Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1184 | 1185 | (Page 1186) | 1187 | 1188 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,(katikati) wakifuatana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe,Ayoub Mohamed Mahmoud (mbele) walipokuwa wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani jana katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma (Mabodi),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Mhe,Borafya Silima na Waziri wa Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto Mhe,Moudline Cyrus Castico (kulia) wakiwa katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani jana

  Wakuu wa Wilaya mbali mbali za Unguja wakiwa katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar jana


  Mwimbaji wa Kikundi cha Calture Misical Club Iddi Suwedi alipokuwa akiimba wakati wa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar jana

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Juma Abdalla Juma Mabodi (katikati) wakiwa na Viongozi wengine katika Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Dk.Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar jana

  Baadhi ya Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri wakiwa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar jana,

  Wasanii wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini kikitoa burudani wakati wa Tamasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar jana,
  Mwimbaji wa Kikundi cha Big Star cha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mjini Munira Mngwame Ame alipotoa burudani ya wimbo na Kikundi chake jana wakati wa amasha la Taarab rasmi ya kusherehekea Ushindi wa CCM na Kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein kwa kutimiza mwaka mmoja tokea kuchaguliwa kuwa Rais,katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Mjini Zanzibar,[Picha na Ikul.]27/03/2017.

  0 0

  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma (hawapo Pichani) kuhusu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuachiwa huru kwa msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Anastazia Wambura.

  Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kutokana na wimbo wake Wapo unaosadikiwa kukiuka madili.

  Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe amesema kuwa Msanii huyo ametumia haki yake ya kikatiba ya kujieleza na ni Haki ya kila Mtanzania kujieleza kwa namna moja au nyingine pasipo kuvunja katiba ya Nchi.

  Waziri Mwakyembe amesema Mwanamuziki huyo ni Mmoja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na Mhe Rais kutokana na kazi zake za muziki zinazoelimisha na kueleza changamoto mbalimbali zinakumba taifa letu.

  “Mhe. Rais anaupenda wimbo wa msanii huyu na ameshauri auboreshe zaidi asipunguze chochote ila aongezee tu tabia nyingine ambazo hajazitaja katika wimbo wake” alisisitiza Dkt Mwakyembe.

  Aidha Mhe. Waziri ameeleza kuwa Mhe Rais ametoa ushauri kwa msanii huyo kuboreshe wimbo huo zaidi kwani mengi aliyoyaongelea katika wimbo wake yanatokea katika jamii na kutolea mfano kama akiboresha na kuelezea zaidi kuhusu wakwepa kodi,wauzaji, wasambazaji na watumiaji madawa ya kulevya,na watanzania wasipoenda kufanya kazi kwani makundi haya yote yapo katika jamii.

  0 0

   Mkurugenzi wa Masoko wa Basata, Vivian Shaluwa akizungumza na wadau walifika katika hafla ya ugawaji vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika mtihani wa somo la Sanaa.
   Baadhi ya washiriki waliofika kushuhudia ugawji huo wa vyeti
   Rais wa Shirikisho la Sanaa Maonyesho , William Chitanda akizungumza juu ya umuhimu wa wanafunzi kufanya sanaa pindi wanapokuwa mashuleni
   Baadhi wanafunzi wa Sekondari wakiwa wana fatilia hafla hiyo
   Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo wakitoa burudani katika sherehe za kukabidhi vyeti kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliofanya vizuri katika mtihani ya kidato cha nne
   Afisa wa Basata Bonnah Masenge akizungumza na wadau wa Sanaa walifika katika hafla hiyo
   Mwanamuziki mkongwe John Kitime akitoa somo kwa wanafunzi ju ya ushikaji wa kipaza sauti hili waweze kusikika vizuri
   Mwanafunzi Royola Sekondari , Shadrack Mboya akikabidhiwa  Cheti na psesa Taslim shilingi laki tano baada ya kufanya vizuri katika mtihani wa kidato cha nne
   Mwanafunzi wa Royola Sekondari , William Mukasa  akikabidhiwa zwadi ya cheti na fedha tslim shilingi laki mbili na amsini
   Mwanafunzi wa Royola Sekondari Josia Sooi akikisitiziwa jambo mara abaada ya kupewa zawadi yake na William Chitanda
   Wanafunzi  Royola Sekondari walifanya vizuri wakiwa katika picha ya pamoja
  Mwanafunzi wa Azania Sekondari , Benjamini Kulwa akipokea cheti na fedha kutoka kwa mgeni rasmi William Chatanda

  0 0

  BCO
   Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akipokea sehemu ya vifaa vya michezo kutoka kwa Mdau Mkubwa wa Michezo nchini, Athuman Tippo maarufu kama Zizzou, kwa ajili ya kuhamasisha Michezo kwa vijana wa Wilaya hiyo, kupitia Kampeni ya Michezo kwa vijana ya Uchumi Cup iliyoianzisha DC Gondwe kwa ajili ya kuwahamasisha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia fursa ya Michezo. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Duka la Vifaa vya Michezo la Zizzou Fashion, Sinza Jijini  Dar es salaam.
  Sehemu ya vifaa vya michezo vilivyokabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.

  0 0

  Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akionyesha mifuko ya saruji 500 aliyochangiwa na wadau mbalimbali ili kusaidia katika ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi,ambao umezinduliwa rasmi
  Mbunge wa jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud Jumaa akishiriki nguvu kazi na baadhi ya wananchi katika uzinduzi rasmi wa ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi .(picha na Mwamvua Mwinyi)

  ……………..

  Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

  WADAU na viongozi mbalimbali jimbo la Kibaha Vijijini,wamejitokeza kumuunga mkono mbunge wa jimbo hilo, Hamoud Jumaa kufanikisha ujenzi wa uzio wa kituo cha afya Mlandizi.

  Ujenzi huo unatarajiwa kugharimu mil. 200 na ukikamilika utaondoa kero hiyo iliyodumu miaka mingi . Jumaa aliyasema hayo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi huo ambapo hivi karibuni alianza kwa kuweka alama ya msingi.

  Alieleza kwamba, wameshakubaliana na wananchi na wenyeviti wa vitongozi 26 kuwa kila kitongoji kitachangia sh.240,000 . “Madiwani kila mmoja atachangia 240,000 hivyo wanatarajia kukusanya zaidi ya sh. mil.4, mfuko wa jimbo sh. mil. 4 kununulia tofali zitakazoanzia ujenzi”alisema .

  Hata hivyo,tayari wadau wamemkabidhi mifuko 500 ya saruji iliyogharimu sh. mil. 6, kokoto tani 7 kwa sh. mil. 9.1, mchanga mil. 2.4 tofali sh. mil 8.4, nondo tani moja sh. mil. 3.6.

  Jumaa alisema ,kwa msingi kero ya ukosefu wa uzio ni kubwa inayosababisha usumbufu kwa wagonjwa kutokana na watu,pikipiki kupita na kupiga kelele.

  Alieleza kuwa ujenzi huo utafanyika kwa awamu nne ambapo awamu ya kwanza unatarajia kutumia zaidi ya sh. mil. 40. Baada ya uchimbaji wa msingi itafuata kumimina zege kisha kuanza ujenzi wa tofali na awamu hiyo itachukua wiki mbili.

  Jumaa alisema hadi sasa ni juhudi za mbunge na wafadhili ambazo wanategemea kuanza ukuta wa mbele, kuchimba msingi na kumwaga zege . “Tumezindua rasmi ujenzi ,lengo ni kutekeleza moja ya vigezo vya kituo chetu kupanda hadhi ya hospitali ya wilaya”

  Alitaja vigezo vinavyotakiwa kuwa ni pamoja na kuwepo kwa chumba cha upasuaji na kuhifadhia maiti ,kuongeza watumishi wa afya, madaktari na kigezo kikubwa ni ujenzi wa ukuta.

  Jumaa alisema, kwa sasa amejipanga kwenda sambamba na kauli mbiu yake ya “Sisi kwanza serikali baadae “. Anawaomba wadau wa afya na serikali kuendelea kumuunga mkono ili tatizo hilo libakie historia.

  Mbunge huyo alimshukuru makamu wa Rais mama Samia Suluhu kwa kuahidi kushirikiana nae kujenga uzio huo. Diwani wa kata ya Mlandizi Ephrasia Kadala alimpongeza Jumaa kwa kuanzisha suala hilo na kusema kwa muda mrefu kituo hicho kilikuwa kikipata usumbufu.

  Makamu Mwenyekiti Godfrey Mwafulilwa alisema walipokea wazo la ujenzi kutoka kwa mbunge huyo kwenye kikao ambapo alishauri kwenye mpango wa mwaka 2016/2017 halmashauri iangalie namna ya kuchangia.

  Tatu Jalala Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji Mdogo wa Mlandizi alisema wamekubaliana kila mwenyekiti wa Mji huo atachangia sh.240,000 kwa ajili ya ujenzi huo

  0 0

  Jana March 26,2017 ilikuwa siku muhimu kwa mwanahabari wa 102.5 Lake Fm Mwanza na mwanablogu wa BMG, George Binagi wa Tarime Mara pamoja na Miss Upendo Kisaka wa Moshi Kilimanjaro baada ya kuuaga ukapela.

  Wapendanao hao walifunga pingu za maisha katika Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza na baadaye hafla kufanyika Ukumbi wa Sun City Hotel, Ghana Green View Jijini Mwanza.

  "Ahsanteni nyote mliotusaidia kutimiza ndoto yetu kubwa katika maishani yetu. Familia yangu, ndugu, jamaa na marafiki zangu. Waumini wote wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Jijini Mwanza chini ya Mchungaji Daniel Kulola na kila mmoja kwa nafasi yake, Mungu awabariki. 

  Mmenionesha upendo wa ajabu mno.
  Wazazi wangu hususani mama mpendwa, nimetimiza deni mliloniachia duniani, hakika sasa mtapumzika kwa amani, pahali pema, peponi, Amina. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, Mungu atuongoze vyema". Mr & Mrs George Binagi.
  Shukurani za pekee pia ziwaendelee best man na best lady, Mr and Mrs, Joel Maduka kutoka Storm Fm Geita na Maduka Online kwa kufanikisha shughuli hiyo kwenda vyema.

  BMG inakusihi uendelee kutazama picha za awali za shughuli hiyo wakati wataalamu wetu wakiendelea kukuandalia picha nyingine ikiwemo picha za kanisani.

  0 0

  Habari ya kazi mkuu, pokea code Zao la korosho nchini lipo hatarini kuporomoka kufuatia kugundulika kwa ugonjwa mpya wa mnyauko wa mikorosho ambao umeua mikorosho zaidi ya elfu 40 hadi sasa katika mikoa ya LINDI na MTWARA.

  0 0

  Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na waandishi wa habari juu ya kufanyika Kongamano la Kimataifa la maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na kensa ya ubongo litakaloanza kesho katika kituo cha Neurosurgical Mnazimmoja.
  Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib (kushoto) na Dkt. Mahmoud Quresh wakimsikiliza Waziri wa Afya (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kituo cha NED Mnazimmoja.
  Dkt. Mahmoud Quresh anaesimamia upasuaji wa maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na kensa ya ubongo katika wodi ya maradhi hayo Hospitali ya Mnazimmoja akitoa ufafanuzi wa masuala ya waandishi wa habari kuhusu kufanyika Kongamano hilo Zanzibar.
  Mwandishi wa habari mwandamizi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ramadhani Ali akiuliza swali katika mkutano wa waandishi uliofanyika kituo cha NED Mnazimmoja.

  Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

  …………………….

  Na Ramadhani Ali/Maelezo Zanzibar

  Zanzibar itakuwa mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la maradhi ya vichwa maji na uti wa mgongo na kensa ya ubongo litakalofanyika kwa siku tatu kuanzia kesho katika kituo cha maradhi hayo Hospitali Kuu ya Mnazimmoja.

  Akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha upasuaji wa maradhi hayo NED, Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo alisema nchi tisa kutoka Afrika, Ulaya na Marekani zitashiriki Kongamano hilo.

  Amesema Zanzibar imepewa nafasi hiyo kutokana na juhudi za Rais Shein katika masuala ya elimu na utafiti pamoja na ubora wa kituo hicho na utulivu wa wananchi.

  Waziri Mahmoud ameongeza kuwa tokea kuanzishwa kituo hicho miaka miwili iliyopita zaidi ya wananchi 600 kutoka ndani na nje ya Zanzibar wamefanyiwa upasuaji ambapo asimilimia 92 zimefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

  Amesema kuwepo kwa kituo hicho Zanzibar kimeipunguzia Serikali mzigo wa kutumia fedha nyingi kuwapeleka nje wagonjwa wanaokabiliwa na matatizo hayo ambapo gharma zake ni zaidi ya shilingi milioni 12 kwa mgonjwa mmoja.

  Ameeleza kuwa kongamano hilo litakalosimamiwa na Daktari bingwa wa maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na kensa ya ubongo kutoka Marekani Professa Paul Young litakuwa ni fursa pekee kwa madaktari wa Hospitali za Serikali na za watu binafsi kujifunza njia bora za kutibu maradhi ya hayo.

  Akieleza malengo ya baadae ya Serikali ya kituo hicho Waziri Mahmoud Thabit Kombo alisema ni kufungua tawi Pemba na kukifanya kuwa kituo kikuu kwa nchi za Afrika Mashariki.

  Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib alisema juhudi zinaendelea kusomesha madaktari wazalendo wa kada mbali mbali ikiwemo maradhi ya vichwa maji, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu ili kupata madaktari wa kutosha watakaoendesha kituo hicho baada ya kuondoka wataalamu wa kigeni waliopo hivi sasa.

  0 0

  Na Lydia Churi- Mahakama, Tanga

  Mahakama Kuu Kanda ya Tanga inakusudia kuwanunulia Mahakimu wake 67 kompyuta Mpakato (Laptops) ili kurahisisha kazi zao na kuondosha mashauri kwa wakati katika Mahakama mbambali za mkoa wa Tanga.

  Akizungumza kwa niaba ya Mtendaji wa Mahakama Kuu kanda ya Tanga, Afisa Utumishi wa Kanda hiyo, Bwana Farid Mnyamike amesema kompyuta hizo zitawasaidia waheshimiwa Mahakimu katika kuandika hukumu ili wananchi waweze kupati haki kwa wakati.

  Alisema katika kanda yake, baadhi ya Mahakama zina uhaba wa watumishi hasa Makatibu Muhtasi pamoja na vitendea kazi jambo ambalo limekuwa likichelewesha utolewaji wa hukumu pamoja na upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati. Aliongeza kuwa kwa Mahakimu kupatiwa kompyuta hizo kutarahisisha upatikanaji wa haki.

  Aidha, Afisa Utumishi huyo alisema hivi sasa Mahakama Kuu kanda ya Tanga inao mpango wa kuhakikisha inazipatia umeme baadhi ya Mahakama za Mwanzo kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) ili kurahisisha upatikanaji wa nakala za hukumu kwa wakati.

  Mahakama ya Tanzania ilimwekea malengo kila Hakimu nchini ya kuhakikisha anasikiliza kesi zaidi ya 250 kwa mwaka ili kuondosha mrundikano wa mashauri yaliyoko kwenye Mahakama mbalimbali nchini.

  Bwana Mnyamike aliitaja mipango mingine iliyowekwa na Kanda yake katika kuitekeleza nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania kuwa ni kuwapeleka Mahakimu wenye mashauri machache kwenye Mahakama zenye mashauri mengi ili kuhakikisha mashauri yote ya muda mrefu yanaondoshwa na yaliyofunguliwa yanamalizika kwa wakati.

  Ili kuleta mabadiliko ndani ya Mahakama, Mahakama ya Tanzania iliandaa Mpango Mkakati wa Miaka mitano 2015-2020 unaotekelezwa kupitia nguzo tatu ambazo ni Utawala bora, Upatikanaji wa Haki kwa Wakati na pamoja na kurudisha na kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama.

  0 0

   Mkurugenzi  wa  Hope Art  Factory Hellen Tegga akizungumza katika mafunzo ya wanawake juu ya ujasiliamali  na kupaza sauti yaliyofanyika Millenium Tower jijini Dar es Salaam.
   Mratibu  wa Mfuko  Graca Machel , Manuel Akinyi akitoa mada katika mafunzo ya wanawake juu ya ujasiliamali  na kupaza sauti yaliyofanyika Millenium Tower jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi  wa  Hope Art  Factory ,Hellen Tegga akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wanawake  ya Ujasiliamali  , Ainde Ndanshau yaliyofanyika katika ukumbi wa Milllenium Tower jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi  wa  Hope Art  Factory ,Hellen Tegga akimkabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo ya wanawake  ya Ujasiliamali  ,  Mrcy Mchechu  yaliyofanyika katika ukumbi wa Milllenium Tower jijini Dar es Salaam.
  Washiriki wakiwa katika mafunzo ya wanawake yaliofanyika katika ukumbi wa Milleniumm Tower jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)
  Picha ya pamoja.

  0 0


  0 0

  Mgeni Rasmi Bw. Maduka Paul Kessy, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (aliyesimama) akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kwa washiriki kutoka Idara za Sera na Mipango za Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali. Wengine ni Bi. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (kulia) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (kushoto).
  DOM1
  Dkt. Lorah Madete, Kaimu Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Uchumi Jumla, Tume ya Mipango (aliyesimama), akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi ili afungue mafunzo hayo ya siku tano.  Waliokaa ni Bw. Maduka Paul Kessy, Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango (katikati) na Bw. John Mduma, Mhadhiri Mwanamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  DOM3
  Washiriki wa Mafunzo wakimsikiliza kwa makini Mgeni Rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
  DOM4
  Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada zilizotolewa.
  DOM5
  Dkt. John Mduma, Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (aliyesimama), akitoa neno kwa washiriki wa mafunzo mara baada ya mafunzo hayo kufunguliwa rasmi.
  DOM6
  Washiriki wa mafunzo kuhusu Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma kutoka Idara za Sera na Mipango za Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala za Serikali pamoja na wawezeshaji wa mafunzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
  …………………………………………………………………………….
  Na Thomas Nyindo.

  Maofisa wa Idara za Sera na Mipango kutoka Wizara, Idara na Wakala za Serikali wametakiwa kuongeza ufanisi na ubunifu katika kuandaa na kusimamia miradi ya maendeleo ili kuharakisha malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

  Kauli hiyo imetolewa leo na  Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bw. Maduka Kessy wakati akifungua mafunzo ya Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji wa Umma yanayoendelea katika ukumbi wa Chuo cha Mipango Dodoma.

  Kessy alieleza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maofisa wanaosimamia masuala ya Sera na Mipango katika kuibua na kutekeleza miradi ya maendeleo, hususan, ile inayogharamiwa kwa fedha za Serikali ili kufanya Tanzania kuingia kwenye nchi za kipato cha kati kama ilivyoaninishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo.

  “Mipango ya maendeleo tunayojiwekea, kama taifa, inapaswa kutafsiriwa katika miradi na programu za utekelezaji, hivyo mafunzo haya yatatusaidia kuongeza ufanisi, ubunifu na uwajibikaji katika kuandaa miradi na kusimamia miradi yenye tija kwa wananchi,” alisema Kessy.

  Aliwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo kuwa wao ni miongoni mwa wadau muhimu katika kuifanya Tanzania ipige hatua za maendeleo kwa kuwa ndio wanaohusika katika kupanga na kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

  Aidha, Kessy alieleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia washiriki kuongeza ufanisi na ubunifu katika kuchagua miradi, kutafuta fedha za ugharamiaji na  kuboresha uratibu wa kufungamanisha uwekezaji wa umma kwa kubainisha hatua za kufuata katika kujumuisha miradi ya maendeleo katika bajeti za maendeleo.

  “Mwongozo huu utawasaidia kufanya maamuzi katika kuchagua miradi sahihi ya uwekezaji katika sekta ya umma na kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wake. Sote tunafahamu kuwa azma yetu ya maendeleo kitaifa ni kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo 2025,” alisema.

  Kaimu Katibu Mtendaji huyo alieleza kuwa zipo changamoto zinazokabili usimamizi wa miradi ya maendeleo, kuanzia hatua ya kubuni, kutekeleza hadi kukamilisha miradi hiyo. Kwa hiyo Mwongozo wa Usimamizi wa Uwekezaji waRasilimali za Umma ni mojawapo ya maandiko muhimu ambayo yamebuniwa kukabiliana na changamoto hizo.

  0 0  0 0

  Faida ya Hifadhi endelevu ya Mazingira. Pichani ni eneo la Ngaresero Wilaya ya Meru ambapo kuna uhifadhi mzuri wa mazingira. Hata hivyo eneo hilo limeanza kuvamiwa na wananchi kwa shughuli za kibinadamu na kuhatarisha uhai wake. Waziri Makamba ametembelea eneo hilo na kumtaka Bw. Timoth Leach mmiliki wa Ngaresero Mountain Lodge kufanya ukaguzi wa mazingira mara moja ili kubaina matumizi sahihi ya rasilimali maji.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Edward Moringe Sokoine. Waziri Makamba yuko katika ziara ya kikazi Mkoani Arusha na alitembelea msitu wa Enguiki na Lendikinya kisha alizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara.

  0 0


   Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye wakitia saini hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma akishuhudia makabidhiano hayo ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof Elisante Ole Gabriel.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Nape Moses Nnauye wakibadilishana  hati za makabidhiano rasmi ya Ofisi yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara Mjini Dodoma.  0 0

   Baadhi ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na  Serikali za Mitaa wakionyeshwa  mabati aliyoyanunua mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mlanda ,Iringa Vijijini ,Bi. Konjeta Lyambafu aliyevaa kitambaa kichwani. Kushoto kwake Mwenyekiti wa kamati hiyo Venance Mwamoto akimkabidhi fedha zilizochangwa na wajumbe kuongeza uwezo wa mlengwa huyo kukamilisha mabati ili aezeke nyumba yake iliyoko nyuma yao kwa bati.
   ‘’Ninaishukuru serikali kupitia TASAF kwa kuniwezesha kuboresha maisha kwa kujenga nyumba ya bati na kumudu kuwatunza na kuwasomesha wajukuu zangu wanane ’’ ndivyo mmoja wa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini Bi. Claudia Kanyita mkazi wa kijiji cha Mlanda, wilaya ya Iringa Vijijini anavyoelekea kuwaeleza wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Angellah Kairuki .
   Mmoja wa walengwa wa TASAF katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa Vijijini Claudia Kanyita akiwa na wajukuu zake watatu alioachiwa baada ya watoto wake kufariki, akitoa maelezo kwa kamati ya kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa iliyotembelea kijiji hicho kuona utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF. Nyumba inayoonekana nyuma yao imejengwa na Mlengwa huyo kwa ruzuku ya TASAF.Wa  kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Ladislaus Mwamanga.
   Wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge wavutiwa na jitihada za mlengwa wa TASAF Bi.Claudia kijijini Mlanda na kumchangia fedha ili aanzishe mradi wa kumwongea kipato, fedha hizo alikabidhiwa na Waziri Kairuki.
   ‘’Mgeni njoo mwenyeji apone ’’ndivyo ilivyo kwa mlengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya masikini wa  kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa vijijini  Konjeta Lyambafu aliyechangiwa fedha na wajumbe wa  kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa ili aweze kuongezea fedha anazozipata kupitia ruzuku inayotolewa na TASAF kuanzisha mradi wa kujiongezea kipata. Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Venance Mwamoto akimkabidhi fedha hizo mlengwa, kulia kwao ni Waziri Angellah Kairuki . Nyumba iliyoko nyuma yao imeezekwa na mlengwa huyo kwa bati alizozinunua kupitia ruzuku kutoka TASAF  na hivyo kuboresha makazi yake.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala bora, Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na TASAF katika kijiji cha Mlunda ,Iringa Vijijini, wakati kamati ya kudumu ya Utawala na Serikali za Mitaa ilipotembelea kijiji hicho kukagua namna walengwa wa Mpango huo wanavyonufaika na mpango huo.
   Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge Utawala na Serikali za Mitaa , Venance Mwamamoto, Waziri Kairuki na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Mlanda , wilaya ya Iringa Vijijini wakati kamati hiyo ilipofanya ziara kijijini hapo kuona namna walengwa wa Mpango huo unaotekelezwa na TASAF wanavyonufaika na ruzuku itolewayo kupitia mfumo wa Uhawilishaji fedha.
  Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa wakilakiwa kwa shangwe na walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii,TASAF,katika kijiji cha Mlanda wilaya ya Iringa mkoani Iringa kuona namna walengwa hao wanavyonufaika na fedha za Mpango huo.

  0 0

  Mkurugenzi wa Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (aliyesimama) akisalimiana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Morogoro.
  Wajumbe wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mjini Morogoro.
  Viongozi waliokaa meza kuu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima, mjini Morogoro.
  Wajumbe wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza kwa makini maelezo ya mafanikio ya Mkutano wa Baraza hilo kwa mwaka 2015/2016 ambayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, Mkutano uliofanyika Mjini Morogoro.
  Katibu wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava, akizungumza wakati wa Mkutano wa 13 wa Baraza hilo, Mjini Morogoro.
  Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akitoa hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
  Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, akitoa nen0 la shukrani baada ya hotuba iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akifungua mkutano wa Baraza hilo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
  Meza Kuu (Walioketi Mbele) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dorothy Mwanyika, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa idara na vitengo wa Wizara hiyo, mjini Morogoro.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika akitoka ukumbini alipoongoza Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Mkutano unaofanyika mjini Morogoro.


  (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).


  ……………..


  Na Benny Mwaipaja, WFM-Morogoro


  Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuiletea nchi Maendeleo ya haraka kupitia falsafa ya uchumi wa viwanda utakao iwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusimamia matumizi yake ipasavyo.

  Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika Hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, wakati akifungua mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo unaofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili.

  Bi. Mwanyika amesema kuwa Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi, yana malengo ya kuongeza tija, ufanisi na ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 likisomwa pamoja na miongozo mingine linavyo elekeza. 

  Aidha amewataka wajumbe wa Baraza hilo kukumbuka maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kuhusu kusimamia ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi ya Fedha za Umma, ili kujenga uchumi wa Viwanda na kufikia maendeleo stahiki.

  “Tuunge mkono juhudi za Serikali kwa kutafsri maelekezo ya viongozi kwa vitendo ili kuthibitisha msemo usemao Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo moyo wa Serikali” alisisitiza Bi. Mwanyika.

  Pia Bi. Mwanyika amewashukuru viongozi wa Wizara hiyo kwa kufanikisha mpango wa Serikali wa kuhamia Dodoma ambapo katika awamu ya kwanza wafanyakazi 184 wameripoti mkoani humo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa makazi. Hata hivyo amewataka watumishi hao kushirikiana katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja.

  Kwa upande wake Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bw. Cyprian Kuyava, amebainisha mafanikio yaliyopatikana kutokana na maazimio mbalimbali ya Mkutano uliopita wa mwaka 2015/2016 kuwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kazi na kuongezeka kwa mshikamano miongoni mwa wafanyakazi licha ya ufinyu wa Bajeti.

  Naye Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana Mkapa amesema Watumishi wa Wizara hiyo wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali za ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na hatua ya Serikali kuhamia Dodoma.

  Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha unafanyika kwa siku mbili kuanzia Machi 27 hadi 28, 2017, huku ajenda kuu ikiwa kufanya mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka 2017/2018.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahamoud alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi mnazi mmoja mjini unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za sekondari za unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi mnazi mmoja mjini unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za sekondari za unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma pamoja na Viongozi wengine alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi mnazi mmoja Mjini Unguja katika mkutano maalum wa Walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Serikali alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi Mnazi mmoja Mjini Unguja katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za Sekondari za unguja.
  Baadhi ya Walimu wa skuli za Sekondari za Unguja wakiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
  Baadhi ya Walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja wa Mikoa Mitatu ya Unguja wakiwa katika mkutano wa pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja.
  Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiwa katika mkutano maalum wa walimu wa skuli za Sekondari za Unguja, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Zanzibar mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
  Baadhi ya Watendaji mbali mbali wakiwa katika mkutano maalum wa walimu wa Skuli za Sekondari za Unguja, uliofanyika leo katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la zamani Kikwajuni Mjini Unguja,ambapo mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.[Picha na Ikulu.] 28/03/2017.

  0 0

  Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.Mkuu wa Jengo la Sewahaji Bibi. Salome Mayenga (kushoto) na Mkuu wa Wodi namba 24 Sewahaji, Muhimbili Bibi. Georgina Kabaitileki.
  Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari kuhusu kuruhusiwa kwa mgonjwa aliyekuwa anapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi, Bibi. Neema Mwita maarufu kama mgonjwa wa Magufuli. Neema alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali hiyo kufuatia msaada wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli baada ya kuguswa na taarifa za mgonjwa huyo mapema mwezi wa pili mwaka huu hali iliyompelekea kuchukua jukumu la kumsaidia.
  Mkazi wa mkoa wa Mara ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa ajili ya matibabu ya upasuaji wa mgonjwa kufuatia majeraha ya kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi,Bibi. Neema Mwita akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (hayupo pichani) kwa kitendo chake cha kumfariji na kumsaidia kupata matibabu ya hayo wakati akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Daktari bingwa wa Upasuaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Ibrahim Mkoma.

  Picha na: Frank Shija – MAELEZ

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( kulia) na Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen,(kushoto) akizungumza wakati wa mafunzo ya kufunga wa migodi yanayotolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi.Mafunzo hayo ya siku tano yanatolewa na Serikali ya Canada jijini Dar Es Salaam.
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( katika waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakati wa mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada. Kushoto kwake ni Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen, na kulia kwake ni Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu.
  Washiriki wa mafunzo ya ufungaji migodi ambao ni Kamati ya Kitaifa ya ufungaji Migodi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.
  Afisa Rasilimali Watu Mkuu kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Suzan Kiwelu ( kulia) na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi John Shija( kushoto) wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku tano jijini Dar es salaam na Serikali ya Canada.
  Wakufunzi wa mafunzo ya ufungaji migodi kutoka nchini Canada wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ( hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.


  ………………..


  Na Zuena Msuya DSM,


  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo amefungua mafunzo ya ufungaji wa migodi yanayotolewa kwa wataalam wa mbalimbali wanaoshiriki katika Kamati ya Kitaifa ya ufungaji wa Migodi.

  Watalaam hao wanatoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazojitokeza wakati wa ufungaji wa migodi nchini.Mafunzo hayo yanatolewa jijini Dar Es Salaam,na Serikali ya Canada kwa siku tano kuanzia 27-31 machi 2017.

  Akizungumza wakati wa akifungua wa mafunzo hayo, Dkt. Pallangyo alisema kuwa mafunzo hayo yatawawezesha wataalamu wa migodi nchini kuwa na uelewa zaidi juu ya hatua zote zinazotakiwa kufuatwa wakati na baada ya ufungaji wa migodi ili kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza baada ya migodi kufungwa.

  Dkt. Pallangyo, alifafanua kuwa, kwakuwa Serikali ya Canada imejikita katika Sekta ya Madini kwa zaidi ya miaka 200, hivyo mafunzo hayo yatawasaidia wataalam wa ndani kufahamu na kujifunza namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kupitia migodi iliyokwishafungwa katika nchi hiyo ili yasijitokeze hapa nchini.

  ” Tusiwe watu wa kusoma tu na kufunga migodi, tujifunze kwa vitendo kutoka kwao makosa waliofanya wakati wa ufungaji wa migodi kwa kuwa Canada ipo katika Sekta ya madini kwa zaidi ya miaka 200 na tujirekebishe, ili makosa yaliyotokea kwa yasijirudie katika migodi yetu,” alisisitiza Dkt.Pallangyo.

  Vilevile, ameiomba Serikali ya Canada kutoa mafunzo hayo mara kwa mara na kwa muda mrefu ili kupata wataalam wengi zaidi na wenye uelewa mpana katika Sekta ya Madini hasa ufungaji wa migodi hapa nchini: Mafunzo hayo yatawawezesha watalaam kubaini kodi halisi inachotakiwa kulipwa Serikalini pamoja na njia rahisi ya utunzaji wa ardhi na mazingira kwa ujumla.

  Kwa upande wake, Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Canada, Sue Steffen aliesema kuwa nchi yake inauzoefu wa zaidi ya miaka 200 katika sekta ya madini, hivyo wameona ni busara kutoa mafunzo hayo kwa nchi zinazoendelea na zinazochimba madini mbalimbali.

  Alisema, lengo ni kutoa elimu na kuzijengea uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizowahi kujitokeza katika ufungaji wa migodi nchini Canada, na hivyo kuziepusha nchi hizo katika madhara yanayoweza kujitokeza.

  Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Mhandisi Elizabert Nkini alisema kuwa mafunzo hayo yatawaongezea uelewa zaidi katika ufungaji wa migodi, licha kuwepo kwa vigezo vya ufungaji wa migodi hiyo lakini uelewa umekuwa ni mdogo kutokana kutofahamu kwa vitendo changamoto nyingi.

  “Migodi nchini ni muhimili mkubwa wa mapato, lakini pia ni chanzo kikubwa cha uharibu wa mazingira, hivyo kama mazingira na ardhi yetu havitatunzwa vizuri kabla na baada ya kuchimbwa tutaicha nchi yetu katika hali ya jangwa isiyofaa na vyanzo vya maji vitaharibiwa, hivyo mafunzo hayo yatatuwekea utatatibu mzuri wa kuacha mazingira yetu yakiwa salama na ardhi salama pia,”. alisema Mhandisi Nkini.

  Aidha alisema kuwa elimu hiyo waliyoipata wataifikisha kwa wananchi wanaozunguka Migodi husika ili na wao wawe na uelewa juu ya ufungaji wa migodi kwa kufahamu taratibu na hatua mbalimbali za kufuata kwa maslahi yao na taifa kwa ujumla.

older | 1 | .... | 1184 | 1185 | (Page 1186) | 1187 | 1188 | .... | 1898 | newer