Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 10,2017


TECC - Vijana watakiwa kuchangamkia fursa za mafunzo ya ujasiriamali

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC), Bw. Sosthenes Sambua (katikakati) akizungumzia awamu ya pili ya program ya VIA Jiandalie Ajira ambayo imetangaza fursa za mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 kwa manispaa ya Mtwara, Mikindani, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais na Kujitegemea (PTF), Bi.Haigath Kitala na kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani (TECC), Bw. Sosthenes Sambua (wa pili kutoka kulia) akizungumzia awamu ya pili ya program ya VIA Jiandalie Ajira ambayo imetangaza fursa za mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana wenye umri wa miaka 18 hadi 24 kwa manispaa za Mtwara, Mikindani, Manispaa zote za Mkoa wa Dar es Salaam, Dodoma na Kibaha mkoani Pwani. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Rais na Kujitegemea (PTF), Bi.Haigath Kitala, wa pili kutoka kushoto ni Afisa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, na kushoto ni Bi. Zahra Mahmoud,Meneja Biashara wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA).

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,MALIASILI NA UTALII YATEMBELEA ENEO LENYE MGOGORO LA PORI TENGEFU LA LOLIONDO.

$
0
0
Msafara wa Magari ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Malisili na Utaalii,yakpita katika maeneo mbalimbali ya Pori Tengefu la Loliono kwa ajili ya kujionea hai halisi ya mgogoro ulioo katika eneo hilo.
Mwenyekii wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi ,Maliasii na Utalii,Atashasta Ndetiye (katikati) akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo kutizama vyanzo vya maji vilivyoko katika Pori Tengefu la Loliondo.
Waziri wa Malisili na Utalii ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo,Prof Jumanne Maghembe akiongozana na wataalamu katika ziara ya kamati hiyo.
Mtafiti Mkuu wa Idara ya Ikolojia (TAWIRI) Dkt Edward Khoi akitoa maelezo ya kitaalamu kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Malisili na Utalii wakati wakitembela Pori tengefu la Loliondo.
Baadhi ya wajumbe wa kamato hiyo wakifuatilia maelezo kutoka kwa wataalamu wa Ikolojia na Uhifadhi.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiwaeleza wajumbe w kamati hiyo madhara yatakayojitokea endapo eneo la Pori Tengefu la Loliondo halita hifadhiwa.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili na Utalii,wakitizama eneo linalotajwa kutengenezwa na wafugaji kwa ajili ya kunyweshea maji mifugo yao ndani ya Pori Tengefu la Loliondo.
Eneo linalouiwa na wafugaji unyweshea mifgo yao.
Sehemu ya Mabirik yanayotajwa kutengenezwa na jamii ya wafugaji kwa ajili ya kunywesha mifgo yao.
Mwenyekiti a Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Atashsta Ndetiye (kulia) pamoja na Waziri wa Malisili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe wakitizama eneo ambalo i mapiio ya maji katik Pori Tengefu la Loliondo.
Moja ya Makundi ya Ng'ombe yaliyokutwa na Kamati hiyo katika Pori Tengefu la Loliondo.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakizungumza na mmoja wa wafugaji waliokutwa wakichunga Ngombe ndani ya Pori Tengefu la Loliondo. 
Kamati ilikutana pia na Changamoto ya uboovu wa Miundombinu ya barabara hali iliyolazimu magari kupita kwa tahadhari .
Wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakitizama moja kati ya vyanzo vy maji vinavyotiririsha maji yake katika mto Gurumeti uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mbunge wa Jimbo la Sumve ambaye pia ni mjube wa kamati hiyo,Richard Ndasa akizungumza jambo mara baada ya kutizama moja ya vyanzo vya maji vilivyoko katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.
Sehemu ya Makundi ya Mifugo pamoja na Mashamba yaliyopo katika eneo la Pori Tengefu la Loliondo.


Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazinia

NSSF YAHAMASISHA WAKULIMA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS), wakati wa uhamasishaji wakulima wilayani humo. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania.
Meneja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Dodoma, Rehema Chuma, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao  (AMCOS), wakati uhamasishaji wa wakulima wilayani humo. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania. 
Meneja wa NSSF Mkoa wa Manyara, Alexander Josephat, akizungumza na viongozi wa Vyama vya Ushirika wa Mazao (AMCOS), wakati wa uhamasishaji wa wakulima wilaya ya Kiteto. Mpango huo umeanzishwa na NSSF kwa ushirikiano wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) na Benki ya Azania. 

DC GONDWE ANG'ARISHA SIKU YA WANAWAKE HANDENI

$
0
0


Mkuu wa Wilaya akitazama moja ya bidhaa na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na akina mama katika kutengeneza Tanzania ya Viwanda.

Kikundi cha kinamama cha umoja ni nguvu wakiwa wamebeba bango lao
Wanafunzi shule ya msingi Msule wakisheresha kwa ngoma wakati wa maadhimisho hayo
Mkuu wa Wilaya Mh. Gondwe akajumuika kucheza na kinamama kusherehekea sikukuu yao
Moja ya kikundi cha kinamama wakipokea cheti cha utambulisho kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.
Mkuu wa Wilaya akikata utepe kuashiria ufunguzi wa maonesho ya bidhaa za kinamama.

Mkuu wa Wilaya ya Handeni (suti nyeusi), akiambatana na kundi la wamamama na wanafunzi siku ya maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani kwenye maandamano iliyofanyika kata ya Kwamgwe Wilayani Handeni.
Mh. Gondwe akihutubia wananchi siku ya wanawake ambapo alieleza Halmashauri kutoa kipaumbele cha mikopo kwa vikundi vya kinamama na kulinda watoto wa kike kuhakikisha wanamaliza masomo yao bila kukwamishwa.

Diwani wa Kata ya Kwamgwe Bi. Sharifa Abebe akizungumza na wananchi wakati wa maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe akisoma moja ya bango la wanawake wa kikundi cha Umoja ni nguvu linaloonesha taswira ya mama aliebeba mtoto mgongoni, kichwani kabeba kuni na jembe na mkononi akiwa amebeba chakula huku mwanaume akiwa ameketi nyumbani kumngoja mama alietoka shamba aje kuandaa chakula.
Picha na Alda Sadango,Afisa Habari,wilaya ya Handeni

WAKURUGENZI WA SHIRIKA MISAADA YA KIMAENDELEO LA UINGEREZA WAWATEMBELEA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI UNAOTEKELEZWA NA TASAF WILAYANI KISARAWE,MKOANI PWANI.

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji waShirika la Misaada ya Maendeleo la Uingereza DFID katika Benki ya Dunia Bw.David Kinder amepongeza hatua iliyofikiwa na serikali ya Tanzania kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii –TASAF- katika kuteleza Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini,PSSN.

Bw. Kinder ametoa pongezi hizo baada ya kukutana na walengwa wa Mpango huo katika vijiji vya Mzenga A na Vilabwa katika wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ambako amejionea mafanikio makubwa yaliyopatikana katika sekta za uboreshwaji wa makazi,elimu,lishe na afya kwa walengwa hao.

Amesema hatua iliyofikiwa na walengwa hao inapaswa kuungwa mkono zaidi ili hatimaye waweze kuondokana na madhira ya umasikini unaowakabili.

Kwa upande wao, baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika vijiji hivyo wamesema tangu kuanza utekelezaji wa Mpango huo wameanza kuona fursa za maendeleo ikiwemo kuezeka mabati nyumba zao, kufuga kuku, na hata kuongeza shughuli za kilimo.

‘’Sikuwahi kuota kuwa siku moja nitamiliki na kuishi kwenye nyumba ya bati,lakini kupitia TASAF nimeweza , ninaishukuru sana serikali na TASAF kwa mpango huu mzuri’’ alisisitiza bi. Asha Khalifan Kikombe anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 70 hivi.

Amesema ili kufikia mafanikio hayo amekuwa akinunua mabati kidogo kidogo kila anapolipwa ruzuku hiyo na hatimaye kumwezesha kupata mabati yaliyotosheleza kuezeka nyumba yake na kuondokana na adha ya kuishi katika nyumba iliyoezekwa kwa majani.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kisarawe B. Happinness William Seneda ameshukuru nchi wahisani wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa kuiunga mkono serikali ya Tanzania katika jitihada za kuwaondolea kero ya umasikini wananchi wake.

Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika vijiji vya Vilabwa na Mzenga A pia hutekeleza mpango wa ajira ya muda kwa miradi wanayoibua wakati wa kipindi cha hari (kigumu) ukiwemo ukame,mafuriko na kisha kulipwa ujira ikiwa ni sehemu ya kuwaongezea kipato.


Bi.Asha Khalifan Kikombe mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotelezwa na TASAF katika kijiji cha Vilabwa ,Wilaya ya Kisarawe ,mkoani Pwani akiwaonyesha wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza (hawako pichani) nyumba aliyoezeka kwa mabati alizozinunua kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF
Ujumbe kutoka DFID wakiwa na baadhi ya watendaji kutoka TASAF na Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe wakipata maelezo ya mradi wa kutunza mazingira unaotekelezwa na walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa utaratibu wa Ajira ya Muda unaotekelezwa wakati wa kipindi cha hari kwa lengo la kuwaongezea walengwa kipato.
Baadhi ya walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Msikini katika kijiji cha Mzenga A wilaya ya Kisarawe wakishiriki katika mkutano ulioitishwa kuzungumzia mafanikio ya utekelezaji wa shughuli za Mpango uliohudhuriwa pia na wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.

Bi.Asha Khalifan Kikombe mmoja wa Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini unaotelezwa na TASAF katika kijiji cha Vilabwa ,Wilaya ya Kisarawe ,mkoani Pwani akiwaonyesha wageni kutoka Shirika la Misaada la Uingereza (hawako pichani) nyumba aliyoezeka kwa mabati alizozinunua kwa kutumia fedha za ruzuku kutoka TASAF.
Ujumbe kutoka Shirika la Misaada la Uingereza DFID ukipata maelezo kutoka kwa mmoja wa walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika kijiji cha Vilabwa juu ya namna alivyonufaika na fedha zinazotolewa na serikali kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jmii TASAF.

Benki ya NMB, Mastercard yawaingiza wakulima kidijitali

$
0
0
 
BENKI ya NMB imesaini makubaliano na Kampuni ya Mastercard kufanya kazi kiushirikiano ili kuhakikisha inaiinua sekta ya kilimo nchini Tanzania kwa kuanzishwa kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu waliokuwa wakiupata wakulima hapo awali. Huduma hiyo ya 'eKilimo’, ni jukwaa la kidigitali ambalo litamsaidia mkulima kupata uwazi na usalama wa bidhaa zake kimasoko na hata urahisi wa upatikanaji taarifa, huku ukiondoa urasimu uliokuwa ukifanywa na madalali sokoni, jambo ambalo wakulima wengi wamejikuta wakishindwa kunufaika kiufasaa kwa bidhaa zao. 
 
Ushirikiano huo umesainiwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker pamoja na Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Raghu Malhotra, ambapo kwa pamoja wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema huduma hiyo itawainua wakulima kwa kiasi kikubwa endapo itatumiwa na wakulima. Kwa upande wake, Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra, alisema kupitia huduma hiyo mkulima anaweza kufanya mauzo na kulipwa kwa kutumia simu iliyo na programu maalum huku benki ikipata taarifa, jambo ambalo litamrahisishia shughuli zake na kuokoa muda mwingi wa kuzunguka.
 
 Alisema takwimu zinaonesha kilimo kinachangia kiasi kikubwa cha fedha katika pato la taifa 'GDP', ambapo takribani shilingi bilioni 13.9 ikiwa ni takribani asilimia 30, hivyo kuna kila sababu ya kuinua sekta hiyo ili iendelee kufanya vizuri na pia kuwainua wakulima. "Kwa kutumia teknolojia ya kidigitali huduma hii italeta uwazi kwenye mchakato wa mauzo na ununuzi na kuongeza ufanisi katika eneo la ugavi, hivyo kuleta manufaa ya kiuchumi. 
 
Teknolojia inapaswa kusaidia wakulima kupata ufumbuzi kwa huduma za kifedha, hivyo kuwawezesha kuwa na maisha bora na familia zao hata baadae," alisema Rais wa Kampuni ya MasterCard barani Afrika, Bw. Malhotra. Akizungumzia huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker alisema lengo kubwa ni kumuwezesha mkulima kunufaika zaidi na kilimo anachokifanya, huku benki ikiendelea kujenga mazingira ya mteja kupata huduma bora na kuaminika ili aendelee kupata mikopo kwa shughuli za kilimo.
 
Alisema mkulima anapokuwa na uhakika wa kupata taarifa sahihi za masoko na kuweza kufanya mchakato mzima pasipo na urasimu hunufaika zaidi na kuendelea kuaminika kwa taarifa zake benki jamboa ambalo ananufaika moja kwa moja kupata mikopo ya kilimo, ambayo humuongezea tija. "Nia yetu sisi ni kukua sekta ya kilimo Tanzania, na ndio maana tumeshirikiana na Mastercard na kuja na teknolojia ambayo inaweza kubadilisha maisha ya wakulima. 
 
Uzoefu wetu katika sekta ya kifedha unatufanya kutafuta wadau kama Mastercard ambapo tumeona wamefanya vizuri nchini Kenya kuwasaidia wakulima kupitia programu ya '2KUZE'. Ndio maana nasi tumeungana kuhakikisha wakulima wadogo, wanunuzi na mawakala wananufaika kiuchumi," alisema Mkurugenzi Mtendaji, Bi. Bussemaker. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) pamoja na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra wakisaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali. Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin. Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB, Bi. Ineke Bussemaker (wa pili kushoto) wakibadilishana nyaraka za makubaliano na Rais wa MasterCard Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika, Bw. Raghu Malhotra (wa pili kulia) mara baada ya kusaini makubaliano ya kiushirikiano jijini Dar es Salaam kuhakikisha sekta ya kilimo nchini Tanzania inakuwa na kilimo mtandao 'eKilimo' kinaomuwezesha mkulima kupata taarifa za masoko na bidhaa kuondoa urasimu aliokuwa akiupata mkulima hapo awali. Wa kwanza kushoto akishuhudia ni Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Wateja wadogo, Abdulmajid Nsekela na Rais wa MasterCard wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara, Daniel Monehin.

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUU WA CCM YAKIENDELEA MJINI DODOMA

$
0
0
 Naibu katibu Mkuu CCM Bara,Ndugu Rodrick Mpogolo akimsikiliza Katibu Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole walipokuwa wakipanga mikakati kufanikisha mkutano mkuu wa CCM uatakaofanyika katika ukumbi wa mikutano, Dodoma leo
 Katibu Itikadi na Uenezi  Humphrey Polepole akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jitegee,Bwa.Antony Machundewalipokuwa wakikagua maandalizi ya mkutanao Mkuu wa CCM,utakaofanyika mjini Dodoma
Msaidizi wa Mwenyeikiti wa CCM Suleiman Mwenda akimuelekeza jambo  Naibu katibu Mkuu CCM Bara,Ndugu Rodrick Mpogolo walipokwenda kujionea maendeleo ya maandalizi ya ukumbi kwa ajili ya Mkutano mkuu wa CCM,unaotarajiwa kufanyika mjini Dodoma

DC Kanali Ndagala kuwachukulia hatua watakaoshindwa kumaliza miradi ya ujenzi wa shule kwa wakati wilayani Kakonko,mkoani Kigomamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya shule

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
 
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, endapo watashindwa kukamilisha miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika kwa muda muafaka kutokana na changamoto iliyopo ya upungufu wa vyumba vya madarasa kutatuliwa.

Maagizo hayo aliyatoa jana wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali inayo pelekea kusua sua kwa ujenzi huo.

Mkuu huyo alisema mradi huo ulitakiwa kuwa umekabidhiwa, lakini mpaka sasa bado haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya wasimamizi Wa mradi huo kushindwa kuwasimamia mafundi ipasavyo waweze kukamilisha ujenzi huo, na ifikapo mwezi wa tatu Mwishoni ujenzi huo uwe umekamilika na wanafunzi wapate madarasa yao waendelee kuyatumia.

" niwatake Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na Watendaji wa kijiji kuwasimamia mafundi kwa karibu ilikuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati endapo mtashindwa kusimamia ipasavyo tutawajibishana, Wananchi wamejitahidi kuchangia na Serikali imetoa fedha kwa wakati ni lazima muhakikishe mnakamilisha suala hili ilikuwatia moyo wananchi kuendelea kuchangia jitihada za Serikali",alisema Kanali Ndagala.

Hata hivyo Ndagala alisema katika Wilaya hiyo kuna upungufu wa madarasa ambapo mpaka sasa juhudi za kumaliza changamoto hiyo inaendelea kwa kuhakikisha Wananchi wanachangia kwa kushirikiana kujenga na kufyatua tofari na serikali inasaidi a kiasi kidogo cha fedha pamoja na kuezeka bati katika majengo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kakonko, Novatus kalobagwa alisema Shule hiyo ina zaidi ya Wanafunzi 1000 na ina madarasa tisa ambapo matano yamekamilika na manne yanaendelea kujengwa , hali hiyo inapelekea kila darasa kuwa na Wanafunzi 100-105 hali inayo pelekea mwalimu kuwa na wakati mgumu katika ufundishaji.

Alisema kutokana na Changamoto hiyo bado Wanafunzi katika shule hiyo wanaendelea kufauru, ambapo mwaka jana Wanafunzi wote wa darasa la saba Walifauru kwa asilimia miamoja na watano walipelekwa katika shule za vipaji maalumu kutokana na ufauru wao kuwa mzuri.

Aidha aliiomba serikali kihakikisha inamaliza kero hiyo kutokana na Maelekezo ya elimu ni kwamba ilikuhakikisha Mwanafunzi anaelewa ni lazima darasa moja liwe na Wanafunzi 45 kila chumba ambapo itamsaidia mwalimu kujua maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja na kuongeza ufauru kwa kiasi kikubwa.
 Sehemu ya Madarasa hayo ambayo bado hayajakamilika
 MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akizungumza na baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Kakonko,alipofana ziara ya kukagua madarasa manne na ofisi mbili zilizoko katika ujenzi katika shule hiyo.
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo, ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali iliyo pelekea kusua sua kukamilika kwa ujenzi huo.

JAJI WARIOBA AZINDUA KITABU CHA KIONGOZI MWANAMKE

$
0
0
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba akionesha kitabu juu mara baada ya kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali.
 Aisha Bdel na Liliani Lihundi wakifurahi mara baada ya Jaji wa Rioba kuzindua kitabu cha Mwanamke kiongozi
 Jaji Joseph Sinde Warioba akizungumza na Wanawake waliofika katika kongamano la Wanawake na Wasichana  juu ya uongozi ndani ya Tanzania na kuzindua kitabu kinachohusu Mwanamke
 Dkt Mwele Malecela akizungumza juu ya mambo aliyojifunza wakati anagombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi na kuwataka wazazi kuwa ndio waangalizi na kuwatoa hofu wasichana pindi wanapohitaji kujaribu jambo lolote lenye manufaa kwa Jamii
 Muendesha Mjadala Liliani Lihundi akizungumza wakati wa kongamano hilo ambalo lilihusisha wasichana na wanawake
 Mbunge Viti Maaalum Chadema , Susan Lymo akichangia jambo juu ya uozefu wake kama mwanamke katika Bunge la Jamhuri wa muungano
 Waziri mkuu Mstaafu Jaji  Joseph Sinde Warioba akiwa na Mama Anna Abdalah wakiwasalimia wanafunzi wasichana wa chuo kiku cha Dar es Salaam ambao walifika katika kongamano hilo
Baadhi ya washiriki waliokaa Safu ya mbele katika kongamno hilo

Wafanyakazi wanawake wa Barclays Tanzania washerehekea mafanikio yao

$
0
0
 Mkuu wa Mafunzo,  Uongozi na Usimamizi wa Talanta wa Benki ya Barclays Tanzania, Veronica Muumba (wa pili kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya benki hiyo, Fatma Karume (wa pili kulia), wakikata keki kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani katika hafla waliyoiandaa jijini Dar es Salaam jana. Wanaongalia kutoka kushoto ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo, Elizabeth Willilo, Faith Majiwa, Flavian Siweya na Mkurugenzi Mtendaji wa Barclays Tanzania, Abdi Mohamed.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania Abdi Mohamed akizungumza katika hafla hiyo.
 Mjumbe wa Bodi ya Barclays, Fatma Karume akitoa ushuhuda wake ambapo pia alitoa changamoto kwa wafanyakazi wanawake wa benki hiyo kujiamini ili waweze kushika nafasi mbalimbali za kiuongozi.

 Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Elizabeth Willilo, akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na benki hiyo jijini Dar es Salaam.
 Meneja Mawasiliano na Huduma za Jamii wa Barclays Tanzania, Hellen Siria akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Benki ya Barclays jana.
 Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Benki ya Barclays Tanzania wakipozi kwa picha ya kumbukumbu katika hafla hiyo.

 Baadhi ya wafanyakazi wakifuatilia hotuba zilizokuwa zikitolewa na wenzao wakieleza siri ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi za kila siku.

 Wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania wakimsikiliza mmoja wa wafanyakazi wa muda mrefu katika benki hiyo, Jane Mbwilo alipokuwa akitoa ushuhuda wake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Barclays Tanzania wakifurahia keki kuadhimisha siku ya wanawake jijini Dar es Salaam jana.

SSRA WAADHIMISHA SIKUKUU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MISAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya vifaa kwa Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi ya hospitali ya Mwananyamala, Sista Eva Njalla, Dar es Salaam katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kushoto), akiwashukuru wafanyakazi wa SSRA, mara baada ya kupokea misaada hiyo.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala, Dk. Daniel Nkungu (kulia), akiwatambulisha wafanyakazi wa SSRA kwa baadhi ya wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Meneja Utawala na Utumishi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bi. Amina Ally, akikabidhi baadhi ya msaada kwa mmoja wa wazazi waliokuwepo kwenye wodi hiyo.
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakiwa na baadhi ya vifaa kwa ajili ya kukabidhi Hospitali ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni katika kuadhimisha Sikukuu ya Wanawake duniani.

Telkom and Business Connexion yazindua BCX, Suluhisho la Teknolojia mahiri inyoongoza barani Afrika

$
0
0
 Mashirika na asasi zote ambazo hazikumbatii na kukubali mfumo wa kuendesha biashara kidigitali zinajiweka pabaya kutemwa na wateja wao.

Kutokana na tishio hili, Telkom and Business Connexion inazindua rasmi BCX, mfumo mpya na wa kisasa kidigitali unaoongoza barani Afrika, unaotumika kurahisisha mawasiliano ya miamala ya biashara na mawasiliano.

Toleo hili jipya la teknolojia, lililoandaliwa kwa ushirika kati ya Telkom Business na Business Connexion, ni la kipekee katika ufumbuzi wa kitekinolojia unaosambaa kwa kasi barani Afrika kuwezesha na kurahisisha mawasiliano na ufanisi wa kibiashara.

“Uzinduzi wa BCX kwa kweli unafungua ukurasa mpya katika mwelekeo wa ufanisi wa kibiashara kwa tekinoljia pevu barani Afrika,” alisema Seronga Wangwe ambaye ni Mkurugenzi wa BCX Tanzania, katika hotuba yake ya ufunguzi aliyoitoa hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar Es Salaam.

“BCX imejengwa kutoka katika msingi imara wa Telkom Business yenye maarifa na elimu pevu ya miundombinu ya mawasiliano pamoja na taaluma ya muunganisho wa kibiashara inayojali kutoa huduma kwa ukaribu na unyenyekevu kwa wateja wake.

“BCX sasa ni bidhaa mpya ya mawasiliano barani Afrika yenye ufanisi wa kutoa huduma kwa umakini mkubwa’, aliongeza Bwana Wangwe.

Mfumo wa kidigitali uliopevuka unapewa kipaumbele na aina zote za biashara barani Afrika. Kwa sasa inaelewaka bayana kuwa kampuni yeyote ambayo inakwepa au kudharau kuendesha miamala yake kidigitali ipo hatarini kutorokwa na wateja katika mwelekeo wa kudorora kabisa!

BCX inatoa mwelekeo mpya popote barani Afrika katika kutoa huduma kidigitali ili kutoa huduma bora kibiashara kwa sasa na kwa muda mrefu kwa wateja wake.

“Hakuna kitu kilichonifurahisha zaidi leo hii kama uzinduzi huu mpya wa BCX,” alisema, mkuu wa BCX international ALTHON BEUKES. 

BCX inaweka bayana aina ya mawasiliano na mahitaji yote ya makampuni yaliyomo barani Afrika katika kutoa ufumbuzi sahihi wa matatizo ya mawasiliano kibiashara, katika masoko yake ya ndani na hatimaye kupenya nje ya mipaka na kusambaa barani kote. Itasawazisha uwezo wa makampuni katika kujitanua kitekinolojia na mahitaji ya mawasiliano ya makampuni barani Afrika.

“BCX’s imetandaza nyayo zake kibiashara barani Afrika ikiwa na makampuni tanzu katika nchi kama vile Kenya, Nigeria, Tanzania, Namibia, Zambia na Botswana, halikadhalika uwepo wake huko Dubai na Uingereza, inatufanya tuwe mfano pekee na bora kwa mwasiliano na washirika na wateja wetu wote wanaofanya biashara nasi barani Afrika na wale walio katika matarajio ya kujiunga nasi katika mwelekeo wa ufanisi kibiashara ili kuliongoza bara la Afrika kwenye ushindi wa nafasi za kibiashara,” aliongeza.

Uzinduzi wa BCX ni hatua ya mwisho katika kunyumbulisha Telkom Business na Business Connexion. BCX itaendelea kujikita ndani ya Telkom Group, lakini itajali kufanya biashara katika ufanisi mkubwa. Wafanyakazi wote wanafahamu umuhimu wa tekinolojia hii mpya na ofisi zote zina thamini bidhaa hii mpya ya mawasiliano. Kwa kuongozea, miamala yote ya kibiashara na wateja itajikita katika sura mpya ya utambulisho wa BCX.

BCX kwa kwenda mbele itaendelea kuangalia kwa umakini mahitaji ya wateja wake na kutoa ufumbuzi wa uhakika hususan kwa matumizi ya kompyuta, mawasiliano na ushirikainao wa karibu, na mnyumbulisdho wa kibiashara wenye usalama wa uhakika kwa mtandao pamoja na uchambuzi makini wa takwimu za kibiashara.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya BCX Tanzania Bw. Seronga Wangwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam katika uzinduzi wa kampuni ya BCX ambayo imejumuisha kampuni za Business connexion na Telkom katika hafla fupi iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency, Kulia ni meneja mauzo wa kampuni hiyo Bw. Ebenezer Massawe.

Kutoka kushoto ni Bwa. Seronga Wangwe, (mwakilishi) kutoka Mozambique High Commission, Bwa.Frans Van Aardt- Councelor kutoka ubalozi wa Afrika kusin,Bi.Monica Patricio Clemente- Balozi wa Msumbiji, pamoja na Bwa.Althon Beukes- mkuu wa BCX International wakiwa katika picha ya pamoja.

. Mgeni rasmi Bw. Frans Van Aardt ambaye ni Councelor wa Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania. Akizungumza katika Uzinduzi wa kampuni ya BCX uliofanyika Hyatt hotel Dar es salaam
Mkuu wa BCX International Bw. Althon Beukes akizungumza na wageni katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni ya BCX, iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam 
Wasanii kutoka kikundi cha Kigamboni Community Centre (KCC) wakitoa burudani ya ngoma za asili kwa wageni na waalikwa katika siku ya uzinduzi wa kampuni ya BCX nchini Tanzania uliofanyika katika hoteli ya Hyatt regency (the Kilimanjaro).
Wageni mbalimbali waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa BCX Tanzania 
Bw. Seronga Wangwe (Mkurugenzi mtendaji wa BCX Tanzania) akizungumza na wageni waalikwa katika hafla fupi ya uzinduzi wa kampuni hiyo siku ya jumatano katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es salaam

UPELELEZI KESI YA KITILYA WASUBIRI USHAHIDI KUTOKA ULAYA

$
0
0

Watuhumiwa wa kesi ya uhujumu uchumi Miss Tanzania wa Zamani Shose Sinare na kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya n Sioi Sumari wakiwa katika kizimba cha mahakama ya kimu mkazi kisutu mara baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili
Kamishna mstaafu wa TRA ,Harry Kitilya na Sioi Sumari




Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upepelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta liugha za ujanja ujanja.

“Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndaniya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilina inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi Fulani hivyo ameugiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

aliyekuwa Miss Tanzania Shose Sinare akishuka katika ngazi za mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam

MWENYEKITI WA CCM DKT JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA USALAMA NA MAADILI YA CHAMA CHA CCM MKOANI DODOMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza  Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Usalama na Maadili kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,Chamwino mkoani Dodoma.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma,pichani kati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
  Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma.

LEMA: MADIWANI WA CHADEMA WAOGA NIPO TAYARI KUWAKANA MBELE YA WANANCHI

$
0
0
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha Leo.
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma
Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la leo Arusha
Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini Arusha.

Na,Vero Ignatus ,Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoika rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho. 

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Ameataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ASHIRIKI MISA YA NJIA YA MSALABA KATIKA KANISA KUU LA KATOLIKI LA MTAKATIFU PAULO WA MSALABA MJINI DODOMA

$
0
0
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine katika misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
  Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine katika misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akitakiana amani na watawa wakati wa  misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Katoliki la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma leo Ijumaa Machi 10, 2017
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akijumuika na waumini wengine kupokea Ekaristi  Takatifu wakati wa misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akisalimiana na waumini baada ya misa ya Njia ya Msalaba katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo wa Msalaba mjini Dodoma  Ijumaa Machi 10, 2017 PICHA NA IKULU

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MACHI 11,2017

CCM ipo kamili kuanza kwa mikutano yake maalum mjini Dodoma

$
0
0

Chama cha Mapinduz (CCM) kimeelezea kuwa kamili katika kuelekea kwenye  mkutano wake maalum hapo keshokutwa Machi 12 mwaka huu mjini Dodoma.

Tayari  maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma  umeanza kupepea bendera za Chama hicho cha Mapinduzi huku shamrashamra za hapa na pale zikitarajia kunoga zaidi kuanzia leo Machi 11 na siku ya mkutano wenyewe.

 Kwa sasa mji wa Dodoma umekuwa na pilikapilika za hapa na pale huku Ulinzi na usalama ukiwa umeimarishwa na wa hali ya juu hasa ikizingatiwa kuna ugeni mkubwa ikiwemo wa wajumbe kutoka kila kona ya nchi nzima  na viongozi wa nchi.

Awali akizungumza  katika makao makuu ya CCM Mjini hapa,  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Humphrey Polepole  amesema  maandalizi yote yamekamilika  na tayari wajumbe wamefika na wanaendelea kufika huku vikao maalum vikiendelea kufanyika ni vile vya ndani

“Maandalizi yote yamekamilika ya mkutano wetu wa hapa Dodoma. Kwa sasa CCM imeanza safari madhubuti na kuongeza tija katika kuisimamia serikali katika ushahuri na maelekezo. Mkutano huu unakuja kuweka uhalali na kuja kusimika mageuzi haya rasmi kikatiba. Mkutano huu utakuwa rasmi kama chama cha Wanachama na kitashughulika na shida za wanachama na umma wa watanzania.” Ameeleza Polepole.

Humphrey Polepole ameweka wazi kuwa,  licha ya kuwa, halmashauri kuu ina uwezo wa kupitisha mabadiliko  hata hivyo wao kupitia Mwenyekiti (Rais John Magufuli) Wameamua kuitisha mkutano wa dharura ili kupitisha mabadiliko hayo.Polepole amesema mabadiliko yatasaidia kufanya mageuzi makubwa na chama kurejea kwa wananchi wote na katika misingi imara 

Aidha, mikutano ya awali  inatarajia kuanza mapema ikiwemo ule wa Kamati Kuu ya CCM uliotarajia kufanyika jana Machi 10 huku ule wa Halmashauri Kuu ukitarajia kufanyika leo Machi 11 na mwisho mkutano huo wa Machi 12.

Kwa uzoefu wa mikutano hiyo mikuu ya  Kichama hasa ya CCM, inapofanyika mjini hapa, pamekuwa na wingi wa watu huku nyumba za wageni karibu zote zinakuwa zimejaa, Hali kwa mkutano huu huenda ikawa na changamoto kwani kwa sasa tayari baadhi ya watumishi wa Serikali hasa baadhi ya Wizara kuhamia Dodoma kama Makao makuu ya nchi,

karibu nyumba nyingi za wageni wamekuwa wakizikodisha hivyo kwa muingiliano wa mkutano huu changamoto hiyo inaweza kuwa maradufu kwa muda hasa kwa kipindi hiki cha mkutano.
Na Andrew Chale-Dodoma

WAZIRI SIMBACHAWENE:MAAFISA UTUMISHI KUWENI WAADILIFU

$
0
0

 Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tamisemi mhe,George Boniface Simbachawene

Na. Vero Ignatus, Arusha.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene amewaagiza maafisa utumishi kuwa waadilifu na wakweli katika kutunza nyaraka zinazowahusu watumishi wenzao.

Aidha serikali inatambua kuwa inadaiwa na mifuko ya hifadhi ya jamii na inajitahidi kulipa madeni hayo inayodaiwa na mifuko ya Hifadhi za Jamii .

Simbachawene amesema hayo wakati akifungua mkutano wa tisa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Amesema baadhi ya maafisa utumishi wamekuwa kama miungu watu na kupoteza nyaraka za watumishi huku wanapobanwa na waajiriwa kuhusu taarifa za watumishi husema uongo  wakijua wenzao wanafamilia kama wao.

Pia amekemea tabia ya watumishi wa masijala ambao wanapoteza kumbukumbu za watumishi kwa makusudi hali inayosababisha baadhi yao kupunjwa madai yao kutokana na baadhi ya kumbukumbu kupotezwa.

"Nawaomba nyie maafisa utumishi muwe makini sana na maisha ya watumishi wenzenu oneni huruma kwao mnapoteza kumbukumbu au kutoa ruhusa kwa watumishi halafu mkibanwa mnasema hamna taarifa hii inawaumiza watumishi wenzenu maana wanafamilia zao kwanini muwafanyie mambo yasiyofaa mjirekebishe nyie pamoja na watu wa masijala ".

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Lapf, Profesa Faustine  amesema kuwa mfuko huo unajitahidi kutoa huduma kwa wakati ikiwemo kuongeza idadi ya wanachama na kubuni mbinu za kukuza uchumi katika sekta ya viwanda.

Alisema mfuko huo utaendelea kutoa huduma kwa wakati akiwemo fao la kulipwa jana kwa wanachama wastaafu sanjari na kutoa mkopo wa maisha popote unaotolewa kwa waajiriwa wapya kwakushirikiana na Benki ya CRDB.

Naye Mkurugenzi wa mfuko huo, Eliud Sanga alishukuru wanachama hao kwa kushiriki katika mkutano huo sanjari na kuuchagua mfuko huo ambao utatoa jana na hivi sasa wapo katika uchambuzi wa Kiwanda cha chai cha Mponde, kilichopo Tanga, Kiwanda cha Kuchataka nyama kilichopo Morogoro pamoja na kiwanda cha vifaa vya hospitali Mkoani Shinyanga ambapo miradi hiyo itaanza kutekelezwa mwishoni mwa mwaka huu
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live


Latest Images