Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1153 | 1154 | (Page 1155) | 1156 | 1157 | .... | 1898 | newer

  0 0


  Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel Kitengo cha Uhasibu Bw. Ally Abdallah akichangia damu kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana na wingi wa watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi hilo lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena. 


  Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel Kitengo cha Ugavi Bi. Mainda Madiwa Chanika akichangia damu kwa hiari wakati wa zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia ya kukabiliana na wingi wa watu wengi wenye uhitaji wa huduma hiyo kila mwaka. Zoezi hilo lilifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena.
  Mfanyakazi wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Zantel Kitengo cha Ugavi Bi. Mainda Madiwa akiweka sahihi kwenye fomu kabla ya kuingia katika zoezi la hiari la uchangiaji wa damu salama ili kuokoa maisha ya watanzania wengine lililofanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kushoto) ni Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Fatuma Mjungu.
  Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Fatuma Mjungu akizungumza na vyombo vya habari wakati wa zoezi la uchangiaji damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya watanzania wengine lilowahusisha baadhi ya wafanyakazi wa Zantel lililofanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam.
  Mkurugenzi wa Kitengo cha Mauzo ya jumla wa Kampuni ya Zantel, Deo Ngonyani akishiriki katika zoezi la uchangiaji damu salama lililowahusisha wafanyakazi wa kampuni hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji mkubwa wa huduma hiyo. Zoezi hilo lililifanyika mwishoni mwa juma katika makao makuu ya Kampuni hiyo jijini Dar es salaam. (Kulia) ni Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa damu Salama-Kanda ya Mashariki Bi. Cecilia Meena. 

  0 0

  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akikinga maji kwenye ndoo kuashiria sasa kisima cha maji kimefunguliwa na kuanza kutumia kwa wakazi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa akiwa na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove wakati wa uzinduzi wa kisima hicho.
  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalam wa kujimba visima ambaye pia ndiye aliyechimba kisima hicho. 
  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wanatumia wananchi mtaa wa Igungandembwe manispaa ya Iringa.
  Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiangalia maji waliyokuwa wakitumia wananchi wa mtaa huo
  Na haya ndio maji waliyokuwa wanatumia wananchiwa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa kabla ya kujimbiwa kisima   Na Fredy Mgunda,Iringa.

  Wananchi wa mtaa wa Igungandembwe manispaa ya iringa wamemshukuru mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) na diwani wa kata ya Nduli Bashir Mtove kwa msaada wa kuwachimbia kisima cha maji safi na salama.

  Wakizungumza na blog hii wananchi hao wamesema kuwa wanatakribani miaka hamsini na tatu (53) hawajawahi pata maji masafi na salama.

  “Angalia maji haya machafu ndio tulikuwa tunakunywa na kupikia ila mungu alikuwa anatusaidia tu kutuepusha na magonjwa mbalimbali kiukweli leo tunafuraha sana kuanza kutumia haya maji na ndio maana unaona wananchi wanafuraha nawameanza kunywa maji hapa hapa kwenye kisima hiki kwa kuwa bado hawaamini kilichotokea”,walisema wananchi.

  Wananchi wao wamemuomba mbunge Ritta kabati na Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove kuendelea kutatua changamoto za wananchi kwa kuwa walichaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia.

  Kwa upande wake mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) alisema kuwa wataendelea kutatua changamoto mbalimbali za wananchi kwa kuwa yeye ni mbunge wa wananchi wote bila kubagua vyama.

  Kabati alisema kuwa ataendelea kuwachimbia visima na kukarabati majengo ya shule zilizochakaa katika mkoa wa Iringa kwa kuwa yeye ni mbunge wa mkoa wa Iringa hivyo aliwaomba wananchi kuendelea kuiamini serikali ya chama cha mapinduzi kwa kazi kubwa wanayoifanya kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli.

  “Hivi hamuoni nimeamua kufika huku ambako hata viongozi wengi hawajafika ila mimi nimekuja nimewaleta kisima na maji safi na nitaendelea kuja kutatua matatizo ya mtaa huu kwa kuwa tumetumwa na Rais kufanya kazi kwa wananchi wa chini ndio maana hata mimi nimeanza kufanya kazi huku mbali japo kuwa ndio jadi yangu kuwatumikia sana wananchi wa chini sasa naombeni mniunge mkono katika juhudi zangu za kuwaletea mandeleo”.alisema Kabati

  Aidha Kabati alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuleta maendeleo kuanzia huku chini kupanda juu hivyo tufanye kazi kwa kujituma ili tuende sambamba na kasi ya Rais wetu.

  Naye Diwani wa kata ya nduli Bashir Mtove alimshukuru mbunge huyo kwa jihada zake za kuleta maendeleo na kumuomba kushugulikia changamoto alizozitoa kwa wananchi ili kuendelea kujijengea imani kwa wananchi wa kata hiyo.Mtove aliongeza kuwa atahakikisha kata yake inamaliza tatizo la maji ambao limetumu kwa miaka mingi hivyo wananchi wanatakiwa kufanya kazi kwa kujituma ili kukuza uchumi wa kata hiyo.

  “Angalia hadi saizi tumechimba visima zaidi ya sita kwenye kata yangu japo bado sana kumaliza tatizo hili la maji hivyo naendelea kujituma kutafuta marafiki,wafadhili na kumshirikisha mbunge Kabati kusaidia kutatua tatizo la maji na changamoto nyingi ili wananchi wangu wafanye kazi kwa kujituma bila kuwa na vikwazo vyovyote vile vya kiafya”.alisema Mtove.

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.

  Serikali imeweka kipaumbele kikubwa katika  ujenzi wa miundombinu ya Umma  kwani ni muhimu kuwa na miundombinu mizuri na bora ili kutoa huduma bora na kurahisisha ufanyaji kazi hivyo kuharakisha maendeleo ya nchi katika nyanja zote muhimu zikiwemo za biashara, utalii na mawasiliano.

  Matumizi makubwa ya fedha za Serikali yanatumika katika ujenzi wa miundombinu ya Umma ambapo matumizi hayo yanahusisha karibu asilimia 53 ya Bajeti nzima ya nchi.

  Miradi ya ujenzi wa miundombinu ya Umma inayoelezewa hapa ni ile ambayo inajengwa kwa fedha za Serikali kwa ajili ya matumizi ya wananchi wote ikiwemo ya barabara, hospitali na vituo vya afya,shule na vyuo,nyumba za kuishi pamoja na ofisi mbalimbali. 

  Ingawa Serikali inajitahidi kuhakikisha nchi inakuwa na miundombinu bora itakayochochea maendeleo, lakini jitihada hizo zimekuwa zikikwamishwa na changamoto mbalimbali zinazojitokeza pindi mradi husika unavyoanza kwani wahusika hawatumii fedha kama zilivyopangwa na badala yake wanafanya kwa makadirio ya chini na kufanya ujenzi kutokuwa imara.

  Hali hiyo inasababisha Serikali kupata hasara kwa kupoteza fedha nyingi na kuambulia kubaki na majengo yasiyo na viwango ambayo mwisho wake hushindwa kutumika na kuilazimu Serikali kuanza upya ujenzi husika. 

  Kwa kuwa Serikali hii ni sikivu na imejipanga kuhakikisha nchi inafika katika uchumi wa kati basi mambo hayo hayana nafasi na hayawezi kutokea tena katika nchi hii watu kuachiwa huru kutumia vibaya fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu. 

  Kwa kuhakikisha hilo,Serikali kupitia Baraza la Ujenzi la Taifa (NCC) chini ya Mkakati wa Kukuza Uwazi na Uwajibikaji katika Sekta ya Ujenzi Tanzania (CoST-Tanzania) imejipanga kuimarisha uwazi na uwajibikaji katika sekta hiyo ili kuondokana na rushwa pamoja na ubadhilifu wowote wa fedha za Umma zinazotolewa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo.

  Mkakati huo unalengo la kupambana na rushwa, usimamizi mbaya katika ujenzi pamoja na changamoto zingine zinazopelekea ubadhilifu wa fedha zinazotengwa kwa ajili ya miundombinu ya Umma kwa kukusanya taarifa za miradi hiyo ya ujenzi ili  kuhakikisha kama thamani ya miundombinu iliyojengwa inalingana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika. 

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,(Ujenzi), Mha. Joseph Nyamuhanga alikaririwa akisema kuwa “Sekta ya Ujenzi ni sekta moja wapo inayoonekana kukithiri kwa rushwa duniani kwa sababu takribani asilimia 10 hadi 30 ya Bajeti yake inapotea kwa njia ya rushwa na usimamizi mbaya hivyo ili kuondoa dhima hii ni lazima kukusanya na kutoa taarifa kwa wananchi juu ya ujenzi wa miundombinu hiyo”.

  Mha. Nyamuhanga aliongeza kuwa ni muhimu CoST-Tanzania ikapewa hadhi ya kujitegemea na kuwa na madaraka yake kwani ni kitengo ambacho ni muhimu na kinafanya kazi kubwa ya kuchochea uwepo wa uwazi na uwajibikaji katika miradi ya ujenzi.

  Akifungua mkutano wa wadau wa ujenzi kutoka nchi mbalimbali uliofanyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi), Mha. Leonard Chamuriho alisema rushwa inazungumzwa sana katika suala la ujenzi wa miundombinu ya umma hivyo huu ni wakati wa kuweka wazi taarifa za ujenzi wa miundombinu hiyo ili wananchi waelewe kinachoendelea katika miradi inayotumia fedha zao.

  Aliongeza kuwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kupambana na rushwa na hivyo kufuta kabisa taswira ya rushwa katika miradi hiyo kwani msimamo wa Serikali ni kuhakikisha thamani ya fedha inazingatiwa.

  Maendeleo ya nchi yanachangiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya ukusanyaji wa kodi na ushuru mbalimbali hivyo hata miundombinu ya umma inajengwa kwa kutumia fedha za wananchi zinazopatikana kwa njia ya ukusanyaji mapato.

  Hivyo, ili kuifanya Serikali kuwa na taswira nzuri kwa wananchi wao pamoja na kuwafanya wananchi kuiamini Serikali yao ni vizuri kuwapa taarifa juu ya matumizi ya fedha hizo wanazozikusanya.

  Kuwapa taarifa wananchi juu ya miradi mbalimbali haswa ya ujenzi wa miundombinu kutaamsha ile hali ya watu kuona umuhimu wa kulipa kodi kwa sababu watajua matumizi ya fedha wanazozikusanya.

  Taarifa hizo pia zitaendeleza uwajibikaji na uwazi katika ujenzi wa miundombinu hiyo hivyo kupunguza vitendo vya rushwa,kujenga miundombinu inayoendana na thamani ya fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi husika pamoja na kujenga miundo mbinu bora na imara.

  Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki amesema kuwa shughuli inayofanywa na CoST- Tanzania inalenga kuimarisha uwazi katika sekta ya ujenzi kwa kutoa taarifa juu ya ujenzi wa miundombinu ya Umma kitu ambacho kitasaidia kutambua uwezo, akiba pamoja na ufanisi wa majengo hayo.

  "Kazi inayofanywa na CoST- Tanzania ni fursa kwa Serikali na Umma kwa ujumla kufuatilia jinsi fedha za Umma zinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ambapo ukweli na uwazi wa taarifa zinazokusanywa zitasaidia katika kupunguza rushwa na kuboresha usimamizi wa miundombinu hiyo, " alisema Waziri Kairuki.

  Nae Mwenyekiti wa CoST-Tanzania, Mha. Kazungu Magili alieleza kuwa utoaji wa taarifa hizo kwa Umma kuhusiana na miradi ya ujenzi ya Umma itaruhusu umma kujua hali ya miradi mbalimbali hivyo kuifanya Serikali kuwa na sifa nzuri mbele ya wananchi.

  CoST-Tanzania imejipanga kufanya tathmini ya miradi ya ujenzi isiyopungua kumi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madaraja, majengo yaliyojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) hasa ujenzi mpya wa hosteli  za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pia majengo yanayojengwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF ) pamoja na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).

  Ni muhimu kwa Serikali kupitia miradi yote iliyojengwa na inayoendelea kujengwa kwa kutumia fedha za Umma ili kugundua thamani halisi ya majengo hayo na kutoa taarifa kwa wananchi.

  Jambo hili pia litasaidia vyombo husika vya kisheria kuwachukulia hatua watu wote walioshiriki kutumia vibaya fedha za wananchi kwa kujenga miundombinu iliyo chini ya kiwango au isiyoendana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa ajili ya ujenzi husika.

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akimkabidhi vifaa vya michezo mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Vuai Naimu wakati wa utoaji wa Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,ambapo majimbo mbali mbali walikabidhiwa vifaa hivyo hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akimkabidhi vifaa mbali mbali vya michezo mwakilishi wa Jimbo la Kwahani CCM Sufiani khamis wakati wa utoaji wa Vifaa hivyo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,ambapo majimbo mbali mbali walikabidhiwa vifaa hivyo,hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akimkabidhi vifaa mbali mbali vya kuendeshea mashindano ya mpira wa Miguu kwa timu za Vijana majimbo ya CCM wilaya za Unguja,Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Abdalla Mwinyi Hassan,vifaa hivyo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani,
  Baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa majimbo ya Unguja CCM na Vijana wakiwa katika hafla ya kukabidhi vifaa vya Michezo vilivyotolewa na Mhe,Mohamed Raza Daramsi Mwakilishi wa Jimbo la Uzini,katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo ya Unguja,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa CCM Mkoa Amani leo.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) alipokuwa akizungumza na Viongozi mbali mbali na Vijana wa Majimbo na ya CCM Unguja katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini CCM Mhe,Mohamed Raza Daramsi,ikiwa ni katika kuimarisha Michezo kwa Vijana wa CCM Majimbo, hafla iliyofanyika leo ukumbi wa CCM Mkoa Amani .

  [Picha na Ikulu.]

  0 0


  0 0

  Mwanariadha, Charles Maroa kutoka nchini Kenya amefikwa na mauti katika hospitali ya KCMC mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, baada ya kuanguka katika geti la viwanja vya Ushirika wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro zilizofanyika jana Februari 26.

  Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, RPC Raymond Mtafungwa alisema kuwa Mwanariadha huyo alikutwa na umauti huo jana majira ya saa tano asubuhi katika hospitali la KCMC mjini Moshi baada ya kuanguka.

  "Tumepokea taarifa za kifo cha Mwanariadha huyo alietambulika kwa jina la Charles Maroa,ambaye ni raia wa Kenya (Mkurya), baada ya kukumbwa na hali hiyo alikimbizwa hospitali ya KCMC kupatiwa huduma ya kwanza baada ya kuanguka ghafla katika geti kuu la kuingia katika viwanja vya Ushirika hapa mjini Moshi wakati alipokuwa akielekea kumaliza mbio za nusu Marathon za Kilimanjaro na tunaendelea na uchunguzi kujua nini kilitokea mpaka kuelekea kifo chake" alisema.

  Mwili wa Mwanariadha huyo umehifadhiwa katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.

  0 0

  Baada ya malalamiko kuzidi kutokana na kuwapo biashara zisizo rasmi katika baa maarufu ya Corner Bar a.k.a Club Ambiance, iliopo maeneo ya Afrika sana (Sinza) sasa baa hiyo imeamriwa kufungwa.
  Akiwa katika ziara ya kawaida mwishoni mwa wiki (Jumamosi) Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amemuagiza Ofisa Biashara wa Kinondoni, Mohamed Nyasama kuifunga baa hiyo.
  “Hatuwezi kuvumilia vitendo hivi vikaendelea kufanyika huku tukiwa kimya…natoa agizo kesho.nendeni kaifungieni hiyo baa kwa kuwa inakiuka maadili,”amesema Hapi.Hata hivyo Nyasama amesema walishaitoza baa hiyo faini ya Sh 300,000 kwa kosa hilo.
  “Mkuu hii baa ni sugu, nimewahi hata kuipiga faini na bado imeendelea na utaratibu huo huo wa kuruhusu kina dada kujiuza.Kwa amri yako mkuu naanza taratibu za kuifungia leo, hadi kufikia kesho itakuwa tayari,” amesema.

  Source: Mwananchi

  0 0

  SERIKALI imeahidi kutoa pembejeo za kilimo cha kisasa yakiwemo matrekta kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kupitia taasisi inayojihusisha na kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT) ili waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo cha kisasa hususani cha kibiashara.

  Ahadi hiyo ya Serikali ya serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha kwa Niaba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akizungumza kwenye harambee kukusanya fedha kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara iliyoandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali ya Land O’ Lakes kwa kushirikiana na CAWAT na kufanyika jijini Dar es salaam mwshoni mwa wiki.

  “Serikali ipo tayari kutoa pembejeo hizo za kilimo cha kisasa yakiwemo matrekta bora kabisa ambayo yataolewa kwa vikundi vya kina mama wanachama wa CAWAT ambao wataonyesha nia na uwezo wa kutekeleza kilimo cha kisasa hususani cha kibiashara. Zaidi wanufaika hao watahakikishiwa soko la uhakika kwa kile watakachozalisha,’’ alisema Ole Nasha ambae pia yeye binafsi alitoa mchango wa mil. 2 kwenye harambee hiyo.

  Alisema serikali ipo tayari kushirikiana na taasisi yeyote nchini yenye nia ya dhati katika kuleta mabadiliko yenye tija yatakayoliwezesha taifa kuongeza kasi yake katika kuelekea uchumi wa viwanda na mapinduzi ya kilimo.

  Hatua hiyo ya serikali inakwenda sambamba na ahadi ya Benki ya Maendeleo ya kilimo nchini (TADB)kwa CAWAT ambapo kupitia Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wake Bw Francis Assenga, ilitangaza kwenye warsha hiyo kwamba ipo tayari kushirikiana na CAWAT ili kutoa ushauri utakaoambatana na fursa ya kutenga sh milioni 600 kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake katika kuendesha kilimo hicho cha kibiashara kupitia taasisi hiyo.

  "Kupitia ushirikiano wetu huo na CAWAT ni wazi kwamba TADB tunakwenda kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo hasa cha kisasa kupitia wanawake nchini. Baada ya kupitia malengo ya CAWAT tumelizika moja kwa moja kuwa tuna kila sababu ya kushirikiana nao ili kuifikisha hii nchi kwenye uchumi wa viwanda kupitia kilimo,’’ alisema.

  Katika harambee hiyo kiasi cha pesa zaidi ya milioni 27 kilipatikana ikiwa ni ahadi na taslimu, huku pia ikielezwa kuwa Balozi za Japan na Switzerland hapa nchini zimeonyesha nia ya kusaidia miradi mbalimbali itakayoendeshwa na taasis hiyo ya CAWAT.

  Awali wakizungumza kwenye hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi ya CAWAT Dk Victoria Kisyombe pamoja na Mkurugenzi Mradi kutoka taasisi ya Land O’ Lake Dr Rose Kingamkono walisema kwa sasa taasisi ya CAWAT ipo kwenye mchakato wa awali wa kuanza kujitegemea yenyewe kiuendashaji bila kutegemea msaada iliyokuwa ikiupata kutoka shirika la msaada la Marekani USAID. 

   Mkurugenzi Mradi kutoka taasisi ya Land O’ Lake Dr Rose Kingamkono akizungumza kwenye harambee ya kukusanya fedha  kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
   Baadhi ya washiriki wa harambee hiyo.
   Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha  akizungumza kwenye harambee hiyo.  Ole Nasha alimuwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye harambee hiyo iliyofanyika kwa mafanikio makubwa!
   Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini  (TADB) Bw Francis Assenga akizungumza kwenye harambee hiyo.Benki hiyo ilitangaza nia yake ya kutenga sh milioni 600 kuwezesha miradi ya taasisi  ya CAWAT.
   Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi inayojihusisha na kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT)  Dk Victoria Kisyombe (Kushoto) akipeana mkono wa pongezi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) Bw Francis Assenga kwenye harambee hiyo ikiwa ni ishara kuanza kwa ushirikiano baina ya taasisi hizo. Wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Mradi kutoka taasisi ya Land O’ Lake Dr Rose Kingamkono.
   Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha (katikati waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa taasisi za CAWAT, Land O’ Lake, SAGCOT pamoja na maofisa wa juu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) kwenye harambee hiyo.
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi William Ole Nasha akipeana mkono wa pongezi na Meneja Uhusiano wa Mfuko wa pesheni wa PPF, Lulu Mengele ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa mfuko huo kwenye harambee hiyo.


  0 0

   
  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kesho (28 Februari 2017) atafungua mkutano wa siku moja wa Watendaji Wakuu na Wenyeviti wa Bodi za Mashirika ya Umma utakaojadili nafasi za Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa II wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano.

  Mkutano huu ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina utafanyika Ikulu – Dar es Salaam kuanzia saa 2.30 asubuhi.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja amesema kwamba malengo ya mkutano ni kukusanya maoni ya viongozi kuhusu nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano; kuzungumzia changamoto tarajiwa katika utekelezaji wa majukumu haya na; kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

  “Mashirika ya Umma yana nafasi na uwezo mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17–2020/21 wenye kaulimbiu ‘Maendeleo ya Viwanda kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu’,” alisema Profesa Semboja.

  Profesa Semboja aliendelea, “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli mkutano huu unawakutanisha viongozi kutoka Serikalini na Mashirika ya Umma kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu wa jinsi mashirika haya yatakavyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa maendeleo endelevu.”

  Pamoja na mambo mengine, mkutano utajadili namna ya kuboresha mifumo ya  kiundetaji ndani ya mashirika na mahusiano miongoni mwa mashirika na taasisi za Serikali; kufungamanisha mipango ya mashirika ya Umma na Mpango wa Pili wa Maendeleo; kutathmini kiwango na aina ya rasilimali zinazohitajika kuwezesha utekelezaji wa mipango na; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango.

  Mkutano utawakutanisha zaidi ya washiriki 100 kutoka Wizara, Mashirika ya Umma na Mamlaka za Udhibiti takribani 52 hapa nchini.

   Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano –Taasisi ya Uongozi.  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo wikiendi hii alipata nafasi ya kutembelea nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani Hayati Edward Moringe Sokoine huko Monduli juu Wilayani Monduli. 

  Mh.Gambo alipata wasaaa wa kuzungumza na wajane wa kiongozi huyo mkubwa wa Kitaifa aliyefariki kwa ajali ya gari mwaka 1984 eneo la Dumila huko Mkoani Morogoro, Mkuu wa mkoa alipata wasaa wakuzungumza na familia hiyo pamoja na wakazi majirani wanaozunguka familia hiyo na kusema maneno machache ambapo Alisema 

  "Kutembelea maeneo haya ambapo zipo kumbukumbu za mashujaa wetu waliolipigania Taifa letu kwa uzalendo mkuu, inatusaidia sisi viongozi vijana kuzirudia hadhiri zetu za uongozi ili tuweze kuwatumikia wananchi wanyonge kwa Uadilifu na uwajibikaji,ili kuacha alama katika nafasi tulizopewa na kuwatumikia wananchi kama walivyofanya wazee wetu hawa." 
  Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo,Akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine.
  Kutoka Kulia ni Diwani wa Monduli juu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli na pia ni Diwani wa Monduli Mjini Mh:Issack Joseph,akisalimiana na Mjane wa Hayati Sokoine .
  Mh: Gambo akiwa ameambatana na Mjane wa Sokoine Pamoja na watumishi mbalimbali wa Serikali,Wakitoa Heshima kwenye kaburi la Hayati Sokoine.  
  Mkuu wa mkoa wa Arusha Mh: Mrisho Gambo akipanda mti wa kumbukumbu nyumbani kwa Hayati Sokoine.Picha na Msumbanews.com

  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Arusha huku akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa FNB, Dave Aitken(wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la Arusha, Mh. Calist Bukhai (kulia). 
  Meneja wa Tawi la FNB Arusha, Genevieve Massawe akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji jinsi mashine ya kisasa ya kuweka fedha (cash deposit) na kutoa fedha. Mashine hiyo ya kisasa inamuwezesha mtumiaji kuweka fedha zake benki muda wa masaa 24 imewekwa kwenye tawi hilo jipya ili kuwawezesha wananchi kuweka akiba fedha zao muda wowote ule. 
  Mshauri wa Huduma kwa Wateja na Mauzo wa FNB Tawi la Arusha, Cecyline Ayo akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kuhusu bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo wakati wa uziduzi wa FNB Tawi la Arusha mwishoni mwa wiki. 
  Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akimrekebishia kipaza sati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la FNB Tanzania la Arusha mwishoni mwa wiki. 

  Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akiongea na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo jijini Arusha mwishoni mwa wiki.


  -- First National Bank (FNB) Tanzania imeendelea kupanua wigo wake kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la PPF Plaza jijini Arusha kwa lengo la kuhudumia ongezeko la idadi ya wateja katika mkoa huo.

   Akizungumza wakati wa ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dave Aitken alisema uzinduzi wa tawi la FNB Arusha umelenga kukidhi ongezeko kubwa la wateja na mahitaji ya huduma za kibenki na kifedha katika kanda ya kaskazini. 

  “ Uzinduzi wa tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wa uwekezaji endelevu uliolenga kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia ni kwa maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania” Aitken alisema tawi la Arusha ni la kumi miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mitandao ya matawi kwa kusudi la kuyafikia maeneo mengi ya nchini.

   “First National Bank (FNB), daima tunafikiria njia ambazo zinaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Arusha litasaidia kuwapatia huduma zote za kibenki wananchi wa mkoa wa Arusha na wanaoishi maeneo jirani kwani maeneo haya yote yamedhiirika kuwa na biashara mbalimbali zinazokua kwa kasi,” alisema Aitken. 

  Akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi rasmi wa tawi hilo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji alisema mkoa wa Arusha una uwezo mkubwa wa kiuchumi na ukuaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kudhihirisha kuwa mji unakuwa kwa kasi. 

  “Tunakaribisha uwepo wa FNB Tanzania Arusha na tunatazamia kuwasaidia kuimarisha huduma zenu hapa na mikoa mengine,” Alisema Naibu Waziri. Alisema pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili na utalii, mkoa wa Arusha umechangia sana katika kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta nyingine za uzalishaji mali na biashara. 

  “Arusha ina fursa na hazina kubwa ya rasilimali jambo ambalo limechangia ukuaji wa haraka wa biashara katika sekta zote muhimu za kiuchumi. Ni matumaini yetu uwepo wa FNB katika mji huu utachangia katika kuleta maendeleo ya biashara kupitia ubunifu wa huduma za kibenki,” Kijaji alisema. 

  Vile vile Kijaji ameitaka sekta ya fedha nchini zimetakiwa kutoa mikopo inayosaidia wananchi kukuza mitaji yao ambayo kwa sehemu kubwa itawawezesha katika uzalishaji mali na kuongeza pato lao na nchi kwa ujumla. Amesema kuwa serikali haiwezi kufanikiwa kutekeleza sera na mipango yake kwa ufanisi bila kuwepo sekta binafsi hususani sekta ya fedha hivyo kama serikali inathamini sana mchango wa benki hiyo ya FNB ambayo kwa kiasi kikubwa itasaidia wananchi wa Arusha. 

  Tawi la Arusha lililopo jengo la PPF Plaza linakuja na bidhaa na huduma mbalimbali zilizobuniwa mahususi kwa ajili ya kuwaongezea tija wateja wa kawaida na wafanyabiashara katika eneo hili la kanda ya kaskazini.

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe amewaagiza Viongozi wa Serikali Mkoani humo ngazi ya Wilaya hadi kata kuwa na madaftari ya kuwasajiri wakulima ifikapo Machi 31, mwaka huu.

  Dkt. Kebwe ametoa agizo hilo Februari 22 mwaka huu wakati anatembelea kiwanda cha kuzalisha Mpunga cha KPL kilichopo katika Wilayani ya Kilombero ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tano aliyoifanya Wilayani humo.

  Katika maelezo yake Dkt. Kebwe amesema zoezi la usajiri wa wafugaji pamoja na mifugo yao lazima liende sambamba na zoezi la usajiri wa wakulima kwa lengo lilelile la kupata takwimu halisi kwa Mkoa mzima na si kuwa na takwimu za mezani.

  “Sambamba na kazi ambayo tuliianza mwaka jana mwezi wa sita ya utambuzi wa mifugo kazi ambayo inaendelea awamu ya pili, madftari ya wafugaji sehemu kubwa yameanza kuwepo wafugaji wanatambuliwa. Kwa hiyo vitu hivi viwili lazima viende sambamba hii inasaidia kutengeneza maoteo katika Halmashauri zetu. Huwezi kufanya maoteo bila kuwa na tax base” alisema Dkt. Kebwe

  Mkuu huyo wa Mkoa ameonekana kuridhishwa na juhudi zinazooneshwa na baadhi ya wakulima hususani wa Wilaya ya Kilombero kujihusisha katika kilimo na kusema amejionea mwenyewe watu wamelima mashamba makubwa ingawa mvua zimechelewa kunyesha tofauti na maeneo mengine ambapo wamelima maeneo madogo.

  Hata hivyo amesema ametoa maelekezo kwa Mkoa wote kufikia tarehe 31 ya mwezi wa tatu kila Halmashauri iwe na madaftari haya ya wakulima. Hii itatusaidia sana kujua kiasi mtu anacholima na anachotegemea kuvuna hivyo kuwa na takwimu zenye uhakika.

  Amesema kuwa na madaftari ya kutunzia takwimu kwa masuala ya kilimo ni maelekezo ya siku nyingi ya Serikali na ni takwa la kisheria na hiyo inasaidia kupata msingi wa mapato katika Halmashauri zetu (tax base) kwani bila kuwa na madaftari hayo takwimu ambazo zitakuwa zinatolewa kwa sehemu kubwa zitakuwa hazina uhalisia.

  Lakini Dkt. Kebwe pia alishauri uongozi wa kiwanda cha KPL kuwa pamoja na kujishughulisha na kilimo cha mpunga waongeze jitihada ya kulima zao la mahindi ambalo kwa sasa lina soko la uhakika na kuwataka pia kuuza ziada ya mahindi watakayoyapata kwa Wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula – NFRA.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. James Ihunyo amesema, madaftari ya wakulima na wafugaji yatasaidia kupunguza kama sio kuondoa kabisa migogoro baina ya wakulima na wafugaji Kwani Kwa kujua takwimu zao kwa usahihi itasaidia Serikali kufanya maandalizi ya kutenga maeneo ya kilimo na malisho ya mifugo kwa usahihi pia, kupitia mradi wa Serikali unaohusika na kupima maeneo yote ya Ardhi na kuyarasimisha kwa wananchi (Land Tenure supporting Program).

  Aidha, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero …….Londo amesema, uwepo wa madaftari ya wakulima kwanza itasaidia kujua idadi ya wakulima wote wa Halmashauri yake, kujua mazao wanayolima na ukubwa wa mashamba yao pamoja na takwimunyingine. Lakini pia kuwa na maoteo sahihi ya mazao yatakayopatikana na tatu kuondoa mchezo mchafu unaofanywa na baadhi ya wafanya biashara wanaojificha nyuma ya wakulima wakati wa kulipa kodi za mazao kwani sekta ya Kilimo ndiyo inabeba Halmashauri hiyo kiuchumi.
   
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh. Steven Kebwe akishiriki katika kazi ya kiwekea mifugo alama ikiwa ni utambuzi wa mifugo hiyo.
  Ng’ombe ambao tayari wamesha wekewa alama.

  0 0

  Na Anthony  John Glob Ya Jamii. 

  Watendaji katika Manispaa ya Kinondoni wakiwemo venyeviti wa mitaa wametakiwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za vyama vyao.

  Akitoa wito huo, mkuu wa wilaya hiyo ALI HAPI wakati akizungumza na watendaji wa kata ya Ndugumbi, amesema baadhi ya watendaji hasa wenyeviti wa mitaa katika baadhi ya sehemu wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwanabagua wananchi kwa itikadi za vyama vyao ,hali inayochangia pia kukosa huduma muhimu za kijamii.

  Ametolea mfano upo mtaa mmoja ukionekana chama fulani hupati maji ,kwasababu kiongozi wa mtaa huo anatoka chama fulani na chama kingine huruhusiwi kuchota maji.

  Ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha, hivyo siasa na vyama vya siasa visiwagawe kwani hivyo husaidia ktk kuzipata nafasi hizo za uongozi tu.

  Mkuu wa wilaya pia amekagua mradi wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Mwalimu Nyerere huku akimuagiza injinia wa manispaa hiyo SIMON LIACHEMA kuangalia mfumo wa kisasa katika utengenezaji wa matundu hayo ya vyoo ili kuwapa urahisi wanafunzi pindi wanapotumia vyoo hivyo.

  Katika hatua nyingine amekagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu mkuu katika shule ya sekondari Turiani na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa walimu wa shule hiyo pindi watakapoanzisha chama chao cha kuweka na kukopa SACCOS pamoja na kutembelea soko la Babati.    


   .mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi  Akizungumza na wananchi katika soko Babati lililopo kinondoni Jijini dar es salaam.
   .Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akikagua mradi wa majengo  mbali mbali katika  shule ya msingi Mwalimu Nyerere akiwa na walimu  wa Shule Hiyo leo hii iliyopo kinondoni Jijini Dar es salaam.

  0 0

  Mabeste ni rapper wa muziki in Tz  ambaye mpenzi wake anafahamika kama Lisa, Mungu mkubwa mbali na kupitia changamoto za hapa na pale ukweli penzi lao limedumu kwa muda mrefu kidogo.

  Moja kati ya mafanikio makubwa katika mahusiano yao Mabeste na Lissa walipata mtoto mmoja wa kiume 'Kendrick' and soon wanaweza kupata mtoto wa pili coz Lisa anakibendi kingine.Sio rahisi kama ambavyo unafikiria ku-maintain penzi, ndio maana relation nyingi za mastaa huishia kwenye maua.

  Mabeste amezitaja sifa za mpenzi wake BK ambazo zimepelekea kudumu kwa Relation hiyo, Sambamba na hilo ametaja sababu ya kukimbiwa na  marafiki zake pamoja na ndugu zake wa karibu baada ya Penzi la Mabeste na Lisa kuanza.

  0 0

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Idi amewaasa wana CCM na wananchi nwote Nchini kuacha tabia ya kuhamanika kutokana na uvumi unaoenezwa mitandaoni kwamba yapo mabadiliko ya utawala wa Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

  Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mirai yao ya maendeleo.

  Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye Hfla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.

  Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

  Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ataendelea kuviongoza Visiwa vya Unguja na Pemba hadi utakapofanyika uchaguzi mwengine mwaka 2020 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

  Othman Khamis Ame

  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Michezo kwa Timu zinazoshiriki Mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja hapo ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya Wanamichezo wa Timu za Majimbo wakifuatilia hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zao hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
  Kikundi cha Utamaduni cha CCM Mkoa Mjini Big Star kikitoa burdani wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamuj Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
  Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa Kusini Unguja Mh. Mohamed Raza ambae ia ni mdhamini wa mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja nje ya ukumbi wa CCM Aman Mjini Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

  0 0

  [Barcelona, Spain, Feb 26, 2017] At the Digital Transformation Forum held today, Huawei outlined its role as an all-round strategic partner to countries looking to advance economic and social development. Huawei is committed to creating value for communities by collaborating with operators to help them maximize network assets, deploy home broadband and indoor digitalization, and drive connectivity to enhance the user experience, while promoting economic and social growth.
  William Xu, Executive Director of the Board and Chief Strategy Marketing Officer of Huawei, outlined opportunities for growth in emerging markets.

  As we enter a fully connected era, digital infrastructure is facilitating economic growth and emerging markets are on the cusp of a major transition towards digital economies. The Global Connectivity Index (GCI) published by Huawei in 2016 reported that for each GCI score point increase a country improved its innovation capacity by 2.2%, competitiveness by 2.1%, and productivity by 2.3%. Operators around the world are in a unique position to invest in these emerging markets to capitalize on huge ICT industry potential, untapped demographics, and national ICT strategies.

  Huawei is committed to helping operators increase efficiency and drive profitable growth by promoting the sustainable development of emerging markets. William Xu, Executive Director of Board and Chief Strategy Marketing Officer, Huawei, explained: "We work hand-in-hand with operators to help them identify valued customers, develop valued businesses, and build valued networks. We enable operators to combine industry policy with the utilization of existing network resources, and integrate technological and business innovation. Our goal is to help operators drive new revenue streams and a positive business cycle of service development and network construction." 

  Huawei has analyzed the current landscape in emerging markets to formulate its strategic approach from four angles: user+, family+, asset+, and efficiency+. Rapid deployment of home broadband and indoor digitalization will improve coverage and the user experience. Existing network assets are leveraged to maximize network value and spectrum efficiency, improve O&M, and serve every economic level. Interconnecting all users promotes the development of economy, society, and humanity.

  "By 2025, we will see 2 billion more people with mobile connections, and another 500 million broadband homes. Our commitment has always been to enable world’s operators to build roads to new growth," Mr. Xu emphasized. "Huawei continues to drive its social responsibility to help emerging markets grow by at least 1 GCI point while guaranteeing coverage in times of major world events or natural disasters."

  MWC 2017 will be held between February 27 and March 2 in Barcelona, Spain. Huawei will showcase products and solutions at booth 1J50 in Fira Gran Via Hall 1, booth 3130 in Hall 3, and the Innovation City zone in Hall 4. For more information, please visit http://www.huawei.com/en/events/mwc/2017/.

  0 0  Na Lawrence Raphaely-Bunge.

  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndugai amewaahidi Viongozi wa Chama cha Skauti Tanzania ushirikiano katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za chama hicho ikiwemo maadhimisho ya Siku ya Skauti Afrika na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.

  Mhe Spika aliyasema hayo wakati alipokutana na kuzungumza na Viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam ambao walimuomba awaunge mkono katika shughuli zao.

  Spika Ndugai aliwaeleza Viongozi hao kwamba kwa niaba ya Wabunge wote ameupokea ujumbe huo na atajitahidi sana katika kuhufikisha kwa Waheshimiwa Wabunge.

  “Ninawashukuru sana kwa ujumbe huu na niwaahidi kwamba tupo pamoja si katika hili tu bali katika mambo yoyote ambayo mtakuwa mkiyafanya na nawaahidi pia ushiriki wa Waheshimiwa Wabunge katika maadhimkisho hayo,” alisema Mhe Spika.

  Awali akimuelezea Mhe Spika kuhusiana na Shughuli mbalimbali za Skauti hapa nchini Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Stella Manyanya ambaye aliambatana na Viongozi hao wa Skauti alisema pamoja na majukumu mengine Chama hicho cha Skauti kina kazi kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Skauti Dunia na Maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini.

  Mhe Manyanya alisema kuwa maandalizi ya Maadhimisho ya siku Skauti Afrika ambayo yanatarajiwa kufanyika tarehe 8 hadi 11 Machi mwaka huu mkoani Arusha yanaendelea vizuri ingawa kuna changamoto kubwa ya kifedha katika maandalizi ya maadhimisho ya miaka mia moja ya Skauti hapa nchini ambayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia Juni hadi Julai Mkoani Dodoma.

  “Mhe Spika kumekuwa na jitihada mbalimbali za kufanikisha maadhimisho haya lakini kumekuwa na changamoto katika kufikia malengo na ndio maana tumefikana hapa ili kukuomba utuunge mkono” alisema Mhe Manyanya.

  Mhe Manyanya aliongeza kuwa Wizara imendelea kutambaua kazi kubwa ambayo Chama cha Skauti inafanya katika kuendelea kuhimiza nidhamu miongoni mwa Vijana na kuwajengea moyo wa kujitolea.

  “Chama hiki Mhe Spika kimekuwa kikiendelea kufanya kazi kubwa katika kuwajengea Vijana wetu moyo wa kujitolea na kwa sasa tunataka kazi zao zifanyike kwa nguvu zaidi tofauti na hapo mwanzo”

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga alisema anathamini sana mchango wa Mhe Spika na kwamba anashukuru kwa kauli yake ya kuwaunga mkono.

  Balozi Kuhanga aliongeza kuwa kwa sasa Uongozi wake unajipanga katika kuhakikisha kuwa Skauti inazidi kukua hapa nchini.

  “Mhe Spika nia ni kuona Vijana wa Shule za Msingi hadi Chuo Kikuu wanaingia katika Skauti na hivyo tunataka twende mbele zaidi ya hapa tulipo kwa sasa,” alisema Balozi Kuhanga.

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti waliomtembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mapema leo. Wa pili kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) na anayefutia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) aliyeambatana na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipotembelea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Utendaji ya Skauti Tanzania Balozi Nicholas Kuhanga akimueleza jambo Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai wakati walipomtembelea ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (aliyekaa kulia) na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Tenkonolojia Mhe Eng. Stella Manyanya (Mb) katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Skauti Tanzania mara baada ya kuzungumza nao Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
  Picha na Ofisi ya Bunge

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba  akiwa katika kikao  na wawakilishi wa sekta binafsi wakizungumza kuhusu masuala ya ufanisi katika mchakato wa Tathmini ya athari za Mazingira. Wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Profesa Faustin Kamuzora. Kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais jijini Dar es Salaam.
   Baadhi ya Wadau wa sekta binafsi waliohudhuria kikao hiko wakiwa pamoja na Watumishi na Wataalamu toka Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Usimamizi wa mazingira(NEMC) wakimsikiliza Mh. Waziri January Mkamba(hayupo pichani) wakati wa kikao hiko.
  Mmoja wa Wadau toka sekta binafsi za wenye mahoteli, viwanda na fukwe Bi. Lathifa K. Sukes akichangia jambo katika kikao hiko. (PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI OMR)

  0 0

  KATIKATI ya foleni katika jiji la Dar es Salaam ndani ya gari nyeupe aina ya Mercedes S550, Jacqueline Ntuyabaliwe, mrembo wa miaka 38, macho yake yalikuwa yametulia katika simu yake ya mkononi. Alikuwa akiangalia seti ya samani za eneo la kulia chakula. 

  Kwa bashasha, baada ya muda kidogo anatanua picha hiyo kisha ananisogezea simu yake ya mkononi kunionesha picha anayoiangalia. “Hii ni moja ya samani tulizonazo,” anasema huku akinionesha seti hiyo ambayo imetengenezwa na Molocaho by Amorette, kampuni ya kutengeneza samani aliyoianzisha hivi karibuni. “Samani hizi zimetengenezwa kutokana na mbao zilizotwaliwa kutoka katika mashua za zamani za mizigo kwenye fukwe za Tanzania upande wa bahari ya Hindi,” anasema mjasiriamali huyo.

   Samani hizo za eneo la kulia chakula (Dining Table) anasema zimeagizwa na familia moja iliyopo Ulaya ambayo siku za karibuni ilitembelea duka lake (showroom) Dar es Salaam wakati wakiwa likizo na kwamba anajiandaa sasa kuisafirisha seti hiyo ya samani kwa wateja wake wapya wa Ulaya. Lakini kwanza alichokuwa anakifanya kwa siku ile ni kwenda kiwandani kuangalia seti hiyo ya samani kwa mara ya mwisho kabla ya kusafirishwa ili kujihakikishia kwamba imemaliziwa urembeshaji kwa namna inavyotakiwa kuwa.
  Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi.

  Jacqueline Ntuyabaliwe, anayetaka umaridadi uliokamilika, ni binti ambaye huangalia vitu vidogo vidogo kuona kama vipo sawa katika hali inayokubalika viwe. Pamoja na kuwa na ratiba yenye changamoto sana (Yeye ni Balozi wa WildAid na yumo ndani ya bodi kadhaa; mama wa watoto pacha wavulana; mke kwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa na akiendesha taasisi ya hisani ya elimu), Ntuyabaliwe huhakikisha anakagua kila samani inayozalishwa kiwandani kwake kabla ya kuuzwa au kusafirishwa. “Napenda kitu bora chenye uhakika!” anasema mlimbwende huyo wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mwanamuziki. 

  “Kila kitu tunachokifanya Molocaho lazima kiwe chenye uhakika hakina makosa wala dhaifu, lazima kiwe kimetulia,” anasema mrembo huyo. “Tunashindana na watu maarufu duniani wanaofanya vyema kwa hiyo kama sisi tusipofanya vyema kuliko wao tutashindwa,” aliongeza. 

  Ntuyabaliwe, mzaliwa wa Tanzania, aliyefunzwa kubuni uzuri wa ndani, ni mwanzilishi na mbunifu mkuu wa Molocaho by Amorette, kampuni ya Tanzania inayojishughulisha na utengenezaji wa samani bora kwa namna mteja anavyohitaji, samani, nyuzi, taa, urembaji, samani za nje na kwenye bustani. 

  Molocaho inatengeneza samani zenye mahadhi ya kiafrika ikichanganya utamaduni wa Tanzania katika mazingira ya kisasa na kumalizia na ubunifu wa kimataifa. Molocaho, moja ya makampuni ya Afrika Mashariki ya samani yanayokua kwa kasi, imejipatia nafasi kubwa ya heshima kwa kuhakikisha kwamba inatumia mali ghafi na mbao njema pekee za Tanzania kutengeneza samani zenye kwenda kimataifa.

   “Mpango wetu mkubwa ni kujenga nembo ya biashara ya samani za Tanzania inayotambulika kimataifa. Ni dhahiri itatuchukua muda kufikia huko , lakini tumedhamiria,” alisema wakati tukizunguka naye katika duka kubwa la maonesho la Molocaho lililopo eneo la Masaki jijini Dar es Salaam. Ntuyabaliwe ni mojawapo ya watu wanaotambulika kirahisi kabisa nchini Tanzania. 

  Mwaka 2000 alishinda taji la urembo la Miss Tanzania na kuiwakilisha Tanzania katika shindano la ulimbwende la dunia ( Miss World). Baada ya muda alipata heshima ya kuwa mmoja wa wanamuziki mahiri na kuweza kutoa nyimbo kadhaa zilizoshika chati Afrika Mashariki. Pamoja na kuwa mlimbwende na mwanamuziki anasema mapenzi yake makubwa ni ubunifu wa uzuri wa ndani wa nyumba. "Mimi ni mbunifu kutoka moyoni,” anasema. 

  “Kwa namna ninavyokumbuka, mimi ninavutiwa na ubunifu wa ndani na wa samani, sanaa na fasheni na nimekuwa mwanafunzi bora kabisa wa masuala ya ubunifu na historia yake. Kama mtoto mara zote nilikuwa nachora vitu mbalimbali. Ni mojawapo ya vitu ninavyovifanya kwa raha kubwa.” Wakati muziki wake unakamata chati akajiona amekinai na hivyo kuingia katika awamu nyingine ya maisha yake. Alitoka na kwenda shule Uingereza. Huko alienda kujifunza ubunifu wa ndani na lengo kubwa ni kuboresha weledi katika hilo na mwaka 2012 alianzisha kampuni ya Amorette, yenye makao makuu Dar es Salaam iliyokuwa inajishughulisha na masuala ya urembaji wa ndani. Amorette imepata mafanikio makubwa na Ntuyabaliwe amekuwa akifanya kazi na watu wengine wenye kaliba ya juu katika masuala ya ubunifu wawe binafsi au makamapuni ya kimataifa nchini Tanzania, akichanganya mawazo na ubunifu wao kutengeneza bidhaa zenye kaliba ya juu katika ubunifu, staili, rangi ili wateja wake wawe na maisha mazuri ama majumbani mwao au katika mazingira yao ya kazi. 

  Na katika muda wote wa kufanya hayo, mjasiriamali huyu alikuwa na tabia ya kuchora muonekano wa samani. “Napenda samani , sijui kwanini labda kwa sababu ya kazi yangu ya ubunifu wa maeneo ya ndani, lakini nadhani ni kwa kuwa naamini samani zako zinakuonesha wewe ni mtu wa namna gani. Awali nilitengeneza michoro ya samani kwa ajili ya kujenga ubunifu tu, lakini mara nyingi mume wangu huangalia michoro hiyo na kunipongeza. 

  Alikuwa akisema kwamba situmii vyema kipaji changu. Mara nyingi amekuwa akinihimiza kujikita katika usanii na kuanzisha kampuni ya kushughulika nao,” anasema Ntuyabaliwe akikumbuka alivyoanza. Mume wake, Dkt.Reginald Mengi, ni tajiri mwenye mafanikio makubwa nchini Tanzania ambaye ameujenga utajiri wake kwa kufanya karibu kila kitu kuanzia uzalishaji wa kinywaji cha Coca-Cola hadi uchimbaji wa madini na kumiliki vituo vya televisheni na magazeti. 

  “Ukiwa na mume mwenye mafanikio makubwa namna hii, unashawishika kusaka mafanikio. Kwa hiyo nikatengeneza mpango biashara, kuanza kuajiri wafanyakazi na hivyo kuiweka hai ndoto yangu.” Amorette, ikiwa ni chata yenye mafanikio makubwa miongoni mwa watu wa daraja la juu nchini Tanzania na huku ikipanda kwa kasi na watu wakiifuata, Septemba 2016 Ntuyabaliwe alizindua Molocaho by Amorette kama kampuni ya kubuni na kutengeneza samani.

   Miezi michache tu tangu kuundwa kwake kampuni imefanya vyema na inaonekana kunedelea kukua kimafanikio. "Tumekuwa katika pilikapilika sana," anasema na kuongeza: " Sikuwa natarajia kufanya biashara kama tulivyofanya katika miezi michache iliyopita." Ntuyabaliwe ndiye mbunifu mkuu wa Molocaho. Akitumia ufundi wa asili katika mazingira ya sasa, Ntuyabaliwe hubuni na kutengeneza samani za kuvutia kwa ajili ya majumbani na maofisini na hata kwa watu binafsi. 

  Ukiangalia samani za Molocaho utabaini uzuri wake kusukwa kwa namna rahisi lakini yenye hisia kali na hivyo kufanya ubunifu wake kuwa wa bashasha , uliotulia na wenye kutuliza kiu. Lakini ukiangalia kwa karibu zaidi utabaini kwamba kile unachokiona rahisi ni tata, kimeumbwa kwa namna ambayo ni makini na yenye ugumu wa aina yake kwa lengo la kukupatia kitu bora kabisa. Hivyo ndivyo Ntuyabaliwe anavyotaka unapoangalia samani zake yaani unaziona za kawaida lakini zenye uzuri na ubora wa hali ya juu. Kwa Ntuyabaliwe,ubunifu wa samani za Molocaho unatokana na wakati mwingine na mambo ambayo hukuyatarajia kabisa. Wakati mwingine tukio asili linaweza kabisa kusababisha ubunifu wa aina Fulani. Mathalani tukio la radi (mwale na mlipuko) ndio uliotengeneza kiti kinachoitwa radi ambacho kimefanya vyema katika mauzo ya ndani na nje. Katika kiti hiki sehemu ya kuegemea kuna mwale wa radi. 

  Molacaho hutengeneza vitu kwa namna ambavyo mteja anataka na maana yake kazi zake nyingi ni za oda. “Wateja wetu huangalia kitabu chetu cha aina mbalimbali za samani kisha wanachagua wanachotaka na kutueleza kitu gani cha ziada wanataka kiwepo. Na hapa huwa tunafanya mazungumzo na wateja wetu ili tuweze kufahamu hasa wanachofikiria na wanachohitaji,” anasema Ntuyabaliwe. Samani zinazotengenezwa kutokana na maagizo kwa kawaida ni gharama kwa kuwa hutengenezwa kwa mahitaji ya mteja.

  Ntuyabaliwe anakiri kwamba Watanzania wengi hawana uwezo wa kununua bidhaa zake. Wengi wa watanzania ni maskini; Bidhaa za Molacaho zinaanzia kokote kule kuanzia dola za Marekani 250 kama stuli hadi dola za Marekani 6,000 kwa kitanda. “Bidhaa zetu zimepambanua wateja,” anasema na kuongeza kwamba wao si rahisi lakini pia si ghali sana.

   “kazi zetu si rahisi sana na wala si ghali sana hapa mjini. Mwishoni wa siku huwa tunapata taarifa kutoka kwa wateja wetu kwamba tuna bei nzuri kulinganisha na bidhaa tunazotengeneza.” Wakati Ntuyabaliwe anatengeneza fedha amesema pia anatengeneza mfumo wa kuwaendeleza mafundi nchini Tanzania. Mapema mwaka huu, Amorette, kampuni yake inayoshughulika na ubunifu wa masuala ya ndani ilianzisha programu ya kusimamia mafunzo kwa mafundi wa hapa Tanzania.

  Lengo kuu ni kuwafanya mafundi wa Tanzania kufikia uwezo wa kubuni na kutengeneza bidhaa zenye hadhi ya kimataifa. Chini ya programu hii, mafundi ambao tayari wana ujuzi na kufanya shughuli za useremala au kitu kinachofanana na hicho wanapewa mafunzo ya miezi miwili na mafundi wanaotambulika kimataifa. 

  Nia ni kuhamisha maarifa, ujuzi na teknolojia kutoka kwa wataalamu hao wa kimataifa na kuwawezesha watanzania kubadilika katika utendaji. Molocaho pia wamejikita katika kuhifadhi mazingira kwa kuhakikisha kwamba hakuna wanachotupa kinachotokana na mchakato wa kutengeneza samani. Kampuni hii hutumia bidhaa za mbao kutoka katika vyanzo mbalimbali na pia inaunga mkono kampeni mbalimbali za upandaji miti nchini Tanzania. “Mwishoni mwa siku biashara si tu iwe inayoleta faida lakini pia lazima ijali maslahi ya jamii ambapo biashara hiyo ipo,” 

  anasema. Leo hii, Molocaho imeajiri zaidi ya wafanyakazi wa kudumu 30 huku wakiwa katika njia nzuri ya kutengeneza faida katika kipindi cha mwaka mmoja tu tangu kuanzishwa kwake. “Hakika tumeanza,” anasema Ntuyabaliwe wakati tunaondoka katika duka la Molocaho. "Tutaendelea kumkuza mtoto huyu ili siku moja awe kampuni kubwa. Wewe tufuatilie tu" Imeandikwa na Mfonobong Nsehe , wa Forbes na kutafsiriwa kwa wasomaji wa Kiswahili na Mzige Media kupitia TheBeauty.co.tz

older | 1 | .... | 1153 | 1154 | (Page 1155) | 1156 | 1157 | .... | 1898 | newer