Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1152 | 1153 | (Page 1154) | 1155 | 1156 | .... | 1903 | newer

  0 0


  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataija wa Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni akikagua gwaride la heshima mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere,jijini Dar.

  Makamu wa Rais Mama Samia akimkaribisha Rais wa Uganda,Yoweri Museveni mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege mapema leo kwa ziara ya siku mbili,anaeshuhudia pichani kati ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni wakiwa wamesimama wakati wa nyimbo za Taifa zikipigwa.

  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Masharika,Dkt Augustine Mahiga kwa pamoja wakiwa tayari kumpokea mgeni wao,Rais wa Uganda Yoweri Museveni
  Baadhi ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika uwanja wa Ndege kumlaki Rais wa Uganda,Yoweri Museveni

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake Rais wa Uganda,Yoweri Kaguta Museveni wakifurahia vikundi vya ngoma za asili vilivyokuwa vikiburudisha mara baada ya Rais huyo kuwasili.

  0 0

  Mkurugenzi Mtendaji wa Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Agness Kijazi akizungumza leo kwenye warsha ya wanahabari kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017. Kushoto Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.
  Mkurugenzi wa TMA, Dk. Agnes Kijazi akiongea pambeni ni sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa warsha kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017 iliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
  Sehemu ya wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiwa warsha kuhusu mwelekeo wa msimu wa mvua za masika kwa kipindi cha mwezi Machi hadi Mei 2017 iliyofanyika Kibaha, mkoani Pwani.
  Mkurugenzi wa TMA, Agnes Kijazi (katikati) waliokaa kwenye viti akiwa katika picha ya pamoja na wanahabari katika Warsha hiyo. Pembeni yake  Kushoto ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa na Meneja Kituo Kikuu cha Utabiri Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Samwel Mbuya (kulia).

  0 0  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaomba viongozi wa Dini kuendelea kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kufanya hivyo kunaipunguzia serikali mzigo.

  RC Makonda ameyasema hayo alipokuwa anafungua semina kwa Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) na kusisitiza kuwa viongozi wa dini wakiwafundisha mema waumini ambao ndiyo wananchi, Taifa halitakuwa na wahalifu au matukio ya wizi, ujambazi, utumiaji wa dawa za kulevya na ufanyaji wa biashara hiyo, jambo ambalo litaipunguzia gharama serikali ya kuwahudumia waathirika kwa kuwapa vidonge vya Methadone, na serikali haitatumia nguvu kubwa kujenga magereza kwa ajili ya wanaokiuka sheria na taratibu za nchi.

  Na kusisitiza kuwa serikali itaendelea kuwaunga mkono viongozi wa dini kwani wanamchango mkubwa kwenye maendeleo ya Taifa hili.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa JUWAQUTA ambaye pia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum amesema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwaelimisha walimu hao juu ya kuunga mkono kauli mbiu ya HAPA KAZI TU ya serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwani kufanya kazi ni agizo kwa mujibu wa dini hiyo ya kiislamu ambapo waumini wake wameambiwa wafanya kazi za halali ili wapate ridhiki halali na siyo vinginevyo.

  Huku akifafanua kuwa hata manabii walikuwa wakifanya kazi hivyo ni vyema kama viongozi kufuata nyayo hizio na kuwaamrisha wengine kufuata utaratibu huo.
  .Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
  Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum akizungumza katika unafunguzi semina ya Walimu wanaosomesha Qur-an Tanzania (JUWAQUTA) leo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiombewa dua na viongozi dini, leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Glob ya Jamii. 

  Picha ya Pamoja

  0 0

   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akitangaza mkusanyiko huo kuwa mahafali ya 20 ya Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) kulia ni Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Bw. Augustino Nongwe wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
   Baadhi ya wahitimu wakiwa katika mahafali hayo
   Mhitimu katika Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) Elias Eliakim akisoma risala kwa Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi ambapo mbali na mambo mengine aliomba viongozi wa Serikali kuweka utaratibu wa kutembelea vyuo vya kati vya uandishi wa habari ili kujenga hamasa kwa wanafunzi.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiongea na wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) ambapo alisisitiza umuhimu wa wanatasnia ya habari kuwa watendaji na sio waongeaji bila vitendo ikiwa ni moja ya mkakati wa kuikuza tasnia hii na kuendana na Sheria mpya ya Huduma za Habari wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
   Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwapa vyeti vya uhitimu wa Diploma na cheti katika uandishi wa habari waliokuwa wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) 
  Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha ya pamoja wahitimu,wafanyakazi wa Chuo cha Uandishi wa Habari Morogoro (MSJ) wakati wa mahafali ya 20 ya chuo leo Mjini Morogoro.
  PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO.


  0 0

  Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akimtunuku Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), Fadhil Innocent baada ya kuhitimu katika mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) yaliyofanyika leo katika Viwanja vya Chuo hicho, Kawe jijini Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu. Kificho alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.
   Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho (katikati), akiwa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu (kushoto) na Mwenyekiti wa Baraza la chuo hicho, Jaji mstaafu Steven Bwana baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
  Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), katika chuo hicho, Fadhil Innocent (wa kwanza kushoto), akiwa na wahitimu wa wengine katika mahafali hayo.


  Maandamano yakifanyika kuelekea eneo yalipifanyika 
  mahafali hayo.
  Maandamano yakiendelea.
  Wahitimu ndani ya majoho.
  Wageni waalikwa wakiwa kwenye mahafali hayo.
  Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
  Wimbo wa taifa ukiimbwa wageni waalikwa wakiwa wamesimama kwa heshima ya wimbo huo.
  Mgeni rasmi Mheshimiwa Kificho (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wengine. Kutoka kulia ni Mkuu wa Chuo cha Sayansi, Dk.Abdillah Chande, Dean Chuo cha Elimu, Dk.Mary Mosha, Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Dk. Costa Mahalu, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Dk.William Kudoja na Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Jaji mstaafu, Steven Bwana.
  Wahitimu wa shahada ya kwanza katika ngazi mbalimbali wakiwa kwenye mahafali hayo.
  Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk.Costa Mahalu akihutubia.
  Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Mheshimiwa Pandu Ameir Kificho, akisoma hutuba yake.
  Ndugu na jamaa za wahitimu hao wakiwa kwenye mahafali hayo.
  Wageni waalikwa ndani ya mahafali hayo.
  Mwonekano katika mahafali hayo.
  Mtoto wa Mwanahabari Happyness Katabazi, Queen Japhet  Mwaijande, akimpongeza mama yake kwa kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria katika mahafali hayo.
  Mtihimu wa kwanza wa Falsafa ya Udaktari (PhD), katika chuo hicho, Fadhil Innocent akiwa katika picha ya pampja na ndugu zake.


  Na Dotto Mwaibale

  CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimefanikiwa kutoa   falsafa ya kwanza ya  Udaktari (PHD), licha ya  changamoto ya utoaji elimu katika majengo ya kupanga kwa gharama kubwa.

  Kauli hiyo imetolewa na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Dk. Costa Mahalu kwenye mahafali ya nne yaliyofanyika leo katika viwanja vya chuo hicho, Kawe jijini Dar es  Salaam.

  Alisema  katika mahafali hayo jumla ya wahitimu 499  wamefanikiwa kumaliza masomo yao kwenye fani mbalimbali, wanafunzi 45 ngazi ya cheti na Stashahada 47.

  Wengine waliohitimu  shahada 334,Shahada ya udhamiri 71 na shahada ya udamivu ni mmoja licha  ya uongozi wa chuo hicho kukutana changamoto  nyingi ndani ya miaka mitano lakini wanamshukuru mungu kwa hatua hiyo.

  “Namshukuru mungu kwa kutupatia kibali cha  kufikia hatua hii ya kufanya mahafali, lakini bado tumekuwa na changamoto ya majengo kwa bado tupo kwenye  majengo ya kupanga,” alisema.

  Alisema iwapo serikali itabariki kama ambavyo vibali tayari vimetolewa, hivyo watakuwa na uhakika wa mahafali ya mwakani yatafanyika  kwenye majengo ya chuo  yanayojengwa Kiromo  wilayani Bagamoyo.

  Aliongeza kuwa chuo kimekuwa na malengo  ya kuwasomesha wahitimu wa chuo  kwa kuwapeleka vyuo vingine katika shahada ya uzamivu ili kupunguza tatizo la wahadhiri ambalo vyuo vingi nchini wanakabiliana nalo.

  Spika Mstaafu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Amier Kificho aliupongeza uongozi wa chuo hicho kwa jitihada zao za kuendeleza  chuo hicho katika mazingira magumu.

  Alisema kitendo cha kuendelea kutoa huduma ya elimu inaonesha dhamira ya dhati  ya watoa maona kuhusu namna ya kuendeleza elimu nchini Tanzania katika fani mbali mbali.

  “Kwa hatua hii hata aliyekuwa anabeza ameanza kujiuliza kuwa tulidhani watashindwa kumbe wameweza, hivyo hiyo itakuwa sifa nzuri ya kusonga mbele,”alisema.

  Awali Kaimu Mkuu  wa Chuo hicho Taaluma, Dk.William  Kudoja alisema  wanaendelea na utaratibu wa kuongeza kozi zingine baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo yao Bagamoyo.

  “Tunaomba wadau, ikiwamo serikali kuhakikisha  wanatusaidia  ili kumiliki majengo yetu wenyewe na kuepuka gharama kwenye majengo ya kupanga,” alisema.


  0 0


  0 0

  Kituo cha utalii mkoa wa Ruvuma kinatarajia kuandaa tamasha la miss utalii mkoa wa Ruvuma, kwa kuwatumia wazawa kutoka wilaya za SONGEA,MBINGA,NYASA , TUNDURU na NAMTUMBO kwa lengo la kumpata balozi mmoja atakaye wakilisha kutangaza utalii uliopo katika mkoa wa huo.Hii hapa video yake.


  0 0

  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila.
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
  Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila. 
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na ujumbe wa Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
  Wananchi wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  0 0

  Maeneo ambayo wananchi walibomolewa nyumba zao.
  Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini ,Constatine Kanyasu,akizungumza na wananchi wa kata ya Buhala hala wakati aliipokwenda kusikiliza kero ambazo zimekuwa zikiwakabili kwenye maeneo ambayo wanaishi.
  Moja kati ya wananchi ambao wameuzulia Mkutano huo akielezea kero yake kwa Mbunge wa Geita mjini wakati wa Mkutano huo.
  Meza kuu ikiongozwa na Mbunge wa Geita,Mjini,Diwani wa kata ya Buhala hala pamoja na baadhi ya wajumbe wakifatilia maelezo kutoka kwa wananchi.
  Wananchi ambao walikuwa wamejitokeza kwenye mkutano huo wakisikiliza wakati Diwani wa kata ya Buhala hala alipokuwa akitoa maelezo na kujibu baadhi ya changamoto za wananchi.
  Steven John ambaye ni moja kati ya wananchi ambao wamebomolewa makazi yao akielezea namna ambavyo alivyo bomolewa makazi yake.
  Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita,ambaye pia ni afisa Mipango Luciano Bundala,akijibu kero za wananchi wakati wa mkutano wa mbunge wa Geita Mjini.
  Diwani wa kata ya Buhala hala,Mussa Kabesse akifafanua na kutoa majibu juu ya maswali ambayo yalikuwa yameulizwa na wananchi.

  IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

  Mbunge wa Geita Mjini Constatine Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha wananchi waliokuwa wamejenga kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku wengine wakiachwa katika maeneo hayo na kuahidi kushughulikia ili haki itendeke sawa na wale ambao hawajabomolewa.

  Hayo aliyasema kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye mtaa wa Mwatulole kata ya buhala hala wilaya na Mkoa wa Geita,wenye lengo la kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika jimbo ambalo analiongoza.

  Mh Kanyasu amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za watu wengine huku wale wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye maeneo hayo kutokana na hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale waliobomolewa pale yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.

  “Naomba Nikiri na mimi iliniuma sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo na sijui kama walitumia sheria mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake ya msingi alete na mimi nitashughulikia”Alisema Kanyasu

  Hata hivyo Bi,Chausiku Lusetula ambaye ni miongoni mwa wanananchi waliobomolewa makazi yao amemuomba Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao za msingi na kwamba kwa sasa hawana makazi ya kuishi baada ya makazi yao kubomolewa.

  “Mheshimiwa Mbunge sisi ni watu ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi tutaishi na chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee kukaa kwenye maeneo ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni hivyo ni vyema haki itendeke kwa wote”Alisema Chausiku

  Diwani wa kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa jimbo la Geita Mjini tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana barua ambayo imemwomba matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na kuwekwa taasisi ambazo zitawasaidia wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya shinde na magogo kupata mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na afya.

  Hatua hii imekuja ni baada ya takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi ambao wamejenga kwenye hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa misitu nchini TFS kubomolewa makazi yao.

  0 0


  Wachezaji wa Simba wakishangilia mara baada ya kuichapa Yanga bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom.
   Kiungo wa kati wa Yanya Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka beki wa SimbaJanvier Bukungu
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka sawa mpira mbele ya beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondan
   Golkipa wa Yanga Deogratius Munishi akiokoampira uliopigwa na mshambualiaji wa Simba Laudit Mavugo
   Kiungo wa Simba Said Ndemla akiwania mpira na kiuongo wa kati wa Yanga,Justin Zulu (Mkata umeme)
   Mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib akimtoka beki wa Yanga Mwinyi Haji katika mchezo huo ambao Simba imeshinda bao 2-1
   Wachezaji wa Simba wakishangilia bao la kusawadhisha liliwekwa kimyani na mshambuliaji Laudit Mavugo
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akipiga mpira mbele ya beki wa Yanga , Andrew Vicent katika mchezo ambao Simba waliweza kutoka na ushindi wa bao 2-1
   Mshambuliaji wa Yanga , Obrey Chirwa akiwania mpira mbele ya kiungo wa Simba Said Ndemla
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akiweka swa mpira mbele ya beki wa Yanga Mwinyi haji
   Wachezaji wa Simba wakiwa wamembeba winga wa kulia wa timu hiyo Shiza Kichuya mara baada ya kuipatia Simba bao la ushindi katika mchezo wake wa ligi kuu ya Viodacom Tanzania
   Mameneja wa timu ya Simba wakiwa wamembeba mchezaji Shiza kichuya mara baada ya kuipatia timu hiyo bao la kuongoza katika mchezo wake dhidi ya Yanga
   Mashabiki wa Yanga wakiwa wamekaa kwa huzuni mara baada ya timu yao kupigwa bao 2-1 na timu ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania.
   Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi wa bao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacoma Tanzania
   Askari wa jeshi la Zimamoto wakiwa wamembeba mtu mabaye amezimia kwa furaha mara baada ya Simba kushinda
   Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akimtoka beki wa kati wa Yanga Kelvin Yondani.

   Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni , Nape Nnauye akisalimiana na Nahodha wa Yanga Haruna Niyonzima.
   Waziri wa Habari Sanaa, Michezo na Utamaduni , Nape Nnauye akisalimiana na Nahodha wa Simba Abdi Banda

  0 0


  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania), Bw. Sanjay Rughani pamoja na Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chamawachezaji wakiwa katika picha ya pamoja na timu mbalimbali kabla ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania), Bw. Sanjay Rughani pamoja na Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chamawachezaji wakifanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wa timu kabla ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.
  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa timu mbalimbali zilizojiunga na mashindano baada ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na wachezaji (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania) Bw. Sanjay Rughani akiongea na wageni waalikwa pamoja na wachezaji wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chama akiongea na wageni waalikwa pamoja na wachezaji (hawapo pichani) wakati wa Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akipiga mpira kuashiria ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (katikati), Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Standard Chartered (Tanzania), Bw. Sanjay Rughani (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Uamuzi Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw. Salum Chamawachezaji wakifuatilia mpira katika mechi ya ufunguzi kati ya Standard Chartered na Wenyeji (JK Youth Park) baada ya Ufunguzi wa Mashindano ya Kombe la Standard Chartered kwa Mwaka 2017 yaliyoanza leo 25/02/2017 katika Viwanja vya JK Youth Park (Kidongo Chekundu) Jijini Dar es Salaam.


  (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM)

  0 0

  Na: Lilian Lundo – MAELEZO

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni kwa pamoja wamekubaliana kutosaini mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA).

  Makubaliano hayo yamefanyika jana Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo  Rais Yoweri Museveni yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 25 – 26  Februari, 2017.

  Akiongea na waandishi wa habari Rais Magufuli amesema kuwa mkataba wa EPA hauna faida bali ni aina nyingine ya ukoloni ambao unataka kurejeshwa kwa nchi za Afrika.

  “Nimeongea na Rais Yoweri Museveni amekubali kutosaini mkataba wa EPA, nitawaagiza wataalamu waliosaidia kutupa maelezo juu ya madhara ya mkataba huo kwenda pia Uganda kuwapa maelezo ambao waliyatoa kwa Tanzania,” alifafanua Dkt. Magufuli.

  Kwa upande wake, Rais Yoweri Museveni amesema kuwa ameongea na Rais Magufuli na wamekubaliana kutosaini mkataba huo na kuongeza kuwa suala la EPA ni lazima lijadiliwe na nchi zote za Afrika Mashariki ili kuwepo na msimamo wa pamoja kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  Aidha Rais Museni amempongeza Rais Magufuli kwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya Sita, hivyo amekaribisha shirika hilo kutoa huduma za usafiri wa anga nchini Uganda kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

  Vilevile amempongeza Rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Dar es Salaa mpaka Mwanza na Isaka mpaka Rwanda ambapo itapelekea ujenzi wa bandari kavu katika mkoa wa Mwanza hivyo wafanyabiashara wa Uganda kunufaika na bandari hiyo ambayo itakuwa karibu zaidi kuliko ilivyo kwa Dar es Salaam.

  Wakati huohuo Mawaziri wa Nje kutoka Tanzania na Uganda Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Oryem Henry Okello wamesaini makubaliano ya uhusiano katika mambo ya Diplomasia baina ya nchi hizo mbili.

  Museveni yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo atatembelea baadhi ya maeneo kadhaa ikiwemo kiwanda cha Juice cha mfanyabiashara Mtanzania Said Bakhressa ambaye pia amewekeza nchini Uganda.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni alipowasili Ikulu jijini Dar es salaam kuanza ziara rasmi ya kiserikali ya siku mbili leo Februari 25, 2017 .

  PICHA NA IKULU

  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Thobias Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kasim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi (wapili kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba(Wakwanza kulia) , Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Hamad Masauni (Wakwanza kushoto) pamoja na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye(Watatu kutoka kushoto waliosimama mstari wa nyuma) na Mabalozi Pindi Chana(Wakwanza kulia walisimama mstari wa nyuma ) , Balozi Matilda Masuka(Wapili kutoka kulia waliosimama mstari wa nyuma), Balozi Abdallah Kilima(Wapili kutoka kushoto mstari wa nyuma) na Balozi Silima Kombo Haji (Wakwanza kushoto waliosimama) mara baada ya tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.


  PICHA NA IKULU

  0 0

  Na. Immaculate Makilika na Lilian Lundo- MAELEZO.

  Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.

  Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi vya Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.

  “Nawakaribisha wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira” alisema Rais Museveni.

  Kauli hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.

  Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.

  Aidha, amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.

  Kwa upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda.

  Amesisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.

  “Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi” alisema Waziri Mwijage.

  Waziri Mwijage alitoa Wito kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima matunda au mbogamboga.

  Rais Yoweri Museveni aliwasili nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo akiwa nchini alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kutembelea Viwanda vya Said Salim Bakhresa vya Tazara na Vingunguti.

  0 0


  Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) akishirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela na Katibu Tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo (kulia) wakifanya usafi katika maeneo ya buguruni kwa malapa kutimiza kauli ya Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. (PICHA NA ELISA SHUNDA) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Msongela Palela akizungumza na wananchi wa eneo la Buguruni kwa Malapa na Darajani kuhusu kufanya usafi katika maeneo yanayowazunguka ili kujikinga na kujiepusha na magonjwa ya milipuko kama Kipindupindu baada ya kufanya usafi kutekeleza agizo la Rais Dk.John Magufuli ya kufanya usafi kila mwisho wa wiki ya mwezi jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Diwani wa Kata ya Buguruni,Adamu Fugame (Cuf) na Katibu tawala wa wilaya hiyo,Edward Mpogolo.


   
  NA EMERISIANA ATHANAS .

  DIWANI wa Kata ya Buguruni wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Adam Fugame ameagiza viongozi wa kata akiwemo Ofisa Afya, kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wasiofanya usafi au kuchangia kwaajili yakuzolewa uchafu.

  Akizungumza jijini hapa jana, wakati wa zoezi la ufanyaji usafi ulioshirikisha viongozi mbalimbali wa Manispaa ya Ilala akiwemo Mkurugenzi Msongela Palela, alisema ni vema viongozi wakafanya kazi kwa mujibu wa sheria ili kuwashughulikia watu hao.

  "Suala hili sio rai bali tufanye kama sheria ili kufanikisha zoezi la kuimarisha usafi katika maeneo yetu, kwani tusipofanya hivi hakuna litakalotekelezwa, watu hawafanyi usafi," alisema.

  Kutokana na umuhimu wa kufanya usafi alisema ni vema watakaokutwa hawachangii wala kujishughulisha na kufanya usafi wakachukuliwa hatua na kutozwa fedha.

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Palale alisema kuwa katika kata tisa zilizoko katika manispaa hiyo kata ya Buguruni ndiyo imekuwa na ugonjwa wa kipindu pindu ambacho husababishwa na hali ya uchafu.

  Alitumia nafasi hiyo kuwataka wakazi wa kata ya Buguruni kuhakikisha wanafanya usafi na kuwa walinzi katika kuhakikisha wanalinda mazingira na kuimarisha usafi kwenye maeneo yao

  0 0


   Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 
  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
   Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).

   Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.
   Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
   Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
  Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
  Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  
   Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akimwelezea jambo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 
   Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Bakhresa  Bw. Salim Aziz.
   Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiangalia namna Juisi ya Azam inavyotengenezwa alipofanya ziara katika Kiwanda hicho leo Jijini Dar es Saalam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage.

   Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la Makampuni  ya Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo.

  0 0

  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke akipewa maelezo na Mchoraji wa picha, Bw. Douglas Kahabuka katika Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji mjini Songea. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu akiwa pamoja na viongozi wenzake wa kabila la wangoni.
  Mtaalamu wa Tafiti za Historia, Lili Reyels (kulia) akimueleza Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke ( wa tatu kushoto) ,kuhusiana na Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu ( wa pili kulia) akiwa pamoja na viongozi wa Mila ya wangoni. 
  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke (kushoto) akiwa na Chifu wa Kabila la Wangoni, Emannuel Zulu ( wa kwanza kulia) akizungumza mara baada ya kupata maelezo kwa Mchoraji wa picha, Bw.Douglas Kahabuka (katikati) katika Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni Chifu wa kabila la Wangoni, Emmanuel Zulu akiwa pamoja na viongozi wenzake wa kabila la wangoni.
  Balozi wa Ujerumani Nchini Tanzania, Egon Kochanke (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kabila la wangoni huku wakipeana mikono na Chifu wa Kabila la Wangoni, Emannuel Zulu (kushoto) mara baada ya kuzindua Maonyesho ya kitalii ya kazi za sanaa na uvumbuzi wa kitaalamu juu ya Watanganyika waliokuwa wakipambana na Utawala wa Wajerumani, Onyesho hilo limepewa jina la ‘Kuishi Ndani ya Simulizi’ linahusisha vitu, michoro, picha za kuchora, filamu, vifaa na utafiti yaliyofanyika jana mjini Songea katika Jumba la Makumbusho ya vita vya Majimaji. Wengine ni watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

  0 0

  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni .Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.
  Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambae pia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria mwema,Tahir Othman (hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (aliyesimama) katikati alipokuwa akitangaza mchango wake wa fedha Shilingi za Kitanzania Millioni Kumi zilizochangwa jana wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar (HIPZ).
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akisalimiana na Mwenyekiti wa HIPZ RU Mac Donagh wakati alipowasili viwanja vya Park Hayatt Hoteli jana katika hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya katika ukumbi wa kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar (HIPZ).
  Baadhi ya Viongozi na Wageni mbali mbali wakiwa katika hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa na Wizara ya Afya ya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) RU Mac Donagh alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa jana na Wizara ya Afya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyotayarishwa jana na Wizara ya Afya kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia Hospitali ya Makunduchi na Kivunge pamoja na maadhimisho ya miaka kumi ya Mradi wa kuendeleza huduma za Afya Zanzibar,(HIPZ) hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Park Hayatt Hoteli Mji mkongwe wa Zanzibar.[Picha na Ikulu.]

older | 1 | .... | 1152 | 1153 | (Page 1154) | 1155 | 1156 | .... | 1903 | newer