Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46339 articles
Browse latest View live

MREMA AMSHUKURU RAIS MAGUFULI KWA MATIBABU NCHINI INDIA

$
0
0
 Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza tarehe ya uzinduzi wa bodi mpya ya parole taifa tarehe 3 na 4 Machi 2017 mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Msaidizi wake Bw. Clemence Munisi na kulia ni Mkewe Bi. Rose Augustino Mrema.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema (katikati mwenye kofia) wakati akitangaza tarehe ya uzinduzi wa bodi mpya ya parole taifa tarehe 3 na 4 Machi 2017 mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Eliphace Marwa - Maelezo


Na Eliphace Marwa -Maelezo

Mwenyekiti wa Bodi ya Parole ya Taifa, Dkt. Augustine Lyatonga Mrema amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanikisha safari ya kwenda nchini India kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa afya yake.

Dkt. Mrema ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waaandishi wa habari kuhusu uteuzi uliofanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba kwa kuwateua wajumbe wawili wa bodi hiyo.

“Nachukua nafasi hii kumshukuru Rais Magufuli , Waziri Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Wizara ya Afya na Ikulu, kwa kunipeleka nchini India kufanyiwa uchunguzi wa afya yangu na kupatiwa matibabu na sasa afya yangu imeimarika na niko tayari kutekeleza majukumu yangu”, alisema Dkt. Mrema.

Akizungumzia uteuzi uliofanywa na Waziri Nchemba, Mrema amesema kuwa toka alivyoteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Bodi hiyo haikukaa vikao kutokana na baadhi ya wajumbe wa Bodi hiyo kumaliza muda wao.

“Nilipoteuliwa na Rais kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa, Bodi ilikuwa bado haijakutana na kufanya vikao kwasababu kuna wajumbe walikuwa wamemaliza muda wao na Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa bado hajateua wajumbe wengine lakini kwa sasa amakwisha fanya kazi ya uteuzi”, alisema Dkt. Mrema.

Mrema aliwataja walioteuliwa kuwa wajumbe wa Bodi ya Parole Taifa ni pamoja na Bwana Francis Kistola na Bwana John William Nyoka.

Aidha Mrema amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kukamilisha kazi ya uteuzi na amewapongeza wajumbe walioteuliwa na kuwakaribisha kwa mikono miwili kwenye bodi hiyo na kuomba ushirikiano wao na uzoefu wao ili kukamilisha majukumu ya bodi ya Parole.

Vilevile Mrema amesema kuwa kikao cha kwanza cha bodi mpya ya parole kitafanyika tarehe 3 na 4 Machi 2017 jijini Dar es Salaam na bodi hiyo mpya itazinduliwa siku hiyo na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba.

WACHIMBAJI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KUEPUSHA AJALI MIGODINI

$
0
0
Wachimbaji wadogo wa madini nchini wametakiwa kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama migodini ili kuepusha ajali.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye mgodi wa Musasa uliopo Kata ya Makurugusi, wilayani Chato.

Dkt. Kalemani alisema njia bora ya kuepukana na ajali migodini ni kufanya shughuli za uchimbaji kwa kutii sheria za uchimbaji madini bila shuruti na kuzingatia kanuni za usalama kwenye maeneo ya machimbo na wakati wa shughuli za uchimbaji.

Aliwaasa wachimbaji wadogo wa madini kote nchini kujifunza kutokana na ajali mbalimbali zilizotokea migodini ili kuepuka sababu zilizopelekea kutokea kwa ajali hizo kutojirudia tena kwenye maeneo mengine.

Aidha, Dkt. Kalemani aliwasisitiza wachimbaji wa madini kote nchini kuhakikisha wanafanya shughuli za uchimbaji kwa kutunza mazingira na afya zao pamoja na afya za wengine wanaozunguka machimbo husika.

Alisema suala la mazingira linapaswa kupewa kipaumbele wakati wa shughuli husika, na kwamba ni jukumu la kila mchimbaji na kila anayeishi ama kufanyia shughuli zake maeneo ya machimbo kuhakikisha anaboresha mazingira ili kuepusha majanga mbalimbali ikiwemo ya magonjwa ya mlipuko.

“Chimbeni madini kwa kutunza mazingira na afya zenu ili mpate kufaidi matunda yatokanayo na shughuli hii, alisema Dkt. Kalemani.
Kwa wakati huohuo, Naibu waziri huyo aliwakumbusha wachimbaji wadogo wa madini kulipa kodi na ushuru stahiki ili kuepuka usumbufu.
Aliwahakikishia wachimbaji wadogo wa madini kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa endapo watafuata maelekezo ya sheria.

“Mkitaka kuishi salama na kufanya shughuli zenu bila kubughudhiwa, hakikisheni mnalipa kodi na tozo mbalimbali mnazopaswa kulipa,” alisema.
Dkt. Kalemani alizipongeza kampuni za watanzania zinazomiliki leseni kwenye machimbo hayo ya Musasa ambazo ni Godfrey and Partners, Kilimo Kwanza Group na Hapa Kazi Tu Group kwa kuonesha njia na kutunza usalama kwenye machimbo hayo na hivyo kuwataka wachimbaji wengine kuiga mfano huo.
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa yaliyopo kwenye Kata ya Makurugusi, Wilayani Chato. Nyuma yake ni baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini.
 Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
 Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato.

Serikali yaunga Mkono uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (TDF).

$
0
0
  Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi nyaraka za Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kwa  Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe (kushoto), ambaye ni mjumbe wa bodi hiyo ,katikati ni  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi.Leo Jijini dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akimkabidhi nyaraka za Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kwa  Meneja Mwandamizi wa Benki ya NBC Salmi Rupia(kushoto), katikati ni   Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF)  mara baada ya kuuzindua leo Jijini Dar es Salaam .(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM).

 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea na wadau wa michezo katika  ufunguzi  wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulioanzishwa na  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo  Jijini Dar es Salaam.
  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi akisoma risala wakati  wa ufunguzi  wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulioanzishwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu lengo ikiwa ni kubuni vyanzo mbalimbali vya rasilimali ili kuwezesha shirikisho hilo katika kutekeleza kazi zake.
  Mkuu wa Kitengo cha Ufundi  wa Maendeleo ya Soka nchini Bw. Kim Poulsen akiongea na wadau wa michezo katika uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo  Mhe. Nape Moses Nnauye (kulia) akijadiliana jambo na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi katika hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) leo Jijini .
 Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) kushoto ni  Meneja wa PPF Kanda ya Ziwa Meshack Bandawe, Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Beatrice Singano na kulia ni Meneja Mwandamizi wa Benki ya NBC Salmi Rupia.


Na Lorietha Laurence-WHUSM
Serikali imeunga mkono uwanzishwaji wa Bodi ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu (TDF)  wenye lengo la kuratibu vyanzo mbalimbali vya mapato ili kutekeleza maendeleo ya mpira nchini ikiwemo  kukuza vipaji vya michezo kwa vijana wa kike na wa kiume.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipozindua Bodi hiyo iliyo chini ya uratibu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania leo Jijini Dar es Salaam ambapo aliwataka wadau wa michezo,wananchi na sekta binafsi kuunga mkono jitihada  hizo.
“Jambo hili ni jema sana katika sekta  ya michezo nchini hivyo ni jukumu letu sote kuhakikisha tunaunga mkono juhudi hizi zenye lengo la kuleta matokeo chanya katika sekta hii muhimu mfano mzuri ni vijana wetu wa Serengeti Boys  wameshatuonyesha kuwa tunaweza kufika mbali” alisema Waziri Nnauye.
Aidha, aliitaka Bodi hiyo kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu ili kuhakikisha mfuko huu unakua na hivyo kuwezesha utendaji fanisi wa kukuza vipaji vya michezo wa kike na wa kiume na kwa wale watakaokiuka miiko ya kazi uongozi usisite kuchukua hatua za kinidhamu dhidi yao.
Naye, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu wa Tanzania (TFF) Bw.Jamal Malinzi  alieleza kuwa lengo la kuunda mfuko huo ni kusaidi katika kuendesha shughuli za Shirikisho ambapo kutakuwa na utaratibu maalum wa kuomba fedha kutoka katika mfuko huo.
“Kiutaratibu Sekretrarieti ya TFF ikiwa na mahitaji itakuwa inatuma maombi kwenda bodi na pale bodi inaporijiridhisha na uhalali wa maombi hayo itatoa ruhusa kwa Shirikisho kuendelea na utaratibu wa kupatiwa fedha “alisema Bw.Malinzi.
Bw. Malinzi aliongeza kwa kuahidi kuwa TFF itahakikisha Tanzania inang’ara kimataifa katika mpira wa miguu kwa kufuzu kucheza fainali za kombe la Dunia mwaka 2026 kwa upande wa wanaume (Taifa Stars) na kwa upande wa wanawake (Twiga Stars) 2019.
Akiongea kuhusu kuwekeza katika mpira wa vijana Bw. Malinzi alisema kuwa Msingi mkubwa wa mafanikio ya timu za taifa duniani kote ni kuwekeza katika mpira wa vijana ili kuhakikisha wanafundishwa mpira kwa kiwango cha kimataifa katika umri mdogo utakaowasaidia kuwa imara.
Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) ulirasimishwa rasmi katika Mkutano Mkuu wa TFF wa mwaka 2015 hivyo mfuko huo upo katika katiba ya TFF huku jukumu lake kubwa ikiwa ni kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo vitasaidia Shirikisho hilo katika kutekeleza kazi zake mbalimbali za maendeleo ya mpira wa miguu nchini.

NAMAINGO BUSSINESS AGENCY NA NHIF YAWAKUTANISHA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA TANGA PAMOJA LENGO KUHAMASISHA KUJIUNGA NA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA (NHIF)

$
0
0

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wajasiriamali na Taasisi ya Kibiashara ya Namaingo Bussiness Agency uliokuwa na lengo la kuwahamasisha kujiunga na bima ya Afya na kuhalalisha biashara zao

MENEJA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wajasiriamali na Taasisi ya Kibiashara ya Namaingo Bussiness Agency uliokuwa na lengo la kuwahamasisha kujiunga na bima ya Afya na kuhalalisha biashara zao

Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Bi Ubwa Ibrahima akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wa wafanyabiashara na wajasiamali mkoani Tanga leo

Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Bi Ubwa Ibrahim akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa pamoja.

Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akifafanua namna ya wajasiriamali na wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu kupitia mfuko huo
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akifafanua namna ya wajasiriamali na wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za matibabu kupitia mfuko huo ikiwemo kufanya biashara zinazotambulika kisheria ili kuisaidia serikali kupata mapato


Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wafanyabishara waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Police Mess mkoani Tanga
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akisistiza jambo katika mkutano huo kwa baadhi ya wafanyabiashara namna wanayoweza kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kupata matibabu
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

MAWAZIRI 15 WA NCHI ZA SADC KUKUTANA DAR KESHO

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Mawaziri 15 wa Nchi Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC), wanatarajia kufanya mazungumzo kesho jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa mawaziri hao wanatarajiwa kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo elimu, ushiriki wanchi za SADC, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia haliinayoendelea nchini Msumbiji.

“Tanzani ni mwenyeji na wenyekiti wa Mkutano huo, ambapo pia inaongoza Kitengo Maalumu cha Masuala ya Ulinzi,Usalama pamoja na Siasa, pia kamati ya siasa na diplomasia inatarajiwa kukutana pia wiki hii” alisema Waziri Mahiga

Kila mwaka mawaziri hao hukutana mara moja, kwa lengo la kuzungumzia masuala mbalimbali yanayohusu nchi wanachama wa umoja huo.Katika hatua nyingine, Waziri Mahiga alisema kuwa ,Tanzania inashirikiana na Msumbiji kufanyia kazi suala la watanzania walihamishwa nchini.

“ Hili ni zuala gumu kidogo tusitoe majibu rahisi, na hivyo Serikali zote mbili zinaendelea kufanya mazungumzo zaidi juu ya suala hili” alisema Waziri Mahiga.

Rais Magufuli awapongeza madaktari Muhimbili na amsaidia Neema Mwita Wambura aliyeunguzwa moto kifuani

$
0
0
 Dada Neema Mwita Wambura (32) akizungunza na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu akimshukuru kwa msaada aliompatia wa kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Pia Rais Dkt. Magufuli ameahidi kumpatia hifadhi mama huyo pamoja na watoto wake watatu ambao kwa sasa wapo Bunda mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpatia msaada Dada huyo kiasi cha Shilingi laki tano.  Dada Neema Mwita Wambura aliungua vibaya mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa unachemka jikoni na mume wake katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara.
 Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) ambaye amempa hifadhi Neema Mwita Wambura nyumbani kwake Tandika Davis Corner akiomba dua kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kupitia njia ya Simu kumshukuru mara baada ya kuzungumza naye kuhusiana na kumsaidia Dada Neema Mwita Wambura (32). Rais Dkt. Magufuli amempongeza Mama huyo Mjane ambaye ameonesha moyo wa kizalendo na kumpa hifadhi Dada huyo aliyemwagiwa uji wa moto na mumewe katika kijiji cha Kyagata, Tarime mkoani Mara. Pia Rais Dkt. Magufuli alimpa Mjane huyo kiasi cha Shilingi laki tano.
  Dada Neema Mwita Wambura (32) wakwanza kulia akiwa pamoja na Mama Mjane Mariam Amir ( Bibi Mwaija ) wakiwa ndani ya gari mara baada Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kumsaidaia ili aweze kufanyiwa tena uchunguzi wa afya yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakimpokea Dada Neema Mwita Wambura (32) na kuanza mara moja kumfanyia tena uchunguzi wa afya yake katika majeraha aliyoyapata mara baada ya kumwagiwa uji wa moto uliokuwa ukichemka jikoni  kitendo kilichofanywa na mume wake.
 Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Lawrence Museru akimjulia hali Dada Neema Mwita Wambura (32) mara baada ya kufikishwa tena hospitalini hapo. Dada Neema Mwita alifanyiwa upasuaji mara nne katika siku za nyuma hospitalini hapo Muhimbili ili kutibu majeraha yake hayo ya moto.
 Daktari Bingwa wa magonjwa ya dharura na Ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga akizungumza kuhusu hali ya mgonjwa Dada Neema Mwita Wambura (32) aliyefikishwa tena katika Hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi wa Afya yake.
 Dada Neema Mwita Wambura (32) akiwa katika hali ya majonzi kufatia majeraha makubwa mwilini mwake kufatia kumwagiwa uji wa moto na mume wake mkoani Mara.
Daktari Bingwa wa upasuaji wa ngozi kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  Dkt. Ibrahim Mkoma akizungumzia historia ya mgonjwa huyo ambaye yeye pamoja na jopo la madaktari bingwa walimfanyia upasuaji ili kutibu majeraha yake ya ngozi katika kipindi cha nyuma. PICHA NA IKULU.

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewapongeza Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa juhudi kubwa walizofanya kunusuru maisha ya Neema Mwita Wambura ambaye alijeruhiwa kwa kuunguzwa na maji ya moto kifuani, shingoni na mkononi. 

Pongezi hizo za Mhe. Dkt. Magufuli zimetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bw. Gerson Msigwa muda mfupi baada ya kumfikisha Neema Mwita Waitara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako Rais Magufuli ameagiza apelekwe kwa mara nyingine kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa maendeleo ya afya yake. 

Katika Pongezi hizo Mhe. Dkt. Magufuli amesema Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wamefanya kazi kubwa na ya kizalendo kuhakikisha Neema anapona licha ya majeraha makubwa aliyoyapata miaka miwili iliyopita na ambayo yalitishia uhai wake. 

Pia Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mama Mariam Amir (Bibi Mwanja) kwa upendo wake wa kumchukua Neema na kisha kumpa hifadhi nyumbani kwake huko Tandika Devis Kona Jijini Dar es Salaam. 

“Nakushukuru sana Mama na ninakupongeza, umeonesha mfano mzuri wa kujali umoja na upendo kwa Watanzania wenzako bila kujali dini, kabila wale kanda unayotoka na hivi ndivyo Watanzania wote tunapaswa kufanya” amesema Mhe. Rais Magufuli. 

Kabla ya kutoa pongezi hizo, mapema leo asubuhi Mhe. Rais Magufuli amewatuma wasaidizi wake wakiongozwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Bw. Gerson Msigwa kwenda Tandika Devis Kona katika Wilaya ya Temeke Jijini Dar es Salaam kumuona Neema Mwita Wambura ambaye alipatiwa hifadhi katika nyumba ya Mama Mjane aitwaye Mariam Amir (Bibi Mwanja) baada ya kuona picha na kusoma taarifa za mkasa uliomkuta katika mitandao ya kijamii. 

Mhe. Rais Magufuli ametoa Shilingi laki 5 kwa Neema kwa ajili ya kumsaidia chakula yeye na watoto wake waliohifadhiwa na rafiki yake huko Bunda Mkoani Mara na pia ametoa Shilingi laki 5 kwa Mariam Amir aliyejitolea kumsaidia na kumpa hifadhi nyumbani kwake. Pia ameahidi kumsaidia wakati wote wa matibabu na pia familia yake. 

Baada ya kumpokea daktari bingwa wa magonjwa ya dharula na ajali katika kitengo cha dharula cha Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Juma Mfinanga amesema wameanza kumfanyia uchunguzi ili kujua maendeleo yake na kama kumpa matibabu zaidi. 

Nae Daktari Bingwa wa Upasuaji Dkt. Ibrahim Mkoma ambaye amekuwa akimfanyia matibabu Neema Mwita Wambura tangu Julai 2015 alipofikishwa hospitalini hapo kwa mara ya kwanza amesema Neema anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji mara nne. 

Dkt. Mkoma amesema baada ya upasuaji huo, sasa Neema anaweza kuinua na kugeuza shingo yake na kwamba kwa sasa wataendelea kumfanyia uchunguzi zaidi ili kujua maendeleo yake. Mhe. Rais Magufuli ameagiza vyombo vyote vinavyohusika kufanyia kazi mkasa uliomkuta Neema Mwita Wambura na kuhakikisha haki inatendeka.

RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI ASHIRIKI MAADHILISHO YA MIAKA 25 YA CSSC

$
0
0
 Rais Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitembelea  mabanda mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 25 ya Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) yaliyofikia kilele siku ya tar 22/02/2017 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam
   Rais Mstaafu Mzee Mwingi akiwa katika Banda la Elimu la "Life Oriented Approach (LOA)" , njia ya ufundishaji wa Elimu ya awali, katika mradi unaotekelezwa na Kanisa Katoliki katika Majimbo ya Arusha na Same
 Mkuu wa Shirika la "Pressures Blood" Tanzania Padre Chesco Msanga, akimkabidhi zawadi ya picha Rais Mstaafu Mzee Mwinyi kama kumbukumbu alipoifungua Hospital ya St. Gaspar Itigi inayoendeshwa na shirika hilo
 Mzee Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC)
 Rais Mstaafu Alhaji Ally Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake katika siku ya kilele ya kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 25 tangia kuanzishwa kwa Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii Tanzania
Mzee Mwinyi akitoa Cheti kwa  Profesa Costa Mahalu, moja ya watu waliyotoa msaada mkubwa wa masuala ya Sheria kipindi Tume hiyo ilipokuwa inaanzishwa


Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya pili, Alhaji Alli Hassan Mwinyi, ameipongeza Tume ya Kikristu ya Huduma za Jamii (CSSC) kwa kutimiza miaka 25 tangu ilipoanzishwa mwaka 1992.  Akiongea katika maadhimisho hayo, Mzee Mwinyi amesema kuwa Serikali imekuwa ikitambua na kuthamini mchango wa makanisa na Taasisi za dini katika kuboresha huduma za Jamii.

“Nimefarijika sana kwa kupata taarifa kuwa hadi kufikia Septemba 2016, hospitali za Kanisa 87 na vituo vya afya 45, vimeingia Mkataba na Serikali katika kutoa huduma za afya”, alisema Rais Mstaafu Mwinyi.

Katika hatua nyingine, Mzee Mwinyi aliongeza kuwa kwa upande wake yeye amekuwa mstari wa mbele kwa kuwaasa ndugu jamaa na marafiki zake na Watanzania wote kwa ujumla, kutumia huduma zitolewazo na hospitali za kanisa kwa kuwa wanatoa huduma bora, kwa kuzingatia upendo
“ Ikiwa mnaona kazi zinawazidia na mnafikia sehemu mnanung’unika kwa kuzidiwa na kazi nyingi, basi ningesema mgomvi wenu ni mie. Maana nawaambia ndugu na Watanzania wenzangu, kuwa huduma nzuri za afya zinapatikana katika hospitali za Kanisa, kwa kuwa unahudumiwa kwa upendo pamoja na tabasamu,” aliongeza Rais Mstaafu, Mwinyi.

Rais Mstaafu Mwinyi alimuomba Rais wa Tume aendelee kupanua na kuboresha huduma za jamii, kwa utaalamu na ubunifu huku akiwaasa watumishi wa sekta hiyo, kutofanya kazi kwa mazoea.  Aliongeza kuwa uamuzi wa kuanzisha Tume hiyo ulikuwa ni wa busara sana kwa manufaa ya Watanzania walio wengi.

Mheshimiwa Rais Mstaafu pia aliongezea kuwa Tume imefanya kazi kubwa ya kutekeleza majukumu na malengo yake, kwani kwa taarifa alizo nazo ni kuwa katika sekta ya elimu, idadi ya shule za makanisa imeongezeka  kutoka 350 mwaka 1997, na kufikia takribani 1000 mwaka 2016, wakati katika Afya kutoka idadi ya taasisi za afya 500 mpaka 900 kwa sasa.  Alipongeza kwa mafanikio haya makubwa yaliyopatikana ndani ya miaka hii 25 ya utendaji wa Tume.

Katika hatua nyingine, ameiomba Tume kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na Serikali katika kuboresha uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya rasilimali kwani ni chache na zinahitajika kutumiwa na Watanzania wengi wenye uhitaji pia.

Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC) ni chombo kilichoundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) mwaka 1992 kwa dhumuni la kuratibu na kusimamia huduma za kijamii zitolewazo na Taasisi za Makanisa husika za Elimu na Afya nchini.

RAIS MUSEVENI KUWASILI NCHINI JUMAMOSI

$
0
0

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili nchini kuanzia Jumamosi wiki hii.

Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuendeleza uhusiano mzuri uliopo baina ya Uganda na Tanzania, pamoja na kujadili masula mbalimbali ya kikanda, kimataifa na sekta mbalimbali za ushirikiano kati ya nchi hizi mbili hususani katika sekta za nishati, biashara na uchukuzi.

“ Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Uganda yameendelea kuimarika katika miaka ya hivi karibuni, ambapo mwaka 2016 Tanzania ilifanya mauzo nje kwa Nchi hiyo ya kiasi cha shilingi bilioni 66.849, ikilinganishwa na shilingi bilioni 78.31 za mwaka 2015” alisema Waziri Mahiga.

Aliongeza kuwa Uganda ni muhimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo haina Bandari na hivyo inategemea Tanzania kwa ajili ya kupitisha mizigo yake.

Nchi ya Uganda imezidi kuwa na umuhimu kufuatia uamuzi wa kupitisha bomba la mafuta nchini Tanzania, kutoka Kabaale –Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, ambapo bomba hilo lina urefu wa kilimeta 1443 na kipenyo cha inchi 24.Bomba hilo la mafuta litakalokamilika mwaka 2020 limnatarajiwa kupatia nchi hizi mbili fursa mbalimbali.

“ Utekelezaji wa mradi huu utafungua fursa za ajira kwa watanzania, kuchochea shughuli za kiuchumi kwa mikoa inayopita bomba hilo, pamoja na kufungua ukanda wa biashara wa kaskazini mwa Tanzania na Uganda pamoja na kuimarisha uhusiano katika soko la Afrika Mashariki” alifafanua Waziri Mahiga.

Katika hatua nyingine, Waziri Mahiga alisema kuwa kuhusu mgogoro wa nchini Burundi, kumekuwepo na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Rais Museveni pamoja na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa ili kuhakikisha amani inarejea nchini humo.

Katika ziara hiyo ya Rais Museveni nchini, atapokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Johm Magufuli ambapo atatembelea Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maboresho yaliyofanywa katika bandari hiyo, pamoja na Kiwanda cha kutengeneza Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es salaam.

ZIFAHAMU FAIDA ZITOKANAZO NA RASILIMALI ZA BONDE LA MTO NILE KWA TANZANIA

$
0
0


Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

Mto Nile ni miongoni mwa mito mikubwa iliyopo upande wa Mashariki ya Bara la Afrika naDuniani kote ukiwa na urefu wa kilomita 6,695 ambapo beseni ya Nile hukusanya maji ya eneo linalojumuisha 10% za eneo la Afrika yote.

Kwa muonekano wa juu Mto Nile unaonekana kama pembetatu wakati upande wa chini wa eneo la Nile (Kaskazini) na upande wa juu (Kusini) kuna mimea mbalimbali inayoota kwa wingi pia katika kipindi cha mwisho wa mwaka eneo la mto Nile huwa linakuwa na mwonekano mwekundu na kuwa na maua yanayojulikana kama lotus flowers.

Japokuwa mimea hii haioti kwa wingi wakati huu kama ilivyokuwa hapo awali, mimea inayoota kwa wingi katika eneo la Mto Nile kwa upande wa chini ni yale yanayojulikana kama Egyptian lotus na kwa upande wa juu hujawa na mimea inayoitwa Cyperus papyrus.

Chemchemi za Nile ni mito yote inayopeleka maji kwenda Ziwa Viktoria katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Uganda na Kenya na kwa upande mwingine wa Nile unaanzia Ethiopia ukiitwa Abbai au Nile ya Buluu unatoka katika Ziwa Tana wakati chanzo cha mbali kabisa ni mto wa Luvironza huko Burundi unaoingia katika mto wa Kagera na kufika Ziwa Viktoria.

Mto huo ambao unaanzia Ziwa Victoria nchini Tanzania, ni chanzo  kikubwa cha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, viwandani, kilimo cha umwagiliaji na kuzalisha umeme kwa wakazi wa nchi za bonde hilo.

Kutokana na nchi nyingi kuzungukwa na mto Nile, suala la ushirikiano katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto huo limepewa kipaumbele ili kuzuia migogoro inayoweza kuzuka baina ya nchi ambazo wanatumia mto huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia shughuli za wanachama wa Bonde la Mto Nile (NBI), Innocent Ntabana anasema kuwa azma ya kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto Nile limepewa kipaumbele na nchi zote zinazozungukwa na mto huo, jambo hilo ndilo limesababisha kuanzishwa kwa Sekretarieti ya NBI mwaka 1999 jijini Dar es Salaam.

NBI ina jukumu la kusimamia na kuendeleza rasilimali za maji za Bonde la Mto Nile kwa niaba ya nchi wanachama zipatazo 10 ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Sudan, Sudan ya Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Misri,” anasema Ntabana.

Kwa upande wa Mratibu wa Kanda wa Kitengo cha Uratibu cha Bonde la Mto Nile (NELSAP-CU), Elicad Nyabeeya anasema kuwa mto huo una manufaa makubwa kwa nchi wanachama kwani muunganiko wa nchi hizo umeleta mawasiliano mazuri ambayo yanapelekea kuinua uchumi wa nchi hizo pia kwa upande mwingine uwepo wa ushirikiano huo umesaidia nchi wanachama kufahamu tamaduni za watu tofauti tofauti.

Nyabeeya anakaririwa akisema kuwa “Nchi ya Tanzania inafaidika kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na NBI kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya ujenzi wa bwawa la Bisrawi na usanifu wa bwawa la Borenga, mkoani Mara”.

Kwa mujibu wa Nyabeeya, nchi hii itanufaika na miradi ya maji na nishati ya umeme, pamoja na miradi mingine mingi ambayo NBI inaendelea kuitekeleza kama vile ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme wa Rusumo na umwagiliaji katika mabonde ya mito Kagera na Ngono iliyopo mkoani Kagera.

Anaendelea kufafanua kuwa mradi wa umeme wa Rusumo utazalisha megawati 80 za umeme ambazo zitatumiwa na nchi za Tanzania, Rwanda na Burundi ambapo Tanzania inatarajiwa kupata megawati 16.

Miradi mingine ni ya kuunganisha umeme kutoka Ethiopia, Kenya hadi Tanzania, mradi wa umeme kati ya Tanzania na Zambia.

Aidha, NBI wanatarajia kukamilisha upembuzi yakinifu wa kina wa miradi ya Mara na Ngono ifikapo mwezi Aprili mwaka huu ambapo wananchi 20,000 pamoja na hekari 13,630 katika vijiji 21 vinatarajiwa kunufaika na mradi wa Ngono wakati Bonde la Mara litanufaisha wanachi 10,000. Miradi hiyo itahusisha usambazaji wa maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani, mifugo na shughuli za umwagiliaji.
Wakati huo, Bwawa la Borenga litakuwa likisambaza maji katika Bonde la Mara kwa wakazi wa vijiji 13 kwa ajili ya umwagiliaji na 17 vitapata maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na mifugo.
Madhumuni ya miradi hiyo ni kuhakikisha kunakuwa na upatikanaji wa maji ya uhakika, kuimarishwa kwa soko na mahusiano na kukuza sekta binafsi, kilimo, usalama wa chakula na kupunguza umaskini.
Kutokana na kuwepo kwa umuhimu wa rasilimali za Bonde la mto huo, iliamuliwa kuwa Februari 22 ya kila mwaka iwe ni siku rasmi ya kuadhimisha uanzishwaji wa muunganiko wa matumizi ya pamoja ya rasilimali za mto huo baina ya nchi 10 wanachama .
Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Sylvester Matemu amesema kuwa lengo la Siku ya Nile ni kukuza uelewa kwa watu wote kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote wanachama, masuala yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali za Bonde la Mto huo.  
“Maadhimisho ya siku ya Nile kuadhimishwa katika nchi fulani ni tukio la kihistoria kwasababu ni tukio ambalo halifanyiki katika nchi moja kila mwaka hivyo kwa vile nchi wanachama tuko 10 basi  linatokea mara moja kila baada miaka 10,”anasema Mhandisi Matemu.
Maadhimisho ya 11 ya Siku ya Nile kwa mwaka huu yameadhimishwa nchini Tanzania kwa ushirikiano wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji pamoja na Sekretariati ya Nile Basin Initiative (NBI) ambapo mgeni rasmi wa maadhimisho hayo alikuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 600 wakiwemo Mawaziri wa nchi wanachama kutoka kwenye nchi husika, mabalozi mbalimbali, wabunge, watu kutoka taasisi na mashirika mbalimbali pamoja na wanafunzi wa shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Vikuu.
Shughuli hizo zilianza kwa maandamano yaliyoongozwa na Bendi ya Polisi kuanzia Viwanja vya Mnazi Mmoja hadi Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambako maonesho pamoja na ufunguzi rasmi wa maadhimisho hayo vilifanyika.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA GUINEA CONAKRY

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa zamani wa Guinea Conakry Mhe. Kabine Komara ambaye sasa ni Balozi wa Taasisi ya Maendeleo ya Bonde la Mto Senegal, Ikulu jijini Dar es salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika jijini Abidjan, Ivory Coast

$
0
0
Rais Mstaafu na  Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa za ELimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina alipomtembelea katika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast.
Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha kwa Rais Adesina ripoti ya Kamisheni ya Elimu na kuwasilisha rai ya Kamisheni hiyo ya kuiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia nchi za Afrika kugharamia miradi na mageuzi ya sekta ya elimu katika nchi zao. 

Rai hiyo ya Kamisheni inatokana na ripoti kubaini kuwa misaada na mikopo inayotolewa kwa sekta ya elimu imekuwa ikishuka ikilinganisha na zile zinazotolewa kwa miradi ya afya na miundombinu. Kamisheni inaamini kuwa bila kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, watoto wapatao milioni 223 duniani (takribani milioni 160 wakiwa Afrika) watakosa fursa ya kupata elimu ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Rais Adesina ameupokea ujumbe huo na kusema kuwa takwimu zilizoibuliwa na Ripoti ya Kamisheni 'zinakatisha tamaa na pia zinatoa changamoto'. Rais Adesina ameahidi kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika itaitizama Ripoti hiyo na mapendekezo yake na iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Kamisheni katika kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo katika elimu barani Afrika. Amesema kuwa Benki yake inatambua kuwa kuwekeza katika vijana na nguvu kazi ya Afrika ndio jawabu la maendeleo ya uhakika huko mbeleni.
Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Makhtar Diop pembezoni mwa mkutano wake na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Ziara ya Rais Mstaafu nchini Ivory Coast itahitimishwa kwa kukutana na Rais wa Ivory Coast Mhe. Alassane Ouattara.
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya ELimu, Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa kwa furaha na mwenyeji wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina ofisini kwake jijini  Abidjan, Ivory Coast
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha ripoti ya Kizazi cha Elimu kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Adesina
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt, Makthar Diop pembezoni mwa mkutano huo.

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI AHUDHURIA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT USIKU HUU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Augustine Mahiga
  Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Augustine Mahiga
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Augustine Mahiga
Keki ya hafla hiyo  ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. 
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kulia kwake  ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Augustine Mahiga.

Prof.Mkenda aelezea vituo vya pamoja vya forodha mipakani na umuhimu wake kwa uchumi wa nchi

$
0
0
 Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda, Akihojiwa na Watangazaji mahiri wa TBC Taifa, Paul Alphonce na Anna Mwasyoke, Mikocheni Jijini Dar es salama, mapema leo asubuhhi, ambapo mada iliyokuwa mezani ni kuanza kutumika kwa Kituo cha Pamoja cha Forodha mpaka ni Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia) pamoja na umuhimu wake katika uchumi wa Taifa.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda, Akihojiwa na Watangazaji  wa TBC1, Chunga Runza, Mikocheni Jijini Dar es salama, mapema leo asubuhhi, ambapo mada iliyokuwa  mezani ni kuanza kutumika kwa Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia) pamoja na umuhimu wake

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO IJUMAA FEBRUARY 24,2017

Friedkin Conservation Fund yachangia Saruji mifuko 3000 na Mabati 1000 Simiyu

$
0
0
Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia) shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 ikiwa ni msaada. Wengine ni viongozi mbalimbali walioshiriki katika tukio hilo Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Pratik Patel akizungumza katika tukio la kampuni hiyo kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni hiyo kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kampuni hizo yaani Mwiba Holdings pamoja na Tanzania Game Trackers pia zimekubali kusaidia mabati 1000 kama msaada Mkurugenzi wa Friedkin Conservation Fund (FCF), Abdulkadir Mohamed (kulia) akimtamkia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) kuwa mbali na kampuni hiyo kutoa mifuko 3000 ya saruji kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Wataongeza msaada wa mabati 1000. Wengine ni Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa FCF, Pratik Patel (wa pili kulia) wakishuhudia tukio hilo.

 KAMPUNI kitalii zilizo chini ya Friedkin Conservation Fund (FCF) Tanzania iliyowekeza katika pori la Makao wilayani Meatu na Maswa Mkoani Simiyu imechangia mifuko 3000 ya saruji na mabati na 1000 kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani humo. Misaada hiyo yenye thamani ya zaidi ya sh milioni 70 imetolewa na kampuni hizo ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa serikali ya awamu ya tano ya Rais Dk. John Magufuli kuendeleza elimu ya hasa katika maeneo ya wafugaji ambako kampuni hizo zinafanya shughuli za uwindaji wa kitalii. 

Kampuni zilizokabidhi misaada hiyo juzi katika sherehe zilizofanyika mjini hapa ni pamoja na Mwiba Holdings na Tanzania Game Trackers ambazo kwa pamoja zimetoa saruji hiyo yenye thamani ya sh milioni 48 na mabati yakiwa na thamani ya sh milioni 25. Vifaa hivyo vya ujenzi vitatumika kujenga vyumba vya madarasa na mabweni kwa ajili ya shule zitakazotumiwa na watoto wa jamii za wafugaji zinazoishi jirani na maeneo ya shughuli za uwindaji wa kitalii wilayani Meatu katika mkoa wa Simiyu. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto) akifurahia tamko la Mkurugenzi, Abdulkadir Mohamed (hayupo pichani) kuahidi kuongeza msaada wa mabati 1000 huku Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akikabidhiwa kipaza sauti kurudia kauli ya neema za mabati 1000 toka FCF. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meatu (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kampuni ya FCF kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka pamoja na Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack.

 Akizungumza kabla ya kumkabidhi mchango huo Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, wakati wa hafla iliyofanyikia katika viwanja vya stendi Mjini Mwanhnuzi, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Abdulkadir Mohamed alisema kuwa mchango huo unatokana na kuanzishwa kwa mfuko uwekezaji katika pori hilo. "Tunatoa msaada huo ikiwa ni kuunga mkono Serikali yetu ya awamu ya tano katika jitihada za kuimarisha sekta ya elimu nchini,na tumeanza kuwasaidia wananchi tunaoshirikiana nao katika shughuli za uhifadhi na huu ndio mwanzo wa kuendeleza ushirikiano huu ikiwa ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii,” alisisitiza Mkurugenzi huyo .

Alisema kuwa pamoja na kuchangia misaada hiyo,kampuni yake imekuwa ikitoa misaada katika vijiji tisa vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi za Wanyama Pori Makao (WMA) na ranchi ya Mwiba hasa katika kusaidia uboreshaji wa huduma za jamii na hasa elimu. 

“ Mpaka sasa Kampuni kupitia makampuni yake matatu tayari wamechangia kiasi cha sh Milioni 3000 kwa vijiji tisa pamoja na vingine 15 vinavyopakana pori hilo, ambapo shule, zahanati, pamoja na vituo vya maendeleo vimejsengwa katika vijiji hivyo kwa kushirikiana na halmashauri” Alisema Mohamed.

 Aidha, aliongeza kuwa mchango huo umechangiwa na mafanikio mazuri ya shughuli za utalii zinazoendelea katika maeneo hayo na uwekezaji wa kampuni hiyo wilayani humo, huku akibainisha kuwa shughuli hizo zinazidi kupanda kila mwaka wilayani humo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiongozana na wageni wake katika hafla hiyo. Miss Universe Tanzania 2016/17, Jihan Dimack akijitambulisha katika hafla ya FCF kukabidhi shehena ya mifuko 3000 ya saruji ikiwa ni jitihada za kusaidia ujenzi wa shule za sekondari wilayani Meatu.

Mkurugenzi huyo aliahidi kuwa kutokana na kuimarika kwa shughuli hizo na kuwepo kwa mazingira mazuri ya uwekezaji,hasa ushirikiano wanaoupata kutoka kwa wananchi, hasa wavijiji vinavyopakana na pori hilo, wamepanga kuongeza uwekezaji wao kwa dola za kimarekani milioni 100. Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mkoa (CCM) Leah Komanya alipongeza mchango wa mwekezaji huyo, huku akiunga mkono kwa kuchangia mabati 50 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni shule ya sekondari Makao. 

“ niwaombe hawa wawekezaji wetu wasichangie kwenye vijiji hivyo tisa peke yake, bali wachangie hata kwenye kata nyingine za wilaya yetu ambayo ipo chini sana kielimu ili kila mwananchi atambue mchango wao, na niwapongeze kwa kuunga mkono ujenzi wa shule hasa mabweni kwa watoto wa kike” 

Alisema Komanya Mkuu wa mkoa wa Simiyu, akizungumza kabla ya kupokea msaada huo, alimtaka Mkurugenzi huyo ambao alidai kuwa wamekuwa chanzo cha migogoro ya kila mara kati ya wananchi na kampuni hiyo ili kurejesha imani ya kuendelea kushirikiana na wawekezaji hao. Mbali na hilo Mtaka alipongeza Kampuni hiyo kwa mchango wake, huku akielelekeza saruji hiyo pamoja na mabati vitumike kwa ajili ya kujenga mabweni katika shule za sekondari zinazopakana na pori hilo.

 Mtaka aliwataka wawekezaji hao kuwa karibu na wananchi kwa kushirikiana na watendaji wa halmashauri na alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo kuwapatia kiwanja cha kujenga ofisi ili iweze kuratibu kwa karibu ushirikiano huo na wananchi. 

Kwa sasa mgogoro uliodaiwa kuwapo kati ya mwekezaji huyo na wanakijiji wa Makao, umemalizika baada ya msuluhishi aliyeteuliwa na pande zote mbili, Jaji Thomas Mihayo, kutoa uamuzi hivi karibuni baada ya walalamikaji kushindwa kuwasilisha utetezi wao kwa wakati. Hata hivyo, taarifa zimeeleza kwamba hali hiyo imetokana na kurejea kwa mahusiano kati ya pande hizo mbili na kuonekana njia bora zaidi ya kusuluhisha migogoro ni mazungumzo yasiyo na gharama zinazoweza kuigharimu serikali ya kijiji na wilaya.

MISA YA KUMBU KUMBU YA MAREHEMU MAMA JOYCE KALLAGHE

$
0
0
Familia ya marehemu Balozi Cecil A Kallaghe itakuwa na misa ya kumbukumbu ya marehemu mama Joyce B Kallaghe, aliyefariki tarehe 1 Februari 2017. Misa itafanyiks nyumbani kwa marehemu Mbezi kwa Msuguri siku ya Jumamosi tarehe 25 Februari 2017 saa 3 asubuhi. Wote mnakarbishwa.

TPDC WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

$
0
0
Wanahabari mkoa wa Iringa walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa.

Wanahabari mkoa wa Njombe walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa 
Wanahabari mkoa wa Ruvuma walioshiriki warsha ya siku moja ya gesi asilia wakiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela wa tatu kutoka kushoto na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka TPDC,warsha iliyofanyika ukumbi wa VETA Iringa kwa kushirikisha wanahabari kutoka mkoa wa Njombe ,Ruvuma na wenyeji Iringa 
Meneja mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu (TPDC) akitoa neno wakati wa utangulizi wa warsha hiyo kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Ruvuma.



Na Fredy Mgunda,Iringa.


Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.

“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa kwa kuona umuhimu wa vyombo vya habari katika kupata uelewa mpana wa Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi ili waweze kuhabarisha na kuelimisha watanzania kwa ujumla ili watambue shughuli za shirika na faida zake haswa katika uchumi wa nchi”, alieleza Mkuu wa Wilaya.

Aidha Mh Kasesela amewaomba Waandishi wa Habari kuwa wazelendo katika kuisaidia Serikali kutekeleza miradi mbalimbali yenye maslahi mapana katika maendeleo ya nchi yetu. ‘’Waandishi Wahabari mnapaswa kuisaidia Serikali katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye tija kwa uchumi wa Taifa, mfano katika vita ya kiuchumi ya kugombania mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda kati ya Tanzania na Kenya, wenzetu Kenya walijitahidi kuandika habari zenye kutoa wasifu wa nchi yao ili kuisaidia kupata mradi huo, hivi ndivyo mnavyopaswa kufanya kazi kiuzalendo.”

Aliongeza kuwa leo hii mmeweza kuifahamu TPDC sasa mnapaswa kuwaeleza wananchi miradi inayofanywa na Shirirka hili na manufaa yake katika uchumi wa Taifa, mwende mkatafiti namna mradi wa bomba la mafuta utakavyonufaisha wananchi wanaoishi kando ya njia ya bomba hilo, vilevile namna bomba hilo litakavyosaidia kukuza uchumi wa nchi, hivi ndivyo tunavyoweza kujenga nchi yetu kupitia taaluma ya uandishi wa habari.

Kasesela alisisitiza kuwa ili tujenge Taifa imara ni vyema tuandike habari kwa weledi, uzalendo huku tukiondoa tofauti zetu za kiitikadi ziwe za kikabila, kisiasa au kidini kwa namna hii tutaweza kuandika habari zenye kujenga nchi yetu na si vinginevyo.

Alisisitiza vile vile juu ya utoaji taarifa mapema pale mtu anapoona kuna hujuma au uharibifu wa aina yoyote katika miundombinu hii, akiongea katika warsha hiyo alisema “miundombinu hii ya gesi na mafuta ni mali ya watanzania hivyo kuilinda ni jukumu letu sote kama wazalendo wa nchii hii”.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, Afisa mahusiano wa Shirika la Maendeleo ya Petroli na gesi Tanzania Maria Mselemu alisema warsha hii inalenga kuendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wetu wa habari kuweza kuripoti kwa umahiri na ustadi habari za mafuta na gesi. 

Mselemu aliwashukuru waandishi wa habari kwa juhudi zao za kuupasha habari umma na kuwaasa kwamba kalamu yao ina nguvu hivyo ni vyema ikaendelea kutumika kujenga uchumi wa Taifa kwa kutoa taarifa sahihi kila wakati.Katika taarifa yake Faustin Kayombo kutoka mkondo wa juu (TPDC) alisisitiza juu ya matarajio yasiyo halisia yaliyopo miongoni mwa wanajamii na kuwaomba waandishi wa habari kusaidia kuwaeleza wananchi juu ya uhalisia wa sekta. 

Kayombo alisema kwamba uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi ni wa gharama kubwa na hata mafaniko kwa maana ya mapato makubwa kwa Serikali huchukua muda mrefu kuonekana. 
Akitolea mfano mradi mkubwa wa kusindika gesi asilia (Liqufied Natural Gas-LNG), Kayombo alifafanua kwamba itachukua takribani miaka 8 hadi 10 kabla ya mzigo wa kwanza wa LNG kusafirishwa kwenda katika soko la dunia kwa mauzo. 


Hata hivyo Kayombo alisisitiza juu ya ushiriki wa wazawa katika sekta hii hususan katika kutoa huduma na kuuza bidhaa. 

Naye mwanasheria wa TPDC Barnabas Mwashambwa alisema sheria mpya ya petroli ya mwaka 2015 inawataka wawekezaji wote kutumia bidhaa zinazozalishwa hapa nchini na kama ikitokea bidhaa hizo hazipo nchini basi kampuni iingie ubia na kampuni ya kizawa ili kuweza kutoa huduma inayohitajika.

Sheria imeeleza kwamba ubia huo lazima umpe mzawa ushiriki usiopunguza asilimia 25%, hii ni fursa kwa wazawa na ni vyema ikachangamkiwa. Hata hivyo Mwenyekiti wa Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa frank leornad ameliomba Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kutenga muda wa kutosha zaidi katika uelimishaji ili walengwa waweze kuelewa vyema sekta, ombi ambalo liliungwa mkono na Mkuu wa Wilaya.

Katika mafunzo hayo waandishi wa habari walipata fursa ya kujifunza kuhusu maendeleo ya Sekta Ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Gesi Asilia na Faida Zake, Mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanga na Usambazaji wa Gesi Asilia Majumbani, Viwandani na kwenye Vituo vya Kujaza Magari. 

TPDC imeendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ikiwa na lengo la kuongeza uelewa zaidi katika sekta hii mpya na changa ya mafuta na gesi hapa nchini.

Tata Motors wazindua toleo jipya la basi na lori la mizigo ya Tata Ultra jijini Dar es Salaam

$
0
0
 Maofisa wa kampuni ya magari ya Tata Motors, wakioneysha magari mapya aina ya Tata Ultra Truck na Tata Ultra Bus wakati wa uzinduzi rasmi wa magari hayo jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Magari cha Kampuni ya Tata Africa Holdings (T) Ltd, Prashant Shukla (wa tatu kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa toleo jipya la gari la abiria na la mizigo la Tata Ultra jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara ya Magari cha Kampuni ya Tata Africa Holdings (T) Ltd, Prashant Shukla (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa toleo jipya la gari la abiria na la mizigo la Tata Ultra jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo.
 Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa kampuni ya magari ya Tata Motors,   Rudrarup Maitra (kushoto), akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa toleo jipya la gari la abiria na la mizigo la Tata Ultra jijini Dar es Salaam. Kushoto kwake ni baadhi ya maofisa wa kampuni hiyo.
Wasanii wa kikundi cha Mama Afrika wakitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa magari mapya ya Tata Ultra Truck na Tata Ultra Bus jijini Dar es Salaam jana.

TAARIFA KUTOKA JWTZ:UTAPELI AJIRA JWTZ

$
0
0


JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA
KURUGENZI YA HABARI NA UHUSIANO

Simu ya Upepo  : “N G O M E”        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo: DSM 22150463     Sanduku la Posta 9203,
Telex                   : 41051                       DAR ES SALAAM, 20  Februari, 2017.
Tele Fax              : 2153426
Barua pepe       : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti                  : www.tpdf.mil.tz
Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limeshitushwa na kusikitishwa na taarifa za kutapeliwa wananchi kuhusu ajira za JWTZ. 

Hivi karibuni kumezuka kundi la watu wanao jiita mawakala wa kutafuta vijana wa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania na mara nyingi hutumia majina ya viongozi wa JWTZ kutapeli, huwataka wananchi hao kuwapa fedha ili kuweza kuwapatia nafasi hizo.

JWTZ linapenda kuwafahamisha wananchi kuwa nafasi za ajira Jeshini hutangazwa kwa kufuata taratibu za ajira ambapo JKT imepewa mamlaka ya kuwachukuwa vijana kutoka uraiani kwa kutoa matangazo ya wito wa vijana wa kujitolea ambapo matangazo hayo hutolewa hadi ngazi ya wilaya, vijana hao hutakiwa kuwa na  nyaraka mbali mbali zikiwemo za elimu, uraia na nyaraka nyingine kama hizo ili kukidhi vigezo  vya kupatiwa mafunzo ya kijeshi.

Baada ya kumaliza mafunzo hayo wahitimu hubaki JKT kwa muda wakisubiri vyombo vya ulinzi na usalama likiwemo JWTZ kutoa ajira kulingana na hitajio la vyombo hivyo. Wananchi wanatakiwa kufuata taratibu hizo ili kuepuka udanganyifu unaoweza kusababisha kutapeliwa fedha zao. Jeshi halitahusika na madai yoyote yatakayotokana na udanganyifu huo.

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

AFD/SUNREF HOLDS A WORKSHOP ON HIGHLIGHTING THE CHALLENGES AND SOLUTIONS OF RENEWABLE ENERGY AND ENERGY EFFICIENCY IN TANZANIA

$
0
0
Above are the panelists during an open discussion from guests and panelists discussing the topic “Challenges and solutions of renewable Energy and energy efficiency sector in Tanzania”, the panel was moderated by Mr. David Sacotte at the center with other panelists that included: Emmanuel Baudarn (AFD Tanzania Representative), Mr. Kumar Krishan (Chairman CTI), Ms. Davikarani Williams (Head of Enterprise Banking BANK OF AFRICA – TANZANIA) Halfan Swai (Director Baobab school, Kemilembe Kafanabo (Principal Financial Analyst EWURA), Styedean Rwebangila (Moem Acting Assitant Commissioner (New and renewable Energy).
Ms. Davikarani Williams (Head of Enterprise banking, BANK OF AFRICA – TANZANIA) at the center answering a question during the panel discussion at the luncheon event (SUNREF East Africa).
Audience during the workshop at Serena Hotel on 24th February 2017 at Serena Hotel Dar es salaam, the main topic of discussion was the role of AFD/SUNREF in highlighting the challenges and solutions of renewable energy and energy efficiency in Tanzania.
Mr Emmanuel Baudran (AFD Country Representative) giving a speech during the luncheon event.
H.E. Mr. Roeland Van De Geer (Head of Delegation of the European Union) giving a speech during the opening of the renewable energy and Energy efficiency workshop at Serena Hotel.

Viewing all 46339 articles
Browse latest View live




Latest Images