Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1164 | 1165 | (Page 1166) | 1167 | 1168 | .... | 1897 | newer

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Taasisi ya Kova Foundation (Sukos) imetoa mafunzo kwa wanawake namna ya kuweza kukabili majanga mbalimbali yanayoweza kutokeza.

  Akizungumza katika mafunzo kwa wakazi wa Tandale,  Mkuu wa Mikakati na Mipango wa Sukos,  Mariam Leisan amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani wamemua kutoa mafunzo ya majanga kutokana na wanawake ndio waathirika wa majanga hayo.

  Mariam amesema kuanza kwa mafunzo hayo eneo la Tandale ni kwasababu miongoni mwa watu waliopata majanga ikiwemo mafuriko na kushindwa kujiokoa katika sehemu salama.Amesema wanawake na watoto ndio waathirika wa majanga hivyo wakipewa elimu ya kujiokoa katika majanga ni sawa kuokoa familia nzima pale janga linapoingia.

  Aidha amesema kuwa wataendelea kutoa mafunzo mbalimbali juu ya wananchi kujiokoa pale yanapotokea.
  Mkuu wa Mikakati na Mipango wa Sukos,  Mariam Leisan akizungumza na waandishi habari katika mafunzo ya wanawake kuhusu kujiokoa na majanga kwa wakazi wa Tandale leo jijini Dar es Salaam.
  Balozi wa Sukos, Salim Ahmedy  (Gabo Zigamba) akizungumza katika mafunzo ya wanawake wa Tandale juu ya kujiokoa katika majanga mbalimbali kwenye jamii leo. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
  Baadhi ya wanawake wa Tandale wakiwa katika mafunzo ya kujikinga na majanga ambayo yameandaliwa na Sukos leo.

  0 0

  Waziri Kairuki (wa pili kutoka kushoto) akifanya usafi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) leo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Kushoto ni Mkurugenzi wa Uuguzi wa Muhimbili, Agness
  Mtawa. Kutoka kulia wa kwanza ni Katibu wa Umoja wa Wanawake katika Wilaya ya Ilala, Joyce Ibrahimu Mkaugala na Zuhura Mawona wakifanya usafi Leo katika hospitali hiyo.
  Waziri Kairuki akizungumza na kinamama waliojifungua watoto kabla ya kuwapatia zawadi ya nguo za watoto, pampazi na sabuni.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akizungumza na  wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo kabla ya kukabidhi vitanda 10 na magodoro 10 kwa uongozi wa hospitali hiyo. Katika kusherekea siku ya wanawake duniani leo, pia Waziri huyo amewapatia kinamama zawadi mbalimbali zikiwamo nguo za watoto na sabuni. Kushuto Mkurugenzi wa Uunguzi katika hospitali hiyo, Agness Mtawa.

  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejementi ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mheshimiwa Angellah Kairuki akikabidhi vitanda 10 na magodoro 10 kwa Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),Agness Mtawa.
  Mkurugenzi wa Uuguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agness Mtawa akimshukuru Waziri Kairuki baada ya kupokea msaada wa vitanda na magodoro leo.Picha na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

  Hospitali ya Taifa Muhimbili –MNH- leo imeungana na wanawake
  wengine ulimwenguni kote kuadhimisha siku ya wanawake Duniani kwa kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya hospitali hiyo.

  Zoezi hilo limeongozwa na Mbunge wa Vitimaalum mkoa wa Dar
  es salaam Mheshimiwa Angellah Kairuki kwa niaba ya Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi –UWT- mkoani humo.

  Mheshimiwa Kairuki ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya
  Rais Utumishi na Utawala Bora amesema katika kusheherekea siku ya wanawake Duniani UWT imeona ni vema wakashiriki
  katika shughuli mbalimbali za kijamii ili kuonesha dhamira ya dhati kwamba CCM inawajali wananchi wake bila kujali itikadi ya chama.

  ‘’ Sisi tumekuja hapa Muhimbili kushiriki na nyinyi katika kuadhimisha
  siku hii kwa kufanya usafi bila kujali itikadi ya chama kwani Hospitali hii
  inahudumiwa wananchi wote , pia siku hii ya leo tunatoa msaada wa vifaa mbalimbali vya watoto na wenzetu wengine wameenda katika Hospitali
  zingine wote tukiwa na lengo moja’’. Amesema Waziri Kairuki.

  ‘’Msaada tuliotoa ni vitanda kumi, magodoro kumi , mashuka na vifaa vingine mbalimbali vya watoto zikiwamo nguo ,sabuni na Pampers lengo
  ni kuunga mkono juhudu za serikali za kuboresha huduma za afya hususani afya ya mama na mtoto na kuhakikisha hakuna mgonjwa anayelala chini kwa kukosa kitanda’’ . Amesema Mheshimiwa Kairuki.

  Akipokea msaada wa vitanda hivyo Mkurugenzi wa Huduma za
  Uuguzi na Ukunga wa MNH Agnes Mtawa amewashukuru UWT kwa msaada walioutoa ambao amesema umekuja wakati muafaka kwani utasaidia katika kutekeleza majukumu yao .

  Hata hivyo Mkurugenzi Mtawa amewakumbusha wauguzi kuendelea
  kufanya kazi kwa kufuata maadili na kusisitiza kuwa kazi hiyo inahitaji kujitoa na kuwa na moyo wa huruma .

  Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila Machi nane ambapo
  kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘’ Tanzania ya Viwanda , Wanawake ndio msingi wa mabadiliko ya kiuchumi .

  0 0

  Asasi ya Kibunge inayojihusisha na masuala  ya Idadi ya watu na maendeleo (TPAPD) imeelezea umuhimu wa kuweka kipaumbele kwenye masuala ya uzazi wa mpango ili kukabiliana na ongezeko la kasi la idadi ya watu  ambayo kwa sasa ni wa asilimia 2.7 kwa mwaka.

  Tamko la TPAPD lilitolewa leo katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, limesema matumizi ya njia za uzazi wa mpango yanaweza kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi (MMR) kwa asilimia 44, na kupunguza vifo vya watoto kwa asilimia 35. Vifo vya wanawake katika uzazi vimefikia 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2015 kutoka vifo 454 katika kila vizazi hai mwaka 2010.

  TPAPD chini ya Mwenyekiti wake Mhe Dkt Mary Mwanjelwa iliamua kutoa tamko hili hivi karibuni katika kikao cha kamati tendaji mjini Dar es Salaam kilichojadili umuhimu wa uzazi wa mpango katika harakati za kujenga Tanzania ya uchumi wa kati na uchumi wa viwanda.

  Tamko hilo lililotiwa saini na Mwenyekiti Dkt Mwanjelwa limesema:
  “uzazi wa mpango unahitajika katika kuiwezesha nchi kukabiliana na ongezeko la kasi la idadi ya watu inayochangiwa na uzazi wa kiwango cha wastani wa watoto sita kwa kila mwanamke aliye katika umri wa uzazi. Hali hii huchangia utegemezi pamoja na umaskini; na pia hudumaza juhudi za taifa za kufikia malengo ya maendeleo”.

  “TPAPD inatambua na kuunga mkono kwa dhati kasi ya  utekelezaji wa mpango Mkakati wa Taifa wa kuimarisha afya ya uzazi, afya ya mama na mtoto, na vijana (RMNCAH II 2016-2020),” na inaahidi kuwa bega kwa bega  katika kufanikisha upatikanaji wa  huduma bora za  uzazi wa mpango kwa wote hapa nchini”, limesema Tamko hilo.

  Mhe Mwanjelwa amesema TPAPD inatambua mafanikio yaliyopatikana katika kulifanya suala la uzazi wa mpango kuwa  nguzo muhimu katika mpango wa taifa wa RMNCAH ambao pia unajulikana kama One Plan II, unaolenga kuongeza matumizi uzazi wa mpango kila mwaka, kupunguza vifo vya wanawake na watoto, na kuimarisha afya ya uzazi kwa vijana. Ifikapo 2020, Tanzania imeweka lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kufikia 293 kwa kila vizazi hai 100,000.

  Ikitambua mchango wa wabunge wote katika kuweka mazingira wezeshi ya kisera na kwa serikali kutenga bajeti ya uzazi wa mpango, TPAPD imetaka jitihada za dhati ziendelee kufanyika kuhakikisha ununuzi na usambazaji wa taarifa sahihi, njia za uzazi wa mpango, na vifaa vya kuimarisha afya ya uzazi kote nchini.

  0 0

  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua kituo na kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkazi wa shirika la UN women Tanzania Maria Karadenizli. 
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akitazama jiwe la msingi la kiwanda na kituo cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida. 
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi wakikagua hatua za uongezaji wa thamani wa mazao ya nafaka kama mahindi, mtama na uwele katika kiwanda kinachomilikiwa na kikundi cha akina mama VICOBA wa Wilaya ya Singida.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi wakikagua kiwanda cha mafuta cha Mount Meru Millers kilichopo mjini Singida, kiwanda hicho huzalisha mafuta ya alizeti ambayo ni mazuri kwa afya.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akionyesha ndoo ambayo ni kifungashio cha mafuta ya alizeti
  yanayozalishwa katika kiwanda cha mount Meru millers Mkoani Singida.
  Akina mama wa Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Waziri wa afya,
  Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi wakiandamana na kutoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani.
  Akina mama wa Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Waziri wa afya,
  Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi wakiandamana na kutoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani.
  Mbunge wa Viti maalum CCM mkoa wa Singida Aisharose Matembe akiwa na
  akina mama wa Mkoa wa Singida wakipita mbele ya Waziri wa afya,
  Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi wakiandamana na kutoa ujumbe wa siku ya wanawake duniani.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akionyesha ndoo ambayo ni kifungashio cha mafuta ya alizeti
  yanayozalishwa katika kiwanda cha mount Meru millers Mkoani Singida.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akikagua kitanda cha chumba cha upasuaji katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki (kulia) na mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Singida Aisha rose Matembe (kushoto) wakiwa nje ya jengo la utambuzi wa magonjwa la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida.
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akiwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta John Mwombeki (kulia) na mbunge wa viti maalumu CCM mkoa wa Singida Aisha rose Matembe (kushoto) wakiwa nje ya jengo la utambuzi wa magonjwa la hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Singida
  Waziri wa afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia, wazee na watoto Ummy Mwalimu akipanda viazi katika eneo la kituo na kiwanda cha kuongeza thamani mazao ya nafaka cha Ititi kinachomilikiwa na vikundi vya akina mama VICOBA wa wilaya ya Singida, kulia kwake ni Mbunge wa viti maalumu CCM Mkoa wa singida Aisha rose Matembe na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkaziwa shirika la UN women Tanzania Maria Karadenizli wa kwanza kabisa kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dokta Rehema Nchimbi .

  0 0

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwa ameambatana na baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, CCM wakikabidhi vitu mbalimbali Kwa mkurugenzi wa hospitali ya Ocean Road hii leo jijini DSM.
  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiwa ameambatana na viongozi wa hospitali hiyo muda mfupi baada ya kuwasili katika hospitali hiyo.
  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlojia Profesa Joyce Ndalichako akiwajulia hali wagonjwa mbalimbali ambao alifika kuwajulia hali pamoja na kuwapatia msaada wa vitu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) imekanusha juu ya uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uuzaji wa viwanja katika eneo ka Mkonze lililopo mkoani Dodoma.

  Tamko hilo limetolewa hivi karibuni mkoani Dodoma na Kaimu Meneja Uhusiano wa CDA, Angela Msimbira kutokana na kusambaa kwa ujumbe huo katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

  Bi. Angela amesema taarifa hizo ambazo hazieleweki zimekuwa zikidai kuwa viwanja hivyo ni halali na ukinunua unapewa hati na CDA ambayo ndiyo imepewa dhamana ya ugawaji wa viwanja mkoani humo.

  “Mamlaka yetu inapenda kuutarifu Umma kuwa taarifa hizo si za kweli hivyo wananchi wanatakiwa kuzipuuza na kuendelea kufata utaratibu kwani mamlaka hiyo ina utaratibu uliopangwa wa namna ya kupata viwanja vilivyo halali,”alisema Bi. Angela.

  Amefafanua kuwa Mamlaka hiyo inapotaka kuuza viwanja hutumia utaratibu wa kutangaza kwenye vyombo vya habari, mitandao ya kijamii pamoja na kutoa matangazo kwa umma kwa njia ya vipaza sauti.

  Aidha, Bi. Angela ametumia fursa hiyo kuendelea kuwakumbusha wananchi kufuata taratibu za upatikanaji wa viwanja.

  Kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Jinai Mitandaoni ya mwaka 2015, ni kosa kwa mtu yoyote kutangaza, kuchapisha au kueneza habari za uongo au uzushi katika mitandao.

  0 0


  Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifurahia wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2018.  NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

  WAFANYAKAZI Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, leo Machi 8, 2017, wameungana na wenzao katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe- Yanga jijini Dar es Salaam.

  Katika maadhimisho hayo yaliyohanikizwa na mvua za rasharasha, wanawake hao wakiwa na furaha, walipita mbele ya viongozi wakuu wa mkoa na kuonhyesha mabango yao yaliyokuwa na ujumbe tofauti tofauti.


  Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.


  Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

  Katika maadhimisho hayo ya siku ya Wanawake Duniani Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye awali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ilisema Mkuu huyo wa Mkoa ndiye angekuwa mgeni rasmi lakini hakutokea.
  Katika hotuba yake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, alisema jamii inapaswa kutimiza wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
  Baadhi ya akina mama wa taasisi ya THTU nao wakipita mbele ya jukwa kuu
  Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2018.

  Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Felix Lyaviva, (kushoto), akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, wakati wakipokea maandamano ya akina mama. Lyaviva alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


  Baadhi ya wanawake wa TANESCO nao wakipita mbele ya jukwaa kuu

  Mwanadada mwenye kipaji cha kusakata kabumbu akionyesha umahiri wake, hii ilikuwa ni sehemu ya burudani zilizokuwepo uwanjani

  Picha ya pamoja ikionyesha wafanyakazi wanawake ya PPF walioshiriki kwenye maadhimisho hayo

  0 0


  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza katika kipindi cha michezo kinachorushwa na Radio Efm katika ziara yake ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye ( kulia) akizungumza na wafanyakazi wa Radio Efm (hawapo katika picha) wakati wa ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Meneja Mkuu wa Radio Efm Bw.Denis Ssebo.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (wa pili kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Radio ya Efm Francis Ciza (wa kwanza kulia) alipoitembelea Radio hiyo leo Jijini Dar es Salaam wengine ni Meneja Mkuu wa radio hiyo Bw. Denis Ssebo (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas (wa kwanza kushoto).
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watangazaji wa Radio ya Efm a) alipoitembelea Radio hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kushoto) akipata maelekezo wa namna uuandaji wa habari unavyofanywa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kutoka kwa Mhariri wa Habari wa kituo cha televisheni cha TV1 Bibi. Lulu Sanga(kulia) katika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (aliyekaa) akionyeshwa muundo wa studio ya kituo cha Televisheni cha Tv1 na Mkuu wa Uzalishaji wa Vipindi Bw.Mukhsin Mambo (kushoto) wakati wa ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kituo cha Televisheni cha TV 1 wakati wa ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa radio Times fm Bw.Rehule Nyaukwa (katikati) na kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas wakati wa ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akionyeshwa namna urushwaji wa matangazo unafovyanywa kwa kutumia la matangazo ya nje (OBVAN) na Afisa Tehama wa radio Times Fm Bw Dickson Zuri watika ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Radio ya Times Fm wakati ziara ya kuvitembelea vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam. (Picha na Lorietha Laurence WHUSM).

  0 0
  Maafisa Afya na Mazingira kutoka (SUZA) Nahya Khamis Nassor Mwanafunzi wa mwaka wa Tatu wa Chuo cha SUZA anayetowa mafunzo ya Afya na mazingira kwa Wanafunzi wa Skuli ya Kijini Matemwe akizungumza na waandishi wa habari kufanikiwa kwa zoezi hilo la kutowa elimu kwa wanafunzi wa Skuli hiyo jinsi ya kuhifadhi mazingira na afya yao. Mradi huo unaosimamiwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Kitalii Matemwe Pennyroyal kwa kutowa elimu hiyo.

  Amesema umeleta mafanikio makubwa kwa watoto hao jinsi ya kujilinda na maradhi ya mripuko kwa kupata elimu hiyo.

  Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu wa SUZA Nahya Khamis Nossor akitowa mafunzo ya Afya ya Mazingira kwa Wanafunzo wa Skuli hya Sekondari ya Kijini Matemwe jinsi ya kujikinga na maradhi ya mripuko kwa kutunza mazingira safi katika maeneo yao na skuli, Mradi huo wa Elimu hiyo unafadhiliwa na Kampuni ya Ujenzi wa Kijiji cha Utalii Matemwe Pennyroyal.
  Wanafunzo wa Skuli ya Sekondari na Msingi Kijiji cha Kijini Matemwe Wilaya ya Kaskazini A Unguja wakifuatila mafunzo hayo wakiwa katika darasa wakifuatilia kwa utulivu wakiangalia vipeperushi vinavyoelezea utungaji wa Afya na Mazingira katika jamii.
  Afisa Afya na Mazingira Bi Zeldat Masoud Khamis akitowa mafunzo kwa wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe jinsi ya elimu ya afya ya mazingira kwa wanafunzi hao.
  Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatilia Mafunzo hayo yanayotolewa na Maafisa wa Afya na Mazingira wakitowa elimu hiyo.
  Wankatika mafunzo ya vitendo jinsi ya kusafisha mikono kujinginga na maradhi na kuweka mazingira mazuri ya afya yake. kwa kutumia maji na sabuni kufanya usafi kabla ya kula na baada ya kutoka msalani.

  Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari Kijini Matemwe wakifuatilia kipeperushi kinachoelezea Afya ya Mazingira. wakati wa mafunzo yao.
  Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja wakifuatila vipeperushi vinavyoeleza utunzaji wa Afya na Mazingira ili kujikinga na maradhi ya matumbo na kipindupindu, Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa Kampuni ya Pennyroyal inayojenga Kijiji cha Utalii Matemwe Zanzibar.

  Imetayarishwa na OthmanMapara. Blogspot.com

  Zanzinews.com

  email.othmanmaulid@gmail.com.

  0 0

   Mkuu wa maduka ya rejareja  wa Vodacom Tanzania,Brigita Stephen (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu mjasiliamali Neema Nzuki aliyejiajiri na  kuwaingiza  wateja wapya wa Vodacom Tanzania wa manispaa ya Dodoma,Wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa  ujasiliamali mkoani hum oleo yaliyoandaliwa na Vodacom Tanzania.
   Akina mama wajasiliamali wa Mkoa wa Dodoma wakiwa kwenye picha ya pamoja baad ya kushiriki mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na Vodacom Tanzania leo  katika maadhimisho ya siku ya wananawake Duniani.
   Mkuu wa maduka ya rejareja ya Vodacom Tanzania, Brigita Stephen akikata keki na Katibu wa Voice of Women Entrepreneurs Tanzania (VOWET) Anna Otieno ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Wananawake Duniani leo mjini Dodoma.
   Mkuu wa maduka ya rejareja ya mauzo ya simu Vodacom Tanzania,Brigita Stephen  akizungumza na akina mama wajasiliamali wa mkoa wa Dodoma leo,Wakati wa mafunzo ya ujasiliamali kwa akina mama hao katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani.
  Mwezeshaji wa masomo ya ujasiliamali Ben Mwambela akitoa mada ya ujasiliamali kwa akinamama wa mkoa wa Dodoma  leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani,mafunzo hayo yalifadhiliwa na Vodacom Tanzania. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na mfuko wa Maendeleo wa mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication Services Fund.Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu mkoani Dodoma.
   Meneja Mauzo wa Airtel Tanga  John Nada alisema  "Airtel tumejipanga kuendelea kutoa mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba ileile ikiwa hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre  Airtel ndio mtandao wenu wa ukahika kwa sasa”
  “Tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa wabunifu zaidi,  tumumieni  huduma ya Airtel Money kwa kuwa pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada
  Kauli ya wananchi  juu ya tatizo la mawasiliano zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa  Kata hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye vilele vya milima wakitafuta mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara na mambo mengine ya kijamii.
  “Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema, awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu yenye muinuko” alieleza Mh Mahunda-Diwani. 
   Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo  wa Airtel Tanga John Nada wakikata autepe kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
   Vifijo baada ya uzinduzi wa mnara huo
    Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda akiongea na wananchi waliojawa na furaha baada ya uzinduzi wa mnara huo.
   Mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga vikiwemo Balangai, Hebangwe, Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme, Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre . Airtel mwaka huu imeanzisha kampeni hiyo na UCSAF ili kupanua mawasiliano katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mawasiliano.
  Diwani wa kata ya  kata ya Mponde Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga Mh Edwin Mahunda pamoja na Meneja mauzo  wa Airtel Tanga John Nada wakiwa katika picha ya pamoja na baasdhi ya wananchi baada ya kuzindua mnara wa mawasiliano uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na mfuko wa maendeleo wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ili kutoa mawasiliano kwa zaidi ya vijji 16 mkoani Tanga

  0 0


  Wanawake wanaofanya kazi katika Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu uliopo katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wameadhimisha siku ya wanawake duniani Machi 8,2017 kwa kutoa zawadi ya baiskeli kwa wanafunzi wa shule za sekondari pamoja na kuwatembelea na kuwapatia zawadi wagonjwa waliolazwa kwenye vituo vya afya.

  Wanawake hao wametoa zawadi ya baiskeli 10 zikiwemo 8 kwa ajili ya wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao katika shule ya Sekondari Bulyanhulu na Bugarama na baiskeli mbili kwa ajili ya walimu wa kike walezi wa wanafunzi hao.

  Mbali na kutoa zawadi kwa wanafunzi,pia wametembelea kituo cha afya cha Bugarama na Lunguya vilivyopo jirani na mgodi huo kisha kutoa zawadi ya shuka 70 kila kituo na kuwapa wauguzi na wagonjwa sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 12.

  Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake,Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo alisema wameamua kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kuwapongeza wanafunzi wanaofanya vizuri shuleni ili kuwapa ari ya kujifunza zaidi na kuwarahisishia usafiri kufika shuleni.

  “Tuwatembelea wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama,tumetoa msaada wa baiskeli 10 hivyo kila shule imepata tano ambapo nne kwa ajili ya wanafunzi kike na moja ni kwa ajili ya walimu wa kike kwa kila shule”,alieleza Senkondo.

  “Pia tumetoa shuka 140 kwa ajili ya vituo vya afya viwili,Bugarama na Lunguya kisha kugawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa waliopo katika vituo hivyo”,aliongeza Senkondo.

  Senkondo alisema wameamua kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kukutana na watoto wa kike na wanawake ili kuwahamisha wanawake katika jamii kushiriki katika shughuli za migodi kwani wanaweza.

  Mwandishi wetu Kadama Malunde,alikuwepo wakati wa maadhimisho hayo,ametuletea picha za matukio yaliyojiri mwanzo hadi mwisho…Tazama hapa chini
  Wanafunzi wa shule ya sekondari Bulyanhulu wakiwa katika shule hiyo iliyopo katika kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga wakisubiri kupata zawadi kutoka kwa wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia dhahabu wa Bulyanhulu uliopo jirani na shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 920 wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi baiskeli nne kwa ajili ya wanafunzi wa kike waliofanya vyema katika mitihani yao ili ziwasaidie kurahisisha usafiri kufika shuleni lakini pia baiskeli moja kwa ajili ya mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule hiyo

  Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwalimu mlezi wa wanafunzi katika shule ya sekondari Bulyanhulu ,mwalimu Bumi Mwasalujonja
  Mwalimu Bumi Mwasalujonja akiwa amebeba juu baiskeli wakati akikabidhiwa na wanawake kutoka mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi baiskeli kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi aliyefanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 baada ya kupata daraja la kwanza

  Mwanafunzi wa kidato cha tatu Irene Gimi akiondoka na baiskeli yake

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akishikana mkono na mwanafunzi wa kidato cha tatu Zainab Kisambale aliyepata daraja la pili katika mtihani wa kidato cha pili mwaka 2016 na anaongea kwa ufasaha zaidi lugha ya Kiingereza

  Wanawake kutoka mgodi wa Bulyanhulu akiwa na wanafunzi wanne waliofanya vizuri katika mtihani

  Hapa ni katika shule ya Sekondari Bugarama iliyopo kata ya Bugarama ambayo imejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu.Katika shule hii pia wanafunzi wanne wa kike waliofanya vizuri katika masomo yao walipata zawadi ya baiskeli,huku mwalimu wa nidhamu naye akipata zawadi ya baiskeli

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidh baiskeli kwa mwalimu wa nidhamu/mlezi shule ya sekondari Bugarama Prisca Mwanantemi

  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi baiskeli kwa mwalimu Prisca Mwanantemi

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Bulyanhulu Zuwena Senkondo akimtambulisha mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo Jesca Peter ambaye hivi karibuni alifanya vizuri katika mtihani wa majaribio. Mwanafunzi huyo amepata zawadi ya baiskeli

  Wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo yao pamoja na mwalimu wao wakiwa wameshikilia baiskeli zao

  Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika shule ya sekondari Bugarama yenye jumla ya wanafunzi 766

  Hapa ni katika Kituo cha afya Bugarama kilichopo katikakata ya Bugarama halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama.Kituo hiki cha afya kimepewa shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa.Kulia ni Muuguzi katika kituo hicho Mwalushani Mabula akizungumza wakati wa kupokea shuka 70,sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa waliokutwa katika kituo hicho siku ya siku ya wanawake duniani Machi 8,2017

  Wa pili kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza wakati wa kukabidhi shuka 70 kwa ajili ya wagonjwa lakini pia sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka kwa ajili ya wauguzi na wagonjwa katika kituo hicho cha afya

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Muuguzi kituo cha afya Bugarama Mwalushani Mabula

  Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Bugarama

  Zoezi la kugawa shuka likiendelea. Kituo cha afya Bugarama kimejengwa na mgodi wa Acacia Bulyanhulu

  Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi za wagonjwa kwa ajili ya kuwapatia zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akiwa katika wodi ya wazazi akiwaeleza akina mama waliojifungua kuwa wameamua kuwatembelea ili washerehekee kwa pamoja katika siku ya wanawake duniani kwa kuwapatia msaada

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akitoa zawadi ya sabuni kwa Tedy Paul

  Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wamebeba mtoto aliyezaliwa na Salome Raphael baada ya kumpatia zawadi ya vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno

  Zoezi la kugawa zawadi wodini likiendelea,ambapo kila mgonjwa alipewa vipande 10 vya sabuni,mafuta ya kupaka na dawa ya meno

  Ndani ya wodi ya wazazi baada ya kumaliza kutoa sabuni,dawa za meno na mafuta ya kujipaka

  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakifurahia baada ya kutembelea kituo cha afya Bugarama

  Wanaendelea kufurahia


  Picha eneo la kituo cha afya Bugarama baada ya kutoa zawadi kwa wagonjwa

  Hapa ni katika kituo cha afya Lunguya ambapo pia wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu walitoa zawadi ya shuka 70,sabuni,mafuta na dawa za meno kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho cha afya. Kulia ni Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza katika kituo hicho

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza kabla ya kutoa zawadi hizo.Kulia ni wauguzi katika kituo hicho

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo kwa ajili ya wagonjwa katika kituo hicho

  Afisa Uhusiano wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akikabidhi shuka kwa wauguzi wa kituo cha afya Lunguya

  Akina mama kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakigawa sabuni,mafuta na dawa za meno kwa akina mama ndani wodi ya watoto

  Ugawaji wa zawadi unaendelea

  Mama akifurahia baada ya kupata zawadi ya sabuni,dawa ya meno na mafuta ya kujipaka

  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakielekea katika wodi nyingine ya wagonjwa

  Wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakimpatia zawadi mama aliyelazwa katika wodi ya akina mama

  Zoezi la kugawa zawadi likiendelea

  Mwanamme anayeuguza mama yake mzazi wodini naye akapewa zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa ya meno

  Kulia ni Afisa tabibu wa kituo cha afya Lunguya,Dkt. John Malongo akiwaaga wanawake kutoka mgodi wa Acacia Bulyanhulu

  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiondoka katika kituo cha afya Lunguya baada ya kumaliza kutoa zawadi kwa akina mama na akina baba waliokuwa katika kituo hicho wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog WANAWAKE MGODI WA BULYANHULU WASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTOA MSAADA KWA WANAFUNZI NA WAGONJWA

  0 0


  0 0


  Na Rhoda Ezekieli Kigoma

  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amepiga marufuku vitendo vya baadhi ya wanaume Mkoani humo kuwadhurumu na kuwatishia kuwafukuza wake zao pindi wanapothubutu kutetea haki zao,badala yake amewataka washirikiane nao kutambua na kuchangamkia fursa za maendeleo zilizopo nchini.

  Mkuu huyo wa Mkoa aliitoa kauli hiyo wakati akifunga maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Mkoani humo ambayo kimkoa yalifanyika katika kijiji cha kinyinya kata ya nyamutukuza wilayani kakonko Mkoani humo .
   
  RC Maganga alisema kuwa pamoja na mambo mengine, wakati umefika kwa wanawake kuamka na kusimamia haki zao ikiwa ni pamoja na kutokukubali kubaki nyuma kwa kuchangamkia fursa hizo zinapozitokeza.

  Alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi,Wake wanapo kuwa wakijishughulisha kutafuta fedha ili kuzitunza familia zao, wanawanyang'anya na kwenda kuzitumia kwenye  starehe zao, suala ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya Wanawake wengi.
   
  Katika kuhakikisha suala la kuwa Nchi ya viwanda, ni lazima wanawake kushirikiana na wanaume katika kufanya kazi ili kuongeza kipato katika familia na taifa kwa ujumla.

  " wanawake Msikubali hawa wanaume wawanyanyase, akikutishia uondoke njoo ushitaki kwangu ataondoka yeye na akuache wewe unalea familia, nataka mpaka muda wangu utakapo fika wa kuondoka Kigoma kila mtu awe na eneo lake mwanamke na mwanaume, na eneo moja kwa ajili ya familia lazima tuhakikishe tunatoka katika mfumo wa unyanyasaji katika kuelekea, uchumi wa viwanda", alisema Maganga.

  Aidha Maganga alisema ni wakati wa Wanawake kufanya mapinduzi ya ghafla katika kuelekea hamsini kwa hamsini kama kaurimbiu ya mwaka huu inavyo sema Tanzania ya Viwanda mwanamke ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi kwa kutambua uthamani huo wanawake wanatakiwa kutumia Fursa hiyo kuunda vikundi vya ujasiliamali na kuanza kuzalisha bidhaa na kuziongezea ubora.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala aliwataka wanawake Wilayani humo kuunda vikundi vya ujasiriamali iliwaiwe rahisi kwa baadhi ya taasisi zinazo jitolea kutoa elimu za ujasiriamali na mikopo mbali mbali ilikuwawezesha iwe rahisi kupata msaada huo.

  Ndagala alisema katika vikundi watakavyo anzisha wajitahidi kuanzisha vikoba pamoja na ununuzi wa hisa vitakavyo wasaidia kuinuana kiuchumi na kauri mbiu ya kuelekea katika Nchi ya viwanda kufikiwa kwa urahisi.

  Nae Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Kigoma Zilpa Kisonzela alisema mpaka sasa Mkoa wa kigoma umekwisha toa shilingi milioni 375 kwa vikundi mbali mbali vya wajasiriamali vinavyo endelea kuwawezesha wanawake wengi kufanya biashara zao kwa kuzalisha bidhaa mbali mbali zenye ubora na kuziuza ndani na nje ya Nchi.

  Sambamba na kutoa fedha hizo kumekuwa na elimu inayo tolewa kwa wajasiriamali wanao thubutu katika vikundi mbali mbali kwa kuwaelimisha jinsi ya kuzalisha bidhaa zenye ubora na usindikaji wa matunda, katika eneo la Viwanda vidogo vidogo SIDO mkoani humo kumekuwa na wajasiliamali wakubwa wanao zalisha unga wa muhogo, mafuta ya mise, Sabuni za magadi na sabuni za kusafishia chooni ni bidhaa wanazo ziuza nje na ndani ya Nchi na zinaendelea kuwaongezea kipato.

  Maadhimisho ya siku ya wanawake Mkoani Kigoma yameanza kwa mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga kuongoza zoezi usafi na uchangiaji damu katika kituo cha afya cha nyanzige na kutoa zawadi mbali mbali kwa wanawake walio jifungua na waliojitokeza katika maadhimisho hayo.
  Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa zawadi kwa mmoja wa akina mama aliyejifungua katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma.
  RC Maganga akiwasikiliza akina mama mbalimbali waliofika katika kituo cha afya cha Nyanzige,Wilayani Kakonko mkoani Kigoma kujipatia matibabu mbalimbali,kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko,Kanali Hosea Ndagala
  Akina Mama wakisherehekea siku ya Wanawake hapo jana
  RC Maganga akiwa ameongozana na DC wa Kakonko,Kanali Hosea Ndagala wakipata maelezo mbalimbali kutoka kwa wajasiliamali,kufuatia bidhaa zao walizozitengeneza

  0 0
 • 03/08/17--22:00: RAIS DKT SHEIN AREJEA NCHINI
 • Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakiagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo akimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakizungumza na kuagana na Mhe, Airlangga Hartarto ambae ni miongoni mwa Viongozi wakuu Nchini Indonesia katika uwanja wa Ndege wa Soekarno Hatta Mjini Jakarta Nchini Indonesia baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi IORA Nchini humo Dk.Shein alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli, 

  [Picha na Ikulu.] 09/3/2017.

  0 0


  NA Evelyn E. Mkokoi – Pemba

  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masula ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, ameipongeza Miradi ya tasisi za Muungano Kisiwani Pemba, kwa kile alichodai, kutekelezeka kwa asilimia kubwa na kutatua kero za wananchi.

  Naibu Waziri Mpina Aliyasema hayo Kisiwani Pemba katika ziara yake ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi inayotekelezwa chini ya taasisi za muungano na mashirika ya TASAF na MIVARF, ikiwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa soko, barabara, hospitali shule, ujenzi wa mabwa, matuta kama makingio ya maji ya chumvi yanayosaidia kuhimili madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na miradi mbali mbali ya maendeleo.

  Mpina aliwataka wakazi wa kaskazini na kusini Pemba kwa Pamoja kushirikiana na waithamini na kuitunza miradi hiyo inayotekelezwa kwa thamani ya shilingi za kitanzania Bilioni 14.297,na kusema kuwa ina manufaa kwa wakazi hao, na itaweza kudumu na kuwasidia kwa muda mrefu, akitolea mfano wa barabara yenye urefu wa kilometa 80 iliyojenjwa kusini Pemba.

  Alipotembelea mradi wa umeme unaopita chini ya Bahari kutoka mkoani Tanga, Mpina alisema kuwa, awali kisiwani Pemba umeme ulikuwa unawafikia watu wachache, lakini kwa sasa umeme umekuwa ni wa Bei nafuu wa uhakika naunawafikia watu wengi.

  Katika Ziara yake kisiwani Pemba, Naibu Waziri Mpina Pia alitembelea jengo la Makazi ya Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Kusema kuwa jengo hilo linatakiwa kutengewa fedha maalumu kwa ajili ya ukarabati, “viongozi wetu wakifanya kazi katika mazingira mazuri itaongeza ufanisi katika utendani wao.” Alisisitiza Mpina.

  Naibu Waziri Mpina takuwepo kisiwani Unguja na Pemba kutembelea na kukagu miradi ya Muungano.
   Naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, akipongeza miradi ya muungano kisiwani Pemba, wakati wa Ziara yake ya kutembelea Miradi Hiyo, kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya ChakeChake Bi Salama Mbarouk.
  Mratibu wa Mradi wa TASAF kisiwani Pemba Bw. Mussa Said Kissenge akielezea utekelezaji wa majukumu ya Mradi huo kisiwani pemba Kwa Mhe. Luhaga Mpina na ujumbe wake (hawapo pichani) wakati wa Ziara ya Naibu Waziri Huyo ya kutembelea Mirani ya Muungano kisiwani Pemba.
  Katika Picha ni moja ya tuta lililojengwa na mradi wa TASAF kisiwani Pemba, kunusuru maji ya chumvi kuingia katika mashamba ya wakulima na kuharibu mazao kisiwani Pemba, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa miradi ya Muungano.
  Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Luhaga Mpina akichanganya Saruji na mchanga kuwasaidia mafundi wanaojenga bwawa la kuhifadhia maji ya mvua, litakalotumika kuhifadhi maji kwa matumizi ya kilimo na mifugo kisiwani Pemba, ikiwa ni moja ya utekelezaji wa miradi ya Muungano chini ya TASAF.
  Katikati Injinia Said Kiure, wa Kiure Contraction ya Kisiwani Pemba, akimuelezea jambo Naibu Waziri Mpina, kuhusu ujenzi wa soko la wilaya ya Mwanakwerekwe linalojengwa chini ya mradi wa Muungano wa MIVARF.kushoto ni Mkurugenzi msaidizi Idra ya Muungano Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Lupi Mwaikambo.

  0 0

  Jovina Bujulu – MAELEZO.

  Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ni hatua muhimu kwa wanawake kujipambanua na kufanya tathmini jinsi wanavyoshiriki katika ujenzi wa taifa kiuchumi, kijamii na kisiasa.

  Serikali imeweka mikakati na mipango mbalimbali yenye lengo la kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, mama Sihaba Nkinga hivi karibuni alipokuwa akizungumzia mipango na mikakati mbalimbali iliyofanywa na Serikali katika kumkomboa na kumuinua mwanamke kiuchumi.

  Pamoja na kuwa wanawake wengi wameamka na wanajishughulisha katika masuala mbalimbali ya kiuchumi, Serikali pia inahakikisha inawawezesha ili waweze kufikia malengo yao katika masuala ya kujiinua kiuchumi na kuondokana na dhana ya utegemezi.

  “Serikali ina mipango mbalimbali katika kuhakikisha kuwa wanawake wamewezeshwa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kuanzisha benki ya Wanawake ambayo moja ya majukumu yake ni kuhakikisha wanawake wanapata mikopo kwa kuzingatia viwango wanavyoweza kulipa” alisema mama Nkinga.

  Aliitaja mikakati mingine kuwa ni pamoja na kuwa na mfuko wa maendeleo ya wanawake ambapo wanawake wanapewa mikopo yenye riba nafuu ambayo wanamudu kuilipa.

  Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wameweza kuwasaidia wanawake katika masuala ambayo yamekuwa yakiwasumbua kwa muda mfefu kama vile umiliki wa ardhi. Kupitia elimu hii kwa sasa wanawake wanaruhusiwa kumiliki ardhi kisheria na kuondoa utata kuhusu suala hili.

  Pamoja na mikakati hiyo, Serikali imeenelea kushirikiana na wadau kuhakikisha kuwa vikwazo mbali mbali vya mitaji na mikopo vinaondolewa ili kuhakikisha kuwa wanawake wengi wanapata fursa ya kukopa na kulipa kwa muda hivyo kuwa huru kuendelea na shughuli zao za kiuchumi.

  “Idadi kubwa ya wakina mama wapo kwenye ujasiriamali na viwanda vidogo vidogo hivyo Serikali imekuwa ikitoa elimu kwao na kuwahimiza kukopa kwenye vyombo na taasisi za fedha kwa sababu huko wanakopa kulingana na uwezo wao na hii itawasaidia kufanikisha shughuli zao za ujasiriamali“ aliongeza mama Sihaba .

  Aliwaasa wanawake kuachana na sekta isiyo rasmi na badala yake wajikite katika sekta rasmi maana huko kuna uzalishaji mkubwa ambao utawapatia soko la nje na aliwataka kuboresha bidhaa zao ili wawe tayari katika ushindani mkubwa zaidi wakati nchi yetu ikielekea katika uchumi wa viwanda.

  Akizungumzia fursa na mlingano wa ajira kati ya wanawake na wanaume alisema kuwa upande wa ajira wote wanawake na wanaume wana nafasi sawa na kinachozingatiwa ni vigezo na sifa za waombaji wa ajira.

  Katibu Mkuu huyo aliendelea kusema kwa sasa hakuna kazi za wanaume peke kwani upo uhalisia juu ya ushiriki wa wanawake wengi katika kazi za uhandisi, ukandarasi na udaktari.

  Alitoa wito kwa wanawake, jamii na watanzania kwa ujumla kuitumia siku hii kutoa hamasa kwa wanawake na kuangalia nafasi yao katika jamii kipindi hiki ambapo Tanzania inaelekea katika uchumi wa kati na viwanda.

  Ili kufikia azma ya uchumi wa viwanda, ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anadumisha Umoja wa nchi yetu na Utanzania wetu kwa kuwashirikisha wanawake, kwa kutoa elimu na kuwapa nafasi ili watoe mchango wao ipasavyo katika kuinua uchumi wa nchi.

  Aidha, mama Nkinga alihimiza jamii kusimamia watoto wa kike na kuhakikisha wanapewa haki inayostahili ili nao wafike mahali waweze kutoa mchango wao kwa taifa.

  Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8, Machi kwa shughuli mbalimbali kama vile maandamano na hotuba, pia wanawake hutumia nafasi hiyo kutathmini mafanikio ya shughuli zao za maendeleo, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo. Kauli mbiu ya mwaka huu inasema “Tanzania ya viwanda, wanawake ni msingi wa mabadiliko ya kiuchumi.”

  0 0


  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela(katikati) akionyesha kwa waandishi wa habari bia mpya ya chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki., kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha na Meneja kiwanda Dominic Mkemangwa.

  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa kampuni ya bia ya Serengeti John Wanyancha, akifafanua jambo jijini Mwanza jana wakati wa uzinduzi wa bia mpya ya Allsopps, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela.
  Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL na waandishi wa habari mara baada wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiongozana naviongozi wa SBL na waandishi wa habari maeneo ya kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza mara baada ya uzinduzi wa wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.

  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella leo ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuzalisha bidhaa zenya ubora wa hali juu jambo ambo limiweizesha kampuni hiyo kushinda tuzo mbalimbali za ubora ndani na nje ya nchi.

  Mongella alitoa kauli hiyo wakati alipokitembelea kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza ambako pia aliipongeza kampuni kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi kupitia uzalishaji wa ajira, ulipaji kodi na hali kadhalika programu za kusaidia jamii.

  “SBL ni mdau katika ajenda ya maendeleo ya nchi yetu. Kama serikali tutajaribu kuanzisha mazingira ambayo yanawezesha biashara kama hii ili istawi vizuri na kuvutia uwekezaji pia,” alisema Mongella.

  SBL inazalisha chapa za bia ambazo ni Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick na hali kadhalika kusambaza pombe kali zinazofahamika duniani ambazo zinazalishwa na kampuni yake uwekezaji Diageo.

  Mwezi uliopita Kiwanda cha SBL cha Mwanza kilianza uzalishaji wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.

  “Hatua ya kuzalisha Allsopps katika kiwanda chetu cha Mwanza ni sehemu ya mbinu ya uendeshaji kikanda ya EABL. Hili limekuwa na matokeo ya kunufaisha kwa masoko yote na kwa biashara yetu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha.

  Kwa mujibu wa Wanyancha, SBL inaendesha miradi kadhaa ya kuisaidia jamii nchi nzima katika maeneo ya upatikanaji wa maji, utoaji wa elimu- ambapo wanafunzi walio na weledi mkubwa kutoka mazingira yenye uhitaji hupatiwa udhamini wa masomo kwa ajili ya kusomea kozi za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vya ndani na hali kadhalika kampeni ya Ukiwa Umekunywa Usiendesha gari ambayo inahamasisha unywaji wa kistaarabu.

  0 0


  Hapa ni katika ukumbi wa Jensen Complex Hotel uliopo Kakola katika halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo usiku wa Machi 08,2017 ,wanawake wanaofanya kazi mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu wamefanya hafla fupi ili kusherehekea siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 8 mwezi Machi.


  Hafla hiyo imeambatana na utoaji zawadi kwa wanawake wanne shupavu mgodini lakini pia wanawake wote wanaofanya kazi mgodini wamepatiwa zawadi mbalimbali na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu,Graham Crew katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
  Awali kabla ya kufanya hafla hiyo,wanawake hao walitoa zawadi ya shuka 140 kwa ajili ya kusaidia huduma za afya kwa akina mama katika vituo vya afya Bugarama na Lunguya ambapo pia walitoa zawadi ya sabuni,mafuta ya kujipaka na dawa za meno.
  Wanawake hao wametumia fursa hiyo kuwataka wanawake wengine kujitokeza kufanya kazi katika migodi badala ya kuamini kuwa kazi za migodini ni kwa ajili ya wanaume tu.
  Naye Meneja Mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu,Graham Crew alisema mgodi huo hivi sasa unafanya jitihada za kuwahamasisha akina mama kufanya kazi mgodini ili kuhakikisha kuwa wanafikia usawa wa kijinsia yaani 50 kwa 50.
  Crew aliongeza kuwa hivi sasa wanawake wanashika nyadhifa za juu za uongozi hali inayoonesha wazi kuwa mgodi unajali wanawake.
  Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo wakati wa hafla hiyo ametusogezea picha 43....Tazama hapa chini
  Machi 8,2017 usiku-Mtaalamu wa Mawasiliano mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu,Mary Lupamba akimkaribisha Meneja mkuu wa mgodi huo Graham Crew
  Meneja Mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu,Graham Crew akizungumza wakati wa hafla ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyokutanisha wanawake wanaofanya kazi katika mgodi huo unaokadiriwa kuajiri wanawake zaidi ya 100
  Meneja Mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akizungumza na wafanyakazi wanawake katika mgodi huo ambapo alisema hivi sasa wafanyakazi wanawake ni wachache sana ukilinganisha na idadi ya wanaume na kuongeza kuwa mgodi unafanya jitihada za kuhakikisha kuwa idadi ya wanawake inaongezeka ili kuwe na usawa wa 50 kwa 50 kwa wanaume na wanawake
  Wafanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu wakipiga makofi wakati wakimsikiliza meneja mkuu wa mgodi huo
  Meneja Mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew alisisitiza pia kuhusu umuhimu wa kuhamasisha elimu kwa watoto wa kike katika shule za msingi na sekondari kwani elimu ndiyo itaweza kubadilisha maisha yao
  Wanawake wanaofanya kazi mgodi wa Bulyanhulu wakifurahia jambo
  Meneja Mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew (kushoto) akiteta jambo na Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila
  Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kakola kata ya Kakola bi Apaikunda Nathan Palanjo akizungumza wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani ambapo aliushukuru mgodi huo kwa kuwasaidia akina mama katika vituo vya afya na kuwasaidia baiskeli wanafunzi wa shule ya sekondari Bugarama na Bulyanhulu
  Meneja Mkuu wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew (wa pili kulia) akiwa ameshikana mkono na viongozi mbalimbali kuonesha ishara ya umoja wakati wa maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani.Wa kwanza kulia ni Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila.Wa kwanza kushoto ni Meneja wa Usalama Acacia Bulyanhulu Terry Little akifuatiwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bulyanhulu 'A',Joyce Lwanji na Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kakola kata ya Kakola bi Apaikunda Nathan Palanjo
  Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakiwa wameshikana mkono kuonesha ishara ya umoja
  Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakicheza ukumbini
  Wanawake wanaofanya kazi katika mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakicheza muziki ukumbini.Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry
  Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akizungumza ukumbini namna walivyoshiriki katika siku ya wanawake duniani kwa kutembelea vituo vya afya Bugarama na Lunguya na kutoa zawadi ya baiskeli katika shule ya sekondari Bulyanhulu na Bugarama
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew( katikati) akijiandaa kukabidhi zawadi kwa wanawake wanne shupavu katika mgodi huo ambapo walipewa zawadi ya picha na shilingi 100,000/= kila mmoja
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi zawadi ya picha kwa bi Sivirina baada ya kuonesha utendaji mzuri zaidi kutoka kitengo cha Mazingira.
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi zawadi ya picha kwa mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Terry 
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry ambaye anashikilia nafasi ya juu katika uongozi akipokea zawadi ya picha 
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akikabidhi zawadi ya picha kwa mwanamke mdogo kiumri Mwanaisha Moshi ambaye ameonekana kuwa mchapakazi zaidi
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew na Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila wakiwa wamejifunga mitandio ya akina mama baada ya kuwavalisha mitandio wanawake wanaofanya kazi mgodini kama sehemu ya zawadi ya meneja mkuu wa mgodi huo
  Wanawake wanaofanya kazi mgodini wakiwa wamevaa mitandio waliyozawadiwa na Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew 
  Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila akicheza muziki na wanawake wanaofanya kazi mgodini
  Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akiangalia wafanyakazi wa mgodi huo wanavyocheza muziki
  Muziki unaendelea
  Mtaalamu wa Mawasiliano mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu,Mary Lupamba akicheza muziki
  Muziki unaendelea
  Akina mama wakicheza muziki
  Meneja wa Usalama Acacia Bulyanhulu Terry Little akicheza muziki na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Acacia Bulyanhulu Sarah Ezra Terry
  Muziki umekolea......
  Muziki umenoga haswaaa....
  Kushoto ni Maria na Sarah wakifungua shampen
  Maria na Sarah wanafungua shampen
  Maria na Sarah wameshafungua shampen
  Wafanyakazi wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu wakigonga cheers
  Mjumbe wa serikali ya kijiji cha Kakola kata ya Kakola bi Apaikunda Nathan Palanjo akigonga cheers na Meneja wa Ustawi wa Jamii na Kampuni ya Acacia Bulyanhulu,Elias Kasitila.
  Zoezi la kugonga cheers linaendelea
  Cheers!!!!
  Meneja mkuu wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew akigonga cheers na wafanyakazi wake
  Meneja wa Usalama mgodi wa Acacia Bulyanhulu Terry Little akigonga cheers na wanawake wanaofanya kazi mgodini
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Terry akiwa na furaha ukumbini 
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Terry na Meneja mkuu wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Graham Crew
  Picha ukumbini
  Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Jamii mgodi wa Bulyanhulu Sarah Ezra Terry akiwaasa wafanyakazi wenzake kufanya kazi kwa juhudi huku akieleza kuwa wanawake wana nafasi kubwa ya kushika uongozi mgodini
  Kushoto ni Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Acacia Bulyanhulu Zuwena Senkondo akibadilishana mawazo na wafanya kazi wenzake.

  0 0

  Hiki ni  kipindi cha Utekelezaji wa Serikali Mtandao nchini kinachotoa elimu kwa umma jinsi Serikali mtandao ilivyorahisisha utendaji kazi kwa Taasisi za Serikali na utoaji huduma kwa umma kupitia mtandao.
older | 1 | .... | 1164 | 1165 | (Page 1166) | 1167 | 1168 | .... | 1897 | newer