Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46362 articles
Browse latest View live

WAZIRI MKUU ATEMBELEA MGODI öWA BUZWAGI NA KUCHUKUA SAMPULI ZA MCHANGA

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa afanya ziara katika Mgodi wa Buzwagi 27 March 2017 kwa ajili ya kuangalia Mchanga uliowekwa katika Makontena kwa ajili yakusafirishwa nnje ya nchi katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki, na kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Bwana Stewart Hamilton
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia Sampuli ya Mchanga wenye Dhahabu unao safirishwa Nnje ya Nchi na Mgodi wa Buzwagi uliopo Kahama Mkoani Shinyanga Waziri Mkuu Alifika katika Mgodi huo 27march2017 kuangalia na kuchukua Sampuli ya Mchanga ili Serekali Ikaupime katika Maabara za Serekali
A0227 Mtaalamu wa Madini akiweka Sampuli ya Mchanga katika Mfuko kutoka katika baadhi ya Makontena na kumkabidhi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa nakuondoka nao kwa ajili ya kuupeleka katika Maabara ya Serekali inayo shugulika na Upimaji wa Madini Wziri Mkuu alifanya ziara katika mgodi wa Buzwagi 27March2017 kwalengo ya kujionea aina ya Mchanga unao safirishwa nnje ya Nnchi na Baadhi ya Migodi inayo Chimba Dhahabu hapa Nchini
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro katika Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi 27March2017 katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telaki Viongozi hao walifika kumpokea Waziri Mkuu alipofika kuangalia shughuli za Mgodi wa Buzwagi uliopo wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga

Picha zote na PMO

…………

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga katika makontena mbalimbali kwa lengo la kwenda kuyapima kwa wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.

Amesema wanataka kuona mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo unakiasi gani cha dhahabu, pia Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.” Hata hivyo tayari Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli alishatoa tangazo la kuzuia usafirishaji wa michanga kwenda nje ya nchi,”.

Waziri Mkuu alitembelea mgodi huo jana jioni (Jumatatu, Machi 27, 2017) na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kuondoa mashaka juu ya kinachosafirishwa. Sampuli hizo amezichukuwa kwenye makontena yaliyofungwa kwa ajili ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

“Tumeamua kuchukua sampuli za mchanga ambao mwekezaj anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,”

Waziri Mkuu amesema sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo wa mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.

Aliongeza kwamba “Hili lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na kukuza sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.

Wakati huohuo Waziri Mkuu amewataka Watanzania kuwa nasubira wakati Serikali ikiendelea na zoezi la kuchunguza athari zitokanazo na kusafirisha mchanga wa madini nje ya nchi. Pia amewatoa wasiwasi wafanyakazi katika migodi na wamiliki kutowapunguza na badala yake waache waendelee na majukumu yao.

Kwa upande wake Meneja Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka 2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.

Alisema kwa siku wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.

Bw. Mkanza alisema wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.

“Hapa Buzwagi tuna makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,
L. P. 980,

DODOMA.

JUMANNE, MACHI 28, 2017.

KIGOMA YANUFAIKA NA TAASISI YA MKAPA

$
0
0

Mkoa wa Kigoma umenufaika na nyumba mpya 30 za watumishi wa Afya pamoja na vitendea kazi (baiskeli 200, mabegi 225, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) kwa ajili ya wahudumu wa Afya ngazi ya jamii vikiwa na ujumla wa thamani ya Shs 1,806,985,822 billioni kutoka kwa Taasisi ya Benjamin W. Mkapa. 

Akizungumza wakati wa ukabidhiwaji wa nyumba na vitendea kazi hivyo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, alisema ya kuwa mkoa wa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa watumishi wa afya kwa asilimia 65 ya mahitaji kamili na moja wapo ya sababu zinazopelekea upungufu huo ni ukosefu wa mahali pazuri pa kuishi. 

Hivyo nyumba hizi zilizojengwa na Serikali kwa usimamizi wa Taasisi ya Mkapa zitasaidia kupunguza makali ya uhaba wa watumishi kwa mkoa wa Kigoma na nchi nzima kwa ujumla. 

Mkuu wa mkoa aliwasisitizia Wananchi pamoja na watumishi wa afya wanaotumia nyumba hizo kuzitunza na kuzithamini kwani zimejengwa kwa faida yao. Hivyo hivyo kwa upande wa vitendea kazi aliwasisi wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuvitumia kwa lengo lililokusudiwa ambalo ni kuwafikia wana jamii ndani ya jamii zao na kuweza kuwapa huduma bora za afya. 

“Napenda kutoa wito kwa mashirika yanayojenga nyumba kama vile shirika la nyumba la Taifa, Mifuko ya hifadhi ya jamii, watumishi ujenzi n.k wafirikie zaidi kujenga kwenye vituo vyetu vya Afya na Zahanati ambapo Serikali inaweza kuwapangishiwa watumishi wake” alisisitiza, Mh. Maganga

Nae mkurugenzi wa halmashuri ya kigoma Bi. Hanji Yusuph alisema, halmashauri ya wilaya ya kigoma pekee ina uhitaji wa nyumba 166 na kufikia siku ya makabidhiano halmashauri ya wilaya ya kigoma ilikuwa na nyumba 56, hivyo kupatiwa nyumba 10 inaongeza na kuwa 66. Bado kuna uhitaji wa nyumba 100. 

Nae Dr. Ellen Mkondya-Senkoro, alifafanua kuwa nyumba hizo mpya 30 za wahudumu wa afya na vitendea kazi vya watumishi wa Afya ngazi ya jamii vimetolewa kupitia miradi miwili ya Taasisi ya Benjamin Mkapa ambayo wa kwanza ni mradi wa Uimarishwaji wa Mifumo ya Afya ambao ulifadhiliwa na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) umetekelezwa kwa miaka mitano 2011 hadi 2016. 

Mradi huu umekuwa unalenga katika kuimarisha masuala ya raslimali watu wa sekta ya afya. Moja wapo ya majukumu ya Taasisi ya Mkapa tuliyopewa na Wizara ya Afya, ni ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya ambapo jumla ya nyumba 480 zimekuwa zinajengwa katika Halmashauri 51 nchini tokea mwaka 2011.Miongoni mwa nyumba hizo 480, 30 zipo katika Mkoa wa Kigoma kwa Halmashauri ya wilaya Kigoma, Kasulu na Kibondo.

Mradi wa pili ni wa Kifua Kikuu na Ukimwi unaotekelezwa kwa kushirikiana ya Wizara ya Afya kupitia – Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma pamoja na Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi inatekeleza mradi wa Ukimwi na Kifua Kikuu chini ya Shirika la Save the Children kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria. 

Mradi huu unaotekelezwa kwa kipindi cha miaka 3 katika mikoa ya Rukwa, Katavi, Tabora na Kigoma unalenga kuisaidia Serikali kupunguza maambukizi ya Kifua kikuu kwa 25% na kupunguza vifo vitokanavyo na Kifua Kikuu kwa 50% mpaka kufikia 2020. Pamoja na hayo mradi unalenga kupunguza maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi, Kupunguza vifo vitokanavyo na Ukimwi, kutokomeza unyanyapaaji na kuongeza upatikanaji wa urahisi wa huduma za Ukimwi hasa upimaji wa VVU.

Mfano wa moja kati ya nyumba mpya 30 zilizojengwa na kukabidhiwa kwa mkoa wa kigoma na Taasisi ya Mkapa. 
Kikundi cha kina mama wa mkoa wa kigoma wakiimba kwa furaha mbele ya Mkuu wa Mkoa, Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga wakati wa hafla ya kukabidhiwa nyumba mpya 30 za watumishi wa afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa mkoani Kigoma. 
Watu waliohudhiria hafla ya ukabidhiwaji wa vitendea kazi vitendea kazi (baiskeli 200, mabegi 225, mabuti 25 na makoti ya mvua 25) kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 
Dkt. Ellen Mkondya-Senkoro, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa akitoa ufafanuzi wa jiwe la ufunguzi kwa Mhe. Brigedia Jenerali (Mstaafu) Emmanuel Maganga, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa halfa ya ukabidhishwaji wa nyumba mpya 30 za watumishi wa Afya iliyofanyika katika zahanati ya Kalinzi mkoani kigoma.

BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA AFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA WILAYA YA GAIRO BI. SIRIEL SHAIDI MCHEMBE LEO JIJINI

$
0
0
Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing hii leo hii tarehe 28/3/2017 akiwa ofisini kwake amefanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe.Katika mazungumzo yao ambayo yalijikita katika maeneo makubwa matatu, ambayo ni Kilimo cha Kibiashara kwa ushirikiano na Serikali ya China, Kupatia vikundi vya wanawake viwanda vidogo vidogo vya kukamua mafuta ya alizeti, pamoja na kuweka  Mkakati wa kujenga Soko la Kisasa la Mahindi na ghala la kuhifadhi chakula.

Mhe Mchembe amemwambia Balozi huyo kwamba kutokana na ukweli kuwa mvua zinazoendelea nchini zimeliweka Taifa katika mazingira mazuri ya kuvuna chakula kingi, ni vizuri pia kujipanga ili ziada iuzwe vizuri bila kumnyonya mkulima kama ilivyokuwa kwenye zao la korosho.
"Kauli ya Mhe. Rais Magufuli ya hapa kazi tu, ilimfanya kila mtu akafanye kazi hivyo kilimo kimefanyika cha kufa na kupona. Tunamshukuru Mungu kwa hali ya hewa nzuri, alisema Mhe Mchembe.

Katika mazungumzo hayo Balozi Youqing alisema Serikali ya China itaendelea kutoa misaada na kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hasa katika sekta ya Viwanda, Kilimo na Mifugo Endelevu kama ambayo alimuahidi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Dr. Steven Kebwe.

Aidha alimuahidi kutembelea Mkoa wa Morogoro mapema mwezi wa nne 2017 ili kitimiza ahadi yake.Mkuu wa Wilaya alimshukuru Balozi Youqing kwa kupeleka Wakuu wa Wilaya 20 nchini China kwa mafunzo ya Serikali za Mitaa ambapo nae alikuwa miongoni mwao.Vile vile Mkuu wa Wilaya huyo alimkaribisha Balozi Youqing Wilayani Gairo ili kujionea mafanikio ya mafunzo hayo.
 Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing akimkaribisha  Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe ofisini kwake jijini Dar es salaam leo,kabla ya kufanya mazungumzo nae
 Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. LU Youqing akiwa katika mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Bi. Siriel Shaidi Mchembe ofisini kwake jijini Dar es salaam leo

SERIKALI KUTENGENEZA MWONGOZO WA KUWARUDISHA SHULE WALIOPATA MIMBA

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Serikali imejipanga kutengeneza mwongozo wa kuwarudisha shuleni wanafunzi waliopata mimba wakiwa masomoni ili kuhakikisha wanapata elimu hadi kufikia ngazi za juu.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori alipokuwa akifungua warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia jinsia katika elimu kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo Prof. Joyce Ndalichako.

Manori amesema Serikali ya Tanzania inajitahidi kuzingatia jinsia katika utoaji wa elimu ambapo takwimu zinaonyesha kuwa elimu ya Msingi na Sekondari uwiano wake ni moja kwa moja japo kuwa idadi ya wasichana hupungua kutokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba hivyo lengo la warsha hiyo ni kuwasaidia wadau kuweka mipango ya elimu inayozingatia usawa wa kijinsia.

“Serikali yetu imejipanga kuhakikisha wasichana wanapata elimu hadi ngazi za juu lakini mpango huo unakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mimba na ndoa za utotoni hivyo ili kuhakikisha mtoto wa kike anafikia ngazi za juu za elimu tuko kwenye mchakato wa kuandaa mwongozo kwa ajili ya wanafunzi waliopata mimba wakiwa bado wanasoma kupata nafasi ya kuendelea na masomo,”alisema Manori.

Mkurugenzi Msaidizi amezitaja changamoto zingine zinazowapelekea wanafunzi wa kike kuacha shule zikiwemo za umaskini, mazingira rafiki ya kusomea, mila na desturi zinazomkataza msichana kupata nafasi ya kusoma pamoja na kukosa muda wa kujisomea kwa sababu ya kufanya kazi nyingi wanaporudi majumbani.

Manori ametoa rai kwa Watanzania kuelewa kuwa kila mtoto ana haki na wajibu wa kupata elimu bila kujali jinsia pia ameiasa jamii kuacha kuwaozesha wasichana wenye umri chini ya miaka 18 ili waweze kufikia malengo yao waliyojipangia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen ameahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha mipango ya elimu nchini inaangalia usawa wa kijinsia kwa kuwa ni njia moja wapo itakayochochea maendeleo ya elimu kwa watoto wa kike.

“Warsha hii imeandaliwa kwa ajili ya wadau wote kutoa mawazo yao juu ya changamoto za usawa wa kijinsia zinazoikumba sekta ya elimu pamoja na kuwapa fursa wadau hao kushauriana kuhusu mikakati mbalimbali ya kutatua changamoto hizo ili kuinua sekta ya elimu sio tu kwa Tanzania bali kwa Afrika nzima,”alisema Haldorsen.

Haldorsen ameongeza kuwa mfumo wa elimu umetambua uhusiano uliopo kati ya elimu na usawa wa kijinsia ndio maana wadau wa masuala ya elimu wa Serikali kutoka katika baadhi ya nchi za Afrika wameamua kuungana kwa pamoja kujadili juu ya tathmini, mpangilio na ufuatiliaji wa elimu unayozingatia jinsia.

Tanzania imekua nchi ya kwanza kuendesha warsha hiyo ya siku tatu iliyoshirikisha maafisa waandamizi wa Serikali wanaoshughulikia mipango ya elimu kutoka nchi za Mozambique, Zambia, Malawi, Uganda, Zanzibar na Tanzania Bara.

Imeandaliwa kwa ushirikiano wa shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI).
 
Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Venance Manori akiwa katika picha ya pamoja na waandaaji wa warsha ya kuwawezesha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu kutoka shirika la Plan International- Tanzania, Global Partnership for Education (GPE), Dubai Cares pamoja na United Nations Girls’ Education Initiative (UNGEI) mara baada ya ufunguzi wa warsha hiyo uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Plan International- Tanzania, Jorgen Haldorsen akitoa neno fupi kwa ajili ya kuwakaribisha Maafisa Waandamizi wa Serikali kutoka nchi sita za Afrika katika ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu. Ufunguzi wa warsha hiyo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Serikali wanaohusika na elimu kutoka nchi sita za Afrika wakisikiliza hotuba ya Mkurugenzi Msaidizi Masuala Mtambuka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (hayupo pichani), Venance Manori wakati wa ufunguzi wa warsha ya kuwawezesha maafisa hao katika kutengeneza mipango inayozingatia usawa wa kijinsia katika elimu.Warsha hiyo ya siku tatu imefunguliwa jana jijini Dar es Salaam.

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII WA MIKOA WAJENGEWA WELEDI KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO NCHINI

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Julius Mbilinyi akifungua Kikao Kazi cha Maafisa wa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa (hawapo pichani) katika cha siku mbili kinachoanza leo katika Hotel ya Edema Mkoani Morogoro.
Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Julius Mbilinyi akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa wanaohudhuria kikao kazi kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika mkutano unaofanyika Hotel ya Edema Mkoani Morogoro.
Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Maafisa Maendelo ya Jamaii wa Mikoa wakifuatilia maelezo ya wawezeshaji kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto katika Hotel ya Edema, mkoani Morogoro.

………………….

Na erasto ching’oro- Msemaji: Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo imefungua kikao cha siku mbili cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mikoa kwa ajili ya kuwajengea uwezo kuhusu utekelezaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (2017-2022).

Akifungua kikao hicho, Mwakilishi wa Katibu Mkuu Bw. Julius Mbilinyi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia aliwashukuru Washirika wa Maendeleo katika kuhakikisha kuwa tatizo la ukatili dhidi ya wanawake na watoto linatokomezwa hapa nchini. Aliyataja mashirika haya kuwa ni pamoja na UN-WOMEN, Shirika la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Haki na Ustawi wa Watoto (UNICEF).

Mgeni Rasimi Kaimu Mkurugenzi wa Jinsia, aliwapongeza Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitekeleza katika maeneo yao ya kazi, juhudi ambazo zimekuwa na mchango katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto nchini. Alifafanua kwamba, baada ya mafunzo haya, maafisa hao wataendelea kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2021/20122.

Wanawake na watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili kwa kisingizio cha mila na desturi. Aidha, mfumo dume umesababisha wanawake kutoshiriki kikamilifu katika maamuzi yanayohusu maendeleo yao, katika ngazi ya kitaifa, katika ngazi ya jamii na hata katika familia zao. Mara nyingi tumesikia wanawake na watoto wakipigwa, kubakwa na wakati mwingine kuuwawa na watu wa karibu. Vitendo hivi ni ukatili wa hali ya juu na vinaleta simanzi na madhara makubwa katika jamii yetu.

Akiongea na Maafisa Maendeleo wa Mikoa, Bw. Mbilinyi alieleza kuwa madhara ya vitendo vya ubaguzi, unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake na watoto huwaathiri kiafya na kisaikolojia na kijamii ambapo uthoofisha ushiriki wa wanawake katika shughuli za maendeleo na hivyo kurudisha nyuma jitihada za kuiwezesha nchi yetu kuwa ya viwanda na uchumi wa kati. Wizara kwa kuzingatia changamoto hizo, imekuwa ikifanya juhudi za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, ikiwemo uandaaji wa Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Katika kuhakikisha kuwa Mpango Kazi huu unaeleweka na kutekelezwa ipasavyo Wizara imetoa mafunzo kuhusu Mpango huu kwa wadau mbalimbali. Mafunzo yaliyotolewa ni mwendelezo wa mafunzo yaliyotolewa kwa waratibu wa Madawati ya Jinsia kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali kuhusu Mpango kazi huo ili kuwezesha utekelezaji wake.

Kaimu Mkurugenzi wa maendeleo ya Jinsia amefafanua kuwa, Tafiti mbalimbali ikiwemo Taarifa ya Idadi ya Watu na Afya ya mwaka 2015-2016 inaonesha kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo. Taarifa hii inaonyesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15. Taarifa hiyo inaonesha kuwa wanawake 2 kati ya 10 walikumbana na ukatili wa kimwili wakati utafiti huo ukifanyika. Ukatili wa kimwili unaongezeka kadri umri unavyoongezeka; asilimia 22 ya wanawake wenye umri wa miaka 15-19 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili, ukilinganisha na asilimia 48% ya wanawake wenye umri wa miaka 40-49.

Akitoa nasaha zake Afisa Mendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Paul Shayo alieleza kuwa mafunzo haya yatawajengea umahiri, kuweza kutekeleza Mpango Kazi kwa ufanisi. Mbinu watakazopata zitakuwa mwongozo wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto katika jamii. Vile vile, amekiri kwamba, uzoefu na weledi utakaoupata kupitia mafunzo haya utawasaidia wahanga wa vitendo vya ukatili kupata huduma stahiki kwa kuwaunganisha na watoa huduma katika maeneo mbalimbali.

Mikoa ambayo itajumuishwa katika awamu ya pili ya mafunzo hayo ni Kagera, Mara, Kigoma na Katavi.

WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PROF PALAMAGAMBA KABUDI AWASILI OFISINI MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Prof.Palamagamba Kabudi amewasili katika Ofisi za Makao makuu ya Wizara zilizoko ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kulakiwa na watumishi wa Wizara walioko makao makuu ya Serikali mjini Dodoma. 

Prof Kabudi aliapishwa tarehe 24/03/2017 Ikulu jijini Dar Es Salaam kuchukua nafasi hiyo baada ya Mhe.Rais kufanya mabadiliko madogo kwenye Baraza la Mawaaziri ambapo Dkt. Harrison Mwakyembe alihamishiwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. 

Nje ya Ofisi za Wizara Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alilakiwa na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Amon Mpanju, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Aloyce Mwogofi, Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma na wafanyakazi wengine wa Wizara waliopo Makao Makuu ya Serikali mjini Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akipokea shada la maua kutoka kwa mtumishi Joyce Mtuma mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akiangaalia kadi ya Pongezi iliyoasiniwa na watumishi wa wizara mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma
WaziriwaKatibanaSheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana naNaibu Katibu Mkuu Bw. Amon Mpanju mara baada ya kuwasili Wizarani mjini Dodoma


Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisalimiana na Jaji mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Mwanaisha Kwariko alipowasili Wizarani mjini Dodoma




Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Prof.Palamagamba Kabudi akisikiliza maelezo mbalimbali alipokutana na watendaji wa Wizara na Mahakama katika ukumbi wa mikutano Wizarani mjini Dodoma

WACHIMBAJI WADOGO WAMUOMBA RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI KUACHIA MCHANGA ULIOKAMATWA BANDARINI

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Wachimbaji wadogo wa madini wamemuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwaachia mchanga wa madini uliozuiwa bandarini kutokana na kuwepo kwa mchanga katika bandari kavu huku wakiendelea kutozwa ushuru wa kuhifadhi.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wamesema kuwa mchanga uliozuiwa na bandarini sio wa dhahabu ambao mashine za kuchanjulia ziko hapa nchini.

Mmoja wa wachimbaji hao , King Selemani amesema kuwa mchanga wanaosafirisha kwenda nje ni shaba, Nickel ,Manganise ore ,Zinc ore, Galena pamoja na lead ore ambapo hapa nchini hakuna mtambo wa kuchenjua mchanga huo.

Selemani amesema kuzuiwa kwa mchanga huo kumewaathiri pamoja na kusitisha ajira kwa baadhi ya wafanyakazi katika machimbo ya madini hayo.

Aidha amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mstari mbele hivyo wamemuomba kuwachia kuendelea na biashara hiyo.
Mchimbaji Mdogo wa Madini, King Selemani akizungumza leo na waandishi wa habari juu ya kumuomba Rais Dk.John Pombe Magufuli kutoa ruhusa ya kuwaachia mchanga wa madini uliozuiwa katika bandari ya Dar es Salaam.
Mchimbaji Mdogo na msafirishaji wa Madini , Paul Kalyembe akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwaruhusu kufanya biashara hiyo huku serikali ikisubiri kufanya taratibu zungine za kuwa na kiwanda cha kufanya kazi ya kuchenjua madini katika mchanga wa Nickel, Shaba na madini megine leo jijni Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii.
Sehemu ya waandishi habari wakiwasikiliza wachimbaji wadogo wa madini leo jijini Dar es Salaam .

Kampuni za ujenzi kutoka China zaaswa kushirikana

$
0
0
KAMPUNI za ujenzi nchini zimeshauriwa kuungana na kushirikiana na kampuni za ujenzi kutoka China ili kujifunza namna wanavyofanya kazi kwa ufanisi.

Akizungumza ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Asasi ya Ushirikiano kati ya Tanzania na China, Bwana Joseph Kahama alibainisha kuwa kampuni za ujenzi nchini bado zina safari ndefu ya kuongeza ujuzi na mbinu za kibiashara.

“Wachina ndio wanaoongoza katika ujenzi duniani, mataifa mengi yaliyoendelea majengo yao yanasimamiwa na kampuni za kichina, hivyo hakuna namna kwa kampuni za Kitanzania kushindana nazo wakitaka kufanikiwa wajipenyeze na kuomba ushirikiano hapo watajifunza mengi.

“Kujifunza kuna njia nyingi, ni utaratibu mzuri katika biashara kujipanga,” alisisitiza Bw. Kahama na kuongeza: “zaidi ya asilimia 80 ya kampuni kubwa za ujenzi duniani zinatoka China, na hapa nchini zipo nyingi kwa sasa huu ndio wakati wetu wa kuchota ujuzi.”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC East Africa Limited), Bwana Yigao Jiang alisema kampuni yake imekuwepo nchini tangu miaka ya 1960 na wapo tayari kuwasaidia Watanzania katika nyanja zote ikiwemo masuala ya kijamii.

“Mbali ya kushiriki ujenzi wa magorofa na miundombinu mbalimbali kampuni yetu inaguswa na matatizo ya kijamii kwa sababu Watanzania ni ndugu zetu sasa, tumeshiriki ujenzi wa reli ya Tazara, tumejenga jengo la Ushirika (Mnazi Mmoja), tumejenga jengo la Nasaco (Dar es Salaam).

“Vilevile jengo la ukumbi mpya Ikulu jijini Dar es Salaam tumeshiriki kuujenga na sasa tunajenga makutano ya barabara za juu Ubungo,” alisema.Alibainisha kuwa “Hili linatufanya kuwa sehemu ya jamii, hadi sasa tumeshiriki kutoa misaada mbalimbali ya kuchimba visima vya maji, kugawa vitanda vya wagonjwa katika wilaya mbalimbali za vijijini na hivi karibuni tumegawa jumla ya madawati 150 katika Wilaya ya Chato mkoani Geita na Ruangwa mkoani Lindi yenye jumla ya thamani ya Sh milioni 10, ambapo kila dawati wanakaa wanafunzi watatu.”

Aidha kampuni hii pia ilishiriki kutoa misaada ya blanketi na vyakula kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera yenye thamani ya Sh mil 10.Kuhusu fursa zinazopatikana kutokana na kampuni za ujenzi kutoka China anaeleza Bw. Kahama: “Watanzania wanapata ajira kwa sababu wasimamizi ni Wachina lakini wafanyakazi wanatoka hapahapa, vilevile wananunua mchanga, saruji, kokoto, nondo na vifaa vingine vya ujenzi kutoka nchini.

“Kampuni hii ya CCECC East African Limited ni ya tatu kwa ukubwa duniani, hivyo nasisitiza tusiache kunufaika kutoka kwao wana mengi ya kutufunza kuhusu sekta ya ujenzi.”
Mkuu wa wilaya ya Chato, Bw Elias Makory akimkabidhi cheti Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) Bw.An Yi kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo kwa jamii mara baada ya kupokea madawati 50 kwa matumizi ya wanafunzi 150. Kampuni hiyo imeshatoa jumla ya madawati 150 yenye thamani ya milioni 30 na itaendelea kuchangia huduma mbalimbali za kijamiii.
Mkuu wa wilaya ya Chato, Bw Elias Makory (wapili kushoto) akipokea rasmi madawati 50 toka kwa Mkurugenzi wa Operesheni wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) Bw.An Yi (watatu kushoto). Kampuni hiyo imeshatoa jumla ya madawati 150 yenye thamani ya milioni 30 na itaendelea kuchangia huduma mbalimbali za kijamiii.


MENEJA WA SIDO MKOA WA MTWARA AZINDUA RASMI MAFUNZO YA KUWAWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI CHINI YA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

$
0
0

 Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa Akizungumza Machache wakati Akizindua Rasmi mafunzo ya Ujasiriamali kwa Wanawake wa Mkoa Mtwara akiwa wa Wawezeshaji kutoka Taasisi Ya Manjano Foundation
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mtwara Joel Chidabwa kawataka wanawake wa Mkoa wa Mtwara kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema mkoani Mtwara alipokuwa akifungua mafunzo hayo kwa wanawake wajasiriamali katika sekta ya vipodozi na urembo. Mafunzo hayo yanatolewa bure kwa wanawake 30 waliotuma maombi na kuchaguliwa na Taasisi ya Manjano Foundation.
Akieleza zaidi amesema “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kutumia bidhaa za LuvTouch ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake kupata elimu ya ujasiriamali ili waweze kujiajiri na kujiongezea kipato kupitia bidhaa hizo” 
Baada ya kuhitimu mafunzo haya washiriki hao wataunganishwa na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ya kupata mitaji ya kuanzisha bishara
Mwezeshaji Kutoka Taasisi ya Manjano Foundation Bi Ester Lukindo Akizungumza Machache wakati wa Uzinduzi Huo .
Bi Ester Lukindo aliyesoma hotuba kwa niaba ya afisa mtendaji mkuu wa Shear illusions na Muasisi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama “Shekha Nasser alisema kuwa "wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo."
Washiri wakiwa Katika Picha ya Pamoja na Mgeni Rasmi..
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi Mtwara ukiwa ni mkoa wa tatu tayari kufikiwa.

makamishna wapya wa uhamiaji waapishwa leo mjini dodoma

$
0
0
 Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha,  Edward Peter Chogero  katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira  na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi  Hassan Simba Yahaya.
 Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr.  Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   na Naibu  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
 Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza  Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa  kiapo cha Maadili ya Viongozi wa  Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika  leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. 
 Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira   akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao  leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.  

Solly Mahlangu kutoka nchini Afrika kusini athibitisha kushiriki tamasha la Pasaka jijini Dar

$
0
0


Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.



MWIMBAJI wa kimataifa wa nyimbo za injili, Pastor Solly Mahalangu kutoka nchini Afrika Kusini, amethibitisha kushiriki Tamasha la Pasaka linaloadhimisha miaka 17 tangu kuasisiwa kwake mwaka 2000 chini ya uratibu wa kampuni ya Msama Promotions.

Solly ambaye amekuwa king’ara vilivyo katika muziki wa injili kama mwimbaji anayejipambanua na wengine kama mchangamshaji zaidi jukwaani, pia ni kiongozi wa kanisa nchini Afrika Kusini , hivyo kuenfesha huduma zote mbili kila moja kwa wakati wake.

Alex Msama, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo litakalozinduliwa April 16, mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kabla ya kuelekea katika mikoa mingine mitano, alisema jana kwamba mwimbaji huyo amethibitisha kushiriki tukio hilo lenye kubeba hadhi na vionjo vya kimataifa.

“Nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka, nina furaha kubwa kusema kuwa mwimbaji wa kimataifa wa nyimbo za injili kutoka nchini Afrika Kusini, amethibitisha kushiriki tamasha la Pasaka la mwaka huu litakalofanyika katika mikoa sita ikiwemo Dar es Salaam,” alisema.

Alisema ujio wa Mahlangu katika tamasha hilo, kunafanya maandalizi ya Tamasha hilo yazidi kuimarika kutokana na umaarufu wa mwimbaji huyo anayesifika ndani na nje ya Afrika Kusini kwa huduma ya uimbaji wa nyimbo zenye ujumbe wa kuvutia wengi na kuchangamsha jukwaa.

Msama alisema kwa vile si mara ya kwanza kwa Mahlangu kushiriki Tamasha la Pasaka, wadau na wapenzi wa Tasmaha hilo wajitokeze kwa wingi kuja kufaidi Baraka za Mungu kupitia ujumbe wa Neno la Mungu kutoka kwa mwimbaji huyo na wengine kibao akiwemo malkia wa muziki wa injili Afrika Mashariki, Rose Muhando.

Alisema Mahlangu ambaye atakuwa na kundi lake, atashirikiana na waimbaji wengine walitangazwa tayari ambao tayari wapo katika maandalizi ya nguvu kwa lengo la kutoa huduma bora siku hiyo ya uzinduzi wa Tamasha hilo lenye kubeba maudhui ya kueneza ujumbe wa neno la Mungu na sehemu ya mapato kusaidi makundi maalumu.

Msama alisema Tamasha la mwaka huu litabeba uzinduzi wa albamu mbili; moja ya Muhando inayoitwa Jitenge na Ruth pamoja na albamu mpya ya Kwaya ya Kinondoni Revival ya jijini Dar es Salaam, iitwayo ‘Ngome Imeanguka.’

MTANZANIA ALIYEWEKA REKODI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO KWA MUDA MFUPI AMUANGUKIA WAZIRI MWAKYEMBE

$
0
0

Gaudence Lekule akiwa katika kilele cha Uhuru ,Mlima Kilimanjaro baada ya kukimbia kwa muda wa wa saa 8:36 mpya akiwa Mwafrika na Mtanzania wa kwanza kutumia muda huo kupanda kilele cha mlima Kilimanjaro na kushuka.

Gaudence Lekule akipanda mlima Kilimanjaro huku akikimbia wakati akiweka rekodi baada ya kutumia muda wa saa 8:36 mapema mwaka huu.
Lekule akifurahia mara baada ya kufanikiwa kuweka ekodi ya kutumia muda wa saa 8:36 kupanda Mlima Kilimajaro na kushuka.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

MTANZANIA ,Gaudence Lekule (31) anayeshiriki michezo ya kupanda milima kwa kasi (Mountain Run) amemuomba Waziri mpya wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo ,Dkt Harison Mwakyembe kutupia jicho michezo mingine kwani ina nafasi kubwa ya kutangaza na kuletea sifa taifa.

Lekule anayeshikilia rekodi ya kuwa Mwafrika wa kwanza Duniani kupanda kwa muda mfupi katika Mlima Kilimanjaro akitumia muda wa jumla wa saa 8:36 alitoa wito pia kwa kampuni,taasisi binafsi na za serikali kujitokeza kudhamini wanamichezo kutokana na eneo hilo upo uwezekano wa kujitangaza zaidi kidunia.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalum,Gaudence alisema kwa sasa yupo katika maandalizi ya kuweka rekodi mpya katika milima mirefu na maarufu Duniani kwa kufanya mazoezi ya awali hapa nchini na baadae nje ya nchi.

“ Nashukuru kuitangaza Tanzania kidunia na tayari nimepata mialiko mingi ya kwenda nje kushiriki mashindano ya Mountain Run ,Lengo langu ni kuweka rekodi katika milima mirefu duniani hivyo bado naendelea na mazoezi na nitaendelea kufanya mazoezi hapa kwetu na badaae nje ya Tanzania”alisema Gaudence .

Alisema hadi sasa rekodi ya Dunia inashikiliwa na raia wa nchi ya Ecuador, Karl Egloff aliyetumia muda wa saa 6:53 kupanda na kushuka Mlima Kilimanjaro ,rekodi aliyoweka mwaka 2014 akivunja rekodi ya Kilians Jornet raia wa Hispania aliyetumia muda wa saa 7:20 kupanda na kushuka mlima Kilimanjaro mwaka 2010.

Lekule alisema changamoto iliyopo kwa sasa ni mabadiliko hali ya hewa inayochangia kushindwa kufanya mazoezi na upatikanaji wa mahitaji kama chakula pamoja na mavazi kwa ajili ya mchezo huo unafanyika kuanzia urefu wa mita 3500 hadi 5800.

Akizungumzia kilichomsukuma kushiriki mcezo mchezo huo,Lekule ,mkazi wa kiraracha Marangu wilaya ya Moshi alisema raia wa kigeni wamekuwa wakishiriki katika michezo ya aina hiyo kwa ajili ya kuweka rekodi hivyo akaona ni wakati wa waafrika pia kushiriki katika uwekaji wa rekodi Duniani.

Alisema raia wa Ecuador ,anayeshikilia rekodi ya dunia aliposikia ameweka rekodi akiwa ni mwafrika na Mtanzania wa Kwanza alituma salamu za pongezi huku akimtaka kwenda kwenye milima iliyopo nchi za nje kutafuta rekodi nyinine.

“ Egloff alifurahi sana na kunipa moyo na kunitaka nikatafute rekodi nje ya Afrika kwa sababu nina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri Ulaya na kuipa sifa Tanzania,ni ngumu sana mtu kukimbia kwenye urefu kama uliopo Mlima Kilimanjaro na katika maisha inahitaji moyo sana.”alisema Lekule.


Rekodi za kidunia.

Mara ya kwanza rekodi ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa kasi kwa Afrika ilikua inashikiliwa na Saimon Mtui akitumia muda wa saa 9 : 20 mwaka 2006, baadae raia wa Hspania Kilians Jornet alitumia muda wa saa 7:20 mwaka 2010.

Mwaka 2014 ndipo Karl Egloff raia wa Ecuador anayeshikilia rekodi ya Dunia hadi sasa alitumia muda wa saa 6 :53 mwaka 2014 na sasa Mtanzania Gaudence Lekule ameweka rekodi ya kuwa Muafrika na Mtanzania wa Kwanza akitumia muda wa saa 8:36 .

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 29,2017

Hamba kahle Comrade Ahmed Mohamed Kathrad

$
0
0
RIP Comrade Ahmed Mohamed Kathrada, ANC Stalwart, ANC Elder, Graduate of Robben Island, Prison-mate of Nelson Rolihlahla Mandela, Walter Sisulu,  Raymond Mhlaba, Govan Mbeki, Elias Motsoaledi, Denis Goldberg, and Andrew Mlangeni. We do not mourn but celebrate the life of a distinguished South African, above all an African.

 Greet Mandela, Mwalimu Nyerere, Kwame Nkrumah, Sekou Toure, Patrice Lumumba, Samora Machel, and Chris Hani. What a momentous occasion that will be when you meet these great Africans, and your fellow Robben Island graduates, at the avenue of everlasting tranquility. We will forever be grateful. Hamba Kahle Kathrada.

By Prof Mark Mwandosya

RC Simiyu amaliza mgogoro wa wanakijiji na wawekezaji

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki.
 
 
 MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka amefanikiwa kumaliza mgogoro wa muda mrefu kati ya mwekezaji katika Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) Makao iliyopo wilayani Meatu, na baadhi ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo. Mwekezaji huyo Mwiba Holdings, amekuwa na mgogoro wa mipaka, mkataba wa kumiliki ardhi na uanzishaji wa ranchi na baadhi ya vijiji hivyo kiasi cha kusababisha kuwa na mahusiano mabaya na wananchi ambao wamekuwa wakisusia misaada mbalimbali inayotolewa na mwekezaji huyo. 
 
Hata hivyo, chanzo halisi cha mgogoro huo kimegundulika kuwa ni viongozi wa baadhi ya vijiji ambao wamekuwa wakipigania maslahi yao binafsi huku wakisambaza taarifa za upotoshaji juu ya mwekezaji huyo na kujenga chuki kwa wananchi. 
 
Vijiji vinavyounda WMA ya Makao ni pamoja na Makao, Iramba ndogo, Sapa, Mwangudo, Jinamo, Lukale, Mbushi, Mwabagimu na Sunga. Baadhi ya viongozi hao wa vijiji pia wamekuwa wakisambaza taarifa potofu kwa wananchi kwamba Mkuu huyo wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Meatu wamehongwa na mwekezaji ili kuwakandamiza wananchi, jambo lililothibitika kuwa si la kweli.
 
 Kutokana na mgogoro huo kuzidi kuota mizizi huku uongozi wa CCM Mkoa wa Simiyu nao ukichukua upande, Mtaka alilazimika kuitisha kikao cha usuluhishi kilichoshirikisha wadau wote wakiwamo Kamati ya Siasa ya CCM mkoa na wilaya, viongozi na watendaji wa serikali ngazi ya mkoa na wilaya, viongozi wa vijiji tisa vinavyounda WMA Makao, mwekezaji na wadau wengine akiwamo Mbunge wa Meatu na Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu. 
 
Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika mwishoni mwa wiki mjini hapa, Mtaka aliwakemea viongozi wanaoeneza taarifa potofu wilayani humo na kusababisha shughuli za maendeleo kukwama huku akiahidi kuwachukulia hatua zinazostahili viongozi wa namna hiyo. “Katika masuala ya maendeleo ya wananchi sina mzaha. Nipo tayari kuwa kiongozi unpopular (asiyependwa) ili mradi shughuli za maendeleo za wananchi zinaenda mbele. 
 
“Mgogoro na Mwiba umekuwa kama mkuki mnaojichoma wenyewe kila siku kwa sababu wenyewe ndiyo mlioingia mikataba na mwekezaji wakati sisi hatukuwapo na wala hatuna maslahi yoyote binafsi hivyo acheni maneno maneno, kaeni chini mzungumze tusonge mbele,” alisisitiza Mkuu huyo wa mkoa. “Mmefikisha malalamiko, tena kwa maandishi hadi kwa Waziri Mkuu lakini uhalisia ni kuwa mengi mliyopeleka hayana ukweli, ni hisia na mengine ni fitna tu. Sasa wekeni kila kitu hadharani hapa, tumalize suala hili leo na tujikite zaidi katika mambo ya maendeleo,” alisema. Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk Titus Kamani akizungumza katika kikao cha usuluhishi baina ya wananchi wa Meatu na Mwekezaji wa Mwiba Holdings kilichofanyika mjini Mwanhuzi mwishoni mwa wiaki. Mkuu wa Mkoa wa Simiiyu, Anthony Mtaka akifungua kikao cha usuluhishi baina ya mwekezaji wa Mwiba Holdings na wadau wa maendeleo mkoani Simiyu kilichofanyika mwishoni mwa wiki
 
Kuhusu mgogoro wa mpaka hasa katika kijiji cha Buhongoja ambako alama ya mpaka yenye namba 314 inadaiwa kusogezwa kinyemela kwa umbali wa kilomita 10, Mkuu huyo wa mkoa alizitaka pande zinazohusika kukutana na kutatua tatizo hilo kwa kurejea katika eneo la awali bila ya mikwaruzano yoyote. Aliamuru pia pande zinazohusika katika suala la mkataba wa umiliki wa ardhi,kukaa meza moja na kuacha mambo ya kukimbilia kwa wasuluhishi ambao wamekuwa wakidai fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika kwa maendeleo ya vijiji au wilaya ya Meatu.
 
 Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini aliahidi kupeleka wataalam watatu watakaosaidiana kutatua mgogoro huo wa umiliki wa ardhi watakaosaidiana na wake wa wilaya ili kutatua suala hilo ndani ya wiki mbili. Awali, Mwenyekiti wa Kijiji cha Makao, Anthony Phillipo alieleza kuwa kijiji kilazimika kupelaka suala hilo kwenye Tume ya Usuluhishi wa Migogoro Dar es Salaam ambako kijiji walishindwa kulipa gharama za usuluhishi huo walizotozwa na Jaji Mstaafu Thomas Mihayo. 
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Dk. Titus Kamani alieleza chama hicho tawala kusikitishwa na mgogoro huo unaokwamisha shughuli za maendeleo ya wananchi na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya chama hicho. “Ndugu zangu, sisi tunajiandaa kushinda katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, kwa hiyo tunawaomba tusikubali kuingizwa katika migogoro kama hii ambayo haina tija kwa wananchi.
 
 “Tunataka wakati wa uchaguzi utakapofika tushinde pila pressure (msukumo) yoyote na tunachotaka ni mshikamano,maelewano mazuri baina ya wadau wote ili tufanye shughuli za maendeleo kwa faida ya mkoa wetu wa Simiyu na wilaya ya Meatu,” alisisitiza. 
 
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Mpina Luhaga ambaye pia ni mbunge wa Kisesa wilayani Meatu alisema katikA kikao hicho kuwa mwekezaji huyo amekuwa akifuata sheria zote za nchi katika utekelezaji wa majukumu yake na ni wazi kwamba wananchi watashindwa katika madai yote wanayofungua katika Tume ya Usuluhishi wa migogoro. 
 
“Mimi nimefuatilia malalamiko haya ya wananchi serikalini na hasa Wizara ya Maliasili na Utalii na hawa jamaa wamefuata taratibu zote na wanalipa tozo zote wanazostahili kulipa hivyo tunapaswa kuwa waangalifu,” alisema. Mkurugenzi wa Mwiba Holdings, Abdulkadir Mohamed Luta alisema kuwa Kampuni hiyo ipo tayari kukaa meza moja na kusaidia usuluhishi wa mgogoro wowote ili wajikite zaidi katika shughuli za maendeleo ya wananchi.
 
 Aliongeza kwamba kampuni hiyo ilikuwa tayari kugharamia hata suala la mkataba wa umiliki wa ardhi lililofikishwa Tume ya Usuluhishi wa Migogoro ili mradi tu suala hilo liishe na waendelee na mambo ya maendeleo Alisema watazifanyia kazi hoja zote zilizotolewa na wananchi katika kikao hicho na kwamba sera ya kampuni hiyo ni kushirikiana na wananchi na wamekuwa wakitekeleza sera hiyo kwa vitendo. 
 
Mbunge wa Meatu, Salum Khamis maarufu kwa jina la Mbuzi, alisema kuwa hana mgogoro na mwekezaji yoyote lakini hatakaa kimya kutetea maslahi ya wananchi wake ambao ndio waajiri wake kila atakapoona kuna sababu ya kufanya hivyo. 
 
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Pius Machungwa aliahidi kuipatia kiwanja cha kujenga ofisi Kampuni ya Mwiba Holdings katika makao Makuu ya wilaya hiyo ili iwe karibu na wananchi, na kwamba watashirikiana na kampuni hiyo katika shughuli za maendeleo wilayani humo.

MATUKIO ZA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA

$
0
0
 Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiimba wimbo wa uzalendo wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi yake Dodoma Machi 28, 2017.
A 1
Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa uzalendo wakati wa mkutano wao wa mwaka katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
A 2
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Flora Bilauri akitoa neno la utangulizi wakati mkutano wao wa mwaka uliofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma Machi 28, 2017.
A 3
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa ofisi yake ukumbi wa mikutano Dodoma Machi 28, 2017.
A 4
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Packshard Mkongwa akiwasilisha hoja za bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika Dodoma Machi 28, 2017.
A 5
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya ufunguzi wa mkutano huo katika ukumbi wa ofisi hiyo Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU-DODOMA)

MAHAKAMA KUU KANDA YA MWANZA YAJIPANGA KUONDOSHA MLUNDIKANO WA MASHAURI

$
0
0

Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu-Kanda ya Mwanza akiongea jambo katika kikao hicho, pamoja nae wanaoonekana katika picha ni baadhi ya Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza ambayo ina jumla ya Majaji saba (7).


Baadhi ya Watumishi wa Mahakama na Wadau wakiwa katika kikao hicho.
Waheshimiwa Majaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza wakiwa katika kikao pamoja na Wadau wa Mahakama wa Kanda hiyo (hawapo pichani) kilichofanyika hivi karibuni, wa kwanza kulia ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Eugenia Rujwahuka.


Pichani ni Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vincent Makaramba.
Afisa Habari, Mahakama, Bi. Mary Gwera akiwa katika Mahojiano maalum na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Makaramba ofisini kwake, Mahakama Kuu-Mwanza.



Na Mary Gwera, Mahakama.

MAHAKAMA Kuu, Kanda ya Mwanza imejipanga kuondoa Mashauri yote yenye umri zaidi ya miaka miwili yaliopo katika Kanda hiyo ili kuendana na azma ya Mahakama ya Tanzania ya kutokuwa na mlundikano wa kesi katika Mahakama za ngazi zote nchini.

Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi, Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vincent Makaramba katika Mahojiano maalum aliyofanya na Mwandishi wa habari hii hivi karibuni ofisini kwake, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza.

“Mbali na agizo la Mahakama la kutaka kila Mahakama ishughulikie mashauri ya muda mrefu Mahakamani, Mahakama, Kanda ya Mwanza tayari tulishajipanga katika kuondosha Mashauri haya, na kila Jaji amejipangia namna ya kusikiliza na kutolea maamuzi mashauri hayo,” alisisitiza Jaji Makaramba.

Aliongeza kuwa ili suala hili liweze kufanikiwa ni vyema kuwa kitu kimoja na Wadau wa Mahakama kuwezesha zoezi hili kufanikiwa na vilevile kuwa na rasilimali wezeshi kama fedha.

Aidha; ili kuweza kufanyika kwa zoezi hili la kuondoa mlundikano wa Mashauri Mahakamani, Majaji wote saba (7) wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama hiyo ikiwa ni pamoja na Naibu Msajili na Mtendaji wa Mahakama walikutana na Wadau wa Mashauri ya Jinai na Madai ili kujadili namna bora ya kuondosha mashauri yenye umri wa miaka miwili Mahakamani.

Kwa upande wake, Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Kanda ya Mwanza, Mhe. Eugenia Rujwahuka alisema kuwa zoezi la kuondosha mashauri haya linatakiwa liwe limekamilika kufikia mwezi wa tano mwaka huu.

“Kikao hicho kilichojumuisha Wadau mbalimbali kama Mawakili, Waendesha Mashitaka, Magereza n.k, kililenga katika kujipanga ili kufanikisha usikilizaji wa Mashauri ya Mauaji katika vikao maalum vitakavyoanza Aprili, 24, mwaka huu hadi hadi Mei, 24 mwaka huu,” alisema Naibu Msajili.

Mhe. Rujwahuka aliongeza kuwa jumla ya Mashauri 107 yamepangwa kusikilizwa katika vikao hivyo ambavyo vitafanyika Tarime, Sengerema, Magu, Geita, Mwanza na Musoma.

Hata hivyo; katika kikao hicho kati ya Mahakama na Wadau wake walikubaliana kushirikiana ili kufanikisha zoezi zima la uondoshaji wa mrundikano wa mashauri.

Katika muendelezo wa uboreshaji wa huduma ya Utoaji haki nchini Mahakama ya Tanzania imedhamiria kuondoa mlundikano wa kesi katika Mahakama zake.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA MFUMO MPYA WA KIELEKTRONIKI WA KUFUATILIA UTEKELEZAJI WA AHADI, ILANI YA CHAMA TAWALA NA MAAGIZO YA VIONGOZI WAKUU

$
0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akieleza umuhimu wa mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma na kulia kwake waliokaa ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt. Hamisi Mwinyimvua akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Agustino Tendwa akiratibu shughuli ya uzinduzi wa mfumo wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu uliofanyika Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Machi 28, 2017
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano huo (hawapo pichani) Dodoma.
Mchumi Idara ya Uratibu wa Shughuli za Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Novatus Tesha akionesha namna mfumo wa Kielektroniki wa Ufatiliaji wa Taarifa za Serikali unavyofanya kazi kwa wajumbe wa mkutano wa uzinduzi wa mfumo huo Machi 28, 2017 Dodoma. PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU).


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama amezindua mfumo mpya wa Kielektroniki wa Kufuatilia Utekelezaji wa Ahadi, Ilani ya Chama Tawala na Maagizo ya Viongozi Wakuu ulianzishwa kwa lengo la kusaidia upatikanaji na utoaji wa taarifa za utekelezaji kupitia mfumo wa kisasa (kidigitali).

Akizindua mfumo huo wakati wa mkutano na waandishi wa habari Machi 28, 2017 Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni, Waziri alieleza umuhimu wa mfumo huo kuwa umejikita katika kusaidia Viongozi Wakuu kupata Taarifa za utekelezaji wa Maagizo yao na yale yaliyoelekezwa katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

“Mfumo huu utasaidia sana katika kufuatilia shughuli za Serikali ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa maazigo yote na ahadi zilizotolewa ili kuona utekelezaji wake kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali” Alisema Mhe.Waziri.

Aidha mfumo utasaidia pia Ofisi ya Waziri Mkuu kuongeza ufanisi wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kila siku za Serikali kwakuwa taarifa zote zitapatikana kwa wakati na takwimu za uhakika.

Alibainisha kuwa, kuanzishwa kwa mfumo ni moja ya sehemu ya kuondoa changamoto kadhaa ikiwa ni kuongeza ufanisi maeneo yetu ya kazi “kuanzishwa kwa mfumo huo kutatua changamoto za uchelewashwaji wa taarifa, na kutowajibika kwa ujumla na kuleta ufanisi kazini”.Alisisitiza waziri.

Aidha kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamisi Mwinyimvua alibainisha kuwa mfumo umepitia hatua zote muhimu ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Wasaidizi wa Mhe.Rais Jonh Magufuli na Watendaji wa Serikali.

Kwa kumalizia Waziri alipongeza Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Wakala wa Serikali Mtandao kwa kuona umuhimu wa kuwepo kwa mfumo huu na kutoa rai kwa Watendaji wote wa Serikali kuutendea haki kwa kufanya kazi bila uzembe wowote. “rai yangu kwa Watumishi wa Umma wote Nchini kuwajibika kwa kufanya kazi kwani kupitia Mfumo huu, mzembe atajulikana na mchapa kazi atajulikana. Na ikumbukwe tu, wazembe na wavivu hawana nafasi katika Serikali ya Awamu ya Tano”.

TIRA Yajizatiti Kurudisha Thamani ya Huduma za Bima Nchini.

$
0
0

Kamishna wa Bima, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania Bw. Baghayo Abdallah Saqware akiongea na waandishi wa habari kuhusu mwelekeo wa sekta ya Bima nchini na mikakati ya kuendeleza na kupanua shughuli za bima nchini, leo Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa mamlaka hiyo Bw. Eliezer Rweikiza
Meneja TEHAMA, Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Bw. Aron Mlaka akiwaeleza waandishi wa habari mikakati ya mamlaka hiyo ya kuongeza na kupanua matumizi ya Teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) katika kuboresha huduma zao. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo Bw. Juma Makame.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti TIRA Bi. Adelaide Muganyizi akifafanua jinsi Mamlaka hiyo inavyotoa elimu kwa Umma pamoja na umuhimu wa Bima wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo Jiji Dar es saam. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Mamlaka hiyo Bw. Juma Makame.(Picha na Georgina Misama).

…………

Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imejizatiti kurudisha thamani ya huduma za bima kwa kubadilisha baadhi ya sheria na kanuni za bima pamoja na kutengeneza mfumo wenye kutoa tija kwa Wananchi, Serikali pamoja na Kampuni za Bima nchini.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Bima, Baghayo Saqware alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya namna mamlaka hiyo ilivyojipanga kurudisha thamani ya bima kwa wananchi na makampuni ya bima hapa nchini, leo Jijini Dar es Salaam.

Baghayo Saqware amesema kwamba moja ya kanuni na sheria zitakazoboreshwa ni pamoja na kupeleka biashara ya bima (Insurance business – risks) nje ya nchi badala ya kutumia makampuni ya ndani.

“Tutaweka kanuni itakayolazimisha Kampuni za bima hapa nchini kuongeza mitaji au kutengeneza mfuko wa pamoja au mfumo wa makampuni kushirikina kimtaji ili kuweza kuandikisha na kubakisha sehemu kubwa au biashara yote ya bima nchini,” alifafanua Saqware.

Aliendelea kwa kusema kuwa utawekwa utaratibu wa kisheria utakaohakikisha waingizaji wa mizigo kutoka nje ya nchi wanakatia bima za mizigo yao kupitia kampuni za bima nchini.

Aidha amesema kwamba ikibidi mamlaka hiyo itabadilisha sheria ya bima nchini ili wafanyabiashara wanaoagiza bidhaa kutoka nje ya nchi (import goods) iwe ni lazima kukatia bima nchini ili kuongeza mapato ya kodi (VAT) pamoja na bima (Premium Levy).

Katika kurudisha thamani ya huduma ya bima kwa wananchi mamlaka hiyo itahakikisha makampuni yanayotoa huduma ya bima yanatoa huduma stahiki kwa wateja wa bima pamoja na kuhakikish malalamiko ya wateja yanayofikishwa katika mamlaka husika yanashughulikiwa kwa wakati.

Aidha, katika kupanua shughuli za bima mamlaka hiyo iko katika hatua za mwisho za kukamilisha bima ya kilimo, mifugo pamoja na bima za watu wenye kipato cha chini (Micro-insurance) pamoja na kukamilisha utekelezaji wa sera ya Taifa ya Bima.

Vile vile inapanua matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama) kwa kutumia utaratibu wa kusajili na kutoa leseni za biashara ndani ya siku saba hadi thelathini, aidha mfumo huo utaondoa tatizo la bima bandia za vyombo vya moto pamoja na kuhakiki uhalali wa stika za bima kwa walionazo.

Nae, Meneja Tehama TIRA, Aron Mlaki amesema kwamba mfumo huo wa Tehama utamuwezesha mwananchi kupata maelezo ya bima yake kupitia intanenti na meseji za kawaida ambapo kwa upande wa message za kawaida ataandika neno ‘STIKA’ likifuatiwa na namba ya Stika na kuituma kwenye namba 15200 baada ya hapo atapokea taarifa za bima yake.

TAARIFA KWA UMMA

Viewing all 46362 articles
Browse latest View live




Latest Images