Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live

WANANCHI WA MKURANGA WAPATA HUDUMA ZA VIPIMO VYA AFYA ZAO BURE

$
0
0
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani) wakati wa upimaji wa afya kwa wananchi wa Wilaya ya Mkuranga leo.
  Muuguzi Mariam Adamu akipima kipimo cha Sukari na Msukumo wa Damu
 Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii 

Wananchi wa Mkuranga wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa mbalimbali na pale wanapokutwa kuweza kutibu kwa wakati mwafaka.

Akizungumza katika upimaji wa Afya huo,Mkurugenzi wa Taasisi ya Ibun Jazar na Mwenyekiti wa Jumuiya kuhifadhisha  Qur-uan  Tanzania, Othman Kaporo amesema kuwa katika dunia ya sasa jamii inawajibu wa kupima afya kujua ana tatizo au hana ili kuweza kuchukua hatua pamoja na kujinga na magonjwa mbalimbali yanatokana na mfumo wa maisha.

Othman amesema kuwa huduma hiyo itatolewa  kwa wa wananchi wa Mkuranga, Vikindu, Mwanambaya, Mbagala na maeneo  mengine yaliyo karibu.

Amesema wamechagua Wilaya hiyo kutokana watu wengi wanashindwa kuifikia na kuona kwa taasisi hiyo inawajibu wa kupima afya za wananchi ha.

Aidha amesema kuwa watu wengine ambao wanauwezo wajitokeze katika kutoa huduma ya upimaji ili waweze kujikinga na magonjwa ambayo yanatokana na mfumo wa maisha.

Amesema tangu jana walipoanza kupima watu zaidi ya 500 wamwjitokeza kupima na mwitikio umekuwa  mkubwa wa kuweza kuvuka malengo ya upimaji huo.

Huduma ya vipimo walivyotoa ni Msukumo wa Damu (BP), Sukari , Unene na Urefu kuendana sawa na mwili (BMI) Ushauri Nasaha  na Upimaji wa VVU,Utafiti wa Saratani ya matiti pamoja na utafiti wa Saratani ya Kizazi.
 Wananchi wakisubiri huduma ya vipimo vinavyotolewa na Taasisi ya Ibun Jazar leo.





RAIS DKT MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBI RAMBI KWA FAMILIA KUFUATIA KIFO CHA BALOZI SIR GEORGE KAHAMA

$
0
0
Balozi,Sir George Kahama enzi za uhai wake,ambaye amefariki leo alasiri katika hospitali ya Taifa  Muhimbili,alikokuwa amelazwa kwa matibabu.Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi-Amen.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMATATU MACHI 13,2017

TAARIFA KWA UMMA

UJERUMANI YAIOMBA TANZANIA KUIUNGA MKONO KATIKA UCHAGUZI WA NAFASI YA MJUMBE WA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA.

$
0
0

Na Immaculate Makilika- MAELEZO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augustine Mahiga amefanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Balozi Harro Adt, ambapo alipokea, niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ujumbe maalum kutoka kwa Kansela Markel.

Akizungumzia ziara ya Balozi Adt nchini, Balozi Dk. Mahiga alisema kuwa "Kansela Merkel amemtuma Balozi Adt, kuleta ujumbe maalum ambao ni ombi kwa Rais Magufuli la kuisaidia Ujerumani katika kugombea nafasi ya kuwa mjumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa uchaguzi wa nafasi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwaka 2018".

Balozi Dk. Mahiga alieleza kuwa dhamira ya Ujerumani ya kugombea nafasi hiyo ni kusaidia mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kuridhia nchi za Afrika katika mchakato wa kupokea nafasi mbili za kudumu katika baraza hilo. Nchi nyingine zinazogombea nafasi hizo ni Israel na Ubelgiji.

Balozi Mahiga alisema kuwa, Ujerumani imeahidi masuala kadhaa kama vile kusimamia amani katika jumuiya ya kimataifa na katika ukanda wa Afrika, kusimamia haki za binadamu katika ngazi ya dunia na kuendelea kuimarisha uhusiano wake na nchi nyingine.

Aidha, Ujerumani imesisitiza nia yake ya kuunga mkono mageuzi mapya katika bara la Afrika ambayo yataikomboa Afrika na kuleta maendeleo zaidi barani humu.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Dk. Mahiga alisema kuwa ameiomba Ujerumani isaidie ujenzi wa jengo mahususi la mahakama ya Afrika iliyopo mjini Arusha ikiwa ni pamoja na kuboresha mfumo mzima wa mahakama barani Afrika pamoja na kuisaidia Afrika katika kupambana na masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake, mjumbe maalum kutoka Ujerumani Balozi Adt, alisema kuwa amefurahishwa na mapokezi aliyoyapata alipowasili nchini.

Aidha, Mjumbe huyo Maalum wa Kansela wa Ujenrumani alieleza matumaini yake kuwa Tanzania ambayo ni rafiki wa Ujerumani kihistoria itatoa msaada juu ya nafasi hiyo ili kusaidia kutekeleza malengo waliojiwekea kiufanisi kuhakikisha Afrika inapata nafasi mbili za kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Uhusiano kati Tanzania na Ujerumani ni wa kihistoria na wakati wote nchi mbili hizo zimekuwa zikifanya kila jitihada za kuuimarisha.

Chini ya uhusiano huo, Ujerumani imekuwa ikiisaidia Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile elimu, miundombinu na wanyamapori.

KAMATI YA UTALII WATEMBELEA YALIYOKUWA MAFICHO YA MWALIMU NYERERE WAKATI WA HARAKATI ZA UHURU MKOANI MBEYA

$
0
0
Kamati ya Utalii ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya ikiongozwa na Afisa Utalii wa Jiji Bi.Levina Modest na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Geofrey Kajigili wanaofanya kampeni hii kabambe ya utambuzi wa Vivutio vyote vilivyopo Jijini Mbeya kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali za Uyole Cultural Tourism Enterprise pamoja na Elimisha .

Pia wamemtembelea Mzee Mkongwe wa Siasa nchini, Mzee Rashid Ally Sinkala ambaye amewahi kuwa Diwani wa iliyokuwa ikiitwa Kata ya Soko Matola (sasa Kata ya Maendeleo) kwa miongo kadhaa,na amewahi kutumika kama Meya ya Halmashauri ya Mbeya Mjini.

Mzee Sinkala ameiambia Kamati ya Utalii kuwa Miaka zaidi ya 50 iliyopita wakati wa Siasa za Ukombozi wa Tanganyika enzi za Chama cha Tanganyika African National Union (TANU)Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa akifikia kwenye nyumba ya mwanasiasa Mkongwe mwanamke aliyejulikana kwa majina ya Zaituni Binti Matola.Binti Matola alitenga chumba kimoja nyumbani kwake kama Maficho ya Mwalimu Nyerere.
Mzee Sinkala akiwa mlangoni mwa Chumba maalum alipokuwa akifikia Mwalimu Nyerere ndani ya nyumba ya muasisi wa TANU na mwanamke mashuhuri Hayati Zaituni Binti Matola aliyesababisha maeneo hayo kuitwa "Soko Matola" Jijini Mbeya
Wajumbe wa Kamati ya Utalii Jijini Mbeya wakimsikiliza kwa makini Meya mstaafu wa Halmashauri ya Mbeya Mjini Mzee Sinkala ndani ya nyumba ya kihistoria ya Binti Matola.




BASATA YAITAKA KAMATI YA MISS TANZANIA KUMKABIDHI MSHINDI GARI YAKE

$
0
0

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamiii

Ikiwa imepita zaidi ya miezi minne tangu shindano la Miss Tanzania 2016  lifanyike huko jijini Mwanza na taji lake kuchukuliwa na mrembo Diana Edward, bado mrembo huyo hajakabidhiwa zawadi yake ya gari na kiasi cha pesa Shilingi milioni mbili.

hata hivyo katika siku ya mwisho wa shindano hilo, mrembo Diana alionekana akikabidhiwa gari aina ya Toyota IST, Ukumbini hapo kumbe ilikuwa danganya toto kwa watu wote waliofika katika shindano hilo ili waweze kuamini kuwa mrembo huyo kuwa kapewa gari.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akionekana kumkabidhi gari mrembo huyo siku muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi.

Diana ambaye alikaa kwenye gari hiyo akiwa na furaha kubwa sana akimini kuwa ndio mchuma wake wa kwenda nao nyumbani kwao lakini mpaka leo mrembo huyo bado ni mtu wa kupanda daladala , Bajaj na Bodaboda.

Akizungumza na Ripota wetu, afisa habari wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Agnes Kimwanga amesema kuwa waliwaita kamati ya Miss Tanzania katika kikao cha tahmini na wao kukiri kuwa hawajampatia zawadi zake zote mshindi huyo pamoja na washiriki wengine  wanne.

“mara baada ya kujieleza katika kikao chetu cha Tathmini wakajitetea kuwa watatoa zawadi hizo tarehe 30 Aprili mwaka huu kwa kumpa Miss Tanzania 2016 zawadi yake ya gari na kiasi chake cha pesa Milioni mbili ambacho kimebaki” Amesema Agnes.
Miss Tanzania 2016, Diana Edward akiwa na washiriki wenzake siku aliyotwaa taji hilo.

Akithibitisha hilo, Afisa habari wa Miss Tanzania, Haiden Ricco alikiri kutomlipa mrembo huyo stahiki zake zote ikiwepo gari.

"Ni kweli mrembo wetu hajawalipwa na sio yeye peke yake, hata wale warembo wengine wanne hawajalipwa pia" alisema Ricco.

Amesema kuwa fedha zilizobakia wanazodaiwa na warembo hao ni kiasi cha jumla ya shilingi milioni nane hivyo zote watalipwa kuanzia mwezi huo wanne.

Rico ametaja kuwa shindano lao kwa kutegmea wadhamini wamejipanga kuanzia mwezi ujao kuanza kuwalipa warembo hao kadri watakavyokuwa wanapata fedha kutoka kwa wadhamini na wadau wa shindano hilo.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN, MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. Picha na IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongozana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.


JK AZINDUA RASMI TAASISI YA MAENDELEO YA JAKAYA MRISHO KIKWETE (JMKF)

$
0
0
 Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete (kulia), akizungumza alipokuwa akizindua rasmi Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) ikiwa ni sehemu pia ya uzinduzi wa taasisi hiyo kwenye Hotel ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro Dar es Salaam leo. Kikwete ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Jakaya Kikwete, alisema kuwa Taasisi hiyo pamoja na mambo mengine  itajihusisha na masuala ya Maendeleo ya Binadamu nchini, Afrika na Duniani.


Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Kikwete amesema kuwa anapenda kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na jamii.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa  akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete Foundation)  alisema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo Taasisi yake itamsaidia katika kufikia malengo yake.

“Nimetumia muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule, nilikitumikia Chama cha Mapinduzi(CCM), nilitumikia Jeshi na baadae Serikali, kwangu Taasisi hii imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza maono yangu na kutimiza ndoto zangu katika kuendelea kusaidia watu” alisema Dkt. Kikwete.

Akiizungumzia taasisi hiyo Kikwete alisema kuwa, Taasisi yake ina wajumbe 9 kutoka sehemu mbalimbali duniani wenye nyadhifa na heshima kubwa katika nchi zao.

Ameongeza kuwa Taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne, maendeleo ya jamii  hasa katika kujikita kuondoa umaskini, mabadiliko ya hali ya nchi na kilimo  kwa wakulima wadogo.

Pia Taasisi hiyo imejikita katika huduma za afya, kutokomeza malaria na afya ya mama na mtoto.

Maeneo mengine ambayo Taasisi hiyo inajihusisha nayo ni  ni elimu kwa  vijana ili  kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.

Aidha, alisisitiza kuwa Taasisi yake itaisaidia Serikali, mashirika na Taasisi mbalimbali ili kushirikiana kuwaletea maendeleo watanzania na watu mbalimbali duniani.

Dkt. Kikwete amewataja Wajumbe wa Bodi ya Udhamini ya Taasisi yake kuwa ni Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Profesa Rwekaza Mukandala Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Willium Mahalu Mhadhiri Mwandamizi  katika Chuo Kikuu cha Tabibu cha Bugando.

Wengine ni Balozi Mwanaidi Maajar aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Abubakar Bakhresa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa, Genevieve Sangudi  Mtaalamu wa Masuala ya kibishara ya Kimataifa kutoka Marekani.

 Pia wapo Dato’ Sri  Idris Jala, Waziri asiyekuwa na Wizara Maalumu nchini Malyasia,  Balozi Charles R. Stith aliyekuwa Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania pamoja na Dkt. Carlos Lopes ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taaisi ya Mafunzo na Utafiti ya Umoja wa Mataifa (UNITAR).

Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya Kikwete ilisajiliwa tarehe 17, Februari 2017, na hii ni mara ya kwanza kwa wajumbe wa bodi ya wadhamini kukutana tangu kuanzishwa kwake.
 Kikwete akizungumza na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi yake ya JMKF
 Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi wa zamani wa Marekani nchini Tanzania, Charles Stith
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo, Mfanyabiashara maarufu Mtanzania aishie Marekani, Genevieve Sangudi
 Mwenyekiti wa Taasisi ya JMKF, Jakaya Kikwete akisalimiana na mjumbe wa Bodi hiyo ya Wadhamini , Dato' Sri Idris Jala, Waziri asiye na Wizara Maalumu Ofisi ya Waziri Mkuu wa Malaysia na Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Pamendu) nchini humo.
 Mwenyekiti wa JMKF, Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la Taasisi hiyo.
 Jakaya akijadiliana jambo na Balozi Charles Stith
 Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa Taasisi hiyo.
 Jakaya Kikwete akifafanua mambo mbalimbali kuhusu Taasisi hiyo

 Dato' Sri Idris Jala kutoka Malaysia
 Genevieve Sangudi kutoka Marekani
 Mwanasheria Maarufu nchini, Balozi Mwanaidi  Sinare Maajar. Alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza 2006 na Marekani 2013



 Daktari Bingwa wa Upasuasi, Profesa Wiliam Mahalu
 Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa  Rwekaza Mukandara
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Makampuni la SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa
 Balozi wa zamani wa Marekani nchini, Charles Stith

ASIA IDAROUS ANOGESHA VIP RECEPTION AWARDS GALA FAIRFAX, VIRGINIA

$
0
0

Warembo wakiwa katika picha ya pamoja siku ya Jumamosi March 11, 2017 Fairfax, Virginia kwenye V.I.P. Reception Awards Gala iliyohudhuriwa na Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae
Balozi wa Kenya nchini Marekani Mhe. Robinson Njeru Githae
Mwanamitindo nguli wa kimataifa Asia Idarous Khamsin akiwa katika picha ya pamoja na

 Mrembo akiwa katika vazi la mwanamitindo nguli wa kimataifa Asia Idarous Khamsi.
 Vazi kutoka kwa mama mitindo wa kimataifa Asya Idarous Khamsin.


RC MAKONDA AKABIDHIWA BARABARA KURASINI JIJINI DAR LEO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva na watendaji wakitembelea barabara Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika uzinduzi wa wa akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika uzinduzi wa kukabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  wakikata utepe kuashilia kukabidhiwa barabara ya Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Muonekano wa Baarbara hiyo.


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika  katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa. Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema  barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.

Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.

"Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita haijapita" amesema Makonda .

Amesema barabara hiyo imejengwa na kampuni ya kizalendo ya Grant Tech Company ya jijini Dar es Salaam na maombi ya barabara ni miezi miwili iliyopita lakini imekamilika kwa muda mwafaka .

Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.

Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni  ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.

Mkandarasi huyo (Grant tech), Masito Mwasingo amesema kuwa wamefanya ujenzi kwa muda mwafaka kutokana umuhimu na kuunga kuunga mkono utendeji kazi wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam.

KUANZA KWA MVUA:TANESCO YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI

KOMREDI KINANA AFUNGUA SEMINA ELEKEZI YA MABADILIKO NDANI YA CHAMA KWA WENYEKITI NA MAKATIBU WACCM, MJINI DODOMA, LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akifungua semina elekezi kuhusu mabadiliko ndani ya Chama, kwa Wenyeviti na Makatibu wa mikoa na wa wilaya na watendaji, leo katika Ukumbi wa Sekretarieti katika Jengo la Ofisi ya Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma 
 Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Katibu wa Sekretarieti ya CCM, Anamringi Macha (kulia) akiratibu semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.
 Sekretarieti ikisimamia kufanyika kwa Washiriki wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. 
Baadhi ya viongozi wakiwa kwenye semina elekezi kuhusu mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi, leo katikaUkumbi wa Sekretarieti Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu mpya wa CCM-Zanzibar Dk. Abdalla Juma Abdallah, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu- Zanzibar, Vuai Ali Vuai, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, na kutoka kulia ni Katibu mpya wa NEC Oganaizesheni, Lela Ame Silima na Katibu wa NEC Oganaizesheni mstaafu Mohammed Seif Khatib. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

TTB YAANDAA MKAKATI MAALUMU KUKAMATA MASOKO YA ULAYA NA MAREKANI

$
0
0
Na Geofrey Tengeneza - Berlin

Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeingia mkataba na kampuni tatu za Ulaya na Marekani ili kutayarisha mikakati maalumu ya utangazaji utalii mahsusi katika nchi za Ujerumani, Uingereza na Marekani ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuhakikisha inajipenyeza zaidi kaika masoko ya makuu ya utalii yalioanishwa katika mkakati wa Utangazaji utalii wa kimataifa wa miaka mitano katika masoko mbalimbali ya utalii duniani.

Mkataba huo umesainiwa katika maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB katika banda la Tanzania na Mkurugeni Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bi Devota Mdachi na Wakurugenzi wakuu wa kampuni hizo ambazo ni Africa Oracle Company kwa ajili ya soko la Uingereza, 7o7 Marketing GmbH Ltd kwa ajili ya soko la Ujerumani na Tourism Intelligence International kwa jili ya soko la Marekani.
Bw. Recknagel Markus, Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya7o7 Marketing GmbH ya ujerumani na Mkurugenzi mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi wakionyesha jarida la TTB lililotayarishwa kwa lugha ya Kijerumani kwa lengo la kuutangaza utalii na vivutio vya utalii vya Tanzania katka soko la ujerumani na nchi zinazozungumza Kijerumani.

Kwa Mujibu wa Meneja Masoko wa TTB Bw. Geofrey Meena pamoja na kuwa mkakati wa Kimataifa wa miaka mitano umeainisha masoko kumi na mbili ya utalii duniani, wameamua kuanza na masoko hayo matatu kwa kuwa ni miongoni mwa masoko muhimu kwa Tanzania hivi sasa. Masoko makubwa manne yanaoongoza kwa watalii wengi kutembelea Tanzania ni Marekani, Uingereza, Italia na Ujerumani.

“Kwa kuanzia tumeanza na masoko haya na baadae tutakwenda pia katika masoko mengine. Wataalamu hawa kutoka masoko hayo matatu wakikamilisha kututayarishia mikakati hiyo maalumu kwa kila soko itatusaidia kujua mbinu gani sahihi za kujipenyeza na kulikamata kikamilifu kila soko” alisema Bw. Meena

Kusainiwa kwa mikataba hii kumefanyika siku moja tu baada ya Bodi ya Utalii Tanzania kusaini mkataba wa ushirikiano na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius katika utangazaji wa pamoja wa utalii wa nchi hizo mbili.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Bi Devota Mdachi (kushoto) na Dr. Auliana Poon Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni Tourism Intelligence International wakisaini mkataba kwa ajili ya mkakati wa TTB kwa ssoko laMarekani huku Mwenyekiti wa TTB Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akishuhudia utiaji saini huo.
Bi Devota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji w TTB akibadilishana mkataba na Mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya 7o7 Marketing GmbH Limited Bw. Recknagel Markus mara tu baada ya kusaini mkataba huo kwa ajili ya soko la Ujerumani.
Dr. Auliana Poon wa Kampuni ya Tourism Intelligence International ya Marekani akibadilishana mkataba na Bi Deota Mdachi, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TTB mara baada ya kusaini.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AZINDUA MPANGO WA UGAWAJI WA VIFAA VYA KIDIJITALI KWA SHULE 10 ZA JIMBO LA DODOMA MJINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan leo amezindua mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.

Mama Samia  amesisitiza kuhusu utunzaji wa vifaa hivyo na matumizi sahihi ya vifaa hivyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kusaidia kuinua kiwango cha Elimu katika Jimbo la Dodoma Mjini

Aidha Makamu wa Rais amepongeza jitihada na ubunifu wa Mbunge wa Jimbo hilo la Dodoma Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Ndg Anthony  Mavunde na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuwahudumia wanadodoma Mjini.

Pamoja na hilo Mama Samia ameahidi kuunganisha Jimbo la Dodoma Mjini na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia watoto wa kike kupitia mfumo wa ufundishaji kidigitali wa Sillicon Valley.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mradi wa Pro Futuro Bi. Rosemary Terry (kushoto) juu ya Vishikwambi (Ipad) vitakavyotumika katika kufundishia shule 10 zilizopo ndani ya jimbo la Dodoma mjini, kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Anthony Mavunde . (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
 Makamu wa Rais Mama Samia  Suluhu Hassan (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wageni waalikwa wengie wa meza kuu wakionesha baadhi ya Vishwambi mara baada ya kuuzindua mpango huo wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini. 
  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla fupi uzinduzi wa mpango wa Ugawaji wa Vishwambi"Tablets" 5000,laptops na projectors kwa Shule za Msingi 10 za Jimbo la Dodoma Mjini.
 Baadhi ya Wageni waalikwa kwenye hafla hiyo wakifuatilia kwa umakini tukio hilo
 Baadhi ya wanafunzi wakishuhudia tukio hilo adhimu kwao


MAXCOM AFRICA (MAXMALIPO) INAWAKARIBISHA WATANZANIA KUSHIRIKI MANUNUZI YA HISA KWA NJIA YA MTANDAO

$
0
0

C:\Users\Deogratius Lazari\AppData\Local\Microsoft\Windows\Temporary Internet Files\Content.Word\IMG_4247.jpg
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu  Bwana. Deogratius Lazari Mosha akifafanua jambo kwa Waandishi wa habari (hawapo pichani)
Kampuni ya Maxcom Africa (Maxmalipo) inawakaribisha watanzania kushiriki manunuzi ya hisa za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye Soko la hisa la Dar es salaam(DSE)  kwa njia ya mtandao (simu za kiganjani) na kufanya malipo kupitia kwa mawakala wa  Maxmalipo waliopo nchi nzima Tanzania.
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Ubunifu  Bwana. Deogratius Lazari Mosha, Leo 13/03/2017 amewaambia waandishi wa habari kwamba Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na soko la hisa la  Dar es Salaam(DSE) kwa kutumia mfumo madhubuti wa simu za viganjani unamwezesha Mtanzania kuweza kushiriki kwenye Manunuzi ya hisa  za makampuni yaliyoorodheshwa kwenye soko la awali  la mitaji (primary markets ) kwa kupiga *150*36#, ameongeza kwamba baadhi ya makampuni hayo kwa sasa ni Vodacom na TCCIA.
Akifafanua hili Bw. Deogratius Lazari amesema ili Mtanzania aweze kushiriki Manunuzi ya hisa kwa mfumo huu anatakiwa kubonyeza *150*36# kisha ataingia kwenye Menyu ya soko la hisa na Kuchagua IPO kisha atachagua kampuni anayotaka kununua hisa, baada ya kufanya hivyo mteja atalazimika kujisajili na kisha atapata nafasi ya kuainisha idadi ya hisa anazohitaji(zisizo pungua 100 katika awamu ya kwanza).
Bw. Deogratius Lazariameongeza kwamba baada ya hatua ya uanishaji wa hisa, mteja atapokea ujumbe mfupi wa simu kutoka DSE wenye  nambari ya kumbukumbu ya malipo, idadi ya hisa na kiasi anachotakiwa kulipia. Ili kukamilisha  malipo haya mteja  atatakiwa kufika kwa wakala yeyote wa Maxmalipo aliye karibu naye na kufanya malipo kama ilivyo ainishwa kwenye ujumbe aliopokea kwenye simu yake. Mteja anahimizwa kuhakikisha kwamba anapatiwa risiti pindi anapolipia hisa kwa mawakala wa Maxmalipo ili kutunza kumbu kumbu zake.
Kwa kuongezea Bw.Deogratius Lazari ameeleza kwamba mfumo huu rafiki unamwezesha mteja kushiriki manunuzi ya hisa kadiri ya uwezo wake (Mfano, Mteja Anaweza kila siku akanunua hisa 100 kulingana na kipato chake au zaidi). Pamoja na mwakala wa Maxmalipo mteja anaweza  kulipia kwa kutumia mitandao ya simu.
Mfumo huu wa kununua hisa kwa simu za kiganjani  ( *150*36#) umetengenezwa na kampuni ya kitanzania ya Maxcom Africa (Maxmalipo) ikishirikiana na Soko la hisa la Dar es Salaam(DSE)  na ni mfumo rasmi wa kuuza na kununua hisa kwenye soko la hisa .
Bw. Deogratius Lazari ametoa wito kwa watanzania kushiriki ununuzi wa hisa kwa njia ya simu ya kiganjani na kuhakikisha wanafanya malipo mapema  kupitia kwa mawakala wa Maxmalipo  walioko nchi nzima  takribani Mawakala Elfu kumi na sita .

DK.SHEIN AREJEA ZANZIBAR KUTOKA DODOMA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi pamoja na Viongozi wengine  waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar akitokea Dodoma katika Mkutano Mkuu malaaum uliofanyika juzi,[Picha na Ikulu.] 13/03/2017.
REE
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini Christina Mndeme (kushoto) pamoja na ujumbe aliofuatana nao wakati alipokuwa akiondoka katika uwanja wa ndege wa Dodoma leo baada ya kumalizika kwa Vikao vya Chama cha CCM Ukiwemo Mkutano Mkuu maalum uliofanyika juzi katika ukumbi wa mpya wa Kiwete Hall uliopo nje ya Mji wa Dodoma,

MAAFISA MAWASIALIANO SERIKALINI WATAKIWA KUUZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI.

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao (hayupo pichani) wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini mapema hii leo Mjini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi cha maafisa hao mapema hii leo mjini Dodoma, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass .
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi mapema hii leo mjini Dodoma.
Bw. Dotto Paul toka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (IJMC) akitoa mada kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao (hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi mapema hii leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Theophil Makunga akitoa mada kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao (hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
Afisa Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. Innocent Mungi akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali mapema hii leo mjini Dodoma.

Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo


………..


Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru Millao amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuuza huduma zitolewazo na Wizara au Taasisi husika kwa lengo la kutekeleza shughuli za Serikali.

Bibi Nuru Millao ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina ndogo wakati wa Kikoa Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kilicholenga kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini.

“Katika kikao hiki tutapata nafasi ya kujadiliana namna bora ya kuboresha mawasiliano katika maeneo yetu ya kazi, kuisemea Serikali, kuitendea haki Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za Serikali” alisema Bibi. Millao.

Kwa upande wake Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. Dotto Paul alisema kuwa wajibu mkuu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni Kufuatilia kwa ukaribu nini kimeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa lengo la kuwa tayari kujibu au kufuatilia habari zinazohusu Serikali.

Bw. Paul aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini katika kutoa taarifa za Serikali kwa Umma kupitia vyombo vya habari na Wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa habari za Serikali kwa Umma.

Aidha alisema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za maafisa Mawasiliano katika kutimiza wajibu wao ikiwemo upungufu wa mafunzo kuhusu tasnia na ujuzi wa kutosha ambapo kuna fursa chache za mafunzo na masomo katika kuongeza ujuzi kwa maafisa mawasiliano.

Akisisitiza zaidi Bw. Paul alisema kuwa mbali na hayo vyombo vya Habari vina Wajibu wa kutoa Habari za Serikali kwa Umma na kuutarifu umma kuhusu mipango, shughuli na vipaumbele vya serikali pamoja na utekelezaji wake.

“Vyombo vya Habari vinatakiwa kuwa daraja na sauti muhimu kati ya umma na serikali kwa kuzingatia maoni, mahitaji ya umma na kuyawasilisha kwa walengwa kama taasisi a uviongozi kwa kusikiliza upande wao, na kuyaripoti” Alisema Bw. Paul.

Nae Bw. Theofil Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa Wahariri kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali, amewataka Maafisa Mawasiliano kuhakikisha wanasimamia idara zao ipasavyo kwa kutoa taarifa sahihi kwani vyombo vya habari vinawategemea kwa kiwango kikubwa.

“Mawasiliano na mahusiano ya Wahariri na Maafisa Mawasiliano Serikalini yawe ya ukaribu na kuelewana ili kuweza kupata taarifa sahihi na kwa upana zaidi kuhusu tukio fulani kwa lengo la kuboresha shughuli za Serikali” alisema Bwa. Makunga.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 14,2017

WANANCHI WA JAMII YA WAFUGAJI NGORONGORO WATOA MALALAMIKO YAO KWA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI,MALISILI NA UTALII.

$
0
0
Wananchi wa jamii ya wafugaji waliposimama katikati ya barabara ya kuingia Makao makuu ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro kwa lengo la kuzuia msafara wa Kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii ilipotembelea Ngorongoro.
Wananchi wa jamii ya wafugaji wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wakilelekea makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro mara baada ya kuomba kutoa kero zao mbele ya kamati hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro,Rashid Taka akitoa neno la ukaribisho kwa wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii ilipotembelea wilaya ya Ngorongoro.
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakiwa katika kikao hicho.
Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Atashasta Ndetiye akizungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji  makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro
Wananchi wa Ngorongoro wakifuatilia maelezo ya Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Atashasta Ndetiye alipozungumza nao.
Mbunge wa jimbo la Siha na Mjumbe wa kamati ya Bunge ya Ardhi,Maliasi na Utalii ,Godwin Mollel akizungumza wakati wa kikao hicho. 
A 
Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Edward Maura akitoa malalamiko yao kwa kamati ya kudumu ya Bunge ya Maliasili na Utalii ilipofika makao makuu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuzungumza naao.
Wananchi wa jamii ya Wafugaji wanaoishi katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro wakifanya maombi mara baada ya kumalizika kwa kikao na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.
Viewing all 46334 articles
Browse latest View live




Latest Images