Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1148 | 1149 | (Page 1150) | 1151 | 1152 | .... | 1903 | newer

  0 0

   Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na taaisisi ya Land O Lakes, na kufadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Watu wa Merekani (USAID),  Dk Rose Kingamkono (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harambee iliyoitishwa na taasisi hiyo kesho Alhamisi ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo biashara  kupitia taasisi iliyojikita kwenye kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT). Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi ya CAWAT Dk. Victoria Kisyombe.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi ya CAWAT Dk. Victoria Kisyombe (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na harambee itakayofanyika kesho (Alhamisi) jijini Dar es Salaam ikilenga kukusanya fedha kwa ajili ya uwezeshaji wa wanawake katika kilimo biashara. Kulia ni Mkurugenzi wa Mradi wa Ubunifu  Katika Maswala ya Kijinsia na Kuimarisha Uhakika wa Chakula Katika Ngazi ya Kaya, unaoendeshwa na taaisisi ya Land O Lakes,  Dk Rose Kingamkono (kushoto)

  Taasisi isiyo ya kiserikali ya Land O’ Lakes imewaomba wadau wa kilimo na biashara nchini kushiriki kwenye harambee inayolenga kukusanya fedha kiasi cha Tsh 150 milioni kwa ajili ya kuwezesha mradi wa kuwajengea uwezo wanawake waweze kushiriki kikamilifu katika kilimo biashara, inayotarajiwa kufanyika kesho Alhamisi.

  Harambee hiyo inayotarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa itafanyika jijini Dar es Salaam, huku kiasi cha fedha kitakachopatikana kikitarajiwa kuelekezwa katika kuijengea uwezo wa kiutendaji taasisi inayojihusisha na kuendeleza wanawake katika kilimo Tanzania (CAWAT).

  Harambee hiyo imebeba kauli mbiu: ‘Wezesha kilimo biashara kwa ajili ya ajira, jamii na viwanda endelevu’.

  “Mafanikio tutakayoyapata kupitia harambee hii yataiwezesha CAWAT kutoa mafunzo na kuwajengea uwezo wanawake wanaojishughulisha na kilimo hapa nchini kubadilika na kujikita zaidi katika kilimo biashara kwa maana kwamba watajengewa uwezo wa kufahamau fursa za masoko ya bidhaa wanazozalisha, kujitangaza pamoja kuwaunganisha na wawekazi wakubwa,’’ alisema Mkurugenzi wa Mradi kutoka Land O’ Lakes, Dk Rose Kingamkono.

  Hatua hiyo inakuja huku takwimu zikionyesha kwamba zaidi ya asilimia 70 ya watu hapa nchini wanaishi vijijini na kwamba asilimia 98 ya wanawake wanaoishi vijijini wanajishughulisha zaidi na kilimo ambacho hata hivyo kinachangia asilimia 26 ya pato la nchi.

  Pamoja na wanawake kuwa wahusika wakuu na wanatumia muda mwingi kwenye shughuli za awali za kilimo, mara nyingi wamekuwa hawafaidiki na jasho la kazi zao.Hali hii ni kwa kuwa wanaume wamekuwa wakihodhi masuala yote yanayohusiana na faida zitokanazo na kilimo kwa kuhusika zaidi mwisho wa mnyororo wa kilimo ikiwemo masoko,’’

  “Ni katika mazingira kama hayo ndipo unaonekana umuhimu wa kuwekeza jitihada zetu za hali na mali katika kuhakikisha kwamba huyu mwanamke ambae hanufaiki na jasho lake licha kusota katika msimu wote wa kilimo sasa ananufaika na hili litawezekana iwapo atajengewa uwezo wa kufanya kile ambacho jamii inaamini mwanamke hawezi kukifanya yaani kilimo biashara,’’ aliongeza Dk Kingamkono katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam

  Akizungumzia kuhusu taasisi ya CAWAT, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa taasisi hiyo Dk Victoria Kisyombe, alisema kwa sasa ipo kwenye mchakato wa awali wa kuanza kujitegemea yenyewe kiuendashaji bila kutegemea msaada iliyokuwa ikiupata kutoka kwenye mradi  unaohusu Ubunifu katika masuala ya kijinsia na kuimarisha uhakikaka wa chakula katika ngazi ya kaya (IGE), unaotarajiwa kuisha Machi  mwaka huu.

  Kuelekea katika kujiendesha yenyewe bila kutegemea msaada tunaoupata kutoka mradi wa IGE, CAWAT tunaona kwamba tuna safari ndefu inayohitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa maendeleo ili tuweze kutimiza wajibu wetu wa kuwasaidia wakina mama walio kwenye sekta hii muhimu ya uzalishaji. Tunawaomba sana  watanzania mmoja mmoja, taasisi, mashirika, balozi mbalimbali waguswe katika kusaidia hili.’’ Alisema Dk. Kisyombe.

  0 0

  Wakazi wa mtaa wa NAMANYINGU kata ya MSHANGANO Manispaa ya Songea Mkoani RUVUMA, wamewalazimisha mume na mke kuchimba kabuli la mtoto wao aitwaye DANROAD MAHUNDI mwenye umri wa miaka 36 ambaye inasemekana wazazi wake wamemua kwa njia za kishirikina,


  0 0
  0 0

  2


  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam. baada Mahakama hiyo kutoa amri kuzuia Polisi wasimkamate Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe hadi maombi yake ya kupinga asikamatwe, yatakaposikilizwa Alhamisi wiki hii.

  PICHA NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG

  0 0


  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (aliyevaa miwani) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyakayondo kuhusiana na utekelezaji wa miradi mbalimbali kijijini humo na jimboni kwa ujumla.
  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa kisima (kilichofunikwa kwa nyasi) kilichochimbwa katika kijiji cha Nyakayondo. Jumla ya visima virefu 30 vinatarajiwa kuchimbwa jimboni humo.
  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi ya Nyarututu, iliyopo Kata ya Bwanga. Jumla ya vyumba vya madarasa vitano na matundu 30 ya vyoo vinatarajiwa kujengwa katika shule hiyo.
  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (katikati) akiongozana na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Chato, Ibrahim Bagula (kushoto) na Diwani wa Kata ya Bwanga, Nuhu Mahmoud (kulia) wakati wa ukaguzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa Jimboni humo.

  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Chato, Shaban Ntalambe (kulia) na Diwani wa kata ya Bwanga, Nuhu Mahmoud (katikati) wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na ofisi ya walimu katika shule ya Msingi ya Bwanga B. Mradi huo unahusisha ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa, ofisi ya walimu na matundu 30 ya vyoo.
  Mbunge wa Jimbo la Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (wa pili kushoto) akielekeza jambo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi mbalimbali jimboni humo. Kulia ni Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Mali Misango. Nyuma ya Dkt. Kalemani ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato, Christian Manunga.

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto)akipokea kutoka kwa Mhandisi Shin Pil Soo sehemu ya msaada mabati 300 na mifuko ya Sementi 500 iliyotolewa na Kampuni ya ujenzi ya Hanil Jiangsu Joint Venture Ltd inayojenga barabara ya Sakina hadi Tengeru yenye urefu wa kilometa 14.1 ,kulia ni Meneja wa Tanrods mkoa wa Arusha,Mhandisi John Kalupale,msaada huo umetolewa kwa Mkuu wa mkoa ili umwezeshe kusaidia shughuli za maendeleo zilizoanzishwa na wananchi na alikabidhi ili utumike kwaajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Makuyuni wilayani Monduli. 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishirikiana na askari wa JKT kambi ya Makuyuni na wananchi wa Kata ya makuyuni katika ujenzi wa Kituo cha Afya katika ziara yake wilayani Monduli. 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(katikati) akilakiwa na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Rifit Valley Kata ya Majengo wilaya ya Monduli,kushoto ni Mkuu wa wilaya hiyo,Idd Kimanta na kulia ni Mkuu wa Shule,Julius Maghembe. 
  Mkuu wa Shule ya Sekondari Rift Valley ,Julius Maghembe akiinua Sh 500,000 zilizotolewa na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho gambo kwaajili ya kununua viti vitano vya walimu. 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo(kushoto) akiwa na viongozi wa wilaya ya Monduli ndani ya moja vya vyumba viwili madarasa vilivyozinduliwa baada ya ujenzi wake kukamilika katika Shule ya Sekondari Rifit Valley. 
  Wananchi wakichangia nguvu zao katika ujenzi wa jengo la Upasuaji kwenye Kituo cha Afya Mto wa Mbu 
  Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Mrisho Gambo akishiriki kazi za mikono pamoja na wananchi katika ujenzi wa jengo la Uapsuaji katika Kituo cha Afya Mto wa Mbu aliahidi kutoa mifuko 100 ya Sementi na Mabati 100.   0 0


  Upatikanaji wake ni rahisi, wa haraka na ni huduma
  salama ya kibenki kupitia mtandao

  Benki ya Stanbic Tanzania imezindua huduma mpya ya malipo kupitia intaneti na simu za mkononi inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha ukusanyaji wa pesa na ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali mbali, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kutoa huduma rahisi na salama za kibenki

  Akizungumza katika uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki hiyo, Bw. Charles Mhina alisema mabadiliko hayo ya ufanyaji malipo na makusanyo yaani malipo ya pamoja kupitia internet na mitandao na uwekaji fedha benki – yatawahakikishia wateja wa benki katika sekta mbalimbali maboresho makubwa katika utoaji huduma

  Akizindua huduma hiyo ya kipekee katika soko ijulikanayo kama Malipo ya Pamoja Kupitia simu ( Mobile Bulk Payment), Bw. Mhina alisema huduma hiyo itayawezesha mashirika kufanya malipo kutoka katika akaunti zao za Stanbic kwenda kwenye mitandao mbali mbali ya simu ikiwa ni pamoja na Tigo Pesa, Airtel Money,Mpesa na Ezypesa wakati wowote na popote walipo

  Alisema Malipo ya Pamoja kupitia Simu yatatolewa kupitia mfumo wa utoaji huduma mtandaoni wa benki hiyo, ambao unawahakikishia wateja upatikanaji wa huduma wakati wowote, kwa njia rahisi, ya haraka na salama, jambo linaloongeza ufanisi zaidi katika ufanyaji wa miamala yao ya kibiashara. 

  “Uzinduzi wa huduma hii ni uthibitisho wa jitihada za Benki ya Stanbic katika kuboresha huduma zetu za ufanyaji miamala, lengo kuu likiwa ni kuleta tija katika biashara za wateja wetu,” alisema Bw. Mhina

  Akizungumzia juu ya huduma ya malipo bila kutumia pesa taslim (Till to Bank Cashless Payment) ambayo itawawezesha wafanyabiashara kupokea malipo ya moja kwa moja kutoka katika mitandao ya simu, Bw. Mhina alisema huduma hiyo itaruhusu wamiliki wa akaunti za biashara kupokea malipo kupitia Mpesa, Tigopesa na Airtel Money kutoka kwa wateja wao kupitia namba maalum na fedha zitaelekezwa moja kwa moja kwenye akaunti zao za Benki za Stanbic

  Alieleza kwamba kutokana na kuwa soko limetawaliwa na pesa taslim, huduma hii imelenga katika kupunguza mzigo mkubwa kwa wafanyabiashara wa upokeaji wa malipo ya fedha taslim na kubadilisha tabia ya wateja kwenda kwenye malipo ya mtandao

  “Benki ya Stanbic ipo katika mstari wa mbele katika ugunduzi. Leo hii pia tunatambulisha huduma ya Till-to-Bank kwa wateja wetu. Malipo kupitia mtandao sasa yameyapita malipo ya pesa taslim na tunatizamia kuwa asilimia kubwa ya malipo hayatakuwa ya fedha taslim katika miaka michache ijayo. Tumesimama katika mhimili wa kulirahisisha hili kwa wateja wetu,” alisema.
  Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa na Huduma za Miamala wa Benki ya Stanbic Tanzania, Bw. Charles Mhina(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya malipo kupitia internet na simu za mkononi inayoambatana na huduma nyinginezo zinazolenga kuboresha ukusanyaji wa pesa na ufanyaji wa malipo kwa mashirika na biashara mbali mbali jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mkuu wa kitengo cha  upatikanaji wa huduma kwa wateja wa benki hiyo, Allen Chiombola.


  0 0

   Baba mmoja mabaye jina lake halikupatikana akiwa amembeba mwanae kwa mtindo wa 'Kangaroo Style' wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza na wanakijiji  wa Singu wilayani  Babati, Februari  21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiweka jiwe la Msingi la daraja la Bonga- Endanachan wilayani Babati,  Februari 22, 2017.  Kulia ni Mkoa wa Manyara, Dkt, Joel Bendera na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Babati, Raymound Mushi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Na Bashir Yakub.

  Wenye nyumba hawako salama ikiwa wapangaji wao ni wahusika wa dawa za kulevya. Ni muhimu kulijua hili ili kujihadhari na kile ambacho kinaweza kukuletea madhara. Sheria mpya ya kupambana na kuzuia dawa za kulevya “The Drug Control and Enforcement Act, No 5 of 2015” imeeleza kwa mapana uhusika wa watu wa kada mbalimbali katika dawa za kulevya.

  Tunachotakiwa kujua ni kuwa uhusika haumlengi tu yule mwenyewe mhusika halisi bali umeelekezwa mbali na hata kufika kwa wenye nyumba au wamiliki wa nyumba/eneo.

  Pia uhusiano katika sheria hii haumlengi tu mwenye nyumba na mpangaji wake, bali pia mwenye nyumba na wale walio katika nyumba yake wawe watoto, mke, ndugu, rafiki n.k., madhali ni watu wako katika nyumba yako au eneo unalomiliki basi watakuhusu katika hili .

  Hata hivyo kabla ya kuona hatia ya mwenye nyumba/eneo tutizame kwanza ni vitu gani vinaitwa dawa za kulevya ili kama unajihadhari ujue lipi la kujihadhari nalo.

  1.NI VITU GANI VINAITWA DAWA ZA KULEVYA.

  Sheria ya Kupambana na dawa za kulevya inataja aina nyingi mno ya vitu ambavyo imeviita dawa za kulevya. Vipo jamii ya kimiminika, jamii ya unga,  jamii ya miti, majani, mbegu n.k.

  Kifungu cha 2 cha sheria hiyo kinachosomwa sambamba na Schedule ya 1 ya sheria hiyohiyo kimeorodhesha zaidi ya sampuli 100 ya vitu ambavyo vinahesabika kuwa ni dawa za kulevya hapa Tanzania. Humo imo pia bangi, mirungi, cocaine, heroine, mandrax, morphine, cannabis resin au opium,coca  leaf, alphaprodine, etorphine n.k.

  Ni vigumu kuzitaja kwa Kiswahili lakini pia ni vigumu kuzitaja zote kwa kuwa ziko zaidi ya mia. Muhimu ni kuwa jihadhari na mienendo ya wapangaji au wale uliowaweka katika nyumba/eneo lako. 

  Pia ujue kuwa mirungi nayo ni dawa za kulevya tofauti na wengi wanavyodhani kuwa ni kiburudisho cha starehe halali kama ilivyo sigara au vingine. 

  2. HATIA YA MWENYE NYUMBA IKIWA MPANGAJI ANAHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA.

  Kifungu cha 19 ( 1 ) cha sheria hiyo kinakataza mmiliki wa muda au wa kudumu kuruhusu eneo lake kutumika kwa namna yoyote katika shughuli yoyote ya dawa za kulevya.

  Mmiliki wa muda anaweza kuwa muangalizi wa nyumba labda ameachiwa jukumu hilo na mmiliki halisi au anaweza kuwa mpangaji aliyempangisha mpangaji mwingine( sublease). Wote hawa wanaweza kuwa na hatia katika kifungu hiki.

  Mmiliki wa kudumu ndiye mmiliki halisi wa nyumba/eneo. Huyu naye anawajibika katika kifungu hiki. 

  KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com.

  0 0


  Bwana Jackson Oganga akiwa anatoa maelezo kwa vijana jinsi ya kupata 'Scholarship' katika zinazotolewa sehemu mbalimbali.
  Mwakilishi wa Asasi ya Kiraia  Global Peace Foundation (GPF) Tanzania aliyewakilisha katika Semina hiyo Bi. Anna Mwalongo akielezea kwa kifupi kuhusu Asasi hiyo.
  Mshauri wa mambo mbalimbali ya Kijamii na uchumi  Bw. Anthony Luvanda akitoa masomo mbalimbali ya namna vijana wanavyoweza kujikwamua na kujitegemea kwa kufanya shughuli mbalimbali.
  Baadhi ya vijana wakiendelea kusikiliza kwa makini mambo mbalimbali katika Semina Hiyo
  Bi. Bernice Fernandes akielezea namna alivyopata nafasi ya kwenda kusoma Marekani kupitia 'Scholarship'  na kuwasihi vijana wasikate tamaa kwa kuwa nafasi za kwenda kusoma nje zipo nyingi 
  Muandaaji wa Semina hiyo na Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash akieleza namna ambavyo vijana wanaweza kujiunga katika programu mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
  Mwakilishi kutoka Raleigh Bi. Alice Norbert akitoa maelezo namna ya vijana ambavyo wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea katika Asasi mbalimbali za Kiraia.
  Baadhi ya vijana wakiuliza maswali mbalimbali kwa wasemaji
   Picha ya pamoja ya watoa mada mbalimbali Kutoka Kushoto ni Frank Joash,Anthony Luvanda, Evance Exaud,Alice Norbert, Anna Mwalongo, Bernice Fernandes, Nelson Amar na Jackson Ogonga.
   Watoa Mada wakiwa pamoja na Baadhi ya washiriki waliohudhuria Semina hiyo

  Picha na Fredy Njeje


  Katika kuhakikisha vijana wanashiriki na kujikwamua katika mambo mbali mbali UNESCO  Youth Forum waliandaa semina ambayo ilihusu vijana kushiriki katika programu mbalimbali za umoja wa mataifa, Kudumisha amani kutoka ngazi ya vijana na jamii kwa ujumla ambapo Global Peace Foundation Tanzania walitoa mafunzo juu ya maswala hayo, kuhusu kusoma nje na kuelekezwa njia mbali mbali za kufanya kazi kwa kujitolea katika asasi mbalimbali za kiraia.


  Akizungumza na vijana hao kutoka vyuo mbalimbali na wale ambao walimaliza vyuo mwakilishi wa    asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Anna Mwalongo alisema kuwa Global Peace Foundation ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ileina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.” Alisema Anna.


  Aliongeza kuwa Mnamo mwezi wa saba mwaka 2015 Global peace foundation waliandaa Mkutano mkubwa wa amani uliofanyinka Zanzibar uliojulikana kwa jina la Global peace Leadership Conference (GPLC Zanzibar) ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa pili wa Rais Mh. Balozi Seif Ali na kuhudhuriwa na marais wastaafu kutoka nchi mbalimbali. 

   "Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015 walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kuendesha kampeni ya “AMANI KWANZA” ambapo aliwalenga wanawake na vijana kushiriki katika uchaguzi huo kwa amani, alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa GPF wanampango wa kupanua wigo zaidi ili kuwafikia watanzania wengi zaidi kueleza mambo mbalimbali ya amani kupitia kampeni yao ya “VIJANA NA AMANI” " Alisema Anna


  Kwa upande wake Mwenyekiti wa UNESCO Youth Forum Bw. Frank Joash alisema vijana wengi hawana uwelewa wa program mbali mbali za umoja wa mataifa hivyo waliamua kuwakutanisha ili kuwapa uelewa ili wapate kujiunga.


  Nae Bi. Bernice Fernandes pamoja na Bw. Jackson Oganga ambao walishawahi kusoma nje ya nchi kupitia ufadhili ‘Scholarship” walielezea kwa kina namna walivyo fika huko, changamoto na jinsi zinavyotokea na kuwasihi vijana hao kutokata tamaa na kuendelea kuomba nafasi hizo mpaka pale watakapo fanikiwa nao kutimiza ndoto zao za kwenda kusoma nje.


  Mwisho Mshauri na mwezeshaji katika mambo mbalimbali ya Bw. Anthony Luvanda aliwasihi vijana kujitambua na kufahamu vipaji vyao na kujua namna ya kutimiza ndoto zao, ambapo aliwaomba pia vijana wasitegemee sana kazi za kuajiliwa bali wawe na mawazo chanya ili kuweza kutimiza malengo yao


  Semina hiyo ilihudhuriwa na vijana kutoka vyuo vya, Chuo kikuu cha Dar es salaam, DUCE,TIA, NIT,Bagamoyo University,DIT na TIA , wanavyuo waliomaliza pamoja na vijana wengine ambapo jumla yao walikuwa zaidi ya 196.

  0 0

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Masaka.

  Na Benjamin Sawe.

  Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa asilimia 62 ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.

   Mkoa wa Dar es Salaam una jumla ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya kazi (miaka 15 - 64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara na ajira viwandani.

  Awali Tanzania iliweza kutoa ajira kwa vijana wengi kupitia viwanda vyake vya nguo vilivyokuwa katika mikoa mbalimbali kama kile cha Urafiki cha Dar es Salaam na vinginevyo ambavyo hata hivyo kwa sasa viko hoi kutokana na kuhujumiwa na watendaji wasio waaminifu.

  Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu katika uchumi wa Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya aina mbalimbali kufuatana na bidhaa zinazozalishwa.

  Katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna bidhaa za aina mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango kikubwa na kupelekwa nje ya Mkoa.
  Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.

  Tanzania haiwezi kubadilika ikiwa mawazo ya watu hayatabadilika katika ujenzi wa viwanda vidogo nchini kote na kuondoa mawazo ya kujenga viwanda vikubwa kama vya wafanyanyabiashara wakubwa, kwa kuwa vinahitaji mtaji mkubwa wakati ajira zake ni chache.

  Ama kwa hakika kila mmoja wetu anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya tano ya Dr. John Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu ya kuwa na taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera ya Tanzania ya viwanda.

  Ni kwasababu hiyo tu, watendaji wake aliowaamini na kuwapa  dhamana, hawana budi kuendelea kuwaza zaidi, kutenda zaidi na kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja waikamilishe  ndoto hii ya Rais wetu mpendwa. 

  Ushirikiano baina ya Makonda na Azimio Housing Estate kampuni ambayo imekubali  kutoa eneo lililopo Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470 litakalotumika kama eneo maalumu mbalo litagawiwa kwa wajasiriamali zaidi ya 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo ni mfano wa kuigwa na kupongezwa kwani hii inaonyesha wazi dhamira ya Mheshimiwa Makonda ya kuwakomboa wajasiriamali wadogo wa jiji la Dar es Salaam.

  Pamoja na mambo mengineyo mpango huo unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo kupata maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo, kuwaepusha na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika wa kuwa na anuani (address) za kudumu.

  Kutokana na kauli ya Mheshimiwa Makonda kuna matumaini kwamba neema inawajia wanadar es salaam ya ajira na soko la bidhaa zao kutokana na ujio wa viwanda hivyo.

  Watu wenye viwanda vidogo wana changamoto nyingi za maeneo na wengine kulazimika kuweka katika maeneo ya watu na kusababisha kero kwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo hayo.

  Kwa ujumla, ujenzi wa viwanda si kitu kidogo, unahitaji muda na rasilimali nyingine nyingi kufanikisha hatua inayotarajiwa na umma.

  Ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, inaelekea kutimia baada ya Serikali ya Awamu ya Tano kuonesha kwa vitendo dhamira yake ya kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.

  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Paul Makonda anastahili pongezi kubwa na za dhati kabisa kwa mkakati wake wa kujenga Dar es Salaam mpya.

  0 0

  Leo Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, anayeshughulikia Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga amezuru kituo cha Radio cha CCM, Uhuru FM, mtaa wa Lukoma, jijini Dar es Salaam, na kuzungumza na uongozi baada ya kuona baadhi ya shughuli zinavyofanyika kwenye kituo hicho. Pichani Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru FM, Angel Akilimali akimpatia maelezo. Na ziafuatazo ni picha mbalimbali Ngemela akiwa kwenye kituo hicho cha Radio. Picha zote kwa hisani ya Uhuru FM

  0 0

  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Kamishna Generali Mpya wa Idara ya Uhamiaji, Dk. Anna Makakala wakati alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Dk. Makakala ni mara ya kwanza kufanya mazungumzo ya kiutendaji Naibu Waziri huyo tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni. 
  Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimfafanulia jambo Kamishna Generali Mpya wa Idara ya Uhamiaji, Dk. Anna Makakala wakati alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo. Dk. Makakala ni mara ya kwanza kufanya mazungumzo ya kiutendaji na Naibu Waziri huyo tangu alipoteuliwa na Rais John Magufuli hivi karibuni. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

  0 0

  .
  Msanii Wema Sepetu akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kesi yake ya kuahirishwa hadi March 15 mwaka huu.Kesi hiyo imeaihirishwa na Hakimu Mkazi Thomas Simna baada ya wakili wa Serikali Constantine Kakula kuieleza mahakama kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo bado haujakamilika

  0 0


  Fatma Salum-MAELEZO
  Serikali imedhamiria kuzalisha wataalamu wa maji wa kutosha kukidhi mahitaji ya sasa na kuwafikishia wananchi wote maji safi na salama kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa kote nchini.

  Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Chuo cha Maji cha Dar es Salaam Dkt. Shija Kazumba wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliolenga kueleza mikakati ya chuo hicho ya kuzalisha wataalamu wenye sifa na weledi.

  “Wanafunzi waliopo sasa ni 1849, kati yao 489 ni wanawake na dhamira yetu ni kuhakikisha  kuwa kuna mafundi sanifu wa kutosha kulingana na mahitaji ya sasa na ukuaji wa sekta ya maji”alisisitiza Dkt. Kazumba.
  Alifafanua kuwa chuo hicho kimeanzisha mfuko maalum kwa ajili ya kuwainua wanafunzi wa kike ili wajiunge katika masomo ya uhandisi wa maji, mafundi sanifu, upimaji wa ubora wa maji, umwagiliaji na hali ya hewa lengo likiwa ni kuchochea ukuaji wa sekta hiyo.

  “Dhamira ya kuwainua wanafunzi wa kike inaonyesha nia ya Serikali kuwawezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika kukuza na kuendeleza sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo sekta ya maji”. Aliongeza Dkt. Kazumba.

  Pia alibainisha kuwa Serikali imewezesha kuwepo kwa maabara ya kisasa kwa ajili ya kupima ubora wa maji, kupima ubora wa mita na maabara ya kukata mabomba zote zikiwa na lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa maji safi na salama.

  Dkt Kazumba alitoa rai kwa Halmashuri zote nchini kuajiri Mafundi Sanifu na Wahandisi wa Maji kwa ajili ya kuongeza tija katika sekta ya maji.
  Alifafanua kuwa Mafundi Sanifu waliohitajika kwa kipindi cha mwaka 2013 ilikuwa ni 3000 na mwaka 2014 ilifikia 6000 na dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa kila mhandisi mmoja anakuwa na mafundi 5 wa kumsaidia kutekeleza majukumu yake.

  Chuo cha Maji kilianzishwa mwaka 1974 kwa lengo la kuendeleza na kuzalisha wataalamu wa sekta ya maji kupitia mafunzo, ushauri na tafiti mbalimbali.
  Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt.Shija Kazumba akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu mkakati wa Chuo kuhakikisha Tanzania inakuwa na Mafundi Sanifu wa kutosha katika sekta ya maji ili kuendana na kasi ya Serikali kufikisha huduma ya maji kwa wananchi wote. Kulia ni Afisa Habari na Masoko wa chuo hicho Bw. George Karumuna.
  Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Chuo cha Maji na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.


  0 0

   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akizungumza na Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, wakati Kamishna huyo alipomtembelea ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
   Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga (kushoto), akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati Kamishna huyo alipomtembelea Masauni ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kupambana na dawa za kulenya nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimkaribisha Kamishna wa Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu kupambana na dawa za kulevya nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

  0 0

  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia Mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati  kuhitimisha  ziara ya mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Babati wakati alipowasili kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati kuhutubia mkutano wa hadhara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wazee  wakati alipoingia kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati,  kuhutubia mkutano wa hadhara Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya wananchi wa Babati wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa wakati  alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Kwaraa mjini Babati, Februari, 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa serikali na Halmashauri za mkoa wa Manyara kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
  Baadhi ya  watumishi wa serikali na Halmashauri za mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao kwenye viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Februari 22, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange au Deal (28), amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia dawa za kulevya.

  Mrembo huyo anayeishi Makongo Juu ambaye alikuwa akitumia muda mwingi kujiziba sura yake kwa mtandio na miwani ya Giza alisomewa tuhuma zake mbele ya Hakimu Mkazi Willbard Mashauri. Hata hivyo, ameachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowekwa na mahakama.

  Mahakama ilimtaka Masogange kuwekwa dhamana ya milioni kumi hali kadhalika na wadhamini wake wawili nao walitakiwa kuwekwa kiasi hicho cha fedha.

  Aidha mahakama imemuamuru kutosafiri nje ya Dar ea Salaam bila ya kupata kibali cha Mahakama.Akisoma hati ya mashtaka, wakili wa serikali, Constantine Kakula amedai kuwa kati ya Februari 7 na 14 mwaka huu katika Eneo na Wilaya isiyojulikana lakini ndani ya jiji la Dar es salaam, Masogange alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
  Katika hatua ya pili, Mshtakiwa Masogange siku na mahali pasipojulikana alitumia dawa za kulevya aina ya OXazempam.

  Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.Masogange amekana kujihusisha na tuhuma hizo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 21, mwaka huu.
   Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange au Deal (28) akielekea kwenye chumba cha Mahakama ya  Hakimu Mkazi  Kisutu ambapo alisomewa Mashtaka ya Matumizi ya Dawa za Kulevya.
    Mrembo anayepamba video za wasanii nchini, Agnes Gerald Waya maarufu kama Masogange au Deal (28)akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo jijini Dar es Salaam.
  Agnes Masogange akitoka katika Mahakama hiyo akiwa na Wakili wake, Nictagon Itege baada ya kutimiza masharti ya dhamana leo ijini Dar es Salaam.
   Agnes Masogange akiondoka katika Mahakamani


  0 0

   Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Italia nchini Tanzania,  Reborto Mengoni kuhusu namna ambavyo wawekezaji wa Italia  wanavyoweza kuja  nchini Tanzania kuchangamkia fursa   za Utalii kwa  kujenga hoteli za hadhi ya nyota tano katika mwambao wa Bahari ya Hindi walipokutana leo  jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mwambata anayeshughulikia masuala ya utamaduni, Bi. Valeria La Scala ( wa kwanza kulia) na Mwambata anayeshughulikia masuala ya Biashara,  Bi. Michelangela Adamo ( wa pili kulia) ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Balozi wa Italia nchini Tanzania,  Reborto Mengoni ( wa kwanza kulia)  akizungumza na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ( wa kwanza kushoto)  kuhusu namna ambavyo wawekezaji wa  Italia  wanavyoweza kuja   kuchangamkia fursa   za Utalii kwa  kujenga hoteli za hadhi ya  nyota tano katika mwambao wa Bahari ya Hindi walipokutana leo  jijini Dar es Salaam( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
    Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Balozi wa Italia nchini Tanzania,  Reborto Mengoni kuhusu namna ambavyo wawekezaji wa Italia  wanavyoweza kuja  nchini Tanzania kuchangamkia fursa   za Utalii kwa  kujenga hoteli za hadhi ya nyota tano katika mwambao wa Bahari ya Hindi walipokutana leo  jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mwambata anayeshughulikia masuala ya utamaduni, Bi. Valeria La Scala ( wa kwanza kulia) na Mwambata anayeshughulikia masuala ya Biashara,  Bi. Michelangela Adamo ( wa pili kulia) ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
   Msemaji  wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  (TFS) Glory Mziray (kulia) akiwa na Katibu wa Waziri, Ephraimu Mwangomo ( wa pili kulia) wakimsikiliza Balozi wa Italia nchini  Tanzania, Reborto Mengoni  (hayupo pichani) mara baada ya kufanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe kuhusu masuala ya uwekezaji katika sekta ya Utalii kwa  kujenga hoteli za nyota tano katika mwambao wa Bahari ya Hindi walipokutana leo  jijini Dar es Salaam. Wengine ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mambo kale, Dkt.Fabian Kigadi pamoja na Mwambata anayeshughulikia  masuala ya utamaduni, Bi. Valeria La Scala ( wa kwanza kushoto) ( Picha na Lusungu Helela- Maliasili)
  Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Maliasli na Utalii wakiagana na Waambata wa Ubalozi wa Italia  nchini Tanzania walipokutana leo jijini Dar es Salaam.

  0 0

   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kulia mbele) akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kalemie, Kongo kwa ajili  ya kushiriki mkutano  wa kubadilishana data na uzoefu kuhusu mafuta katika Tanganyika uliofanyika hivi karibuni nchini Kongo. Nchi nyingine zilizoshiriki ni pamoja na Burundi, Kongo na  Zambia. Wengine kutoka kushoto ni  Gavana wa Jimbo la  Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala, Waziri wa Migodi na Madini Nchini Zambia, Chris Yaluma na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (kushoto) na Gavana wa Jimbo la  Tanganyika – Kongo, Richard Ngoy Kitangala (kulia) wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa (hayupo pichani) katika mkutano huo.
   Mkurugenzi Msaidizi wa Sheria, Wizara ya Nishati na Madini, Anna Ngowi (kushoto) pamoja na wataalam wengine kutoka Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa katika mkutano huo.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo (katikati) akiweka mchanga kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa Chuo Kikuu cha Mafuta na Gesi katika mji wa Kalemie. Kulia kwake ni Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa.
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kutoka kushoto, mbele) pamoja na viongozi wengine wakishikana mikono kama ishara ya umoja mara baada ya kuzindua ujenzi wa  Chuo Kikuu cha Mafuta na  Gesi katika mji wa Kalemie hivi karibuni .
   Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa tatu kutoka kushoto mbele) na Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo, Profesa Aime Ngoi-Mukena Lusa ( wa sita kutoka kulia mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji  wengine mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa  Chuo Kikuu cha Mafuta na  Gesi katika mji wa Kalemie hivi karibuni .
   Mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Athur Lyatuu (kushoto) akibadilishana mawazo na mmoja wa wajumbe wa mkutano huo.
  Ujumbe kutoka Tanzania ukifuatilia hoja mbalimbali zilizokuwa zinajadiliwa katika mkutano huo.older | 1 | .... | 1148 | 1149 | (Page 1150) | 1151 | 1152 | .... | 1903 | newer