Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

WIZARA YA ARDHI YABORESHA OFISI ZA KANDA

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi akikabidhi funguo ya gari kwa Kamishna wa kanda ya Dar es Salaam; Matthew Nhone.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi, Naibu wake Mhe. Dkt. Angeline Mabulla, Katibu Mkuu; Dkt Yamungu Kayandabila na Viongozi wengine wakuu wa wizara wakikagua magari ya kuhudumia ofisi za ardhi za kanda nchini.


Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeboresha ofisi zake za kanda za ardhi zilizopo nchini ili kuongeza ufanisi katika kutoa huduma za ardhi karibu zaidi na wananchi.

Wizara imegawa magari katika kanda zake zote ili kurahisisha utekelezaji wa kazi za ardhi na kuharakisha huduma za sekta nzima ya ardhi katika maeneo yote ya nchi badala ya wananchi kuja ofisi za Dar es Salaam ambazo kwa sasa zinahamia makao Makuu ya Nchi Dodoma. 

Hatahivyo, huduma nyingine za kisekta kama vile za malipo ya kodi ya pango la ardhi, kituo cha huduma kwa mteja na ofisi za kanda za Dar es Salaam zitaendelea kufanyika kama ilivyokuwa awali.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wakati akitangaza kuhamia rasmi kwa Wizara yake mkoani Dodoma amesema kuwa Wizara imepanga kuwaweka wataalam wa sekta nzima ya ardhi katika ofisi za kanda ili kuondoa usumbufu uliokuwepo wa kufuata huduma za hati, usajili, Uthamini upimaji na ramani na mipango miji na vijiji – Dar es Salaam na Dodoma.

Katika kutekeleza hili kila Kanda itakuwa na viongozi wake walio na mamlaka za utoaji wa huduma za ardhi na kuidhinishwa kwa nyaraka mbalimbali za ardhi na hata utoaji wa hati miliki kutolewa katika kanda.

Viongozi ambao watakuwepo katika kanda hizo ni pamoja na Kamishna na Kanda Msaidizi wa Ardhi, Msajili Msaidizi wa Hati wa Kanda, Mthamini Mkuu Msaidizi wa Kanda, Mkurugenzi Msaidizi wa Upimaji na Ramani wa Kanda, Mkurugenzi Msaidizi wa Mipango Miji na Vijiji wa Kanda na Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi na Nyumba wa Kanda.

Aidha jumla ya kanda ni nane ambazo ambazo zimeboreshwa na kuundwa upya. Kanda hizo ni; Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, ambayo itahusika na mikoa ya Dar es Salaam na Pwani, na Dar es Salaam ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Nyanda za Juu Kusini; itahusika na mikoa ya Mbeya, Njombe, Rukwa na Songwe, ambapo Mbeya ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Kati; ni pamoja na mikoa ya Dodoma, Singida, Iringa na Morogoro na Dodoma ni makao yake makuu.

Aidha, Kanda ya Kaskazini; ni mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Manyara, ambapo makao yake makuu ni Arusha. Kanda ya Ziwa; Ni mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera, ambapo Mwanza ndio makao yake makuu. Nyingine ni Kanda ya Magharibi; yenye mikoa ya Tabora, Kigoma na Katavi na Tabora ndio makao makuu ya kanda. Kanda ya Kusini; Ni mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma na Mtwara ndio makao makuu ya kanda, na kanda ya nane ni Simiyu; yenye mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara na Simiyu ndio makao makuu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

WAZIRI DKT TIZEBA AWAONYA WENYE VIWANDA VYA CHAI KUTOWANYONYA WAKULIMA WADOGO WA CHAI

$
0
0
mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza aliyemwakilisha  waziri wa wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akifungua mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini uliofanyika wilayani Mufindi
Wadau  wa  zao  la chai nchini  wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu  wa mkoa  wa Iringa Amina Masenza(mwenye hijabu ) aliyemwakilisha  waziri wa wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba katika  ufunguzi wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini leo  katika ukumbi wa TRIT Ngwazi Mufindi , kulia kwake ni mwenyekiti wa bodi ya chai nchini Spika (mstaafu ) Anne Makinda ,mkurugenzi wa bodi ya wakurugenzi hamis Umande ,Mathias Ndengi mkurugenzi wa wakala wa chai , Nicholaus Mauya mkurugenzi wa  bodi ya  chai   kutoka kulia wa kwanza waliokaa ni mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa chai Dkt Emmanuel Simbua ,Twahili Nzalewaye mkurugenzi wa maendeleo ya mazao ya  kilimo  na mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam

.......................................................................................

Na MatukiodaimaBlog ,Mufindi 


WAZIRI  wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amewaagiza  wamiliki  wa viwanda  vya  chai  nchini  kununua  chai  ya  Wakulima  wadogo kwa  kuzingatia bei  elekezi ya  serikali na sio bei wanayojipangia  wao  ya  kuwanyonya Wakulima  wadogo  wa  zao  hilo la  chai nchini .

Kuwa  serikali  imedhamilia   kuwakomboa  Wakulima  wadogo wa  zao la  chai hapa nchini kama njia ya  kukuza soko la bidhaa  zitokanazo na chai hapa nchini ya  duniani ,hivyo  njia  pekee ni  kuona Wakulima  wadogo  wanaendelea  kuhamasika  kuongeza kasi ya  kilimo  hicho  cha  chai  ili  kuviwezesha  viwanda vya  chai  nchini  kuzalisha chai kwa  wingi na ubora  zaidi.

Alisema  kuwa zao la  chai ni moja kati ya mazao  yanayopelewa  kipaumbele kama mazao ya  biashara hapa  nchini na  kuwa zao  la  chai  pekee  huliingizia Taifa  wastani  wa  dola  za kimarekani milioni 50  na  kutoa ajira kwa watu  milioni 2 kwa mwaka hivyo ni zao lina lina fursa  kubwa ya  kuongeza wigo  wa kiuchumi nchini pamoja na kuendeleza  kilimo cha  zao  hilo.

Waziri Dkt Tizeba  aliyewakilishwa na mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza  katika  ufunguzi huo wa mkutano mkuu wa wadau wa chai nchini  uliofanyika katika  ukumbi wa taasisi ya utafiti wa chai (TRIT) Gwazi  Mufindi leo alisema  kuwa uzalishaji wa chai nchini kwa upande wa majani makavu ni wastani  wa  tani 35 kwa  mwaka wakati kwa  wakulima  wadogo  wanazalisha wanazalisha  kilo 1000 kwa hekta  kwa mwaka na  Wakulima wakubwa ni wastani wa kilo  2000 za majani makavu kwa hekta kwa mwaka  ukilinganisha takwimu  za nchi ya Kenya  ambayo tija  ni kwa  mkulima  mdogo ni wastani wa kilo 2500 kwa hekta  takwimu  ambazo zinaonyesha   sekta  ndogo ya  chai  nchini ipo nyuma  ukilinganisha na Kenya.

“Ukuaji  wa  sekta  ndogo ya  chai  Tanzania ni mdogo  sana  ukilinganisha na nchi  kama Rwanda na Uganda ila  kuna uwezekano mkubwa wa kuongeza uzalishaji wa tija ya  chai ya  Tanzania  kwa  kuwa nia ya  kuendeleza  zao la chain a ardhi  ipo ….naomba  kutoa rai  kwenu  wadau kuweka mipango ya  kuendeleza  kilimo hiki na serikali ipo nyuma yenu “

Alisema kuwa serikali  imedhamilia  kushirikiana na wadau wa  chai kwa kuongeza ardhi  kwa maeneo yanayolima  chai hadi kufikia hekta  27000 kuwa mwaka 2021/2022 hekta  kutoka  22721 kwa  sasa  pia  kuongeza uzalishwaji wa chai  kavu kutoka wastani wa tani 32 kwa mwaka hadi kufikia  zaidi ya tani 50,000 mwaka  2021/2022 na  kuongeza uzalishaji wa tija kutoka  kilo  1000 kwa mwaka hadi  zaidi ya  kilo 2000 za majani makavu.

Awali mwenyekiti wa mkutano huo spika  wa  bunge la jamhuri ya muungano ya Tanzania (mstaafu)  Anne Makinda ambae ni mwenyekiti wa boi ya chai nchini  alisema  kuwa kero  kubwa ya  Wakulima  wadogo wa chai ni mbolea kwa ajili ya kukuzia zao  hilo kwani  zao  hilo Wakulima hawana  ruzuku ya serikali Kuwa  mbolea  inayotumika kwa zao la chai ni tofauti na ile ya mazao ya mahindi japo  changamoto hiyo wanaendelea  kuijadilia pamoja na  serikali  huku  akidai kuwa  chai ya Tanzania  inauzwa kwa bei ndogo  sana  kutokana na ubora  wake kuwa duni  ukilinganishwa na chai ya Wakulima  wadogo wa Rwanda ambao  walikuwa katika vita leo  wamefikia  chai kavu zaidi ta tani 20,000 lakini Tanzania  ambayo ilipata  uhuru miaka  50  iliyopita  chai haina ubora

“ Yawezekana  wenzetu kwa  kuwa ni Wakulima  wapya  wanatumia  vikonyo vipya na maeneo mapya ndio maana  wanatuzidi ila  sisi  bado  tunatumia  vikonyo vya  zamani na ardhi  iliyochoka “

Makinda  alisema migogoro  midogo midogo inayoanzishwa na viongozi  katika maeneo ya  Wakulima wa chai  ni changamoto ya kurudisha  nyuma kasi ya  uzalishaji wa  zao la  chai nchini hivyo  zinahitajika  jitihada za  kuondoa migogoro  hiyo ili  kukuza zao la chai nchini
MWISHO 

MKUTANO WA KUHITIMISHA MCHAKATO WA RASIMU YA SERA YA MILIKI BUNIFU WAFANYIKA JIJINI DAR

$
0
0

 Kikao cha siku tano cha wabobezi/wataalamu katika mambo ya miliki bunifu,kinaendelea kufanyika katika moja ya ukumbi wa mikutano katika Shirika la Utafiti na maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO),Msasani jijini Dar,ambapo kikao hicho kimejumuisha Wadau kutoka Serikalini sambamba na Sekta binafsi.

Mchakato wa kikao hicho unafuatia wakati shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) lilipoanza kufanya mchakato wa tatifi ya sera ya miliki bunifu  tangu miaka minne iliyopita kwa kufadhiliwa na  wahisani ‘Best Dialogue’ ,ambapo mwaka 2013 inaelezwa kuwa tafiti hiyo ndio ilipelekwa rasmi Wizarani  kwa ajili ya kuendelea na mchakato zaidi.

Rais wa Shirikisho la Filamu hapa nchini (TAFF),Simon Mwakifwamba,alisema kuwa Mkutano huo wa kuhitimisha rasimu ya sera ya miliki bunifu,ni sera ambayo ilipatikana kwa kufuata taratibu zote, kwa maana ya ushirikishwaji kwa upande wa serikali na Sekta binafsi,Mwakifwamba alisema kwa upande wao kama wasanii hiyo ndio sehemu yenyewe muhimu ambayo wasanii wamekuwa wakiiliia kwa muda mrefu.

"Kwa mchakato huu sisi kama wadau tunasema kwamba hapa tulipofika tuko pazuri, na nina imani na wataalamu hawa kwamba tukiwa  na juhudi za pamoja tutaweza  kuhitmisha hii rasimu hii ya miliki bunifu na mwisho  wake tutatoka na sera nzuri ,na kama tutakuwa na msingi mzuri wa kuwa na sera nzuri itatupelekea na kuwa na sheria nzuri,tukiwa na sheria nzuri tutakuwa na  kanuni nzuri,tukiwa na vitu hivyo vitatu tunaamini serikali itakuwa imetengeneza mazingira mazuri kwa wabunifu wote katika nyanja   mbalimbali, kwamba hii sera itakuwa  yenye tija na mafanikio makubwa kwa nchi na hata kwetu  wasanii kwa ujumla".alisema Mwakifwamba.

 
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Biashara ya nje,Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Wilson Malosha akizungumza mbele ya wanahabari na Wadau  mbalimbali katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,Kulia ni Rais Shirikisho la Filamu hapa nchini,Simon Mwakifwamba.
 Wadau mbalimbali wakifutilia yaliyokuwa yakizungumzwa kutoka meza kuu,katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadh ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,
 Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini yaliyokuwa yakijadiliwa katika kikao cha siku tano cha kuhitimisha mchakato wa rasimu ya sera ya miliki bunifu,kilichofanyika jijini Dar na kuhudhuriwa na baadhi ya Wadau kutoka serikalini na Sekta binafsi,

Kaya 1600 Njombe kupata umeme mwakani

$
0
0
Na Greyson Mwase, Njombe

Kaya 1600 katika vijiji kumi mkoani Njombe zinatarajiwa kupata umeme wa uhakika mara baada ya kukamilika kwa mradi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia maporomoko ya maji wa Luponde Hydro Ltd unaotekelelezwa na kampuni ya Rift Valley Energy.

Hayo yalielezwa leo na Meneja Mradi wa Luponde Hydro, Mugombe Maxwell katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini katika mkoa wa Njombe ili kujionea maendeleo ya miradi midogo ya umeme wa maporomoko ya maji na nishati jadidifu inayotekelezwa katika mkoa huo.

Maxwell alisema kuwa kampuni ya Rift Valley Energy ina miradi miwili ambayo ni Mwenga Hydro Grid wenye uwezo wa Megawati 4.1na Luponde Hydro Ltd utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 3 mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wake hivyo kuwezesha vijiji kumi katika mkoa huo kupata umeme wa uhakika ifikapo mwakani.

Akielezea mradi huo wa Luponde Hydro Ltd, Maxwell alisema kuwa mradi ulianza mwaka 2016 na kuongeza kuwa mradi huo upo katika maeneo mawili ambayo ni Luhololo na Igola yote yakiwa mkoani Njombe.

Akielezea ujenzi wa mradi huo, Maxwell alieleza kuwa mradi umegawanyika katika awamu mbili na kuendelea kusema kuwa awamu ya kwanza inahusisha usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji saba vyenye kaya 1120, shule tisa na vituo vya afya vitano

Aliongeza kuwa, awamu ya pili inahusisha usambazaji wa umeme wa uhakika katika vijiji vitatu vyenye kaya 180.

Akielezea hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi huo, Maxwell alisema kazi katika eneo la Luhololo imekamilika kwa asilimia 60 kwa kazi za kawaida na asilimia 40 katika ujenzi wa mitambo.

Aliongeza kuwa katika eneo la Igola mradi umekamilika kwa asilimia 40 na kusisitiza kuwa kampuni itahakikisha kuwa ujenzi katika maeneo yote unakamilika ifikapo mwakani ili wananchi wapate umeme wa uhakika.

Alisisitiza kuwa lengo la mradi ni kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa na umeme wa uhakika na kuchangia ukuaji wa uwekezaji kwenye viwanda hususan katika maeneo ya vijijini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi.
Mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Stephan Kashushura (kulia) akibadilishana mawazo na Sister Richardis Chiwinga katika ziara ya wataalam wa nishati jadidifu katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (katikati) akielezea hali ya maji katika bwawa la mradi huo kwa wataalam wa nishati jadidifu kutoka Wizara ya Nishati na Madini.
Sehemu ya bwala la maji katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole, Mbinga mkoani Ruvuma.
Sister Richardis Chiwinga kutoka katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole (kushoto) akiongoza watalam kutoka Idara ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati Jadidifu katika ziara kwenye eneo la mradi.
Moja ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji katika mradi wa kuzalisha umeme kwa kutumia maji wa Benedict Sisters of Saint Agnes Chipole.
Meneja Uendeshaji kutoka kampuni ya kuzalisha umeme kwa kutumia maporomoko madogo ya maji ya kampuni ya Rift Valley Energy, Joel Gomba (kulia) akionesha sehemu ya kuchepushia maji katika mradi wa Luponde Hydro Ltd uliopo katika hatua ya ujenzi mkoani Njombe kwa mtaalam kutoka Sehemu ya Nishati Jadidifu, Wizara ya Nishati na Madini, Emillian Nyanda (kushoto).

Operesheni ya Viroba Yaibua Wafanyabiashara Wasiokuwa na Vibali vya TFDA.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO.

Operesheni ya kuondoa pombe kali zilizofungwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) inayoendelea nchi nzima imeibua wafanyabiashara wanaofanya biashara ya pombe bila kuwa na vibali vya Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).

Hayo yamebainishwa na Afisa Afya na Mratibu wa Masuala ya Chakula wa Manispaa ya Temeke Rehema Sadick, leo Jijini Dar es Salaam wakati wa operesheni hiyo inayoendelea nchini.

“Katika operesheni hii ya kuondoa pombe za viroba tumegundua wafanyabiashara wengi wanaojihusisha na uuzaji wa pombe kutokuwa na kibali cha TFDA ambacho hutolewa katika Halmashauri husika,” alifafanua Rehema Sadick.

Aidha amebainisha kuwa katika msako uliofanyika leo Kigamboni, ambapo wamekagua zaidi ya maduka matano yanayouza pombe kwa jumla, ni duka moja tu la Mangale Store lililoko Tuangoma ndilo lililokutwa na kibali cha TFDA.

Aliongeza kuwa, maduka yote ambayo hayakuwa na vibali hivyo yameamuliwa kufungwa na kufuatilia vibali katika Halmashauri husika na taarifa za maduka hayo ikiwemo jina la duka, majina ya mmiliki eneo lilipo pamoja na namba za mawasiliano vimechukuliwa kwa ajili ya kuchukua hatua.

Afisa Afya huyo ametoa rai kwa wafanyabiashara wote kuacha kufanya biashara kwa mazoea na kuhakikisha wanakuwa na vibali vyote muhimu pamoja na leseni za biashara, kwani kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na kanuni za nchi.

Operesheni ya kuondoa viroba ilianza rasmi Machi 01, 2017 kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa la kutaka kusitishwa kwa utengenezaji, usambaaji, uuzaji na utumiaji wa pombe hizo kali maarufu kama viroba.ifikapo Machi mosi mwaka huu ambapo mpaka sasa operesheni hiyo imeingia siku ya tano tangua kuanza kwake.

BILIONI 568 KUNUFAISHA WABUNIFU SEKTA YA AFYA

$
0
0
Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Atamizi ya DTBi yenye lengo la kuleta mapinduzi katika Sekta ya Afya, Mhandisi George Mulamula, Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hassan Mshinda, Mratibu wa Kikanda wa MCC/PEPFAR Bwana Mitch Blasser pamoja na Meneja Mkuu wa Mradi wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLI), Agapiti Manday wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mradi huo.

Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hassan Mshinda, akikabidhi Hundi ya millioni 568 kwa wajasiriamali wavumbuzi 12 waliovumbua miradi mbalimbali ya kuiendeleza Sekta ya Afya chini ya mradi wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLI) unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani katika Vita dhidi ya Makali ya UKIMWI (PEPFAR) na kusimamiwa na taasisi ya serikali ya marekani ya Changamoto za Millenia (MCC),



Wajasiriamali vijana 12 waliovumbua miradi mbalimbali ya kuiendeleza Sekta ya Afya chini ya mradi wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLI) unaofadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani katika Vita dhidi ya Makali ya UKIMWI (PEPFAR) na kusimamiwa na taasisi ya serikali ya marekani ya Changamoto za Millenia (MCC) wakiwa katika picha ya pamoja na hundi ya mfano ya millioni 568 walizokabidhiwa.

…………………………………………………………………………………..

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inategemea kukabidhi jumla ya shilingi bilioni 568.575, 000/= kwa vijana 12 waliobuni mawazo bora yatakayosaidia kuondoa changamoto zinazoikabili sekta ya Afya hapa nchini.

Mkurugenzi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dkt. Hassan Mshinda aliyasema hayo hivi karibuni Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua mradi wa Data for Local Impact Innovation Challenge (DLI) uliopo chini ya Atamizi ya DTBi yenye lengo la kuleta mapinduzi katika matumizi ya taarifa na takwimu mbalimbali katika sekta ya Afya.

Dkt. Mshinda alisema shughuli za ujasiriamali na ubunifu ni muhimu na chachu ya maendeleo ya nchi yoyote kwa kuwa zinasaidia kutengeneza ajira, kuongeza wigo wa shughuli za uzalishaji mali pamoja na kuchangia katika pato la taifa.

Alisema Serikali kupitia COSTECH iliamua kuanzisha Atamizi ya DTBi mwaka 2011 ili kuwasaidia wajasiriamali wanaoshughulika na suala la TEHAMA.

“Nafahamu mradi huu umejikita katika changamoto za matumizi ya taarifa katika sekta ya afya, maendeleo ya kiuchumi na usawa wa kijinsia kama yalivyotanabaishwa katika malengo ya maendeleo endelevu, ubunifu hasa katika eneo la TEHAMA ni muhimu sana kwa sababu unasaidia kuongeza tija na ufanisi wa utoaji huduma katika sekta mbalimbali nchini”,Alisema.

Aidha Dkt. Mshinda alisema nia ya DTBi ni kuwawezesha Vijana, kuwajengea uwezo na kuwapa misaada ya msingi wataalam na wabunifu wa kitanzania waliopo katika eneo la TEHAMA ili kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya kitanzania kwa kutumia teknolojia.

Dkt. Mshinda aliwahakikishia wajasiriamali hao kuwa COSTECH itaendelea na juhudi zake za kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwemo Serikali na taasisi za fedha kukabiliana na changamoto ya masharti ya mikopo kwa wajasiriamali.

Kwa upande wake Meneja Mradi wa DTBi, Agapiti Manday alisema wanapokea mawazo mbalimbali ya vijana na kuyachuja na baadae wanachukua vijana wachache walio na mawazo bora zaidi na kuwawezesha ili waweze kuweka mawazo yao katika vitendo.

“Tunafahamu kuwa wapo vijana wengi mtaani wanaomaliza elimu katika ngazi mbalimbali ikiwemo vyuo vikuu ambao wana mawazo bora ya kuipeleka Tanzania mbele kimaendeleo lakini fursa hiyo wanaikosa kutokana na kukosekana kwa fedha na miongozo ya kuyafanya mawazo yao kuwa katika vitendo hivyo mradi huu unawasaidia vijana kuweka mawazo kuwa vitendo,”alisema Manday.

Bw. Manday Amefafanua kuwa changamoto kubwa ya wajasiriamali wa kitanzania ni ukosefu wa mitaji ya kufanikishia au kuendeleza shughuli zao za kiujasiriamali hivyo kwa kupitia mradi huo wataendelea kusaidiwa hadi pale watakapoweza kusimama kwa nguvu zao wenyewe.

Mradi huo mpya kwa Tanzania, umefadhiliwa na Mfuko wa Rais wa Marekani katika Vita dhidi ya Makali ya UKIMWI (PEPFAR) na kusimamiwa na taasisi ya serikali ya marekani ya Changamoto za Millenia (MCC), Mradi huu umeanza utekelezaji mnamo mwezi Aprili mwaka 2016.

TADB, BODI YA NYAMA KUWAWEZESHA WADAU WA UFUGAJI WA NG’OMBE

$
0
0

 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (wa pili kushoto) na Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (wa pili kulia) wakionesha fulana kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017. Wengine pichani ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John (kushoto) na Afisa Sheria wa TMB, Bw. Praisegod Lukio (kulia).

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (Kulia) akiwakaribisha maafisa kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017. Kushoto ni Afisa Masoko na Utafiti, Bw. Nicholai Chiweka na Afisa Sheria, Bw. Praisegod Lukio (katikati).

Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (aliyeinama) akisaini Kitabu cha Wageni wakati alipomtembelea TADB. Wanaoshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto), Afisa Sheria wa TMB, Bw. Praisegod Lukio (wa pili kushoto). Kulia ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga (kushoto) akizungumza na maafisa kutoka Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) Afisa Sheria, Bw. Praisegod Lukio (wa pili kushoto) na Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (wa pili kulia) wakati walipomtembelea Ofisini kwake kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017. Kulia ni Mkuu wa Huduma na Sheria wa TADB, Bibi Neema Christina John.

Afisa Masoko na Utafiti wa TMB, Bw. Nicholai Chiweka (kulia) akizungumza wakati walipomtembelea Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB (hayupo pichani) kujadiliana juu ya Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Bodi ya Nyama Tanzania (TMB) zimejidhatiti kusaidia mnyororo wa thamani wa ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa ili kuongeza tija kwenye sekta ya ufugaji wa ng’ombe nchini.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga na Afisa Masoko na Utafiti, Bw. Nicholai Chiweka kutoka TMB wakati wa majadiliano kuhusu Mkutano Mkuu wa Wadau wa Bodi ya Nyama utakaofanyika mkoani Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 9 Machi, 2017.

Bw. Assenga amesema kuwa TADB imejidhatiti katika kuongeza tija kwa Ufugaji wa Ng’ombe wa Nyama na Maziwa kwa kutoa mikopo na kusaidia shughuli mbali mbali za uongezaji tija wa ufugaji huo.

“Katika kuhakikisha sekta hii inaendelea na kuongeza tija, TADB imejipanga kutoa mikopo itakayotumika kama mtaji kwa ajili ya uendeshaji wa mashamba, uongezaji wa thamani na gharama za uhifadhi wa nyama/maziwa na miundombinu masoko kwenye sekta hii,” alisema Bw. Assenga.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB ameongeza kuwa kwa kushirikisha wadau wa Kilimo, utafiti, huduma za ugani na madaktari wa mifugo TADB imelenga kuwapatia wafugaji mafunzo ya ufugaji wa kisasa wa ng’ombe wa nyama na maziwa kwa kutumia mbinu bora za ufugaji ili kufuga kibiashara na hivyo kujiongezea kipato na kupambana na umaskini.

Kwa upande wake Bw. Chiweka amesema kuwa TMB ina Mamlaka yenye dhamana ya kusimamia maendeleo ya tasnia ya nyama, iliyoanzishwa kwa Sheria ya Nyama Na. 10 ya Mwaka 2006 hivyo ina wajibu wa kuratibu mnyororo mzima wa thamani wa tasnia ya nyama na kuiomba TADB kushirikiana na TMB kunyanyua sekta ya nyama.

“Kifungu Na. 17 (1) cha sheria hii, kinazuia mtu yeyote kufanya shughuli ya aina yoyote katika tasnia ya nyama bila ya kuwa na cheti cha usajili kutoka Bodi ya Nyama Tanzania hivyo kama mdau wa kuendeleza sekta hii tunaiomba TADB kuwasaidia wadau wa mnyororo mzima wa thamani wa tasnia ya nyama ambao wamesajiliwa na TMB,” alisema.

Kwa mujibu wa Bw. Chiweka wadau wa tasnia ya nyama inajumuisha Wafugaji wa mifugo ya aina zote inayozalisha nyama; Wafanyabiashara wa Mifugo; Wasafirishaji wa mifugo na nyama; na Wenye machinjio za aina zote. Wengine ni Wenye bucha za kuuza nyama za aina zote; Wasindikaji wa nyama; maduka makubwa na duka la bucha, Wasambazaji wa bidhaa za nyama; Waingizaji wa nyama nchini; Wasafirishaji wa mifugo, nyama na bidhaa zake nje ya nchi; na Waendesha matamasha ya nyama choma.

Mnyororo wa thamani wa Ufugaji wa ng’ombe wa nyama na maziwa ni miongoni mwa minyororo ya mwanzo inayopatiwa mikopo na TADB ili kuongeza thamani mazao na mifugo mbalimbali nchini.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MACHI 8,2017


HUAWEI YATUNUKIWA TUZO YA UBORA KATIKA MKUTANO WA MWC 2017

$
0
0
Mwakilishi wa Huawei (kushoto) akipokea Tuzo ya Simu yenye Mfumo Bora kwenye Mkutano wa Dunia wa Mawasiliano 2017.

Huawei kupitia kitengo chake cha Active Antenna Unit (AAU) imeshinda tuzo ya Simu yenye Mfumo Bora zaidi katika Mkutano wa Wadau wa Mawasiliano (MWC) 2017.

Tuzo hiyo ilitambua mchango wa Kampuni ya Huawei katika ubunifu wa teknolojia na mfumo wake mzuri wa mawasiliano na kuimarisha kituo chake kwa kizazi kijacho. Ukiratibiwa na GSMA, mkutano huo wa MWC ni miongoni mwa mikutano mikubwa yenye ushawishi duniani na Taasisi hiyo inayoandaa Tuzo za Global Mobile ni miongoni mwa tuzo zinazoheshimika katika sekta ya mawasiliano.

Kitengo cha AAU kimelenga kuanzisha mfumo huo wa mawasiliano ya simu unawezesha kupata huduma ya redio kutoka vituo mbalimbali. Hiyo ndiyo kizazi kipya cha Huawei ambacho kimelenga katika kutafuta ufumbuzi kutokana na kutambua umuhimu wa kusambaza taarifa.

Kitengo hicho cha Huawei ni mwendelezo wa uvumbuzi kwa ajili ya kufikia mahitaji wa watumiaji wa mtandao katika maeneo tofauti. Huduma hii itaendelea kuboreshwa taratibu kadiri mabadiliko ya kimtandao yanavyoendelea.

Mkuu wa Huawei Huduma za Mtandao, Zhou Yuefeng alisema “Kulingana na maendeleo ya haraka ya MBB, huduma mpya kama vile VR, HD Video na mtandao wa wirelesss kwa matumizi ya nyumbani yote hayvyote vimesababisha kuwapo na hitaji kubwa la kuimaraisha uwezo wa mitandao,

Wakati huohuo, watumiaji wanahitaji kupunguza gharama za umiliki (TCO). Mfumo wa Huawei wa AAU ndiyo unaoweza kuwa msaada kwa watumiaji wa huduma a mitandao kuepukana na changamoto ya kutopata video zenye ubora. Hivi sasa kitengo cha Huawei cha AAU kimekuwa suluhisho la biashara ambayo inamwezesha mtu kutazama video kupitia simu yake mfumo uliounganishwa katika nchi zaidi ya 60 ulimwenguni kote.

Kwa kutumia teknolojia ya 4.5/5G imeleta mabadiliko kwa kuongeza ufanisi na kutumia antena ya teknolojia ya kisasa zaidi. Mfumo huo umefanikiwa kuongeza ubora wa matumizi ya mtandano mara tano zaidi huku pia ikisaidia kupunguza gharama kiasi fulani na kuimarisha uzoefu kwa watumiaji wake.

Huawei tayari imeshaanza kutumia mfumo wa FDD na MIMO pia kitengo cha AAU kimeanza kutumia teknolojia hiyo kwenye kampuni ya mawasiliano ya China Unicom na vilevile umeshaanza kutumiwa kwa majaribio kwenye simu China na Japan kwenye mfumo wa simu kibenki.

Mfumo huo wa Huawei unawawezesha watu kutumia vyema rasilimali zilizopo katika maeneo ya mijini kwa ajili ya kuona video, kupunguza utegemezi kwenye vyanzo vingine, kuokoa muda kutokana na upatikanaji wake wa urahisi kwa asilimia 60 na kupunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.

Huawei ilianzisha mfumo wa Easy Macro 2.0 mwaka 2017 ambao unawezesha GSM/UMTS/LTE, ambayo inaweza kukuwezesha kuona video kwa mlalo au mshazari. Mfumo huo wa Huawei umekuwa mkombozi kwa kutumika katika mitandao ya kibiashara duniani ikiondoa kikwazo kilichokuwapo awali katika kupatikana video kwenye simu.

Mfumo wa Huawei wa multi band unaosimamiwa na kitengo cha AAU unaweza kuwezesha mpaka bendi 7 pamoja na 4t4R na kupunguza uwingi wa vifaa na kuandaa video iwapo unahitaji kukodisha eneo.

Mfumo wa Huawei wa AAU ndio unaoongoza katika mabadiliko ya matumizi ya mtandao. Kuwapo kwa mfumo mpya wa 5G hii imerahisisha zaidi na watumiaji kupata video zenye ubora.

Mkutano wa wadau wa mawasiliano mwaka huu ulifanyika kuaniza Februari 27 hadi Machi 2 jijini Barcelona, Uhispania. Huawei ilifanya maonyesho ya bidhaa zake za mfumo wa ndani wa mawasiliano ambazo eneo la 1J50 in Fira Gran Via katika ukumbi 1, sehemu ya 3130 kwenye ukumbi 3 na Mji wa Ubunifu kwenye ukumbi 4. Kwa maelezo zaidi tafadhari tembelea kwenye tovuti yetu.

http://www.huawei.com/en/events/mwc/2017/.

UZINDUZI WA MAFUNZO YA KUJENGA AJIRA KUPITIA VIPODOZI KWA WANAWAKE JIJINI MBEYA WAFANA

$
0
0
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akizungumza wakati Akifungua Mafunzo ya Ujasiriamali Mkoa wa Mbeya 

Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede kawataka wanawake wa Mkoa wa Mbeya kuchangamkia fursa ya ujasiraiamali inayotolewa na Taasisi ya Manjano Foundation. Amesema hayo mapema leo jijini Mbeya alipokuwa akifungua mafunzo ya wanawake 30 juu ya masuala ya ujasiriamali na urembo yanayoendeshwa ta Taasisi ya Manjano Foundation .
Meneja wa SIDO Mkoa wa Mbeya Henrick Mdede Akiwa Ameambatana na Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Mama Fatuma Kange Pamoja na Mkurugenzi wa Manjano Foundation Mama Shekha Nasser “Shekha Nasser ni moja ya wawekezaji wa ndani ambao wanapaswa kuungwa mkono na kila mmoja kwani ameamua kuwekeza na kuwawezesha wanawake kwa kutumia bidhaa ambazo zimesajiliwa hapa hapa nchini kuwawezesha wanawake wadogo kupata mafunzo ili waweze kuingiza pesa kupitia bidhaa hizo” amesema meneja wa SIDO.
Mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser Akizungumza Machache kwenye ufunguzo huo.

Ameongeza kuwa mbali na Taasisi ya Manjano Foundation kutoa elimu ya ujasiliamali kwa wasichana hao pia ipo katika mpango kabambe kuwaunganisha wanawake hao na Taasisi za kifedha ili kuweza kupata mikopo ili kupata mitaji ya kuanzisha biashara zao.
Mgeni Rasmi akiwa katika Picha ya Pamoja na Washiriki wa Mafunzo ya Ujasiriamamli Mkoa wa Mbeya.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Manjano Foundation Shekha Nasser amesema kuwa wasichana ambao wanapata mafunzo kutoka taasisi hiyo wanaweza kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuchangamkia fursa zilizopo kwenye tasnia ya Urembo.
Aidha ametaja kuwa program hiyo katika mwaka huu itaweza kuwafikia wanawake katika mikoa mitano nchini hili waweze kujikwamua kiuchumi.

Makamu wa Rais Mama Samia alaani na kukemea vikali vitendo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinavyoendelea katika jamii

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan amelaani na kukemea vikali vitendo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinavyoendelea katika jamii na amewataka wananchi kote nchini kushirikiana katika kukabiliana na vitendo hivyo nchini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo tarehe 8-March-2017 wakati akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji wa Tanzania (TBC) mjini Dodoma kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema vitendo hivyo vya ukeketaji wa wanawake na ubakaji vinamchukiza sana hivyo ametoa wito maalum kwa wananchi na wadau wote bila kujadili dini, kabila wala rangi kupambana ipasavyo na vitendo hivyo ambavyo vinarudisha nyuma jitihada za kumkwamua mwanamke kiuchumi.

Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema anafurahishwa na hatua na jitihada zinazochukuliwa na wanawake kote nchini katika kujikwamua kiuchumi kwa kuimarisha shughuli zao za ujasiriamali katika kuelekea katika uchumi wa viwanda.

Amesema jukumu kubwa la serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha wanawake wanaboreshewa ipasavyo mazingira ya kufanyia kazi hasa shughuli za ujasiriamali ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.

“Inapofika katika shida zetu wanawake ni lazima tuwe na kitu Kimoja na sauti Moja katika kulinda na kutetea haki zetu bila kujali itikadi za kisiasa”Amesisitiza Makamu wa Rais.

Katika uundaji wa majukwaa ya kuwawezesha wanawake kiuchumi nchini, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesema kazi hiyo inaendelea vizuri na kutaka mikoa na wilaya ambazo bado haijaunda majukwaa hayo kufanya hivyo haraka iwezekanavyo.

Ameeleza kuwa lengo la uundaji wa majukwaa hayo katika ngazi ya wilaya na mikoa nchini ni kuwakutanisha wanawake pamoja katika kujadili na kutafutia ufumbuzi changamoto zinazowakabili ikiwemo tatizo la masoko za bidhaa wanazozizalisha.

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa majukwaa hayo ambayo yameanza kuundwa katika mikoa mbalimbali nchini yatakuwa sio ya kisiasa.

Katika Mahojiano hayo na mtangazaji Shaban Kissu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mjini DODOMA, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu ametumia sehemu ya mahojiano hayo kwa kuwatakia heri na mafanikio wanawake wote nchini katika kuadhimisha Siku ya wanawake Duniani.

Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya wanawake Duniani ni “Tanzania ya Viwanda,Wanawake ni msingi wa mabadiliko ya Kiuchumi”.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dodoma. 8-Mar-2017

JKCI KUANZA UPASUAJI WA KUPANDIKIZA MOYO.

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO

Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) inatararajia kuanza upasuaji wa kupandikiza Moyo kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo nchini.

Mkurugenzi wa Upasuaji na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Moyo na Mishipa ya Damu Dkt. Bashir Nyangasa ameyasema hayo leo Jijini, Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari kuhusu malengo ya Taasisi hiyo.

“Tuko katika maandalizi ya kuandaa mapendekezo kwa ajili ya kupeleka Bungeni ili Bunge lilidhie na kupitisha sheria itakayoruhusu mtu kuandika wosia wa viungo vyake kutumika mara baada ya kufariki, ikiwemo moyo, figo na viungo vingine,” alifafanua Dkt. Nyangasa.

Aliendelea kwa kusema kuwa, umefika wakati kwa watanzania kujiwekea utaratibu wa kuacha wosia wa kutumika kwa viungo vyao mara baada ya kufariki kwa ajili ya kuhifadhiwa katika benki za viungo ili viweze kutumika na watu ambao wanauhitaji.

Aidha Dkt. Nyangasa amesema hospitali ya Apolo Bangalole ya India na hospitali nyingine za kimataifa za magonjwa ya moyo kwa sasa zimehamia JKCI kutokana na huduma pamoja na vifaa vinavyopatikana katika hospitali hizo vinapatikana katika Taasisi hiyo.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Huduma za Tiba, Daktari Bingwa wa Wagonjwa wa Moyo Dkt. Tulizo Shemu amesema kwa mwaka 2016 Taasisi imefanya uchunguzi wa tiba kwa wagonjwa 973, kati ya wagonjwa hao 620 walipatiwa matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua kwa kupitia mishipa ya damu (Catheterization) na wagonjwa 353 walifanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.

Vilevile amesema kuwa kwa mwaka huu wa 2017 Taasisi hiyo imejipanga kufanya upasuaji wa kupasua kifua kwa wagonjwa 700 na wagonjwa wengine 1000 watafanyiwa operesheni bila ya kufungua kifua kwa kutumia mtambo wa ‘Catheterization’.

Taasisi hiyo inategemea kuwa na kambi maalum ya matibabu ya moyo kwa kushirikiana na Taasisi ya Open Heart International ya nchini Australia kuanzia Machi 10, 2017 ambapo wagonjwa 25 wakiwemo watoto 15 na watu wazima 10 watafanyiwa upasuaji.

Wananchi wameombwa kujitokeza kuchangia damu kutokana na uhitaji wa damu nyingi katika upasuaji huo.

WAKAZI WA KATA YA WINO – MADABA MKONI RUVUMA WACHANGIA MILIONI 30 ILI KUKAMILISHA MRADI WA MAJI SAFI.

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Mhagama akichangia Shilingi milioni 7 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji
..............................
Wakazi wa kata ya WINO halmashauri ya wilaya ya MADABA mkoani Ruvuma, wamechukua jukumu la kuchangishana fedha kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji unaogharimu kiasi cha shilingi million sabini ili kuondokana na kelo ya maji.

DC GONDWE APOKEA MSAADA WA MBEGU KUTOKA WORLD VISION

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondwe (wa kwanza kushoto) pamoja na  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bw. William Makufwe wakipokea mbegu za mahindi ya njano kutoka kwa Msimamizi wa mradi Bw. Kelvin Metta wa World Vision.
  Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh. Godwin Gondweakiwa ameshikilia mbegu za miche ya Viazi, kushoto ni Mkurugenzi  Mtendaji, kulia Kaimu Afisa kilimo Bi. Rosemary Bughe,Wakuu wa Shule  na Maafisa ugani  wakipata maelekezo mafupi kuhusu mbegu.
Kaimu Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni Bi. Rosemary Bughe  akiwa ameshikilia kifurushi kimojawapo cha mbegu za miche ya mihogo.

MASAUNI ATEMBELEA BANDARI YA ZANZIBAR, AAGIZA JESHI LA POLISI KUSHIRIKIANA NA UONGOZI WA BANDARI KUDHIBITI UINGIAJI WA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar,  ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari,  kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akitembea kuelekea sehemu inayokaguliwa mizigo  wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar, kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kulia  ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma.
 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akikagua jinsi ukaguzi wa mizigo unavyofanyika kupitia komputa wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya, huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Kulia ni Afisa wa Bandari anayeshughulika na ukaguzi, Adam Masoud.
 Mfanyakazi wa kitengo cha mizigo Bandari ya Zanzibar, Saleh Masoud akikagua moja ya mzigo wa abiria wanaoingia kupitia bandari hiyo ambapoNaibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,ameliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari hiyo kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa Dawa za Kulevya ambazo zimekuwa zikiharibu nguvu kazi ya Taifa.
 Mkurugenzi Mkuu Bandari ya Zanzibar, Kapteni Mstaafu Abdula Juma (wapili kushoto), akimsikiliza Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni,  wakati wa ziara ya kutembelea bandari hiyo  ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi  kushirikiana na Uongozi wa Bandari kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa.Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na  wakwanza kulia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,  Johari Masoud Sururu.
Kifaa cha kubebea kontena kikiwa kimebeba kontena tayari kupelekwa kwenye mashine maalumu ya ukaguzi ambayo hutumia mionzi kukagua mzigo uliopo ndani, ambapo Naibu  Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni  ameliagiza Jeshi la Polisi kushirikiana na Uongozi wa  Bandari ya Zanzibar kukagua mizigo yote inayoingia ili kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


WAZIRI MKUU AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA YAKE MDOGO KIKWETE

$
0
0
Rais Mstaafu Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohudhuria mazishi ya Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishiriki ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Bibi. Nuru Halfan Kikwete ambaye ni mama mdogo wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne mheshimiwa Dk. Jakaya Kikwete nyumbani kwa marehemu Bagamoyo mkoani Pwani leo Machi 8, 2017. Kulia ni Rais Mstaamu Dk. Kikwete (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIA AFANYA ZIARA MKOANI KAGERA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA KABYAILE MISSENYI

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Venance Mabeyo amefanya ziara ya kikazi Mkoani Kagera kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Afya Kabyaile Wilayani Missenyi kinachojengwa upya na Jeshi la Wananchi Tanzania mara baada ya kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi lililotokea Mwezi Septemba mwaka jana.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo alifanya ziara hiyo Machi 2, 2017 na lengo kuu ilikuwa ni kuona maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho mara baada muda alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli kuisha mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu 2017.

Rais Magufuli alipofanya ziara Mkoani Kagera Januari 1, 2017 alitembelea eneo la Kabyaile Wilayani Missenyi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho cha afya na kuagiza kuwa ujenzi huo uwe umekamilika ifikapo Mwisho mwa mwezi Februari 2017.

Mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi huo Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo akiongea na viongozi wa mkoa na wananchi waliofika kumuona kituoni hapo alisema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi huo, pia alishukuru upanuzi wa majengo kuwa ni manufaa kwa wananchi wa Kabyaile na Wilaya ya Missenyi kwa ujumla.

Pia aliwashukuru wananchi kwa ushirikiano wao na kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania kinachojenga kituo hicho kuwa kikosi hicho kinafanya kazi katika hali ya utulivu na amani na wananchi wenyeji, aidha aliwaomba wananchi kuwaona wananjeshi kama raia wengine na kuendelea kuwapa ushirikiano kwani wanatokana na Watanzania wenyewe.

Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo baada ya kukagua ujenzi na kupata maelezo ya kina alisema kuwa muda alioutoa Rais Magufuli wa hadi mwishoni mwa Mwezi Februari 2017 ujenzi haukuweza kukamilika kwasababu kuna kazi zingine za ziada ambazo zilijitokeza na kushindwa kukamilisha kituo hicho kwa muda uliotolewa.

?Kwa kazi alizoelekeza Rais Magufuli tayari zipo katika hatua za mwisho kabisa za umaliziaji, pia na kazi zilizoongezeka zipo katika hatua nzuri ya ujenzi na kufikia mwishoni mwa mwezi Machi 2017 kazi zote zitakuwa zimekamilika zote? Aliwaeleza wananchi Mkuu wa Majeshi Jenerali Mabeyo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Jenerali Mabeyo alitembelea pia ujenzi wa Shule ya Sekondari Omumwani Katika Manispaa ya Bukoba kunakojengwa vyumba viwili vya mabweni na Kikosi cha Jeshi la Wananchi Tanzania, aidha alimalizia ziara yake katika Shule ya Sekondari Ihungo na kukagua ujenzi mpya wa shule hiyo iliyoharibiwa na tetemeko pia mwezi Septemba Mwaka jana 2016.

JOKATE AWATAKA WASICHANA KUJIAMINI HILI WAWEZE KUFANIKIWA

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mwanamitindo maharufu nchini,Jokate Mwegelo amewataka watoto wa kike kujiamini,ili waweze kufikia mafanikio katika maisha hayo kwa kuweka juhudi katika elimu.

Jokate amesema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam

“nataka niwaambie watoto wa manzese sekondari,siri kubwa ya mafanikio ni kujiamini lakini usijiamini katika ujinga hivyo mnapaswa kujiamini katika vitu vya msingi ambavyo vitweza kusaidia jamii yetu kutoka sehemu moja kwenda nyingine” amesema Jokate.

Kwa upande wake program meneja wa TAI, Edith James amesema kuwa umefika wakati wa wanawake kujiamini hasa kwa kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi na usafi wa mwili kwa ujumla hasa wakati wanapokuwa katika siku zao.

Amesema kuwa taasisi ya TAI imekuwa katika kampeni kwa zaidi ya shule kumi za mkoa wa Dar es Salaam,kwa kutoa elimu kwa watoto wa kike waweze kupata elimu bora juu ya afya ya uzazi.
 Picha kwa juu ikionyesha namna Jokate alivyokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese
 Jokate akiwa katika picha ya Pamoja na wanafunzi wa shule ya Sekondari Manzese
 Daktari kutoka tasisi ya TAHMEF, Victoria Joseph  akitoa maelekezo juu ya tasisi yao inavyotoa huduma kwa watoto wa kike mashuleni
 Joakate Mwegelo akikabidhi taulo za kike kwa mmoja wanafunzi wa sekondari ya Manzese jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kampuni ya Kays Hygiene product Malik Mtui akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Manzese
 Jokate Mwegelo akipima afya katika zoezi liliondeshwa shule ya sekondari Manzese jijini Dar es Salaam
 Mratibu kutoka tasisi isiyo ya kiserikali ya TAI, Edith James akizungumza na mabinti wa shule ya sekondari Manzese
 Mwanamitindo Jokate Mwegelo akizungumza na Mabinti wa shule ya Sekondari Manzese jijini Dar es Salaam juu ya kujitambua na kujiamini hili kufikia mafanikio


TANZANIA YAONGOZA KWA KASI NDOGO YA ONGEZEKO LA MFUMUKO WA BEI KATIKA AFRIKA MASHARIKI.

$
0
0

Na: Frank Shija – MAELEZO.

Kasi ya mfumuko wa bei za bidhaa na huduma nchini Tanzania umeongezeka kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mfumuko wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari mwaka 2017.

Ruth amesema kuwa mfumuko huo umeongeka kutoka asilimia 5.2 mwezi Januari hadi kufikia 5.5 mwezi Februari, 2017 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 0.3 kiasi ambacho hakina athari katika uchumi wa nchi.

“Ongezeko hilo la mfumuko wa bei umeendelea kukua kwa kiasi kidogo ukilinganisha na nchi zingine za ukanda wa Afrika Mashariki zikiwemo Uganda na Kenya ambazo tunashabihiana kwa kiasi kikubwa”. Alisema Ruth Minja.

Kwa upande wa mfumuko wa bei kwa bidhaa za Vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi cha mwaka, umeongezeka hadi asilimia 9.3 kutoka asilimia 8.2 mwezi Januari, 2017, wakati badiliko la fahirisi kwa bei zisizo za vyakula limebaki kuwa asilimia 3.6 kama ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.

Ameongeza kuwa farihisi za bei zimeongezeka hadi 106.97 mwezi Februari,2017 kutoka 101.44 mwezi Januari, 2017 wakati mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Februarii,2017 zimeongezeka hadi asilimia 8.7 kutoka asilimia 7.6 ilivyokuwa mwezi Januari, 2017.

“Mwenendo wa fahirisi za bei za Taifa na Mfumuko wa Bei kutoka mwezi Februari 2016 hadi mwezi Februari, 2017 umeendelea kuimarika ambapo katika kipindi hicho, mfumuko wa bei umekuwa na mwenendo imara kutoka asilimia 5.6 mwezi Februari, 2016 hadi asilimia 5.5 februari,2017,”alisema Kaimu Meneja huyo.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kupitia Sheria ya Takwimu na 9 ya mwaka 2015 inao wajibu na mamlaka ya kuratibu upatikanaji na utoaji wa takwimu rasmi nchini.
Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtakwimu kutoka Ofisi hiyo Hashim Njewele.
Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei Ruth Minja kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) akizungumza na waadishi wa habari kuhusu hali ya mfumuko wa bei kwa mwezi Februari 2017 leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia maelezo kuhusu hali ya mfumuko wa bei kutoka kwa Kaimu Meneja wa Ajira na Takwimu za Bei kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Ruth Minja (hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi ha oleo Jijini Dar es Salaam.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

DAWASCO YASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE KWA KUTOA MSAADA KWA WAZEE

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

Shirika la maji safi na Taka jijini Dar es Salaam (Dawasco) katika siku ya wanawake duniani  imetoa msaada kwa Kituo cha Kulelea Wazee na Watoto cha Mather Theresia kilichopo Kigogo.

Dawasco imetoa msaada wa mchele, mafuta ya kupikia, Sukari, Sabuni , unga wa mahindi, Nepi za watoto pamoja na chumvi.

Akizungumza na baada kutoa msaada huo Mkurugenzi wa Sheria wa Dawasco, Benadetha Mkandya amesema kuwa  Dawasco wanatoa huduma kwenye jamii hivyo wanawajibu kusaidia wazee kwani ipo siku watakuwa wazee na kwenda kuishi katika kituo hicho.

Amesema Dawasco kutokana na kuthamini kile wanachokipata wanaona katika siku ya wanawake kuweza kusaidia wazee.

Benadetha amesema katika kuadhimisha siku ya wanawake iwe ni sehemu kila mwanamke kuweza kujiamini kwa kile anachokiamini katika kuleta matokeo chanya.

Amesema mwanamke sio mtu ambaye yuko kwa ajili ya kupika bali anaweza kufanya jamii ikawa na mabadiliko katika nyanja mbalimbali
 Mkurugenzi wa Sheria wa Dawasco, Benadetha Mkandya(wa kwanza kulia) akikabidhi msaada kwa Mwakilishi wa Wazee katika kituo cha Mother Theresia  leo katika Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
  Baadhi wafanyakazi wa Dawasco wakiwavisha nguo wa wazee wa kituo cha mother Theresia leo.
Wafanyakazi wa Dawasco wakiwa kwenye picha ya pamoja na Wazee wa Kituo cha Mother Theresia Kigogo leo.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images