Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 117 | 118 | (Page 119) | 120 | 121 | .... | 1903 | newer

  0 0


   Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiwahutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matamba wilayani Makete
  Wakazi wa Matamba Wilayani Makete wakimsikiliza Waziri Mkuu Pinda  alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara.

  Serikali imesema itahakikisha hivi karibuni barabara ya Chimala – Matamba itapandishwa hadhi kutoka halmashauri ya wilaya ya Makete na kuwa ya mkoa kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Makete ina mzigo mkubwa wa kuihudumia barabara hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa wanamatamba.

  Hayo yamesemwa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matamba wilayani Makete

  Waziri Pinda amesema amepita kwenye barabara hiyo ambayo ina mlima na kona kali zipatazo 57 na kujionea hali halisi ambapo amesema barabara hiyo inatakiwa kufanyiwa matengenezo makubwa ambapo kwa uwezo wa halmashauri itakuwa na mzigo mkubwa wa kuihudumia barabara hiyo

  “kwa kweli halmashauri ya makete itakuwa inapepesa tu kuihudumia biashara hiyo, inahitaji matengenezo makubwa ikiwemo kuibomoa miamba na milima, hivyo nikirudi wizarani nakwenda kumuandikia barua Magufuli kwa mkono wangu mwenyewe ili aipandishe hadhi iwe ya mkoa, maana mkoa wenu umeshaandika maombi ya barabara hiyo kupandishwa hadhi” alisema waziri mkuu Pinda

  Hatua hiyo pia inafuatia ombi alilolitoa mbunge wa makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge kumuomba waziri mkuu kusaidia barabara hiyo ipandishwe hadhi kwani itasaidia wakulima wadogo kusafirisha mazao yao kwenda Mbeya na hata kwa usafiri wa kawaida kwani ni fupi

  Katika hatua nyingine waziri mkuu Pinda ametoa sh. Milioni 10 kwa ajili ya kituo cha fema matamba ambacho kinalea watoto yatima ambao hawana wazazi wote wawili.

  Kituo hicho ambacho kipo chini ya kanisa kimeonesha kumgusa waziri mkuu Pinda ambapo amesema kama sio kituo hicho hawafahamu watoto hao wangekuwa wapi hivi sasa hivyo kuunga mkono uamuzi uliofanywa na kituo hicho kwa kutoa kiasi hicho cha fedha

  Akiwa matamba waziri mkuu amesomewa taarifa ya wilaya na kuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro

  Na Edwin Moshi

  0 0

  Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.

  WAJUZI wa mambo na wanaharakati wanaendelea kuumiza vichwa vyao katika baadhi ya mambo yanayochelewesha maendeleo ya Tanzania, licha ya kuwa na mbiu nyingi, ikiwamo hii ya Maisha bora kwa kila Mtanzania.


  Kauli mbiu hii ilianzishwa na kusimamiwa kwa ukaribu kabisa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, wakati huo anawania nafasi hiyo kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).


  Kikwete alibanwa kwa karibu na wagombea kutoka vyama mbalimbali, akiwamo Profesa Ibrahim Haluna Lipumba kutoka Chama Cha Wananchi (CUF), Dk Willbroad Slaa kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na wengineo.


  Sio lengo langu kuelezea mbiu hizo au mchakato wa urais, ila jinsi sera ya umeme vijiji inaposhindwa kufanyiwa kazi kwa ufanisi na Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Hali hii inasababisha wananchi wengi wa vijijini waendelee kuishi maisha magumu. Wapo wapo tu. Leo hii Mtanzania anayeishi vijijini anashindwa kumiliki hata simu ya mkononi maana ni gharama kwake.


  Kama kijiji kina umeme, walau maisha yanaweza kuwa rahisi kidogo, maana wajasiriamali wengi wanaweza kujikwamua, hata kwa kugandisha ice cream, kuuza juisi, soda na maji baridi.


  Kama hivyo haitoshi, bado huduma mbalimbali zinazohitaji umeme zinaweza kuanzishwa na kuwanufaisha watu wote, ndio maana kila Mtanzania ana haki ya kupata nishati ya umeme.


  Mwishoni mwa mwaka jana, Wakala wa Umeme Vijijini REA, walitoa matangazo katika baadhi ya magazeti ya Mwananchi na Rai Mwema, kati ya Jumanne ya Desemba 18 na 19 kwa kurasa mbili ya umeme vijijini.


  REA walielezea mikakati ya mwaka 2013 ambapo vijiji kadhaa vilitajwa kupelekewa umeme kwa ajili ya kuwasogezea huduma hiyo, ikiwa ni tamko lililotolewa na REA, wakisisitiza kuwa mpango huo utakuwa tunu kwa Watanzania wote, hususan wale wanaoishi maeneo ya vijijini.


  Ikumbukwe kuwa, huduma ya umeme katika Taifa hili bado si ya uhakika na ndio maana mara kwa mara kunatangazwa mbinu na kuwataka wananchi watowe maoni juu ya nishati ya umeme.


  Inashangaza. Mtu anaombwa atowe maoni anataka TANESCO iweje, wakati tangu azaliwe hajawahi kutumia nishati ya umeme nyumbani kwake.


  Huyu atowe maoni yanayohusu nini? Au aitusi serikali, REA na TANESCO yao? Haya ni matamko ya kisiasa yanayoleta wasiwasi mkubwa na suala la maendeleo ya Watanzania wote, kwa kupitia nishati ya umeme ambayo ndio inayoweza kuukwamua uchumi wetu unaojikongoja siku baada ya siku.  Angalia, Waziri wa Nishati na Madini Tanzania, Sospeter Muhongo anakutana na wadau wa umeme Mlimani City.


  Kikubwa kinachojadiliwa hapo ni siasa, maana baada ya majibu yake mara nyingi huishia kwenye karatasi, maana wananchi wengi wa vijijini wanaishi maisha ya dhiki kwasababu ya kukosa nishati hii muhimu.


  Nasema haya baada ya hata vile vijiji ambavyo vinasifa ya kupewa umeme, lakini wanaendelea kuwekwa visogoni na serikali kwa kupitia REA wenyewe ambao ndio kila kitu katika kuwasambazia wananchi hao.


  Kwa mfano, ukitoka katika wilaya ya Korogwe kwenda Handeni, kijiji cha kwanza kinachoitwa Komsala, hiki hakina umeme tangu nchi ipate uhuru, licha ya kupitwa na njia mbili za umeme.


  Ipo njia inayopeleka umeme wilayani Handeni, ambapo vijiji mbalimbali vya mbele kama vile Kwamatuku, Sindeni, Misima na Makao Makuu ya wilaya hiyo, hivyo inashangaza kwanini vijiji vya nyumba yake havina umeme?


  Pia ipo ile njia kubwa ya umeme iliyopita pia katika kijiji cha Komsala, hivyo hakika ni aibu kama REA wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi sambamba na kuwasogea maisha bora wananchi wao.


  Ukiangalia yale matangazo yaliyotolewa na REA mwaka jana mwishoni, utagundua kuwa yalikuja baada ya wadau wa umeme sambamba na wananchi wa vijiji vya Komsala na Kwakiliga kulalamika kutengwa licha ya kuwa kwenye (Underline Transformers ).


  Sera ya umeme vijijini inasema vile vinavyopitwa na njia ya umeme, yani Underline Transformers vinastahili kupewa huduma hiyo, badala ya kuwa watazamaji wa nguzo za umeme zinazopita kando ya nyumba zao na kuelekea kwingine.


  Kama hivyo ndivyo, kulikuwa na haja gani REA kuwadanganya wananchi wa vijijini, hasa hivi vya Komsala na Kwakiliga, ukizingatia kuwa wao wenyewe walitangaza mkakati wao wa kuwaunganisha mwaka huu ili waweze kujikwamua kiuchumi.


  Ukiacha Komsala, vijiji vingine vilivyotajwa kupewa umeme ni Msasa, Kwedisemi, Kwamkole, Mkuyuni, Kwinji, Teleguru na Kisangasa.


  Katika wilaya ya Korogwe, REA ilitangaza kuunganisha umeme kwa vijiji vya Kilole Mzee, Kwasunga, Kwamaraha, Batini, Mswaha, Kwamtawazi, Mgobe, Lusanga, Kieti, Vugiri na Bagamoyo Ambanguru.


  Ni aibu kama vijiji vinavyopitwa na njia ya umeme vikashindwa kupatiwa huduma hiyo tangu Tanzania ipate Uhuru wake, ingawa kunakuwa na sera za kila zinazotangazwa na kuzua maswali na taharuki za aina yake katika Taifa letu, ukizingatia kuwa Bajeti ya 2013/2014 haijavilenga vijiji vingi, vikiwamo vile vilivyotajwa kutekelezewa mwaka huu.


  Tangazo lenye kurasa mbili linapotoka katika gazeti hapa nchini ni zaidi ya Shilingi Milioni nne, hivyo linapotoka katika magazeti mawili, kama vile Mwananchi na Rai Mwema, REA walitumia kiasi kisichopungua Milioni nane, kama majibu yaliyoandikwa na wadau wa umeme katika gazeti la Mtanzania.


  Gharama hizo zingetumika vizuri, walau zingeweza kununulia transformer moja kwa ajili ya kijiji kimoja kilichokuwa kwenye Underline Transformers, kama hiki cha Komsala, ambapo kina sifa zote na kipo karibu na wilaya ya Korogwe, licha ya kuwa chini ya wilaya ya Handeni.

  Lakini si kwa REA.


  Fedha hizi zimetumika bure tu, ukizingatia kuwa hata yale yaliyochapishwa katika matangazo waliyotoa yameshindwa kutekelezwa kwa namna moja ama nyingine.

  Hatuwezi kukubaliana na suala la matamko kama walivyotangaza kuwa jumla ya shilingi bilioni 826.1 zilitengwa kwa ajili ya upatikanaji wa umeme na kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati.


  Baadhi ya miradi iliyotekelezwa ni pamoja na: kuanza ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ikijumuisha ujenzi wa kituo cha kupokelea gesi Kinyerezi; kukamilisha ujenzi na kuanza kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito katika vituo vya Ubungo - Dar es Salaam (MW 105) na Nyakato - Mwanza (MW 60); kuendeleza miradi ya umeme vijijini katika mikoa 16; na kuendeleza upembuzi yakinifu katika miradi ya Makaa ya Mawe – Mchuchuma na Liganga.


  Aidha, hadi kufikia mwezi Desemba 2012, kiasi cha umeme kilichoingizwa kwenye Grid ya Taifa kilikuwa MWh 5,759,756 ikilinganishwa na MWh 5,153,400 mwaka 2011, sawa na ongezeko la asilimia 11.8. Mara nyingi maneno kama haya yanakuwa ni porojo tu ili siku ziende. Hakuna mipango kabambe na ile inayotekelezeka.


  Na ndio maana malalamiko yamekuwa mengi kutoka kwa wananchi na kuwa chuki dhidi ya serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Umeme ndio kila kitu, ndio maana katika mjadala wa Bajeti ya mwaka 2013/2014, wabunge walipigia kelele juu ya nishati ya umeme, hasa katika maeneo ya vijiji ambapo huko kumekuwa na kero sugu.


  Wananchi ambao simu zao za mkononi zinahitaji gharama za kupelekwa mjini ili zichajiwe na kuwafanya waishi kwa tabu na maisha ya kubahatisha. Kwa mfano, wananchi wengi wa kijiji cha Komsala, wanalazimika kwenda Korogwe Mjini ili wachaji simu zao, kusaga nafaka na huduma nyingine.


  Kwa mtindo huu, utajiuliza ile kauli mbiu ya Maisha bora imetokea wapi? Itaishaje? Je, serikali ya CCM inafahamu haya yanayoendelea?


  Hivi kweli wanakosa umeme wakati kijiji chao kinajitosheleza, huku juu ya nyumba zao ukipitishwa umeme unaokwenda mjini, yani Handeni Mjini.


  Wananchi hawa wana tofauti gani na wengine wanaoishi kwa raha hasa maeneo ya mjini? Je, tunasahau kuwa wananchi wa mjini kwa asilimia kubwa wanahitaji uwapo wa vijijini?

  Nini matarajio ya wananchi hawa kama Bajeti ya mwaka huu vijiji vya aina hii havijaguswa, wakati mwaka jana mwishoni


  REA walitolea ufafanuzi na kugusia mkakati huu wa underline transformers kwa kijiji hiki cha Komsala, ambacho licha ya kuwa wilayani Handeni, lakini huduma nyingi, ikiwamo TANESCO wanahuumiwa na wilaya ya Korogwe?

  Je, waendelee kusubiria kama watoto wadogo wa ndege?


  Wananchi hawa wamekosa nini kwa serikali yao chini ya Kikwete, maana yeye mwenyewe aliahidi na mawaziri wake wanasisitiza juu ya umuhimu wa umeme vijijini?

  Kama vyenye vigezo vyote vinanyimwa umeme kwa makusudi, itakuwaje majirani zao kwa Kweingoma, ambao hawa njia ya kawaida ya umeme haijapita kijijini kwao?


  Waziri Muhongo anayajua haya? Wataalamu wake wanampa picha gani kabla ya kuandaa ‘project’ ya umeme vijijini?

  Mtindo huu sio mzuri, maana tunazalisha wananchi wenye chuki na serikali yao. Ni vyema Wizara ya Nishati na Madini kwa kushirikiana na wadau wake, kama vile REA na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania TANESCO kuliangalia suala hili kwa kina.


  Umeme ndio kila kitu, ndio maana ziara ya Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama Tanzania, ilizingatia zaidi nishati ya umeme, akisisitiza ndio inayoweza kulikwamua Taifa.


  Maneno ya Obama yanakuja ikiwa ni ishara mbaya kwa serikali ya Tanzania, maana hakuna mipango ya wazi zaidi ya siasa kuchukua nafasi kila wasaa, ndio maana licha ya baadhi ya vijiji kutimiza masharti na vigezo vya kupatiwa umeme, ila wananyimwa.


  Huu sio mpango mzuri unaoweza kuwapatia maisha bora Watanzania na wale wanaoishi maeneo ya vijijini, hivyo REA lawama hizi ni zao.  0 0

  PICHA NA MAELEZO KWA KWA HISANI YA GAZETI LA MAJIRA TOLEO LA LEO.

  0 0


  BAADHI YA WATENDAJI WAKUU NA MAAFISA WAANDAMIZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAKIWASHUKURU WANANCHI MBALIMBALI WALIOKUWA WANAPITA NJE YA BANDA LA MALIASILI NA UTALII KWENYE MAONYESHO YA 37 YA KIMATAIFA YA BIASHARA MWAKA HUU KWA KUWAPUNGIA MIKONO NA KUWAONYESHA MOJA KATI YA TUNZO WALIZOZIPATA
  =======  ========   =========  ========
  ASANTENI KWA KUTUFANYA KUWA NAMBA MOJA

  WIZARA inawashukuru watu wote waliotembelea Banda la Maliasili na Utalii katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salam na kutuwezesha kuibuka mshindi wa Kwanza wa Banda Bora katika kundi la Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya 37 ya Saba Saba 2013.

  Ushindi huu unaama kubwa sana kwetu kwani haikuwa rahisi kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiingia kwa wengi bandani kwetu wanapata elimu yakutosha kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale waliokuwa wakitoa elimu mbalimbali zikiwemo za uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ufugaji nyuki na utalii.

  Aidha wale ambao hawakujaaliwa kwa sababu moja ama nyingine kufika kwenye banda letu wasiwe na wasiwasi wanaweza kuungana nasi kwenye Maonyesho ya Nanenane Dodoma ambapo tutahakikisha tunafanya vema zaidi. 

  Sambamba na hilo Wizara inachukua fursa hii kuomba radhi kwa wale wote wailiokwaza kwa namna yoyote ile katika kipindi chote cha Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 37 kwani tunatambua wananchi wengi mlikuwa na kiu ya kutembelea banda la wanyama hai hata muda ambao tulilazimika kulifunga (saa kumi na mbili jioni) kutoa fursa kwa wanyama kupumzika na kupata mlo wao wa usiku.

  Mwisho kabisa Wizara inawatakia Ramadhani Kareeem wale wote waliofunga na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la heri katika mwezi huu mtukufu Amin.

  0 0


   Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati akizungumza jambo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi,mara Mbunge huyo alipokwenda kutazama maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha polisi kinachojengwa na Mbunge huyo,kilichopo maeneo ya Tumaini.
   Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akipata maalezo mafupi kuhusiana na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi,pichani kati anaeshuhudia ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
   Baadhi ya Mafundi wakiendelaea na ujenzi wa kituo hicho kidogo cha polisi
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa,Bwa. Athumani Mungi akimuelekeza jambo Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati. 
  ======  =======  =======

  Viongozi mbalimbali mkoani Iringa wamekutana kujadili suala la uboreshaji wa miundombinu (barabara) katika kikao cha bodi ya barabara kwa kushirikiana na mamlaka ya barabara TANROADS mkoa wa Iringa akiwemo mkuu wa mkoa Dr.Christine Ishengoma ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho.

  Viongozi hao wamefikia maadhimio kadhaa ili kuongeza ufanisi na ukarabati wa barabara katika mkoa wa iringa ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi,ikiwemo na kupitisha sheria ya kukaguliwa kwa magari yasiyokuwa na vyombo maalum kwa ajili ya utupaji taka na gari yoyote itakayokamatwa ikiwa haina kifaa hicho itachukuliwa hatua ili kuwa fundisho kwa wengine,.

  Sambamba na hilo vingozi hao wamempongeza Mh.Ritta Kabati kwa kuwawakilisha vyema wanawake na wananchi wa mkoa wa Iringa hasa katika kupigania maendeleo ya mkoa,miongoni mwa mambo ambayo amekuwa akiyapigania ni pamoja na Ukarabati wa miundombinu,elimu pamoja na Benki ya akina mama iliyoko Dar es Salam pekee ikiwa ni benki ya akina mama wote nchini, hivyo amewataka viongozi wanaohusika na benki hiyo kuifikisha katika mkoa wa Iringa ili hata akina mama wa mkoa huo waweze kunufaika,   kutokana na kilio cha wanachi wa maeneo ya Tumaini,Semtema na maeneo jirani kudai kituo kidogo cha Polisi ,Mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa Mh.Ritta Kabati amejitolea kujenga kituo cha Polisi katika maeneo hayo ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waliokuwa wakionelewa na watu wasio wema, hivyo amesema kituo hicho kitaweza kusaidia kupunguza idadi ya uharifu katika maeneo hayo kwani kituo hicho ni moja kati ya vituo vingi vinavyohitajika mkoani ha Iringa.  Akimuonesha Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Bw.Athumani Mungi Mh.Kabati amemhakikishia kamanda kuwa ujenzi huo utakamilika mapema iwezekanavyo ili kuepusha adha kwa wananchi wa maeneo hayo.

  Kwaupande waka kamanda wa Polisi mkoani hapa amempongeza Mbunge huyo kwa moyo wake wa kujitolea katika mambo ya jamii ambapo amesema Jeshi la Polisi linapenda kushirikiana na wadau wanaounga mikono jitihada za jeshi hilo katika kuboresha amani nchini huku akitoa wito kwa wadau wengine kuiga mfano huo kwa umoja ni nguvu utengano ni Udhaifi.

  0 0

  Mwenyekiti wa TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile pichani akifafanua jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani} zaidi kuhusiana na maandamano hayo kumuondoa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.

  Chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo wamepanga kufanya mandamano ya kumuondoa mkuu wa wilaya ya kilolo,Mh. Gerald Guninita kwa madai kuwa anawanyanyasa na kuwadhalilisha watumishi wa umma.


  Wakizungumza na wandishi wa habari mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU,Bwa, Andrea Mwandimbile, wamesema kuwa hawamwitaji mkuu huyo wa wilaya kutokana na utendaji wake wa kazi kwa wafanyakazi wa umma, kuwa wa vitisho.


  Wamesema kuwa kutokana na kutoa kauli za vitisho kwa watumishi hao wa umma, zimekuwa zikiathiri utendaji na uhusiano makazini kutokana na wengi wao kufanya kazi kwa hofu.


  Kwa upande wake katibu wa chama cha wafanyakazi wilaya ya kilolo TALGWU ,John Mbingi ,wamewataja watu ambao tayari wamefanyiwa udhalilishaji na mkuu huyo kuwa ni Thomas Nyambage, ambaye ni afisa mifugo na kaimu wao kata ya Mlafu pamoja na Beatus Nyato,Afisa usafirishaji kilolo ambao walipigwa pingu hadharani na kuwekwa ndani na kisha kuachiwa huru bila kufunguliwa mashitaka.


  Aidha amesema tayari uongozi umeshafanya taratibu za kutoa taarifa kwa viongozi wa ngazi za juu akiwemo mkuu wa mkoa.kutokana na malalamiko hayo mkuu wa wilaya hiyo GERARD GUNINITA ambaye ndiye mlalamikiwa amekanusha mashitaka hayo na kusema kuwa hajapata malalamiko hayo. 

  0 0

  The Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO) Business  
  Development Manager Christine Mwakatobe (third left) poses for a group photo with other Tanzanian delegates during the 8  in Kampala this week. Looking on at the left is Mkunde Senyagwa from the Arusha International Conference Centre (AICC) and right is John Weatherill from  intervistas. 
  ========  ======  ========
  KIA, JNIA win Africa Airport Marketing Awards 2013

  By Correspondent, Kampala
  TANZANIA’S two international airports, Kilimanjaro International Airport (KIA) and Julius Nyerere International Airports (JNIA) have scooped the top awards during the 8th Routes Africa event held in Kampala between 7th to 8th of July, 2013.

  The event hosted by Civil Aviation Authority of Uganda and Entebbe International Airport brought together Over 300 aviation professionals from across the world.  During the event, KIA emerged winner for the under 4 million passengers per annum category while JNIA was highly recommended in under 4 million passengers per annum category.

  Speaking shortly after award ceremony, the Tanzanian delegation head Bakari Murusuri from Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO) said the awards won is a land mark to in the country’s aviation sector. “The awards are not only an inspiration to the two airports but Tanzania’s aviation sector as a whole. Our focus should now ensure that the two airports meet international standards,”.

  He added that as the overall winner of the Africa Heat, KIA will automatically be shortlisted for world routes marketing awards taking place in Las Vegas, Nevada, USA in October, 2013. The KADCO Business Development Manager Christine Mwakatobe said “This has been one of the most amazing evenings for us at Kilimanjaro International Airport to win this award. 

  “We would like to thank all of the airlines that serve the airport for voting for us in this process and we are pledging our commitment that we will keep working hand-in-hand with all of our partners,” she added.

  Other Tanzanian delegates present at the occasion included Scholastica Mukajanga from TAA, Efatha Lyimo from JNIA and Elisilia Kaaya from AICC, Mkunde Senyagwa from AICC and John Weatherill from intervistas. Meanwhile, Zimbabwe is set to host next year’s 2014 Routes Africa event between June 22-24, 2014and will be hosted by the Civil Aviation Authority of Zimbabwe.

  Nigel Mayes, VP Commercial – Routes, UBM Live said of the announcement:  “We are thrilled at the decision to take Routes Africa to the stunning destination of Victoria Falls which is a World Heritage Site.  Hosting Routes Africa will deliver the route development community to Victoria Falls providing the opportunity to market this destination extensively whilst also showcasing the potential of the airport once it has undergone the major infrastructure changes which began earlier this year.”

  0 0

   Afisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humudi Abdulhussein wapili toka kushoto na Meneja ukuzaji wa biashara ya huduma ya M PESA wa Vodacom Tanzania,Moses Krom,wakimshuhudia Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu akizungusha gurudumu lenye majina ya washiriki wa Promosheni  ya lipa kwa M pesa na Ushinde ukiwa Sabasaba na kujishindia zawadi ya shilingi Elfu 40 sanjari na muda wa maongezi wa shilingi 1000   kila siku ambapo washindi watano walipatikana,Promosheni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania wakati wa maonesho ya 37 ya kimataifa ya sabasaba.
  Afisa wa bodi ya michezo ya kubahatisha nchini,Bw.Humudi Abdulhussein na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania Bw.Matina Nkurlu wakiweka karatasi zenye majina ya washiriki wa Promosheni  ya lipa kwa M pesa na Ushinde ukiwa Sabasaba na kujishindia zawadi ya shilingi Elfu 40 sanjari na muda wa maongezi wa shilingi 1000   kila siku ambapo washindi watano walipatikana, Promosheni hiyo inaendeshwa na Vodacom Tanzania wakati wa maonesho ya 37 ya kimataifa ya sabasaba,anaeshuhudia kulia ni Meneja ukuzaji wa biashara ya huduma ya M PESA wa Vodacom Tanzania,Moses Krom.

  0 0
 • 07/10/13--05:26: BRELA KUIMARISHA HUDUMA ZAKE
 •  Kaimu Meneja Huduma, Utawala na Fedha wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA) Bosco Gadi (kushoto) akieleza Vyombo vya Habari juu ya uimarikaji wa huduma za BRELA,katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari,kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.

  Naibu Msajili, Mkuu wa Idara ya Sheria na Biashara wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA)Andrew Mkapa(kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kulia ni Kaimu Meneja Huduma, Utawala na Fedha (BRELA) Bosco Gadi.


  (PICHA NA ELIPHACE MARWA).  =======  ==============  ========
  WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (BRELA)


  HUDUMA ZA BRELA KUIMARIKA.


                              
  Ndugu waandishi wa Habari Habari ya Asubuhi!!


  Tumekuja kuzungumza nanyi kuhusu namna Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inavyoimarisha huduma kwa kuhakikisha kuwa wateja wake wanapata huduma bora, kwa wakati na kwa kutumia mikakati mbali mbali ya kisheria, kiutendaji pamoja na mbinu za kimtandao kwa kutumia njia za kielektroniki kwa ajili ya kupeleka huduma karibu na wananchi.


  Ndugu Waandishi; Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuzingatia dhana ya ushirikiano na Sekta Binafsi yaani “PPP”  imeingia kwenye Mkataba wa ushirikiano na Chama Cha Wafanyabiashara na wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA),  ili waweze kutoa huduma saidizi za awali za usajili wa Makampuni na Majina ya Biashara katika ngazi ya Mikoa na wilaya Tanzania Bara.


  Kuchaguliwa kwa TCCIA kumetokana  na wao kuwa na mtandao mpana wa kielektroniki unaounganisha ofisi zao wilayani takriban mikoa yote ya Tanzania bara hivyo kuifanya BRELA kuona umuhimu wa kuzitumia ofisi zao zilizoko nchi nzima.


  Wateja wa BRELA waliopo mikoani wanahimizwa kutumia ofisi za TCCIA na kuendelea kuwasilisha maombi yao ya huduma za Usajili kupitia ofisi za Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture-TCCIA) mikoani ambapo taasisi hiyo hutuma maombi hayo BRELA ambako usajili hufanyika na kurejesha vyeti vya usajili TCCIA mkoani hivyo kutokulazimika kusafiri kuja Dar es Salaam kwenye Ofisi za BRELA kupatiwa huduma za usajili.


  Utaratibu huu wa ushirikiano baina ya BRELA na TCCIA ulianza Decemba 2012, na zaidi ya maombi 500 yamesajiliwa  kupitia ofisi za TCCIA mikoani.


  Kupitia utaratibu huo, gharama za usajili wa Jina la Biashara ni sh. 6,000/= ambazo wateja hulipia na kupatiwa stakabadhi za BRELA na pia TCCIA inatoza kiasi kidogo cha fedha sh. 2,000/- kwa kila Jina la Biashara kwa ajili ya huduma za kiutawala ikijumuisha gharama za utumaji wa maombi hayo.


  Aidha, Kwa upande wa Usajili wa Makampuni ada ya usajili inayotakiwa kulipwa itategemeana na kiasi cha mtaji Mteja anachokiandika kwenye Katiba ya Kampuni anayotarajia kuisajili. Gharama yake inaanzia sh. 50,000/= kwa mtaji wa zaidi ya Sh. 20,000/= - 500,000/= na  kiwango cha ada cha juu kabisa ni sh. 300,000/= kwa mtaji ambao ni zaidi ya 30,000,000/= ambapo utapata stakabadhi ya BRELA na TCCIA watatoza gharama ndogo ya sh. 5,000/= kwa kila kampuni kwa ajili ya gharama za kiutawala ikijumuisha gharama za usafirishaji.


  Utaratibu huu wa ushirikiano wa kutoa huduma kati ya BRELA na TCCIA umesaidia kwa kiasi kikubwa kusogeza huduma za BRELA karibu na wananchi, hususan wa mikoani ambapo sasa hawalazimiki kuja Dar es Salaam kufuata huduma za BRELA. Hii ni hatua ya awali wakati tunaendelea kuboresha zaidi huduma mikoani ikiwa ni pamoja na kutumia mifumo ya TEHAMA.  Ndugu Waandishi wa Habari, Mabibi na Mabwana;


  Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) hutoa baadhi ya huduma za usajili kwa njia ya mtandao, hivi sasa Majina yote ya Makampuni na Majina ya Biashara yamewekwa kwenye mtandao.


  Mteja akiingia kwenye tovuti ya BRELA www.brela-tz.org, anaweza  kuona orodha ya Makampuni yote yaliyosajiliwa Tanzania Bara na kufanya upekuzi wa majina “Online name search” ili kutambua iwapo jina la biashara analolitaka kusajili limeshasajiliwa au la, kabla ya kutuma maombi ya Usajili.


  Aidha, fomu zote za usajili zinapatikana kwenye tovuti hiyo. Pia tumeweka katiba mfano inayojulikana kwa lugha ya kigeni kama “Memorandum and Article of Association” kwenye tovuti ambayo mteja anaweza kutumia bila gharama yeyote kujitengenezea katiba ya kampuni yake. 


  BRELA ipo katika mkakati wa kuweza kutoa huduma kwa njia ya mtandao wa kielektroniki (online registration), kwa kuanza, imekwisha kuweka nyaraka za mafaili kwenye mfumo wa kieletroniki ambapo unaweza kupata jalada kwenye kompyuta.


  Ndugu Waandishi wa Habari, Mabibi na Mabwana;


  BRELA ipo mbioni kurahisisha njia za malipo kwa kutumia mabenki kwa kuanzia na CRDB na NMB. Mpango huu unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 15.7.2013 na benki ya CRDB


  Mpango huu utawawezesha Wadau  kulipa ada za usajili kwa njia ya benki popote walipo. Mpango wa baadaye ni kuweza kusajili na kupata huduma popote alipo kwa kutumia mtandao ambao utatuwezesha kufikia kwenye ndoto yetu ya kutoa huduma bora na kwa wakati kwa kuzingatia viwango vya kisasa vya  kimataifa kulingana na dira ya Wakala.


  BRELA ilianzishwa na kuzinduliwa rasmi tarehe 9 Desemba 1999 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Sheria ya Wakala za Serikali namba 30 ya mwaka 1997.


  Makujumu makuu ya BRELA ni kusajili Makampuni; kusajili Majina ya Biashara; Alama za Biashara na Huduma; kutoa Hataza - Uvumbuzi kwa muda maalum (patents of inventions)  na Kutoa leseni za Viwanda na kusajili Viwanda.


  Lengo kubwa la BRELA ni kuhahikisha kuwa huduma za usajili zinapatikana pale zinapotakiwa kwa wepesi na urahisi wakati wote na popote kwa kutumia njia za kisasa.  0 0
  *       Kodi ya Nyumba kwaheriii, tumia AIRTEL YATOSHA ujishindie yako
  *       Kelele za wapangaji tupa kuleee, Airtel Yatosha ndo habari ya Tanzania
  *       Zimebaki siku 20 tu mwenye nyumba ya kwanza ya YATOSHA hadharani

  Huu ndo mjumba wa kifahari utakaoshinda kupitia droo ya mwisho wa
  mwezi Hii ni sehemu ya mbele ya Nyumba mojawapo ya AIRTEL YATOSHA
  Nyumba hizi zimejengwa kwa mpangilio maalum  na wataalam  kutoka
  shirika makini la nyumba Tanzania (National Housing Corporation).

  Mahali iliko ni Kigamboni Kibada wilaya ya Temeke General View ukiwa
  maeneo ya nyumba iliko Vitu vizuri unavyoweza kuviona ukiwa nyumbani
  kwako endapo utaibuka mshindi ni pamoja na Uwanja wa Taifa, uwanja wa  ndege na utaweza kujione vizuri vikwangua anga vya jijini dar es


  salaam kama vile PPF Tower, Uhuru height, Jubilee Tower, Serena Hotel
  n.k Jiunge na kifurishi cha Airtel Yatosha SIKU, WIKI au MWEZI kwa
  kupiga *149*99# na chagua kifurushi kitakachokufaa ili uwe mmoja wa
  washindi watakaofaidika na nyumba hizi

  NB:
  Nyumba zote Tatu zina vyumba vitatu vyakulala, Sebule, Jiko na Public
  toilet na Garden nzuriiiii/ kaliiiiii

  0 0

  Imeelezwa kuwa Jeshi la Polisi na Mahakama bado hawajalichukulia hatua za makusudi suala la ubakaji watoto ambalo linaonekana likiendelea kuengezeka siku hadi siku.  
  Kutolichukulia hatua  huko ni pamoja na adhabu ndogo wanazo pewa wahalifu  na kutoridhishwa na ushahidi wa kuona unao tolewa na watu mbali mbali mahakamani.
   Hayo yamesemwa leo huko katika ukumbi wa  Baraza la wawakilishi  chukwani   wakati walipokuwa wakichangia bajeti ya Wizara ya Ustawi wa Jamii ,Vijana Maendeleo ya Wanawake na Watoto juu  ya suala zima la udhalilishaji na ubakaji  wa watoto  ulivyokithiri hapa nchini.
  Wamesema hali hiyo mbaya  inatokana na jeshi   hilo na Mahakama kutochukua  hatua za makusudi za kisheria kwa watuhumiwa ambao wanahusika na kesi za uzalilishaji watoto na  na kuwachilia kuwapa adhabu ndogo au kuto kamilika ushahidi wakuona.
   “Polisi wanataka ushahidi  wa aina gani ? kila siku suala la ubakaji linaongezeka hivi karibuni mtu kafungwa miezi sita kwa kosa la ubakaji hio ni adhabu ndogo  kulingano na kosa lenyewe, alisema mmoja wawalikilishi hao.
  Aidha walisema kuwa masuala ya udhalilishaji yanafanywa na watu wazima wenye akili zao timamu jambo ambalo linawasababisha   watoto hao kuona aibu  na kuweza kuathirika kisaikolojia .


  Nae Farida Amour Mohamed   alimuomba Rais wa  Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kulishughulikia suala hilo kwa  makini ili uzorotaji wa kesi pamoja na hukumu  zisicheleweshwe .
  Nae asha Bakari Makame mwakilishi wa viti maaluma wanawake  amesema suala la ubakaji watoto linauma sana hasa kwa sisi wazazi  ,kwahivyo kama kuna tatizo la kisheria lirekebishwe haraka sana .
  “Hatuta kubali kabisa kabisa  Taifa la kesho kudhalilishwa, Wizara hii ndio iliyozaa marais,i mawaziri, duniani   kote  hii ni wizara nyeti “alisema Asha Bakari .
  Mwakilishi huyo aliiomba Serikali ya Mapinduzi  ya  Zanzibar  kutoa  nafasi maalum  ya msaada kwa   Wizara ya UStawi wa Jamii Maendeleo ya Vijana wanawake na Watoto   kutopewa  nafasi  mtuhumiwa  yeyote wa  ubakaji  wa watoto na hatua kali zichukuliwe  dhidi yake .
  Aidha wawakilishi hao walisema kuwa  kutokana na  sula hilo  la kutokamilika ushahidi  wa kesi za uzalilishaji ikiwa unaonekana kuwa haukidhi haja, serikali itafute kifaa maalumu cha kipimo  kinacho tumia utalamu DNA ili kuweza  kugundua ushahidi wa uhakika ili vyombo vya sheria viridhike.
  Wakilishi hao kwa umoja wao walilani suala la omba omba ambalo linachukuwa nafasi kubwa hapa nchini pamoja kutumishwa kazi watoto wakiwa na umri mdogo .
  Wakati huo huo Naibu Waziri wa Afya Dkt Sira Ubwa Mamboya alijibu suali la  nyongeza la muakilishi viti maalumu  Panya Ali Abdalla  aliyetaka kujua  kwanini serikali na washirika wa maendeleo watumia pesa nyingi kujenga  nyumba  za Daktari katika vituo vya afya  na kwa nini nyumba hizo hadi sasa hazikaliwi na madaktari ?.
  Alisema kuwa ni kweli  kuna baadhi ya vituo vya afya vimejengewa nyumba za  kukaa madaktari kama vile ukongorani na sehemu za Pemba ,nyumba hizo zimepelekewa  Madaktari kuzikaa  lakini kwa makusudi madaktari waliopelekwa nyumba hizo hawataki kuzikaa kwa madai waume zao hawataki  na wengine wamejitia sababu za kutaka  kuimarisha maisha yao .
  Alisema watu hao iwapo hawatakua na sababu za kimsingi kuna hatari kufutiwa posho ambazo zime ambatanishwa na ishahara yao kwa kukiuka agizom la wizara kuukaa katika vituo hivyo.
  Aidha alisema kwa wale abao nyumba haziko na hawajakataa kukaa karibu na vituo nap engine wanatumia nauli zaidi maramoja kweli hao inafaa wafikiriwe na watachukua hatua kulifanyia kazi vipi waone kuwasaidia. 
  Na Ali Issa  Maelezo  Zaznibar   10 / 7 /2013


  0 0

  IMG_9901

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya Mwaka 2013 ambayo imejikita kiundani zaidi kuangalia muunganiko wa Mahusiano ya Kibiashara na Uwekezaji Duniani.Bi. Kairuki amesema Tanzania imeweza kupata Uwekezaji mara dufu katika maeneo ya Mafuta na Utafiti wa Gesi Asilia katika kusukuma pato la taifa kuongeza ajira na kupambana na umaskini.

  Ameongeza Muunganiko wa Biashara na uwekezaji umepata mwamko mkubwa sana kutoka kwenye makampuni makubwa duniani na umeleta fursa kwa nchi maskini na zinazoendelea kama Tanzania kuwa na uhusiano mzuri kiuchumi na nchi zilizoendelea. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirika la Kazi Duniani (ILO). Picha na Zainul Mzige.
  IMG_9892
  Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali na mabalozi wakifuatilia uzinduzi rasmi wa ripoti hiyo ya Uwekezaji Duniani.
  IMG_9876
  Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA akizungumzia umuhimu wa sera za nchi za Uwekezaji kuhakikisha zinatoa fursa ya ajira na kupunguza umaskini katika nchini zinazoendelea.
  IMG_9857
  Viongozi wa taasisi mbalimbali, Mabalozi, Waandishi wa habari katika uzinduzi huo.
  IMG_9934
  Mwezashaji katika uzinduzi wa Ripoti ya Ywekezaji wa Kigeni Duniani ya Mwaka 2013 Stella Vuzo Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akiwakaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kuzindua rasmi ripoti hiyo.
  IMG_9918
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara Manuela TORTORA kwa pamoja wakizindua rasmi Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 iliyobeba kauli mbiu Muunganiko wa Biashara na Uwekezaji Duniani "Global Value Chains".
  IMG_9924
  Sasa imezinduliwa rasmi nchini Tanzania.
  IMG_9967
  Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuendeleza Viwanda (UNIDO) Emmanuel Kalenzi akichangia mada baada ya uzinduzi wa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013.
  IMG_9929
  Kutoka kushoto Meza kuu ni Mkurugenzi wa Utafiti na Mifumo ya Teknolojia kutoka Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) John Kyaruzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Juliet Kairuki na Mkuu wa Masuala ya Ufundi Ushirikiano na Huduma wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Biashara (UNCTAD) Manuela TORTORA.
  IMG_9940
  Usia Nkhoma Ledama kutoka Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) akigawa Ripoti ya Uwekezaji Duniani ya Mwaka 2013 kwa wadau waliohudhuria uzinduzi wa ripoti hiyo.
  IMG_9952
  Mdau akipitia ripoti hiyo mara baada ya kuzinduliwa rasmi nchini.
  IMG_9894
  Pichani juu na chini ni sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
  IMG_9891

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani AFrika, uliofanyika jana jioni Julai 9, 2013 kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam.
   Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel,akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
   Baadhi ya Wabunge wakiwa katika chumba cha mkutano huo, kutoka (kushoto) ni Mbunge wa Kahama James Lembeli, Mbunge wa Mafia, Abdulkarim Shah, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, wakiwa katika mkutano huo jana.
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (katikati) akiwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, (wa pili kulia) Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel (wa pili kushoto) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela (kulia) wakifuatilia moja ya mada zilizokuwa zikitolewa ukumbini hapo kupitia Screen kwa njia ya TV
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu (katikati) na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela, baada ya kufungua rasmi mkutano huo jana Julai 9, 2013 jijini Dar es Salaam. Picha na OMR.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Baraza la Dunia ya baadaye wa Dunia, 'World Future Council' Alexandra Wandel, wakati alipowasili kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es Salaam, jana jioni Julai 9, 2013 kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mabunge wa kujadili Sera za Misitu Barani Afrika, uliohudhuriwa na wabunge mbalimbali kutoka Bara la Afrika. Katikati ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Getrude Mongela.Picha na OMR
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge waliohudhuria Mkutano Mabunge wa kujadili Sera na changamoto za Misitu Barani Afrika uliofanyika jijini Dar es Salaam, jana Julai 9, 2013. 

  0 0


  0 0

  20130708_112501_resized

  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu Mh.Jerry Silaa akipokelewa na viomgozi mbalimbali wa Chama Mkoani Simiyu mara tu baada ya kuwasili mkoani humo.
  20130708_112507_resized
  20130708_112643_resized
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu Mh.Jerry Silaa akisaini kitabi cha wageni katika ofisi za Chama Mkoani Simiyu.
  20130708_121852_resized
  Mh. Jerry Silaa akiangali burudani ya ngoma (haipo pichani) mara tu baada ya kuwasili mkoani humo.
  20130708_122106_resized
  Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mlezi wa CCM Mkoa wa Simiyu Mh.Jerry Silaa na viongozi mbalimbali wa Chama Mkoani Simiyu wakiimba nyimbo za Chama.
  20130708_122154_resized
  MC akitambulisha meza kwa Wanachama wa CCM mkoani Simiyu.

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Balozi wa Netherland nchini Tanzania, Mhe. Ad Koekkoek, aliyemaliza muda wake nchini, wakati alipofika kumuaga Makamu Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Julai 12, 2013. Picha na OMR.


  0 0

   Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini,Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bi. Riziki Abraham (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari nchini juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma, kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO)Jijini Dar es Salaam,kulia ni Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi hiyo Bw. Malimi Muya. 

  Katibu Msaidizi Idara ya Ajira kutoka Ofisi ya Rais Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Malimi Muya (kulia) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya Uendeshaji wa Mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma, kwenye mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Jijini Dar es Salaam, katikati ni Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini wa Ofisi hiyo Bi. Riziki Abraham na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.

   ====  =======  ======  =====.

  Uendeshaji wa mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.


  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29 (1). Jukumu la msingi la Sekretarieti ya Ajira ni kuendesha mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma.  

  Hapa ina maana  kuwa jukumu la kuajiri, kuthibitisha watumishi kazini pamoja na masuala ya nidhamu ya Watumishi yanabaki kwa Watendaji Wakuu wa Wizara na Taasisi katika Utumishi wa Umma  mitarafu ya Kifungu cha 6(1) (b) cha Sheria ya Utumishi wa Umma no 8 ya mwaka 2002. Ambapo katika kuendesha mchakato huo, Sekretarieti ya Ajira inapaswa kuzingatia Sheria, Kanuni, na Taratibu zilizopo ili kuhakikisha Utumishi wa Umma unapata Watumishi weledi na wenye maadili mema. Hadi sasa jumla ya waombaji 4891 tumeshaendesha mchakato wao wa ajira na kuwapangia vituo vya kazi.


  Hata hivyo, Sekretarieti ya Ajira kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilipeleka Mswada Bungeni unaopendekeza kukasimu madaraka ya kuendesha mchakato wa Ajira ili baadhi ya Waajiri wakasimiwe madaraka hayo ili kurahisisha utendaji kazi katika kushughulikia  mchakato wa ajira kwa baadhi ya kada. 

  Huku Sekretarieti ya Ajira ikiendelea kuhakikisha kuwa jukumu hilo linaendelea kutekelezwa kwa ufanisi. Tunapoongelea suala la ufanisi hapa Kitengo cha Udhibiti na Ubora kinasimamia suala zima la uhakiki wa taarifa za mhusika, uhakiki wav yeti na uadilifu wake kwa ujumla. Ambapo hadi sasa tumeshakamata  jumla ya vyeti vya kughushi 677 ambavyo wahusika wanadai wamevipata kutoka RITA, VETA na NECTA.


  Nafasi  wazi za kazi zitakazokuwa zikitangazwa na mchakato wake kuweza kukasimiwa ni pamoja na Kada ya Wasaidizi wa ofisi, Wahudumu wa afya, Madereva, Maafisa Watendaji wa Kata, Mtaa, Kijiji, Wapishi, Walinzi, Madobi, Wasaidizi watunza kumbukumbu pamoja na Makatibu Muhtasi (walio chini ya cheo cha mwandishi mwendesha ofisi)  au Kada zingine ambazo Katibu wa Sekretarieti ataona inafaa kukasimu.


  Aidha, nitoe ushauri kwa wanafunzi walioko shuleni na wanaotarajia kuingia vyuoni kuchukua masomo ama kozi za fani ya Afya, Elimu, Mifugo na Kilimo maana ni maeneo ambayo bado yana fursa nyingi za ajira Serikalini na wahitimu wake pindi wamalizapo wanapangiwa vituo vya kazi moja kwa moja bila ya kupitia mchakato wetu wa ajira kutokana na uhaba wa Wataalam wa fani hizo katika soko la ajira hivi sasa.


  Sekretarieti ya Ajira katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa  kwa haraka zaidi zinazohusu  mchakato wa ajira katika Utumishi  wa Umma na ili kuweza kuendana na mabadiliko ya sayansi na  teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani kwa ujumla, iliamua kuanzisha tovuti yake (www.ajira.go.tz) ambayo imerahisisha  kwa kiasi kikubwa utoaji na upokeaji wa taarifa mbalimbali  hususani  za matangazo ya fursa za ajira taarifa nyingine zinazohusu masuala ya ajira Serikalini na matangazo mengine yanayohusu shughuli za Sekretarieti ya Ajira. Tangu kuzinduliwa mwezi Aprili, 2013 imeweza kutembelewa na  wadau zaidi ya 2,900,000.


  Pamoja na tovuti Sekretarieti ya Ajira imeanzisha KANZIDATA (DATABASE)  za aina tatu (3) ambazo ni Kanzidata ya Wahitimu wa Vyuo, Kanzidata ya waliofaulu usaili na Kanzidata ya waliopangiwa vituo vya kazi.


  Jambo lingine ambalo ningependa mkalifahamu ni kuwa, Sekretarieti ya Ajira iko katika hatua za awali za mchakato wa kuwawezesha waombaji wa fursa za ajira kuwasilisha maombi ya kazi kwa mfumo wa kielektroniki (e-application) kwa nafasi wazi zitakazokuwa zikitangazwa katika Utumishi wa Umma ili kurahisisha kupunguza mlolongo wa uendeshaji mchakato wa ajira ulivyo hivi sasa.


  Mwisho nimalizie kwa kuwataka waombaji wa fursa za ajira kutokuchagua maeneo ya kufanyia kazi, hususani wale wanaopangiwa vituo vya kazi na Sekretarieti ya ajira na hawaendi kuripoti bila ya kutoa sababu za msingi maana Sekretarieti ya Ajira inaona hili ni kosa na inaandaa utaratibu wa kutowaruhusu kufanya usaili mwingine waombaji kama hao.    
                 

  Imetolewa na Riziki V.  Abraham, Msemaji na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  +255-687624975


  0 0

  ZIFFFashion Week Zanzibar: Mira NairFashion Week Zanzibar
  Javed Jafferji, Founder of Fashion Week Zanzibar getting an award from Hon. Seif Sharif HamadZIFF Celebrity guest Mira Nair with Javed Jafferji at the HotSpot BistroTruly Zanzibar Party
  » DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO
  Dear All
  As our festival partner, Zanzibar International film Festival is over, we had great and exciting moments from the first day of film Festival. Each year, some of the most captivating and cutting-edge cinema from Africa and beyond is screened in venues across the island. From world-premiers to local shorts, its got it all, with a long history of showcasing the highest quality film from all over the world. Films were submitted based on a yearly theme – this year was ‘Season of Visions’ – and entered into various categories and competitions. The final night was an awards night, where the winning films were recognized and celebrated.
  We had truly Zanzibar launch and ZIFF party, On the eve of Friday, June 28th Zanzibari designers Keeping their pieces simple, the designers added glamour by incorporating kanga, kitenge, trims, tassels, braiding, weaves and sequins in the Mtoni Palace Ruins.Participating Designers included Farouque Abdela, Adam, MAGO east Africa, Waiz Houston Shelukindo, Kihag, Upendo, Maskat De haan and Rizwan. Their collections were charming offering any young femme fatale would love to indulge in. The live music was from DCMA.
  ZIFFZIFFFashion Week Zanzibar
  Javed Jafferji, Founder of Fashion Week Zanzibar awarded at ZIFFLover’s Island Film by Javed JafferjiMusic by DCMA at Truly Zanzibar Party
  » DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO
  Our Director and Founder of Fashion Week Zanzibar and many other key players were awarded a certificate of appreciation by Hon. Seif Sharif Hamad the first vice president of Zanzibar at the launch of the festival for supporting and helping ZIFF for last 16 years.
  Fashion Week Zanzibar also engaged in having a tea party with ZIFF Celebrity guest Mira Nair at the HotSpot Bistro. Mira Nair is an Indian film director, actor and producer based in New York. Her production company is Mirabai Films. Her most recent films include Vanity Fair with Reese Witherspoon, The Namesake. Amelia and the Reluctant Fundamentalist which had its African premiere this year at the Zanzibar International Film Festival.Many of singers and M.C.s were dressed by Zanzibar fashion week. By adding glamour to the festival MCs and also we’re pretty sure you enjoyed the music performances after.
  Last day of Ziff brought surprise to our founder Javed Jafefrji who’s production won three awards by ZUKU for Best actor Swahili movie: Bond bin Suleiman (Bobby in Lover’s Island), Best director Swahili movie: Bond Bin Suleiman (Lover’s Island) and Best Swahili featured film: Lover’s Island by Javed Jafferji.
  ZIFFZIFF
  ZIFF participants awarded certificates of appreciationChairman of ZIFF, Mahmoud T. Kombo giving a speech
  » DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO
  Fashion Week Zanzibar From October 25 -27, the Mtoni Palace Ruins will be the center of attraction for all fashionistas with the arrival of more than 25 designers, who will be presenting their exclusive designs and live audiences 400 + celebrity guests who are expected to attend.
  For more information on designers, models, photos, show times and schedule please visit www.fashionweekzanzibar.com
  Fashion Week ZanzibarFashion Week ZanzibarFashion Week ZanzibarFashion Week ZanzibarFashion Week Zanzibar
  Fashion Week Zanzibar Models
  » DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO» DOWNLOAD PHOTO
  Fashion Week ZanzibarZIFFDCMA
  P. O. Box 3181, Zanzibar, TanzaniaE: javedjafferji@fashionweekzanzibar.comW: www.fashionweekzanzibar.com

  0 0

   Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akimkabidhi  mwakilishi wa Bakwata Ustadh Hassan Malangalikatika  hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima (hawapo pichani)  iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam . 
   Meneja  Uhusiano wa Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi  akiwakabidhi  Saida Makope mmoja wa wakilishi wa kituo cha watoto yatima mjini Dar Es Salaam  katika  hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani  vilivyotolewa kwa vituo vitatu vya watoto yatima jijini Dar Es Salaam  iliyofanyika  katika ofisi za Airtel  Morocco jijini Dar Es Salam  akifuatiwa na mwakilishi wa Bakwata ustadhi Ustadh Hassan Malangali .

  Sehemu ya msaada wa vyakula vilivyotolewa kwenye hafla hiyo fupi.

   Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye hafla fupi ya makabidhiano  ya vyakula vya kufuturisha katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani iliyofanyika  katika ofisi za Airtel jijini Dar Es Salam ,akifuatiwa na meneja wa huduma za Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi.


  =======  ========  ========
  AIRTEL YATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA MIKOA MINNE

  *       Wateja Airtel sasa kupata muda wa dua, nukuu za qurani, mawaidha kwa
  kutuma neno Ramadhani kwenda 15322 kwa shilingi 153 tu kwa siku.
  Kampuni za simu za mkononi za Airtel Tanzania kupitia Kitengo chake
  cha huduma kwa Jamii wametoa msaada kwa vituo vitatu jijini Dar Es
  Salaam vya watoto yatima katika mwezi mtukufu wa Ramadhani vikifuatiwa
  na vituo vingine katika mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya ili kusaidia
  watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo.

  Msaada huo umetolewa kwa lengo la kuwalenga watoto kutoka mikoa minne
  ambayo ni Dar Es Salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa watoto hawa
  wanaohitaji upendo  hususani katika kipindi hiki cha mfungo wa
  Ramadhani. Baadhi ya vitu vilivyotolewa ni Mchele,Sukari,
  maharagwe,unga, mafuta ya kupikia,maziwa, juice, majani ya chai na
  sabuni vyenye dhamani ya shilingi milioni tano na nusu.

  Akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano iliyoandaliwa katika
  makao makuu ya  Airtel jijini Dar Es Salaam, Meneja uhusiano wa huduma
  kwa Jamii bi Hawa Bayumi alisema "kwa kutambua umuhimu wa Jamii
  tunayofanya nayo biashara kampuni ya Airtel tumeamua turudishe kiasi
  cha faida tunayopata kwa wananchi ili iwasaidie.

  Akifafanua alisema kwa muda wa miaka 11 iliyopita tumeweza kusaidia
  Jamii mbalimbali ya watanzania ndani ya mfungo wa Ramadhani na bila
  kuacha nyanja za elimu, michezo kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira
  magumu na kukosa huduma mbalimbali za kijamii.

  Kwa mwaka huu kupitia Kitengo chake cha huduma kwa Jamii tutarudisha
  tulichokipata na tutaweza kufikia watoto zaidi ya 300 wa mikoa ya Dar
  Es Salaam, Arusha , Mwanza na Mbeya na mpaka sasa  kwa mwaka huu
  Airtel imegharamia zaidi ya shilingi millini 150 katika kukuza kiwango
  cha elimu kwa watoto wetu hapa Tanzania," alisema Bayumi.

  Bayumi aliongeza kwa kusema kwamba Airtel inapenda kuwatakia kheri na
  Baraka katika mwezi huu mtukufu na tangu kuanza kwa Mwezi mtukufu wa
  Ramadhan, wateja wa Airtel wanaweza kufurahia huduma maalumu ya
  Ramadhani kwa kutuma neno RAMADHANI kwenda namba 15322 kwa shilingi
  153 tu kwa siku. Katika huduma hii mteja atapokea dua, nukuu za
  qurani, mawaidha na taraweh salat moja kwa moja kwenye simu yake, kila
  siku.
  Naye katibu mkuu wa Bakwata Sheikh Suleiman Lolila  ambaye alikuwa
  mgeni rasmi alisema mbali ya hafla hiyo makabidhiano ya chakula imetoa
  fursa kwa waislam kutoka maeneo mbalimbali kukutana pamoja na
  kukumbushana juu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.
  Aidha Lolila licha ya kuishukuru Airtel Tanzania kwa misaada inayotoa
  kwa Jamii alisema jambo hilo linahitaji pongezi na kutaka liungwe
  mkono na kuigwa na kampuni zingine hapa nchini.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia), akizungumza alipotembelea hivi karibuni Kiwanda cha Kibuku cha Darbrew, kilichopo Ubungo Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Kirowi Suma. Kulia ni Akoli Mbilinyi ambaye ni Ofisa Rasilimali Watu wa kiwanda hicho.

   Joel Bendera (kulia) akitembelea kiwanda hicho. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho. Kirowi Suma.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kibuku cha Darbrew Limited, Kirowi Suma (kushoto), akielezea mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kuhusu utendaji wa kiwanda hicho. Bendera alitembelea hivi karibuni kiwanda hicho kilichopo Ubungo Dar es Salaam.
   Bendera akipata maelezo kuhusu uzalishaji bora wa kinywaji cha asili cha kibuku kiwandani hapo
   Bendera akiwa ndani ya kiwanda hicho kilichopo Ubungo karibu na Kituo Kikuu cha Mabasi
   Bendera akiwa na baadhi ya viongozi wa kiwanda hicho alipotembelea kiwanda hicho
  Bendera akiondoka baada ya kumaziza ziara kiwandani hapo

older | 1 | .... | 117 | 118 | (Page 119) | 120 | 121 | .... | 1903 | newer