulu na kuboresha Elimu
  - Asema kushusha vyeo wakuu wa Shule siyo suluhisho kuna mambo mengine yapo nje ya uwezo wao
  Kwa umuhimu wa Elimu amewakaribisha wadau wa Elimu kujadili kwa kina changamoto zilizopo na kuweka Mikakati ya kuboresha elimu na hatimaye Mkoa wa Mbeya uwe Mkoa wa Mfano ikiwemo kufaulisha wanafunzi kwa kiwango cha juu

  0 0

  Na Faustine Ruta, Bukoba
  Timu ya Vijana U17 ya Burudi leo asubuhi imefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Kaitaba kujiweka kisawasawa na kuusoma uwanja huo ili kujiimarisha vyema kabla ya kukutana uso kwa uso leo na Timu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys. 


  Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Mchezo wa kwanza  utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka huu. Hata hivyo Mvua iliweza kunyesha na kukatisha zoezi lao asubuhi na hatimae kurudi kwenye makazi waliyofikia jana baada ya kuchelewa kufika Bukoba na kutoweza kufanya mazoezi kwenye uwanja huo.

  Nayo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys jana Jamatano walifanya mazoezi asubuhi saa nne kujiweka tayari na mchezo wao wa leo na Timu hii ya Burundi. 


  Serengeti Boys itakuwa kambini mjini hapa Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako Serengeti Boys ambayo inajiandaa na michuano Afrika huko Gabon itarejea Dar es Salaam Aprili 2, mwaka huu ambako imepangwa kucheza na Ghana Aprili 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo huo utatanguliwa na hafla ya kuagwa kwa kukabidhiwa bendera.
  Vijana wa Burundi wakiwa wanateta jambo na kufurahia Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii ambako wanataraji kupambana na Serengeti Boys leo hii kwenye mchezo wa kwanza wa Kirafiki wa Kimataifa. Pia watarudiana siku ya Jumamosi.


  Timu hii itacheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Mchezo wa kwanza  utaanza kuchezwa leo hii Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi.
  Viongozi wa Timu hiyo yaBurundi wakiwaangalia kwa Makini Vijana wao ambako mapaka tunatoka kwenye Uwanja huo tuliweza kupata habari kuwa hakuna mchezaji hata mmoja ambaye ameumia  au ana jeraha la kuweza kumfanye awe nje ya Uwanja, Wote wako fiti kwa Mchezo wa leo dhidi ya Serengeti Boys.


  Mvua kubwa ilinyesha na kukatisha Tizi lao kwenye Uwanja huo wa Kaitaba asubuhi hii na kwenda jukwaa kuu


  Wakisikilizia Mvua...

  0 0

   Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akitoa mada katika mdahalo ulioandaliwa na REPOA juu ya mapinduzi ya Viwanda,Jana jijini Dar
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Profesa Adolf Mkenda akitoa ufafnuzi juu ya nini kifanyike katika kufikia malengo ya mapinduzi ya Viwanda nchini
   Mzee Butiku akifuatilia mjadala huo ambao ulikuwa wa aina yake
   Mkurugenzi mkuu wa Benki ya CRDB nchini , Charles Kimei akizungumza namna mabenki yanavyoweza kutoa mchango mkubwa katika mapinduzi ya Viwanda nchini wakati wa mjadala ulioandaliwa na REPOA juu ya nini kifanyike kuelekea mapinduzi ya Viwanda kwa kushirikisha Tasisi,jana jijini Dar
   Waziri wa Fedha Mstaafu wa awamu ya nne ,Bazili Mramba akizungumzia juu ya nini kifanyike katika serikali kuu ili tuweze kufanikiwa katika maendeleo ya Viwanda
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara , Profesa Adolf Mkenda akiwa na baadhi ya washiriki mara baada ya kumalizika kwa mjadala huo

older | 1 | .... | 1186 | 1187 | (Page 1188) | 1189 | 1190 | .... | 1897 | newer