Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live

UN SECRETARY GENERAL STOPS IN DAR ON HIS WAY TO NEW YORK

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Mhe. Antonio Guterres (kushoto) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam jana. Mhe. Guterres alisimama kwa muda katika uwanja huo akitokea nchini Kenya kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Balozi Mahiga. 

Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Mhe Guterres aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa Mgogoro huo Rais wa awamu ya tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe. Benjamin Willium Mkapa. Aidha, Dkt. Mahiga aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 
Waziri Mahiga akizungumza jambo huku Mhe. Guterres akimsikiliza kwa makini. 

Dkt. Mahiga akiendelea kuzungumza na Mhe. Guterres huku Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa pili kutoka kulia) na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy wakiwasikiliza kwa makini. 
Picha ya pamoja 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Bi. Mindi Kasiga naye akiagana na Mhe. Guterres 
Mhe. Guterres akiagana na Dkt. Mahiga mara baada ya kumaliza kufanya mazungumzo yao. 




H.E. Dr. John Pombe Magufuli, the President of the United Republic of Tanzania has urged the United Nations to continue its support in bringing about political stability in Burundi and the Democratic Republic of Congo.

In his special message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres President Magufuli explained that the recent instability in the two countries has created refugees’ influx in Tanzania and its neighbors, hence the region is committed to ensure political stability is restored. 

Delivering President Magufuli’s message to the United Nations Secretary General Mr. Antonio Guterres, Tanzania’s Foreign Minister Augustine Mahiga said that as the chair of EAC, Tanzania is hopeful with the progress been made in the mediation process in Burundi under the leadership of President Yoweri Museveni of Uganda and facilitated by the former President of Tanzania, H.E. Benjamin William Mkapa. Hon. Mahiga also informed the UN Secretary General that the upcoming EAC Summit is expected to receive a progressive report about the process. 

With regards to the Democratic Republic of Congo, Minister Mahiga revealed that the Southern African Development Community is intending to include the agenda of political transition in DRC, whereby SADC member states are expecting positive deliberations. Tanzania is the current chair of the SADC organ of political, defense and security with the mandate to support the achievement and maintenance of peace and security as well as the rule of law in the SADC region. 

Upon receiving President Magufuli’s message, Mr. Guterres praised Tanzania for its ability to uphold principles of good governance in the country as well as maintaining peace and creating a peaceful environment in the EAC and SADC regions.

Mr. Guterres commended President Magufuli’s efforts in Burundi peace process, and his readiness to host refugees from Burundi, emphasizing the role played by regional communities in Africa in resolving leadership crisis in African countries. 

“The United Nations appreciates the work done by President Mkapa in Burundi under the EAC and its leadership. If the region come together the way EAC has done in the case of Burundi, I am sure together they will be able to establish lasting solutions” he remarked. 

Minister Mahiga told the reporters that President Magufuli met Mr. Guterres during the AU Summit in Addis Ababa earlier this year, where the two leaders exchanged cordial discussions about various issues concerning the region. 

“President Magufuli instructed me to deliver his message to Mr. Guterres, and has also extended an invitation to the Secretary General at an appropriate time to have a working visit in the country” concluded Hon. Mahiga.

Mr. Guterres was met and held talks with Foreign Minister Mahiga at the Julius Nyerere International Airport yesterday night where he was on transit from Somalia and Kenya for a working visit. Also present at the airport was the United Nations Resident Coordinator, Mr. Alvaro Rodriguez and officials from the Ministry of Foreign Affairs including the Director of Multilateral Cooperation Ambassador Celestine Mushy and Ministry’s Spokesperson Ms. Mindi Kasiga. 


Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dar es salaam, Tanzania
March 9, 2017.

WAZIRI SIMBACHAWENE AFANYA ZIARA KUKAGUA USAFI WA MAZINGIRA MJINI DODOMA

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiambatana na Afisa Masoko Manispaa ya Mji wa Dodoma, Stephen Maufi katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene na Naibu Katibu Mkuu Afya , Dkt. Zainabu Chaula wakiangalia mfereji wa maji machafu uliopo katika Soko la Mwembeni katika ziara fupi ya kutembelea na
kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akifurahia ubunifu wa uhifadhi wa mbogamboga na matunda katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa
Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akizungumza na mmoja wa wafanya biashara katika soko la Mwembeni Bw. Mjahidina Hassani katika ziara fupi ya kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Afya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) , Dkt. Zainabu Chaula akisisitiza juu ya Uhamisho wa wafanya biashara ndogo ndogo kwenda Uwanja wa Barafu katika ziara fupi ya
kutembelea na kukagua usafi katika maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. George Simbachawene akiongea na waandishi wa habari
kuhusu tamko la utekelezaji na ufatiliaji wa ugonjwa wa Kipindupindu katika Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa Ofisini kwake, Dodoma.

Picha na: TAMISEMI.

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA LAPF,JIJINI ARUSHA

$
0
0
Na Pamela Mollel Arusha.

MFUKO wahifadhi ya wafanyakazi wa serikali za mitaa,LAPF,umeipongeza serikali kwakulipa malimbikizo ya madeni ambayo mfuko huo na mingine ilikuwa ikiidai kwamiaka mingi na hivyo kuathiri usitawi wa mifuko hiyo.

Meneja wa LAPFkanda ya kaskazini, Rajabu Kinande, amesema hatua ya serikali kulipa madenihayo kumeiongezea mifuko ya hifadhi ya jamii uwezo wa kuhudumia wanachama waokwa wakati. Kinande, ameyasemahayo Marchi 7 jijini Arusha,alipokuwaakizungumza na vyombo vya habari kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa, AICC,kuelezea hatua ya maandalizi ya mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa wadau waLAPF.

Amesema mkutanohuo utafunguliwa na Waziri mk
uu waJamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh,Majaliwa KassimMajaliwa,Marchi 10 mwaka huu ambapo zaidi ya wanachama 1000 wa mfuko huo wanatarajiwa kuhudhuria.

Awali MenejaMawasiliano na Masoko wa LAPF,James Mloe, amesema kuwa kwenye mkutano huokutawasilishwa mada mbalimbali zikiwemo Uendeshaji wa shughuli za mfukohuo,Hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG)za mwaka 2015/16ambapo mfuko huo umepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu ,UKusanyaji wa michango ulipaji wa mafao kwa wanachama na uwekezaji,Utawala bora na usimamizi wa uendeshajiwa mfukohuo na Raslimali fedha .

Amesema sikuya kwanza ya mkutano huo Marchi 9 kwa kuzingatia kuwa ni siku ya Figo dunianimfuko umeandaa upimaji wa figo bure kwa wanachama wote ambao utafanywa naMadaktari bingwa

.Mloe,amesema siku ya pili yamkutano huoWaziri mkuu Kassim Majaliwa atazindua program mpya ya mikopo kwa wanachama kwa kushirikiana na benki ya CRDB,iitwayo Maisha popote ambao ni mkopo wakwanza kutolewa na mfuko huo.

Amesemakauli mbiu ya mwaka huu ni kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo endelevu kwa watanzania.Kuhusuuwekezaji kwenye viwanda,Mloe, amesema kuwa LAPF, imeweka mitaji kwenye viwanda ambako tayari wameweka hisa zao .

Amesema kuwaLAPF,haiwezi kujenga viwanda na kuvisimamia uendeshaji wake bali itaweka mitajina kusisitiza kuwa LAPF itabakia kwenye jukumu lake la msingi la kulindamichango ya wanachama wake. Mwisho .

RAIS DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI MJINI DODOMA

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo tarehe 9/03/2017. Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU.
Rais Dkt Magufuli akiagana na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan mapema leo mchana mara baada ya kumaliza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma,kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akijadiliana jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kutoka kwenye kikao cha Baraza la Mawazili,kilichofanyika leo mjini Dodoma
Waziri wa habari,Utamaduni Sanaa na Michezo,Nape Nnauye akizungumza jambo na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage kabla ya kuanza kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma leo.PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS.

NIMR NA CHUO CHA SAYANSI CHA NELSON MANDELA WATOA UTAFITI WA UGONJWA MARALE

$
0
0
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Utafiti unaonesha kuwa jamii ya wafugaji wamekuwa wakikumbwa na ugonjwa wa marale, hali ambayo usipodhibitiwa mapema unaweza kusababisha vifo katika jamii hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila amesema kuwa mradi wa utafiti huo kama serikali kutafuta namna ya kuweza kudhibiti ugonjwa huo.

Amesema kuwa mradi wa utafiti wa ugonjwa wa marale ulifanywa kuangalia mabadiliko Tabia ya Nchi na matumizi ya ardhi kwa jamii ya wafugaji wa Wilaya ya Simanjiro na Monduli.

Dk.Neema amesema utafiti huo utasaidia kwa watunga sera wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto pamoja Wizara ya Maendeleo ya Kilimo na Uvuvi kuweza kuangalia namna ya kudhibiti ugonjwa huo ili usiwe tatizo kwa jamii ya wafugaji.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa mradi huo umefanywa na NIMR pamoja na Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela katika kuangalia ugonjwa marale.

Amesema ugonjwa wa Marale kwa nchi zilizo kusini mwa Jangwa la sahara zimekuwa zikikumbwa na ugonjwa huo hasa katika jamii za wafugaji.

Kwa upande wa Mkuu wa Mradi wa Utafiti wa Ugonjwa wa Marale , Profesa Paul Gwakisa amesema kuwa mradi huo ni wa miaka mitatu ambapo wamekuja kutoa matokeo juu ya utafiti walioufanya.

Amesema ugonjwa wa marale ni tatizo kwa jamii ya wa wafugaji ambapo unahitaji kudhibitiwa kabla ya tatizo hilo halijawa kubwa.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akizungumza wakati kuzindua majadiliano ya utafiti wa ugonjwa wa marale katika Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo jijini Dar es Salaam.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Profesa Yunus Mgaya akitoa neno katika majadiliano ya ugonjwa wa marale uliofanywa kati ya NIMR na Chuo cha Sayansi cha Nelson Mandela leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu wa Mradi wa Utafiti, Profesa Paul Gwakisa akizungumza jinsi walivyofanya utafiti wa ugonjwa marale katika jamii ya wafugaji kwa Wilaya Simanjiro na Monduli mkoani Arusha leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara ya Afya Maendele ya Jamii , Jinsi, Wazee na Watoto, Dk. Neema Rusibayila akiwa katika picha ya pamoja na Watafiti , Watendaji Wizara na Taasisi leo jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA UWANJA WA UHURU JIJINI DAR

$
0
0
Mkurugenzi wa Msama Promotions,Alex Msama akizungumza mbele ya waandishi wa habari mapema leo mchana jijini Dar kuhusiana na maendeleo ya maandalizi ya tamasha la pasaka linatlotajia kuanza hivi karibuni.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.

Tamasha kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama "Tamasha la Pasaka" sasa kufanyika katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mratibu wa Tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanja wa uhuru ndio sehemu maalum ya kufanyia Tamasha hilo.

“Malengo ya tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wa nchi Dkt John Pombe Magufuli  ili aendelee kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema

Ametaja kuwa tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa albamu mbili

Airtel Money yaisaidia WFP kutuma Pesa kwa Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu

$
0
0
Airtel Tanzania imeanzisha njia  mpya  na rahisi ya Near – Field Communication (NFC) ambayo ni mfumo wa malipo utakaoisaida Shirika la chakula Duniani  (WFP)  kuhamisha fedha kwa wakimbizi wapatao 10,000 kama sehemu ya mgao wao wa chakula kwa miezi mitatu ikiwa ni  mpango wa majaribio wa kuboresha huduma katika kambi ya wakimbizi ya  Nyarugusu.

Chini ya majaribio hayo, kwa sasa wakimbizi hao watapokea fedha kwa njia ya simu ya mkononi yenye dhamani ya  fedha za kimarekani $ 4.50 (shilingi 10,000) mara mbili kwa mwezi wakiwa katika kambi hiyo. Fedha hizo zitawekwa katika kadi zao za  Airtel Money Tap Tap kadi zilizounganishwa na teknolojia ya malipo ya NFC ambao umeunganishwa na akaunti zao za Airtel Money. 

Tap Tap kadi inatoa urahisi wa malipo na ni njia rahisi inayomfanya mteja kufanya malipo bila ya kuwa na simu yake ya mkononi  wakati wowote. Ni ufumbuzi  mzuri kwa wakimbizi  unaowawezesha kufanya shughuli za haraka na kwa urahisi kwa kugusisha tu kadi  kadi zilizounganishwa  na akaunti zao za Airtel Money na kufanya malipo ya kupokea au kununua bidhaa.
 "Tap Tap  kadi imeungwanishwa na huduma ya Airtel Money ili inatoa huduma ya kipekee na urahisi kwa wateja wetu  katika utumiaji wa  wa fedha kwa njia ya mtandao, inawawezesha  wateja kutumia teknolojia ya kisasa kabisa yakufanya malipo au kuwa na uwezo wa kumiliki akaunti zao za fedha kwa njia ya mtandao hata kama simu ikiwa imezima," alisema Mkuu wa kitengo cha huduma cha  Airtel Money, Isack Nchunda. "Tunafura kubwa kuona kadi hizi mpya zinawawezesha  kufanya manunuzi ya chakula na kusaidia maisha ya wakimbizi waishio Tanzania."

Baada ya kupokea fedha kutoka kwenye kadi ya Tap Tap, wakimbizi wanauwezo wa kununua  chakula katika soko la Nyarugusu ambalo lilifunguliwa mwaka 2016. soko, hilo lipo maeneo ya buffer zone kati ya kambi na wenyeji wa maeneo hayo, ambapo imewapa nafasi  wafanyabiashara wa maeneo hayo kuweza  kuuza mazao yao kwa wakimbizi.

"Matumizi ya kadi hizo inawarahisishia wakimbizi kukidhi mahitaji yao ya chakula na wakati huo huo  kuinua uchumi wa nchi kwakuwa wanyeji hujipatia soko kwa bidhaa zao," alisema Mwakilishi wa WFP nchini Michael Dunford. "Pamoja na fursa kubwa ya kununua aina mbali mbali ya vyakula vinavyozalishwa ndani ya nchi na kuwasaidia kukidhi malazi, vilevile inasaidia kuboresha hali ya lishe ya kaya na kuhakikisha kwamba jamii na wenyeji pia wanafaidika kupitia shughuli nyingi za kiuchumi."

Katika kipindi hiki cha majaribio , wakimbizi wataendelea kupokea mafuta, uji na vitu vingine vidogo wakati mgawo wa wa nafaka, kunde na chumvi vitabadilishwa kwa fedha taslimu.alisisitiza Dunford.
Baadhi ya wakimbizi katika kambi ya wakimbizi Nyarugusu wakipewa mafunzo toka kwa wafanyakazi wa Airtel huduma kwa wateja ya jinsi ya kutumia huduma ya Airtel Money tap tap card, kadi hiyo Inasaidia WFP kutuma Pesa kwa Wakimbizi katika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu. Kadi ya Airtel Money Tap tap imeunganishwa na akaunti za Airtel Money ili kutoa usalama wa utumiaji wa huduma za fedha kwa njia ya mtandao bila ya kuwa na simu ya mkononi.

MARY MWANJELWA AONGOZA MAHADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MKOANI MBEYA

$
0
0
 Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwa akipiga makofi wakati wa mahadhimisho ya Siku ya Wanawake mkoa wa Mbeya.
  Mbunge wa Viti Maalum Mbeya, Mary Mwanjelwaakinyoosha mikono juu pamoja na wageni wengine wa meza kuu katika mahadhimisho ya Siku ya Wanawake Mbeya
Mbunge wa Viti Maalum Mbeya akipunga mkono kwa Wanawake wa mkoani mbeya

TAMASHA LA PASAKA MAMBO YAZIDI KUNOGA,SAFARI HII KUFANYIKA UWANJA WA UHURU

$
0
0
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo , Alex Msama alisema baada ya uzinduzi huo kufanyika Aprili 16 katika Uwanja wa Uhuru, litahamia mikoa 10 ambayo itateuliwa na kamati ya maandalizi.

“Nichukue fursa hii kuwatangazia wadau wa Tamasha la Pasaka na muziki wa injili kwa ujumla wake kwamba, tamasha la Pasaka lipo kama kawaida na litaanzia jijini Dar es Salaam April 16, kabla ya kwenda mikoani,” alisema Msama.

Kuhusu uteuzi wa uwanja wa Uhuru, Msama alisema hiyo ni kutokana na uamuzi wa Kamati ya maandalizi kuangalia vigezo mbalimbali yakiwamo maoni ya wadau wakubwa wa muziki huo.

“Tunaamini Uwanja wa Uhuru (zamani Taifa), ni mahali muafaka baada ya kujiridhisha kwa vigezo vingi. Tunaamini hata wadau, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili wataukubali,” alisema.

Juu ya kukawia kwa maandalizi tofauti na miaka mingine, Msama alisema ni kusubiri mambo mengine muhimu yakamilike, ikiwemo taratibu husika kwa mujibu sheria za nchi.

Msama ambaye pia ni Mkurugenzi wa Msama Promotions Ltd, alisema mikakati ya Kamati yake ni kuhakikisha tamasha la mwaka huu linakuwa bomba zaidi kwa kuongeza vionjo muhimu tofauti na miaka mingine.

Kuhusu maudhui, Msama alisema mbali ya kuutukuza ufalme wa Mungu kwa njia ya nyimbo na kutumia sehemu ya mapato kusaidia makundi maalumu kama yatima, wajane na walemavu, pia litahimiza upendo na amani katika nchi.


Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande).
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha Pasaka, Alex Msama, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya tamasha hilo litakalofanyika Aprili 16 kwenye Uwanja wa Uhuru.
KAMPUNI ya Msama Promotions inayoratibu Tamasha la kimataifa la Muziki wa injili tangu mwaka 2000, imesema maandalizi ya tukio la mwaka huu yanakwenda vizuri ambapo tukio la mwaka huu litafanyika katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

TANESCO YATOA SIKU 14 KWA WADAIWA BILI ZA UMEME KULIPA, VINGINEVYO HUDUMA YA UMEME INASITISHWA

$
0
0
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limetoa siku 14 kwa Wateja wake wote linalowadai kulipa madeni yao, vinginevyo litasitisha utoaji wa huduma ya nishati kwa wahusika.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Machi 9, 2017 ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (pichani juu), alisema, Shirika linadai jumla ya shilingi Bilioni 275.38.

Akifafanua zaidi alisema, Wizara na Taasisi za Serikali zinadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 52.53, Shirika la Umeme Zanzibar, (ZECO), linadaiwa zaidi ya Shilingi Bilioni 127.87, na Makampuni binafsi na wateja wadogo wadogo deni ni zaidi ya Shilingi Bilioni 94.97.

“Zoezi hili litaambatana na utoaji taarifa (notice) kwa wadaiwa wote kulipa madeni yao ndani ya kipindi cha siku 14, baada ya hapo Shirika litachukua hatua ya kusitisha Huduma kwa Wateja watakaoshindwa kuanza kulipa madeni yao pamoja na hatua zingine za kisheria.” Alisema Dkt. Mwinuka.
Aidha, alisema kwa wale wateja wadogowadogo, Shirika halitawaandikia barua kwani ni wengi, isipokuwa kupitia ofisi ya Uhusiano ya Shirika, wataarifiwa kupitia vyombo vya habari.

Alisema Malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya Shirika kwa wakati, ikiwemo shighuli za Uendeshaji Shirika, Matengenezo ya Miundombinu pamoja na utekeelzaji wa miradi mbalimbali.

“Ni matarajio ya Shirika kuwa kuli[wa kwa malimbikizo haya ya madeni, kutasaidia TANESCO kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi mkubwa zaidi na hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme hapa nchini.” Alihitimisha Dkt. Mwinuka.

Taarifa hii ya TANESCO imekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuliagiza Shirika hilo, kuwakatia umeme wale wote wanaodaiwa ikiwemo taasisi nyeti za Serikali na hata Zanzibar.

Rais alitoa agizo hilo wakati akizindua ujenzi wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme wa Kilovolti 132 mkoani Mtwara ambacho kitaboresha upatikanaji wa umeme kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi.
 Baadhi ya viongozi wa TANESCO, kutoka kushoto, Dudu Fuime, (Kaimu Meneja Mwandamizi TEHAMA), Mhandisi Kahitwa Bishaija,(Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji umeme), Mhandisi Theodory Bayona,
(Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme)
  na Renata Ndege, (Afisa Mkuu wa Fedha) wakibadilishana mawazo kabla ya kuanza kwa mkutano huo
Baadhi ya viongoziwa juu wa TANESCO na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo

UMOJA WA AZAKI ZA VIJANA WAKUTANA KUJADILI VIPAUMBELE VYAO KATIKA BAJETI YA 2017/2018

$
0
0
  Mbunge wa viti maalum wa Pwani, Hawa Mchafu Chakoma (CCM) akizungumza kwenye kongamano la vijana kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Picha na Geofrey Adroph
 Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine (CCM) akizungumza na vijana kwenye kongamano lililoandaliwa na Asasi ya Dira ya Vijana (TYVA) kwa kushirikiana na asasi za mbalimbali za vijana katika kujadili vipaumbele vya vijana katika bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kuhusu namna ambavyo wabunge wanajaribu kupigania maslahi ya vijana kwenye bajeti. 

Mbunge wa viti maalum wa Katavi, Rhoda Edward Kunchela(CHADEMA) akizungumza na vijana kuhusu mchakato wa bajeti unavyofanyika kutoka ngazi ya chini mpaka ya juu kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ukumbi wa Wanyama jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa AZAKI akizungumza na vijana kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 leo kwenye ukumbi wa Hoteli ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo.
 Mratibu wa Mtandao wa Vijana na Bajeti, Saddam Khalfan akizungumzia suala la bajeti ya taifa hasa kwa bajeti ya mwaka 2017/18 kuwa ni sera na sheria mama ya masuala ya mapato na matumizi ya serikali hivyo serikali ni lazima ifahamu umuhimu wa kuzingatia mahitaji ya vijana na ushirikishwaji wao katika mipango ya maendeleo kwenye kongamano lililowakutanisha vijana leo katika ukumbi wa hoteli ya Wanyama jijini Dar.
Majadiliano yakiendelea kuhusu mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha  2017/2018 hasa kwa bajeti inayowahusu vijana lililoandaliwa na Asasi ya Dira Vijana (TYVA) kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za vijana kwenye hotel ya Wanyama leo jijini Dar es Salaam.  
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye kongamano lililowakutanisha ili kujadili masuala ya bajeti hasa bajeti ya mwaka 2017/18 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Bi. Stella Vuzo( katikati) akiwa kwenye kongamano la vijana lililofanyika leo kwenye ukumbi wa hotel ya Wanyama jijini Dar es Salaam leo. Wa kwanza kulia ni Victoria Mwanziva ambaye ni mtafiti wa masuala ya Demokrasia na Maendeleo. 
 Mbunge wa Kasulu Vijijini, Vuma Augustine (CCM) akichokoza mjadala wa bajeti kwa vijana
Baadhi ya vijana wakichangia mada juu ya bajeti kwa vijana pamoja na upatikanaji wa ajira
Mshauri wa Demokrasia na utawala bora, Frederick Fussi akitoa mada kwenye mkutano huo
 Baadhi ya vijana wakiwasilisha maoni
Mbunge Viti Maalum CHADEMA, Anatropia Theonest akifunga kongamano la vijana lililokuwa linajadili mchakato wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018.
 Mbunge wa Kasulu Vijijini Vuma Augustine akizungumza na waandishi wa habari na waandishishi wa habari kuhusu ukusanyaji wa maoni kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye bujeti ya mwaka 2017/2018.
  Mbunge wa viti maalum wa Katavi Rhoda Edward Kunchela(CHADEMA) jinsi alivyoshiri kwenye mchakato wa vijana kutaka kujua ni kwa jinsi gani vijana wanaweza kunufaika na bujeti ya Taifa.
Makamu wa Rais wa DARUSO, Shamira Mshangama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu bujeti zinazowekwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu pamoja changamoto wanazozipata katika upatikanaji wa fedha za mikopo zinazotengwa na serikali katika bajeti yake.

Mkuu wa Idara ya Mafunzo (TYVA), Dianarose Lyimo akizungumza na waandishi wa habari kuhusi taasisi ya Vijana ya TYVA inavyojihusisha na mijadala pamoja na makongamano kwa vijana kutambua umuhimu wa bajeti hasa bajeti ya Vijana.
Picha ya Pamoja 

CHUO CHA MIPANGO- DODOMA CHAHIMIZA MATUMIZI YA TAFITI KUKABILIANA NA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Wajumbe wa mkutano wa Mabadiliko ya tabia ya nchi na athari zake kiuchumi hapa nchini uliokishirikisha Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini –Dodoma na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU), wakiingia kwenye ukumbi wa Mikutano mmoja Jijini Dar es salaam, siku ya kwanza ya mkutano huo wa Siku mbili.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina (kulia) akifafanua jambo wakati wa mkutano uliohusu changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi wakati wa mkutano uliowashirikisha wadau wa maendeleo kutoka ndani nan je ya nchi na kuandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma.
Mmoja wa washiriki wa mkutano huo akichangia mada mbalimbali kuhusu mabadiliko ya tabia ya nchi yanavyoathiri uchumi wa wananchi vijijini nchini Tanzania, zilizowasilishwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini-Dodoma, na kufanyika Jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wadau wa mkutano uliohusu changamoto za athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia ya nchi wakifuatilia kwa makini mjadala kuhusu suala hilo, Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina (kushoto) na Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Frank Hawassi (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja nje ya ukumbi wa mkutano kuhusu Mabadiliko ya Tania Nchi uliowashirikisha wadau kutoka ndani na nje ya nchi uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma Dkt. Frank Hawassi akizungumza na wajumbe wa Taasisi na Washirika wa Maendeleo kuhusu, umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi, katika Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina akizungumza na wadau na Washirika wa Maendeleo kuhusu mradi wa Chololo Ecovillage uliopo Dodoma unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) wakati wa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM).


Na Benny Mwaipaja,WFM

Wadau wanaofanya tafiti mbalimbali za Maendeleo ya uchumi nchini hasa maeneo ya vijijini kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi wametakiwa kuwasilisha matokeo ya tafiti hizo Serikalini na katika Mashirika mengine ya Maendeleo ili matokeo yake yafanyiwe kazi na kusudio la tafiti hizo liweze kufikiwa.

Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo vijijini – Dodoma, Prof. Razack Lokina wakati wa Mkutano uliohusu mabadiliko ya tabia nchi na athari zake kiuchumi uliozihusisha Taasisi za Serikali na Binafsi pamoja na Washirika wa Maendeleo.

Amesema Chuo cha Mipango kimekuwa kikifanya kazi zake vijijini, zikiwemo za tafiti mbalimbali na matokeo hayo huwasilishwa katika ngazi husika ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais inayoshughulikia mazingira pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kutumia matokeo hayo kwa manufaa ya maendeleo ya jamii hasa vijijini. 

“Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia nchi ambao umejadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na athari za kiuchumi zinazotokana na Mabadiliko hayo, umetokana na andiko la Wanafunzi wa Chuo hicho waliokwenda katika mafunzo kwa vitendo vijijini na kushuhudia namna mabadiliko ya tabia nchi yalivyoathiri maendeleo ya wananchi”. Alifafanua Prof. Lokina

Tayari Chuo kina mradi ujulikanao kama Chololo Ecovillage unaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) Mkoani Dodoma, ambao huwafundisha wanakijiji njia bora za uzalishaji mali, hivyo kuwafanya baadhi ya Wananchi waliokuwa wanakosa chakula, kutokana na hali ya Ukame wa Mkoa huo kuanza kupata mazao ya kutosha na kuongeza pato lao.

Naye Mkuu wa Chuo hicho cha Mipango ya Maendeleo vijijini- Dodoma, Dkt. Frank Hawassi, amezitaka Taasisi na Mashirika ya umma na Binafsi kuunganisha nguvu katika kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi kwa kuwa kama juhudi hazitachukuliwa athari zake zitampata kila mmoja.

Aidha, amesema hakuna nchi inayoweza kufanikiwa kukabiliana na tatizo hilo bila kushirikiana hata kama nchi hiyo imeendelea kwa kiasi kikubwa. Pia Jamii inapaswa kujua kuwa hata matatizo ya wafugaji, wakulima na wengine kuhusu ardhi ni matokeo ya athari za Mabadiliko ya Tabia nchi, hivyo kila mmoja anatakiwa kuwa chachu ya utunzaji wa mazingira, ili maendeleo yanayopatikana yawe endelevu.

Ameongeza kuwa Chuo cha Mipango Dodoma kinatoa nafasi kwa wadau kote nchini kukitumia kikamilifu katika kutatua changamoto za kimazingira kwa kuwa ipo Idara iliyo na jukumu la kushughulikia suala la Mazingira na Mabadiliko ya Tabia nchi. 

Kwa upande wake aliyekuwa Balozi wa Umoja wa ulaya nchini Tanzania Tim Clarke, ambaye ameongoza timu ya washirika wa Maendeleo katika Mkutano huo ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini kujitahidi kuwahamasisha wananchi kutumia Nishati mbadala ikiwemo Gesi ili kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu kwa kukata miti kwa ajili ya kupata Mkaa.

Vilevile ametoa rai kwa Serikali kuwa karibu na jamii na kuwaelimisha kuhusu kutunza mazingira katika shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato ili kusaidia kulinda mazingira ya asili yatakayochochea kukua kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

WLAC YATOA ELIMU JUUYA HAKI ZA MTOTO KWA WANAFUNZI WA ANANASIFU SEKONDARI

$
0
0
 Mwanasheria wa WLAC , Wigayi Kisandu akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Kinondoni ananasifu juu ya umuhimu wa mtoto wa kike katika kukuza uchumi wa Tanzania na familia kwa kuweza kutambua haki zake na majukumu yake
 Kaimu Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Ananasifu Fatuma Niyopa akizungumza wakati wa mkutano huo ambao umewezesha wanafunzi wa kike kujitambua juu ya haki za mwanamke
Wanafunzi wa Shule ya sekondari Ananasifu wakiwa katika kikao hicho na tasisi ya Msaada wa Kisheria kwa Wanawake WLAC

Utumiaji Holela dawa za maumivu waweza kusababisha magonjwa ya Figo

$
0
0

Watanzania wametakiwa kuepuka utumiaji holela wa dawa za maumivu ili kuepuka uwezekano wa kupata magonjwa ya Figo.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Jakline Shoo alipokua akiwasilisha mada katika maadhimisha siku ya figo Duniani, katika kongamano la kitaaluma lililofanyika leo katika ukumbi wa CPL uliopo ndani ya Hospitali hiyo.

Akifafanua Dk. Shoo amesema ni vema watu wakaepuka matumizi holela ya dawa za maumivu kwani ni chanzo cha magonjwa ya figo lakini pia kuepuka unene uliokithiri kwa kula mlo bora na kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa ya Kisukari na shinikizo la damu ambayo yanachangia mtu kupata ugonjwa sugu wa figo.

Akielezea kuhusu wagonjwa wanaohudumiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Shoo amesema katika Kiliniki yao kwa kila mwezi huwaona wagonjwa watu wazima kati ya 120 hadi 150 .

Pia takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 10 ya watu Duniani tayari wanaugua ugonjwa sugu wa figo na kwamba inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 asilimia 70 ya wagonjwa watakua wanatokea katika nchi zilizopo Ukanda wa Jangwa la Sahara.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya Figo Duniani mwaka huu ni ugonjwa wa figo na uzito uliozidi , mienendo bora ya maisha kwa ajili ya afya bora ya Figo.
Dk. Gudila Valentine akiwasilisha mada kuhusu ugonjwa wa Figo katika kongamano la kitaaluma ikiwa ni maadhimisho ya siku ya Figo Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 9.
Baadhi ya Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali kuhusu magonjwa ya Figo zilizowasilishwa katika kongamano hilo leo .
Wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakimuhudumia mgonjwa katika kitengo cha Figo, kushoto ni kiongozi wa kitengo hicho Sister Judith Mwaipopo na kulia ni Sister Lucy Kyombo.

CRDB YATOA MSAADA KATIKA HOSPITALI YA SARATANI YA OCEAN ROAD

$
0
0
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka  (kulia)akizungumza kabla ya kukabidhi msaada kwa taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
 Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road wakifatlia kitendo hicho cha utoaji wa Msaada kutoka benki ya CRDB
 Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto akizungumza kabla ya kupokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka benki ya CRDB
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto ,vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni 10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka (kulia)akimkabidhi Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Taasisi ya Saratani Ocean road, Beatrice Erasto kabati la kuhifadhia vifaa vya mgonjwa ikiwa ni moja ya vitu vilivyotolewa msaada vyenye thamani ya Milioni10 kwa taasisi hiyo jana Dar es Salaam

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUTEMBELEA KITUO CHA PEDDEREF SOBER HOUSE KIGAMBONI

$
0
0
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Jennifer Shirima ambaye aliambatana na msemaji wa Jeshi hilo katika ziara hiyo akiwasisistizia wanawake hao kutoajiingiza tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya na kuwakumbusha kuwa “Wanawake ni msingi wa mabadiliko kiuchumi” (kulia) ni Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe na (kushoto) ni Mrakibu Msaidizi Puyo Nzalayaimisi ambaye pia ni msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Moja ya wanawake waathirika wa madawa ya kulevya bi.Jacqueline Samson aliyesimama (katikati) akitoa shukrani kwa viongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambao hawapo picha kwa kuwatembelea kituoni hapo pia kwa msaada waliowapatia. 

Maafisa na Askari (Wanawake) wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mkurugenzi wa People With Drugs Dependence Relief Foundation (Pedderef)bi. Nuru Salehe wa kwanza mbele (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake waliopata kuathirika na madawa ya kulevya kituoni hapo, ambapo wanawake hao wameanza kurejea katika hali zao za kawaida mara baada ya kupewa elimu na malezi yanayostahili.

Katika kuadhimisha siku ya wanawake Duniani Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeungana na wanawake duniani kuadhimisha siku hiyo

Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambaye pia ni msemaji wa Jeshi hilo Puyo Nzalayaimisi alisema katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya tano (5) kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya, kupitia Jeshi hilo Nzalayaimisi aliwaongoza Askari (wanawake) kutembelea kituo cha Pedderef Sober House na kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali.

Ambapo aliiomba jamii isiwanyanyapae pamoja na elimu wanayoendelea kuipata kituoni hapo ameiasa jamii kujitokeza kuwasaidia na kuwawezesha kwa hali na mali ili waweze kujiajili wenyewe kwani wanapotoka kituoni hapo wanakuwa hawana uwezo wakujiajili na kujikuta wanarudia tena kwenye janga la madawa hayo.

Pia Nzalayaimisi aliendelea kusema kwa kutoa pongezi kwa serikali na wadau mbalimbali wote waliojitokeza na kuthubutu kufanya maamuzi ya kujitoa katika kupambana na janga hilo na pia alimpongeza mkuu wa mkoa wa dar es salaam paul makonda kwa kuongoza mapambano hayo.

Mkurugenzi wa kituo hicho bi. Nuru Salehe naye alisema napenda kutoa shukrani za kipekee kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa msaada wao wa hali na mali waliotupatia na kuomba taasisi nyingi na wadau mbalimbali kujitokeza katika kusaidia kituo hiki kwani wengi wamenufaika kutokana na elimu na malezi wanayoendelea kuyapata kituoni hapo.

WIZARA YA MALIASILI KWA KUSHIRIKIANA NA SPANEST KUTOA MAFUNZO YA HUDUMA KATIKA SEKTA YA UTALII NA UKARIMU KWA MIKOA YA MBEYA, NJOMBE NA IRINGA

LUGALO YAJIVUNIA MAFANIKIO YA MCHEZAJI WAKE UGANDA

$
0
0
Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.

Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
Klabu ya Gofu ya jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo imejivunia kuanza vyema mwaka 2017 baada ya Mchezaji  wake Vicky Elias kuibuka na ushindi  wa Divisheni A Nett katika Mashindano ya Wanawake  Enntebe Ladies Open  yaliyomalizika hivi Karibuni nchini Uganda.

AKizungumza na Waandishi wa habari mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali  Mstaafu Michael Luwongo alisema Ushindi huo ni ishara tosha ya Mafamikio ya Kimchezo kwa mwaka 2017 kwani alikuwa mtanzania pekee kati ya Wachezaji 53  walioshiriki.

" Unajua tunajipanga kimataifa na tuliahidi kuweka nguvu katik mashindano kimataifa ,kwa mwaka 2017 na huu ndio mwanzo hivyo mashabiki wa Lugalo na Wanachama wajipange kufuarahia Timu yao kutokana na mafanikio yatakayopatikana kimataifa.

Aliongeza kuwa licha ya matokeo ya Kimataifa pia Michezo yeyote ambayo  Timu ya Gofu ya Lugalo itaalikwa basi watahakikisha wanafanya vyema ili adhama ya Timu ya Gofu ya Lugalo kuwa Timu Bora inatimia.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ushindi wa Vicky ni Ushindi Mkubwa kutokana na Maandalizi pamoja na Washiriki waliojitokeza kushiriki michuano hiyo lakini ni sifa kwa Nchi kw sababu mbali na kutoka Klabu ya Lugalo lakini kubwa zaidi ni Mtanzania.

Kwa Upande wake Vicky Elias alisema mashindano yalikuwa magumu lakini alipambana kufa na kupona kurejesha heshima ya Klabu na Nchi kwa Ujumla na kufanikiwa kurejea na ushindi ambao haikuwa rahisi kwani siku ya kwanza alipiga mikwaju 83 na kutoa kiwango chake cha uchezaji ambacho ni Tisa.

Katika siku ya pili ya mashindano hayo Vicky aliibuka na Mikwaju ya Jumla 81 baada ya kutoa kiwango chake cha Uchezaji  cha Tisa na hivyo kuibuka na Ushindi wa Kwanza Divisheni  A na kuwashinda Wachezaji Wenzake kutoka Uganda na Kenya waliokuwa wakiwania nafasi hiyo.

Wakati huo huo  kufuatia Maandalizi ya mashindano ya wachezaji wa Ridhaa nchini Tanzania Amature Stoke Play yanayotarajiwa kufanyika Moshi mkoani Kilimanjaro machi 12  Wachezaji wa Timu ya Lugalo wanaendelea na Mazoezi kujiwinda na Michuano hiyo.

Bingwa mtetezi wa mashindano ya   hayo kutoka Lugalo  Nicholous Chitanda amesema yuko katika maandalizi kujiandaa na michuano hiyo ili kutetea Ubingwa wake alionyakua mwaka jana ili kuhakikisha unabaki katika Klabu ya Lugalo.
Mshindi wa Divisheni A Nett Mashindano ya Enntebe Ladies Open 2017 kutoka Klabu ya Gofu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika harakati ya Mchezo huo katika Michuano iliyofanyika Uganda Hivi Karibuni.
Bingwa Mashindano ya Wachezaji wa Ridhaa ya Moshi Mwaka 2016 Nicholous Chitanda akiwa katika harakati za mchezo huo.( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

MAHAKAMA YA TANZANIA YAENDELEA NA MABORESHO

$
0
0
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(Mwenye shat ijeupe) akifuatilia Mada kuhusu Mpango Makakati wa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Maboresho ya Mahakama iliyokuwa ikitolewa leo na Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit-JDU) jijini Dar es Salaam
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Ndg. Hussein Kattanga akifafanua jambo kuhusu Mada ya Maboresho ya Mahakama ya Tanzania iliyokuwa ikitolewa na Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) leo jijini Dar es Salaam
Wajumbe wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) wakiwa na Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(mwenyeshatijeupe) kwa ajili ya kutoa taarifa za Maendeleo ya Maboresho ya Mahakama
Mratibu wa Kitengo cha Usimamizi wa Maboresho ya Mahakama ya Tanzania (Judiciary Delivery Unit) Mhe. Zahara Maruma (mwenyemiwani) akimuelezea Kaimu Jaji Mkuu waTanzania Mheshimiwa Prof. Ibrahim Juma(hayupo Pichani) Maendeleo ya Maboresho ya Mahakama leo jijini Dar es Salaam


PICHA NA LYDIA CHURI WA MAHAKAMA YA TANZANIA

RC MASENZA AWAONYA WAZAZI KUACHA KUTUMA WATOTO USIKU WALA KUWALAZA WAGENI CHUMBA KIMOJA NA WATOTO

$
0
0

Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya R.D.O ambayo inajihusisha na huduma za kijamii wilaya ya Mufindi na Kilolo Fidelis Filipatali akimkabidhi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza zawadi ya keki
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa katika picha ya pamoja na watenda kazi wa R.D.O

Filipatali akimkabidhi keki mkuu wa mkoa Masenza kwa ajili ya katibu tawala wa Iringa

Wanawake wakiwa na furaha tele


Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kulia na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini wakichota maji

Diwani wa kata ya Mdabulo akiwa amebebwa juu juu na wanawake baada ya diwani huyo kuimba shairi lenye mvuto kwa wanawake
Mkurugenzi wa R.D.O Bw Filipatali kulia akiuongoza msafara wa mkuu wa mkoa wa Iringa

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwahutubia wanawake

Katibu wa CCM wilaya ya Mufindi Jimson Mhagama kulia na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini na mratibu wa wanawake mkoa wa Iringa mama Sanga wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa
Watumishi ofisi ya RC Iringa wakitoa zawadi kwa ajili ya Yatima
Wasanii wa Ibwanzi wakiigiza kama Rais
Mkuu wa mkoa akitembelea banda ya benki ya Mucoba



Mkuu wa mkoa akipokea risala ya R.D.O

Kazi zinazofanywa na wanafunzi wa R.D.O

Mwenyekiti wa sherehe za wanawake Mufindi

Wafanyakazi ofisi ya mkuu wa mkoa wakiingia kwa maandamano
Wanafunzi wa sekondari ya Mdabulo wakicheza igizo la unyanyasaji wa mwanamke

Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa msaada kwa yatima wanaolelewa na R.D.O






Wafanyakazi ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa wakitoa misaada yao kwa yatima









Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na mwenyekiti wa UWT Marcelina Mkini ambae ni mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Mufindi wakimtwisha ndoo ya maji mmoja kati ya wanawake wakazi wa Ikanga kata ya Mdabulo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na RDO



















































































Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akiwa na wa wafanyakazi wa RDO na viongozi wa wilaya ya Mufindi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za siku ya wanawake duniani









Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na mwenyekiti wa UWT Mufindi Marcelina Mkini wakiongoza maandamano ya wananchi Ikanga kata ya Mdabulo







Wanawake kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa







Na MatukiodaimaBlog

MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza awataka wananchi mkoani hapa kutowaruhusu wageni kulala na watoto chumba kimoja.

























Kuwa kuanzia sasa mgeni akifika nyumbani kwako apewe godoro na kulala sebuleni na sio kushusha watoto vitandani na kumpa heshima mgeni Kulala kitandani chumba cha watoto.


Mkuu huyo wa mkoa ametoa ushauri huo leo wakati akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ikanga kata ya Mdabulo wilayani Mufindi ambako maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yalifanyika kwa mkoa wa Iringa.

Alisema kuwa hatua kuwapa vitanda vya ama wageni kuchanganywa chumba kimoja na watoto baadhi yao si wema wapo kwa ajili ya kuwabaka watoto hao"

Pia aliwataka wazazi kutowatuma watoto nyakati za usiku madukani ama nje ya nyumba zao kwani kuendelea kuwatuma watoto hao usiku ni kuwahatarishia usalama wao na wabakaji

Alitaka ikifika usiku wazazi wenyewe mama na baba ndio watumane dukani kama hakuna mtu mzima wa kutumwa na sio mtoto mdogo

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa amepongeza taasisi isiyo ya Kiserikali ya RDO inayojishughulisha na huduma mbali mbali za kijamii wilayani Mufindi ikiwemo ya maji na malezi ya yatima.

Pamoja na kuishukuru taasisi hiyo ya RDO chini ya mkurugenzi wake Fidelis Filipatali, bado aliwaonya baadhi ya wanasiasa wanaotaka kukwamisha mradi wa maji kwa kuingiza siasa.

Kuwa mradi huo wa maji hauna siasa na kuwa wananchi wanahitaji maji na sio siasa na kuahidi kuendelea kuwa karibu na asasi hiyo ya RDO.

Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Mufindi Marcelina Mkina ambae mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Mufindi na katibu wa CCM wilaya ya Mufindi walimpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kumteua Masenza kuwa mkuu wa mkoa wa Iringa na kuwa maendeleo na ushirikiano mkubwa wa serikali na chama umefanikisha maendeleo Kwa wananchi.

Mkini alisema kuwa pongezi za utendaji kazi wa mkuu huyo wa mkoa atazifikisha rasmi kwenye mkutano mkuu wa CCM .

Hata hivyo alipongeza mapambano dhidi ya dawa za kulevya yanayofanya na serikali ya awamu ya tano pamoja na Vita dhidi ya ufisadi na rushwa na kuwa wao UWT na CCM wapo pamoja na Rais
Viewing all 46329 articles
Browse latest View live




Latest Images