Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1167 | 1168 | (Page 1169) | 1170 | 1171 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Muonekano wa Picha ya Mtambo wa kisasa wa ED–XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ambao umezinduliwa  rasmi Mkoani Mbeya.

  Na EmanuelMadafa,JamiiMojablog 

  OFISI ya Mkemia Mkuu wa Serikali, leo imezindua  na kusimika mtambo mpya wa ED-XRF utakao tumika kufanya uchunguzi wa sampuli na vielelezo mbalimbali vikiwemo vya makosa ya jinai.

  Akizungumzia Mtambo huo, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele,alisema lengo kuu ni kurahisisha shughuli za kimaabara pamoja na usimamizi wa sheria zilizo chini ya wakala hiyo.

  Alisema, baadhi ya kazi zitakazofanywa na maabara hiyo ni kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa, sampuli za mazingira, sampuli zinazohusisha makosa ya jinai kama vile sampuli za vinasaba na dawa za kulevya.

  “Awali vipimo vya namna hii vilikuwa vikifanyika Jijini Dar es Salaam tu, ofisi za mikoa zilikuwa zikifanya kazi ya kukusanya sampuli na kusafirisha lakini sasa mtambo huu, umesimikwa Mbeya na utatumiwa na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kufanya kazi hiyo“alisema  

  Amesema maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali ni taasisi pekee ambayo inafanya uchunguzi wa vielelezo vya sayansi ya makosa ya iinai ili kusaidia vyombo vya sheria hususani jeshi la polisi na mahakama katika kufanya uchunguzi ili kutoa haki kwa jamii.

  “Maabara inachaangia katika kutekeleza sera ya afya ya mwaka 2007 kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara  kwa kuhakiki ubora na usalama wa bidhaa zinazo zalishwa viwandani “alisema Profesa Manyele.

  Amesema maabara ya Mkemia mkuu wa serikali inasimamia utekelezaji wa sheria ya usimamizi wa udhibiti wa kemikali na majumbani sura  182 na sheria ya usimamizi wa teknolojia ya vinasaba vya binadamu sura 732009.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul Ntinika ametoa wito kwa viwanda ,mashirika wajasiriamali na wananchi kwa ujumla kutumia huduma zinazotolewa na maabara ya mkemia mkuu wa serikali ili kuhakiki ubora wa  bidhaa zinazozalishwa  viwandani.
  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Paul Ntinika (kushoto) pamoja na Mkemia Mkuu wa Serikali (kulia  aliyeshika utepe Profesa Samwel Manyele  kuashiria uzinduzi rasmi wa mtambo wa kisasa wa ED–XRF ajili ya uchunguzi wa kimaabara mkoani mbeya.
  Mkemia Mkuu wa Serikali Profesa Samwel Manyele akizungumza katika uzinduzi rasmi wa mtambo wa kisasa kwenye kikao cha uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED–XRF kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara ,ambapo hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa hospital ya Mkoa jijini Mbeya.
  Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Ndugu Paul Ntinika akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED–XRF  kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara leo Machi 10 katika hospital ya Mkoa jijini Mbeya.

  Wadau kutoka taasisi mbalimbali mkoani mbeya wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa mtambo wa kisasa wa ED–XRFkwa ajili ya uchunguzi wa kimaabara.
  Meza Kuu katika Picha ya Pamoja na wageni waalikwa.Picha David Nyembe
  0 0  Diwani wa Kata ya Kilungule Mh. Saidi Fella leo amepokea msaada wa vitabu vya kufundishia na  kujifunzia kwa wanafuzi wa shule za msingi pamoja na Sekondary kutoka kwa rafiki zake wa Oxford University Press Tanzania, Vitabu hivyo vimegawiwa katika shule ya msingi Charambe, Chemchem pamoja na Kingugi na kwa upande wa Sekondary ni Charambe na

  Diwani Saidi Fella amewashukuru Oxford na kuwasisitiza wanafunzi kusoma kwabidii kupitia vitabu lakini pia kuvitunza kwa maana ya wadogo zao kuju kuvitumia vitabu hivyo kwa baadae, hata hivyo amewata walimu kuhakikisha wanavipiga mihuri vitabu ili wanafunzi wanapo azima kwenda kusoma nyumbani wakumbuke kuvirejesha.

  Maria Mlay kutoka Oxford amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii kupitia vitabu hivyo ili kutimiza ndoto zao katika maisha lakini pia kuvitunza vitabu hivyo.

  Aidha Saidi Fella amewashukuru Oxford kwa mchango huo wa vitabu katika kata yake na ameendelea kusisitiza wadua kuendelea kumsapoti katika kata yake ya Kilungule kwani ni Kata mpya na bado inamaitaji mengi zaidi ya miundo mbinu, Afya pamoja na Elimu.

  Picha ya Pamoja wanafunzi na walimu baada ya kupokea vitabu


  0 0
  TAARIFA:


  SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO) linakanusha Taarifa iliyotolewa na Shirika la Maji Safi na Maji taka jijini Dar es Salaam (DAWASCO), kuhusu kukosekana kwa Huduma ya maji kwa siku ya Jumapili  tarehe 12/03/2017 kwa wakaazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani  ili kupisha TANESCO kufanya matengenezo ya ukamilishaji kazi ya  kuunganisha umeme kwenye mtambo mpya wa maji wa Ruvu Juu.

  Aidha, Taarifa hiyo ya DAWASCO iliainisha kuwa ukosefu huo wa Huduma ya maji unatokana na matengenezo yatakayofanywa na TANESCO kwa siku husika.(12/03/2017).
  TANESCO inapenda Umma ufahamu yafuatayo;
  Mosi,  TANESCO ilipokea ombi  la DAWASA kupitia Mkandarasi wao (M/s Mollel Electrical Engineering) wiki iliyopita la kuomba kuzimwa umeme ili wakamilishe kazi ya mradi wa kuongeza mashine za kusukuma maji kwenye kituo cha Ruvu juu kilichopo Mlandizi, kupitia mradi huo mashine nne zinazohitaji megawati 2 kila moja zimefungwa.
  Wataalam wa TANESCO waliishauri DAWASA wajenge laini ya kilovolti 33 kutoka Chalinze hadi Mlandizi ili kuzipatia umeme  mashine hizo mpya walizoongeza.
  Pili,  Baada ya wataalam wa TANESCO kutembelea eneo hilo na kufahamu uharaka wa mradi huo wa maji kwa Wananchi ilishauri DAWASCO kwa barua kuwa umeme uzimwe siku ya ijumaa tarehe 10/03/2017 ili Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi hiyo, ushauri ambao DAWASCO iliupinga wakiomba umeme uzimwe siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ili wapate muda wa kuwaarifu Wateja wao na TANESCO iliridhia.
  TANESCO imeshangazwa na Taarifa hiyo ya DAWASCO kuwa TANESCO inafanya matengenezo ambayo yatapelekea ukosefu wa huduma ya maji huku ikitambua TANESCO inatekeleza ombi lao walilolileta.
  Tunasisitiza kuwa,  taarifa za TANESCO kufanya matengenezo si za kweli na uzimaji umeme siku ya Jumapili tarehe 12/03/2017 ni kwa ajili ya kupisha Mkandarasi wa DAWASCO kufanya kazi kama walivyoomba na  si TANESCO.
  Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu.

  0 0


  Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili ukumbini kuendesha kikao cha Kamati Kuu ya CCM mjini Dodoma leo. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein na  kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

  Mwenyekiti wa chama cha CCM, Rais Dkt Magufuli akiwakaribisha wajumbe kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM na kufungua kikao hicho mapema leo asubuhi,kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar).Dkt Shein,wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman .
   

  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati Kuu kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,leo mkoani ni Dodoma,Kulia Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar).Dkt Shein.
  Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi,Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha kamati kuu ya CCM, mapema leo Mkoani Dodoma.
  Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akizungumza jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi Hamphrey Polepole mapema leo kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu,mjini Dodoma 
  Wajumbe wa Sekretarieti wakijadiliana jambo ukumbini kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
  Kikao cha kamati kuu ya CCM kikendelea.


  0 0

  Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali halisi ya mgogoro uliopo .
  Magari yaliyokuwa yamebeba wajumbe wa kamati hiyo yakiwa yameegeshwa baada ya wananchi kuzuia msafara huo wakishikiza kamati kusikiliza kero walizokuwa nazo.
  Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
  Wajumbe wa kamati hiyo wa kuzungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
  Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
  Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati hiyo.

  Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.


  Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero zao.


  Katika Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro  uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.


  Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara


  Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.


  Wajumbe wa kamati ya Ardhi,Maliasili na Utalii waliozungumza na Clouds Tv ,Sebastian Kapufi na Dkt Godwin Mollel wamesema hatua ya wafugaji hao kuzuia msafara wa kamati ililenga kuvuruga ziara hiyo.


  Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii wakiwemo wataalamu na wanasheria imewasili Loliondo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi,Atashasta Nditiye na kufanya ziara ya kutembelea eneo lenye ukubwa kilomita 1500 za mraba linalokusudiwa kurejeshwa katika hifadhi .


  Eneo hili linatajwa kuwa na vyanzo vingi vya maji yanavyotiririka katika mto Gurumeti  unaopita katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti ambao ni muhimu kiikolojia kutokana na maji yake kutumiwa na wanyama pori katika hifadhi hiyo.


  0 0


  DISCOUNT RATE REDUCTION SHOULD MAKE BANKS THINK ABOUT LENDING RATES
  The Bank of Tanzania Governor, Prof. Benno Ndulu, has urged banks and financial institutions to take note of the downward review of the discount rate from 16 per cent to 12 per cent in their operations.
  “The Bank of Tanzania’s expectations are that the move will enhance credit growth and reduction in lending rates, he said.
  Prof. Ndulu made the call during a meeting with chief executive officers (CEOs) of banks and financial institutions at the Bank of Tanzania headquarters in Dar es Salaam.
  He, however, cautioned them, when disbursing loans, to ensure that only customers with good track record are being considered. This is due to the recent increase in non-performing loans (NPLs) among many banks.
  The Bank of Tanzania reviewed the discount rate from 16 to 12 per cent effective from March 6, 2017. In its letter to banks, the Bank said the revised discount rate took into account the prevailing 91 and 182-day weighted average yields and the monetary policy stance geared towards sustaining price stability. It will also be used to discount Treasury securities.
  On their part, CEOs of banks and financial institutions sought assurance from BoT as to the duration of being in force of the newly announced discount rate, lest they adjust their loan policies only for the discount rate to move upward without a warning.
  The Governor assured them that the rate can hold for a while and that any adjustments would depend on prevailing economic conditions, but assured them that such changes will not be drastic.
  Earlier, the CEOs of banks and financial institutions were briefed about the economic trends nationally, regionally and globally.
  Nationally, Tanzania attained a 7 per cent GDP growth during the 2016 which is a good record in the region, the leading sector being mining and quarrying followed by transportation and storage, power generation and manufacturing.
  Headline inflation increased to 5.5 per cent in February 2017 from 5.2 per cent the previous month. He attributed the increase to food prices.
  The risk of upward inflationary pressures may persist in the coming few months due to rising food prices.
  The Governor said the Bank of Tanzania would continue to be cautious of the risk of inflationary pressures coming from the food supply outlook in the East African Community and Southern African Development Community and would be ready to take appropriate measures
  Monetary aggregates sustained slow growth of 2.9 per cent in the year ending December 2016 as against 18.8 per cent growth recorded in the corresponding period in 2015. The slow growth is attributed to decline in net foreign assets of the banking system and net credit to the government.
  Also credit to the private sector grew by only 7.2 per cent in the year ending December 2016, compared with 24.8% in the year ending December 2015. This was associated with banks’ elevated cautiousness in lending in the face of increase in non-performing loans (NPLs) and low foreign budgetary inflows
  The report said however, that the shortfall was partially compensated by Increase in transaction velocity.
  During the period under review, current account deficit narrowed by 47 per cent, driven largely by increase in receipts from tourism gold and traditional exports, decrease in import bill, mainly of oil, consumer goods, building and construction, machinery and transport equipment.
  The government’s official reserve amounted to US $4,331.7.6mn at the end of January 2017, which is about 4.2 months of projected imports.
  Exports in 2016 grew by 4.1 per cent to US $9,285.6m, mainly driven by gold due to recovery of world market price and increase in export volume, travel receipts on account of increase in number of tourist arrivals and ttraditional goods consistent with increase in prices of some commodities in the world market.
  The value of imports in 2016 was $10,774.5m, which is 13.9 per cent lower than the value for 2015. Imports were largely for machinery, transport equipment, building and construction materials and consumer goods. Value of oil imports declined by 4.9 per cent due to fall in the world market prices.
  Zanzibar recorded GDP growth of 4.4 per cent during the first three quarters of 2016 compared with 8.0 per cent in similar period of 2015. The decline in growth was attributed to decline in the slower growth in construction, and information and communication activities. Major contributors to growth were: arts and entertainments, finance and insurance, mining and quarrying and administrative and support services.
  CEOs of Banks were told that global and domestic conditions remain favorable for continued price stability and that the Bank of Tanzania will continue to manage liquidity short-term liquidity fluctuations with using various monetary instruments., with the reduction of discount rate also contributing to ease liquidity conditions among banks.
  The Governor meets CEOs of commercial banks every two months to discuss about economic trends and get feedbacks from them.
  Issued by:
  PUBLIC RELATIONS AND PROTOCOL DEPARTMENT
  March 10, 2017

  0 0


  Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
  Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
  Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya mauzo ya shirika la ndege la Condor Bw. Andre Horn muda mfupi baada ya TTB na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius kusaini makubaliano ya ushirikiano. 


  Na: Geofrey Tengeneza -Berlin

  Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano baina yao katika kutangaza wa nchi hizo mbili kwa pamoja katika baadhi ya masoko ya masoko ya Marekani, China, Australia, India na masoko mengine barani la Ulaya. 

  Mkataba huo uliosainiwa leo katika maonesho ya Utalii ya ITB na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambao ni Bi Devota Mdachi kwa upande wa Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Kelvin Ramkaloan kwa upande wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius una lengo kuvutia watalii zaidi kutoka barani Ulaya, Amerika na Asia. 

  Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi amesema kuwa katika mkataba huo wamekubaliana kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi hizo mbili sambasamba na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea Mauritius ambayo ni maarufu kwa utalii wa fukwe wanatembela pia Tanzania kwa ajili ya utalii wa kutazama wa wanyama katika hifadhi zetu mbalimbail za Taifa , kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea maeneo mengine ya vivutio vya utalii. 

  “Tutazitangaza nchi zetu kama maeneo pacha ya utalii lengo likiwa ni kutumia fursa ya watalii wanaotembelea Mauritus kwa ajili utalii wa fukwe kuunganisha safari zao na kujakutembela pia Tanzania kupitia shiika la ndege la Mauritus kwa ajili ya kujionea vivtio vyetu kama vile wanyama , mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, na vingine vingi ambavyo Mauritus hawana.” alisema Bi Devota Mdachi.

  0 0

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Akiwaongoza wakazi wa Jiji la Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika jijini Mbeya akiwa ameambatana na aibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Pamoja na Wadau Mbalimbali waliojitokeza kwenye Mbio hizo leo.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Leo ameongoza Wakazi wa Mkoa wa Mbeya kwenye Mbio za Tulia Marathoni zilizoandaliwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu Kupitia Taasisi yake ijulikanayo kama Tulia trust. Mbio hizo zilizohusisha KM 21 ,KM 5 na KM 2 kwa wazee zilifana baada ya Wakazi Wengi wa Mbeya Kujitokeza kwa Wingi Wakiwemo Viongozi Mbalimbali na Mabalozi wanaoziwakilisha Nchi zao Hapa Nchini,Lengo la Mashindano hayo ni kupata fedha kwa ajili ya uboreshaji wa huduma za afya na elimu hususani uboreshaji Majengo na vyoo katika sekta hizo.
    Rais wa Chama cha Riadha Nchini na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mh Anthony MtakaAkimweleza Jambo Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Tulia Ackson Mwansasu kabla ya Mbio za Tulia Marathoni zilizofanyika Jijini Mbeya leo wakiwa Pamoja na  Pamoja naAfisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange
   Tulia Marathon lengo lake ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya na elimu, maeneo yanayolengwa kwenye afya ni Kituo cha Afya cha Ruanda kilichopo Mwanjelwa na Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Makandana ambako utafanyika uboreshaji wa wodi ya wazazi,”

   Katika Elimu maeneo yanayokusudiwa kuboreshwa ni pamoja na Shule ya Wasichana ya Loleza ambayo itafanyiwa maboresho kwenye mabweni mawili na vyoo pamoja na shule tatu za msingi,” alisema Lwiza.Mshindi wa Mbio hizo Amejishindia kitita cha Sh. Milioni moja wa Pili Sh. 700,000 na wa tatu atapata Sh. 500,000.Katika Mbio fupi za kilomita mbili ambazo ziliwahusisha wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo Naibu Spika Mwenyewe .
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye Katika Picha ya Pamoja na Afisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange  Waliposhiriki Mbio Hizo leo Jijini Mbeya.

   Rais wa Chama cha Riadha Nchini na Mkuu wa Mkoa wa Simuyu Mh Anthony Mtaka akiwa na Afisa Mtendaji wa Shear Illusions Tanzania Mama Shekha Nasser ( Kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa GS1 Tanzania Mama Fatma Kange pamoja na Mdau Hassan Ngoma.  0 0


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akielezwa jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo. kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akielezwa jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo.


  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akishiriki kikao cha NEC mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipokuwa akimfafanulia jambo kabla ya kuanza kwa kikao cha NEC mjini Dodoma leo
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akishiriki kikao cha NEC mjini Dodoma leo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo wakati wa mkutano wa NEC mjini Dodoma leo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na mjumbe kutoka mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa katika kikao cha NEC mjini Dodoma leo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha NECmjini Dodoma leo kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein .

  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Dk. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati akifungua kikao hicho leo kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana kabla ya kuanza kwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kikao hicho kufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kikao hicho kufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Dodoma.
   Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana akizungumza mara baada ya kikao hicho kufunguliwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mkoani Dodoma.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
   Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.
  Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika foleni ya kuchukua chakula pamoja na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mkoani Dodoma.

  0 0  0 0

  Mgeni rasmi, Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Mwanza, Kizito Wambura (kulia), akikabidhi kombe kwa washindi wa mashindano hayo yaliyofanyika leo katika viunga vya shule ya msingi Nyamagana.

                                                                         #BMGHabari
  Wanafunzi wa shule ya msingi Nyamagana wameibuka washindi kwenye mashindano elimishi kwa klabu za mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani dhidi ya wakubwa zao kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma, zote za Jijini Mwanza.

  Mashindano hayo yaliyoandaliwa na taasisi ya kutetea haki za mtoto mfanyakazi wa nyumbani (WoteSawa) ya Jijini Mwanza, yalijumuisha michezo mbalimbali ikiwemo maigizo, ngonjera pamoja na mashairi yenye jumbe za kuainisha aina za ukatili wanaokumbana nao watoto wafanyakazi wa majumbani ikiwemo vipigo, utumikishwaji na fursa ya kukosa elimu, na kuiasa jamii kuachana na vitendo hivyo.

  "Ukiona mtoto anatendewa ukatili wa aina yoyote, paza sauti (toa taarifa) sehemu mbalimbali ikiwemo WoteSawa, polisi kupitia kitengo cha dawati la jinsia, kwa Mwenyekiti wa Mtaa ama Mtendaji wa Kata". Amesisitiza mgeni rasmi, Wambura.

  Naye Mkurugenzi wa taasisi ya WoteSawa, Angel Benedicto, amebainisha kwamba bado watoto wafanyakazi wa majumbani wanakabiliwa na vitendo mbalimbali vya ukatili ikiwemo kutumikishwa kwa kuajiriwa ili kutembeza bidhaa mtaani kwa ujira mdogo, kunyimwa fursa ya kusoma pamoja na vipigo kutoka kwa baadhi ya waajiri hivyo taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu katika jamii ili kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.

  "Lengo ni kupunguza ukatili wa watoto majumbani, kulinda haki za watoto, kuibua vipaji ikiwemo uchoraji na uigizaji ili kuvitumia katika kufikisha elimu ya kupambana na ukatili dhidi ya watoto". Imefafanua sehemu ya risala ya klabu za wanafunzi mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya msingi Nyamagana na Nyakurunduma sekondari, iliyosomwa na Neema Christopher. 
  Shule ya msingi Nyamagana wakifurahia ushindi wao ambapo igizo wamepata asilimia 93 dhidi ya 92 za Nyamagana sekondari, Shairi Nyamagana wamepata asilimia 74 dhidi ya 85 za Nyakurunduma huku Ngonjera Nyamagana wakipata asilimia 91 dhidi ya 77 za Nyakurunduma. Ushindi wa jumla, shule ya Msingi Nyamagana wamepata asilimia 86 dhidi ya 85 za Nyakurunduma sekondari.
  Mabalozi kutoka shule ya sekondari Nyakurunduma wakipokea kombe baada ya kushika nafasi ya pili kwenye mashindano hayo
  Pia mabalozi wote wamepatiwa vyeti kwa kujitoa kuwa mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani
  Mabalozi wakipokea vyeti
  Mabalozi kutoka shule ya msingi Nyamagana wakionesha makali yao katika ngonjera na mashairi
  Mabalozi kutoka Nyakurunduma sekondari wakighani mashairi na ngonjera
  Afisa Ustawi wa jamii Jijini Mwanza, Davis Justine (katikari) akitoa matokeo ya mashindano hayo kwa niaba ya majaji wengine
  Mkurugenzi wa WoteSawa, Angel Benedicto, akizungumza wakati wa mashindano hayo
  Diwani wa Kata ya Nyamagana, Bhiku Kotecha, akizungumza kwenye mashindano hayo
  Taasisi ya WoteSawa imechora mchhoro huu katika shule ya Msingi Nyamagana, ukiwa na jumbe mbalimbali ikiwemo "Mpe elimu siyo kumuajiri kazi za nyumbani" ikiwa ni mwendelezo wa kufikisha elimu juu ya mapambano dhidi ya ukatili wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani.
  Mgeni rasmi akizungumza jambo kwenye mashindano hayo na kuzindua pia mchoro huo
  Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya sekondari Nyakunduruma Jijini Mwanza wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
  Mabalozi wa mtoto mfanyakazi wa nyumbani kutoka shule ya shule ya msingi Nyamagana Jijini Mwanza wakiwa na vyeti vyao walivyotunukiwa na taasisi ya WoteSawa
  Mabalozi wote wakiwa kwenye picha ya pamoja

  0 0

  Muswada binafsi wenye lengo la kutungwa kwa sheria ya kuwalinda albino umewasilishwa kwenye kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda. Muswada huo umewasilishwa bungeni na Mheshimiwa Shyrose Bhanji, mbunge wa Tanzania. Katika muswada huo, Bhanji ameelekeza haki za msingi zinazopaswa kutolewa kwa walemavu hao kutoka Serikalini, Taasisi binafsi na kwenye jamii zetu. Muswada huo kama utapitishwa na Bunge na hatimaye kukubalika na Marais wa Afrika Mashariki, utatumika kwa nchi zote za Afrika Mashariki na utakuwa umesaidia watu wenye Ualbino. Mheshimiwa Shyrose Bhanji[/caption] "Ninamshukuru Mungu kwa fursa hii, " anasema Bhanji huku akisema kwamba kwake yeye jana ilikuwa ni siku ya furaha kubwa kwani hatimaye aliweza kuwasilisha bungeni muswada huo binafsi ambao unaoitwa The EAC Protection Of People with Albinism Bill 2017. Mwanamuziki mahiri nchini Chege Chigunda aliandika katika page yake ya Instagram ambapo alimpongeza mbunge huyo kwa namna anavyofikiri na kutetea walemavu aliandika: “Hongera sana Mbunge wetu wa Afrika Mashariki Mhe. ShyRose Bhanji @shyrosebhanji kwa kupigania haki za ndugu zetu wenye ualbino. Hakika umeacha alama kubwa ya uwakilishi wako Tanzania na Afrika Mashariki. Tunajivunia.”
  Kipande cha nakala ya muswada huo.

  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwahutubia wajumbe wapatao 2356,ambapo walipaswa kuwa wajumbe 2380 katika mkutano huo Mkuu Maalum wa CCM uliokuwa na lengo kuu la kufanya baadhi ya mabadiliko ndani ya Katiba ya chama hicho,ambapo mabadiliko hayo yamepitishwa kwa asilimia 100 na wajumbe hao waliohuhudria mkutano huo.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum mjini Dodoma.

  Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.

   Sehemu ya baadhi ya wajumbe wa mkutano huo pamoja na wageni waalikwa wakiwa tayari ukumbini.
   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Kikwete wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano mkuu wa CCM, Mjini Dodoma
   Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akisalimiana na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,Waziri Mkuu Mh. Kasim Majaliwa wakati akiwasili katika ukumbi wa mkutano huo.
    Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwa pamoja na viongozi wengine wastaafu wa Serikali na kichama walipowasili kwenye ukumbi wa mkutano na kukaribishwa na wajumbe.
   Mabalozi na wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali  ndani na nje ya nchi wakiwa wamehudhuria Mkutano Mkuu Maalum wa CCM,mjini Dodoma.

  0 0

  MBUNGE wa Viti maalum Wanawake mkoani Ruvuma, Jackline Msongozi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameipongeza serikali ya awamu ya tano kupitia Wakala wake wa barabara Tanroads mkoani hapa, kwa kusimamia na kukamilisha ujenzi wa barabara kiwango cha lami inayounganisha upande wa Mangaka mkoani Mtwara hadi Namtumbo mkoani Ruvuma kwa madai kuwa baadhi ya wanawake wameanza kunufaika na mradi huo kiuchumi kutokana na kuuza bidhaa mbalimbali.

  Msongozi alisema hayo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani ambapo kiwilaya yalifanyika katika viwanja vya soko la Mjimwema lililopo mjini Songea.Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kumechochea kasi ya maendeleo kwa akina mama wajasiriamali kujiinua kiuchumi kutokana na kuanzisha biashara ndogo ndogo pembezoni mwa barabara hiyo pamoja na kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

  Aidha amewataka wanawake hao kutumia fursa ya kukamilika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, kujikita kwenye shughuli za uzalishaji mali ikwemo katika nyanja ya kilimo na ufugaji kwa lengo la kujipatia kipato badala ya kuwa tegemezi.

  Mbali na mambo mengine Mbunge huyo ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, amewapongeza pia wanawake hao kwa kuonesha moyo wa ujasiri katika kugombea nafasi mbalimbali za uongozi za kisiasa mkoani humo.

  Awali akisoma risala kwa niaba ya wanawake wenzake mbele ya mgeni rasmi, Joyce Mwanja alisema kuwa kutokana na uhamasishaji wa wanawake wengi kujiunga katika vikundi vya uzalishaji mali kumesaidia kuongeza uelewa na ari ya utendaji kazi kiuchumi ambapo jumla ya vikundi 300 vya wanawake wazalishaji mali vimeundwa mjini hapa.

  Mwanja alisema kuwa katika kipindi hicho chote shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zimefanyika ikiwemo usindikaji, kilimo, uanzishwaji wa magenge ya kuuzia biashara, ufugaji, kilimo, ufumaji na uhifadhi wa mazingira ambapo katika kipindi cha mwaka 2014/2015 hadi mwaka 2016/2017 jumla ya vikundi 172 vya wanawake wajasiriamali vimepatiwa mikopo midogomidogo yenye masharti nafuu yenye thamani ya shilingi milioni 87.1.Habari na www.ruvumatv.com

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akizungumza na Mjumbe Maalum, Balozi Harro Adt aliyewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Kansela wa Ujerumani, Mhe. Angela Merkel kwenda kwa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Pamoja na mambo mengine walizungumzia pia namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.
  Mazungumzo yakiendelea.
  Waziri Mahiga akiagana na Balozi Adt mara baada ya kumaliza mazungumzo. 
  Waziri Mahiga (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mjumbe Maalum, Balozi Adt (wa nne kushoto) pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizarani pamoja na Ubalozi wa Ujerumani nchini. 

  =================================================== 
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa Tanzania na Ujerumani zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo yale yanayohusu kudumisha amani na usalama duniani pamoja na kuheshimu misingi ya haki za binadamu kupitia Jumuiya za Kikanda na Kimataifa.

  Mhe. Waziri Mahiga ameyesema hayo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Harro Adt, Mjumbe Maalum wa Kansela wa Ujerumani, Mhe. Angela Merkel kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha ujumbe huo.

  Katika mazungumzo yao, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa, Ujerumani na Tanzania zina mahusiano ya kihistoria tangu enzi za ukoloni hadi sasa. Katika masuala ambayo Tanzania inanufaika na ushirikiano huo ni pamoja na ujenzi wa miundombinu, maboresho katika sekta ya elimu na mchango katika uhifadhi wa wanayamapori.

  “Uhusiano wa Tanzania na Ujerumani ni wa kihistoria tangu ukoloni. Hata hivyo Ujerumani wamejaribu kutafsiri ushirikiano wetu katika misingi bora sasa kuliko ile ya kikoloni. Ujerumani imekuwa ikiisaidia Tanzania moja kwa moja katika sekta mbalimbali kama elimu, wanyamapori na miundombinu na misaada mingine imekuwa ikipitia Umoja wa Ulaya” alisema Waziri Mahiga.

  Akizungumzia ziara ya Balozi Adt nchini, Mhe. Waziri Mahiga alisema Mjumbe huyo Maalum wa Kansela wa Ujerumani ameleta ombi kwa Mhe. Rais na kwa Watanzania la kuiunga mkono Ujerumani kwenye nafasi ya Mjumbe asiye wa Kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa uchaguzi utakaofanyika mwaka 2018. Aliongeza kusema kuwa, Ujerumani imedhamiria kugombea nafasi hiyo ikiwa na dhamira ya kuunga mkono mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwemo kuziunga mkono nchi za Afrika kwenye harakati za kupatiwa nafasi mbili za kudumu kwenye Baraza hilo.

  Aidha, Mhe. Waziri Mahiga alifafanua kwamba, katika kufikia malengo hayo Ujerumani imejiwekea misingi mikuu minne ambayo ni:- Kusaidia jitihada za amani na usalama duniani; Kusimamia Haki ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa; Kuhamasisha mageuzi ya Teknolojia na Kuhimiza ushirikiano na Ubia wa Kimataifa.

  Mhe. Mahiga alieleza kuwa kwa kuzingatia misingi hiyo, amemueleza Balozi Adt azma ya Tanzania kuiomba Ujerumani iisadie Afrika kujenga Jengo la Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu ambapo Tanzania ndio Makao yake Makuu huko Mjini Arusha.

  Mhe. Mahiga pia alimhakikishia Balozi Adt kuwa ameupokea ujumbe wa Kansela wa Ujerumani na atauwasilisha kwa Mhe. Rais.

  Kwa upande wake Balozi Adt, Mjumbe Maalum kutoka Ujerumani alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata baada ya kuwasili nchini. Pia ana imani kuwa Tanzania ambao ni rafiki wa kihistoria wa Ujerumani itawaunga mkono kwenye nafasi hiyo ili kuwawezesha kutekeleza malengo waliyojiwekea ikiwemo kuhakikisha Afrika inapata nafasi mbili za kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Imetolewa na:
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, 
  Dar es Salaam, 12 Machi, 2017

  0 0

  RAIS wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Mrisho Kikwete (JMKF) .

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na taasisi hiyo, uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na baada ya uzinduzi huo, Dk. Kikwete ataendesha kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo.

  Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na maendeleo endelevu.Aidha taasisi hiyo itajikita katika maendeleo endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umasikini, kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za tabianchi.

  Taasisi hiyo itasaidia pia katika afya ya mama na mtoto, kukabiliana na ugonjwa wa malaria na kuboresha lishe ya wananchi.Katika elimu, itaboresha elimu katika kuwasaidia wajasiriamali kwa mafunzo na pia itasaidia katika utawala bora na utafutaji amani.

  Taasisi hiyo imesajiliwa na itakuwa chini ya uongozi wa bodi ya wadhamini wa kimataifa yenye wajumbe kutoka ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Guinea Bissau na Marekani.

  Wajumbe kutoka Tanzania ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, Daktari Bingwa wa Upasuaji Profesa William Mahalu, Balozi Mwanaidi Maajar, Genevive Sangundi na Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la makampuni ya SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa.

  0 0

  Picha ya mchoro wa binadamu wa kale wakitembea katika eneo la Laetoli lililoko km 45 kusini mwa Olduvai gorge. 
  Na Geofrey Tengeneza- Berlin.

  Nyayo na picha za michoro ya binadamu wa kale (zamadamu) zinazooneshwa katika banda la Tanzania kwenye maonesho ya Kimataifa ya ITB yanayoendelea hapa Berlin Ujerumani sambamba na maelezo sawia ya historia yake inayotolewa na mhifadhi wa Paleontolojia (masalia ya kale) Dkt. Agnes Gidna kutoka Makumbusho ya Taifa Bi wakishirikiana na maafisa waandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania inawapagaisha maelfu ya wageni wanaotembela banda la Tanzania katika maonesho hayo.

  Nyayo na michoro hiyo ya binadamu wa kale anayesadikiwa kuishi miaka takribani milioni 4 iliyopita katika eneo la Laetori kilometa 45 kusini mwa Oldvai gorge pamoja na vielelezo mbalimbali vya vivutio kadhaa muhimu vya Tanzania kama vile mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro, wanyama wanaohama katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti n.k vimekuwa chachu ya kuvutia wageni wanaotembelea banda la Tanzania ambao pia wameonesha dhamira kubwa ya kuitembelea Tanzania.

  Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi pamoja na utangazaji mkubwa wa vivutio mbali mbali vya utalii vya Tanzania unaofanywa katika maonesho haya, TTB imeamua pia mwaka huu kuweka mkazo maalumu katika kuitangaza Tanzania kama chimbuko la binadamu wa kale.
  Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania Bw. Geofrey Meena (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa wageni kuhusu vivutio mbalimbali vilivyopo Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania katika maonesho ya ITB.
  Mhifadhi wa Masalia ya kale (Palentolojia) wa makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Gidna akitoa maelezo kuhusu historia ya binadamu wa kale pamoja na nyazo zake zilizo umbuliwa Laetori Tanzania kwa wageni wanaotembelea banda la Tanzania .
  Mtangazaji wa kituo cha Umma cha televisheni cha Ujerumani Bw. Hoeks akifanya mahojiano mubashara na Mhifadhi wa Palentolojia wa Makumbusho ya Taifa Dkt. Agnes Digna mbele picha ya mchoro na nyayo za zamadamu ndani ya banda la Tanzania lililopo katika maonesho ya ITB Berlin Ujerumani.

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo na Warsha ya Wanahabari za michezo  juu ya maadili ya utangazaji kwenye radio na Televisheni na kuzingatia taaluma
   Mwandishi wa habari mkongwe kutoka kituo cha Azam Televisheni , Baruani Muhuza akitoa somo kwa wanahabari hao walifika katika mkutano huo juu ya umuhumu wa weledi wa taaluma
   Mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya Superdoll, Jamal Baiser akizungumza wakati wa mafunzo hayo kwa watangazaji wa waandishi wa habari za michezo
   Evance Mhando akichangia mada katika mkutano huo ambao uliweza kuwajenga watangazaji kufuata weledi
   Mwalimu Alex Kashasha akitoa mada juu ya kuwaleta wasikilizaji na watazamaji kuwa sehemu ya watu waliopo uwanjani pasipo kusababisha mfarakano wa moyo na kulaumu marefa na wachezaji kutokana na aina ya utangazaji tulionao sasa
   Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifuatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo

   Baadhi ya washiriki wa Semina hiyo wakifatilia kwa makini  masomo yalikuwa yakitolewa katika mafunzo hayo
   Msemaji wa shirikisho la Soka nchini ,Alfred Lucas Mapunda akizungumza juu ya watangazaji kusoma na kufuata kanuni za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara na mashindano mengine hili kuweza kuwa na majibu sahii pindi wanapokuwa wanatangaza mpira
  Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Superdol , Jamal Baiser akikabidhi zawadi kwa  Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari ambaye alimwakilisha waziri wa haabri Vijana utamaduni na Michezo Nape Nnauye

older | 1 | .... | 1167 | 1168 | (Page 1169) | 1170 | 1171 | .... | 1897 | newer