Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46397 articles
Browse latest View live

KASEBA AINGIZA FILAMU YA BONGO MAFIA MTAANI

$
0
0

BINGWA wa mchezo wa Kick Boxing nchini Chapion Japhert Kaseba ameingia katika fani ya utoaji filamu za mapigano Live akianzia na picha yake ya kwanza itakayo mtambulisha inakwenda kwa jina la Bongo Mafia

Filamu hiyo iliyo rekodiwa katika ubora wa hari ya juu sasa ipo mtaani Ikisambazwa na Kampuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya wapenzi wa filamu nchini wajionee vitu tofauti kidogo kwani kuna wakali kibao alio washirikisha 
Picha hiyo ni mfululizo za picha zake nyingine ambazo zipo njiani kwani amekuja kufanya kazi katika jamii  ili watambue ipi pumba na upi mchele
Bongo mafia ilioshilikisha wasanii kama vile ,Dotnata,Kelvin,Muhogo Mchungu,Pendo Njau Champion na Rogers MASTER SHIVO,na Wasanii wengine kibao

Amesema filamu hiyo kwa sasa ni gumzoo mtaani wakati ndio kwanza inamaliza wiki moja tangu kuingia sokoni 

Kaseba ambaye hivi karibuni ali mdunda bondia Rasco Simwanza wa Malawi amejitamba kuendeleza ubabe  kwa mabondia wengine huku akifanya kazi zake za sanaa ambazo kwa kiasi kikubwa anamshukuru sana Dotnata kwa kuona kipaji chake hicho ambacho kilikuwa kimejificha na sasa kipo mtaani

Kaseba amesisitiza kwa mashabiki wake wamuunge mkono kwa kununua kazi hiyo kwani ndio kwanza ananza kulishika soko la filamu hapa nchini endapo wataendelea kumunga mkono na ndipo watakapofuraia kazi zake nyingi zilizopo jikoni kwani nina kazi tofauti tofauti Nne hivi na sijui nianze na ipi ndio mana nimeamua kutoa hii kwanza alisema Kaseba.

SMILE COMMUNICATION YAWAKARIBISHA KATIKA BANDA LAO LILILOPO KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
 Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile Wauzaji wa Router kwa ajili ya matumizi ya intaneti akiwa na tabasamu la nguvu kama jina la kampuni anayoifanyia kazi katika banda lao lililopo katika Viwanja Vya Sabasaba
 Bwa Deogratias Kabeho, Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Smile (Wa kwanza Kushoto) akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake katika banda lao lililopo Katika Viwanja Vya Sabasaba barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.
 Wafanyakazi wa Smile wakiwahudumia wateja waliofika katika banda lao kwaajili ya kupata maelezo juu ya kufungiwa router za smile ambazo zina spidi ya hali juu kabisa kuliko mitandao mingine ya intanet hapa nchini,nyuma yao ni runninga inayoonyesha video za muziki unaochezwa katika laptop iliyounganishwa na intanet ya Smile yenye Spidi ya 4G LTE
Wafanyakazi wa Kampuni ya Smile inayohusika na ufungaji na uuzaji wa router za intanet zenye spidi ya 4G LTE wakimuelekeza mteja wao aliyefika katika banda lao lililopo katika viwanja vya sabasaba kwaajili ya kupata huduma ya kufungiwa intanet na kampuni ya Smile ambayo ina spidi ya hali ya juu ya 4G LTE.Picha na Josephat Lukaza wa http://josephatlukaza.blogspot.com
..............
Smile ni Moja ya Kampuni inayotoa huduma za ufungaji wa Intanet kwa kutumia router ambazo unaweza kuunganisha mpaka kompyuta sita hadi 10 na zaidi na kwa spidi ya juu kabisa ya 4G LTE.

Smile ndio kampuni pekee ya inayotoa huduma ya kufunga intanet yenye spidi ya juu ya 4G LTE peke yake nchini Afrika Mashariki.
Vilevile Smile wanauza router zao kwa bei nafuu kabisa ambapo mteja akinunua router pamoja na modem zaoo anapata kifurushi cha GB 20 ambacho mteja ataweza kuperuzi mitandao mbalimbali kwa spidi ya Juu kabisa ya 4G LTE.

Watembelee katika banda lao lililopo sabasaba kwaajili ya kupata maelezo na vilevile kujipatia modem na router zao ili uweze kupata huduma nzuri na bei nafuu kuliko zote nchini Tanzania.

WALEMAVU WA KUSIKIA WANUFAIKA NA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION.

$
0
0
 Nyota wa mchezo wa mpira wa miguu wa Marekani(American Football) Rays Lewis akimpa  RaisDkt. Jakaya Kikwete zawadi ya kofia yenye nembo ya timu yake wakati nyota huyo alipomtembelea Rais Kikwete mjini Arusha.Nyota huyo yuko nchini ambapo ni mmoja wa wafadhili wakubwa wa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu wa kusikia inayotolewa na taasisi ya Starkey Hearing Foundation ya nchini Marekani.Wagonjwa zaidi ya 3500 wanatarajiwa kunufaika na huduma hiyo inayotolewa bure na taasisi hiyo.
 Muasisi wa Taasisi ya Strakey Hearing Foundation  Bwana Bill Austin Starkey akimhudumia mtoto Lissa Frank(9) ambaye alikuwa kiziwi tangu kuzaliwa na kuweza kusikia baada ya kupata tiba na huduma ya kuwekewa kifaa maalumu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mkoani Arusha leo.
 Waasisi wa Taasisi ya Starkey Foundation Bwana Bill Austin Starkey(kulia aliyeinama) na Mkewe Tani Austin(Wapili kushoto) pamoja na mhudumu kutoka hospitali ya Seliani(kushoto) wakifurahi baada ya mtoto Lissa Frank(9) kuweza kusikia vyema baada ya kupatiwa matibabu katika kliniki maalumu iliyofanyika katika hospitali ya Seliani mjini Arusha leo(picha na Freddy Maro)
======  =====  =========
WALEMAVU WA KUSIKIA WANUFAIKA NA HUDUMA ILIYOTOLEWA NA TAASISI YA STARKEY HEARING FOUNDATION.

Na.Freddy Maro,Seliani Arusha.
Julai, 7 ,2013.

Zaidi ya Watanzania 3500 wenye maradhi ya kusikia wanatarajiwa kunufaika kwa huduma ya tiba inayotolewa na Taasisi ya Starkey Hearing Foundation yenye makao yake jijini Washington nchini Marekani.

Muasisi wa Taasisi ya Starkey Hearing foundation  Bwana Bill Austin  Starkey ameyasema hayo wakati wa kliniki maalumu ya kuwatibu watu wenye maradhi mbalimbali ya kusikia iliyokuwa ikifanyika Katika hospitali ya Seliani mjini Arusha baada ya kutoa huduma hiyo katika miji ya Dar es Salaam na Moshi mkoani Kilimanjaro. 

“Nimefurahishwa sana na kutiwa moyo kwa kazi tuliyoifanya ya kuwahudumia watu na kuwawezesha kusikia ambapo wengine ndiyo wameweza kusikia kwa mara ya kwanza tangu walipozaliwa.Furaha yao ni kitu cha kutia moyo sana katika juhudi zetu.Madaktari wa kitanzania tulioshirikiana nao wamefanya kazi kubwa na nzuri” alisema Bwana Starkey ambaye ameambatana na timu ya wataalamu na watu mashuhuri kutoka nchini Marekani ambao wametoa misaada mbalimbali kugharamia kampeni hiyo.

Bwana Starkey amesema kuwa watu wengi walijitokeza wakati wa kliniki hiyo maalumu kwa watu wenye ulemavu wa kusikia na kuongeza kuwa katika siku tatu walizokuwa mjini Arusha wagonjwa zaidi ya 600 walipatiwa huduma hiyo ya matibabu  kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yako na kuwawezesha kusikia vyema na kusema kila mwaka shirika lake litafanya mipango ya kuhakikisha kwamba huduma hiyo inakuwa endelevu.

Mwandishi wa habari hizi alishuhudia wazazi wenye furaha baada ya kuona watoto wao wenye umri kati ya miaka mitano na kumi wakiweza kusikia vyema kwa mara ya kwanza katika maisha yao  baada ya kupatiwa matibabu kwa kuwekewa vifaa maalumu katika masikio yao huduma ambayo imetolewa bure na shirika hilo na isingekuwa rahisi kuipata kwa watu wengi walio na kipato cha chini.

Bwana Bill Austin Starkey aliwashukuru wafadhili mbalimbali waliowezesha mpango huo wa matibabu kufanikiwa  na kuongeza kuwa falsafa ya taasisi yake ni “Ili Dunia ipate kusikia” imeweza kutekelezwa kwa vitendo kwa sababu  anaamini kuwa kukiwa na nia ya dhat na moyo wa kushirikiana kutekeleza jambo fulani mafanikio ni bayana na mabadiliko mengi chanya yatawezekana katika ulimwengu.

Bill Austin Starkey  na mkewe Tani Austin ambaye ni muasisi mwenza wa taasisi hiyo pamoja na washirika wao wanatarajia kwenda nchini Malawi kutoa huduma kama hiyo na baadaye kurejea tena nchini kutoa huduma  kabla ya kuondoka kurejea nchini marekani.

Mmoja wa wataalamu wanaotoa huduma katika kliniki hiyoDkt. Ron Brouillete alisema mbali na kuzaliwa na ulemavu wa kutosikia wangojwa wengine waliotibiwa katika kliniki hiyo walipata madhara ya kutosikia kutokana na matumizi holela ya dawa ya kutibu Malaria aina ya Quinine.

“Napenda kutoa ushauri kwa madaktari na wahudumu katika sekta ya afya kuepuka kuwapa dawa ya Quinine wagonjwa wa Malaria.Dawa hii itumike kwa uangalifu mkubwa na pale ambapo dawa nyingine zimeshindwa kumtibu Mgonjwa,” alisisitiza mtaalamu huyo kutoka nchini Marekani .


Mmoja wa wafadhili wa mradi huo anayefuatana na Bwana Bill Austin Starkey ni mcheza mpira  wa miguu maarufu wa Marekani(American Professional Football) Bwana Ray Lewis ambaye pia anachezea ligi ya taifa ya mpira wa miguu ya nchi hiyo(National Football League).
 
Awali Mchezaji huyo alimtembelea Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa mapumzikoni mjini Arusha na kusema kuwa Rais Kikwete ni mmoja kati ya viongozi mashuhuri barani Afrika wenye maono ya mbali na nia ya dhati ya kuwahudumia wananchi wake.

“Nimesoma habari nyingi mambo mangi yenye mafanikio makubwa anayoyafanya Rais Kikwete na nilipopata fursa ya kuja nchini Tanzania nikatumia nafasi hiyo kuja kumsalimia,kumsikiliza na kumpongeza.Ni mtu mnyenyekevu sana na nimefurahi sana kumtembelea na kuongea naye,” alisema nyota huyo wa mpira wa miguu Marekani muda mfupi baada ya kukutana na Rais Kikwete ambapo alimzawadia kofia yenye nembo ya timu yake.

Bill Austin Starkey na mkewe Tani Austin waliunda Taasisi ya Starkey Hearing foundation mwaka 1984 kwa lengo la kusaidia watu wenye maradhi ya kusikia na mpaka sasa maelfu ya watu katika sehemu mbalimbali duniani wamenufaika na huduma inayotolewa na taasisi hiyo.

RAIS KIKWETE AZINDUA TAMASHA LA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA LEO JIJINI DAR.

$
0
0
Rais kikwete akifungua tamasha la matumaini hivi sasa uwanja wa Taifa,jijini Dar.Picha zaidi zitawajia hapo baadae kidooogo.

Waimba injili Ambwene Mwasongwe (kulia) na Edson (kushoto) wakiimba sambamba katika Tamasha la Matumaini 2013.
Edson kazini.
Ambwene Mwasongwe.
Sehemu ya nyomi ikilipuka kwa burudani.

NSSF WASHINDI WA JUMLA KATIKA MANONESHO YA SABASABA

$
0
0

 Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akionesha vikombe walivyopata baada ya kuibuka washindi
  Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akipokea kikombe cha ushindi kwa upande wa taasisi za fedha.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabibidhi kombe, Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume baada ya kuibuka washindi wa jumla katika Maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam
   Meneja Kiongozi, Uhusiano Huduma kwa Wateja wa NSSF, Eunice Chiume akimkabidhi Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Juma Kintu.  
 Furaha ya ushindi.
 Ilikuwa ni siku nzuri kwa wafanyakazi wa NSSF. 
Wafanyakazi wa NSSF wakielekea kaika banda la NSSF baada ya kukabidhiwa zawadi zao.

rais kikwete achezesha MECHI YA SIMBA NA YANGA (WABUNGE TAMASHA LA MATUMAINI) uwanja wa taifa leo.

$
0
0
Rais Kikwete akisaini mpira utakaotumika.
...Akiwakagua Yanga.
..Akiwakagua Simba.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Eric Shigongo, Waziri Fenella Mukangara, marefarii na manahodha wa Simba na Yanga.
Vikosi vya Simba na Yanga.
JK akipuliza kipenga.
Rais Kikwete akielekea kukagua timu.
Mtanange ukiendelea.
Score board ilisomeka hivi.
Mashabiki.

TBL YATWAA TUZO YA UFADHILI MAONESHO YA 37 YA BIASHARA YA KIMATAIFA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (kulia) akimkabidhi tuzo Meneja Uhusiano Mambo ya Nje wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Emma Orio kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo wa kufadhili sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam.Katikati ni Dk. Abdallah Kigoda Waziri wa Viwanda na Biashara.
                                                                            Orio akifuara tuzo hiyo
Orio akiwa na washiriki wa maonesho hayo kabla ya kupokea tuzo

RAIS KIKWETE AONGOZA TAMASHA LA MATUMAINI UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO.

$
0
0
 Muziki wa Injili ulitawala. Hapa Solomon Mukubwa akitumbuiza
 MC wa Tamasha la Matumaini Godwin Gondwe a.k.a Double G akiwa kazini
 Bango lajieleza
 Uzalendo kwanza
 Nnape Nnauye akiwa na wadau
 JK akitete jambo na Eric Shigongo, mwandaaji wa Tamasha la Matumaini
 Wagunge wapenzi wa Simba wakipiga jalamba
 Profesa Maji Marefu akiongoza wabunge wapenzi wa Simba
 Wabunge wapenzi wa Simba
 Mwigulu Mchemba na skafu yake akiwa na  wabunge wapenzi wa Yanga
 Halima Mdee (kati mbele, bukta nyeusi) akiongoza kikosi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Kikosi kazi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Da' Asha Baraka akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Dionis Malinzi
 Mwandaaji wa Tamasha la Matumaini akisema machache
 Millard Ayo wa Clouds FM akirusha vitu live
 Wapiganaji wakila mzigo
 Wapiganaji kazini
 Wapiganaji wakishuhudia
 Wapiganaji wakirekodi matukio
 JK akifungua rasmi Tamasha la Matumaini
 JK akiwaasa Watanzania wasidanganyike na watu wanaotaka kuwatenganisha
 Hatudanganyiki....
 JK akilisifia Tamasha la Matumaini kuwa ni moja ya majibu ya wanaotaka kutenganisha Watanzania kwa misingi ya kikabila ama kidini
 JK akijiandaa kupiga filimbi kuanzisha mechi ya wabunge wpenzi wa Yanga na Simba
 JK akiwa refarii akihesabu wachezaji kabla ya kuanzisha mechi
 JK akiaga baada ya kuanzisha mpambano huo 
 JK akikaribishwa na mwandaaji Eric Shigongo. Kati ni Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara
 JK akiingia uwanja wa Taifa akiongozana na Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na Eric Shigongo
 JK akiwa meza kuu
 Meza kuu
 Mwandaaji wa tamasha Eric Shigongo akiongea machache
 JK akimpongeza Eric Shigongo kwa hotuba nzuri
 Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akimkaribisha JK kutoa hotuba yake
 Tamasha la Matumani Oye!
 JK akiongea na kadamnasi kwenye tamasha hilo katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na TBC
 TUSIDANGANYIKE...
 JK akiongea na kadamnasi
 "Tamasha hili ni majibu kwa wanaotutakia mabaya Tanzania...."
 JK akiongea na kadamnasi
 JK akisalimiana na wachezaji wa Bongo Movie
 JK akipeana mikono na kipa wa zamani  Yanga na Taifa Stars Peter Manyika ambaye sasa ni msanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie
 Jk akisalimiana na Bongo Movie Stars
 JK akisalimiana na Katibu Mkuu wa FAT mstaafu Mwina Kaduguda
 JK akisalimiana na kipa (wa kweli)  wa Yanga Barthez
 JK akiingia uwanjani
 Kikosi cha wabunge wapenzi wa Simba
 Waamuzi na wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akilakiwa na refa Othman Kazi
 JK akiweka saini katika mpira utaochezewa
JK akiweka saini 
 JK akitambulishwa waamuzi
 JK akikagua wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akisalimiana na straika mkali wa Yanga kutoka DRC
 Hiki kifriji vipi.....
 JK akisalimiana na wabunge wa Yanga. Huyu ni Esther Bulaya
 JK akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa Yanga
JK akisalimiana na kiongozi-mchezaji wa Yanga
 JK akisalimiana na mshambuliaji hatari wa yanga Halima Mdee

 JK akisalimiana na nahodha wa Simba Amos Makala
 JK akisalimiana na Simba
 JK akisalimiana na mchezaji wa kulipwa wa wabunge toka Nzega, Dkt Hamisi Kigwangalla
 JK akisalimiana na Profesa Maji Marefu
 JK akisalimiana na wachezaji wabunge wa Simba
 JK akisalimiana na mshambukliaji hatari wa Simba William Ngeleja
 JK akiendelea kusalimia wabunge wana Simba
 JK akisalimiana na beki tatu wa wabunge wa Simba Joshua Nassari
 Haya waheshimiwa... mchezo mwema...
 Nyimbo ya Taifa ikipigwa, kila mtu mguu sawa
 Wimbo wa Taifa 
 JK akipungia umati unaomshangilia kwa nguvu
 JK akipena mkono na mashabiki
 JK akiteta jambo na JB huku Dkt Cheni akiwa pembeni
 Mashabiki wakiwa nje ya uwanja
 Nyomi ya nje inapita ya ndani
Mshabiki wa Yanga akielekea uwanjani

UMOJA WA MATAIFA YANYAKUA TUZO MAALUM KWA KUTAMBUA MCHANGO WAO WA KUHAMASISHA JAMII KATIKA MAONYESHO YA 37 YA KIMATAIFA YA BAISHARA JIJINI DAR.

$
0
0
photo (26)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofikia tamati jana kwenye viwanja vya Mwl. Julius Nyerere jijini Dar. Waziri Mkuu aliambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou.
photo (29)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ( wa pili kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa Wajasiriamali wanaofadhiliwa na UNIDO kwenye banda la Shirika la Umoja wa Mataifa akiwa ameambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara Dk. Abdallah Kigoda (kushoto) pamoja na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou (wa pili kulia) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa jijini kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere leo.
photo (33)
Tuzo maalum waliyokabidhiwa shirika la Umoja wa Mataifa nchini kwa kutambua mchango wao wa kuhamasisha Jamii (UN Special recognition for community awareness) wakati wa sherehe za kufunga Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere.
photo (25)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Dk. Alberic Kacou akipokea Tuzo ya Ngozi iliyotengenezwa kinyumbani kutoka kwa Wajasiriamali wanaodhaminiwa na UNIDO wakati alipotembelea Banda la Shirika hilo leo kwenye maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara yalifungwa rasmi jana na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda.
photo (31)
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (kulia) akitoa maelezo kwa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou ya malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wajasiamali wanaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
photo (24)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa vitengo mbalimbali vya Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini. (UN-Tanzania Delivering as one).
photo (30)
Banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba likiwa limeandika ujumbe unaosema "Umoja wa Mataifa inafanya kazi kwa ajili yako-kuboresha maisha ya watoto, wakinamama na vijana".
photo (28)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou alipotembelea banda la Wizara ya Fedha wakiwa ni wadau washirika wa Maendeleo nchini.
photo (27)
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dk. Alberic Kacou akibadilishana mawazo na mmoja wa wadau alipotembelea banda la Wizara ya Fedha ikiwa ni kudumisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania.
Maendeleo

Oxford na Vodacom zaungana kuendeleza Elimu nchini

$
0
0
 Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni ya Oxford University Press,  Asia Mhina (kushoto) na Meneja  Mauzo na Masoko wa kamnpunoi hiyo Bi.Fatma Shangazi(kulia) wakifatilia neno kutoka kwa Meneja wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu katika moja ya Kamusi  zinazouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya  biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.
 . Meneja  Mauzo na Masoko wa Oxford University Bi.Fatma Shangazi(kulia)akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya vitabu vinavyouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano kati ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja wanaotumia huduma ya M PESA kununua vitabu, wanaoshuhudia kutoka kushoto ni  Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu na  Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni hiyo Asia Mhina.
 Meneja  Mauzo na Masoko wa Oxford University Press Bi.Fatma Shangazi(kulia)akimuonesha Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu (kushoto) na Meneja maendeleo ya kibiashara wa kampuni hiyo Asia Mhina, moja ya vitabu vinavyouzwa kwenye  banda lao katika viwanja vya maonesho ya 37 ya biashara ya kimataifa (sabasaba) wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya kampuni yake na Vodacom utakao wawezesha wateja kutumia huduma ya M PESA kununua vitabu.
Ili kuongeza kasi ya usomaji wa vitabu kwa watanzania suala ambalo limekuwa ni changamoto kubwa hapa nchini kampuni ya Oxford University Press imeingia ubia na Vodacom Tanzania ili kuwawezesha wateja mbalimbali kununua vitabu kupitia huduma ya M pesa, Vitabu vitakavyo weza kununuliwa na kuuzwa ni pamoja na vile vya kiada na Ziada kutoka katika kampuni hiyo. 

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Ushirikiano huo uliofanyika katika  maonesho ya 37 ya Sabasaba Meneja Ukuzaji Biashara wa Vodacom Asia Mhina amesema kuwa kutokana na kukua zaidi kwa huduma ya M-Pesa hapa  nchini pamoja na kuepuka usambazaji kwa wateja wa Oxford ndiyo sababu iliyosababisha wao kuingia ubia huo. 

Mhina alibainisha pia ubia huo umekuja katika wakati muafaka kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wa vitabu kuepukana na foleni zilizopo kwenye mabenki pamoja na kuokoa muda wa malipo kwa wateja pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu kwa Watanzania. 

“Lengo la huduma hii ni kuwarahisishia wateja na wananchi kufanya malipo ya vitabu kwa urahisi , pia kuongeza kasi ya ununuaji na usomaji wa vitabu kwa Watanzania suala ambalo limekuwa ni changamoto kubwa sasa, hivyo hatua hii itawezesha kukabiliana na changamoto hizo,” alisema Mhina na kuongeza kuwa, “Mteja wa Vodacom sasa atalipia vitabu hivyo kwa njia rahisi zaidi ambapo akitaka kufanya malipo atafungua orodha ya M pesa kama kawaida na kisha kuchagua malipo na kuweka namba ya biashara ya Oxford ambayo ni 870870 na kisha kufanya malipo.” 

Kwa upande wake meneja masoko wa Oxford Fatma Shangazi alisema kuwa huduma ya malipo ya vitabu kwa M-Pesa itawarahisishia wateja wao kufanya malipo kwa urahisi pasipo usumbufu wowote wala kupoteza muda na pia itawaweka katika hali ya usalama zaidi. 

“Tunafurahi kuingia katika ubia na kampuni ya Vodacom ni hatua kubwa kwetu na tunaamini kuwa ushirikiano huu utakuwa chachu ya kuongeza hali ya usomaji wa vitabu kwa Watanzania, alisema Shangazi.

JUMUIYA YA WAZAMIAJI NA UOKOZI ZANZIBAR YATAKIWA KUTANUA WIGO WA UTENDAJI KAZI WAKE

$
0
0
 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Zanzibar Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud akitoa hutuba ya Uzinduzi wa Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja. 
 Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar Faki Bakar Faki akitoa taarifa ya jumuiya yao katika haflaya uzinduzi wa jumuiya hiyo iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Zanzibar Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud na kulia ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Malindi OCS Omar Kharib .
 Baadhi ya Wajumbe wa Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar wakifuatilia hutuba ya Uzinduzi wa Jumuiya yao iliyokuwa ikitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Zanzibar Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud (hayupo pichani)katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar

======  ======  =======
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  .

Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar imetakiwa kutanua wigo wa utendaji kazi zake ili pia ijishughulishe na uhifadhi wa mazingira badala ya kufanya kazi za uokozi baharini pekee.Mkuu wa Wilaya ya Mjini Kanali Mstaafu Abdi Mahmoud alitoa wito huo katika uzinduzi wa Jumuiya hiyo uliofanyika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja. Alisema maafa hayatokei upande wa baharini pekee bali yanaweza kutokea popote hivyo Jumuiya hiyo itanue wigo wake katika kukabiliana na mambo hayo.

Aliongeza kuwa kazi ya uokozi sio tu kufanywa wakati Maafa yanapotokea bali hata kutunza mazingira ya Baharini na Nchi kavu ni njia nzuri ya kujikinga na maafa mengi. “Malengo yenu yasiishie tu kusubiri ajali za baharini kutokea ili muokoe bali tanueni pia fikra zenu katika  kujishughulisha na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake” Alisema Mkuu huyo wa Wilaya.

Katika kutekeleza hayo Mkuu huyo wa Wilaya amepanga kufanya harambee ya kujitolea na Wanajumuiya hiyo ili kufanya usafi wa kupigiwa mfano katika Manisapaa ya Mji wa Zanzibar. Amewaasa Wanajumuiya hiyo kutokujihusisha na makundi ya kisiasa au dini katika kufanya mambo yao badala yake waangalie utu na Mustakabali wa Wananchi. Kanali Mahmoud amewataka Wanajumuiya hiyo kuzidisha mashirikiano na upendo miongoni mwao ili Jumuiya iweze kusonga mbele.

“Uzinduzi wa leo umejumuisha zaidi ya Watu 200 na nyuso zimejaa upendo naamini kama mashirikiano  haya yataendelea basi Jumuiya itakuwa ya kupigiwa mfano ” Alisema Mstaafu huyo wa Jeshi.Kwa upende wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Faki Bakar Faki amesema wameamua kuazisha Jumuiya hiyo ili kufanya shughuli za uokozi pale yanapotokea majanga bila kujali itikadi yoyote.


Faki amedai kuwa Uzoefu unaonesha kila panapotokea Majanga hasa ya baharini Asasi za kiraia na Watu binafsi ndio wanaokuwa wakwanza kufanya harakati za uokozi kabla ya Serikali kupitia Vikosi vyake kufika eneo la tukio na kuendelea na uokozi. “Jumuiya yetu si ya kidini wala siasa tupo kuisadia jamii pale linapotokea tatizo lolote na tuko tayari kufanya uokozi hata wa mazingira ya nchi kavu pale ambapo itatubidi” Alisema mwenyekiti.

Aliiomba Idara ya Sayansi ya bahari kuwa karibu na Jumuiya hiyo na kuwawezesha kupata Kamera ambazo zitasaidia kupiga picha mambo mbalimbali wanayokutana nayo baharini. Aliongezea kuwa Wamekuwa wakikutana na mambo mengi chini ya bahari wakati wa kufanya shughuli za uokozi au uvuvi na kwamba kama wangepiga picha zingesaidia kufanyiwa tafiti mbalimbali na kupatiwa majibu.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Wilaya  Afisa Tawala wa Wilaya ya Mjini Muhammed Abdallah Ahmed ameisifia Jumuiya hiyo na kusema kuwa itasaidia sana katika kukabiliana na majanga ya baharini na hata nchi kavu.

Aidha ameongeza kuwa kwa muda mrefu Wavuvi wengi wamekuwa wakituhumiwa kwa kuvua Uvuvi haramu na kuongeza kuwa Jumuiya hiyo pia itumike katika kukabiliana na aina zote za uvuvi haramu “Kuna aina nyingi za uvuvi haramu ikiwemo utumiaji wa Mabomu, Kukokota na Utupa hivyo Jumuiya hii itumike kama msimamizi wa Wale watakaojihusisha na Uvuvi huo kwa kutoa taarifa sehemu husika”

Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya hiyo Walishiriki moja kwa moja katika Ajali za kuzama kwa Meli kadhaa Zanzibar ikiwemo Mv. Skirgit, Mv. Spice Islander1 na Mv. Fatih na hivyo kuamua kuunganisha nguvu kwa kuanzisha  Jumuiya ili waweze kufanya kazi kwa pamoja.Jumuiya ya Wazamiaji na Uokozi Zanzibar  yenye Wanachama 200 Wazamiaji imeanzishwa kwa lengo la kusaidia Jamii pale yanapotokea maafa ambapo Makao makuu yake yapo Mtoni mjini Unguja.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR.

Mwanza mabingwa ARS 2013 , Kinondoni wasichana watwaa kombe

$
0
0
 Wachezaji 6 nyota ( waliokaa) waliochaguliwa kuhuduria Clinic itakayoongozwa na makocha wa kabla ya Manchester united wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutangazwa katika final za Airtel Rising stars zilizofanyika katika katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akikabidhi kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars kwa nahaodha wa timu ya Mwanza Kelvin Faru kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.
 Timu ya Mwanza ikifurahia  ushindi  mara baada ya kuibuka mabingwa wa fainali za Airtel Rising Stars kwa mwaka 2013
 Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos Makala akiongea wakati wa kufunga michuano ya Fainali ya mashindano ya Airtel Rising Stars katika viwanja vya karume jijini Dar es saalam
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos, akifatiwa na Raisi wa TFF sir Leodgar Tenga pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso wakikangua timu kabla ya kucheza mechi ya finali katika michuano ya Airtel Rising Stars , mechi ilikuwa kati ya Morogoro na Mwanza. 
 Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Amos akiongea na wachezaji kabla ya kuanza mechi za fainali
 Mlinzi wa Mwanza Ally Mnasi (kushoto) akipambana na Evance Robert wa Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.   Mwanza walishinda 1-0
 Mchezaji Kelvin Matale wa  Mwanza (kushoto) akichuana na Dickson Mwesa wa of Morogoro wakati wa fainali kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar mwishoni mwa wiki.   Mwanza walishinda 1-0.
 Rais wa TFF Leodegar Tenga akimvisha medali kocha wa timu ya taifa ya vijana Jacob Michaelsin kutambua mchango wake kwenye mashndano ya Airtel Rising Stars ngazi ya Taifa yaliyomalizika uwanja wa Karume mwishoni mwa wiki
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Levi Nyakundi akikabidhi mfano wa hundi kwa  mchezaji bora wa Airtel Rising Stars  Anna Hebron kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania lamalizika jijini mwanza.

$
0
0
Meya wa jiji la Mwanza (pili shoto),Mh.Stanslaus Mabula akiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu walioibuka katika mashindano ya kucheza,kwenye tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza.Mshindi wa kwanza pichani kati ni Laulencia Francis aliyejinyakulia kitita cha sh laki 2,Mshindi wa pilia ni Victoria Pascal (kwanza kulia) aliyeibuka na sh laki moja,na watatu ni Mariam Vincent aliyejinyakulia shilingi elfu hamsini.Pichani nyuma ni kushoto ni Muaandaji wa tamasha hilo,Mussa Kisoky na wakiwa na wadau wengine wa jiji la Mwanza.
Mshindi wa Kwanza wa tamasha hilo  la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza,Laulencia Francis aliyejinyakulia kitita cha sh laki 2.
 Meya wa jiji la Mwanza pichani kulia,Mh.Stanslaus Mabula akimkabidhi mshindi wa kwanza wa kucheza jukwaani,Laulencia Francis aliyejinyakulia kitita cha sh laki 2.
Msanii wa ngoma za asili Wanne Star akitumbuiza jukwaani hapo jana kwenye  kiha lele cha tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza
  Sehemu ya mashabiki na watazamaji waliofika kwa wingi kwenye tamasha hilo  la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lililokuwa likifanyika kwa wiki nzima kwenye uwanja wa Nyamagana,jijini Mwanza,ambapo kilele chake ilikuwa jana.Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 32 WA WADAU WA POSTA KWA NCHI ZA AFRIKA, JIJINI ARUSHA LEO

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika.  
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya Viongozi, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine (kulia) na Prof. John Nkoma, Mkurugenzi wa Mawasiliano Tanzania (wa pili kulia), wakati akiwasili kwenye Ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Julai 8, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Posta kwa Nchi za Afrika (PUPA) Younouss Djibrine, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 32 wa Wadau wa Posta kwa Nchi za Afrika, ulioanza jijini Arusha leo, Juliai 8, 2013. Mkutano huo umehudhuriwa na wadau wa Posta kutoka nchi za Afrika
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akifungua rasmi mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa AICC, jijini Arusha. 
 Kikundi cha Kwaya cha Jijini Arusha kikitoa burudani.
 Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mhe. Makamu wa Rais kufungua mkutano huo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki baada ya kufungua mkutano huo. Picha na OMR.

Antony na Gema Wameremeta.

$
0
0
 Harusi:Ndugu Antony David Mtavangu na Gema Nicholaus Temba wakila kiapo cha kuishi pamoja katika kanisa la Mtakatifu Peter ,siku ya Jumamosi tarehe 6 Julai 2013.
 Antony na mkewe Gema wakiwa wamependeza sana katika siku yao ya harusi.
 Antony Mtavangu na Bi. harusi Gema wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi wao.
Saleh Saphy akizungumza kwa niaba ya wanafunzi waliosoma na Antony, chuo kikuu cha Mysore India, pamoja na kumtaka Antony maarufu kama 'Tony Yayo' kumtunza mkewe , vijana hao walimtakia maisha mema na kamwe kutomlisha mkewe 'Egg Puf '.

Mkoa wa Kilimanjaro watia fora Onyesho la Kili Music Tour 2013

$
0
0
Wanamuziki wakongwe katika medani ya muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee na Joseph Haule au ukipenda waweza muita Profesa Jay wakiburudisha maelfu ya mashabiki wa muziki waliofurika katika Uiwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki katika muendelezo wa Maonyesho ya Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Nassib Abdul a.k.a Diamond akiwajibika jukwaani sambamba na madansa wake wakati Onyesho Kabambe la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika Mjini Moshi ndani ya Mkoa wa Kilimanjaro mwishoni mwa wiki na kuhudhuliwa na maelfu ya wakazi wa Moshi na mikoa ya Jirani waliokataa kupitwa na Onyesho hilo.

Mkali wa RnB,Ben Pol akifanya vitu vyake jukwaani.
Barnaba Elias nae kwa nafasi yake na uwezo wake akiwajibika stejini.
Snura Mushi a.k.a Mamaa wa Majanga akionesha umahiri wake mbele ya mashabiki wake wa mkoa wa Kilimanjaro waliofurika kwa wingi katika Uwanja wa Ushirika kushuhudia onyesho la Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013.
Kundi bora la muziki wa Reggae Tanzania kwa mujibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013.  Warriors from the East, wakionesha uwezo wao katika kulimiliki jukwaa kwenye onyesho la tatu la Tamasha la Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013,lililofanyika kwenye Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mwishoni mwa wiki.
Mkali wa Miondoko ya Miduara,AT akiwapagawisha mashabiki wake lukuki ndani ya Uwanja wa Ushirika mjini Moshi.
Kundi bora la muziki kwa mujibu wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,Jambo Squard, wakionesha ubora wao katika jukwaa la tatu la ziara Kilimanjaro Tanzania Music Tour 2013 zinazoendelea nchi nzima.
Mwamba wa Kaskazini, John Makini akifanya vitu yake jukwaani.
Roma Mkatoliki.
Mwanamuziki bora wa Hip Hop 2013, Kala Jeremiah akiwarusha mashabiki wake juzi katika viwanja vya Ushirika jijini Moshi.

UANZISHWAJI WA MIRADI MBALIMBALI AMBAYO IPO KATIKA HATUA ZA UTEKELEZAJI

$
0
0
 Meneja Uhusiano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Abel Ngapemba(katikati) akielezea uanzishwaji wa miradi mbalimbali ambayo ipo katika hatua za utekelezaji,kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha  Miundombinu na Nishati Mhandisi Pascal Malesa kutoka NDC na kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Zamaradi Kawawa.
Mkuu wa Kitengo cha Miundombinu na Nishati Mhandisi Pascal Malesa kutoka Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano uliofanyika katika idara ya habari,kulia ni Meneja Uhusiano wa Shirika la Maendeleo la Taifa Abel Ngapemba

========  ======  ======== ======
Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ni taasisi inayoongoza kuleta na kukuza maendeleo ya viwanda Tanzania kwa kushirikiana na sekta binafsi kama inavyobainishwa katika Waraka namba 6/1996 wa Baraza la Mawaziri. Chimbuko lake ikiwa ni Sheria ya Bunge ya  mwaka 1962 iliyotungwa kuendeleza miradi ya kiuchumi na kimaendeleo na kuchukua nafasi ya shirika la Maendeleo la kikoloni, Colonial Development Corporation (CDC) lililoanzishwa mwaka 1950.


Katika waraka wa Baraza la mawaziri, NDC inatakiwa:-


·         Kuendelea kuwa shirika la umma kwa asilimia mia moja (100%) na kuwa na mamlaka kamili ya kusimamia maendeleo.

·         Kuanzisha miradi mipya ya maendeleo kwenye sekta yoyoye ya uchumi nchini.

·         Kuwa na majukumu ya moja kwa moja ikiwemo ya kuendeleza na kutekeleza Miradi ya Mkaa wa mawe ya Mchuchuma, Mradi wa chuma wa Liganga  na mradi wa Magadi Soda wa Ziwa Natron.

·         Kutekeleza majukumu yake yote kwa kufuata utaratibu wa Ushirikiano kati ya umma na sekta binafsi.



Hadi hivi sasa, Shirika tayari limeanzisha miradi mbalimbali ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.


Ujengaji wa kituo cha kufua umeme wa Upepo cha Singida chenye uwezo wa kuzalisha megawatts 300 ni mmoja ya miradi ambayo imeanzishwa na Shirika kwa kushirikiana na sekta binafsi ambapo pia ni mradi uliopo ndani ya mpango wa Taifa wa “Tekeleza sasa kwa matokeo makubwa”.(Big Result Now) Mradi huu unatakiwa uwe umekamilika kabla ya mwisho wa mwaka 2015. Lego la Big Result now ni kuongeza umeme katika Msongo wa Umeme wa Taifa (National Grid) kufikia megawatts 2700.


Ili kufanikisha mradi huu, Shirika limeanzisha kampuni ya ubia ijulikanayo kwa jina la Geo Wind Power Tanzania Ltd ambayo wamiliki wake ni NDC yenye hisa asilimia 60,   TANESCO yenye hisa asilimia 20 na kampuni binafsi ya kizawa ya Power Pool East Africa Ltd yenye hisa asilimia 20.


Awamu ya Kwanza (Phase I) itahusisha ujenzi wa kituo cha kufua umeme la Megawati 50 kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 136 ambazo zitatolewa na Benki ya EXIM ya China  kama mkopo wa masharti nafuu. Ujenzi wake utakamilika ndani ya miezi 12 na kuanza kufua megawati 50 ifikapo 2015 na baadaye kuongeza megawatt 50 kila mwaka hadi kufikia megawati 300 ifikapo 2019.


Hadi sasa utafiti wa mradi, tathmini ya mazingira, makubaliano ya awali ya ununuzi wa umeme kati ya Geo Wind na TANESCO, ulipwaji wa fidia kwa wananchi wa eneo hilo, uhakiki wa mradi na wajazi wa mitambo umeshakamilika na mkataba wa ujenzi umesainiwa tayari.


Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kupunguza tatizo la  umeme nchini kwa kuwa umeme huo utaunganishwa katika msongo wa Taifa kupitia kituo chake cha  Singida ikiwa ni mradi wa kwanza wa aina hiyo kuunganishwa katika Msongo wa Taifa. Kwa maana hiyo utasaidia pia kupunguza gharama za uendeshaji wa mitambo kwa kupunguza matumizi ya mafuta wakati wa ukame na hivyo kuhifadhi fedha za kigeni. Kituo kitatoa ajira za moja kwa moja 250 na ajira nyingine 2000 kitakapoanza kazi.


NDC mbali na mradi huu, imepanga kuanzisha mradi mwingine wa kuzalisha umeme wa upepo katika eneo la Makambako. Mradi huu bado haujapata mbia atakayetekeleza mradi huu kwa kushirikiana na NDC.


Miradi mingine ya umeme  inayotekelezwa na NDC kwa kushirikiana na sekta binafsi ni Miradi ya Mchuchuma na Ngaka itakayozalisha umeme kutumia mkaa ya mawe. Uchorongaji wa kina katika mradi wa Mchuchuma umekamilika na katika mradi wa Ngaka, uchimbaji wa mkaa ya mawe unaendelea. Majadiliano kati ya TANESCO na kampuni ya ubia juu ya manunuzi ya umeme wa Ngaka yako katika hatua nzuri. Lengo ni kuzalisha megawati 400 katika mradi wa Ngaka ifikapo 2016/17 na kuzalisha megawati 600 katika mradi wa Mchuchuma ifikapo 2018/19.


Imetolewa na: Abel Ngapemba

Meneja Uhusiano wa Shirika

8 Julai 2013



TECNO kuwekeza zaidi katika soko laTanzania

$
0
0
Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, Patrick Karogila, akionyesha moja ya simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphone” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo pamoja na nyingine zimebuniwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Afisa Uhusiano wa kampuni hiyo Boukali Mounir.
Meneja Uhusiano wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, akionyesha moja ya simu zenye teknolojia ya hali ya juu “Smartphones” ambayo imeingizwa katika soko la Tanzania hivi karibuni, Simu hiyo imebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa watumiaji wa simu nchini, pamoja nae ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo Patrick Karogila.
Meneja Mauzo wa kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi aina ya TECNO, Patrick Karogila, akizungumza na waandishi wa habari, (hawapo pichani) katika hafla ya kutambulisha simu zilizotengenezwa kwa teknolojia ya hali ya juu kutoka katika kampuni hiyo, Simu hizo zimebuniwa kukidhi mahitaji ya mawasiliano kwa Watanzania wa aina zote. Pamoja nae ni meneja mahusiano wa kampuni hiyo, Boukali Mounir.


Kampuni ya uuzaji wa simu za mkononi ya TECNO imeendelea kuwekeza zaidi katika soko la Tanzania ili kukidhi haja ya mawasiliano na ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu ya matunda ya ushirikiano mzuri kati ya nchi ya Tanzania na China.

Kukua kwa uwekezaji wa kampuni hiyo kwa kasi katika siku za karibuni kumefuatana na utengenezwaji wa simu za teknolojia ya hali ya juu “Smartphones” ambapo sasa kampuni hiyo inazitengeneza na kuuzwa katika soko la nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania kwa bei nafuu.

Pamoja na simu nyingine za teknolojia ya hali ya juu, simu mpya ambayo imeingizwa katika soko ni aina ya TECNO P3 ambayo imetengenezwa kukidhi mahitaji ya watumiaji kwa kuwa na teknolojia ya hali ya juu ya mawasiliano iliyowezeshwa kwa teknolojia ya Android 2.3 na kuiweza kufanya kazi sawa na simu za teknolojia ya juu yaani Smartphones.

Kwa kutumia simu hiyo ya P 3 wateja wataweza kupata uwezo mzuri wa kutumia internet kwa kasi ya hali ya juu pamoja na kuunganishwa na mitandao mablimbali ya kijamii, hususani kwa watanzania wa kada ya chini na wale wa vijijini abao matumizi ya intanet kwao imekuwa changamoto kubwa.

Kampuni hiyo ambayo imeendelea kujiimarisha katika soko la Tanzania kwa kuanzisha uuzwaji wa simu za teknolojia ya juu inatarajia kuingia katika ushirikiano na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom katika kuwawezesha watanzania zaidi kufurahia mawasiliano.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Meneja mahusiano wa kampuni ya TECNO, Mounir Boukali amesema, “ Tunatambua kuwa idadi kubwa ya watanzania wanauhitaji wa kutumia simu zenye teknolojia ya hali ya juu na yenye uwezo wa kuwa na intanet yenye kasi, matarajio haya hakika yanaletwa na simu hii ya TECNO P3 ambayo tumeiingiza sokoni punde.

Mounir alifafanua zaidi kuwa kampuni yake pia imeingiza katika soko aina nyingine ya Smartphones ambazo zinauzwa kwa bei ambayo watanzania wengi wanaweza kuimudu.

“Soko la mawasiliano na simu limeshuhudia ongezeko kubwa la matumizi ya intanet katika nyanja mbalimbali, hivyo ni wakati muafaka kwa makampuni ya simu na watengenezaji wa simu kuungana pamoja katika kuhakikisha wanakidhi mahitaji ya wateja wao,”

Akizungumzia simu hiyo Mounir alisema, TECNO P3 ina kioo cha kushika kwa mkono ( Touch screen) pia ina Wi – Fi, na imeunganishwa na huduma ya Facebook, Google Play Store, Gmail , Yahoo , Opera Mini, Whatsup na nyinginezo, na la muhimu zaidi ni kwamba simu hiyo ina laini mbili za simu. 

Pamoja na kujiimarisha huko katika soko la biashara kampuni hiyo pia imeendelea kujenga ajira kwa watanzania ikiwa ni sehemu mojawapo ya faida za uwekezaji wa kampuni hiyo nchini.

Dunia ya sasa imeshuhudia mapinduzi makubwa ya kiteknolojia ambapo nchi zinazoendelea zinahitaji maendeleo haya katika kuhakikisha zinaendana na kasi ya maendeleo kulingana na teknolojia hiyo katika kufikia malengo yao ya kiuchumi na kijamii.

Vodacom yazawadiwa Tunzo ya kuwa mdhamini mkuu wa sabasaba

$
0
0


 Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda, akimkabidhi tuzo ya udhamini bora Meneja Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania, Liginiku Milinga,Kampuni ya hiyo iliibuka kidedea kwa kuwa mdhamini mkuu wa maonesho hayo na pia ilipata cheti kwa kushika nafasi ya pili katika sekta ya mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa “sabasaba” yaliyofanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Pamoja nao katika picha ni Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Abdallah Kigoda. 
 Meneja wa Malipo ya ziada wa Vodacom Tanzania Liginiku Milinga akipozi katika picha baada ya kupoke tuzo ya mdhamini mkuu wa mawasiliano katika maonesho ya 37 ya kimataifa  “sabasaba”  Tuzo hizo zilitolewa na Waziri Mkuu. Mhe. Mizengo Pinda.

The Government of Tanzania, AngloGold Ashanti and African Barrick Gold sign Multi-Stakeholder Partnership

$
0
0


The Multi-Stakeholder Partnership Initiative to Improve Artisanal and Small-scale Mining (ASM) – Large Scale Mining (LSM) Coexistence in Tanzania met today in Dar es Salaam to launch its collaboration


DAR ES SALAAM: A full day meeting of the Multi-Stakeholder Partnership Initiative to Improve ASM-LSM Coexistence in Tanzania was hosted by the government of Tanzania on Friday, 28 June in Dar es Salaam. In attendance were representatives from the Ministry of Energy and Minerals, the Ministry of Home Affairs, small scale mining operators, civil society, the World Bank, and the large scale mining (LSM) industry.


The Multi-Stakeholder Partnership (MSP) initiative seeks to improve ASM-LSM coexistence in Tanzania by fostering the legal, regulated, safe, sustainable development of an ASM sector that operates within the rule of law and with respect for human rights. Specifically it aims to ensure that all who are legally engaged in ASM work under fair labor standards and in proper health and safety environments, allowing small scale operators to exercise a scale of mineral activity that suits their financial capacities and long-term ambitions.


The meeting signed the MSP Framework Agreement that serves as the Terms of Reference (TORs) for the stakeholder collaboration. A national Steering Committee is responsible for ensuring the implementation of MSP activities, meeting on a quarterly basis to review progress.


The first stage of actualizing the MSP is the establishment of two pilot schemes—one in near the Geita Gold Mine and one near the North Mara Gold Mine in Tarime region. Planning of the pilots has been underway since April 2013 in the two respective areas. The pilots aim to model practical approaches towards ASM-LSM coexistence in the country. Activities may include: 

improved geological support to small-scale operators, further processing and value-addition opportunities for mine operators, developing responsible gold supply chains from mine to market, mainstreaming gender in the entire value chain, and improving revenue and benefit flows back to local governments and communities.


On behalf of the Government of Tanzania, the Permanent Secretary for the Ministry of Energy and Minerals stated: “The sustainable development of the artisanal and small-scale mining sector has always been a top priority for the government. Over the past four years, we have embarked on reform initiatives including the development of a small-scale mining loan scheme to operators and the design of a small grants program for operators and communities. This MSP Initiative complements activities already underway within our Ministry by leveraging additional technical knowledge and resources from the private sector and the World Bank to promote greater national participation in our mining industry.” 


Through its Tanzania Country Director, Mr. Philippe Dongier, the World Bank stated: "The World Bank is committed to supporting initiatives aimed at strengthening the artisanal and small-scale mining sector in Tanzania as this sector impacts on a significant number of people in the rural areas and is therefore relevant to any effort intended to reduce poverty among the rural populations." In addition, Mr. Christopher Sheldon, Sector Manager for the Oil, Gas and Mining division of the World Bank, responsible for Africa: “The World Bank is pleased to assist in this important initiative. It reflects our institution’s commitment to transform the artisanal and small-scale mining sector into a positive contributor to poverty reduction whilst equally increasing the national share of mining benefits.”


The initiative also received endorsement from the private sector, “AngloGold Ashanti believes strongly in the need to engage with all stakeholders in finding strategies to address ASM in Tanzania, and we are excited to be part of the MSP pilot scheme in Geita”, Laurent Coche, Senior Vice President for Sustainability at AngloGold Ashanti, said at the launch. 


ABG Vice President Corporate Affairs, Deo Mwanyika, echoed this industry commitment, “Today consolidates our commitment to supporting the artisanal and small mining Industry. The MSP offers a unique opportunity to commence concerted efforts with numerous partners to deliver a successful outcome.”.


Viewing all 46397 articles
Browse latest View live




Latest Images