Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1188 | 1189 | (Page 1190) | 1191 | 1192 | .... | 1897 | newer

  0 0

   Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akitoa ufafanuzi  kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara yake kwa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 
   Katibu Mkuu wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara  hiyo, Balozi  Hassan Simba Yahaya anayemfuatia wakifuatilia ufafanuzi uliokuwa ukitolewa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini [IGP] Ernest  Mangu aliyesimama  kuhusu Oparesheni mbalimbali za kuzuia uhalifu hapa nchini, wakati wa Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 
   Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala, akiwa pamoja na watendaji wengine wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, akimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mhe. Balozi  Adad Rajab wakati Mwenyekiti huyo hayupo pichani, akiwaongoza Wajumbe wa Kamati hiyo kuipitia Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bjeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma.   
   Katibu Mkuu wa Wizara Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira wa kwanza kulia na Naibu Katibu Mkuu wake, Balozi  Hassan Simba Yahaya wakifuatilia kwa makini Bajeti ya Jeshi la Polisi ya mwaka ujao wa fedha,  katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo, ambapo kwa siku ya leo Kamati hiyo imepitisha Bajeti za Jeshi la Polisi na Fungu Hamsini na Moja inayobeba Idara Saidizi ndani ya wizara, hatua ambayo ni muhimu kufikiwa kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma [UDOM] mkoani Dodoma. 

  Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba,  akisoma taarifa ya utekelezaji wa Bajeti ya mwaka wa fedha wa  uliopita katika Kikao cha Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kabla ya Mapitio ya Bajeti  ya mwaka ujao wa fedha kwa Taasisi ziliko katika Wizara hiyo,  ikiwa ni hatua muhimu kabla ya kuanza kwa  Vikao vya Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linalotarajiwa kuanza mapema tarehe nne mwezi Aprili mwaka huu, Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa  Chuo Kikuu Dodoma  mkoani Dodoma.
  PICHA ZOTE NA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YANCHI

  0 0

   Alpherio Moris Nchimbi Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa “Baseball/Softball” Tanzania – TaBSA .
  .............................................................................

  Umoja wa Mataifa (UN) pamoja na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa(IOC) kwa pamoja mnamo tarehe 23 Agosti, 2013 walitiliana saini na kukubaliana kuanzishwa rasmi kwa tarehe 6 April ya kila Mwaka iwe ni SIKU YA KIMATAIFA YA MICHEZO KWA AJILI YA AMANI NA MAENDELEO. “International Day of Sport for Development and Peace”

  Chama cha Mchezo wa “Baseball/Softball” Tanzania – TaBSA, kimeamua kushiriki siku hii kwa kutoa Kombe Maalum la AMANI ambalo litashindaniwa na timu mbili zitakazojumuisha watu wa rika kuanzia miaka 15 na kuendelea bila kujali viwango vya wachezaji katika kuucheza mchezo huu wa Baseball. Mechi hiyo itakuwa katika mfumo wa Bonanza.
  Timu zitakuwa ni TIGERS na GIANTS.

  Kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Chama, ninachukua fursa hii kuwaalika wote kuhudhuria na kushiriki Bonanza hili la AMANI katika viwanja vya Azania Sekondari kuanzia saa 13:30 mchana siku ya Jumamosi ya tarehe 8 April, 2017.
  Karibuni wote!.

  Alpherio Moris Nchimbi – KATIBU MKUU.
  Tumeamua kuifanya tarehe 8 April kwa kuwa tarehe 6 April ni siku ya Kazi!

  0 0


  Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Dkt. Medard Kalemani akiongea jambo wakati akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Dotto Biteko, akichangia Hoja baada ya Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17 kuwasilishwa kwa Kamati.
  Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. Susan Kiwango akichangia Hoja baada ya kuwasilishwa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2016/17.
  Mjumbe Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini, Mhe. Oscar Mkasa akichangia jambo wakati wakati wa kikao baina ya Kamati na Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake, ambapo Wizara na Taasisi ziliwasilisha Taarifa za Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17.
  Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gisima Nyamo- Hanga, akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya REA kwa mwaka 2016/17 kwa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Nishati na Madini.
  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka 2016/17 ya shirika hilo kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Haji Janabi, akiwasilisha Taarifa ya Utekelzaji wa Wizara kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.
  Baadhi ya Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakifuatilia kikao baina ya Wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

  …………………………………………………………………..

  Wizara ya Nishati na Madini imekutana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuanzia tarehe 27 Machi, 2017, ambapo Wizara na Taasisi zilizo chini yake zimewasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2016/17.

  Akielezea baadhi ya mafanikio ya Wizara kwa Kamati ya Bunge, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, ametaja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na;
   
  Kukamilika kwa asilimia 100 kwa Mradi wa Kusafirisha Umeme kutoka Iringa hadi Shinyanga wenye msongo wa kilovoti (kV), 400.

  Kukamilika kwa asilimia 98.5 ya Awamu ya Pili ya Mradi Kambambe wa Kupeleka umeme Vijijini unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini- REA.
  Kuzinduliwa rasmi kwa Awamu ya Tatu ya Mradi Kabambe wa Kupeleka umeme Vijijjini unaolenga kusambaza umeme katika vijiji vyote visivyofikiwa na huduma hiyo.
   
  Kukamilika kwa Kanuni za:
  The Petroleum (Retail Operations in Townships and Villages) Rules,2016
  The Petroleum (Natural Gas Pricing) Rules,2016
  The Electricity (Supply Services) Rules, 2016

  The Electricity (Market re- organization and competition) Rules,2016 na
  The Mining (Minimum shareholding and Public Offering) Regulations 2016. Kanuni hizi zinasimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Sekta za Nishati na Madini.

  Kuanza kwa maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, Tanzania.

  Kuendeleza shughuli za utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini ambapo hadi sasa jumla ya Futi za Ujazo Trilioni 57.25 za gesi asilia zimegunduliwa.
  Kukamilisha utafiti wa jio-sayansi (jiolojia, jiokemia na jiofikizia katika mikoa ya Lindi na Mtwara na kuchora ramani za kuanisha kuwepo kwa madini mbalimbali ili kuhamasiaha uwekezaji kwenye maeneo ya Nachingwea, Ruangwa na Masasi.

  Wizara kutenga maeneo 11 kwa ajili ya wachimbaji madini wadogo yaliyopo Msasa na Matabe Mkoani Geita, Biharamulo na Kyerwa yaliyopo Mkoani Kagera, Itigi, Mkoani Singida, D- Reef, Ibindi na Kapanda Mkoani Katavi, Ngapa Mkoani Songea, Nzega Mkoani Tabora na Kitowelo Mkoani Lindi. Maeneo hayo yana ukubwa wa takriban hekta 38.567
   
  Kufanyika kwa minada miwili (2) ya madini ya vito hususan tanzanite jijini Arusha ambapo Serikali ilipata jumla ya shilingi milioni 793 ikiwa ni mrabaha uliolipwa Serikalini kutokana na minada hiyo.

  0 0  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisalimiana na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko Ofisini kwake Mjini Dodoma kufanya mazungumzo yahusuyo mambo ya Sanaa ya Muziki.

  Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma kwa mazungumzo.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akisisitiza jambo kwa Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego mara baada ya mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego Ofisini kwake Mjini Dodoma.
  Msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) mara baada ya kumaliza mazungumzo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe Mjini Dodoma.Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa wasanii nchini kutovuka mipaka katika utengenezaji wa kazi zao mpaka kufikia hatua ya kuvunja Sheria na taratibu za nchi.

  Ameyasema hayo Mjini Dodoma jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kwa mwaliko wa Waziri huyo.

  Amesema kuwa wasanii ni nguzo muhimu katika nchi sio kwa kufanya kazi ya kuburudisha na kuelimisha bali katika kuujenga Utamaduni wa nchi ambao ndio nguzo muhimu sana kwa malezi na makuzi ya wanajamii.

  “Niwaombe wasanii nchini kuzingatia Sheria na taratibu za nchi katika utunzi wao na utenegenezaji wao wa kazi zao” Alisisitiza Mhe. Dkt Mwakyembe.

  Aidha ameongeza kuwa Serikali haina nia ya kuwanyima uhuru wa kujieleza bali watambue kuwa nchi inaendeshwa kwa taratibu na Sheria ambazo zinatakiwa zifuatwe na watu wote.

  Kwa upande wake Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kwa kuwaunga mkono wasanii nchini na kuahidi kuongeza baadhi ya mambo katika wimbo wake wa “Wapo” na kuwaalika watanzania kama kuna kero zingine zinazowasumbua katika jamii wasiwasilishe kwake ili azizungumzie katika wimbo huo.

  “Namshukuru Mhe. Rais kwa kutuunga mkono pia naahidi kufanya “remix” ya wimbo wa “Wapo” kwa kuongeza maneno niliyoshauriwa na Mhe Rais na Mhe. Waziri na kama kuna mengine kutoka kwa wananchi pia niko tayari kuyapokea na kuyafanyia kazi” alisema Bw. Elibariki.

  Hivi karibuni wimbo wa “Wapo” wa Msanii Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego ulifungiwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kosa la kutozingatia maadili na baadae kufunguliwa kwa agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kupitia Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe.

  0 0


   A stop order issued by Tanzania Government on March 3rd 2017 barring mining companies to export copper concentrates for smelting outside the country has significantly exposed Acacia, which exports the stuff from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects.

  Acacia statement opens a can of worms
  On March 15th 2017 Acacia Chief Executive Officer (CEO), Brad Gordon responded officially pertaining to the Government order. The CEO is quoted expressing jittery for Acacia incurring loss of US$17 million (Tzs. 37 billion) in just two weeks of executing Government stop order.

   He is concerned if the stop order is maintained Acacia may fail to continue running operations because export of copper concentrates accounts for 50 percent of Acacia earnings from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects. This statement exposes the vital information not previously disclosed to Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative (TEITI). Actually, it opens a can of worms. Acacia is TEITI member with obligation to correctly disclose material production and Government payments information pertaining to its mining operations in Tanzania.

  But reading Acacia statement we note the implication that Acacia had since TEITI launch (2009) disclosed only half the production and payments value data from Buzwagi and Bulyanhulu mining projects. And this sends bad signal to TEITI because it discounts material information and data compiled and published in the successive annual reports since 2011. The credibility of TEITI reports’ data and integrity of entire EITI work in Tanzania is exposed to irreparable risk if corrective remedies are not done in real time. Acacia has the obligation and should therefore come out immediately to patch up the anomaly.   

  Acacia statement exposes a gap in the TEITI reports.

  The quantity of gold or money value declared as having been produced or earned by Acacia and therefore payments made to government in the form of royalties, taxes, fees, levies, duties and statutory contributions should be correctly captured and documented in the TEITI reports. However, that may not be the case when we evaluate inherent logic exposed by Acacia statement. The payment data documented in the TEITI reports from Pangea Minerals Ltd (Buzwagi) and Bulyanhulu only present half the story. None of the six TEITI reports (2008/09 – 2013/14), has documented either quantity or value of copper concentrates, which according to Acacia, account for 50 percent of Bulyanhulu and Buzwagi revenue combined.

  The documented evidence available at TEITI indicates during the 2012/13 fiscal year, Pangea Minerals Ltd (Buzwagi goldmine) produced 205,240 ounces of gold worth Tzs. 520.9 billion (US$328,025,425) while Bulyanhulu goldmine produced 197,571 ounces of gold worth Tzs. 477.1 billion (US$300,413,402) (TEITI Report 5th, 2015:11). Again, the data documented during the subsequent fiscal year show no difference. 

  Bulyanhulu is recorded to have produced 192,550 ounces of gold worth Tzs. 430.5 billion (US$265,884,907) while Pangea Minerals (Buzwagi) produced 198,995 ounces of gold worth Tzs. 384,539,239,000 (US$237,516,516) (TEITI Report 6th, 2015:10). Not only are the quantity and value of copper concentrates exported from Buzwagi and Bulyanhulu missing from the duo fiscal years’ TEITI reports, but also are entirely not documented in the previous four reports.

  There is one more controversial issue, which previously, Acacia hadn’t disclosed yet, but it is implied in the statement. The statement underscores that Acacia exports (sells) copper concentrates to foreign buyers rather than sending the stuff for smelting outside the country where appropriate technology is available. This means the ownership title of copper concentrates changes from Acacia to a foreign buyer immediately the stuffs are exported. 

  This notion is new to Tanzanians, who hitherto held common knowledge that Acacia sends copper concentrates to foreign countries with appropriate technology for smelting the stuff, which whatsoever, wouldn’t involve ownership title transfer from Acacia to a foreign entity. That being the case, Acacia would be expected to report such significant transaction to TEITI because copper concentrates and gold are materially different. The local media quoting persons involved in the export of copper concentrates from the Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA), Tanzania Ports Authority (TPA) and Acacia officials estimate 50,000 [8ft (2.43m) x 8.5ft (2.59m) x 40ft (12.2m)] containers of copper concentrates have had been shipped annually.    

  Our Position and recommendations
  The Coalition of Tanzania Civil Society Members of global EITI Association (TEICS) considers the amount of money raised from export of copper concentrate but Acacia hadn’t reported to TEITI for public scrutiny is significant enough to alter both TEITI reports and Government records of payment received from Acacia. Disclosure of these payments is even more urgent than ever considering Acacia nonpayment of Corporate Income Tax (CIT) since the company started (1998) operating in Tanzania up to 2016, on the ground that the company is still recuperating losses incurred during the investment startup phase.
           
  We, TEICS, recommend and call upon:-

  1.That Acacia should disclose all details related to quantity and proceeds obtained from exports of copper concentrates since 2001 to 2017. Data presentation should comply with the EITI recommended pattern of data disaggregation – project by project and year by year – to allow and facilitate ease use by TEITI and Government.

  2. That TETI Committee should immediately start retrospective review and upscale all previous TEITI reports’ data to accommodate significant material information disclosed by Acacia reflecting proceeds from annual exports of copper concentrates.

  3. That the Government of the United Republic of Tanzania should assume leadership to evaluate the Mineral Development Agreement (MDAs) entered with Acacia to establish parties’ consistency and compliance with agreed terms therein, and thereafter, in consultation with Acacia, correct inconsistencies in the MDAs, if any, and ensure Acacia repays all the unpaid royalties, taxes, fees, levies, duties and statutory contributions resulting from exports of copper concentrates for entire period effectively from 2001 to 2017.    

  4.  That the media should follow up and report to public about the actions taken by Acacia, TEITI Committee and the Government to correct the anomaly caused by Acacia not disclosing copper concentrates export business to TEITI and Government.


  Issued and signed on behalf of TEICS members today, 30th March 2017, by

  Bubelwa Kaiza
  Coordinator

  0 0

  Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM) akizungumza na waandishi wakati wa mkutano huo.

  Washiriki wa mkutano huo wakifatilia mada zilizowasilishwa wakati wa mkutano huo


  Wanawake na vijana ni nyenzo muhimu katika uhamasishaji wa kumaliza machafuko yanayoendelea nchini Somalia, wakati kundi hilo pia likilengwa zaidi na vikundi vya kigaidi kutumika katika matukio ya kigaidi.

  Hayo yamebainishwa na Bi. Mane Ahmed, Afisa Jinsia kutoka African Union Mission in Somalia (AMISOM), wakati wa mkutano wa siku tatu unaomalizika leo (Ijumaa) jijini Dar es Salaam jana.

  Mkutano huo ulioandaliwa na AMISOM kwa ushirikiano na serikali ya Somalia unalenga kutafuta njia stahiki za kuzuia vijana kudahiliwa na vikundi vya kigaidi nchini humo.

  Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umebainisha umuhimu wa ujengaji uwezo kama hatua madhubuti katika kueneza hali ya kuvumiliana ndani ya jamii na kuwapa sifa mbaya Al-Shabaab.

  Akizungumza mkutanoni hapo, Bi Mane amesema kuwa Serikali ya Somalia imeanzisha ofisi ijulikanayo kama Counter-Violent Extremism (CVE) ikiwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu na kukamilisha rasimu ya kwanza ya Sera ya Kuzuia na Kupambana na Vikundi vyenye msimamo mkali.

  Bi Mane alisema kuwa AMISOM imeanzisha Mtandao wa Kijinsia ambao umelenga katika kuzuia na kupambana na vikundi vyenye msimamo mkali kwa lengo la kusaidia juhudi za Shirikisho katika kuunganisha mtazamo wa kijinsia katika mpango na mikakati yake.

  Bi Muna alisema: "Mkutano huu utawajengea uwezo viongozi wa dini, watendaji wa Somalia na kuongeza ufahamu wao juu ya umuhimu wa kuwajumuisha wanawake katika njia yao za kupambana na siasa kali na kubadilishana uzoefu na mbinu bora na wataalamu, watafiti, watendaji kutoka barani ambao wana ufanisi mkubwa katika kukabiliana na masuala yahusuyo vikundi vyenye misimamo mikali."

  Aidha naye, Naibu Kamishna wa Polisi wa AMISOM, Christine Alalo alisema kuwa katika hatua hii muhimu ya safari ya Somalia kuelekea kwenye amani na utulivu, jukumu la wanawake, wanaume na vijana katika kukabiliana na vikundi vyenye msimamo mkali ni muhimu kutiliwa mkazo kwa kiasi kikubwa.

  "Siyo siri kwamba wakati wa miongo miwili na nusu ya vita, wanawake na vijana wadogo wamekuwa wakitumika na makundi ya kigaidi katika Nyanja mbalimbali ikiwemo kukusanya taarifa za kiusalama, na kubeba mabomu,” alisema.

  Alibainisha kuwa AMISOM wamefanya mengi katika kupambana na hilo kupitia kitengo cha jinsia, wanawake na ulinzi wa mtoto.

  Alisema kuwa AMISOM pia imesaidia wizara ya wanawake, jinsia na haki za binadamu katika kuandaa sera ya taifa ya jinsia, kwa kufanya mafunzo ya ujengaji uwezo kwa wanawake wa Somalia na viongozi wa dini katika kumaliza mambo hatarishi.

  Mkutano huo wa siku tatu ambao unamalizika leo jijini Dar es Salaam, umewaleta pamoja watendaji, viongozi wa dini na asasi za kijamii kutoka nchi nane (Somalia, Tanzania, Ethiopia, Nigeria, Kenya, Mali, Djibouti, Alger) ukijadili juu ya mada zinazohusiana na kukabiliana na siasa kali na ugaidi.

  Jumla ya viongozi hamsini, wa kidini; watafiti na watendaji, na wadau muhimu kutoka taasisi za kitaifa, kikanda na kimataifa wameshiriki katika mkutano huo.


  0 0

   Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpokea mgeni wake ,Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn,aliyewasili hivi punde katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar Es Salaam.
   Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akipewa maua ikiwa ni ishara ya kumkaribisha kwa upendo nchini Tanzania,mara baada kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

  Waziri Mkuu wa Ethiopia ,Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye ndege mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere mapema leo mchana,na baadae kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli,Waziri Mkuu Kassim Majliwa na viongozi mbalimbali wa Kitaifa.

  Imeelezwa kuwa ujio wa Waziri huyo Mkuu wa Ethiopia ni pamoja na kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na Ethiopia pamoja ‎na kujadili fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ikiwemo uwekezaji na biashara.

   Mhe. Dessalegn atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo na kushuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali kabla ya kuzungumza na Waandishi wa Habari.

  HABARI ZAIDI ZITAWAJIA BAADE KIDOOGO.


  0 0  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege la ATCL, Bw. Lasislaus Matindi anasema wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9 kwa Miezi minne tu kwa kutumia ndege hizo mbili zilizonunuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, nakuleta utata mkubwa na wapinzani wa siasa nchini waliodai kuwa hazikuwa na tija kwa Taifa. 
  Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL) ilianzishwa mwezi Novemba 2002 baada ya Serikali kubinafsisha lililokuwa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania Corporation, ATC); katika Shirika hilo, Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) lilinunua hisa asilimia 49 ndani ya ATC. Hata hivyo ubia kati ya ATCL na SAA ulikabiliwa na matatizo ya kiuendeshaji na kulazimika kusitishwa mwezi Agosti 2006 na ATCL kurejeshwa tena Serikalini kwa asilimia 100.
  KUMBUKUMBU:
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na maafisa na viongozi wengine mbalimbali akikata utepe kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na maafisa wengine waandamizi wakiwa kwenye ndege mojawapo baada kuzindua rasmi ndege mbili mpya aina ya Bombadier Q400 zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam Jumatano Septemba 28, 2016. PICHA NA IKULU.

  0 0


  0 0
 • 03/31/17--02:37: TANZIA


 • 0 0

  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwahutubia wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) katika kikao chao cha baraza. Kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala Bi. Khadija Mwenda na viongozi wa baraza hilo.
  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi, akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mara baada ya kufungua kikao chao cha baraza.)
  Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Eric Shitindi (hayupo pichani) alipofungua kikao cha baraza lao mjini Dodoma jana.


  Mabadiliko ya mazingira ya ufanyaji biashara yanayoletwa na maendeleo ya uchumi wa viwanda pamoja na mnyororo wa thamani, yameelezwa kuwa changamoto kubwa katika jitihada za kuimarisha hali ya usalama na afya za wafanyakazi katika sehemu za kazi hapa nchini.

  Changamoto hiyo imetolewa na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Bw, Eric Shitindi, wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) mjini Dodoma leo.

  Amesema mabadiliko hayo yanahusisha matumizi ya teknolojia za kisasa na ongezeko kubwa la idadi ya wafanyakazi katika sekta zote za umma na za binafsi jambo ambalo linahitaji utaalamu mkubwa katika kuweka na kusimamia mifumo ya kulinda afya na kuwahakikishia usalama wafanyakazi wote wanapokuwa katika sehemu zao za kazi.

  “Hivyo mkiwa kama wataalamu katika masuala ya Usalama na Afya mahali pa kazi mnatakiwa kuwa na mikakati mipya ya kukabiliana na changamoto hizo. Hii itakuwa ni pamoja na kubadilika kifikra na kimtazamo katika utendaji kazi,” alisema Katibu mkuu Shitindi.

  Katibu mkuu huyo amesisitiza muhimu wa kutafuta mbinu mbadala ya kuweza kupanua wigo wa kufanya kazi hasa kwa kuzingatia ukubwa wa kazi zilizopo.

  Aidha Bw. Shitindi ameupongeza OSHA kwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa mpango kazi wake katika kipindi cha robo tatu za mwaka huu wa fedha (2016/2017) ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyowasilishwa katika baraza hilo, taasisi imevuka malengo katika kaguzi, utoaji wa mafunzo ya usalama na afya kazini pamoja na huduma mbali mbali zitolewazo mahali pa kazi.

  Katika hotuba yake, Katibu Mkuu aliahidi kuendelea kuisaidia OSHA kutatua changamoto zilizopo zikiwemo za kiutendaji na kuwaasa watumishi wa Wakala kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ikiwemo kuepuka kujihusisha na vitendo vya upokeaji rushwa wanapotekeleza majukumu yao.

  “Wizara imekuwa ikipokea malalamiko mengi ya namna mnavyohudumia wateja na kushuka kwa maadili ya kiutendaji miongoni mwa watumishi, mfano masuala ya rushwa, hivyo wakati tunaendelea kushughulikia matatizo hayo ni vyema sasa mkaanza kubadilika kwa kufuata sheria, taratibu, kanuni na miongozo mbalimbali ya utendaji kazi katika taasisi,” amesisitiza Bw, Shitindi.

  Kikao hicho cha baraza la wafanyakazi wa OSHA ambacho kimeanza leo kitamalizika kesho ambapo pamoja na mambo mengine kitapitia na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa (2017/2018) ili kujiridhisha kama itawawezesha kufanikisha utekelezaji wa malengo ya wakala yaliyowekwa

  0 0

  Kaimu Katibu Mkuu UVCCM,Shaka Hamdu Shaka .

  Tunawashukurukwa kupokea wito wetu na kuja, karibuni sana tunawaahidi kwamba tutaendelea kushirikiana nanyi katika kila hatua.

  Aidha Umoja wa Vijana wa CCM unavipongeza sana vyombo vyote vya habari nchini kwa juhudi zenu za kuhabarisha, kuelimisha, kuwaasa, kuwaelekeza na kuihabarisha jamiii katika masuala kadhaa yanayohusiana na mipango ya maendeleo, mikakati, sera na malengo ya Serikali na mipango ya vyama vya siasa.

  Ndugu Waandishi wa habari.

  Tumewaita leo kuzungumzia mambo 2 makubwa, na suala zima la mtikisiko wa demokrasia katika mchakato wa uteuzi wa wagombea Ubunge katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulivyoendeshwa ndani ya vyama vya upinzani nchini.

  Bunge la Afrika Mashariki kama mjuavyo ni chombo kikubwa na chenye heshima ya pekee katika kanda yetu. Kuwepo kwake kunaashiria muendelezo wa kufufua dhana, dhamira, mikakati, fikra na malengo ambayo yaliasisiwa na waasisi wa Mataifa yote yaliyomo katika Kanda yetu ili hatimaye siku moja ishuhudiwe Kanda hii na Bara zima la Afrika likiunda dola moja.

  Ni jambo la heri na faraja kuona EAC ya sasa ikiwa ni yenye kufikia
  malengo ya utengamano na mafanikio hususan katika nyanja za kiuchumi na kiusalama kama vile kuwa na Pasi moja ya kusafria, miingiliano ya
  wananchi wake katika ufanyaji wa biashara pia mkakati kuelekea kupata
  viwango sawia vya ushuru wa Forodha.

  Masuala mengine ni kuona maeneo ya mipaka yetu kukiendelea kuwa na ustawi wa hali ya utulivu na usalama, wakati huo EAC ikifanya kila linalowezekana kumaliza migogoro yake ya kisiasa ambapo mazungumzo ya upatanishi huko Burundi yamekuwa yakiendelea chini ya mpatanishi mkuu Rais mstaafu Benjamin Mkapa sambamba na wananchi wa pande zote za nchi wanachama tukishuhudia wakiishi kwa maelewano, umoja, udugu na mafahamiano.

  Ni katika jumla ya mambo yanayofurahisha na pengine yakiwasuta na
  kuwaaibisha maadui na vibaraka ambao aghalab hutumiwa kwa malipo yenye ujira wa dhambi toka kwa mabeberu katika kuhakikisha mipango batili ya kutaka kudhoofisha, kuigawa na kukwamisha juhudi za EAC isiimarike..

  Aidha kuibuliwa na kupokewa kwa mpango uitwao ” One Stop Boarder” yaani (OSB) sasa umefanikiwa huko mipakani baina ya nchi wanachama. Pia kuanzishwa miradi mikubwa ya kiuchumi mfano bomba la mafuta toka
  Kampala (Uganda) hadi Tanga (Tanzania) ujenzi wa reli toka kigali hadi
  Uganda huku EAC ikielekea kuwa na sarafu moja kabla ya kufikiwa azimio
  la uundwaji wa Shirikisho moja.

  Umoja wa Vijana wa CCM tumelazimika kuyataja na kuyaainisha maeneo hayo yaliopata mafanikio kwa uchache lengo likiwa ni kuonyesha uwepo na
  ustawi wa EAC pamoja na umuhimu wa bunge lake kama ni jambo nyeti na
  wala si suala dogo au la mchezo mchezo kama ambavyo baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeonyesha udhaifu.

  Ndugu Waandishi wa Habari,

  Baadhi ya vyama vya siasa nchini vimeshindwa hata kuteua wagombea ubunge wengi ili kuwania nafasi katika bunge hilo la Jumuiya ya Afrika
  Mashariki kwa sababu zinazotokana aidha na ubinafsi, umimi na udikteta.

  Tunachukua fursa hii kwanza kukipongeza Chama Cha Mapinduzi na wanachama wake wote 450 ambao kwa ujasiri, uwezo na kujiamini kwao wamethubutu kujitokeza na kuchukua fomu za kuwania nafasi za ubunge wa EAC.

  Kitendo cha wanachama hao wa CCM kujitokeza kwa wingi kimsingi
  kimeidhihirishia dunia kwamba chama chetu bado ni cha kidemokrasia
  kinachoungwa mkono na kuaminiwa na wananchi wengi wakiwemo Vijana,
  wanawake na wana taaluma mbali mbali wakitambua ndicho chama pekee imara chenye kujali, kuthamini na kufuata misingi ya usawa na demokrasia ya kweli.

  Wanachama 450 wa CCM walichukua fomu kwa kufuata taratibu baada ya mchujo wa kidemokrasia kufanyika ndani ya CCM, wanachama 12 wamebahatika kuteuliwa na vikao vya kikatiba ambapo sasa wagombea hao watasimama mbele ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kusaka ridhaa kwa kujieleza na kuomba kura.

  Ndugu Waandishi wa habari,

  Umoja wa Vijana CCM kwa tunasikitishwa sana na mwenendo wa demokrasia ndani ya vyama vya upinzani katika uteuzi wa kuwapata wagombea wa ubunge wa bunge la Afrika Mashariki (EALA) Chadema, CUF na NCCR Mageuzi kwa jinsi walivyowasilisha uwakilishi haba na finyu lakini pia kujitokeza kwa wagombea wachache hali inayoonyesha uminyaji wa demokrasia ndani ya vyama vyao.

  Chadema na washirika wao mara kadhaa hujigamba vichochoroni na kujionyesha kuwa wao ni watetezi wa demokrasia lakini unapofikia wakati wa utekelezaji wa jambo hilo kwa vitendo, ndani ya chama hicho humea ukandamizaji wa haki na kujitokeza upendeleo, ukanda, kubebana aidha kwa asili, ujamaa na urafiki au kulipana fadhila.

  Katu huu si mwenendo mwema ulioonyeshwa na vyama vya upinzani. Vimejipaka matope ya fedheha kwa kushindwa kuonyesha kama ni waumini wa kweli wa demokrasia badala yake havikujali wala kuheshimu dhana ya demokrasia na kujikuta vimejianika na kuuthibitishia umma wa watanzania kuwa vyama hivyo ni vya watu maalum vya kibwanyenye na vya kiimla .

  Kufanya uteuzi wa wanachama wanaogombea nafasi za kidemokrasia kwa kumtazama asili yake, anatoka kanda ipi, kabila, imani yake au nasaba licha ya kwenda kinyume na misingi ya Taifa letu lakini pia ni kinyume na
  matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  UVCCM kwa kauli moja tunawaamsha na kuwatumia ujumbe watanzania wenzetu hususan Vijana mahali popote walipo wavikatae na kuvikwepa vyama vya aina hiyo, wasikubali kugawanywa kwa asili zao, imani au rangi na nasaba.

  Taifa letu ni alama pana ya kuenzi na kudumisha demokrasia si tu barani Afrika lakini vile vile duniani kote, hivyo kwa umoja wetu, kwa nguvu zetu, akili na maarifa tulionayo, abadan tusijaribu kuichezea amani yetu, umoja na mshikamano wetu uliojengwa na waasisi wa Taifa letu na kukubali
  kuvishabikia vyama na viongozi wasaka madaraka kwa hila ambao ni
  wafujaji na wakandamizaji wa misingi ya demokrasia ndani ya vyama kama
  ilivyojionyesha kwa vyama vya upinzani vya Tanzania katika uteuzi wa
  wabunge EAC.

  Mchakato wa Uchaguzi ndani ya UVCCM.

  Uchaguzi Mkuu wa CCM wa mwaka 2017, unafanyika wakati ambapo CCM inatimiza miaka 40 tokea kuasisiwa kwake tarehe 5 Februari, 1977 na ni wakati ambapo nchi yetu inatimiza miaka 25 ya Mfumo wa Vyama Vingi ulioridhiwa na Mkutano Mkuu wa CCM kutokana na busara za Viongozi wake.

  Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa Chama na Jumuiya zake inaonesha mchakato wa Uchaguzi wa Jumuiya za CCM kuwa unaanza kabla ya ule wa CCM. Utaratibu huu unalenga kuwawezesha wanachama wa Jumuiya za CCM ambao watakuwa ni wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika CCM, au wale waliochaguliwa kuwakilisha Jumuiya zao katika Vikao vya CCM ili waweze kuhudhuria mikutano ya Chama inayowahusu.

  Umoja wa Vijana wa CCM umekamilisha maandalizi yote ya msingi ya awali kwa ajili ya Uchaguzi unaotarajia kuanza tarehe 1 April, 2017 ikiwemo
  kusambaza vifaa katika Mikoa na Wilaya zote nchini wa ajili ya
  kufanikisha uchaguzi kwa wakati.

  Aidha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi
  imekamilisha mapitio na uteuzi wa Makatibu wa Mikoa na Wilaya katika
  Jumuiya ambao watakuwa ndio wakurugenzi wa Uchaguzi katika maeneo yao.

  Tunaendelea kuwakumbusha Watendaji wetu muda wote kusimamia haki, ukweli na usawa lazima vijana wa CCM muda wote tuishi katika maneno na maagizo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.

  Hatutamvumilia mtendaji yeyote atakayekiuka Kanuni, Taratibu na miongozo kwa makusudi ili kufurahisha kikundi au watu fulani. Uchaguzi huu 2017 UVCCM tunataka kuidhihirishia dunia na Vyama vya Upinzani kuwa CCM ni Chuo Cha Demokrasia ulimwenguni.

  Mwisho niendelee kuwahamasisha vyema wote nchini yenye sifa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali za uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake kuanzia ngazi ya Shina, Tawi, Kata, Wilaya, Mikoa na Taifa.

  KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
  Shaka Hamdu Shaka (MNEC)

  KAIMU KATIBU MKUU

  0 0

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afaya Zanzibar Dkt. Fadhil Mohammed Abdalla akieleza mipango iliyoandaliwa ya kukabiliana na maradhi ya kipindupindu iwapo yatatokezea katika kikao kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongo chekundu Mjini Zanzibar.
  Mkuu wa Kitengo cha Afya ya Mazingira Rukaiya Mohamed Said akiwasilisha taarifa ya kikao kilichopita cha Kamati hiyo kilichofanyika mwezi uliopita.
  Afisa kutoka Jumuia ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi Zanzibar Jokha Masoud Salim akitoa mchango wakati wa kikao hicho.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Kamati ya kukabiliana na kipindupindu wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu.
  Afisa uperesheni na huduma za kibinadamu, Kamisheni ya kukabiliana na maafa Makame Khatibu Makame akitoa mada juu ya mpango wa kukabiliana na maafa Zanzibar katika cha Kamati hiyo kilichofanyika Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidongochekundu. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.  Na Khadija Khamis –Maelezo

  Mkurugenzi Kinga na Elimu ya Afya Dkt Fadhil Moh’d Abdalla ameitaka jamii kubadili tabia kwa kuweka mazingira yaliyowazunguka safi na kuhakikisha wanatumia maji safi na salama ili kujiepusha na maradhi ya mribuko .

  hayo ameyasema wakati wa kikao cha kamati ya kitaifa ya kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti maradhi ya kipindupindu hasa kipindi hichi ambacho mvua za masika zimeanza kunyesha.

  Alisema lengo kuu la kamati hiyo ni kufanya tadhmini ya muendelezo wa mpango kazi wa kudhibiti maambukizi ikiwemo kutoa elimu ya usafi wa mazingira kwa jamii na kupambana na mazingira hatarishi katika maeneo mbali mbali ya Manispaa ya Zanzibar.

  Ameishauri Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kuhakikisha maji yanayotumiwa na wananchi yapo katika hali ya safi na salama kwa kutia dawa vianzio vyote vya maji na kuwataka wananchi kuacha tabia ya kufanya uharibifu kwenye njia za maji kwa kutoboa mabomba yanayosamba maji .

  Alieleza changamoto zinazowakabili kwa sasa ni kuwepo kwa wafanyabiashara wasiofuata taratibu za usafi wa chakula na mazingira katika utendaji mzima wa biashara zao.

  Alisema uzoefu unaonyesha maradhi ya kipindupindu mara nyingi hutokea wakati wa kipindi cha mvua hivyo tahadhari zinahitajika katika kuweka mazingira katika hali ya usafi

  “Wananchi wahakikishe wanakunywa maji ya kuchemsha au kuyatia watergard ili kuweka tahadhari wakati huu wa kipindi cha mvua za masika kwani kunauwezekano mkubwa wa kuchafuka vyanzio vya maji kwa kuingia maji machafu,” Alisema Mkurugenzi kinga .

  Aliwashauri wananchi wanaoishi sehemu za mabondeni kuchukue juhudi za makusudi kuhama katika maeneo hayo ili kuepuka majanga katika kipindi hichi cha mvua za masika

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumpokea mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akipiga ngoma mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam, Pembeni yake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpigia makofi.

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn wakati nyimbo za mataifa mawili (Tanzania na Ethiopia) zikipigwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akishuka kwenye jukwaa kwenda kukagua gwaride la Heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikagua Gwaride la heshma lililoandaliwa kwa ajili yake.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza mkutano wa pamoja na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akifurahia jambo wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akizungumza na Wanahabari Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya mkutano wake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi kwa mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Shamra shamra zikiendelea wakati wa kuwasili Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Dessalegn akikaribishwa kwa kupewa ua na mtoto Xyleen Mapunda mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal One jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

  0 0

  Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel (kulia), akizungumza katika Warsha ya siku moja kwa Wanafunzi wa vyuo vikuu, ikiwa ni katika kuwahamasifa wanafunzi hao kuufahamu umuhimu wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira jijini Arusha, Machi 30, 2017. Jumla ya Wanafunzi 190 kutoka vyuo mbalimbali nchini, walihudhulia Warsha hiyo.
  Naibu Balozi wa vijana wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Suzane William Mollel, akisikiliza maoni ya mmoja wa wanafunzi waliohudhulia kwenye warsha hiyo, juu ya ufahamu wake wa Ushirikiano wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Makumira jijini Arusha, Machi 30, 2017.

  0 0


  Waziri wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako mapema leo asubuhi amewasili katika Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Nelson Mandela Arusha kwa ajili ya Uzinduzi wa mpango wa African Capacity unaofadhiliwa na Benki ya ADB.
   
  Akizungumza na wanafunzi wa Chuoni hapo Profesa Ndalichako amesema Atawachukulia hatua kali waajiri katika sekta ya Elimu watakaowakataza baadhi  ya wafanyakazi waliopata ufadhili wa kwenda masomoni kujiendeleza .

  Pia akiwa kwenye uzinduzi huo waziri alifanikiwa kutembelea maabara mbalimbali za idara tofauti za Chuo hicho zinazotumika na wanafunzi kwa ajili ya majaribio na pia alipata wasaaa wakutembelea shamba la migomba lililopo nje kidogo ya chuo hicho.
  Waziri wa Elimu akisalimia na watumishi ya Chuo cha Nelson Mandela leo Asubuhi baada ya kuwasili chuoni hapao .Waziri wa Elimu profesa Joyce Ndalichako ( katikati ) Akimsikiliza Mkuu wa Maabara ya Taasisi ya Chuo Kikuu cha Nelson Mandela jijini Arusha .
  Pichani ni wanafunzi wa PHD in material science and Energy lub,Agatha Wagotu na Joyce Elisadiki wakiwa ndani ya Maabara wakifanya majaribio.
  Habari Picha na Imma Msumba.
   
   
   

  0 0


   Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan  Abbasi, (wapili kulia), akipeana mikono na Kaimu Meneja wa Uendeshaji wa BoT, tawi la Zanzibar, Bi.Graceana Bemeye, muda mfuoi baada ya kufungwa kwa semina ya mafunzo wka waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, kwenye ukumbi wa BoT, tawi la Zanzibar mjini Unguja, leo Machi 31, 2017. Wakwanza kushoto ni Kaimu Meneja Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina.
  Dak. Hassan Abbasi akizungumza wakati akiwasilisha mada juu ya Sheria mpya ya Huduma za vyombo vya Habari wakati wa kufunga semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha mjini Zanzibar
  Kaimu Meneja wa Uendeshaji wa Bot, tawi la Zanzibar, Bi.Graceana Bemeye, (aliyesimama), akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Bi. Vicky Msina
  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MKURUGENZI wa Idara ya Habari MAELEZO, ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (pichani juu), ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), kwa kuandaa semina ya mafunzo kwa waandishi wa habari za Uchumi na Fedha, iliyomalizika mjini Unguja, Zanzibar leo Machi 31, 2017.

  Dkt. Abaasi alisema, BoT, kama taasisi ya serikali inao wajibu wa kuwapatia habari wananchi kupitia waandishi wa habari na uamuzi wa kutoa mafunzo hayo ni ishara tosha ya ushirikishaji wa waandishi katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa habari sahihi kutoka BoT.

  "Tumekutana hapa wakati serikali imepitisha sheria mbili, moja ni ile inayohusu huduma za vyombo vya habari, na ya pili ni ile ya haki ya waandishi kupata taarifa kutoka taasisi za serikali na mimi nikiwa kama msimamizi mkuu katika eneo hili la utoaji habari kwenye taasisi za umma, ninawaalika mtusumbue sana katika kupata taarifa maana utoaji wa habari kwa sasa si suala la utashi tena bali ni  la kisheria." Alisema Dkt. Abbassi.

  Dkt. Abbasi pia aligusia wajibu wa waandishi wa habari katika kutekeleza majukumu yao chini ya sheria ya sasa,

  “Lengo la sheria hii ni kuwajengea heshima Waandishi wa habari ili waweze kufanya shughuli zao katika mazingira ya heshima na bora, tofauti na hivi sasa ambapo taaluma ya uandishi wa habari imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchafuliwa na baadhi ya waandishi ambao kimsingi hawana sifa za kuwa waandishi wa habari.” alisema na kuongeza,
  “kila taaluma, iwe taaluma ya Sheria, iwe taaluma ya udaktari, lazima wote walio kwenye taaluma hizo wanasimamiwa na kanuni na sheria, kwa hivyo sheria hii itatenganisha kati ya waandishi wana taaluma na wale ambao si wana taaluma.” Alisema.
  Dkt. Abbasi pia amekanusha habari kuwa Serikali kupitia sheria hii inataka kuwazuia baadhi ya watu wasifanye kazi za uandishi kwa kigezo cha kitaaluma.
  “Hii si kweli, hata Yule anayeitwa Kanjanja, anaweza kufanya kazi ya uandishi lakini kwa kuzingatia kanuni mpya zinazoangazia sheria hii mpya, hivyo hata wale ambao si wanataaluma na wanafanya kazi za kiuandishi wanayo fursa ya kufikia vigezo vya kuitwa waandishi wa habari kwa mujibu wa kanuni hizo ambazo tayari zimeanza kufanya kazi.” Alifafanua.
  Aidha Dkt. Abbasi amesema, Sheria hii ya sasa inatoa fursa kwa chombo cha habari kuomba radhi na kuchapisha habari ambazo zina makosa kwa nia ya kuzisahihisha, na swala hilo likakubaliwa kisheria na halitapelekwa mahakamani chini ya kifungu cha 40 cha sheria ya Huduma za vyombo vya habari.
  Akifunga maunzo hayo, Kaimu Meneja Uendeshaji wa BoT tawi la Zanzibar, Bi. Graceana Bemeye aliwashukuru waandishi hao kwa ushiriki wao uliotukuka. "Niwahakikishie kuwa BoT, inatambua umuhimu wa waandishi wa habari katika shughuli zake za kila siku, hivyo tutaendelea kutoa mafunzo haya ili kujenga uwezo wa waandishi kuandika kwa usahihi habari zinazohusu BoT kwa manufaa ya taifa.Aidha Kaimu Meneja Uhsuiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina, alisema mafunzo yaliyotolewa na BoT kwa waandishi hao wa habari ni moja ya majukumu ya BoT katika kuelimisha umma na kwamba mafunzo hayo yalijumuisha waandishi wa habari kutoka vyombo vya habari vya Bara na Zanzibar, vikiwemo vile vya kielektroniki, magazeti na Mitandao ya Kijamii. 

  "Lengo ni kuhakikisha tunawajengea uwezo waandishi wa habari za Uchumi na Fedha ili waweze kuripoti kwa usahihi habari za BoT. "Lakini pia BoT, kupitia website yake imeanza kutafsiri baadhi ya taarifa zake kwa lugha ya Kiswahili ili kutoa wigo mpana kwa wananchi kuzielewa taarifa za BoT." Alisema. Akizungumza kwa niaba ya washiriki wa semina hiyo, Bw. Ezekiel Kamwaga, aliishukuru BoT kwa kuandaa semina hiyo na kuhimiza ushirikiano zaidi katika utoaji wa habari zinazohusu taasisi hiyo nyeti hapa nchini.


   Kaimu Meneja Uhsuiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bi. Vicky Msina
   Mwenyekiti wa Semina, Bw. Ezekiel Kamwaga, akizungumza
   Afisa Uhusiano Mkuu kutoka Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki wa BoT, Bw. Lwaga Mwambande
   Baadhi ya wanasemina wakisikiliza hotuba
   Maafisa wa BoT, Bw.Lusajo Mwankemwa, (kushoto), na Bi.Flora Mkemwa
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, (Kushoto), akipeana mikono na Mmiliki wa K-VIS Blog, Bw. Khalfan Said mwishoni mwa semina hiyo
  Dkt. Abbasi akitoa semina
  Dkt. Abbasi (kushoto), akimsikiliza Mchumi Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, BoT, Bw.Lusajo Mwankemwa, wakati wa ufungaji wa semina hiyo


  Mwandishi wa habari wa Sauti ya Ujerumani, (DW),  mwenye makazi yake Zanzibar, Bi. Salma Said, akizungumza

  Bi. Vicky Msina, (kushoto) na Bw. Lusajo Mwankemwa
  Picha ya pamoja


  0 0


  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akitubia wananchi wa wilaya ya Muheza na wadau wa elimu  katika maadhimisho ya ya Juma la Elimu wilayani Muheza kushoto ni Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa
  Kaimu Afisa Elimu Msingi wilayani Muheza,Stuart Kuziwa akizungumza katika maadhimisho hayo ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani humo


  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akimsikiliza kwa umakini Kaimu Afisa Elimu Msingi wilaya ya Muheza,Stuart Kuziwa kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka
  Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza,Dkt Paul Kisaka akizungumza wakati wa maadhimisho hayo kushoto akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wakati wa maadhimisho hayo
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
  Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akikagua maonyesho ya Juma la wiki ya Elimu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Jitegemee wilayani Muheza
  Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia akipata maelekezo kutoka kwa Mwanafunzi wa Kidato cha nne  Shule ya Sekondari Chief Mang'enya,Janet Justice wakati wa maadhimisho ya Juma la wiki ya Elimu 
  Wanafunzi wa Shule za Msingi kutoka Maeneo mbalimbali wilayani Muheza wakiwa kwenye maandamano kuelekea kwenye uwanja wa Jitegemee ambako kumefanyika maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu.
  Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
  Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mlingano wenye mahitaji maalumu ya ulemavu wa kutokusikia na wale wenye ulemavu wa macho wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo
  Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.
  Wanafunzi kutoka shule mbalimbali wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza kunakofanyika Juma la Wiki ya Elimu.

  Umati wa wanafunzi na wananchi wilayani Muheza wakiwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho hayo

  Wanafunzi wa Shule ya Msingi Muheza wakitumbuiza kwenye maadhimisho hayo

  Wanafunzi wa shule ya Sekondari Mkurumuzi wakicheza ngoma kwenye maadhimisho hayo
  Walimu wakishriki kwenye mchezo wa kukimbiza kuku kwenye maadhimisho hayo
  Walimu wakishinda kwenye mchezo wa kuvuta kamba kwenye kilele cha maadhimisho ya Juma la Wiki ya Elimu wilayani Muheza Mkoani Tanga
  Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

  0 0


older | 1 | .... | 1188 | 1189 | (Page 1190) | 1191 | 1192 | .... | 1897 | newer