Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46401 articles
Browse latest View live

JWTZ YAPANIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA MICHEZO IKIWEMO GOFU NCHINI .

$
0
0

Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akikabidhi Zawadi kwa mshindi wa Jumla wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Amani Saidi Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Venance mabeyo akisalimiana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Mrisho Sarakikya wakati akishiriki Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mshindi wa kundi la Wanawake wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Vicky Elias akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Angel Eaton akiwa katika Harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Mmoja wa Wachezaji wa Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Dkt Edmund Mndolwa akiwa katika harakati za Mchezo huo Jana Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Wasanii wa Ngoma kutoka kundi la Ngoma la Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Band Coy wakitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Miaka 10 ya Klabu ya Gofu ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam(Picha na Luteni Selemani Semunyu).

…………………………………………………………………
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ.

Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania limepania kukuza Mchezo wa Gofu kwa kujenga Miundombinu na Viwanja vya kanda katika maeneo mbalimbali nchini kwa Kuanzia Mkoani Dodoma ambapo Serikali imetangaza kuhamia.

Hayo yalibainishwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo wakati akifunga Mashindano ya Maadhimisho ya Miaka 10 tangu Kuanzishwa kwa Klabu ya Golf ya Lugalo Jana Jijini Dar es Salaam.
“ Tumeshapata eneo la Jeshi Dodoma hivyo Tutatumia uzoefu tulioupata kwa Ujenzi wa Klabu hii ili Kujenga Klabu ya Kisasa ya Gofu Mkoani Dodoma ili watakaokwenda Dodoma kikazi au kwa shughuli nyingine wasikose sehemu ya Kucheza Gofu.” Alisema Jenerali Mabeyo.

Aliongeza kuwa mbali na Ujenzi wa Uwanja wa Golf Dodoma lakini pia kuna Uwezekano wa kujenga Viwanja vya kanda na Lugalo kuwa na mashina katika Mikoa ya Arusha,Morogoro,Mwanza na Simiyu ili kuchangia katika ukuzaji wa Michezo na ukizingatia Serikali imetilia Mkazo suala la Michezo kwa Wananchi.

Jenerali Mabeyo ambaye ni Mlezi wa Klabu hiyo alisema mbali na Ujenzi wa Viwanja hivyo vya Gofu lakini bado wataendeleza Uwanja wa Lugalo pale ambapo watangulizi wake wameishia na kuhakikisha unakuwa wenye sifa za kuchezeka wakati wote kwa kuangalia miundombinu ya Maji.

“ Nilikuwa naongea na mwenyekiti kamati ya mashindano Dk Edmund Mndolwa alinidokeza tatizo la kukauka kwa Uwanja kipindi cha Kiangazi na kutochezeka Vizuri nimelichukua na tutalifanyia kazi tunashukuru Afande waitara kwa Ubunifu na namshukuru Mtangulizi wangu Jenerali Mwamunyange kwa kuilea klabu kwa Mafanikio nami kwa kushirikiana na Wanachama nitaendeleza ili klabu izidi kuimarika”. Alisema Jenerali Mabeyo.

Pia aliwashukuru Waandishio wa habari na wadau Mbali mbali katika kuitangaza na kufanikisha shughuli mbalimbali zinazoandaliwa na Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa na imejidhihirisha kutokana na Umati mkubwa uliojitokeza katika maadhimisho hayo.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Mstaafu Michael Luwongo alisema katika kipindi cha Miaka 10 wamepata mafanikio makubwa hivyo sasa licha ya kufanya uwanja kuwa na hadhi ya kimataifa na mpango maalumu wa ukuzaji vipaji kwa watoton lakini walenga kupata viwanja kwa ajili ya Michezo mingine ikiwemo kuogelea.
Aliongeza kuwa Lugalo itabaki kitovu cha Ukuzaji vipaji kutokana mpango maalum wa watoto ambao idadi yao sasa inafikia zaidi ya 50 ambayo ni kubwa ukilinganisha na Klabu zote nchini.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano hayo Dkt Edmund Mndolwa alisema wanashukuru JWTZ kwa kutoa fursa kwa raia kushiriki katika Klabu hiyo hali iliyoondoa adha kubwa kwa wazalendo.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MBULU

$
0
0
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimiana wanakwaya wa Shule ya Sekondari ya Singiland wilayani Mbulu wakati alipowasili kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu kuhutubia Mkutano wa hadhara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa michezo wa Mbulu mkoani Manyara, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

TANGAZO LA MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA LAPF

NAIBU SPIKA DR. TULIA ACKSON ASHIRIKI IBADA YA SHUKURANI NA WAFANYAKAZI WA BENKI YA CRDB KWENYE KANISA LA KKKT MSASANI

$
0
0
Mchungaji Melgad Metili wa Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani Dayosisi ya Mashariki na Pwani akiwaombea Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkewe Rose Kimei pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na waumini wengine kwenye ibada ya shukurani kwa jinsi mungu aliyvowatendea katika kila jambo maishani mwao, Ibada hiyo imefanyika jana jumapili kwenye kanisa hilo lililopo Msasani jijini Dar es salaam.
 
Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa kushoto na Mama Rose Kimei wakiimba moja wa nyimbo katika ibada hiyo wakati ilipokuwa ikiendelea.
Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei wakishiriki kuimba wimbo katika ibada hiyo.
Naibu Spika wa Bunge Dr. Tulia Ackson na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dr. Charles Kimei , Mkurugenzi wa Masoko Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB,Tully Mwambapa kushoto na Mama Rose Kimei pamoja na waumini wengine wakiwa katika maombi.
Baadhi ya wafanyakazi wa CRDB na waumini wengine wakiwa katika ibada hiyo.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu kushoto pamoja na watendaji wengine wa benki hiyo wakishiriki katika ibada hiyo iliyofanyika jana kwenye kanisa la KKKT Msasani.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu kushoto pamoja na watendaji wengine wa benki hiyo wakiwa katika maombi wakati wa ibada hiyo iliyofanyika jana kwenye kanisa la KKKT Msasani.
Mchungaji Melgard Metili wa Kanisa la KKKT Usharika wa Msasani Dayosisi ya Mashariki akitoa mahubiri yake katika ibada hiyo iliyofanyika kwenye kanisa la KKKT Usharrika wa Msasani jijini Dar es salaam jana.

“OPERESHENI LIPA KODI YA PANGO LA ARDHI”

$
0
0
Mhe. Mabula akikagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi sambamba na kuhakiki kumbukumbu za umiliki wa Ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Ikiwa Operesheni Lipa Kodi ya Pango la Ardhi inaendelea, ambapo Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inaendelea kutoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa sugu wa Kodi ya pango la Ardhi huku ikiendelea na kuhabarisha Umma kuhusu umuhimu wa kuzingatia Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999, katika vifungu Na. 49 na 51 ambavyo vinadhihirisha ruhusa ya mmiliki kufutiwa umiliki wa ardhi kama mmiliki hatazingatia kulipa Kodi ya Pango la Ardhi.

Kwa upande wake; Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendelea ya Makazi, Dkt Angeline Mabula (Mb), amekuwa akifanya ziara ya kukagua mifumo ya ulipaji kodi ya pango la Ardhi sehemu mbalimbali nchini.

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA UINGEREZA,CHINA NA AFRIKA KUSINI

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Wawekezaji kutoka Uingereza, China na Afrika ya Kusini ambao wameonyesha nia ya kuwekeza kwenye Sekta ya Afya na Nishati,wengine waliopo kwenye picha hii ni Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage, na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk.Hamisi Kigwangalla. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Muhimbili Yafanya Upasuaji Mkubwa wa Kwanza watoto Leo

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imefanya upasuaji mkubwa kwa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) kwa watoto ambao haujawahi kufanyika hapa nchini.

Upasuaji huu umefanywa na Madaktari Bingwa wa Muhimbili waliobebea katika upasuaji wa watoto kwa kushirikiana na mtaalam kutoka Hospitali ya King Faisal ya nchini Saudia Arabia.

Kwa mujibu wa Daktari Bingwa wa Upasuaji wa watoto wa Hospitali hiyo, Zaitun Bokhary leo umefanyika upasuaji wa nyama iliyojitokeza sehemu ya haja kubwa kwa mtoto pamoja na upasuaji wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula.

Upasuaji huu mkubwa ambao umefanyika leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili hufanyika nchi zilizoendelea hivyo Tanzania ni mara ya kwanza kufanyika na utaleta mageuzi makubwa nchini.Moja ya faida kubwa ya upasuaji wa aina hii ni mgonjwa kupona haraka na gharama kidogo hutumika wakati wa upasuaji tofauti na upasuaji wa kufungua tumbo.

Upasuaji ambao umeanza leo unahusisha upasuaji wa nyama iliyojitokeza katika sehemu ya haja kubwa kwa watoto, upasuaji wa kushusha kokwa katika korodani, upasuaji wa kushusha utumbo mkubwa na kutengeneza njia ya haja kubwa kwa watoto ambao wamezaliwa bila kuwa na njia ya haja kubwa, upasuaji wa kuondoa mfuko wa ziada kwenye koo kwa watoto na upasuaji kwa watoto wadogo ambao hawana celi mbalimbali na hivyo kushindwa kusukuma choo kwenye utumbo mkubwa.
Kutoka kushoto ni daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Zaitun Bokhary, Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Profesa Zakaria Habib kutoka Falme za Kiarabu na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto wa Muhimbili, Dk Mbaga wakifanya upasuaji LEO wa njia ya matundu madogo ( Laparoscopy Surgery) wa kuondoa kifuko cha ziada katika mfuko wa chakula kwa mtoto mwenye umri wa miaka 10.
Madaktari wakifanya upasuaji wa njia ya matundu madogo kwa mtoto huyo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Dk Zaitun wa Muhimbili akizungumza na waandishi wa habari kuhusu upasuaji huo uliofanyika leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mahakama ya Tanzania kujenga majengo ya mahakama 70 nchini

$
0
0
Na Lydia Churi-Mahakama

Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha miradi ya ukarabati na ujenzi wa majengo 70 ya Mahakama katika kipindi cha miaka miwili ili kusogeza karibu huduma ya utoaji haki kwa wananchi.

Ili kusogeza huduma hiyo kwa wananchi, majengo ya Mahakama kuu katika mikoa tisa yanatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka miwili, Mahakama za Mikoa sita zitajengwa ndani ya miezi 6-12 wakati Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 zinatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 2017.

Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika hivi karibuni, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma alisema Mahakama kwa kushirikiana na Wakala wa Majengo (TBA), Chuo Kikuu cha Ardhi, Baraza la Ujenzi la Taifa, Benki ya Dunia na wadau wengine wanaendeleza na kukamilisha miradi ya ujenzi wa Mahakama Kuu katika mikoa tisa nchini. 

Aliitaja mikoa ambayo majengo ya Mahakama Kuu yatafanyiwa ukarabati na mengine kujengwa ndani ya kipindi cha miezi 24 kuwa ni Mbeya, Kigoma, Mara, Tanga na Dar es salaam. Mikoa mingine ni Arusha, Morogoro, Mwanza na Dodoma.

Alisema nia ya Mahakama ni kuwa na Mahakama Kuu katika kila Mkoa ili kusogeza huduma za Mahakama kwa wananchi.

“Tunapaswa kuwa na Mahakama Kuu 26 kwenye kila ngazi ya Mkoa, kwa sasa tunazo Mahakama Kuu kwenye kanda 14 tu”, alisema Kaimu Jaji Mkuu.

Aidha, mikoa 12 isiyokuwa na Mahakama Kuu ni pamoja na Songwe, Katavi, Njombe, Lindi, Kigoma na Mara. Mikoa mingine ni Singida, Morogoro, Pwani, Simiyu, Geita na Manyara. 

Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa wakati huo huo, Mahakama ya Tanzania inatarajia kukamilisha ujenzi wa Mahakama za Hakimu Mkazi katika mikoa sita ya Manyara, Geita, Simiyu, Njombe, Katavi na Lindi katika kipindi cha kati ya miezi 6 na mwaka mmoja.

Kwa upande wa Mahakama za Wilaya na zile za Mwanzo, Kaimu Jaji Mkuu alisema wanakusudia kujenga Mahakama za Wilaya 19 na za Mwanzo 36 ambazo zitakamilika ifikapo Desemba 2017.

Alisema hatua hii ya ujenzi wa Mahakama hizi si tu kwamba itasogeza karibu huduma za Mahakama kwa wananchi bali pia italeta mabadiliko makubwa ya miundombinu ya mahakama na kuweka historia ya upatikana wa miundombinu kwa wingi na kwa kifundi kifupi. 



“Tunatamani ifike mahali watanzania wakiweke kiswahili kwenye roho zao” Prof. Ole Gabrieli

$
0
0
Immaculate Makilika- MAELEZO

Serikali imesema inatamani kuona watanzania wanakiweka kiswahili kwenye roho zao kwa kufikiri na kuzungumza lugha hiyo katika maeneo na shughuli mbalimbali za kitaifa na kimataifa ili kukienzi pamoja na kuipa heshima inayostahili.

Akizungumza katika kipindi cha Je tutafika? kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Channel ten, Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alisema kuwa “Tunatamani ifike mahali kila mtanzania aone fahari kuongea lugha ya kiswahili, hii itasaidia kuipa hadhi lugha hiyo kitaifa na kimataifa na hatimaye kuifanya lugha ya kiswahili kuwa bidhaa ili iweze kuuzwa”. Alisema Prof. Ole Gabrieli.

Ambapo aliongeza kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Habari imeendelea kufanya jitihada mbalimbali za kuikuza lugha hiyo ikiwemo Baraza kiswahili Tanzania kutoa kamusi mpya yenye maneno zaidi ya milioni moja na nusu, na zaidi ya istilahi 40.

Aidha, Profesa Ole Gabriel, alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuzungumza lugha ya kiswahili katika mikutano mbalimbali ya kimataifa, kwani hatua hiyo inasaidia kuikuza lugha hiyo na kuwavutia watu wengi zaidi kuizungumza kwa vile ni lugha inayounganisha watanzania pamoja na wananchi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

” Lugha ni nyenzo muhimu ya kuhifadhi utamaduni, kwasababu utamaduni ndio namna tunayoishi na tunavyofikiri, hivyo watanzania tunatakiwa kufikiri na kuzungumza lugha ya pamoja ambayo kila mmoja ataelewa”.Alisema Prof. Ole Gabrieli.

Alitoa wito kwa watanzania kuwa na utamaduni wa kuongea lugha ya kiswahili ikiwa ni pamoja kuwafundisha watoto wao kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha.

Katika hatua nyingine Prof. Ole Gabrieli aliviomba vyombo vya habari nchini kuandaa vipindi na vipindi mbalimbali vyenye lengo la kukuza lugha ya kiswahili kwa kuielekeza jamii juu ya matumizi sahihi ya lugha hiyo.

FAO YATOA KIASI CHA SHILINGI MILIONI 280 KATIKA MCHAKATO WA KUPITIA UPYA SERA YA TAIFA YA MISITU YA MWAKA 1998

$
0
0

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero (kulia) wakisaini hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia) wakibadilishana hati ya makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa akionesha kitabu cha Sera ya Taifa ya Misitu ya Mwaka ya 1998 ambayo imepitwa na wakati kutokana na mabadailiko mengi kutokea nchini. Wengine ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akiwa na Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Fred Kafeero (kulia).( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi ( kushoto) akizungumza kabla kutia saini hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa. ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)



Serikali ya Tanzania na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) wameisaini makubaliano ya kupitia upya Sera ya Taifa ya Misitu ya mwaka 1998 ambayo imekuwa ikitumika kwa takribani miaka 19 hadi hivi sasa.

Akizungumza mara baada ya kusaini makubaliano hayo leo jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi amesema mpango huo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 280 ambazo zimetolewa na FAO kwa ajili ya kufanya utafiti wa kuongezea takwimu ambazo zitaboresha Sera ya Misitu ya Taifa ili iweze kufikia hadhi ya kimataifa.

Amesema hatua hiyo imekuja Kutokana na Sera ya Misitu ya Taifa ya mwaka 1998 inayotumika hadi hivi sasa kupitwa na wakati yakiwemo mabadiliko ya Kiuchumi, Kuongezeka kwa idadi ya watu pamoja na Mabadiliko ya tabia ya nchi.

Maj. Gen. Gaudence ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la ufyekaji misitu na hivyo kumechangia kupunguza uoto wa asili kutoka hekta milioni 55.9 kwa mwaka 1990 hadi kufikia hekta milioni 46 kwa sasa lakini Sera ya Misitu ni ile ile.

‘’ Sera ya Taifa ya Misitu ilishafanyiwa mapitio kuanzia mwaka 2009, Lakini kutokana na Sera hii kukaa kwa muda wa takribani Miaka 9 hadi hivi sasa tumegundua kuwa baadhi ya wadau wengi hawakupata nafasi ya kutoa mawazo yao. Hata wale waliotoa mawazo yao mengi yameshapitwa na wakati.’’ Alisema Maj. Gen. Milanzi

Naye Mwakilishi Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) , Fred Kafeero amesema kuwa Mradi huo utasaidia wananchi wengi kushiriki na kutoa mawazo mengi kuhusiana na Sera ya Misitu ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo watumishi kuweza kukusanya taarifa nyingi ili ziwezeshe kuboresha sera kupitia tafiti. 

Aidha,Kafeero amesema kutokana na mabadiliko hayo FAO itasaidia katika kuhuisha sera mpya ambayo itatoa majibu kwa changamoto zinazoikabili nchi hivi sasa na kukidhi mikataba ya kimaifa kama vile mabadiliko ya tabia ya nchi .

MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA YASHIKA KASI MKOANI MOROGORO,WATU 66 WASHIKILIWA

$
0
0

Na John Nditi, Morogoro

JESHI la Polisi mkoani Morogoro limewatia mbaroni watu  66 kwa tuhuma za  makosa ya kupatikiana na dawa za kulevya aina za heroine, mirungi na bangi viroba 39.

Watuhumiwa hao walikamatwa wakati  wa operesheni maalumu dhidi ya mapambano ya dawa za kulevya iliyofanyika kuanzia Februari 19, mwaka huu kutoka wilaya za mkoa wa  Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema  hayo Feb 20, mwaka huu ofisini mwake wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mafanikio ya  operesheni inayoendelea kufanyika kuhusu  mapambano dhidi ya dawa za kulevya  kwenye  wilaya  za mkoa huo.

Matei alisema , watuhumiwa hao wanaendelea kuhojiwa na   watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili .
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akionesha kifurushi kilichohifadhi dawa za kulevya aina ya heroine iliyokamatwa  wakati wa oparesheni ya mapambano  dhidi ya  dawa za kulevya iliyofanyika  kuanzia Februari 18, mwaka huu  sambamba na ukamataji wa viroba 39  vya bangi pamoja  na mirungi  kama alivyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari Februari  20, mwaka huu  kwenye  uwanja wa Jengo la Polisi la mkoa huo.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akionesha kifurushi kilichohifadhi dawa za kulevya aina ya heroine iliyokamatwa  wakati wa oparesheni ya mapambano  dhidi ya  dawa za kulevya iliyofanyika  kuanzia Februari 18, mwaka huu  sambamba na ukamataji wa viroba 39  vya bangi pamoja  na mirungi  kama alivyokuwa akiwaonesha waandishi wa habari Februari  20, mwaka huu  kwenye  uwanja wa Jengo la Polisi la mkoa huo.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, akitoa taarifa ya operesheni ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa waandishi wa habari , Februari 20, mwaka  huu ofisini kwake .
 Gari aina ya Totota Noah yenye namba za usajili T. 799 BUG ikiwa imeshikiliwa na Polisi baada ya kukmatwa ikisafirish  bangi  viroba 21 kutoka katika kijiji cha Lubungo, Kata na Tarafa ya Mikese, wilaya ya Morogoro kwenda Jijini Dar es Salaam.( Picha na John Nditi). 

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akutana na Rais wa Tunisia

$
0
0
Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya ziara nchini Tunisia na kukutana na Rais wa Tunisia Mhe. Beji Caid Essebsi tarehe 17 Februari, 2017. Ziara hiyo ambayo ni muendelezo wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu ya kuwafikia viongozi wa nchi 14 za Afrika za kipaumbele katika kutekeleza mapendekezo ya Ripoti ya Kizazi cha Elimu (The Learning Generation).

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha kwa Rais Essebsi mapemdekezo ya ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  na kuiomba Tunisia kujiunga katika mpango wa nchi za mstari wa mbele (pioneer countries) katika kufanikisha Kizazi cha Elimu ifikapo mwaka 2040. Mazungumzo hayo yalihudhuriwa pia na Waziri wa Elimu wa Tunisia Mhe. Neji Jalloul.

Kwa upande wake, Rais Essebsi wa Tunisia amemuhakikishia Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete uthabiti wa azma ya nchi yake kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu. Ameelezea utayari wa nchi yake kujiunga na mpango huo wa kufanikisha mapinduzi ya sekta ya elimu ndani ya kizazi kimoja ifikapo mwaka 2040.

Mbali na mkutano wake na Rais wa Tunisia, awali, Rais Mstaafu alikutana na kuwa na Mkutano na Waziri wa Elimu wa Tunisia na kutembelea Kituo cha Uendelezaji Teknolojia katika Elimu kilichoko Tunis na baadae kuzungumza na wanahabari kuhusu kazi za Kamisheni na Ripoti yake.

Kwa taarifa zaidi: 

 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete katika mazungumzo na Rais wa Tunisia Mhe. Beji Essebsi
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokelewa na Rais Beji Essebsi katika Ikulu ya Tunisia
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Rais Essebsi wa Tunisia mara baada ya kumkabidhi Ripoti ya Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu

CHAMA CHA WANASHERIA WANAWAKE TAWLA CHAKUTANA NA MADIWANI WA WILAYA TATU ZA JIJI LA DAR ES SALAAM

$
0
0
1
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akizungumza na Waganga Wakuu wa Wilaya, Maafisa Maendeleo wa Jamii, Wanasheria, Madiwani na Maafisa Mipango wa Halmashauri/Wilaya kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar Es Salaam Kinondoni Ilala na Temeke pamoja na Waandishi wa habari waliopata fursa ya kushiriki wakati akifungua semina ya kupata mrejesho wa maazimio kuhusu rasilimali zinazoboresha haki ya afya ya uzazi kwa upande wa mamlaka za Halmashauri ya jiji la Dar Es Salaam; na pia Kupata mrejesho juu ya utekelezwaji wa maazimio yaliyowekwa na kila Halmashauri/Wilaya kufuatia semina shirikishi iliyofanyika mwaka 2016 Mkoani hapa.Semina hiyo imefanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
2
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akizungumza jambo wakati wa semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam anayefuatia kwenye picha ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile pamoja na washiriki wengine wa semina hiyo.6
Nancy Richard Mkuu wa Idara ya Huduma za Msaada wa Kisheria TAWLA akifafanua jambo wakati wa semina hiyo kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile.
3
Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki za wanawake na wanaume Mary Lusimbi ambaye ndiye alikuwa mwezeshaji wa semina hiyo akitoa mada kwa washiriki wakati semina hiyo ilipokuwa ikiendelea.
7
Bi. Halili Katani Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kulia ni Balima Omari Afisa Maendeleo ya Jamii Manipaa ya Kinondoni na katikati ni Tausi Kheri Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni
8
Baadhi ya washiriki waki wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam leo.
9
Tausi Kheri Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni akichangia hoja wakati wa semina hiyo kutoka kulia ni Kheri Missinga Diwani Kata ya Bunju, Balima Omari Afisa Maendeleo ya Jamii Manipaa ya Kinondoni na Kushoto ni Bi. Halili Katani Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Kinondoni
1011
Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA, Tike Mwambipile akifafanua mambo mbalimbali kwa waandishi wa habari mara baada ya kufungua semina hiyo kwenye hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMANNE FEBRUARY 21

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE YAWAAGA WAFANYAKAZI WAKE WANAOHAMIA HOSPITALI YA BENJAMINI MKAPA NA CHUO KIKUU CHA TIBA NA SAYANSI SHIRIKISHI (MUHAS) KAMPASI YA MLOGANZILA

$
0
0
Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Agnes Kuhenga akiongea na baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanne wa Taasisi hiyo ambapo watatu kati yao wanahamia Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na mmoja anahamia Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiongea na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi wanne wa Taasisi hiyo ambapo watatu kati yao wanahamia Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma na mmoja anahamia Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.
Viongozi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi hiyo wanaohamia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo Dodoma na Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaammara baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaaga wafanyakazi hao iliyofanyika jana.
Baadhi ya Maafisa Wauguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa katika picha ya pamoja na wenzao wawili wanaohamia katika Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Dodoma na Hospitali ya kufundishia ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila kiliyopo Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha shukurani ya kufanya kazi katika Taasisi hiyo Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Robert Mvungi ambaye anahamia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti cha shukurani ya kufanya kazi katika Taasisi hiyo Afisa Muuguzi Mkuu Salome Kassanga ambaye anahamia katika Hospitali ya Benjamin Mkapa iliyopo mkoani Dodoma.

WANACHAMA WA TANZANIA GIRL GUIDS WAFANYA USAFI MAGOMENI KOTA, COCO BEACH DAR

$
0
0
 Walimu na wanafunzi wa shule za Msimbazi na Mongo la ndege ambao ni wanachama wa chama cha Tanzania Girl Guids (TGGA), wakijitolea kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya maadhimisho ya wiki ya utoaji huduma kwa wahitaji.

Wanachama hao walioongozwa na Mwenyeikiti wa chama hicho, Profesa Martha Qorro pamoja na Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba walifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota na Ufukwe wa Coco.

Walimu na wanafunzi kutoka shule za Mugabe, Urafiki, Mongo la Ndege na Msimbazi ambao ni wanachama wa TGGA walishiriki ipasavyo kwenye usafi huo.

Pia baadhi ya wanachama wa TGGA walikwenda kutoa msaada wa vitu mbalimbali katika Kituo cha Taifa cha Yatima cha Kurasini, Dar es Salaam.

 PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Wanafunzi wa Shule za Mugabe na Urafiki na walimu wao wakifanya usafi katika Ufukwe wa Coco Oysterbay, Dar es Salaam wakati wa kuadhimisha waiki hiyo ya utoaji huduma kwa wahitaji
 Wanachama wa TGGA wakifanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota
 Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro (kushoto) na Juma Rashid wakiungana na wanachama wengine wa chama hicho kufanya usafi katika Ufukwe wa Coco, Oysterbay Dar es Salaam 
 Mwenyekiti wa TGGA, Profesa Martha Qorro (kushoto) na Juma Rashid wakiungana na wanachama wengine wa chama hicho kufanya usafi katika Ufukwe wa Coco, Oysterbay Dar es Salaam 
 Usafi ukiendelea katika viwanja vya Magomeni Kota. Katikati ni Raia wa Madagascar Andriambolamanana Vahatrimama ambaye yupo TGGA kujifunza utamaduni, maadili, mila za Tanzania pamoja na masuala ya uongozi



 Mwanachama wa Girl Guids kutoka Rwanda Michelline Uwiringiyimana (katikati), ambaye yupo nchi kwa ajili ya kujifunza utamaduni na maadi pamoja masuala ya uongozi, akishiriki kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota,
  Mwanachama wa Girl Guids kutoka Rwanda Michelline Uwiringiyimana (kulia), ambaye yupo nchi kwa ajili ya kujifunza utamaduni na maadi pamoja masuala ya uongozi, akishiriki kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota,
 Rehema (kulia) wa TGGA akiwa na wanafunzi wa shule ya sekondari Msimbazi wakifanya usafi Magomeni Kota
 Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba akishiriki kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam
  Katibu wa Taifa wa TGGA, Grace Shaba (kulia) akishiriki kufanya usafi katika viwanja vya Magomeni Kota, Dar es Salaam
 Wanafunzi wa shule za Mugabe na Urafiki wakishiriki kufanya usafi katika eneo la Coco
 Wanafunzi wa shule za Mugabe na Urafiki wakishiriki kufanya usafi katika eneo la Coco
 Wanafunzi wa shule za Mugabe na Urafiki wakishiriki kufanya usafi katika eneo la Coco


 Mwalimu wa shule ya Mugabe, Notceris Seus ambaye ni mwanachama wa TGGA akishiriki kufanya usafi katika ufukwe wa Coco,
 Mwalimu wa Shule ya Msingi Urafiki, Scolastica Mpunga akiungana na wanafunzi kufanya usafi katika ufukwe wa Coco

NAIBU WAZIRI NISHATI NA MADINI ATEMBELEA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA NYAKATO JIJINI MWANZA

$
0
0
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akielezwa jambo na Meneja wa Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza, Mhandisi Mathew Mwangomba (kushoto). Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi John Mageni. 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akikagua Kituo cha Kufua umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) cha Megawati 60 cha Nyakato Jijini Mwanza. Kushoto ni  Meneja wa kituo hicho, Mhandisi Mathew Mwangomba.

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akielekeza jambo wakati wa ziara ya kukagua mitambo ya kuzalisha umeme ya Nyakato Jijini Mwanza. Kulia ni Meneja wa Mitambo, Mhandisi Mathew Mwangomba.
 Moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) kwenye Kituo cha kufua umeme cha Nyakato jijini Mwanza. Kituo hicho kina jumla ya mitambo 10 yenye uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati 60 huku kila mtambo ukiwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha Megawati sita. 
 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akikagua moja ya mtambo wa kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito kwenye kituo cha Nyakato jijini Mwanza 
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja wa Mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta mazito (HFO) ya Nyakato Jijini Mwanza, Mhandisi Mathew Mwangomba alipofanya ziara ya kukagua mitambo hiyo ili kujionea utendaji wake.

MABADILIKO MADOGO NA NYONGEZA YA WAJUMBE KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE

Waziri Nape akutana na Ujumbe wa Kampuni ya LandesSport Bund Niedersachsen e.v ya nchini Ujerumani.

$
0
0
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na Makamu wa Rais  wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani  Bw.Reinhard Rawe   kuhusu jinsi wanavyoweza kushirikiana katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo hapa nchini walipokutana jana Jijini Dar es Salaam.
 Makamu   wa Rais  wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani  Bw.Reinhard Rawe  akimueleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kushoto) namna ambavyo kampuni yake inaweza kushririkiana na Wizara katika Sekta ya Maendeleo ya Michezo hapa nchini walipokutana jana Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia zawadi aliyopewa na Ujumbe wa  Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo  hapa nchini yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe wa Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani Bibi Angie (wa kwanza kulia) akimueleza jambo Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye wakati wa mazungumzo baina yao kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo hapa nchini yaliyofanyika jana Jijjini Dar es Salam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja  na ujumbe kutoka  Kampuni ya Landes SportBund Niedersachsen e.v ya nchini  Ujerumani baada ya kumaliza mazungumzo kuhusu maendeleo ya Sekta ya Michezo  hapa nchini yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.

MONDULI YAUNGA MKONO KUPIGA VITA MADAWA YA KULEVYA

$
0
0

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo akizungumza na watumishi katika wilaya ya Monduli ,alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo,aliyeko pembeni yake ni mkuu wa wilaya Monduli Idd Kimanta.picha na Vero Ignatus Blog.
Mkuu wa mkoa akipokea kadi ya CHF wilaya ya Monduli kutoka kwa mkuu wa wilaya hiyo Idd Kimanta,ili kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo.Picha na Vero Ignatus Blog
Baadhi ya watumishi katika halmashauri ya wilaya ya momduli wakifuatilia yaliyokuwa yanaendelea kwa makini.Picha na Vero Ignatus Blog
Mkutano unaendele wadau pamoja na watumishi wa wa halmashauri hiyo wakifuatilia yale yanayoendelea.Picha na Vero Ignatus Blog




Na.Vero Ignatus, Monduli.


Halmashauri ya wilaya ya Monduli imeendelea kuungana na vyombo vya ulinzi na usalama na wananchi katika kupiga vita dhidi ya madawa ya kulevya .

Hayo yamebainika katika taarifa iliyosomwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo Steven Ulaya kwa mkuu wa mkoa Mrisho Mashaka Gambo, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo katika halmashauri hiyo ambapo taarifa hiyo imesema kuwa Mirungi imekuwa ikiingizwa kutoka nchi ya jirani ya Kenya kupitia mpaka wa Namanga.

Ripoti hiyo imeendelea kusema kuwa jeshi la polisi lilefanya operesheni maalum na kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya madawa hayo,ambapo takwimu za mwaka 2016 hadi januari 2017 kesi za bhangi 11 dhidi ya 8 mwaka 2015 na mirungi ni kesi 12 kwa mwaka 2016 dhidi ya 10

Aidha ripoti hiyo imeonyesha kuwa halmashauri inaendelea na zoezo la uhakiki wa watumishi hewa limewabaini 24 ambapo kiasi cha shilingi 54,798,300 kilihojiwa kwa watumishi hao,kiasi cha shilingi 32,988,963.19 kilirejeshwa hazina baada ya kuzuia mishahara ilitolewa na baadhi ya watumishi walirejesha fedha hizo walionufaika nazo ambapo makato ya mishahara kiasi cha shilingi 21,809,336.81 yaliyokuwa yanalipwa moja kwa moja na wizara ya fedha ikiwa ni kodi ya mishahara ya watumishi husika na makato ya mifuko ya pensheni tayari mfuko umeandikiwa barua za kurejesha fedha hizo .

Sambamba na hayo halmashauri hiyo ina jumla ya watumishi 1,867 sawa na asilimia 71.3 ya mahitaji halisi ya watumishi 2,615,ikiwana upungufu wa watumishi 723 katika mchanganuo ufuatao :Idara ya elimu ya msingi walimu 191,elimu ya sekondari (walimu wa sayansi 54)Mmaendeleoa jamii watumishi 18,Utawala (watendaji wa vijiji na kata 20)Kilimo (watumishi 25)Mifungo (watumishi(21)Afya watumishi 391.

Wilaya ina jumla ya watumishi 295 wa sekta ya Afya ambapo ni sawa na asilimia 43 tu ya mahitaji ya watumishi wote 686,upungufu mkubwa upo katika kada ya Tabibu,wauguzi,wateknolojia ,,mahabara,Dawa na Daktari wasaidizi.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mapato ya halmashauri hiyo kwa mwaka 2016/2017 imekasimia kukusanya jumla ya shilingi 2,457,310,003 kutoka katika mapato ya ndani hadi kufikia januari 2017,halmashauri iliuwa imekusanya jumla ya shilingi 1,120,7147,542.32 sawa na 46% makisio ya mwaka mzima.

Ikumbukwe kuwa Wilaya ya Monduli miezi ya hivi karibuni ilipatwa na matukio 4 kuungua moto kwa badhi ya mabweni na shule za sekondari 1.Lowassa Sekondari tarehe 27/01/2016 na 31/7/2016,Nanja Sekondari tarehe 2/8/2016 na Ole Sokoine Sekondari tarehe 11/8/2016 ambapo matukio haya ya moto yalileta athari kubwa kwa jamii ikiwemo baadhi ya wanafunzi kurejeshwa majumbani kwa muda kwa mahitaji ya shule .

Viewing all 46401 articles
Browse latest View live




Latest Images