Quantcast
Channel: JIACHIE
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live

Rais wa Zanzibar Dk Shein Akutana na Mkurugenzi wa NMB Tanzania

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi. Ineke Bussemaker, alipofika Ikulu Zanzibar leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania Bi Ineke Bussemaker, baada ya mazungumzo yao leo Ikulu Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania baada ya mazungumzo yao Ikulu leo 

PICHA NA IKULU

BURUDANI MURUA KABISA YA TWANGA PEPETA KILA JUMAPILI PALE MZALENDO PUB.

RED CROSS YAKABIDHI KADI ZA UANACHAMA IDARA YA MAAFA

$
0
0
 Rais wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw. Mwadini Jecha (katikati) akiweka saini kitabu cha wageni Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu walipotembelea Idara hiyo na kukabidhi Kadi za Uanachama kwa Idara  hiyo, tarehe 16 Februari, 2017.
 Mkurugenzi wa Chama Cha Msalaba Mwekundu Tanzania Bw.Renatus Mkaruka (wa kwanza kulia) akizungumza jambo wakati wa zoezi la kukabidhi kadi za Uanachama wa chama hicho kwa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Februari 16, 2017 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brig.Jenerali Mbazi Msuya (kulia) akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kutoka kwa Rais wa Chama hicho Bw. Mwadini Jecha Februari 16, 2017 katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
Mratibu wa Maafa Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Charles Msangi akipokea kadi ya uanachama wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania kutoka kwa Katibu wa chama hicho Bw. Julius Kejo Februari 16, 2017 katika Ofisi za Idara hiyo Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

UNDP WAKUTANA NA WANAFUNZI WA SHULE YA WASICHANA ,WERUWERU MKOANI KILIMANJARO KUJADILI MALENGO MAPYA YA MAENDELEO ENDELEVU

$
0
0
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez (katikati) akiwa ameongozana na Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushi (kushoto) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ya mkoani Kilimanjaro,Rosalia Flavian wakiingia katika ukumbi wa shule hiyo kwa ajili  kongamano.
Wanafunzi wa kidato cha Tano na Sita pamoja na wageni wakiimba wimbo kabla ya kuanza kwa kongamano hilo lililolenga kuzungumzia juu ya Malengo ya Maendeleo endelevu .
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ,Rosalia Flavian akizungumza wakati wa Kongamano hilo.
Baadhi ya Walimu katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Weruweru wakifuatilia maelezo ya awali yaliyotolewa na Mkuu wa Shule hiyo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Weruweru akiteta jambo na  Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez.
 Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akizunguza katika Kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi katka shule ya Sekondari ya Wasichana  ,Weruweru wakiwa katika kongamano hilo.
Mtaalamu wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania ,Hoyce Temu akizungumza katika kongmano hilo.
  Mkurugenzi anayesimamia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushi akitoa mada kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru juu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu .
Baadhi ya Wananfunzi wa Shule ya Sekondari ,Weruweru wakiwa wameshikilia vibao vinavyoonesha baadhi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu wakati Balozi Mushi akiwasilisha mada .
Balozi Mushi akionesha Malengo mapya 17 ya  Maendeleo Endelevu kwa wananfunzi wa Shule ya sekondari Weruweru wakati akiwasilisha mada.
Balozi Mushi akitoa zawadi ya Pesa kwa wanafunzi wawili wa kidato cha Tano na Sita katika shule ya sekondari ya Wasichana ya Weruweru baada ya kuuliza na kujibu vyema maswali . 
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguezakiwa katika picha ya pamoja na walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru pamoja na wafanyakazi wengine wa Serikali.
Mwakilishi wa Mashirika ya Kimataifa nchini na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Alavaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini. 

TASAF KISHAPU YAWAPIGA MSASA WADAU

$
0
0
 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga akifungua rasmi mafunzo kwa wadau wa TASAF kwa vijiji vitatu katika Kata ya Mwakipoya ili kuwajengea uelewa katika kuwaudumia walengwa.
 Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamhanga akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ambaye alikuwa mgeni rasmi kufungua rasmi mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza mgeni rasmi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (hayupo pichani).
 Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Stephen Magoiga ameagiza watendaji wa vijiji kuhakikisha wananchi waliochukua fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Taifa (TASAF) bila kuwa na sifa wanarudisha mara moja.

Magoiga alitoa agizo hilo jana wakati akifungua mafunzo kwa wadau wa TASAF kwa vijiji vitatu katika Kata ya Mwakipoya ili kuwajengea uelewa katika kuwaudumia walengwa.

Alisema lengo la mpango wa TASAF ni kusaidia kaya zisizo na uwezo hivyo ni wajibu wa wadau hasa wajumbe wa Serikali za vijiji kuhakikisha wanawatambua wananchi wa maeneo yao ili kubaini kaya maskini.

Mkurugenzi aliwataka wadau kusimamia vizuri walengwa akisisitiza kuwa Serikali kupitia TASAF ina jukumu la kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na maisha bora kwa kuwapa ruzuku ili kujiendeleza.

Magoiga aliongeza kwa kuwahimiza wadau hao kufuatilia maendeleo ya watoto wa walengwa wa mpango huo wanaopata ruzuku kwani elimu ndiyo inaweza kuondoa umaskini.

“Mpango wa TASAF ni pamoja na matumizi mazuri ya fedha na mimi nawapongeza kwa kazi nzuri ya kuzihudumia kaya maskini, natambua kuwa ninyi ni watu muhimu katika kushughulikia mpango huu,” alisema.
Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Kishapu, Sospeter Nyamhanga alisema mafunzo hayo yataongeza ufanisi kwa wadau hao katika kutoa huduma kwa walengwa.

Nyamhanga alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa wanabaki na kaya maskini na zenye sifa mfuko huo ngazi ya wilaya itaendelea kufanya uhakiki mara kwa mara kwenye vijiji lengwa.

Alisema mafunzo hayo tayari yametolewa katika vijiji 15 kati ya 78 vilivyopo kwenye mpango na kuwa lengo ni kufikia vijiji vyote ili wadau wapate elimu ya ufanisi wa kutoa huduma.

Kwa upande wa mafanikio ya TASAF wilayani humo, alisema kuwa hadi sasa walengwa wamepata maendeleo kupitia ruzuku wanayopokea .Alitaja mafanikio hayo ni baadhi yao wameweza kununua mifugo, kuanzisha biashara ndogondogo, kilimo na hata kuboresha makazi yao kwa kuezeka kwa mabati badala ya nyasi kama ilivyokuwa awali.

Hata hivyo, alisema pamoja na hayo bado kuna changamoto ya ufinyu wa bajeti kwa ajili ya kuedeshea mafunzo kwa wadau wa mpango wa TASAF hali inayochangia kuwa idadi chache ya mafunzo.

Tayari mafunzo hayo yametolewa kwenye vijiji vitatu kata ya Mwakipoya na yanahusisha wadau mbalimbali wanaohudumia kaya maskini wakiwemo watendaji kata na vijiji, mratibu elimu kata, watumishi wa afya pamoja na walimu. Ngeme,Mwangongo na Mwakipoya.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo waliipongeza TASAF na kusema kuwa yamewapa mwanga na kuwa yatawasaidia katika utendaji kazi wao.

WAZIRI MAKAMBA AZUNGUMZA NA MABALOZI KUHUSU UHARIBIFU WA MAZINGIRA

$
0
0
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba (katikati) akiongea wakati wa mkutano na na Mabalozi ambao ni Washirika wa Maendeleo. Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Makamu wa Rais liliko barabara ya Luthuli.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwasilisha mada na kuonyesha picha mbalimbali za uharibifu wa mazingira zilizopigwa wakati wa ziara yake ya mikoa 10 mwaka jana kwa Mabalozi ambao ni Washirika wa Maendeleo ya masuala ya mazingira.
 Sehemu ya Washiriki wa Mkutano huyo ambao ni Mabalozi  wakifuatilia kwa makini  wakati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiwasilisha mada kwenye mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (wa pili toka kulia)  akifanunua jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. January Makamba wakiongea jambo Mwakilishi wa UN Nchini Tanzania Alvaro Rodriguez baada ya kumaliza mkutano huo.

WAZIRI MKUU: SERIKALI KUPIGA MARUFUKU POMBE ZA VIROBA

$
0
0
​​
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi mosi, 2017 Serikali itapiga marufuku matumizi ya pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

“Tumekaa na wenye viwanda na kukubaliana kuwa wanaotengeneza Pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. “Sasa hivi viroba vimeenea kila kona hata watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo. Kuanzia tarehe moja Machi, tutakayemkamata ameshika pombe ya viroba, sisi na yeye.”

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 16, 2017) wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

Amesema agizo hilo linaenda sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya kwani mji wa Mererani unaongoza kwa matumizi ya dawa hizo haramu.

“Tutawakamata wanaosambaza, wanaouza na wanaokula. Hapa Mererani kuna bangi, kuna mirungi, cocaine na heroine. Mkuu wa Mkoa hapa panahitaji operesheni kupambana na dawa za kulevya. Piteni kwenye vijiwe na kukagua wale waliolegealegea, kisha tuwapime,” alisisitiza.

Akifafanua suala la uwekezaji kwenye eneo la Shambalai kutokana na ujumbe ulioandikwa kwenye mabango, Waziri Mkuu alisema katika eneo hilo zimetengwa ekari 500 kwa ajili ya EPZA ili kujenga miundombinu mbalimbali.

“Hilo eneo ni la uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, masoko na maduka makubwa (malls). Sote tunafahamu kuwa Tanzania hivi sasa inaweka msisitizo juu ya ujenzi wa viwanda. Pale tunataka tuwe na viwanda vya nyama, vya kushona nguo na kuchakata madini ya Tanzanite ili kjongeza thamani,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema kama kuna mtu ana uhakika kuwa nyumba yake bado haijalipwa fidia katika eneo lile, aende akaonane na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Joel Bendera lakini taarifa alizopewa ni kwamba hakuna mtu ambaye hajalipwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaita wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite One ili wampatie taarifa juu ya malalamiko yanayotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwamba hali ilikuwa nafuu wakati kampuni hiyo ikimilikiwa na wazungu kuliko hivi sasa.

“Nikimaliza ziara ya mkoa huu, nataka tarehe 27 Februari, Wakuu wa hii kampuni waje ofisini kwangu na taarifa kuhusu shughuli za uendeshaji wa madini. Nitawashirikisha na wabunge wenu ili waje waseme kwa nini mzungu ni bora kuliko Mtanzania,” alisema.

“Serikali hii inatarajia kuona Watanzania wakinufaika na rasilmali zao. Haiwezekani tukahimiza uwekezaji wa ndani halafu leo anasifiwa mzungu kuliko mzawa,” alisema.



IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 17, 2017.

WAZIRI NAPE AFANYA MSAKO KARIAKOO LEO WA KUKAMATA WANAODURUFU KAZI ZA WASANII

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakia katika oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza msafara huo wa kufanya oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo. Picha na Iman Nsamila.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiangalia baadhi ya DVD feki zilizokuwepo katika moja ya maduka ya Kariakoo, Jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiingia katika moja ya stoo za Duka mojawapo linalouza na kudurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.


NEWZ ALERT:WATUMISHI WAWILI WA TRA WANASHIKILIWA NA VYOMBO VYA DOLA KWA TUHUMA ZA KUJIHUSISHA NA BIASHARA HARAMU YA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Watumishi Wawili Wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanashikiliwa na vyombo vya dola wakituhumiwa kujihusisha na upitishaji Wa kemikali ambazo hutumika kutengenezea dawa za kulevya aina ya Heroin.

Kukamatwa kwa watumishi hao wa umma kumetangazwa  leo na Kamishina Wa Operasheni ya Mamlaka ya kupambana na dawa za kulevya Mihayo Msekela.
Kamishina wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini,ambapo katika Oparesheni hizo zinazoendelea nchini,ilionesha mafanikio kwa baadhi ya mikoa kama taarifa inavyoonesha hapo chini.PICHA NA MICHUZI JR.
Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini
Kamishina wa Operesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na kupambana na dawa za kulevya,Mihayo Msikhela akifafanua japo alipokuwa akizungumza na baadhi ya Waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali mapema leo,katika ofisi za Mamlaka hizo zilizopo Upanga,jijini Dar Es salaam kuhusiana na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa waliojihusisha na biashara haramu ya usafirisha wa dawa za kulevya hapa nchini,ambapo katika Operesheni hizo zinazoendelea nchini,ilionesha mafanikio kwa baadhi ya mikoa kama taarifa inavyoonesha hapa chini.

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAGENI MBALIMBALI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Amadou Hott mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga  Mutamba Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi huyo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo(DRC) nchini Jean Pierre Tshampanga  Mutamba mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterrprise, Sunil Bharti Mittal Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

OPERESHENI YA SAKATA LA DAWA ZA KULEVYA LAENDELEA KILA KONA YA NCHINI ,KIGOMA NAKO KWA TIKISA

$
0
0
Na Rhoda Ezekiel-Globu ya Jamii, Kigoma.

JESHI la Polisi Mkoani Kigoma limekamata Wahamiaji haramu 226, Kete za bangi 191, Heroin kete tano , pombe ya moshi lita 300 na silaha aina ya gobore moja, katika msako wa kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji haramu pamoja na uhalifu uliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo salama.

Akitoa taarifa ya Msako huo leo mbele ya Waandishi wa habari Mkoani humo , Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui alisema kuanzia Februal 2 mwaka huu jeshi la polisi Mkoani humo lilianza Msako wa kuhakikisha wanakomesha vitendo vya uhalifu, matumizi ya Dawa za kulevya na uuzaji pamoja na wahamiaji haramu wanaoingia Nchini bila vibali, hali inayo sababisha uhalifu kuongezeka kutokana na vitendo hivyo.

Mtui alisema kuwa mnamo februali 16 ulifanyika msako na kufanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 203 katika kijiji cha Mganza Wilayani Kasulu wakitokea nchini Burundi wakiwa katika mashamba ya Wakulima,alisema na kuongeza kuwa Kigoma mjini walikamatwa wahamiaji 7 , kibondo 9 na Buhigwe 7a na jumla yao ni wahamiaji 226 ambao waliingia nchini Kinyume na utaratibu huku wakipokelewa na Wenyeji na wanawahifadhi.

Alisema Wengi wa wahamiaji hao wanatoroka Nchini mwao wakiwa wamefanya uhalifu na wanakuja Nchini na wanapokelewa na wenyeji na wanawatumia katika kilimo pia wengi wao ndio wanaotumika kifanya uhalifu mkoani humo ambapo Kamanda Mtui aliwaomba Wananchi kuacha kuwapokea Wahamiaji hao ambao wengi wao husababisha madhala makubwa katika maeneo yao.

Aidha Mtui alisema kwa upande wa madwa ya kulevya jeshi la polisi lilikamata katika Wilaya ya Kigoma kete za bhangi 191 sawa na gram10 pamoja na Heroin kete tano, Kasulu walikamata robo eka na gram 500 , kibondo miche 10 na Kakonko miche 60 ,kilo moja ya Bhangi madawa hayo yalikuwa yakiuzwa kwa vijana ambao wengi wao hawafanyi kazi na wanaendelea kufanya vitendo vya uhalifu.

" tumeweza kutoa kipaumbele katika uhalifu unao tusumbua kwa kiasi kikubwa Mkoani Kigoma ambao ni wahamiaji haramu , na matumizi ya Dawa za kulevya, kwa mujibu wa upelelezi tulio ufanya wengi wanaoingia bila vibali ni wale wahalifu wanao kimbia mikono ya sheria kutokana na uhalifu kama tunavyo fahamu muahalifu hawezi kuacha uhalifu kiurahisi ndio ambao wanakuja kiendelea kufanya uhalifu niwaombe Wananchi kuacha kupokea Wahamiaji halamu kwasababu kwa sasa tutakae mkamata anawahifadhi wahamiaji halamu watafikisha mahakamani", alisema Kamanda Mtui.

Alisema katika msako huo zilipatikana idadi ya kesi katika msako huo ni kesi ya uhamiaji haramu ni nane , kupatikana pombe ya moshi kesi 11, kupatikana Bhangi kesi tisa , kupatikana na silaha kesi moja na kupatikana na heroini kesi moja, watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ilikuweza kujibu tuhuma zinazo wakabili.
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoani Kigoma, DCP Fredinand Mtui akizungumza na baadhi ya wandishi wa habari mapema leo kuhusiana na operesheni walioifanya ya kupambana na dawa za kulevya, wahamiaji halamu pamoja na uhalifu iliofanyika kwa kipindi cha Wiki moja ili kuhakikisha Mkoa upo salama.
Madumu ya pombe ya moshi (gongo),lita 300 zikiwa zimekamatwa
Kete za bangi 191 zikiwa zimekamatwa 

TFF YAWAONYA MASHABIKI WATAKAOENDA NA MABANGO YASIYOSTAHILI UWANJANI

$
0
0
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewatahadharisha wanachama na wapenzi wa klabu ya Yanga, kutobeba mabango ya kukashifu Serikali wala kiongozi yeyote wa nchi kesho wakati wa mchezo wa marudiano na Ngaya Club de Mde ya Comoro.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema jana kwamba wanawaonya mashabiki wa soka nchini waliopanga kuleta vurugu na kuonyesha viashiria vya kukashifu viongozi wa soka na Serikali katika mchezo wa wa kesho na wa Februari 25 dhidi ya Simba, wasithubutu kabisa kwani vyombo vya dola vinawajibika katika kushughulika nao.

Lucas amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethubutu kufanya kitu cha namna hiyo na kwamba kutakuwa na ulinzi mkali kesho Uwanja wa Taifa kwa ajili hiyo na kuwasihi mashabiki kuacha dhana hiyo kabisa na waje uwanjani kuja kushangilia mpira na kuipa sapoti timu yao

Yanga watakuwa wenyeji wa Ngaya katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mechi ya awali waliweza kutoka na ushindi wa goli 5-1 na hata hivyo tayari uongozi wa klabu ya Yanga ulishawasihi mashabiki wa timu hiyo kwenda kwa amani uwanjani na kutokufanya vurugu ya aina yoyote.

Kiingilio cha chini katika mchezo wa kesho kitakuwa Sh. 3,000 Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, VIP A Sh 20,000, VIP B Sh 10,000 na VIP C Sh 10,000.

Mechi hiyo itachezeshwa na marefa kutoka Uganda ambao ni Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na washika vibendera Ronald Kakenya na Lee Okello.

Refa wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro huku Kamishna akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas

BENKI YA UBL YAONESHA NIA YA KUWEKEZA KATIKA KILIMO NCHINI TANZANIA

$
0
0

Na Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam

Benki ya UBL imesema iko tayari kuwekeza Tanzania katika Sekta ya Kilimo ambayo itawezesha Tanzania kupata fursa ya kuweza kuuza mazao yake katika nchi za ughaibuni na pia kufanya kazi na Watanzania pamoja na Serikali yake. 

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Tanzania, Bw. Faisal Jamall wakati akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Bw. Jamall alisema kuwa kwa sasa Tanzania inaenda vizuri hasa katika suala la ukuaji wa uchumi ingawa kuna baadhi ya wananchi wanalalamika kuwa fedha zimeadimika mitaani lakini ni wazi kwamba Taifa linarudi kwenye utaratibu. Hivyo wameonesha nia ya kuwekeza hasa katika Sekta ya Kilimo.

Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) amesema kuwa hali inabadilika na Jumuiya ya Mabenki inaanza kuwa na imani na Tanzania. Na kuongeza kuwa kitendo cha Benki ya UBL kuonesha nia ya kufanya kazi na Serikali katika Sekta ya Kilimo ni jambo jema katika maendeleo ya haraka ya Tanzania kwa kuwa Sekta hii mama bado inakabiliwa na changamoto nyingi.  

Alisema dhamira kubwa ya Benki ya UBL ni kuwekeza katika kilimo cha umwagiliaji, uboreshaji wa mifugo pamoja na uvuvi. Na Serikali imeahidi kuitumia vizuri fursa hii ili nchi iweze kupiga hatua ya haraka zaidi hasa katika kipindi ambacho imedhamiria kuwa nchi ya Viwanda.

Akitoa ufafanuzi kuhusu matumizi ya dola katika uchumi badala ya shilingi ya Tanzania, hasa kwenye mikopo, Waziri Mpango alisema kuwa suala hili Serikali imeshaanza kulifanyia kazi kwa kuchukua hatua, ikiwa ni pamoja na kusimamia kwa karibu biashara ya maduka ya fedha za kigeni. 

“Tumepiga hatua ya kufunga mashine za kielektroniki (EFDs) ili Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuona kinachofanyika ili wamiliki wa maduka hayo walipe kodi inayostahili. Aidha zoezi hili litaweizesha Benki Kuu ya Tanzania – BoT, kuona kiasi cha fedha za kigeni zilizopita katika maduka na itaimarisha matumizi ya shilingi ya Tanzania; japo tuna changamoto kubwa ya wananchi kutokudai risiti pindi wanapopata huduma ya kubadilisha fedha za kigeni,” Alisisitiza Dkt. Mpango.

Katika kuhitimisha majadiliano hayo Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mpango alisema Serikali itaongeza ushirikiano na Benki ya UBL ili waweze kufanya biashara, ikizingatiwa kuwa Benki hiyo ni miongoni mwa Benki kubwa katika nchi za Uarabuni.

Imetolewa na: 
Kitengo na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango
16 Februari, 2017
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia), akielezea namna matumizi ya vifaa vya Kielektroniki (EFDs) yalivyoongeza Makusanyo ya Mapato ya Serikali alipotembelewa na Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), Ofsini kwake jijini Dar es salaam.

Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), akielezea nia ya Benki yake ya kutaka kuwekeza kartika Sekta ya Kilimo, alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (hayupo pichani) ofisini kwake jijini Dar es salaam. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kulia) akichukua maelezo ya Mtendaji Mkuu wa Benki ya UBL Nchini Tanzania Faisal Aliza Jamall (Kushoto), baada ya ya Mtendaji huyo kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam na kueleza nia ya kuzitumia fursa zilizopo katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (kushoto) akifafanua jambo kuhusu uwekezaji katika Sekta ya Kilimo unaotaka kufanywa na Benki ya UBL Nchini Tanzania baada ya kukutana na Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw. Faisal Aliza Jamall OfIsini kwake jijini Dr es salaam. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

OLE MILLYA AIPONGEZA SERIKALI KUTATUA KERO ZA WANANCHI

$
0
0
 MBUNGE wa Simanjiro, Mheshimiwa James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyojali na kuwahudumia wananchi.

Ametoa pongezi hizo jana (Alhamisi, Februari 16, 2017) kwenye mikutano miwili ya hadhara iliyofanyika Orkesumet na Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, baada ya kupewa nafasi asalimie wananchi kabla Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hajazungumza na wakazi wa maeneo hayo.

“Serikali hii ina viongozi wachapakazi akiwemo Waziri Mkuu. Kwa mara ya kwanza katika jimbo hili, wananchi watapata maji safi kupitia mradi wa maji kutoka mto Ruvu unaoendelea kujengwa hivi sasa,” alisema kwenye mkutano wa hadhara wa Orkesumet.

Alitumia fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la ujenzi wa hospitali ya wilaya kwani sasa hivi wanategemeakituo cha afya na hali ikibadlika inabidi mgonjwa apeekewe Arusha mjini ambako ni umbali wa km. 150 kutoka Orkesumet yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.

Pia aliomba ijengwe barabara ya lami ya kuunganisha wilaya hiyo pamoja wilaya jirani za Hai na Kiteto.

Akiwa Mererani, Bw. Ole Millya aliipongeza Serikali kwa kujenga barabra ya lami kutoka uwanaja wa ndege wa KIA hadi Mererani. Hata hivyo, aliiomba serikali iongeze juhudi ili barabara hiyo iweze Mererani na Orkesumet.

Akihibu hoja hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza mbunge huyo kwa uungwana wake wa kutambua juhudi ambazo Serikali imezifanya kwa wananchi wa jimbo lake.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara, aliwaambia wakazi hao kwamba Serikali itaendelea kufanya nao kazi bila kumbagua mtu yeyote kwa sababu ya itikadi za kisiasa.

“Mmempa yeye dhamana ya kuwawakilisha kama mbunge wenu lakini dhamana ya kuongoza nchi mmempa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapigia kura. Kwa hiyo, kazi yetu ni kuwatumikia ili tutatue kero zinazowakabili wana-Simanjiro,” alisema.

Akizungumzia sekta ya afya, Waziri Mkuu alisema kituo cha afya cha Orkesumet kimepokea sh. milioni 49 kati ya sh. milioni 57 zilizoombwa ili kukiimarisha katika utoaji wa huduma za tiba.

“Tumeshatuma fedha nyingine sh. milioni 163 kati ya sh. milioni 190 zilizoombwa ili kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Pia kun ash, milioni 483 zimetengwa kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya vijijini,” alisema.

“Nia yetu ni kujenga hospitali kubwa ya wilaya lakini ni lazima tuimarishe miundombinu ya utoaji tiba ili wananchi wapate huduma stahiki.Ombi la hospitali ya wilaya nimelipokea na nitafuatilia kujua limefikia hatua gani,” alisema.

Kuhusu ujenzi wa barabara za kuunganisha wilaya, Waziri Mkuu alisema Serikali itaanza kufanya upembuzi na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Arusha – Kiteto – Kongwa ili ijengwe kwa kiwango cha lami.

Kuhusu migogoro ya ardhi iliyotajwa na wananchi kwenye mabango yao, Waziri Mkuu alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Eng. Zephania Chaula aende na mbunge huyo kwenye maeneo yanayolalamikiwa na wananchi ili akabaini chanzo cha migogoro na aitafutie ufumbuzi.

Kuhusu umeme, Waziri Mkuu alisema vijiji 18 katika ya 57 vya wilaya vimeshapatiwa umeme na vilivyoakia vimeshaingizwa kwenye mpango wa serikali wa kuvipatia umeme vijiji 8,000.

Aliwaonya wakazi wa Mererani wachukue tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwani takwimu zinaonyesha kuwa kasi ya maambukizi katika mji huo iko asilimia 18 kiwango alichosema ni kikubwa kuliko kiwango cha kitaifa.

MFAHAMU MISS TANGA 2001 ALIYEJIKITA KATIKA KUSAIDIA JAMII

$
0
0
 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KAMA Mwanamke ukiamua kujitoa na kupigania nini unafanya lazima utafanikiwa, nami naweza kusema kufika kwangu ni pale nilipoamua kujituma, kujiamini na kutambua nini malengo yangu.

Hayo ni baadhi ya maneno aliyotoa mwanamke mjasiriamali Sophia Khalid Byanaku, ambaye ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Doctor's Plaza, alikuwa akizungumza na Globu hii. 

Sophia Khalid Byanaku  ni mke wa Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), ana Elimu ya Shahada ya sosholojia (Degree in Sociology), Shahada ya uzamili Sera za afya Mipango na Usimamizi (Master in Health Policy Planning and Management.

Ulianzia wapi,


Byanaku : Mwaka 2001 nilishiriki mashindano ya urembo kwa mkoa wa Tanga na kufanikiwa kuchukua taji la Miss Tanga 2001 na kupata nafasi ya kuwa katika kumi bora ya Miss Tanzania ambapo taji lilichukuliwa na mrembo Millen Hapiness Magese. 

Unajivunia nn kupitia Miss Tanzania,
Byanaku: Najivunia mambo mengi kupitia ushiriki wa Miss Tanzania mwaka ule kwani umeweza kunipa ujasiri wa kuweza kupambana kwa namna nyingine na hata miaka yetu tuliweza kupata nafasi nyingi za kushiriki kijamii zaidi.

Baada ya kumalizika kwa Miss Tanzania ulijikita wapi zaidi:
Byanaku:  Kabla ya kufungua Kliniki ya Doctor's Plaza, nilikuwa mfanyakazi wa benki Stanbic Bank Tanzania kwa takribani miaka 6, baadae nikafanya kazi benki ya NMB kwa muda wa mwaka mmoja na African Life Assurance (Sanlam).

Doctors Klinik ilianza lini?

Byanaku: Rasmi mwaka 2012 kwa kituo kimoja wakiwa wamejikita katika kutibu magonjwa ya moyo tu lakini sasa wanatoa matibabu ya ya magonjwa mbalimbali ya binaadamu na tayari wana vituo  vitatu ambavyo vyote vipo jijini Dar es Saalam.

Madhumuni ya kufungua Doctors Kliniki ni nini?
Byanaku: Lengo kuu la kufungua vituo hivyo ni kwa sababu napenda sana kujishughulisha na jamii, hivyo kuwa na vituo hivyo amejua mambo mengi kuhusu jamii inayomzunguka. 

Matarajio ya Byanaku ya baadae:
Byanaku:  Matarajio yangu ya  baadae ni kuwa na Hospitali kubwa ya kisasa Tanzania ambayo itaweza kutoa huduma karibia zote kwa wahitaji,na pia nataka kuwa Mtaalam wa Health care Management kwa Tanzania,yani nataka kukiwa na uhitaji wa ushauri kuhusu masuala ya uongozi wa Afya Tanzania mimi niwe mtu wa kwanza kufikiria kusaidia.

Changamoto anazozipata katika vituo  Doctor's Plaza
Byanaku: Kuna changamoto mbalimbali zinazotukabili kwenye vituo vyetu vya Doctor's Plaza ila kikubwa zaidi  ni madaktari kwani ni wachache ambapo mpaka sasa tuna madaktari 32 kutoka Muhimbili ila tunaendelea kufanya jitihada kuhakikisha  watu wanapata huduma wanazohitaji za matibabu. 



Anachojivunia kama mwanamke mjasiriamali:

Byanaku: Naweza kusema katika kufanikisha jambo uliloamua kulifanya, kwenye hili hakuna mwanaume wala mwanamke ili kuweza kufikia mafanikio yoyote,lazima kufanya kazi kwa bidii na kujituma,na sio kwa bidii tu lakini pia kwa akili,kusimamia malengo yako na pia kutokukubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote yule,ilhali huvunji heshima ya mtu.
Wanawake tusiogope wala kuona aibu fursa zinapotokea tuzikimbilie bila aibu wala woga na tuonyeshe uwezo wetu, kwa kusema haya haya Mimi mwenyewe bado sijafikia malengo yangu lakini nashukuru nimeweza kufikia kidogo safari bado ni ndefu tunajifunza kila siku na nina amini nitafika.
Unapaswa kujiwekea malengo na kuyafanyia kazi ili kuyafikia, kila unachoona kinaweza kufanyika na kufanikiwa kwa asilimia kubwa. 

Byanaku nje ya kazi ni nani?

Byanaku: Sophia Khalid Byanaku ni Mama wa watoto wawili, Nayla (6) na Akim(4), na nimeolewa na Profesa Mohamed Janabi (Mtaalamu wa magonjwa ya Moyo), muda wangu mwingi napokuwa nyumbani napenda kukaa na familia yangu.
Kama Mwanamke mara nyingi nakuwa na suluhisho na nafanikiwa kujigawa kwa usawa katika majukumu yangu ya nyumbani, napenda sana kuwa na familia pale ninapoukuwa nyumbani  bila kuchanganya yote haya nayafanya na naweza ndiyo maana natarajia kuongeza zaidi hapa nilipoanza, kikubwa mwanamke unaweza kufanikiwa kama kweli umeamua kulifanya lako katika kuleta maendeleo katika jamii hasa iliyokuzunguka

Anasema hata hivyo bado anajitahidi kuwa nkujifunza kwa kusoma vitabu na hata kuuliza watu walionitangulia waliwezaje na kufanikiwa, lakini pia kuweza kufanikiwa haya ni lazima pia upate ushirikiano kutoka kwa familia,ambayo nashukuru ninapata ushirikiano.

Unapendelea nini? 

Byanaku: Ni mpenzi wa kusoma vitabu Sana kwa sasa nasoma vitabu viwili; My Personal MBA By Josh Kaufman na The E Myth Revisited By Michael Gerber na kitabu ninachotarajia kusoma ni The Miracle Morning by Hall Elroy. Napenda Kusafiri,Mziki,na kusoma.

VIJUSO VYA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARY 18,2017

MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI STEPHEN MASELE AMALIZA ZIARA JIMBONI MWAKE,ASIKILIZA MATATIZO YA WANANCHI

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) amemaliza kufanya ziara yake ya siku tatu katika jimbo la Shinyanga.

Katika ziara hiyo ya kikazi iliyoanza Februari 15,2017 kumalizika Februari 17,2017 ,Mheshimiwa Masele amekagua miradi ya maendeleo na kufanya vikao na wananchi wa kata 14 kisha kujadili na kuzitafutia ufumbuzi kero za wananchi. 

Katika maeneo mengi aliyopita,Mheshimiwa Masele amekutana na kilio kikubwa cha tatizo la njaa linalowakabili wananchi ambao walidai wamekuwa wakiendesha maisha yao kwa kunywa uji hivyo kuiomba serikali iwaone kwa jicho la huruma na kuwapatia chakula. 

Mheshimiwa Masele pia amekumbana na kilio cha bei kubwa ya maji inayotozwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira katika manispaa ya Shinyanga (SHUWASA),huku wananchi katika maeneo ambayo hayajafikiwa na mtandao wa maji kutoka ziwa Victoria wakiomba huduma hiyo ili kuondokana na kero ya maji. 

Viongozi wa shule za msingi nao walipaza sauti zao juu ya uhaba wa walimu katika shule,matundu machache ya vyoo ukilinganisha na idadi kubwa ya wanafunzi,upungufu wa madarasa huku wengine wakiomba kupatiwa huduma ya maji na umeme katika shule zao. 

Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Mheshimiwa Masele alisema yeye kama mbunge hayupo tayari kunyamaza juu ya matatizo yanayowakabili wananchi wake na kuahidi kuendelea kushirikiana na mamlaka zinazohusika ili kumaliza changamoto hizo. 

“Naomba serikali yetu itambue kuwa wananchi wa jimbo la Shinyanga Mjini wana njaa,wanahitaji chakula,hatuhitaji chakula cha bure bali tunataka chakula cha bei nafuu,wananchi wanalala njaa,shule zetu hazina walimu wa kutosha,bado bei ya maji iko juu sana ukilinganisha na kipato cha wananchi”,alieleza Masele. 

Siku ya kwanza ya ziara,mheshimiwa Masele alitembelea mradi mkubwa wa ujenzi wa daraja la Galamba na kuangalia,siku ya pili na tatu katika ziara yake ametembelea shule za msingi na kufanya vikao mbalimbali. 

Mwandishi wetu,Kadama Malunde,alikuwepo kwenye ziara hiyo…Ametuletea Picha 53 za Matukio yaliyojiri siku ya pili na ya tatu ya Ziara ya Mheshimiwa Stephen Masele…Tazama hapo chini 

SIKU YA PILI ZIARA YA MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI MHESHIMIWA STEPHEN MASELE 

Hapa ni katika Shule ya Msingi Twende Pamoja iliyopo katika kijiji cha Mwamalili kata ya Mwamalili katika Manispaa ya Shinyanga.Katikati ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akienda kuangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya wanafunzi wa shule hiyo.Kulia ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul Machela (CCM),wa kwanza kushoto 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiangalia eneo ambapo patajengwa choo kwa ajili ya shule ya msingi Twendepamoja yenye jumla ya wanafunzi 820 wanaotumia matundu 6 ya choo na walimu 8 pekee.Wa kwanza kushoto ni mwalimu Cephrine Philip anayefundisha katika shule hiyo. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Twende Pamoja ambapo alisema kupitia mfuko wa jimbo ametoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa shule hiyo. 
Hapa ni katika shule ya Msingi Ujamaa katika kijiji cha Seseko kata ya Mwamalili.Kulia ni Mwalimu mkuu Msaidizi katika shule hiyo Regina Bundala akimwonesha mheshimiwa Masele eneo ambapo watajenga choo kipya kwa ajili ya shule hiyo yenye wanafunzi 662 wakitumia matundu manne ya choo huku walimu nane waliopo katika choo hicho wakiwa hawana choo. 
Katikati ni Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza akiwa katika ofisi ya walimu shule ya msingi Ujamaa ambapo alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha wanafunzi na walimu wa shule hiyo.Kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai,kushoto ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul Machela. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Ujamaa na kuwataka wasome kwa bidii kwani elimu ina faida na itawasaidia kujikomboa katika maisha yao. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa amebeba mtoto katika ofisi ya mtendaji wa kijiji cha Seseko inayotumika kama Zahanati ambapo kulikuwa kunatolewa huduma ya kliniki kwa watoto 
Hapa ni katika shule ya Msingi Old Shinyanga iliyopo katika kata ya Old Shinyanga, Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akikagua choo kipya (kushoto) cha wanafunzi kinachojengwa chenye matundu 8 baada ya choo cha zamani kujaa na kuhatarisha maisha ya wanafunzi. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa ndani ya choo kipya akiangalia ujenzi unavyoendelea.Kushoto kwake ni diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM). 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akizungumza nje ya choo hicho ambapo alisema mfuko wa jimbo umetoa shilingi milioni 2.3 kusaidia katika shughuli za maendeleo ya kata ya Old Shinyanga. 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele akiwa katika jengo la kituo cha Maendeleo ya awali ya watoto kilichojengwa na shirika la Save the Children kilichopo katika shule ya msingi Old Shinyanga katika kata ya Old Shinyanga 
Diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM) akielezea changamoto zilizopo katika kata ya Old Shinyanga wakati wa kikao cha mbunge Masele na wananchi wa eneo hilo ambapo alisema ni pamoja na uhaba wa matundu ya vyoo, katika shule,zahanati ya Old Shinyanga kukosa chumba kwa ajili ya akina mama wajawazito na eneo la zahanati kukosa uzio kutenganisha na mnada uliopo katika zahanati hiyo 
Mbunge wa Shinyanga Mjini Mheshimwa Stephen Masele akizungumza wakati wa kikao na wananchi wa kata ya Old Shinyanga kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto za wananchi.Masele alilipongeza shirika la Save the Children kujenga jengo kwa ajili ya maendeleo ya awali ya watoto katika kata hiyo na kwamba serikali itaendelea kusaidia katika miradi mbalimbali katika kata hiyo.Kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi 
Mkazi wa Old Shinyanga akimwelezea Mbunge Masele jinsi wakazi wa eneo hilo wanavyoshinda na njaa kutokana na uhaba wa chakula inayochangiwa na chakula kuuzwa kwa bei kubwa 
Mheshimiwa Masele akifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya msingi Old Shinyanga 
Mheshimiwa Masele akizungumza na baadhi ya vijana wa Old Shinyanga walioamua kuzuia gari lake asiendelee na safari ili asalimiane nao 
Hapa ni katika shule ya Msingi Chibe katika kata ya Chibe manispaa ya Shinyanga.Aliyesimama ni ni Diwani wa tarafa ya Old Shinyanga mheshimiwa Picca Chogelo (CCM) akizungumza katika kikao cha mbunge na wananchi wa kata ya Chibe ambapo alisema kata hiyo haina shule ya sekondari watoto wanalazimika kusafiri umbali mrefu kwenda Old Shinyanga,eneo hilo halina huduma ya maji huku akiomba kata hiyo ijengewe barabara kwa kiwango cha lami kwani mji huo unakua kwa kasi 
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele akizungumza na wakazi wa Chibe ambapo alisema anachofanya hivi sasa ni kuhakikisha shule zote za msingi katika jimbo lake zinamaliza changamoto ya uhaba wa matundu cha choo 
Wananchi wa Chibe wakimsikiliza mbunge wao 
Wananchi wakiwa katika kikao 
Hapa ni katika kata ya Lubaga: Katikati ni diwani wa kata ya Lubaga mheshimiwa Obeid Jilala (CHADEMA)akimpokea mheshimiwa Stephen Masele 
Mheshimiwa Masele(CCM) akiwa na Obeid Jilala (CHADEMA) katika kikao cha kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa kero za wananchi 
Diwani wa kata Lubaga mheshimiwa Jilala akimkaribisha mheshimiwa Masele (kushoto) ili azungumze na wananchi wa kata ya Lubaga.Kulia ni katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rajabu Makuburi 

Mheshimiwa Masele akizungumza katika kikao cha majadiliano kuhusu maendeleo ya kata ambapo alisema ametoa shilingi milioni moja kwa ajili ya kusaidia shughuli za maendeleo ya kata hiyo 
Mheshimiwa Masele akijibu hoja ya ongezeko la bei kubwa ya maji na kero ya maji machafu yanayotoka kwenye mabomba ya maji ambayo yanasambazwa na SHUWASA 
Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai akielezea kuhusu namna serikali ilivyojipanga kukabiliana na changamoto ya uhaba wa walimu na matundu ya vyoo katika shule mbalimbali za manispaa ya Shinyanga 
Hapa ni katika kata ya Chamaguha:Aliyesimama ni diwani wa kata hiyo Morice Mugini (CCM) akimkaribisha mheshimiwa Masele katika shule ya msingi Ushirika iliyopo katika manispaa ya Shinyanga 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ushirika Lucia Amede akielezea changamoto ya matundu ya choo katika shule hiyo ambayo ina wanafunzi 844,matundu 6 pekee ya choo hali inayosababisha wanafunzi wapange foleni wakati wa kujisaidia 
Mheshimiwa Masele alizungumza katika kikao na wakazi wa kata ya Chamaguha ambapo alisema amesema pia kuna pesa kutoka mfuko wa jimbo imetolewa kusaidia ujenzi wa choo kipya cha shule hiyo 
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akielezea jinsi ilani ya uchaguzi ya CCM inavyoendelea kutekelezwa katika kata mbalimbali za jimbo la Shinyanga 
Mheshimiwa Masele akiangalia choo kipya inachojengwa katika shule ya msingi Ushirika 
SIKU YA TATU KATIKA ZIARA YA MBUNGE STEPHEN MASELE-Hapa ni katika kata ya Kizumbi,pichani Kaimu Afisa Elimu wa manispaa ya Shinyanga Gideon Kyungai akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kizumbi Neema Mkanga akitoa taarifa fupi kuhusu shule ya msingi Kizumbi kwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele.Alisema shule hiyo ina wanafunzi 502,matundu ya choo 6 ya wanafunzi,walimu 10 wanaotumia ambao hawana choo bali wanatumia tundu moja la choo cha wanafunzi 
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Rajabu Makuburi akizungumza katika shule ya msingi Kizumbi 
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi 
Mheshimiwa Masele akisisitiza kuhusu huduma ya maji katika eneo hilo ambapo alisema huduma hiyo inatakiwa iwafikie kutokana na bomba la maji kupita eneo la kata hiyo 
Mheshimiwa Masele akizungumza na wananchi wa Kizumbi 
Mzee Paul Kashinje mkazi wa kijiji cha Bugayambele kata ya Kizumbi akiomba serikali iwapatie chakula kwani wanashinda na njaa kunywa uji 
Mheshimiwa akiwa katika eneo la choo cha shule ambacho kinatumiwa na walimu na wanafunzi,eneo hilo ndipo pia patajengwa choo kipya 
Mheshimiwa Masele akiwasalimia wanafunzi wa shule ya msingi Kizumbi 
Mheshimiwa Masele akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya msingi Kizumbi 
Hapa ni katika shule ya msingi Ibinzamata-Wanafunzi wakimpokea mheshimiwa Masele 
Mheshimiwa Masele akiangalia matofali yanayotumika katika ujenzi wa choo cha shule ya msingi Ibinzamata 
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ibinzamata Vaileth Lumelezi akisoma risala kwa mheshimwa Masele ambapo alisema shule hiyo haina huduma ya umeme japo nguzo za umeme zinapita hapo.Alisema shule ina jumla ya wanafunzi 965 na matundu manne pekee ya choo 
Mheshimiwa Masele akizungumza katika shule ya msingi Ibinzamata.Kulia kwake ni diwani wa kata ya Ibinzamata Reuben Kitinya 
Wazazi wakimsikiliza mheshimiwa Masele 
Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi wa wanafunzi


Hapa ni katika shule ya msingi Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga,Pichani ni diwani wa kata ya Kitangiri Hamis Ngunila (CHADEMA) akimkaribisha mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ili azungumze na wakazi wa wanafunzi katika shule hiyo 




Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kitangiri Chrizestom Kitale akisoma risala kwa mheshimiwa Masele ambapo alisema shule hiyo ina wanafunzi 1265,na kwamba inakabiliwa na uhaba wa madarasa na matundu ya vyoo 


Mheshimiwa Masele akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ametoa shilingi milioni moja kusaidia maendeleo ya kata hiyo ikiwemo ujenzi wa matundu ya choo 


Mheshimiwa Masele akizungumza na wazazi 




Diwani wa Viti Maalum Mariam Nyangaka(CCM) akisisitiza jambo katika kikao hicho 




Wazazi wakiwa kwenye kikao Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog BOFYA <<HAPA>>KUONA PICHA ZIARA YA MASELE SIKU YA KWANZA

WAZIRI NAPE NNAUYE AWAWASHIA MOTO WAHARAMIA WA KAZI ZA WASANII

Waziri Mkuu aonya watakaopokea rushwa kwa wafanyabiashara dawa za kulevya.

$
0
0

 
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa atakayepokea rushwa kutoka kwa wauzaji, wasambazaji na watumiaji wa Madawa ya Kulevya.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa kikao cha kwanza cha Baraza la Taifa la kudhibiti dawa za kulevya nchini.

“Sheria ya udhibiti wa madawa ya kulevya itumike vizuri, Serikali na Baraza halitahitaji mtu yeyote mwenye mamlaka kupokea rushwa ikigundulika hatua kali zitachukuliwa” alifafanua Waziri Mkuu Majaliwa.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini ambayo yamekuwa yakifanywa na Serikali za Awamu zilizotangulia.

Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya ni vita inayotakiwa kupigana kwa nguvu kubwa kwani madhara ya dawa hizo ni kubwa kwa jamii hususani vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa.

“Tunahitaji ushirikiano wa karibu wa pande zote mbili za Muungano kwani tatizo hili limeathiri pande zote na ukanda wa bahari unatumika sana kama njia ya kuingiza dawa hizo” 

“Wakuu wa Mikoa mna kazi kubwa katika vita hii, mkiwa wenyeviti wa Kamati za Ulinzi na Usalama mpo kwenye nafasi nzuri ya kuendesha vita hii kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo” alisema Waziri Mkuu.

Hata hivyo Waziri Mkuu alibainisha kuwa, wajibu wa Baraza ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Udhibiti wa Dawa za Kulevya nchini, ambapo jukumu hilo ni kubwa na wajumbe wa Baraza hilo wanatakiwa kulitekeleza kwa uadilifu na umahiri mkubwa.

Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya limeanzishwa chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Na. 5 ya mwaka 2015 ambapo Waziri Mkuu ndiye Mwenyekiti wa Baraza hilo pamoja na wajumbe wengine wakiwemo Waziri anayeshughulikia Mambo ya Sheria, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Ndani ya Nchi.

Wengine ni Waziri anayeshughulikia Afya, waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Waziri anayeshughulikia Mambo ya Nchi za Nje, Waziri anayeshughulikia Fedha, Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Vijana, Waziri anayeshughulikia Elimu, Waziri anayeshughulikia Kilimo, Waziri anayeshughulikia Uchukuzi na Waziri anayeshughulikia Ulinzi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKIZINDUA BARAZA LA TAIFA LA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
 Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia Dawa za Kulevya Nchini Rogers William Sianga akijitambulisha mbele ya Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya wakati Waziri Mkuu alipokuwa akizindua Baraza Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
 Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na  Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Taifa la Udhibiti wa Dawa za Kulevya Nchini  wakati akifungua kikao cha Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.Picha na Daudi Manongi-MAELEZO.
 
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda wakizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Jenerali Venance Mabeyo akizungumza jambo na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya kupambana na kuzuia dawa Za Kulevya Nchini Rogers William Sianga wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Augustine Mahiga,Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Nape Nnauye, Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Harrison Mwakyembe na Waziri wa Mambo ya NdaniMhe Mwigulu Nchemba wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu wakati wa uzinduzi wa kikao cha Baraza la Taifa la kudhibiti Dawa za Kulevya.
Viewing all 46389 articles
Browse latest View live




Latest Images