Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live

WAZIRI MBARAWA AZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA BENKI YA EXIM YA KOREA

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akimsikiliza Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong (wa pili kushoto), ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong, kuhusu uwekezaji wa miradi inayotekelezwa na Wizara hiyo, ofisini kwake leo, jijini Dar es Salaam.
Moja ya mradi uliokuwa ukijadili na ugeni kutoka Mwakilishi wa Dar es Salaam kutoka Benki ya Exim ya Korea Bw. Lee Hyonjong na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa leo, jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

MADIWANI MUFINDI WAPITISHA ENEO JIPYA LA UJENZI WA OFISI ZA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI

$
0
0
Hatimaye baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limepitisha na kulitambua rasmi eneo lililopo kata ya Igowole kuwa ndipo zitakapojengwa Ofisi za makao makuu ya halmshauri hiyo hivyo, kuruhusu kuanza kwa ujenzi wa mradi wa kwanza wa hospitali ya halmshauri ya Wilaya katika eneo teule.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Ofisa habari na mawasilino wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Ndimmyake  Mwakapiso, amesema baraza hilo limefanya uamuzi huo wa  kihistoria wakati wa kikao cha baraza maalum lililoitishwa kwa mujibu wa kanuni  kwa agenda maalum ya kuridhia mapendekezo ya kamati teule ya wataalamu iliyopendekeza maeneo katika   vijiji vya Ibatu na Nzivi vilivyopo kata ya Igowole.

Ofisa habari huyo, ametaja baadhi ya vigezo vilivyozingatiwa wakati wa kulipitisha eneo hilo, kuwa ni pamoja na utayari wa wananchi na halmshauri za vijiji kulitoa eneo bure bila kudai fidia, Eneo kuwa ubali wa km 13 kutoka barabara kuu, eneo  kupendekezwa kwa asilimia 29 wakati wa mchakato wa kusaka maoni katika kata 27 za halmshauri, likifuatiwa na Nyololo kwa asilimia 25 sanjari na Ukubwa wa eneo lenyewe likiwa na ekali 127.

Uamuzi huo umefikiwa ikiwa ni takribani mwaka mmoja baada ya kuzaliwa kwa halmshauri mpya ya Mji wa Mafinga ambao kwa sasa ndiyo wenye mamlaka kamili ya kuuendesha mji huo. Aidha, uongozi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi umewashukuru wenyeviti wa kamati za kata na wanamufindi kwa ujumla wao kwa ushirikiano waliounesha wakati wa  kupendekeza eneo la ujenzi wa  makao makuu ya halmshauri.
 Mkurugenzi wa halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Profesa Riziki Shemdoe akizungumza mara baada ya kupitishwa kwa eneo la ujenzi wa makao makuu.
Mwenyekiti wa kamati  iliyokuwa imeundwa kwa ajili ya kutafuta eneo la ujenzi Bw. Ubisimbali Jeswald akiwasilisha kazi yao kwa baraza la Madiwani la halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mufindiwakimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa kamati wakati anawasilisha kazi walioifanya na kamati hiyo.

PROF. MUHONGO AZINDUA MAFUNZO YA TAA, CHAJA ZA MIONZI YA JUA

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
 Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
 Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung   Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.
 Mtaalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emmanuel Yesaya, akizungumza jambo kuhusu utekelezaji wa REA awamu ya Pili na ya Tatu, katika Kata hiyo wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) na wananchi wa Kata ya Nyegina.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua vitabu ambavyo baadhi alivigawa katika katika Kituo cha Sekondari ya Nyegina katika shule mbalimbali Mkoani Mara. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegina na Paroko wa Parokia hiyo, Padri Leo Kazeri.
 Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung (wa tatu kulia) akiwa ameshika Taa za mfano ambazo vijana 20 kutoka Kata ya Nyegina watapewa mafunzo ya namna ya kuzitengeneza. Wengine wanaofuatilia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini Dkt. Vicent Naano,(wa tatu kushoto) Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Dkt. Hong-Kyu Choi (wa pili kushoto) na wawakilishi wa mafunzo hayo.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiweka tofali katika moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Msingi Kata ya Bwasi, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. Wengine ni Viongozi wa Vijiji, Halmashauri na wananchi wa Kijiji cha Kome.
 Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye tisheti nyeusi) akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kome mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuongea na wananchi wa Kijiji hicho.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimsikiliza mmoja wa wananchi aliyehudhuria katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kijiji cha Kome. Wengine ni wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Kome.


Waziri wa Nishati na Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo amezindua Mafunzo ya  namna ya Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20  katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.

Akifungua mafuzo hayo Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa  wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.

Profesa Muhongo amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu kutokana na umuhimu  na mchango wake kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Akizungumzia kuhusu Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa, awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa, mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe vimeunganishwa na nishati hiyo.

" Vijiji vyote vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza  awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.

Kwa upande wake Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili mafunzo hayo, amesema kuwa,  uwepo wa taa hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado hayajaunganishwa na nishati hiyo.

Aidha, amesema kuwa, mafunzo hayo ni fursa ya ajira kwa wahitimu watakaopata mafunzo hayo ikiwemo nafasi za kuajiriwa na hivyo kuwataka kutilia mkazo mafunzo hayo na kueleza kuwa, mafunzo hayo ni mwanga kwa vijana.

Aidha, ameongeza kuwa,  kutokana na urafiki wa miaka mingi baina ya nchi za Tanzania nasini , hirikinchi hiyo itlea kushirikiana na Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na umeme wa uhakika."Kama ilivyo kwa kaulimbi ya Awamu ya  Tano ya Rais Dkt. John Magufuli, Hapa Kazi Tu' na mimi napenda kusema tusiende polepole twende 'Haraka, Haraka", amesisitiza Balozi  Geumyoung.

Kwa mujibu wa Professa Muhongo mafunzo hayo yanatarajiwa pia kutolewa katika  Kata za Mwirangi, Bukima na Mgango. Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dkt.  Hong- Kyu Choi, amesema kuwa, baada ya kuzifikia Kata zote zilizoainishwa, watachaguliwa wanafunzi bora ambao watakuwa mabalozi wa mafunzo hayo na hivyo kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia mafunzo hayo na kuyachukulia kwa uzito mkubwa.

Mbali na kufungua mafunzo hayo, Profesa Muhongo pia amekagua miradi ya umeme Awamu ya Pili inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kome katika kijiji cha Kome, Kata ya Bwasi. Mafunzo hayo yamezinduliwa tarehe 20 Februari,2017

NHC KUJENGA NYUMBA 300 KWA AJILI YA WATUMISI WA UMMA DODOMA

$
0
0
Na Georgina Misama – MAELEZO.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limejipanga kumaliza kero ya makazi ya nyumba kwa watanzania ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamesemwa na Meneja Mauzo wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) Bw. Erasto Chilambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Ili kutimiza azma hiyo,Chilambo alibainisha kuwa nyumba zisizopungua elfu 30 zitajengwa kwa ajili ya kuuzwa na kupangishwa ambapo katika nyumba hizo watu wa kipato cha chini, kati na juu ndio walengwa.

“Katika mkakati huu, Shirika limekusudia kujenga nyumba 12000 kwa ajili ya watu wa kipato cha chini, nyumba 13500 kwa ajili ya watu wenye kipato cha kati na nyumba 2700 kwa ajili ya watu wenye kipato cha juu.” Alisema Chilambo.

Aidha, Shirika linajenga majengo 1800 ya kibiashara katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo yanatazamiwa kukamilika ifikapo 2025.

“Katika kuunga mkono uamuzi wa serikali wa kuhamia Dodoma, shirika linajenga nyumba za makazi 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa Serikali, ambazo zina ukubwa tofauti zenye vyumba 3 kila moja.” Alisema Bwn.Charahani.

Tangu kuanzishwa kwake Shirik la Nyumba limekuwa likimiliki na kuuza majengo mbalimbali. Hivi sasa shirika linamiliki MAJENGO 2483 yenye sehemu 18121 za makazi na biashara katika Mikoa ya Tanzania Bara.
Meneja Mauzo wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) Bw. Erasto Chilambo akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es salaam kuhusu mkakati wa shirika hilo kujenga nyumba 300 zitakazouzwa kwa watumishi wa umma Mkoani Dodoma ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa makazi kwa watumishi wanaohamia Mkoani humo na kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamia mkoani humo.kushoto ni Afisa Habari wa Shirika hilo Bi Edith Nguruwe.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa NHC leo Jijini Dar es Salaam.

MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM PAUL MAKONDA AKABIDHIWA HEKALI 1500 NA AZIMIO HOUSING ESTATE LEO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekabidhiwa hekali 1500 na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate Mohamed Iqbal kwa ajili ya viwanda vidogo.

Akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni Mkurugenzi huyo amesema wameamua kumkabidhi eneo hilo RC Makonda kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli za kuijenga Tanzania ya viwanda ili kuwakomboa wananchi wenye uchumi wa kati.

Kwa upande wake RC Makonda ameeleza kuwa dhamira ya viwanda ya Rais Magufuli inabidi itafsiriwe kwa vitendo, hivyo eneo hilo litatumika kwa ajili ya ufugaji, kilimo, usindikaji, utengenezaji wa sabuni na eneo hilo litatumika na wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam.

Pia RC  Makonda ameongeza kuwa Mkoa wa Dar es Salaam unajengwa na wana Dar es Salaam wenyewe hivyo kama kuna watu wanataka kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Dar es Salaam wafanye hivyo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo  eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul  Makonda akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa wakiangalia ramani ya eneo hilo, leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe: Paul Makonda  (watatu kutoka kulia)  akiwa amefuatana na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa, na Mkurugenzi wa Azimio Housing Estate,Mohamed Iqbal    wakikagua eneo hilo
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa,
Muomoneke wa  eneo hilo alilokabidhiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

WAZIRI MKUU AENDELEA NA ZIARA MKOANI MANYARA LEO

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi ya Katesh wilayani Hanang, Mkoani Manyara leo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanya uzinduzi wa madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu Wilayani Hanang Mkoani Manyara leo, wakati akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoa wa Manyara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wananchi wa Hanang Mkoani Manyara baada ya kuzindua madarasa ya shule ya Msingi ya Mogitu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na baadhi ya wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiangalia ngoma ya asili.

KATIBU MKUU WA MAMBO YA NJE AFUNGUA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA SADC-ISPDC

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz P. Mlima, akifungua Mkutano cha Makatibu Wakuu nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Kamati Ndogo ya Mawaziri ya Siasa na Diplomasia ya SADC (Inter State Politics and Diplomacy Sub Committee-ISPDC) unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 na 24 Februari, 2017. Mkutano wa Makatibu Wakuu unafanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. 
Sehemu ya wajumbe wa Mkutano kutoka katika mataifa ya nchi wanachama wakifuatilia mkutano. 
Kaimu Mkuu wa Mabalozi Mhe. Balozi Edzai Chimonyo (wa kwanza kushoto) na wajumbe wengine wakifuatilia mkutano.
Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. Stergomena Tax (wa pili kushoto) na wa kwanza kulia ni Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakifuatilia mkutano. 
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Mkutano.

WASTAAFU WANAOLIPWA NA HAZINA WAJITOKEZA KUHAKIKIWA ZANZIBAR-WAILIIA SERIKALI IWAONGEZE PENSHENI

$
0
0
Mkaguzi wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha na Mipango-Bara, Bw. Paison Mwamnyasi (aliyenyoosha mkono) akitoa maelekezo kwa wastaafu wanaolipwa pensheni zao na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, waliofika katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, eneo la Vuga, kwa ajili ya uhakiki.
Zoezi la uhakiki likiwa linaendelea katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, kulia ni mstaafu Bw. Amir Apacho akifanyiwa uhakiki na Mkaguzi Bi. Mary Mauki.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe (kushoto) akimfanyia uhakiki Bw. Abas Abdulan (kulia) pembeni yao ni baadhi ya wastaafu wakisubiri kupata huduma ya kuhakikiwa, katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, zilizoko katika eneo la Vuga.
Mchambuzi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta Bi. Magreth Ambrosi Akipokea namba kutoka kwa mstaafu (aliyeko dirishani) aliyopewa kwa ajili ya uhakiki. Uhakiki wa Wastaafu unafanyika katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, katika eneo la Vuga.
Baadhi ya wastaafu ambao ni wagonjwa wakisubiri kupata huduma wakiwa wametengewa sehemu maalumu kwa ajili ya kupata huduma hiyo ya uhakiki.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu Msaidizi Bw. Stanslaus Mpembe, akifanya mahojiano na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar. kushoto kwake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Paison Mwamnyasi.
Watumishi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakibadilishana mawazo kuhusu namna uhakiki unavyoendelea. Kutoka kulia ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Paison Mwamnyasi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bw. Benny Mwaipaja, Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane pamoja na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar Bw. Abdulrahim Mohamed
Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango akimfanyia uhakiki Bw Uleja Edward katika ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, zilizoko eneo la Vuga visiwani humo.
Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko-Zanzibar, Mhe. Balozi Amina Salum Ali, alipowasili katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki. Aliyesimama mbele yake ni Mkaguzi wa Ndani Bw. Nicholaus Jalane.

…………………………………………………………………….

Benny Mwaipaja, WFM, Zanzibar

MAMIA ya wastaafu wa Taasisi za Muungano kutoka visiwa vya Pemba na Unguja-Zanzibar, wanaolipwa na Wizara ya Fedha na Mipango ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wamejitokeza kwa wingi kuhakikiwa huku wakiiomba Serikali iwaongezee pensheni kutokana na wengi wao kukabiliwa na hali ngumu ya maisha.

Wakizunguza katika Ofisi za Wizara ya Fedha na Mipango-Zanzibar, iliyoko katika eneo la Vuga, wastaafu hao wamepongeza hatua ya Serikali ya kuwahakiki ili kufahamu hali zao na kwamba hatua hiyo itasaidia kuwabaini watu wasio na sifa ya kupata malipo hayo kutoka Serikalini

Wastaafu Bi Sauda Ramadhani Mpambalyoto na Abuu Ali Hamisi, wameiomba Serikali iangalie namna ya kuwaongezea pensheni wataafu ambao wengi wao ni wagonjwa hawajiwezi na wengine wana afya njema, wanalima, lakini wanahitaji kuwezeshwa na Serikali ili waweze kumudu maisha ambayo wamesema yamepanda.

Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali Msaidizi, Bw. Stanslaus Mpembe, amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango inaendesha zoezi la kuhakiki wastaafu wanaolipwa pensheni na wizara hiyo ili kuhuisha taarifa za wastaafu kwa lengo la kupata kanzidata (database) iliyo ili kuiwezesha Serikali kuwalipa wastaafu wanaostahili.

Amesema kuwa wastaafu wanaolipwa na Wizara hiyo ambao hawatahakikiwa wataondolewa kwenye orodha ya malipo ya pensheni kwa kuwa watakuwa wamekosa sifa.

Aidha Bw. Mpembe amesisitiza wastaafu hao kufika wenyewe na sio kutuma wawakilishi, wakiwa na nyaraka zote muhimu zikiwemo barua ya tuzo la kustaafu, barua ya kustaafu au kupunguzwa kazini, nakala ya hati ya malipo ya kiinua mgongo au mkupuo, barua ya ajira ya kwanza, kitambulisho cha pensheni, barua ya kuthibitishwa kazini, kadi ya benki na picha mbili ndogo zilizopigwa hivi karibuni.

Amesema kuwa zoezi la uhakiki wa wastaafu wanaolipwa na Hazina, litakamilika Mkoa wa Dar es salaam kuanzia Machi 6 hadi 10, mwaka huu 2017

Zoezi hilo la uhakiki linaloendelea Zanzibar, lilianza Oktoba 20, 2016 katika mkoa wa Pwani na limeshafanyika katika mikoa 25 ya Tanzania Bara ambayo ni Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma, Songwe, Katavi, Rukwa, Morogoro, Dodoma, Singida, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Tanga, Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Simiyu, Geita, Kigoma na Tabora, Lindi na Mtwara.

Bayport yatoa kompyuta nne kwa shule za Msingi Dodoma Mjini

$
0
0
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mvunde (kulia) akipokea msaada wa Kompyuta Nne kwa Meneja Masoko na Mawasiliano wa Taasisi ya Kifedha Bayport Tanzania, Ngula Cheyo mjini Dodoma leo asubuhi. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa taasisi hiyo, Kushoto ni Meneja wa Kanda ya Kati wa taasisi hiyo, Christopher Kihwele.


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

TAASISI ya Kifedha ya Bayport Financial Services, jana imemkabidhi kompyuta nne Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mheshimiwa Anthon Mavunde kwa ajili ya shule za Msingi za Majengo, Chigonge, Mahomanyika na Uhuru zilizopo mjini Dodoma.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Majengo, wakinyoosha mikono juu katika tukio la kukabidhiwa kompyuta nne za Bayport Financial Services, zikipokewa na Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.

Makabidhiano hayo yalifanyika katika shule ya Msingi Majengo, ambapo kompyuta hizo zina lengo la kuongeza kiwango cha elimu mkoani Dodoma. Akizungumza leo mjini Dodoma, Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo, alisema kwamba msaada huo wa kompyuta umetokana na dhamira yao ya kusaidia jamii kwenye sekta ya elimu kama njia ya kuikomboa jamii.

Alisema kwamba si mara ya kwanza kusaidia sekta ya elimu kutokana na kujitokeza mara kadhaa kujenga madarasa, kununua thamani za shule pamoja na kudhamini mikopo ya elimu ya juu na vitabu.
Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Majengo, wakisoma shairi mahususi kwa ajili ya Naibu Waziri wa Kazi, Ajira, Vijana, Anthony Mavunde wakati anakabidhiwa kompyuta nne kutoka kwenye taasisi ya Bayport Financial Services.

“Bayport tuna lengo la kuikwamua jamii katika maendeleo kwa kuhakikisha kwamba tunakuza kiwango cha elimu, hivyo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali kuhamia Dodoma, tumeamua kutoa kompyuta nne kwa kuboresha miundo mbinu ya elimu ili nchi yetu isonge mbele.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo akizungumza jambo katika makabidhiano ya kompyuta nne kwa Naibu Waziri, wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde.
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mvunde (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhiwa msaada wa kompyuta Nne kutoka Taasisi ya Kifedha ya Bayport Tanzania mjini Dodoma jana.


“Hatujaanza leo kusaidia jamii, ukizingatia kwamba kompyuta hizi nne zenye thamani ya Sh Milioni 10 kwa shule za msingi mjini Dodoma ni tofauti na zile 205 tunazotoa kwa serikali,” Alisema Cheyo.


Akipokea kompyuta hizo, Naibu Waziri aliwashukuru Bayport kwa msaada wao, akisema umekuja wakati muafaka na kuamini kuwa utasaidia kukuza kiwango cha elimu katika Mkoa wa Dodoma ambapo ndio Makao Makuu ya Tanzania.


“Tunawashukuru Bayport kwa msaada wenu, wananchi wa Dodoma tumeupokea kwa furaha kwa sababu unatufanya tupige hatua kubwa kukuza elimu, ukizingatia kuwa mipango yangu kama mbunge ni kusambaza kompyuta kwa kila shule ili wanafunzi wetu wafanye mitihani kila mwisho wa wiki kama sehemu yao ya kujiandaa na mitihani ya Taifa,” Alisema Mavunde.


Naye Afisa Elimu wa Manispaa ya Dodoma, Scolastica Kapinga, alisema juhudi zao za kukuza kiwango cha elimu utafanikiwa kwa kupokea kompyuta hizo zilizotolewa na Bayport kwa juhudi kubwa za mbunge wao.


Bayport ni taasisi inayotoa mikopo ya fedha na bidhaa, ikiwamo ardhi yenye hati, ambapo pia imekuwa ikijitokeza mara kadhaa kusaidia mambo ya kijamii kwa kutoa misaada mbalimbali kama sehemu ya kurudisha faida kwa jamii.


KATIBU WA NEC IDARA YA SIASA NA UHUSIANO WA KIMATAIFA CCM KANAL MSTAAFU NGEMELA LUBINGA ATEMBELEA UVCCM OFISI NDOGO DAR ES SALAAM LEO.

$
0
0
Kaimu katibu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa pili kulia akimuonyesha ofisi mbalimbali Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo Makao Makuu ya UVCCM Taifa

Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akitoa ufafanuzi na kumkaribisha Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga kuzungumza na wajumbe Wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

Viongozi Wakimsikiliza kwa makini

Mkuu wa Utawala UVCCM Taifa Omary ng’wanangwalu akimsikiliza Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga


Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga akizungumza Wajumbe Sekretariet Ya UVCCM TAIFA pamoja na wafanyakazi Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.

picha ya Pamoja ya Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Wajumbe wa Sekretariet Ya UVCCM TAIFA Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Taifa Shaka Hamdu Shaka akizungumza jambo na Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga Ofisi ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.



Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi Ndogo Makao Makuu ya UVCCM Taifa.

Naibu Katibu UVCCM Bara Ndg:Mfaume kizingo akiagana na Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu
Ngemela Lubinga Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam.
wajumbe wa Sekretariet ya UVCCM Taifa wakimuaga Katibu wa NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga Ofisi Ndogo Makao makuu Uvccm Dar es Salaam. picha zote nz fahady siraji

KITUO CHA FORODHA CHA MPAKA WA TUNDUMA/NAKONDE (TANZANIA NA ZAMBIA) CHAANZA KUFANYAKAZI

$
0
0
Kaimu Afisa Uhamiaji Mfawidhi wa Kituo cha mpakani Tunduma/Nakonde, Bw. Tabaran Mzee, (aliyevaa sare za uhamiaji), akieleza namna idara hiyo ilivyoanza utekelezaji wa uanzishwaji wa Kituo cha Pamoja cha Forodha kati ya Tanzania na Zambia, ambapo wafanyakazi wa idara hizo kutoka nchi hizo mbili wanafanyakazi katika jengo moja kila upande wa nchi ili kuboresha ufanyaji biashara mpakani.
Maafisa Forodha na Idara ya Uhamiaji katika Mpaka wa Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia), wakiwa katika picha ya pamoja na Ujumbe wa Serikali uliotembelea mpaka huo ili kukagua uanzishwaji rasmi wa Kituo cha pamoja cha Forodha kati ya nchi hizo mbili. Waliosimama mstari wa kwanza kuanzia kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, Mkuu wa Wilaya ya Momba-Mbeya, Bw. Juma Irando, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia biashara na uwekezaji), Prof. Adolf Mkenda, akionesha kibao chenye namba za simu kilichowekwa Idara ya Forodha katika mpaka wa Tunduma/Nakonde zitakazotumiwa na wadau endapo watakuwa na malalamiko yoyote, lengo likiwa ni kuboresha huduma katika mpaka huo ambapo huduma ya pamoja ya forodha kati ya Tanzania na Zambia imeanza kutolewa rasmi tangu Februari mosi mwaka huu.
Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha, Viwanda, na Mambo ya Ndani, wakizungumza na Afisa Forodha wa Zambia aliyeko katika Kituo cha Forodha cha Tunduma upande wa Tanzania, baada ya Ujumbe huo wa Serikali kutembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara ikiwa ni siku kadhaa baada ya kuanza rasmi kwa huduma ya Kituo cha Pamoja cha Forodha katika mpaka huo wa Tunduma/Nakonde (Tanzania na Zambia).
Mkuu wa Wilaya ya Momba mkoani Mbeya Bw. Juma Irando (aliyenyoosha kidole) akieleza jambo baada ya ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea mpaka huo kukagua shughuli za biashara baada ya kuanza rasmi kwa huduma za Kituo cha Pamoja cha Forodha mpakani Tunduma/Nakonde.
Makatibu Wakuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, pamoja na maafisa waandamizi kutoka Ofisi ya waziri Mkuu, Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Idara ya Uhamiaji na vyombo vya ulinzi na usalama, wakikagua shughuli za biashara katika mpaka wa Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde)
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia, Bw. Nase Lungu (Kulia) akitoa maelezo kwa Ujumbe wa Tanzania namna shughuli za Kituo cha Pamoja cha Forodha Mpakani, upande wa Nakonde (Zambia) zilivyoanza kwa mafanikio na kupunguza usumbufu ambao watumiaji wa mpaka huo wakiwemo wafanyabiashara walikuwa wakiupata kabla ya kuanzishwa kwa huduma hiyo
Ujumbe wa Tanzania ukidodosa mambo mawili matatu namna shughuli za Kituo cha Pamoja cha Forodha Mpakani, upande wa Nakonde (Zambia) kinavyo fanyakazi pamoja na changamoto wanazokumbana nazo katika siku za mwanzo za utoaji wa huduma ya forodha kwa pamoja katika mpaka huo wa Tunduma/Nakonde, mapema mwezi Februari, 2017.
Kituo cha Uhamiaji na Forodha cha Tanzania kilichoko kwenye jengo la Zambia upande wa Nakonde, baada ya kuanzishwa kwa Kituo cha pamoja cha Forodha cha Mpakani mwa Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde)
Meneja wa Mamlaka ya Mapato Zambia, Bw. Nase Lungu (Kushoto) akiusindikiza Ujumbe wa Tanzania uliotembelea Kituo cha Forodha cha Zambia (Nakonde), uliokwenda kukagua huduma ya pamoja ya forodha baada ya huduma hiyo kuzinduliwa rasmi mapema mwezi Februari, 2017.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji (anayeshughulikia Biashara na Uwekezaji) Prof. Adolf Mkenda, akifanya mahojiano na dereva wa lori lililokuwa likivuka mpaka kuelekea nchini Zambia, ili kubaini changamoto zinazo wakabili wasafirishaji hao wa shehena, ambapo walipongeza kuanza kwa utaratibu wa pamoja wa utoaji huduma mpakani na kuomba mfumo huo usaidie kuwapunguzia muda wa kukaa mpakani.

………………………………………………………………..

Benny Mwaipaja, WFM, Tunduma

KITUO cha Pamoja cha Forodha cha mpaka kati ya Tanzania na Zambia (Tunduma/Nakonde) kimeanza rasmi kutumika licha ya kukabiliwa na msongamano mkubwa wa magari unaotakiwa kupatiwa ufumbuzi wa haraka.

Kituo hicho kimeanza kufanyakazi tangu Februari mosi mwaka huu, ambapo watumiaji wa mpaka huo watakuwa wakihudumiwa upande mmoja wa mpaka badala ya utaratibu uliokuwa ukitumika awali ambapo watumiaji walilazimika kukaguliwa mizigo yao kila upande hatua iliyokuwa ikichelewesha biashara katika mpaka huo

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda na Naibu Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, wameeleza kuridhishwa na kazi inayofanyika mpakani hapo kupitia mfumo huo mpya.

Hata hivyo baadhi ya madereva wanaosafirisha bidhaa kupitia mpaka huo wa Tunduma na Nakonde, pamoja na kupongeza utaratibu huo mpya, wameiomba Serikali iwasiliane na upande wa Zambia, ili waongeze kasi ya kuruhusu malori kuendelea na safari yanapofika mpakani hapo bila kucheleweshwa ili kwenda sambamba na kasi ya upande wa Tanzania, ambao umeboresha kwa kiwango kikubwa utoaji wa huduma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Adolf Mkenda, amesema kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na watoa huduma katika mpaka huo yalikuwa ni kuwahudumia wadau wanaotumia mpaka huo kwa muda usiozidi siku moja na kuwataka madereva wa malori wanaokwazwa kuwasiliana na mamlaka zinazohusika.

Prof. Mkenda amewaonya mawakala wa Forodha katika mipaka yote nchini watakao bainika kwa namna moja au nyingine kuwachelewesha wenye malori kwa makusudi watafutiwa leseni zao za kufanya biashara hiyo

“Tunataka mpaka huu wa Tunduma na Nakonde ufanye kazi kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu ili kuiwezesha bandari yetu ya Dar es Salaam kufanyakazi kwa kiwango cha juu ili kukuza biashara nchini” Alisisitiza Prof. Mkenda

Amesema kuwa Serikali imeunda timu ya wataalam wanaopitia kero mbalimbali za mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji hapa nchini, itakayo peleka mapendekezo namna ya kuboresha mazingira hayo kwa kuwa mchango wa sekta binafsi wakiwemo wawekezaji, unatambuliwa na Serikali

Kwa upande wao, Afisa Mfawidhi wa Forodha , Idara ya Forodha na Ushuru wa Bidhaa-Tunduma, Bw. Magori Magori, na Mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka, wameelezea kukithiri kwa vitendo vya magendo mpakani na kero ya vizuizi lukuki kwenye njia kuu ya Dar es salaam hadi Tunduma, hatua inayokwaza biashara kati ya Tanzania na Zambia.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuchunguza na kuishauri Serikali namna ya kuboresha matumizi ya pesa ya Zambia (kwacha) ili kupunguza changamoto ya ufanyaji holela wa biashara ya kubadilisha fedha hiyo katika mpaka wa Tunduma/Nakonde upande wa Tanzania na Zambia na mpaka wa Kasumulu/Songwe, upande wa Tanzania na Malawi.

Maagizo hayo yanafuatia kuwepo kwa biashara holela ya ubadilishaji fedha hiyo mpakani huku Benki Kuu ikieleza kuwa fedha hizo (kwacha) haziko kwenye orodha ya fedha za kigeni zinazotambulika rasmi hapa nchini hivyo kuwa vigumu kudhibiti mwenendo wake.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya, ameahidi kuwa wizara yeke itaifanyia kazi changamoto ya uwepo wa vizuizi vingi vya malori yaendayo masafa marefu kwakuwa vinasababisha adha isiyo ya lazima na kukwamisha biashara nje ya nchi.

“Kwa kuwa malori mengi yaendayo masafa marefu kutoka Bandari ya Dar es Salaam yanafungwa vifaa maalumu vya ufuatiliaji mwenendo wake, hakuna sababu ya trafiki kuyasimamisha kila wakati, tunataka lori likikaguliwa Dar es Salaam lisafiri bila kusimamishwa hadi litakapofika mpakani ambapo litafanyiwa ukaguzi wa mwisho” aliongeza Balozi Yahya.

Kuanza kufanyakazi kwa kituo cha pamoja cha Forodha cha mpaka wa Tunduma/Nakonde kunafuatia maagizo yaliyotolewa na Marais Dkt. John Pombe Magufuli na Edgar Lungu wa Zambia, alipofanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni ili kurahisisha biashara katika ya nchi hizo nan chi wanachama wa Jumuiya ya Madola-SADC, na kama mambo yatabaki kama yalivyopangwa, kitazinduliwa rasmi na Mawaziri wa kisekta mwezi Machi, mwaka huu.

KANALI MSTAAFU NGEMELA LUBINGA AMTEMBELEA NAIBU WAZIRI MASAUNI OFISINI KWAKE JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita. Mazungumzo hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam.Katikati ni msaidizi wa Katibu huyo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga,akizungumza na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akifafanua jambo kwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC), Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, alipomtembelea kujadili masuala mbalimbali yaliyohusiana na utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi Mkuu uliopita.Mazungumzi hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

MSAADA UNAHITAJIKA KWA MTOTO CATHERINE

$
0
0
Mzazi wa mtoto Catherine anaomba msaada wako wa hali na mali kumuweza mtoto huyu mwenye ulemavu aweze kulipa ada yake ili aendelee na masomo . Mtoto huyu anasoma shule ya St.Bernard, lakini kutokana na mama yake kutokuwa na uwezo hivi sasa wa kulipa ada mtoto yuko nyumbani. Mama wa mtoto huyu Flora anaomba wasamaria wema kuweza kumsaidia kulipa ada ya mtoto ili aweze kurudi shuleni. Kwa wale walioguswa mnaweza kutuma msaada kwa kupitia akaunti ya Evelyn Kamukuru 0112014797900 CRDB BANK

DKT. KIGWANGALLA ATEMBELEA VITUO VYA TIBA YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Naibu wa Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla afanya ziara ya kushtukiza kwenye kituo cha kuwahudumia watu wanaotibiwa kuacha dawa za kulevya kwa kutumia methadone kilichopo Hospitali ya Mwananyamala ili kuona namna huduma zinavyotikewa. 

Ameamua kufanya ziara hiyo sababu kuna ongezeko kubwa la wateja siku za hivi karibuni kutokana na kuongezeka udhibiti. Na kuna taarifa kwamba wanaouza dawa za kulevya (drug dealers) wameathiriwa sana kwa kupoteza mapato ya sh bilioni 70 kwa uwepo wa vituo hivi ambavyo kwa sasa vinahudumia wateja 3351, na hivyo wameanza kubuni mbinu za kuwarudisha kwenye matumizi ya dawa za kulevya kwa mbinu mbalimbali ikiwemo kudai kuwa methadone haifanyi kazi.

Dkt. Kigwangalla ameagiza:

1. Hospitali zote za kanda zianzishe vituo vya rehab ndani ya miezi 6

2. Hospitali zote za mikoa nchini zianzishe kliniki ya kutoa methadone ndani ya miezi 6

3. Katibu Mkuu afya ahakikishe kuna Daktari bingwa wa afya ya akili kwenye kila mkoa ili kuanzisha na kusimamia vituo vya kutoa tiba ya methadone

4. Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kinondoni aongeze eneo la kliniki sambamba na watumishi kwenye kituo hiki 

5. Kamishna wa polisi wa operesheni maalum afuatilie wateja (exit follow-up) wanaotoka kliniki ili kudhibiti mkakati wa drug dealers wanaolenga kuwarubuni na kuwarudisha kwenye dawa za kulevya wateja wa vituo hivi. 

Msafara wa Dkt. Kigwangalla umeelekea Temeke Hospitali kwenye kituo kingine kama hiki.

WADAU WA SEKTA YA FILAMU WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUJADILI SERA YA FILAMU

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.


SBL yaanza kuuza bia Kenya

$
0
0
Kwa mara ya kwanza, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imeanza kuuza nje ya nchi bidhaa zake katika soko la kikanda, eneo la kwanza likiwa ni nchi jirani ya Tanzania kwa upande wa Kaskazini, Kenya.

Shehena ya kwanza ya bia inayofahamika kama Allsopps ilisafirishwa kwenda Kenya wiki iliyopita na hivyo kukiweka kiwanda cha SBL kuwa mmoja wachangiaji wakubwa katika soko la kanda.

Akizungumzia kuhusu hatua hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha alisema; “Hii ni hatua nyingine ya kufurahisha katika kampuni yetu na kimsingi kwa bidhaa zetu. Ukweli unabakia kwamba kumudu kupenyeza ndani ya soko la Kenya kunaonesha kuwa ubora wa bidhaa zetu sio tu kwamba unakubalika na wateja wetu wa ndani bali pia zinakubalika katika soko kubwa la kikanda.”

Wanyancha alisema kuwa SBL inaangalia uwezekano wa kupanua mauzo ya biashara katika masoko mengine ya kikanda, hatua ambayo iko katika mkondo wa kuhamasisha Jumuia ya Afrika Mashariki na kada nyingine za kiuchumi kuongeza biashara yake ya kuvuka mpaka ndani ya ukanda huo.

SBL imekuwa inazalisha aina za bidhaa zinazotambulika kimataifa kama vile Pilsner Lager,Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness Stout, Uhuru, The Kick pamoja na bidhaa kuu ya Serengeti Premium Lager-ambayo peke yake imeshajizolea medali kumi zinazotambuliwa kimataifa.

WIMBO WA TAIFA WAZUA MJADALA BARAZA LA MADIWANI JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji
 Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam , Saed kubenea akizungumza wakati wa kikao cha baraza
 Diwani wa kata ya Kibonde Maji , Abdalah Mtinika akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani kilichafanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam
Mayor wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam
Madiwani wakiwa katika kikao baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee


Tatizo la wimbo wa Taifa na dua katika mkutano wa baraza la madiwani wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam umeweza kuzua mjadala kwa zaidi ya dakika kumi katikati ya mkutano huo.

Mjadala huo ambao uliibuliwa na mtoa hoja ,Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ambaye alitoa hoja ya kukiukwa kwa kanuni za uendeshwaji wa baraza hilo.
  
Mara baada ya kutoa hoja mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana alimuomba mwanasheria wa halmashauri kutoa ufafanuzi juu ya swala hili na kusema kuwa hakuna kitu kilichoaribika jambo ambalo lilipingwa vikali na madiwani wote.

Mara baada ya madiwani kumpinga mwanasheria huyo na Mstahiki meya waliamuliwa na madiwani hao kurudia kuimba wimbo wa taifa kasha kufuatiwa na dua jambo ambalo liliridhia kuanza kwa mkutano huo bila mgogoro.

Hoja nyingine aliyoibua kubenea ilikuwa ni kitendo cha kuanzishwa kwa mkutano huo bila ya akidi kutimia na kumlazimu kurudia tena kuhesabu watu hili kujiridhisha kuwa akidi imetimia.

Hata hivyo dakika chache baadae mkutano ulivyoanza ulikuwa kwa majibizano ya hoja mbalimbali ikiwemo juu ya namna uwasilishaji wataharifa hiyo.

Hata hivyo baraza hilo lilimalizika kwa Meya wa jiji Isaya Mwita kuairisha mkutano mpaka kesho

KAPUMZIKE KWA AMANI MPIGANAJI MWENZETU,TULIKUPENDA SANA LAKINI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI

$
0
0
Pichani Mpendwa wetu Jennifer Livigha aliyekuwa Mmiliki wa Libeneke la Chinga One na Mwanachama wa TBN Enzi za uhai wake. Marehemu alizaliwa 25.01.1979 Nachingwea, alifariki nyumbani kwake kinyerezi 18.02.2017 Jijini Dar es salaam. Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Ini. Atapumzishwa katika nyumba yake ya milele nyumbani kwao Nachingwea.
 Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika Ibada ya kuaga Mwili wa Marehemu Jennifer Livigha aliyekuwa mmiriki wa Blog ya Chinga One katika Hospitali ya Amana.
 Waongozaji wa Ibada ya kuaga mwili wa Marehemu Jennifer
 Waombolezaji wakiwemo baadhi ya wana Tanzania Bloggers Network (TBN) ambapo Marehemu Jennifer alikuwa mwanachama
 Mmoja ya waombolezaji akitoa historia fupi ya Marehemu
Mmoja wa wanafamilia akitoa utaratibu kabla ya kuanza kutoa heshima za Mwisho kwa mpendwa wetu Jennifer
 Baadhi ya wanachama wa Tanzania Bloggers Network (TBN) wakiwa wanaaga mwili wa aliyekuwa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer 'Chinga One'
Baadhi ya ndugu wa karibu, Jamaa na Marafiki wakiwa wanaaga Mwili wa Marehemu Jennifer
Baadhi ya waombolezaji wakiwa wanaimba nyimbo za maombolezo 
Baadhi ya wanachama wa TBN , ndugu, jamaa na marafiki wakiwa wanapeleka mwili wa Marehemu Jennifer katika Gari tayari kwa safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi
Baadhi ya wanafunzi wakilia kwa uchungu 
Baadhi ya ndugu, jamaa na mafafiki pamoja na wanachama wa TBN wakiwa wanawaaga wanaosafiri na mwili kuelekea Nachingwea
 Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (Aliyevaa T-Shirt ya Mistari) akiongea jambo kabla ya safari ya kuelekea Nachingwea kwa mazishi.
Baadhi ya wana TBN wakiwa katika Msiba wa mwanachama mwenzao Marehemu Jennifer
 Safari ya kuelekea Nachingwea ikiwa imeanza ..
Picha zote  na Fredy Njeje wa TBN

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete Akutana na Rais wa Chad na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa

$
0
0
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete jana tarehe 20 Februari 2016 amekutana na kufanya mazungumzo  na Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu yake jijini N'Djamena, Chad. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Chad Mhe. Ahmat Ghazali Acyl na Waziri wa Fedha Mhe. Diguimbaye Christian.

Ziara hiyo ya Rais Mstaafu nchini Chad ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Deby wamezungumzia janga kubwa linaloinyemelea dunia na hasa nchi za uchumi wa kati na chini ikiwa hakutafanyika mapinduzi makubwa katika sekta ya elimu. 

Viongozi hao wamezungumzia haja ya nchi za bara la Afrika kuchukua hatua z amakusudi kufanya maboresho na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu katika nchi zao ili kuweza kuendana na kasi ya nchi zilizoendelea. Azma hiyo inatokana na stadi kuwa nchi za uchumi wa kati na chini zko nyuma kielimu kwa miaka 50 hadi 70. Aidha, lipo tishio kuwa ifikapo mwaka 2050, kazi na ajira takribani bilioni 2 zitakuwa zimefutwa kutokana na maendeleo na matumizi ya teknolojia (automation).

Rais Deby amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.

Mbali na mkutano wake na Rais wa Chad, Rais Mstaafu amekutana pia na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake N'Djamena. Rais Mstaafu amempongeza Mhe. Fakhi kwa kuchaguliwa na Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja huo na kumtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya. Viongozi hao wawili wamekuwa pia na mazungumzo yaliyohusu mipango ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu barani Afrika na masuala ya hali ya usalama ya Libya.
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo  jijini N'Djamena, Chad.
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na  Rais wa Chad, Mhe. Jenerali Idrissa Deby Itno katika Ikulu ya nchi hiyo  jijini N'Djamena, Chad.
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
  Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena
 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa  na Mwenyekiti Mpya wa Kamisheni Umoja wa Afrika Mhe Moussa Fakhi nyumbani kwake jijini N'Djamena.

DC KINONDONI AENDELEA NA ZIARA YAKE MZIMUNI,APIGA MARUFUKU UUZWAJI WA MAGARI BARABARANI

$
0
0
AWAPA SIKU 14, WAFANYA BIASHARA NJE YA SOKO KUAMIA NDANI YA SOKO

Na Anthony John Glob Jamii. 
 
MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ameendelea na ziara ya kutembelea Kata za wilaya ya kinondoni, ikiwa siku ya pili ya ziara yake mkuu wa wilaya ametembelea kata Mzimuni, akiwa katika soko la Magomeni, ametoa siku 14 kwa uongozi wa soko hilo kuhakikisha wanaondoa baa na ghala vilivyopo katikati ya soko hilo.

Akiwa ndani ya soko hilo, Hapi alisema inasikitisha kuona hata wamiliki wa ghala hizo hawafahamiki.Alisema uwepo wa ghala na baa katikati ya soko hilo inasababisha kuwanyima fursa wafanyabiashara walio wengi hasa wale wadogo.

"Ninatoa siku 14 kwa viongozi wa soko na manispaa kuhakikisha wanaaondoa maghala haya kwani inaonyesha ni ya wafanyabiashara wakubwa hivyo waende kwa wenzao hapa hapawafai,"alisema Hapi.

Sambamba na hilo mkuu huyo ametoa siku 14 nyingine kwa wafanyabiashara wanaofanya biashara nje ya soko hilo kurejea ndani ya.soko.Alisema sheria zipo wazi na hakuna aliyejuu ya sheria zaidi ya kuzingatia sheria hizo.

"Hakuna aliyeruhusu wafanyabiashara wengine kufanya biashara nje ya soko,  hivyo naagiza ndani ya siku 14 wote mhamie ndani kwa sababu mnaleta usumbufu kwa wengine na kuleta malalamiko,"alisema Hapi.

Baadae mkuu wa wilaya alifanya mkutano wa adhara katika shule msingi Mikumi, katika mkutano huo wananchi waliuliz maswali mbali mbali lakini kero kubwa imeonekana kuwa viongozi wao sio waaminifu hukusanya pesa kwa wananchi lakini hafanyi yaliyokusudiwa, mkuu wa wilaya akijibu hoja hiyo ameagiza viongozi wote kutoa risit za EFD kwa kila malipo yanapofanyika
 MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akizungumza na Wananchi mapema leo kwenye muendelezo wa ziara yake jijini Dar
  MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi akisikiliza kero mbalimbali za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi
Wanachi wa Mzimu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi
Viewing all 46343 articles
Browse latest View live




Latest Images