Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

For the first time, an East African film garners a prestigious award at the Khouribga African Film Festival.

$
0
0

PRESS RELEASE
JUNE 2013
KHOURIBGA AFRICAN FILM FESTIVAL
 
FOR THE FIRST TIME, AN EAST AFRICAN FILM GARNERS A PRESTIGIOUS AWARD AT THE KHOURIBGA AFRICAN FILM FESTIVAL.
The Khouribga African Film Festival is pleased to announce that the film, ZAMORA, Directed by Shams Bhanji and Produced by Javed Jafferji (ZG Films, Zanzibar) is the winner of this year’s Special Jury Prize. This historic win represents several firsts: the first time a film from Zanzibar/Tanzania has been included in the Khouribga African Film Festival, and a first time win for a film from East Africa. Jury member Sanaa Alaoui emphasized the jury’s difficulty in discerning this year’s prizes, because of the overall high quality of the films in competition.

Seventeen films from fifteen African countries competed in this 16th edition of the Khouribga festival, the second most important rendezvous for African film on the continent after FESPACO. She added that ZAMORA nevertheless stood out for its originality, its poetry, and its imagery. Earlier this year ZAMORA won a special award at FESPACO for best digital film.

ZAMORA earlier won a special jury prize (Silver Dhow) as well as Best East African Film at the 2012 Zanzibar International Film Festival. The film’s director, Shams Bhanji, was accompanied by his two lead actors, Richard Bezuidenhout and Richa Adhia.

Zamora is is much more than a swahili love story.....it is a poetic evolution of one man's hidden desires, and his quest to find true love. This is the director's first feature. Lahoussaine Ndoufi, the Director of the Khouribga African Film Festival added that he hoped that the award would encourage Shams Bhanji to consider co-producing his next film with the Centre Cinématographique Marocain.

KUNDI JIPYA LA MUZIKI LAJA JIJINI, KUJULIKANA KWA JINA LA NDEGE WATATU.

$
0
0
 Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina laNDEGE 3.
 
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
 
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 

Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

BIBI KIDUDE KUENZIWA TAMASHA LA ZIFF.

$
0
0
WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa na  Sit bin Saad ambaye ni mjukuu wa marehemu Bi.Kidude,Synerg,Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar  Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya  kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha ya ZIFF yaliyowahi kufanyika.
  
Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu kama ZIFF linaendelea kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika kumuenzi  marehemu Bi.Kidude katika tamasha hilo.
 
Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu kuanza kwake limekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona ya dunia  kuwapa burudani kulingana na mahitaji.
 
Usiku  wa wanawake unatarajia kufanyika jioni ya leo ndani ya Mambo klabu ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni wanawake pekee  ambapo  mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua dimba kutoa  burudani hiyo. Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi kwakuwa  tamasha la siku ya leo ni kwa ajili ya wanawake.
 
 katika tamasha hilo la usiku wa wanawake wasanii hao wataweza kukonga nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa tamasha hilo ambalo linamkumbuka Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa akiutoa katika kipindi chake chote cha uhai wake.
 
Hata hivyo burudani hiyo itaambatana na kuonyeshwa kwa filamu mbili tofauti ikiwemo ya The Last Fishing Boat kutoka Malawi na Lilet never Happened kutoka Netherland.

Na Andrew Chale, Zanzibar

Serikali ya Marekani yatoa dola milioni tatu kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi

$
0
0

Na Anna Nkinda – Maelezo.

Serikali ya Marekani kupitia  Mpango wa dharula wa kupunguza makali ya VVU  na Ukimwi (PEPFAR) imeipatia Serikali ya Tanzania dola za kimarekani millioni tatu fedha ambazo zitatumika kuwapima na kuwatibu wanawake wanaosumbuliwa na matatizo ya saratani  ya mfuko wa kizazi.

Hayo yamesemwa jana na Balozi Leslie Rowe kutoka ofisi ya Serikali ya Marekani anayeshughulikia mambo ya afya wakati akiongea na watu mbalimbali walioshiriki mkutano wa wake wa Marais wa Afrika uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Aidha Serikali ya Marekani pia imetoa  mashine 16 za cryotherapy ambazo zitatumika kama sehemu ya matibabu kwa ugonjwa wa saratani ya mfuko wa  kizazi katika Hospitali ya Kansa ya Ocean Road.

Balozi Rowe alisema  kuwa upatikanaji na mashine hizo  utawasaidia wanawake  wengi ambao wanasumbuliwa na ugonjwa wa Kansa ya shingo ya kizazi kuweza  kupata huduma ya vipimo  na matibabu mapema na haraka.

"Kutokana na maambukizi ya VVU wanawake wengi wako katika hatari kubwa  ya kupata ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi na matiti  kwa kushirikiana na PEPFAR tutaendelea kuwaunga mkono utepe wa pink,utepe mwekundu kuokoa maisha  ya wanawake.

Jitihada za pamoja  zinahitajika kwa kushirikiana na vikundi vya kijamii na kuimarisha miundombinu ili  kuhakikisha kuwa tunatoa vipimo na matibabu ya saratani kwa wakati”, alisema Balozi Rowe.

Alisema kuwa uongozi wa Rais Obama umeridhishwa na Serikali ya Tanzania kwa jinsi unavyolishughulikia tatizo la saratani  ya shingo ya kizazi na utaendelea kuwaunga mkono wanawake na wasichana Duniani kote ikiwa ni pamoja na katanua program mbalimbali na kutoa fedha  kwa ajili ya elimu, maendeleo ya kilimo na afya.

Akiongea na waandishi wa Habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mama Kikwete aliishukuru Taasisi ya Bush kwa kufanya mkutano huo nchini na kusema kuwa mambo yaliyojadiliwa ni upatikanaji wa elimu kwa mwanamke, upatikanaji wa Afya bora na kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema kuwa mwanamke ni mtu muhimu sana katika jamii haijalishi ana elimu kiasi gani yeye ni mlezi wa familia na  ukimwezesha mwanamke kielimu ni ukombozi mkubwa katika jamii kwani ni rahisi kwake kukabiliana na magonjwa mbalimbali ikiwemo saratani ya shingo ya kizazi.

“Miaka ya nyuma kutokana na baadhi ya watu kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusu ugonjwa wa Ukimwi waliweza kuamini kuwa mtu akiwa na maambukizi ya ya VVU amerogwa lakini  hivi sasa baada ya watu kupata elimu wkamekuwa na uelewa mkubwa.

“Ukimwezesha mwanamke kielimu na kiuchumi anakuwa na uhuru wa  kufanya mambo yake bila ya kutegemea msaada kutoka kwa mme wake ninachowaomba wanawake wenzangu mfanye  kazi kwa bidii kwani mwanamke  akiwa na kipato cha  kutosha hawezi kudharaulika”, alisema Mama Kikwete.

Alisema kuwa zamani wanawake wasiokuwa na kazi walikuwa wanaitwa magoli kipa ingawa  walikuwa na kazi kubwa ya kuangalia familia na jamii ikasahau kuwa wanawake ndiyo wazalishaji mali. Pia aliwaomba wanawake wasiogope kuchangamkia fursa zinazopatikana  na wasiache kumuunga mkono mwenzao pale anapoomba nafasi ya kupata fursa hizi  kwani wakiwa pamoja wanaweza.

Katika mkutano huo pia Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa zamani wa Marekani  George Bush walitambulisha rasmi  Utepe wa Pinki , Utepe mwekundu  ambayo ni alliance inayofanya  kazi ya kupambana na kansa ya saratani ya mfuko wa kizazi na saratani ya matiti  katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara na Amerika ya Kusini.

Tanzania  ni nchi ya tatu Barani Afrika kutambulisha  Utepe wa Pinki , Utepe mwekundu  alliance nchi zingine ni  Zambia na Botswana.

Mkutano huo wa siku mbili  uliomalizika jana  uliandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

VIWANJA VILIVYOPIMWA VYA UKUBWA MBALIMBALI VINAUZWA.

$
0
0
VIWANJA VILIVYOPIMWA VINAUZWA VYA UKUBWA MBALIMBALI.VIPO VIKAWE HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA,NI KARIBU ZAIDI KUPITIA BARABARA YA BAGAMOYO,SHUKA NJIA PANDA YA VIKAWE/BAO BABU SEKONDARI,NI KILOMETA 9 MPAKA KWENYE VIWANJA.KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU AMA WASILIANA KWA NAMBA HII 0782122885 KWA MAZUNGUMZO ZAIDI.
KARIBUNI NYOTE.

Naibu Waziri wizara ya fedha Janet Mbene Atembelea Banda la Wizara ya Fedha Sabasaba

$
0
0
Ofisa Maendeleo ya Jamii Idara ya Kuondoa Umasikini, William Ghupi akimpa maelezo Naibu Waziri, Janet Mbene juu ya huduma anuai zinazotolewa na kitengo hicho kilichopo chini ya Wizara ya Fedha.[/caption] [caption id="attachment_34907" align="aligncenter" width="640"] Ofisa Masoko Benki ya Posta, Godbright Mlay akimpa maelezo Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo. Ofisa Mradi wa Huduma ya Popote Akounti, Catherine Ntangeki akimkabidhi Naibu Waziri, Janet Mbene kadi ya benki ya akaunti ya popote mara baada ya kufungua, katika banda la Wizara ya Fedha. Ofisa Utumishi wa GPSA, Leah Yeriko akimfisha beji yenye nembo ya taifa Naibu Waziri, Janet Mbene alipotembelea banda hilo. Naibu Waziri wa Wizara ya Fedh, Janet Mbene akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Wizara ya Fedha leo Ofisa Mawasiliano Mfuko wa PSPF, Hawa Kikeke (wa kwanza kushoto) akimpa maelezo Naibu Waziri Mbene, juu ya mafao anuai yanayotolewa na mfuko huo. Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene akiwa katika taasisi ya TIA, akipokea maelezo juu ya huduma anuai zinazotolewa na banda hilo, anaezungumza (kwanza kulia) ni Ofisa Mawasiliano wa TIA, Lilian Mpanju Ofisa Masoko Muandamizi, wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi (GEPF), James Mlowe akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri, Mbene juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo. Naibu Waziri Wizara ya Fedha, Janet Mbene akiondoka katika banda la wizara ya Fedha mara baada ya kutembelea taasisi mbalimbali zilizopo chini ya Wizara ya Fedha.

MASANJA, SHILOLE WATEMBELEA VOA NA JENGO JEUPE WASHINGTON, DC

$
0
0
Kutoka kushoto ni Mery Mgawe, Hadija Riyam, Shilole, Sunday Shomari, Dr. Hamza Mwamoyo, Ilham Dirran, Masanja na Raymond Maro katika picha ya pamoja wakati wasanii Shilole n Masanja walipotembelea studio za Voice Of America Idhaa ya Kiswahili Jijini Washington.
Msanii Shilole akifanyiwa mahojiano ya Luninga na mtangazaji wa VOA, Sunday Shomari
Msanii Masanja Mkandamizaji akifanyiwa mahojiano ya Luninga na mtangazaji Sunday Shomari.
Wasanii Shilole na Masanja wakifanyiwa mahojiano ya Radio na mtangazaji wa VOA idhaa ya Kiswahili, Sunday Shomari.
Wasanii Masanja na Shilole wakipata picha nje ya mjengo wa Voice Of America.



Msanii Masanja akipata picha nje ya jengo jeupe (white House), Ikulu ya ya Rais wa Marekani
Msanii Shilole akipata picha nje ya jengo jeupe alipokwenda yeye na Masanja kutembele mjengo huo.
Shilole na Masanja wakiwa nje ya jengo jeupe
Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na Mdau Liberatus Mwang'ombe kulia ni watoto waliokua wakipata nao picha za kumbukumbu kutoka kwa wazazi wao (hawapo pichani)
Masanja akiwa katikati ya mktaa wa Pennsylvania, mtaa ulipo jengo jeupe.
Wasanii Masnja na Shilole wakikatiza kitaa cha Pennsylvania

Hao dagaa mnaokula muwe makini nao,wengine si kwa matumizi ya binadamu.

$
0
0
 Sehemu ya Magunia ya Dagaa yakiwa yamepangwa vyema ndani ya soko hilo tayari kwa kusafirishwa sehemu mbalimbali kwa matumizi ya binadamu na mifugo.
 Dagaa 'wachafu' wakiwa wameanikwa chini kwa ajili ya kukaushwa.!Globu ya Jamii pia ilipata nafasi ya kuzugumza na mmoja wa wafanyabishara wa dagaa,kuhusiana na bei,akaeleza kuwa dagaa wazuri kwa sasa wanauzwa kati ya elfu 8 mpaka 12 kwa ndoo ya plastiki,"Lakini pia hawa walioanikwa hapa chini sisi wakazi wa Mwanza huwa hatuli,tunatengeneza maalum kwa ajili ya kuwauzia watu wenye mifugo,lakini pia kuna baadhi ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nje ya jiji la Mwanza wamekuwa wakija kuwanunua dagaa hawa "wachafu" kwa ajili ya matumizi ya chakula na kwenda kuwauza huko mikoani ikiwemo jijini dar es salaam kwa bei yao"alisema mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe hapa mtandaoni. 
 Sehemu ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza kama lionekanavyo mapema leo mchana
 Wakina mama wakijishughulisha na biashara yao ya ndizi ndani ya soko kuu la Kimataifa la Samaki-Kirumba Mwaloni jijini Mwanza
Baadhi ya Wafanyabiashara hao wakiwa bize kuwachambua Dagaa wasiofaa na wanaofaa kwa matumizi mbalimbali. 
Sehemu ya bango la soko hilo kama lionekanavyo pichani.

HAFLA YA KUWATUNUKU VYETI WAHITIMU WA KOZI YA UANDISHI WA KITAALUMA NA MBINU ZA UTAFITI.

$
0
0
 Dkt. Henrik Bregnhiy Wadhamini kutoka Denmark, akimkabidhi Cheti mmoja wa wahitimu wa mafunzo ya uandishi wa kitaaluma na mbinu za Utafiti  Thani Rashid katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Chuo Kikuu SUZA. (Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
 Kaimu Makamo Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa SUZA, Dkt. Haji M.Haji akitoa nasaha katika hafla ya kuwatunuku vyeti wahitimu wa Kozi ya uandishi wa kitaaluma na mbinu za Utafiti,ambao pia ni Wakufunzi wa Chuo cha Afya Mbweni na Chuo Kikuu cha Taifa SUZA huko katika ukumbi wa Chuo Kikuu Suza.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo Dkt. Bernard Keraita,akitoa shukurani kwa wahitimu kwa mashirikiano wakati wote wa mafunzo yao.
 

WAZIRI WA KATIBA ZANZIBAR NA MAONI YA WANANCHI KUHUSU KATIBA MPYA

$
0
0
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeendelea na msimamo wake wa kuwahahakikishia Wazanzibari kuwa itasimamia na kuyatekeleza matakwa yao watayokubaliana katika Mabaraza ya Katiba ili kupata Katiba Mpya yenye kukidhi mahitaji yao.

Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Abubakar Khamis Bakary ameyasema hayo wakati akisoma hotuba ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara yake mwaka wa fedha 2013/2014 Katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema jambo la msingi kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni kufanya maamuzi ya kujua wanataka Muungano wa aina gani na Katiba ipi ili Wananchi watakapoenda kutoa Maoni yao katika Mabaraza ya Katiba wawe na hoja za msingi.

“Kwanza ni sisi wenyewe kujua tunataka Muungano upi na Katiba ipi kasha tuwaelimishe wananchi wetu”Alisema Waziri Bakary.  Amesema Wanachi wasiwe na wasiwasi na kwamba kupitia kwa Wawakilishi wao waijadili Rasimu ya Katiba na kuona kama inakidhi haja ya kuleta Maendeleo, Maisha mazuri na haki za Wazanzibar kwa kizazi kilichopo na kijacho.

“Tuhakikishe kuwa Katiba ijayo inafufua matarajio ya Wazanzibari kwa Zanzibar yetu ya leo na siku za usoni”alisema Waziri Bakary

Aidha Waziri Bakary ameitaka jamii kufahamu kuwa Katiba inayotakiwa itabadilisha sana Taifa kisiasa, kiuchumi na kijamii na kwamba Wananchi wanatakiwa kuwa imara na mazingatio ya mabadiliko hayo.
Alieleza kuwa mabadiliko yatakayotokana na Katiba Mpya yanaweza kuwa ya karibuni na mengine kuchukua muda mrefu hivyo wananchi wajitayarishe kukabiliana nayo

Katika hatua nyingine Waziri Bakary amesema Wizara yake kupitia Idara ya Mahkama imepanga kupunguza mrundikano wa kesi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa haki.  Aidha Majengo ya Mahkama ya Unguja na Pemba yanatarajiwa kufanyiwa matengenezo ili kuyapa hadhi ya kisasa.

Katika kutekeleza majukumu yake Waziri huyo ameliomba Baraza la Wawakilishi limuidhinishe jumla ya sh. 8,188,000,000.00 kwa matumizi ya kazi za kawaida.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

AJALI YA BASI LA ABOOD HAKUNA ALIYEPOTEZA MAISHA.!

$
0
0

BASI LA ABOOD LIKITOKEA DAR ES SALAAM KUELEKEA MBEYA LAPATA AJALI ENEO LA SAO HILL MAFINGA MUDA MFUPI ULIOPITA

 BASI LA ABOOD LIKIWA LIMEPINDUKA

 ABIRIA WAKIWA WAMETOKA NJE BAADA YA AJALI KUTOKEA
HIVI NDIVYO BASI LA ABOOD LILIVYO PINDUKA 
===========  =======  =========
Basi la Abiria la Abood lililokuwa linatokea Dar es salaam kuelekea Mbeya Limepata Ajali Jioni Hii eneo la Msitu wa Sao Hill Mafinga Mkoani Iringa, Chanzo cha ajali hiyo hakija Fahamika mara moja, Na abiria wote waliokuwemo katika Basi hilo WamenusurikaPicha zote hisani ya  Blogs za Mikoa

kampeni ya upasuaji wa mtoto wa jicho yafanyika kwa siku mbili mkoani iringa

$
0
0
ZAIDI ya watu 200 wamefanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho bila malipo yoyote katika mkoa wa Iringa wakati wa kampeni ya upasuaji wa macho iliyofanyika kwa siku mbili mkoani hapa.

Wagonjwa hao wenye matatizo ya kutokuona mbali na karibu na wenye upofu walijitokeza kwa wingi katika  hospitali ya misheni ifunda na hospital ya halmashauri ya wilaya ya kilolo iliyopo ilula ili kupata huduma hiyo.


Kutokana na upofu kuwa tatizo la kidunia Shirika la Sightseves kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la kusaidia jamii la nchini Uturuki (IHH) limeendesha kampeni hiyo ya upasuaji wa macho ili kupambana na tatizo la upofu mkoani hapa.


Akizungumza na Mwandishi wakati wa kampeni hiyo Mratibu wa macho mkoa wa Iringa, Dokta George Kabona alibainisha kuwa Iringa  upofu upo kwa kiasi kikubwa ambapo zaidi ya watu 9,412 wanakabiliwa na tatizo hilo.


Kwa upande wao mmoja wa wagonjwa Martini Msasa ambaye alifanyiwa upasuaji katika hospitali teule ya Ilula alisema kuwa anawashukuru sana madaktari pamoja na mradi wa IHH kwa kuwakumbuka kwani umewafanya kuweza kuona na hivyo wataweza kwenda kufanya kazi mashambani na biashara ili kujikimu kiuchumi tofauti na mwanzo walikata tamaa na kuwa watu wa kukaa ndani na kuhudumiwa kwa kila kitu.


Huduma hiyo ya upasuaji hutolewa bila malipo yeyote na hivyo watu wenye upofu na matatizo ya macho walijitokeza kwa wingi kupima katika vituo hivyo vya afya na kupata huduma wengi wao wakiwa ni wazee.


Sambamba na hayo pia wameshauri kuwatumia wenyeviti wa mtaa kufikisha taarifa za huduma kama hiziili taarifa ziwafikie walengwa wote mara zinapojitokeza vijijini ili watu wengi waweze kujitokeza zaidi.


UNESCO YAKABIDHI WIZARA YA HABARI VITENDEA KAZI

$
0
0

 Picha no-01- Mkurugenzi wa Shirika la kimatifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Vibeke Jense katikati akimfahamisha kitu Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande mara baada ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya Idara ya Habari Maelezo, kulia Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk.Hafla hiyo ilifanyika  Wizara ya Habari Kikwajuni mjini Zanzibar.


  Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Saidi Ali Mbarouk, akimkabidhi zawadi ya mlango  Mkurugenzi Shirika la Kimataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni Vibeke Jense, huko Ofisini kwake Kikwajuni Mjini Zanzibar. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo-Zanzibar).
========  ======= ======
Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO limeikabidhi vifaa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar vyenye thamani ya Shilingi Milioni 46 ili kuijengea uwezo Wizara hio.

Vifaa hivyo ni pamoja na Kamera mbili, Lenzi mbili, Digital Recorder 7, Vipaza sauti viwili, TV moja, pamoja na Mashine 2 za kutayarishia vipindi.

Akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa UNESCO Tanzania Bi Vebeke Jense amesema lengo la kuletwa vifaa hivyo ni kuijengea uwezo Wizara hiyo ili kuleta mabadiliko hasa katika upande wa tasnia ya habari.

Baada ya Makabidhiano hayo Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amelishukuru Shirika hilo kwa kuwa karibu na Wizara yake na kuahidi Vifaa hivyo vitatumika ipasavyo ili kutimiza lengo lililokusudiwa.

Waziri Mbarouk amesema iwapo Wafanyakazi watavituza Vifaa hivyo na kuvifanyia kazi ipasavyo hapana shaka mabadikliko katika wizara hiyo yataonekana hasa ikizingatiwa kuwa ni vifaa vya kisasa.

Amesema kwa muda Mrefu Idara ya Habari Maelezo imekuwa na upungufu wa Vifaa katika kukabiliana na majuku yake ya kila siku na kwamba upatikanaji wa Vifaa hivyo itakuwa ni suluhu ya tatizo hilo.

Kwa upende wake Mkurugenzi wa Tume ya Utangazaji Omar Chande amesema itakuwa ni jambo jema iwapo Vifaa hivyo pia vitatumika katika kuandaa habari za vijijini badala ya mijini pekee.

Aidha amefahamisha kuwa baadhi ya vifaa vinatarajiwa kufika siku za karibuni ili kuiwezesha Idara ya Habari Maelezo kuwa ya kisasa na kutimiza maelengo yake.

Msaada huo wa Vifaa vyenye thamani ya Milioni 46 umekuja kufuatia ahadi iliyotolewa na Shirika la UNESCO kwa Idara ya Habari kuiwezesha kupata Vifaa ambavyo vitasaidia katika kuendeleza majukumu yake ya kila siku.

 Na Miza Othman –Maelezo Zanzibar  
IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR 

TBL YASAIDIA MIRADI YA MAJI YA SH. MIL 50 CHUO KIKUU CHA ST AUGUSTINE, SH. MIL. 49 MISUNGWI, MWANZA

$
0
0
 Meneja Mauzo wa Na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki wa kwanza (kulia), kushoto kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino, Dkt,Charles Kitima, kwa pamoja wakitaka utepe kuzindua moja ya matanki ya kuhifadhi maji,katika chuohicho.Mradi huo umetekelezwa na TBL kwa gharama y ash. Milioni 50.
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Dkt Charles Kitima kushoto akimshukuru  Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, muda mfupi baada ya kuzindua mradi wa matanki ya kihifadhi maji chuoni hapo jana.Mradi huo wa ujenzi wa mantaki hayo mawili yenye ujazo wa lita 100,000 kila kila mmoja umegharimu sh. Milioni 50.

 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Dkt Charles Kitima wa nne kutoka kushoto, Meneja Mauzo na Usambazaji wa TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki, wa nne  kutoka kulia wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi matanki mawili ya maji kwa chuo hicho.Wa pili kutoka kulia ni Askafu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza, Askofu Yuda Thadeus  Ruwa’ich.wa kwanza , kulia ni  Askofu Paul Luzoka .kulia kwa Dkt Kitima ni Padri Mwanjonde.



 Mkurugenzi wa Uhusiano na  Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,akizungumza na baadhi ya  wenyeviti  (hapo pichani) wa Vijiji vya Wilaya ya Misungwi ()muda mfupi kabla ya kukabidhi hundi ya sh.49 milioni kwa ajili ya kukarabati visima vya maji wilayani humo.Kushoto ni Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya hiyo, Nathan Mshana  na Meneja Mauzo na Usambazaji a TBL Kanda ya Ziwa, Malaki Staki.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana akizungumza na baadhi ya  wenyeviti wa vijiji  wilayani humo (hawapo pichani), muda mfupi kabla ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 49 kutoka Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)

  Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa.Malaki Staki akimkabidhi mfano wa hundi Mkurugenzi wa Ufundi wa kampuni ya Nyagama Investment Ltd  Simon Mazuka, kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa visima 20 vya maji katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi.Wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa TBL, Stephen Kilindo,wa pili ni kutoka kushoto ni Mhandisi wa Maji Wilayani Misungwi,Jumanne Kitiku.Nyuma ya Malaki ni DED wa Halmashauri ya Misungwi, Nathan Mshana na wa kwanza kushoto ni Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo,Pastory Mkaruka.
Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Ziwa Malaki Staki ,akiwa katika picha ya pamoja na wenyeviti wa baadhi ya vijiji vya wilaya ya Misungwi ambao mradi ya ukarabati wa visima utakaoanza kutekelezwa mapema mwezi huu,  baada ya Kampuni ya TBL kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 49.

UJIO WA LOWASSA LEO WATIKISA MWANZA KWA MAPOKEZI

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Baraka Kunisaga (DC. Nyamagana) akimpokea Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa (MB-Monduli) alipowasili leo uwanja wa ndege wa Mwanza.
Na Peter Fabian

MWANZA.


WAZIRIMkuu mstaafu Edward Lowassa leo amelitikisa Jiji la Mwanza baada ya mamia ya wananchi,viongozi mbalimbali na wamachinga waendesha pikipiki (Bodaboda) kujitokeza kwa wingi katika mapokezi yaliyoanzia uwanja wa ndege wa Mwanza hadi Mjini kati.


Mapokezi hayo yaliyoongozwa na viongozi wa serikali,madhehebu ya dini,wamachinga ambao ni waendesha pikipiki,wafanyabiashara na makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliweza kufunika mapokezi ya awali ya leo asubuhi ya  Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyekuwa amewasili Jijini Mwanza kwa ajili ya kufungua Kongamano na Mkutano wa wadau wa sekta ndogo ya Pamba unaofanyika jijini hapa.


Baadhi ya wananchi na wakazi wa Jiji hilo walioongozwa na viongozi wa serikali na Makada mbalimbali wa CCM na Taasisi na Madhehebu ya kidini walifurika kwa mamia kumpokea na wengi wa wananchi walikuwa pembezoni mwa barabara kuu ya kutoka uwanja wandege wakimshangilia huku msafara wake ukiwa na magari zaidi ya 90 na pikipiki zaidi ya 200 zilizopamba msafara huo.


Waziri mkuu mstaafu huyo leo  anataraji kushiriki harambee ya kuchangia kituo cha redio IQRA Fm cha jiji Mwanza ili kusaidia kuongeza usikivu wa matangazo yake na kukidhi haja za kujiendesha katika hafla itakayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest kuanzia majira ya saa 1:00 usiku kabla ya tukio hilo Lowassa atatembelea ofisi za Umoja wa Machinga wa jijini Mwanza (SHIUMA) na kisha kuzungumza nao katika ukumbi wa New Mwanza Hotel majira ya saa 4:00 asubuhi.


Mheshimiwa Lowassa katika harambee hiyo anatarajiwa kuungwa mkono na baadhi ya wabunge wenzake, makada mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi, wafanyabiashara, Taasisi na makampuni ili kufanikisha adhma na lengo lililokusudiwa kutokana na ushawishi alionao na kwa muonekano wa mapokezi yaliyofanyika uwanja wa ndege imeonyesha Mhe. Lowassa ni kipenzi cha watu na bado ananguvu ya kukubalika kwa wananchi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee ya kituo cha radio IQRA ambayo inaongozwa na taasisi ya kiislamu chini ya BAKWATA mkoa wa Mwanza Shekhe Hassan Kabete alisema maandalizi tayari yamekamilika kwa asilimia 100 yakichagizwa na kuwasili kwa mgeni rasmi Lowassa ambaye ni mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha.


“Tunayo matumaini kwamba tutatimiza lengo la kile tunachotaraji kukusanya kwenye harambee yetu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 400, ambapo tayari mfuko wetu umekwisha kusanya kiasi cha shilingi milioni 190 hivyo tunataraji lengo litafikiwa nap engine kuvukwa” alisema Shekh Kabete. NA G. SENGO

Je una ndoto za kuwa model?

$
0
0
Wanahitajika wasichana 3, warefu, mabega mapana, macho makubwa,na ngozi laini .......kwa ajili ya kupiga picha za kuwajenga wao kikazi zaidi......tafadhadhali e-mail : kamerayangu@gmail.com ,jitahidi utume picha yako kabisa na utajibiwa mara moja.

Hii ni nafasi pekee ya kupigwa picha na mpiga picha wa kimataifa .

Asanteni.

MAKETE TWASEMA KARIBU WAZIRI MKUU PINDA ILI BARABARA ZIWE SAFI.

$
0
0
 Ukarabati wa barabara ya Ipelele - Bulongwa wilayani Makete unaendelea kwa kasi kama unavyoona hali inayohusishwa na ujio wa waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ambaye anatarajiwa kuja makete Julai 8 mwaka huu, na anatarajiwa kupita kwenye barabara hii
 Kazi imepamba moto kama unavyoona mpendwa msomaji
 Baada ya greda kupita ndio iko hivi, je pakishindiliwa fresh, si ndio kama mkeka vileeeee
Hongera serikali kwa kuliona hilo na kuikarabati barabara hii ambayo inategemewa kwa kuwa ni kiunganishi kizuri cha wilaya ya Makete na mkoa jirani wa Mbeya (Picha na Edwin Moshi, Makete)

RAIS KIKWETE ATEMBELEA BANDA LA UMOJA WA MATAIFA VIWANJA VYA SABASABA.

$
0
0
   6
Rais Jakaya Kikwete akipata maelezo ya kazi mbalimbali zinazofanywa na taasisi mbalimbali za Umoja wa Mataifa nchini.
2
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu (kulia), akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kusaini kitabu cha wageni baada ya kumaliza kuzungumza na maofisa wa UN katika banda lao.
3
Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha wageni katika banda la Umoja wa Mataifa Tanzania. Kulia ni Ofisa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa Tanzania Hoyce Temu.
5
Rais Jakaya Kikwete akiangalia moja ya bidhaa za wajasiriamali wanaowezeshwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wakati alipotembelea banda la Shirika la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
10
Mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa nchini akitoa maelezo ya machapisho mbalimbali kwa kijana aliyetembelea banda hilo wakati wa maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar.
11
Ofisa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania (UN), Hoyce Temu akifafanua jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Umoja wa Mataifa kwenye maonyesho ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea jijini Dar.
12
Wananchi wakiendelea kumiminika katika banda la Umoja wa Mataifa kupata taarifa mbalimbali za shirika hilo linavyofanya kazi zake na Serikali ya Tanzania.(Picha na http://mwaibale.blogspot.com).

MZEE RUKSA AWASILI WASHINGTON DC TAYARI KWA TAMASHA LA UTAMADUNI WA KISWAHILI NA SHEREHE YA MIAKA 3 YA VIJIMAMBO

$
0
0
 Mhe. Rais Mustaafu Ali Hassani Mwinyi akishuka kwenye gari akitokea uwanja wa ndege wa kimataifa Dulles Sterling, Virginia Mhe. Mwinyi amekuja kwa ajili ya Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili na sherehe ya miaka 3 ya Blog ya Vijimambo litakalofanyika Jumamosi July 6, 2013.
 Rais Mustaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa habari Mindi Kasiga wakati alipokua akiingia Hotelini.
 Rais Mustaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Afisa Ubalozi Bwn. Mwafongo huku Kaimu Balozi Mama Lily munanka akiwatambulisha.
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV na mwanakamati wa kamati ya maandalizi ya miaka 3 y.a Vijimambo na Tamasha la Utamaduni wa Kiswahili Marekani
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Katibu wa kamati ya maandalizi, Asha Nyang'anyi.
 Juu na chini ni Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na watoto watakaompa maua.
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na katibu msaidizi Bwn. Julius Katanga, na Masanja Mkandamizaji akiwatayari kusalimiana na Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akisalimiana akisalimiana na Shilole.
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi akipokea maua toka kwa Munirah
 Rais Mustaafu, Ali Hassan Mwinyi pamoja na mkewe Sitti Mwinyi katika picha ya pamoja na Brian, na Munirah, watoto waliowapa maua.


VIWANJA VINAUZWA JIJINI MWANZA

$
0
0

Viwanja vinauzwa, Malimbe,Sweya Jijini Mwanza umbali wa Nusu Kilomita kutoka SAUT University. Vipo ziwani (ziwa Victoria) ni low Density, viwanja hivyo ni namba 95 na 96 kama vinavyoonyeshwa katika ramani hiyo.kiwanja namba 95 ukubwa wake ni 2431 sm na namba 96 ni 2766 sm square mmiliki ni mmoja na kuna miti na nyumba,bei 450 milioni.

Mawasiliano zaidi ni +255 757181351,

Madalali hawahitajiki.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images