Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live

Pombe za Viroba Zenye Thamani ya Shilingi Bilioni 2 Zakamatwa.

$
0
0
 Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche akionesha kwa waandishi wa habari moja ya pombe kali aina ya Nguvu zilizokamatwa wakati wa operesheni inayoendelea mapema leo hii jijini Dar es Salaam wakati wa siku ya nne ya operesheni ya kusaka wasambazaji wa kinywaji hicho ambacho Serikali imepiga marufuku kutumika.
 Msimamizi wa ghala la Love kira  Enterprises lililopo Wazo Bi. Sia Mboya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwanasheria toka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Bw. Manchare Heche (katikati) wakati wa operesheni ya kuondoa pombe hiyo katika soko, kulia ni Afisa Afya toka Manispaa ya Kinondoni Bw. John Kijumbe.

  Gari lililokutwa limebeba pombe kali aina ya kiroba original likiwa limeegeshwa nje ya duka kuuza vinywaji la Love Kira lililopo Wazo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

RAIS MAGUFULI AZINDUA UWANJA WA NDEGEVITA WA KAMBI YA NGERENGERE, MOROGORO

$
0
0
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt wakifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017

 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akihutubia wakati wa  uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli akijiandaa kufyatua risasi ya bastola kuashiria matumizi rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017
 Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt John Pombe Magufuli na Balozi wa China nchini Dkt katika picha ya pamoja na viiongozi mbalimbali baada ya uzinduzi  rasmi ya Uwanja wa kisasa wa ndegevita wa  Ngerengere mkoani Morogoro leo Machi 6, 2017.

PICHA NA IKULU

KUTOKA VOA SWAHILI: Zulia Jekundu S1 Ep 113: Ariana Grande, Remy Ma na Nicki Minaj, The Weeknd na Drake

$
0
0
Zulia Jekundu ni kipindi cha televisheni cha kila wiki kinachotayarishwa na kutangazwa na Mkamiti Kibayasi toka Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya America (VOA).

Kipindi hiki hukuletea habari mbalimbali za burudani zinazotamba. Humu utapata kujua juu ya habari za mastaa zinazogonga vichwa vya habari, kujua baadhi ya wanaosherehekea siku zao za kuzaliwa wiki husika na hata filamu 5 zilizoongoza kwa mauzo katika wiki hiyo

Juma hili, video mpya ya Ariana Grande, mzozo mkali kati ya Nicki Minaj na Remy Na unavyoendelea, matatizo ya iPhone 7plus, The Weekend alipokutana na Drake Ujerumani, Obamas ndani ya New York, kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake duniani na kadhalika

KATIBU TAWALA IRINGA JOSEPH CHITINKA CHEZENI MPIRA ACHENI KUKAA VIJIWENI

$
0
0
Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwasalimia wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup. Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
 Katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka akiwa katika picha ya pamoja na  wachezaji wa timu ya kijiji cha Mangalali kabla ya mchezo kati yao dhidi ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) uliochezwa katika uwanja wa kalenga kwenye mashindano ya Mbuzi Cup.
Na Fredy Mgunda,Iringa.

MASHINDANO ya kombe Mbuzi Cup yatafikia tamati tarehe 30 mwezi wa tatu kwa kuzikutanisha timu za Mkwawa Rangers na Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na fainal hiyo itachezwa katika kijiji cha Kalenga kata ya Kalenga wilayani Iringa mkoani Iringa ikiwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji kata hiyo.

Akishudia mchezo wa nusu fainal kati ya timu ya Waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IMFC) na timu ya kijiji cha Mangalali uliochezwa katika uwanja wa kalenga katibu tawala wilaya ya Iringa Joseph Chitinka ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,

"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Chitinka

Aidha Chitinka aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.

 “Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu mbalimbali na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema Chitinka
  
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Obeid Msigwa aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya bora ambayo itakuwa ikiwakilisha katika mashindano ya mbalimbali.

“Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Msigwa

Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo kamanda wa vijana wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya Iringa Jackson Kiswaga alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya Iringa.

“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema Kiswaga.

Mashindano ya Mbuzi Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.

WANAUME WAASWA KUACHA TABIA YA KUWANYANYASA WANAWAKE NA KUWAACHIA MAJUKUMU YA KUZIHUDUMIA FAMILIA ZAO.

$
0
0

Na Rhoda Ezekiel Kigoma,

KATIKA kuelekea siku ya Wanawake Duniani, Baafha ya Wanawake Mkoani Kigoma Wamewaomba Wanaume Mkoani humo kuacha tabia ya kuwanyanyasa wanawake kwa kuwaachia majukumu ya kuzihudumia familia zao, hali inayosababisha Watoto wengi kukosa elimu na wanawake kushindwa kufikia Malengo yao ya kujikomboa na umasikini.

Akizungumza na Globu ya Jamii ofisini kwake jana, katibu wa umoja wa Wanawake Mkoani Kigoma , Salome Luhinguranya alisema kumekuwa na tabia ya Wanaume wengi kukimbia familia zao na kuwaachia mzigo wa malezi na kusomesha watoto wanawake wao hali inayo wapelekea wanawake wengi kishindwa kufanikiwa katika biashara zao kuyokana na Mzigo mkubwa unao Walemea.

Luhinguranya alisema Watoto wengi wamekuwa wakikosa elimu Mkoani humo kutokana na matatizo ya Wanajme wengi kuwatelekeza wake zao na familia zao na kwenda kuoa wake wengine hali inayo wapelekea Wanawake kushindwa kuhudumia familia zao kutokana na ufinyo wa mitaji waliyo nayo.

"Kauli mbiu ya Mwaka huu katika maadhimisho ni Tanzania ya Viwanda wanawake ni msingi wa mabadiliko Kiuchumi,kuelekea. Mkoa wa kigoma wanawake wengi wanajishughulisha katika Shughuli mbali mbali na Wengine ni wafanya kazi ,
 
UWT Mkoa imewahamasisha kuingia kwenye ujasiliamali huo na wanaume wengi wamekuwa Wakiwarudisha Nyuma kutokana na mizigo wanayo waachia , niwaombe wanaume kuepukana na fikra mgando ya kuwanyanyasa wanawake pindi wanapo jishughulisha kwa kuwaachia kulea familia ,
 
Baba ni kichwa katika familia wanatakiwa kutafuta fedha na kuwasaidia wanawake kulea familia zao ilikuwasaidia watoto kupata elimu na malezi bora", alisema Katibu wa Umoja wa Wanawake Mkoa wa kigoma.

Mipango ya umoja wa UWT ni kuwashauri wanawake na kufanya makongamano ya kuelimishana jinsi ya kufanya biashara na kuunda vikundi vya kununua hisa na kupata mikopo ambayo haina riba ilikuweza kuepukana na umasikini na suala hili limefanikiwa kwa mkoa wa Kigoma zaidi ya Wanaume wengi ndio wamekuwa wakiwarudisha nyuma katika sula la kuinuka kiuchumi.


Kwa upande wake Sadda Msomali ni mfanya biashara wa Samaki soko la Buzebazeba Mkoani humo ni mama wa Watoto saba alisema kwaupande baada ya kuanza biashara hiyo Mume wake alimuacha na watoto wake kwa madai kiwa dini yake hairuhusu mwanamke kufanya biashara, mwanamke ni mtu anaetakiwa kukaa ndani na kulea watoto.

Alisema baada ya kuona Maisha yamekuwa magumu katika familia yake alimuomba Mumewake aweze kufanya biashara ilikulea watoto wake, mume wake alimwambia endapo ataanza biashara hiyo atatakiwa kumpa taraka na amrudishe nyumbani kwao ndipo alipo muacha na watoto wake saba ambao watano anatakiwa kulipa ada zao na kutafuta Chakula chao hali ambayo inafanya maisha kuwa magumu kwake.

Kwa upande wake Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa kigoma , Zilpa Kisonzela alisema katika Mkoa Wakihoma kuna jitahada nyingi za kujikwamua na uchumi, wanawake wengi wamekuwa wakitumia fursa hizo katika kuzalisha Sabuni za Magadi , kutengeneza unga wa muhogo na kununua mazao ya ziwa Tqnganyika na kuyaongezea uthamani na kupeleka kuuza katika Nchi jirani za burundi na Congo Drc.

Alisema dhumuni hilo limefanikiwa na wafanya biashara wakubwa Wa vitenge na biashara mbalimbali Mkoani humo ni wanawake , kumekuwa na changamoto kubwa kwa Wanaume kuwarudisha nyuma kwa kuwatelekezea familia kutokana na mfumo wa malezi uliopo katika mkoa huo ambao umemuandaa mwanaume kuishi kama mfalme na Wanawake kuwa watafutaji hali inayo pelekea kushindwa kufikia malengo yao.

Aidha Kisonzela aliwataka wanaomu kushirikikana na Wanawake zao katika kulea familia na kujenga uchumi wa familia zao ilikuweza kuepukana na umasikini, endapo mwanaume atatafuta na mwanamke atatafuta itasaidia kujenga uchumi wa familia na kuepukana na malalamiko ya utegemezi


 

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE MACHI 7,2017

WAZIRI MAHIGA AHUDHURIA MAOMBI YA TAIFA YALIYOENDESHWA NA BILL WINSTON LEO JIJINI DAR.

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii 

MAOMBI kwa ajili ya Taifa yamefanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa naWaziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki,Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston kutoka nchini Marekani.

Mkutano huo uliokuwa na lengo la kuliombea taifa uliweza kuhudhuriwa na viongozi wa dini na serikali na Bishop kutoka nchini Zambia Bernard Nwaka aliendesha maombi hayo. 

Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili aliweza pia kuchangia mada juu ya kuliombea taifa na namna wananchi wanavyotakiwa kuishi ndani ya nchi yao.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga akzungumza katika mkutano wa maombi ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuendeshwa na Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston. 
Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania National Prayer uliofanyika leo Jijini.
Aliyewahi kuwa Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa maombi kwa taifa ujulikanao kama Tanzania Natipnal Prayer uliofanyika leo Jijini.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kingdom Leadeship Network Tanzania (KLNT), Dk. Charles Sokile akijadiliana jambo na Mratibu wa Kamati ya Maandalizi, Carol Mbaga 
Bishop Bernard Nwaka kutoka Zambia akiongoza maombi kwa ajili ya taifa yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustino Mahiga,Mchungaji maarufu na mfanya biashara na mwanzilishi wa Huduma ya Bill Winston, Bill Winston na Aliyewahi kuwa makamu wa raisi wa benki ya Dunia kanda ya Afrika Dr Oby Ezekwesili.
Mkutano ukiwa unaendelea.Picha zote na Zainab Nyamka.

WANAWAKE WAZIDI KUMIMINIKA KUFUNGUA AKAUNTI YA MALKIA CRDB

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura amesema kuwa mpaka kufikia Machi 06 zaidi ya akaunti 100 za Malkia zimefunguliwa na zaidi wanawake wengi bado wanaendelea kujitokeza kwa wingi.

Mary amesema kuwa kuelekea katika kilele cha Wanawake Duniani bado wanaendelea kuhamasisha wanawake wajitokeze kufungua akaunti hizo kwani zina manufaa kwao na zinawapatia faida baada ya mwaka mmoja.

Akaunti ya Malkia inamuwezesha mwanamke kuweza kupata mtaji au faida ya kujiendeleza kiuchumi baada ya kuifungua na kuweka fedha kwa kipindi cha mwaka mzima bila kutoa.
Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimkabidhi fomu ya klufungulia akaunti moja ya kina mama waliojitokeza kufungua akaunti hiyo kuelekea kilele cha maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani Machi 08.
 Muhamasishaji wa akaunti ya Malkia katika wiki ya wanwake Duniani kutoka benki ya CRDB tawi la Water Front Mary Gekura akimuelekeza namna ya kujaza fomu  ya kufungua akaunti ya wanawake ijulikanayo kama Malkia.
Wafanyakazi wa CRDB tawi la Water Front wakiwa katika picha za pamoja.

MKUTANO WA JUMUIYA YA NCHI ZINAZOPAKANA NA BAHARI YA HINDI(IORA) NCHINI INDONESIA

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) kabla ya kuanza kwa mkutano huo uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,Rais Dk.Shein anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli
Rais wa Indonesia Joko Widodo,ambae ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) akisalimiana na Rais wa Msumbiji Philipe Nyusi wakati wa mkutano IORA uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia ambao ulihudhuriwa na Viongozi wakuu wa Nchi mbali mbali 
Viongozi Wakuu wa Nchi mbali mbali wakiwa nkatika Picha ya pamoja wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Nchi zinazopakana na Bahari ya Hindi (INDIAN ASSOCIATION-IORA) uliofanyika leo katika ukumbi wa Balai Sindang Mjini Jakarta Indonesia,ambapo Rais Dk.Shein (wa tatu kulia)anamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli katika mkutano huo,[Picha na Ikulu.]

MAADHIMISHO YA GIRL GUIDES TEMEKE YA KUMUENZI MWASISI WA TGGA DUNIANI

$
0
0
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania (TGGA) ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho Duniami, Roden Barden Powell yaliyofanyika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TGGA Tanzania, Profesa Martha Qorro na Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi . PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi akiwasalimia wanafunzi ambao ni wanachama a TGGA Temeke
Wanafunzi wanachama wa TGGA Temeke wakiandamana wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Tandika wilayani Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa TGGA wakipiga makofi wakati wa kuyapokea matembezi ya wanachama wa TGGA
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA
Kaimu Ofisa Tarafa Chang'ombe, Hezron Mweladzi (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza jambo wakati wa Madhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho. Roden Barden Powell... Kulia ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi na Mwenyekiti wa Chama hicho,Martha Qorro
Wanafunzi hao wakiimba nyimbo wakati wa maadhimisho hayo
Wanafunzi wakiwa katika igizo la mchezo wa kuelimisha na kukataa kurubuniwa na wanaume. wa katikati ni Eunice Joseph, kushoto ni Hajra Mhamedy na kulia ni Seiph Kingwande ,
Wanafunzi wakiwa katika igizo, kushoto ni Eunice Joseph kama mwanafunzi, kulia aliyekaachini ni ni kama Daktari aliyekuwa akimpima mwanafunzi aliyekuwa na ujauzito Husna Mussa na wakatikati ni Farider Mohammed kama mzazi wa mwanafunzi 
Kamishna wa TGGA Temeke, Komba akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo
Profesa Qorro akihutubia wakati wa maadhimisho hayo
Profesa Qorro akiwaelekeza jambo wanafunzi
Profesa Qorro akiagana na wanafunzi baada ya maadhimisho hayo kumalizika

MAKONDA MGENI RASMI SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani yanayotarajiwa kufanyika Machi 8 Mwaka huu, katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam jana maadhimisho hayo yataongozwa na maandamano ya Wanawake na wadau mbalimbali, na yataanzia katika Shule ya Msingi Mabatini kuelekea viwanja vya Mwembeyanga.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.

Kauli mbiu hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.

Taarifa hiyo pia imeikumbusha jamii kuhusu wajibu wake ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Maadhimisho hayo yataambatana na maonesho ya kazi za ujasiriamali yanayoendelea katika uwanja wa Mwembeyanga, ambapo Asasi za kiraia na vikundi mbalimbali vya wanawake vitaonesha bidhaa zao.

Aidha, Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wanakumbushwa kushiriki kwa wingi katika maadhimisho hayo ikiwa ni pamoja na kuwa na mikakati ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinanazowakabili Wanawake kuanzia ngazi ya kaya hadi Taifa.

WAZIRI MBARAWA AWATAKA TEMESA KUONGEZA UJUZI UTENGENEZAJI WA VIVUKO.

$
0
0
Kivuko cha MV. Kazi kikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake.Kiuvko hicho kitakamilika na kuanza tarehe 15 mwezi huu na kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport inayojenga Kiuvko cha MV. Kazi, Bw. Major Songoro, akitoa ufafanuzi wa mashine kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alipokagua Kivuko hicho jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia), akiangalia moja ya vifaa vilivyoko kwenye chumba cha kuendeshea kivuko katika kivuko cha MV. Kazi kinachojengwa jijini Dar es Salaam. Kivuko hicho kitakabidhiwa tarehe 15 Mwezi huu. Wa pili kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Dkt. Musa Mgwatu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kulia),  akifafanua jambo kwa Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi ambacho kinatengenezwa jijini Dar es salaam na Kampuni ya Songoro Marine Transport.
Mafundi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, wakiendelea na kazi ya kufunga mashine katika Kivuko cha MV Kazi. Kivuko hicho kitakamilika na kukabidhiwa wiki ijayo na kina uwezo wakubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.
…………………………………………………………………………….

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameutaka uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA) kushiriki kikamilifu shughuli za matengenezo ya vivuko ili kupata ujuzi wa ufungaji wa mifumo kutoka Kampuni zinazotengeneza vivuko vya Serikali.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha MV Kazi, Bandarini jijini Dar es Salaam, Waziri Prof. Mbarawa amesema kuwa kupitia mafunzo hayo Serikali itaweza  kuokoa fedha nyingi ambazo kwa sasa inatumia kulipa kampuni binafsi zinazojenga na kukarabati vivuko

“Hakikisheni mnapata ujuzi kama walionao hawa, hatutaki kutumia fedha za Serikali kwa ajili ya kukarabati au kutengeneza vivuko wakati nyinyi TEMESA mpo”, amesema Waziri Prof. Mbarawa

Pamoja na ujenzi wa kivuko hicho Waziri Mbarawa amewataka Temesa kuhakikisha wanasimamia na kukitunza kivuko hicho ili kiweze kudumu kwa muda mrefu.

Aidha, Profesa Mbarawa ameuagiza Wakala huo kuhakikisha wanakamilisha mifumo ya ukusanyaji mapato kwa njia ya kielektroniki ili ili kudhibiti mianya ya rushwa.

Kuhusu huduma za kivuko mkoani Lindi Serikali imesema itahakikisha inapelekea huduma haraka iwezekanavyo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mkoa huo.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Dkt. Musa Mgwatu, amemtaka mkandarasi wa kampuni ya Songoro Marine Transport kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kivuko hicho kwa muda uliopangwa.

Dkt. Mgwatu amefafanua kuwa kukamilika kwa kivuko hicho kutarahisisha usafiri kwa wakazi wa Kigamboni na maeneo mengine ya jiji la Dar es salaam ambao wamekuwa wakitumia huduma hiyo katka shughuli zao za kila siku.

Nae, Meneja Mradi wa Kampuni ya Songoro Marine Transport, Bw. Major Songoro amemhakikishia Waziri Mbarawa kumaliza kivuko hicho kwa wakati ambapo amesema ifikapo tarehe 15 mwezi huu kivuko hicho kitakabidhiwa kwa Serikali.

Bw. Songoro amefafanua kuwa kwa sasa mafundi wanamalizia kazi ndogo ndogo zilizobaki pamoja na kusubiri injini ambazo zinatarajiwa kuwasili mwishoni mwa wiki hii.

Kivuko kipya cha MV Kazi kimegharimu kiasi cha shilingi bilioni Saba na kina uwezo wa kubeba abiria 800 na magari 22 kwa wakati mmoja.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Serikali Yaahidi kushirikiana na vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya Viwanda

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Serikali imeahidi kuendelea kutengeneza mazingira rafiki kwa kushirikiana na vyombo vya habari ili kwa pamoja kuweza kuhamasisha, kuunda na kujenga nchi ya viwanda katika kuunga mkono azma ya Rais Mhe. John Pombe Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Mchezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokutana na wamiliki na watendaji waandamizi wa vyombo vya habari leo Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa mkutano huo Mhe. Nnauye amesema kuwa serikali na vyombo vya habari wakishirikiana na kuwa na lengo moja wataweza kuileta Tanzania pamoja na kuiweka katika mwelekeo ulio sahihi. 

“Tukiamua leo kila chombo cha habari kikawa na dawati maalumu linalozungumzia Tanzania ya viwanda kama ilivyo kwa madawati mengine ndani ya vyombo vyetu vya habari, na serikali ikaendelea kutoa hamasa za uanzilishwaji wa viwanda ambavyo vitasukumwa na dawati hilo maalumu la viwanda, tutaweza kutimiza ndoto yetu ya Tanzania ya Viwanda” amesema Mhe. Nnauye

Akizungumza wakati wa mkutano huo Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi amesema kuwa ili vyombo vya habari viweze kutangaza habari vinahitaji kupata ushirikiano wa kutosha kutoka serikalini kuonyesha mikakati na malengo ya serikali kuwezesha vyombo vya habari kujenga Tanzania ya viwanda na kuwapa fursa wananchi kupata taarifa sahihi za nchi. 

Naye Mtendaji kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Bibi. Mabe Masasi amesema kuwa Mapinduzi ya viwanda yanaweza kufanyika kama vyombo vya habari vitatoa taarifa sahihi za upatikanaji wa malighafi za uwekezaji kulingana na mahitaji yaliyopo katika maeneo husika na kuwekeza katika viwanda vidogovidogo vitakavyozalisha viwanda vikubwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassani Abbas amesema kuwa atahakikisha maafisa habari wa serikali hususani maafisa wanaohusika na Sekta ya viwanda wanatoa ushirikiano wa kutosha kwa vyombo vya habari ili kuweza kuelimisha umma namna Tanzania ya Viwanda inavyojengwa.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akiongea na wamiliki wa vyombo vya Habari (hawapo katika picha) wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam. katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na kushoto ni  Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi.

 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas akitoa ufafanuzi kwa wamiliki wa vyombo vya habari namna uratibu wa matangazo utakavyokuwa ukiendeshwa  na Serikali wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze leo Jijini Dar es Salaam. 
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya Serikali (TSN) Dkt. Jimy Yonazi akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa vyombo vya Habari  nchini kujadili nafasi ya vyombo vya habari katika kujenga Tanzania ya viwanda. Wanaomsikiliza kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na . Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dkt. Hassani Abbas 
 Mkurugenzi wa Vipindi kutoka Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akichangia wakati wa mkutano uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo vya Habari ikiwa ni muenedelezo wa vipindi vya Wadau Tuzungumze kinachoratibiwa  na Wizara wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo lengo likiwa ni kuimarisha ushirikaiano baina ya Wizara na wadau wa sekta zake.
 Mdau wa Habari Bw. Hamza Kasongo akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Wadau Tuzungumze uliowakutanisha wamiliki wa Vyombo 
Baadhi ya Wadau waliohudhuria mkutano wa Wadau Tuzungumze kuhusu namna vyombo vya habari vinavyoshiriki katika kufanikisha azma ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda leo Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA MICHUZI JR.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa habari mara baada ya kumaliza mkutano wa Wadau Tuzungumze ambapo uliwakutanisha wamiliki wa vyombo vya habari huku mada kuu ikiwa ni nafasi ya vyombo vya habari katika kuijenga Tanzania ya Viwanda leo Jijini Dar es Salaam.

 Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel
Bw. Francis Nanayi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Mwananchi
 Mwakilishi wa ITV/Radio One Steven Chua
 Mdau Mkubwa wa vyombo vya habari,Theophil Makunga

Maandalizi Ya TANZANIA DAY 2017 Dallas Texas

$
0
0


Aprili 29, 2016, Mstahiki Meya wa jiji la Dallas, jimbo la Texas aliitangaza rasmi siku hiyo kuwa SIKU YA TANZANIA.

Na mwaka huu, Jumuiya ya waTanzania waishio jimboni humo kwa kushirikiana na Baraza la waTanzania waishio nchini Marekani (Diaspora Council of Tanzanians in America) wanaandaa maadhimisho makubwa ya siku hiyo yatakayofanyika katika jiji la Dallas.

Viongozi Ben Kazora wa Jumuiya ya Dallas na Charles Bishota wa DICOTA wamezungumza na Mubelwa Bandio kuhusu maandalizi ya siku hiyo
KARIBU USIKILIZE

NMB yamwahidi Rais Magufuli kuendelea kutumia mfumo wa kieletroniki

$
0
0
Benki ya NMB imemwakikishia Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuwa itaendelea kutumia mifumo ya kiteknolojia ili kuwawezesha wateja wa benki hiyo kutumia Zaidi mifumo ya kietroniki kuliko unaotumika Zaidi kwa sasa wa malipo kwa kutumia pesa taslim.

Hayo ya mesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Kibiashara cha Mtwara na kueleza kuwa nia ya benki ni kuendelea kukua Zaidi huku ikitoa suluhu ya vipau mbele vya serikali na kujikita katika ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa njia zakielektroniki.

“Kwa kutumia teknolijia mbalimbali, NMB tumewekeza Zaidi kwenye kutatua changamoto mbalimbali za wateja wetu na hivyo kutoa fursa za kutumia Zaidi njia za benki kuliko kutumia njia za malipo kwa kutumia pesa taslim,” alisema Ineke.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NMB, Prof. Joseph Semboja alisema kuwa NMB imefanya maboresho makubwa na hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kutoa huduma za kifedha kwa kila kada ya watanzania na serikali kwa ujumla.

Prof. Semboja alisema kuwaSerikali kwa sasa inamiliki hisa asilimia 32 ndani ya benki ya NMB zenye thamani ya Zaidi ya Bilioni 430 hivyo kuiwezesha serikali kupata gawio la Zaidi ya bilioni 75 ndani ya miaka mitano.

“Kwa mwaka huu mheshimiwa raisi, kama mkutano mkuu wa wanahisa utakaokaa mwezi wa sita mwaka huu, utabariki Kiwango cha gawio, serikali itapata gawio la shilingi Bilioni 16.5 zinazotokana na faida iliyopatikana mwaka 2016,” alisema Prof. Semboja.

Nae Rais Magufuli aliwapongeza NMB kwa huduma wanazotoa na kutoa wito kwa viongozi wa serikali na wakuu wa wilaya na viongozi waliopo ndani ya serikali kufanya biashara na NMB kwani serikali ina hisa kwenye benki hiyo na hupata faida kutoka NMB.

“Nikuombe Waziri, toa maelekezo kwa sababu wewe ndo unasimamia pesa, pesa ya serikali ipitie NMB ili nipate gawio kubwa zaidi, wale wengine wanaofanya biashara bila kuifaidisha serikali na kugawana gawio wao kwa wao huku serikali haipati faida yoyote, hatutafanya biashara nao,” alisemaRaisiMagufuli.

Rais Magufuli pia aliiomba NMB kushiriki katika kuunga mkono ajenda ya serikali katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.

Rais Magufuli alisema kuwa,“Naomba NMB mshiriki katika kukopesha viwanda hasa viwanda vidogovidogo na hivyo kuunga Mkono juhudi za serikali katika kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.”
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Ineke Bussemaker mara baada kukifungua rasmi kituo cha Biashara cha NMB mjini Mtwara kijulikanac ho kama Mtwara Business Centre. Pamoja na mambo mengine, rais magufuli alimuagiza Waziri wa fedha Dr Philip Mpango kuhakikisha kuwa fedha zote za serikali zinapita NMB.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkurgenzi wa NMB – Ineke Bussemaker wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa kituo cha kibiashara cha NMB – NMB Business Centre mjini Mtwara juzi. Kutoka kulia niAfisa Mkuu wa wateja wadogo na wa kati – Abdulmajid Nsekela, Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi – Prof Joseph Semboja na kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara – Halima Dendegu na Waziri wa Fedha na Uchumi – Dr Philip Mpango.

WAZIRI MWIGULU AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI KUJADILI MASUALA YA USALAMA NA MAENDELEO KWA MASHIRIKA NA VIKUNDI VYA KIJAAMII

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisalimia na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijamii katika masuala ya usalama wa raia na haki zao.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser akisaini kitabu cha wageni alipofika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi alipomtembelea waziri wa wizara hiyo (anayesoma kadi) kwaajili ya kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijamii katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jamal Jafari.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akisisitiza jambo wakati alipokua akiongea na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijaa katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Kaimu Balozi huyo aliambatana na Jamal Jafari ambaye ni aliambatana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba akimsikiliza Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Bi Virginia Blaser aliyefika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujadiliana namna wanayoweza kusaidia Mashirika na vikundi vya kijaa katika masuala ya usalama wa raia na haki zao. Kaimu Balozi huyo aliambatana na Mwakilishi wa Ubalozi wa Marekani nchini, Jamal Jafari.

MANISPAA YA UBUNGO YABAINISHA MPANGO WA KUKUZA UCHUMI NA KUPUNGUZA UMASIKINI ILI KUFIKIA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake. (Picha zote na Nassir Bakari)
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea Makadirio ya Mapato na Matumizi ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob akielezea jinsi Bajeti ya Manispaa hiyo ilivyopitishwa kwa kuungwa mkono kwa 100% kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kilichofanyika 4/03/2017.






Na Mathias Canal, Dar es salaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imebainisha namna ya kuboresha maisha ya wakazi wake kwa kuweka mpango mzuri wa muda wa kati wa mwaka 2017/2018 – 2019/2020 ambao unalenga kukuza uchumi, na kupunguza umaskini ili kufikia maendeleo endelevu ya kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa wananchi wake. 

Mpango huo umeandaliwa kwa kuzingatia sera na miongozo ya Kitaifa, kwa mujibu wa sheria ya bajeti Na. 11 ya mwaka 2015, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ambapo Mpango mkakati ni kutekelezwa kwa matokeo makubwa sasa (BRN), Sera ya Taifa ya UKIMWI, Sera za kisekta, Mipango Shirikishi Jamii ya Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O&OD) ya Kata na Mitaa. 

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuelezea juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya kawaida na ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka 2017/2018, Makadirio yalijadiliwa na Waheshimiwa Madiwani katika Kamati za Kudumu,na kuidhinishwa na baraza maalumu la madiwani jumamosi ya tarehe 04/03/2017 kwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. 

Mstahiki Meya alisema kuwa ili kutekeleza dhana nzima ya ung’atuaji wa madaraka, mpango huu umeshirikisha jamii katika mpango shirikishi ambao huanzia ngazi ya Mtaa ambapo Hali hiyo imezingatia vipaumbele na mahitaji halisi ya wananchi katika maeneo yao.

Alisema kuwa Mpango huo umejielekeza katika kutoa kipaumbele maeneo yanayoweza kutoa matokeo ya haraka (quick wins) ambayo yatasaidia ukuaji wa uchumi kwa haraka katika kipindi kifupi na kutoa huduma bora kwa wananchi wa Ubungo.

Aidha alieleza maeneo yaliyopewa kipaumbele katika mpango huo kuwa ni pamoja na Kuboresha na kuimarisha ukusanyaji wa Mapato ya Manispaa, Ujenzi wa ofisi za makao makuu ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Kuboresha miundombinu ya Afya, Shule za Msingi na Sekondari, Kuboresha miundombinu ya maji, mifereji, taa za barabarani barabara na Kilimo mjini, Kuboresha hifadhi ya mazingira na ukusanyaji wa taka, Kuimarisha ushirikishwaji wa jamii katika upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Kuboresha mazingira ya wafanyabiashara ndogo ndogo.

Katika harakati za kuyafikia mafanikio yaliyotajwa Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ameeleza kuwa Manispaa hiyo Uimarisha mahusiano mazuri kati ya Serikali, mashirika yasiyo ya Kiserikali na wadau wengine, Kuendelea kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma zilizo bora na haraka, Kuimarisha Utawala bora, Uwajibikaji na Uwazi sambamba na Kujenga uwezo wa viongozi wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa serikali za mitaa katika kusimamia shughuli za wananchi.

Sambamba na hayo pia amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mwaka 2016/2017 ilikadiria kutumia Sh. 116,045,935,228.99 ikiwa ni pamoja na fedha za mfuko wa barabara. 

Kuanzia Julai hadi Disemba, 2016, Halmashauri ilikuwa imekusanya Sh. 1,024,839,737.74 fedha za vyanzo vya ndani sawa na asilimia 8 ya maoteo ya Tsh 13,300,416,090.50 ya vyanzo vya ndani yaliyotarajiwa kukusanywa kwa nusu mwaka wa bajeti yaani Julai 2016 hadi Disemba 2016.

Katika kipindi hiki Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeweza kutumia kiasi cha Sh. 150,764,997.88. ya makusanyo yake ya ndani yaliyoanza kukusanywa mwezi Novemba 2016, na hakuna fedha yoyote ya ruzuku iliyopokelewa hadi sasa kama inavyooneshwa katika Jedwali hapa chini. 


Jacob ametaja changamoto mbalimbali zinazopelekea ucheleweshaji katika kutoa huduma na kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwa ni pamoja na Mwamko mdogo wa wananchi kuchangia shughuli za maendeleo, Fedha za miradi za Serikali kuu na wafadhili kutoletwa kwa wakati na hivyo kuathiri utekelezaji wa miradi kama ilivyopangwa. Miradi yote iliyopangwa kutekelezwa kwa fedha za ruzuku haijaanza, Makusanyo hafifu ya mapato ya ndani kutokana na mgawanyo wa Halmashauri na upya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Hivyo miradi iliyopangwa kutekelezwa kwa mapato ya ndani mingi haijaanza kutekelezwa, Ukosefu wa maeneo ya kujenga majengo mapya kama vile Shule za Msingi na Sekondari, pamoja na Madai makubwa ya fedha za fidia katika maeneo mbalimbali.

Hata hivyo Sababu zilizopelekea kukusanya mapato ya ndani chini ya malengo ni pamoja na Serikali kuhamishia kodi ya Majengo kukusanywa na Mamlaka ya mapato TRA ambapo kwa wigo wa makusanyo uliopo wa kodi ya majengo ni shilingi bilioni 6, kwa bajeti ya mwaka 2016/2017 ya makusanyo ya ndani yenye makadirio ya Tsh. 26.6 bilioni, Kushuka kwa mauzo ya wafanyabiashara hali inayopelekea biashara kufungwa na malipo ya ushuru wa huduma kupungua, na SUMATRA kubadilisha route za mabasi ya kariakoo (160) na mikoani (350) kimepunguza makusanyo katika kituo chetu cha Simu 2000 (Sinza bus terminal) ambapo takribani magari kati ya 510 yaliyokuwa yanaingia kituoni yamepungua na kusababisha upungufu wa Sh. 12,900,000/= kwa kila mwezi.

Sababu zingine ni Upungufu wa vitendea kazi baada ya Mgawanyo wa Halmashauri na hasa ukosefu wa magari yanayotumika kukusanyia mapato, Kipindi cha mpito tangu kuanzishwa kwa Halmashauri hadi kuanza kukusanya mapato ya ndani kwa Halmashauri yetu mpya ilipoanzishwa rasmi tarehe 1/07/ 2016, imeanza kukusanya mapato yake ya ndani yenyewe kuanzia mwezi Novemba 2016, Walipakodi kuendelea kulipia katika Halmashauri mama (Kinondoni) kwa kipindi cha Oktoba hadi Disemba 2016 kwa mazoea kiasi cha takriban Sh. milioni 500 kimekusanywa kimakosa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni mawasiliano yanafanyika ili kurejesha makusanyo hayo. 

Ili kukabiliana na changamoto hizo Mikakati ya Halmashauri imetajwa kuwa ni pamoja na Kuendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi ili kutambua kuwa miradi ya maendeleo wanayochangia ni kwa ajili ya manufaa yao wenyewe na vizazi vijavyo, Kendelea kupanua wigo wa ukusanyaji wa mapato kwa kubuni vyanzo vipya kwa mujibu wa sheria na kuimairisha ukusanyaji wa mapato katika vyanzo vilivyopo. 

Mikakati mingine ni Kukusanya mapato yote kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, na Kununua maeneo ya pembezoni mwa mji na kuhakikisha tunalipa fidia kabla ya kuyatwaa maeneo ya watu.

Vipaumbele vitakuwa katika maeneo yafuatayo:-Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe Boniface Jacob amebainisha kuwa Bajeti hiyo imelenga katika kuboresha maisha ya wananchi na kukuza kipato cha mkazi ili kukuza uchumi wa ndani ambapo ametaja vipaumbele 13 ambavyo vitapaswa kufanyiwa kazi katika bajeti hiyo kuwa ni pamoja na Kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kutumia mfumo wa kielektroniki, na Kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa kununua madawa na vifaa tiba na kuboresha miundo mbinu ya afya kwa kupanua hospitali ya Sinza kwa kujenga ghorofa ya pili jengo la OPD, Ujenzi wa wodi ya wazazi kituo cha afya mbezi, ujenzi wa jengo la kuhifadhia chanjo Mabibo, kujenga zahanati ya King’azi Kwembe Jumla ya Tsh. 5,732,424,610.00 zimetengwa. 

Kuboresha miundombinu ya barabara kwa kujenga Madaraja/ Makalvati, barabara kwa kiwango cha lami, kufanya matengenezo ya kawaida ya barabara, muda maalum, maeneo korofi, njia za waenda kwa miguu, Ujenzi wa Mifereji katika barabara za Manispaa ambapo Jumla ya Tsh 6.2 bilion zimetengwa, Kuboresha miundo mbinu ya shule za Msingi na Sekondari kwa kununua madawati, kujenga madarasa, vyoo, nyumba za walimu, maabara na ukarabati wa miundombinu. Jumla ya Tsh.5.5 billion zimetengwa na Kutoa mikopo kwa wajasiliamali wa dogo kwa vikundi vya wanawake na vijana ili kuongeza ajira na kukuza kipato cha Mkazi. Jumla ya Tsh.1.9 billion  zimetengwa.

Kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kutoa huduma kwa kujenga Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo. Tsh.1.7 billion zimetengwa, Kununua magari na mitambo magari 6 ya ofisi, gari moja la maji machafu na gari 1 la maji safi, jenereta. Jumla ya Tsh 1.35 billion zimetengwa, Kulipa fidia kupisha ujenzi wa miradi mabali mbali ya maendeleo na kufanya uthamini wa mali za Manispaa. Jumla ya Tsh.1.2 billion zimetengwa, Kuboresha usafi wa mazingira na na ukusanyaji taka na kununua magari makubwa ya taka Jumla ya Tsh.1 billion zimetengwa, Kuboresha upatikana maji safi na salama kwa wakazi wa Ubungo kwa kujenga na kukarabati miundo mbinu ya maji. Jumla ya Tsh.550 million zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji na Mipango miji, kupima na kumilikisha maeneo ya umma na kutekeleza mfumo wa anuani za makazi (Postcode). Jumla ya Tsh.550 million zimetengwa.

Aidha Halmashauri ya Maninspaa ya ubungo imetenga Tsh 42 milioni kwa mwaka huu kwa ajili ya kijiji cha michezo kilichopo kibwegele ambapo kijiji hicho kitakuwa na kiwanja cha mpira wa miguu na viwanja vya michezo ya watoto, kwa Mwaka wa fedha 2017/2018 ambapo Tsh 50 milioni zimetengwa, na Kuboresha na kukarabati masoko Manispaa tumetenga Tsh 1.2 Bilioni, kwa ajili ya kuboresha masoko ambayo ni Mabibo, Shekilango, Sinza one, na Mbezi pia fedha hizo zitatumika kulipa fidia na kupima maeneo kwa ajili ya wamachinga na maeneo ya uwekezaji.

Jokate aanzisha mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi wa kike

$
0
0
Mrembo mwenye vipaji lukuki nchini, Jokate Mwegelo ameanzisha mpango maalum wa kufundisha somo la ujasiriamali kwa wanafunzi wa kidato cha pili wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai iliyopo Vingunguti katika Manispaa ya Ilala.

Jokate ataanza mafunzo hayo maalum kwa wanafunzi wa kike kuanzia wiki ijayo na lengo la mafunzo hayo ni kuwapa ufahamu wanafunzi hao na kuanzisha biashara zao mara baada ya kumaliza elimu yao ya sekondari.

Alisema kuwa mafunzo ya ujasiriamali kwa wanafunzi ni muhimu kwani yanawawezesha kujiandaa vizuri kukabiliana na maisha mara baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari na kushindwa kuendelea na masomo ya ngazi ya juu.
Kwa mujibu wa Jokate, unaweza kusoma mpaka Chuo Kikuu ndani na nje ya nchi, lakini bado utakabiliana na ugumu wa kupata ajira ambazo kwa sasa ni haba.

“Kuna wengine wamesomea taaluma fulani  kwa ngazi ya Chuo Kikuu lakini mpaka sasa hawana ajira na kukata tama katika maisha, pia unaweza kufanya kazi tofauti na taaluma uliyosomea, lakini kwa ujasiriamali ni tofauti, utajifunzi jinsi ya kupata mtaji, kukopa na kurejesha, kufanya biashara gani na mbinu zake,”

“Mfano halisi mimi mwenyewe, nimesomea mambo tofauti na kazi ninazozifanya ni tofauti, ni mbunifu wa mitindo, mavazi, muigizaji wa filamu, mwanamuziki na pia ni mfanyabiashara, haya yote sikusomea, ila najivunia kwani ndiyo yanaendesha maisha yangu, wanafunzi wana vipawa tofauti, naamini katika programu hii nitapata wengi na kupata mafanikio,” alisema Jokate.

Alisema kuwa atakuwa anafundisha mafunzo hayo mara moja kwa wiki kuanzia wiki ijayo. “Nimeamua kuanza rasmi siku ya wanawake duniani, maandalizi yamekamilika na nawaomba wanafunzi wajiandae kwani mafunzo ni mazuri na yatawajengea moyo wa kujiamini kwani si kila anayesoma anatakiwa kuajiliwa,” alisema.
Jokate Mwegelo akicheza muziki na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Majani ya Chai ya Ilala wakati wa mahafari ya mwaka jana.
Jokate Mwegelo akikabidhi zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Majani ya Chai wakati wa maafali ya mwaka jana ya kidato cha nne.

WAKULIMA WA VIAZI MVIRINGO MKOANI NJOMBE WAIOMBA SERIKALI KUWASIDIA KUPANDA SOKO

$
0
0
Mkoa wa njombe ni kati ya mikoa inayolima viazi mviringo kwa wingi hapa nchini Tanzania na ni mkoa unaosifika kwa kilimo cha viazi hivyo, Wakazi wa mkoa huo wanategemea zao hilo kwa kuwaongezea kipato.

MASAUNI ATEMBELEA KIWANJA CHA NDEGE CHA KIMATAIFA ABEID AMANI KARUME, AAGIZA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UINGIAJI DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Maafisa wa Idara ya Uhamiaji Zanzibar, wakati wa ziara ya kukagua udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani humo, huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana kudhibiti madawa hayo ambayo yanaharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, akitoa taarifa za utekelezaji wa zoezi la kudhibiti Dawa za Kulevya Visiwani humo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), wakati wa ziara ya naibu waziri kufuatilia utekelezaji wa zoezi la kudhibiti uingiaji wa dawa za kulevya Visiwani humo.
Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (wakwanza kushoto), juu ya hatua zinazochukuliwa na Idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama kukabiliana na udhibiti wa uingiaji wa Dawa za Kulevya kiwanjani hapo.Wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mohamed Ahmada Salum na anayefuatia ni Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar, Johari Masoud Sururu.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto), akisikiliza jinsi mifumo ya kudhibiti uingiaji haramu inavyofanya kazi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Uhamiaji anayesimamia Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume, Fulgenze Mutarasha.Ziara ya Naibu Waziri huyo ilikua na lengo la kukagua mifumo inayotumika kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akitoa maelezo kwa watumishi wa Idara ya uhamiaji waliopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya Visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, akiteta jambo na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Mohamed Ahmada Salum wakati wa ziara ya ukaguzi wa mifumo ya kudhibiti uingiaji wa Dawa za Kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Sheikh Abeid Amani Karume.


Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Viewing all 46379 articles
Browse latest View live




Latest Images