Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live

HAYA MDAU KATUTUMIA HII TUELIMIKE KIDOGO KUHUSIANA NA AIR FORCE ONE


Ally Rehmtullah 2014 - Fashion Avenue.

Tonight & Every 1st Friday of The Month Grooveback @ Rouge-Hyatt, Kempinski!

HARUSI FASHION SHOW JULY 6, 2013

$
0
0
The fourth edition of  the Tanzania first and premier wedding show preparation are all under way slated to be held this year on 6th July at Hyatt Kilimanjaro filled with the very best of wedding suppliers and stakeholders for all wedding requirements.

The founder and the organizer of this huge and remarkable annual event Mustafa Hassanali stated “Now in its Fourth year, the event is growing Bigger and Better compared to previous years and we look forward to the growth of the Wedding industry and its stakeholders”

True to the quote, this years wedding show has already attracted more wedding gown designers and bridal boutique owners most of them who have been participating since its inception in 2010. The Wedding show will take place from 7pm onwards.

“Wedding is the union of families and communities, a once in a life time indulgence, so our plan is to give the astute bride and grooms all their requirements they need under one roof, and this is the perfect time for them and their friends and family to see and experience all the services and products for their big day” said PR and Media Manager Esi Mgimba.

The Harusi trade Fair brings various wedding related vendors and suppliers all together, a melting and networking point for only the best in the Tanzanian Wedding Industry thus making Harusi Fashion Show a premier Wedding Show in Tanzania. The designers and bridal boutiques showcasing at this years event are An Nisaa Abayas, Manjuu, The Wedding Kingdom, Mustafa Hassanali, Gracella Bridal Boutique, Sinta Bridal lounge, Twaiba Classic Wear and The Brand House.

The following will be exhibiting at Harusi Fashion Show ,Rupam Stores LTD, Wedding Kingdom Boutique, AVP, MC Luvanda, Flying Chefs, Mbezi Garden Hotel , The Cake Shop, Liquid Lab, Gogo Shop, Queens Gems & Jewellers, Asila Bridal Packages, Harusi Nzuri, Malaika Media, E – Cakes, VanRoy, Omni Studios and Shayland Photogenic

We urge the public to attend this show in Large Numbers so as to appreciate creativity, and the entrance to the show will be 50,000 tsh for the front row VIP seats and 20,000 tsh for normal seats, support Tanzanian enterprises and promote Made In Tanzania products” concluded Ms. Mgimba
Harusi Trade Fair 2013 is proudly sponsored by 361 Degrees, Clouds FM, Clouds TV, Events lite, Prime Advertising, Century Cinemax and Baileys Cream and Spirit.

Wateja Airtel sasa kujishindia Nyumba 3 za kisasa kupitia huduma ya YATOSHA

$
0
0

 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa promosheni ya Airtel Yatosha Shinda Nyumba 3,  iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi Anethy Muga.
Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiwaonyesha waandishi wa
habari (hawapo pichani)  nyumba watakayojishindia washindi wa Airtel
Yatosha Shinda Nyumba 3 iliyozinduliwa leo  katika ofisi za Airtel
Morrocco jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja masoko wa Airtel bi
Anethy Muga
======  ======  ====== ======
Wateja Airtel sasa kujishindia Nyumba 3 za kisasa kupitia huduma ya YATOSHA


*         Kila siku mshindi mmoja kuondoka na kitita cha shilingi milioni moja

*         Mteja mmoja kujinyakulia nyumba 1 kila mwisho wa mwezi kwa miezi mitatu


jumaa Julai 5, 2013 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania
inayotoa huduma ya mawasiliano bora na nafuu zaidi nchini leo
imezindua promosheni mpya kabambe itakayowawezesha wateja wote wa
Airtel Yatosha kujishindia zawadi mbalimbali huku wakiendelea
kufurahia huduma ya Airtel yatosha ya siku, wiki au mwezi kama
kawaida.



Uzinduzi wa promosheni hiyo mpya ya Airtel Yatosha inadhihirisha
dhamira halisi ya Airtel kupitia huduma yao kabambe ya Airtel Yatosha
yenye lengo la kutoa huduma nafuu huku wakiendelea kuwafaidisha wateja
wao nchi nzima



Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo katika ofisi kuu ya
Airtel Tanzania, Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Bw, Suni Colaso alisema
"Leo Airtel tunafanya tukio la kihistoria mara baada ya uzinduzi wa
huduma ya Airtel yatosha. Sasa tunawazawadia wateja wetu wa Yatosha
kwa aina ya kipekee kabisa, Kila atakaejiunga na huduma ya Airtel
Yatosha moja kwa moja atakuwa amejihakikishia nafasi ya kujishindia
zawadi ya Nyumba ya kisasa au kitita cha Pesa taslim. 


 Tutakuwa na  
mshindi mmoja wa kila siku atakaeibuka na shilingi milioni moja, na 
kama hiyo haitoshi kila mwisho wa mwezi tutatoa nyumba moja kwa 
mshindi mmoja kwa muda wa  miezi mitatu" 
Nyumba tunazotoa kwa wateja wetu ni za kisasa kabisa ili kudhihirisha  
kuwa Airtel Yatosha, ni nyumba yenye vyumba vitatu, sebule pamoja na  
jiko, itakuwa ndani ya fance iliyonakishiwa katika hali ya mvuto zaidi  
ili kumfanya mshindi wetu kufurahia zaidi kuwa mteja wa Airtel  
yatosha", aliongeza kusema Bw Colaso



Akifafanua jinsi ya kushiriki promosheni hiyo Meneja Masoko wa Airtel
Bi Anethy Muga alisema  " Ili mteja kushiriki promosheni hii, mteja
atatakiwa kuendelea kujiunga na kutumia huduma yetu ya Airtel Yatosha
ya Kila SIKU, WIKI, au MWEZI kwa kupiga *149*99#,  kwa kufanya hivyo
moja kwa moja utakuwa umeingia kwenye nafasi ya droo ya kila siku,
wiki  au ya mwezi na unaweza kujishindia zawadi zetu kabambe Ikiwemo
Nyumba.



Promosheni hii ya Airtel Yatosha ni maalum kwa wateja wote wa Airtel
yatosha wa malipo ya kabla, Ikiwa hujajiunga na Airtel jiunge leo na
utumie huduma ya Airtel Yatosha ili upate nafasi ya kujishindia nyumba
ya kisasa kila mwisho wa mwezi au pesa taslimu ndani ya siku tisini
kila siku




Airtel ilizindua huduma ya Airtel Yatosha miezi mitatu iliyopita kwa
lengo la kuwawezesha wateja wake kupata huduma bora na nafuu zaidi,
lengo la huduma hii ni kumpatia mteja huduma nafuu ya sms , muda wa
maongezi pamoja na kufurahia mtandao wa interneti wa 3.75G kwa masaa
25 tangu kujiunga.  Kujiunga mteja anatakiwa kupiga *149*99# na
kujichagulia kifurushi kinachomfaa kwa SIKU, WIKI au MWEZI.

Tamasha la filamu Grand Malt lazua mambo jijini mwanza.

$
0
0
 WASANII mbalimbali wanaojitokeza katika Tamasha la Wazi la Filamu la Grand Malt Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ linalofanyika katika Uwanja wa Nyamagana, jijini hapa wamezua mambo kwa kutaka wapambanishwe na wakongwe.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, baadhi ya wasanii hao walisema wana uhakika mkubwa wa kuwafunika wakongwe na wanataka mpambano wa ‘live’ siku ya kufunga tamasha hilo hapo kesho.
Akizungumza kwa kujiamini, Paul Mabula ‘Bonge’ alisema msanii Jacob Steven ‘JB’ hawezi kutamba kwake, kwani yeye anajiona ni mkali zaidi kuliko yeye na akikubali wachuane ‘live’ hapo kesho atafanya vitu vya ajabu vitakavyowashangaza wengi.   “Yule JB ni bwa’mdogo tu kwangu, kama anajiamini mwambie Jumapili nipambane naye halafu aone nani mkali, mimi najiamini mno katika kila kitu,” alisema Bonge kwa kujiamini mno.
Isha Rama ambaye mwenyewe anajiita Irene Uwoya, alimtaka msanii huyo pamoja na Jacqueline Wolper wapambane naye, kwani anaweza kuwafunika wote wawili kwa wakati mmoja. “Nitakuja na dogo wangu hata yeye ana uwezo wa kumfunika (Vicent Kigosi) Ray na watatambua Mwanza kuna vipaji vingi na vyenye uwezo zaidi kuliko wao,” alisema Isha.
Akizungumzia hilo, Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam alisema, amefurahi kuona wasanii wa Mwanza wanavyojiamini mno na kuwatahadharisha wakongwe wakae chonjo kesho kwa upinzani mkubwa watakaoupata.    “Hapa Mwanza tumeshuhudia vipaji vya kila aina, nimefurahi kwa kiasi kikubwa kwa jinsi wanavyojiamini, kwetu Grand Malt tunaamini lengo letu limefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema naye amefurahishwa pia na wazo la wasanii hao na kuwaonya wakongwe watakutana na vitu visivyo vya kawaida hiyo kesho.   
“Hapa Mwanza kuna balaa tupu, maana hawa wasanii sikutegemea kama wanajiamini kwa kiasi kikubwa kama hivi, tutaona hiyo Jumapili mambo yatakavyokuwa,” alisema.

Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na linatarajiwa kumalizika kesho, huku wakati wote wa tamasha hilo zikionyeshwa filamu mbalimbali za Tanzania.
Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

SJMC,TASWA kuendesha mafunzo kwa waandishi habari za michezo

$
0
0

 SHULE Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) wataendesha mafunzo ya siku tano kwa waandishi wa habari za michezo nchini.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Makamu Mkuu wa SJMC, Dk. Michael Andindilile alisema mafunzo hayo yatafanyika Agosti mwaka huu na yataendeshwa na wahadhiri kutoka chuoni hapo, waandishi wa siku nyingi na wataalamu wa michezo mbalimbali.

“Tunao wahadhiri waliobobea katika tasnia ya habari, lakini pia wapo waandishi wa habari wakongwe ambao ni waalimu kitaaluma, pia tutachukua wataalamu wa michezo mbalimbali kuja kufundisha kwa siku hizo tano,” alisema Dk. Andindilile.

Makamu Mkuu huyo wa SJMC, aliupongeza uongozi wa TASWA kwa wazo lao la kushirikiana na SJMC na kuongeza kuwa mafunzo hayo yatachukua siku tano na yatafanyika Dar es Salaam yakihusisha washiriki 45 kutoka vyombo mbalimbali vya habari katika tarehe itakayotangazwa.

Alisema wataalamu wa michezo mbalimbali kama vile soka, riadha, netiboli, gofu, kikapu, wavu na mikono watapata fursa ya kutoa mada kuhusiana na michezo yao na kwamba TASWA na SJMC wanashirikiana katika kuomba wadhamini wasaidie mafunzo hayo.

“Hii ni awamu ya kwanza kwa waandishi wachanga na baadhi ya wa kada ya kati, baada ya hapo tutaendesha mafunzo ya namna hii kwa waandishi wa siku nyingi wa habari za michezo na wahariri wa habari za michezo, tunaamini baada ya hapo kutakuwa na mabadiliko upande wa uandishi wa habari za michezo,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliishukuru SJMC kwa kukubali kushirikiana na TASWA na kwamba siku zote chama chake kimekuwa kikipigania kuandaa mafunzo kwa wanahabari wa michezo kama sehemu mojawapo ya kukuza weledi.

“Fursa hii ni moja ya jitihada za TASWA kuhakikisha waandishi wa habari za michezo wanapata nafasi ya kujifunza zaidi kuhusu namna bora ya kuripoti habari za michezo kwa ujumla wake, hivyo nafasi hii si tu itasaidia wanachama wa TASWA bali pia na vyombo vya habari na washiriki hawatalipia chochote.

“Tunaamini waandishi wanapoboresha uandishi wao inachangia kwa kiasi kikubwa kukuza heshima ya vombo vya habari, hivyo tunaomba wadau mbalimbali washirikiane nasi kudhamini mafunzo haya,” alisema Pinto na kuongeza kuwa kwa kushirikiana na SJMC wanaamini siku za usoni wanaweza kuandaaa mafunzo ya muda mrefu.

tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi laendelea mkoani iringa.

$
0
0
Pichani ni Muuguzi wa UMATT,Bi.Mery Biseko  akionesha namna ya kutumia Kondom za kike kwa vijana mbalimbali  (hawpao pichani) waliojitokeza katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.
Mratibu wa mradi wa TUWALEE kutoka katika shirika la UMATT,Bi Jemida Kulanga, akitoa elimu ya Afya ya Uzazi kwa vijana mbalimbali waliokuwa wamejitokeza katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.
========  ======= =======
Shirika la UMATT linakabiriwa na  changamoto ikiwemo ya kutokuaminika katika huduma wanazotoa, hasa katika suala la upimaji afya kwa wateja wao na walio wengi  hawana elimu juu ya afya ya uzazi.


Hayo yamesemwa na Mratibu wa mradi wa TUWALEE kutoka katika shirika hilo,Bi Jemida Kulanga, wakati akizungumza na wandishi wa habari katika tamasha la mafundisho ya afya ya uzazi yanayoendelea katika viwanja vya Kihesa sokoni,mkoani Iringa.


Bi.Jemida amesema kuwa kuna haja kubwa ya kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana ambapo itasaidia kupunguza magonjwa mbalimbali yatokanayo na ngono pamoja na mimba zisizotarajiwa .


Amesema kuwa wameamua kufanya tamasha hilo kutokana na asilimia kubwa ya wateja wao waliofika katika ofisi zao ,wameonekana kuwa na uelewa mdogo juu ya afya ya uzazi ikiwemo matumizi ya mpango wa uzazi.


Hata hivyo katika mafunzo hayo pia wameweza kufundisha matumizi ya Kondomu za kike kwa wanawake ,kwani wanawake wengi wameonekana kutokujua matumizi yake na wengine kutokuijua kabisa kondom hiyo ya kike.


Aidha amewataka vijana kutafuta habari zinazohusu afya ya uzazi ili kuepuka magonjwa hatarishi yanayohusiana na suala zima la uzazi.



TID EXCLUSIVE INTERVIEW WITH SPORAH..!

MDAU KAMBI MBWANA NA KILIO CHAKE CHA USHURU WA KODI KWENYE MITANDANO YA SIMU

$
0
0
DUH NI HATARI. NATUMIA namba line sita za simu. Mbili ni maalum kwenye modem, yani Vodacom na Airtel. Pia line nne ni zangu za mkononi na zote zipo active. Sasa najiuliza maswali nitazimudu? 

Kama kila mwezi elfu 1000 sawa na elfu 6000+12 yani mwaka mmoja. Bado utitiri wa kodi nyingine, kama vile umeme, Dstv vocha za kwenye simu au bando la internet. Bado usafiri wa ndani na matumizi mengine ya kimaisha. 

Naajiuliza tena kama nastahili kuendelea kutumia namba zote hizo japo najua mara nyingi zimekuwa na manufaa na mimi. Pamoja na yote hayo, sidhani kama Watanzania wanastahili kutozwa kodi hizo kwa line zao wakati tuna vyanzo vingi vya mapato. Lol. 

Watanzania sisi? Viongozi hawa wasiotumia vichwa vyao, hasa waliokuwa Wizara ya Fedha, hasa watalaamu ndio wanaoifanya serikali ya CCM ichukiwe na wananchi jamani? Nani amepitisha upupu huu? Kwanini wabunge wote wasigome? Duh. Kichwa kinauma.

RAIS KIKWETE MGENI RASMI TAMASHA LA MATUMAINI 2013

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
 ======  =======  =========

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Matumaini ambalo litafanyika keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa tamasha hilo, Abdallah Mrisho, amesema Rais Kikwete ambaye hivi karibuni alikuwa na ugeni mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Obama, amekubali kuwa mgeni rasmi ambapo atatoa neno la matumaini kwa maelfu ya watu watakaojitokeza uwanjani hapo.

Eric Shigongo.

Akizungumzia zaidi juu ya ugeni huo mkubwa, Mrisho alisema: “Rais Kikwete amekubali ombi letu la kuwa mgeni rasmi, atatumia nafasi hiyo kutoa neno la matumaini kwa wote watakaojitokeza uwanjani hapo.

“Rais pia ndiye atakayefungua mechi ya Wabunge wa Simba dhidi ya Yanga ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa. Kama ujuavyo rais wetu ni mtu wa watu na ni mpenda michezo, hilo linajulikana siku zote.”

Rais Kikwete.

Aidha, Mrisho aliongeza kwa kusema kuwa shabaha ya tamasha hilo ni kuamsha upya imani ya Watanzania kwa nchi yao. Kuwafanya wawe wazalendo na kila mmoja kujiona analo jukumu la kufanya, kuhakikisha Tanzania yetu inapiga hatua.

“Mbali na Rais Kikwete, wengine watakaotoa neno la matumaini siku hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.

Zitto Kabwe.

“Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya East Africa Speakers Bureau Limited (EASB), Paul Mashauri, mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali, James Mwang’amba na mwanamitindo, Jokate Mwegelo.

“Wote hao, kila mmoja atakuwa na fursa ya kufikisha Neno la Matumaini ili kila atakayehudhuria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, aondoke akiwa mpya, akiwa na matumaini mapya kwa taifa lake na maisha yake kwa jumla,” alisema Mrisho.

Nape Nnauye.

Kwa upande wake Shigongo amesema kuwa udini, ukabila na kila aina ya ubaguzi, vitachimbiwa shimo na kuzikwa.
“Taifa linapita kwenye kipindi kigumu ambacho ni changamoto nzito. Unazungumzwa ufisadi, migomo imekuwa mingi, udini na ukabila vinapenyezwa kwa kasi, pamoja na aina zote za ubaguzi, hivi vyote tunapaswa kuvizika.
“Tuna makusudio ya kuwafanya Watanzania wajione wamoja licha ya tofauti za kiitikadi zilizopo. Mahitaji yetu ni kupaza sauti kuwa kila mtu yupo huru kusimamia anachokiamini lakini linapokuja suala la umoja wa kitaifa, tofauti zote zinapaswa kuwekwa kando,” alisema Shigongo.

Paul Mashauri.
Akizungumzia juu ya tamasha hilo, Shigongo alisema: “Hivi karibuni matokeo ya kidato cha nne yalitoka hapa nchini na kuonyesha watoto wengi walikuwa wamefeli. Kilichoniuma zaidi ni niliposikia baadhi ya watoto waliamua kukatisha maisha yao kwa sababu matokeo yao yalikuwa mabaya.”

BancABC yakaribisha Wateja kujiunga na VISA Cash Card

$
0
0
IMG_9016
Baadhi ya wafanyakazi wa BancABC wakisajili wateja wapya wa huduma ya VISA Cash Card ni Kadi ya malipo ya kabla ambayo hupunguza usumbufu wa kubeba fedha usio salama. Ambapo Mteja kuwa na kadi hii si lazima uwe na akaunti ya BancABC.
IMG_9032 
Afisa Mahusiano wa BancABC Sarah Pima akitoa maeleozo ya namna ya kutumia VISA Cash Card kwa mmoja wa wateja aliyetembelea banda la Bank hiyo lililopo karibu na Banda la Home Shopping Centre katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Wa pili kulia ni Afisa Mahusiano wa Bank hiyo Shamsa Aboud.
IMG_9038
Wananchi wakiendelea kupatiwa huduma na wafanyakazi wa Bank hiyo.
IMG_9045
Muonekano wa Banda la BancABC katika maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.


IMG_9050
Moja ya Bango la Benki hiyo lililopo uwanjani hapo.

Zijue faida za VISA Cash Card kama ifuatavyo:-

- Una saa 24 siku 7 za juma kupata huduma kwenye akaunti yako popote, zaidi ya ATM 400 zenye nembo ya VISA ndani ya Tanzania na zaidi ya ATM milioni 1.3 duniani kote.

-Unaweza kufanya manunuzi kwenye sehemu za biashara zaidi ya 1000 zinazokubali VISA Tanzania na sehemu za biashara zaidi ya milioni 35 duniani.
-Rahisi kuipata.
-Inaweza kutumika papo hapo.
-Kuweka fedha na kuzitumia papo hapo.
-Rahisi kuweka fedha na kuzitumia haraka.
-Manunuzi ya moja kwa moja kupitia mtandao.
-Hudhibiti matumizi yako(unatumia ulichonacho kwenye kadi).
- Faraja na Usalama kupitia CHIP na namba za siri(PIN) hudhibiti udanganyifu na matumizi ya ulaghai.
-Fedha hurudishwa na kupata kadi nyingine pindi inapopotea/kuibiwa.
Ni nani anayeweza kutumia BancABC VISA Casha Card?
-Wateja na wasiokuwa wateja wa BancABC.
-Makampuni- kwa malipo ya posho na mishahara.
-Wazazi-fedha ya kujikimu kwa wanafunzi/gharama za maisha. Bora zaidi kwa usalama wa fedha.
-Mashirika ya Pensheni na Makampuni ya Bima- kwa malipo yenye faida.
-Wafanyabiashara ya Utalii- kwa malipo ya ada Utalii wa mbuga.
-Serikali- kwa malipo ya ruzuku na mikopo.
Na Unawezaje kupata BancABC VISA Cash Card?
Tembelea moja ya matawi yao ili uweze kujaza fomu fupi ya maombi ukiwa na viambatanishi vifuatavyo:
Raia-Kitambulisho cha Kura/Leseni ya Udereva/ Passport.
Sio Raia-Passport na Kibali cha makazi.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa namba zifuatazo:
Upanga-Simu 255 22 2121537, 2121538, 2121539.
Kariakoo-Simu 255 22 2180212, 2180182, 2180108.
Quality Centre- Simu 255 22 2865904-910.
Arusha-Simu 255 27 2546390.

GEREZANI PAMENIFANYA NIMJUE MUNGU NA KUMUAMINI KUWA YUPO-TAKE ONE EXCLUSIVE NA LULU

PROFESA LIPUMBA AONGOZA MAZISHI YA MLINZI WA MAKAO MAKUU YA CUF MUHARAMI ABDALLAH SHAABAN TANGANYIKA

$
0
0
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akikabidhiwa daftari la michango wakati alipowasili Tabata, jijini Dar es salam, nyumbani kwa Marehemu Muharami Abdallah Shaaban Tanganyika aliyefariki juzi katika hospitali ya Amana. Marehemu alikuwa ni mfanyakazi ya ulinzi katika makao makuu ya CUF, Buguruni. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiandika kwenye daftari la michango. Mwenye pama ni Naibu katibu Mkuu wa CUF Mhe. Julius Mtatiro na kulia ni kaka wa marehemu Ismail
 Sehemu ya waombolezaji
 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akipata chakula na waombolezaji weng 
ine

 Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongea machache kabla ya safari ya kuelekea makaburini kuanza. Alimsifia marehemu Tanganyika kama mmoja wa wafanyakazi waaminifu na makini waliojituma sana. Pia alisema wamepoteza askari hodari ambaye alikuwa nguzo muhimu ya ulinzi katika makao makuu ya chama hicho cha ulinzi

Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiongoza mazishi hayo yaliyofanyika kwenye makaburi ya familia ya mama wa marehemu huko Segerea

MTANGAZAJI DIDA SHAIBU (WA KIPNIDI CHA MITIKISIKO YA PWANI) AOLEWA NA SASA NI MRS EZDEN JUMANNE.

$
0
0

Dida wa Ezden ndo habari ya mujini
Maharusi wakiwa na nyuso za furaha mara baada ya kufunga ndoa 
Bwana harusi akimchum mke wake halali wa ndoa Dida
Mashallah the newly weds Mr & Mrs Ezden Jumanne.
Hongera sana Dida na Ezden tunawatakia kila la kheri katika ndoa yenu.
PICHA KWA HISANI YA http://www.jestina-george.com.

MWAKILISHI WA FAO NCHINI ATEMBELEA BANDA LA UMOJA WA MATAIFA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
IMG_8897 
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (katikati) akipata maelezo ya kazi mbalimbali za Shirika hilo kutoka kwa Afisa Habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Usia Nkhoma Ledama wakati alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8935
Mkufunzu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam ( DIT) Marwa Wambura (katikati) akimuonyesha Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman (kulia) malighafi za ngozi zinazotumika kutengeneza bidhaa mbalimbali na wanafunzi wa Chuo hicho ambapo mafunzo hayo yanadhaminiwa na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza viwanda Duniani (UNIDO).
IMG_8946
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akiangalia viatu vya ngozi vilivyotengenezwa na wanafunzi wa Chuo cha DIT kwenye banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
IMG_9000
Baadhi ya bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Wanafunzi wa Chuo cha DIT cha Mwanza.
IMG_8976
Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo nchini (FAO) Diana Templeman akizungumza na waandishi habari ambapo amefafanua changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia katika mabadiliko ya tabianchi ambapo wao kama Umoja wa Mataifa wanafanya kazi ya kuelemisha Umma, Wakulima, Wafanyabiashara na Wasindikaji jinsi ya kuelelewa mabadiliko ya tabianchi katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa njaa duniani na upatikanaji wa chakula. Kulia ni Mratibu wa kazi za vijana vijijini katika masuala ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji wa FAO Bw.Eliamoni Lyatuu.
IMG_8968
Afisa habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) Usia Nkhoma Ledama akitoa ufafanuzi wa vipeperushi mbalimbali vinavyozungumzia kazi zinazofanywa na shirika hilo hapa nchini kwa baadhi ya vijana na watoto waliotembelea banda hilo leo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
IMG_8980
Baadhi ya watoto waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa wakifurahia picha.

OFFICIAL DSTV BIG BROTHER PARTY AT NYUMBANI LOUNGE

$
0
0
DSTV pamoja na AIRTEL wanakuletea special Viewing party ya Big Brother Eviction Show Kila Jumapili ndani ya NYUMBANI LOUNGE kuanzia saa mbili usiku. Wiki hii Ndani ya Big Brother Rapper Mtanzania WAKAZI atatumbuiza. 

AJALI MBAYA YA BASI LA SUMMRY YAUA WATU TISA NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA.

$
0
0




Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni Iku na kuuwa watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.



Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendesha na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa  jina la Ntungu.



Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana 
Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.

HABARI KWA HISANI YA http://lukwangule.blogspot.com

MLEZI WA CCM MKOA WA DAR, MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM MKOA WA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
 Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Julai 6, 2013.
  Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakiwa katika Ukumbi wa Karimjee wakimsikiliza Mlezi wao, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipozungumza nao leo. 


Baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakisimama kumkaribisha Mlezi wao katika Ukumbi wa Karimjee, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipofika ukumbini hapo kuzungumza nao leo, Julai 6, 2013. 
  Mlezi wa CCM Mko wa Dar es Salaam, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mbunge wa Temeke, Mhe. Abas Mtemvu, wakati alipowasili kwenye Ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, leo Julai 6, 2013 kwa ajili ya kuzungumza na wajumbe hao. Picha na OMR

Lowassa awapa milioni 20 wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza !

$
0
0

Mhe. Lowassa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 20 Bw.Matondo ambaye ni mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa wafanyabiashara wadogowadogo wa jijini Mwanza (SHIUMA) huku akishuhudiwa na diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha (anayepiga makofi). 
Bw. Lowassa alisema kwamba kutokana na marafiki zake ambao aliwataja Bw.Christopher Mwita Gachuma (MNEC- Tarime), Bw.Mathias Manga (MNEC-Arumeru), Bw.Raphael Chegeni (MNEC-Busega) Bw.Shanif Hiran Mansoor(Mbunge-Kwimba) na Bw.Altaf Mansoor (Mkurugenzi wa MOIL) ambao waliniomba na kunisisitiza kuwaona na kuwasikiliza nami nimewapa utaratibu wa kuandaa Harambee kubwa ya kuwachangia na marafiki zangu wengine.

“Leo hii siyo harambee bali nataka kuwachangia kianzio katika mfuko wenu na siku zote CCM inasema kwamba ni lazima kuwapatia mtaji vijana hivyo nawapatia Cheki ya milioni 10 na jioni ntwapatia shilingi milioni 10 jumla zitakuwa shilingi milioni 20 za kuanzia ili kujipanga na harambee kubwa





Mmoja kati ya wanakamati wa SHIUMA akionyesha hundi ya shilingi milioni 20 waliyokabidhiwa na Mhe. Lowassa kama sehemu ya harakati ya kutatua masuala mbalimbali ya changamoto zao walizoziainisha kwenye risala.
Lowassa akiwapa somo wamachinga Mwanza.

WAZIRI Mkuu mstaafu Bw.Edward Lowassa amewataka wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwawezesha wafanyabiashara wadogo maarufu kwa MACHINGA ili kuwawezesha kupata mitaji ya kujikwamua kiuchumi.


Akizungumza na Machinga wa shirika la SHIUMA kwenye eneo la Makoroboi Jijini Mwanza leo mchana Mhe. Lowassa ambaye ni Mjumbe wa NEC  Wilaya ya Monduli na Mbunge wa Jimboni humo alisema njia pekee ya kuwawezesha wamachinga hao ni kuwachangia fedha ili kuwawezesha kujiendeleza kupitia biashara zao na kuwapatia maeneo maalumu ya kufanyia shughuli zao.


Maneno yaliyowagusa.
“Ninyi ni watanzania wenye kujiamini na kujitafutia ridhiki kwa kufanya biashara zenu kwewnye Taifa lenu mkiwa huru na amani, lakini mkiwa hamna mijati hamtaweza kufika pahali popote hivyo niwaombeni sana wafanyabiashara wa Jiji na Mkoa wa Mwanza kuwachangia ili kuwawezesha kupata mtaji wa kuwaendeleza  na kujiingizia kipato katika biashara zenu za ujasiliamali”alisema.
Makoroboi jijini Mwanza.
Mjumbe huyo wa NEC alisema kwamba Ilani ya CCM inatambua na inaelekeza kwamba vijana wataandaliwa na kuanzisha vikundi vya ujasiliamali (SACOS) na kusajiliwa ili kuwapatia fedha ikiwa ni mitaji ya kuwawezesha kujiendesha jambo ambalo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ukurasa wa 88 na 89 hivyo tunataitekeleza kwa vitendo kama ambavyo ninyi tayari mmeanza kuitikia na hilo ndilo limenileta hapa leo nikiwa kiongozi ndani ya CCM.


“Nitaka nirudie msimamo wangu kwenu kwani kuna baadhi ya vyombo vya habari vinaniandika kwamba nimekuja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Taifa Bw. Mwiguru Mchemba (Mbunge wa Jimbo la Iramba)kuvunja ngome ya Chama furani hapa maeneo ya Jiji la Mwanza siyo kweli mimi niko na marafiki zangu nimekuja kutokana na wito wenu ili kuwasikiliza sasa puuzeni hayo”alisema.
Mkutano huo wa muda mfupi ulipo malizika tu Mhe. lowassa akiwa ameambatana na wamachinga mguu kwa mguu walimsindikiza hadi hoteli aliyofikia. PICHA ZOTE KWA HISANI YA G-SENGO
Viewing all 46395 articles
Browse latest View live




Latest Images