Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live

MTANZANIA OMAR SYKES AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NCHINI MAREKANI.

$
0
0

POLISI wametambua mwili wa mwanafunzi wa Howard University aliyeuawa kwenye jaribio la uhalifu Alhamisi usiku. Omar Sykes, 22, na mwanafunzi mwenzake walikuwa  wanatembea maeneo ya 700 block of Fairmont Street NW kabla ya saa 5.30 usiku walipofuatwa na watu wawili. 


Polisi wanaamini kulikuwa na jaribio la uhalifu ila yalitokea mabishano kabla mmoja ya wale watu kutoa bastola na kumuua Sykes. Alifikia mauti kwenye hospitali ya maeneo ya jirani.


“Tunadhani ilikuwa jambo la ghafla na hatuna uhakika kama wanafunzi hao waliibiwa mali yoyote” alisema Kapteni Bob Alder wa kituo cha polisi DC  alipohojiwa na News4. Mwanafunzi mwingine alipigwa na kitako cha bastola na kujeruhiwa kichwani ingawa hana majeraha makubwa. 


“Wanafunzi wengi wamepatwa na hofu ya kutoka na kutembea usiku kwani hali hii inaogopesha sana,” alisema mwanafunzi mmoja alipohojiwa na Megan McGrath kutoka News4.


Maelezo kamili kuhusu watuhumiwa bado hayajapatikana. Kulikuwa na matukio mengi ya kujumuisha watu wakati wa tukio hivyo polisi wanatumaini kuwa haitawia vigumu kwa wahalifu hao kujulikana. Sykes alipenda uandishi na mara ya mwisho aliandika makala kwenye mtandao unaoitwa Our Black Pages  mnamo tarehe 11 Juni. Wasifa wake unaonesha  kwamba alikuwa anasomea Marketing na Public Relations. Mkesha wa sala kwa ajili ya marehemu utafanyika shuleni  kwao Jumamosi kuanzia saa 1 usiku.

 Howard University imetoa maelezo yafuatayo kuhusiana na kifo cha Alhamisi:
“Tuna huzuni kubwa kufuatia kifo cha mmoja wa wanafunzi wetu kilichotokea nje ya shule. Mwanafunzi mwingine alijeruhiwa kwenye tukio hilo na anaendelea na matibabu…. Polisi wa Howard University wanashirikiana polisi wa mji ili kupeleleza tukio hili hatari. Tunawapa pole familia, shule na wale wote walioguswa na tukio hili kwa namna moja au nyingine. Huduma ya ushauri nasaha itapatikana masaa 24 kwa wanafunzi wote watakaohitaji msaada katika kipindi hiki kigumu.

DC Ilala awaomba wadau kuwekeza katika mpira wa miguu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Stakishali waliokuwa mabingwa katika fainali ya Diwani Bonnah Cup iliyochezwa jana. Katikati ni Diwani wa kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa. Stakishali waliokuwa mabingwa walipata shs laki tano pamoja na kombe. 
====== = ====== ====== =====
MKUU wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amewasisitiza wadau mbali mbali kuwekeza katika mpira wa miguu kwani hutoa ajira nyingi kwa vijana na kuwafanya wajipatie kipato.


Akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunga mashindano ya Bonnah Cup yaliyoandaliwa na diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Mkuu wa wilaya alisema kuwa kwa miaka ya sasa mpira umekuwa kimbilo kubwa la ajira kwa vijana kwani huweza kuwasaidia kujiingizia kipato.


Mushi alisema kuwa pamoja na wadau kuwekeza katika mpira wa miguu, Tanzania itaweza vile vile kukuza vipaji ambavyo huwa vinapotea.


“Tanzania tuna vipaji vingi sana vya mpira wa miguu, tatizo ni vipaji hivyo kuvumbuliwa hivyo nawaombeni wadau mbali mbali kutoka sekta zote kujitokeza kuweza kuwekeza katika tasnia hii, ambapo tutawezesha vijana wetu kujipatia ajira,” alisema.


Timu ya Stakishari kutoka Mogo iliifunga timu ya Vipaji Halisi kutoka eneo la airport katika fainili na kukabidiwa kombe pamoja na kiasi cha shilingi laki tano, ambapo mshindi wa pili alipata kiasi cha shilingi laki tatu na mpira moja na mshindi wa tatu alipata shilingi laki moja na mpia. Jumla ya timu 20 kutoka katika kata ya kipawa zilishiriki katika mashindano hayo.

Muandaaji wa mashindano hayo diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa  alisema “Lengo kubwa ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja iliwaweze kufahamiana na kushirikiana lakini pia kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa miguu. Vijana wengi wanaocheze katika ligi hapa nchini wamechipukia katika kata ya Kipawa.  “ Napenda kuendeleza na kukuza vipaji wa vijana iliwaweze kufikia kiwango cha juu zaidi katika mchezo huu”, alisema


Said Mkuwa, Mwenyekiti wa mashindano hayo aliongezea: “Tunamshukuru sana diwani kuandaa mashindano haya kwa ajili ya vijana, alisema Nimefurahi kwamba mashindano yamekwenda vizuri tangu mechi za mwanzo hadi fainali na vijana wameshirikiana vizuri katika michezo yote”



Welcoming Ramadhan Conference - 2013

$
0
0
 Sheikh Suleiman Amran Kilemile, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam akiwakilisha Mada Juu ya Utukufu wa Mwezi wa Ramadhan na Umuhimu wa Kujitahidi kuisoma Qur'an kwa kuielewa ndani ya Mwezi huo Mtukufu.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Kongamano la Welcoming Ramadhan Confernce-2013 wakisikiliza moja ya maada iliyo wasilishwa katika mkutano huu
  Mbunge Al-Shaymaa Kwegyir akipata Maelezo Kutoka kwa Afisa wa Huduma za Benki ya Kiislam ya Amana ambao walikuwa Wadhamini wakuu wa Kongamano wa Wanataaluma wa Kiislam Kukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani
 Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu, Al-Shaymaa Kwegyir alipokuwa akizungumza na Waandishi Habari katika mkutano wa Welcoming Ramadhan Confernce-2013 jijii Dar es salaam.
 Viongozi na Masheikh wa Taasisi Mbali Mbali za Kiislam wakifuatilia kwa makini mada ya Nafasi ya Mwanamke wa Kiislam katika Kujenga jamii yenye Maadili Iliyowakilishwa na na Ustaadh Bakari Kombo Bakari wa Zanzibar.
 Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Kongamano la Kuukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani wakipata chakula cha Mchana na Kubadilishana Mawazo
Welcoming Ramadhan Conference
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria Kongamano la Kuukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa Ramadhani wakibadilishana Mawazo wakati wa chakula cha Mchana

RAIS SHEIN AFUNGUA BANDARI YA ABIRIA ZANZIBAR

$
0
0
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiria uzinduzi rasmi wa jengo la abiria katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohamed Shein,akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bakhresa Said Salum Bakhresa,huko Malindi Mjini Zanzibar.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohamed Shein, akiwahutubi wananchi wakati wa uzinduzi wa Jengo la abiria katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohamed Shein,akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Said Salum Bakhresa,kulia ya Rais ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Abdallah Juma Abdallah.
  Wananchi wakiskiliza hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dkt Ali Mohamed Shein, wakati wa Uzinduzi wa Jengo la abiria katika bandari ya Malindi Mjini Zanzibar.
 Muonekano wa sehemu ya nje ya Jengo jipya la Bandari ya abiria iliopo Malindi Mjini Zanzibar ambal;o limezinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein. 
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
=======  ====== =======

Dk. Shein afungua bandari ya Zanzibar kwa mkwara

Khadija Khamis na Miza Othman, Maelezo-Zanzibar  08/07/2013.

RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, amekemea tabia ya baadhi ya watendaji wa serikali, wanaokwamisha jitihada za kuleta maendeleo, kwa kuwawekea vikwazo visivyokuwa na msingi wawekezaji wanaojitokeza kutaka kuwekeza katika miradi mbalimbali.  Amesema kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watendaji wenye dhamana serikalini, kuwazungusha wawekezaji wenye nia  njema kwa Zanzibar, hata kwa mambo yanayoweza kumalizwa taratibu zake kwa muda mfupi.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa majengo mapya ya wasafiri katika bandari ya Malindi mjini Zanzibar, Dk. Shein amesema tabia hiyo inawavunja moyo wawekezaji hao wakiwemo wageni na wazawa, na kuchelewesha kasi ya kuiletea nchi maendeleo.  “Utakuta watu wanawasumbua wawekezaji kwa madai ya kuwa sheria haziruhusu. Jambo la kufanywa kwa wiki moja litachukua miezi sita au hata mwaka mmoja. Kama ingekuwa wageni, wangekimbia tu”, alisema Dk. Shein.   

Alifahamisha kuwa, kwa utendaji kama huo wa kimazoea na kutojali maslahi ya nchi, kuna hatari kwa Zanzibar kuachwa nyuma, kwa kuwa hakuna wewekezaji walio makini watakaokubali kusumbuliwa hasa kwa kuwa wanayotaka kuyafanya ni kwa ajili ya Zanzibar.

Kwa upande mwengine, Rais alimpongeza na kumshukuru kwa dhati Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya S.S.Bakhresa, aliyefadhili mradi huo, kwa moyo wake wa kizalendo, aliouonesha kwa maslahi ya nchi yake ya Zanzibar.  Amesema ujenzi huo uliogharimu shilingi bilioni moja, ni kielelezo cha mapenzi aliyonayo mwekezaji huyo kwa nchi yake, na kuwataka wafanyabiashara wengine kuiga mfano huo.

Aidha, aliwataka wafanyakazi wa Shirika la Bandari na wananchi watakaokuwa wakisafiri, kuyatunza vyema majenzi hayo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu, kwani kuwepo kwake, ni faraja kwa wananchi wote wa Tanzania na wageni wanaofika kutembelea visiwa vya Zanzibar.

Dk. Shein pia, alisisitiza kwa kuwaambia wafanyakazi wa shirika hilo kuwa, uzuri wa majengo hayo, uendane nma utiaji mzuri wa huduma kwa abiria, ili kila mmoja ajisikie furahani kutumia bandari za Zanzibar.  Alisema serikali itaendelea kuwaunga mkono wawekezaji na kutoa ushrikiano kwa kila hatua ya maendeleo wanayokusudia kuifanya hapa Zanzibar.

Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi, amesema kuwa ujenzi wa bandari hiyo uliochukua miezi sita, ni miongoni mwa jitihada za serikali kwa kushirikiana na wafadhili, kuibadilisha sura ya Zanzibar.

Rais Kikwete akutana na Waziri wa Mambo ya nje wa India, Spika wa bunge la Korea ya Kusini na Aagana na Balozi wa Uholanzi

$
0
0
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Uholanzi Mhe.Dkt.Ad Koekkoek anayemaliza muda wake wa uakilishi nchini. Balozi huyo baadaye alifanya mazungumzo na Rais Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi. 
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Spika wa bunge la Korea ya Kusini Mhe.Hee Chang wakati  spika huyo na ujumbe wake walipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Spika wa Bunge la korea ya Kusini Mhe.Hee Chang baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Spika wa bunge la Korea Mhe.Hee Chang (kulia) akimfurahia  Simba aliyekaushwa na kupamba lango la  ikulu  leo asubuhi. Kushoto ni mwenyeji wake,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya nje wa India Mhe.Preneet Kaur(wapili kushoto) na ujumbe wake  ikulu jijini Dar es Salaam leo.kulia ni Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe.Bernard Membe(picha na Freddy Maro) 

Naibu Waziri Charles Kitwanga ziarani Morogoro

$
0
0
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akikagua mfumo wa maji taka katika kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro
 Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akiangalia sehemu ya kuni/magogo yaliyokusanywa na kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya Morogoro Bw. Said Amanzi
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga (kulia) akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Bw. P.V.Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha  Century Textile Mill mkoani Morogoro juu ya uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na nishati ya kuni/magogo yanayotumiwa kiwandani hapo katika shughuli za uzalishaji. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkururenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Eng. Bonaventure Baya.


Exim Bank introduces hi-tech Queue Management System

$
0
0
 The Exim Bank Sales Manager Heena Khakharia (right) helps to register new Exim Bank clients bank’s pavilion at the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend. Centre is the Exim Bank Relationship Officer Cosmas Nade
 The Exim Bank Relationship Officer Cosmas Nade (second left) hands over a wheel cover to Rajabu Ramadhani during a visit to the bank’s pavilion at the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the left is the bank’s Direct sales Agent Ntalamu Thomas
 The Exim Bank Relationship Officer Cosmas Nade (centre) explains a point to Nora Isaac (right) during a visit to the bank’s pavilion at the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend. Looking on at the left is the bank’s Direct Sales Agent, Fred Said
Exim Bank Tanzania staff pose for a group photo at bank’s pavilion during the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend. 
Exim Bank Tanzania staff pose for a group photo at inside the bank’s mobile ATM moving van during the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend

======= ========  ======= =====
Exim Bank introduces hi-tech Queue Management System
By Staff Reporter

EXIM Bank Tanzania has introduced a Queue Management System to its key branches with larger number of customer influx as part of the bank’s efforts to enhance customer service delivery.

Speaking during the 37th Dar es Salaam International Trade Fair (DITF) in Dar es Salaam at the weekend, the Exim Bank Tanzania Customer Service Manager Frank Matoro said the new system will help to increase customer service offering delivery of real-time centralized motoring. “Waiting time and Service time metrics will be used to improve customer service bringing a higher degree of transparency and promoting an analytical driven culture.

“The comparative data from Queue Management System will be sent out every week to all branch heads, motivating them to better their branch performance to a higher level,” Matoro said.Matoro said the bank has also introduced Online Chat Service for its customers to   chat online with the bank’s representatives and get their queries / grievances resolved on the real time basis.

 “We are very pleased to introduce another 'First' of its kind online service for our valued consumers. We are confident that the service will not only save precious time of our esteemed consumers giving them freedom to get their issues resolved on real time basis, from any location."  “To avail the service, consumers are required to log on to the company's website www.eximbank-tz.com,” he added.

The Exim Bank Sales Manager Heena Khakharia during the event said the bank will continue investing in research to come up with more tailor-made banking products that fit interests of various communities.“Our products and services stand out for their innovative engineering and long-term value. We will continue investing in research to come up with more tailor-made banking products,” she said.

This fresh initiative, incidentally, comes at a time when Exim Bank was recently emerged winner in the aspect of Ccustomer Care in Tanzania according to the latest report released by audit firm KPMG last month that surveyed 32 banks operating in Tanzania.

MASHINDANO YA RAMADHANI SUPER CUP 2013 KATA YA CHAMAZI KUANZA RASMI HAPO KESHO

$
0
0

MASHINDANO YA RAMADHANI SUPER CUP 2013 KATA YA CHAMAZI KUANZA RASMI HAPO KESHO YAKIWA NA BARAKA ZOTE ZA TEFA, TIMU 16 ZATHIBITISHA KUSHIRIKI.

Mashindano ya Ramadhani Super Cup Kata ya Chamazi yanatarajiwa kuanza rasmi hapo kesho tarehe 10 Julai, 2013 yakiwa na lengo la kutoa burudani ya mpira wa miguu kwa wakazi wa Kata ya Chamazi iliyopo wilayani Temeke nje kidogo mwa jiji la Dar es salaam kwa kipindi chote cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Mashindano haya yanafanyika kwa mara ya kwanza katika kata ya Chamazi ikishirikisha timu mbalimbali kutoka Kata hiyo, huku timu kumi na sita tayari zimeshajisajili na kukubali kushiriki katika mashindano haya yanayotarajiwa kutoa bingwa siku ya sikuu ya Iddi itakayotegemea muandamo wa mwezi.

“Mashindano haya yanayotarajiwa kuwa na upinzani mkali kutoka kwa timu shiriki, yatazinduliwa na Mgeni Rasmi ambae ni Diwani wa Kata ya Chamazi lakini pia ni mlezi wa Mashindano Mh. John Lawrence Gama. Timu zote kwa sasa zipo katika maandalizi ya mwisho tayari kabisa kuanza kuonyesha ufundi wao katika mashindano haya yanayongojewa kwa hamu na wakazi wa Chamazi na maeneo ya jirani” Alisema Sady Mrope, Muanzilishi na Mratibu wa Ramadhani Super Cup.

Timu zimegawanywa katika makundi manne, yenye timu nne kwa kila kundi, ambapo kila kundi litatoa timu mbili kuelekea hatua ya mtoano. Timu 16 zitakazoshiriki katika Mashindano haya ni Boda Boda FC, Chamazi FC, Chamazi Islamic, Chamazi United, Fahari, FC Zarau, Inkaza, Kazembe, Magole, Mchele Koka, Mzux Family, Roma, St. Emmanuel, Vigoa, Wakali wa Rodi na Yatima. Huku mshindi wa Kwanza anatarajiwa kunyakuwa Jezi Seti Moja na mshindi wa pili atajinyakulia Mpira Mmoja.

Akiyataja malengo ya Mashindano haya, Mratibu wa Mashindano alisema kwamba Ramadhani Super Cup kiujumla ina malengo Mengi kubwa zaidi ni Kutengeneza jamii yenye umoja kwa wakazi na viongozi wake. “Malengo mengine ni Vijana kuwa karibu na viongozi wetu, Kukuza vipaji vya vijana, Kudumisha umoja na mshikamano, Kuhimiza vijana kutunza Afya zao, pamoja na kutoa burudani” aliongezea Bw. Mrope.  

“Kwa upande wa Maandalizi tuko vizuri sana na tungependa kuchukua nafasi hii mimi na wenzangu kuwashukuru viongozi wote wa wilaya tuliyowafikia kwa ushirikiano wao wa dhati juu ya kutoa vibali kwa mashindano haya kuanzia Serikali ya Mtaa wa Msufini na Kata ya Chamazi, Diwani wa Kata ya Chamazi kwa utayari wake kushirikiana nasi na kusaidia Zawadi ya mshindi wa kwanza, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chamazi kwa Kutukubalia kutumia uwanja huo, lakini pia Halmashauri ya Wilaya ya Temeke Idara ya Michezo na pia Chama Cha Mpira wa Miguu Wilayani Temeke” Bw. Sady Mrope alisema.

Aidha Muasisi na Mratibu wa Mashindano haya Ndugu Sady Mrope ambae ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam akisoma shahada ya Elimu ya Michezo, ameamua kujitolea kuweza kulisaidia soka la Tanzania Kusonga Mbele kwa kuanzia ngazi ya Chini kabisa ya kata na kuwataka wataalamu wengine wa Elimu ya Michezo wasaidie jamii yao katika kutambua umuhimu wa Michezo kwani ni moja katika ya nyenzo nzuri ba Muhimu ya Ajira, kujenga umoja na kuimarisha afya kama ikitumiwa ipasavyo. 

Pia amewaomba wakazi wa Maeneo ya Mbagala na vitongoji vyake, Chamazi na Mbande kuhudhuria kwa wingi katika kila mechi ili kuweza kutoa hamasa kwa timu zao.

Imetolewa na:
Sady Mrope
Muanzilishi na Mratibu | Ramadhani Super Cup

Umoja wa Watanzania Ujerumani kushiriki maonyesho ya Kimataifa mjini Aschaffenburg,

$
0
0

Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya
"Brüderschaft der völker " mjini      Aschaffenburg " Ujerumani.
                   Kuanzia 19 hadi 21 Julai 2013

Watayarishaji wa Festival ya "Brüderschaft der völker " mjini Aschaffenburg,
nchini Ujeruamani,wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayo
anza 19 hadi 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana sana na shughuli
za Umoja wa Watanzania ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza
Tanzania,wandaaji wa onyesho hilo wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU Bw.Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko
huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi
ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia
nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na watanzania, Umoja wa
Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.

Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na

CHADEMA YAGOMEA KUSHIRIKI KONGAMANO LA AMANI.

$
0
0
Ndugu,

Tumewaiteni hapa mchana huu kwa dharura, kutokana na kujitokeza kwa jambo moja muhimu sana katika mustakabali wa chama chetu na taifa kwa ujumla. Jambo lenyewe ni hili:

Kwa muda wa siku mbili, kuanzia kesho (leo)– tarehe 9 Julai 2013 hadi 10 Julai – kutakuwa na “KONGAMANO LA AMANI” lililoitishwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania – Tanzania Center For Democracy (TCD).


Kongamano hilo litajadili na kutafakari Amani ya Taifa, litafanyika kwenye hoteli ya White Sands ya jijini Dar es Salaam. Litafuguliwa na Mwenyekiti wa TCD, Mbunge wa kuteuliwa na Rais, Mheshimiwa James Mbatia na litafungwa na Rais Jakaya Kikwete.

Baadhi ya washiriki, ni pamoja na mawaziri, viongozi wakuu wa vyama vyenye wabunge ambavyo ni wanachama wa TCD – Chama Cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), United Democracy Party (UDP), Tanzania Lebour Party (TLP), NCCR- Mageuzi na CHADEMA.  Aidha, chama cha UPDP nacho kitashiriki mkutano huo kwa niaba ya vyama vingine ambavyo havina wabunge.


Ndugu waandishi wa habari,
CHADEMA kikiwa mmoja wa wadau wakubwa wa TCD, kimepokea mwaliko wa mkutano huo. Hata hivyo, tunapenda kutumia nafasi hii, kupitia kwenu, kuutangazia umma na Watanzania wote wanaotutakia mema na kulitakia mema taifa hili, kwamba hatutashiriki mkutano huo kwa sababu zifuatazo:


Kwanza, Mwenyekiti wa TCD, Mheshimiwa Mbatia kwa makusudi amekiuka maazimio ya kikao ya kuteuwa Mwezeshaji wa mkutano huo na badala yake akafungamana na CCM kuteuwa watu wanaowataka wao. Pili, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa Amani haijadiliwi. Amani inatengenezwa na kuwapo kwa mazingira ya haki na usawa; na kwamba aliyebobea katika uvunjaji wa haki hizo, ni serikali yenyewe. 

Katika mazingira haya, CHADEMA inaona hakuna umuhimu wa kushiriki kwenye mkutano ambao washiriki ni wale wale wanaotuhumiwa kuvunja haki za binadamu.

Tatu, Amani siyo ya vyama vya siasa pekee yake. Amani inahusisha wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kidini, taasisi za kiraia na mashirika yasiokuwa ya kiserikali. Taarifa zilizopo, ni kwamba mkutano huu haukushirikisha viongozi wa kidini, na hivyo, tunadhani kuwa siyo jambo zuri kama kweli tunataka kutafuta amani ya taifa.


Nne, Chadema haitashiriki mkutano huo kwa kuwa aliyepanga, aliyefadhili na aliyeitisha mkutano huo kwa mgongo wa TCD, ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, Mizengo Kayanza Peter Pinda, ambaye ndani ya nafsi yake, haonekani kuwa na dhamira ya dhati ya kuwapo amani katika taifa letu.

Ndugu waandishi wa habari;
Ninyi ni mashahidi wa jinsi Waziri Mkuu Pinda alivyo mstari wa mbele katika kuhubiri kauli za chuki, uhasama, uchochezi, ubabe na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini. Siyo mara moja wala mbili, Waziri Mkuu Pinda amesikika, tena ndani ya Bunge, akihamasiha vyombo vya usalama kuvunja sheria kwa kupiga, kuteka na kung’oa meno watu wanaotumia haki zao za kikatiba kushinikiza serikali kuchukua hatua dhidi ya maovu.


Tano, CHADEMA haitashiriki katika mkutano huo kwa kuwa Serikali ya CCM inayofadhili mkutano huu, imejaa unafiki kwa kuhubiri amani mchana, wakati usiku inachochea uhasama wa kidini, kisiasa na inawagawa Watanzania kwa misingi ya imani za kidini na vyama.

CHADEMA inao ushahidi usio na chembe ya mashaka, kwamba mifarakano mingi inayotokea kwenye jamii, mapigano katika koo mbalimbali, ugomvi wa kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji, machafuko kwenye mikutano ya hadhara ya vyama vya upinzani, sababisho lake kuu ni CCM kuvitumia vyombo vya dola, ili kukibeba chama hicho.


Tunataka umma utuelewe, kwamba tuna dhamira ya dhati ya kuona Tanzania inakuwa kisiwa cha amani, lakini hatutakubali kushiriki katika vikao ambavyo wanaoviongoza hawana dhamira hiyo. Ili amani iweze kupatikana, ni sharti kuwepo mijadala inayoingia kwenye viini vinavyosababisha amani ikosekane na hatua hiyo ianze kuchukuliwa na ionekane inachukuliwa na serikali.

CHADEMA iko tayari, kufanya kazi ya kutafuta amani na wale wanaopenda demokrasia. Chadema haifanyakazi na wanafiki wa amani.


Imetolewa na:
Benson Singo Kigaila,
Mkurugenzi wa Oganaizesheni ma Mafunzo, 
Dar es Salaam

Mashindano ya Diwani Bonnah Cup yalivyofanyika jijini dar.

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi ikimpa mfano wa zawadi ya hundi ya shs laki tatu Kapteni wa timu ya Vipaji halisi Hassani Juma ambapo timu yao ilikuwa mshindi wa pili wa mashindano hayo ya Bonna Cup kwenye picha katikati ni Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonna Kaluwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi ikimpa mfano wa zawadi ya hundi ya shs laki moja mfungaji bora wa mashindano hayo.
 Wanenguaji wa bendi ya Mashujaa wakicheza katika viwanja vya Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki baada ya baada ya kumalizaika kwa mashindano ya Diwani Bonnah Cup ambapo timu ya stakishari ilikuwa mabingwa.

 Charles Baba, Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akitumbuiza baada ya mashindano ya Diwani Bonnah Cup yaliyomalizika mwishoni mwa wiki. Anaye pga makofi ni muuandaji wa mashindano hayo Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa katika viwanja vya Social Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
 Diwani wa Kata ya Kipawa Mh. Bonna Kaluwa akifurahi kwa kucheza mziki ulikuwa   ukipolomoshwa na bendi ya Mashujaa katika viwanja vya Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki.
Charles Baba Mwimbaji na Meneja wa bendi ya Mashujaa akiimba wimbo wa risasi kidole uliokonga nyoyo za wapenzi wa muziki baada ya mashindano ya Diwani Bonnah Cup katika viwanja vya social Stakishali, Segerea mwishoni mwa wiki

wawanawake walionaswa na madawa ya kulevya nchini afrika kusini hawa hapa,ni watanzania.!

$
0
0
picha kwa hisani ya mtandao wa kijamii.

HATIMAYE wale Wanawake wawili walionaswa na madawa ya kulevya Afrika kusini wametambuliwa kuwa ni mabinti wa KITANZANIA ..

Mabinti hao wanadaiwa kuingiza shehena ya dawa za kulevya zenye thamani ya zaidi ya Sh. bilioni 6.8 nchini Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Geofrey Nzoa, alisema haijafahamika wanawake hao wanatoka mikoa gani.

Kamanda Nzoa aliwataja wanawake hao kuwa ni Agnes Jerald, ambaye alisema hajapiga hesabu ya umri wao, ila alizaliwa mwaka 1988 kwa maana hiyo ana umri wa miaka 25 na Melisa Edward ambaye alisema amezaliwa mwaka 1989 kwa maana hiyo atakuwa na umri wa miaka 24. Wawili hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi wa Afrika Kusini.

Alisema Jeshi la Polisi Nchini kwa upande wake linaendelea kufanya uchunguzi kubaini kama dawa hizo walitoka nazo wapi na pia linawasaka watu ambao watakuwa ndiyo wamiliki wa dawa hizo.

Jumapili iliyopita mtandao huu ulipata taarifa za kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania.

Taarifa hizo zilionyesha kuwa wanawake wawili walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Oriver Tambo uliopo eneo la Kempton Park siku ya Ijumaa wiki iliyopita wakitokea Tanzania.

Wanawake hao walikamatwa na maofisa wa Mamlaka ya Mapato ya Afrika Kusini wakiwa na masanduku sita ambayo yalipokaguliwa yalikutwa na takribani kilo 150 za dawa hizo ambazo pia zinajulikana kama ‘Tik’ zikiwa na thamani ya bei ya mtaani ya Randi milioni 42 sawa na Sh. bilioni 6.8.

Baada ya kukamatwa na dawa hizo wanawake hao walikabidhiwa polisi. Tukio hilo linatoka takribani wiki moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Juni 28, mwaka huu kutangaza kuwa tatizo la dawa za kulenya hivi sasa ni janga la kitaifa nchini.


Alisema kumekuwa na wimbi kubwa la Watanzania wanaojiingiza katika biashara haramu ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi na kwamba, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, watuhumiwa 10,799 walikamatwa kwa kujihusisha na dawa hizo.

Pia alisema katika kipindi hicho, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini, na hivyo kuharibu taswira ya nchi na kusababisha Watanzania wasio na hatia kupata usumbufu na masharti magumu wanapotaka kusafiri kwenda nchi mbalimbali duniani.

Pinda alisema mwaka huu pekee kumekuwa na ukamataji mkubwa wa dawa za kulevya katika eneo la kimataifa la Bahari ya Hindi karibu na Tanzania.

Alisema hivi sasa mikate, maandazi na askrimu zinazouzwa kwenye shule za msingi, zinawekwa dawa za kulevya.

Alisema vitendo hivyo vinafanya vijana wengi wa shule za msingi na hata sekondari kuwa na tabia za ajabu, ikiwamo kuingia darasani wakiwa na kiatu kimoja mguuni, mkufu wenye nyembe na kidani chenye nyembe kifuani.

Melezo Kwa hisani ya Nipashe.

MAFANIKIO YA TIC KUHAMASISHA UWEKEZAJI KWA WAWEKEZAJI WA NDANI KUANZAI JANUARI 2012 MPAKA DISEMBA 2012

$
0
0
 Meneja Huduma wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Revocatus Arbogast akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya mafanikio ya kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 mpaka desemba 2012, kushoto ni Meneja Uhusiano wa Kituo hicho Pendo Gondwe.(PICHA NA ELIPHACE MARWA).
Meneja Uhusiano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Pendo Gondwe akiwaelezea waandishi wa habari juu ya mafanikio ya kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 mpaka desemba 2012  katika ukumbi wa Idara ya Habari, kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi kawawa na kulia ni Meneja Huduma Revocatus Arbogast.


----------  --------  -------  -----
Kituo cha Uwekezaji  Tanzania TIC kinapenda kutoa taarifa kwa Umma kuhusu mafanikio ya kuhamasisha uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 mpaka Decemba 2012.

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) ni moja Taasisi ya Serikali ilianzishwa chini ya Sheria ya Uwekezaji Tanzania, Namba 26 ya mwaka 1997 kwa kuendeleza, kuratibu na kuwezesha uwekezaji katika Tanzania. Kama sehemu ya jukumu letu, TIC ina jukumu la kuhamasisha uwekezaji na masuala yanayohusiana na Uwekezaji kwa Watanzania ili Uwekezaji uweze kuwa na manufaa kwa Watanzania kwa ujumla.

Katika kipindi cha mwaka Januari 2012 mpaka Desemba Watanzania wameweza kutambua umuhimu wa kuwekeza na wameweza kuchangamkia fursa katika sekta mbalimbali. Katika kipindi hicho zaidi ya miradi 869 iliweza kusajiliwa miradi ambayo inategemea kuzalisha kazi zaidi ya 174,412 yenye thamani ya mitaji ya dola 11,420 milioni. Namba ya miradi hii ni kubwa kuwahi kusajiliwa na Kituo.

Miradi ya watanzanzia iliweza kuongoza kwa kwa TIC kusajili miradi 469 ya wazawa ambayo ni asilimia 54% ya miradi yote iliyoweza kusajiliwa.Sekta tano zilizoongoza katika kusajiliwa ni sekta ya Utalii, Usafirishaji, Uzalishaji viwandani , majengo ya biashara na kilimo. Sekta ya utalii iliongoza kwa kusajili miradi 144, Usafirishaji miradi 92, Uzalishaji viwandaji miradi 86, majengo ya biashara miradi 78 na kilimo miradi 28.

Katika usajili wa miradi hiyo wawekezaji wa nje waliweza kusajiri miradi 205 ambayo ni asilimia 23.5, kiwango ambacho ni chini ya nusu ya kiwango cha usajili wa miradi ya wawekezaji wa ndani. Miradi ya Ubia kati ya wageni na watanzania ilikuwa ni 195 ambayo ni asilimia 22.5.

TIC katika jitihada zake za kuongeza faida za uwekezaji katika uchumi wa Tanzania pia walifanya shughuli kuu ikiwa ni pamoja na kuwawezesha wawekezaji kupata vibali vyote vinavyohitajika chini ya One Stop Shop na utoaji wa huduma kwa wawekezaji aftercare.

uvccm yaamua kutumia wazee wa chama dhidi ya wanasiasa wanaopotosha misingi ya mapinduzi ya muungano-

$
0
0

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umeamua kutumia wazee wa Chama dhidi ya wanasiasa wanaopotosha na kutaka kutikisa misingi ya Mapinduzi na Muuungano wa Tanganyika na Zanzibar .

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema watatumia wazee hao, wanaowaita silaha nzito, katika kukabiliana na maadui na mashetani wanaotaka kutishia ustawi wa amani, utulivu na Umoja wa Kitaifa.

Amesema kuwa katika kuyaimarisha Mapinduzi na Muungano   vijana hao wameamua kuwatumia wazee ili kusafisha hali ya hewa inayochafuliwa na wapinga umoja na mshikamano.

Amewataja miongoni mwa wazee hao ni pamoja na Rais mstaafuu, Komandoo Dk Salmin Amour Juma, Mzee Hamid Ameir Ali, Mzee Ibrahim Amani, Abdulrazaq Simai Kwacha, Mzee Ali Khamis Jaribu na Mzee Ali Ameir.

“Tumedhamiria kufanya kazi bega kwa bega na viongzi hao wakisimama upande wa UVCCM  katika kukiamsha na kukielezea kizazi kipya wapi tulikotoka, mahali tulipo sasa na kule tunakoelekea”.alieleza Naibu katibu Shaka.

Aidha alifahamisha kuwa viongozi hao watawatanguliza mstari wa mbele katika mikutano yote ya  UVCCM ili kuamsha ari ya kufanikisha mapambano dhidi ya wale wanataka kuvunja umoja na mshikamano uliopo.

“UVCCM hatukubali kuona mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar yanavurugwa na Viongozi wachache wenye hulka ya na tama  namaslahi yao binafsi”, alisisitiza nd. Shaka .

Akizungumzia uchumi, Katibu huyo amesema kuwa utalii ni nguzo kuu inayojenga uchumi wa Zanzibar ambao unachangia asilimia 25 katika pato la Taifa na kufanikiwa  kwake linahitaji kuwepo na mazingira ya utulivu na amani.

Amesema UVCCM inalaani vikali kwa kujitokeza maneno ya ubaguzi dhidi ya Upemba, Uunguja na Ubara  kwa kisingizio cha mjadala wa uundwaji wa katiba mpya na kuwataka wananchi kuendelea kuishi kwa maelewano, umoja na kudumisha mshikamano nchini.

Ameeeleza kuwa UVCCM imejipanga kuzifufua maskani za CCM, kuimarisha mashina na vijana katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Aidha amewataka wananchi wapewe nafasi ya kutoa maoni yao katika mchakato wa katiba unaoendelea badala ya kujitokeza mamluki wachache kutaka kuwasemea wazanzibari

“Katiba ni matakwa ya wananchi hivyo waachiwe watowe maoni yao bila ya shindikizo na kushawishiwa na kundi au chama chochote cha siasa”, alielzea katibu huyo.

MIZA KONA - MAELEZO ZANZIBAR  09/07/2013.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

MIAKA 10 YA MAFANIKIO YA MFUKO WA UWEKEZAJI TANZANIA UTT

$
0
0

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Hamis Kibola akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu shughuli za mfuko huo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2003 ambapo unatimiza miaka 10. Kushoto ni Kaimu Ofisa Uendeshaji Mkuu Uwekezaji, Rashid Mchatta. 
 CEO, Hamis Kibola akifafanua jambo.
 Ofisa Uendeshaji Mkuu, Asset Management & Investor Services akifafanua jambo.
 Dk. Gration Kamugisha Acting CEO, Project
 James Washima akifafanua jambo.

Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ilianzishwa tarehe 19 juni, 2003. Tangu kuanzishwa kwake, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania imeendelea kutekeleza madhumuni yake. 

Mojwapo ya madhumuni ya Dhamana ya Uwekezaji Tanzania ni kuanzisha na kuendesha mifuko ya uwekezaji wa pamoja hapa nchini. Katika kufanikisha madhumuni yake, Dhamana ya Uwekezaji Tanzania imeweza kupata mafanikio ya kuanzisha mifuko mitano ya uwekezaji wa pamoja, ambayo hadi kufikia tarehe 08/07/2013 imekuwa na jumla ya wawekezaji hai wapatao 91,516.


Alliance One anticipates a good buying season Or It’s all systems go at Alliance One for a good buying season

$
0
0
 
Mark Mason showing Minister Chiba around AOTTL Unprocessed tobacco Storage. Elizabeth Chuma- Receiving and and Green Storage Manager
--------- --------  ------------
Alliance One anticipates a good buying season
Or It’s all systems go at Alliance One for a good buying season 

Morogoro: The 2013 tobacco buying season began earlier this year in May and Alliance One Tobacco Tanzania Limited (AOTTL) is anticipating an encouraging season for tobacco growers. The buying targets that AOTTL is working towards are 29.93 million kilograms for Flue Cured Virginia (FCV) tobacco and 1.04 million kilograms for Dark Fire Cured tobacco (DFC). Currently the season is midway and the tobacco already purchased stands at 16.42 million kilograms for FCV tobacco and 0.06 million kilograms for DFC tobacco.

“Alliance One prides itself in being well prepared for every new tobacco buying season, this helps us focus on maintaining our high standards and quality. Working with all our stakeholders from the farmer right through to regulators; our employees and our customers, we work hard  to ensure out industry leading quality is maintained at all levels of the production chain. This year we are focusing on increasing our efficiencies in our production chain, to build on the successes of last year where we produced in excess of 30 million kilograms of tobacco at our facility in Morogoro,” said Mark Mason, Alliance One’s MD

The targets set by AOTTL agronomy experts annually are in line with growing the Company, and satisfying local and international clientele with both the quantity and quality they expect from Alliance One. AOTTL farmers are also considered in the annual strategies through the investment by the Company in enhancing farmers’ skills to improve their methods. The signs of better yields are already evident as reflected in the current average price per kilogram of US$2.40 for FCV, which exceeds the targeted average price of US$2.06. The same positive results are reflected in DFC average prices which currently stand at US$1.68 from a target of US$1.47. AOTTL has already purchased US$39.90 million worth of FCV and US$960,000.00 worth of DFC as of 30th June 2013.

Tanzania’s tobacco farming has experienced tremendous growth in recent years due to the conditions prevailing within the industry including, improved marketing transparency; effective production management; greater crop compliance; organising smallholder farmer units into Primary Societies and increased productivity potential. The improvements noted in the last few years are the culmination of a successful partnership between all stakeholders in the tobacco farming industry. 

“Alliance One continues to be a significant contributor to Tanzania’s annual tax revenue, and welcomes the on-going and planned developments to infrastructure especially the road networks. A better road network can only help enhance the Company’s efficiencies, considering the fuel levy increase mentioned in the recent budget speech. I am excited that Alliance One continues to play its part in contributing to Tanzania’s development, especially in light of a buying season that already looks positive at this stage,” said Mason.
 

DAWASCO ya zindua Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment).

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Eng. Jackson Midala akionyesha mita mpya ya malipo ya kabla katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji wa kieletroniki (e-Bill payment) makao makuu Dar es salaam.
 DAWASCO yazinduwa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill Payment) makao makuu Dar es salaam
 Eng. Jackson Midala, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco (Katikati) akizungumza na waandishi wa habri kuhusu wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-bill payment) makao makuu Dar es salaam
  Wadau mbalimbali katika tafrija ya uzinduzi wa e-Bill payment, DAWASCO makao makuu- Dar es salaam
 Wawakilishi wa mabenki katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam.
Wawakilishi wa mitandao ya mawasiliano katika uzinduzi wa Mfumo mpya wa ulipaji bill za maji kwa kieletroniki (e-Bill payment), DAWASCO makao makuu- Dar es salaam

RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WAPYA LEO IKULU, DAR ES SALAAM

$
0
0


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi saba walioteuliwa hivi karibuni na kuagana nao kabla hawajaripoti kwenye vituo vyao katika nchi mbali mbali leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mabalozi hao toka kushoto ni Mhe Modest Melo anayekwenda Umoja wa Mataifa, The Hague, Geneva, Mhe Mabrouk n. Mabrouk (Abu Dhabi – Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE), Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (Beijing, China), Mhe Anthony Cheche (Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), Mhe Chabaka Kilumanga (Visiwa vya Comoro), Mhe Wilson Masilingi (The Hague, Uholanzi) na Mhe Liberata Mulamula (Washington DC, Marekani).  PICHA NA IKULU

waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais yapongeza ushirikiano kati ya bodi ya madawa ya kulevya ma vapidozi zamzibar

$
0
0
Na Ali Issa  Maelezo  Zanzibar. 9/7/2013
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu  wa kwaza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Ofisi hiyo, Bodi ya madawa na vipodozi Zanzibar na Baraza la mazingira la Tanzania Bara kwa mashirikiano ya kufanikisha  zoezi la kuangamiza unga mbovu uliokuwepo bandarini Zanzibar kuazia mwezi  wa April mwaka uliopita hadi Julai mosi mwaka huu.
Pongezi hizo alizitoa leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi  juu ya hali halisi ya unga huo ambao haufai kwa matumizi ya binaadamu  .
Amesema unga huo ulioharibika  umeanza kuangamizwa kwa  ushirikiano wa pande mbili   za Muungano  baaada ya Zanzibar kukosa  eneo ambalo litaweza kuhifadhi afya za wananchi wakati wa kuuangamiza.
Amesema Serikali ya Muungano  ilikubali ombi lao  na kuanzia tarehe 14  Mei hadi tarehe  15 Juni kontena 15 za unga  mbovu  ulisafirishwa  kupelekwa Tanzania Bara kwenda kuangamizwa.     
“Tulizungumza na wezetu Tanzania Bara kutupatia eneo la kuteketeza unga huu tuna shukuru wezetu hawakutuvunja moyo walikubali na sasa umeshateketezwa chini ya usimamizi wa Baraza la Mazingiara ”, alisema Waziri huyo.   
Aidha alifahamisha kuwa unga huo unateketezwa na kiwanda cha saruji cha Twiga simenti kilioko Tanga kwa makubaliano ya Wizara yake , Bodi ya madawa na vipodozi na msimamizi baraza la mazingira la Tanzania Bara.
Amesema kuanzia sasa hakutakuwa na muhali na vyakula vibovu vinavyo letwa na wafanya biashara  na  amewaomba  wananchi washirikiane kufichua maovu hayo ili kulinda afya zao .
Unga huo  unaofikia tani 780 uliingizwa nchini Aprili mwaka jana na  Kampuni ya  Bopary  Inteprise   kutoka nchini uturuki.

NHC YAMPIGA TAFU MISS TANZANIA 2012 KUJENGA BWENI LA ALBINO BUHANGIJA.

$
0
0
Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia) akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Susan Omari jijini Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa Bweni la wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya Msingi Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya kununulia mabati ya kuezekea bweni hilo.  Kwa mujibu wa Brigitte zaidi ya Shilingi milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
Viewing all 46360 articles
Browse latest View live




Latest Images