Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli amteua Dkt. John Kedi Mduma kuwa Mwenyekiti Bodi ya CMSA


TAARIFA YA KUKANUSHA UZUSHI KUHUSU AFYA YA RAIS MSTAAFU ALLI HASSAN MWINYI

MBUNGE ILEJE AWATOA HOFU WANANCHI JUU YA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA-ISONGOLE

$
0
0
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Mbunge wa Jimbo la Ileje, Janet Mbene amewatoa hofu wakazi wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kutokuwepo kwa ujenzi wa barabara na kusema kuwa muda wowote kuanzia sasa Barabara ya Isongole Mpemba itaanza kujengwa.

Akizungumza na wakazi wa Ileje alipokuwa akijibu maswali kupitia mtandao wa kijamii wa Whats up, Mbene amesema kuwa Sasa hivi Evaluation ya tenda documents imemalizika.

“Wamemaliza kupitia makabrasha ya 'Tender' wanaendelea na majadiliano na Mkandarasi juu ya gharama na vipengele mbalimbali, na watamtangaza Mkandarasi muda si mrefu kabla ya Mwezi wa Sita kama nilivyoelezwa na meneja wa Tanroads mkoa wa Mbeya” amesema Janet Mbene.

Barabara hiyo ya Mpemba-Isongole ni moja ya barabara ambazo zipo katika ahadi ya Rais John Pombe magufuli hivyo muda si mrefu wakazi wa Wilaya ya Momba na Ileje wataunganishwa katika barabara hiyo.

Ujenzi wa barabara hiyo utaweza kuinua fursa za kiuchumi katika Wilaya ya Ileje hasa kufungua biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Malawi.

Baada ya kuachiwa huru na kukamatwa tena Hatma ya kesi ya mauaji ya mke wa Bilionea Msuya mwezi ujao.

$
0
0
Wakili wa utetezi, katika kesi ya mauaji ya inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita, Peter Kibatala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa haina mamlala ya kisikiliza kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa walishaachiwa huru.Kibatala amedia kuwa kitendo cha Mahakama hiyo kusikiliza kesi ambayo Jana watuhumiwa waliachiwa huru ni sawa na kuichonganisha Mahakama na kufanya maamuzi ya Hakimu aliyewaachia huru kuonekana hapana maana. 

Jana, Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa wa Mahakama hiyo aliwachia huru Mrita anayeshtakiwa pamoja na Revocatus Muyela baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri ya mahakama iliyowataka kurekebisha hati ya mashtaka kwa kuwa inamapungufu.Hata hivyo, washtakiwa hao walikamatwa tena jana hiyo hiyo na jeshi la polisi na kisha Leo asubuhi wamepandishwa mahakamani hapo kusomewa upya tuhuma za mauaji ya Aneth.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mrita anadaiwa kumuua wifi yake Aneth Msuya  akishirikiana na Revocatus Muyela.Inadaiwa kuwa mauaji hayo yalifanyika Mei 25, mwaka Jana huko Kibada Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 

Mata baada ya kusomewa tuhuma hizo za mauaji, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ambazo zinasikilizwa Mahakama Kuu.
Kabla upande wa jamuhuri haujasoma kesi hiyo Wakili Kibatala aliiomba mahakama kutoyasikiliza mashtaka hayo kwa kuwa Kisutu haina mamlaka. 

Lakini Hakimu Thomas Simba aliwaamuru upande wa mashtaka kuisoma kwanza kesi hiyo ndipo awasikilize hoja zao.Mara baada ya kusomewa tuhuma zao na kutotakiwa kujibu kitu, ndipo Kibatala alipoibuka na hoja hizo ambazo zilipingwa na upande wa Jamuhuri.Akijibu Hoja hizo, wakili wa serikali mkuu, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa uamuzi wa Hakimu Mwambapa kuwaachia huru washtakiwa hao uliishia hapo hapo.
Aidha aliitaka mahakama kuzitupilia mbali hoja za upande wa utetezi na kudai kuwa hati ya mashtaka dhidi ya washtakiwa imekamilika na naona mapungufu.

Aliongeza kuwa kitendo cha kuwakamata washtakiwa hao Jana na kuwaleta tena Leo mahakamani ilikuwa ni halali kwao kwa sababu,Uamuzi wa mahakama kuwaachia huru uloosha kana ile ile.Awali, Hakimu Mwambapa aliuapatia upande wa mashtaka muda wa siku tatu kurekebisha hati ya mashtaka.

Lakini mpaka siku hizo tatu zinaisha hawakuwa wamefanyia bali Wakili wa Serikali, Hellen Moshi aliiambia mahakama kuwa baada ya ofisi ya DPP kutafakari kwa kina wameamua kuwa hawana cha kubadilisha kwa kuwa hati hiyo ya mashtaka inajitosheleza. 

Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo alikuwa mke wa aliyekuwa kaka wa Aneth, marehemu Erasto Msuya, maarufu kama bilionea Msuya. 

Erasto Msuya, ambaye alikuwa mfanyabiashara bilionea wa madini ya Tanzanite, pia aliuawa kwa kupigwa risasi, Agosti, 2015 eneo la Mijohoroni, kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.
 Mke wa aliyekuwa Bilionea Erasto Msuya na mwenzake Revocatus Muyela wakiwa mahakamani wakisubiri kusomewa mashtaka yao mapya ya mauaji baada ya Jana kuachiwa huru na kisha kukamatwa tena.   
Mrita na mwenzake wanatuhumiwa kumuua kwa kukusudia Aneth Msuya ambaye ni Dada wa Marehemu wa Bilionea Msuya 
Washtakiwa hao wakijadili jambo na wakili wao Peter Kibatala(wa pili kutoka kushoto).

KAMPUNI YA RESOLUTION INSURANCE IMEWADHAMINI KAWE JOGGING CLUB KUSHIRIKI MASHINDANO YA KILI MARATHON 201

$
0
0
Kampuni ya Resolution Insurance imekabidhi rasmi mchango wao kwa Kawe Jogging Club kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon yatakayo fanyika Tarehe 26 Februari 2017. Mchango huu ulikua ni mwitiko kwa ombi la klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon. 

Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance, Bi. Maryanne Mugo alisema kuwa mchango huo upo ndani ya vipaumbele vya kampuni katika uwekezaji jamii hasa katika sekta ya afya. 

Resolution Insurance inadhamini uwajibikaji kwa jamii ambayo kwa kiwango kikubwa inalengo maeneo ya vipaumbele vya Elimu, Afya, Mazingira, Ujasiriamali na malengo yake hasa ni kujikita katika masuala ya ubinadamu.” Bi. Maryanne alisema na kubainisha kwamba hii ni mara ya pili wanaidhamini Kawe Jogging Club kushiriki mashindano hayo na inawahimiza wananchi kwa ujumala kujihusisha na mazoezi kwa ajili ya kuwa na afya njema. 
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance Maryanne Mugo (kushoto), akikabidhi tishirt ya jersi kwa Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club Bw. Al Haj Seif Muhere, ikiwa ni moja ya vivaa vilivyotolewa na kampuni hyo kwa ajili ya kuwawezesha klabu hiyo kuweza kushiriki mashindano ya Kili Marathon. Pamoja nao kwenye picha ni Diwani wa Kawe Mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na Mwenyekiti wa Kawe Jogging club Bw. Abdul Risasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Resolution Insurance, Maryanne Mugo akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa walivyodhamini kwa Kawe Jogging Club kwa ajili ya kusaidia klabu hiyo kushiriki mashindano ya Kili Marathon. 
Katibu Mkuu wa Kawe Jogging Club, Al Haj Seif Muhere (wa kwanza kushoto) akitoa shukrani kwa Kampuni ya Resolution Insurance kwa niaba ya klabu yake. 
Diwani wa Kawe, Mheshimiwa Muta Rwakatare akiongea na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa walivyodhamini Kampuni ya Resolution Insurance kwa Kawe Jogging Club. Mheshimiwa Diwani alitoa shukrani kwa kampuni hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Resolution Insurance, Maryanne Mugo (wa kwanza kushoto), Ofisa masoko wa kampuni ya Resolution Insurance, Laura Lyabandi (wanne kushoto), Meneja mauzo wa kampuni ya Resolution Insurance Nilufar Manalla (watano kushoto), Meneja wa wakala wa kampuni ya Resolution Insurance (njuma) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Diwani wa Kawe mheshimiwa Muta Rwakatare (wapili kushoto) na baadhi ya washiriki kutoka Kawe Jogging Club watakao shiriki kwenye mashindano ya Kili Marathon.


KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AENDESHA KIKAO CHA IDARA ZA WIZARA HIYO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiongoza kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam
Kamishna wa Jeshi la Magereza Divisheni ya Utawala na Fedha,Gaston Sanga, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna wa Fedha Jeshi la Polisi Albert Nyamuhanga.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Afisa Tawala wa Idara hiyo,Jenita Ndone(Kulia), wakifuatilia kwa makini kikao cha ndani cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Regasira (hayupo pichani) .Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.
Maafisa kutoka idara ya Uhamiaji wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara. Kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MWIJAGE: TAASISI ZINAZOHUSIKA NA UWEKEZAJI ZIACHE UKIRITIMBA

$
0
0

Ramani ya kiwanda



Wa kwanza kushoto mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, alhaj Magid Mwanga ,wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo na Jack Feng mkurugenzi wa kiwanda, wa tatu kushoto ni waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage na Ridhiwan Kikwete na Cliford Tandari wakiweka udongo kwenye jiwe la msingi.(picha zote na Mwamvua Mwinyi)


Na Mwamvua Mwinyi, ChalinzeWaziri wa biashara, Viwanda na Uwekezaji, Charles Mwijage, amezitaka taasisi zinazohusika na uwekezaji kutokuwa na ukiritimba ili hali kufikia malengo ya serikali ya kukuza sekta ya viwanda.Aidha ameeleza kwamba, wizara hiyo, imeweka mazingira mazuri ya uwekezaji ambayo yatawezesha kuvutia wawekezaji wa ndani na nje.

Hayo aliyasema huko kitongoji cha Pingo Chalinze,Bagamoyo,wakati akiweka jiwe la msingi kwenye kiwanda cha Vigae cha Twyford Ceramics Ltd.
Mwijage alisema, uwekezaji huo unaendana na dhana ya Rais Dk John Magufuli wa kuifanya nchi kuwa ya Viwanda .Alisema kwa kuanzishwa viwanda vingi vya aina hiyo kutasaidia kuongeza pato la nchi na kuzalisha ajira kwa wingi.

“Zipo idara ambazo zinafanikisha uwekezaji ikiwemo brela, idara ya uhamiaji, kazi, mamlaka ya mapato TRA, wizara ya ardhi, shirika la viwango TBS, baraza la Mazingira NEMC ambazo zinapaswa kufanya kazi kwa wepesi ili kufanikisha uwekezaji,” alisema Mwijage.

Alisema kati ya idara hizo baadhi zimekuwa zikifanya vizuri lakini nyingine zimekuwa zikiwapa usumbufu mkubwa wawekezaji.“Wizara yangu haina tatizo lakini kuna baadhi ya idara zimekuwa kero na ukiritimba usio na sababu .,naomba kama kuna idara zinakuwa kikwazo niambieni ili tuwachukulie hatua,” alisema Mwijage.

Mwijage alisema nchi zilizofanikiwa kukuza uchumi wake kupitia viwanda zimeweza kutoa ajira nyingi kwa vijana kupitia sekta rasmi na isiyo rasmi.
Mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho Jack Feng alieleza, kiwanda hicho asilimia 95 ya malighafi itakuwa inatoka nchini ambapo kigae kinatumia maliahafi zaidi ya 10.
Alisema mara kiwanda hicho kitakapokamilika agosti mwaka huu kitaweza kupunguza asilimia 30 ya uagizaji wa vigae toka nje ya nchi.

Feng alisema wanatarajia kuajiri wafanyakazi 2,000 moja kwa moja na 4,000 kazi za muda na gharama ya mradi huo ni dola mil. 56 sawa na bil. 120 .Alisema watauuza hadi nje ya nchi ikiwa ni pamoja na Zambia, Uganda, Rwanda na Burundi .

Nae mkurugenzi mtendaji wa kituo cha uwekezaji Cliford Tandari alisema kuwa uwekezaji wa kiwanda hicho ni wa mfano kwani utavutia makampuni mengi.Alisema kwasasa kituo hicho kimeweza kutoa wigo mkubwa katika kuandikisha miradi mbalimbali toka china na kufikia miradi 667 ambayo itazalisha ajira 83,141 kwa watanzania ,miradi 452 ni miradi inayohusiana na sekta ya uzalishaji viwandani.Mkuu wa mkoa wa Pwani Injinia Evarist Ndikilo alisema ,mkoa huo una viwanda 264 huku vikubwa vikiwa ni viwili.

Ndikilo alisema uwekezaji huo ni mkubwa na unatarajia kukuza ajira kwa vijana wa mkoa wa Pwani na Tanzania kwa ujumla.Alisema mkoa wa Pwani bado una maeneo makubwa ya uwekezaji na tayari kuna eneo lenye ukubwa wa hekari 5,000 linahitaji wawekezaji .
Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete aliwapongeza wawekezaji hao kutoka nchi ya China .

Alisema Chalinze imejipanga kuwa sehemu ya uwekezaji ambapo kuna ujenzi wa viwanda mbalimbali.Ridhiwani alisema kuwa changamoto kubwa inayokabiliwa wananchi na wawekezaji ni ukosefu wa maji,.Alibainisha wamekuwa wakijitahidi kuikabili lakini bado hawajafanikiwa kuidhibiti aliomba wawekezaji hao kutoa ajira bila ya kuwabagua wenyeji.

MAFUNZO YA UKAKAMAVU KIDATO CHA KWANZA JITEGEMEE JKT SEKONDARY YAFUNGWA RASMI JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

 Mgeni rasmi wa kufunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Jitegemee Sekondari Mgulani JKT, Meja Haule (katikati), akiwa na viongozi wengine wakati wa hafla ya kufunga mafunzo hayo Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia ni Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga, Msanifu wa Shule, Meja Rehema Wanjara, , Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila na Makamu Mkuu wa Shule Taaluma, Ema Mosha.
 Paredi la ukakamavu na uzalendo likifanyika.

 Gwaride likitoa heshima mbele ya mgeni rasmi.

 Ndugu, wazazi na jamaa wa wanafunzi hao wakifuatilia kwa karibu shughuli hiyo.
 wanafunzi wa shule hiyo wakifuatilia gwaride hilo.

 Gwaride likiendelea.
 wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 Wimbo maalumu ukiimbwa.
 Kiongozi wa gwaride hilo, Pelegia Nyunga akikabidhiwa zawadi na mgeni rasmi.
 Francis Christopher akipewa zawadi.
 Mwanahawa Shabani akikabidhiwa zawadi.
 Salehe Hemedi akipata zawadi yake.
 Nuhu Sajilo akipata zawadi.
 Furaha na utamu wa gwaride hilo.
 James David akikabidhiwa zawadi.


 Miriam Simon akipata zawadi

 Ofisa Tawala wa Kombania wa shule hiyo, Kepteni Zaujia Shemahonga akizungumza katika hafla hiyo.
 Makamu Mkuu wa Shule Utawala, Kepteni Benitho Lubila, akitoa hutuba fupi kaba ya kumkaribisha mgeni rasmi.


Wimbo wa taifa ukiimbwa.

 Wimbo wa Taifa ukiimbwa.

Brass Band ya JKT ikiongoza gwaride hilo.

Na Dotto Mwaibale

WANAFUNZI nchini wametakiwa kuacha kujiingiza katika makundi yasiofaa ili kujiepusha na kujihusisha na dawa la kulevya.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mgulani, Meja Haule wakati akifunga mafunzo ya ukakamavu kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza wa Shule ya Sekondari ya Jitegemee Dar es Salaam leo.

"Wanafunzi acheni kujihusisha na makundi yasiofaa ili kujiepusha kuingia katika vishawishi vya matumizi ya dawa za kulevya" alisema Meja Haule.

Aliwataka wanafunzi hao kutumia muda wao wote kwa kusoma ili kutimiza ndoto za maisha yao kwa kupata elimu bora.

Meja Haule aliwataka wanafunzi wa kike kujiepusha na tamaa mbalimbali kwani wao wapo katika hatari ya kupata vishawishi na aliwataka kujifunza kwa wanawake waliofanikiwa na kufanya vizuri kwa kuwa viongozi katika taifa.

Haule aliziomba shule zilizopo chini ya jeshi kuiga mfano wa shule ya Jitegemee ya kutoa mafunzo hayo ya ukakamavu kwani yanawafanya wanafunzi hao kuwa wazalendo wa nchi yao.

Makamu Mkuu wa Shule Utawala Kepteni Benitho Lubida alisema wanafunzi waliopata mafunzo hayo ni 604 na walitumia wiki tatu kufuzu.

Alisema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wanafunzi hao wa kujitegemea, kuwafanya wawe na nidhamu, kujiamini, kuwa wavumilivu na kujiamini.

Aliwaomba wazazi wa wanafunzi hao kuwa wa kwanza kutoa mafunzo mbalimbali kwa watoto wao ili kuwajenga katika misingi mizuri kuanzia ngazi ya familia.



BAADHI YA VIONGOZI WAKILA KIAPO CHA UADILIFU KATIKA UTUMISHI WA UMMA.

$
0
0
 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia kulia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Robert Boaz Mikomangwa (kushoto).
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akila Kiapo cha Uadilifu mbele ya Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa(kushoto) akiweka saini katika Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma leo jijini Dar es Salaam. Anayeshuduia ni Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna wa Maadili katika Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Mhe. Harold Reginald Nsekela akimkabidhi Hati ya Kiapo cha Uadilifu kwa viongozi wa umma Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Ally Malewa.

Picha zote na: Frank Shija - MAELEZO.

SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUSOMBWA NA MAJI, RPC ATOA TAHADHARI

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Mkumbo


Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha

Jeshi la Polisi mkoani hapa limewataka wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari zote katika kipindi hiki cha Masika. Akizungumza na waandishi wa habari mchana wa leo ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna Charles Omari Mkumbo alisema katika kipindi hiki cha mvua wananchi hawatakiwi kuvuka mito na mabonde yenye maji kwa hisia badala yake wanatakiwa wawe na subira.

“Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha katika kipindi hiki cha masika hamtakiwi kujipa ujasiri na kuyakadiria maji ya mvua hivyo zinahitajika tahadhari za kutosha dhidi ya watoto, au vyombo vyovyote vya usafiri kwani maji hayo huwa yanakwenda kwa kasi, yasubirini yapite acheni hisia ili kuhakikisha maisha yenu hayahatarishwi na mvua”. Alisisitiza Kamanda Mkumbo.

Kamanda Mkumbo alitoa wito huo baada ya jana usiku kunyesha mvua kubwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa huu na kusababisha vifo vya watu saba. Alisema katika tukio la kwanza jana Usiku wa saa 4:00 katika kijiji cha Kimbolo kata ya Enaboishu wilayani Arumeru, watu watano wote wakazi wa kijiji cha Kyoga walifariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.

Akiwataja watu hao waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Shengai Saiguran (30), Nembris Mungaya (20), Minis Loyi (25), Inoti George (40) na Ngaisi Moluo ambaye umri wake bado haujafahamika mara moja huku dereva wa gari hilo Yusuph Jacobo akinusurika.

Kamanda Mkumbo alisema mbali na vifo vya watu hao pia watu wengine wawili walifariki dunia katika maeneo tofauti ambapo katika kijiji cha Keriani mtu aitwaye Babu Robikeki alisombwa na maji kisha kufariki dunia wakati anavuka mto wakati akitokea matembezini.

Wakati mtu wa saba ni Seuli Meseyeki (37) dereva wa boda boda ambaye alikuwa anaendesha pikipiki aina ya T-Better yenye namba za usajili T. 726 DFD naye alisombwa na maji eneo la Olorieni Ngaramtoni wakati anavuka barabara. Pia pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 892 ACR iliokotwa maeneo ya Olasiti kwa Mawala halmashauri ya jiji la Arusha huku dereva wake hajulikani alipo.

DC MTATURU AITUMIA SIKU YA ALHAMISI KUSHUKA KWENYE TARAFA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI NA KUZITATUA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akimkabidhi mashuka Dk. Frank kwa ajili ya kituo cha afya cha Ihanja wakati akiwa katika ziara ya kukagua huduma zinazotolewa kituoni humo na kusikiliza kero za wananchi.
Dk. Frank wa kituo cha afya cha Ihanja akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu na diwani wa kata ya Kituntu Said Tumbwi wakati walipofika kituoni hapo.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu akikagua shamba la mtama la mwananchi wa kijiji cha Puma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake aliyoifanya katika tarafa ya Ihanja.
Miraji Mtaturu mkuu wa wilaya ya Ikungi akiwa na afisa kilimo wa tarafa ya Ihanja Azizi Mwamakula wakikagua shamba la viazi la hekari mbili linalomilikiwa na vijana wa tarafa hiyo.
Baadhi ya wakazi wa tarafa ya Ihanja wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu hayupo pichani alipokuwa anasikiliza kero zao na kuzijibu katika ukumbi wa kanisa lililopo makao makuu ya tarafa ya ihanja.

……………………………………..

KATIKA moja ya mambo ambayo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wa rais dokta John Magufuli inasisitiza kuyafanya ni kwa viongozi kushuka kwa wananchi kwa kuwatembelea ,kusikiliza kero zao na kuzitatua.

Ili kulitekeleza hilo mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu ameitenga siku ya alhamisi ya kila wiki kuhamishia ofisi yake kwenye tarafa maalum kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi kutoka kwa wahusika.

Alhamisi hii akiwa ameweka kambi tarafa ya Ihanja wilayani humo Mtaturu amemuagiza kaimu mkurugenzi wa wilaya hiyo Haika Massawe kumuelekeza mwanasheria wa halmashauri kutoa msaada wa kisheria kwa Fatma Mohammed ambaye anasumbuliwa kupata haki yake ya ardhi.

Mama huyo anafuatilia shamba la baba yake mzazi ambaye ni mzee na anaumwa lililovamiwa na mtu bila ya mafanikio pamoja na kwamba alishinda kesi katika baraza la kata na wilaya lakini alikatiwa rufaa mahakama ya rufaa ya Dodoma.

“Mkurugenzi fuatilia kwa mwanasheria ilia toe msaada wa kisheria,kesi hii imeelekezwa na jaji wa mahakama ya rufaa ya Dodoma kuwa kuna makosa yamefanyika kwenye baraza la kata huku,”alisema Mtaturu.

Katika ziara hiyo alitembelea kituo cha afya cha Ihanja na kutoa agizo kwa kaimu mkurugenzi Massawe kuhakikisha anamsimamia mhandisi wa maji wa halmashauri hiyo afanye tathimini ya kuchimba kisima kirefu cha maji ili kumaliza tatizo la maji kituoni hapo.

“Serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi hivyo nawaelekeza viongozi wote wa vijiji,kata na tarafa kujenga utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi hawa na zilizo ndani ya uwezo wenu mzitatue ili kutimiza zana ya utawala bora,”alisema Mtaturu.

Kwa upande wake afisa tarafa Modesta Manyungu akisoma taarifa alisema wananchi wa tarafa hiyo wanaendelea kufanya kazi ya kujiletea maendeleo pamoja na changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo upungufu wa walimu,watumishi wa idara ya afya,polisi na afisa ugani,upungufu wa visima vya maji na wanasiasa wenye nia ovu kurudisha kukwamisha juhudi za kuwaletea maendeleo wananchi.

“Pamoja na changamoto hizo yapo mafanikio ikiwemo uandikishaji wa asilimia mia moja kwa wanafunzi katika elimu ya msingi,kuongezeka kwa mwamko kutokana na serikali kutekeleza ahadi ya elimu bila ya malipo,”alisema Manyungu.

Mbali na kutembelea kituo cha afya cha Ihanja Mtaturu alitembelea pia mashamba ya mtama,viazi na wafugaji wa kuku,alikagua ujenzi wa maabara na madarasa mawili yaliyopo katika shule ya sekondari ya Masinda ambapo katika kuunga mkono ujenzi huo mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Kingu alichangia mabati 106 na Mtaturu alikabidhi mashuka 20 kwa ajili ya kituo hicho cha afya.

KIWANJA CHA NDEGE CHA DODOMA, KUPOKEA NDEGE ZENYE UWEZO WA KUBEBA ABIRIA 90

$
0
0
Kiwanja cha ndege cha Dodoma, sasa kinauwezo wa kupokea ndege zenye uwezo wa kubeba abiria 90, baada ya kurefushwa kwa barabara ya kutua na kuruka kwa ndege kwa kilometa 2.5.

Ndege ya Shirika la ndege la Tanzania (ATCL), leo ikitua kwenye kiwanja cha ndege cha Dodoma ikitokea mkoani Kigoma.
Mizigo ya abiria wa ndege ya shirika la ndege Tanzania (ATCL), ikiwa ndani ya gari la kampuni inayotoa huduma ya mizigo ya National Aviation Services (NAS), kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma.
Mkuu wa Dodoma (kushoto) Mhe. Jordan Rugimbana akielekea kupanda ya ATCL akiwa ni mmoja wa abiria akitokea kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma na kuelekea Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Kulia ni Meneja wa kiwanja hicho, Bw. Julius Mlungwana.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana (kulia) akiagana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma, Bw. Julius Mlungwana kabla ya kupanda ndege ATCL, akielekea Jijini Dar es Salaam, leo.
Wanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Uwela ya kitongoji cha Kikuyu mkoani Dodoma wakiwa katika ziara ya mafunzo kwenye Kiwanja cha ndege cha Dodoma, leo.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Ivory Coast Mheshimiwa Alassane Ouattara jijini Abidjan

$
0
0
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 23Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Ivory Coast, Mhe. Alassane Ouattara katika Ikulu yake jijini Abidjan.. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha na Waziri wa Elimu.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Ouattara wamezungumzia hali ya elimu bara la Afrika na Ivory Coast kwa ujumla na haja ya kufanya mageuzi makubwa katika elimu ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea.
Rais Mstaafu Kikwete amempongeza Rais Outtara kwa jitihada kubwa anayoifanya kuinua elimu nchini mwake. Kwa mujibu wa utafiti wa Kamisheni, Ivory Coast iko katika nafasi nzuri ya kufikia viwango vya juu vya ubora wa elimu vya nchi zilizoendelea iwapo itaongeza juhudi ya kufanya mageuzi kulingana na mapendekezo ya Kamisheni hiyo.
Rais Outtara amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini mwake. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.
Akiwa jijini Abidjan, Rais Mstaafu ametembelewa na viongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika na Watoto  wa Watanzania hao ambao walitaka kujua kuhusu masuala ya uongozi na maisha baada ya kustaafu. 
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa na Rais Alassane Ouatara wa Ivory Coast jijini Abidjan katika Ikulu ya nchi hiyo.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akimkabidhi ripoti ya 'Kizazi cha Elimu' Rais Allasane Ouatarra wa Ivory Coast
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazungumzo na Rais Alassane Ouattara. Kulia kwake ni Makamu wa Rais wa nchi hiyo Mhe. Daniel Kablan Duncan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiagana na Rais Alassane Ouattara baada ya mazungumzo yao   Ikulu ya Ivory Coast.

 Rais MStaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Uongozi wa Watanzania wanaofanya kazi Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akifurahia mazungumzo na baadhi ya watoto wa Watanzania waishio Ivory Coast waliomtembelea hotelini kwake Abidjan
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwasainia autograph  watoto waliomtembelea hotelini kwake  jijini Abidjan

AMSCO yawakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi kujadili umuhimu wa mafunzo na ujuzi katika kukuza uchumi

$
0
0
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Anne S. Makinda akizungumza kwenye mkutano uliowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi ili kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao umeandaliwa na kampuni ya African Management Services (AMSCOukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.(Picha na Geofrey Adroph)
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza kuhusu upatikanaji wa ajira katika nyanja mbalimbali hasa pale ukuaji wa uchumi unapoimarika wakati wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao uliwakutanisha dawau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti wa Taasisi ya ATMS, Balozi Jan Berteling akizungumza jambo kwenye mkutano huo uliowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi kuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.
Meneja wa Heineken Afrika Mashariki na Kati, Kayode Adeuja akizungumzia jinsi kufanya biashara na kukuza mtani kama kampuni hiyo ilivyoimarika wakati wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Recency jijini Dar.
Mwezeshaji wa Majadiliano Bi. Catherinerose Barreto(aliyesimama) akitolea ufafanuzi moja ya jambo lililokuwa likijadiliwa katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Hyatt Recency jijini Dar
Baadhi ya wadau wakichangia mada kwenye majadiliano
  Mwenyekiti wa AMSC, Ali Mufuruki akizungumza na waandishi wa habari walivyowakutanisha viongozi wa mashirika na taasisi ili kujadili  uuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference'
Baadhi ya viongozi wa mashirika na taasisi mbalimbali wakifuatilia majadiliano kuhusu ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' kwenye ukumbi wa Hyatt Recency jijini Dar

Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Anna Makinda amesema ukuaji wa uchumi hauwezi kufikiwa endapo hakutakuwa na uwekezaji wa kutosha katika mafunzo kwa rasilimali watu.

Mama Makinda ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kujadili ukuaji wa uchumi 'Business Transforming Africa Conference' ambao umeandaliwa na kampuni ya African Management Services (AMSCOukiwa na lengo la kujadili umuhimu wa mafunzo kwa rasilimali watu katika kukuza uchumi.

Amesema hakuna usawa kati ya ujuzi unaotolewa mashuleni na mahitaji ya soko la ajira jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa ukosefu wa ajira kwa wahitimu wengi ambao hushindwa kukidhi mahitaji ya soko la ajira.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde alisema kuwa  pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau wote wanaoshiriki katika kukuza uchumi ni muhimu kwa wadau hao kwenda sambamba na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ili kuweza kufikia malengo ya pamoja yaliyokusudiwa.

AMSCO imekuwa ikiandaa mikutano ya namna hii kwa lengo la kukuza uchumi wa taasisi, mashirika nchi kwa ujumla.

taarifa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.


WATAALAMU KUPELEKWA VIWANJA VYA NDEGE VYA KUSINI KUJIRIDHISHA

$
0
0
Serikali imesema itatuma wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA), kuangalia Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanja vya ndege katika Wilaya ya Masasi na Tunduru ili kujiridhisha na kushauri Serikali namna ya kutekeleza miradi hiyo. 

Akizungumza mara baada ya kuonyeshwa maeneo hayo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema pamoja na maeneo hayo kutengwa na Wilaya hizo kuna ulazima wa kuwatuma wataalam wa Viwanja ili kuwa na Viwanja bora vinavyozingatia viwango vya kimataifa. 

“Nawapongeza sana kwa kutenga maeneo kwa ajili ya kujengaViwanja vya ndege kwani ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi, hivyo ili kukidhi viwango vilivyowekwa kimataifa katika ujenzi wa viwanja vya ndege nitatuma wataalam kutoka TAA ili kukagua maeneo haya na watoe muelekeo kwa kuishauri Serikali kuhusu utekelezaji wa miradi hii muhimu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa. 

Kuhusu kiwanja cha Masasi Waziri Mbarawa ameiagiza TAA na Halmashauri ya Wilaya yaMasasi kukaa pamoja na kuainisha mipaka ya kiwanja hicho ili kuepuka uvamizi wa miundombinu ya kiwanja hicho. 

Aidha, Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kuiandikia Wizara mahitaji ya eneo hilo na kuainisha sababu ya kuhamisha kiwanja cha ndege cha Tunduru kutoka mjini kwenda nje ya mji. 

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani Mtwara, Bi. Zitta Majinge, amemhakikishia Waziri huyo kuleta maombi ya mapendekezo ya viwanja hivyo makao makuu ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto za viwanja hivyo. 

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Masasi, Bi.  Zita Majige (wa pili kushoto) Kuhusu kuweka mipaka kwenye eneo la kiwanja ili kunusuru uvamizi, mara baada ya kukagua kiwanja hicho, wilayani Masasi.
Muonekano wa Kiwanja cha ndege cha Masasi, ambacho kina uwezo wa kuhudumia ndege za abiria saba mpaka kumi.


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Masasi, Bi.  Zita Majige (wa pili kushoto) Kuhusu kuweka mipaka kwenye eneo la kiwanja ili kunusuru uvamizi, mara baada ya kukagua kiwanja hicho, wilayani Masasi.
Muonekano wa Kiwanja cha ndege cha Masasi, ambacho kina uwezo wa kuhudumia ndege za abiria saba mpaka kumi.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Masasi, Bi.  Zita Majige (wa pili kushoto) Kuhusu kuweka mipaka kwenye eneo la kiwanja ili kunusuru uvamizi, mara baada ya kukagua kiwanja hicho, wilayani Masasi.
Muonekano wa Kiwanja cha ndege cha Masasi, ambacho kina uwezo wa kuhudumia ndege za abiria saba mpaka kumi.

MKURUGENZI MANISPAA YA KINONDONI ATAKIWA KUPELEKA MAMENEJA NA MASHINE ZA KIELEKTRONIC (EFD) KWENYE MASOKO.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh.Ali Hapi amemtaka Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhakikisha anapeleka Mameneja pamoja na mashine za kielektronic(EFD),kwenye masoko kwa lengo la kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea. 

Ametoa agizo hilo jana  alipokuwa akisomewa taarifa ya mapato na matumizi ya Masoko na Mtendaji wa Kata ya Kijitonyama Bi. Elizabeth Minga  ambapo ilionesha upotevu mkubwa wa fedha kwenye masoko hasa soko la wamachinga lililoko Mwenge. 

Amesema fedha nyingi zinapotea kutokana na kutokuwepo utaratibu mzuri wa kukusanya mapato kwenye masoko. 

Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Wilaya amepiga marufuku uanzishwaji wa vikundi vya kiholela vya kusimamia masoko ili kudhibiti upotevu wa mapato unaoendelea.

Kijitonyama ni Kata ya nne kati ya Kata kumi za awamu ya pili zinazotembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni akiongea na Wamachinga wa soko la Mwenge ,Jijini Dares salaam
 Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi akiendelea na ukaguzi soko la Mwenge, Jijini Dares salaam

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 25,2017

BASATA YAOMBA WADAU KUNUNUA SANAA ZA TANZANIA

$
0
0
Kundi la wasanii wa uchoraji la 14+ ikiwa katika maonyesho ya uchoraji picha katika maeneo ya wazi.
Msemaji wa kundi la 14 +, Aman Abeid akitoa maelezo kwa afisa habari wa Barza la Sanaa nchini (BASATA) Agnes Kimwaga wakati wa maonyesho hayo
Mchoraji Nguli wa sanaa za uchoraji, Raza Muhamed akichora wakati wa maonyesho hayo ya uchoraji wa moja kwa moja katika eneo la wazi
Mchoraji Lutengano Mwakisopile akionyesha ufundi wake wa kuchora katika eneo la busatani ya kaburi moja Posta jijini Dar es Salaam
Mchoraji Chilonga Haji akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Baraza la Sanaa nchini (BASATA) limeziomba tasisi za Serikali na mashirika mbalimbali , kununua kazi za Sanaa za uchoraji za wasanii watanzania na kuacha kununua michoro kutoka nje ambayo aina ubora.

Hayo yamesemwa na Afisa habari wa Basata, Agnes Kimwaga alipotembelea maonyesho ya wazi ya uchoraji wa michoro mbalimbali yaliyoandaliwa na kundi la 14 + la hapa nchini.

“Sanaa za uchoraji na uchongaji za hapa nchini zinatengenezwa katika ubora wa hali ya juu ndio maana michoro mingi inayopelekwa nje kutoka hapa inapata sifa kubwa hivyo ni wakati wa taasisi zetu za umma na ofisi za serikali kuanza kupambwa na michoro hii” amesema Agnes.

Kwa upande wake kiongozi wa kikundi cha 14 +, Lutengano Mwakisopile amewataka watanzania kuendelea kuwaonga mkono katika harakati zao hili waweze kujivunia sanaa hiyo kama ilivyo kwa nchi jirani.
Mchoraji Mins Mims akionyesha ufundi wake wa kuchora katika maonyesho hayo
Mchoraji Caludia Chatanda akitoa maelezo kwa watu waliofika katika maonyesho hayo
Mchoraji wa vibonzo Nathan Mpangala akichora mchoro wake mbele ya wadau katika maonyesho hayo ya wazi
Nathan Mpangala akitoa somo kwa wadau wakifika katika maonyesho hayo
Mchoraji kutoka Vipaji House akionyesha umahiri wake wa kuchora katika maonyesho hayo
wanafunzi wakitazama kwa makini moja ya michoro iliyochorwa na wasanii wa kundi la 14+

NAOMBA RADHI KWA VIONGOZI WOTE NILIOWATAJA KWENYE MAZUNGUMZO YANGU NA MAMA SEPETU-STEVE NYERERE.

$
0
0
Msanii wa Filamu na Muigizaji mahiri hapa nchini Steve Nyerere, akizungumza mbele ya Waandishi wa habari mapema leo jijini Dar kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyotokea hivi karikuni ,likiwemo suala la ujumbe wa sauti ambao umekuwa ukisambazwa katika mitandano ya kijamii ukimuhusisha yeye Steve pamoja na Mama Wema Sepetu
''Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu,Maneno yasipindishwe",amesema Steve Nyerere na kuongeza kuwa yeye ana miaka 25 kwenye sanaa, inakuaje leo mtu anatoa ama anasambaza mambo binafsi waliokuwa wakiyazungumza kwa ajili ya kumsaia Mtoto wake.
Msanii wa Filamu nchini Steve Nyerere, leo amekutana na Waandishi wa Habari, ambapo katika mkutano huo amekanusha kuwa Wasanii nchini hawakidai Chama Cha Mapinduzi fedha kwa ajili ya Mradi wa Mama Ongea na Mwanao, wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika Mkutano huo STEVE NYERERE amesisitiza kuwa kilichosemwa na WEMA SEPETU kuwa anaidai CCM fedha ni uongo, kwani walilipwa huku akisema Msanii aliyelipwa fedha nyingi katika kazi hiyo ni Wema Sepetu, hivyo anashangaa kusikia akidai kuwa hajalipwa.

Mradi wa Mama Ongea na Mwanao uliratibiwa na Steven Nyerere huku akisaidiwa na Wema Sepetu na kazi yake ilikuwa ni kutoa elimu kwa wazazi kuwa karibu zaidi na vijana wao wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Hata Hivyo, Steve Nyerere, ametumia mkutano huo kukiri kuwa Sauti iliyotumwa kwenye Mitandao ya Kijamii inayohusisha mazungumzo yake na Mama yake Wema Sepetu ni ya kwake, hivyo amewaomba radhi viongozi wote aliowataja katika mazungumzo hayo.

'Kulikuwa na maongezi ya simu kati ya mimi na mama Sepetu, mimi ndio nilikuwa naogea na mama Sepetu yasipindishwe,"Ile Sauti imekuja kuachiwa juzi wakati watu wanahama chama, kwanini nirekodiwe? naamini wamefanya hivyo makusudi" ,alisema Steve Nyerere

"Namuomba radhi Rais Magufuli na Chama changu cha CCM, yanaongelewa mengi ninayasikia, naomba radhi familia pia, niliteleza,Nimetaja viongozi katika ile sauti halafu mtu anakuja kuisambaza nimetaja viongozi wa Nchi, Mama alichofanya amenikosea sana,Lakini namuachia Mungu"alimaliza kusema.
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images