Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1183 | 1184 | (Page 1185) | 1186 | 1187 | .... | 1898 | newer

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaagiza watendaji wa serikali kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Mkoa kusimamia na kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu ya miradi yote inayotekelezwa na serikali pamoja na wahisani hasa miundombinu ya maji ambayo imekosa usimamizi wa kutosha.

  Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji mara baada ya kusimamia makabidhiano ya mradi wa maji ulioibuliwa na halmashauri ya Iramba kabla ya kuundwa kwa halmashauri ya Mkalama ulipo mradi wa maji wa Iguguno wenye thamani ya shilingi milioni 847,099,550 na unahudumia watu elfu kumi.

  Amesisitiza kuwa serikali na wadau mbalimbali wamekuwa wakitumia fedha nyingi kutengeneza miradi ya maji ili kuwapunguzia wananchi adha ya upatikanaji wa maji safi na salama ambapo miradi hiyo imekuwa haileti mafanikio yaliyotarajiwa kutokana na kukoa usimamizi wa kutosha.

  “Naelekeza taarifa ya miradi yote ya maji iletwe ofisini kwangu, nataka nifahamu miradi ambayo imefikia lengo la kuwapatia wananachi maji na ile ambayo wananchi hawajaanza kunufaika kwa kupata maji safi na salama lakini fedha za umma zimetumika”, amesema Dokta Nchimbi. 

  Aidha, Dkt. Nchimbi amewaaigiza watendaji wa vijiji na kata kusimamia na kutunza miundo mbinu mbalimbali ikiwemo ya maji katika maeneo yao huku akielekeza kuwa endapo uharibifu utatokea mtendaji aliyepo katika eneo husika atawajibishwa kwa uzembe. 

  Awali Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Nchimbi ametembelea chanzo cha maji cha Mwankoko kinachotoa maji katika halmashauri ya manispaa ya Singida na kisha kupanda miti ili kutunza mazingira na kuhifadhi chanzo hizo.

  Akitoa taarifa ya chanzo hicho, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA) mjini Singida Hosea Maghimbi amesema zaidi ya shilingi bilioni 1.5 sawa na asilimia 99.2 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2016/17 kwa ajili ya fidia kwa wakazi walio jirani na chanzo hicho.

  Maghimbi amesema SUWASA iko katika ujenzi wa mradi wa mtandao wa maji na mfumo wa maji safi Singida mjini pamoja na kuboresha huduma ya maji kwa miji midogo ya Manyoni na Kiomboi.

  Amesema baadhi ya changamoto zinazokabili SUWASA ni pamoja na wateja kutolipa madeni kwa wakati hasa taasisi za serikali, wateja wanaokatiwa huduma kwa sababu ya madeni kutorejeshewa huduma hizo na badala yake kununua maji kwa majirani, kujifungia maji na kuchepusha dira za maji.

  Maghimbi ametoa wito kwa wananchi kutokata miti, kuchoma moto, kuchungia mifungo na kufanya shughuli zangine za binadamu kwenye vyanzo vya maji. 

  “Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi kufichua watu wanaojiunganishia maji kiholela, wanaojifungia maji na kuchepusha dira ya maji, kwamba SUWASA inatoa zawadi ya shillingi 50,000 kwa ye yote atakayetoa taarifa sahihi kuhusiana na watu hao, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria”, amesema Maghimbi.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akijitwisha ndoo ya maji baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama ikiwa ni maadhimishi ya kilele cha wiki ya maji yaliyofanyika katika kijiji hicho cha Iguguno, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mkalama Injinia Jakson Masaka.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Iguguno wilaya ya Mkalama Bi Joyce ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kilele cha wiki ya maji.
  Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akihutubia baadhi ya wananchi wa kijiji cha Iguguno Wilaya ya Mkalama kwenye maadhimishio ya kilele cha wiki ya maji. Pamoja na mambo mengine Dkt. Nchimbi ameagiza askari wa usalama barabarani kupanda miti ya matunda ili waweze kula matunda kuboresha afya za macho yao waweze kuona vizuri kipindi wanatekeleza majukumu yao barabarani.

  0 0

  Na Lulu Mussa,Mwanga - Kilimanjaro .

  Imebainika kuwa Ziwa Jipe liko hatarini kutoweka endapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika kulinusuru. Hayo yamesemwa  na Waziri mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira Mh. January Makamba alipofanya ziara ya kukagua ziwa hilo ambalo sehemu kubwa imezungukwa na magugu maji.

  Waziri Makamba amesema kuwa ziwa hilo ni rasilimali muhimu na hivyo ni lazima kuwe na mpango wa muda mfupi na ule wa muda mrefu. Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamiza wa Mazingira (NEMC) ameazimia kutangaza kupita Tangazo la Serikali kuwa eneo hilo ni eneo nyeti kimazingira."Tutatanga eneo hili kuwa eneo nyeti kimazingira na tutaweka masharti ya matumizi katika eneo hili" Alisisitiza Makamba.

  Azimio hilo la kutangaza kuwa eneo mahsusi ama nyeti kimazingira itasaidi katika kuandika maandiko mbalimbali ya miradi na kupata fedha kutoka kwa wadau na washirika wa maendeleo. Pia litawekwa chini ya uangalizi maalumu na kuweka masharti ya matumizi bora ya eneo hilo. " Tutaweka masharti makali na magumu zaidi ili watakao kiuka wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria" Aliongezea Waziri Makamba.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Mtendaji wa Kijiji cha Butu, Kata ya Jipe Wilayani Mwanga Bw. Nassor Abdul wakati Waziri Makamba alipotembelea Ziwa Jipe ambalo limeathiriwa kwa kiasi kikubwa na magugu maji ambayo yanasababisha kupungua kwa shughuli za uvuvi ambazo ndio chanzo kikubwa cha mapato kwa wakazi wa eneo hilo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Bw. Aron Mbogho.
   Mifano kwa vitendo: Pichani Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwa amembeba mtoto Meshack Ombeni  katika Kijiji cha Butu pembezoni mwa Ziwa Jipe. Waziri Makamba amewaasa wananchi hao kulinda Ziwa hilo ili liweze kunifaisha vizazi vijavyo na kuwatahadharisha kuwa uharibifu wa mazingira utahatarisha uhai wa ziwa hilo. .
  Upungufu mkubwa maji katika bwawa la nyumba ya Mungu. Inasemekana kupungua kwa kina cha maji kunatokana na ukame wa muda mrefu na uharibifu mkubwa  wa mazingira kutokana na shughuli za binadamu katika vyanzo vya maji vinavyopeleka maji katika bwawa hilo ukiwemo Mto Kikuletwa. Kwa tarifa kamili BOFYA HAPA

  0 0


  Na,Abel Daud-Globu ya Jamii Kigoma.

  Wakati Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania ikiunga mkono juhudi zinazofanywa na Asasi,Makanisa,Mashirika na watu binafsi,wamisionari wa kanisa la Baptist kutoka Marekani wameunga mkono juhudi za serikali kwa kujenga jengo la wodi ya watoto katika hospitali teule ya Manispaa ya Kigoma Ujiji lenye thamani ya shilingi milion 420.

  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga-akizindua jengo hilo ameupongeza uongozi wa kanisa hilo na kusema kuwa serikali inaendelea kuchukua hatua ili kumaliza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya,ikiwa ni pamoja na kuwataka wakazi wa kigoma kutumia jengo hilo vizuri na kupata huduma zitakazotolewa ili kuimalisha afya za watoto.

  Aidha akisoma risala ya uzinduzi wa jengo hilo katibu wa Hospitali teule ya Manispaa ya kigoma ujiji Bw.Anania Raiton ameeleza kuwa bado kuna changamoto nyingi katika sekta ya afya,na kuongeza kuwa kama serikali itachukua hatua katika kumaliza changamoti hizo za huduma itakayo kuwa inatolewa kwa uma,itasaidia kuokoa maisha ya wahitaji wa matibabu.

  Hata hivyo kwa upande wao wafadhili wa jengo hilo akiwemo Dr.Larry Pepper ambaye ni mwakilishi wa wafadhili katika hospitali ya Baptist ameeleza kuwa gharama zilizotumika ni kubwa,hivyo ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma kutumia huduma vizuri ikiwa ni pamoja na kuepuka kuharibu vifaa ambayo vitatumika kutolea huduma.

  Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Baptist Kilawa Shido amesema kuwa kuwepo sasa kwa jengo hilo,wakazi wa Kigoma watarajie kunufaika sambamba na kutoa shukurani kwa wafadhili,huku akiitaka serikali kuongeza wahudumu katika sekta ya afya kwani uhitaji wao ni mkubwa mno.

  Pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Samson Anga akikata utepe kuashiria uzinduzi jengo la wodi ya watoto katika hospitali teule ya Manispaa ya Kigoma Ujiji lenye thamani ya shilingi milion 420.
  Baadhi ya Vitanda hivyo vilivyomo ndani ya wodi ya watoto .

  Mganga Mfawidhi wa Hospital ya Baptist Kilawa Shido akimuelezea Mkuu wa Wilaya Samson Anga jinsi kifaa hicho kitakavyokuwa kinafanya kazi.  Baadhi ya Vitanda vingine vilivyomo wodini humo.

  Jengo la wodi ya watoto lililozinduliwa .


  0 0

  KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka chini ya Mwenyekiti wake Alex Msama, amemtangaza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Tamaska la mwaka huu utakaofanyika April 16 katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuelezea maandalizi ya tukio hilo linalowaleta watu wengi bila kujali tofauti za dini zao kusikiliza ujumbe wa Neno la Mungu kupitia nyimbo mbalimbali, Msama wao wamefurahi kuona Mama Samia amekubali kubeba jukumu hilo kwa mikono miwili.

  Msama alisema pamoja na Mama Samia kukubali kubeba jukumu hilo lenye heshima na hadhi yake katika jamii, pia amemteua Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kumwakilisha kwani siku hiyo atakuwa nje ya nchi.

  “Tunamshukuru Mama yetu Makamu wa Rais, Mama Samia kwa kukubali kubeba jukumu la Tamasha la Pasaka kwa sababu ni jambo kubwa kweyu sisi waandaaji. Kwa mikono miwili amekubali heshima hiyo, lakini kutiokana na siku hiyo atakuwa nje ya nchi, amemteua Waziri Mwigulu kumwakilisha,” alisema Msama.

  Alisema baada ya Uwanja wa Uhuru, siku itakayofuata uhondo huo utakuwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kabla ya kwenda Simiyu, Mwanza, Shinyanga na Iringa kwa tarehe zitakazotajwa kulingana na ratiba kamili.

  Kuhusu waimbaji, Msama amesema waimbaji watatu kutoka Kenya, wamethibitisha kushiriki Tamasha hilo ambao ni mwimbaji mkongwe, Faustine Muhishi, Danny ‘M’ na Messi Masika ambao watashirikiana na wengine waliotajwa.
   
  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi  wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Tamasha la Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi  wa habari jijini Dar es Salaam, wakati akimtangaza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


  0 0
  0 0
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo,(wanne kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (watano kushoto), Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI (anayeshughulikia Afya), Dkt. Zainabu Chaula,(kulia), Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe. Daniel Chongolo, (wapili kushoto), na viongozi wengine, wakiangalia kitanda cha kujifungulia wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa tiba vilivyotolewa na PPF.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mhe. Jenista Mhagama,(watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kushoto), Viongozi wa Mkoa wa Arusha na Wilaya ya Longido, wakitembelea wodi ya wagonjwa ya Kituo cha Afya Longido, ambapo ni moja kati ya vituo vilivyonufaika na msaada huo wa vifaa tiba kama sehemu ya mchango  wa PPF kwenye Jamii.

  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
  MFUKO wa Pensheni wa PPF, umekabidhi vifaa tiba katika Mkutano wake wa 26 wa Wanachama na Wadau. Vifaa tiba hivyo vyenye jumla ya shilingi 99,983,700/- vilikabidhiwa kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango kwa niaba ya Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa PPF.
  Msaada huo utatolewa katika hospitali na vituo vya afya 16 nchini kama mchango wa PPF kwa shughuli za kijamii.
  Wakati wa kufunga Mkutano huo, mgeni rasmi Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu aliungana na Bodi ya Wadhamini wa PPF, Menejimenti na baadhi ya Wafanyakazi wa PPF walienda kukabidhi vifaa tiba hivyo katika Kituo cha Afya, Longido, ambacho ni moja kati ya vituo vya  Afya 16 nchini vitakavyonufaika na  msaada wa vifaa hivyo.
  Mhe. Jenista Mhagama, alisema, PPF imefanya jambo zuri la kusaidia Jamii na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwapatia huduma bora za afya wananchi wake.
  “Hivi sasa akina mama wa Longido, mtajifungua katika mazingira mazuri nimeona kati ya vifaa tiba vilivyotolewa leo ni pamoja na kitanda cha kujifungulia hongereni sana PPF.” Alisema Mhe. Mhagama.Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, alisema, msaada wa vifaa hivyo ni moja ya majukumu ya Mfuko kusaidia jamii.(CSR), hivyo PPF itatoa msaada kama huo kwa hospitali na vituo vya afya vingine 15.
  Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, Dkt. Zainabu Chaula,Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Longido, Mhe.Daniel Chongolo, na  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Bw.Juma Mhina.
   Waziri Mhe. Mhagama akitoahotuba yake
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Ramadhan Khijjah, (aliyesimama), akitoahotuba yake
   Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, akitoa hotuba yake
  Wakurugenzi wa PPF; Waliovaa suti kutoka kushoto, Mkurugenziwa Mifumo ya Kompyuta, Bw. Riobert Mtendamema, Mkurugenzi wa Fedha, Bw. Martin Mmari, Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji, Bw.Steven Alfred na Meneja Kiongozi, Uandikishaji wanachama na Elimu, Mbarouk Magawa
   Mkuu wa Mkoawa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, akitoa hotuba yake
   Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Bw. William Erio, (wapili kulia), akizungumza jambo na mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bi.Sara Barahomoka
   Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Bw. Aggrey Mlimuka, (katikati), Mjumbe wa Bodi Bi.Amelye Nyembe, (kushoto), na Mkurugebnzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Longido, Bw. Juma Mhina, wakiwa kwenye hafla hiyo
   Mkurugenzi wa Udhibiti Majanga wa PPF, Bi. Uphoo Swai, (katikati), akiwa na mwenyeji wa Longido wakifuatilia hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Fedha wa PPF, Bw. Martin Mmari
   Wakurugenzi na Mameneja wa PPF pamoja na watumishi wa Halmashauriya Wilaya ya Longido wakijumuika kwenye hafla hiyo
   Wananchi wa Longido walikuwa ni mashahidi wakati wa kupokea msaada huo
  Mkurugenzi Mkuu wa PPF naujumbe wake wakipokewa na viongozi wa Kituo cha Afya Lungido walipowasili kukabidhi msaada huo

  0 0

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakizindua huduma za mtandao wenye kasi zaidi wa 4G wa Zantel na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni hiyo kwa kushirikiana na Benki hiyo kisiwani Pemba. Wanaoshughudia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kushoto) na Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba. 

  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki zinazofuata misingi ya Kiislamu wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ) Said Mohamed Said wakipongezana mara baada ya uzinduzi wa mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na benki hiyo kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Katikati ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada (wa tatu kushoto) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel Tanzania Benoit Janin (wa pili kushoto), Mkuu wa Zantel-Zanzibar, Mohamed Musa Baucha (kushoto) na Meneja wa Benki ya watu wa Zanzibar-Pemba Mohamed Musa (kulia) mara baada ya kuzindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.
  Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuzindua rasmi mtandao wenye kasi zaidi wa 4G na huduma za kibenki zinazofuata kanuni za kiislamu zitakazotolewa kwa njia ya simu na Kampuni ya Zantel kwa kushirikiana na Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) kwa wananchi wa kisiwani Pemba. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki Kisiwani Pemba.


  Kampuni ya mawasiliano ya ZANTEL imezindua mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma za kibenki zinazozingatia kanuni za kiislamu kwa njia ya simu ikiwa ni hatua ya kuboresha na kupanua huduma zake kwa wateja. 

  Katika hatua ya kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya simu, Zantel imeshirikiana na BENKI ya watu wa Zanzibar (PBZ) katika kuhakikisha wateja wake wanapata huduma zote za kibenki kama vile kuweka au kutoa fedha, mikopo, kulipia ankara zao za huduma mbalimbali kama vile maji, umeme au kununua vocha za simu n.k. 

  Akizindua huduma hizo leo (23/03/2017) kisiwani Pemba, Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Mohamed Ahmada alisema huduma hizo kutoka Zantel zimekuja katika wakati muafaka kwa wananchi wa Pemba na kuongeza kuwa yeye na Wizara yake wanaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na mitandao mingine ya simu katika kuhakikisha huduma za simu zinaboreshwa zaidi visiwani humo. 

  “Uzinduzi wa huduma ya mtandao wenye kasi zaidi wa 4G sambamba na huduma ya kibenki kwa njia ya simu ni vitu ambavyo wananchi wa Pemba wamekua wakivisubiria kwa muda mrefu. Niipongeze Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kwa kulitambua jambo hili na kulifanyia kazi kwa haraka” alisema. 

  Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin amesema uzinduzi wa huduma hizo mpya ni moja kati ya jitihada zinazofanywa na kampuni yake katika kutoa huduma zenye ubora nchini ili kutimiza mahitaji mbalimbali ya wateja wao. 

  Aliongeza kuwa huduma ya kibenki kwa njia ya simu za mkononi imewalenga watu wote ila zaidi ikiwa ni jamii ya kiislamu kwani inazingatia kanuni na misingi yote ya kiislamu wakati wa utoaji wa huduma. 

  “Pamoja na kurahishisha huduma za kibenki huduma kwa njia ya simu, huduma hii pia itasaidia kuokoa muda, ni huduma rafiki kwa kila mtu na yenye usalama mkubwa” alisema Benoit. 

  Kwa mujibu wa Taarifa za Benki kuu ya Tanzania (BoT) ni kuwa watumiaji wa huduma za kifedha kupitia simu za mikononi wamefanya miamala yenye thamani ya bilioni 988.9 katika kipindi cha pili cha mwaka jana,huku mitandao ya simu ikigeuka kuwa njia muhimu katika miamala ya malipo mbalimbali. 

  Janin aliendelea kuwahakikishia wateja wa Zantel kuwa kampuni ya Zantel imekuwa katika ushindani kwa muda mrefu na kuwa bado wanaendelea kuwekeza ili kuhakikisha wateja wake wanapata huduma bora zaidi kwa kiwango kikubwa na teknolojia bora zaidi 

  “Tutaendelea kufikisha huduma hizi kwenda sehemu mbalimbali za hapa nchini, huu ni mwanzo tu kwa wateja wa Zantel ningependa wategemee mambo mazuri zaidi”. 

  Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Zantel, inaongoza kwa asilimia 80 kwenye soko la mitando ya simu kwa Zanzibar na ndiyo kampuni ya kwanza kutambulisha huduma za kibenki kwa njia ya simu hapa nchini. 

  Ni hivi karibuni tu ambapo, Zantel kwa kushirikiana na Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) walizindua huduma mpya ya “Zantel Madrasa” inayolenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha wadau wa dini hiyo kujifunza zaidi juu ya uislamu kwa kupitia simu zao za mikononi au kujipatia jumbe mbalimbali na mawaidha ya kiislamu kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15586. 

  0 0


  Na Rhoda Ezekiel Kigoma,


  KAMATI ya ulinzi na Usalama Wilayani Kasulu imeteketeza Shamba la bhangi hekari moja iliyo kuwa ikilimwa katika hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusini pamoja na kukamata Watuhumiwa wanne wawili wakiwa ni raia wa Burundi wakiwa wanatumiwa katika Kilimo cha hicho.

  Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali Marko Gaguti wakati wa kuteketeza shamba hilo alisema kumekuwa na tabia ya wakulima wengi kulima bhangi pembezoni mwa mji wakichanganya na mazao Mengine suala linalopelekea watoto wengi kuharibika na uharifu kuongezeka.

  Gaguti alisema baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Wananchi kwamba kuna mtu analima bhangi jeshi la polisi kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama ilifanya msako na kukamata shamba la Mkulima, Yotham Ngeze aliekuwa akiwatumia vibarua wanne wakiwemo warundi wawili na vijana wawili ambao walikuwa wakilima shamba hilo.

  Aidha Gaguti aliwataka wakulima kuacha tabia ya kulima bhangi zao ambalo ni haramu na badala yake watumie aridhi nzuri waliyo nayo kulima mazao ya chakula kutokana na hali ya upatikanaji wa chakula ulivyo kwa sasa, na kwa atakae kutwa analima zao hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake Serikali inamacho mengi wataendelea kuwafuatilia popote pale .


  Pia Mkuu huyo aliwataka Wakulima kuacha tabia ya kuwatumia Wahamiaji haramu katika mashamba yao hali inayo sababisha Migogoro ya Wakulima kuongezeka kutokana na ugomvi unaotokea baada ya kuwatumia vibarua hao na kuacha kuwalipa, kulikuwa na kesi nyingi za raia kutoka Burundi kuwauwa watanzania kwa kuwalipizia kisasi baada ya kuwatumia bila malipo.


  "Niwaombe wakulima Muachane na tabia ya kuja kulima bhangi katika hifadhi zetu za misitu uhalifu umekuwa ukiongezeka kila siku ni kutokana na Vijana wanapo tumia madawa ya kulevya wengi wao huishia kufanya uhalifu na wengine kushindwa kuendelea na masomo hatutavumilia watoto wetu na Wananchi waendelee kuteseka tutakae Mkamata atalipa faini na kifungo pia",alisema Gaguti.

  Kwa upande wake Kamanda Wa jeshi la polisi Mkoa wa Kigoma DCP Fredinandi Mtui alisema kwa Kipindi cha mwezi mmoja huu wa tatu walikamata hekari saba za bhangi na watuhumiwa nane, ambapo hekari sita ziliteketezwa katika Wilaya ya Kakonko na Hekari moja katika Wilaya ya Kasulu na jeshi la polisi linaendelea na kuwasaka wote wanao lima na kutumia bhangi ilikuweza kukomesha madawa ya kulevya.

  Nae Mmiliki wa shamba la bhangi katika msitu wa hifadhi Makere Yotham Ngeze alikili kulima zao hilo na kwamba analima kwaajili ya matumizi yake binafsi na kwamba anapo tumia bhangi anajikuta anafanya kazi kubwa sana ya kulima kwa siku anaweza kulima nusu heka akiwa amwtumia zao hili.

  Alisema alianza kutumia bhangi tangu mwaka 1973 akiwa katika Mashamba ya Mikonge Mkoani tabora na amekuwa akilima zao hilo liweze kumsaidia kupata bhangi kwa urahisi kutokana na mazoea aliyo jiwekea tangu akiwa kijana hawezi kuishi bila bhangi.

  Nao baadhi ya vijana waliokuwa wakimlimi0a mzee huyo akiwemo Simoni Ndayahimana raia wa Burundi wamejikuta wakianza matumizi ya bhangi baada ya kulima katika shamba hilo hali inayopelekea vijana wengi kupoteza nguvu kazi kutokana na matumizi na ulimaji wa madawa ya kulevya.
  Kaimu Mkuu wa wilaya ya Kasulu ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwa Kanali Marko Gaguti akishiriki kuteketeza bhangi iliyokuwa imelimwa huku ikiwa imechanganywa na mazao mengine
  Zoezi la kuteketeza Bhangi likindelea
  Baadhi ya Watuhumiwa waliokamatwa wakiohojiwa na vyombo vya habari kufuatia kukamatwa kwa tuhuma za kulima Bhangi katika hifadhi ya poli la Akiba Makere Kusin,

  0 0
  Afisa kilimo na Mratibu wa MIVARF Mkoa wa Singida akimsikiliza mkulima wa Alizeti Mkoa wa Singida akipalilia zao hilo, mkulima huyu amefuata ushauri wa kitaalamu wa kupanda kwa mistari, kuweka mbolea na kutumia mbegu mpya ya record ambayo huzalisha kwa wingi.
  Mkulima wa Alizeti Mkoa wa Singida akipalilia zao hilo, mkulima huyu amefuata ushauri wa kitaalamu wa kupanda kwa mistari, kuweka mbolea na kutumia mbegu mpya ya record ambayo huzalisha kwa wingi.

  Wakulima wa alizeti Mkoani Singida wameazimia kuwa wazalishaji namba moja nchini wa alizeti kwa wingi na ubora wa hali ya juu kutokana na kutumia mbinu bora na za kisasa huku wakiachana na kilimo cha mazoea kilichowapa matokeo kidogo na yasiyo na ubora.

  Wakulima wa Wilaya tatu za Iramba, Manyoni na Singida wamefikia uamuzi huo katika vikao kati yao na kamati ya ufuatiliaji wa progamu ya Uboreshaji wa Miundombinu ya Masoko, Uongezaji wa thamani ya mazao na Huduma za kifedha vijijini (MIVARF) iliyokuwa ikifanya tahmini ya mradi huo kwa kutembelea mashamba na kuzungumza na wakulima hao.

  Mwenyekiti wa Kikundi cha Mwangaza cha wakulima wa Alizeti kata ya Sanjaranda Wilayani Manyoni Bi. Janeth Emmanuel amesema, mradi wa MIVARF umewahamasisha kutumia mbegu ya alizeti ya kisasa aina ya record ambayo huzalisha wastani wa gunia 12 mpaka 16 kwa ekari moja wakati mbegu ya zamani ambayo walikuwa wakiitumia ya zebra imekuwa ikizalisha gunia mbili mpaka nne kwa ekari moja.

  Bi Janeth amesema kutokana na wakulima wengi kuhamasika kutumia mbegu mpya ya record na kufuata elimu waliyopewa na MIVARF, Mkoa wa Singida utazalisha alizeti nyingi na bora kwa ajili ya viwanda vya ndani na nje ya Mkoa.

  Amesema wakulima wa alizeti walikua hawafuati ushauri wa kupanda zao hilo kwa mistari, kuacha nafasi pamoja na kuweka mbolea ambapo awali walidhani alizeti haihitaji kuwekewa mbolea kitu ambacho sio sahihi na hivyo kupelekea mkulima kutumia eneo kubwa na kuzalisha kidogo.

  Bi. Janeth ameongeza kuwa kutokana na matarajio ya kuvuna alizeti nyingi elimu zaidi juu ya uongezaji wa thamani wa alizeti itolewe kwa wakulima ili waweze kupata faida kubwa tofauti na awali ambapo wamekuwa wakimwaga mashudu ambayo huzalisha kiwi na mkaa na kuuza alizeti ghafi badala ya mafuta.

  Naye Mtoa huduma wa MIVARF Wilaya ya Manyoni Anthony Mtu amesema mradi huo umewafikia wakulima elfu mbili katika kata ya Sanjarada huku wakianzisha mashamba darasa 12 ya zao la alizeti yenye ukubwa wa ekari 24 huku matarajio ya mavuno kwa mashamba darasa yakiwa ni magunia 288.

  Mtu amesema wakulima wamehamasika kutumia mbegu ya record baada ya kuelimishwa kuwa mbegu hiyo, inatumia maji kwa ufanisi, inatoa mavuno mengi na haishambuliwi na magonjwa kwa urahisi.

  Kwa upande wake Afisa Kilimo na Mratibu wa MIVARF Mkoa wa Singida Lucas Mkuki amesema mradi huo umeanza kutekelezwa mwaka 2011 ukiwa unafadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

  Mkuki amesema katika wilaya zote Mradi umeweza kukarabati barabara ili kurahisisha wakulima kusafirisha alizeti ambapo barabara zilizokarabatiwa ni ya Muhanga-Mwakajenga wilaya ya Manyoni kilometa 20, Njiapanda-Ngimu Wilayani Singida Kilometa 28 na wilayani Iramba kilometa 1.4 ujenzi wake utaanza hivi karibuni.

  Ameongeza kuwa mradi umefanikisha ujenzi wa maghala yenye uwezo wa kuhifadhi mazao kiasi cha tani 1000 katika kijiji cha Mtinko wilayani Singida, kijiji cha Nselembwe wilayani Manyoni na kijiji cha Sanjaranda wilayani Manyoni.

  Mkuki amesema mradi wa MIVARF umewajengea uwezo wazalishaji wa alizeti kuyafikia masoko na kuongeza thamani ya zao hilo huku akiwasisitiza wakulima kuendeleza elimu na vikundi vilivyozalishwa na mradi huo endapo mradi utafikia ukomo wa utekelezaji wake.

  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Nakala ya Vitabu vya  Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016, kutoka kwa CAG  Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   . Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa anapiga makofi pamoja na Katibu Mkuu Ikulu, Alphayo Kidata mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kupokea Ripoti hizo kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo za Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad mara baada ya kupokea ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Katibu Mkuu wa Ikulu Alphayo Kidata pamoja na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wakati akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Ripoti hizo kutoka kwa CAG Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad akizungumza kabla ya kuwasilisha Ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam.  
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea Ripoti hizo ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad Ikulu jijini Dar es Salaam. 
  Maafisa kutoka katika Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) wakifatilia kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa Ripoti hizo Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU
  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakiongozwa na askari wa kikosi cha bendera kuingia ukumbini kwa ajili ya ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akitoa hotuba ufunguzi wa kikao kazi cha mwaka kinachowahusisha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) akiongea na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa wakuu wa jeshi la Polisi na makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.
  Baadhi ya maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi wakiimba wimbo wa maadili ya afisa wa polisi wakati wa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi cha maafisa hao na  makamanda wa mikoa na vikosi kinachofanyika mkoani Dodoma. Picha na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi. Picha Na Hassan Mndeme.

  Na Frank Geofray-Jeshi la Polisi.

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba amewataka maofisa na askari Polisi kote nchini kuendelea kufanya kazi kwa uadilifu ili kujenga taswira nzuri kwa wananchi wanaowahudumia jambo ambalo litaongeza imani na ushirikiano katika kukomesha vitendo vya uhalifu nchini.

  Waziri Nchemba ameyasema hayo wakati alipokuwa akifungua kikao kazi cha Maofisa wakuu wa Jeshi la Polisi kutoka makao makuu, Makamanda wa Polisi wa Mikoa na vikosi kutoka bara na Zanzibar kinachoendelea mkoani Dodoma.

  Alisema Pamoja na Jeshi hilo kufanya kazi nzuri bado linakabiliwa na changamoto ya baadhi ya askari na maofisa wasio waadilifu wanaofanya vitendo vya  kuwabambikia wananchi kesi na wakati mwingine kuwabadilishia kesi ili kujenga mazingira ya kupatiwa rushwa jambo ambalo ni kinyume na maadili ya askari Polisi.

  “Fanyeni kazi kwa weledi hasa kwa kuwasimamia waliopo chini yenu kwa kuwa wapo baadhi yao bado hawataki kubadilika na katika awamu hii lengo letu ni kutoa haki kwa maskini hivyo ninyi kama wasimamizi wa sheria mnapaswa kutenda haki mnapofanya kazi zenu na wale wasiotaka kubadilika hamna budi kuchukua hatua ” Alisema Nchemba.

  Aidha alilitaka Jeshi hilo kuwachukulia hatua bodaboda wanaofanya makosa na wale wasiokuwa na makosa waachwe waendelee na majukumu yao ya kujipatia kipato na kuachana na dhana ya kuwa kila bodaboda ni mhalifu.
  Kwa upande wake Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Ernest Mangu alisema kikao hicho kinafanyika kwa siku tatu kwa lengo la kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka uliopita na kuweka mikakati kwa mwaka huu ili kuendeleza juhudi za kukabiliana na vitendo vya uhalifu hapa nchini.

  Mangu alisema Jeshi hilo litaendelea na Oparesheni zake za kupambana na uhalifu zikiwemo za dawa za kulevya, uhalifu wa kutumia silaha na wizi wa mtandao kwa mikakati mipya ambayo itaibuliwa katika kikao kazi hicho ili kuhakikisha hakuna mhalifu anayetamba hapa nchini.

  Naye Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge mambo ya nje na usalama Balozi Adadi Rajabu alisema kamati hiyo itaendelea kuishawishi Serikali kuboresha maslahi na vitendea kazi vya Jeshi la Polisi ili Jeshi hilo liweze kufanya kazi zake kwa ufanisi.

  Ufunguzi wa Kikao kazi hicho ulihudhriwa pia na Waziri Mkuu mstaafu Samweli Malechela, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana pamoja na baadhi ya wabunge na Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dodoma.


  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Vikundi mbalimbali vya Jogging viliweza kufanya mazoezi kwa pamoja kwa mbio zilizoanzia Uwanja wa Taifa na kumalizikia viwanja vya Mwembe Yanga na kuhamasisha ushirikiano baina yao.

  Mbio hizo zilizofanyika jana, vilikutanisha vikundi zaidi ya 15 kutoka sehemu mbalimbali za wilaya ya Temeke pamoja na baadhi kutoka wilaya ya Kinondoni ikiwa ni kuunga mkono katila jitihada za ushirikiano baina yao.

  Mwenyeji wa Mbio hizo Kikundi cha Dar Jogging kutoka maeneo ya Chang'ombe kiliwaalika vikundi vingine ikiwa ni moja ya malengo ya kujenga ushirikiano baina yao ikiwemo kujihusisha na masuala ya upatu (saccoss).

  Mwenyekiti wa umoja wa vikundi hivyo ujulikanao kama Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia amesema kuwa vikundi hivyo vinatakiwa kushirikiana kwa njia mbalimbali ili kuweza kujiwezesha kiuchumi na zaidi kuanzishwa kwa upatu baina yao ni mwanzo mzuri wa maendeleo.

  Amesema kuwa, kuanzishwa kwa upatu baina ya vikundi ni moja ya malengo chanya katika kujiinua kiuchumi na kuweza kuanzisha miradi mbalimbali itakayokuwa inasimamiwa na wana vikundi hao ambapo amewapongeza Dar Jogging kwa hatua waliyofikia.

  Naye Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka amewashukuru vikundi vya Jogging vilivyokubali mwaliko wao na zaidi amewataka kushirikiana kwa pamoja kuona wanatafuta ufumbuzi wa masuala yanayowakabili hususani kwenye vikundi mbalimbali na changamoto wanazokutana nazo.

  Namkoveka ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea (TSA) amesema katika fedha walizozipokea za Upatu takribani kiasi cha shilingi laki saba (700,000) watahakikisha wanazifanyia malengo waliyoyapangia ikiwemo kuhitaji kununua boda boda za kufanyia biashara.
   Mwenyekiti wa Kikundi cha Dar Jogging and Sports Club akiwa anazungumza na wanajogging waliojitoeza katika mbio hizo zikiwa na malengo ya kuhamasisha ushirikiano baina yao na kujitafutia njia za kujiinua kiuchumi jana kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga.
   Mwenyekiti wa umoja wa vikundi  Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia akizungumza na wanajogging waliojitoeza katika mbio hizo zikiwa na malengo ya kuhamasisha ushirikiano baina yao na kujitafutia njia za kujiinua kiuchumi jana kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga.
   Mwenyekiti wa umoja wa vikundi  Temeke Jogging Association (TEJA) Mussa Mtulia akikabidhi pesa taslimu kiasi cha shillingi laki sabai (700,000) zilizopatikana katika mchezo wa upatu unaochezwa na vikundi hivyo vya Jogging akishuhudiwa na wajumbe wengine kutoka umoja wa vikundi hivyo. 
  Wanachama wa kikundi cha Dar Jogging wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mbio hizo.
  Vikundi vya Jogging wakiwa katika mazoezi.Picha na Zainab Nyamka.

  0 0
  Meneja Mauzo wa mkoa wa Pwani, Philiph Nkupama (watatu kushoto) akimweleza jambo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Maisha Maganga wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel lililopo maeneo ya stendi ya Msamvu mkoani Morogoro. Ambapo Airtel ilitangaa rasmi maduka 15 mapya ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
  Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Maisha Maganga akiongea wakati wa uzinduzi wa duka la Airtel l lililopo maeneo ya stendi ya Msamvu mkoani Morogoro ambapo Airtel pia ilitangaa rasmi maduka 15 mapya ambayo yanatoa huduma katika maeneo mbalimbali mkoani hapo.
   
   kufuatia kutangaza mpango wake wa kuzindua maduka zaidi ya 2000 nchi nzima, kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua maduka 15 katika mkoa wa morogoro kwa lengo la kuhakikisha bidhaa na huduma zake zinawafikia wateja wake kwa ukaribu na urahisi zaidi

  Akiongea wakati wa uzinduzi , Meneja Mauzo kanda ya Morogoro, Albert Mtalemwa alisema “ leo tunazindua maduka 15 mojawapo likiwa hapa ndani ya kituo cha mabasi kilichopo Msavu Morogoro kwa lengo la kuwawezesha wasafiri na wale wanaoingia kutoka maeneo mbalimbali, wafanyabiashara na wakazi wa Morogoro wanaotembelea kituo hiki kupata huduma zetu za Airtel husasani huduma ya kifedha kupitia simu za mkononi kwa urahisi zaidi na wakati wowote.

  Maduka mengi ya Airtel ambayo yanafanya kazi ya kutoa huduma yapo katika maeneo mbalimbali ambayo ni pamoja na Itigi, Gairo,Kilombero na,mjini, Kilosa karibu na kituo cha mabasi, Kimamba mjini, Ruaha, Dumila, Dakawa karibu na soko, Mikese karibu na mizani, kituo cha Kisaki, Soko la Bwawani, Ifakara mjini na Ifakara kituo cha basi.

  Lengo letu ni kuziweka huduma zetu karibu na wateja wetu ili kutatua changamoto zao za mawasiliano kwa wakati na kuwawezesha kupata huduma za kifedha kwa urahisi. Tunaamini maduka haya yataongeza idadi ya vituo vyetu na kuboresha kiwango katika huduma zetu”. aliongeza Mtalemwa

  Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, , Maisha Maganga alisema” nawapongeza sana Airtel kwa mpango huu unaochochea kuboresha huduma zake kwa wateja lakini pia kuhakikisha usalama katika huduma za kifedha kupitia maduka haya. 
   
  Hii ni fursa pekee kwa kwa wenye maduka kushirikiana na Airtel na kuongeza mitaji yao lakini pia tunaamini kupitia maduka haya yataongeza ajira kwa vijana na kuboresha usalama wakazi na pesa zao kwani sasa wakazi wa maeneo ya hapa yatatunza pesa zao kwenye simu na kuzitoa kwa urahisi kupitia maduka haya

  Uzinduzi wa maduka ya Morogoro umefatiwa na uzinduzi wa maduka 8 mkoani Shinyanga wiki iliyopita na huku mpango wake mzima ni kuwa na maduka mengine kama hayo ya 2000 nchi nzima

  0 0  Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kulia akipokea taarifa ya Tume aliyounda kuchunguza kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele jijini  Dar es Salaam leo
  Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa kulia akionyesha taarifa ya Tume aliyounda kuchunguza kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele jijini Dar es Salaam leo .  Na: Lilian Lundo - MAELEZO

  Tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza kifo cha Faru John imethibitisha kuwa Faru huyo alikufa katika eneo la Sasakwa Grumeti kutokana na kukosa matunzo, uangalizi wa karibu na matibabu alipoumwa.

  Hayo yamesemwa leo Jijini, Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samwel Manyele alipokuwa akikabidhi ripoti ya uchunguzi wa Kifo cha Faru huyo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

  “Sampuli zilizochukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa vinasaba ni mifupa ambayo ilichukuliwa katika mzoga wa Faru John uliokutwa eneo la Sasakwa Grumeti, Pembe zilizochukuliwa hifadhi ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), damu kutoka maabara ya NCAA na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), ngozi kutoka kwenye mzoga na kinyesi kilichokaushwa kutoka SUA,” alifafanua Prof. Manyele.

  Aliendelea kwa kusema kuwa matokeo ya uchunguzi wa awali yameonyesha damu, pembe, mifupa na ngozi ni vya Faru John ambapo mpangilio wa vinasaba umeonyesho kuwa Faru huyo ni mweusi (Black Rhinoceros) mwenye jinsia ya kiume.

  Aidha vielelezo hivyo vilitumwa Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini ambapo timu ya wataalam kutoka Tanzania chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali walishiriki katika uchunguzi wa awali wa vinasaba na kujadili matokeo kabla ya kuyatuma kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo Matokeo yameonyesha sampuli na vielelezo vyote ni vya mnyama pori Faru John.

  Vile vile amesema, uchunguzi umeonyesha kuwa sababu za kifo cha Faru huyo ni kukosa matunzo, uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria pamoja na mapungufu ya kiuongozi kwa Wizara, Hifadhi na Taasisi zake.

  Baadhi ya mapungufu yaliyobainishwa katika uchunguzi huo ni pamoja na kutokuwepo na kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru John kutoka NCAA kwenda Grumeti.

  Prof. Manyele amesema kuwa hakukuwa na mkataba rasmi kati ya Serikali na mwekezaji unaoonyesha mnyama ametoka Serikalini kwenda kwa Mwekezaji.

  Tume hiyo imeishauri Serikali kuchunguza viwanja vya ndege ndani ya hifadhi vinavyomilikiwa na wawekezaji kutokana na kuwepo na uwezekano wa viwanja hivyo kuwa njia ya majangili au matajiri kufanikiisha shughuli za ujangiri nchini.

  Aidha kutokana na mapungufu ya kiutendaji yaliyofanywa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini (kutokutoa kibali rasmi) na mapungufu ya kiuongozi yaliyofanywa na Mhifadhi wa NCAA kuruhusu Faru John kuondolewa bila kibali, Tume inashauri hatua za kiutawala zichukuliwe dhidi ya wahusika.

  Kwa upande wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza timu hiyo kwa kazi nzuri waliyoifanya. Ameahidi kufanyia kazi maoni ya tume hiyo na kutolea maelezo ya hatua zitakazochukuliwa na Serikali muda mfupi ujayo.

  Tume ya uchunguzi ya kifo cha Faru John iliundwa baada ya Waziri Mkuu kufanya ziara ya kikazi Ngorongoro Disemba 6, 2016, ambapo alibaini kuhamishwa kinyemela kwa faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumeti. 

  Waziri Mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa Faru huyo na kuamua kuunda tume hiyo ili kubaini ukweli wa Faru huyo kama alikufa au alitoroshwa.

  0 0  Na. Georgina Misama – MAELEZO

  Serikali imewataka wamiliki wa ardhi kuhakikisha wanalipia kodi ya pango la ardhi kwa wakati ili kuepuka kunyang’anywa umiliki wa ardhi zao.

  Hayo yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino kutoka Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi. Mboza Lwandiko wakati akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es Salaa.

  Mboza alisema kwamba Wizara inakusudia kufanya mnada wa viwanja takribani 10 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Temeke na Kinondoni ambavyo havijalipiwa kodi ya pango la ardhi mpaka Machi 24, 2017.

  “Usipolipa Kodi ya Pango la Ardhi kwa wakati, utanyanganywa umiliki wa ardhi yako, kutokana na sheria ya Ardhi, Na. 4 ya mwaka 1999, katika kifungu cha 49 na 51”, alisema Mboza.

  Naye Mkuu wa Kitengo cha Kodi kutoka Wizara hiyo Bw. Denis Masami alitoa ufafanuzi wa utaratibu unaotumika kuwasiliana na wamiliki wa ardhi walioshindwa kulipa kodi kwa wakati na kusema kwamba wadaiwa wanapewa hati ya madai na kupewa muda wa kukamilisha madeni yao.

  Muda wa kukamilisha malipo ukipita, amri ya mahakama ya kukamata mali hufuata, ambapo mmiliki wa ardhi atatakiwa kuikomboa ardhi yake kwa kulipa deni mara moja, akishindwa Mahakama hutoa amri ya kuuza mali.

  Mahakama imetoa amri ya kwanza tarehe 27/01/2017 ya kukamata mali kwa wadaiwa sugu na tarehe 24/01/2017 mahakama ilitoa kibali kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuuza kwa mnada wa hadhara viwanja ambavyo havijalipiwa kodi ya pango la ardhi.

  “Tarehe 20 Machi, 2017 Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ilitoa tangazo la mnada wa hadhara wa kuuza viwanja ambavyo havijalipiwa kodi ya ardhi unaotarajiwa kufanyika Machi 26, 2017”, alisema Denis.

  Denis aliongeza kwamba Wizara imeandaa orodha ya wadaiwa sugu, mpaka sasa katika orodha hiyo baadhi ya viwanja vimelipiwa sehemu ya kodi inayodaiwa baada ya wamiliki kuomba kukamilisha sehemu iliyobaki kabla ya kumalizika kwa muhula huo.

  Wizara inatoa rai kwa watanzania wanaomiliki ardhi kujifunza utamaduni wa kulipia kodi pasipo shurti. Kodi ya ardhi hulipiwa kila ifikapo Julai Mosi ya kila mwaka katika Manispaa au Halmashauri husika na katika Ofisi za Malipo ya Kodi-Dar es salaam.

  0 0


  0 0


  Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

  Timu ya Tanzania "Taifa Stars" inatarajiwa kushuka tena kesho Machi 28 katika mchezo wa pili wa kirafiki unaotarajiwa kuanza majira ya saa 10:00 jioni kumenyana na timu ya taifa ya Burundi.

  Stars inaingia tena Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kucheza na Intamba Murugamba ya Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, kwa mujibu wa kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa ya FIFA.

  Huu ni mchezo wa pili kwa Taifa Stars kucheza ndani ya wiki moja baada ya ule wa awali dhidi ya The Zebras ‘Pundamilia’ wa Botswana uliofanyika Uwanja huo wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita.

  Katika mchezo huo wa Jumamosi, Taifa Stars ambayo kwa sasa inanolewa na Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwangata ambao ni makocha wapya wa kikosi hicho, walishinda kwa mabao 2-0.

  Tayari Intamba Murugamba wametua nchini tangu jana Jumapili saa 4.30 asubuhi na kufikia Hoteli ya De Mag iliyoko, Kinondoni, Dar es Salaam na jioni yake walifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Karume, Ilala jijini. Leo Jumatatu, inafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Kwa upande wake, Mayanga alifurahishwa na ushindi wa Jumamosi iliyopita dhidi ya The Zebras ya Botswana na hivyo amehimiza Watanzania kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho.

  Katika kuunga mkono wito wa Kocha Mayanga, TFF imebakiza viingilio vya mchezo huo kuwa sawa na vile vya Jumamosi iliyopita kwani katika mzunguko ambao unachukua mashabiki wengi kiingilio kitakuwa ni Sh 3,000.

  Kwa upande wa VIP “A” Kiingilio kitakuwa ni Sh 15,000 wakati VIP “B” na VIP “C” kiingilio kitakuwa ni Sh 10,000. Viingilio hivyo vimelenga kuwaalika Watanzania wengine kwenda uwanjani.

  0 0

  Na Veronica Simba – Dodoma

  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesaini leseni za madini kutoka kwa wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kutimiza taratibu zote zinazotakiwa kwa mujibu wa sheria.

  Leseni ya kwanza iliyosainiwa ni ya uchimbaji wa kati wa dhahabu katika eneo la Masagalu, Handeni yenye namba ML 570/2016. Leseni hiyo imehamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali ambaye ni Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investments Tanzania Ltd.

  Aidha, Waziri Muhongo alisaini leseni namba ML 572/2017 ya Sisti Mganga. Leseni hiyo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi katika eneo la Itiso, Chamwino mkoani Dodoma.

  Leseni nyingine iliyosainiwa na Waziri Muhongo ni ya uchimbaji wa kati wa madini ya ujenzi aina ya kokoto, ambayo mmiliki wake ni Said Abdallah. Leseni hiyo namba ML 573/2017 ipo eneo la Chipite, Masasi.

  Profesa Muhongo aliwataka waombaji na wamiliki wote wa leseni za madini nchini, kuhakikisha wanatekeleza ipasavyo taratibu zote kama zilivyobainishwa katika Sheria ya Madini ikiwemo ulipaji wa mrabaha na kodi mbalimbali, kujenga mahusiano mema na jamii zinazowazunguka pamoja na kuzingatia utunzaji na uhifadhi wa mazingira.

  Zoezi hilo la utiaji saini lilifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma na kushuhudiwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto), akisaini leseni za madini za wawekezaji mbalimbali waliowasilisha maombi na kukamilisha taratibu zote zinazotakiwa. Anayeshuhudia ni Mwanasheria wa Wizara, Khadija Ramadhan.
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kutoka kulia), akikabidhi leseni iliyohamishwa kutoka kwa mmiliki wake wa awali Najim & Company Ltd kwenda kwa Shale Investment Tanzania Ltd.


  0 0   Askofu wa Kanisa la Good news Minstry Dk. Charles Gadi akizungumza na waandishi wa habari juu ya kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli leo jijini Dar es Salaam.

  Askofu wa Kanisa la Good news Minstry Dk. Charles Gadi amempongeza Rais Dk.Jonh Pombe Magufuli kwa hatua yakuzuia mchanga uliokuwa wanataka kusafirisha nje ya nchi ilikuweza kuchakata dhahabu .

  Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Askofu Gadi amesema kuwa kusafirisha mchanga wa`madini ya dhahau ni sawana kuiuza Tanzania nje ya nchi.

  Amesema kuwa Rais Dk. John Pombe Magufuli amekuwa mtu wa kuthubutu kuona nchi ya Tanzania inakuwa ya maendeleo na wananchi baada wataona mafanikio hayo.

  Gadi amesema kuwa wakiwa viongozi wa dini wanajibu wa kumuombea Rais Dk. John Pombe Magufuli kuwa Tanzania ifanikiwe kutokana na harakati zake. Aidha wa amesema kuwa Tanzania ya viwanda inawezekana kutokana na Rais kuweka kipaumbele kwa wawekezaji ili Tanzania kuingia katika rekodi ya uchumi wa kati .

  0 0


  Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa sekta hiyo, kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Mkoani Dodoma leo.
  Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa Sekta ya Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamuriho (wa pili kulia) na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa sekta hiyo wakiimba wimbo wa ‘Solidarity’ kabla ya kuanza kikao cha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/18, kilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Mkoani Dodoma leo.
  Mkurugenzi wa Sera na Mipango (Sekta ya Uchukuzi), Bw. Gabriel Migire akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/18, kwenye Baraza la Wafanyakazi lilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Mkoani Dodoma leo.
  Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa sekta ya Uchukuzi wakisikiliza taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na mpango wa bajeti kwa mwaka 2017/18, kwenye Baraza la Wafanyakazi lilichofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Mkoani Dodoma leo.

  Picha na Biseko Lisso Ibrahim WUUM (T)

older | 1 | .... | 1183 | 1184 | (Page 1185) | 1186 | 1187 | .... | 1898 | newer