Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1145 | 1146 | (Page 1147) | 1148 | 1149 | .... | 1897 | newer

  0 0

    Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa  kiwanda hicho  kuandika barua ya kumuaomba radhi  Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho.  Kushoto ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
   Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha mfuko wa kubebea mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Manyara wenye maandishi yanayoonesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa nchini Kenya. Jambo hilo lilimkera sana Waziri Mkuu na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kuandika barua ya kumuaomba radhi Rais  John Pombe Magufuli kwa kitendo hicho. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  *Ataka waandike barua ya kuomba radhi kwa Rais Magufuli
  *Aagiza Waziri wa Biashara aje na timu yake

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.

  Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.

  “Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.

  “Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?”

  Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

  Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.

  Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

  “Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.

  “Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”

  “Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza.

  Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.

  Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.


  0 0

  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo katika akiingia kwenye kituo cha Afya Cha Ubwari leo wakati alipokwenda kuangalia zoezi la upasuaji wa macho kwa wakazi wa wilaya hiyo wanaokabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo ya mtoto wa Jicho iliyoendeshwa na Taasisi ya Medewell Charitable Health Centre kulia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo,Mathew Mganga na kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo,Luiza Mlelwa. 
  Baadhi ya wazee waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani 
  Baadhi ya wananchi waliofanyiwa upasuaji wakisubiri zoezi la kupatiwa dawa na miwani 
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akizungumza wakati wa zoezi hilo la upasuaji 
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa zoezi la upasuaji huo.
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa tatu kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee waliojitokeza kupatiwa huduma za upasuaji wa macho waliokuwa na matatizo ya mtoto wa Jicho
  MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kulia akimkabidhi msaada wa vyakula mbalimbali mwakilishi wa wazee waliofanyiwa upasuaji wa macho ili viweze kuwasaidia baada ya kumalizika upasuaji huo watakapokwenda majumbani mwao wanaoshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa ,Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo,Mathew Mganga wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza Desderia Haule
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Luiza Mlelwa akipongezwa na mwakilishi wa wazee hao mara baada ya Mkuu wa wilaya hiyo,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo wa pili kulia kuwakabidhi vyakula vitakavyowasaidia watakapotoka kwenye matibabu hayo na kurejea makwao Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akikagua jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kiombamvua lililojengwa na Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff kutekeleza ahadi za kusaidia huduma na Miradi ya Kijamii.Wa kwanza kulia ni Mshauri muelekezi wa Hoteli hiyo ya Sea Cliff ambae pia ni msimamizi wa Ujenzi wa jengo hilo la Skuli Nd. Yassir De Costa.
  Balozi Seif mbae pia ni Mwakilisihi wa Jimbo la Mahonda akikagua Bara bara ya Kinduni iliyopitia Kichungwani na kuelekea Kitope iliyojengwa na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar katika kiwango cha kifusi.
  Balozi Seif akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Kinduni na Kichungwani mara baada ya kuikagua bara bara iliyomo ndani ya Kijiji chao.Kushoto ya Balozi Seif ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahme Salum na Mbunge wa Viti Maalum Mh.Angelina Adam Malembeka.
  Mzee Juma Abdulrahman wa Kijiji cha Kichungwani anayesumbuliwa na maradhi ya macho na Miguu akitoa shukrani kwa niaba ya wanakijiji wenzake mbele ya Balozi Seif kwa hatuanjema iliyochukuliwa na Serikali kuijenga bara bara yao.Picha na – OMPR – ZNZ.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Ujenzi wa Bara bara ya Kinduni, Kichungwani na hatimae kuelekea Kitope unaofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utasaidia kuharakisha maendeleo ya Wananchi hasa wakulima wa Vijiji hivyo.

  Alisema Ujenzi wa Bara bara hiyo ambao umo ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM unatekelezwa kufuatia ahadi iliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mstaafu wa Awamu ya Sita Dr. Amani Karume.

  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na baadhi ya Wananchi wa Vijiji vya Kinduni na Kichungwani baada ya kuikagua Bara bara hiyo iliyojengwa na Wahandisi wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar katika kiwango cha kifusi kuanzia Kinduni hadi Kichungwani.

  Alisema Bara bara hiyo itakapokamilika rasmi itarahisisha mawasiliano ya usafiri kwa Wananchi wa maeneo hayo ambao wengi wao wanajishughulisha na kazi za Kilimo mchanganyiko katika kujipatia riziki zao za kila siku.

  Balozi Seif aliwahakikishia Wananchi hao kwamba lengo la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika hatua ya baadae ya Bara bara hiyo ni kuikamilisha katika kiwango cha lami ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.

  Mapema Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Mh. Mohamed Ahmed Salum alisema Bara bara ya Kinduni iliyopitia Kichungwani hadi Kitope ni miongoni mwa Bara bara za ndani lakini kwa agizo la Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein itajengwa katika kiwango cha Lami.

  Mh. Mohamed alisema Ahadi zote za Chama cha Mapinduzi zilizotolewa kupitia Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2015 – 2020 zitaendelea kutekelezwa na Wizara yake kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano.

  Alisema ahadi zozote zinazotolewa na Viongozi Wakuu popope pale ni agizo maalum linalostahiki Taasisi au watendaji wahusika kuzitekeleza kulingana na mazingira yaliyowazunguuka.

  Naye Mzee Juma Abdulrahman akikaguliwa na Mh. Balozi Seif kutokana na hali yake ya afya Kijijini hapo kwa niaba ya wananchi wenzake aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua iliyofikia ya ujenzi wa Bra bara hiyo.

  Mzee Juma alisema Bara bara hiyo iliyokuwa kilio cha miaka mingi kilicholeta changamoto na matatizo kwa Wananchi hao itakuwa mkombozi mkubwa hasa kwa wakulima pamoja na kizazi kijacho.

  Alisema kero la Bara bara hiyo ilipelekea wananchi Vijiji hivyo wakati wa Awamu zilizopita walilazimika kukata miti ilimradi kupunguza usumbufu waliokuwa wakiupata hasa kwa akina Mama waja wazito wanapokwenda kujifungua.

  Mapema asubuhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitembelea Jengo jipya la Skuli ya Msingi ya Kiombamvua lililomaliza ujenzi wake.

  Jengo hilo limejengwa na Uongozi wa Hoteli ya Kimataifa ya Sea Cliff ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake ilizotowa wakati wa Vikao vyake mbele ya Kamati ya Bandari ya Kiombamvua kwamba itasaidia huduma na miradi ya maendeleo ya Vijiji vinavyoizunguuka Hoteli hiyo.


  Othman Khamis Ame

  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  0 0


  Familia ya Mzee Meinuf Wapalila na Victoria Bernard Ngowi wanasikitika kutangaza kifo cha mtoto wao Innocent Wapalila kilichotokea Leeds, Uingereza tarehe 17/02/2017.

  Msiba na utaratibu wa kusafirisha mwili na mazishi unafanyika Mbezi Beach jijini Dar es salaam mtaa wa Almasi nyumba namba 7.

  Kwa uingereza, msiba upo nyumbani kwa marehemu Innocent, 18 Bayswater Mount, LS8 5LP, Leeds.

  Gharama za kusafirisha mwili wa mpendwa wetu ni kubwa, ukiwa kama ndugu na rafiki, tunaomba mchango wako wa hali na mali utumwe kwa dada wa marehemu Bi Mariaconsolata Wapalila kwa namba ya M-Pesa 0754 270 433 au Airtel Money 0787 376 278 au akaunti ya benki namba 10300101003 (BANK OF AFRICA).

  Asante sana na mungu awabariki,
  ‘Bwana ametoa na bwana ametwaa jina la bwana lihimidiwe’

  0 0


  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akisalimiana na Mwenyeji wake,Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana.
  Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa umakini sherehe hizo. Watoto nao hawakuwa nyuma katika shughuli hiyo. Mawaidha yakiendelea kwenye sherehe hiyo ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamed S.A.W
  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,akitoa mawaidha katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W katika Mtaa wa Ada Estate wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. (PICHA ZOTE NA ELISA SHUNDA)


  Imamu Mkuu wa Msikiti wa Kinondoni Mkwajuni,Almasi Saidi,Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita (katikati) na Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro wakifuatilia kwa makini sherehe hizo.


   
  Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro,akizungumza katika maulid hiyo ya sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W.Kushoto ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita.
  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.  Wananchiwaliohudhuria katika sherehe hizo za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mtume Mohamad S.A.W


  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro.


  Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita,akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Katikati ni Diwani wa Kata ya Kinondoni,Mustapha Muro na Muandaaji wa kumbukizi hiyo,Daluwesh Dume.


  Kikundi cha Al Farouq kikipiga dufu wakati wa sherehe ya Maulid ya Mtume Mohamed S.A.W iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

  MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwia amewaomba Mashehe na Wazee wa jiji kumuunga mkono katka shughuli anazofanya ili kuweza kutatua changamoto zilizopo katika jiji hili.

  Meya Isaya ametoa kauli hiyo jiji hapa leo wakati wa maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume wao Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwama jiji la Dar es Salaam bila dua za waze, mashehe na viongozi wote wadini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto zilizopo.

  “ Najua changamoto zilizopo kenye jiji hili ni nyingi wazee wangu naomba mnisaidie sana, peke yangu siwezi, dua zenu na ushauri wenu ndio unaweza kunisaidia mimi kufanya mambo mazuri” na wananchi wakaishi kwenye mazingira wanayopenda” amesema Meya Isaya.

  Leo hi mimi nikiwa na kiburi kweu kwa ajili ya madaraka haya ambayo nyie ndio mlionipa, sitaweza kutatua changamoto hata moja,zipo changamoto za kimiundombinu ya elimu, na nyingine, ambazo zote zinahitaji kupatiwa ufumbuzi, nawaombeni saa waze wangu mnipe baraka zenu” aliongeza.

  Akizungumzia suala la maadili Meya Isaya amesema wazazi hawana budi kuwasaidia walimu, serikali na viongozi kwa ajili ya malezi bora hususani wakiwa shuleni.

  Amesema ni jambo la ajabu na mtihani mkubwa kwa walimu ikiwa mzazi atakuwa mstari wa mbele kumnunulia mwanae simu hali yakuwa yupo masomoni jambo ambalo linafanya ashindwe kuzingatia masomo na badala yake kushinda kwenye mitanda ya kijami.

  “ Leo hi mzazi unapomnunulia mwanao simu wakat unajua kabisa anasoma, huu simtihani jamani, leo hii mzazi unaposhindwa kufuatilia maendeleo ya mtoto wako shuleni huu simtihani jamani, nawaombeni sana tusaidiane kulea watoto wetu” ameongeza Meya Isaya.

  Aidha Meya Isaya amewataka vijana kuacha tabia a kukaa vijiweni badala yake wajikite kwenye kufanya kaz, huku akiwaaka wazazi kutokufumbia maco vijana wao aba hatawai kujishuguisha.

  Amesema vijana waliowengi hawataki kujishugulisha na badala yake husubiri kila abacho wazazi wa hutafuta jamo abalo humjengea kijana mazingira ya watto kuanza kugawaa mali kaba ya wazazi hawaja toweka duniai.

  “ Wazazi msiwavumilie vijana wenu ambao wanasubiri nyie muende mkatafute wao waje wale, leo hii nyumbani unakuta baba, au Mama anapishana na kijana wake ambaye angekuwa anajitegemea mwenyewe, lakini kuendelea kuishi nao nyumbani mnataka kuwaongezea umasikini” amesema Meya Isaya.

  Matokeo yake, unakuta kijana anasema Baba unakufa lini, am wanaanza kugawana mali ambazo mmetafuta nyinyi, kabla hata bado hamjatoweka duniani, jambo hili jamani sio mtihani ndugu zangu?, lazima tuwalee watoo wetu kwenye misingi ya kuwaeleza kwama dawa ya kupambana na umasikini kufanya kazi” amesisitiza.

  Hata hivyo Meya Isaya amewaomba wananchi wa jiji la Dar es Salaam kutunza mazingira ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

  0 0

  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye lebo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini. 

  Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, Februari 22, 2017 apate nakala ya barua hiyo.

  Ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Februari 19, 2017) baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo wilaya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu amerejea Babati leo akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa. 

  “Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania,” amesema.

  “Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? Kwani malighafi iko Kenya? Haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?” 

  Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya, na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

  Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja. Pia amesema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage aje hapa na wanasheria wake na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waje kuangalia hatua gani zinapaswa kuchukuliwa. “Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” amesisitiza.

  “Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?”

  “Nataka wakati namaliza ziara nipate taarifa ya hili jambo pamoja na nakala ya barua ambayo imetumwa kwa Mheshimiwa Rais,” amesisitiza. 

  Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Bw. Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi. Waziri Mkuu kesho anaendelea na ziara yake wilayani Mbulu ambako atatembelea hospitali ya Haydom, kuzungumza na watumishi wa wilaya hiyo na kuzindua shule ya sekondari Singland.

  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,

  JUMAPILI, FEBRUARI 19, 2017.

   Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akikagua mgodi wa kiwanda cha mbolea cha  Minjingu wakati alipotembelea kiwanda hicho mkoani Manyara, Februari 19, 2017.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara, Februari 19, 2017
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kabala ya kutembelea kiwanda cha mbolea cha Minjingu mkoani Manyara kuanza awamu ya pili ya ziara yake mkoani humo Februari 19, 2017. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Uvuvi, Dkt, Charles Tizeba na kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa ManyaraDkt. Joel Bendera. Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0  0 0

   Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi  (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya Kampeni ya akaunti ya  Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu.  Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo.

   Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Filbert Mponzi  (katikati), akizungumza wakati wa droo kubwa ya Kampeni ya akaunti ya  Malengo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam jana. Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka  2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu.  Kushoto ni Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo. 
  Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akizungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa kampeni ya akaunti ya Malengo katika droo iliyofanyika  jijini Dar es Salaam jana.   Mkazi wa Dar es Salaam Aldo Aidan Nsuha na mkazi  wa Mtwara, Lawrence Cletus Njozi walijishindia kila mmoja Toyota Hilux double cabin mpya ya mwaka 2016 katika kampeni hiyo iliyochukua muda wa miezi mitatu. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi,  Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza Dorothea Mabonye na aliyesimama ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Bakari Maggid.

  0 0

  Mgeni rasmi wa kongamano la kuchangia damu lililoandaliwa na Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga akizungumza umuhimu wa kila Mtanzania kujitolea damu ili kuinusuru jamii yake. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.

  MBUNGE wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, mwishoni mwa wiki aliongozana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, katika tukio la uchangiaji wa damu lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Yemen Professional Foundation (TYPF), lililofanyika katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo, watu mbalimbali walishiriki katika uchangiaji damu kama sehemu ya kutatua changamoto ya upungufu wa damu kwa wenye uhitaji, wakiwamo akina mama wajawazito, ajali za barabarani na majanga mengine.
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, H.E Jasem Al Najem akitolewa damu katika tukio la kuchangia damu lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa City Garden, jijini Dar es Salaam.

  Akizungumza katika uchangiaji huo, Mbunge Ulega alisema kwamba jukumu la kuchangia damu linamuhusu kila Mtanzania, huku akiwataka watu kujenga mazoea ya kujitolea damu ili kuondoa upungufu wa damu.

  Alisema kwamba mahitaji ya damu kwa nchi yetu ni makubwa, hivyo amefarijika kwa kupata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi sambamba na kuongoza tukio hilo la uchangiaji wa damu, akiamini amejitolea jambo la msingi na la lazima.
  Mbunge wa Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega, akizungumza na Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem wakati wanatoa damu kwenye tukio lililoandaliwa na TYPF mwishoni mwa wiki.
  Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem wakati anapima uzito dakika chache kabla ya kutoa damu katika tukio lililofanyika mwishoni mwiki.

  “Nimefarijika kwa mwaliko wenu na jinsi nilivyoshiriki juu ya utoaji wa damu nikiamini kwamba naweza kusaidia wenye uhitaji wanapokuwa Hospitalini ambapo juu ya damu inayohitajiwa kwa kiasi kikubwa ili kuwanusuru wagonjwa wetu,” Alisema Ulega na kuwataka TYPF kuelekea jimboni kwake Mkuranga kwa ajili ya kuandaa matukio ya aina hiyo ili waendeleze juhudi zao za kuchangia damu.

  Naye Balozi Najem alisema kuchangia damu ni sehemu ya malengo yake binafsi pamoja na ofisi yake, hivyo yupo tayari kusaidia kwa namna moja ama nyingine ili kuwasaidia watu wote wenye uhitaji wa damu nchini Tanzania.

  “Nimejiwekea utaratibu wa kujitolea katika jamii yakiwamo haya mambo ya damu, hivyo pamoja na kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo pamoja na mliohudhuria kuja kutoa damu, naomba niwaambie bado nipo tayari kujitolea wakati wowote itakapohitajika,” Alisema Balozi Najeem.

  Awali Mtendaji Mkuu msaidizi wa TYPF, Swalehe Jabri, aliwashukuru waliojumulika nao kutoa damu, akisema wamefanya jambo kubwa linalohitaji kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo, akiamini utaratibu huo umelenga kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwenye hospitali nchini.

  0 0  0 0

   Katibu wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Zulfa Mohd Masanja akisoma risala wakati wa sherehe za ufunguzi wa Baraza hilo  zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki, Wilaya ya Magharibi ‘B’. 
   Watoto wa Baraza la watoto Shehia ya Kiembesamaki wakionyesha igizo lenye maudhui ya udhalilishaji watoto wakati wa sherehe za kulizindua baraza hilo.
   Mgeni rasmi katika uzinduzi wa Baraza hilo, Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae pia ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akifuatilia maonyesho ya watoto wa Baraza hilo (kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya watoto Zanzibar  Mundhir Hamdan Said. 
   Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Shehia ya Kiembesamaki Bimkubwa Haji Hassan akimkaribisha mgeni rasmi kuzindua Baraza la watoto la shehia hiyo.
   Mwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki ambae ni Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akizindua Baraza la Watoto wa Shehia ya Kiembesamaki katika sherehe zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki. 
  Baadhi ya watoto wa Shehia ya Kiembesamaki wakimsikiliza Mwakilishi wao Mahmoud Thabit Kombo  wakati wa uzinduzi wa Baraza lao kwenye sherehe zilizofanyika Tawi la CCM Kiembesamaki Wilaya Magharibi ‘B’.
  Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

   Mwenyekiti wa Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji wa Leseni Zanzibar Vuai Mussa Vuai akimkaribisha Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali kufungua mafunzo ya siku moja ya Wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyofanyika Ofisi ya Baraza Malindi, Mjini Zanzibar. 
   Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko Balozi Amina Salum Ali akifungua mafunzo ya siku moja ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi yaliyoandaliwa na Baraza la Kusimamia Mfumo wa Utoaji Leseni katika Ofisi yao iliyopo Malindi Mjini Zanzibar.
   Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi wakimsikiliza Waziri wa Fedha Balozi Amina Salum alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyofanyika Ofisi ya Baraza hilo Malindi.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi Yussuf Hassan Iddi ambae ni muwakilishi wa Jimbo la Fuoni akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi baada ya kufungua mafunzo ya siku moja ya Kamati hiyo.Picha na Makame Mshenga/Maelezo Zanzibar.

  0 0

  MAMLAKA ya Elimu Tanzania (TEA) imesaini mkataba wa makubaliano ya utekelezaji wa miradi mbalimbali na Kampuni ya SunShine Group kutoka China kwa miaka mitano kuanzia sasa.

  Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kusaini mkataba huo wa makubaliano, Kaimu Mkurugenzi wa TEA, Graceana Shirima alisema makubaliano hayo yataifanya TEA kuwa mratibu wa miradi ya kuboresha elimu hapa nchini huku Sunshine ikifadhili na kutekeleza miradi hiyo.

  Kwa mujibu wa Shirima miradi hiyo itatekelezwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mara na Mtwara ambapo miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule na vifaa itatekelezwa na kampuni hiyo huku akibainisha kwamba mikoa hiyo ndiyo yenye miradi mikubwa ya kampuni ya Sunshine.

  “Miradi ya kwanza kutekelezwa kupitia makubaliano haya ni ujenzi wa maabara mbili za sayansi katika shule za sekondari Matundasi iliyopo Jijini Mbeya na miundombinu ya maji kwenye sekondari ya Bunda mkoani Mara ambapo Zaidi ya sh. Milioni 210 zitatumika,” alisema Shirima.

  Akiishukuru TEA, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sunshine Goup, Tony Sun alisema kampuni yake inaona fahari kusaidia sekta ya elimu Tanzania huku akiahidi kuendelea kuwekeza katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya taifa.

  Alisema kampuni yake imeingia Tanzania mwaka 2012 na tayari imetumia zaidi ya Dola 500,000 za Marekani katika elimu kwa miaka mitano ya uwepo wao hapa Tanzania.

  “Tumedhamiria kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuhakikisha mazingira ya upatikanaji wa elimu yanakuwa rafiki na yenye kuvutia. Tunaamini TEA watatusaidia kuzifikia shule zenye uhitaji zaidi ili watoto wetu wapate elimu bora kwa ajili ya kujenga taifa imara,” alisema Sun.
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima akifafanua jambo wakati  wa hafla ya kutiliana saini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
   Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
   Mkutano ukiendelea.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mipango, Dk. Erasmus Kipesha akisaini mkataba wa makubaliano hayo.
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, wa makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
   Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. 
  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Graceana Shirima (kushoto), akibadilishana mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Sunshine Group Ltd, Tony Sun, ya makubaliano ya miaka mitano ya kushirikiana katika kuratibu na kufadhili miradi ya elimu nchini. Kushoto anayeshuhudia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mipanga, Dk. Erasmus Kipesha na Mwakili Mkazi wa Sunshin Group, Harison May.
  Picha ya pamoja.

  0 0

  Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

  Serikali imewataka bodi ya ligi kufanya maamuzi sahihi katika kuchagua  waamuzi wenye uwezo mkubwa wa kutafsiri sheria 17 za soka kwenye mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi ijayo kwenye uwanja wa Taifa ili kuzuia athari ambazo zinaweza kujitokeza ikiwemo uharibifu wa mali za uwanja.

  Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa michezo kutoka Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Yusuph Singo leo Jijini Dar es salaam ikiwa ni katika maandalizi ya kuelekea mechi ya watani wa jadi na kuwaasa viongozi wa bodi ya ligi kufanya maamuzi sahihi ili kuepusha vurugu zitakazoweza kujitokeza.

  Singo alisema kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika Oktoba mosi mwaka jana na kushuhudiwa vurugu kubwa zilizopelekea viti 1781 kuvunjwa, zilitokana na maamuzi mabovu ya waamuzi wa mchezo huo.

  “Tunaitaka bodi ya ligi kupanga waamuzi wazuri kwenye mchezo huu kwakuwa unavuta hisia za watu wengi na pia tunawaomba mashabiki kuwahi mapema na kutojihusisha na vurugu zozote kwani ulinzi utakuwa wa kutosha” alisema Singo.

  Kwa upande mkuu wa kitengo cha ulinzi na usalama wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Inspekta Hashim Abdallah alisema ulinzi utaimarishwa vya kutosha na wale wote watakaovunja sheria watachukuliwa hatua stahiki ukizingatia uwanja wa huo umefungwa kamera maalum kwa ajili ya ulinzi.

  “Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kushangilia timu zao kwa amani lakini watakao jihusisha na vurugu tutawashughulikia ipasavyo” alisema Inspekta Hashim.

  Wakati huo huo mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amevitaja viingilio hivyo kuwa viti vya bluu na kijani itakuwa shilingi 7,000 viti vya ‘orenji’ itakuwa shilingi 10,000, VIP B na C itakuwa shilingi 20,000 huku VIP A ikiwa ni shilingi 30,000.

  Mbali na hilo, uongozi wa uwanja huo uliweza kuwapeleka waandishi katika chumba chenye mitambo ya kamera za ulinzi (CCTV) ambapo takribani uwanja mzima kuna kamera 119 zilizozunguka kila sehemu.
  Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na michezo Yusuph Singo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi Boniface Wambura.
  Mkuu wa kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Inspekta Hashim Abdallah akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa na kutoa rai kwa mashabiki wa timu hizo kuja kwa ustaarabu.
  Waandishi wa habari wakiwa wanapata maelekezo ya namna kamera zilizopo uwanjani zinavyotumika.


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha ofisini kwake, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo, leo Feb 20, 2017. 
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuonyesha sehemu ya kuketi, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya kufika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya mazungumzo, leo.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, wakifurahia jambo, baada ya kuketi kwa ajili ya kuanza mazungumzo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo. Feb 20, 2017.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, Ofisini kwake, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,  leo Feb 20, 2017.
   Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga ambaye alihudhuria mazungngumzo hayo
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagana na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, baada ya mazungumzo yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 20, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpugia mkono wa kwa heri, Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke, wakati akiondoka katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 20, 2017. Kulia ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali mstaafu Ngemela Lubinga. 
   Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akimpokea Balozi wa Uingereza hapa nchini,  Darah Cooke alipowasili kwa ajili ya kukutana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
   Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akiwa na Balozi wa Uingereza hapa nchini,  Darah Cooke baada ya kumpokea alipowasili kwa ajili ya kukutana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.
  Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali mstaafu Ngemela Lubinga akimpeleka Balozi wa Uingereza hapa nchini,  Darah Cooke katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kwa ajili ya kukutana na Katibu Mkuu huyo wa CCM,  katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.

  BALOZI WA RWANDA NA WA KOREA KASKAZINI
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Balozi wa Korea Kaskazini  hapa nchini, Kim Yong Su, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, katikati ya wiki iliyopita.
   Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Balozi wa Rwanda hapa chini, Eugene Kayihura, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, katikati ya wiki iliyopita.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akiagana na Balozi wa Rwanda hapa chini, Eugene Kayihura, baada ya mazungumzo yao, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, katikati ya wiki iliyopita.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

  0 0

  Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

  Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira , January Makamba amesema kuwa Tanzania ni nchi ambayo pombe inapatikana kirahisi.

  Kauli hiyo inatokana na agizo la waziri mkuu juu ya kuzuia matumizi ya  pombe  za mifuko ya Plastiki kutokana na adhari za pombe katika jamii.
  Makamba ameyasema hayo leo wakati akitangaza juu ya uzuiaji wa viroba katika mifuko ya plastiki, amesema kuwa kuanzia Machi moja ni marufuku kwa  pombe za mifuko ya plastiki ni mwisho na wataofanya biashara hiyo watachukuliwa hatua.

  Amesema kuwa wanaanda kanuni ambazo zitabana biashara hiyo kutokana na kufanywa kwa muda mrefu bila serikali kupata kodi biashara ya pombe katika mifuko ya plastiki.

  Makamba amesema kuwa biashara hiyo itakuwa ngumukwa watengenezaji kutokana na masharti  yaliyokuwepo kwa wale ambao wataomba biashara hiyo.Aidha amesema  kuwa kamati za ulinzi wilaya kufanya operesheni katika maeneo yao ikiwa katika mipaka ambayo pombe za  viroba zinaweza  kuingia.

  Makamba amesema kuwa pombe za viroba inatakiwa kuwa historia na kuanza kuwepo kwa pombe katika chupa za plastiki au kioo kwa milimita 250 .
   Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo Richard Muyungi.
  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo Richard Muyungi.


  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Rosemary Mshama (kulia) wakati alipotembelea Kituo cha Utafiti cha hospitali hiyo Februari 20, 2017. 
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sanamu ya binadamu wakati alipotembelea moja ya darasa la Chuo cha Uuguzi katika hospitali ya Haydom wilayani Mbulu, Februari 20, 2017. 
   
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama sukari na nishati ya kuni inayotengenezwa kwa kutumia makapi ya miwa inayokamuliwa katika kiwanda cha sukari cha Manyara wakati alipotembelea kiwanda hicho Februari 19, 2017. Kuni hizo zina ubora unaofanana na ule wa makaa ya mawe na hutumika zaidi katika mitambo inayotumia nishati ya kuni. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Charles Tizeba na kulia kwa Waziri Mkuu, ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia ngoma ya asili ya kabila la Wahatzabe wakati alipowasili kwenye hospitali ya Haydom kuanza ziara ya wilaya ya Mbulu, Februari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa wilaya mstaafa, Mama Sanka baada ya kuwasili kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara mjini Babati akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 19, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)  Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali haina kipingamizi na wazo la kuifanya hospitali ya rufaa ya Haydom kuwa ya kanda kwani hatua hiyo itaupunguzia mzigo Serikali.

  “Serikali hii ni sikivu, na kuifanya hospitali hii kuwa ya kanda ni kazi ndogo. Kwa hiyo nitamleta Waziri wa Afya aje awaongoze kusimamia vigezo vya kuifanya hospitali hii iwe ya kanda,” amesema.

  Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Februari 20, 2017) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Haydom kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa kata.

  "Serikali haina kipingamizi na wazo lenu, cha msingi ni vigezo muhimu vifuatwe. Kwa hiyo, nitamleta Waziri wa Afya awasaidie kuangalia vigezo," amesisitiza.

  “Kama vigezo havipo, tushirikiane kuvikamilisha kwa sababu uwepo wa hospitali hii kwa hadhi ya kanda kunaisadia Serikali kutokana na nafasi yake kijiografia,” amesema Waziri Mkuu

  “Nia yetu ni kupunguza gharama kwa mgonjwa anayelazimika kutoka Simiyu hadi Bugando (Mwanza) au kutoka Arusha hadi Muhimbili (Dar es Salaam).  Hapa ni katikati na nimearifiwa kuwa wagonjwa kutoka mikoa mitano ya Tabora, Simiyu, Arusha, Singida na Manyara wanafika hapa kupatiwa matibabu,” amesema.

  Amesema Serikali imepokea maombi kwa ajili ya watumishi wanaotakiwa kwenye hospitali hiyo na kwamba hivi karibuni itaajiri watumishi kati ya 5,000 hadi 6,000 wa sekta ya afya peke yake. “Tumekwishaanza kuajiri, tumeanza na sekta ya elimu kwa kuajiri walimu 4,693 ambao wote ni wa fani ya sayansi. Na sekta inayofuata ni ya afya, kwa hiyo hao watumishi 90 wanaohitajika watapatikana kwenye kundi hilo hilo,” amesema.

  Hospitali hiyo inahudumia wananchi kutoka wilaya nane za Mbulu, Hanang, Babati, Karatu, Mkalama, Iramba, Kondoa na Meatu.

  Wakati huohuo, Balozi wa Norway nchini Tanzania, Bibi Hannamarie Kaarstad ambaye alikuwepo kwenye mkutano huo, alisema amefarijika na mchango unaotolewa na Serikali ya Tanzania kusaidia juhudi zinazofanywa na marafiki wa hospitali walioko Norway.

  “Hospitali ya Haydom ni mahali thabiti ambapo mshikamano baina ya Tanzania na Norway unaweza kuonekana kwa dhahiri. Nawashukuru watumishi wa hospitali kwa moyo wao wa kujitoa kuwahudumia wananchi wa wilaya ya Mbulu na maeneo ya jirani,” amesema.

  Hospitali hiyo ambayo inaendeshwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mbulu kwa ufadhili kutoka Serikali za Tanzania na Norway, ilianzishwa mwaka 1955 ikiwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 50. Hivi sasa ina uwezo wa kulaza wagonjwa 420 kwa wakati mmoja.

  Pia inatoa huduma za upasuaji, magonjwa ya macho, tiba ya mifupa na mazoezi ya viungo. Ilipandishwa hadhi kuwa ya rufaa baada ya mkoa wa Manyara kuanzishwa.

  Mapema, akisoma taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa Tiba wa hospitali hiyo, Dk. Emanuel Q. Nuwass alisema wameomba kibali cha ajira kwa watumishi 90 kupitia bajeti ya mwaka 2016/2017.

  “Tumeomba pia hospitali ipandishwe hadhi na kuwa ya rufaa ya kanda (Kaskazini kati au Kanda maalum) ili iweze kutoa huduma bora kwa mkoa wa Manyara na mikoa jirani kwani wahisani wa maendeleo wako tayari kuchangia ujenzi wa miundombinu,” alisema.

  Pia aliomba waongezewe ruzuku ya dawa ikilinganishwa na ya sasa hivi ambayo ni asilimia 15 na pia waongezwe malipo ya on call allowancekwa ajili ya madaktari  na watumishi wengine wa hospitali hiyo.


  IMETOLEWA NA:
  OFISI YA WAZIRI MKUU,
  JUMATATU, FEBRUARI 20, 2017.

  0 0

  Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule.
   
  Na Mathias Canal

  Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule amewaagiza walimu wakuu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kusimamia zoezi la upandaji miti kwa kumkabidhi kila mwanafunzi mti mmoja ambao atautunza katika kipindi chake cha masomo.

  Dc Senyamule ametasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilayani humo kilichohudhuriwa na walimu wote wa shule za msingi na sekondari, Waratibu elimu, Maafisa Tarafa, Wazazi, Wanafunzi wawakilishi pamoja na baadhi ya Viongozi wa dini. 

  Kikao hicho kilichokuwa na lengo la kukubaliana na kupata namna bora ya kuboresha elimu na kiwango cha ufaulu Wilayani Same, Mkuu huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo kwa namna maalumu kwa ajili ya wanafunzi kufundishwa kwani mafanikio ya jitihada zao pekee katika kujisomea na kufundishwa darasani haitoshi bali wanahitaji kuongezewa msukumo na utaalamu zaidi kwa masomo ya ziada.

  “Sote hapa kwa umoja wetu ni lazima tutambue kuwa matokeo bora ya wanafunzi waliopo darasa la saba, wanafunzi wa kidato cha nne na cha sita yapo mikononi mwa walimu hivyo njia bora ni kutatua matatizo yanayowakabili walimu ili tuweze kufikia lengo” Alisisitiza Mhe Senyamule

  Ameeleza kuwa endapo Changamoto za makundi yote zitatekelezwa kwa kufuata utaratibu ikiwemo kila mmoja kutumia nafasi yake ipasavyo katika kufuatilia mwenendo wa wanafunzi kwa kuanzia Walimu, Serikali, Wazazi, na Wanafunzi Wilaya hiyo itakuwa na matokeo makubwa katika matokeo yajayo.

  Staki alisema kuwa Wilaya ya Same imeanza imeanza kukua kielimu kupitia matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwani Wilaya hiyo imeshika nafasi ya 62 kati ya Halmashauri 184 ambapo kwa Mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 103.Aidha katika matokeo ya kidato cha pili Wilaya ya Same imeshika nafasi ya 37 kati ya 184 kwani mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 47.

  Pia amewataka viongozi wote katika kada mbalimbali kutumia vyema uongozi wao kwa kuwatumikia wananchi huku akiwasihi kutumia lugha nzuri pindi wanapozungumza nao kwani kiongozi yeyote atakayetumia lugha mbaya anapaswa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo. 

  Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Same amepinga vikali matumizi ya Dawa za kulevya ambapo amesema kuwa kwa Wilaya hiyo baadhi ya wananchi wake ni wazalishaji wakubwa wa zao aina ya Mirungi ambalo pia limepelekea vijana wengi kutumia huku wakijiweka kando na elimu kwa kuamini kulima zao hilo sehemu ya mafanikio yao ya haraka.

  Dc Staki amesema uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea na oparesheni ya kuteketeza matumizi ya mirungi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matumizi ama uuzaji wa zao hilo.
   

  0 0

  Mkufunzi wa Maswala ya Biashara Ndugu Felix Maganjila Akitoa Mada kwenye Mradi wa kuwejengea Uwezo wanawake Kwenye Ujasiriamali kupitia Taasisi ya Manjano Foundation. Mafunzo hayo yalianza wiki iliyopita kwa lengo la kuwajengea Uwezo wanwake wa Kitanzania kupitia bidhaa za vipodozi vya LuvTouch Manjano. Washiriki wataweza kujisimamia na kujikita vizuri kwenye biashara ya vipodozi na kujua mbinu mbalimbali za biashara kwa lengo la kumjengea uwezo mwanamke wa Kitanzania.
  Image may contain: 3 people, people sitting and text
  Washiriki wa Mafunzo ya Usajiriliamali na Urembo yalio chini ya Manjano Foundation wakisiliza kwa makini mada mbalimbali kuhusu mafunzo hayo ya kuwapa uwezo wa kuthubutu kufanya biashara, kujisimamia na kujua mbinu mbalimbali za biashara.Image may contain: 5 people, people standing
  Mkurugenzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Mama Shekha Nasser Akiwa Katika Picha ya Pamoja na Baadhi ya Washiriki walionufaika na Mradi huo.
  Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili uwezo wake ikiwa pamoja na kuisaidia jamii yake iliyomzunguka. Taasisi hii limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano.
  Awamu ya Pili ya Mradi huu Ulizinduliwa na waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charles Mwijage mnamo tarehe 14 Februari 2017, ambapo alisema amefurahishwa sana wwa mwanamke wa Kitanzania kuzindua mradi unaowawezesha wanawake kujiongezea kipato na kujiajiri hasa kwenye sekta ndogo ya Urembo yenye fursa kubwa ya kukua.

  0 0


  Mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya Taifa(NHIF)Anna Makinda akifungua mkutano wa wadau wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

  Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Benard Konga akiongeo na wadau wa mfuko huo(hawapo pichani)wakati wa kikao cha wadau wa mfuko wa NHIF kilichofanyika leo Mkoani Kagera

  Meneja wa mfuko wa bima ya afya(NHIF)Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akieleza changamoto na mafanikio ya mfuko katika Mkoa wa kagera kwa wadau wa mfuko wa Bima.

  Meneja wa mfuko wa bima ya afya Mkoa wa Kagera Elias Odhiambo akiteta jambo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wakati wa kikao cha wadau wa mfuko huo,Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi wa mfuko huo Anne Makinda  Baadhi ya wadau wa mfuko wa bima ya afya wa Mkoa wa Kagera wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa wadau wa bima ya afya na viongozi kutoka makao makuu ya mfuko huo.


  Na Editha Karlo wa blog ya jamii,Kagera

  MWENYEKITI wa Bodi ya mfuko wa Taifa wa bima ya afya(NHIF) Anne Makinda amesema kuwa kituo chochote kilichosajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma ya afya kwa wateja wa mfuko wa bima ya afya, ambacho kimeajiri wahudumu wenye mfumo wa unyanyasaji kwa wagonjwa ikiwemo Lugha za kejeli kwa wateja vitaondolewa kwenye mpango wa huduma ya afya.

  Makinda alisema hayo leo wakati wa mkutano wa wadau wa NHIF na CHF Mkoani Kagera katika ukumbi wa mikutano wa mkuu wa mkoa wa Kagera Mjini Bukoba.

  "Hivi wewe mtoa huduma wa afya unapotoa lugha ya kejeli na vitisho,matusi kwa wagonjwa unapata faida gani?,unapata fedha kiasi gani?sasa naagiza vile vituo ambavyo tumevisajiri kutoa huduma zetu ambavyo bado vinaendekeza mfumo wa kunyanyasa wagonjwa, sasa tunasema basi hatuwezi kuvumilia kinachofuata kuwafuatia sajili alisema Makinda.

  Aidha aliwaagiza wamiliki wa vituo hivyo kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja kuweka mkakati madhubuti wa kuhakikisha wanaondoa kero hiyo haraka iwezekanavyo kwani watu wakijiunga na bima lengo ni wapate huduma stahiki ikiwemo mapokeo mazuri jambo ambalo linampa mgonjwa faraja hata kabla ya kupata dawa.

  Pia aliwashauri wadau wa mkoa wa Kagera kutoa maoni yao hata kama mfuko huo una mapungufu ili kwa ushirikiano wa pamoja yaweze kutafutiwa ufumbuzi wa kina na huduma ziendelee kutolewa ipasavyo.

  Kaimu mkurugenzi mkuu wa Nhif makao makuu Bernard Konga alisema kwasasa wamejikita katika kuboresha huduma na kuondoa chamgamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili wateja wao ambazo amezitaja kuwa ni,kupewa majina ya kejeri na watoa huduma wa afya kama vile nyie wa bure,unyanyapaa,uhaba wa dawa ikiwemo misongamano wa wateja ambapo kwa sasa zinaendelewa kutatuliwa kwa kina.

  Meneja wa Nhif mkoa wa Kagera Elius Odhiambo alitaja changamoto zinazowakabili katika utendaji wao kuwa ni pamoja na kuwepo na vitendo vya udanganyifu na kughushi madai ya malipo kwa huduma za matibabu,mwitikio Mdogo wa wananchi kujiunga na mpango wa bima ya afya na ucheleweshwaji wa michango ya wanachama kwa baadhi ya waajiri.

  Odhiambo alisema ili kukabiliana na changamoto hizo pia wamejiwekea mipango endelevu katika kufanya kazi zao ambapo ni pamoja na kuhamasisha watoa huduma ili watumie fursa ya mikopo ya vifaa,tiba,ukarabati wa majengo,dawa na vitendanishi ili kuboresha huduma za matibabu.

  Pia kuendelea kuchukua hatua kali kupambana na vitendo vya udanganyifu kwa baadhi ya watoa huduma wasio waaminifu.

older | 1 | .... | 1145 | 1146 | (Page 1147) | 1148 | 1149 | .... | 1897 | newer