Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1144 | 1145 | (Page 1146) | 1147 | 1148 | .... | 1897 | newer

  0 0


  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wahanga wa Ajali ya kufukiwa na kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa RZ uliopo katika Kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Mkoani Geita iliyotokea tarehe 26 Januari, 2017.

  Aidha, Prof. Muhongo amewataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kuchukua hatua za haraka kusimamia mazoezi ya uokoaji pindi zinapotokea ajali migodini pasipo kusubiri miongozo ya Waziri.

  Pia amewaagiza Makamishna hao kufanya ukaguzi katika migodi mikubwa na midogo katika maeneo nayo na kuongeza kuwa, zoezi hilo la ukaguzi linatakiwa kufanywa haraka.Pia amemtaka Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, kufuta leseni zote za uchimbaji madini ambazo hazifanyi kazi.

  Akizungumzia kuhusu kuwaendeleza wachimbaji wadogo chini, Prof. Muhongo amesema kuwa, Sera na mipango ya Serikali ni kuwandeleza wachimbaji hao na kuhakikisha kuwa, wanatoka katika uchimbaji mdogo kwenda uchimbaji wa Kati.

  Katika hatua nyingine, Prof. Muhongo ameitaka Migodi Mikubwa yote nchini kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam na kueleza kuwa, migodi hiyo imepewa wiki 6 iwe imejiandikisha katika soko hilo.

  Pia Prof. Muhongo amemshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkoa wa Geita, Viongozi wa Wizara, Wachimbaji na kampuni zote zilizoshiriki zoezi la uokoaji na kufanikiwa kuokolewa kwa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi.
  Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya Wahanga wa ajali ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ, Mkoani Geita. Prof. Muhongo alifika mgodini hapo wakati wa ziara yake mkoani humo.
  Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati) akimuongoza Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi wa dhahabu wa RZ.
  Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
  Mkuu wa MKoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na kifusi.
  Wachimbaji wadogo wakimwonesha Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake namna walivyookolewa baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa dhahabu wa RZ, uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita.
  Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi akiwaongoza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi ambako wachimbaji 15 walifukiwa na kifusi na kuokolewa wote wakiwa hai.

  0 0


  Na Eliphace Marwa, Dar es salaam

  Chama cha Wakandarasi Tanzania kimeiomba Serikali kuwashirikisha katika zabuni za ujenzi wa miradi mbalimbali ya umma Wakandarasi wazawa.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Chama hicho, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki wakati mkutano na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mipango mbalimbali ya Serikali katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

  Alisema kuwa wanaiomba Serikali ya Awamu ya Tano kuwashirikisha wakandarasi wa kitanzania , wakimemo wakandarasi wa madaraja yote ili waweze kujijengea kitaalamu katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali mkoani Dodoma.

  Mhandisi Mwakyambiki aliongeza kua hatua hiyo itasaidia kuongeza ajira kwa vijana na Kampuni za kitanzania katika shughuli za ujenzi hapa nchini.

  Aidha, Chama hiyo kimeipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuwa mstari wa mbele katika kutekeleza mikakati na kusimamia sekta ya ujenzi hapa nchini.

  Aidha Mwakyambiki aliongeza kuwa kutokana na uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhamia Dodoma ni vema wakandarasi wa ndani wakapewa fursa ya kushiriki katika kandarasi mbalimbali ambazo serikali inatarajia kuzifanya huko Dodoma.

  Kwa upande Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi John Bura alimshukuru Rais Magufuli na Serikali yake kwa kuitikia wito wa wakandarasi kwa kuwatengea miradi michache ambayo ilikwisha tangazwa.

  Aliwataka wakandarasi kuunda umoja kwa ajili ya kuitekeleza kwa weledi ili kuongeza imani kwa Serikali. 
  Mwenyekiti wa Chama Cha Wakandarasi Tanzania, Mhandisi Lawrence Mwakyambiki akisistiza jambo kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam kuhusu Serikali kuwapa kipaumbele wakandarasi wa ndani katika miradi ya ujenzi.

  0 0


  MAMLAKA ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi (EPZA)na Kiwanda kilichopo ndani ya Mamlaka hiyo ya Tooku kinachojishughulisha na utengenezaji wa nguo zimetozwa faini ya kiasi cha sh.mill 30 kwa kosa la kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 

  Ambapo EPZA inapaswa kulipa faini ya Mill20 huku Kampuni ya TOOKU kulipa faini ya mill 10 na kuhakikisha zinarekebisha mifumo yake ya kupitisha maji taka ipasavyo na kuunganisha katika Mfumo maalum wa Dawasco . 

  Akizungumza Jijini Dar es Salaam ,Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina wakati wa ziara yake ya kukagua baadhi ya viwanda nchini,kuangalia hali ya mazingira ambapo aliambatana na Maofisa mbalimbali kutoka 

  Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC),alisema faini hizo zinapaswa kulipwa ndani ya siku 14.Mpina alisema anahasira zaidi na taasisi za serikali zisizofata sheria ya mazingira na kutililisha maji machafu katika makazi ya watu. 

  "Nina hasira na taasisi hizi za serikali kwani serikali yenyewe haiwezi kugeuka kupeleka sumu kwa wananchi wake, ambao muda wote inawazuia na kuwakinga wananchi hao hao wasipatwe na 
  madhara,"alisema 

  Alisema wanapokuta na taasisi ya serikali zinazokiuka miiko iliyoweka katika utunzwaji wa mazingira ni lazma wawapige faini kubwa zaidi kuliko taasisi binafsi ili kuweza kuwa mfano mkubwa kwa jamii.Mpina alisema Mamlaka hiyo ya Uendelezaji Kanda Maalum za Kiuchumi EAPZ ilisema kuwa mfumo wao wa kuyabeba maji taka na kuyapeleka katika mfumo rasmi wa maji taka wa Dawasco umeharibika lakini hawakuweza kuwaandikia NEMC barua ya taarifa juu ya matatizo hayo. 

  "Nawataka EPZA ndani ya siku saba mfumo wa kupitishia maji taka wa EPZA uwe umetengenezwa na kukamilika hivyo kuzuia maji taka yanayotoka kutotoka tena kwa sababu yatakuwa yanaingia rasmi katika mfumo wa Dawasco,"alisema.Aidha alisema kwa upande wa Kampuni ya TOOKU yenye inatakiwa kufanya marekebisho makubwa katika mitambo yake ya kutibu maji taka kwani inaonekana kuwa na kasoro. 

  "Sheria ya mazingira inakataza utililishaji huu wa maji taka katika mazingira kwani maji yanayotililishwa yanakuwa na kemikali mbalimbali ambazo zinadhuru wanyama,mimea na maisha ya binadamu,kwahiyo viwanda vyetu nchini hatuviruhusu kutililisha maji taka nje kwenda kwenye mazingira na endapo yatatililishwa yanapaswa kupimwa,kuhakikiwa na kudhibitishwa kuwa hayana madhara,"alisema . 

  Aidha alisema katika ukaguzi walioufanya mamlaka hiyo na kiwanda hicho hakikuweza kuonyeshwa ubora wa maji yanayotililika kuja katika mazingira ya watu kwani maji yanayotililika kutoka katika Mamlaka hiyo na Kiwanda hicho cha yanatoka na rangi. 

  Kwa Upande wake Mratibu wa Kanda ya Mashariki NEMC , Jafari Chimgege alisema katika kiwanda cha Tooku kimekuwa mbaya wa kutibu maji taka na kusababisha kumwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu ambapo ni kinyume cha sheria. 

  "Viwanda vinafahamu kuwa vinapomwaga maji machafu katika mazingira bila kuyatibu au kuyapeleka katika mifumo rasmi ni kosa,kiwanda hiki cha TOOKU na Mamlaka hii ya EAPZ vimefanya kosa,"amesema.Chimgege amesema maji yanayotilishwa na viwanda mbalimbali 
  katika mito ni makosa kwani maji hayo yanakuwa na madhara kwa wananchi. 

  Nae Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Muongozo,James Ngoitanile alisema wananchi wake wamekuwa wakipata shida na maji hayo wakati mwingine yanawaletea madhara.Amesema wapo watu wanaolima michicha ambao wanatumia maji ya mto huo kumwagilia hivyo yanavyochanganyika na maji hayo yanasababisha watu kula mbogamboga zenye kemikali.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kituo cha uwekezaji cha EPZA, kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kituo cha uwekezaji cha EPZA mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kituo hicho kilichopo Ubungo Jijini Dar es salaam. 
  . Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia suruali aina ya Jinsi zinazozalishwa katika kituo cha uwekezaji cha EPZA wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mapema hii leo Jijini Dar es salaam. 
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia mfereji wa maji machafu yanayotiririshwa na kituo hicho ambayo yamekuwa ni kero kwa wananchi.

  0 0


  Fundi wa kuchoma vyuma kwa kutumia teknolojia ya gesi akiendelea na zoezi la kuchoma kufuli ya lango la ghala lililofichwa kwenye hoteli ya Butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda eneo la Kariakoo. Ghala hilo limekutwa na shehena kubwa ya kazi haramu za muziki na filamu.
  Mmiliki wa ghala lilolokutwa chini ya hoteli ya Butterfly Phili Ulaya akijaribu kujitetea mbele za Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye mara baada ya zoezi la kuvunja kufuli ya lango la ghala hilo kukamilika. Waziri Nape kwa kushirikiana na viongozi wa taasisi zinazosimamia maslahi ya kazi za ubunifu wamefanya operesheni iliyofanikisha kukamtwa kwa shehema kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki kwenye ghala la bwana Ulaya liliofichwa chini ya hoteli ya Butterfly.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akimfafanulia sheria mbalimbali ambazo mfanyabishara wa kazi za filamu na muziki anastahiki kuzifuata kabla ya kuanza kufanya biashara hiyo. Anaemsikiliaza Mheshimiwa Nape ni mmiliki wa ghala ambalo shehena kubwa ya kazi haramu za filamu na muziki zimekamatwa wakati wa operesheni iliyofanyika leo eneo la Kariakoo jijini Dar-es-Salaam.
   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akikagua rundo la filamu zilizokamatwa kwenye opersheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Kwenye operesheni hiyo shehena kubwa ya kazi za filamu na muziki imekamatwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya Butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo jijini Dar-es-salaam.

   Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisikiliza maelezo kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Filamu wa Bodi ya Filamu Tanzania Wilhad Tairo wakati wa operesheni ya kutokomeza kazi haramu za filamu na muziki nchini. Operesheni hiyo imefanikisha kukamatwa kwa shehena kubwa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ghala lililofichwa chini ya hoteli ya butterfly iliyoko mtaa wa Muhonda, Kariakoo.

  Pichani ni jengo la hoteli ya butterfly iliyopo mtaa wa Muhonda, Kariakoo ambalo ghala lenye shehena kubwa ya kazi za haramu za filamu na muziki

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao .
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, alipowasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo, Februari 18, 2017, kwa ajili ya mazungumzo baina yao .
  Wakienda eneo la kufanyia mazungumzo 
  Wakiwasili eneo la mazungumzo Ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM. 
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akizungumza na Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Feb 18, 2017. (Picha zote na Bashir Nkoromo) .  0 0

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo alikuwa akipatiwa matibabu mpaka aliporuhusiwa kurejea nyumbani kwake mara baada ya kupata nafuu.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuombea Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumaliza mazungumzo yao nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam.
   Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya akimsindikiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye alifika nyumbani kwake Upanga kwa ajili ya  kumjulia hali.  
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya mara baada ya kumjulia hali nyumbani kwake Upanga jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

  0 0

  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akikagua gwaride wakati wa sherehe za Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akitunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika hati ya Kamisheni muda mfupi kabla ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwasili Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.

  Kikundi cha ngoma cha JWTZ kikitumbuiza kwa ngoma ya Chaso ya Pemba wakati Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipotunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.
  Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa rais Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Waziri wa ulinzi nja Jeshi la Kujenga taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Juma Kijazi na viongozi wengine katika picha ya pamoja baada ya Kutunuku Kamisheni kwa Maafisa wapya wa Jeshi la Ulinzi la Tanzania na kadhaa kutoka nchi marafiki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Jumamosi Februari 18, 2017.PICHA NA IKULU

  0 0


  0 0

  Katika Mkoa wa Simiyu kumefanyika Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfumo wa Bima ya afya nchini (NHIF), Mkutano ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo Nchini Anne Makinda ambaye ni Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Mkuu wa mkoa huo Antony Mtaka.

  Akongea wakati wa Mkutano huo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko huo, alionekana kukerwa na uwepo wa baadhi ya watoa huduma kutoka katika zahanati, vituo vya afya pamoja na hospitali nchini kutoa lugha chafu kwa wagonjwa na kusababisha kuwepo kwa malalamiko mengi juu ya mfuko huo.

  Mbali na hilo Mwenyekiti huyo alikerwa kwa baadhi ya watoa huduma wa serikali pamoja na watu binafsi, kukidhiri kwa udanganyifu wa madai kwenda NHIF, ambapo alisema wengi wao wamekuwa wakipeleka madai hewa katika mfuko huo kwa ajili ya kulipwa.

  " hii ni changamoto kubwa sana kwa watoa huduma wetu, wamekuwa wakituletea madai ambayo siyo halisi, na kuashiria kuwepo kwa vitendo vya rushwa kwa baadhi yao, jambo hili limekuwa kero kubwa sana mfuko na, hivyo ni lazima wachukuliwe katua kuanzia ngazi za halmshauri na mikoa" Alisema

  Mkutano huo umeshirikisha wadau wengi wakiwemo viongozi wa kisiasa, wabunge, Madiwani, wenyeviti wa halmashauri, wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wahuduma wa afya, watoa huduma binasfi, viongozi wa dini, walimu, watumishi wa serikali kutoka idara mbalimbali, pamoja na wananchi.

  Wakichangia mada mbalimbali wadau wengi wamelalamikia changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye sehemu za kutolea huduma, licha ya kuchangia mfuko huo kila mwaka, lucha chafu kutoka kwa baadhi ya wahudumu wa afya.

  " tumekuwa tukitumia muda wetu na wananchi wanatusikiliza na kutuunga mkono kuchangia mfuko huu, lakini malalamiko yamekuwa mengi sana, ukosefu wa dawa pamoja na lugha chafu, hapo ndipo na sisi tunavunjika moyo na hali ya kuendelea kuchangia maana kila tukienda kuhamasisha tunakumbana na maswali hayo na tunakosa majibu" Alisema Makondeko

  Mbali na hilo wadau hao walilalamikia mamlaka ya dawa nchini (Msd) kwa kushindwa kutoa dawa za kutosha kwa vituo mbalimbali vya afya nchini, ambapo baadhi waliiomba serikali kuifuta Msd, na kuunda chombo kipya kutokana na kushindwa kazi, huku halmashauri zikiomba kuruhusiwa kununua dawa moja kwa moja bila ya kupitia msd.
  Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda, akiongea wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa Mfuko huo Mkoa wa Simiyu, mkutano uliofanyika Mjini Bariadi katika Kanisa Katoliki Bariadi.
  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akifungua Mkutano mkuu wa wadau wa mfuko wa Bima ya afya (NHIF) uliofanyika hivi karibuni jini Bariadi katika kanisa katoliki, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa alitoa onyo kali kwa watoa huduma katika mkoa huo binafsi pamoja na serikali kuacha mara moja tabia ya kupeleka madai yasiyo halisi NHIF kwa ajili ya malipo.
  Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.
  Wadau mbalimbali katika Mkutano huo.


  Katibu wa Itikadi na uenezi chama cha mapinduzi mkoa wa Simiyu (CCM) Geremia Makondeko akichangia mada wakati wa Mkutano mkuu wa wadau wa mfuko wa bima ya afya mkoani humo, mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa kanisa katoliki mjini Bariadi.
  Diwani kutoka wilaya ya Meatu akichangia mada.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Nchini (NHIF) Bernard Konga, akitoa taarifa ya mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa wadau wa NHIF mkoa wa Simiyu, ulifanyika leo katika kanisa katoliki Mjini Bariadi.
  Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) mkoa wa Simiyu, Amani Emmanuel akitoa taarifa ya mfuko huo ya mkoa wa Simiyu, wakati wa Mkutano Mkuu wa wadau wa NHIF mkoani humo, mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa kanisa katoliki mjini Bariadi.
  Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Bima ya afya Nchini (NHIF) Bernard Konga, akitoa taarifa ya mfuko huo, wakati wa mkutano mkuu wa wadau wa NHIF mkoa wa Simiyu, ulifanyika leo katika kanisa katoliki Mjini Bariadi.

  Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.

  Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.

  Wadau wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo.
  Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa Bima ya afya Tanzania (NHIF) Anna Makinda (kushoto) akiwa katika Mkutano wa wadau wa mfumo wa bima ya afya Mkoani Simiyu, (kulia) ni Mkuu wa Mkoa huo Antony Mtaka.
  Wadau mbalimbali walioshiriki wakiwemo viongozi wa Dini, (wa kwanza kushoto) Shekhe wa mkoa wa Simiyu Mohamud Kalokola.

  0 0


  0 0

  Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
  Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Nile “Nile Day” yatakayofanyika wiki ijayo  (Februari, 22), jijini Dar es Salaam.

  Maadhimisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa kushirikiana na taasisi inayosimamia shughuli za wanachama wa Bonde la Mto Nile-Nile Basin Initiative (NBI).

  Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mha. Gerson Lwenge ameyasema hayo hivi karibuni alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii kuhusu maadhimisho hayo.

  Mha. Lwenge amesema kuwa maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka miongoni mwa nchi wanachama 10 zilizo katika bonde la mto huo; ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan, Sudan ya Kusini na Misri, ambapo kwa mwaka huu siku hiyo inasherekewa nchini Tanzania.

  “Lengo la Siku ya Nile ni kukuza uelewa kwa watu wote kuhusu umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zote wanachama, masuala yanayotekelezwa na faida inayopatikana kutokana na matumizi bora ya rasilimali za Bonde la Mto Nile,” alisema Mha. Lwenge.

  Amefafanua kuwa maadhimisho hayo yatasaidia kufahamu zaidi kuhusu umuhimu wa mto huo katika kutupatia chakula cha uhakika, maji, nishati ya umeme na faida nyingi kiuchumi pamoja na kubadilishana mawazo ya jinsi ya kulinda na kutumia rasilimali za mto huo kwa pamoja na kwa usawa na uendelevu kwa ajili ya kizazi cha leo na vizazi vijavyo.

  Mha. Lwenge ameongeza kuwa maadhimisho hayo yataambatana na maandamano kutoka viwanja vya Mnazi Mmoja mpaka Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, upandaji wa miti, maonesho ya vitu mbalimbali vinavyohusu Sekta za Maji na Umwagiliaji, burudani za kiutamaduni, pamoja na za watoto wa shule za msingi na sekondari.

  Aidha, Waziri Lwenge amewataja washiriki wa maadhimisho hayo kuwa ni mawaziri wanaohusika na maji kutoka nchi wanachama, mabalozi, wawakilishi kutoka NBI, wabunge, washirika wa maendeleo, wataalamu, wanafunzi wa vyuo, sekondari na shule za msingi, taasisi binafsi, vyombo vya habari pamoja na umma kwa ujumla.

  NBI ilianzishwa rasmi mwaka 1999, jijini Dar es Salaam, ambapo nchi wanachama waliungana na kukubaliana kuanzisha umoja wa ushirikiano katika kusimamia na kuendeleza rasilimali za Bonde la Mto Nile.


  0 0


  0 0

  Na Ismail Ngayonga, MAELEZO, Mwanza 
  MAAFISA Habari na Mawasiliano katika sekretarieti za Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini  wametakiwa kujitokeza na kuwajibika kikamilifu ili kuwawezesha waaajiri wao kutambua wajibu na majukumu yao ya msingi katika kutangaza shughuli na mafanikio ya Serikali katika maeneo yao ya kazi. 

  Rai hiyo  imetolewa leo Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali,  Dkt. Hassan  Abbas wakati alipokuwa akizungumza na Maafisa Habari na TEHAMA katika mafunzo elekezi ya tovuti yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). 

  Kwa Mujibu wa Dkt. Abbas alisema katika ulimwengu wa sasa suala la teknolojia ni jambo lisiloupekika, hivyo ni wajibu wa Afisa Habari kutmia nyenzo za kisasa za mawasiliano ikiwemo tovuti ili kuhakikisha kuwa wananchi na wadau wa maendeleo wanapata taarifa sahihi na zilizozingatia wakati. 

  “Zipo taarifa za miradi mbalimbali ambayo Serikali imeifanya, pamoja na taarifa za bajeti za halmashauri ambazo wananchi watapenda kuzifahamu, hivyo ni wajibu wenu Maafisa Habari kuweka taarifa hizi” alisema Dkt. Abbas. 

  Aidha aliongeza kuwa ni wajibu wa kila Afisa Habari aliyopo katika Mkoa na Halmashauri nchini aweze kujiwekea malengo ya utekelezaji ili aweze kujitafakari kwa kuwa kuwa kupitia malengo hayo ataweza kutatua changamoto mbalimbali zinazomkabili katika eneo lake la kazi. 

  Akifafanua zaidi Dkt Abbas alisema ili kufikia malengo hayo Maafisa HabariHabari hawana budi  kutengeneza mtandao wa mawasiliano baina yao ili kuwawezesha kutatua changamoto mbalimbali  zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi. 

  Dkt. Abbas alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili maafisa Habari katika maeneo yo ya kazi, ambapo baadhi ya changamoto hizo zimeanza kupatiwa ufumbuzi ikiwemo suala la miongozo ya majukumu ya Afisa Habari na Mawasiliano.

  Kwa Upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebbeca Kwandu alisema katika mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Maafisa Habari na TEHAMA yatasaidia kwa kiasi kikubwa kujibu hoja na kero mbalimbali za wananchi ambazo zimekuwa zikiwasilishwa mara kwa mara katika halmashauri mbalimbali nchini.

  “Afisa Habari atakuwa ndiye mhusika wa karibu zaidi  atayekuwa akiweka maudhui ya tovti hizi lakini pia Afisa TEHAMA yeye atawajibika kwa kiasi kikubwa katika eneo la la ufundii” alisema Kwandu. 

  Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, John Mlyambato alisema baadhi ya Mikoa nchini ikiwemo Mkoa wa Tabora kwa kipindi umekuwa hauna watumishi wa kada ya Maafisa Habari hatua inayosababisha taarifa mbalimbali za Serikali kutowafikia kuwafikia wananchi. 
  Mkurugenzi wa Habari na  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti katika Mikoa na Halmashauri za Wilaya nchini yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao. Mafunzo hayo yalianza tarehe 9-20 Februari, 2017, kulia ni Mkuuwa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais TAMISEMI, Rebecca Kwandu.

  0 0

  Mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege Tanzania ATCL LADISLAUS MATINDI, amerizishwa na matengenezo ya uwanja wa ndege ulipo songea mkoani Ruvuma, kwa ajili ya kuanza kutoa huduma za safari toka SONGEA hadi DAE ES SALAAM,


  0 0

  Serikali imesema itatoa eneo linalomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Buhemba, Mkoani Mara kwa wachimbaji Wadogo wa Madini baada ya kufanyika kwa tathmini  na taratibu za kumilikishwa eneo ili wachimbaji hao wafanye shughuli hizo kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu ikiwemo kulipa kodi.

  Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo leo tarehe 18 Februari,2017, wakati wa ziara yake katika mgodi huo ili kuangalia shughuli za uokoaji zinazoendelea katika mgodi huo, kufuatia  ajali ya kufukiwa na kifusi kwa Wachimbaji 18  iliyotokea tarehe 13 Februari,2017, ambapo wachimbaji 13 waliokolewa siku hiyo hiyo

  Prof. Muhongo  amesema kuwa, wachimbaji hao hawakuwa na leseni wala vibali halali vilivyotolewa kwao  kufanya shughuli za utafutaji dhahabu na kwamba eneo hilo linamilikiwa kisheria na STAMICO kwa leseni  PL N0. 7132/2011, na kuongeza kuwa, wachimbaji hao walivamia eneo hilo ambapo ni kosa kisheria na wanatambulika kama wavamizi.

  Ameongeza kuwa, shughuli za uchimbaji katika eneo hilo zilifungwa tangu mwaka 1971 ambapo awali eneo hilo lilikuwa chini ya wakoloni kabla ya kuwa chini ya uangalizi wa Jeshi  la Kujenga Taifa (JKT), Kampuni ya Meremeta na baadaye kuwa chini ya umiliki wa STAMICO.

  Aidha, amezuia shughuli zote za uchimbaji kufanyika katika eneo hilo na kusema kinachofanyika sasa ni kuutafuta mwili wa mchimbaji mmoja ambaye bado haujatolewa. ''Hadi sasa wachimbaji 15 wamekwisha okolewa, bahati mbaya wawili walitolewa wamefariki na sasa tuendelee na zoezi la kutafuta mwili uliobaki,"ameongeza Prof. Muhongo.

  Pia Prof Muhongo amewshauri wachimbaji hao kujiunga katika vikundi na kusajili vikundi hivyo ili kuwezesha shughuli zao kufanyika kwa kuzingatia taratibu za uchimbaji. "Jiungeni katika vikundi , lakini ni marufuku kwa familia moja kuwa na kikundi,"amesisitiza Prof. Muhongo

  Kwa upande wake Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Viktori Mashariki Mhandisi Juma Sementa amesema kuwa, tayari Kanda hiyo imeshatoa maeneo yapatayo 35 kwa wachimbaji wadogo katika eneo la Lwabasi, mkoani humo na kueleza kuwa, leseni zote katika eneo hilo zinamilikiwa na wachimbaji  wadogo na hivyo kuwataka kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia usalama na ikiwemo kulipa kodi.
   Mmoja wa wachimbaji waliokolewa katika ajali ya kifusi akimweleza Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) jinsi ajali hiyo ya kufikiwa na kifusi wachimbaji 18 ilivyotokea. Katikakti  anayesikiliza ni Kaimu Kamishna wa Madini Mhandisi Ally Samaje.
   Mmoja wa wachimbaji wadogo akishuka chini ya shimo la kuingilia katika mgodi kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji kufuatia ajali ya kufukiwa na kifusi wachimbaji 18 katika eneo la Buhemba mkoani Mara.
   Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgodi wa  North Mara (ACACIA)  ambao walishiriki katika zoezi la uokoaji wa wachimbaji wadogo kwa kutoa msaada wa mashine ya kuvuta maji  na tope ili kuwezesha zoezi la ufukuaji kuendelea
   Sehemu ya Wachimbaji wakifuatilia mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo wakati wa ziara yake katika mgodi wa Buhemba  unaomilikiwa na STAMICO.
   Mmoja wa wachimbaji wadogo anayeshiriki zoezi la uokoaji katika eneo la Buhemba akimweleza Waziri wa Nishati na Madini , Profesa Sospeter Muhongo na wananchi waliokuwa eneo hilo kuhusu hali ilivyo ndani ya mgodi huo. 
  Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akiongea na wachimbaji wadogo katika eneo la Buhemba ambapo ajali ya wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi tarehe 13 Februari,2017.

  0 0

  Jumamosi Februari 18,2017,kumefanyika kikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017. 

  Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga ambapo mamia ya wachungaji,viongozi na waumini wa kanisa hilo dayosisi ya Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mheshimiwa Josephine Matiro. 

  Mnenaji mkuu katika kikao hicho alikuwa Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala. 

  Akizungumza wakati wa kikao hicho Askofu Dkt. Makala aliwapongeza viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakiongozwa na Katibu mkuu wa kanisa hilo,Mchungaji Jakobo Mapambano kwa kuandaa sherehe ya kumuaga Askofu Nkola ambaye amekuwa askofu wa Kanisa hilo tangu tarehe 24.10.1993. 

  Askofu Makala alitumia fursa hiyo kuwaonya waumini wa kanisa hilo kutokuwa na tamaa ya madaraka ya uongozi kwa nafasi itakayoachwa na Askofu Nkola hili kuepuka vurugu zinazoweza kujitokeza na kusisitiza kuwa ni vyema kiongozi atakayeziba nafasi hiyo apatikane kwa utaratibu unaotakiwa.

  Akizungumza wakati wa kufungua kikao hicho,mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa dini kuongeza nguvu katika kueneza neno la mungu kwani watu wengi katika mkoa wa Shinyanga bado hawajamjua vyema mungu,wengi wao hawana dini.

  Katika hatua nyingine Matiro aliwaomba viongozi wa dini kuiunga mkono serikali katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhubiri watu waachane na vitendo.Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde,alikuwepo katika kikao hicho…Ametuletea picha 50 za matukio yaliyojiri katika kikao hicho…Tazama hapa chini.
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga wakati akiwasili katika ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga kuhudhuria kikao chakikao cha kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt. John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017 .Kulia ni Makamu wa Askofu Dayosisi ya Shinyanga mchungaji Aaron Malyuta
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasalimia viongozi wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga akisalimiana na wachungaji wa kanisa la AICT
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala 
  Ndani ya ukumbi wa NSSF: Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala baada ya kuwasili ukumbini.
  Maombi yakiendelea baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini
  Wajumbe wa kikao hicho wakisali ukumbini
  Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano akitambulisha viongozi na wageni mbalimbali waliohudhuria kikao hichoAskofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga, Dr. John Nkola.Hakuwepo wakati wa Kikao cha leo(Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
  Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano alisema kikao hicho ni hatua ya awali ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola ambaye anastaafu uaskofu mwezi Agosti mwaka 2017.
  mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala wakimsikiliza mchungaji Mapambano
  Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano akiwapungia mkono wajumbe wa kikao hicho kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga
  Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akizungumza wakati wa kuthibitisha tamko la kuwakaribisha wajumbe na wageni katika kikao hicho
  Wajumbe wakiwa ukumbini
  Kwaya AICT Shinyanga wakiimba ukumbini
  Kwaya ya AICT Shinyanga ikiimba
  Wajumbe wakiwa ukumbini
  wajumbe wa kikao hicho wakiwa wamesimama
  Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akizungumza ukumbini


  Kikao kinaendelea


  Wajumbe wakiwa ukumbini


  Kikao kinaendelea
  Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola,Erasto Kwilasa ambapo aliwaomba viongozi na waumini wa kanisa hilo kushirikiana naye katika kufanikisha mkutano huo na sherehe hizo
  Kwaya AICT Kambarage ikiimba
  Viongozi wa kamati ya Maandalizi ya Mkutano Mkuu na sherehe za kumuaga Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga Dkt.John Kanoni Nkola wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
  Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano na mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro wakiwa wamesimama ukumbini
  Viongozi wa Kanisa wakiwa ukumbini
  Maombi yakiendelea kabla ya Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala
  Maombi yanaendelea
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo aliwataka waumini kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga kuyaenzi mambo mazuri yote yaliyofanywa na Askofu Dkt. John Nkola
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala pia aliwahamasisha waumini wa kanisa hilo kudumisha upendo
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akizungumza ukumbini
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akiendelea kuzungumza
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akitoa neno ukumbini
  Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala akiwa amesimama baada ya kumaliza kuzungumza
  Meza kuu wakiwa wamesimama,wa kwanza kushoto ni mchungaji Samwel Njile kutoka Kanisa la AICT Pastoreti ya Masumbwe mkoani Geita
  Kikao kinaendelea
  Wajumbe wa kikao wakiwa ukumbini
  Maombi yanaendelea
  Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akizungumza ukumbini
  Mchungaji Samwel Njile kutoka Kanisa la AICT Pastoreti ya Masumbwe mkoani Geita akiteta jambo na Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano
  Wajumbe wa kikao 
  Makamu wa Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Aaron Malyuta akimkaribisha mgeni rasmi,mkuu wa wilaya ya Shinyanga ili azungumze na wajumbe wa kikao hicho
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini ambapo aliwapongeza waumini wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga kuandaa sherehe maalum kumuaga Askofu Dkt. Nkola
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza ukumbini
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza umuhimu wa kufikisha neno la mungu katika maeneo mengi zaidi ili wananchi wawe na hofu ya mungu
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akisisitiza jambo
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiendelea kuzungumza
  Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishikana mkono na mchungaji Mapambano baada ya kumaliza kuzungumza
  Kushoto ni Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano,katikati ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga ,Josephine Matiro na Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala wakiwa ukumbini
  Katibu mkuu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Shinyanga,Mchungaji Jakobo Mapambano akimsindikiza Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria,Dkt. Emmanuel Joseph Makala kutoka ukumbini baada ya kikao hicho kufunguliwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.

  Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

  0 0

   Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.
   Kada wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari - MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini.Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

  0 0

  Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya BIMA ya UAP Raymond Komanga.
  KAMPUNIya Bima ya UAP tawi la Mwanza imeamua kuchukuwa jukumu la kuosha magari ya wateja wao wote wa Mwanza bure.


  Zoezi hilo limeanza jana Jumamosi tarehe 18 na litadumu kwa muda wa siku mbili hadi leo Jumapili tarehe 19 February saa kumi na mbili jioni.  TMS Car Wash au kwa Makaptura ndo eneo ambalo limepewa dhamana ya kuosha magari ya wateja walio mkoani Mwanza, hawa jamaa wakipatikana ndani ya eneo la uwekezaji la Rock City Mall Kirumba.  Raymond Komanga ambaye ni Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya BIMA ya UAP anasema kuwa lengo la kufanya zoezi hili ni kuwashukuru wateja wao wa Mwanza kwa ushirikiano wao kibiashara kwa takribani miaka mitatu tangu tawi lilipofunguliwa.


  BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
  Usafi Zaidi kwa mchuma wako mpaka ung'are kwa hisani ya Kampuni ya BIMA ya UAP.

  Wadau wa Kampuni ya BIMA ya UAP pamoja na wadau wa kituo cha uoshaji magari cha TMS kikazi Zaidi.

  Mkuu wa Masoko wa Kampuni ya BIMA ya UAP Raymond Komanga akizungumza nasi.
  "UAP ambayo ni kampuni yenye mtaji kubwa kuliko zote za Bima Tanzania in
  wahakikishia watanzania kuwa wana uwezo wa kulipa madai ya wateja kwa haraka Zaidi" Alisema Komanga.


   "Tangu kuingia sokoni miaka mitatu na nusu iliyopita tumeweza kupanda hadi nafasi ya nne kati ya makampuni ya bima 31 yaliyoko Tanzania"  Pia tumefungua matawi saba nje ya Dar es salaam na Mwanza ikiwa na tawi mojawapo katika barabaraya Pamba.  TMS Car Wash au kwa Makaptura ndo eneo ambalo limepewa dhamana ya kuosha magari ya wateja walio mkoani Mwanza, hawa jamaa wakipatikana ndani ya eneo la uwekezaji la Rock City Mall Kirumba.BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
  Mmoja wa mabalozi wa Masoko wa Kampuni ya BIMA ya UAP akitoa darasa kwa wamiliki wa magari waliofika mahala hapa kwaajili ya kuoshewa magari yao.
  Ze Muonekano na selfie.
  Eneo la huduma.
  UAP na wewe.

  TMS Car Wash Mwanza.


  0 0


  Benny Mwaipaja, WFM, Kyela

  UJENZI wa meli mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi wilayani Kyela Mkoani Mbeya, MV Njombe na MV Ruvuma, umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98 na kwamba meli hizo zinatarajiwa kufanyiwa majaribio Ziwa Nyasa, mwishoni mwa mwezi Februari na kukabidhiwa rasmi Serikalini mwezi Machi, 2017

  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro MarineTransport Ltd ya Jijini Mwanza, inayounda meli hizo, Mhandisi Saleh Songoro, amesema hayo wakati ujumbe wa Serikali ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizaya ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo ukiwa katika zaira ya kukagua hali ya biashara mipakani mkoani Mbeya.

  Amesema kuwa kukamilika kwa meli hizo mbili za mizigo za kisasa zenye uwezo wa kubeba tani elfu moja (1,000) za mizigo kila moja na kugharimu shilingi bilioni 11, kutaiwezesha Kampuni hiyo kuanza kuunda meli nyingine ya tatu itakayokuwa na uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 200 za mizigo.

  Pamoja na meli hizo, Mhandisi Songoro amesema kuwa mradi huo pia umewezesha kujengwa kwa cherezo cha kwanza na cha pekee kitakacho iwezesha Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA katika uundaji wa meli na kuzifanyia matengenezo meli nyingine za ndani na nje ya nchi zikiwemo Malawi na Msumbiji.

  Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Bandari ya Itungi, Bw. Ajuaye Msese, amesema kuwa uamuzi wa Serikali wa kuunda meli hizo ulikuwa kutatua changamoto ya muda mrefu ya ukosefu wa vyombo vya baharini vya kusafirisha abiria na mizingo ndani na nje ya nchi kupitia Ziwa Nyasa.

  Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, , pamoja na kupongeza kazi kubwa iliyofanywa na mkandarasi mzawa, Songoro Marine Transport Ltd, kuunda meli hizo, wamesema kuwa kukamilika kwa meli hizo kutachochea biashara na mapato ya serikali kupitia shughuli za usafiri na usafirishaji katika Ziwa Nyasa.

  Prof. Mkenda amesisitiza kuwa Serikali itaangalia uwezekano namna ya kumtumia Mkandarasi huyo, Bw. Saleh Songoro, kuunda meli nyingi zaidi za ndani na nje ya nchi ili kukamata soko hilo la utengenezaji wa meli kitaifa na kimataifa hatua itakayoliletea Taifa sifa, kukuza uwekezaji na ajira.

  Ujenzi wa Meli zote tatu, mbili za mizigo pekee, na moja ya mizigo na abiria, umekadiriwa kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 20 na utakuwa umetekeleza ahadi ya Serikali ya muda mrefu ya kuboresha usafiri wa abiria na mizigo kupitia Ziwa Nyasa, ambapo unatarajiwa kukuza biashara kati ya Tanzania, Malawi na Msumbiji, kusisimua uchumi wa wakazi wa wilaya ya Kyela na ukanda wote wa Kusini.

  Aidha kukamilika kwa ujenzi wa meli hizo kutapunguza matukio ya ajali za mara kwa mara zinazogharimu maisha ya watu wengi wanaotumia Ziwa Nyasa, linalo tajwa kuwa la pili kwa kuwa na mawimbi makali na la tano kuwa na kina kirefu cha maji duniani.
  Meli mbili za Mv. Ruvuma na Mv Njembe zikiwa katika cherezo katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela Mkoani Mbeya, zikiwa katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kufanyiwa majaribio ndani ya Ziwa Nyasa Mwishoni mwa Februari, 2017.
  Bw. Juma Nassoro akipaka rangi meli ya mizigo ya Mv Ruvuma, ikiwa ni hatua za mwisho wa ukamilishaji wa uundaji wa meli hiyo yenye uwezo wakubeba tani 1000 za mizigo itakayokuwa ikifanya safari zake Ziwa Nyasa, wakti Ujumbe wa Serikali kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ulipofanya ziara katika Bandari ya Itungi, wilayani Kyela mkoani Mbeya.
  Kaimu Mkuu wa Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, Bw. Ajuaye Msese akitoa maelezo mafupi kuhusu Bandari ya Itungi, na majukumu yake kwa ujumla kwa wageni waliotembelea Bandari hiyo mkoani Mbeya. 
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd, inayounda meli tatu katika Bandari hiyo, Bw. Saleh Songoro, akielezea historia fupi ya kampuni yake iliyoingia mkataba na Mamlaka ya Bandari Tanzania-TPA kuunda meli tatu Ziwa Nyasa, baada ya Ujumbe wa Serikali ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, ulipotembelea Bandari hiyo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mchoro wa meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja anazoziunda kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa Serikali unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya.


  Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha moja kati ya ya meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 kila moja anazoziunda kwa ajili ya matumizi katika Ziwa Nyasa, katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela mkoani Mbeya, baada ya kutembelewa na ujumbe wa Serikali unaofuatilia masuala ya biashara mipakani mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionyesha mchoro wa meli mbili za mizigo za MV Ruvuma na Mv Njombe alizoziunda wakati Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Amina Khamis Shaaban (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Balozi Hassan Simba Yahya (wa pili kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda (wa tatu kushoto) walipozulu Bandari ya Itungi, iliyoko Wilayani Kyela mkoani Mbeya.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akiongoza ujumbe wa Serikali kutoka Wizara za Fedha, Uwekezaji, na mambo ya Ndani kujionea kazi ya ujenzi wa Meli mbili za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 1000 za mizigo kila moja zinazojengwa katika Bandari ya Itungi iliyoko Wilayani Kyela mkoani Mbeya
  Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine Transport Ltd, Bw. Saleh Songoro, akionesha mfumo wa kuongoza meli katika chumba cha nahodha wa meli ya Mv Njombe, huku Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biasha na Uwekezaji Prof Adolf. Mkenda, akiangalia kwa makini mfumo huo wa kisasa namna unavyofanya kazi.
  Baadhi ya wajumbe wa Serikali waliofanya ziara katika Bandari ya Itungi mkoani Mbeya kujionea uundwaji wa meli mbili za mizigo wakishuka kwenye ngazi baada ya kumaliza kukagua meli ya Mv Njombe inayotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Ltd inayoshughulika na kutengeneza vyombo vya usafiri vya majini katika Bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoani Mbeya. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

  0 0

  Na Jacquiline Mrisho - MAELEZO.

  Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la Plan International limezindua Mpango Kazi wa miaka 5 utakaowawezesha wasichana wanaoishi katika mazingira magumu kujitambua na kujisimamia wenyewe katika nyanja mbalimbali zitakazowaletea maendeleo. 

  Mpango kazi huo unaanza mwaka 2017- 2022 ukiwa na lengo la kuwasaidia wasichana 1,000,000 ulimwenguni kote.

  Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kanda ya Nchi za Afrika Mashariki na Kusini – Plan International, Roland Angerer alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu malengo ya mpango kazi huo.

  Angerer amesema kuwa Shirika hilo limepanga kuisaidia Serikali ya Tanzania kufikia Mpango wa Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo mwaka 2030 kwa sababu mpango huo umelenga kutengeneza mazingira mazuri kwa watoto hasa wasichana na kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika suala zima la maendeleo.

  “Plan International wameweka mpango mkakati wa ulimwengu mzima ambao utawasaidia wasichana sio tu katika kupata elimu bali kuwafanya wawe na nguvu itakayowasaidia kujifunza, kujiongoza, kuamua pamoja na kujipigania katika mambo mbalimbali yanayowahusu,”alisema Angerer.

  Ameongeza kuwa usawa wa kijinsia ni moja ya Mpango wa Maendeleo Endelevu hivyo wataweka juhudi kubwa katika kuhakikisha wasichana wanapata haki sawa na wavulana kwani usawa huo utasaidia kuharakisha maendeleo.

  Nae Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo- Tanzania, Jorgen Haldorsen amesema kuwa nchini Tanzania mpango huo utalenga zaidi katika kuzuia ndoa za utotoni kuanzia katika ngazi ya Kitaifa hadi Vijiji ili kuhakikisha mtoto wa kike anapata haki zake.

  ”Kwa kushirikiana na Serikali , tumeanzisha miradi ya kuzuia ndoa za utotoni katika Mikoa ya Mara, Geita,Morogoro na Rukwa na katika mikoa hiyo tunategemea kuwafikia moja kwa moja wasichana 12,000 na kuwafikia wasichana 120,000 kwa njia zingine tofauti,”alisema Haldorsen.

  Amefafanua kuwa pamoja na jitihada zote na rasilimali mbalimbali kuelekezwa kwenye jamii kupitia Mikoa,Wilaya na Kata lakini bado wanatambua umuhimu wa kufanya kazi na Serikali katika ngazi ya kitaifa kwa kutoa maoni na uzoefu wao katika kutengeneza sera zinazomuhusu mtoto na usawa wa kijinsia.

  Kwa upande wake Muhamasishaji kutoka Mradi wa Vijana wa ‘Youth for Change’, Upendo Abisai amelishukuru shirika hilo kwa kufanya jitihada katika kuhakikisha msichana anapata haki zake kwani ulimwengu mzima wasichana ndio wanaokumbwa na changamoto nyingi zinazowapelekea kutotimiza malengo yao. 

  “Sisi kama vijana wa ‘Youth for Change’ tumepewa fursa kubwa ya kuwafikia na kuwaelimisha vijana wenzetu juu ya haki zao za msingi pia tuna nafasi ya kuwasemea wale ambao hawajapata nafasi ya kusema ili kuhakikisha wote kwa pamoja wanapata haki zao”,alisema Bi. Upendo.

older | 1 | .... | 1144 | 1145 | (Page 1146) | 1147 | 1148 | .... | 1897 | newer