Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 112 | 113 | (Page 114) | 115 | 116 | .... | 1897 | newer

  0 0
   Rais Obama na mkewe wakikwea pipa lao la Air Force One.
   Rais Obama na mkewe wakipunga mikono kuaga Watanzania.
   Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiaga wageni wao  Rais Kikwete, Mama Salma Kikwete, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Adam Malima (kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Balozi wa Marekani hapa nchini Mhe  Alfonso Lenhardt wakipungia kuaga wageni wao. 


   Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Barack Obama wakipokea saluti wakati nyimbo za Taifa zikipigwa wakati wa kuondoka kwa Rais huyo wa Marekani leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. Nyuma yao ni Mama Salma Kikwete na Mama Michelle Obama pamoja na Mkuu wa majeshi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na IGP Saidi Mwema . Kushoto ni  Mkuu wa Itifaki Balozi Mohamed Maharage na Mkuu wa Itifaki wa Ikulu ya Marekani (White House) Balozi Capricia Marshall. Ziara ya Rais Obama nchini imetajwa kuwa moja ya ziara za viongozi wa nje zilizofanikiwa sana, ambapo maelfu ya Watanzania walijitokeza kumlaki na kumuaga.
   Rais Barack Obama akiagana na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam huku Mstahiki Meya wa Ilala pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakisubiri zamu zao.
   Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete,leo walitembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo. 
   Picha hizi zimepigwa wakati Rais Obama na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete,leo walipotembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam na kuzindua rasmi mradi huo. Picha hizi kwa hisani ya mdau 2jiachie.

  0 0

  Its going down for the 1st time in Tanzania...with the most respected Dj's in town, pure red carpet treatment , free cocktails, prizes, a chance to take snaps, post and comment instantly, iTs ON!! on 07th -07- 2013 @ ESCAPE 1 INSTAGRAM PARTY for only 25,000/entrance on V.I.P basis with a free cocktail and 15,000/= on V.I.M.E Basis ...water plays, good music with good people...come, snap, post and comment... Contact;  +255717 070 101  Or +255-714-204490

  0 0

  Mratibu wa Tamasha la RAHA ZA JANA NA LEO Bw.Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha rasmi Tamasha hilo kwa waandishi wa habari leo jijini Dar katika hoteli ya Chichi iliyopo manispaa ya kinondoni jijini Dar.
  Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni ya Yuneda namna ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta kijitinyama.
  Baadhi ya viongozi wa bendi tofauti wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuthibitisha ni namna gani wamejiandaa naTamasha  hilo linalokutanisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania.Bendi hizo ni Mashujaa,Bantu group,Twanga pepeta,Msondo,Sikinde na king kikii"wazee sugu".
   Mwanamuziki Bichuka(Sikinde) akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma jukwaani ikiwa ndiyo waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine wanakutana jukwaa moja viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
  King Kikii(kushoto) akielezea namna alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya jumamosi hii katika viwanja vya posta .kulia ni mwanamuziki mkongwe Hamza Kalala.Milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku mnene,Watoto bureeee mpaka saa kumi na mbili,wakubwa Tsh 8,000/= tu mpaka chwee.Michezo ya watoto,nyama choma na vinywaji vyakutosha vitakuepo.

  0 0

  Jacob Steven 'JB' akijifua kwa ajili ya mpambano wake na Idd Azzan utakaofanyika katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013.
  Jb akipiga pushapu kadhaa wakati wa maandalizi hayo.
  JB akiwa tayari kumkabili Idd Azzan.
  MSANII nguli wa Filamu nchini, Jacob Steven 'JB' akifanya mazoezi ndani ya The Atriums Hotel kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wa ndondi kati yake na Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan utakaofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Julai 7 mwaka huu katika Tamasha la Usiku wa Matumaini.(Picha na Denis Mtima/GPL)

  0 0

  Rais Jakaya Kikwete akiwa na Mke wake Mama Salma Kikwete wakizungumza na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush wakati wa kikao cha wake wa Marais wa Afrika kinachofanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam.
   Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Rais Mstaafu wa Marekani Mheshimiwa George Bush muda mfupi kabla ya kuhudhuria ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais wa Afrika unaofanyika Serena hotel, leo.
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Rais Mstaafu wa Marekani  Mheshimiwa George Bush wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais na wakuu wa nchi za Afrika unafanyika Dar es Salaam kwa ufadhili wa Taasisi ya George Bush.  
  Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Marekani  Mheshimiwa George Bush na baadhi  ya wake wa marais na wakuu wa nchi za Afrika  muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kuufungua rasmi mkutano huo kwenye hoteli ya Serena.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kkulia) Mke wa Rais wa Marekani, Michelle Obama (katikati) na Mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Mama Laura Bush, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wake wa Marais barani Afrika unaofanyika kwenye hoteli ya Serena.

  ======== =========  =========

  MAMA OBAMA AMPONGEZA MAMA KIKWETE KWA KAZI KUBWA ANAYOFANYA YA KUWASAIDIA WATOTO WA KIKE

  Na Anna Nkinda - Maelezo 

  Mke  wa Rais  wa Marekani  Mama  Michelle Obama amempongeza  Mke wa Rais  Mama  Salma  Kikwete  kwa kazi  kubwa anayoifanya  ya kutoa elimu bure  kwa watoto Wa kike ambao ni yatima  na wanaoishi katika mazingira hatarishi .

  Mama Obama  alizitoa pongezi hizo leo wakati wa majadiliano baina yake na Mama Laura Bush kwenye mkutano wa   wake Wa Marais Wa afrika unafanyia katika hoteli ya Serena  jijini Dar es  Salaam.

  Mama Obama alisema kuwa wake Wa Marais wanakazi kubwa ya kuhakikisha kuwa wanawasaidia  wanawake na watoto hasa katika upatikanaji Wa elimu na mahitaji mengine muhimu.

  "Jana nilitembelea  makumbusho ya taifa, nilikutana na watoto  ambao  baadhi yao walikuwa ni wale wanaosomeshwa na Mama Kikwete , niliongea nao watoto hawa wanapatiwa bure elimu, chakula na maladhi hakika nampongeza sana kwa kazi nzuri anayoifanya", alisema Mama Obama.

  Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mama Kikwete alisema kuwa wake wa Marais waliohudhuria mkutano huo wanawawakilisha wanawake wa Afrika  ambao wanahitaji kusaidiwa katika mambo ya afya,  elimu na ujasiriamali.

  Mama  Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA)  alisema kuwa katika mkutano huo washiriki watapata nafasi ya kubadilishana ujuzi wa kazi  na kutembelea hospitali ya Kansa ya Ocen Road,kituo cha Mabinti na hospitali ya CCBRT ambako watajionea jitihada kubwa zinazofanywa na watanzania za kuisaidia jamii inayowazunguka.

  Alisema kuwa baada ya kumalizika kwa mkutano huo anaamini kuwa washiriki watarudi katika nchi zao na kuweza kukubaliana na Serikali zao pamoja na wadau Wa wengine kuwekeza zaidi kwa wanawake ili kuimarisha bara  la Afrika.

  Mkutano huo wa siku mbili   umeandaliwa na Taasisi ya Rais mstaafu wa Marekani George Bush na kuhudhuriwa na baadhi ya wake Wa Marais wa Afrika na Mke wa Waziri mkuu mstaafu Wa Uingereza Cherie Blair.

  Mada kuu ni wekeza kwa wanawake imarisha Afrika lengo l ikiwa ni kuimarisha upatikanaji wa Afya  kwa wanawake, upatikanaji Wa elimu na uchumi katika Afrika.

  0 0

   

  0 0

  scb
  Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya National Bank Of Commerce (NBC),Bi.Mizinga Melu (pichani kulia) akizungumza jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chatered,Bi.Liz Lloyd, mara baada ya Mke wa Rais wa Marekani Mama Michelle Obama kumaliza majadiliano katika mkutano wa African First Ladies Summit 2013 unaomalizika leo jijini Dar es salaam kwenye hoteli ya Serena, Mkutano huo ulidhaminiwa na taaisis ya George W. Bush Institute ya George Bush Rais mstaafu wa Marekani, katikati ni Mkuu wa Masoko, Mawasiliano/Mahusiano ya Biashara NBC,Bi.Mwinda Kiula .

  0 0


  Wind East Africa is proud to share a noteworthy development of our Singida Wind project receiving support from President Barack Obama and the White House in the "Power Africa Initiative" launched June 30th, 2013. 
  This comes through our partners Aldwych International which has committed to developing 400 MW of clean, wind power in Kenya and Tanzania – which will represent the first large-scale wind projects in each of these countries, and an associated investment of $1.1 billion. 


  This is a much-welcomed development to our project, which already enjoys the support of the Government of Tanzania, Tanesco and the World Bank.


  The Shareholders of the Singida Wind East Africa Project are Six Telecoms, Aldwych International and the International Finance Corporation [IFC] the investment arm of the World Bank.


   For further information please visit:


  0 0


  The Tanzanian International Bongoflava Artist has signed a licensing deal with one of the world biggest and top Music labels "Universal Music, South Africa". His content will be distributed through the Kleek, a mobile streaming service available on all Samsung smart phone in Ghana, Angola, Kenya, South Africa and Nigeria. CPwaa is one of the A-List Artists signed by Universal Music from East Africa for its Kleek continental platform.

  On March 13, 2013 Universal Music Group, in partnership with Samsung, as well as African and international music labels and publishers, has launched a pan-African mobile music streaming service called the Kleek.  Designed and built specifically for Africa, the Kleek will bring music lovers closer to their favorite artists, while also providing artists with valuable access to a wider pan-African audience.

  This new deal will make CPwaa not only to gain more revenues from his music but also a worldwide exposure and global outreach through the Kleek.


  0 0


  0 0

   Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  KILA mtu anajua kuwa sheria na haki ni vitu viwili tofauti. Usilazimishe kupata haki, kwasababu sheria imeonyesha juu ya madai yako. Kufanya hivyo ni kujipotezea muda wako unaoweza kuutumia katika kazi nyingine za maendeleo yako.
   
  Pamoja n ayote hayo, lakini wakati mwingine si sahihi kujificha kwenye mhimili wa kisheria kwa kufanya mambo ambayo ni tofauti katika jamii. Kila mmoja anapaswa kuishi kwa upendo bila kuweka u-mimi, vyama vyetu na mengineyo pia.
   
  Nasema haya baada ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu kama ‘Sugu’kutoka (CHADEMA)kuachiwa huru na Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, kwa madai kuwa hati ya mashitaka ina mapungufu kisheria.
   
  Sugu alipandishwa kizimbani katika mahakama hiyo, mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa wa Dodoma, Elinaza Luvanda na kusomewa shitaka linalomkabili kuhusu kutoa lugha ya matusi katika mtandao wa kijamii, moja ya vitu vinavyotumiwa vibaya na watu wengi.
   
  Katika mitandao hiyo, kila mmoja anaandika kile anachojisikia, bila kujali faida au hasara inayopatikana kwa kuandika upupu wake.
  Sugu aliandika hivi;”Tanzania haijawahi kupata Waziri Mkuu mpumbavu kama Pinda”.
   
  Kauli hii ilisababisha maswali mengi kwa Watanzania, hasa wakiamini kuwa imetokana na matamshi ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwataka watu wapigwe watakapokaidi amri halali za jeshi la Polisi. Bila kuangalia sheria inasemaje juu ya sakata hilo, lakini kiubinadamu, Sugu hakupaswa kuandika maneno ya matusi dhidi ya Pinda.
   
  Nasema hivi kwasababu Sugu kama mbunge wa Tanzania, alikuwa na nafasi kubwa ya kukataa agizo la mtu yoyote, kwa kutangaza bungeni. Angeweza hata kushawishi kutokuwa na imani na Pinda, kama wabunge wengi walivyowahi kufanya. Lakini Sugu alifanya haya kihuni tu. Akiamini kuwa mihemko ya kisiasa au sheria zitambeba.
   
  Mambo kama haya yanasababisha kutokuelewana katika jamii. Leo hii kama sheria hazitamki wazi juu ya kosa hilo, basi yoyote anaweza kufanya anavyojisikia bila kuogopa chochote.
   
  Je, mwingine ajitokeze mchana kweupe, kuandika au kusema kiongozi mfano wa Pinda ni mpumbavu? Je, serikali hii inaongozwa na wapumbavu? Je,Msajili wa Vyama vya siasa, John Tendwa naye ni mpumbavu?  Kiubinamu ukilizungumzia neno upumbavu, hasa kwa viongozi wetu ni jambo la kutia kichefu chefu.
   
  Sugu angeyasema hayo kwa watu anaofanana nao, iwe kicheo au kiumri. Umri wa Sugu na Pinda haufanani kamwe. Hivyo kuusema upumbavu wa Pinda hadharani ni kumvunjia heshima kupita kiasi. Tuukatae hadharani.
  Mtindo huu ukidhihiri hauwezi kudumisha utu na uungwana wetu. Siku zote uungwana ni vitendo.
   
  Angalia, mwendesha mashitaka ambaye ni Wakili wa Serikali, Harieti Lopa  alidai mtuhumiwa alitenda kosa la kutoa lugha ya matusi kwa Waziri Mkuu, Pinda Juni 24, mwaka huu eneo la Manispaa ya Dodoma.
   
  Alifika mbali zaidi kwa kudai mshitakiwa huyo, ambaye ni Sugu aliandika ujumbe huo bila kuutaja, ambao unaleta uvunjifu wa amani kwa Waziri Mkuu, hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa Sheria kifungu kidogo namba 89 (a).
   
  Sakata hili wakati linaendelea kuchambuliwa kwa mujibu wa sheria zetu, mshitakiwa alikana shitaka ndipo Wakili wa Serikali kuiomba mahakama itaje tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo.
   
  Hata hivyo, Sugu alitetewa na mwanasheria wake, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, alikataa kesi hiyo kupangiwa siku nyingine, akisema hati ya mashitaka ni mbovu na haikukidhi matakwa ya sheria ya jinai.
   
  Lissu anasema “Hati ya mashitaka,  inatuhumu kosa ni kutumia lugha ya matusi kifungu cha 89 (i) kifungu kidogo (a) katika Sheria zetu ambapo matusi yenyewe hayajatajwa, bali yanatolewa maelezo ya kosa kuwa lugha ya matusi ambayo inaweza kuvunja uvunjifu wa amani kwa Pinda, hiyo lugha ya matusi ni ipi,” Lissu alihoji.
   
  Lissu alifika mbali zaidi kwa kusema kuwa upungufu mwingine wa kisheria ni hati ya mashitaka ipo kimya, hivyo kushangaa mshitakiwa atajitetea kwa lipi na ataandaa utetezi namna gani, wakati anachodaiwa kukiweka mtandaoni kikiwa hakijasemwa?
   
  Maneno ya mwanasheria huyu yalipatiwa ufumbuzi na hakimu kujiridhisha kisheria na kukiri kuwa ni kweli  hati hiyo ina upungufu wa kisheria kwa mujibu wa kifugungu cha Sheria Namba 132 sura ya 20 na hivyo kuifutilia mbali  hati hiyo ya mashitaka ikiwa ni pamoja na kumuachia huru Mbunge huyo.
   
  Pamoja n ayote hayo, si malalamiko yangu kuachiwa kwa Sugu, ila namna watu watakavyoweza kutumia udhaifu huo kuwatendea wengine.
   
  Kila mtu anaweza kufanya kama alivyotenda Sugu, dhidi ya mwingine. Nani anaweza kukamatwa leo akiandika kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willbroad Slaa ni mpumbavu kwasababu ameacha upadre na kuhamia kwenye siasa, tena Chadema?
   
  Ni kutokana na hilo, nadhani kuna haja sasa wanasiasa wetu, akiwamo Sugu kuona kuwa siasa haziwezi kumfanya ajipachike uwendawazimu.
  Lazima ajuwe kuwa heshima ni kitu ch abure, hivyo aihusudu ili afike mbali zaidi katika harakati zake.
   
  Sina chuki dhidi ya wanasiasa hawa.Kila mtu anataka mabadiliko ya kisiasa na kiutawala, ila si kwa njia ya uvunjifu wa amani.
  Kwa sasa wapo watu ambao hawataelewa uvunjifu wa amani utatokea wapi juu ya sakata la Sugu na Pinda.
   
  Lakini Pinda kama Waziri Mkuu pia ni kiongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), chini ya Mwenyekiti wake Jakaya Mrisho Kikwete.
  Ukiacha uongozi wake katika chama na serikali, anabaki kama binadamu wa kawaida mwenye ndugu au marafiki.
   
  Hivyo basi, katika sakata hili, kuna siku baadhi yao watashindwa kukubali utu wa mtu unavyotolewa kwa ajili ya siasa za maji taka. Hao watagoma kusubiri. Watataka kulipiza kisasi, hivyo kuashiria kuwa usalama utakuwa kwenye mashaka makubwa. Haya si ya kukubali yaendelee kufanyika katika Taifa hili linalokabiriwa na sekeseke la siasa.
   
  Tusikubali kabisa, hivyo Sugu kama Mbunge alipaswa kujiheshimu na kuheshimu wengine, akiamini kuwa chochote atakachosema kitaonekana.
  Mitandao ina nguvu kubwa mno. Watu wengi sasa wamekuwa humo. Ndio maana maandishi machache aliyosema, lakini yameibua mzozo hadi kufikishwa polisi.
   
  Kuukosoa uamuzi wa mahakama juu ya kutukanwa kwa Pinda, hakuendi sambamba na kuwalimisha kumfikisha tena Sugu mahakamani, ila kumfanya ajuwe anapaswa kujichunga na anachokisema.
   
  Hati ya mashtaka kama ina makosa, mapungufu, inaweza kuwekwa sawa, lakini hatua hiyo itaendeleza kujenga uhasama kati ya viongozi hawa.
  Suala hili la Pinda juu ya amri yake kwa polisi ni tatizo, ila hakumfanyi atukanwe kama mtoto.
   
  Ndio maana alipotoa tamko hilo wanaharakati walilipinga, ila si kwa njia ya kumvunjia heshima kama alivyofanya Mbunge Sugu.
  Nadhani tunawajibu wa kuishi kwa upendo na kuheshimiana, ukizingatia kuwa kutaleta maendeleo ya kweli.
   
  Tusitumie udhaaifu wa mapungufu kaatika sheria zetu kuwakandamiza wenzetu, maana leo kwa Pinda kesho Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Hai, Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Haluna Lipumba, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na viongozi wengine.
  0712 053949

  0 0


  MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umempongeza Rais wa Marekani,   
  Barack Obama na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete kutambua mchango wa  
  wasanii, wachezaji wa mpira hasa pale walipocheza ngoma na mpira wa  
  miguu na mpira wa kikapu.

  Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Caasim Taalib
  alisema jana kuwa kitendo cha Rais Obama na mwenyeji wake Rais Kikwete
  kucheza ngoma za asili alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa
  wa Mwalimu Nyerere (DIA) imeonesha namna ambavyo wanaguswa na
  utamaduni wa mtanzania.

  Alisema pia kuwa hatua ya Rais Obama kutambua mchango wa mtanzania,
  Hasheem Thabit anayecheza mpira wa kikapu ligi ya NBA nchini Marekani
  kunaimanish anatambua Tanzania ilivyojaliwa na vipaji ndiyo maana
  mchezaji huyo amekuwa nyota kati ya waliosajiliwa kuchezea timu za
  ligi hiyo.

  Taalib alisema ni faraja kubwa kuona Rais Obama kuonesha ufundi wake
  kumiliki mpira kwa kichwa na kumpasia Rais Kikwete alipotembelea
  mitambo ya kufua umeme ya Symbion ambayo ni mshirika wa Klabu ya
  Sunderland.

  ‘SHIWATA baada ya kujua mchango wa Rais Obama iliahirisha Tamasha la
  Mastaa Chipukizi lililokuwa lifanyike Jumamosi Juni 29 kijiji cha
  wasanii Mwanzega Mkuranga ili kutoa nafasi kwa  wasanii na viongozi
  mbalimbali kushiriki kikamilifu katika maandalizi na mapokezi ya  Rais
  Obama’

  SHIWATA ambayo inaundwa na wasanii, wanamichezo, wanahabari na vijana  wapatao 7,000 iliahirisha tamasha hilo na sasa litafanyika Agosti


  mwaka huu ambapo itakabidhi nyumba kwa mchezaji wa zamani wa Timu ya    
  Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Jellah Mtagwa na wasanii wengine 14
  ambao wamekamilisha michango ya ujenzi  wa nyumba zao katika kijiji
  chao cha Mwanzega Kimbili, Mkuranga.

  Wengine watakaokabidhiwa nyumba zao ni msanii maarufu nchini, Lumole
  Matovola ‘Big’ wa Bongo movie ambaye ni mwanachama wa SHIWATA wangine    
  ni Mwandishi wa Habari, Josephine Moshi, Farida Ndimbo wa Jeshi la  
  Magereza, Flora Kafwembe wa JKT Mgulani na Nyanza Kisadugwa wa Jeshi 
  la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

   Mpaka sasa SHIWATA imejenga nyumba 24 kwa ajili ya wasanii katika
  eneo la hekari 300 na wanajiandaa kulima shamba la hekari 500
  walizonazo ili kujikwamua kimaisha.

  0 0

   Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa  Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo.
   Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.
  Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD), Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.

  0 0

  Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza wakitazama moja ya filamu iliyokuwa ikioneshwa jana usiku kwenye viwanja vya Nyamagana,ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Filamu ya wazi lililojulikana kwa jina la  ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’.Tamasha hilo lilizinduliwa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya na kusababisha shangwe tupu kwa wote waliokuwepo ndani ya uwanja huo.
   Katika uzinduzi wa tamasha hilo,kuna burudani mbalimbali zikitolewa ikiwemo na wakazi wa Mwanza wenye vipaji vya kucheza na kuimba,walipewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao kama ionekanavyo pichani,ambapo mwisho wa mashindano hayo kuna atakaeibuka na kitita cha shilingi laki mbili.
   Baadhi ya Wakazi wa jiji la Mwanza waliojitokeza jana kushuhudia muenedelezo wa tamasha la filamu,lijulikanalo kama   ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ kwenye uwanja wa Nyamagana

  =========  ========  ========

  KWA sasa Jiji la Mwanza mambo ni tofauti kabisa pale inapofika saa 10 jioni, wakati kunapokuwa na burudani za kila aina katika Tamasha la Wazi la Filamu Tanzania, maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ ambalo linafanyika katika Uwanja wa Nyamagana.

  Wakazi wa Mwanza wamejikuta wakishuhudia kitu kingine kabisa, huku kukiwa na burudani za kila aina pamoja na maonyesho ya filamu yanayofanyika mpaka saa 5 usiku, ambapo mamia ya watu wanahudhuria.
  Kama kuna sehemu walipagawa zaidi ni pale tamasha hilo lilipozinduliwa mwishoni mwa wiki, uzinduzi ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya na kusababisha shangwe tupu kwa wote waliokuwepo ndani ya uwanja huo.
  Tamasha hilo maarufu kama ‘Grand Malt Tanzania Open Film Festival’ lilinogeshwa zaidi na burudani kali kutoka kwa bendi ya Extra Bongo, waliokuwa wakiongozwa na Ally Choki.
  Wakati wa uzinduzi huo, wasanii waliokuwepo uwanjani hapo wakiongozwa na Hashima Kambi, walijikuta wakizongwa kwa muda wote, huku mashabiki wakitaka kuwashika au kupiga nao picha.
  Aunty Ezekil, Irene Uwoya, Jacqueline Wolper, Vicent Kigosi ‘Ray’ na Jacob Steven ‘JB’ walijikuta wakishangiliwa muda wote kama ilivyokuwa kwa Hashim Kambi, Isa Musa ‘Cloud’ na Steve Nyerere.

  Lakini wasanii hao wakati wa uzinduzi walionekana ‘kupelekeshwa’ zaidi na Steve Nyerere ambaye aliwaita mmoja mmoja kusalimia mashabiki, huku akiwataka wacheze sebene lililokuwa likiporomoshwa na Extra Bongo.
  Irene Uwoya alizusha shangwe zaidi pale alipoomba shabiki yoyote a kiume ajitokeze jukwaani na kucheza naye sebene, hali iliyozusha tafrani kwa mashabiki wengi waliokuwa wakigombania kwenda kucheza naye, kabla ya mmoja wao kutumia njia za mkato hadi kumfikia.
  JB alionyesha unene si kitu, kwa sebene alilokuwa akicheza, huku Ray naye akishangiliwa zaidi kwa jinsi alivyozirudi ngoma za Extra Bongo na wengi kubaki kujiuliza amejifunza wapi kucheza kama madansa wanavyofanya.
  Hali ilikuwa hivyo kwa Jacqueline Wolper ambaye naye alitaka wa kucheza naye, huku Shamsa Ford akionekana wamo katika mambo makali ya muziki kama ilivyokuwa kwa Hashim Kambi.
  Lakini kubwa zaidi ni kwa Mkuu wa Wilaya ya Busega, Paul Mzindakaya, aliyesema amefurahishwa mno na tamasha hilo na hasa watu waliokuwa wamejitokeza kwa wingi kushuhudia wasanii wao.
  “Hii kali, kusema kweli Serikali itaendelea kuthamini kwa kiasi kikubwa wasanii wetu na huu ni wakati wa wasanii wa Mwanza kujifunza kutoka kwa mastaa wetu hawa,” alisema na kuzusha shange kubwa kutoka kwa mashabiki aliokuwepo hapo.
  Meneja wa kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam alisema, kile alichokiona Mwanza hakukitegemea na anaamini kwa dhati kabisa kujitokeza kwao kudhamini tamasha hilo ni njia mojawapo ya kuwaendeleza wasanii hapa nchini.
  “Pia tunapenda kuwashauri muendelee kutumia kinywaji cha Grand Malt ambacho hakina kilevi, badala ya kumpa mtoto vinywaji ambavyo manufaa unaweza pia kumfungashia kinywaji hiki katika matumizi yake,” alisema.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wasanii hao walisema tamasha hilo limewafungua macho na wamejiona wana deni kubwa kwa Watanzania hususani mashabiki wa Kanda ya Ziwa ambao wamewapokea kwa furaha kubwa.
  “Nimefurahishwa mno na hiki kitu, kusema kweli Mwanza tutaendelea kupakumbuka na ni wakati kwetu wa kujifunza mengi na kuthamini Watanzania wenzetu,” alisema JB.
  Jacqueliene Wolper alisema ile kupokelewa kwa shangwe tu, kwake ni changamoto kubwa na hawezi kusahau tamasha hili na hasa kinywaji cha Grand Malt kwa kuwawezesha kuwafikia kwa karibu zaidi.
  Irene Uwoya alienda mbali zaidi na kusema, kila akiona mashabiki walivyokuwa wakiwashangilia, ameamini kwa dhati kuna kitu ambacho wanatakiwa kukifanya kwa ajili yao.
  “Hili ni deni kubwa sana, umati wa atu kama huu wanakuunga mkono ni kitu cha kujivunia na si kulewa sifa. Tunatakiwa kufanya makubwa zaidi kwa ajili yao ili wasione kama tumewatenga,” alisema.
  Mratibu wa Tamasha hilo, Musa Kissoky, alisema mpaka sasa wanaamini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa tamasha hilo kufanyika Mwanza, huku akisema pia limewapa funzo kwa mambo mbalimbali.
  Kissoky alisema, tamasha hilo ambalo ni la bure kwa watu wote na kushirikisha mastaa wa filamu hapa nchini, litaendelea kuwa la aina yake kutokana na vitu vingi vinavyofanyika kila siku ya tamasha.
  “Tunawashukuru mno Grand Malt kwa kutuwezesha kufika hapa tulipo, kusema kweli wamefanya mambo makubwa zaidi ambayo kwetu sisi ni faraja na tutaendelea kukithamini kinywaji chao,” alisema.
  Naye Meneja wa kinywaji cha Grand Malt walio wadhamini wakuu wa tamasha hilo, Consolata Adam, alisema wameamua kufanya kweli zaidi kwani wanataka kuona Watanzania wanapata kitu chenye uhakika.


  “Kusema kweli hata sisi tumefarijika mno. Tunawakaribisha watu wote wenye mapenzi na filamu zetu za Tanzania kufika na kushuhudia tamasha hili ambalo mwaka huu limeboreshwa zaidi,” alisema Consolata.

  Meneja Habari na Mawasiliano wa TBL, Edith Mushi, alisema, kutokana na ubora wa kinywaji cha Grand Malt hata tamasha hilo litaendelea kuwa la aina yake na litakaloiteka mikoa yote ya Kanda ya Ziwa.

  “Tumeona jinsi wananchi wanavyozipenda filamu za Tanzania, maarufu kama ‘Bongo Movies’ na jinsi walivyo na kiu ya kuwaona wasanii wa filamu ana kwa ana, sasa kazi kwao kuwashuhudia na kuona tamasha bora zaidi,” alisema.

  Tamasha la Filamu la Grand Malt lilianza rasmi mwishoni mwa wiki na litakuwa la siku saba, huku kukiwa na filamu mbalimbali zitakazooneshwa katika kipindi hicho. Filamu zote hizo ni kutoka Tanzania.
  Tamasha hilo la filamu limedhaminiwa na kinywaji cha Grand Malt kisicho na kilevi ambacho kinazalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

  0 0


  Hayo yamebainika katika kikao cha wadau wa asasai za kupambana na ukimwi kilichofanyika katika ukumbi wa community center uliopo katika manispaa ya Iringa . Akizungumza Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa GEREVAS NDAKI (pichani juu) amesema kuwa asasi zinazopambana na masuala ya ukimwi zinapaswa kushirikiana ili kuweza kutokomeza kabisa suala hilo kwani ni moja ya chanzo cha maambukizi ya virusi vya ukimwi.


   Mratibu maendeleo ya jamii manispaa GASPAR  NSANYE amethibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo na kusema kuwa baadhi yao wanaishi maeneo ya kihesa,katika manispaa ya Iringa huku baadhi wakiwa ni raia wa Mombasa nchini Kenya na wengine ni wazaliwa wa iringa.


  Kwa upande mwingine Asasi zinazojishugulisha na masuala ya kupambana na kupunguza  kasi ya  maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi, wameombwa kuwajibika ipasavyo katika shuguli zinazowahusu ili kuweza kufikia malengo waliyokusudia.


  Wakati huo huo wahusika wanaoendesha kampeni za tohara wametakiwa kuangalia upya ujumbe wao unaosema kufanyiwa tohara kutapunguza kwa asilimia 60 za maambukizi ya virusi vya ukimwi kwani kauli hiyo bado imekuwa changamoto kwa vijana juu ya matumizi ya kinga.


  Wakichangia wadau mbalimbali katika kikao hicho wamewataka mamlaka inayohusika na usambazaji wa kondomu kuliangalia kwa undani suala zima la upatikanaji wa kondomu za kike kwani zimekuwa zikipatikana kwa shida na kwa garama kubwa tofauti na condom za kiume.


  Aidha wamewaomba wananchi kutokukata tama katika suala la kupambana na gonjwa la ukimwi na kuona halina mafanikio yoyote katika suala la tiba kwani limekuwa la muda mrefu sasa ,cha msingi ni kutoa ushirikiano kwa serikali na wadau wote wanaojishugulisha na suala la kupambana maambukizi ya virusi vya ukimwi katika kutokomeza suala hilo.  0 0

    Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili kushoto ni mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tz Albert Makoye
      Mkuu wa itifaki wa kamati ya Miss Tz Albert Makoye akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam juu ya shindano la Redd’s kanda ya temeke linalotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa TCC Club Chang,ombe ijumaa ya juma hili ,kati ni  .Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Temeke Beny Kisaka pamja na msanii mahiri wa bongofleva Ben Paul.

  ======== ======== =======
  MREMBO atakayetwaa taji la Redds Miss Temeke 2013, linalofanyika Ijumaa Julai 5, mwaka huu ataondoka na zawadi za jumla ya Sh. Milioni 3,250,000 ikiwa ni zawadi kubwa zaidi kutolewa katika mashindano yote ya urembo, yaliyofanyika mwaka huu.
  Mshindi huyo, atapata ofa ya mwaka mzima kutoka RIO gym & Spa, iliyopo Quality Center, kutumia vifaa vyote ndani ya gym hiyo ambayo gharama yake ni Milioni 1,400,000, pia atajinyakulia simu ya kiganjani yenye thamani ya Sh 700,000 , dinner set kutoka AKO Catering yenye thamani ya Sh,150,000 sanjari na pesa taslim Sh. Milioni 1, hiyo jumla yake ni Milioni 3,250,000.
  Mshindi wa pili katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi atakuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abas Mtemvu atajinyakulia kitita cha Sh.800,000 pesa taslim na dinner set ambayo thamani yake ilikuwa bado haijathibitishwa na mdhamni wa zawadi hiyo wakati mshindi wa tatu ambao wote kwa pamoja ni wawakilishi wa Miss Temeke, yeye atajipatia fedha taslimu Sh 700,000.
  Sh , 400,000 zitakwenda kwa mshindi wa nne na atakayeshika nafasi ya tano yeye ataibuka na Sh 300,000. Washiriki wengine ambao hawatabahatika kuingia katika nafasi ya tano bora, wote watapewa Sh,200,000 kwa maana ya kifuta jasho. Tumelenga zawadi za fedha zaidi, hii ni kutokana na ugumu wa maandalizi kwa warembo ambao hugharamika zaidi, kiasi nasi kuona kuna kila namna ya kuwapunguzia maamivu hayo.
  Shindano hilo, linatarajiwa kuwa na burudani ya kipekee kutoka kwa mshindi wa tungo bora ya Bongo Fleva ya Kili Music mwaka huu, Ben Paul sanjari na Twanga Pepeta ambayo mwishoni mwa wiki, ilizindua albamu yake ya 13 kwa mafanikio makubwa.
  Warembo watakaopanda jukwaani Julai 5 ni kutoka Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambao wanawania taji linaloshikiliwa na Miss Tanzania namba tatu, Edda Sylvester walikuwa chini ya wakufunzi Suzy Mwenda na Shadya Mohamed wakati kwenye kucheza nako walikuwa na walimu wawili Super Bokilo na Charles.
  Warembo hao ni pamoja na Axsaritha Vedastus, Darling Mmary, Esther Muswa,  Hyness Oscar, Irene Rajab, Jamila Thomas, Latifa Mohamed, Margreth Gerald, Margreth Olotu, Mey Karume, Mutesi George, Naima Ramadhan, Narietha Boniface , Stella Mngazija na Svtlona Nyameyo .                                                                 
  Shindano hilo limedhaminiwa na kinywaji cha Redd's, Dodoma Wine, Gazeti la Jambo Leo, Cloud’s Media, Blogu ya Wananchi (Le Mutuz), Fredito Entertainment, CXC Africa tours & Safaris, RIO Gym & Spa, 100.5 Times FM na Kitwe General Traders. Mbali ya wadhamini hao pia Redds Miss Temeke imechangiwa katika ufanikishaji na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu na mwanamichezo maarufu nchini Geofrey Nyange Kaburu hasa kwa upande wa zawadi.
  Temeke, imewahi kutoa warembo kadhaa miaka ya nyuma waliopata mafanikio katika mashindano hayo, mitindo na kazi nyingine hasa kupata uzoefu wa kujiamini katika njanja mbalimbali. Miongoni mwao ni Miriam Odemba(1997) aliyepata kuiwakilisha Tanzani katika fainali za mitindo zilizofanyika Nice Ufaransa na kupata mkataba wa Elite Model Look, baadaye kufakinikiwa kutwaa nafasi ya pili ya Miss Earth World, zilizofanyika China.
  Pia, Temeke ilimtoa Happines Millen Magesse(2001), na kutwaa taji la Miss Tanzania na kwa sasa anang'ara sana katika tasnia ya mitindo katika nchi za Marekani, Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla. 2003 Temeke ilimtoa Miss Tanzania, Sylvia Bahame na 2006 kuwatoa Jokate Mwegelo na Irene Uwoya.
  Jokate alitwaa taji la Miss Temeke mwaka huu na pia kushika nafasi ya pili Miss Tanzania na pia kushinda taji la ubalozi wa Redd's na gazeti la Citizen. Uwoya ambaye alikuwa mshindi wa pili Temeke alishika nafasi ya nne kwenye Miss Tanzania mwaka huo. Genevieve Mpangala mwaka 2010 alitwaa taji la Miss Temeke baadaye kushinda taji la Miss Tanzania.
  Nafasi nyingine za juu zilizowahi kutwaliwa na warembo kutoka Temeke ni pamoja na Irene Kiwia, mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2000, Regina Mosha mshindi wa nne Miss Tanzania mwaka 2002, Cecylia Assey mshindi wa pili Miss Tanzania 2004, Queen David mshindi wa tatu mwaka 2007 na Edda Sylvester mshindi wa tatu Miss Tanzania akiwa anashikilia taji la Redds Miss Temeke.
  BMP Promotions inayoandaa mashindano haya kwa mwaka wa 18 sasa, inatanguliza shukrani zake wadhamini wetu kwa miaka hiyo, sanjari na vyombo vyote vya habari kwa ujumla wake, kwani ndio waliofanikisha kuandaa Miss Temeke kwa ufanisi katika muda wote huo, shukrani sana.
   
  Benny Kisaka
  Mkurugenzi BMP Promotions

  0 0

   Mtafiti wa Mbegu,Geremiah Mrimi  (wa pili kushoto) akimuonesha Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi mbegu aina ya Shayiri zilizokubaliwa na Wizara ya Kilimo, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa Shayiri, wilayani Karatu, Arusha mwishoni mwa wiki. Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia  Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
  Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.
   Mtaalamu wa Kilimo cha Shayiri, Joel Msechu (kulia) akitoa maelezo juu ya mbegu za Shayiri kwa Meneja wa Kiwanda cha Kimea cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Moshi, Vitus Mhusi (katikati) na Mhasibu wa Mashamba, Optaty Minja.Wakulima wa zao hilo wana mkataba wa kuiuzia TBL, shayiri kwa ajili ya kutengenezea bia.


   Anatoly Lohay,mkulima wa Rhotia kati Karatu.

  Editha Temu,Afisa Ughani kiwanda cha TBL akielezea umuhimu wa zao hilo

  0 0

  IMG_8738
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiangalia baadhi ya bidhaa zenye ubora zinazouzwa na Kampuni ya HSC katika maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara katika viwanja vya Sabasaba jijini Dar. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
  IMG_8748
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia kifaa cha kusafishia mazulia jinsi kinavyofanya kazi. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed.
  IMG_8743
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed na baadhi ya wafanyakazi wa HSC katika Banda lao lililopo kwenye viwanja vya Sabasaba.
  IMG_8744
  Umati wa wakazi wa jijini Dar es Salaam ukiwa umefurika kwenye Banda la Home Shopping Centre kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani.
  IMG_8808
  Mtsahiki Meya Jerry Silaa akipewa maelezo ya jinsi Mfuko wa Fursa sawa kwa wote unavyopambana na kutokomeza Ugonjwa wa Saratani ya Matiti kwa wakina mama nchini. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa.
  IMG_8797
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal walipokutana kwenye Banda la Mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) kwenye viwanja vya maonyesho ya Kimataifa ya Biashara jijini Dar.
  IMG_8830
  Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa akiagana na Mstahiki Meya Jerry Silaa mara baada ya kutembelea Banda la (EOTF) linalotoa fursa kwa wajasiriamali nchini Tanzania kuonyesha bidhaa zao katika maonyesho hayo kila mwaka.
  IMG_8558
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akipata maelezo jinsi ya kutumia Kizimamoto Fanisi cha kurusha (Fire Extinguisher) ambacho ni rahisi kutumia na hakihitaji matengenezo na hudumu kwa miaka mitano pia Kifaa hicho ni rafiki wa mazingira na mvumbuzi bora kwa uokoaji wa dharura wakati alipotembelea Banda la GreenBat Fire Solutions katika maonyesho ya Sabasaba yanayoendelea.
  IMG_8574
  Mstahiki Meya Jerry Silaa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa GreenBat Fire Solutions.
  IMG_8542
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni katika banda la Arusha International Conference Centre (AICC) wanaoshughulika kutoa huduma za kumbi za Kimataifa za mikutano na Utalii jijini Arusha.
  IMG_8531
  Mstahiki Meya Jerry Silaa akingalia jinsi mtoto Range Jackson ( wa pili kushoto) mwenye ulemavu wa Ubongo akionyesha ramani ya Tanzania na Sehemu ya mipaka yake iliyotumika kumfundishia kujua kusoma na kuandika na ufundi stadi kupitia kituo cha VETA. Kulia ni Mkufunzi wa kuchomea (Welding Instructor) na Mwalimu wa watu wenye mahitaji maalum Bw. Kintu Kilanga na Wa tatu kulia ni Baba mzazi wa kijana huyo Bw.Jackson Range.
  IMG_8364
  Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika viwanja vya maonyesho ya 37 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea jijini Dar ambapo alitembelea mabanda mbalimbali.(Picha na Zainul Mzige).
  IMG_8735
  Mkurugenzi Mtendaji wa Home Shopping Centre (HSC) Fahad Said Mohamed (kushoto) akimkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kwenye Banda la HSC kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

  0 0

   Kwa mbali utawaona wananchi wakiangalia ujenzi wa tanki la kuhifadhia maji linalojengwa katika shule ya msingi Maulu kata ya Kipagalo wilayani Makete, kutokana na shule hiyo kukumbwa na uhaba wa maji hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea wanafunzi kupata tabu ya kujisaidia kutokana na vyoo kutumia maji. Ujenzi huo umefadhiliwa na AMREF
   Hapa mafundi wakiwa kazini kama uonavyo
   bado kidogo tuu ujenzi huo utakamilika
  Jamaa hasubiri apikiwe, hapa aliamua kuingia jikoni mwenyewe kujipikia ugali kwa ajili yake na mafundi wenzake wanaojenga tanki hilo(Picha zote na mdau Edwin Moshi)

  0 0

  IMG_8550Rais Jakaya Kikwete (aliyenyoosha mkono) akitembelea  Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam.kushoto kwake ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk. Abdallah Kigoda. 
  IMG_8637 IMG_8571Rais   Jakaya   Kikwete  akipata maelezo kutoka kwa n Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo  na Makazi(UNHABITANT) Phillemon  Mutashubirwa  kuhusu wanavyofanya kazi ya kusaidia watoto wa shule  na  wanawake kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam.
   IMG_8636Rais Jakaya  Kikwete (kulia)  akiangalia  mafuta ya ubuyu  na bidhaa zingine kwenye banda la  Mfuko wa Fursa Sawa Kwa wote(EOTF) kwenye Maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa  yanayoendelea katika viwanja  vya  Mwalimu  J. K Nyerere  jijini  Dares Salaam .Kutoka (kushoto)  wa pili ni Mwenyekiti wa EOTF Mama Anna Mkapa  (kushoto) ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Stephen Emmanuel. 

older | 1 | .... | 112 | 113 | (Page 114) | 115 | 116 | .... | 1897 | newer