Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Karibuni Jamvini Wanajamii

older | 1 | .... | 1142 | 1143 | (Page 1144) | 1145 | 1146 | .... | 1904 | newer

  0 0

  Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye kofia) akiongoza watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa mazoezi ya viungo, uzinduzi huo ulifanyika katika ufukwe wa Bahari ya Hindi. Wa tatu kulia Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya. 
  Baadhi ya maafisa, askari na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza wakiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo Dkt. Juma Malewa (wa tatu kushoto) pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza (DCP) Edith Mallya (wa nne kulia) katika kufanya mazoezi ya viungo ufukweni mwa Bahari ya Hindi
  Sehemu ya maafisa, askari na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa ufanyaji wa mazoezi ya viungo kwa watumishi wa Jeshi hilo, mazoezi ya viungo hufanyika mara mbili kwa wiki siku ya Jumatano na Ijumaa kuanzia saa 10 jioni. 
  Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza Gaston Sanga (wa pili kushoto) akiwa pamoja na watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika uzinduzi wa mazoezi ya viungo katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jijini Dar es salaam. 
  Kamishna Jenerali wa Magereza Dkt. Juma Malewa (mwenye kofia) akiongoza uzinduzi wa zoezi la ufanyaji wa mazoezi ya viungo kwa maafisa, askari na watumishi raia katika ufukwe wa Bahari ya Hindi mwishoni mwa juma. 
  Baadhi ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo kwa Jeshi hilo. 
  Sehemu ya watumishi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza katika mazoezi ya kunyoosha viungo siku ya uzinduzi wa zoezi la ufanyaji mazoezi ya viungo yalizinduliwa mwishoni mwa juma katika ufukwe wa Bahari ya Hindi.

  0 0  Na Dotto Mwaibale


  KIKOSI cha Timu ya Ngaya kutoka nchini Comoro kimewasili nchini kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Yanga katika dimba litakalofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Timu hiyo imewasili leo saa saba na nusu mchana kwa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATC), huku ikiwa imeongozana na baadhi ya viongozi wake.

  Mara baada ya kuwasili timu hiyo ilipokelewa na wananchi wa nchi hiyo wanaoishi hapa nchini hata hivyo viongozi wa timu hiyo hawakuwa tayari kuzungumza chochote na wanahabari badala yake walipiga picha ya pamoja na wachezaji na kisha kupanda kwenye magari na kuondoka.

  Katika mchezo wa awali uliofanyika nchini humo Yanga iliibuka kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya timu hiyo.

  Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika na kuwa waamuzi wake wanatarajiwa kufika kesho.

  Wachezaji wa Timu ya Ngaya ya nchini Comoro wakiwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo mchana kwa ajili ya mchezo wa marudiano dhidi ya Yanga utakaofanyika kesho kutwa Uwanja wa Taifa. Katika mchezo wa awali uliofanyika Comoro Yanga ilishinda bao 5-1.

  Picha ya pamoja na viongozi wao baada ya kuwasili.

  Mmoja wa viongozi wa timu hiyo (kushoto), akitoa maelekezo kabla ya kuondoka uwanjani hapo. (Picha na blog ya habari za jamii.com)

  Wachezaji wa timu hiyo wakiingia kwenye gari kuelekea hotelini walikofikia.

  0 0


  0 0


  0 0
 • 02/16/17--06:03: MANJI AACHIWA KWA DHAMANA
 • Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii


  Baada ya kusota rumande kwa takribani siku saba, hatimaeMwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusufu Manji amepandishwa katika kizimba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

  Manji ambae pia ni Diwani wa Mbagala Kuu na mfanyabiashara maarufu ameshtakiwa chini ya kifungu cha sheria namba 17(1)(a) ya sheria ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

  Amesomewa mashtaka yake leo na karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Cyprian Mkeha.

  Manji amekananusha kutumia dawa za kulevya na yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyomtaka kuweka dhamana ya milioni kumi na mdhamini mmoja ambaye nae ameweka kiasi hicho hicho cha dhamana

  Manji alifika mahakamani hapo saa nane kasoro nne na alipandishwa mahakamani majira ya saa tisa. Katibu wa klabu hiyo, Charles Boniphace Mkwasa ndiye aliyemuwekea dhamana Manji na kumfanya awe huru.

  Katika kesi hiyo Manji anatetewa na mawakili watatu waliokuwa wakiongozwa na wakili Alex Mgongolwa, Hudson Ndusyepo na Jeremiah Mtobesya huku upande wa Jamuhuri ukiongozwa na Mkurugenzi Msaidizi wa mashtaka, Oswald Tibabyekomya aliyekuwa akisaidiana na wakili wa serikali Shadrack Kimaro.

  Akisoma hati ya mashtaka, Mulokozi amesema kuwa, kati ya Februari 6 na 9 mwaka huu huko Upanga Sea View ndani ya Wilaya ya Ilala jijiini hapa, mshtakiwa alitumia dawa za kulevya aina ya Heroine (diacefyl Morphine)..

  Mara baada ya kutimiza masharti ya dhamana Manji aliondoka katika viwanja vya mahakama hiyo akiwa katika gari aina ya Hummer lenye namba za usajili T 670 BBX huku akisindikizwa na umati wa mashabiki wa Yanga.

  0 0

    Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimsikiliza Naibu Balozi wa Israel nchini mwenye  makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror alipotembelea Taasisi hiyo jana kwaajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mhe. Naibu Balozi Baror aliahidi nchi yake kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ili watanzania waendelee kupata huduma bora za matibabu ya Moyo. Mwanzoni mwa mwezi ujao jumla ya watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu ya moyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiagana na  Naibu Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror mara baada ya kumaliza kuitembelea  Taasisi hiyo jana kwa ajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mhe. Naibu Balozi Baror aliahidi nchi yake kuendelea kushirikiana na Taasisi hiyo ili watanzania waendelee kupata huduma bora za matibabu ya Moyo. Mwanzoni mwa mwezi ujao jumla ya watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwaajili ya matibabu ya moyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Michael Baror alipoitembelea  Taasisi hiyo jana kwaajili ya  kuona huduma mbalimbali za matibabu ya Moyo wanazozitoa. Mwanzoni mwa mwezi ujao watoto tisa wanatarajia kwenda nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo. Picha na Anna Nkinda - JKCI

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), akipata taarifa ya maendeleo ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani humo, Bi. Zitta Majinge (kulia), mara baada ya kuwasili leo. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.
   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia), akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge (wa pili kulia), kuhusu ukarabati wa uwanja huo mara baada ya kuwasili leo mkoani hapo. Kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Evod Mmanda.
   Muonekano wa jengo la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambalo lina uwezo wa kubeba abiria 100 kwa wakati mmoja.
   Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge (katikati), akimuonesha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), mipaka ya Uwanja wa Ndege huo ambao unahitajika kuwekwa uzio ili kulinda usalama wa uwanja.
   Muonekano wa barabara ya kuruka na kutua ndege katika Uwanja wa Ndege wa Mtwara yenye urefu wa mita 2258 na upana wa mita 30.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kushoto), akifafanua jambo kwa Meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) mkoa wa Mtwara Emmanuel Wanje, wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo.

  Serikali imesema  ina mpango wa kukarabati uwanja wa ndege wa  Mtwara  ifikapo mwezi Julai mwaka huu ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua uwanjani hapo na hivyo kufungua fursa za kiuchumi mkoani humo.
  Akizungumza mara baada ya kukagua uwanja huo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa ukarabati huo utahusisha njia ya kuruka na kutua ndege, maeneo ya maegesho pamoja na barabara yenye urefu wa km 1.5 inayoingia katika uwanja huo.

  "Tunategemea mwisho wa mwezi huu kutangaza zabuni ya ukarabati wa uwanja huu, matumaini yetu tutampata mkandarasi mzuri kwa ajili ya kazi hii", amesema Waziri Mbarawa.Aidha, Profesa Mbarawa amefafanua kuwa Serikali itahakikisha kuwa  inajenga uzio katika uwanja huo ili kuhakikisha usalama wa uhakika uwanjani hapo.

  Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa ametanabaisha kuwa Serikali ina mpango wa ununuzi wa rada nne  mpya kubwa na za kisasa ili kubaini taarifa za ndege  nchini tangu zinapoanza kuruka hadi kutua.
  “Tukiwa na rada kubwa na za kisasa zitatusaidia kubaini ndege zote hata ndogo zinazoingia katika maeneo ya viwanja vya madini kwa lengo la kuona ndege hizi zinaingia na zinatoka na nini?”, amesisitiza Waziri Mbarawa.
   Kuhusu ujio wa ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Bombadier Q 400, Waziri huyo amemhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda,  kuwa Serikali inatarajia kuanzisha safari zake kutoka Dar- Mtwara na Songea hivi karibuni.
  Kwa upande wake Mkuu wa wilaya hiyo, amemuomba Waziri huyo kuharakisha ujio wa ndege hizo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wa Mtwara na kuchochea fursa za kibiashara katika Mkoa huo na mikoa ya jirani.

  Naye Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania(TAA) mkoa wa Mtwara, Bi. Zitta Majinge, amesema kuwa Mamlaka itaendelea kushirikiana na Serikali kuhakikisha kuwa uboreshaji wa miundombinu ya viwanja hivyo inafanyika kwa wakati ili kukidhi mahitaji ya wasafiri wa anga.

  Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua maendeleo ya Kivuko cha MV Kilambo kinachotoa huduma kati ya Kilambo na Namoto nchini Msumbiji na kuhakikisha kuwa kivuko hicho kinafanya kazi katika vipindi vyote vya mwaka.

  Waziri Prof. Mbarawa yupo katika ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Mtwara ambapo ametembelea na kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na Wizara yake.

  Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano, Serikalini Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano


  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia Watendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula (kulia) wakati wa mkutano wa Makamu wa Rais na Watendaji  wa Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella akihutubia mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa mkutano wa watendaji na Halmashauri ya wilaya ya Ilemela jijini Mwanza (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
  Picha ya pamoja

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameunga mkono jitihada za kupambana na dawa za kulevya nchini kama hatua ya kuliokoa na taifa janga hilo ambalo limesababisha madhara makubwa katika jamii.

  Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza.

  Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya yatakuwa ni endelevu lengo likiwa kukomesha kabisa uuzaji,usambazaji na utumiaji wa dawa hizo kama hatua ya kuokoa kizazi cha sasa na kijacho nchini.

  Amesema kamwe serikali ya wamu ya Tano hatarudi nyuma katika vita dhidi ya dawa za kulenya na ameomba wananchi waendelee kutoa taarifa za siri kwa vyombo vya dola zitakazosaidia kuwabaini watu wanajihusisha na biashara hiyo ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

  Kuhusu tatizo la uvuvi haramu, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amewaagiza viongozi wa mikoa ya kanda ya Ziwa wakiwemo viongozi wa Mwanza na mikoa mingine nchini kuanzisha mara moja oparesheni kali ya kupambana na wavuvi haramu katika Ziwa Victoria ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika Ziwa hilo.

  “Viwanda vya samaki kwa sasa havipati samaki wa kutosha hali ambayo imezorotesha shughuli za kuchakata samaki hivyo nawaagiza viongozi wote kupambana ipasavyo na wavuvi haramu na kamwe wasionewe huruma” amesisitiza Makamu wa Rais.

  Makamu Rais Mhe Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini ni muhimu yakaenda pamoja na oparesheni ya kukomesha uvuvi haramu katika Ziwa Victoria na maeneo mengine nchini.

  Amesema wavuvi haramu wamechangia kwa kiasi kikubwa kupungua kwa samaki katika maziwa mbalimbali nchini kwa sababu wanatumia nyavu haramu ambazo zinaharibu mazalia ya samaki hivyo ni lazima hatua stahiki zichukuliwe dhidi yao ili kukomesha kabisa tatizo hilo.

  Wakati huo huo halmashauri ya wilaya ya Ilemela, imetekeleza maagizo  14 yaliyotolewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa mwaka jana alipofanya ziara ya kikazi wilayani humo likiwemo suala la watumishi wa halmashauri kukaa karibu na maeneo ya ofisi ambapo mpaka sasa wakuu wa idara 23 wanaishi ndani ya wilaya ya Ilemela ikilinganishwa na hapo awali ambapo watumishi hao walikuwa wanakaa nje ya wilaya hiyo hali ambayo inatajwa ilichangia kuzorotesha utendaji kazi kwenye halmashauri hiyo.

  Kufutia hali hiyo, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mlezi wa halmashauri hiyo amepongeza viongozi wa wilaya hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri kwa kutekeleza maagiza yake kwa haraka na kwa wakati.

  Amesema yeye kama mlezi wa halmashauri hiyo atahakikisha halmashauri inafanya kazi kwa ubora wa hali ya juu katika utoaji wa huduma za uhakika kwa wananchi na kuondoa haraka changamoto mbalimbali zizowakabili wananchi hao ikiwemo uimarishaji wa miundombinu ya barabara

  0 0

  Jeshi la polisi limetakiwa kufanya kazi kwa waledi ili kuleta ufanisi mzuri wa kazi, pamoja na kuwafichua wale wote wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.


  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uvuvi kutoka Nchini China Bwana Lan Ping Yong kushoto akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi azma ya Kampuni hiyo kutaka kuwekeza mradi wa Uuvi Visiwani Zanzibar. Viongozi hao walikutana katika Ofisi ya Balozi Seif iliyomo ndani ya jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia akizungumza na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J.C Barupal kwenye Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni.   Picha na – OMPR – ZNZ.


  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuimarisha Sekta ya Uvuvi katika azma yake ya kujenga uchumi imara unaojitegemea utakaostawisha maisha ya Wananchi wake.

  Alisema uimarishaji huo utaelekezwa zaidi katika ujenzi wa Viwanda Vidogo vidogovya usindikaji wa mazao ya Baharini utakaotoa fursa ya kukaribisha Makampuni na Taasisi za Kimataifa kuwekeza miradi yao Visiwani Zanzibar. 

  Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong kutoka Nchini China ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Bwana Lan Ping Yong hapo Ofisini kwake Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. 

  Alisema Sekta ya Uvuvi bado ina rasilmali ya kutosha inayoweza kusaidia uchumi wa Taifa unaokwenda sambamba na fursa za upatikanaji wa ajira zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya Wananchi walio wengi Nchini. 

  “ Hii ni njia bora na mwafaka ya upatikanaji wa ajira hasa kwa Vijana ”. Alisema Balozi Seif Ali Iddi. 

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliueleza ujumbe wa Viongozi wa Kampuni hiyo ya Hong Dong ambao amewahi kukutana nao wakati wa ziara yake ya Kiserikali ya hivi karibuni Nchini China kwamba juhudi zitafanywa na Serikali katika kuona azma ya Kampuni hiyo ya kutaka kuwekeza Zanzibar inafanikiwa. 

  Balozi Seif alimuahidi Mkurugenzi Mkuu huyo wa Kampuni ya Hong Dong na Ujumbe wake kuwa pande zinazohusika nchini zitakutana na kuangalia wazo la Kampuni hiyo la uwekezaji kwa lengo la kuchukuliwa hatua za muelekeo wa uanzishwaji wa uwekezaji huo. 

  Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Uvuvi ya Hong Dong ya Nchini China Bwana Lan Ping Yong alisema mradi wa Uvuvi unaotaka kuwekezwa Visiwani Zanzibar utakuwa na uwezo wa kutoa fursa za ajira zisizopungua elfu 1,700. 

  Bwana Ping alisema licha ya nafasi za ajira zikilengwa kwa Wazalendo lakini pia utaambatana na wataalamu wa Kampuni ya Hong Dong kutoa mafunzo ya Uvuvi kwa Wavuvi wa Kienyeji ili waendeshe miradi yao katika Mfumo wa Kisasa unaokubalika Kimataifa. 

  Bwana Ping alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba yapo mafanikio makubwa yaliyokwisha patikana katika Nchi ya Mauritania iliyoko Magharibi ya Bara la Afrika baada ya Kampuni hiyo kuwekeza Mradi wa Uvuvi Nchini humo. 

  Alisema mapato ya Wavuvi wadogo wadogo wa Nchi hiyo waliobahatika kuwemo kwenye mradi huo kwa sasa yameongezeka na kuleta ustawi wa familia zao na Taifa lao kwa ujumla. 

  Mkurugenzi huyo wa Kampuni ya Hong Dong alisema Taasisi hiyo imetenga nafasi Tatu kwa ajili ya Watendaji wa Sekta ya Uvuvi Zanzibar kwenda Nchini Mauritania kujifunza hatua iliyofikia ya Uwekezaji wa Kampuni hiyo katika Nyanja ya Uvuvi. 

  Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alikutana na Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J. C. Barupal Ofisini kwake katika Majengo ya Baraza la Wawakilishi Mbweni Wilaya ya Magharibi “B”. 

  Katika mazungumzo yao Balozi Seif alisema Nchi ya India iliyopo Bara ya Asia imeshapiga hatua kubwa katika masuala ya Teknolojia ya kisasa ambayo Zanzibar kama Nchi inayoendelea inaweza kujifunza kwa kina Taaluma hiyo kutoka kwa Walaalamu wa India. 

  Balozi Seif alimueleza Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar kwamba Makampuni ya India yana uwezo wa kuanzisha miradi yao katika sekta za Kilimo, Biashara na Viwanda Visiwani Zanzibar ili kuitikia wito wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kukaribisha Vitega uchumi vya miradi tofauti Nchini. 

  Naye kwa upande wake Balozi Mdogo wa India aliyepo Zanzibar Bwana J.C. Barupal alimuahidi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba India itaendelea kuunga mkono harakati za maendeleo ya Zanzibar. 

  Bwana Barupal alisema uungaji mkono huo umekuja kufuatia mafungamano ya muda mrefu yaliyopo ya Ushirikiano wa Kihistoaria kati ya pande hizo mbili hasa katika masuala ya Kibiashara yaliyotoa fursa kwa wafanyabaishara wa India kuingiza bidhaa zao Visiwani Zanzibar karne nyingi zilizopita nyuma. 


  Othman Khamis Ame 

  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

  0 0

   Mwanafunzi Ali Askher Walji akifurahia zawadi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile baada ya kufanya vizuri katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 7 ya mwaka 2016.
   Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile, akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 7 ya mwaka 2016.
  Dokta Faraji Lydenge kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika mitihani ya Taifa ya daraja la 4 ya mwaka 2016.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir Bw. Mahmood Ladak akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya katika Mitihani ya Taifa ya Daraja la 3 ya mwaka 2016.
    Sheikh Ali Azim Shiraz akimbusu mmoja wa wanafunzi wa daraja la awali wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir, baada ya kumpatia zawadi.
   Sheikh Ali Azim Shiraz akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya Daraja la 1 ya mwaka 2016.
   Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir, wakishuhudia utoaji wa zawadi.
   Baadhi ya wazazi wakifuatilia utoaji wa zawadi.
   Afisa Mtendaji Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir Bw. Mahmood Ladak, akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile.Katikati ni Dokta Faraji Lydenge kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akishuhudia.
  Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile, akiangalia moja ya vitabu vilivyoko kwenye Maktaba ya shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir wakati alipotembea maeneo mbalimbali ya shule hiyo akiwa na Naibu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zai Abdi.

  Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na viongozi wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir hiyo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu Bw. Mahmood Ladak, Mkuu wa Shule Bi. Shaimuna Chandro na kushoto ni Naibu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zai Abdi.
  Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir   Bi. Shaimuna Chandro wakati alipowasili shuleni hapo kwenye Sherehe ya Kuwazawadia Wanafunzi wa shule hiyo waliofanya vizuri katika mitihani yao leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Naibu Mkuu wa shule hiyo Bi. Zai Abdi.

   Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bi. Giveness Aswile akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa shule hiyo Bw. Mahmood Ladak.
   Mkuu wa Shule ya Msingi ya Wavulana ya Almuntazir   Bi. Shaimuna Chandro akitoa neno la ukaribisho.

  Picha na Hussein Makame, NEC

  0 0

  NA EVELYN MKOKOI – DAR ES SALAAM


  Kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina, amekitoza faini ya shilingi Milioni 25, kiwanda kinachotengeneza biadhaa mbali mbali za matumizi ya manyumbani kama vile mafuta ya kujipaka mwili na dawa za meno cha chemicotex, mkilichopo Mbeji Jogoo jijini Dar es Salaam Kwa uchafuzi wa mazingira.

  Faini hiyo inayotakiwa kulipwa baada ya wiki mbili inatokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria ya mazingira unaofanywa na kiwanda hicho kilichopo katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi, ya kutiririsha maji taka na maji machafu katika mfereji wa maji ya mvua.

  Naibu Waziri Mpina ameshangazwa na uthubutu wa uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda hicho, pamoja na jitihada za serikali kupitia Ofisi yake na NEMC za kuthibiti uharibifu wa mazingira kwa kutoa adhabu mbali mbali kwa waharibifu.

  “Ujio wangu katika kiwanda hiki unatokana na malalamiko ya wananchi ya kututiririshiwa maji machafu katika makazi yao na maeneo ya biashara, hakuna atakaesalimika kwa kosa la kutokutunza mazingira na afya za watu, alisistiza Mpina”.

  “Mpo Barabarani mnachafua mazingira Hadharani bila haibu, mmedharau jitihada za serikali hii ya awamu ya tano na kuona kama ni nguvu za soda, adhabu hii ilipwe kama ilivyo elekezwa hatuta kuwa na uvumilivu kwa muwekezaji yeyote atakaechafua mazingira. Alisema”.

  Kwa Upande wake Mwanasheria kutoka NEMC Bw. Heche Mananche aliongeza kwa kusema kuwa Mmiliki wa kiwanda endapo hatakuwa tayari kulipa faini hiyo anaweza kupelekwa mahakamani.

  Wakati Huo Huo, Naibu Waziri Mpina Amezindua Mfereji wa kutirirsha maji katika kiwanda cha Cement cha wazo, baada ya kujiridhirisha na utekelezaji wa maagizo yake kiwandani hapo katika moja ya ziara zake mwaka jana, ambapo ilibainika kuwa kiwanda hicho kimekuwa ni kero kwa wananchi majirani kwa kutiririsha maji na kusababisha mafuriko hasa katika kipindi cha mvua.

  Kwa upande wake mkazi wa eneo la wazo bwana David kahaga aliupengeza uongozi wa kiwanda hicho kwa ujenzi wa mtaro huo na kusema kuwa umetatua changamoto katika shule ya msingi jirani na kiwanda hicho ambayo ilikuwa ikikumbwa na mafuriko mara kwa mara hasa katika kipindi cha mvua, lakini bado wakazi hao wana hofu na usalama wao baada ya ujenzi wa mtaro huo na kuwa bado wanakabiliana na changamoto kubwa ya vumbi itokanayo na uchimbaji wa malighafi za uzalishaji katika kiwanda hicho.
  Naibu Waziri Mpina akitolea Msisitizo adhabu ya uchafuzi wa mazingira aliyoitoa katika kiwanda cha Chemicotex Jijini Dar esSalaam alipofanya ziara ya kushtukiza leo.
  Kulia Bwana Navneft Meneja katika Kiwanda cha Chemicotex, akieleza jambo kwa wajumbe wa msafara wa Naibu Waziri Mpina katika ziara ya kushtukiza kiwandani hapo leo.
  Pichani Sehemu ya Uchafuzi wa mazingira unaofanywa na kiwanda cha Chemicotex cha jijini Dar es Salaam, kilichopo katika barabara ya Alai Hassan Mwinyi jijini.
  Sehemu ya Mtaro Ulijengwa na kiwanda cha Wazo ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Naibu waziri mpina katika iara yake aliyoifanya awali maka jana kiwandani hapo kupitia malamimiko ya wananchi.

  0 0
  Mkuu wa wilaya ya Ilala, kwa kushirikiana na Wakala wa vipimo Tanzania (WMA), mkoa wa Ilala, amefanya ziara ya kustukiza katika maeneo mbalimbali, katika kampeni yake ya kudhibiti vipimo na mizani 'feki'. Pichani, Mjema akikagua mzani kwenye bucha moja eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, akiwa katika ziara hiyo, Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo na kulia ni mfanyakazi katika bucha hiyo, Omar Khalfan.

  Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia) na Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (kushoto) wakiwa katika Ofisi ya Wakala wa Vipimo Tanzania (WMA), mkoa huo wa Ilala, baada ya kuwasili kwa ajii ya kuanza ziara ya kustukiza kukagua vipimo na mizani feki, katika maeneo mbalimbali leo. Aliyesimamani mwenyeji wao, Kaimu Meneje wa WMA mkoa huo wa Ilala, Alban Kihulla.

  Kaimu Meneja wa WMA mkoa wa Ilala, Alban Kihulla, akimuonyesha Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema (kulia), jinsi ya kutofauisha mizani 'feki' na ile iliyo bora, kabla ya kuendelea na ziara nje ya ofisi hiyo
  Mjema akionyeshwamizani malimbali feki na iliyo bora, katika karakana ya WMA mkoa wa Ilala

  Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akizungumza na wapokea mizigo hasa ya viazi mviringo, katika mitaa ya Kariakoo, Dar es Salaam, kuhusu umuhimu wa akuepuka kupokea magunia yaliyojazwa kwa mtindo wa Lumbesa, kwa kuwa utaratibu huo unakiuka vipimo halisi na hivyo kutia serikali hasara kwa kuwa siyo kipimo halali

  Mjema akiwafafanulia zaidi kuhusu hasara ya Lumbesa

  Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo.
  Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo.
  Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema wakimsikiliza kwa makini mfanyakazi wa bucha hiyo
  Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimhoji mfanyakazi huyo ikiwa kweli ana uhakika mzani wake ni halali
  Ofisa wa MWA (kulia) akijaribu kutumia vipimo vyake, kubaini kama mzani uliokuwa ukitumia katika Bucha ya Ndevu Complete, Kariakoo, siyo feki. Baadaye ulibainika kuwa mzani huo unafaa
  Mfanyakazi wa Bucha hiyo ya Ndevu Complete akiweka nyama kuonyesha mzani unavyopima
  Mjema akizungumza na wananchi na waandishi wa habari baada ya kumaliza sehemu ya ukaguzi wake wa vipimo na mizani, leo. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

  0 0


  0 0  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin akizungumza leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi. (Katikati) ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry ambaye alikuwa mgeni rasmi na Mkuu wa Itifaki BAKWATA Mohammed Nassor.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam katika hafla ya uzinduzi wa huduma mpya kutoka Zantel iliyopewa jina la ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Zantel watakaopenda kutumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo. (katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin na Mkuu wa kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Hamza Zuheri.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin wakionyesha vipeperushi vya huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ kuashiria uzinduzi rasmi wa huduma hiyo uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel ikiwa ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.
   Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeiry akitoa salamu na kugawa vipeperushi kwa baadhi ya wageni waalikwa mapema leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ itakayopatikana kupitia mtandao wa Zantel mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi. (Katikati) ni Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin pamoja na Mkuu wa Kitengo cha huduma na bidhaa Zantel Bw. Hamza Zuheri.

  Mwandishi wa gazeti la The Citizen Alawi Masare (Kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi Mkuu wa Zantel Benoit Janin (katikati) na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Zantel Rukia Iddi Mtingwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma mpya ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo ni mahususi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu za mkononi.


  Waumini  wa dini ya Kiislamu sasa watajifunza masuala ya dini kupitia simu za mkononiZantel kwa kushirikiana na Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) imezindua huduma mpya inayojulikana kama ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawawezesha waumini wa dini ya Kiislamu kujifunza kuhusu imani ya dini hiyo pamoja na kupata mafundisho kupitia simu zao za mkononi.

  Huduma hiyo itajumuisha mambo mbalimbali kama vile Hadithi, Quran, Dua na huduma nyingine nyingi kupitia ‘App’ kwenye simu ya smartphone ((IVR/SMS/Mobile App and Bakwata News), ambapo pia mteja ataweza kupata taarifa kwa kupiga simu.

  Akizungumza wakati wa sherehe ya uzinduzi wa huduma hiyo mpya jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Mkurugenzi Mkuu wa Zantel, Benoit Janin alisema, “Tunafuraha kuzindua huduma hii ya ‘Zantel Madrasa’ ambayo itawaunganisha waumini wa dini ya Kiiislamu nchini na kuwawezesha kupata maarifa ya dini hiyo kwa urahisi zaidi.”

  Kwa upande wake Sheikh Mkuu wa BAKWATA, Mufti Abubakar Zuberi ambae alikua mgeni rasmi alisema, “Hii ni huduma ya kipekee kwa jumuiya ya Waislamu na kila mtu anayependa kujifunza kuhusu dini ya Kiislamu. Nawaomba Waislamu wenzangu kutumia fursa hii mpya na mjiunge kwa wingi ili kujua mambo yanayopaswa kufanywa katika Uislamu.”

  “Ninaamini kwamba huduma hii mpya itarahisha kazi kwetu viongozi wa Kiislamu kwa kuwa mafundisho mengi yatakuwa yanapatikana kupitia Zantel Madrasa,” alisema.

  Aliongeza kwamba BAKWATA itaisaidia Zantel kuitangaza huduma hiyo hapa nchini Tanzania hususan katika misikiti.

  Zantel Madrasa ni huduma ya kwanza kuzinduliwa kwenye mitandao ya simu nchini Tanzania ikilenga kutoa mafundisho ya dini na kuwaunganisha watu kujifunza kuhusu dini nchini.
  Huduma hii inatoa fursa kwa Waislamu wote kujiunga na huduma hii kwa kupitia namba maalumu za mtandao wa Zantel, hivyo kuwezesha watumiaji wa simu zaidi ya milioni 1 kupata mafunzo ya Madrasa kwa siku.

  Watumiaji wa mtandao wa Zantel ambao watapenda kuitumia huduma hii watatakiwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 15586 na kufuata maelekezo utakayopewa ili kuunganishwa na kufurahia huduma hii.

  0 0


  Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka(wapili kushoto) akiangalia athari za moto wa bweni hilo

  Mabaki ya vitu vya wanafunzi vilivyoteketea kwa moto katika bweni hilo

  Mkuu wa mkoa akizungumza na wanafunzi shuleni hapo

  Mkuu wa wilaya ya Makete Mh Veronica Kessy ameagizwa kuunda tume ya kuchunguza tukio la kuwaka moto bweni la wasichana liitwalo Serengeti La Itamba sekondari pamoja na bweni lingine la wasichana lililoungua jumamosi iliyopita

  Agizo hilo limetolewa Jana na Mkuu wa mkoa wa Njombe Mh. Christopher Olesendeka alipotembelea shule hiyo kujionea athari za moto huo ulioteketeza bweni moja lote

  Amesema serikali haiwezi kukubali na ni lazima chanzo cha moto huo kijulikane na hatua stahiki zitachukuliwa kwa wahusika endapo uchunguzi utabainisha kuwa kuna watu wamehusika

  Mh Olesendeka amesema serikali haiwezi kukubali vitendo vya moto kuendelea kuunguza shule mbali mbali hapa nchini

  Pia ameuagiza uongozi wa shule hiyo kuweka Mazingira mazuri kubaini ukweli wa hujuma kama hizi zinazoweza kujitokeza lakini pia kama kuna dosari mbali mbali miongoni mwa wanafunzi au shule nzima zijulikane ili ufumbuzi upatikane


  Na Edwin Moshi


  0 0


  Baadhi ya washiriki katika mkutano wa maendeleo ya mkoa (RCC)wa Arusha kama wanavyonekana pichani.
  Aliyeshika kipaza sauti ni mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli akiwa anachangia mada katika mkutano huo wa( RCC)mkoani Arusha.


  Na.Vero Ignatus Arusha.

  Jamii za wafugaji katika mkoa wa Arusha wameshauriwa kubadili mfumo wao wa maisha ili kutojikaribishia baa la njaa litakaloathiri ustawi wa jamii zao.Hayo yameelezwa na washiriki mbalimbali ambao wamehudhuria kikao cha Ushauri wa Mkoa (RCC) ambacho kimewashirikisha wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Arusha pamoja na wakurugenzi.

  Akichangia mada mkuu wa wilaya ya Longido bwana Daniel Chongolo amesema jamii ya wafugaji wamekariri katika wilaya wilaya hiyo,chakula kilichopo nimahindi ambapo wangeliweza kutojishughulisha kutafuta vyakula vingine kama viazi, mtama na ndizi ambazo vinapatikana kwa wingi kwenye minada hasa ile ya Nanja na Selela.

  Pia ameshauri jamii za wafugaji kua na utaratibu wa kujiwekea akiba ya chakula hasa wakati ule bei ya mifugo iko juu kwani wanaweza kuuza sehemu ya mifugo yao na kununua chakula cha kutosha na kuhifadhi katika maghala ya umma yaliyopo wilayani humo.

  Hoja hiyo imeonekana ikichangiwa na wakuu wa wilaya zingine ambapo mkuu wa wilaya ya Ngorongoro amesema katika utafiti aliofanya katika wilaya yake kwenye minada mbalimbali bei ya mahindi imepanda kutofautisha na vyakula kama ndizi na viazi, kwakua jamii hizi hazina mazoea ya kula vyakula basi hulalamika ya kwamba kuna baa la njaa.

  Akichangia mjadala huo mkuu wa mkoa wa Arusha amewataka wadau hao wa mkoa kuwa huru kuchangia, kushauri na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika mkoa wao.

  Kikao hicho kitaendelea tena kesho katika ukumbi wa mikutano wa mkoa.

  0 0

    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakati  aliposimama  akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
   Mwananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro  akiwasilisha kero yake kwa njia ya bango akidai mawasiliano ya simu za mkononi wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  aliposimama na kuwasalimia wananchi wa kijiji hicho waliokusanyika  barabarani. Alikuwa akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
    Wananchi wa kijiji cha Landanai wilayani Simanjiro wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati aliposimama na kuwasalimia akitoka  Orkesimet kwenda  Mererani Februari 16, 2017.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Mererani mkoani Manyara wakati alipowasili kwenye  eneo la mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye uwanja wa mikutano, Februari 16, 2017.
    Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye  uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara, Februari 16, 2017.
   Baadhi ya wananchi  Mererani mkoani Manyara wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipowahutubia  katika mkutano wa hadhara  kwenye uwanja wa mikutano wa Mererani ,  Februari 16, 2017.
   aziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema wingi wa mabango  katika mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu ni ishara ya wazi kuwa  watendaji wa  Halmashauri  hawawatembelei  wananchi na kutatua kero zao.
   Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa mikutano wa  Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017, Mheshimiwa Majaliwa alimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro na watendaji wake kukusanya mabango  yaliyokuwa yakionyeshwa na wananchi kwani mengi ya matatizo yanapaswa kumalizwa na viongozi hao  na aliwaagiza  kurejea Mererani siku inayofuata ili waitishe mkutano na  kujibu bango moja baada ya jingine.
  Pichani,  watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro wakikusanya mabango hayo.
   Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Ndugu Ali Juma baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara  kwenye uwanja mikutano  wa Mererani mkoani Manyara Februari 16, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

   Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasaliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Kivuko cha MV Kilambo kinachomilikiwa na TEMESA Jaston Mbawala wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya mkoani Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Mhandisi Samwel Chibwana wa TEMESA Mtwara.
   Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Mtwara Mhandisi Saidi Mongomongo akimuelezea jambo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa alipotembelea kivuko cha MV Kilambo kilichopo mkoani Mtwara kinachotoa huduma mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa akikagua injini ya kivuko cha MV Kilambo kinachotoa huduma mto Ruvuma kati ya Kilambo, Tanzania na Namoto, Msumbiji. Picha na Alfred Mgweno, TEMESA

  Na Alfred Mgweno, TEMESA Mtwara.

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Profesa Makame Mbarawa ametembelea na kukagua kivuko cha MV Kilambo kilichopo Mkoani Mtwara mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Kivuko hicho kinavusha magari, abiria na mizigo kati ya Kilambo upande wa Tanzania na Namoto Msumbiji.

  Akiwa katika ziara hiyo Profesa Mbarawa aliambatana na viongozi mbalimbali wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mkoani hapa. Profesa Mbarawa  alikaribishwa na Mkuu wa Kivuko hicho Jaston Mbawala, Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wa Mkoa wa Mtwara Mhandisi Saidi Mongomongo, Mhandisi  Msaidizi wa Kivuko Samwel Chibwana pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko Mhandisi Japhet Y. Maselle.

  Akiwa kivukoni hapo, Profesa Mbarawa alipata wasaa wa kusikiliza baadhi ya  changamoto zinazokikumba kivuko hicho ambapo Mhandisi Saidi Mongomongo alitaja changamoto hizo kuwa ni upungufu wa maji nyakati za kiangazi, ubovu wa maegesho ambayo husababisha magari makubwa kunasa wakati yanatoka au kuingia ndani ya kivuko pamoja na kukosekana kwa boti ndogo za uokoaji ambazo zingesaidia wakati wa dharura.

  Baadae Profesa Mbarawa alipata fursa ya kuongea na watumishi walio chini ya Wizara yake katika kikao kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa mkoa huku akiwataka watumishi  kuendelea kushirikiana na serikali, kufanya kazi kwa kasi na uadilifu kwa kuzingatia weledi. Pia aliwataka watumishi kujenga tabia ya kujitoa kwa ajili ya nchi yao.

  Profesa Mbarawa alikuwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja mkoani humo kwa nia ya kutembelea na kukagua utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya wizara yake.

older | 1 | .... | 1142 | 1143 | (Page 1144) | 1145 | 1146 | .... | 1904 | newer